Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

PSPTB YAZINDUA RASMI MFUMO WA UTOAJI HUDUMA KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0

*Yajizatiti kuzidi kuendelea kuifanyia kazi tuzo waliyoipata katika maonesho ya 43 ya biashara(Sabasaba).


MKURUGENZI wa fedha na utawala wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) Paul Bilabaye amesema kuwa katika maonesho ya 43 ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam  wamezindua rasmi huduma kwa njia ya mtandao ambapo watumiaji watatumia simu za mkononi pamoja na kompyuta zilizounganishwa na intaneti ili kupata huduma za Bodi hiyo.


Amesema kuwa mfumo huo wa kidijitali utarahisisha huduma kwa watumiaji ikiwemo kuokoa gharama na muda sambamba na kuwafikia watumiaji wengi zaidi kwa wakati mmoja.

"Tumeanza rasmi na huduma za mafunzo ambapo wiki chache kutakuwa na warsha ya mafunzo ya tafiti kwa wanafunzi ambao wanamaliza mitihani ya kitaaluma ambapo sasa maombi yote yataombwa kupitia tovuti ya Bodi hiyo"


Aidha amesema kuwa katika maonesho hayo wameshinda tuzo ya Taasisi bora ya udhibiti na kushika nafasi ya tatu jambo ambalo linawapa nguvu na ari katika utendaji kazi zaidi katika kuwahudumia wananchi.


Bilabaye amesema kuwa ushiriki wao katika maonesho haya ya 43 ya Sabasaba kwao yamewapa funzo kubwa, na wamewahudumia wananchi katika huduma zote zinazotolewa na Bodi na hiyo ni kuanzia usajili wa wataalamu, kutoa elimu kuhusiana na mitihani pamoja na na kutatua kero mbalimbali wanazokumbana nao.


Ameeleza kuwa huduma zinazotolewa na Bodi hiyo imekuwa inawaaminisha wananchi na ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli kwa utendaji kazi uliotukuka pamoja na kuwaamini wao katika kusimamia taasisi hiyo ya umma.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Paul Bilabaye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa utoaji wa huduma mbalimbali za PSPTB kwa njia ya mtandao tofauti na awali zilikuwa zikitolewa moja kwa moja kutoka ofisza  za Bodi ya PSPTB.
Kuzinduliwa kwa mfumo huo wa kidijitali utarahisisha utoaji wa huduma kwa wadau wote wa PSPTB kwa haraka na ufanisi zaidi na kwa watunwengi.
Afisa mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Shamim Mdee(katikai) akitoa ufafanuiz kwa mwananchi aliyetembelea banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa Mitihani kutoka PSPTB, Philipo Kibona.
 Afisa mwanadamizi wa Huduma za wanachana wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na Ugavi (PSPTB), Martha Mapalala akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo kwa Leah Mwakabungu kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kijana Idrisa Mtinangi(wa pili kushoto) akiuliza swali kwa maofisa wa PSPTB alipotembelea banda leo  kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Mipango ( PSPTB), James Maghori(wa pili kulia) akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na vijana waliofika katika banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mitihani kutoka PSPTB, Philipo Kibona.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala PSPTB, Paul Bilabaye akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa bodi hiyo katika banda lao kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.  Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Mitihani kutoka PSPTB, Philipo Kibona.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MJI MPYA WA SERIKALI NCHINI MISRI

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mwenyekiti wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Serikali (ACUDO), Ahmed Zaki (kulia), wakati alipotembelea mji huo, mjini Cairo, Julai 8.2019. Kutoka kushoto ni Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mji mpya wa Serikali, wakati alipotembelea mji huo, mjini Cairo, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (kjushoto), wakati alipotembelea kanisa jipya la Katoliki, katika mji Mpya wa Serikali, mjini Cairo Misri, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (kushoto), wakati alipotembelea kanisa jipya la Katoliki, katika mji Mpya wa Serikali, mjini Cairo Misri, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KWENYE ZIARA NCHINI MISRI

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na mwenyeji wake, Waziri Mkuu ya Jamhuri ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, kabla ya mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Misri, katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, mjini Cairo, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu ya Jamhuri ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly katika mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Misri, katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, mjini Cairo, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu ya Jamhuri ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya mazungumzo rasmi kati ya Tanzania na Misri, nje ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Misri, mjini Cairo, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Uwekezaji, Dkt. Sahar Nasr, kabla ya kukutana na Wawekezaji kutoka Misri, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo Misri, Julai 8.2019. 

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wawekezaji kutoka Misri, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo Misri, Julai 8.2019. 
 Wawekezaji kutoka Misri, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipozungumza nao, katika Hoteli ya Almasaa mjini Cairo Misri, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MAUAJI YA WATANZANIA MPAKANI YAWAHAMISHA WANAKIJIJI

$
0
0
 Watanzania wakihamisha mizigo na mazao yao kutoka Kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kufuatia mauaji ya watanzania kumi yaliyotokea Juni 26 mwaka huu mara baada ya serikali ya Tanzania na Msumbiji hivi karibuni kufanya makubaliano ya pamoja kutoa siku tatu kuanzia jana watanzania hao waweze kuhamisha mizigo na mazao yao kutoka Kijiji hicho cha Mtole na kurejea hapa nchini.
Watanzania wakihamisha mizigo na mazao yao kutoka Kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji kufuatia mauaji ya watanzania kumi yaliyotokea Juni 26 mwaka huu mara baada ya serikali ya Tanzania na Msumbiji hivi karibuni kufanya makubaliano ya pamoja kutoa siku tatu kuanzia jana watanzania hao waweze kuhamisha mizigo na mazao yao kutoka Kijiji hicho cha Mtole na kurejea hapa nchini ambapo wanavuka mto Ruvuma huo kwa kutumia miguu .(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU)

TAASISI ZA KIDIJI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KATIKA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KUHAKIKIWA

WAZIRI MKUU ATEMBELEA PIRAMIDI MISRI

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na mwenyeji wake, Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit (kushoto), wakati alipotembelea Piramidi mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishika jiwe lililotumika kujengea Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa amepanda juu ya Piramidi, akionesha jambo wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9, 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ndani ya Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9, 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa anashuka kwenye Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo, mjini Cairo Misri, Julai 9, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy, wakati alipotembelea Piramidi mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. Tokea kushoto ni Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifurahia jambo, baada ya kutembelea Piramidi, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa za wajasiriamali, baada ya kutembelea Piramidi, mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akitembea nje ya Piramidi, wakati alipotembelea Piramidi hizo mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. kulia ni mwenyeji wake, Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkurugenzi wa Piramidi Ashraf Mohy, wakati alipotembelea Piramidi hizo mjini Cairo Misri, Julai 9.2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo na Uhaulishaji wa Ardhi Dkt. Azzeldin Abosteit. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PROFESA IKINGURA ATEMBELEA BANDA LA GST KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Profesa Justinian Ikingura(kushoto) akipata maelezo alipotembelea banda la taasisi hiyo katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara yanaendelea katika viwanja vya sabasaba kwa lengo la kuangalia jinsi taasisi hiyo ilivyoshiriki.
 Mwenyekiti wa Bodi ya GST, Profesa Justinian Ikingura akuzungumza na wataalam wa GST  juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo, ikiwa pamoja kutoa msisitizo juu ya kuendelea kutoa taarifa kwa jamii za matokeo ya tafiti mbalimbali za jiosayansi zinazofanyika ili ziweze kutumiwa na kuleta tija katika sekta ya madini na sekta nyingine za kiuchumi.

LIVE: Matukio mbalimbali ya Kuagwa kwa Miili ya Wafanyakazi watano wa Azam

$
0
0



Mkurugezi na Mmiliki wa kampuni ya Bakhresa Group of Companies Said Salim Bakhresa(kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe(katikati) pamoja na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa kugwa kwa miili ya wafanyakazi watano wa Azam waliofariki kwenye ajali walipokuwa njiani kwenda kurusha matangazo mbashara ya uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato.

Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.







Anayedaiwa kumuua mkewe kujitetea Julai 18

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
DAKTARI bingwa wa uchunguzi wa vifo vyenye utata na magonjwa mbali mbali wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Innocent Mosha ameileza mahakama kuwa kifo cha marehemu Bahati Hussein kilisababishwa na majeraha yakiyokutwa sngoni kwake baada ya pingili zake mbili kutenguka.

Akiongozwa na wakili wa serikali,  Erick Shija kutoa ushahidi wake leo, Julai 9 2019, shahidi huyo amedai, alipoufanyia uchunguzi mwili wa marehemu aligundua pia kulikuwa na mvilio wa damu kuzunguka pingili zake za Shingo na mapafu yake yalikuwa yamejaa damu na hewa.

Katika kesi hiyo, Godfrey Samwel maarufu kama Nkwabi anadaiwa kumuua kwa makusudi make wake Bahati Hussein.

Mbele ya msajili wa Mahakama Kuu, Pamela Mazengo, Dr. Mosha ambae ni shahidi wa sita na wa mwisho katika kesi hiyo amedai, Juni 23,2012   akiwa kazini, alipokea amri kutoka jeshi la polisi Stakishari lililomtaka  kufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Bahati Hussein ambae walikuwa wanahisi kuwa ameuwawa kwa kupigwa.

 Akadai, baada ya kupokea amri hiyo, alipata mashahidi wawili  walioenda pamoja na mpelelezi kwa ajili ya kumtambua marehemu ambao ni Muhidin hamisi na Maxmillian ambapo baada ya zoezi La  utambuzi kabla ya kuanza kufanya uchunguzi alipata maelezo mafupi kutoka kwa mpelelezi E 1279 ditektivu Koplo Peter.
Amesema, alifanya uchunguzi katika sehemu ya nje ya mwili wa marehemu na ndani ambapo katika sehemu ya nje mwili wa marehemu ulikutwa na michubuko kidogo katika sehemu ya shingoni huku macho yake yakiwa na mivilio midogo midogo ya damu na kucha zake zilikuwa zinebadilika ranging Imekuwa dark blue.

Ameendelea kudai kuwa katika uchunguzi wake wa sehemu za ndani za mwili wa marehemu waligundua kuwa pingili mbili za shingo ya marehemu  zilikiwa zimetenguka na kulikuwa na kulikuwa na mvililio wa damu kuzunguka hizo pingili na pia mapafu yake yalikuwa yamejaa hewa na damu.
" katika uchunguzi wangu nilibaini kuwa majeraha kwenye shingo ya marehemu ndio chanzo cha kifo chake", amedai Dr. Mosha.

Kufuatia ushahidi huo, Mahakama imemkuta mshtakiwa na kesi ya kujibu baada ya upande wa mashtaka kufungua ushahidi dhidi ya kesi hiyo kwa kuleta mashahidi sita.

Wiki iliyopita, watoto wawili wa marehemu akiwemo mtoto wa miaka 10, ambae wakati mama yake anauwawa alikuwa na miaka mitano alitoa ushahidi wake na kueleza alivyoshuhudia  baba yao wa kambo, Godfrey Samweli au Nkwabi (mshtakiwa)akimnyonga mama yake Bahati Hussein.

Inadaiwa Juni 21, 2014 huko Ulongoni A wilayani Ilala, Dar es Salaam, Godfrey alimuua kwa makusudi Bahati  Hussein.
Mshtakiwa Godfrey Samwel maarufu Nkwabi akitoka ukumbi wa wazi wa  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi yake ambapo leo Shahidi wa sita ambae ni daktari bingwa wa uchunguzi wa vifo vyenye utata na magonjwa mbali mbali ametoa ushahidi wake.
Hata hivyo, upande wa mashtaka umemkuta mshtakiwa huyo na kesi ya kujibu na kesi imeahirishwa hadi Julai 18 mshtakiwa atakapoanza kujitetea

Serikali yapokea gawio la Sh Bilioni 1.2 kutoka Benki ya Posta

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

BENKI ya Posta Nchini TPB leo imekabidhi gawio la Shilingi Bilioni 1.2 kwa Serikali pamoja na wanahisa wengine kama faida ambayo wameipata kutokana na shughuli zake ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Gawio hilo limekabidhiwa kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango leo katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea gawio hilo, Waziri Dk Mpango ameipongeza Benki ya TPB kwa kuendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takribani 50 yaliyopo nchini.

" Kwa kweli ni jambo kubwa na la kipekee sana ambalo Benki ya Posta imelifanya, nitoe shukrani za dhati kwa Uongozi wa Benki hii kwa gawio hili la Bilioni moja ambalo mmelitoa kwa Serikali, hii ni mara ya pili mfululizo mmetoa gawio hili na hakika mnastahili pongezi.

" Kutoa kwenu gawio hili kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki hisa kwenye Benki yenu," Amesema Dk Mpango.

Dk Mpango pia ametoa wito kwa Taasisi zingine za umma zinazotaka huduma za kibenki kote nchini na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Dk Edmund Mndolwa amesema Benki ya TPB imefanya vizuri kwa mwaka jana kwa kupata faida ya Shilingi Bilioni 17 na hivyo kuweza kutoa gawio la Shilingi Bilioni Moja kwa wanahisa zake na Serikali.

" Najisikia daraja kusimamia Benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki yaliyopo sokoni, ni matumaini yetu kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dk Magufuli katika kuifanya Tanzania inafikia uchumi wa kati," Amesema Dk Mndolwa.

Mkurugenzi Dodoma amtangaza Mbwana Makata kuwa Kocha Mkuu Dodoma FC

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amemtambulisha aliyekua kocha wa zamani wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata kuwa Kocha Mkuu wa Dodoma FC.

Kunambi amesema wao kama Jiji la Dodoma wamejipanga kuhakikisha Timu hiyo inapanda daraja kwenda Ligi Kuu ili kuhakikisha wanampa heshima Rais Dk John Magufuli kwa kuipa Dodoma hadhi ya Jiji.

" Ni lazima tumpe heshima Rais wetu Dk John Magufuli kwa kutupa hadhi ya Makao makuu, kutujengea uwanja wa kimataifa wa ukubwa wa kubeba watu zaidi ya Laki Moja, hivyo ni lazima tuwe na timu imara ambayo itakua Ligi Kuu.

" Lengo letu ni kupanda daraja kutoka Ligi daraja la kwanza kwenda Ligi Kuu, tutampa ushirikiano kocha Makata katika usajili, mchezaji yeyote ambaye atamhitaji sisi tutakua tayari kutoa pesa ili asajiliwe," amesema Kunambi.

Nae Meya wa Jiji hilo Profesa Davis Mwamfupe amewataka wanasiasa kutoiingilia Timu hiyo na kumuahidi ushirikiano kocha Makata huku akimtaka kufanya kazi kubwa ya kuhakikisha Dodoma FC inapanda Ligi Kuu.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Felista Mabula amesema uwezo uliooneshwa na Kocha Makata akiwa anainoa Polisi Tanzania ni mkubwa hivyo wanaamini ataendeleza ubora wake akiwa na Dodoma FC ili iweze kupanda Ligi Kuu.

Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Makata ameahidi kuhakikisha anatimiza malengo aliyowekea na uongozi wa Timu hiyo kwa kuipandisha Dodoma FC Ligi Kuu Tanzania.

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA KUIPANDISHA DARAJA TANZANIA

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma.
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), Jijini Dodoma. 
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dodoma. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru (kushoto), na Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Adrian Njau wakisikiliza kwa makini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru (hawapo pichani), kilichofanyika Jijini Dodoma. 
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru akielezea jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akiwa na mgeni wake Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru aliomtembelea na kufanya naye mazungumzo katika Ofisi Ndogo ya Hazina-Treasury Squire, Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb), akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) (aliyeketi mbele kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dodoma. Waliosimama wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Adolf Ndunguru wa Wizara ya Fedha na Mipango na Maafisa wengine waandamizi kutoka Wizara hiyo. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango (Mb) (kushoto), akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Fedha na MIpango) 

……………………….. 

Na Saidina Msangi na Josephine Majura, WFM, Dodoma 
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inatarajia kuipandisha daraja Tanzania kutoka katika hadhi ya kunufaika na Mfuko wa Maendeleo wa Benki (ADF) hadi kuwa na hadhi itakayoiwezesha Tanzania kuweza kupata rasilimali fedha zaidi kupitia dirisha la African Development Bank (ADB) la Benki ya Maendeleo ya Afrika. 

Endapo Tanzania itafanikiwa kupandishwa hadhi, nchi itaweza kunufaika na ongezeko la fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka hadi Dola za Marekani milioni 812 kwa mwaka. 

Hayo yamesemwa Jijini Dodoma na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo Dr. Alex Mubiru alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha na Mipango-Treasury Square. 

Katika mazungumzo hayo, Dr. Alex ameeleza kuwa hatua hiyo ya kupandishwa hadhi ama kupandishwa daraja inatokana na uchumi wa nchi kufanya vizuri hususani katika maeneo ya kasi ya ukuaji wa uchumi na kuwa na deni himilivu. 

“Hatua hiyo itaiwezesha Tanzania kupata fedha zaidi kutoka katika Benki hiyo na kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na vipaumble kwa Serikali” Alisisitiza Bw. Mubiru. 

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Bw. Alex Mubiru, amesema kuwa benki hiyo inajivunia kufanya kazi na Tanzania ambayo ni miongoni mwa nchi Waasisi wa Benki hiyo. 

Katika mazungumzo yao, Dkt. Mpango ameeleza kuwa Serikali inajivunia kufanya kazi pamoja na Benki ya AfDB kwa kuwa benki hiyo imekuwa na masharti rafiki katika upatikanaji wa mikopo. 

Dkt. Mpango amesema kuwa Benki hiyo ina mtazamo chanya katika maendeleo ya watu na kuwa dira katika mipango ya maendeleo na kuahidi kushirikiana nao vyema katika kukuza uchumi wa nchi. 

Aidha, Waziri Mpango ameipongeza benki hiyo kwa kukubali kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Barabara ya Mzunguko Dodoma (km110.2) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma (Msalato) na kubainisha kuwa uamuzi huo ni mzuri kwani licha ya Dodoma kuwa ni Makao Makuu ya nchi lakini pia miundombinu hii itaunganisha na kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara katika mikoa mingi nchini pamoja na nchi jirani.

UWT MANISPAA YA IRINGA WANAWAKE KOPENI KWA MALENGO

$
0
0
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake manispaa ya Iringa (UWT) Ashura Jongo akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa ya Iringa akiwaasa wanawake kukopa kwa malengo 
Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya akitoa neno kwa wanawake wa UWT manispaa ya Iringa. 




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


Kukosekana kwa elimu ya matumizi bora ya mikopo kwa wanawake kumetajwa kuwa sababu ya wanawake wengi wa manispaa ya Iringa kushindwa kurudisha mikopo katika taasisi za kifedha.

Akizungumza kwenye baraza la UWT manispaa ya Iringa,mwenyekiti wa umoja huo Ashura Jongo amesema kuwa wananwake wamekuwa wanakopa bila ya kuwa na elimu ndio maana wanashindwa kurejesha mikopo ambayo wamekopa kwenye taasisi za kifedha.

“Changamoto za wanawake kutokuaminika katika vyombo au taasisi za kifedha ni kutokana na hali ngumu,wanawake wanaweza wakakopa wakiwa na malengo lakini wakirudi nyumbani wanakutana na matatizo mengi yanahitaji matumizi ya fedha” aliema Jongo

Jongo alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuendelea kuwawezesha kwa kuwa wanauwezo wa kutmia vizuri fedha ambazo zinapatikana hivyo ukimuwezesha mwanamke umewawezesha watu wengi kwa kuwa wanawake ndio nguzo ya familia hasa kwenye maswala ya kiuchumi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve amezitaka taasisi za kifedha kutoa elimu kwa wakopaji ili waweze kuzitumia vizuri fedha hizo.

“Shida moja wapo ya wanawake kushindwa kurudisha mikopo ni kutokana na kutokuwa naelimu ya matumizi ya fedha kwa kuwa pesa hiyo inahitaji nidhamu na matumizi bora ya fedha hizo za mikopo” alisema Tweve

Tweve alisema kuwa tasisi za kifedha zinatakiwa kutoa elimu kwanza kabla ya kutoa mikopo kwa wanawake ili waweze kuzirejesha kwa wakati kwa kuwa tayari ameshapata elimu ya matuzi bora ya mikopo waliyokopa.

“Pale wanapokopa lazima wajue matumizi ya hizo pesa la sivyo watazitumia bila nidhamu fedha hizo na kushindwa kuzirejesha na kujikuta wakiwa matatani kutokana na kushindwa kulipa mkopo huo” alisema Tweve

Naye mgeni rasmi kwenye baraza hilo mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya amewataka wanawake kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ili kufikia malengo waliyojiwekea kabla ya kwenda kukopa.

“Kwa kwali wanawake wa CCM manispaa ya Iringa wengi mnakopa mikopo lakini hamrejeshi kwa wakati na hili ni bomu kubwa kwa chama hivyo mnatakiwa kuwa na nidhamu ya matumizi ya mikopo hiyo” alisema Rubeya

MAJANGIRI HAWANA NAFASI KUFANYA UHARIFU KWENYE MBUGA ZA WILAYA YA IRINGA- DC KASESELA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela akiwa pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Iringa Hashimu Komba wakiwa kwenye picha moja na viongozi na walinzi wa hifadhi Village Game Scouts
Mkuu wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote na akiwa ameshika silaha bora ambazo wanazitumia walinzi wa hifadhi Village Game Scouts ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS
MKUU wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu iliyopo katika wilaya hiyo.



NA FREDY MGUNDA,IRINGA. 


MKUU wa wilaya ya Iringa ambaye ni Mwenyekiti wa baraza la maliaasili na misitu Richard Kasesela wamejipanga kuwadhibiti majangili wote ambao wamekuwa wakifanya uharifu kwenye maliasili na misitu iliyopo katika wilaya hiyo.

Akizungumza wakati alipofanya ziara ya ghafla ya kuwatembelea na kuwapa moyo walinzi wa hifadhi Village Game Scouts ambao wanafadhiliwa na shirika la STEPS kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulinda maliasili zilizopo katika wilaya hiyo.

“Mimi niwapongeze sana maana mnafanyakazi kubwa sana kupambana na majangili huko porini jambo ambalo mnapaswa kupongezwa kwa namna yoyote ile” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa hifadhi hizo zimekuwa zikivamiwa na majangili hasa pembezoni mwa hifadhi hizo kutokana na kuwa jirani na wakazi ambao wamekuwa wakifanya uharifu huo kutokana na tamaa zao. Kasesela aliwaonya majangili kwamba sasa wasirogwe kuingia kwenye mbuga za wanyama kutaka kufanya ujangili wa aina yoyote kwakuwa wanamifumo ya kisasa zikiwemo kamera zimefungwa kwenye maeneo ya mbuga hizo. 

“Yoyote atakaye kamatwa kwa ujangili atafikishwa kwenye vyombo husika na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa atakuwa amefanya uharifu ambao haukubariki kisheria” alisema Kasesela

Aidha Kasesela alilipongeza shirika la STEPS kwa kuwafadhili walinzi wa hifadhi Village Game Scouts kwa kuwapa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo ya ulinzi kwenye mbuga zilizopo katika wilaya ya Iringa. 

Mkurugenzi Dodoma amtangaza Mbwana Makata kuwa Kocha Mkuu Dodoma FC

$
0
0

Na Charles James, Michuzi TV

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amemtambulisha aliyekua kocha wa zamani wa Polisi Tanzania, Mbwana Makata kuwa Kocha Mkuu wa Dodoma FC.

Kunambi amesema wao kama Jiji la Dodoma wamejipanga kuhakikisha Timu hiyo inapanda daraja kwenda Ligi Kuu ili kuhakikisha wanampa heshima Rais Dk John Magufuli kwa kuipa Dodoma hadhi ya Jiji.

" Ni lazima tumpe heshima Rais wetu Dk John Magufuli kwa kutupa hadhi ya Makao makuu, kutujengea uwanja wa kimataifa wa ukubwa wa kubeba watu zaidi ya Laki Moja, hivyo ni lazima tuwe na timu imara ambayo itakua Ligi Kuu.

" Lengo letu ni kupanda daraja kutoka Ligi daraja la kwanza kwenda Ligi Kuu, tutampa ushirikiano kocha Makata katika usajili, mchezaji yeyote ambaye atamhitaji sisi tutakua tayari kubi.
isha Dodoma FC inapanda Ligi Kuu.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Felista Mabula amesema uwezo uliooneshwa na Kocha Makata akiwa anainoa Polisi Tanzania ni mkubwa hivyo wanaamini ataendeleza ubora wake akiwa na Dodoma FC ili iweze kupanda Ligi Kuu.

Akizungumza baada ya kutambulishwa Kocha Makata ameahidi kuhakikisha anatimiza malengo aliyowekea na uongozi wa Timu hiyo kwa kuipandisha Dodoma FC Ligi Kuu Tanzania.

Airtel yatoa msaada wa kitanda cha oparesheni Hospitali ya Mkuranga

$
0
0
Airtel yatoa msaada wa kitanda cha oparesheni Hospitali ya Mkuranga
Ni muendelezo wa kampeini ya Airtel Tunakujali ambapo wafanyakazi wa kampuni huchangia kipato chao kusaidia vikundi mbali mbali katika Jamii wenye uhitaji maalum

MKURANGA, KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha Huduma kwa wateja wakubwa wameshiriki kampeni maalum yakusaidi jamii inayojulikana kama Aitel Tunakujali kwa kutoa msaada wa kitanda cha kufanyia upasuaji (oparesheni) kwa kwa akinamama wanojifungua kwenye thamnai ya Sh. Milioni tano kwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga mkonini Pwani.

Airtel Tunakujali ni programu maalum ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo huchangia sehemu ya kipato chao kwa ajili ya huduma za kijamii zikiwemo afya na elimu.

Akizungumza jijini wilayani Mkurranga wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada huo wa kitanda mwishoni mwa wiki, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema kuwa kitengo cha kuhudumia wateja wakubwa Airtel kiliandaa hafla kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya kulipia bima ya afya ya watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kulipia matibabu na tayari watoto hao washalipiwa bima kwa mwaka mzima.

‘Hapa leo tufanya muendelezo wa kuendelea kusaidia huduma ya afya. Kwa leo tunakabidhi hiki kitanda cha upasuaji kwa akinamama wanaojifungua. Hii inatokana na kuelewa ya kwamba hospitali hii ina changamoto nyingi na upungufu wa vifaa vya hospitali huku hiki kitanda kikiwa ni moja wapo. Sisi Airtel tuna uhakika ya kwamba kitasaidia wale akina mama waliokuwa na utahitaji wa upusuaji lakini wanakosa huduma kama hii. Tunaomba uongozi wa hospitali ukitunze vizuri na sisi Airtel tunahidi kuendelea kusaidia kwenye huduma za afya na zingine zenye kugusa jamii yetu moja kwa moja, Mmbando alisema.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Dkt Stephen Mwandambo mbali na kutoa pongezi kwa Airtel alisema kuwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga inakabiliwa na changamoto kadhaa huku akitoa mfano kuwa hospitali hiyo ina uwezo wa kuhudumia wakinamama waokuja kujifungua kwa wastani wa 70 kwa mwezi lakini kwa hali halisi imekuwa ikihudumia 270 mpaka 400.

‘Kulingana na idadi hiyo kubwa ya wakinamama ambao wanapata huduma ya kufingulia kwenye hospitali yetu ya wilaya tumekuwa tukipata changamoto nyingi huku tukiwa na kitanda kimoja tu kwa ajili ya upasuaji. Kwa msaada huu kutoka Airtel itasaidia sana sisi pamoja na kupunguza wa vifo vinavyotokana na kukosa kitanda hiki, alisema Dkt Mwandambo huku akiongeza kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitoa huduma ya matibabu kwa wakazi wa wilaya ya Mkurunga asilimia 80 na asilimia 20 wanatoka wilaya za Kibiti na Temeke.

Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Mkurunga Injinia Mshanu Munde akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali ya wilaya alitoa pongezi kwa Airtel na hasa wanafanyakazi ambao waliweza kutoa sehemu ya kipato chao na kufanikisha upatikanaji wa kitanda hicho.

Sisi zote tunajua kampuni ya Airtel ni ya kizalendo kwa inamilikiwa na wananchi kupitia serikali yao kwa asilimia 49. Lakini naomba niwapongezi wanafanya kazi kitengo cha kuhudumia wateja wakubwa na uzalendo wao wa kuona umuhimu wa kuimarisha sekta ya afya na kuamua kwa hiari yao kutoa sehemu ya mapato yao na kuweza kufanikisha jambo hilo. Na wakaribisha kwenye wilaya yetu lakini tuna changamoto nyingi kwenye sekta hizi mbili za afya na elimu nawaomba mkipata nafasi siku nyingi kuja na kuendelea kutuunga mkono alisem Injinia Munde.

Meneja wa Kitengo cha kuhudumia wateja wakubwa Airtel Tanzania Alice Maziku akimkabidhi kitanda cha upasuaji Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mkuranga Injinia Mshanu Munde mwishoni mwa wiki. Kampuni ya Airtel Tanzania kupitia mradi wa AIRTEL TUNAKUJALI ilitoa kitanda cha upasuaji kwa wakinamama wanaojifungua kwa hospitali ya Mkurunga ikiwa ni juhudi za kusaidia jamii iiliyo kwenye mahitaji maalum. Wengine ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Dkt Stephen Mwandambo (kati kati), Meneja Uhusiano Airtel Tanzana Jackson Mmbando (wa kwanza kulia) na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Omari Kisali (wa kwanza kulia).
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akisalimiana na Injinia Mshanu Munde baada ya Airtel kukabidhi kitanda cha upasuaji kwa hospitali ya wilaya ya Mkuranga mwisho mwa wiki. Airtel ilitoa kitanda hicho kwenye thamani ya Milioni tano ikiwa ni juhudi za kusaidia jamii kupitia mradi wa AIRTEL TUNAKUJALI. Wengine ni Wengine ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Dkt Stephen Mwandambo (kati kati) na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Omari Kisali (wa kwanza kulia).

NAIBU SPIKA ATAKA MISINGI YA UTAFITI KUFUATWA KATIKA UCHAPISHAJI NA UTANGAZAJI WA TAARIFA

$
0
0
NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema misingi ya utafiti ni jambo muhimu na la msingi litakalopaswa kuzingatiwa katika uchapishaji na utangazaji wa taarifa mbalimbali ili kuweza kulinda misingi ya amani iliyopo nchini. 
Akizungumza leo Jumanne (Julai 9, 2019) Jijini Dar es Salaam katika Kongamano maalum la siku ya Amani lililoandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (DITF), Dkt. Tulia alisema uchapishaji na utangazaji wa taarifa yoyote haina budi kuwa na tija katika taifa. 

Dkt. Tulia alisema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na utamaduni uliozoeleka wa kutangaza na kuchapisha taarifa mbalimbali katika jamii kupitia vyombo vya habari pasipo na kuzingatiwa kwa misingi ya utafiti hatua inayoweza kuleta migongano isiyo na tija kwa taifa. 

“Serikali ya Awamu ya Tano tunaona inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwemo mradi wa umeme katika Mto Rufiji, sni wajibu wetu kulinda misingi ya amani iliyopo ili tuone matunda ya miradi hii katika nchi yetu” alisema Tulia. 

Aidha Dkt. Tulia alisema ni wajibu wa misingi ya utafiti ikazingtiwa katika taaluma mbalimbali ikiwemo ya uandishi wa habari kwani wapo baadhi ya watu wanaofikiri kuwa wanaweza kuandika na kutangaza habari pasipo na kusomea taaluma hiyo, jambo ambalo si la kweli kwa kuwa uandishi wa habari ni taaluma nyeti na muhimu kama zilivyo taaluma nyingine. 

Aliongeza kuwa ni wajibu wa Watanzania wote kusoma vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na waasisi wa taifa vikiwemo vitabu vya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambavyo vimekuwa na wingi wa maarifa na maelekezo yanayopaswa kuzingatiwa ili kuweza kujenga taifa lenye umoja, upendo na mshikamano. 

Naye Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano Zanzibar, Imane Duwe alisema mfumo wa soko huria nchini yameleta mabadiliko makubwa katika tansia ya habari na mawasiliano ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii, ambayo imekuwa imeleta hamasa kubwa kwa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo vijana. 

“Hapo awali mwandishi wa habari alipokuwa akitumwa kazi na mhariri wake ni lazima arudi na atoe taarifa kwa mkuu wake pamoja na habari au taarifa hiyo kuweza kufanyiwa uhariri kabla ya kuchapishwa na kutangazwa lakini kwa sasa hali ni tofauti kidogo, kwani tukio lolote linaweza kutumwa wakati huo huo kupitia vyombo vya kisasa zaidi vya mawasiliano” alisema. 

Aliongeza kuwa vyombo vya habari vya zamani ikiwemo Magazeti, Redio na Televisheni kwa sasa navyo vimeingia katika ushindani mkubwa wa soko kwani kwa upande wao pia wameanzisha mitandao mbalimbali ya kijamii ili kuweza kuwa na njia za kisasa zaidi za mawasiliano. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema ni wajibu wa Viongozi na Watanzania wajenge utamaduni wa kuheshimu tunu na misingi mikuu ya amani nchini ikiwemo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, misingi ya Azimio la Arusha ambayo iliasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. 

Aidha aliongeza kuwa ili kuweza kujenga Taifa lenye misingi bora ya amani ni wajibu wa Serikali kupitia Viongozi kuwa na matumizi na usimamizi bora wa rasilimali za taifa na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi wote pamoja na kuweka misingi imara katika ulinzi rasilimali hizo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema Tanzania inaweza kufikia na kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya viwanda iwapo Viongozi wataweka mkazo katika usimamizi wa rasilimali watu yenye kutambua umuhimu wa kulinda amani, weledi, uzalendo na kujiamini. 

“Moja ya Nguzo muhimu katika kufikia uchumi wa viwanda ni mfanyakazi, hivyo ni wajibu kila mwenye dhamana hiyo kutimiza wajibu wake huku akiogopa kufanya vitendo vya ufisadi kwani hata katika vitabu takatifu vimezungumzia ufisadi ni jambo baya sana” alisema Sheikh Salum.

TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA JAMII KATIKA MIKOA YA MBEYA,IRINGA,NJOMBE,RUKWA NA SONGWE KUHAKIKIWA KUANZIA TAREHE 15 JULAI,2019 HADI 24 JULAI,2019

TARURA KUANZA KUTUMIA MFUMO MPYA WA MALIPO SERIKALINI

$
0
0
Mtaalamu wa Mfumo wa Ulipaji Serikalini kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ndewingia Mashauri, akitoa mafunzo kwa wahasibu na wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA, kutoka maeneo mbalimbali nchini, mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro.
Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis Mwakapalila, akiwahimiza washiriki wa mafunzo ya Mfumo mpya wa Ulipaji Serikalini- MUSE, kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA, kuhakikisha wanauelewa na wanautumia ili kuiwezesha Serikali kupata taarifa za Fedha kwa wakati, katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA, Mhandisi Victor Seff, akieleza uhitaji wa Mfumo wa ulipaji Serikalini katika Taasisi anayoiongoza ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za fedha kwa urahisi, wakati wa mafunzo ya mfumo huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mkoani Morogoro. 
Washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini- MUSE, kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA, wakifuatilia mada zilizotolewa na wataalamu, katika ukumbi wa Hazina ndogo, mkoani Morogoro. 
Mhasibu Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Francis Mwakapalila (katikati), Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA na Wizara ya Fedha na Mipango, baada ya ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo mpya wa ulipaji Serikalini kwa wahasibu na wahandisi wa TARURA, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hazina ndogo mkoani Morogoro. 
(Picha na Geofrey Kazaula, TARURA) 
……………………. 

Na. Geofrey Kazaula, TARURA, Morogoro 
Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) umeanzishwa na wataalamu wa ndani ili kuunganisha mifumo mingine iliyopo, lengo likiwa ni kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za fedha. 

Hayo yameelezwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila, ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya Mfumo wa Ulipaji Serikalini- MUSE kwa wahasibu na wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini- TARURA mkoani Morogoro. 

Bwana Mwakapalila alisema kuwa mfumo huo umetengenezwa na wataalam wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na utaanza kutumiwa na TARURA kisha kutumiwa na Taasisi zote za Serikali pamoja na Wizara baada ya kujiridhisha na ufanisi wake. 
“Nitoe wito kwa washiriki wote wa mafunzo haya kuhakikisha wanauelewa vizuri mfumo na kuwa tayari kuutumia mara tu baada ya mafunzo kukamilika kwa kuwa mfumo huu ni muhimu kutoka na mabadiliko ya teknolojia katika mifumo ya fedha duniani”, alisema Bw. Mwakapalila . 

Naye Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff, amewataka wataalam wa Wakala huo wanaoshiriki mafunzo, kutokuwa na mtazamo hasi kuhusu mfumo na badala yake changamoto watakazo kutana nazo waziwasilishe mahali husika ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa mfumo huo ndio suluhisho la matumizi bora ya fedha za Serikali. Aidha ameeleza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imetoa wataalam wa kutosha ili kuhakikisha wahasibu wote wa TARURA wanapatiwa mafunzo na kuuelewa mfumo kwa kina. Kwaupande wake Mkurugenzi wa Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Sausi, alieleza kuwa mfumo huo utaiwezesha Serikali kuangalia malipo yanayofanyika Katika Taasisi, Kampuni na wadau wengine wanaotoa huduma Serikalini . 

Alisema kuwa mfumo huo ulianza baada ya kukusanya mahitaji kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi Ishirini za Serikali na kwamba Taasisi ya TARURA itakuwa ya kwanza kutumia mfumo huo kupitia wahasibu wake na wahandisi watakao kuwa wakiidhinisha malipo. Bwana Sausi, alisema mafunzo hayo yanawahusisha wahasibu na wahandisi wa TARURA nchi nzima kuanzia ngazi ya Halmashauri lengo likiwa ni kumwezesha Mtendaji Mkuu wa TARURA kuona malipo yote yanayofanyika na Wakala huo katika sehemu mbalimbali kwa wakati. 

Wizara ya Fedha na Mipango imekuwa ikitumia Mifumo ya Fedha tangu miaka ya Sitini na kutokana na ukuaji wa teknolojia imeamua kufanya maboresho ya mifumo hiyo ili kuendana na mahitaji ya sasa na kurahisisha kupata hesabu sahihi za fedha kwa wakati.

KATIBU MKUU DOTO JAMES ATEMBELEA BANDA LA NBAA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeshiriki maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali  kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician)  mpaka  ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama  na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi. 

 Pia Bodi itaanzisha mfumo wa kidijitari wa kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wananchama kupitia tovuti yao.

Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya(kulia) akitoa ufafanuzi wa kazi mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza jambo alipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la NBAA kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiagana na maafisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Evelyn Mcharo(kushoto)  na Magreth Kageya(wa pili kushoto)kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images