Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

KAGERA KUTOA FURSA NA MCHANGO MKUBWA KWA UCHUMI WA TANZANIA


Chadema yameguka Dodoma, Kada mwingine ajiunga CCM

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimeendelea kupoteza viongozi wake, baada ya Aliyekua Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava Mkoani Dodoma kupitia tiketi ya Chama hicho, Sokoine Mndewa kujiuzulu nafasi zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Sokoine amefikia hatua hiyo ya kujiuzulu kutokana na kile alichoeleza kwamba Ni kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wa Chadema pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk John Magufuli.

Kada huyo wa Chadema amejiunga rasmi na CCM mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Wilaya ya Chamwino, Sostenes Tumbo, Gavana wa Tarafa ya Itiso, Remidius Mwema pamoja na ambao walimkaribisha na kumuahidi ushirikiano katika kuwatumikia wananchi.

" Niseme ukweli ninaomba mnipokee Mimi nimezaliwa katika familia ya CCM hivyo ni kama mtoto amerejea nyumbani, sioni haja ya kuendelea kuwa mpinzani ilihali Rais Magufuli anatekeleza yale yote ambayo wapinzani tumekua tukiyapigia kelele kwa muda mrefu.

" Kama ni miundombinu anajenga, elimu ameboresha tena haina malipo, vituo vya Afya vinajengwa Nchi nzima Mimi ni nani niendelee kupinga mambo mazuri kama haya? Hivyo kuanzia leo ninajiuzulu nafasi zangu zote ndani ya Chadema na ninaomba CCM ikiwapendeza mnipokee," amesema Sokoine.

Nae Gavana Remidius amempongeza Sokoine kwa uamuzi huo wa kujiunga na CCM kwani anaamini kutaongeza kasi ya kuwatumikia wananchi wa Tarafa ya Itiso na kutekeleza ilani ya CCM.

" Tunafahamu utendaji kazi wako, wewe ni kiongozi kijana ambaye wananchi walikuamini, CCM ina taratibu zake hivyo naombeni wana-CCM mumpokee kijana wetu bila maneno maneno, tumpe ushirikiano ili kweli ajione yupo kwenye Chama ambacho kinaongoza Nchi," amesema Katibu Muenezi wa CCM, Sostenes Tumbo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava Mkoani Dodoma kupitia tiketi ya Chama hicho, Sokoine Mndewa kujiuzulu nafasi zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM),akikabidhi kadi yake kwa Mwenyekiti wa CCM Kata ya Segala Bw.Benjamin Sadala. 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava Mkoani Dodoma kupitia tiketi ya Chama hicho, Sokoine Mndewa kujiuzulu nafasi zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM),akizungumza na wananchama wa CCM (hawapo pichani) mara baada ya kuhamia chama hicho.
Sehemu ya wanachama wa CCM wakimsikiliza aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Izava Mkoani Dodoma kupitia tiketi ya Chama hicho, Sokoine Mndewa kujiuzulu nafasi zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) akizungumza mara baada ya kuhamia CCM (hayupo pichani).

Kamati ya maudhui ya TCRA yafanya ziara Arusha

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Mhe. Richard Kwitega (Katikati) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, pamoja na Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini waliomtembelea ofisini kwake, jijini Arusha leo. 

Wajumbe hao wako katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya utangazaji vya Kanda ya Kaskazini ili kutoa elimu ya uandaaji na usimamiaji wa maudhui bora ya uchaguzi nchini. Maudhui ya Vyombo vya utangazaji ni muhimu katika kuhimiza amani na utulivu wakati wote wa kipindi cha uchaguzi. Tanzania inatazamia kufanya chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

WAZIRI MBARAWA AANZA KWA KASI UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS

$
0
0
Muonekano wa Mto Kagera kutokea eneo linalopendekezwa kujengwa tenki la maji Kyaka. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga mara baada ya kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa tenki la maji.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kyaka (hawapo pichani) ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.
Baadhi ya wananchi wa Kyaka wakimsikiliza Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani).
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo ya utekelezaji wa mradi wa maji Kyaka kwa wataalam alipotembelea aneo linalopendekezwa kujengwa tenki la maji. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga. 

**************** 

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amewahakikishia wananchi wa Kyaka, Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera kupata huduma ya majisafi na salama kutoka Mto Kagera ifikapo Desemba, 2019. 

Kauli hiyo aliitoa Julai 12, 2019 wakati wa ziara yake Wilayani humo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Julai 11, 2019. 

Akiwa njiani akitokea Wilayani Karagwe kuelekea Wilayani Chato, Rais Magufuli alisimama katika Mji Mdogo wa Kyaka kusalimiana na wananchi na walimueleza kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama. 

Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Waziri Mbarawa kwa njia ya simu mbele ya wananchi hao kufika eneo hilo siku iliyofuata kuzungumza nao na kuhakikisha kero hiyo inatatuliwa na ikifika kipindi cha Sikukuu ya Krismasi mwaka huu wananchi hao wawe wamepata huduma ya majisafi na salama. 

Katika utekelezaji wa agizo hilo, Waziri Mbarawa akiwa ameongozana na Watendaji na Wataalam kutoka Mamlaka za Maji Mwanza (MWAUWASA) na Bukoba (BUWASA) alisisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaondolea wananchi wake kero ya maji na aliwahakikishia wananchi wa Kyaka kwamba kero ya maji inakwenda kuwa historia. 

Profesa Mbarawa alisema Mkandarasi mahiri atapewa jukumu hilo la kujenga mradi wa maji na aliwasihi wananchi hao wa Kyaka kutakapojengwa chanzo cha maji kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi atakayetekeleza mradi ili ukamilike kwa wakati na kwa kiwango. 

“Tumesema sasa imetosha wananchi kuhangaika, tunawahakikishia wananchi wote wa Kyaka kuwa mtapata majisafi na salama kutoka Mto Kagera, tunajenga mradi mkubwa wa maji ambao pia ni endelevu,” alisema Waziri Mbarawa. 

Waziri Mbarawa aliamuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga kushirikiana na Mkurugenzi wa Maji Bukoba, Allen Marwa na wataalam wengine kutoka Wizara ya Maji kusimamia na kuratibu haraka shughuli za awali za ujenzi wa mradi. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Sanga alielezea walivyojipanga kwenye maandalizi ya awali ya ujenzi wa mradi. Mhandisi Sanga alibainisha kwamba shughuli za awali za utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na kumpata Mkandarasi wa ujenzi zitakamilika ndani ya muda mfupi ili kazi za ujenzi ziweze kukamilika katika muda ulioelekezwa na Rais Dkt. Magufuli. 

“Ili kukamilisha ujenzi wa mradi katika kipindi kilichoagizwa na Mhe. Rais inatakiwa taratibu za awali zifanyike kwa muda mfupi kadri iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kumpata mkandarasi atakaye jenga mradi,” aliongeza Mhandisi Sanga. 

Kukamilika kwa mradi huo kutanufaisha wananchi wa maeneo ya Kyaka, Bunazi na maeneo mengine ya Mutukula, Kakunyu na Bubale.

Shirika la KIVULINI lakabidhi vyeti na kompyuta kwa viongozi wachapakazi

$
0
0
Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza
Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI limekabidhi vyeti na kompyuta mpakato 11 zenye thamani ya shilingi milioni 13.2 (Tsh. 13,200,000) kwa viongozi mbalimbali wanaoshiriki vema kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na Halmashauri ya Wilaya Misungwi.


Akizungumza jana Julai 12, 2019 kwenye zoezi la kukabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema hatua ni sehemu ya kutambua utendaji kazi bora wa viongozi hao ambao wamesaidia utekelezaji kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi.


Aidha Yassin alibainisha kwamba kupitia juhudi za viongozi hao, kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi pia kimeongezeka katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019 katika shule mbili za mfano ambazo ni Shule ya Wasichana Bwiru pamoja na Misungwi Sekondari.


Naye mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula aliyekuwa mgeni rasmi, alikemea baadhi ya wanaume wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike na kutoa rai kwa shirika la KIVULINI kuendelea kusaidia utoaji elimu hadi ngazi ya jamii ili kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.


Viongozi waliopata vyeti na kompyuta mpakato (Laptops) ni mbunge jimbo la Ilemela, Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Afisa Elimu Sekondari Ilemela, Mkuu wa Shule ya Wasichana Bwiru.


Wengine ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Afisa Elimu Sekondari Misungwi, Afisa Maendeleo ya Jamii Misungwi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Misungwi pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Chato.

 Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akizungumza baada ya zoezi la kukabidhi kompyuta mpakazo kwa viongozi mbalimbali Ilemela na Misungwi.
 Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akikabidhi cheti kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kulia).
  Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kulia).
  Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) kwa Afisa Elimu Sekondari wilayani Misungwi, Mwl. Diana Kuboja (kushoto).
  Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Misungwi.
Jedwali likionesha kiwango cha ufaulu kilivyopanda katika Shule ya Wasichana Bwiru wilayani Ilemela pamoja na Misungwi Sekondari wilayani Misungwi kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka huu 2019.
 Wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
 Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Tazama Video hapa chini

SPIKA NDUGAI APOKEA WAJUMBE WA MABUNGE JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA ZIARA YA KIKAZI JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiongozana na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi baada ya kumpokea leo katika uwanja wa ndege wa Jijini Dodoma. Spika Muturi pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, wageni wengine ni wajumbe wa jumuiya hiyo. 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi katika Ofisi za uwanja wa ndege leo Jijini Dodoma. Kushoto ni katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai. 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati), Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi (kulia kwa Spika Ndugai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Ndg. Godwin Kunambi wakimsikiliza Mchumi, Mratibu wa dawati la uwekezaji halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ndg. Abeid Msangi wakati walipotembelea eneo lao (Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika) 
pika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wanne kushoto), Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi (wa tatu kushoto) ambae pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika,wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mabunge Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Katibu wa Bunge la Tanzania na Katibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, Ndg. Stephen Kagaigai 

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati), Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi (kulia) ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika wakiingia katika ukumbi wa Bunge la Tanzania wakati wa ziara yao walipotembelea Bunge hilo leo Jijini Dodoma. Wageni wengine ni wajumbe wa Mabunge Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika. 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Spika wa Bunge la Kenya, Mhe. Justin Muturi katika uwanja wa ndege Jijini Dodoma. Spika Muturi ni Mwenyekiti wa kamati tendaji ya Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika amabe aliongoza ujumbe wa jumuiya hiyo katika ziara ya kikazi ya siku moja Jijini Dodoma.

CGP PHAUSTINE KASIKE AKAGUA SHAMBA LA MIFUGO GEREZA RUSUMO, AWATAKA KUONGEZA UZALISHAJI WA MIFUGO

$
0
0

Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (wa tatu toka kulia)
akimsikiliza Mkuu wa Gereza Rusumo, Mrakibu wa Msaidizi wa Magereza,Jackson Murya alipofanya ukaguzi wa shamba la mifugo katika gereza hilo. Kamishna Jenerali Kasike jana Julai 12, 2019 amewataka Wakuu wote wa Magereza yenye mashamba yenye mifugo nchini kuongeza uzalishaji wa mifugo.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike( wa pili toka kushoto) akitoa maelekezo kwa Watendaji wote katika Gereza la Mifugo Rusumo alipotembelea katika ziara yake ya kikazi jana Julai 12, 2019.
Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Ngara, Mrakibu wa Magereza, Phaustine Makonge (kushoto) akitoa taarifa ya utendaji ya Gereza kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike alipowasili Gerezani hapo jana Julai 12, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa na Askari wa Gereza la Mifugo la Rusumo jana Julai 12, 2019. Wa pili toka kulia aliyeketi ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Raymond Mwampashe(Picha zote na Jeshi la Magereza).

DKT BASHIRU AMFAGILIA OLE MILLYA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya alipowasili kwenye ziara yake ya siku mbili. 
Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa mashina, matawi, kata na wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara Simon Lulu na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia mkoa wa Manyara, Joachim Leonce. 
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akizungumza Mji mdogo wa Orkesumet juu ya maendeleo mbalimbali yaliyofanywa na serikali ya awamu ya tano. 

************


KATIBU Mkuu wa CCM, Dkt Bashiru Ally amepongeza Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya kuwa ni mbunge mahiri, makini na mchapakazi ndiyo sababu wakakubali kumpokea CCM kwani waliwakataa wabunge watatu wa vyama vya upinzani waliiomba kujiunga na CCM baada ya kubaini kuwa hawawezi kukidhi vigezo vya kuwa wabunge wa chama hicho. 

Dk Bashiru akizungumza Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro kwenye ziara yake ya siku mbili Mkoani Manyara alisema Ole Millya ni miongoni mwa wabunge 10 mahiri waliokuwa upinzani wakakubaliwa kujiunga na CCM. 

Alisema kwenye mkoa wa Manyara waliwapokea viongozi wawili wa upinzani Ole Millya na Pauline Gekul wa jimbo la Babati Mjini ambaye alikuwa mwanafunzi wake chuo kikuu. Alisema CCM siyo chama cha kuchukua kila mtu ndiyo sababu wamewakataa hao ambao hakuwataja majina kwani wangewakubali kuwapokea wote upinzani ungemalizika. 

“Tumewakataa wabunge hao watatu waliotaka kuja kwetu kwani CCM siyo jalala kwani mtu aliyekata tamaa anaweza kujiumiza mwenyewe au kuumiza wenzake,” alisema Bashiru. Alisema siyo kweli kuwa wanafungua milango na kuchukua kila mtu kwani chama hicho cha CCM kina dhamira ya dhati na majukumu ya kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi. 

Akizungumza kwenye kikao hicho Ole Millya alisema miradi mingi ya maendeleo iliyofanyika Wilayani Simanjiro kupitia Rais John Magufuli ndiyo sababu yeye akajiuzulu Chadema na kujiunga na CCM. 

Ole Millya alisema hivi sasa hospitali ya Wilaya inajengwa, mradi mkubwa wa maji wa mto Ruvu, barabara ya lami itajengwa kutoka Arusha hadi Kongwa Mkoani Dodoma kupitia Simanjiro na Kiteto na ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani. 

Katika kikao hicho katibu mwenezi wa Chadema Wilayani Simanjiro na aliyegombea udiwani kata ya Orkesumet mwaka 2015, Zephania Kituyo alirudisha kadi ya Chadema na kujiunga CCM. 

Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Manyara, Simon Lulu alisema hivi sasa majimbo yote saba ya mkoa huo yanaongozwa na wabunge wa CCM na Halmashauri zote saba zinaongozwa na wenyeviti kupitia CCM. 

Katibu wa CCM wa wilaya ya Simanjiro Ally Kidunda alisema wamejipanga kuhakikisha mbunge na madiwani wa CCM wanafanya mikutano na wananchi na kuwasikiliza kero zao na kuzungumza nao.

UTALII WA SOKWEMTU KUANZISHWA KATIKA HIFADHI YA TAIFA RUMANYIKA NA IBANDA MKOANI KAGERA.

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi, M. B. Moronda mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa Ibanda wilayani Kyerwa katika mwambao wa mto Kagera mpakani mwa Tanzania na Uganda. Katikati ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi , Martin Loibooki. 

Wahifadhi wakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu wilayani Karagwe wakati wa ziara ya Kikazi ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla katika hifadhi hiyo. 


Na. Aron Msigwa – WMU 

Serikali imesema itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu iliyoko wilayani Karagwe na Ibanda iliyoko Kyerwa, mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa kauli hiyo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 

Dkt. Kigwangalla amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam zinaonesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.

Amesema mpango huo hautahusisha upandikizaji wa wanyamapori

TANZIA

$
0
0
Kwa wanaomfahamu Mahad Nur Gurguurte taarifa ni kwamba kafariki dunia jana katika shambulio la kigaidi  la Al-Shabaab katika hoteli moja mjini Kismayu huko Somalia.

Marehemu Mahdi atakumbukwa zaidi kwa biashara za hoteli nchini, ikiwemo ya Paradise Beach ya Bagamoyo kabla ya kuungua, TANSOMA, kiwanda cha uniform na viatu vya viwandani  na Supermarket kadhaa.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un (إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ‎) Mola na aiweke Roho yake mahala pema peponi - AMIN

NCHI ZA SADC ZABEBA MATUMAINI MAKUBWA KWA RAIS MAGUFULI,KUKABIDHIWA UENYEKITI AGOSTI MWAKA HUU.

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Morogoro 

WAKATI Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli, akitarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa nchi 16 zilizopo kwenye Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wachambuzi wabobezi kuhusu jumuiya hiyo wamesema, wakuu wa nchi hizo na serikali zao wana matumaini makubwa na Rais Magufuli.

Hii ni kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwa Tanzania ndani ya muda mfupi, hadi kuonekana ni nchi mfano katika sekta mtambuka za maendeleo.

Aidha, matumaini makubwa yapo kwenye usimamizi wa rasilimali za Afrika ili kumudu kujitawala kiuchumi na kiuongozi dhidi ya mataifa yanayoendelea au nchi wahisani.Hayo, yameelezwa kwenye semina ya siku tatu ya waandishi wa habari inayoendelea mkoani Morogoro kwa awamu ya pili, ambapo watoa mada ni wabobezi katika masuala ya mtangamano wa jumuiya mbalimbali zilizoundwa barani Afrika.

Semina hiyo, inayolenga kuwapa mwanga wanahabari kuhusiana na masuala ya SADC, ikiwa ni mkakati wa kuwaandaa kuelekea mkutano mkubwa wa jumuiya hiyo utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Mtoa mada kwenye semina hiyo Katibu Mkuu mstaafu Mussa Uledi alisema, katika mkutano huo wa SADC pamoja na mambo mengine nchi ya Tanzania itaingia kwenye historia kwani mkutano huo utatumika kumkabidhi kijiti Rais Dk. Magufuli cha kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

"Nchi za zilizomo kwenye SADC kwanza zinatambua nafasi ya Tanzania kwenye jumuiya hiyo na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika."Ukweli uliopo Rais Dk. Magufuli atakabidhiwa Uenyekiti wa SADC na tunafahamu miongoni mwa malengo ya jumuiya hiyo ni kuimarisha uchumi wa nchi hizo na Bara la Afrika kupitia uchumi wa viwanda."

Amesema, katika eneo la viwanda nchi mbalimbali za Afrika zimeona namna ambavyo Rais Magufuli amesimama imara kuhakikisha ujenzi wa viwanda nchini Tanzania unafanyika, na hivyo ukitazama kwa kina utabaini kuwa nchi za SADC zina matumaini makubwa na Rais Magufuli.

"Maono ya jumuiya hiyo yanakwenda sambamba kabisa na maono ya ya Rais wetu ambaye amesimama imara kuimarisha uchumi wa nchi yetu ya Tanzania na mpango wake ni kuona Tanzania inafikia uchumi wa kati kupitia viwanda," alisema.

Amesema, kikubwa kinachosubiriwa kwa Rais Magufuli ni mtindo wake wa uongozi na kusimamia mambo yakamilike kwa wakati badala ya kuendeleza utamaduni wa kuzungumza na kuacha mambo kwenye nyaraka.

kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayoub Rioba wakati akiwasilisha mada yake alisema anashangaa wanahabari hawaandiki ipasavyo namna Rais Magufuli alivyofanya mambo makubwa ndani ya muda mfupi wa uongozi wake.

Ameongeza kuwa haijawahi kutokea hata kwa kiongozi wa kiafrika kujipambanua kama mtu asiyeshidwa na kuaminisha wananchi kuwa Afrika si masikini."Zaidi ya mara moja Rais Magufuli alishasema Tanzania si nchi masikini, kwa pamoja tunaweza kuwa nchi watoa misaada badala ya kuendelea kupokea misaada kutoka nchi zilizoendelea," alisema Dk. Rioba na kuongeza:

"Kuna mambo makubwa katika sekta ya madini, afya, miundombinu na bandari bila kusahau usafirishaji. Yote hii inaongeza hamu kwa nchi wanachama wa SADC, kutaka kuona maendeleo haya yanakwenda katika jumuiya hiyo."

Kingine kilichogusiwa ni namna kiongozi huyo alipogusia umuhimu wa lugha ya Kiswahili kuzungumzwa katika nchi zote za Afrika na dunia.Vilevile, katika mkutano huo wa SADC ambao unafanyika mara ya pili nchini tangu ulipofanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2003, kutakuwa na kipengele cha kujadili matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli mbalimbali za jumuiya.

Hadi sasa, tayari nchi kadhaa za kusini mwa Afrika zimeomba kupelekewa walimu na vifaa vya kufundishia lugha ya Kiswahili ikiwemo Zimbabwe, Afrika Kusini na Namibia.
Mjumbe wa Kamati ya Habari,machapisho na utangazaji wa Kamati Kuu ya maandalizi ya mkutano wa SADC Eshe Muhidin akitoa mrejesho wa mjadala wa siku ya kwanza wa semina ya waandishi wa habari kwa ajili ya kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuripoti mkutano wa SADC unaotarajia kufanyika  Agosti mwaka huu
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifutilia Mafunzo yanayohusu kuandika habari  zenye weledi katika mkutano wa SADC unaotarajia kufanyika Agosti mwaka huu
 Mwandishi Hafidh Kido akifuatilia mjadala katika semina ya waandishi wa habari inayoendelea mkoani Morogoro ambayo inayohusu kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu mkutano wa SADC
 Mjumbe wa Kamati ya Habari ,machapisho na utangazaji wa Kamati kuu ya maandalizi ya mkutano wa SADC Nelly Mtema akifuatilia mjadala wa semina ya kuwajengea uwezo wandishi wa habari katika kuandika habari zinazohusu mkutano wa SADC
 Do.Kanael Kaale ambaye ni moja ya wanafunzi(katikati) katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini Tanzania ikiwa ni maandalizi ya kuelekea mkutano wa SADC
 Mshiriki wa semina ya waandishi wa habari inayolenga kuwajengea uwezo wa kuandika habari za SADC ,Abdallah Majura akisikiliza mada kutoka kwa watoa mada(hayupo pichani) .Semina hiyo inafanyika mkoani Morogoro
 Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zamarad Kawawa akijadiliana jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mkutano wa SADC unaotarajia kufanyika Agosti mwaka nchini Tanzania
 Sehemu ya washiriki wa semina  inayohusu kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini ili kuwawezesha kuandika habari za mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini barani Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti mwaka huu

KLABU YA GOLFU YA VICTORIA YAIKABIDHI SERIKALI ENEO ILILOKUWA IKILIMIKI PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia eneo la pembezoni mwa ziwa Victoria wilayani Magu mkoani Mwanza lenye ukubwa wa ekari 94.1 lililorejeshwa serikalini na Klabu ya Gofu ya Victoria, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt Josephat Sengati. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika eneo la pembezoni mwa ziwa Victoria wilayani Magu mkoani Mwanza ambapo Klabu ya Gofu ya Victoria imelirejesha Serikalini . Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt Josephat Sengati na wa pili kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Biswalo Misuse. 
Mkuu wa Idara ya Ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Magu Wilfred Mkono (Wa pili kulia) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kukagua eneo lenye ukubwa wa ekari 94.1 lililoko pembezoni mwa ziwa Victoria wilayani Magu ambalo limerejeshwa Serikalini. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI) 

********* 

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA 

Klabu ya Golfu ya Victoria (Victoria Golfu Club) imetoa eneo lenye ukubwa wa ekari 94.1 liliko pembezoni mwa Ziwa Victoria wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza kwa Serikali ikiwa ni kuunga mkoni jitihada za serikali ya awamu ya tano katika suala la uwekezaji. 

Eneo hilo ambalo halmashauri ya wilaya ya Magu ililitengea matumizi ya ujenzi wa nyumba za makazi, Hoteli pamoja na matumizi mengine lina jumla ya viwanja saba vilivyokuwa vikimilikiwa na klabu ya Golfu ya Victoria. 

Akizungumza wilayani Magu mkoa wa Mwanza jana alipotembelea eneo hilo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliishukuru Klabu ya Golfu ya Victoria kupitia Wakurugenzi wake kwa uamuzi wa kukubali kulitoa eneo hilo ambapo aliuelezea uamuzi huo kuwa ni wa kizalendo kwa nchi ya Tanzania. 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, eneo hilo la pembezoni mwa Ziwa Victoria linafaa sana kwa shughuli za uwekezaji na sasa litakuwa ni mali ya serikali baada ya wamiliki wake kukubalia kuikabidhi serikali na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi itakuwa na jukumu la kulipangia matumizi. 

Akiwa ameambatana na KatibuMkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika, Naibu Waziri Mabula alionya juu ya uvamizi au udanganiyifu wowote unaoweza kufanywa na wananchi wasiokuwa waaminifu na kusisitiza kuwa eneo hilo kwa sasa litakuwa chini ya Wiazara ya Ardhi mpaka hapo litakapopangiwa taratibu nyingine. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt Phelemon Sengati alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula kuwa wilaya yake itahakikisha eneo lililokabidhiwa linalindwa na hakuna mwananchi atakayeruhusiwa kufanya shughuli yoyote hadi hapo serikali itakapokuja na maamuzi juu ya eneo hilo. 

Dkt Sengati ameomba eneo hilo kupatiwa muwekezaji atakayekuwa na uwezo kwa kuwa ni eneo zuri na linaweza kuifanya wilaya ya Magu mkoani Mwanza kubadilika kwa kiwango kikubwa. 

Mkuu wa Idara ya Ardhi katika Halmashauri ya wilaya ya Magu Wlfred Mkono alisema eneo hilo lenye viwanja saba vyenye hati ya umiliki ardhi ya miaka 99 limerudishwa serikalini tangu April 25, 2019 na ofisi yake ilikuwa mstari wa mbele kuhakikisha eneo hilo linakuwa katika mikono salama.

Serikali kuwasilisha orodha ya tozo zote zilizofutwa

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

SERIKALI itawasilisha orodha ya tozo zote 49 zilizofutwa ambazo zilikuwa ni kero kwa wajasriamali na wafanyabiashara ili waweze kuzielewa na hivyo kulipa kodi bila ucheleweshaji..

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Viwanda na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya shughuli za kibiashara kutoka SIDO pamoja na mkopo kwenye Viwanja vya Sido mkoa wa Arusha .

Waziri,Manyanya,amesema serikali kwenye kikao kilichofanya na wafanyabiashara Ikulu jijini Dar es Salaam,hivi karibuni ilifuta utitiri wa tozo zilizokuwa zikilalamikiwa na hivyo kuwapunguzia mzigo wafanyabiashara na wajasiriamali nchini

Amesema kuwa hivi sasa serikali ipo katika ujenzi wa Viwanda na hivi karibuni alikutana na Waziri wa Uholanzi lengo ni kuwajengea mazingira ya uwezeshaji wafanyabiashara nchini waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi na anatarajia kuona kila mmoja anashiriki .

Waziri Manyanya,amesema Sido imepiga hatua katika teknolojia na jukumu lililopo sasa ni kuendelea kuhamasisha na kuwaomba wajasriamali wazidishe ubunifu ,wazalishe bidhaa zenye ubora zaidi, watumie mitandao kutafuta masoko .

Amewasisitiza wajasriama na wafanyabiashara kutumia lugha za zinazoeleweka za Kiswahili kwa ajili ya soko la ndani na kiingereza kwa ajili ya soko la nje ili kumuwezesha mlaji kuelewa aina ya bidhaa anazotumia.

Amesema wizara imejipanga katika kanda saba kwa ajili ya kuwasikiliza wadau na anatembelea nchi nzima ili kuzungumza nao na kwa kuanza ameanzia Arusha na ameenda Manyara .

Awali Meneja wa Sido mkoa wa Arusha Nina Nchimbi, amesema hivi sasa SIDO inaanza kuwafundisha wajasriama elimu ya haki miliki kwa ajili ya kulinda biashara zao kwani wengi wao hawana elimu hiyo.

Kuhusu Vifungashio vya bidhaa za wajasiriamali Nchimbi,amesema hilo ni tatizo hivyo akakiomba kiwanda cha Kioo Limited cha Dar es Salaam kuzalisha vifungashio vingi ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani.

Ameongeza kuwa Sido katika kazi zake imekuwa ikishirikiana na taasisi zingine za serikali zikiwemo TRA, TMDA, katika kutoa elimu ili kuwaondolea wananchi usumbufu lakini kuna baadhi ya watumishi wa tasisi hizo wanalalamikiwa .

Wakichangia kwenye kikao hicho Wadau hao wameilalamikia ofisi ya mkemia mkuu kuwa ina urasimi hivyo kuwa ni kikwazo katika shughuli zao

Taasisi nyingine iliyolalamikiwa ni pamoja na Mamlaka ya mapato mkoa wa Arusha kuwa kuna baadhi ya watendaji wake ni kikwazo,ambapo kuna kulindana na hivyo kusababisha wajasriamali 67 waliopatiwa mafunzo na SIDO kushindwa kuanzisha Viwanda.

Aidha wameiomba serikali kuongeza fungu kwenye mfuko wa SIDO ili waweze kupata mikopo mikubwa ya fedha badala ya sasa ambapo kikomo cha mikopo inaotolewa na SIdo ni shilingi milioni tano tu.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, alipokuwa akizungumza na wamiliki wa Viwanda na wajasiriamali waliopatiwa mafunzo ya shughuli za kibiashara kutoka SIDO .
 Meneja wa shirika la Sido mkoa wa Arusha,Nina Nchimbi akizungumza katika mkutano huo wa wajasiriamali

SERIKALI KUPELEKA MIRADI YA MAJI MIJI 28 TANZANIA YENYE ZAIDI YA SHILINGI TRIONI 1.2

$
0
0

Anaadika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Karagwe.

Serikali kupitia Wizara ya Maji  ipo mbioni kuanza kujenga miradi ya Maji katika Miji 28 Nchini Tanzania ukiwemo Mji wa Kayanga ambapo Waziri mwenye dhamana Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali imekwisha chukua mkopo nafuu kutoka  Serikali ya India  Shilingi Trioni 1.2 na zabuni ya mradi huo mkubwa itatangazwa Septemba,  na kukamilika kwa Mradi  huo kutatatua kero ya Maji ndani ya Miji ya Kayanga na Omurushaka zaidi ya 100%.

Waziri Mbarawa kabla ya kuelekea Missenyi akitokea Muleba amezindua mradi wa Maji na wenye gharama sh.   Na mradi huo unafanya kazi huku akifurahishwa na Kamati ya Mradi huo kukusanya kiasi cha shilingi Milioni sita mpaka sasa yakiwa ni mauzo ya Maji.

Akiwa Wilayani Karagwe Waziri ametembelea chanzo cha Maji cha Kayanga  ambacho ni Mradi unaosimamiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Bukoba (BUWASA), wenye gharama ya Shilingi Bilioni 1.8 ukiwa  umekamilika kwa 75@%  huku BUWASA wakiahidi kufikia Mwezi Oktoba utakuwa umekamilika 100%.

Katika hatua nyingine Waziri wa Maji Profesa Mbarawa ameagiza kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Karagwe kuwakamata watu watatu wanaosemekana kuwa ni Viongozi wa kamati ya Maji ya Mradi wa Maji Chabuhora Kata Bushangaro, kwa kuhujumu mradi huo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kushindwa kukusanya pesa ya mauzo ya Maji katika mradi huo.Waziri Mbarawa tayari  kamaliza ziara hiyo katika Wilaya ya Missenyi na Karagwe na sasa yupo Kyerwa.
Waziri Mbarawa akijiridhisha katika moja ya DP 23 za mradi wa Maji wa Chabuhora ambapo alielezwa kuwa hazitoi maji.
Mradi wa Maji unaotumia teknolojia ya Polyglue kama unavyoonekana pichani, eneo la Kyaka Darajani Wilayani Missenyi

Mradi wa Maji wa Chabuhora Wilayani Karagwe ambao makusanyo yake hayajulikani na kupelekea Waziri Mbarawa kuagiza wahusika kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi.
Pichani Waziri Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam akiwa katika Mradi wa Maji Kayanga unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji Bukoba (BUWASA) Mara baada ya Kuwasili Wilayani Karagwe.
Pichani Waziri Mbarawa akikagua mradi wa Maji unaotumia teknolojia ya Polyglue ambapo Maji kutoka Mto Kagera huwekewa mbegu za Maharagwe ili kusaidia kuondoa mchanga na vumbi, Wilayani Missenyi chini ya ufadhili wa Shirika la JICA la Nchini Japan.
Pichani ni wakazi wa Kishao Wilayani Karagwe wakiendelea kufurahia huduma ya Mradi wa Maji licha ya Kukamilia asilimia 75, kama walivyokutwa na kamera yetu.
Waziri Mbarawa akiimba pamoja na Wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya CCM Wilaya ya Missenyi, alipopita kuwasalimia akiwa Ziarani Missenyi.

MWENYEKITI MPYA UVCCM ARUSHA AHAIDI KUVUNJA MAKUNDI YOTE YALIOPO NDANI YA UMOJA HUO

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha 

Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Omary Lumato,amesema kuwa kipaumbele chake ambacho amekipanga kuanza nacho katika kipindi cha uongozi wake kuyafuta makundi yote yaliopo ndani ya umoja huo pamoja na chama hicho ndani ya mkoa wa huo na atanje ili kuwafanya wanaccm wote kuwa wamoja.

Aliyabainisha hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa CCM mkoa uliopo jijini hapa mara baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo ya umwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kupata kura 221,huku mgombea wa pili ambaye ni Suleman Msuya akipata kura 199 na mgombea wa tatu akiambulia kura 7 huku vijana ambao ni wajumbe waliojitokeza kushiriki zoezi hilo wakiwa 447 .

Aidha akiongea mara baada ya kutangazwa alisema kazi ya kwanza atakayofanya ni kuvunja makundi yote yaliopo ndani ya chama hicho ,ili kufanya wanachama wote kuwa wamoja na alibainisha kuwa anaamini wakiwa wamoja majimbo yote ya Arusha ambayo yanaongozwa na upinzani yatarudi kumilikiwa na chama cha mapinduzi na sio kurudishwa tu CCM bali Arusha itakuwa ngome ya chama hicho.

"nashukuruni sana kwa kunichagua na kuanzia sasa natangaza rasmi nimevunja makundi yote ,namimi ni kiongozi wa vijana wote na sio wa kundi lolote,nanyie vijana napenda kuwaambia ili tumiliki aya majimbo yote pamoja Arusha tumechukua sehemu mbalimbali ukiangalia kata nyingi zimerudi ccm kwani madiwani wao wamejiuzuru na kurudi chama tawala na kurudi huku kwa hawa ni salamu tosha kwa wapinzani kuwa hawana kitu hapa "alisema Omary 

Alibainisha kuwa tabia ya makundi inatakiwa kpigwe vita vikali na iachwe mara moja ili ushinde wa uchaguzi zijazo kuanzia serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ushindi uwe wa CCM huku akibainisha kuwa mtu ambaye anaendekeza na kuendelea kuwa na makundi huyo atakuwa msaliti wa chama hicho na hafai kuwa kiongozi wala mwanachama wa chama hicho.

Kwa upande msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mbunge wa Mtera pia ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM Livingstone Lusinde alisema kuwa wanawapongeza sana vijana wamefanya uchaguzi kwa amani pia alisema anawapongeza sana wagombea kwani wakati kila mgombea mmoja alipokuwa anajinadi alikuwa anaongelea kuvunja makundi hivyo anawapongeza zaidi kwani vijana wa Arusha wamejifunza na wamejua ni kitu gani kilichokuwa kinafanya majimbo kupotea na kwenda kwa wapinzani .

"nawapongeza vijana wa Arusha kwakuwa vijana wamejitambua na wamejua hatukua tunashidwa uchaguzi wowote bali makundi ndio yanawamaliza na wameahidi kuvunja makundi yao ,naunajua amna uchaguzi bila makundi bali makundi hayo yanatakiwa yavunjwe tu mara baada ya uchaguzi kuisha na tumeona hapa vijana wameyavunja mapema makundi hayo na wametangaza hatharani hivyo napenda sana kuwapongeza"alisema Livingstone

Amewahimiza kuhakikisha wanahamasisha Vijana na wanachama wa ccm kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwenye serikali za mitaa huku akisisitiza kuwa Vijana wanao wajibu kuhakikisha Chama cha Mapinduzi kinaibuka mshindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Lusinde, ambae ni mbunge wa jimbo la Mtera mkoani Dodoma, amewataka Umoja wa Vijana kuhakikisha wanahamasisha Vijana na wananchi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa utakao fanyika nchini kote mwaka huu

Akitoa shukrani zake kwa vijana mmoja wawagombea hao Suleman Msuya alishukuru wajumbe wa vijana hao kwa kushiriki zoezi hilo na kusema kuwa amekubaliana na matokeo na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mwenyekiti mpya alieshinda ,huku akiwasisitiza vijana kuvunja makundi ambayo wanayo ili kujenga CCM moja yenye nguvu.
Wajumbe wa UVCCM wakiwa wamembeba Mwenyekiti mpya wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi  mkoa wa Arusha Omary  Lumato mara baada ya kutangazwa mshindi .


Malkia wa Afrika Yvonne Chaka Chaka akonga nyoyo Zanzibar tamasha la ZIFF

$
0
0
Na Andrew Chale, Zanzibar,  Tanzania

Malkia wa Muziki wa Afrika, Mama Yvonne Chaka Chaka ameweza kufaya onesho maalum katika tamasha la filamu la Kimataifa  Zanzibar  (ZIFF)  ambalo kwa mwaka huu ni la 22 kwa kurejea baadhi ya nyimbo zake zilizotamba miaka ya nyuma na kukonga nyoyo kwa umati mkubwa uliojitokeza kwenye tamasha hilo.

Miongoni mwa nyimbo alizopiga Mama Yvonne Chaka Chaka ni pamoja na  ‘Motherland’, "Umqombothi" ("Pombe ya Afrika"), "I'm in Love with a DJ",  "I Cry for Freedom" na nyimbo ya Mandela.

Awali msanii huyo kabla ya kuanza kuimba kwenye jukwaa hilo la ZIFF, aliwapongeza watu wote na kueleza kuwa Duniani kote watu wote ni sawa huku akiwamwagia sifa viongozi walioletea Uhuru Afrika sambamba na viongozi wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume.

Msanii huyo alizaliwa Dobsonville huko Soweto na alikuja kuwa mototo wa kwanza wa Kiafrika kuonekana kwenye televisheni Afrika Kusini. Mwaka 1981 "Sugar Shack", kipindi cha wenye talanta, kilimjulisha kwa umma wa Afrika Kusini.

Katika harakati za muziki, Chaka Chaka alianza kuimba akiwa na miaka 19 mwaka 1985 wakati Phil Hollis wa Dephon Records alimgundua mjini Johannesburg- Muda mfupi baada ya albamu yake "I'm in Love With a DJ", kuuzwa nakala 35,000.

Pia katika nyimbo zake zilizowahi kushinda tuzo mbalimbali ni kama "Burning Up", "Sangoma", "Who's The Boss", "Motherland", "Be Proud to be African", "Thank You Mr DJ", "Back on my Feet ", " Rhythm of Life "," Who's got the Power "," Bombani (Tiko Rahini), "Power of Afrika", "Yvonne and Friends" na "Kwenzenjani".

KAMPUNI YA SKOL BUILDING AGENCY YAKUTWA IKIIBA MAJI YA DAWASA

$
0
0
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA wamemkamata mmiliki wa Kampuni  SKOL Building Agency Peter Massawe akiiba maji akijiunganishia kiholela.

Tukio hilo lililotea Jumatatu ya Julai 08, 2019 baada ya kupata taarifa ya mvujo ndipo Moja ya wafanyakazi wa DAWASA kuwasiliana na uongozi na kisha kuanza kufanya uchunguzi.

Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Biashara DAWASA mkoa wa Kawe Jimmy Chuma amesema kampuni hiyo ilikatiwa huduma ya maji toka mwezi April mwaka huu baada ya kuwa na malimbikizi ya madeni yanayofikia 109,718 kwa muda mrefu.

Chuma amesema, baada ya kufika na kuanza kuchimba na kuangalia maji yanapotokea walikuja kugundua, mmiliki huyo alijiunganishia maji kabla ha kufika kwenye mita ya DAWASA na kuendelea kuhujumu shirika.

Ameeleza, baada ya kuona hilo waliwataka wamiliki wafike ofisini kwa ajili ya kupata utaratibu wa kulipa na kutokana na mabadiliko ya sheria namba 5 ya mwaka 2019 mdaiwa atatakiwa kulipa milion 50 au kufikishwa kwenye Vyombo vya sheria.

"Baada ya kufika ofisini tulipowapa taarifa ya kuwa wanatakiwa kulipa milion 50 walisema hawana hela ya kulipa na ndipo leo tumefika hapa kuondoa kabisa miundo mbinu yetu na tayari tumeshatoa taarifa kwenye vyombo husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua,"amesema Chuma.

Tukio la uchimbaji wa kuangalia sehemu maji yanapovuja yalishuhudiwa na Mona ya viongozi wa Kampuni hiyo Brenda Massawe na mwenyekiti wa serikali ya mitaa.

DAWASA inaendelea kuwasihi wananchi wasijiunganishie maji kiholela pia watoe taarifa kwa kupiga namba ya huduma kwa wateja wanapoona mtu amejiunganishia maji kwani kufanya hivyo kunanyima mamlaka mapato ya kuwezesha kujenga miradi mipya ya maji.
Afisa Biashara, DAWASA Mkoa wa Kawe, Jimmy Jamal Chuma akionesha  akionesha sehemu ilipokuwa mita ya DAWASA  iliyoondolewa kutokana na kutolipa bili za maji lakini Kampuni  SKOL Building Agency iliendelea kutumia maji kwa njia za kughushi bomba.
Afisa Biashara, DAWASA Mkoa wa Kawe, Jimmy Jamal Chuma akionesha moja ya bomba lililowekwa na DAWASCO lilivyokuwa likiingiza maji kwenye Kampuni  SKOL Building Agency mara baada ya kufungwa na Shirika hilona kampuni hiyo kutumia mchepuko kwa kuunganisha bomba kimaghumashi.
Afisa Biashara, DAWASA Mkoa wa Kawe, Jimmy Jamal Chuma akionesha moja ya bomba la maji lililokuwa linatumika kwenye wizi wa maji wa Shirika hilo walipofanya ukaguzi wa kushtukiza kwenye  Kampuni  SKOL Building Agency  iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Moja ya Tanki lililokuwa linatumiwa na Kampuni  SKOL Building Agency kwa kusafishia maji ya DAWASA  yaliyokuwa yanibiwa na kampuni hiyo.
Mmoja wa mafunzi wa DAWASA  akikata bomba linaloingiza  maji katika ofisi ya Kampuni  SKOL Building Agency iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa DAWASA  wakiwa kazini
Sehemu ya Bomba kubwa la maji ya DAWASA  lililokuwa limekatwa na kuingiza maji kwenye ofisi za Kampuni  SKOL Building Agency  iliyopo Sinza Jijini Dar es Salaam likuwa limeishafungwa na DAWASA.

RAIS WA UGANDA MUSEVENI AWASILI CHATO MKOANI GEITA NA KUPOKEWA NA RAIS DKT. MAGUFULI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.

 Rais wa Jamhuri ya wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wakiangalia vikundi mbalimbali vya Ngoma na Kwaya mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Uganda Yoweri Museveni akizungumza na Wananchi wa Chato mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati akiwapungia mkono wananchi waliofika katika uwanja wa ndege wa Chato.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati waliupokuwa wakiwasalimia wananchi wa Njiapanda Chato mkoani Geita. 
Baadhi ya Wananchi wa Chato waliojitokeza katika mapokezi ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWASILI KIGOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa  Wanawake Tanzania  (UWT), Gaudencia Kabaka wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kigoma kufungua Kongamano la Wananwake  Kitaifa, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Julai 13, 2019. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma, Amandus Dismas  Nzamba.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma kufungua Kongamano la Wanawake (UWT) kitaifa, Julai 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI GEITA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amewaomba wananchi wa mkoa wa Geita pamoja na maeneo jirani na mkoa huo kujitokeza kwa wingi siku ya jumatatu kwenye tukio la uzinduzi wa nyumba za Amakazi ya askari, uzinduzi utakaofanyika katika eneo la magogo mkoani humo.

IGP Sirro amesema kuwa, katika tukio hilo ambalo litaongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, ambapo atazindua zaidi ya nyumba 114 zilizokwisha kamilika huku matarajio ya mradi huo ni kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima. 

Aidha, IGP Sirro amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha askari wanaishi kwenye mazingira mazuri jambo ambalo litachangia weledi na uwajibikaji hususan kulinda maisha ya raia na mali zao.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images