Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA UUZAJI MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO YA NIKKYO YATUA RASMI TANZANIA

$
0
0
Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Nikkyo Japanese Leon Sera(kulia) inayojihusisha na uuzaji wa magari kwa njia ya mtandao akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo nchini Tanzania.Lengo ni kurahisisha watanzania kuagiza magari kupitia kampuni hiyo kwa gharama nafuu kwa magari yenye ubora.Katikati ni Meneja mkazi nchini Tanzania wa kampuni hiyo Abbas Mussa na kushoto ni mmoja wa maofisa wa Nikkyo barani Afrika KentaroIkezawa.. Mkurugenzi Mkaazi wa kampuni ya Nikkyo nchini Tanzania Pili Mkufunzi akizungumza ujio wa kampuni hiyo ambayo ilishaingia nchini mwaka mmoja uliopita na sasa imetangazwa rasmi na kuomba Watanzania kuitumia katika kuagiza magari ya aina mbalimbali kutoka Japan. 
Meneja Usafirishaji wa NIkkyo nchini Tanzania Aaliyah Abdulrhman akifafanua kwa kina kwa wageni waalikwa kuhusu ambavyo wamejipanga kuhakikisha wateja wao wanapata magari yaliyo bora.Ametoa ombi kwa Watanzania kuitumia Nikkyo kuagiza magari pindi. 
Viongozi wa kampuni ya Nikkyo wa nchini Tanzania na Japan wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuizindua rasmi kampuni hiyo ambayo inajihusisha na uuzaji wa magari kwa njia ya mtandao.Utambulisho umefanyika jijini Dar es Sala na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali. Meneja Masoko mkaazi wa kampuni ya Nikkyo nchini Tanzania Abbas Muusa akizungumza wakati wa sherehe za kuitambulisha kampuni hiyo kwa Watanzania ambayo ina uzoefu katika biashara hiyo kwa miaka 24 na kwa Tanzania imeingia mwaka jana. 

KAMPUNI ya uagizaji, usafirishaji na uuzaji magari ya nchini Japan ‘Nikkyo’ imeingia na kuwekeza katika biashara hiyo nchini huku ikiahidi kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali katika kukuza uchumi kupitia mpango wake wa maendeleo ya viwanda. 

Aidha katika kutekeleza adhma hiyo, Kampuni hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1995 na kufanya uwekezaji katika nchi mbalimbali zikiwemo za Uganda na Kenya imewahikikishia wananchi kuwapa huduma bora na zinazokidhi viwango ili kuendana na malengo iliyoyakusudia. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shughuli za kampuni hiyo hapa nchini Mkurugenzi Mtendaji wa Nikkyo Leon Sera alisema kuzinduliwa kwa kampuni hiyo hapa nchini ni mkakati unaolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi kupitia sekta ya usafirishaji. 
Alisema katika kutekeleza mkakati huo Nikkyo ambayo ina ubobezi wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya uuzaji magari, imejipanga kuwafikia wananchi wenye mahitaji ya ununuzi wa magari ya aina mbalimbali kutoka nchini Japan na kuwafikishia pasipo usumbufu wowote. 

“Tumeingia kuwekeza hapa nchini kutokana na uwepo wa mazingira mazuri na kuvutia uwekezaji, kwetu ni fahari kubwa kuja kuwekeza katika Taifa hili ambalo kwa sasa limejielekeza katika kukuza uchumi wake kupitia viwanda, tuna ahidi kuwa tutafanya shughuli zetu kwa uaminifu mkubwa” alisema Sera 
Alisema kampuni hiyo ambayo inauza magari hayo kupitia mtandao kwa mteja kuchagua aina ya gari anayoihitaji, inampa uhahika mteja wa kupata gari analolihitaji likiwa salama na lenye ubora kwa lengo la kutimiza matakwa ya mteja huyo. 

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo tawi la Tanzania Abbas Ally, alisema ujio wa kampuni hiyo hapa nchini kutawawezesha watu wenye mahitaji kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata katika uagizaji magari. 

Alisema ukitifautisha na kampuni nyingine zinazojishughulisha na uuzaji wa magari, Nikko imejiwekea utaratibu mzuri wa kutuma mtu kwenda hadi nchini Japan kulikagua gari linalopendekezwa na mteja kabla ya kumletea hapa nchini hatua iliyolenga kumpatia gari iliyo na ubora. 

Wakati huo huo Meneja Usafirishaji wa Nikkyo nchini Tanzania Aaliyah Abdulrhman alisema wao wanachoangalia zaidi ni kuhakikisha mteja anayehitaji kuagiza gari kupitiakwao anapata gari yenye uhakika na iliyobora kwani kabla ya kuagiza gari wanatuma maofisa wao kwa ajili ya kufanya uchunguzi na baada ya kuridhika ndipo sasa wanamletea mteja wao. 

“Hatuangalii fedha bali kwetu cha kwanza ni ubora wa gari, tunataka kuhakikisha gari inayoagizwa kupitia kampuni yetu inakuwa katika mazingira mazuri na iwapo tutaona kuna tatizo tunamshauri mteja na sio tu kuchukua fedha yake.Tunaomba Watanzania wote wanapotaka kuagiza magari watuitumie Nikkyo kwani inayo uzoefu wa kutosha na kwa Tanzania ndio imeingia lakini katika nchi nyingine barani Afrika na Ulaya imekuwa ikifahamika na maarufu kwa uagizaji magari kutoka Japan,”amesema.

SOKO HURU LA BIDHAA AFRIKA LAANZA RASMI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,  ameshiriki katika Mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika jijini Niamey nchini Niger.

Makamu wa Rais Mhe. Samia ameipongeza Serikali ya Ghana kwa kuchaguliwa kuwa Makao Makuu ya Sekretarieti ya AfCFTA na kuisihi Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuharakisha ukamilishaji wa muundo, wa bajeti na mpango kazi  wa Sekretarieti hiyo ili ianze kufanya kazi haraka.

Mkutano huo wa Wakuu wa nchi na Serikali umepokea taarifa ya Mheshimiwa Mahamadou Issoufou, Rais wa Jamhuri ya Niger kuhusu utekelezaji wa AfCFTA ambayo imepokelewa na kupishwa na viongozi hao. Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) umeanza kazi rasmi tarehe 30 Mei, 2019 na unahusu uasili wa bidhaa zitakazouzwa katika soko la Afrika, kufungua biashara ya bidhaa kwa asilimia 97 na uanzishwaji wa Sekretarieti ya kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA.

Aidha, alimpongeza Mheshimiwa Mahamadou Issoufou, Rais wa Jamhuri ya Niger kwa jitihada zake za kuhakikisha azma ya Umoja wa Afrika ya kuanzisha Soko Huru la pamoja la Afrika inafikiwa. Makamu wa Rais pia alizipongeza nchi 27 wanachama wa Umoja huo zilizoridhia mkataba wa uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kati ya nchi 54 zilizotia saini mkataba huo na kuahidi kwamba Tanzania itaungana nao baada ya kukamilisha taratibu za ndani.

Kwenye mkutano huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo alitoa salam za Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria mkutano huo.

Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa amesema kwa upande wa Afrika Mashariki  Tanzania imepiga hatua zaidi kutokana na kuwepo katika Jumuiya za Afrika Mashariki na SADC, hivyo Tanzania imefaidika sana kutokana na kupanuka kwa Soko hilo.

Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema Tanzania imenufaika na mkutano huo kutokana na kuendelea kujifunza zaidi kuhusiana na Biashara ya pamoja katika Afrika pamoja na kuweza kushiriki kuchagua Muwakilishi wa Bara la Afrika katika nafasi mbalimbali ndani ya Afrika na Duniani kote wakati Tanzania imepata nafasi moja ambapo Bethabina Seja Afisa wa Takukuru amechaguliwa katika Bodi ya kudhibiti Rushwa Barani Afrika.           
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Julai 07,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaojadili masuala mbalimbali kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika (AFRICAN CONTINENRAL FREE TRADE AREA - AFCFTA) Mkutano huo unaofanyika mjini Niamey Nchini Niger umefunguliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU Rais Abdel Fattah el Sisi wa Egypt. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).               

WIZARA YA FEDHA WAASWA KUZINGATIA SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Watumishi wa Wizara ya Fedha ya Mipango wametakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma katika kutekeleza majukumu yao. Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Doto James wakati wa kikao cha watumishi wa Wizara hiyo.

Bw. James alisema kuwa watumishi wote wanawajibu wa kufanya kazi kwa ufanisi na weledi na kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma.

“Ni wajibu wa kila mtumishi kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi  wote wanaohitaji huduma katika Wizara yetu” Alisema Bw. James.

Aidha Bw. James aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali iliyopishwa na Bunge hivi karibuni na kuwataka waendelee kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Bajeti hiyo.

Kwa upande wa Watumishi wa Wizara hiyo waliupongeza uongozi wa Wizara hiyo kwa kutenga muda wa kuzungumza nao na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili pamoja na kuzitolea ufafanuzi.

Waliahidi kutatekeleza maelekezo yote aliyotolewa kwa uadilifu ili kuongeza ufanisi wa kazi kwa maendeleo ya nchi.
 Katibu Mkuu wa Wizara  ya Fedha na Mipango  Bw. Doto James, akifungua kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma, Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru akifafanua jambo wakati wa kikao Kati ya Viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma, ambapo Watumishi waliaswa  kufanya kazi kwa bidii na weledi.
 Mhasibu Mkuu wa Serikali, Bw. Francis Mwakapalila akijibu hoja katika kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara  ya Fedha na Mipango kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Kamisha wa Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Mgonya Benedicto akichangia hoja wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo kilichofanyika Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Alfred Dede akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja zilizoibuliwa wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo ambacho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
 Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Umma (TUGHE) wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenjel James akichangia mada katika kikao cha viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo ambapo Watumishi walitakiwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.
 Katibu Mkuu wa Wizara  ya Fedha na Mipango  Bw. Doto James, akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu kikao cha viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo, kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Doto James (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.
Mtumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Hilder Rugemalira akitoa hoja wakati wa kikao kati ya viongozi na Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.

RAIA WATATU WA KIGENI KORTINI KWA KUKUTWA NA MADINI KINYUME CHA SHERIA.

$
0
0


Na EmanuelMadafa-Michuzi TV Mbeya 

Raia Watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya wakikabiliwa na shitaka la uhujumu uchumi baada ya kukutwa wakisafirisha dhahabu gramu 1043.3 yenye thamani ya shilingi Milioni 98.5 kinyume cha sheria ya madini namba 14 ya mwaka 2010.

Washitakiwa hao Clive Rooney (62) raia wa Trish ,na wenzake raia wa Uingereza Ross Stephan (34) na Robert Charles (59) wamekutwa na madini hayo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya Julai 3,mwaka huu.

Mbele ya Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mkoa Venance Mlingi washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chohote kutokanana mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Upande wa Serikali umewakilishwa na mawakili watatu ambao ni Lugano Mwakilasa ,Jacqueline Nyantori na Ofmed Mtenga wakati upande wa utetezi ukiwa na mawakili watatu Boniphace Mwabukusi James Kyando na Kamru Habib.

Mwanasheria wa Serikali Jacqueline Nyantori ameileza Mahayana hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba Mahakama iendelee na utaratibu.

Akitoa utetezi mbele ya Hakimu Venence Mlingi wakili wa utetezi Boniphace Mwabukusi ameiomba Mahakama kuwapatia dhamana wateja wake kwa madai kuwa mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Clive Rooney (62) anasumbuliwa na Ugonjwa haukutajwa nakwamba anatumia dawa maalumu.

Hata hivyo ombi hilo lilipingwa na wakili wa serikali Jacqueline Nyantori na kudai kuwa Ugonjwa huo utatibiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi akiwa gerezani.Washitakiwa hao wote watatu wamerejeshwa mahabusu mpaka Julai 22 mwaka huu .



IGP SIRRO AKAGUA MRADI UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI YA ASKARI POLISI.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (aliyesimama), akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza, wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo ambapo pia alitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari zinazojengwa katika eneo la
Nyamhongoro. Picha na Jeshi la Polisi. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akikagua gwaride aliloandaliwa kwa ajili yake wakati alipowasili mkoa wa Mwanza kwa ziara ya kikazi ambapo pia alitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi ya askari zinazojengwa katika eneo la Nyamhongoro. Picha na Jeshi la Polisi. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia), akizungumza na baadhi ya
wananchi aliokutana nao katika kivuko eneo la Busisi mkoani Mwanza, wakati akiwa safarini kuelekea mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi, mbele yake ni kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jumanne Muliro. Picha na Jeshi la Polisi.

AGIZO LA WAZIRI JAFO LATEKELEZWA KWA VITENDO WILAYANI PANGANI

$
0
0
KAtibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mkoani Mwalimu Hassani Nyange akiuzngumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani akiwa na viongozi wengine wa Halamshauri hiyo wakati walipotembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo tatu za uzalendo ikiwemo ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mkoani Mwalimu Hassani Nyange akiuzngumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani akiwa na viongozi wengine wa Halamshauri hiyo wakati walipotembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji wa agizo la Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo za uzalendo ikiwemo ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George

Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George kushoto akiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange kulia wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuzungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani wakimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Msingi Pangani
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Funguni.

NA MWANDISHI WETU,PANGANI.

AGIZO La Waziri Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jaffo la kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wanaimba nyimbo za uzalendo ikiwemo ule wa Taifa,Tazama Ramani na Naipenda Tanzania limeanza kutekelezwa kwa vitendo wilayani Pangani mkoani Tanga.

Utekelezaji huo umeanza leo Julai 8 mwaka huu kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani (DAS) Mwalimu Hassani Nyange ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo wilayani humo akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kutembelea shule za Msingi Pangani na shule ya Sekondari Funguni kufuatilia utekelezaji huo.


Agizo hilo la Waziri Jaffo alilitoa hivi karibuni wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Umoja wa shule za Msingi Tanzania (Umitashumta) yaliyokuwa yakifanyika mkoani Mtwara ambapo aliagiza kwamba wakati wanafunzi watakapofungua shule wanatakiwa kuimba nyimbo tatu kabla ya kuingia madarasani asubuhi Nyimbo hizo ni wimbo wa Taifa,Wimbo wa Uzalendo (Tanzania tanzania) na Tazama Ramani utaona nchi nzuri kwa maafisa elimu Kata na wakuu wa shule wasimamie hilo.

Akizungumza mara baada kikao cha wadau wa elimu kilichohusisha wakuu wa shule za msingi na sekondari,Waratibu Elimu Kata,Watu wa tume ya Utumishi wa walimu wa kudhibiti ubora wa elimu ambacho kilikuwa ni mahususi ya kuona namna ya kuendeleza utekelezaji wa agizo hilo na baadae kutembelea kwenye shule hizo kuona namna wanafunzi wanavyoweza kuimba nyimbo za uzalendo wanapokuwa shuleni na hivyo kujiridhisha

Alisema kwamba wao kama wilaya wataendelea kulisimamia ipasavyo na kulitekeleza agizo hilo kwa vitendo huku wakianza na hatua ya kwanza kwa kuwaita kwenye kikao hicho huku akimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Isaya Mbenje na Wakuu wa Idara kwa kuweka mikakati ya kuona namna gani agizo hilo linatekelezwa kwa kuhakikisha wanaandika upya kwenye makaratasi na kubandikwa kila darasa wanalosoma wanafunzi.

"Lakini kubwa ni kwamba kila mwanafunzi achague kwenye somo wanayosoma achukue daftari moja aandika nyimbo hizo vizuri kwa nyuma kujikumbusha mara kwa mara kwa lengo la kuweza kuutambua na kuweza kuimba kwa ufasaha zaidi kila wakati "Alisema

Hata hivyo Katibu Tawala huyo aliwaagiza Waratibu wa kata wahakikishe maelekezo yaliyotolewa yanafanyiwa kazi na kupita kwenye kukagua kuona
kama nyimbo hizo zimefundishwa.

Awali akizungumza Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George alisema kwamba wamefika kwenye shule hizo kutekeleza agizo la Jafoi shule zao zirudi kwenye msingi ya kukumbushia nyimbo za uzalendo kwa wanafunzi.Alisema pia wataendelea kuwajenga vijana kuhusu uzalendo wakiwa wadogo ili kutengeneza Taifa Bora la kesho ambalo litakuwa chachu ya maendeleo kwa watanzania

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Pangani Isaya Mbenje alisema kwamba ni imani yake kwamba watendaji wa sekta ya elimu watakwenda kufanyia kazi kwa kuweka uelewa wa pamoja.

Alisema kwamba uelewa huo unaweza kuwasaidia kuona namna ya utekelezaji wa agizo hilo la serikali katika kujenga nidhamu,uzalendo wa vijana wa shule za msingi na sekondari za serikali wilayani humo.

Hata hivyo naye pia Afisa Elimu Taaluma wa wilaya ya Pangani Marietha alisema kwamba wanamshukuru Waziri Jaffo ambaye alihuisha uzalendo wa nchi kutokana na kwamba watu walikuwa wamejisahau sana nyimbo hizo miaka ya nyuma zilizokuwa ngao lakini kutokana na kwamba hapo katikati walipotea na kusahau hivyo wanahaidi kufanya vizuri sana

SALAMU ZA RAMBI RAMBI ZA MHE. SPIKA KWA AZAM MEDIA LIMITED

BALOZI SOKOINE AFUNGUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA MASHAMBA DARASA

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo amefungua Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nch (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (ldfs),wakiwa kwenye makundi kufanya uchambuzi yakinifu wa mimea na ikolojia shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Profesa Henry Mahoo wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (katikati) na Dkt. Moses Temi Mkufunzi Mkuu wa Shamba Darasa katika kituo cha Mafunzo ya Kilimo Nkindo wilaya ya Mvomero mara baada ya kufunguaMafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro 

……………………………………………. 

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo amefungua Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini (ldfs), katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro.

“Ni matumaini yangu kuwa elimu na ufahamu mtakauopata kupitia mafunzo haya, mtaitumia katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa katika maeneo ya mradi” alisema Balozi Sokoine.Mafunzo hayo ya siku 5 yanalenga kujenga uwezo kwa washiriki katika uanzishaji wa mashamba darasa katika vijiji na shehia ambako mradi wa LDFS unatekelezwa.

Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima. Lengo likiwa ni kuongeza usalama wa chakula na kuongeza kipato cha jamii. Mradi wa LDFS ambao umeandaa mafunzo haya ni mfano wa juhudi hizo za Serikali. Juhudi hizi zinahusisha uingizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea, mbegu zenye ubora; uboreshaji wa nyanda za malisho; utoaji wa huduma za ugani na mafunzo kupitia shamba darasa. Juhudi hizi zote zina lengo la urejesha ardhi iliyoharibika ili iweze kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na misitu.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo wa LDFS Bw. Joseph Kihaule amesema mradi huo utajumuisha na uanzishwaji wa mashamba darasa 100.
Wawezeshaji wa mradi huo ni Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA) ambapo washiriki wa mafunzo hayo wametoka Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii, Maji, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Idara ya Mazingira, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar. Aidha, washiriki wengine ni kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza Mradi za Mkalama, Micheweni, Magu, Nzega na Kondoa, pamoja waalikwa rasmi Daktari Moses Temi na Bwana Charles Mjema. 
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine (katikati)akihutubia wakati wa ufunguzi Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchini (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro, wengine pichani ni Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph Kihaule (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Faraja Ngerageza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya Wajumbe walioshiriki Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (LDFS), yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (ldfs),wakiwa kwenye uchambuzi yakinifu wa mimea na ikolojia shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (ldfs),wakiwa kwenye makundi kufanya uchambuzi yakinifu wa mimea na ikolojia shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

UDHIBITI MAPATO, NIDHAMU KWA WATUMISHI VIMEPAISHA UCHUMI-MAJALIWA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hatua ya kudhibiti upotevu wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali, uboreshwaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma kumesababisha kukua kwa uchumi. 

Amesema Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu na Serikali imeendelea kuongeza nguvu katika kudumisha amani na utulivu kwenye maeneo yote nchini, hali inayotoa fursa kwa wananchi wake kuendeleza shughuli zao za maendeleo. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 8, 2019) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly akiwa katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kikazi nchini Misri. 

Hivyo, amemuhakikishia Waziri Mkuu wa Misri kwamba Serikali ya Tanzanzia na wananchi wake wapo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya nchi hiyo na wananchi wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo mbili. 

Amesema nchi za Tanzania na Misri zinahitaji kutumia nafasi ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika ukuzaji wa uchumi, hivyo Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini. 

Amesema Serikali ya Tanzania imefanikiwa kiuchumi na kwa sasa ni nchi pili ambayo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika, ikitanguliwa na nchi ya Ivory Coast. Uchumi wa Tanzania ulitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka jana kutoka asilimia saba. 

“Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea vizuri, tumeendelea kushuhudia kushuka kwa mfumuko wa bei ambapo kwa sasa tumefikia asilimia 3.2, kiwango hiki ni matokeo ya kukuza sekta za madini, ujenzi, mawasiliano, utalii pamoja na kushuka kwa bidhaa za chakula na mafuta. Tunatarajia kiwango hiki kitashuka zaidi kwa sababu ya uwekezaji”. 

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, kipaumbele chake kilikuwa ni kukuza kiwango cha uchumi kutoka cha chini kwenda cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya viwanda.

TANZANIA ADVENTIST MEDIA CHANNELS YATUMA SALAMU ZA POLE KWA UONGOZI WA AZAM MEDIA GROUP

WADAU WA MAZINGIRA WAIOMBA SERIKALI KUWAENDELEZA,KUWASAIDIA WAGUNDUZI WA NISHATI JADIDIFU ILI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi Blog

WADAU wa mazingira nchini na hasa wanaokabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchini wameiomba kuhakikisha wagunduzi na wabunifu wa nishati jadidifu wanapewa kipaumbele na kusaidiwa.

Wakati kwa upende wa Serikali umesema ugunduzi na ubunifu katika nishati jadidifu ihusishayo nishati endelevu ni miongoni mwa fursa inayoleta ajira,kuongeza uzalishaji,ubunifu na kupunguza umasikini katika kuiletea nchi maendeleo endelevu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Pia imesema jamii inapaswa kubadili mtazamo na kufungua upeo zaidi kwa kuyaona masuala ya nishati jadidifu kwa jicho chanya kwa kuwa yanatoa fursa mbalimbali za kibiashara na uzalishaji.

Akizungumza wakati wa Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi kwenye Maonesho ya biashara Sabasaba, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ( TANTRADE)Ratifa Hamisi kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba amesema Serikali inatambua uwepo wa wabunifu wa kada mbalimbali katika kanuni nishati jadidifu kama moja ya mkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akifafanua zaidi kwenye Jukwaa la Mabadiliko ya Tabianchi ambalo limeandaliwa na Shirika la FORUMCC chini ya mradi wa kutoa elimu kuhusu nishati Jadidifu kupitia ufadhili wa taasisi inayoshugulikia masuala ya Nishati Jadilifu inayofahamika kwa jina la Hivos amesema Serikali inatambua changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira na athari za mabadiliko ya tabianchi kufikia katika maendeleo ya uchumi wa kati .

Amesema utumiaji wa nishati jadidifu utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari hizo za mabadiliko ya tabia nchi. "Changamoto hizo zimeathiri uzalishaji katika sekta ya kilimo ambayo ndio inachangia kwa kiasi kikubwa malighafi za viwanda,uhaba wa maji ambayo hutumika viwandani na uzalishaji wa nishati na uharibifu wa miundombinu ambayo hutumika kukutanisha malighafi, viwanda na masoko,tunaamini utumiaji wa nishati yadilifu itasaidia Kwa kiasi kikubwa kuondokana na janga hili la mabadiliko ya tabianchi," alisema

Ameongeza kutokana na jitihada za Serikali ikishirikiana na washirika wa maendeleo, sekta binafsi na asasi za kiraia, matokeo chanya ya lengo hilo yanaonekana kwani takwimu za sasa zinaonesha takribani nyumba milioni 26 (sawa na watu milioni 100) wanatumia nishati jadidifu .

Amesema nishati jadidifu katika Tanzania inahitaji mpango wenye taarifa sahihi za sekta ya nishati jadidifu ili kuweza kuainisha njia za maendeleo za baadae na kuhakikisha watunga sera na wafanya maamuzi wana taarifa sahihi kuhusu nishati mbadala. 

"Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini imetoa mpango wa mfumo wa umeme tangu mwaka 2016 (The 2016 Power System Master Plan (PSMP))mfumo huu unazingatia ukuaji wa uchumi na sera za serikali na miongozo.

"Ambapo miongozo ya sera ni pamoja na utayari wa Serikali kukuza uchumi kupitia dira ya 2025, MKUKUTA na Mpango wa Miaka Mitano (Five-Year Development PlanII (2016/17-2020/21, FYDPII)ambapo moja ya matokeo ya mpango huu ni kukuza uchumi kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2021 na kupunguza umaskini kwa asilimia 16.7 kutoka asilimia 28.2 ya mwaka 2011/12," amesema

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Amos Maganga ameeleza wao wanatambua na kuthamini mchango unaotolewa na wabunifu wa vyuoni na wabunifu binafsi katika kuzingatia maendeleo ya nchi.

"Takribani miradi 20 REA imeweza kuwasaidia wabunifu mbalimbali katika kuhakikisha wanafanya kazi zao za kiubunifu ipasavyo na kusaidia nchi katika kuondokana nachangamoto mbalimbali.

''REA kuna programu ambazo zinaendelea na tumekuwa tunawasaidia wabunifu mbalimbali Kutoka vyuoni au wale wabunifu binafsi kwani tuna takribani fedha kupitia kwa wahisani dolla Milioni 19 sawa na zaidi ya Bilioni 40 ambazo zipo Kwaajili ya wabunifu Na wanaoweka miradi ya nishati bora vijijini,"amesema Mhandisi Maganga

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Shirika la ForumCC Rebecca Muna amezungumzia umuhimu kwa Tanzania ya viwanda kuwa na nishati ya uhakika lakini ni vema kuangalia kuna fursa gani kama nchi ambazo zitatumika kuleta maendeleo huku kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Hata hivyo Muna ametoa mwito kwa wabunifu kuona fursa iliyopo katika nishati jadilifu huku kwa Serikali akiishauri kuanza kutengeneza mazingira mazuri kwa sera na sheria katika kulea na kukuza vipaji vya wabunifu katika sekta hii ya nishati jadidifu .Amesisitiza kwamba "Kama vipaji hivi vikiendelezwa kwa wabunifu wetu tutaweza kuchangiza kwa kiasi kikubwa sana upatikanaji wa nishati safi na salama kwa viwanda vyetu nchini."

"Tanzania tunavyanzo vya asili vingi sana hivyo uwekezaji ukifanya katika vyanzo hivyo tunauwezo mkubwa wa kuzalisha nishati jadidifu ikiwemo kinyesi cha mifugo," amesema Muna

Kwa upende wake Adam Nalima ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Joseph,amesema wao waliamua kuja na wazo la kuhalikisha wanaboresha mazingira nchini ambalo lilikuwa ni uzalishaji wa umeme kwa njia ya nishati jadilifu kwa kutumia jua na upepo kwa wakati mmoja.
Hata hivyo wadau wa mazingira wakati wa majadiliano wanaonesha kutofurahishwa na kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira ambayo athari zake imeanza kuonekan ikiwemo joto kupanda kiasi katika baadhi ya nchi akitolea mfano ya India watu waliopoteza maisha kwasababu ya joto kali.
 Baadhi ya wadau wa mazingira wakifuatilia masala wakati wa kongamano la Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi ambako limeandaliwa na FORUMCC
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE) Ratifa Hamisi(katikati) akisikiliza maelezo ya mmoja ya wagunduzi wa nishati jadidifu kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandella Profesa Njau (kushoto) wakati wa kongamano la Jukwaa la Mabadiliko ya tabianchi
Mdau wa mazingira na hasa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambaye anajihusisha  na utengenezaji wa mkaa mbadala Yusta Kibona akifafanua kuhusu nishati jadidifu

BALOZI SOKOINE AFUNGUA MAFUNZO YA WAWEZESHAJI WA MASHAMBA DARASA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Balozi Joseph Sokoine leo amefungua Mafunzo ya Msasa ya Uwezeshaji kuhusu Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame nchini (ldfs), katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro.

“Ni matumaini yangu kuwa elimu na ufahamu mtakauopata kupitia mafunzo haya, mtaitumia katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa katika maeneo ya mradi” alisema Balozi Sokoine. Mafunzo hayo ya siku 5 yanalenga kujenga uwezo kwa washiriki katika uanzishaji wa mashamba darasa katika vijiji na shehia ambako mradi wa LDFS unatekelezwa.

Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza miradi inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa kusogeza karibu teknolojia kwa wakulima. Lengo likiwa ni kuongeza usalama wa chakula na kuongeza kipato cha jamii. Mradi wa LDFS ambao umeandaa mafunzo haya ni mfano wa juhudi hizo za Serikali.

 Juhudi hizi zinahusisha uingizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo matumizi sahihi ya mbolea, mbegu zenye ubora; uboreshaji wa nyanda za malisho; utoaji wa huduma za ugani na mafunzo kupitia shamba darasa. Juhudi hizi zote zina lengo la urejesha ardhi iliyoharibika ili iweze kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na misitu.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo wa LDFS Bw. Joseph Kihaule amesema mradi huo utajumuisha na uanzishwaji wa mashamba darasa 100.

Wawezeshaji wa mradi huo ni Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Miti Tanzania (TTSA) ambapo washiriki wa mafunzo hayo wametoka Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii, Maji, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Idara ya Mazingira, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar.

Aidha, washiriki wengine ni kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza Mradi za Mkalama, Micheweni, Magu, Nzega na Kondoa, pamoja waalikwa rasmi Daktari Moses Temi na Bwana Charles Mjema. 


 Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (ldfs),wakiwa  kwenye uchambuzi yakinifu wa mimea na ikolojia shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo ya Msasa ya kuhusu Uwezeshaji Mashamba darasa kwa Maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu za uwezeshaji za wilaya wa mradi wa kurejesha ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame ya nchi (ldfs),wakiwa  kwenye makundi kufanya uchambuzi yakinifu wa mimea na ikolojia shambani katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

UDHIBITI MAPATO, NIDHAMU KWA WATUMISHI VIMEPAISHA UCHUMI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hatua ya kudhibiti upotevu wa mapato na matumizi ya fedha za Serikali, uboreshwaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma kumesababisha kukua kwa uchumi.

Amesema Tanzania ni nchi yenye amani na utulivu na Serikali imeendelea kuongeza nguvu katika kudumisha amani na utulivu kwenye maeneo yote nchini, hali inayotoa fursa kwa wananchi wake kuendeleza shughuli zao za maendeleo. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Julai 8, 2019) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly akiwa katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kikazi nchini Misri.

Hivyo, amemuhakikishia Waziri Mkuu wa Misri kwamba Serikali ya Tanzanzia na wananchi wake wapo tayari kuendelea kushirikiana na Serikali ya nchi hiyo na wananchi wake katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo mbili.

Amesema nchi za Tanzania na Misri zinahitaji kutumia nafasi ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika ukuzaji wa uchumi, hivyo Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Misri waje kuwekeza nchini.

Amesema Serikali ya Tanzania imefanikiwa kiuchumi na kwa sasa ni nchi pili ambayo uchumi wake unakua kwa kasi barani Afrika, ikitanguliwa na nchi ya Ivory Coast. Uchumi wa Tanzania ulitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka jana kutoka asilimia saba.

“Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea vizuri, tumeendelea kushuhudia kushuka kwa mfumuko wa bei ambapo kwa sasa tumefikia asilimia 3.2, kiwango hiki ni matokeo ya kukuza sekta za madini, ujenzi, mawasiliano, utalii pamoja na kushuka kwa bidhaa za chakula na mafuta. Tunatarajia kiwango hiki kitashuka zaidi kwa sababu ya uwekezaji.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano tangu ilipoingia madarakani mwaka 2015, kipaumbele chake kilikuwa ni kukuza kiwango cha uchumi kutoka cha chini kwenda cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia sekta ya viwanda.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya kuwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KAMATI YA UONGOZI NA YA BAJETI YA CPA KANDA YA AFRIKA KUKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

RAIA WATATU WA KIGENI KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0

Na Emanuel Madafa, Michuzi TV, Mbeya 

Raia Watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya wakikabiliwa na shitaka la uhujumu uchumi baada ya kukutwa wakisafirisha dhahabu gramu 1043.3 yenye thamani ya shilingi Milioni 98.5 kinyume cha sheria ya madini namba 14 ya mwaka 2010.

Washitakiwa hao Clive Rooney (62) raia wa Trish , na wenzake raia wa Uingereza Ross Stephan (34) na Robert Charles (59) wamekutwa na madini hayo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Songwe Mkoani Mbeya Julai 3, mwaka huu.

Mbele ya Kaimu Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mkoa Venance Mlingi washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chohote kutokanana mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza shauri hilo.

Upande wa Serikali umewakilishwa na mawakili watatu ambao ni Lugano Mwakilasa ,Jacqueline Nyantori na Ofmed Mtenga wakati upande wa utetezi ukiwa na mawakili watatu Boniphace Mwabukusi James Kyando na Kamru Habib.

Mwanasheria wa Serikali Jacqueline Nyantori ameileza Mahayana hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba Mahakama iendelee na utaratibu.

Akitoa utetezi mbele ya Hakimu Venence Mlingi wakili wa utetezi Boniphace Mwabukusi ameiomba Mahakama kuwapatia dhamana wateja wake kwa madai kuwa mshitakiwa wa kwanza ambaye ni Clive Rooney (62) anasumbuliwa na Ugonjwa haukutajwa nakwamba anatumia dawa maalumu.

Hata hivyo ombi hilo lilipingwa na wakili wa serikali Jacqueline Nyantori na kudai kuwa Ugonjwa huo utatibiwa kwa mujibu wa sheria ya nchi akiwa gerezani.Washitakiwa hao wote watatu wamerejeshwa mahabusu mpaka Julai 22 mwaka huu .







TUNAUNGANA NA AZAM MEDIA KUOMBOLEZA VIFO VYA WANAHABARI WENZETU

NMB Yakabidhi Gawio la Shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango – Dr. Philip Mpango, akipokea gawio la shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya NMB kwa mwaka 2018 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Joseph Semboja (pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Albert Jonkergouw na Afisa Mkuu wa Fedha Ruth Zaipuna.



Benki ya NMB jana ilikabidhi gawio la shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali ikiwa ni sehemu ya faida ya Benki hiyo ya mwaka 2018. 

Akikabidhi hundi kwa Waziri wa Fedha na Mipango – Dr Philip Mpango, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Albert Jonkergouw alisema fedha hizo ni sehemu ya hisa ambazo ni asilimia 31.8 zinazomilikiwa na serikali ndani ya benki ya NMB.
Pamoja na gawio hilo, pia NMB imelipa serikalini jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 168.8 ikiwa ni kodi tofauti tofauti kama kodi ya mishahara ya wafanyakazi, kodi ya bidhaa, kodi uendelezaji ufundi stadi (SDL) na kodi ya ongezeko la thamani (VAT). 

“Tupo imara sana kama Benki ambayo vitabu vyetu vya hesabu vinaonyesha mwelekeo chanya unaosababishwa na utoaji huduma bora za kifedha,” alisema Bw Jonkergouw, na kuongeza kuwa mazingira ya kufanya biashara nchini bado yana fursa mbalimbali na NMB kama Benki yenye mtandao mkubwa ipo katika nafasi nzuri zaidi ya kuiunga mkono jumuiya ya wafanyabiashara nchini ili kufikia malengo yao. 

Akipokea gawio la serikali, Dr. Mpango alifurahi kupokea gawio hili kutoka NMB na kutoa changamoto kwa makampuni na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano. “NMB ni mfano wetu mzuri wa mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika ubinafsishaji nchini, wamekuwa wakifanya vizuri sana wakati wengine wamekuwa wakilalamika tu bila na kuacha kuzitumia fursa nyingi zilizopo nchini kama wanavyofanya NMB katika kupanua zaidi biashara zao,” aliongeza. 

Katika mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam, wanahisa walipitisha kiasi cha shilingi bilioni 33 kama gawio ambalo limegawanywa kwa wanahisa ikiwa ni sawa na shilingi 66 kwa hisa moja. Katika kipindi cha mwaka uliopita, NMB iliweza kupata faida kabla ya kodi ya shilingi bilioni 142 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3 kutoka shilingi bilioni 138 katika mwaka uliotangulia. 

Bw Jonkergouw alisema Benki inaendelea kuweka uwiano mzuri katika kutoa gawio kwa wanahisa na pia kuwekeza ili kuimarisha biashara ya benki na kuifanya ichangie zaidi katika uchumi. NMB ni moja ya makampuni yaliyobinafsishwa na serikali na kuweza kupata mafanikio makubwa ambapo katika kipindi cha miaka kumi imeweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 118 kwa serikali kama gawio. 


“NMB imekuwa ikifanya vizuri sana katika biashara na itaendelea kujizatiti ili kuwa imara na kutoa huduma bora zaidi. Ili kutekeleza hili, NMB itaendelea kujiimarisha kiuwekezaji katika mifumo yake ya malipo ili kuwawezesha wateja kupata huduma bora zaidi na kuchangia ukuaji wa uchumi ,alisema

NMB Yakabidhi Gawio la Shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango – Dr. Philip Mpango, akipokea gawio la shilingi  Bilioni 10.48 kwa Serikali, ikiwa ni sehemu ya faida ya benki ya NMB kwa mwaka 2018 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi Joseph Semboja (pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Albert Jonkergouw na Afisa Mkuu wa Fedha Ruth Zaipuna. 



Benki ya NMB jana ilikabidhi gawio la shilingi Bilioni 10.48 kwa Serikali ikiwa ni sehemu ya faida ya Benki hiyo ya mwaka 2018. 

Akikabidhi hundi kwa Waziri wa Fedha na Mipango – Dr Philip Mpango, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Albert Jonkergouw alisema fedha hizo ni sehemu ya hisa ambazo ni asilimia 31.8 zinazomilikiwa na serikali ndani ya benki ya NMB.
Pamoja na gawio hilo, pia NMB imelipa serikalini jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 168.8 ikiwa ni kodi tofauti tofauti kama kodi ya mishahara ya wafanyakazi, kodi ya bidhaa, kodi uendelezaji ufundi stadi (SDL) na kodi ya ongezeko la thamani (VAT). 

“Tupo imara sana kama Benki ambayo vitabu vyetu vya hesabu vinaonyesha mwelekeo chanya unaosababishwa na utoaji huduma bora za kifedha,” alisema Bw Jonkergouw, na kuongeza kuwa mazingira ya kufanya biashara nchini bado yana fursa mbalimbali na NMB kama Benki yenye mtandao mkubwa ipo katika nafasi nzuri zaidi ya kuiunga mkono jumuiya ya wafanyabiashara nchini ili kufikia malengo yao. 

Akipokea gawio la serikali, Dr. Mpango alifurahi kupokea gawio hili kutoka NMB na kutoa changamoto kwa makampuni na taasisi nyingine za serikali kuiga mfano. “NMB ni mfano wetu mzuri wa mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika ubinafsishaji nchini, wamekuwa wakifanya vizuri sana wakati wengine wamekuwa wakilalamika tu bila na kuacha kuzitumia fursa nyingi zilizopo nchini kama wanavyofanya NMB katika kupanua zaidi biashara zao,” aliongeza. 

Katika mkutano mkuu wa wanahisa uliofanyika mwezi uliopita jijini Dar es Salaam, wanahisa walipitisha kiasi cha shilingi bilioni 33 kama gawio ambalo limegawanywa kwa wanahisa ikiwa ni sawa na shilingi 66 kwa hisa moja. Katika kipindi cha mwaka uliopita, NMB iliweza kupata faida kabla ya kodi ya shilingi bilioni 142 ikiwa ni ongezeko la asilimia 3 kutoka shilingi bilioni 138 katika mwaka uliotangulia. 

Bw Jonkergouw alisema Benki inaendelea kuweka uwiano mzuri katika kutoa gawio kwa wanahisa na pia kuwekeza ili kuimarisha biashara ya benki na kuifanya ichangie zaidi katika uchumi. NMB ni moja ya makampuni  yaliyobinafsishwa na serikali na kuweza kupata mafanikio makubwa ambapo katika kipindi cha miaka kumi imeweza kutoa kiasi cha shilingi bilioni 118 kwa serikali kama gawio. 


“NMB imekuwa ikifanya vizuri sana katika biashara na itaendelea kujizatiti ili kuwa imara na kutoa huduma bora zaidi. Ili kutekeleza hili, NMB itaendelea kujiimarisha kiuwekezaji katika mifumo yake ya malipo ili kuwawezesha wateja kupata huduma bora zaidi na kuchangia ukuaji wa uchumi ,alisema

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 9,2019

Waandishi wa Habari Waaswa Kuzingatia Uzalendo na Weledi Wanapotangaza Fursa Zilizopo SADCo

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Agnes Kayola akieleleza umuhimu wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Tanzania kuhusu masuala ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Hayo yemejiri leo Julai 8,2019 mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yanayofanyika mjini Morogoro kwa siku tatu. 
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo yakuwajemgea uwezo waandishi wa habari hapa nchini ili waweze kuripoti habari zinazohusu Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Hayo yemejiri leo Julai 8,2019 mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mafunzo hayo yanayofanyika mjini Morogoro kwa siku tatu. 

************* 

Na Frank Mvungi- MAELEZO, Morogoro 

Waandishi wa Habari nchini wameaswa kuzingatia uzalendo na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao wakati wote wa kuripoti habari zinazohusu fursa zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na mkutano wa wakuu wa nchi wanachama utakaofanyika Jijini Dar es Salaam Agosti 17 na 18, 2019. 

Akizungumza leo mjini Morogoro wakati akifungua awamu ya kwanza ya mafunzo yakuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika na kuripoti habari za Jumiya hiyo, Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amesema kuwa mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama unakuja na fursa nyingi zitakazowanufaisha wananchi wote. 

“ Tunawaomba Waandishi wa Habari kutekeleza jukumu la kutangaza habari zinazohusu SADC kwa uzalendo, weledi na kwa ufanisi ili watanzania waweze kushiriki kikamilifu kutokana na umuhimu wa Jumuiya hii na kutumia fursa za kiuchumi na biashara zinazopatikana kupitia wananchi takribani milioni 450 wa nchi zote za SADC”. Alisisitiza Mhe Shonza akifafanua Mhe Shonza amesema kuwa kila mwandishi wa habari analo jukumu la kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafahamu fursa zilizopo katika Jumuiya hiyo na mamna zinavyoweza kuwanufaisha wananchi wote katika nyanja za kiuchumi na kijamii. 

Aliongeza kuwa waandishi wa habari wa Tanzania kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na uelewa wa pamoja wakati wa mkutano huo kwa kutambua kuwa wao ni daraja kati ya wananchi na Serikali pamoja na Jumuiya zote ambazo Tanzania ni mwanachama ikiwemo SADC. 

“Ni matumanini yangu kuwa baada ya mafunzo haya mtawaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa SADC kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi wanachama, fursa za kiuchumi, Namna nchi yetu inavyotekeleza mikakati mbalimbali ya SADC, Fursa za masoko ndani ya SADC kutokana na bidhaa na mazao ya kilimo yanayozalishwa katika nchi wanachama” Alisisitiza Mhe Shonza. 

Katika kusisistiza umuhimu wa amani na utulivu Mhe. Shonza aliwaasa wanahabari kuwaelimisha wananchi umuhimu wa amani kipindi choche cha mkutano huo wa wakuu wa nchi wanachama na hata baada ili kuendelea kujenga taswira nzuri ya Tanzania. 

Baadhi ya fursa zinazotokana na mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo utakaofanyika mwezi ujao hapa nchini ni pamoja na usafiri na usafirishaji, malazi na utalii kwa wageni hao zaidi ya 1000 wanaotarajiwa kuja hapa nchini kutokana na mkutano huo. 

Aidha, Mheshimiwa Shonza aliwataka waandishi wote wa habari hapa nchini kutumia nafasi zao kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa amani iliyopo hapa nchini ambayo ni moja ya kivutio kikubwa kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali kuja na kuwekeza hapa nchini. 

“ Sitarajii mwandishi wa habari wa Tanzania kutumia kalamu yake kuchafua taswira ya nchi yetu katika kipindi hiki cha mkutano huu mkubwa na hata baada ya mkutano, matarajio ya Serikali ni kuendelea kuona mnatangaza mafanikio ya Jumuiya na fursa zilizopo ili ziweze kuwanufaisha wananchi” Alisisitiza Mhe. Shonza. 

Katika kutekeleza jukumu hilo amewaasa waandishi hao kuzingatia kuwa jukumu la kutangaza fursa zilizopo katika Jumuiya hiyo ni la kila mwanahabari ili kuwajengea uelewa wananchi juu ya namna watakavyoweza kunufaika na idadi kubwa ya wananchi waliopo katika jumiya hiyo. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) linalodhamini mafunzo hayo kwa kushirikiana na Sekretarieti ya SADC, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Dagmore Tawonezvi amesema kuwa mafunzo hayo yanatokana na maombi ya Serikali ya Tanzania na yatasaidia kujenga uelewa kuhusu fursa zilizopo na namna ya kuzitumia ili kuchochea maendeleo hapa nchini na katika nchi wanachama wa SADC. 

Aliongeza kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na nchi wanachama kujenga uwezo kwa waandishi wa habari ili waweze kutangaza na kuwaelimisha wananchi kuhusu jumuiya hiyo na manufaa yake katika kukuza uchumi. 

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi Agnes Kayola amesema kuwa mafunzo hayo yanafanyika kwa awamu mbili zitakazoshirikisha waandishi wa habari 30 kwa kila awamu. 

Mkutano huo utatanguliwa na maonesho ya wiki ya viwanda yatakayotumika kutangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchinina nchi za SADC kwa madhumuni ya kuhamasisha ukuaji wa viwanda katika nchi za SADC . 

Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo unafanyika Tanzania mwezi Ujao ambapo Tanzania inatarajiwa kupokea wageni zaidi ya 1000 kutoka nchi wanachama wa SADC, katika mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajia kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Agosti 2019 hadi Agosti 2020. 

Mkutano huo wa wakuu wa nchi wanachama utakuwa na kauli mbiu ”Mazingira wezeshi ya Kibiashara kwa Maendeleo Jumuishi na Endelevu ya Viwanda” utatanguliwa na vikao vya awali vya ngazi ya Makatibu Wakuu na Mawaziri wa SADC, Unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi 16 wanachama wa SADC .
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images