Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

Waziri Kabudi atembelea maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba).

$
0
0

Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Tagie Daisy Mwakawago Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Bw. Hassan Mnondwa akielezea picha za Mawaziri waliowahi kuiongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa wanafunzi waliojitokeza kwenye banda hilo. 
Bw. Joseph Mwasoto akifanunua jambo kwa wateja waliyotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba 
Bi. Praxida Gasper akifanunua jambo kwa wateja waliyotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye maonesho ya sabasaba 
Huduma zikiendelea kutolewa kwa Wananchi mbalimbali wanaoendelea kutembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya Sabasaba 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Chuo cha Diplomasia kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akitizama Ramani ya Majengo mapya ya Chuo hicho yanayoyengwa sasa hivi, Kurasini jijini Dar Es Salaam 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akijionea ufanisi wa utengezaji wa bidhaa mbalimbali za Nyumbani zilizotengenezwa na Jeshi la Magereza, alipotembelea banda la Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mahojiano na wanahabari kwenye maonesho ya biashara kimataifa maarufa sabasaba yanayofanyika jijini Dar es Salaam

TBS YAELEZEA MABADILIKO KATIKA SHERIA YA VIWANGO NAMBA 2 YA MWAKA 2009,YAWATOA HOFU WADAU

$
0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi Blog

SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS) limeufahamisha wadau na wananchi kwa ujumla kufahamu kwamba Bunge limepitisha sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo imeleta mabadiliko katika sheria ya viwango namba mbili ya mwaka 2009.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na TBS kupitia Mkurugenzi Mkuu wake Dk.Yusuf Ngeya amesema katika mabadiliko hayo TBS imeongezewa majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi, majukumu ambayo yalikuwa yanatakelezwa hapo awali na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania(TFDA).

Amesema kuwa Wizara, taasisi na halmashauri zilizokuwa zimekasimiwa majukumu na TFDA kwa wakati huo kusimamia masuala ya usalama hasa katika machinjio ,bucha,mama lishe na mahoteli zitaendelea kufanya kazi hiyo wakati hatua za kuweka utaratibu mpya chibi ya TBS ukiendelea.


Pia Dk.Ngenya amesemawa kwa sasa matakwa ya kibali cha usajili wa bidhaa zinazoingizwa nchini,kilichokuwa kinatolewa na TFDA  na kuingizwa kwenye mifumo ya kieletroniki ya TRA kimeondolewa badala yake cheti cha ukaguzi TBS (CoC) au kibali cha shehena husika kinachotolewa na TBS kitatumika.

Pia wafanyabiashara hao leseni za biashara na usajili wa majengo ambazo zimekwisha muda wake, wataendelea kutoa huduma kwa katika kipindi cha mpito cha miezi mitatu wakati shirika likiendelea kukamilisha taratibu za uhuishaji wa vyeti husika .

"Vile vile wafanyabiashara ambao vibali vyao vimekisha muda wake  wafike katika ofisi za TBS iliyokaribu ama watume maombi kwa njia ya barua pepe ili kupatiwa barua itakayokuwa kielelezo katika kipindi cha mpito," amesema.

Pia amesema shirika linatoa hofu wadau wote kuwa wamba mabadiliko hayo hayataathiri utendaji wa taasisi kwani limejipanga vizuri kuhakikisha huduma hizo zinaendelea katika kiwango kinachotakiwa.

BREAKING NEWZZZZZ: Wafanyakazi Azam Media wapata ajali wakielekea Chato...wapo waliopoteza maisha

$
0
0

TAARIFA ambazo zimetufikia chumba chetu cha habari cha Michuzi Media Group, inaelezea wafanyakazi wa Azam Media wamepata ajali ya gari mkoani Singida leo Julai 8 mwaka 2019.

Kwa Mujibu wa taarifa za awali zinadai kuwa katika ajali hiyo kuna waliopoteza maisha na wengine kujeruhiwa.Walikuwa wanakwenda Chato kikazi kwa ajili ya kuonesha LIVE moja ya matukio ya Rais Dkt.John Magufuli.

Baadhi ya Waandishi waandamizi wa Azam Media wameiambia Michuzi Blog na Michuzi TV kuwa kwa sasa wanasubiri taarifa rasmi kutoka wenye mamlaka ili kuuhabarisha umma na wanaodhaniwa kupoteza maisha na wafanyakazi wingine  wakiwamo waandishi na Wapiga picha pamoja na mafundi mitambo.

Tutaendelea kuwajuza kinachoendelea baada ya taarifa rasmi kutumika.Endelea kufuatilia Michuzi Blog na Michuzi TV.

BENKI YA NMB YAJIPANGA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA NGAZI ZOTE WANAKUZA MITAJI YAO

$
0
0

Afisa mkuu wa fedha benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa kwanza kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara cheti kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akishuhudia. NMB imewakutanisha wafanyabiashara mbali mbali kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB mkoa wa Singida kutoa elimu ya biashara.
Afisa mkuu wa fedha benki ya NMB, Ruth Zaipuna (wa kwanza kushoto) akimkabidhi mfanyabiashara cheti kilichotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa kupigiwa mfano. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard akishuhudia. NMB imewakutanisha wafanyabiashara mbali mbali kwenye Kongamano la Klabu ya Biashara ya NMB mkoa wa Singida kutoa elimu ya biashara.


Benki ya NMB imejipanga kuhakikisha wafanyabiashara wa ngazi zote wanakuza mitaji yao, itakayowawezesha kuajiri Watanzania wengi na hivyo kupunguza makali ya uhaba wa ajira nchini.

Pia waajiriwa hao kupitia kodi watakazolipa, zitachangia kukuza uchumi wa Taifa .

Hayo yamesemwa juzi na Afisa mkuu wa fedha benki ya NMB, Ruth Zaipuna, wakati akizungumza kwenye kongamano iliyohudhuriwa na wanachama wa NMB Business Club mkoa wa Singida. Warsha hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach Hotel mjini hapa.

Akifafanua, alisema NMB ina business Clubs 36 nchi nzima, na kila moja ina wanachama kati ya 150 na 300.

“Kundi hilo kubwa la wanachama limekuwa likifaindika na mafunzo mbalimbali tunayotoa. Mafunzo hayo yanajumuisha na bidhaa zinazotolewa kwao na Benki yetu,ikiwemo jinsi ya kutunza vitabu vya mahesabu. Vile vile elimu ya masoko na elimu ya mlipa kodi, ambayo tumekuwa tukifanya kwa kushirikiana na TRA”,amesema Ruth.

Akifafanua zaidi, afisa huyo amesema lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wote wanakuza mitaji yao.Aidha, amesema shughuli za wafanyabiashara wadogo na wa kati (MSMEs) ni muhimu mno kwa uchumi wa Taifa letu.

“Uchumi kwa ujumla wake, unategemea mafanikio ya hizi MSME. Nasi tunajivunia sana kuona kada hii ya biashara imeendelea kukua kadri siku zinavyokwenda. Hayo ni mafanikio makubwa sana, na ya kujivunia”,alisema.

Kwa mujibu wa Afisa Zaipuna, jumla ya wafanyabiashara 200,00 wadogo na wa kati (MSMEs) nchi nzima,mikopo yao inafikia thamani ya shilingi bilioni 600.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha biashara NMB,Donatus Richard,amesema lengo la kuwaunganisha au kuwakutanisha wafanyabiashara hao zaidi ya 200 kwenye warsha hiyo,ni wao kufahamaiana na kupeana uzoefu wa biashara za aina mbalimbali.

“Lengo mahususi kuwa na klabu hizi,ni kuendeleza mahusiano na wateja wetu.Mahusiano haya yamesaqidia mno benki kukua.NMB ikiendelea kukua,biashara nazo zinakua kwa kiwango kikubwa”,amesema Richard kwa kujiamini.

Wakati huo huo,mfanyabishara wa mabasi (Dubai express) Evans Makundi,ametumia fursa hiyo kuipongeza tawi la NMB mkoa wa Singida,kwa madai halina urasimu katika kupata mikopo.

Wafanyabiashara washauriwa kutumia kifaa cha kufuatilia bidhaa zao

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
KAMPUNI ya Techzanite Consultants Ltd inayojishuhulisha na teknolojia imeingiza nchini kifaa cha Roambee ambacho kinatumika kuweza kuonyesha sehemu pamoja na hali ya bidhaa, ambapo ndani yake kuna kamera, kitambuzi na simu kadi.

Meneja wa Kukuza Biashara wa Kampuni hiyo, Hassan Abba akizungumzia kifaa hicho,  katika maonesho ya 43 ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, amesema bidhaa hiyo itasaidia wafanyabiashara kuzuia kufanya maamuzi ya bidhaa zao kabla ya kupata hasara.

Amesema kifaa hicho, ambacho ni kipya hapa nchini kinatoka marekani ambapo wameingia ubia na Kampuni hiyo na masoko ya Tanzania, ambacho kinafanya kazi katika nchi 190.

Abba amesema lengo kubwa la kuingiza kifaa hicho ni hapa nchini ni kuwasaidia wafanyabiashara kufanya maamuzi ya awali na sio kusubiri kupata hasara ndiyo afanye kupata maamuzi, kwa  sababu kitawasaidia kuwapa taarifa za kutochezewa mizigo yao ikiwemo biashara ya nyama kabla hazijafika sehemu ya mwisho.

Amesema kazi kubwa ya kifaa hicho ni kuweza kutambua hali ya bidhaa hasa katika mnyororo wa baridi, mfano bidhaa kama nyama inatakiwa muda mwingi kukaa kwenye friji na iwapo umeme utaleta shida na kupunguza kiwango cha baridi kwenye friji basi kifaa hicho kitasaidia kutoa taarifa ambazo kama mmiliki atazingatia na kuchukua hatua basi nyama hiyo haitaaribika na atakuwa amekoa kupata hasara.

Amesema, mfanyabiashara wa nyama anaweza kutambua bidhaa yake ipo katika hali gani kwa sababu unatakiwa isafiri bila kuwa na hali ya kucheza kama  ni nyuzi joto -4 basi itembee katika temperature hiyo hiyo na iwapo temperature itabadilika hicho kifaa kitampa ishara yule mwenye malu yake, lakini pili inaweza kutumika kama ripoti ya ukaguzi katika mamlaka mbalimbali  na pia unaweza ukapata bima kupitia ripoti hiyo," amesema Abba

Ameongeza kuwa, kifaa hicho kinaweza kuwa kielelezo kwa mteja ambae atasema bidhaa yake imeharibika, ambapo ataoneshwa jinsi ambavyo 'temperature'i iliyowekwa kuanzia pointi A hadi sehemu iliyofikia, kwa hiyo hakutokuwa na malumbano.

Meneja huyo, pia alisema, kifaa hicho inakitambuzi ha mwanga, kama mtu atachezea mzigo wako,mwanga ukipenya kitatoa taarifa kuwa kuna mtu anataka kukuibia mzigo wako, kwa hiyo hatua za haraka zitachukuliwa.
"Nawaomba wafanyabiashara na makampuni makubwa ya nyama kutumia kifaa hiki kwa ajili ya kuokoa bidhaa zao, waje tu tufanye mazungumzo ili tufanye biashara, kwa sababu kifaa hiki kinakodishwa hakiuzwi ambapo mpaka sasa kuna baadhi ya Kampuni ambazo tupo nazo kwenye mazungumzo, lakini bado muitikio ni mdogo kutokana na kifaa hiki kuwa ni kipya hapa nchini, amesema.
Meneja wa masoko wa kampuni ya Techzanite Consultants Ltd, Hassan Abba akifafanua kwa wananchi namna kifaa cha kuonyesha sehemu na hali ya ubora wa bidhaa kinavyofanya kazi katika maonyesho ya 43 ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Balozi Seif kuimarisha michezo jimboni kwake

$
0
0
  Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi na Mbunge wa Jimbo hilo Bahati Abeid Nassir wakizungumza na Wanamichezo wa Mpira wa Pete wa Timu za Wadi za Mahonda na Fujoni kabla ya kuwakabidhi vifaa vya Michezo hapo Tawi la CCM Kitope “B”.
 Balozi Seif na Mbunge Bahati wakiwakabidhi Vifaa vya Michezo Viongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Fujoni Mwanafatu Othman na Ramla Said.
 Balozi Seif na Mbunge Bahati wakiwakabidhi Vifaa vya Michezo Viongozi wa Timu ya Mpira wa Pete ya Mahonda Zawadi Aley na Zainab Issa.
Balozi Seif akimkabidhi Kepteni wa Timu ya Mpira wa Pete ya Mahonda Fedha za Usafiri wa wachezaji hao kwa ajili ya kushiriki mchezo wa majaribio huko Mkokotoni Mkoa Kaskazini Unaguja. Picha na – OMPR – ZNZ.

Azma ya Uongozi wa Jimbo la Mahonda bado ipo pale pale katika kuhakikisha inaimarisha Michezo ili ifikie siku Jimbo hilo liwe na Timu iliyopevuka kimichezo na kushiriki Mashindano makubwa zaidi ya Kimataifa.

Mwakilidhi wa Jimbo hilo Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla fupi ya kuzikabidhi Vifaa vya Michezo Timu mbili za Mpira wa Pete {Netball} za Wadi za Mahonda na Fujoni iliyofanyika katika Ukumbi wa Tawi la CCM Kitope “B” Wilaya ya Kaskazini B.

Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Vifaa hivyo kukamilisha ahadi iliyotolewa na Mke wake Mama Asha Suleiman Iddi aliyoitoa baada ya kushuhudia pambano la kirafiki la Mchezo wa Mpira wa Pete {Netball} uliozikutanisha Timu za Madada wa Fujoni dhidi ya Kitope lililofanyika katika uwanja wa mahonda Kiwandani mnamo Tarehe 5 Febuari Mwaka huu wa 2019.

Alisema uimarishaji huo wa Michezo ndani ya Jimbo hilo unakwenda sambamba na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuimarisha Sekta ya Michezo wa vile hivi sasa mbali ya kusaidia kulinda afya lakini pia imekuwa soko la ajira.

Balozi Seif aliwaomba Vijana wa Kike mbali ya kuendeleza mchezo wa Pete lakini pia wana fursa ya kuandaa Timu ya Jimbo ya mpira wa soka kwa vile tayari upo muelekeo wa kuimarika kwa mchezo huo kwa upande wa akina mama kama hivi sasa inavyoonekana kwenye mashindano ya Dunia ya Soka la Wanawake.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mahonda Bahati Abeid Nassir amesema inapendeza kuona hivi sasa vijana wengi wa kike wamehamasika kushiriki kwenye michezo mbali mbali inayoongeza ajira hasa Vikosini.

Mbunge Bahati aliwataka Wanawake hao wa timu za Mpira wa Pete wa Wadi za Mahonda na Fujoni wafanye mazoezi kwa malengo na kuacha ile tabia ya kuonekana Baadhi ya Wanawake hao huharibika kwenye Michezo jambo ambalo halipendezi hata kidogo.

Aliwaahidi Vijana hao wa kike kwamba iwapo watashinda kwenye mashindano yanayowakabili atakuwa tayari kuwaandalia safari ya matembezi ili kubadilisha mawazo kwa vile kutembea ni kusoma.

Katika hafla hiyo Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi Seti mbili za Jezi zilizokamilika Mipira, Viatu pamoja na Fedha za Soksi kwa Timu hizo za Mpira wa Pete za Wadi ya Mahonda na Fujoni.

BIMA LA TAIFA (NIC) LAKABIDHI HUNDI WASHINDI WA BIMA YA MAISHA ILIYOBORESHWA

$
0
0
 Ofisa mwandamizi wa Bima Washirika la Bima la Taifa NIC, Catherine Nangali,kulia akimkabidhi Elisa Moses Mjema,kushoto mfano wa hundi ya Bima ya maisha iliyoboreshwa. wa pili kushoto ni Ivonne Elisa, Mtoto wake na wapili kulia ni Ofisa Bima wa NIC Vicent Rogath. Makabidhiano hayoyalifanyikaka katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere.

 Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko (Kulia) akimkabidhi Hamadi Rugambwa Ndibalema,mfano wa hundi ya Bima ya maisha iliyoboreshwa.makabidhiano hayoyalifanyikaka katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere 

 Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa Hundi zao za Bima ya maisha iliyoboreshwa katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere 

 Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko (Kulia) akimkabidhi Hamadi Rugambwa Ndibalema,mfano wa hundi ya Bima ya maishailiyoboreshwa.makabidhiano hayoyalifanyikaka katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere 

Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akiwa mbele ya banda la NIC wakati wa maonyesho ya  43 ya  Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere.Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja NIC Elisante Maleko


Balozi Seif awataka wawekezaji kuajiri wazawa

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akisalimiana na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kimataifa ya RIU Palace Zanzibar iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja Bwana Luis Sanchez Sarda alipofika kukagua maendeleo ya ongezeko la ujenzi wa vumba vya kulala wageni.
 Balozi Seif akiupongeza uongozi wa Hoteli ya RIU Palace Zanzibar kwa kujikita katika uwekezaji ndani ya Sekta ya Utalii na kuwatahadharisha kuepuka ujenzi wa majengo yao kutumia makuti. Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mh. Vuai Mwinyi Mohamed na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Kimataifa ya RIU Palace Zanzibar Bwana Luis Sanchez Sarda.
Muonekano wa haiba ya Baadhi ya Majengo mapya ya vyumba vya kulala wageni ya Hoteli ya RIU Palace Zanzibar yaliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewashauri Wawekezaji wa Mahoteli katika Sekta ya Utalii Nchini kuzingatia umuhimu wa kutoa fursa za ajira kwa Wazawa ili kudumisha mahusiano mema katika uendelezaji wa Miradi yao.

Alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na azma ya Serikali Kuu katika kufungua Milango ya Uwekezaji itakayoshajiisha fursa zaidi za ajira hasa kwa Vijana itakayosaidia kupunguza msongamano wa makundi yasiyo na Kazi Mitaani.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa ushauri huo wakati wa ziara yake ya kuangalia maendeleo ya ongezeko la Ujenzi wa vyumba vya kulala Wageni katika Hoteli ya RIU Palace Zanzibar iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unaguja.

Alisemaongezeko kubwa la Vijana wanaomaliza Masomo yao limekuwa kubwa mno na kulazimika Serikali kubuni mbinu za kupambana na changamoto hiyo iliyoenea hata katika Mataifa makubwa yaliyoendelea kiuchumi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameupongeza Uongozi mzima wa Hoteli ya Kimataifa ya RIU Palace Zanzibar kwa uamuzi wake wa kutanua Mradi wao jambo ambalo litaongeza mapato ya Taifa na kukuza fursa zaidi ya Ajira.

Balozi Seif ameutaka Uongozi huo kuepuka uwezekaji wa makuti kwenye majengo yao ili kujikinga na jaribio lolote linaloweza kusababishwa na majanga ya moto hasa wakati wa kiangazi.

Alisema ipo miradi mingi ya Mahoteli iliyowahi kutumia mfumo huo wa makuti kwa dhana ya kuridhisha Wateja wao lakini hatma yake imepunguza uzalishaji na mengine kufungwa kabisa baada ya kupata majanga ya moto.

Mapema meneja Mkuu wa Hoteli ya Kimataifa ya RUI Palace Zanzibar Bw. Luis Sanchez Sarda alisema Uongozi wa Hoteli hiyo umelazimika kuongeza idadi ya vyumba vya kulala wageni ili kukidhi mahitaji ya Wateja wao wanaoongezeka kila kukicha.

Alisema ongezeko la ujenzi huo utafikia vyumba 100 vya kulala wageni vinavyojengwa katika mfumo wa vyumba 50 kwa kila awamu vitakavyoiwezesha Hoteli hiyo kufikia idadi ya vyumba Mia 200.

Meneja Mkuu huyo wa RIU Palace Zanzibar alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba ujenzi wa vyumba hivyo uliofikia asilimia 85% sasa utakamilika rasmi ifikapo Mwezi Novemba Mwaka huu na kuongeza idadi ya Wafanyakazi Wazawa 40.

Kwa upande wake Mkurugenzi Uwezeshaji na Miradi ya Uwekezaji kutoka Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Shariff Ali Shariff alisema mabadiliko ya Sheria ya Uwekezaji yaliyofanywa na Serikali hivi karibuni inaelekeza Muwekezaji ye yote analazimika kuwekeza Mradi wake Nchini usiopungua thamani ya Dola za Kimarekani Milioni Mia Moja.

Shariff alisema uamuzi huo wa mabadiliko ya Sheria ya Uwekezaji umezingatia umuhimu wa kuimarisha Miradi ya Kudumu ya Uwekezaji itakayoendelea kutoa ajira kubwa, kuongeza mapato na kuimarisha Uchumi wa Nchi.

BENKI YA NMB YAAHIDI KUENDELEA KUCHANGIA JAMII KATIKA SEKTA YA ELIMU NA AFYA

$
0
0
SERIKALI Imeishukuru Benki ya NMB kuendelea kusaidia katika Sekta ya Elimu kwa kuchangia madawati baadhi ya Shule zilizo na upungufu na uhitaji mkubwa wa madawati ili wanafunzi waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea madawati 50 yenye thamani ya Sh, milioni 5 kutoka Benki ya NMB, mgeni rasmi Ofisa Habari na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, aliyemwakilisha Mkurugnezi, aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuchangia madawati kwa shule zilizo na upungufu.

Aidha alisema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Benki hiyo ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono juhudi za serikali inayotilia mkazo suala zima la masomo ili kila mtoto aweze kupata elimu.

''Pamoja na Serikali kutangaza kuwa elimu ni bure ili watoto wetu wote waweze kwenda shule, lakini bado inahitahi kushirikiana na wadau wa Elimu kama Benki hii ya NMB ii iweze kufikia lengo la kila mtoto kwenda shule,

Mwaka jana 2018 watoto wa darasa la kwanza walioandikishwa walikuwa ni 22, 000 lakini kwa mwaka huu wameongezeka na kufikia 38,000 hii inaonyesha kuwa hata wazazi wameamka ka kuelewa lengo la Serikali kutoa elimu bure, na idadi hii namini itazidi kuongezeka kila mwaka kutokana na mwamko wa wazazi''. Alisema Tabu

Naye Meneja wa NMB Tawi la Gongolamboto, Rehema Mwibura, alisema kuwa katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Sekta ya Elimu na Afya, NMB itaendelea kuwa karibu na Jamii kwa kutoa sehemu ya faida yao kusaidia Sekta hizo zenye uhitaji.

''Pamoja na kwamba tumeshatoa misaada ya aina hiio kwa shule mbalimbali nchini na vituo vya afya lakini bado tutaendelea kurudisha faida tunayoiapata kwa jamii kwa kuchangia katika masuala ya kijamii. NMB imekuwa ikichangia sekta za Elimu na Afya kwa kutoa vifaa mbalimbali kama vitanda vya Hospitali na vifaa tiba na Madawati pamoja na viti vyake kwa shule za Msingi na Sekondari. 
Ofisa Habari na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa Madawati 50 yenye thamani ya Sh. milioni 5 kutoka kwa Meneja wa Tawi la Gongolamboto, Rehema Mwibura (kushoto) na Meneja Mahusiano Biashara za Serikali wa NMB, Faraja Kaziulaya (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiano ya madawati hayo kwa ajili ya Shule ya Msingi Yangeyange iliyopo Msongola Manispaa ya Ilala, jana.

 


NEW LIGHT WATAKA USHIRIKIANO

$
0
0
WAZAZI, walezi na walimu wametakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kufanikisha wanafunzi waanze wakiwa wadogo kutumia akili zao ipasavyo kwa kutatua matatizo yao kwa sasa ili miaka ijayo wakiwa wakubwa waweze kuwa wabunifu na kufanya maendeleo.

Katibu wa bodi ya shule ya awali na msingi New Light ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Oscar Gunewe aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo.

Gunewe alisema watotot wanapaswa kupewa nafasi na kukuzwa kiakili kwa kutakiwa kufundishwa kujiamini na kutumia akili zao kutatua changamoto walizonazo ili wakiwa wakubwa wasishindwe kuyatatua.

"Nchi zilizoendelea wanasema sisi wa Afrika hatutumii akili zote tulizonazo katika kufikiri, hovyo yatupasa kuwajenga watoto katika msingi wa kutumia akili zao kwa asilimia zote wakiwa wadogo katika kifikiri, alisema.

Alisema maendeleo ya miaka ijayo ya nchi ya Tanzania inawategemea watoto, kutokana na hali hiyo hayo yatakwama bila kujengwa msingi imara katika malezi, makuzi na masomo bora hivi sasa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya awali na msingi New Light, Tumaini Mbise alisema wanajivunia shule hiyo kwani ina walimu wazuri wanaofundisha ipasavyo hivyo wazazi na walezi wasiwe na hofu pindi wakiwaleta watoto wao.

Mbise alitoa mfano wa mwanafunzi wa darasa la tatu wa shule hiyo ambaye alishindikana jijini Arusha akiwa darasa la pili kutokana na utukutu lakini wakaweza kumrudisha akawa na nidhamu.

"Siku ya kwanza alipofika hapa shuleni sisi walimu tulichoka kwani alikuwa mtundu mara apande juu ya mti, lakini tuliweza kukaa naye na kumpa ushauri bila kumchapa na sasa ni mtoto mwenye nidhamu na bidii ya masomo," alisema.

Mmoja kati ya wazazi mwenye watoto kwenye shule hiyo Happy Kayumbo aliwaomba wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu wa shule hiyo ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo katika kuwafundisha wanafunzi.

Kayumbo alisema baadhi ya wazazi na walezi huwa hawafiki shuleni kujua maendeleo ya watoto wao hivyo wanapaswa kufika na wasisubiri hadi waitwe kwenye vikao.
 Wanafunzi wa darasa la sita wa shule ya awali na msingi New Light Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkpani Manyara wakiwa kwenye kikao cha wazazi, walezi na walimu wao.
 Wanafunzi wa darasa la tatu wa shule ya awali na msingi New Light wakiwa kwenye kikao hicho cha wazazi, walezi na walimi wao.
Mmoja kati ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi New Light ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara akiwa na mwanafunzi aliyepata zawadi ya kuwa wa kwanza katika darasa lake.

NIC yakabidhi hundi kwa wateja wa bima za maisha zilizoiva

$
0
0
 Ofisa mwandamizi wa Bima Washirika la Bima la Taifa NIC, Catherine Nangali,kulia akimkabidhi Elisa Moses Mjema,kushoto mfano wa hundi ya Bima ya maisha iliyoboreshwa. wa pili kushoto ni Ivonne Elisa, Mtoto wake na wapili kulia ni Ofisa Bima wa NIC Vicent Rogath. Makabidhiano hayoyalifanyikaka katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere.
 Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko (Kulia) akimkabidhi Hamadi Rugambwa Ndibalema,mfano wa hundi ya Bima ya maisha iliyoboreshwa.makabidhiano hayoyalifanyikaka katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere 
 Baadhi ya wakazi wa jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa Hundi zao za Bima ya maisha iliyoboreshwa katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere 
 Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Elisante Maleko (Kulia) akimkabidhi Hamadi Rugambwa Ndibalema,mfano wa hundi ya Bima ya maishailiyoboreshwa.makabidhiano hayoyalifanyikaka katika banda la maonyesho ya  43 ya  sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere 
Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akiwa mbele ya banda la NIC wakati wa maonyesho ya  43 ya  Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mwalimu Nyerere.Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Huduma kwa Wateja NIC Elisante Maleko

VACANCY ANNOUNCEMENT

$
0
0
 
SOUTHERN AFRICAN DEVELOPMENT COMMUNITY


VACANCY ANNOUNCEMENT


Background


The Southern African Development Community (SADC) is a regional economic community founded and maintained by countries in Southern Africa. It aims to further the socio-economic, political and security cooperation among its Member States and foster regional integration in order to achieve peace, stability and wealth. SADC currently has fifteen Member States[1] with a population of approximately 327 million people and a combined GDP of USD 600 billion (2016). 


The Secretariat is currently recruiting for various positions to enhance its capacity to deliver on the above mandate. The Secretariat is therefore inviting suitably qualified and experienced citizens of SADC to apply for the following positions tenable at its Headquarters in Gaborone, Botswana or as stated in the job advert:


Position                                                                                                               Job Grade


  1. Senior Officer – Defense Affairs and Planning                                                     4

  2. Senior Officer Operations & Training (Based in Harare, Zimbabwe)                     4

  3. Senior Translator – Portuguese                                                                           5 

  4. Senior Programme Officer – Meteorology                                                            4

  5. Re-advert -  Head Civilian                                                                                  4

  6. Re-advert- Senior Programme Officer – Documentation and Information              4

  7. Re-advert - Senior Programme Officer – IN-SITU Conservation                             4

  8. Re-advert - Senior Programme Officer Transport                                                4

  9. Re-advert - Reviser French                                                                                5

  10. Programme Officer - Wildlife                                                                             6

  11. Programme Officer – Value Chains                                                                      6

  12. Programme Officer – Industrial Policy                                                                 6 

  13. Programme Officer – ICT                                                                                    6

  14. Communication Officer –Internal                                                                        6

  15. Programme Officer – Fiscal                                                                                 6

  16. Training and Roster Officer                                                                                6

  17. Officer – Meetings Management and Logistics x 2                                                6  

  18. Programme Officer - Climate Database and IT                                                    6

(Climate Services Centre)

  1. Programme Officer - Climate Diagnosis and Monitoring                                       6

(Climate Services Centre) 

  1. Programme Officer - Climate Modelling                                                              6

(Climate Services Centre)

  1. Programme Officer - Seasonal and Climate Forecaster                                        6

(Climate Services Centre)

  1. Information Systems Officer                                                                              6

  2. Translator x 2 (French)                                                                                      6

  3. Legal Counsel                                                                                                    6

  4. Officer Research and Statistics x 2                                                                     6

  5. Re-Advert -  Programme Officer - Gender Mainstreaming                                    6

  6. Re-advert - Programme Officer - Capital Markets                                                6

  7. Re-advert - Operation and Plan Officer                                                               6

  8. Re-advert - Planning and Budget Support Officer                                                 6 

  9. Re-advert -  Programme Officer – Regional Trade                                                6

  10. Officer Records                                                                                                  6

  11. ITInternalAuditor                                                                                                6

                                             

Remuneration


The SADC Secretariat offers a competitive package for all the positions as outlined below.


Job Grade                 Average Package per Annum:


Job Grade 4              US$ 81, 650

Job Grade 6              US$ 72, 527

Job Grade 5              US$ 77, 090


Tenure of appointment

All appointments for the above positions will be on a fixed term contract for a period of four (4) years, renewable once for an equal period subject to satisfactory performance, retirement age limit of 60 years and the continued need for the position.


Eligibility


The positions are open to qualified applicants who:


·      Are 50 years old or younger.  This requirement is based on the Organization’s need to recruit staff who can serve for a reasonable period of time before reaching the mandatory retirement age of 60 years.


·      Are from the following eligible Member States: Angola, DRC, Madagascar, Mauritius, Mozambique, Seychelles, Tanzania, Zambia and Zimbabwe


Closing Date and Submission of Applications: Applications must be submitted to the SADC National Contact Point https://www.sadc.int/opportunities/employment/national-contact-points/ of the  eligible Member States not later than or on 17th July, 2019.


Applications should be accompanied by the following:


a)       a cover letter stating the position that you want to be considered for and describe how your qualifications, experience and competencies are relevant to the position;

b)               five (5) page updated curriculum vitae;

c)                certified copies of your degree(s), Diploma(s) and Certificate(s); and

d)               duly completed SADC Application Form.


Should you be shortlisted, you will be required to produce evidence of educational and professional qualifications supporting your application, on the day of your interview.


Gender Mainstreaming


SADC is an equal opportunity employer and particularly encourages applications from female candidates.


If you are results orientated, you have a passion for the transformation and development of Southern Africa, and possess the required competencies, please submit your application.


Only applicants who meet the requirements of the SADC Secretariat and being considered for interview, will be contacted. Should you not hear from the SADC Secretariat within two months after the closing date, kindly consider your application as unsuccessful.


For further details on the position that you want to apply for, job profiles and SADC Application Form, refer to the SADC Website: www.sadc.int


Details can also be obtained from the National Contact Point in your respective country.



Issued by:

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

5th July 2019, Dodoma
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        




KIKWETE AFURAHISHWA NA TEKNOLOJIA ZINAZOBUNIWA NA VETA

$
0
0


Rais Mstaafu akielezewana  namna teknolojia ya meza ya kupasha na kupooza vinywaji na chakula (Heating Table) inavyofanya kazi baada ya kutembelea banda la Chuo cha Ufundi VETA katika Maonesho ya biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania akipokea maelekezo namna ya kumfundisha mtoto kwa vitendo kuhusu Sayari zinavyozunguka jua katika muhimili wake (Teaching Aid Kit for outer space bodies), baada ya kutembelea banda la VETA katika maonesho ya biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

NYONGO: SERIKALI IPO MACHO MASAA 24 KULINDA RASILIMALI ZA MADINI

$
0
0

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara wa sekta ya madini, cheti maalum cha ushiriki wa kongamano baina ya wafanyabiashara baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara wa sekta ya madini, cheti maalum cha ushiriki wa kongamano baina ya wafanyabiashara baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara wa sekta ya madini, cheti maalum cha ushiriki wa kongamano baina ya wafanyabiashara baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akimkabidhi mmoja wa wafanyabiashara wa sekta ya madini, cheti maalum cha ushiriki wa kongamano baina ya wafanyabiashara baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini, John Bina akizungumza katika Kongamano baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akizungumza katika Kongamano baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akizungumza katika Kongamano baina ya Wafanyabiashara wa sekta ya madini na Tume ya Madini kwa kushiriakana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) lililofanyika leo Jumatatu (Julai 8, 2019) wakati wa Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
………………….. 
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO 
DAR ES SALAAM 

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema Serikali ipo macho masaa 24 katika siku 7 za wiki na itaendelea kuwabaini kuwakamata na kuwatia hatiani watoroshaji wa madini sambamba na kulinda rasilimali hizo, kwa kuwa watoroshaji hao wamekuwa wakiwahujumu Watanzania na kurudisha nyuma maendeleo yao. 

Akizungumza katika Kongamano baina ya Wadau wa Madini lililoandaliwa na Tume ya Madini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Baiashara Tanzania (TANTRADE) leo (Jumatatu Julai 8, 2019) katika Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Waziri Nyongo alisema kitendo cha utoroshaji wa madini ni kosa kisheria na hivyo Wafanyabiashara wote wanatakiwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali. 

Kwa mujibu wa Waziri Nyongo katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali kupitia Tume ya Madini imevunja rekodi katika ukusanyaji wa mapato ya madini hatua iliyotokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambapo kiasi cha Tsh Bilioni 310 ziliweza kukusanywa hatua iliyotokana na kudhibiti mianya ya utoroshaji wa rasilimali za madini. 

“Tangu uhuru nchi yetu haikuwahi kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni mapato yatokanayo na madini ya kiasi cha Tsh Bilioni 310, hivyo Serikali itaendelea kuweka mkazo kuzuia njia za panya ambazo zimekuwa zikitumiwa na watoroshaji wa madini kutorosha madini yetu na hivyo kuikosesha Serikali mapato” alisema Nyongo. 

Aidha Waziri Nyongo alisema katika mwaka wa fedha 2019/2020 Serikali kupitia Tume ya Madini imepanga kukusanya kiasi cha Tsh Bilioni 470 na hivyo aliwataka watendaji wa Tume hiyo kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu ikiwemo kuendelea kuwafichua na kuwakamata Wafanyabiashara wasiotaka kufuata sheria. 

Naibu Waziri Nyongo alisema Serikali kupitia Tume ya Madini kamwe haitomwonea mfanyabiashara yoyote anayafanya biashara zake kwa kufuata sheria ikiwemo kuuza madini yake katika masoko yaliyofunguliwa na Serikali kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha Serikali kukusanya kodi yake pamoja na kuweza kuongeza mapato ya serikali. 

Aliongeza kuwa hadi sasa kuna jumla ya masoko ya madini 29 yaliyofunguliwa katika maeneo mbalimbali nchini na kusema Serikali imeweza mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara kuuza madini katika maeneo hayo katika masoko hayo kwa kuwa ni salama kwao na pia yataiwezesha Serikali kutambua kiasi cha madini kinachozalishwa na kuuzwa nchini. 

Akifafanua zaidi Naibu Waziri Nyongo aliitaka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuendelea kujenga mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta ya madini ikiwemo kuwatafutia masoko na kuwatakutanisha mara kwa mara ili kuweza kutambuana pamoja na kuweza kupeana ujuzi na maarifa mbalimbali. 

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Zanzibar, Latifa Hamisi alisema Ofisi yake itaendelea kuimarisha ushiriakiano na wadau wote wa sekta ya biashara nchini ikiwemo wadau wa madini kwa kuwajengea uwezo sambamba na kuwafutia masoko ya uhakika wa bidhaa zao ndani na nje ya nchi. 

Aliongeza kuwa TANTRADE itaendelea kutumia majukwaa yake ya kibiashara ikiwemo mikutano ya mara kwa mara baina yake na Wafanyabiashara pamoja na kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara hao ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zinazokithi masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Naye Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Madini Nchini (FEMATA) John Bina aliiomba TANTRADE kuweka utaratibu wa kuwatembelea wachimbaji wadogo wa madini katika maeneo mbalimbali nchini ili kuweza kuzitambua changamoto zao kwa kuwa kupitia utaratibu huo utawawezesha kutambua mchango wao katika uzalishaji wa madini na nafasi waliyonayo katika kukuza uchumi wa nchi.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MTAWALA WA SHARJAH

$
0
0
Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu (UAE) Mhe.Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, kulia akiwasilisha Salamu za rambirambi kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein kwa Mtawala wa Sharjah Sheikh Khalid bin Sultan Mohammed Al Qasimi, kushoto hafla hiyo imefanyika katika makazi yake Sharjah. (Picha na Ikulu)

WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI MISRI KWENYE ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, wakati akiwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu nchini humo, Julai 8.2019 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri Mkuu ya Kiarabu Misri, Dkt. Moustafa Madbuoly, baada ya kuwasili mjini Cairo Misri kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, Julai 8.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais Dkt Magufuli aomboleza vifo vya wafanyakazi wa Azam Media

Takwimu wataja sababu za mfumuko wa bei

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei wa Taifa Kwa mwaka ulioishia mwezi jana umeongezeka hadi asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi, Daniel Masolwa ongezeko hilo linamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Juni imeongezeka ikilinganishwa na Kazi ya mwezi Mei.

" Ongezeko la mfumuko wa bei Kwa mwaka ulioisha mwezi Juni kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwakamwaka ulioisha mwezi Juni, 2019 ikilinganishwa na Juni 2018.

" Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo ni unga wa mahindi asilimia 3.6, ngano asilimia 4.4, mtama asilimia 4.9, samaki wabichi asilimia 27.3," amesema Masolwa.

Amesema bidhaa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dizeli kwa asilimia 11.4, payroli asilimia 4.9, nyumba za kulala wageni asilimia 5.8 na vitabu vya shule vikiwa ni asilimia 2.4.

Pia amefafanua hali ya mfumuko wa bei Kwa Nchi za Afrika Mashariki ambapo Uganda mfumuko wa bei ulioishia Juni mwaka huu ulikua asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.3 huku Kenya ongezeko likifikia asilimia 5.70 kutoka asilimia 5.49.

TANZANIA YAFANIKIWA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VIKOPE

$
0
0
Na.WAMJW,Arusha.

Tanzania imeweza kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Trakoma kutoka wilaya 71 hadi sita ambazo zitaendelea na umezaji kingatiba

Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Dkt.Upendo Mwingira wakati wa mafunzo ya Kimataifa ya uchukuaji wa takwimu za ugonjwa wa vikope(Trakoma) yanayofanyika jijini hapa.

Dkt.Mwingira amesema kuwa kama nchi inajivunia kwa mafanikio makubwa kwani hivi sasa wilaya 65 hazihitaji tena kingatiba kulingana na vigezo vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

"Lengo la WHO hadi ifikapo mwaka 2020 tuwe tumeweza kutokomeza ugonjwa wa Trakoma kama tatizo la kijamii,kwamba hatutaki maambukizi mapya"Alisisitiza Dkt.Mwingira.

Aidha,alisema mwaka 2010 katika tathimini Tanzania kulikua na makadirio ya wagonjwa wa vikope  takribani 160,000,lakini kutokana na jitihada za Wizara ya Afya  hadi Julai 2018 inakadiriwa wagonjwa hao wamepungua mpaka kufikia 17,000.

Hata hivyo Dkt.Mwingira alisema zoezi la kusawazisha vikope hapa nchini linaendelea zaidi ya mikoa kumi sasa hivi katika halmashauri zenye maambukizi.

Mafunzo haya yanahusisha wataalam wa macho kutoka mataifa mbalimbali Duniani na kwa nchi za Afrika yanahudhuriwa na nchi za afrika Mashariki,Magharibi na Kati.
 Mratibu wa Taifa wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Dkt. Upendo Mwingira akifungua mafunzo ya Kimataifa ya uchukuaji wa Takwimu za  ugonjwa wa Vikope(Trakoma) yanayofanyika jijini Arusha.
 Mratibu wa NTD Mkoa wa Arusha Mwanahawa Kombo akitoa salamu za mkoa kwa niaba Mganga Mkuu wa Arusha.Mafunzo haya hapa nchini yanafanyika kwa miaka mitatu mfululizo 
 Wataalam wa Macho kutoka mataifa mbalimbali wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo
 Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya afya,wadau mbalimbali wa macho nchini pamoja na nchi mbalimbali Duniani zikiwemo Afrika Mashariki,Magharibi na Kati


 Afisa Mpango kutoka NTD anayeshughulika na Trakoma Bi.Alistidia Simon akiwakaribisha wataalam wa macho kwenye mafunzo hayo. 

BREAKING NYUUUZZZ.......: TFF YASITISHA MKATABA NA KOCHA EMMANUAEL AMUNIKE, MCHAKATI WA KUTAFUTA KOCHA MPYA WAANZA

$
0
0
 Aliyekuwa Kocha wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", Emmanuel Amunike ambaye mkataba wake usitishwa leo.

Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>