Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110125 articles
Browse latest View live

LUGOLA AAGIZA POLISI KUWAKAMATA WATIA MIMBA WANAFUNZI, WAZAZI WANAOWATUMIA WANAFUNZI SHUGHULI ZA KILIMO, UFUGAJI

$
0
0


WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Karukekere, Jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, leo. Lugola aliwataka wanafunzi hao kupenda masomo na kuacha utoro, na pia aliliagiza Jeshi la Polisi wilayani huko, kuwakamata wazazi wanaowatumia wanafunzi katika shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha masomo yao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akimuhoji Mratibu Elimu Kata ya Namuhura, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda (wapili kushoto), Ibrahimu Kadashali, kuhusu uwepo wa taarifa za wanafunzi watoro, pamoja na wazazi kuwatumia wanafunzi katika shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha masomo yao. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Karukekere, Charles Manyama. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Karukekere, Jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, leo. Lugola aliliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo, kuwakamata wazazi wanaowatumia wanafunzi katika shughuli za kilimo na mifugo na kuwasababishia kukatisha masomo yao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA PIRAMIDS MISRI

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy, wakati alipotembelea Piramidi mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (katikati) Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishika jiwe lililotumika kujengea Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa amepanda juu ya Piramidi, akionesha jambo wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ndani ya Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa anashuka kwenye Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo, baada ya kutembelea Piramidi, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa za wajasiriamali, baada ya kutembelea Piramidi, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitembea nje ya Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy, wakati alipotembelea Piramidi hizo mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mbarawa awataka maafisa wa maji kusimamia rasimali kwa uadilifu

$
0
0

Na Charles James, Michuzi TV

Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa amefungua mkutano wa saba wa Bodi za Maji za Mabonde unaofanyika Ujiji mkoani Kigoma na kuzindua taarifa ya faida na changamoto za ushirikiano na usimamizi wa rasimali za maji Shirikisho pamoja na taarifa za rasimali za maji.

Mkutano huo ni sehemu ya utaratibu wa Wizara ya Maji kufanya mikutano ya pamoja ya usimamizi wa rasimali za maji kila mwaka kwa kuwakutanisha wataalamu wa sekta ya maji ili kujadili na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za sekta ya maji nchini na kikanda kwa Mabonde ambayo ni shirikishi.

Katika mkutano huo Prof Mbarawa amewataka wenyeviti na maafisa maji wa bodi za maji na mabonde kusimamia kikamilifu rasimali za maji kwa uadilifu, kudhibiti uchafuzi na kuhakikisha matumizi sahihi ya maji kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

Prof Mbarawa  amesema ili Taifa lifike katika uchumi wa kati na mapinduzi ya viwanda ni lazima kuwa na rasimali za maji za uhakika

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA HIFADHI YA TAIFA YA BURIGI CHATO MKOANI GEITA

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla pamoja na viongozi wengine wakivuta  utepe kuashiria uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali, Wakuu wa mikoa, Viongozi wa Vyama vya Siasa, Dini pamoja na Mabalozi mara baada ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Chato kabla ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mara baada ya kumkabidhi Hundi ya Shilingi milioni kumi , kama shukrani katika mchango wake alioutoa katika utunzaji wa wa hifadhi mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi wa TANAPA wakati akielekea kwenda kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kuzindua Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
 Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu wakijadiliana jambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa  sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Kikosi cha Jeshi Usu la kukabiliana na vitendo vya Ujangili pamoja na kulinda hifadhi za taifa kabla ya kuanza kwa  sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi (Burigi  -Chato National Park) ilioyopo Chato mkoani Geita.
 Kikosi cha Jeshi Usu cha kukabiliana na Vitendo vya Ujangili pamoja na kulinda hifadhi za Taifa kikipita mbele ya  Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya ukaguzi katika sherehe hizo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Tuzo ya Hifadhi bora ya Serengeti ambayo imekuwa ya kwanza katika Bara la Afrika kwa mwaka 2019 kutoka kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia sanamu ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yenye ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya wanyama pori.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumkabidhi Sanamu hiyo ya Baba wa Taifa. Rais Dkt. Magufuli ametoa maelekezo kuwa Sanamu hiyo aliyokabidhhiwa ijengewe eneo zuri katika hifadhi hiyo ya Burigi Chato ili watalii wakija waweze kumjua zaidi Muasisi wa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI KILICHOANDALIWA NA RAIS WA NIGER

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhutri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuzungumza na Rais Emmason Nangagwa wa Zimbabe walipokutana kwenye Hafla ya Chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Rais Mahamadou Issoufour wa Niger, kwenye mkutano wa 12 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)uliojadili kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika AfCFTA uliofanyika mjini Niamey Nchini Niger. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Gabriel Antonio Tshekedi wa Congo walipokutana kwenye Hafla ya Chakula cha Jioni kilichoandaliwa na Rais Mahamadou Issoufour wa Niger, kwenye mkutano wa 12 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)uliojadili kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika AfCFTA uliofanyika mjini Niamey Nchini Niger. 
Makamu wa Rais wa Jamhutri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania aliouongoza kushiriki mkutano wa 12 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)uliojadili kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika AfCFTA uliofanyika mjini Niamey Nchini Niger, kwenye mkutano huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Miili 5 ya wafanyakazi wa Azam Media waliofariki kwa ajali yaagwa leo Jijini Dar es salaam.

$
0
0

Na.Vero Ignatus,Dar.

Miili ya wafanyakazi 5 wa Kampuni ya Azam Media waliopata ajali katika eneo la Kisonzo katikati ya eneo la Igunga (Tabora) na Shelui (Singida)imeagwa leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waandishi wa hanari wa vyombo mbalimbali,Viongozi wa Serikali,viongozi wa vyama vya siasa,Dini na wananchi kwa ujumla.

Akitoa salam za rambirambi katika msiba huo mzito ulilolikumba Taifa ,Waziri wa Habari,Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Harison Mwakyembe amekemea tabia ya baadhi ya watanzania wanaopiga picha kajali inapotokea na kuzirusha kweye mitandao ya kijamii ambapo amesema Serikali imetoa onyo la mwisho na haitalisemea tena.

Dkt.Mwakyembe amewataka Watanzania kuwa na utu bila kushurutishwa na sheria kwani Sheria ya makosa ya mtandao hairuhusu jambo kama hilo kwani hakuna faida yeyote anayoipata mtu kwa kupiga picha za miili ya watu waliokufa.

"Hebu tuendeleze utamaduni na utu bila kushurutishwa na sheria ,acheni tabia ya kurisha picha za watu waliofariki kwenye ajali na kurusha kwenye mitandao,sheria ya makosa ya mitandao inakataza tutakufunga,hili ni onyo la mwisho hatutasema tena kuanzia hapa"akisisitiza Mwakyembe.

Hamad Masauni ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema kampuni ya Azam imekua ikishirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kutoa elimu kuhusiana na maswala ya usalama na watumiaji.wa barabara.

"Sisi ni miongoni mwa waathirika wakubwa kutikana na kuondokewa na vijana hawa"Jeshi la polisi tayari limeshaanza uchunguzi kuhusiana na ajali hiii na uchunguzi huo unaendelea vizuri na tayari tumeshamkamata dereva wa lori aliyesababisha ajali"Amesema Masauni

Mhe.Masauni ametoa wito kwa watumiaji wa barabara kuendelea kuwa watiifu na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwani jeshi la polisi litaendelea kusimamia sheria za usalama barabarani siyo kwa nia ya kumkomesha yeyote bali kwa kuokoa maisha ya Watanzania.

Mhandisi James Kilaba ni Mkurugenzi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

(TCRA) amesema wao kama wadau wa habari wanaifahamu michango mikubwa ya vijana hao kwani hata wiki iliyopita walikuwa wakifanya nao kazi hivyo ameitaka Azam Media kutokukata tamaa bali waendelee kufanya kazi maana hiyo ni safari ya wote.

Kwa upande wake msemaji muwakilishi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) umesema wameupokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa ambapo waliokatishwa maisha ni vijana na hiyo ni changamoto isiyoepukika kwa ni ratiba ya kila mwanadamu kupitia njia ya kifo.

Mwenyekiti wa Baraza la Wahariri nchini Nevil Meena aliyewakilishwa ndugu Balile amesema matukio hayo yanamkumbusha kila mmoja kukesha maana hatujui kwani hakuna ajuae siku wala saa ya kuondoka duniani huku akisisitiza madereva kuzingatia kuwa mwendo kasi unaua,unaleta hasara ,kwa masikitiko makubwa kwa Taifa.

Rose Ruben ckutoka Tamwa amesema wamekuwa mstari wa mbele na wadau wakubwa wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani na kuepuka ajali za kujitakia."Athari ya kuwapoteza vijana hawa hatutaiona leo ila baada ya miaka 20 ndipo itaonekana kwani vijana hawa wabgeliwafundisha wengine kazi na wakazaliwa watendaji wengi zaidi hii ni huzuni kubwa "alisema

Amewasihi watumiaji wa barabara kuwa makini wakichukua taharhari kubwa kwani ajali zinapoteza nguvu kazi ya Taifa,zinaleta Ulemavu wa kudumu ,na vifo visivyotarajiwa.Tanzania,tumepoteza vijana kwenye kazi chombo cha habari hakipelekwi kama hawana umahiri na usahihi,katika kazi za utangazaji hatuna wataalam wa kutosha na ni pigo kubwa,waandishi waliobakia wawaenzi vijana hawa ili tasnia iendekee kukua.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Telebisheni ya Taifa Ndugu Rhioba ametoa pole kwa Azam Media huku akisema Vijana hao waliopoteza maisha kuna nyakati walisharusha matangazo yaliyonufaisha TBC hivyo Taifa limepoteza nguvu kazi .

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo mchini Haikael Mbowe amewaomba wale wote wanaomiliki vyombo vya habari wasiruhusu vyombo hivyo kuwagawa naomba badala yake watumieni vyombo hivyo kwa weledi na kwa ulinganifu.

Tido Mhando ni Afisa mtendaji mkuu wa Azam media akitoa neno la shukrani salamu za rambirambi amewashukuru watanzania na wanahabari kwa kuwapatia lugha ya faraja kwani walipata taarifa hizo za msiba kutoka kwa wasamaria wema walioona ajali hiyo.

Amesema kwenye gari hiyo walikuwepo wafanyakazi 8 walikuwa wakielekea Chato kwenye kazi ya uzinduzi ilikuwa ifanyike leo kwani wamekuwa wakipata mialiko mingi za kazi za Kitaifa. 

Amesema wafanyakazi hao walikuwa wapo safarini kutoka Dar es salaam kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Bugiri -Chato kwaajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hiyo leo.

Majina ya waliopoteza maisha yao ni pamoja na Charles Wandwi (1980)Florence Bitaliho Ndibalema (1989)Said Haji Hassan (1989)Salum Juma Mhando (1985) Silvanus Waziri Kassongo.(1989)

Tanzania Kuendelea Kunufaika Kiuchumi na SADC

$
0
0

Katibu Mkuu mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Mussa Uledi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 
Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari- MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. 

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi katika kuandika na kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayoendelea mjini Morogoro leo Julai 9, 2019 ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo Bi Nelly Mtema akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofunguliwa Julai 8, 2019 na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza..(Picha zote na Abubakari Kafumba, MAELEZO- Morogoro) 
………………… 

Na Frank Mvungi- MAELEZO- Morogoro 
Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Mussa Uledi amesema kuwa Tanzania inanufaika kiuchumi kama mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na jumuiya nyingine ambazo Tanzania ni mwanachama. 

Akizungumza wakati akiwasilisha mada leo mjini Morogoro ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo kwa waandishi wa habari ya kuwajengea uwezo wa kuandika na kuripoti habari za SADC, Bw. Uledi amesema kuwa nchi yetu imenufaika na utekelezaji wa miradi ya miundomnbinu, biashara, uwekezaji na viwanda. 

“ Mkakati wa maendeleo wa SADC unafafanana kwa kiwango kikubwa na ule wa Tanzania ambao pia unazingatia haja ya utekelezaji wa viwanda na miundombinu hapa nchini hali itakayochangia katika kuimarisha maendeleo na kukuza uchuni na ustawi wa wananchi” Alisisitiza Bw. Uledi 
Akifafanua amesema kuwa vipaumbele vya Tanzania vimejikita katika upanuzi wa Mauzo nje na uongezaji wa michepuo yake lengo likiwa ni kukuza na kuendeleza biashara hali inayowezesha uendelezaji wa viwanda vya kuongeza thamani katika malighafi za ndani hususan mazao ya kilimo na madini. 

Aliongeza kuwa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli katika baadhi ya nchi wanachama wa SADC imeonesha kuwa Tanzania imejipanga vizuri kimkakati inaweza kuwa ghala la Chakula kwa kukuza zaidi uzalishaji kuendana na mahitaji katika soko la jumuiya hiyo na hata nje ya jumuiya. 

Alitaja vipaumbele vingine kuwa ni pamoja na uendelezaji miundombinu kama barabara, reli, usafiri wa anga, uzalishaji na usambazaji huduma za umeme ambayo ni nyenzo muhimu sana katika kuyaunganisha masoko ya nchi wanachama wa SADC. 

Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni utafutaji wa rasilimali na utekelezaji wa miradi ya Kikanda kwa kuundwa kwa kikosi kazi cha Mawaziri wenye dhamana ya Fedha na uendelezaji miundombinu, Amani na Usalama umeendelea kuimarika ndani ya SADC. 

Tanzania inatarajiwa kuleta msukumo mpya kwa nchi wanachama wa SADC katika utekelezaji wa miradi na program za maendeleo za Jumuiya hiyo kwa kuwa itakuwa na dhamana kubwa ya kukidhi matarajio makubwa ya nchi wanachama wakati wote wa uenyekiti wake. 

Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni na Mafunzo, Brigedi ya Magharibi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kanali Wilbert Ibuge akiwasilisha mada katika mafunzo hayo amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa Barani Afrika zilizotoa mchango mkubwa na kuratibu kuanzishwa kwa mtangamano wa SADC. 

“Hadi sasa hali ya amani na usalama imeendelea kuimarika katika SADC kama inavyojidhihirisha kwa takribani nchi zote za SADC ambapo nchi wanachama ziliazimia kusimamia maendeleo ya kiuchumi ya Kanda kwa kuzingatia malengo ikiwemo kukuza uchumi, kuondoa umasikini, kuboresha hali ya maisha ya wananchi. 

Msingi wa SADC ni kusimamia malengo yake ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii sambamba na yale ya ulinzi na usalama unabainishwa katika Ibara ya 2 ya mkataba wa SADC ( Article 2 of SADC Treaty).

MAFUNZO YA MSASA UWEZESHAJI MASHAMBA DARASA KWA MAAFISA VIUNGO NA MRADI YAENDELEA MJINI MOROGORO

$
0
0
Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa Viungo wa Mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini (ldfs) yameendelea leo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo mkoani Morogoro ikiwa ni siku ya pili.
Pichani washiriki wa mafunzo hayo wakijadili masuala ya mabadiliko ya tabia nchi katika makundi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

KAMATI YA BAJETI YA CPA KANDA YA AFRIKA YAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Makamu Mwekahazina wa CPA-Kanda ya Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Uganda akiongoza kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama hicho. Wa kwanza kushoto kulia ni Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi na wa kwanza kulia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. Stephen Kagaigai. Wengine katika picha ni Wajumbe na Sekretarieti ya Kamati hiyo. 
Makamu Mwekahazina wa CPA-Kanda ya Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Uganda akiongoza kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama hicho. Wa kwanza kushoto kulia ni Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi na wa kwanza kulia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. Stephen Kagaigai. Wengine katika picha ni Wajumbe na Sekretarieti ya Kamati hiyo. 
Makamu Mwekahazina wa CPA-Kanda ya Afrika ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Uganda akiongoza kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama hicho. Wa kwanza kushoto kulia ni Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi na wa kwanza kulia ni Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. Stephen Kagaigai. Wengine katika picha ni Wajumbe na Sekretarieti ya Kamati hiyo.
Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi (kushoto) akisalimiana na Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. Stephen Kagaigai kabla ya kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kilichofanyika Ofisi Ndogo za Bunge la Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi (kushoto) akimueleza jambo Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. Stephen Kagaigai kabla ya kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kilichofanyika Ofisi Ndogo za Bunge la Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Kenya Mhe. Justin Muturi (wa kwanza kulia) akizungumza na Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. Stephen Kagaigai (wa kwanza kushoto) kabla ya kikao cha Kamati ya Bajeti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kilichofanyika Ofisi Ndogo za Bunge la Tanzania Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Wasaidaizi wa Viongozi hao. 

PICHA NA BUNGE

JAMII YA KIMASAI YAASWA KULINDA NA KUDUMISHA MILA ZILIZOTAGULIA RIKA NYINGINE

$
0
0
KATIBU mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt Bashiru Ally ameitaka jamii ya kimasai kulinda na kudumisha mila zilizotangulia rika zingine.

Dkt Bashiru aliyasema hayo wakati wa sherehe za kimila za jamii ya kimasai zijulikanazo kwa jina la Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja mmmoja kilichopo kata ya Sepate ambapo alisema kuwa mila hizo ninzuri zinaandaa vijana katika nizamu ,heshima huku akiwataka vijana hao wa rika la nyangulo lina kazi kubwa ya kulinda uhuru wa nchi yetu.

Alichukuwa muda huo kuwapongeza viongozi wajamii ya kimasai kwa kurekebisha mila zote mbaya ambazo zilikuwa zinaenda kinyume na tamaduni za mtanzania pamoja na kurekebisha mila zote zilizopitwa na wakati.

"napenda kuwasisitiza nizamu ni jambo linalopaswa kuenziwa na kufuatwa kama mlivyofundishwa na wazee wa marika makubwa waliowatangulia ,pia swala la ulinzi ni muhimu na lazima nanivyema tuheshimu rasilimali za watu wote na labda nisisitize naniwaambie bado tunakazi sana katika swala la aridhi na hii nivita kubwa ambayo tunayo na nilazima tuwe na mipango mikubwa mizuri yakuitumia ili tuweze kuilinda aridhi yetu"alisema Dkt Bashiru

Akiongea katika mkutano huo mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa wao kama viongozi wa serikali walishatatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili wananchi wa wilaya ya Monduli hususa ni ya ardhi na wataendelea kutatua migogoro yote ambayo itajitokeza kwa wananchi hao .

Alibainisha kuwa katika kutetea maslahi ya jamii ya wafugaji ,wao kama serikali pia wanaweka ulinzi katika maeneo ya malisho ya mifugo ili yasiporwe au yasivamiwe.

kwa upande wake mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Amina Mollel aliwataka jamii hio ya kimasai kuendelea kupiga vita swala la ukeketaji wa mabinti pamoja na ndoa za utotoni kwani maswala hayo yote ni mabaya na ukiukaji wa sheria za nchi,alitumia muda huo kuwaasa wananchi hao kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kujisaidia hapo baada na kuwa viongozi wasomi wa hapo baadae .

MFUMO WA UTOAJI TAARIFA SHULE ZA MSINGI WASAIDIA KUPUNGUZA UTORO KWA WANAFUNZI

$
0
0

Moureen Rogath, Buhigwe. 

Mfumo wa utoaji taarifa katika shule za msingi(Shool Information System), umesaidia kupunguza utoro wa wanafunzi katika shule ya msingi Biharu wilayani hapa mkoani Kigoma.

Akizungumza mwalimu mkuu wa shule hiyo Medani Yohana alisema walipokea Kishwambi(Tablet) kutoka Mpango wa Kuinua Elimu ya Msingi(Equip), kwaajili ya kuendeleza mfumo wa takwimu katika shule mbalimbali.

Alisema mfumo huo umewarahisishia kukusanya taarifa za wanafunzi kwa kuongezeka kwa mahudhurio kutoka asilimia 70 kabla na baada kufikia asilimia 95 ya wanafunzi hali iliyopelekea kupunguza utoro katika shule hiyo.

“Baada ya kupata Kishwambi katika shule yetu tuliwapa elimu waalimu jinsi ya kutumia na kupeleka taarifa Wizarani kwa wakati ukitofautisha na awali ambapo tulikuwa tukitumia madaftari kuhifadhia taarifa hali iliyosababisha kutokufika kwa wakati,”alisema Yohana.

Mwalimu wa shule hiyo Andrea Charukula alisema kifaa hicho kimerahisisha ukusanyaji wa taarifa na kwamba serikali iweze kusambaza vifaa hivyo kwa shule zote nchini kwani itasaidia kupunguza changamoto wanazokutana nazo.

Naye mzazi mwenye mtoto katika shule hiyo Alphonce Kamlenga, alisema walipata muamko wa kuwasimamia watoto wao kufika shule bila kukosa na kupunguza utoro kwa baadhi ya awaalimu.

Equip wametoa vishkwambi (Tablet), 20 kwa waratibu elimu kata na 88 kwa waalimu wakuu wa shule za msingi wilayani Buhigwe lengo likiwa ni kuendeleza mfumo wa takwimu katika shule hizo.
Waalimu wa shule hiyo wakiwa na mwalimu mkuu wakiangalia kishwambi (Tablet)waliyopewa katika kuendeleza mfumo wa takwimu katika shule yao.

NAIBU WAZIRI AWESO AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI WAHANDISI WAWILI RUWASA

$
0
0
Moureen Rogath, Kigoma 

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amemuagiza Naibu katibu Mkuu wa wizara ya maji mhandisi Emmanuel Kalobelo, kuwasimamisha kazi wahandisi wawili wa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA). 

Akizungumza leo katika mkutano wa saba wa Mwaka wa bodi za maji za mabonde, uliofanyika mjini hapa mkoani Kigoma, wahandisi hao ni Elinathan Elisha wa wilaya ya Kakonko na Godfrey Mbuza wilaya ya Kasulu. 

Amesema wahandisi hao wamekuwa sababu ya kukwamisha miradi ya maji katika wilaya hiyo hali iliyosababisha wananchi kushindwa kupata huduma za maji katika maeneo yao. 

"Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika miradi mbalimbali ya maji nchini lakini wapo baadhi ambao wamekuwa wakikwamisha jitihada hizo hali na kuwaumiza wananchi," amesema Aweso.

Aweso amesema zaidi ya kampuni 30 zilizojenga miradi ya maji chini ya kiwango nchini zitabainishwa na hawatapewa miradi yoyote ya maji ili iwe fundisho kwa kampuni nyingine zinazojenga miradi chini ya kiwango.

Amewataka ofisi za mabonde kuhakikisha inakomesha vitendo vya uchafuzi wa rasilimali na vyanzo vya maji katika mabonde na hasa kudhibiti viwanda vinavyotiririsha uchafu kwenye vyanzo vya maji.Naibu katibu mkuu wa wizara ya maji, Mhandisi Emanuel Kalobelo alisema usimamizi wa rasilimali za maji bado ni changamoto kubwa katika wizara hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali mstaafu Emanuel Maganga amewataka wavuvi wanaovua ziwa Tanganyika kuacha kutumia sumu kupata samaki kwani ni hatari kwa watumaji wa maji.

Ameagiza ofisi za bonde kutoa elimu kwa wananchi juu ya utaratibu wa kuchimba visima na mabwawa kwa kufuata utaratibu ikiwa ni pamoja na kupata vibali kutoka ofisi za bonde katika eneo wanapoishi.

Mkutano huo wa siku mbili utajadili masuala ya rasilimali za maji na kutoa maazimio yatakayosaidia kuboresha miundombinu na rasilimali za maji ili kuwa endelevu.
Wadau wa maji wakiwa katika mkutano wa saba wa mwaka wa bodi za mabonde ,uliofanyika mjini Kigoma leo .

SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA SH. BILIONI MOJA KUTOKA TPB BANK

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni moja kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB, Dkt. Edmund Mdolwa katika hafla ya kupokea gawio hilo jijini Dodoma. Benki ya Posta imetoa gawio hilo ikiwa ni faida iliyopatikamna mwaka 2018.
Mkurugenzi wa Benki ya Posta Nchini (TPB) Bw. Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa kukabidhi gawio kwa Serikali. Benki hiyo imetoa gawio la Sh. Bilioni moja kwa Serikali ikiwa ni gawio kutokana na faida ya mwaka 2018. Anayefuatia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Dkt. Edmund Mdolwa. Hafla hiyo imefanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB, Dkt. Edmund Mdolwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh. Bilioni moja kwa Serikali, hafla hiyo imefanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) (kushoto), akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya TPB, Dkt. Edmund Mdolwa (katikati) na Mkurugenzi wa Benki ya Posta Nchini (TPB) Bw. Sabasaba Moshingi baada ya hafla ya kupokea gawio la Sh. Bilioni moja lililotolewa na Benki ya TPB, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya watendaji wa Benki ya TPB na Wizara ya Fedha na Mipango mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupokea Gawio toka Benki hiyo jijini Dodoma. Benki ya TPB imetoa Gawio kwa Serikali kiasi cha shilingi bilioni moja ikiwa ni gawio kutokana na faida ya mwaka 2018.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).



Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali imepokea gawio la Shilingi Bilioni 1 kutoka Benki ya Posta Tanzania (TPB) linalotokana na faida ya uwekezaji wake wa asilimia 83 ya hisa katika Benki hiyo katika mwaka wa fedha 2018/19.

Hafla ya makabidhiano ya Hundi kifani ya gawio hilo imefanyika jijini Dodoma, kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ambaye alipokea kwa niaba ya Serikali, naMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo Dkt. Edmund Mndolwa.

Akizungumza katika hafla hiyo Dkt. Mpango aliipongeza Benki hiyo kwa kutoa gawio kwa Serikali, na kuahidi kuwa fedha hizo zitatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

“Utoaji huu wa gawio ni kiashiria tosha kwa Serikali kuwa Benki inazidi kukua na kuwapa moyo watanzania na wawekezaji kuwa TPB inatoa huduma bora katika jamii”, alisema Dkt. Mpango.

Aliitaka Benki hiyo kuongeza wigo wa utoaji huduma ili kuwafikia wananchi hususani waishio vijijini pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hao kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, kukopa sambamba na kurejesha mikopo kwa wakati.

“Riba katika benki zetu bado ni kubwa taasisi za fedha zione namna ya kuzipunguza sambamba na kutoa mikopo kwa kuzingatia kanzidata ya wakopaji ili kuepuka mikopo chechefu.”, alisisitiza Dkt. Mpango.

Aidha, Dkt. Mpango ameiagiza Benki hiyo kuendelea kuwapa wanawake kipaumbele katika upatikanaji wa huduma za fedha na mikopo ili waweze kuendesha shughuli za maendeleo.

Pia Dkt. Mpango aliiagiza TPB kusimamia uadilifu kwa watumishi wake na kuwa makini na kutoa taarifa za miamala yenye mashaka ili kuzuia utakasishaji wa fedha haramu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Dkt. Edmund Mndolwa alisema kuwa gawio hilo ni sehemu ya faida ya Sh. Bilioni 17.2 kabla ya kodi ambayo Benki yake imeipata katika mwaka wa fedha 2018/19. Pia ameeleza kuwa Benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora ili kukidhi mahitaji ya wanahisa wake na wananchi kwa ujumla.

Aidha, Dkt. Mndolwa aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa utendaji mzuri ambao umeiwezesha Benki hiyo kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kuahidi kuendelea kushirikiana nayo ili kukuza uchumi wa nchi.

KATIBU MKUU JUMUIYA YA MADOLA AKUTANA NA PROF. KABUDI LONDON,UINGEREZA

$
0
0
Jumuiya ya Madola imeonesha kuridhishwa na namna Tanzania inavyotekeleza mageuzi ya kiuchumi,uwajibikaji na uawala bora kwa wananchi wake jambo ambalo jumuiya hiyo inalihimiza na kulisimamia kwa Nchi wanachama wake.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za sekretarieti ya jumuiya hiyo zilizopo London Nchini Uingereza.

Katika mazungumzo hayo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Scotland ameeleza kuridhishwa na maelezo yaliyotolewa na Prof. Palamagamba John Kabudi kuhusu utekelezaji wa masuala ya demokrasia,utawala bora na utawala wa sheria pamoja na Haki za binadamu nchini Tanzania na kwamba Jumuiya hiyo inatambua juhudi hizo na inaunga mkono hatua hiyo.

Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa mbali na kuhimiza utekelezaji wa utawala bora,haki za binadamu na utawala wa sheria pia Jumuiya ya Madola imelenga kukuza na kuwezesha biashara miongoni mwa nchi wanachama ikiwa ni pamoja na fursa zilizopo kupitia shirika la biashara la kimataifa (WTO) na mashirikiano ya biashara ya kikanda. 

Amesema ni jukumu la nchi za Jumuiya ya Madola kuhakikisha uwepo wa amani na utulivu katika jumuiya hiyo ili kuiwezesha kupiga hatua za haraka za kimaendeleo na kuifanya Jumuiya nzima kuendelea bila ya kuacha nchi nyingine nyuma kutokana na uwepo wa migogoro ama machafuko ya wenyewe kwa wenyewe miongoni mwa wanachama wa Jumuiya. Katika hili ameisifia Tanzania kwa kuwa na Amani na utulivu muda wote na pia kushiriki katika juhudi za kutatua migogoro kwa nchi zingine wanachama na wasio wanachama wa Jumuiya.

Kuhusu suala la mabadiliko ya tabia nchi,Katibu Mkuu huyo wa jumuia ya madola amesisitiza umuhimu wa ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi. Ameeleza kuwa Jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika program mbalimbali zinazolenga kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya mazingira kwa ujumla.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba John Kabudi amemhakikishia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuwa Tanzania inaipa umuhimu mkubwa jumuiya hiyo na itaendelea kushirikiana nayo katika masuala ya ukuzaji wa uchumi, utawala bora hususani wakati huu ambapo Tanzania inafanya mageuzi ya kiuchumi katika kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.

Ameipongeza jumuiya ya madola kwa mpango maalum inayoandaa kwa ajili ya kukuza na kuongeza biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine wanachama wa jumuiya hiyo kwa ujumla jambo ambalo litafungua fursa biashara na masoko kwa bidhaa na mazao ya Tanzania. Amemuahidi Katibu Mkuu huyo kuwa Tanzania itashiriki ipasavyo katika mpango huo.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Kabudi pia amekubaliana na Bi Scotland kuangalia namna ya kuwasaidia vijana kuongeza ubunifu ili waweze kujiajiri na kuimarisha uchumi ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana huku akimpongeza Katibu Mkuu huyo kwa mageuzi makubwa anayoyafanya ndani ya jumuiya hiyo ili iweze kuwahudumia wanachama wake kwa ufanisi zaidi.

Profesa Palamagamba John Kabudi yuko London Nchini Uingereza kwa ziara ya siku nne kuhudhuria mkutano wa Mawaziri wa mambo ya Nje wa Jumuiya ya madola pamoja na mkutano wa Kimataifa kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.
 Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) alipomtembelea katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro. July 9, 2019.
 Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akisalimiana na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. July 9, 2019. 
  Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. July 9, 2019
 Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza. July 9, 2019. 
 Katibu Mkuu wa jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland akimsindikiza mgeni wake ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) alipomtembelea katika ofisi za Sekretarieti za jumuiya hiyo zilizopo London,Uingereza.July 9, 2019.

ZAIDI YA MADEREVA BODA BODA100 WAPATIWA KOFIA NGUMU ARUSHA

$
0
0
Na Woinde shizza Michuzi Tv

Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Themi ,jijini hapa kimewawezesha Kofia Ngumu Madereva pikipiki ( bodaboda) wapatao 100 kwa lengo la kuwanusuru na ajali zisizozalazima ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kupunguza nguvukazi ya taifa.

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara wa chama hicho,Mwenyekiti wa CCM kata ta Themi,Thomas Munisi amesema mpango huo umelenga kuondoa changamoto ya kutokuwa na kofia ngumu na kusababisha baadhi ya waendesha pikipiki kukamatwa na askari wa usalama barabarani.

Hatua hiyo iliibuka katika zoezi la kufungua mashina katika kata hiyo, ambapo baadhi ya vijana walionyesha kuwa na changamoto ya ukosefu wa kofia ngumu jambo ambalo chama hicho kililazimika kuwafadhili kupitia mpango wake wa kuwezesha vijana na kuwapatia kofia hizo.

Baadhi ya waendesha pikipiki, Elisha Mbise na simon Swai wamekishukuru chama cha mapinduzi kata ya Themi kwa kuwawezesha kupata kofia ngumu wakidai kwamba zitawasaidia sana katika kujikinga na ajali wakati wakitekeleza mahukumu yao.Katika hatua nyingine Munisi amewaonya wanachama wa chama hicho kuacha kuwabeba baadhi ya wagombea wa CCM kwa maslahi yao kwa kuwa chama hicho kinamfumo mpya wa kupata viongozi wake.

Aidha aliwataka wanachama kuacha tabia ya kutembea na majina ya wagombea mfukoni kwa kuwa kila mwanachama anayetaka kugombea anapaswa kuja ofisini kuchukua fomu.

" ule uongozi wa zamani wa kila mwanachama kuwa na viongozi wake mfukoni kwa sasa hilo halipo na tukigundua kuna mgombea yoyote anatumua wanachama wetu kutaka uongozi tutamfyekelea mbali"Amesema Munisi.

Wakati huo huo Munisi alisema CCM imefanikiwa kuwanyakua baadhi ya wafuasi wa chadema wanaokihama chama hicho akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika kata hiyo,Elias baada ya kuridhishwa na utendaji Kazi wa CCM chini ya mwenyekiti wake Taifa,Dkt John Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM kata ta Themi,Thomas Munisi 

IGP SIRRO AKAGUA MRADI WA NYUMBA ZA ASKARI GEITA

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amekagua mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa Jeshi hilo zinazojengwa katika eneo la Magugu mkoani Geita, mradi unaotekelezwa kutokana na fedha iliyotolewa na Mhe. Rais John Magufuli. 

Katika ukaguzi huo IGP Sirro mesema kuwa, hadi sasa maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo umefikia katika hatua nzuri na kwamba amewaomba wadau wengine welevu kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuendelea kuboresha makazi ya askari jambo ambalo litasaidia kuwajengea morali wakati wanapotimiza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Wananchi Wajitokeza Kufungua Akaunti Banda la Benki ya Mkombozi Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

$
0
0
 Meneja wa Huduma za Benki za Kidijitali wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Boniface Thomas (kushoto), akimkabidhi kadi ya akaunti ya akiba mteja mpya Bi. Lusia Benson alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NAPHILEMON SOLOMON

 Meneja wa Huduma za Benki za Kidijitali wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Boniface Thomas (kushoto), akimkabidhi zawadi ya tisheti Bi. Vitoria Silayo  baada ya kufungua akaunti ya akiba  alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’Jijini Dar es Salaam (katika) Meneja Mikopo wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Andrew Chimazi. 
 Afisa Masoko wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Antony Munyambo (kushoto), akimkabidhi kadi ya akaunti ya akiba mteja mpya Bi. Lucy Peter alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’Jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Huduma za Benki za Kidijitali wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Boniface Thomas (kushoto), akimkabidhi kadi ya akaunti ya akiba mteja mpya Bi. Jesinta  Benson alipotembelea banda la benki hiyo katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mikopo wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Andrew Chimazi (kulia), akimuonesha  Bi. Victoria Silayo kipeperushi chenye maelezo ya huduma za kibenki alipotembelea banda hilo kwaajili ya kufungua akaunti maalumu ya akiba .katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’Jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uendeshaji wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Erick Musiba (kulia),akiwaonesha wananchi kipeperushi chenye maelezo ya MWANA ACCOUNT kwa ajili ya watoto walio na umri chini ya miaka kumi na nane, inayomuwezesha mzazi kuweka akiba kwa ajili ya watoto ili kuwajengea tabia ya kujiwekea akiba wanapofikia umri wa kujitegemea.
 Meneja Mikopo wa Benki ya Biashara Mkombozi Bw. Andrew Chimazi (kushoto), akimuelezea mwananchi kuhusina na akaunti ya bima alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’Jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja.

WAKULIMA WA MAHINDI NCHINI WASHAURIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA RAHISI

$
0
0
Wakulima wa Mahindi nchini wameshauriwa kutumia teknolojia rahisi na ya asili ya Vuta-Sukuma inayohusisha upandaji wa nyasi maalum na mimea jamii ya mikunde katikati na pembeni ya mazao ili kukabiliana na funza wa mabua ya nafaka na magugu hatari aina ya Kiduha ambayo yamekuwa yakifyonza madini na lishe iliyopo kwenye mimea na kuidumaza.

Hayo yameelezwa na Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kudhibiti visumbufu vya mimea kwa njia ya kibailojia Kibaha, kilichopo chini ya kitengo cha Afya ya Mimea, chini ya Wizara ya KIlimo,Chakula na Ushirika, Msami Elibariki, wakati akizungumza na wakulima wadogo wa wilaya ya Morogoro kwenye maonesho ya Kilimo ya wilaya hiyo.

Elibariki amesema Teknolojia hiyo ya Vuta-Sukuma inayotumia upandaji wa mimea jamii ya mikundekunde ijulikanayo kitaalamu kama Desmodium katikati ya mistari ya mahindi shambani, na nyasi aina ya mabingobingo (Black area ) ambayo huoteshwa pembeni kuzunguka shamba la mahindi na imekuwa ikisaidia pia kupatikana kwa malisho ya mifugo ambapo kama jamii yote mbili ya mimea ikitumiwa kwa kuchanganywa, husaidia ongezeko la upatikanaji wa maziwa toka kwa ng’ombe, mbuzi na kondoo.

Teknolojia hiyo ambayo kwa hapa nchini inatekelezwa na kituo cha kimataifa cha Physiolojia na Ikolojia ya wadudu (International Centre for Insects Physiology and Ecology -ICIPE) chenye makao yake makuu Nairobi nchini Kenya, imekuwa na Usimamizi wa kudhibiti wadudu waharibifu kwenye mazao ya Mahindi, Mpunga na Njegere kubwa (Chickpea), kwa nchi za Afrika Mashariki za Kenya,Ethiopia na Tanzania kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la Misaada la Watu wa Marekani USAID.

Meneja Programu na Utawala kutoka ICIPE Nebiyu Solomon, wanaotekeleza mradi huo akasema umeanza kutekelezwa tangu mwaka 2016 kwa nchi za Kenya, Ethiopia na Tanzania kwa kuanza na Morogoro, amesema kutokana na gharama kubwa ya mbegu hizo, wamewawezesha wakulima kuzipata bure kwa kuanzia ili waweze kuzipanda na kusambaziana, na akawahimiza wazalishaji wa mbegu kutumia fursa hiyo kuzalisha kwa wingi mbegu hizo ambazo zilizoletwa nchini zikitokea nchini Australia, ili kurahisisha upatikanaji wake.
Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kudhibiti visumbufu vya mimea kwa njia ya kibailojia Kibaha, Msami Elibariki,  akizungumza na wakulima wadogo wa wilaya ya Morogoro
Msami Elibariki,  , Afisa Mfawidhi wa Kituo cha kudhibiti visumbufu vya mimea kwa njia ya kibailojia Kibaha, akizungumza na wakulima juu ya magonjwa ya mimea.
Teknolojia ya Vuta-Sukuma  inayotumia upandaji wa mimea jamii ya mikundekunde ijulikanayo kitaalamu kama Desmodium katikati ya mistari ya mahindi shambani, na nyasi aina ya mabingobingo (Black area ) ambayo huote

TBS Yateketeza Tani Mbili za Bidhaa Zilizopigwa Marafuku mkoani Arusha.

$
0
0
Baadhi ya Bidhaa zilizopigwa marufuku na TBS kama zinavyoonekana katika picha
Bidhaa hizo zilizopigwa marufuku na TBS zikiteketezwa


Na Vero Ignatus,Arusha.

Shirika la viwango nchini Tanzania (TBS) limeendesha zoezi la kuteketeza bidhaa zilizopigwa ma ndani za mitumba pamoja na vilainishi vya magari visivyo na ubora vilivyokamatwa katika masoko mbalimbali mkoani Arusha.

Fundi Sanifu wa Ukaguzi kutoka TBS Godifrey Nguma amesema uteketezaji wa bidhaa hizo zinazofikia jumla ya tani 2 zilizoteketezwa katika dampo kuu LA mkoa wa Arusha lililoko kata ya Muriet jijini Arusha ,amesema kuwa nguo za ndani za mitumba zina madhara makubwa ikiwemo kusababisha magonjwa sugu kwa watumiaji hivyo zoezi LA uteketezaji linalenga kulinda afya za wananchi.

Stanford Matei ni Ofisa Mdhibiti kutoka shirika hilo mesema kuwa zoezi hilo limefanyika kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinaondolewa masokoni pia kufanya juhudi za kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizokidhi viwango zinazoingizwa kwa njia za panya .

Mkazi wa Arusha Amir Hemed amesema kuwa operesheheni hiyo ya kuteketeza bidhaa zilizopigwa marufuku katika masoko inapaswa kuwa endelevu ili kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinaondolewa sokoni.

Watu wenye Ulemavu waiomba Tume ya Uchaguzi kuwawekea Mazingira Rafiki

$
0
0
Mbarouk Salim ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Taifa akizungumza na na Watu wenye ulemavu (hawapopichani)


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Watu wenye Ulemavu mkoa wa Arusha wameiomba Tume ya uchaguzi kuweka mazingira rafiki kwao ili waweze kushiriki katika zoezi la uandikishaji wa daftrari la wapiga kura na kutimiza haki yao ya kikatiba bila kupata vikwazo vinavyotokana na hali zao.


Yunisi Urassa ni Katibu wa Shirikisho la vyama vya Walemavu wilaya ya Arusha ametoa maombi hayo huku akisisitiza kuwepo kwa mazingira rafiki katika vituo vya kujiandikisha ili viweze kufikika kwa urahisi na watu wote katika kikao cha Tume ya Uchaguzi na wadau wa Uchaguzi wakiwemo wawakilishi wa vyama vya siasa,wawakilishi wa makundi maalumu katika jamii.

Mbarouk Salim ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Taifa amesema kuwa zoezi hilo litaanza hivi karibuni na tayari ziko asasi za kiraia zilizopewa kibali cha kutoa elimu za raia kwa wapiga kura ili waweze kutumia haki yao ya kikatiba.

Wajumbe kutoka katika vyama vya siasa Denis Mwita Katibu wa Ccm wilaya ya Arusha na Innocent Joseph ambaye ni Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha wameiomba tume hiyo kuweka vituo karibu na makazi ya wananchi pamoja na kuhakikisha kuwa sheria za Uchaguzi zinazingatiwa.

Viewing all 110125 articles
Browse latest View live




Latest Images