Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110019 articles
Browse latest View live

ZIADI YA WAFUNGWA 640 WAMENUFAIKA NA MPANGO WA BODI YA PAROLE NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITATU

$
0
0
Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza
BODI ya Taifa ya Parole ya Awamu ya Tano imeelezea mafanikio mbalimbali katika kipindi cha miaka mitatu ambapo Bodi hiyo imewezesha kuachiliwa jumla ya wafungwa 648 katika mpango huo wa Parole na hadi sasa hakuna mfungwa yeyote aliyevunja masharti ya Parole na kurudishwa gerezani.
Hayo yamesemwa mapema leo na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Agustino Mrema katika Kikao cha 41 cha Bodi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dare es Salaam.
 “Jumla ya wafungwa 666 wamejadiliwa na Bodi ya Taifa ya Parole katika vikao vyake saba vilivyofanyika na kupendekeza kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wafungwa 648 wamenufaika na mpango huo na wafungwa 18 hawakupendekezwa kutokana na sababu mbalimbali”. Amesema Mhe. Mrema.
Amesema kuwa katika utendaji wa Bodi yake kwa miaka mitatu umechangia kuimarika kwa hali ya utulivu na usalama ndani ya magereza kwa wafungwa kwani wamekuwa na matumaini makubwa ya kuingizwa kwenye mpango huo sanjari na kupokea programu za urekebishaji katika magereza mbalimbali nchini.
Mafanikio mengine ni kuwa Wafungwa walioachiliwa katika mpango huo katika kipindi hiki wameshiriki na wanaendelea kushiriki vyema katika shughuli za maendeleo katika jamii zao ikiwemo kuziangalia na kuzihudumia familia zao; hivyo kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hao kama wangekuwepo magerezani. 
Aidha, Mhe. Mrema amezungumzia changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili Bodi hiyo ikiwemo ufinyu wa bajeti katika kufanikisha shughuli za Bodi. Changomoto zingine ni katika maeneo ya kiutawala, kisheria ambazo hata hivyo amesema hatua mbalimbali za utatuzi zinaendelea kufanyiwa kazi na mamlaka husika.
“Bodi hii ya tano imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha miaka mitatu, licha ya changamoto hizo nilizozitaja, kipekee nitoe shukrani za dhati kwa wajumbe wa Bodi kwa ushirikiano wao kwangu. Pia natoa shukrani za kipekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuniteua kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi hii katika kutekeleza matakwa ya Sheria ya Bodi za Parole Sura ya 400”. Amesema Mhe. Mrema.
Bodi ya Taifa ya Parole ya Awamu ya Tano ilizinduliwa na kuanza kufanya kazi zake Machi 21, 2019 na inatarajia kumaliza muda wake wa kuwa madarakani kwa miaka mitatu ifikapo Julai 16, 2019.
 Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama(kulia) ambaye pia ni Kaimu Katibu wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole akitoa taarifa fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema(kushoto) afungue rasmi Kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga,  Jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema akifungua kikao cha 41 cha kujadili Wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole.
 Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakifuatilia majadiliano ya wafungwa waliopendekezwa kunufaika/kutonufaika katika mpango wa Parole leo Julai 12, 2019, katika Bwalo la Maafisa Magereza, lililopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wajumbe Sekretarieti wakifuatilia kwa makini majadiliano katika kikao hicho.


Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Mhe. Augustino Mrema (meza kuu) akiongoza Kikao cha 41 cha Bodi hiyo (Picha zote na Jeshi la Magereza).

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI MKUU WA VIET NAM,AWAKARIBISHA KUWEKEZA BANDARI,USAFIRI WA ANGA NA KILIMO.

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Trinh Dinh Dung, katika mazungumzo ya faragha yaliyofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 12, 2019 
………………

*Awakaribisha Waviet Nam waje kuwekeza katika bandari, usafiri wa anga na kilimo 


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekuna na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Viet Nam, Trinh Dinh Dung na amewakaribisha wawekezaji kutoka Viet Nam waje kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo ya mipango miji, madini, bandari, usafiri wa anga, ufundi stadi, kilimo pamoja na uvuvi. 

Amesema kuwa anatambua kwamba nchi ya Viet Nam inafanya vema katika suala la mazao ya kilimo kwa kuongeza tija kwenye mazao hayo na kukifanya kilimo kuwa cha biashara, hivyo amezialika kampuni za Viet Nam zenye teknolojia mahsusi katika maeneo tajwa ili kushirikiana na Tanzania katika mikakati yake ya kuendeleza kilimo. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 12, 2019) wakati wa mkutano wake na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam , ambapo ametumia fursa hiyo kumuhakikishia kwamba Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wake na Viet Nam kwa manufaa ya watu wa nchi mbili hizo. 

Amesema uwepo wa kampuni ya Viettel PLC (Halotel) ya kutoka nchini Viet Nam ni ishara tosha ya imani ya uwekezaji iliyopo kwa wawakilishi wa Viet Nam. “Nawakaribisha sana wawekezaji kutoka Viet Nam kuja kuwekeza Tanzania kwani kwa kufanya hivyo hawatojutia uamuzi wao wa kuwekeza Tanzania.” 

Waziri Mkuu amesema Viet Nam imeendelea kuwa mshirika muhimu wa kiuchumi kwa Tanzania, hivyo ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Viet Nam kwa kuendelea kuunga mkono Serikali ya Tanzania katika jitihada za kuwaletea wananchi wake maendeleo. 

“Kwa mfano, kampuni ya mawasiliano ya Viettel PLC (maarufu kama Halotel) ambayo imewekeza nchini tangu mwaka 2014 inafanya vizuri katika sekta ya mawasiliano. Kampuni hiyo, imewezesha mawasiliano ya simu kuwafikia Watanzania wengi hususan wale waishio vijijini.” 

Waziri Mkuu amesema kampuni hiyo ya Halotel imeweza kuzalisha ajira takriban 1,600 za moja kwa moja kwa wazawa na ajira takriban 100,000 zisizokuwa za moja kwa moja hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2018; 

Amesema lengo la Serikali ya Tanzania ni kuendelea kushirikiana na Serikali ya Viet Nam katika masuala ya mawasiliano na masuala mengine ikiwemo biashara na uendelezaji na masoko ya mazao ya kilimo hususan korosho, kahawa, kilimo mseto cha mpunga na uvuvi wa samaki ambako Viet Nam inafanya vizuri zaidi. 

Akizungumzia kuhusu sekta ya utalii, Waziri Mkuu amesema Tanzania ni nchi nzuri, watu wake ni wakarimu na pia imebarikiwa vivutio vingi vya utalii. Hivyo, amezikaribisha kampuni za Viet Nam kuja kuwekeza katika sekta ya utalii na utamaduni nchini. 

“Halikadhalika, sina shaka kwamba wengi wenu mmewahi kusikia kuhusu Visiwa vya Zanzibar, Mlima Kilimanjaro, pamoja na Mbuga za Serengeti na Ngorongoro. Hivyo ni baadhi tu ya vivutio vingi vya utalii tulivyojaliwa kuwa navyo nchini mwetu.” 

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, Trinh Dinh Dung ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushgirikiano na kwamba ameomba ushirikiano huo uimarishwe kupitia ziara za viongozi wa wakuu wa nchi mbili hizo. 

Naibu Waziri Mkuu huyo wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Viet Nam, amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba Serikali ya Viet Nam itazidi kuimarisha ushirikiano wake na Serikali ya Tanzania hususani katika sekta za kilimo, biasdhara na uvuvi. 

Kadhalika kiongozi huyo amesema kuwa nchi ya Viet Nam iko tayari kununua mazao mbalimbali ya kutoka nchini Tanzania yakiwemo ya korosho na pamba. Amesema lengo la Serikali yao ni kuhakikisha kwamba biashara kati ya Tanzania na Viet Nam inafikia dola bilioni moja ifikapo 2020.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YATWAA TUZO MBILI MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA DARE SA SALAAM

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wapili kushoto), akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, tuzo ya mshindi wa pili miongoni mwa mabanda bora ya Wizara, Idara na Taasisi za serikali.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango na Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Benny Mwaipaja, akionesha moja kati ya tuzo mbili ambazo Wizara imenyakua kwenye maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango na Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Benny Mwaipaja, akionesha tuzo mbili ambazo Wizara imenyakua kwenye maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), Dar es Salaam
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja aliyeshika tuzo, (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania-TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva, muda mfupi baada ya Wizara ya Fedha na Mipango kukabidhiwa tuzo mbili za mshindi wa pili wa Banda Bora na Mfumo Bora wa Ukusanyaji Maduhuli ya Serikali (GePG)
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakifurahia tuzo mbili ambazo Wizara imepata katika Maonesho hayo.
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake, wakifurahia tuzo nne ambazo Banda la Wizara limepata katika Maonesho hayo.
Baadhi ya washiriki wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake, wakifurahia tuzo nne ambazo Banda la Wizara limepata katika Maonesho hayo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
…………………………….

Na Mwandishi wetu, WFM, Dar es Salaam

WIZARA ya Fedha na Mipango, imetwaa tuzo mbili kwa mpigo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayofikia kilele Jumamosi Julai 13, 2019.

Katika hafla ya ufungaji rasmi wa maonesho hayo kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa (Ceremonial dome) , Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, alikabidhi tuzo hizo moja baada ya nyingine, kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja.

Akizungumzia tuzo hizo Bw. Mwaipaja alisema moja ni ya mshindi wa pili katika ubunifu wa mfumo wa ukusanyaji maduhuli ya serikali (GePG) ambao umerahisisha mfumo wa malipo kwa wananchi, wakiwemo pia wafanyabiashara, na wawekezaji.

Aidha, Taasisi mbili za Wizara ya Fedha na Mipango, ikiwemo Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), zimetwaa tuzo ya mshindi wa Tatu katika utoaji wa Elimu bora ya Juu na Usimamizi makini wa wataalamu wa Ununuzi na Ugavi.

Maonesho hayo yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere maarufu Sabasaba, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, yamebeba kauli mbiu isemayo “Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda.”

SERIKALI YAOMBWA KUWEKA UWIANO WA WANAFUNZI WENYE UFAULU DARAJA LA KWANZA

$
0
0

Na Jusline Marco:Arusha

Serikali imeombwa kuweka uwiano wa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza katika shule zote za elimu ya juu ili kuleta motisha kwa wanafunzi wanaojiunga na masomo kwenye shule hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa shule ya sekondari ya Mwandeti iliyopo katika kata ya Mwandeti,Wilayani Arumeru Mkoani Arusha kufuatia shule hiyo kushika nafasi ya nne kitaifa na nafasi ya pili kimkoa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita.

Amesema kuwa pamoja na shule hiyo kutoa wanafunzi 70 wenye ufaulu wa daraja la kwanza na wanafunzi 6 wenye ufaulu wa daraja la pili jitihada kubwa zimetumika ili kufanikisha shule hiyo inafanya vizuri zaidi kwani wengi wao walijiunga wakiwa na ufaulu wa daraja la tatu na daraja la pili katika matokeo ya kidato cha nne.

Vilevile ameeleza kuwa kushika kwa nafasi hiyo kunatokana na jitihada kubwa zilizofanyika na uongozi wa shule hiyo kwa kushirikiana na walimu wao kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji pamoja na kufanya ziara za kimasomo katika shule mbalimbali nchini.

Pamoja na hayo baadhi ya changamoto zilizopo katika kata hiyo zimeoneka kukithiri kwa muda mrefu ikiwemo ubovu wa barabara ambayo huleta madhara makubwa kipindi cha mvua kutokana na miundombinu hiyo kutokarabatiwa na uongozi husika.

Kwa upande wake Mwalimu wa taaluma shuleni hapo Peter Saiguran amesema kuwa ufaulu huo umetokana na misingi waliyojiwekea ya ushirikiano wa walimu kwa walimu,uongozi shule hiyo na shule za jirani,walimu na wanafunzi pamoja uwepo wa maziringira rafiki ya madarasa ba mabweni kwa wanafunzi.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa kutokana na kampeni za kuzuia ndoa na mimba za utotoni kwa watoto wa kike zilizofanywa na shule hiyo katika jamii ya kifugaji ya kimaasai kwa kuwataka wazazi kuwekeza elimu kwa watoto wao imechangi kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu shuleni hapo.
Mkuu wa shule ya sekondari  Mwandeti John Masaawe iliyopo katika Kata ya Mwandeti,Wikayani Arumeru Mkoani Arusha iliyoshika nafasi ya nne kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita.

Naibu Waziri Waitara Afunguka tatizo la mimba za utotoni

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

LICHA ya Serikali kuweka adhabu kali dhidi ya watu wanaowasababishia ujauzito wanafunzi na watoto waliochini ya umri wa miaka 18, lakini bado tatizo la mimba za utotoni ni kubwa huku mila na desturi zikitajwa kuchangia tatizo hilo hapa nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe Mwita Waitara, wakati wa maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani, yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Ripoti ya Idadi ya watu Duniani, tukio lililofanyika jijini Dodoma.

Naibu Waziri Waitara amesema tatizo hilo ni kubwa kwa shule za msingi na sekondari ambapo ni asilimia 29 na limekua likichangiwa kwa kiasi kikubwa na mila na desturi, uendeshaji wa kesi ya kumtia mtu hatiani aliyempa mimba wanafunzi.

“Kuna mila na desturi ambazo watoto wa kike wakifikia umri fulani wanapewa chumba hivyo huko mtaani usiku kucha huwezi jua kinachoendelea, mazingira magumu ya usomaji.

“Hata katika uendeshaji kesi hizi mpaka kumtia mtu hatiani bado ni changamoto sana kwa kuwa wanaofanya vitendo hivyo wengine ni watu wa karibu na familia na wengine wanarubuni ndugu na kumalizana kimya kimya,”amesema Waitara.

Aidha licha ya hayo amesema uelewa wa watoto bado ni mdogo huku mimba nyingi zinazoripotiwa zimekua zikiishia hewani bila kujua mwisho wa kesi hiyo.Amesema wao kama serikali wanafanya vikao na wazazi mara kwa mara ili kuondokana na tatizo hilo, lakini bado mwitikio ni mdogo sana katika kudhibiti vitendo hivyo.

Kadhalika, amesema bado kuna changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi ambapo kati ya vizazi hai 100,000 watu 556 huripotiwa kufariki dunia kwa sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni. 

“Nchi yetu ni moja ya mataifa 179 yaliyokutana nchini Cairo na tulikubaliana kutekeleza Mpango kazi tuliopanga katika Mkutano huo wa Idadi ya watu na maendeleo, serikali ya Tanzania imetekeleza mambo mengi, ni wajibu wetu kushirikiana kumaliza vifo vinavyotokana na uzazi na mimba za utotoni ili kila kijana atimize ndoto zake,”amesema.

Pia amebainisha kuwa serikali imekuwa ikitekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo na inalenga kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 hivyo ni lazima wahakikishe wanatokomeza tatizo hilo.

Kwa upande wake afisa kutoka UNFPA, Samwel Msokwa, akisoma taarifa ya idadi ya watu duniani iliyotolewa na Shirika hilo, amesema kadri watu wanavyoongezeka changamoto nazo zinaongezeka ambapo katika ripoti hiyo inaonesha tatizo la mimba za utotoni duniani bado ni kubwa sana.

“Ripoti inaeleza kinaga ubaga kuwa kuna tatizo la ukatili wa kijinsia licha ya taasisi mbalimbali kufanyiwa kazi, tuelekeze nguvu kukabiliana na tatizo hili,”amesema.

Naye, Mwakilishi wa Mkazi wa Umoja wa Mataifa(UN), Alvaro Rodriguez amesema vifo vinavyotokana na uzazi bado ni changamoto hasa kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 15-19.
Naibu Waziri TAMISEMI, Mwita Waitara (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kulia) na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa,  Alvaro Rodriguez wakiwa na vitabu vyenye ripoti yenye taarifa ya idadi ya watu Duniani iliyotolewa na Shirika la UNFPA.
 Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Idadi Duniani. 

 Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi duniani.

Mgogoro Baina ya Wazee wa Kimila na Chuo cha Ufundi Arusha Watatuliwa

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akisistiza jambo wakati wa kikao cha usuhushi baina ya Wazee wa kimila wa kimasai na uongozi wa chuo cha Ufundi Arusha kuhusu eneo la kimila lililopo ndani ya chuo hicho leo Jijini Arusha. 
Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiwa amemwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Dkt. Noel Mbonde (kushoto) akifafanua jambo katika kikao cha usuluhishi baina ya Wazee wa kimila wa kimasai na uongozi wa chuo cha Ufundi Arusha kuhusu eneo la kimila lililopo ndani ya chuo hicho, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi. 
Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Isack Lekisongo akitoa neno la shukurani katika kikao cha usuluhishi baina ya Wazee wa kimila wa kimasai na uongozi wa chuo cha Ufundi Arusha kuhusu eneo la kimila lililopo ndani ya chuo hicho leo Jijini Arusha. 
Wajumbe wakisikiliza na kufuatilia kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi (hawapo katika picha) wakati wa kikao cha usuluhishi baina ya Wazee wa kimila wa kimasai na uongozi wa chuo cha Ufundi Arusha kuhusu eneo la kimila lililopo ndani ya chuo hicho leo Jijini Arusha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi (kulia) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Isack Lekisongo (kushoto) wakati wa kikao cha usuluhishi baina ya Wazee wa kimila wa kimasai na uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha kuhusu eneo la kimila lililopo ndani ya chuo hicho leo Jijini Arusha 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi( wa pili kulia waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kikao cha usuluhishi wa eneo la kimila lililopo katika Chuo Cha Ufundi Arusha mara baada ya kufikia makubaliano leo Jijini Arusha.( Picha na Lorietha Laurence-WHUSM, ARUSHA) 
…………………. 
Na Lorietha Laurence-WHUSM,ARUSHA 

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wamefanikiwa kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na Wazee wa kimila wa Kimasai kuhusu umiliki wa eneo la kimila lilipo ndani ya chuo hicho. 
Akiongea katika kikao kilichofanyika leo Jijini Arusha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Bi. Susan Mlawi ameueleza kuwa ni muhimu kwa uongozi wa chuo pamoja na uongozi wa wazee wa kimila kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza makubaliano yaliyoafikiwa katika kikao cha awali kilichofanyika tarehe 17 Mei 2019. 

Moja ya makubaliano hayo ni pamoja na uongozi wa chuo kuongeza eneo hilo la kimila la Wazee wa Kimasai kutoka meta mraba 1,118.12 hadi kufikia meta mraba 1,464.92 ili kuwapa nafasi ya kufanya shughuli hizo za kimila. 
“Kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza na kudumisha mila katika jamii yetu ya kitanzania sisi viongozi wa serikali tumeona umuhimu wa chuo kuongeza eneo hili ili muweze kupata nafasi ya kufanya shughuli za kimila “ alisema Bibi. Susan Mlawi 

Aidha aliongeza wa kueleza kuwa mbali na kuongezewa eneo, kikao kimekubaliana na kuruhusu uongozi wa jamii ya kimasai kumalizia ujenzi wa jengo lililopo katika eneo hilo pamoja na kujenga vyoo vya kisasa. 
Vilevile kikao hicho kilisisitiza kuwa eneo hilo litumike kwa masuala ya kimila tu na si vinginevyo huku umiliki wa ardhi ya eneo ukiendelea kuwa chini ya uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha. 

Pia kikao kiliazimia kuwa viongozi hao wa kimila wataendelea kufuata utaratibu wa kuomba kibali kutoka katika uongozi wa chuo ili kuweza kuingia katika eneo hilo kwa ajili ya shughuli zao mbalimbali za kimila. 
Naye Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Dkt. Noel Mbonde amewataka viongozi hao wa kimila kuzingatia makubaliano hayo na kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa uongozi wa Chuo. 

“Makubaliano haya ni mazuri yenya lengo la kujenga mahusiano mema baina ya Serikali na wananchi wake hivyo ni muhimu kuzingatia yale yote tuliyokubalina hapa kwa maendeleo na ustawi mzuri wa nchi yetu” alisema Dkt. Noel Mbonde. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazee wa Kimila wa Kimasai Bw. Isack Lekisongo ameishukuru serikali pamoja viongozi walioshiriki kufikia muafaka wa kuutatua mgogoro huo wa mrefu na kuahidi kutoa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza shughuli zao za kimila.

MATUKIO KATIKA PICHA USAJILI WA NGO’s KANDA YA MASHARIKI

$
0
0

Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ambayo awali yalisajiliwa chini ya Sheria nyingine Bi.Vick Ntetema (kushoto aliyekaa) akipata huduma ya kusajili Taasisi yake ya Khulisa Social Solutions Tanzania (KSST) katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Denis Bashaka (kulia), akifafanua jambo kwa mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati akimpatia huduma ya kusajili Taasisi yake chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Bi.Happy Msimbe akitoa huduma ya kusajili Taasisi kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Victor Rugalabamu akitoa huduma ya kusajili kwa Mmoja wa mdau kutoka Taasisi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na. 3/2019 katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki. 
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa NGO Grace Mbwilo akitoa cheti kwa Bi. Vick Ntetema mmoja wa mdau kutoka Taasisi ya Khulisa Social Solutions Tanzania (KSST) katika zoezi linaloendelea kufanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa Kanda ya Mashariki.

AGIZO LA RAIS MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA KYAKA MISSENYI.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Siku moja baada ya Rais John Pombe Magufuli kuagiza kushugulikiwa kero ya Maji kwa wakazi wa Kyaka, Kata Burifani, na Kata jirani, katika Wilaya ya Missenyi, Waziri wa Maji Professa Makame Mbarawa amefika Wilayani humo ili kuanza utekelezaji wa agizo hilo.

Akiambatana na Safu ya wataalam mbalimbali wa Maji kutoka BUWASA na wengine kutoka Mwanza pamoja na Wizarani, amefika eneo la Kyaka na kufanya Mkutano wa hadhara ambapo katika mkutano huo ameahidi kuanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais kwa haraka ili kutatua kero hiyo ndani ya miezi mitano.

Aidha Professa Mbarawa amesema kuwa kwa sasa Wizara ya Maji imejipanga vyema kuhakikisha miradi ya Maji inatekelezwa na Wakandarasi wenye sifa na uwezo kwani kipindi cha nyuma miradi mingi ilikwama kutokana na Kandarasi wabovu, na kukiri kuwa uwepo wa ukiritimba na urasimu, ambapo watumishi wachache wasiokuwa waadilifu wamekuwa wakishirikana na wakandarasi wabovu kutekeleza miradi ya Maji isiyokuwa na Viwango, lakini sasa marekebisho makubwa yamefanywa na kuahidi usimamizi makini.

Itakumbukwa kuwa Mhe. Rais alitoa agizo la kumaliza kero ya maji eneo la Kyaka, wakati aliposimama eneo hilo kusalimia wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, na baada ya kuelezwa kero hiyo alimpigia simu Waziri Mbarawa na kumtaka afike Mara moja kulishughulikia.
 Pichani Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Wananchi wa Muleba na Tanzania wakati aliposimama Muleba Mjini, waliosimama ni Rc Gaguti, Dc Luyango, na Waziri Mbarawa
  Waziri Mbarawa akihutubia Wananchi na wakazi wa Kyaka alipowasili hapo tayari kuanza kutekeleza agizo la Rais juu ya utatuzi wa Kero ya Maji.
Pichani ni Timu ya wataalam, watumishi wakiongozwa na Waziri wa Maji Profesa Mbarawa wakiwa juu ya Kilima Rubale Kata Kyaka ambapo tanki kubwa la mradi wa Maji litajengwa hapo

TUNATEKELEZA KAULI YA RAIS DKT MAGUFULI YA TANZANIA YA VIWANDA-TROPICAL INDUSTRIES

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

KIWANDA Cha Wazalendo cha Tropical Industies wamemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwapa fursa wamiliki wa viwanda ambao ni wazalendo kuuza bidhaa zao kwa urahisi mkubwa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Charles Mlawa katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Michuzi TV, Mlawa amesema kiwanda chao kinajishugulisha na utengenezaji wa transfoma, nyaya za umeme za usambazaji na nyaya za usafirishaji zikizalishwa hapa nchini.

Mlawa amesema, amemshukuru Rais kwa fursa aliyoitoa kwa wazalendo kuweza kufanya biashara kwani kipindi cha nyuma walijaribu kufanya jitihada za kuuza kwa wateja wa ndani ilishindikana.

“Kauli ya Rais ya Tanzania ya Viwanda kuelekea uchumi wa kati imesaidia sana,wao kama kiwanda wamenufaika kwa kupata wateja wa ndani na nje ya nchi,”amesema Mlawa.

Aidha, amesema ndani ya miaka mine ya Dkt John Pombe Magufuli kwa vitendo na kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora tena kikiwa ni kiwanda cha wazalendo kwa asilimia 100.

Ametoa rai kwa waanzania kuunga mkono bidhaa zinazotengenezwa na watanzania wenzao kwani zina ubora mzuri kama ule wa nje.
Mhandisi wa Kiwanda cha Tropical Industries Jacob Shirima akielezea namna wanavyoanza kutengeneza transfoma kuanzia hatua ya kwanza hadi linapokamilika katika banda lao liliopo ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo wa Kiwanda cha Tropical Industries Rigobert Manega akielezea aina za nyanya wanazozitengeneza kutoka kwenye Kiwanda chao kinachopatikana Jijini Dar es salaam.

UINGEREZA YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin,London Uingereza. July 12, 2019 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo baina yao kuhusu masuala mbalimbali kati ya Tanzania na Uingereza. Mazungumzo hayo yamefanyika London Uingereza. July 12, 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo baina yao kuhusu masuala mbalimbali kati ya Tanzania na Uingereza. Mazungumzo hayo yamefanyika London Uingereza. Pembeni kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dr. Asha -Rose Migizro. July 12, 2019. 

************** 

Uingereza imeihakikishia Tanzania kuwa itaendelea kuwa mshirika wake katika masuala mbalimbali ya ubia wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji wengi kutoka Uingereza kuwekeza Tanzania kama moja ya hatua za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ili iweze kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025. 

Waziri wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza katika Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo, Mhe. Harriett Baldwin ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi, Jijini London, Uingereza kwa nia ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo na ushirikiano baina ya Tanzania na Uingereza. 

Katika mazungumzo hayo Waziri Harriett na Prof. Kabudi wamezungumzia kuhusu hali ya ushirikiano wa ubia wa maendeleo uliopo hivi sasa na kuonesha kuridhishwa na Serikali ya Tanzania inavyosimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Uingereza katika sekta za elimu,afya, maji, kilimo pamoja na miundombinu ya barabara hususani vijijini ikiwemo maboresho ya mifumo ya fedha,utumishi wa umma, serikali za mitaa miongoni mwa miradi mingine mingi. 

Pia, Waziri Harriett ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kupambana na rushwa,kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma katika sekta ya umma, kuongeza uwajibikaji na utawala bora mambo aliyoyataja kama hatua muhimu ya kufikia malengo ya haraka na kuondoa umasikini. 

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba John Kabudi ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa kuwa mbia mkubwa wa maendeleo na kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uwekezaji,biashara na utalii nchini Tanzania. 

Aidha, Prof Kabudi amemhakikishia Waziri Harriett nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kufanya mageuzi muhimu ya kiuchumi na kiutawala yanayolenga kuifikisha Tanzania katika mojawapo ya nchi za uchumi wa kati. 

Miongoni mwa maboresho hayo, Waziri Kabudi ameyataja kuwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara,maboresho katika usimamizi wa utendaji wa Serikali katika kuwahudumia wananchi na utoaji huduma za kijamii hususani sekta zinazowagusa wananchi wengi hususani wa kipato cha chini. 

Akihitimisha mazungumzo hayo Waziri wa masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Mhe. Harriett Baldwin amemhakikishia Waziri Kabudi kuwa Uingereza inafuatilia kwa ukaribu mageuzi na maboresho ya kiutendaji yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli yakiwemo, kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara,kukuza demokrasia na utawala bora na hivyo Tanzania itegemee ongezeko la wawekezaji kutoka Uingereza.

Vijana Morogoro watuma salamu za pongezi na shukrani kwa Rais Magufuli

$
0
0
Na Charles James, Michuzi Tv

Vijana Wilayani Kilosa, Morogoro wamemshukuru na kumpongeza Rais Dk John Magufuli kwa hatua yake madhubuti ya kufuta hati ya mashamba makubwa yaliyokua yanamilikiwa na watu wachache na kuyarejesha mikononi mwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana Kazi na Ajira, Mhe Anthony Mavunde wakati wa mavuno ya mpunga katika shamba linalomilikiwa na Vijana wa Kampuni ya Agri-Ajira ambao ni wahitimu wa Chuo cha Kilimo Sokoine.

" Niwapongeze kwa uthubutu wenu na kazi kubwa mliyoifanya mpaka kufikia mafanikio makubwa, Kama Serikali tutawawezesha kimtaji kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo ili kupanua Kilimo chenu na kugawa ajira zaidi kwa Vijana, na kabla ya kuondoka hapa nimtake Afisa kutoka Benki ya Kilimo kutoondoka hapa bila kuweka sawa andiko la mkopo na mahitaji ya vijana hawa," amesema Mh Mavunde.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi amewahakikishia vijana wilayani hapo kuwa Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega katika kuwapatia maeneo ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao na kuahidi kulifanyia kazi ombi la ekari 500 za ziada zilizoombwa na Kampuni hiyo ya vijana.

Awali wakisoma risala mbele ya Mhe Mavunde, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Charles Ibrahim ameishukuru Serikali ya Rais Magufuli kwa kuwapatia eneo la kilimo la ekari 50 ambapo pia amesema kama wataongezewa ekari 500 walizoomba basi wataongeza idadi ya ajira kutoka 200 kufikia 1000.

SAVE THE CHILDREN WATIMIZA MIAKA 100, WAJA NA MKAKATI WA MIAKA MITATU

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv.

Shirika la Save the Children limesherehekea kutimiza kwa miaka 100 toka kuanzishwa kwake sambamba na kuzindua mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto.

Mkakati huo unaoanzia mwaka 2019 hadi 2021 kwa ajili ya watoto Tanzania umewekwa kwenye vipengele saba ambazo zitaangaliwa changamoto zinazowakabili watoto nchini.

Akizungumzia mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza amesema shirika la save the Children ni wadau wakubwa na wamekuwa wanashirikiana na serikali katika kusaidia na kuwalinda watoto.

Magwiza amesema, shirika hilo lipo nchini kwa miaka 38 na wanafanya kazi kulingana na mipango ya serikali kwa kuangalia namna gani wanawalinda watoto na wamekuwa wakiandaa mikakati mizuri inayomlinda mtoto.

Amesema, wamekuwa wanasaidia kutoa elimu rika kwa vijana waliobalehe, kuwawezesha watoto kielimu na kujitambua jambo ambalo limekuwa na msaada mkubwa sana kwa taifa.Kwa upande wa Save the Children, mpango mkakati wao uliweza kutambulishwa rasmi unaoelezea mambo saba watakayoyaangalia ndani ya miaka mitatu.

Tuma, ameeleza kuwa malengo yao nchini Tanzania ni kuwalenga watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu zaidi. Malengo hayo ni Ishi ambapo mtoto atahitaji afya na lishe, Jifunze ikilenga elimu, Lindwa ikiwa ni Ulinzi wa mtoto, Umasikini wa mtoto na usimamizi wa haki za mtoto.

Malengo yao ni kushirikiana na mashirika yenye mtazamo mmoja ili kuwanufaisha watoto.Mkurugenzi wa Save the Children nchini Peter Walsh amesema wamejikita zaidi katika kuangalia ni namna gani wanamsaidia mtoto na hata katika kutimiza miaka 100 ya shirika hilo waliweza kumleta Anne Chamberlain aliyeigiza na kuelezea stori ya Eglantyne Jebb aliyeweza kujitoa na kuwasaidia watoto waliokuwa wanaishi mazingira magumu nchini Ujerumani na ndiye mwanzilishi wa Save the Children.

Sherehe hiyo ilihidhuriwa na watu mbalimbali na ilihitimishwa kwa wageni kutazama igizo kutoka kwa Anne Chamberlain.

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza  akikata keki pamoja na Mkuruge zj wa Save the Children Nchini Tanzania Peter Walsh wakati wa kusherehekea miaka 100 toka kuanzishwa kwake pamoja na kuzindua mkakati wa miaka mitatu utakaoanzia 2019 hadi 2022 wa kuwalinda na kuwajali watoto.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza  akifuatilia kwa makini maelezo kutoka Save the Children kuhusiana na mkakati wa miaka mitatu utakaoanzia 2019 hadi 2021 wa kuwalinda na kuwajali watoto. 

 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatikia uzinduzi wa mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto sambamba na sherehe ya miaka 100 ya Save the Children toka kuanzishwa kwake.
 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatikia uzinduzi wa mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto sambamba na sherehe ya miaka 100 ya Save the Children toka kuanzishwa kwake.
 Mwakilishi kutoka Save the Children Tuma akielezea mkakati wa miaka mitatu utakaoanzia 2019 hadi 2021 wa kuwalinda na kuwajali watoto uliozinduliwa na Shirika lao.

 Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatikia uzinduzi wa mkakati wa miaka mitatu wa kuwalinda na kuwajali watoto sambamba na sherehe ya miaka 100 ya Save the Children toka kuanzishwa kwake.

uzinduzi wa kiliniki tembezi ya upasuaji wa Mabusha

$
0
0
Mkurugenzi wa Kinga Dkt.Leonard Subi kushoto akimfanyia upasuahi mmoja wa wagonjwa waliofika kupata huduma ya upasuaji wa mabusha kwenye kliniki hiyo 

************** 

Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele imefanya uzinduzi wa kiliniki tembezi ya upasuaji wa Mabusha kwa wananchi wilayani Nachingwea Mkoani Lindi. 

Akizindua kliniki hiyo Mkurugenzi wa Kinga Dkt.Leonard Subi amesema mpaka sasa wagonjwa 353 wamekwishapasuliwa na zoezi hilo litaendelea wilayani hapo na baadae kuhamia wilaya Ruangwa. Matarajio ni kufikia wagonjwa 600 Kwa mkoa wa Lindi. 

Ugonjwa wa Mabusha na Matende umeathiri zaidi ya watu Milioni 120 Duniani na hapa nchini takribani watu 25,000 wanakadiriwa kuwa na Mabusha au Matende .Ugonjwa huu huathiri sehemu mbalimbali za mwili wengi miguuni au mkononi.

Serikali yadhamiria kumaliza tatizo la Maji Kibondo

$
0
0

Na Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha inamaliza tatizo la maji nchini, Serikali imedhamiria kutumia Shilingi Bilioni 1.2 katika Mji wa Kibondo mkoani Kigoma kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Mabamba-Mkarazi na Kitahana utakaotoa huduma ya maji ya Uhakika kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitahama, Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso amesema Fedha hizo zimetolewa ili kutimiza ahadi ya Mhe Rais Dk John Magufuli ya kuwapatia wakazi wa Kibondo huduma ya maji.

" Kibondo ni miongoni mwa miji yenye uhaba wa Maji na kwa kutambua hilo tumetoa Bilioni 1.2 kwa mradi wa Mabamba-Mkarazi na tutatoa Bilioni 1.1 kwa ajili ya ujenzi wa mradi mwingine wa maji wa wakazi wa Kibondo.

" Dhamira ya Rais Magufuli ni kumtua Mama ndoo kichwa ni na kama Wizara tunatekeleza maagizo hayo na nimejionea tayari mradi umeanza kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi, kazi iliyobaki ni mkandarasi kumaliza ujenzi wa Vilula vilivyobaki," amesema Mhe Aweso.

Awali Mhe Aweso ameto matumaini kwa wananchi wa Mji wa Mwandiga uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuwa ifikapo mwezi August, Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 za kuanzia kazi ya ujenzi wa miundombinu itakayopeleka huduma ya Maji kwa wananchi kutoka kwenye mradi wa Maji Kigoma Mjini.
 Naibu Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso akiwa katika katika kijiji cha Kitahama,Kibondo mkoani Kigoma kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kupitia miradi mbalimbali inayojengwa mkoani humo



VIJANA HATUNA BUDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA DKT. MAGUFULI .

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Kagera.

Mbunge wa Viti Maalum anaewakilisha Vijana kutoka Kagera Halima Bulembo,anaendelea na ziara yake Mkoani Kagera ,ambapo ametembelea Wilaya ya Muleba na kutoa msaada wa Vitanda vya hospital,Magodoro,Mashuka na Delivery Pack katika Zahanati ya Ruhanga iliyopo Kamachumu Wilayani Muleba,

Mh Halima amesema kuwa lengo kubwa la ziara na msaada huo ni kuunga Mkono jitahada zinazofanywa na Mh Rais Magufuli ikiwa ni sambamba na kuwasaidia wagonjwa pamoja na akina mama wajawazito pindi wanapoenda kujifungua.

Licha ya changamoto chache katika sekta ya afya, Serikali ya awamu ya Tano imeboresha huduma ya Afya kwa kiwango kikubwa, kwa kuongeza vituo vya Afya, Zahanati, na ujenzi Wa Hospitali Mpya sambamba na upatikanaji wa dawa katika Vituo hivyo, huku jitihada zaidi zikielekezwa katika kuboresha huduma ya Afya ya Uzazi wa Mama na motto.

Katika ziara hiyo amemkuta mwenyeji wake Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage ambaye amepongeza Kwa msaada huo Mkubwa alioutoa huku akiwaomba wadau wengine kuendelea kujitoa katika shughuli za kuchangia maendeleo hususani mambo yanayogusa jamii.
 Mbunge wa Vijana Mkoa wa Kagera, Pichani, Mhe. Halima Bulembo akikabidhi msaada wa Mashuka ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyoahidiwa katika Zahanati ya Ruhanga Kamachumu Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
 Sehemu ya Wakazi wa Kijiji Ruhanga pamoja na wanafunzi, wakiwa wanaendelea kumsikikiza Mhe. Halima Bulembo (hayupo pichani) wakati wa tukio la utoaji Vifaa vya huduma ya Afya katika Zahanati ya Ruhanga Kamachumu. 
Pichani ni Mhe. Halima Bulembo akiwa anaendelea kufuatilia moja ya shukrani kutoka kwa wakazi wa Ruhanga, pembeni ni Mhe . Charles Mwijage (MB) na Fahami Matsawili mwanaharakati wa mambo ya Kisiasa.


WAAANDISHI WA HABARI WANOLEWA KUELEKEA MKUTANO WA SADC, WAKUMBUSHA WAJIBU WAO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Morogoro

WAANDISHI wa Habari nchini Tanzania wametakiwa kuibua masuala ya kimkakati katika kuitangaza nchi kimataifa, hasa kwa manufaa ya kiuchumi, kisiasa na kitamaduni

Hayo yameelezwa mkoani Morogoro jana na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dk. Ayoub Rioba wakati akitoa mada kwa wanahabari waliohudhuria semina ya maandalizi ya mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Dk Rioba, amesema yapo masuala mengi yanayohitaji kuripotiwa kizalendo kwa kuwa hakuna taifa linaloweza kuiinua Tanzania kitamaduni bali Tanzania yenyewe

“Mimi nimewahi kuishi nchi mbalimbali duniani, nimefanya kazia na kusoma katika maeneo mbalimbali ya dunia, sijawahi kuona habari za kwetu zikipewa kipaumbele. Kwa mfano nikiwa Ulaya sikuona habari za mataifa ya Afrika, labda kutokee habati za vita au magonjwa.

“Hivyo, tunatakiwa kuzingatia ni kitu gani tunakipeleka kwa watazamaji na wasomaji wetu. Tujipange kwa ajili ya kujitangaza, kazi hii haiwezi kufanywa na mwengine zaidi ya nyinyi wanahabari,” alisema Dk. Rioba.

Kwa upande wake, Hebert Mrango ambaye kwa nyakati tofauti ameitumikia Serikali ya Tanzania kwenye masuala ya kitaifa, kidiplomasia na kimataifa; wakati akitoa mada alisema vijana wengi kwa sasa huenda hawajui mantiki ya SADC.

Hivyo, ipo haja ya kusoma nyaraka nyingi ili kuujua msingi wa kuanzishwa jumuiya hii. Ambapo Tanzania ina mchango mkubwa katika uanzishwaji wake.“SADC ilianzishwa kwa ajili ya maendeleo endelevu, kwa mfano tulikuwa na makubaliano kuwa hadi ikifika mwaka 2008 iwe asilimia Zaidi ya 80 ya bidhaa zitakazouzwa ndani ya nchi wanachama ziondolewe kodi

“Hii ingeweza kutusaidia kuondokana na utegemezi katika mataifa mengine ya Ulaya, lakini kuna baadhi ya masuala yalikuwa magumu kufuatwa katika uondoaji kodi hasa bidhaa za kimkakati zikizokuwa zikizalishwa katika nchi wanachama ambazo zilikuwa tegemezi la kiuchumi kwa mataifa yao,” amesema Balozi Mrango.

Awali, akieleza lengo la kufanyika semina hiyo ya siku tatu ambayo ni awamu ya pili, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa alisema anaamini waandishi waliopikwa katika semina hiyo watakuwa mabalozi wazuri hata baada ya kustaafu kazi ya uandishi.

“Tunataka muwe na uelewa mpana juu ya suala hili la SADC, si kwa ajili ya vikao tu vitakavyofanyika mwezi ujao lakini hata kuwa na elimu ya kutosha hata kuwasaidia wengine. Tunaamini SADC itaandikwa sana kwa kipindi hiki,” amesema Kawawa.

Kwa mwaka huu SADC itakuwa na vikao vyake nchini katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), kati ya Agosti 17 na 18.

Aidha, kabla yah apo mapema mwezi ujao kuanzia Agosti 5 hadi Agosti 8, mwaka huu kutakuwa na mapnyesho ya viwanda katika ukumbi wa JNICC, Agosti 9 vitaanza vikao vingine vya SADC vikianza na vikao vya kamati, vikao vya mawaziri wa mambo ya nje kwa nchi wanachama, vikao vya makatibu wakuu katika nchi wanachama na wakurugenzi kisha ndio mkutano mkuu ambao utakutanisha viongozi wan chi kwa siku mbili Agosti 17 na 18.

Mara ya mwisho vikao hivi kufanyika Tanzania ilikuwa mwaka 2003 katika Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa.

SADC ina nchi wanachama 16 ambazo ni: Tanzania, Malawi, Angola, Zimbabwe, Msumbiji, Afrika Kusini, Ushelisheli, Zambia, Eswatini, Commoro, Botswana, Lesotho, Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mauritius na Namibia.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi, Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert A. Ibuge akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa kundi la pili la waandishi hao. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini orogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa
akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo kwa waandishi hao.Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika na kuripoti habari za SADC kwa weledi Bw. Henry Mabumo akieleza jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na Jumuiya hiyo kupitia fursa zilizopo katika nchi wanachama, hayo yamejiri leo Julai 12, 2019 mjini Morogoro wakati wa siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi hao. 
Katibu Mkuu mstaafu Balozi Hebert Mrango akisisitiza jambo wakati wa
mafunzo kwa kundi la pili la waandishi wa habari wanaojengewa uwezo ili waweze wa kuandika na kuripoti habari za nchi wanachama wa SADC, hayo yamejiri mjini Morogoro Julai 12, 2019 ambapo mafunzo ya kundi la pili kwa waandishi hao yanafanyika kwa siku tatu.
Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akijibu hoja
mbalimbali za waandishi wa habari walioshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 12, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MHE. CONSTANTINE KANYASU AONYA WAHARIBIFU WA MISITU

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akinyosha mikono kuwasalimia Wachimbaji wadogo wa madini kabala ya kuanza kuzungumza na Wachimbaji hao kwenye mkutano mkoani Geita uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanlaus Nyongo akizungumza na Wachimbaji wadogo wa madini kwenye mkutano uliofanyika mkoani Geita uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 
Baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa madini wakiwa kwenye mkutano uliofanyika mkoani Geita uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanlaus Nyongo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wachimbaji Wadogo wa madini wa wilaya Mbogo mara baada ya Naibu Waziri Madini, Mhe.Nyongo kufunga mkutano huo uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha ,mali 
Mkurugenzi Mwezeshaji wa kutoka MKURABITA,, Dkt. Anastazia Haule akizungumza na Sachimbaji Wadogo wa Madini kabla Naibu Waziri Madini, Mhe.Nyongo kufunga mkutano huo uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha ,mali 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita, Mhe. Leonard Bugomola akizungumza na Wachimbaji Wadogo wa madiini kuhusu umuhimu wa kujiunga katika vikumdi ili waweze kukopesheka. ( Picha zote na Wizara ya Maliasili na Utalii)

…………………….. 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema Tanzania kwa mwaka mmoja inateketeza takribani hekta 400,000 za misitu ambapo endapo hali hii itaachwa hivyo Misitu iliyopo nchini itaisha baada ya miaka 12 

Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amesema Wizara yake itaendelea kulinda misitu hiyo kwa nguvu zake zote ili kuweza kuinusuru. 

Hayo ameyasema mkoani Geita wakati alipokuwa akizungumza na Wachimbaji Wadogo wa madini kwenye mkutano uliolenga kutoa elimu kwa Wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa kurasimisha mali. 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe.Kanyasu amesema shughuli za uchimbaji madini zimekuwa zikichangia kwa kiasi kikubwa katika uteketezaji wa misitu hiyo. 

Amesema Wachimbaji walio wengi wamekuwa ni watu wa kuhama hama na kila mahali wanapohisi kuna madini wamekuwa wakifyeka misitu bila kujali athari zake.. 

Ameongeza kuwa kwa vile Wachimbaji hao wamekuwa wakifyeka misitu hiyo katika maeneo makubwa hata baada ya kumaliza uchimbaji huo hushindwa kupanda miti mingine. Amewaeleza kuwa madhara yake ni makubwa na kama hali hiyo itaendelea kwa vile mara baada ya misitu hiyo kuisha mvua hazitaweza kunyesha na hali ya maisha itakuwa ngumu sana. 

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewataka Wananchi wanaokata miti iwe yao walioyaipanda uwe mwembe au mti wa aina yeyote wafuate taratibu za kupata kibali kwa Maafisa misitu au wenyeviti wa maeneo husika. Amesema kwa wale wanaokata miti hiyo bila kupata kibali kwa mamlaka husika, Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria. 

Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Mhe. Stanlaus Nyongo amewataka Wachimbaji hao kufuata sheria pale wanapohisi uwepo wa madini katika maeneo ya Hifadhi .Amewataka watoe taarifa kwa Wamiliki wa Hifadhi kwa ajili ya kupata idhini badala ya kuanza kuvamiwa maeneo hayo kwa kuanza kufyeka misitu. 

Naye, Hamisi Abdala aliyejitambulisha kama Mchimbaji mdogo amesema atakuwa Balozi kwa Wenzake kwa kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kulinda misitu.

WAFUGAJI WA TANZANIA KUPITIA MRADI WA SAHIWAL WAZURU NCHINI KENYA

$
0
0
Ng'ombe aina ya Sahiwal walioko Transamara nchini Kenya walioboreshwa kupitia Mradi wa Utafiti wa uboreshaji na utunzaji wa Mbari za ng’ombe unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la AU-IBAR.
Mratibu wa Mradi wa Sahiwal kutoka Tanzania, Dk. Zebron Nziku akimpongeza mfugaji wa ng'ombe wa Wilaya ya Kiligoris, Transmara nchini Kenya, Oltetia Ole Oltetia kutokana na juhudi kubwa alizofanya kuboresha mifugo yake.
Wafugaji wa Tanzania na Kenya wakijadiliana kwa pamoja namna bora kuboresha ufugaji wao wakiwa kwenye mafunzo katika Chuo cha Uchakataji Maziwa (DTI), Naivasha Kenya Wafugaji wa Tanzania na Kenya walioko kwenye mafunzo nchini Kenya wakiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Mradi wa Sahiwal , Dk Zebron Nziku na wataalamu wengine kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kutembelea Chuo cha Uchakati Maziwa(DTI), Naivasha Kenya
Afisa Mtafiti wa Mifugo Mkuu (PLRO), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Hassan Mruttu akisalimiana na mfugaji aliyeko kwenye mradi wa Sahiwal, Kantet Ole Kate wa Transmara Narok nchini Kenya mara baada ya wafugaji wa Tanzania kutembelea nchi hiyo kwa ziara ya mafunzo
Mratibu wa Mradi wa Sahiwal Tanzania, Dk. Zebron Nziku wa mwisho kulia akiwa katika picha ya pamoja na wafugaji wakiwa mpaka wa Namanga muda mfupi kabla ya kuingia nchini Kenya kwa ziara ya mafunzo.



Na Mwandishi Wetu, Transmara Kenya

WAFUGAJI wa Tanzania kupitia Mradi wa Utafiti wa uboreshaji na utunzaji wa Mbari za ng’ombe aina ya Sahiwal wako nchini Kenya kwa ziara ya mafunzo yaliyoratibiwa na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la AU-IBAR.

Wafugaji hao kutoka Umoja wa Wafugaji wa Sahiwal Longido (UWASALO) wamekutana na wafugaji wa Transmara nchini Kenya wanaonufaika na ufugaji kwa kutumia teknolojia ya uhimilishaji na kuhifadhi na uendeleza nyanda za malisho ya mifugo. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea wafugaji wa ng’ombe aina ya Sahiwal katika eneo la Kilgoris -Transmara, nchini Kenya, Mratibu wa Mradi huo wa Sahiwal kutoka Tanzania, Dk. Zebron Nziku amesema ziara hiyo imekuwa na tija kubwa kwa wafugaji wa Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inafanya mageuzi makubwa katika uboreshaji Koosafu za Mifugo.

Dk. Nziku amesema mradi huo tayari umeendesha mafunzo yaliyohusisha wataalam na wafugaji kutoka Halmashauri ya Longido nchini Tanzania kwa ushirikiano na wafugaji wa Transmara nchini Kenya juu ya mbinu bora za uzalishaji na utunzaji wa Sahiwal. 

Alisema lengo la ziara hiyo ni kutoa fursa kwa wafugaji wa Sahiwal kutoka Halmashauri ya Longido nchini Tanzania ambapo mradi huo umetekelezwa kwenda kuona na kujifunza kwa wafugaji wenzao waliofanikiwa kufuga ng'ombe wa aina hiyo kwa muda mrefu nchini Kenya ili kubadilishana uzoefu hasa katika eneo la uzalishaji kwa njia ya uhimilishaji. 

Alisema mradi huo umetekelezwa kwa ushirikiano wa nchi za Tanzania na Kenya kwa lengo la kuelimisha wafugaji, namna bora na rahisi ya kuzalisha na kutunza wa ng'ombe wa Sahiwal kwa ajili ya kuongeza tija kwenye uzalishaji

Dkt. Nziku alisema Sahiwal ni ng'ombe wanaopatikana kwenye nchi zote ndani ya Afrika Mashariki (transboundary breed) na wana uwezo wa kutoa nyama nyingi na maziwa kati ya lita 14-16 kwa siku, hivyo mradi umelenga kuboresha, kuendeleza na kutunza Mbari (breed) za ng'ombe wa Sahiwal ili kuboresha maisha ya wafugaji kupitia mifugo hiyo.

Aliongeza kuwa kwa upande wa Tanzania mradi huu umefanikiwa kununua Madume bora Matatu ya Mbegu za Sahiwal ambayo kwa sasa yamehifadhiwa kwenye Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji NAIC -Arusha kwa ajili ya kutoa mbegu zitakazo wanufaisha wafugaji wengi zaidi nchini. 

MRADI WA MAJI MKURANGA KUHUDUMIA WAKAZI 25,500 UTAKAPOKAMILIKA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA wamekabidhi vifaa vya mradi wa usambazaji maji wa Mkuranga utakaohudumia wakazi 25,500 sawa na asilimia 83.

Akielezea kwa kifupi mradi huo, Mhandisi John Kirecha amesema, wameshamkabidhi mkandarasi na tayari kuanzia kesho ataanza kazi ya ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita Milioni 1.5

Amesema kuwa, mradi huo utakapomalizika utahudumia wakazi 25,500 ambapo kwa sasa jumla ya wakazi 4500 sawa na asilimia 17.6 ndiyo wanaopata maji safi na salama.

Kirecha amesema, tayari vifaa vimeshafika katika na vingine bado vinaendelea kuja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa tanki na ulazaji wa mabomba yatakayosambaza maji kwenye maeneo ya mradi yaliyoanishwa kwenye mradi.

"Mradi huu utakuwa ni wa km 63, na kukamilika kwa mradi huu kutakamilisha asilima 83 za wakazi waliobaki watakaofaidika na huduma ya majisafi na salama,"amesema Kireche.Ameeleza, mkandarasi ataanza kazi kesho ya ujenzi wa tanki, kituo cha kusukuma maji (booster pump), ulazaji wa bomba kuu na mabomba ya usambazaji maji.

Kwa upande wa Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalllah Ulega amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuidhinisha na kupeleka mradi huo katika Jimbo lake sambamba na DAWASA kuja kujenga miundo mbinu itakayowawezesha wananchi kupata maji safi na salama.

Ulega ameeleza kuwa, kwa sasa wananchi wa Mkuranga wanaenda kuondokana na kero ya maji ila amewaomba DAWASA kuangalia na vile vijiji ambavyo vipo karibu na mradi unapoishia kupeleka maji ili nao wanufaike kwa kupata maji safi na salama.

Mradi wa Mkuranga ni moja katika ga miradi sita mikubwa iliyosainiwa juma lililopita na tayari mkandarasi ameenda kwenye eneo la mradi kwa ajili ya kuanza kujenga na kukamilisha kwa wakati.

Maeneo yatakayofaidika na mradi huo ni Mkuranga A, Mkuranga B, Viguza, Mgawa, Njia nne, Bigww, Mkalia kitumbo, Uyoyo na Dundani.
 Mhandisi John Kirecha kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA akimuonesha mabomba ambayo tayari yameshawasili kwa ajili ya Mkandarasi kuanza ujenzi wa mradi wa Mkuranga utakaohudumia wananchi 25,500.
Mhandisi John Kirecha kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA akimuonesha mchoro wa ramani ya mradi wa maji utakaohudumia wananchi wa Mkuranga.

 Mhandisi John Kirecha kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA akielezea kwa ufupi mradi wa maji wa Mkuranga utakaohudumia wakazi 25,500.
 Mbunge wa Mkuranga na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalllah Ulega amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuidhinisha na kupeleka mradi huo katika Jimbo lake sambamba na DAWASA kuja kujenga miundo mbini itakayowawezesha wananchi kupata maji safi na salama.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 13,2019

Viewing all 110019 articles
Browse latest View live


Latest Images