Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MAJALIWA AHUTUBIA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE MJINI KIGOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Wanawake  (UWT) kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019.
 Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Kongamano la Wanawake  (UWT) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika  Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri)
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  Stella Ikupa akizungumza katika Kongamano la  Wanawake (UWT) lililohutubiwa na Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka wakitazama hot pot lililotengenezwa kwa mbao wakati alipohutubia katika Kongamano la Wanawake  kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Julai 13, 2019.

SONGAMBELE NA NAISINYAI ZAFAIDIKA NA ZIARA YA DKT BASHIRU

$
0
0
MATAWI ya Chama Cha Mapinduzi ya Naisinyai na Songambele Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara yamepatiwa mabati 200 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kwa ajili kujenga ofisi mpya za matawi hayo. 

Dk Bashiru akizungumza na wanachama wa matawi hayo alisema mabati hayo yanatolewa kupitia mfuko wa kuendeleza chama wa Mwenyekiti wao Rais John Magufuli. 

Alisema uhai wa chama hicho unategemea wanachama waliopo kwenye matawi na mashina hivyo wanayaunga mkono ili kuendelea kuifanya CCM iwe karibu zaidi na wananchi. 

Pia, aliwapongeza baadhi ya wadau wa maendeleo wa mji mdogo wa Mirerani, Paul Mollel na Siria Mepukori kwa kila mmoja kuchangia sh500,000 ya ujenzi wa tawi la CCM Songambele na diwani wa kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga (Mardad) alijitolea mifuko 20 ya saruji kwa tawi la Songambele. 

Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alijitolea mifuko 100 ya saruji ya tawi la Songambele, mbunge wa jimbo la Simanjiro, James Ole Millya alijitolea mifuko 40 kwenye tawi la Naisinyai na mifuko 20 ya saruji katika tawi la Songambele. 

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Yefred Myenzi alisema yeye binafsi anachangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa tawi la CCM Songambele. 

Mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Millya alisema amewatafutia wadau na amewachangia kwani matawi yote ni ya kwake, Naisinyai ni CCM yote japo hapo Songambele diwani ni Chadema.

Kada wa chama hicho Siria Mepukori alisema yeye ni mdau wa maendeleo na aliamua kumuunga mkono Dk Bashiru kwa sh500,000 ili  kufanikisha ujenzi wa tawi hilo la Songambele.

Kada mwingine Paul Mollel alisema amechangia sh500,000 kwenye ofisi hiyo ya Songambele ili kumuunga mkono Katibu Mkuu wa CCM ambaye ana lengo zuri la kuhakikisha matawi yanajengwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa kuzindua Tawi la Oloshonyokiye Kijiji cha Naisinyai Wilayani Simanjiro na kuipatia mabati 100.
 Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akishiriki ujenzi wa Tawi la Songambele Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara na kuipatia mabati 100.
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akipokewa na viongozi mbalimbali alipowasili Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATAKA DHANA YA AFYA MOJA KUTEKELEZWA KWA WAKATI

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amewataka waratibu wa dawati la Afya Moja kutekeleza dhana ya Afya Moja kwa wakati sambamba na kuweka mikakati mahususi itakayowaongoza katika utendaji wa dhana hiyo.  

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha wadau wa afya moja na wataalam kutoka sekta ya Afya, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira kilichofanyika Julai 12, 2019, Jijini Dodoma.

Alieleza kuwa dhana ya afya moja inajumuisha wataalam na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa dhana hiyo ikiwemo kutoa fursa ya kushirikiana pamoja katika kukabiliana na madhara au magojwa hatarishi nchini.

“Nimepitia Sera ya Afya moja na kuona suala hili linatakiwa kusimamiwa vyema, ikiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mratibu wa Dawati la Afya moja kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo, katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa mahala salama,” alieleza Mwaluko

Aliongeza kuwa, suala la kujenga uwezo kwa waratibu wa dawati la afya moja inatakiwa kuangalia ofisi kwa ujumla na si mjumbe mmoja tu ambaye atakuwa anasimamia masuala hayo ya Afya moja wakati wote.

“Mnatakiwa mtambue kuwa mkiwa kama wafanyakazi mna majukumu mengine ya kiofisi ambayo mnatakiwa kuyatekeleza, hivyo mtoe fursa kwa wafanyakazi wengine waliopo kwenye ofisi zenu kujifunza na kuelewa dhana hii ya afya moja,” alieleza Mwaluko.

Aidha, alitoa wito kwa waratibu wa dawati hilo kuelimisha umma kuhusu maana ya Afya Moja na dhana nzima ya Afya moja ili wananchi waweze kuwa na ufahamu wa suala hilo.

Pia, aliwahimiza washauri elekezi wa dawati hilo kutimiza majukumu yao kwa weledi na kutoa ushauri mapema kuhusu dhana ya Afya Moja.

Kwa upande wake, Prof. Robinson Mdegela ambaye ni Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja alisema kuwa kukutana kwao katika kikao hiko ni kuonesha utayari wa kila mtaalamu katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuongeza msukumo juu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Afya Moja.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Afya Moja walipokutana kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akielezea jambo kwa wadau wa Afya Moja walioshiriki kikao hiko kilichofanyika Hoteli ya Morena, Jijini Dodoma.
 Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja Dkt. Kunda John akichangia mada kuhusu umuhimu wa dhana ya Afya Moja wakati wa kikao kilichofanyika Julai 12, 2019 Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wataalamu wa Dawati la Afya Moja nchini wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Wadau wa Afya Moja walipokutana kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.
 Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Afya Moja nchini walipokutana Jijini Dodoma.
 Sehemu ya wataalamu wa dawati la Afya Moja nchini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka (hayupo pichani).
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe mara baada ya kikao kilichowakutanisha na Wadau wa Afya Moja kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini.

MATUKIO KATIKA PICHA USAJILI WA NGO’s UKIENDELEA KANDA YA MASHARIKI KATIKA OFISI ZA WIZARA YA AFYA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Baraka Leonard (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati wakimpata huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo  za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
  Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bw. Faki Shaweji (kulia)akifafanua jambo kwa mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akimpatia huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo  za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
  Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Victor Rugalabamu (kushoto) akitoa huduma ya kusajili kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bw. January Kitunsi (kushoto) akitoa huduma ya kusajili Taasisi kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo  za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

KAMATI YA UONGOZI YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Kamati hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa kwanza Kulia ni Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai na  wanaofuatia upande huo ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo  . Upande wa kushoto ni Wajumbe wa Kamati hiyo na ambao pia ni Wabunge kutoka Zambia, Uganda,Namibia, Ghana na Kenya.
 Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Kamati hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.  Wakwanza kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka.  Pia, wanaofutia upande huo ni Wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Bunge la Zambia, Uganda na Namibia.
  Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka alipowasili kwa ajili ya kikao hicho. PICHA NA BUNGE

Sagini aitaka VETA kupeka mashine Simiyu

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini amesema bidhaa zinazozalishwa na VETA wapeleke kwa wakulima ili kuweza kutatua changamoto zao ikiwa pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

Sagini aliyasema hayo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema wakulima wanahitaji mashine mbalimbali ambazo VETA mnazalisha hivyo zisiishie katika Maonesho.

Amewataka VETA kwenda na mashine hizo na kuziuza kwa wakulima wa Simiyu katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika mkoani humo.
Sagini amesema kuwa VETA wanafanya ugunduzi katika nyanja mbalimbali ambazo zikitumiwa vizuri kutarahisha wakulima kukua kiuchumi kutokana na vitendea kazi kutoka VETA.
Aidha amesema kuwa mashine za VETA zisimbazwe kwani gharama itakuwa rahisi kwa wakulima kumudu kuliko mashine za nje.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akipata maelezo kutoka VETA kwa mwanafunzi wenye mahitaji Maalum vitu wanavyotengeneza wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akipata maelezo kuhusiana na mashine ya kuchakata majani kwa ajili ya Mifugo wakati alipotembelea Banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Jumanne Sagini akizungumza na waandishi habari kuhusiana vitu alivyoona katika banda la VETA katika Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mashine iliyundwa na Watu Wenye mahitaji Maalum kwa kushirikiana na Mwalimu wao wa VETA Chang'ombe.

Waitara ahimiza wazazi na walezi wenye uwezo kuchangia maendeleo ya shule

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Mwita Mwikwabe Waitara (MB) amesema kuwa serikali haijakataza michango shuleni isipokuwa ile iliyokuwa ya lazima na akataka michango hiyo ifuate mwongozo wa serikali wa kuchangia.

Akizindua jengo jipya la bwalo la chakula lililojengwa na shirika lisilo la kiserikali la CDTF jana katika shule ya msingi mlimwa iliyopo katikati ya jiji la Dodoma, Mhe.Waitara amesema kuwa wapo watu wamekuwa wakipita pita huko mitaani na kutoa tafsiri potofu kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano amepiga marufuku michango yote shuleni jambo ambalo si la kweli.

Amesema kuwa michango ambayo Mhe.Rais aliyokataza ni ile ya lazima ambayo ilikuwa ikilazimisha watoto wote shuleni kuchangia ama wana uwezo au la jambo lililokuwa likisababisha watoto wanaokosa kulipia michango hiyo kutokana na wazazi au walezi wao kukosa fedha hufukuzwa shule.

“Ila nafahamu kuwa yapo baadhi ya maeneo ambapo watu wamepotosha, tunao waraka wa serikali wa mwaka 2016, unaoelekeza ni aina gani ya michango inayopaswa kutolewa, namna gani michango ifanywe, na kina nani wasimamie, “ amesema na kuongeza:

“ waraka umeeleza kuanzia mtu wa kawaida hadi ngazi ya taifa, na umeelezwa vizuri kabisa, lakini watu wenye nia zao mbaya walifanya kusudi kabisa kupotosha wazazi wasichangie,” amesema.

Mhe. Waitara ameongeza kuwa maelekezo ya serikali ni kwamba walimu washirikiane na kamati za shule, na viongozi wa serikali, wakae pamoja wajadiliane namna ya kuchangia ili wale wazazi au walezi ambao wana uwezo wa kuchangia wachangie lakini wale wasio na uwezo wasichangishwe na pia wahakikishe watoto wanaotoka familia masikini wasiondolewe madarasani kwa wazazi wao kushindwa kutoa michango.

Akizungumzia hafla hiyo ya kuzindua bwalo hilo la chakula, Mhe.Waitara amelipongeza shirika la CDTF, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania pamoja na uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa bwalo hilo linakamilika ili kuwawezesha wanafunzi wa shule hiyo kupata chakula cha mchana shuleni.

Amesema kuwa ni muhimu kwa wazazi na walezi kutambua kuwa watoto wao wanapaswa kupatiwa chakula shuleni ili waweze kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri masomo yao.

Mhe. Waitara pia amewapongeza wazazi na walezi wa shule ya msingi Mlimwa A kwa kuitikia vizuri wito wa serikali kuhakikisha kuwa wanachangia maendeleo ya shule kwa kuwapatia uji kila siku watoto wote wanaosoma shule hiyo.

“Ndiyo maana katika taarifa ya Mwalimu Mkuu inaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo watoto wote wanaomaliza darasa la saba katika shule hii wameenda sekondari,”amesema.

Mhe.Waitara amesema watu wazima wanaposhiriki semina waandaaji huhakikisha kuwa washiriki wanapatiwa chai asubuhi, na mchana hupewa chakula, na akashangaa kwa nini watoto wanaosoma katika shule wasile chakula hivyo akawahimiza wazazi na walezi wa watoto wanaosoma katika shule zote nchini kuona umuhimu wa kuchangia ili watoto wao wapate chakula shuleni ili wasome kwa bidii na waweze kufaulu vizuri.

Mapema Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mlimwa Bi Salma Machaku alisema kuwa kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2018 katika matokeo ya kumaliza darasa la saba katika shule hiyo ufaulu umekuwa wa asilimia 100, kadhalika pia kwa darasa la nne jambo ambalo alidai limechangiwa na uongozi mzuri wa shule hiyo.

Amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo lenye thamani ya shilingi 81, 592, 478 utawawezesha wanafunzi wa shule hiyo kupata chakula kwenye eneo salama, pia watumishi wataweza kuandaa chakula katika hali ya usafi, na pia ukumbi utaweza kuwaingizia kipato kupitia kuendesha mikutano mbalimbali ikiwemo ile ya shule.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDTF Tanzania bwana Henry Mgingi amesema mradi huo wa ukumbi mbali na shilingi milioni 81 za wahisani, pia wazazi walichangia shilingi milioni 3 na halmashauri ya jiji la Dodoma walichangia shilingi milioni 4.2 hivyo jumla ya kiasi kilichotumika kuwa shilingi milioni 88.2

Bwana Mgingi amesema kuwa mbali na ujenzi wa bwalo hilo la wanafunzi shirika lake pia lilihusika katika ujenzi wa nyumba za walimu na kuwawekea umeme wa jua katika eneo la Losinoni Arusha, na katika mkoa wa Dodoma katika shule za Mlimwa A na B, Kiwanja cha Ndege na Chikoa  katika halmashauri ya jiji la Dodoma ambapo madarasa na samani zilitolewa katika shule hizo kwa vipindi tofauti.

Shirika la CDTF lilianzishwa mwaka 1962 na Mwanamke mwenye asili ya America Bibi Marion Lady Chesham na kwa muda wote huo limekuwa likishirikiana bega kwa bega na serikali za awamu zote katika kusaidia miradi ya maendeleo.

Shirika hili linaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa sasa bwana Leon Msimbe ambaye alichukua uongozi huo kutoka kwa aliyekuwa spika mstaafu Mhe.Pius Msekwa. Miongoni mwa wadhamini wa kwanza wa shirika hili ni pamoja na Marehemu Rashid Kawawa, Spika wa kwanza Adam Sapi Mkwawa na Mzee Job Lusinde.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara akizungumza na walimu, wanafunzi na wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya kuzindua ukumbi wa chakula wa shule ya msingi Mlimwa iliyopo Area C mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara akizindua ukumbi wa chakula wa shule ya msingi Mlimwa iliyopo Area C mjini Dodoma. Ukumbi huo wenye thamani ya shilingi milioni 81.5 umejengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali liitwalo CDTF kwa kushirikiana na kanisa la KKKT.
 Mwenyekiti wa Bodi wa shirika lisilo la kiserikali la CDTF bwana Leon Msimbe aliyenyoosha mkono akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara mara baada ya kuzindua ukumbi wa chakula wa shule ya msingi Mlimwa iliyopo Area C mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara akiwa na Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde wakiwa katika picha ya pamoja na vilanja wa madarasa, dada mkuu na kaka mkuu wa shule ya msingi Mlimwa A mara baada ya Mhe.Waitara kuzindua ukumbi wa chakula wa shule hiyo iliyopo Area C mjini Dodoma.

RAIS WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI AREJEA NCHINI KWAKE MARA BAADA YA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.
 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na wananchi wa Nyabilezi kabla ya kuondoka na kurejea nchini kwake Uganda. Rais Museveni ameahidi kujenga madarasa saba kwa ajili ya Shule ya Msingi Nyabilezi Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwaya ya watoto wa Shule ya Msingi Kalembo Umitashunta mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwaya pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akimsindikiza . PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATAKA DHANA YA AFYA MOJA KUTEKELEZWA KWA WAKATI

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao cha Wadau wa Afya Moja walipokutana kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Bashiru Taratibu. 
Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akielezea jambo kwa wadau wa Afya Moja walioshiriki kikao hiko kilichofanyika Hoteli ya Morena, Jijini Dodoma. 
Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja Dkt. Kunda John akichangia mada kuhusu umuhimu wa dhana ya Afya Moja wakati wa kikao kilichofanyika Julai 12, 2019 Jijini Dodoma. 
Baadhi ya wataalamu wa Dawati la Afya Moja nchini wakifuatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko (hayupo pichani) wakati wa kikao cha Wadau wa Afya Moja walipokutana kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini. 
Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Afya Moja nchini walipokutana Jijini Dodoma. 
Sehemu ya wataalamu wa dawati la Afya Moja nchini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mratibu wa Dawati la Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hansom Chinyuka (hayupo pichani). 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe mara baada ya kikao kilichowakutanisha na Wadau wa Afya Moja kwa lengo la kujadili utekelezaji wa mpango mkakati wa afya moja nchini. 

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU 
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU) 
…………………… 
Na; MWANDISHI WETU 
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Dorothy Mwaluko amewataka waratibu wa dawati la Afya Moja kutekeleza dhana ya Afya Moja kwa wakati sambamba na kuweka mikakati mahususi itakayowaongoza katika utendaji wa dhana hiyo. 
Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha wadau wa afya moja na wataalam kutoka sekta ya Afya, Mifungo, Wanyamapori na Mazingira kilichofanyika Julai 12, 2019, Jijini Dodoma. 
Alieleza kuwa dhana ya afya moja inajumuisha wataalam na wadau mbalimbali kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa dhana hiyo ikiwemo kutoa fursa ya kushirikiana pamoja katika kukabiliana na madhara au magojwa hatarishi nchini. 
“Nimepitia Sera ya Afya moja na kuona suala hili linatakiwa kusimamiwa vyema, ikiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ni mratibu wa Dawati la Afya moja kwa kushirikiana na Wizara, Taasisi za Serikali na wadau wa maendeleo, katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa mahala salama,” alieleza Mwaluko 
Aliongeza kuwa, suala la kujenga uwezo kwa waratibu wa dawati la afya moja inatakiwa kuangalia ofisi kwa ujumla na si mjumbe mmoja tu ambaye atakuwa anasimamia masuala hayo ya Afya moja wakati wote. 
“Mnatakiwa mtambue kuwa mkiwa kama wafanyakazi mna majukumu mengine ya kiofisi ambayo mnatakiwa kuyatekeleza, hivyo mtoe fursa kwa wafanyakazi wengine waliopo kwenye ofisi zenu kujifunza na kuelewa dhana hii ya afya moja,” alieleza Mwaluko. 
Aidha, alitoa wito kwa waratibu wa dawati hilo kuelimisha umma kuhusu maana ya Afya Moja na dhana nzima ya Afya moja ili wananchi waweze kuwa na ufahamu wa suala hilo. 
Pia, aliwahimiza washauri elekezi wa dawati hilo kutimiza majukumu yao kwa weledi na kutoa ushauri mapema kuhusu dhana ya Afya Moja. 
Kwa upande wake, Prof. Robinson Mdegela ambaye ni Mtaalamu Mshauri wa Afya Moja alisema kuwa kukutana kwao katika kikao hiko ni kuonesha utayari wa kila mtaalamu katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuongeza msukumo juu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa Afya Moja.

MAJALIWA AWASILI KIGOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kufungua Kongamano la Wanawake (UWT) kitaifa, Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kufungua Kongamano la Wananwake Kitaifa, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Dismas Nzamba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAFO AFURAHISHWA NA UBORA WA MAJENGO HOSPITALI YA ITILIMA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amefurahishwa na ubora wa majengo ya hospitali mpya inayojengwa wilayani Itilima Mkoani Simiyu. 

Jafo ameonyesha kufahishwa huko akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu.“Hamjamaliza kwa asilimia 100 ujenzi wa hospitali yenu lakini nimeridhika sana kwa kazi nzuri ya majengo yenu,” amesema Jafo. 

Jafo amewataka viongozi na watendaji wa wilaya hiyo kukamilisha ujenzi huo ifikapo Julai 30 mwaka huu. Katika Ziara hiyo, Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga kwa kuwapigania wananchi wake katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Aidha,Njalu ameishukuru sana serikali kwa fedha Sh.Bilioni 1.5 zinazofanikisha ujenzi wa hospitali hiyo sambamba na fedha nyingi za miradi mingine ya maendeleo ikiwemo fedha za ujenzi wa jengo la Utawala.

KAMATI YA UONGOZI YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Kamati hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo.Wakwanza kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka.Pia, wanaofutia upande huo ni Wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Bunge la Zambia, Uganda na Namibia.
Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Justin Muturi akiongoza kikao cha Kamati hiyo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa kwanza Kulia ni Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai na wanaofuatia upande huo ni Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati hiyo . Upande wa kushoto ni Wajumbe wa Kamati hiyo na ambao pia ni Wabunge kutoka Zambia, Uganda,Namibia, Ghana na Kenya.
Katibu wa CPA-Kanda ya Afrika na ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Ndg. Stephen Kagaigai (wa kwanza kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Spika wa Bunge la Kenya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Justin Muturi akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon Mhe. Emilia Lifaka alipowasili kwa ajili ya kikao hicho.

Mbozi kujengwa mabweni kwaajili ya watoto wenye vipaji vya michezo

$
0
0
Watoto wa shule ya Msingi Isangu wakionyesha ujuzi wa kucheza ngoma ya jamii ya wamakua inayochezwa kwenye mavuno, ikiwa ni sehemu ya kupamba mkutano huo ulioambatana na kuutangaza mfuko wa elimu wilaya ya Mbozi ili kukusanya michango kwaajili ya uendelezaji miundombinu ya elimu
Watoto wakiwa mkao wa kula ikiwa ni sehemu ya vionjo vya ngoma ya Wamakua inayochezwa msimu wa mavuno.
Afisa elimu wilaya ya Mbozi Hosana Nshullo akiwasilisha hali ya sekta ya elimu mbele ya wadau wa elimu wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Halima Mpita akizungumzia mkakati wa ujenzi wa mabweni kwaajili ya kuwaweka kambini vijana wenye vipaji vya michezo mashuleni
**************

Na Danny Tweve -Mbozi

Wilaya ya Mbozi imo kwenye mkakati wa kuanzisha mabweni kwaajili ya watoto wenye vipaji vya michezo kwenye baadhi ya shule za kata ili kuwezesha watoto hao kuendelea kukuza vipaji vyao kambini kutokana na wilaya hiyo kuendelea kufanya vyema kwenye eneo la michezo

Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa elimu wilayani humo, Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Mbozi Bi Halima Mpita amesema tayari wameanza mkakati huo kwenye shule zake baada ya kupata wadau wa kuchangia ujenzi huo.

Halima Mpita ni miongoni mwa watanzania waliothibitishwa na wizara ya elimu na ufundi kwenye eneo la Ubunifu akiwa miongoni mwa watanzania 18 waliobainishwa kwenye shindani mbalimbali za ubunifu.

Amesema hatua hiyo itawezesha vipaji vinavyoibuliwa mashuleni kukuzwa na kwamba katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo wilaya hiyo na mkoa wa Songwe kwa ujumla imekuwa miongoni mwa mikoa inayowakilisha vyema kwenye mashindano ya michezo ya UMISETA (kwa shule za sekondari) na UMITASHUMTA (kwa shule za msingi) .

Katika hatua nyingine kikundi cha ngoma cha shule ya Msingi Isangu kiliweza kuwanyanyua watu waliohudhulia mkutano huo kutokana na burudani yake ya ngoma ya jamii ya Wamakua kutoka mkoa wa Mtwara ambapo wengi walishindwa kujizuia na kuwatuza watoto hao.

Mwanariadha wa zamani marehemu Erasto Zambi ni miongoni mwa wanariadha waliowika miaka ya nyuma kwa kufukuza upepo ni sehemu ya matunda ya wilaya ya Mbozi. mwingine katika mchezo wa riadha ni Zaina Mwashambwa.

RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI GEITA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa mkoa wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za makazi ya askari, uzinduzi utakaofanyika katika eneo la magogo mkoani humo. 

IGP Sirro amesema kuwa, katika tukio hilo ambalo litaongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambapo atazindua zaidi ya nyumba 114 zilizokwisha kamilika huku matarajio ya mradi huo ni kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima. 

Aidha, IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri jambo ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.

CHADEMA KUFUNGUA KESI YA KUPINGA LISSU KUVULIWA UBUNGE

$
0
0

NJOMBE

Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimesema kinakwenda mahakamani kupinda utaratibu uliyotumika kumvua ubunge aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Antipas Lissu ambaye yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu .

Siku kadhaa zimepita tangu Spika wa bunge atangaze bunge kuvuliwa ubunge kwa Lissu kwa sababu ya kutojaza fomu ya maadili na utoro wa vikao vya bunge kwa zaidi ya miezi kumi sasa jambo ambalo limeibua hisia tofauti kwa wanasiasa na watanzania kwa kuwa inafahamika kuwa mbunge huyo yupo nje kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana mwaka jana katika eneo la eria D jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mboye ambaye amewasiri mkoani Njombe akitokea Songwe ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikutano ya ndani katika mikoa ya kanda ya Nyasa mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama John Mlema amesema chama kinaendelea na mikutano ya ndani ambayo imebebwa na agenda kuu tatu ikiwemo ya ya kuvuliwa ubunge kwa Lissu na kudai mapema baada ya mikutano hiyo chama kitafungua kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge huo.

Agenda nyingine ambazo zimewekwa bayana katika ziara ya Mboye katika kanda ya Nyasa ni pamoja uchaguzi wa serikali za mitaa,kuwashukuru viongozi na wana chama kwa kazi kubwa waliyofanya wakati akiwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne huku agenda nyingine kubwa ikiwa ni kutoa ufafanuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo imeonyesha kubadili kwa kiasi kikubwa utendaji wa vyama nchini.

Nao baadhi ya viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo Rose Mayemba kiongozi wa chadema msingi na Alatanga Nyagawa ambaye ni katibu wa mkoa wakifafanua jitihada ambazo wamezichukua katika kuimarisha chama wamesema wameanza kuandikisha wanachama katika daftari la maalumu la A3 kuanzia ngazi ya chini na kwamba wanatanzania wategemee chama hicho kupata ushindi mkubwa kwa kuwa kimejihimarisha katika utunzaji wa taarifa.

Katika ziara hiyo Mboye ambayo amekagua na ujenzi wa jengo la ofisi za chama ameongozana na mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi huku kesho akitegemea kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Iringa na kukamilisha ziara ya kanda ya Nyasa yenye mikoa ya Mbeya,Rukwa,Songwe,Iringa na Njombe.

RAIS WA UGANDA YOWERI KAGUTA MUSEVENI AREJEA NCHINI KWAKE MARA BAADA YA ZIARA YAKE YA SIKU MOJA CHATO MKOANI GEITA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.

 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na wananchi wa Nyabilezi kabla ya kuondoka na kurejea nchini kwake Uganda. Rais Museveni ameahidi kujenga madarasa saba kwa ajili ya Shule ya Msingi Nyabilezi Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akielekea kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia kwaya ya watoto wa Shule ya Msingi Kalembo Umitashunta mara baada ya kumsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwaya pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akimsindikiza . PICHA NA IKULU

SUALA LA KUWAONDOA WATUMISHI WALA RUSHWA, WAZEMBE NI ENDELEVU-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Gaudencia Kabaka wakitazama hot pot lililotengenezwa kwa mbao wakati alipohutubia katika Kongamano la Wanawake kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Stella Ikupa akizungumza katika Kongamano la Wanawake (UWT) lililohutubiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Baadhi ya wananchi wa Kigoma wakimsikiliza Mgeni Rasmi Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika Kongamano la Wanawake (UWT) kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Kongamano la Wanawake (UWT) kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema suala la kuwaondoa kazini watumishi wa umma ambao ni wazembe, wala rushwa na wasiotimiza majukumu yao ipasavyo ni endelevu.

‘Serikali inahitaji watumishi wenye heshima na nidhamu ya kazi ili waweze kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote iwe wa kiuchumi, kidini au kikabila.Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Julai 13, 2019) wakati akihutubia mwananchi katika kongamano la kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa utekelezaji wa ilani.

Kongamano hilo limeandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ili kumpongeza Rais Dkt. Magufuli lilifanyika katika uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Amesema Serikali imejipanga vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, hivyo amewataka wananchi watoe taarifa iwapo watabaini uwepo wa watumishi wanaojihusisha na rushwa.

"Watumishi wa umma tunataka watambue kwamba wao ni watumishi wa wananchi, hivyo hawana budi kutambua wajibu wao ambao ni kuwatumikia mwananchi ipasavyo."Amesema kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika vita dhidi ya rushwa ambapo kwa Afrika Tanzania inaongoza kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya Transparency Internation.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi amesema kongamano hilo ni muendelezo wa makongamano mengine ya kumpongeza Rais yaliyofanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya na Unguja na Pemba.

Amesema viongozi hao wameonesha dhamira ya kweli ya kuwaletea wananchi maendeleo. "Tutaendelea kushirikiana na viongozi wetu na hatupo tayari kugawanyika."Awali, Mawaziri na Manaibu Waziri mbalimbali walipata fursa ya kuelezea namna ilani ilivyotekelezwa katika maeneo mbalimbali kupitia wizara zao.

Katika kongamano hilo viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali walivihama vyama vyao na kujiunga na CCM akiwemo na aliyekuwa Kalibu wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.

Waitara ahimiza wazazi na walezi wenye uwezo kuchangia maendeleo ya shule

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara akizindua ukumbi wa chakula wa shule ya msingi Mlimwa iliyopo Area C mjini Dodoma. Ukumbi huo wenye thamani ya shilingi milioni 81.5 umejengwa kwa ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali litwalo CDTF kwa kushirikiana na kanisa la KKKT.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara akizungumza na walimu, wanafunzi na wageni waalikwa kwenye hafla fupi ya kuzindua ukumbi wa chakula wa shule ya msingi Mlimwa iliyopo Area C mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi wa shirika lisilo la kiserikali la CDTF bwana Leon Msimbe aliyenyoosha mkono akimuonyesha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara mara baada ya kuzindua ukumbi wa chakula wa shule ya msingi Mlimwa iliyopo Area C mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Waitara akiwa na Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Antony Mavunde wakiwa katika picha ya pamoja na vilanja wa madarasa, dada mkuu na kaka mkuu wa shule ya msingi Mlimwa A mara baada ya Mhe.Waitara kuzindua ukumbi wa chakula wa shule hiyo iliyopo Area C mjini Dodoma.

Na Mathew Kwembe, Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe.Mwita Mwikwabe Waitara (MB) amesema kuwa serikali haijakataza michango shuleni isipokuwa ile iliyokuwa ya lazima na akataka michango hiyo ifuate mwongozo wa serikali wa kuchangia.

Akizindua jengo jipya la bwalo la chakula lililojengwa na shirika lisilo la kiserikali la CDTF jana katika shule ya msingi mlimwa iliyopo katikati ya jiji la Dodoma, Mhe.Waitara amesema kuwa wapo watu wamekuwa wakipita pita huko mitaani na kutoa tafsiri potofu kuwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano amepiga marufuku michango yote shuleni jambo ambalo si la kweli.

Amesema kuwa michango ambayo Mhe.Rais aliyokataza ni ile ya lazima ambayo ilikuwa ikilazimisha watoto wote shuleni kuchangia ama wana uwezo au la jambo lililokuwa likisababisha watoto wanaokosa kulipia michango hiyo kutokana na wazazi au walezi wao kukosa fedha hufukuzwa shule.

“Ila nafahamu kuwa yapo baadhi ya maeneo ambapo watu wamepotosha, tunao waraka wa serikali wa mwaka 2016, unaoelekeza ni aina gani ya michango inayopaswa kutolewa, namna gani michango ifanywe, na kina nani wasimamie, “ amesema na kuongeza:

“ waraka umeeleza kuanzia mtu wa kawaida hadi ngazi ya taifa, na umeelezwa vizuri kabisa, lakini watu wenye nia zao mbaya walifanya kusudi kabisa kupotosha wazazi wasichangie,” amesema.

Mhe. Waitara ameongeza kuwa maelekezo ya serikali ni kwamba walimu washirikiane na kamati za shule, na viongozi wa serikali, wakae pamoja wajadiliane namna ya kuchangia ili wale wazazi au walezi ambao wana uwezo wa kuchangia wachangie lakini wale wasio na uwezo wasichangishwe na pia wahakikishe watoto wanaotoka familia masikini wasiondolewe madarasani kwa wazazi wao kushindwa kutoa michango.

Akizungumzia hafla hiyo ya kuzindua bwalo hilo la chakula, Mhe.Waitara amelipongeza shirika la CDTF, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania pamoja na uongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha kuwa bwalo hilo linakamilika ili kuwawezesha wanafunzi wa shule hiyo kupata chakula cha mchana shuleni.

Amesema kuwa ni muhimu kwa wazazi na walezi kutambua kuwa watoto wao wanapaswa kupatiwa chakula shuleni ili waweze kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri masomo yao.

Mhe. Waitara pia amewapongeza wazazi na walezi wa shule ya msingi Mlimwa A kwa kuitikia vizuri wito wa serikali kuhakikisha kuwa wanachangia maendeleo ya shule kwa kuwapatia uji kila siku watoto wote wanaosoma shule hiyo.

“Ndiyo maana katika taarifa ya Mwalimu Mkuu inaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo watoto wote wanaomaliza darasa la saba katika shule hii wameenda sekondari,”amesema.

Mhe.Waitara amesema watu wazima wanaposhiriki semina waandaaji huhakikisha kuwa washiriki wanapatiwa chai asubuhi, na mchana hupewa chakula, na akashangaa kwa nini watoto wanaosoma katika shule wasile chakula hivyo akawahimiza wazazi na walezi wa watoto wanaosoma katika shule zote nchini kuona umuhimu wa kuchangia ili watoto wao wapate chakula shuleni ili wasome kwa bidii na waweze kufaulu vizuri.

Mapema Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mlimwa Bi Salma Machaku alisema kuwa kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2018 katika matokeo ya kumaliza darasa la saba katika shule hiyo ufaulu umekuwa wa asilimia 100, kadhalika pia kwa darasa la nne jambo ambalo alidai limechangiwa na uongozi mzuri wa shule hiyo.

Amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo lenye thamani ya shilingi 81, 592, 478 utawawezesha wanafunzi wa shule hiyo kupata chakula kwenye eneo salama, pia watumishi wataweza kuandaa chakula katika hali ya usafi, na pia ukumbi utaweza kuwaingizia kipato kupitia kuendesha mikutano mbalimbali ikiwemo ile ya shule.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CDTF Tanzania bwana Henry Mgingi amesema mradi huo wa ukumbi mbali na shilingi milioni 81 za wahisani, pia wazazi walichangia shilingi milioni 3 na halmashauri ya jiji la Dodoma walichangia shilingi milioni 4.2 hivyo jumla ya kiasi kilichotumika kuwa shilingi milioni 88.2

Bwana Mgingi amesema kuwa mbali na ujenzi wa bwalo hilo la wanafunzi shirika lake pia lilihusika katika ujenzi wa nyumba za walimu na kuwawekea umeme wa jua katika eneo la Losinoni Arusha, na katika mkoa wa Dodoma katika shule za Mlimwa A na B, Kiwanja cha Ndege na Chikoa katika halmashauri ya jiji la Dodoma ambapo madarasa na samani zilitolewa katika shule hizo kwa vipindi tofauti.

Shirika la CDTF lilianzishwa mwaka 1962 na Mwanamke mwenye asili ya America Bibi Marion Lady Chesham na kwa muda wote huo limekuwa likishirikiana bega kwa bega na serikali za awamu zote katika kusaidia miradi ya maendeleo.

Shirika hili linaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa sasa bwana Leon Msimbe ambaye alichukua uongozi huo kutoka kwa aliyekuwa spika mstaafu Mhe.Pius Msekwa. Miongoni mwa wadhamini wa kwanza wa shirika hili ni pamoja na Marehemu Rashid Kawawa, Spika wa kwanza Adam Sapi Mkwawa na Mzee Job Lusinde.

WIZARA YA FEDHA YAPAMBANA NA MATAPELI WANAOZUSHA PROGRAM YA UTOAJI MIKOPO KWA WANANCHI

TCRA KANDA YA KASKAZINI YAFANYA MKUTANO NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha.

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA )Kanda ya kaskazini wamefanya mkutano kwa wamiliki wa vyombo vya habari,watangazaji,wahariri katika mkoa wa Arusha lengo likiwa ni kuwapa elimu waaandishi ya habari kutumia kalamu zao kuandika taarifa zenye usawa na haki katika jamii bila kuweka upendeleo wowote hususani katika kipindi cha uchaguzi 

Valerie Msoka ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui(TCRA) akizungumza na waandishi habari wa vyombo vya habari tofauti katika mkoa wa arusha amesema lengo la mkutano huo wa waandishi ni kutoa elimu ya kuandika taarifa zenye usawa na haki katika jamii pamoja na kujadili changamoto zinazo ikumba tasnia ya habari mkoani arusha 

Mwenyekiti huyo wa Maudhui (TCRA) amesema zipo changamoto nyingi zina zoikumba tasnia ya habari nchini ikiwemo wamiliki wa vyombo vya habari kuingilia ujuzi wa waandishi wa habari kwa lazimisha kufanya jambo kinyume na sheria za vyombo vya habari

Anasema ”Licha ya changamoto nyingi ambazo waandishi wa habari wanazopitia lakini moja ya changamoto kubwa sana ambazo sehemu nyingi tulizo pitia waandishi wa habari wanadai wamili wa vyombo vya habari kuwaingilia katika majukumu yao jambo ambalo lina wafanya kuandisha habari zilizo egemea sehemu moja”Alisema .

Vile vile Kaimu mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano kanda ya Kaskazini Imelda Salum amesema Mamlaka imeweka mikakati mingi ya kuboresha Tasnia ya habari kanda ya kaskazini na moja ya mikakatin ilio weka na mamlaka iyo ni kuwapa elimu waandishi wa habari ili kuandika taarifa zenye usawa na ukweli huku akiwataka waandiishi wa habari wasinyamaze pindi watakapoona na kusikia taarifa zozote za upotoshwaji.

Nao washiriki waliohudhulia mkutano huo wameishukuru mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini kwa kuwapa elimu hio kwani imewapa uelewa wa mambo mengi huku wakiomba mamlaka hio kuboresha njia za upatikanaji wa habari kwa njia rahisi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui mamlaka ya mawasiliano TCRA Valerie Msoka akizungumza na washiriki ambao ni waandshi ya habari juu ya kutoa taarifa zenye weledi na usawa kwa jamiii
Afisa Mawasiliano Makao Makuu TCRA Rolf Kibanja akitoa elimu kwa washiriki walio hudhuria mkutano huo katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Arusha mkoani Arusha. 
Pichani ikionyeshaa washiriki waliohudhulia mkutano wakinakili kinacho fundishwaa na bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Latest Images