Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAIKABIDHI MWAUWASA UJENZI WA MRADI WA MAJI KWIMBA

0
0

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amekabidhi ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima Wilayani Kwimba kwa Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA) baada ya Mkandarasi Kampuni ya Palemon Construction Ltd ya Mwanza kushindwa kukamilisha kwa wakati.

Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Shilima na kushuhudiwa na watendaji mbalimbali wa Serikali na mamia ya wananchi wa Shilima na maeneo ya vijiji vya jirani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mradi, Waziri Mbarawa alieleza kwamba ujenzi wake ulianza tangu mwaka 2013 na kwamba ulipaswa kukamilika ndani ya miezi sita lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika.

Alisema Serikali iliamua kusitisha mkataba na Mkandarasi ambaye alishindwa kutekeleza ujenzi wa mradi kama ilivyo kwenye makubaliano.

Mara baada ya kuukabidhi mradi huo, Profesa Mbarawa aliiagiza MWAUWASA kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya Siku 60 ili kuwaondolea mateso ya muda mrefu wanachi wa maeneo hayo hasa ikizingatiwa kwamba mradi ulipaswa kukamilika tangu mwaka 2013.

“Tunataka wataalam hawa wafanye kazi usiku na mchana na baada ya miezi miwili wananchi wapate maji safi na salama, uwezo tunao, tunaweza kumaliza tatizo la maji hapa kwa muda mfupi sana,” alisema Profesa Mbarawa.

Aliongeza kuwa kuna miradi ipatayo 88 kote nchini ambayo ujenzi wake ulianza kati ya Mwaka 2010 hadi 2015 ambayo ilipaswa kuwa imekwisha kamilika lakini hadi hivi sasa bado inasuasua na huku akiutolea mfano mradi huo wa Shilima.

Alibainisha kwamba Serikali kupitia Wizara ya Maji imeamua kuwa na utaratibu mpya wa kuzikabidhi Mamlaka za Maji miradi ambayo ujenzi wake una changamoto inayosababisha isikamilike kwa wakati.

“Tumeamua kubadilisha utendaji wa Sekta ya Maji, kila mahala tatizo ni maji, hili halikubaliki, tumejipanga na tunadhamira ya dhati kuhakikisha kero hii inakuwa historia kote nchini,” alisema Waziri Mbarawa.

Kuhusu utaratibu huo mpya, Profesa Mbarawa alibainisha kuwa ni wa nchi nzima na kwamba wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi waliyokabidhiwa kwa wakati hawatovumiliwa na watanyanganywa na itakabidhiwa kwa Mamlaka za maji kwenye maeneo husika.

“Tumeamua miradi yote yenye changamoto tutaisimamia wenyewe na tutahakikisha inafanya kazi. Wananchi wamechoka kuendelea kuisubiri miradi hii ikamilke, fedha nyingi zinapotea, Serikali haitokubaliana na Mkandarasi anaechelewesha ujenzi wa mradi tayari tumefanya hivi Rungwe na sasa tumefanya hapa Shilima,” alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga alisema wamepokea agizo hilo la kutekeleza mradi huo ambao umesuasua kwa kipindi kirefu na kwamba wataukamilisha kwa wakati kama ilivyoagizwa.

“Tunaahidi hadi kufikia Septemba 3, 2019 tutakuwa tumeukamilisha mradi kwani itakuwa tayari ni Siku 60 na wananchi wataanza kupata majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria,” alisema Mhandisi Sanga.

Aidha, kwa mujibu wa Mhandisi wa Maji, Wakala wa Maji Vijijini Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Boaz Pius ni kwamba mradi huo utakapokamilika utahudumia wakazi 16,675 kutoka vijiji vinne ambavyo ni Shilima chenye wakazi 7,526, Mhande chenye wakazi 1,967, Kasang’wa wakazi 2,730 na Kijiji cha Izizimba “A” chenye wakazi wapatao 4,452.

Mhandisi Boas aliongeza kwamba kukamilika kwa mradi huo pia kutaweza kuhudumia vijiji vya Sangu, Gurumwa, Mwalubungwe na Kikubiji, ambapo bomba kuu linapita.
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa makabidhiano ya ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima, Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi MWAUWASA, Christopher Gachuma akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi wa Maji wa Shilima. Kushoto kwake ni Mbunge wa Kwimba, Shanif Mansoor, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Senyi Ngaga
 Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akichimba mtaro kwa ajili ya ulazaji wa bomba za maji kuashiria kuanza rasmi kwa utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima, Wilayani Kwimba ambao ulisimama kutokana na Mkandarasi kushindwa kuutekeleza kwa wakati na hivyo ujenzi wake kukabidhiwa kwa MWAUWASA.
 Uchimbaji wa mtaro ukiendelea kwa ajili ya kulaza bomba za maji mradi wa Shilima mara baada ya ujenzi wa mradi huo kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Maji Mwanza (MWAUWASA).
 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza mara baada ya kukabidhiwa ujenzi wa mradi wa maji wa Shilima.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Shilima na vijiji vya jirani waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya ujenzi wa mradi wa maji wakimsikiliza Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani).

MAKAMU WA RAIS AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA 12 WA DHARURA WA AU

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Julai 07,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaojadili masuala mbalimbali kuhusu Eneo Huru la Biashara Afrika (AFRICAN CONTINENRAL FREE TRADE AREA - AFCFTA) Mkutano huo unaofanyika mjini Niamey Nchini Niger umefunguliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika AU Rais Abdel Fattah el Sisi wa Egypt. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).










WAZIRI LUGOLA APIGA MARUFUKU MAKAMANDA WA POLISI KUYAKAMATA MABASI USIKU, ASEMA NCHI INA AMANI, ATAKA YASAFIRI SAA 24 BILA KUBUGUDHIWA

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Namibu, Kata ya Neruma, Jimbo la Mwibara,Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola amepiga marufuku Makamandawa Polisi wa Mikoa nchini kuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa ya Kanda yaZiwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia kuvamiwa na majambazi. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (wapili kushoto),akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Namibu, Kata ya Neruma, Jimbo laMwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo, wakati alipofanya ziara kijijinihapo. Lugola amepiga marufuku Makamanda wa Polisi wa Mikoa nchinikuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es aSalaam au kurudi Kanda ya Ziwa muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia
kuvamiwa na majambazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi. 

********************* 

Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA) 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku
Makamanda wa Polisi wa Mikoa nchini kuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa
ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa
kusafiri muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia kuvamiwa na majambazi. 

Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na kamwe haliwezi kucheka na
majambazi wala kuwaonea huruma majambazi na kuanza kutupangia
majambazi muda gani mabasi yasafiri na yasisafiri, mabasi hayo
yanapaswa kusafiri saa 24. 

Akizungumza na katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Namibu Kata ya
Neruma, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Lugola amesema mabasi
yanayosafiri kutoka Kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam yasizuiwe
Morogoro na yanayotoka Dar es Salaam kwenda kanda ya ziwa yasizuiwe
Shinyanga kwasababu zinazodaiwa za kiusalama. 

“Mimi ndiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hatuwezi kupangiwa
ratiba ya kusafiri na majambazi, Serikali ya Rais Magufuli ipo imara, na
Polisi ipo imara, hivyo agizo hili ambalo pia niliwahi kulitoa lizingatiwe
ipasavyo, niliagiza majambazi wote wasambaratishwe, asakwe mpaka
jambazi wa mwisho, akamatwe kama kuku”.Alisema Lugola na kuongeza. 

“Taarifa ya uhalifu zinaonyesha Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa ya
kupambana na uhalifu na hasa uhalifu wa majambazi, na niliwahi kuagiza
kipindi hiki si cha kuwa na huruma na majambazi ni kipindi cha
kuwashughulikia ili wananchi waishi kwa amani”. 

Lugola alifafanua kuwa, nchi haiwezi kupangiwa na majambazi muda wa
kusafiri, kufanya biashara, hivyo maelekezo aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi
liendelee kupambana na majambazi popote walipo nchini. 

“Nimeelekeza magari yanayosafiri yasizuiwe Morogoro yanpopita muda wa
usiku saa nne usiku na kuendelea, yasizuiwe Shinyanga, ili majambzi wajue
popote walipo wapo imara wamejipanga vizuri na mimi Waziri wao nipo
imara kuhakikisha Jeshi la Polisi linawashughulikia makambazi mmoja
baada ya mwingine ili kuwafanya wananchi katika nchi yao waendelee
kushughulika na masuala ya kujijengea uchumi ili Serikali ya Rais Magufuli,
iweze kuwa na uchumi wa kati na majambazi wote wakamatwe kama
kuku,” alisema Lugola.

SHIDA YA MAJISAFI KWA WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NA PWANI KUISHA IFIKAPO 2020

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wanahabari ndani ya Maonesho ya 43 ya Kitaifa ya Biashara Sabasaba 2019 mara baada ya kutembelea banda lao kungalia jinsi wanavyotoa huduma kwa wananchi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kwanza kushoto) akisikiliza watoa huduma mara baada ya kuwasili bandano hapo kujionea jinsi wanavyotoa huduma.
 Dawati la huduma kwa wateja wakiendelea kutoa huduma kwa wateja waliofika kwenye Banda la Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) kwenye Banda lao la Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akifafanuliwa jambo na dawati la kutoa huduma kwa wananchi.
Mwanahabari Zaynab akipata maelezo ya vifaa vinavyotumika katika kuungalishia wateja maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kushoto) akipata maeleozo kutoka kwa Meneja Uhusiano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kushoto) mara baada ya kutoka katika banda lao lililopo katika Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba 2019. 

 Zainab Nyamka na Cathbert Kajuna, Globu ya Jamii 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ameweka wazi kuwa tatizo la maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani linaenda kuisha.

 Luhemeja ameyasema hayo alipotembelea banda la DAWASA lilipo ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na wanahabari baada ya kupata maelezo kutoka kwa watoa huduma kwa wateja na wahandisi, Luhemeja amesema shida ya maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani inaelekea kuisha kutokana na miradi mbalimbali inayoendelea kujengwa na ile mipya.

 Luhemeja amesema, wameshasaini miradi mikubwa sita ya maji yenye thamani ya bilion 114.5 ambapo itasambaza maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. "Wananchi walikua na shida ya maji na miradi hii mikubwa inaenda kuondoa changamoto ya maji  na malengo kufikia asilimia 95 mwaka 2020," amesema Luhemeja. Amesema, kwa sasa maji yanapatikana kwa asilimia 85 tofauti na miaka ya nyuma ambapo maji yalikua asilimia 68 na mapato yamepanda kutoka bilion 3.2 kwa mwezi hadi bilioni 11.2. 

 Akielezea sheria mpya namba 5 ya mwaka 2019 inayoibadilisha mamlaka ya majisafi na majitaka na kuwa mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira, Luhemeja amesema wameipokea vizuri na itasaidia katika kulinda vyanzo vya maji  na kudhibiti usafi wa mazingira. 

 Aidha, Luhemeja amesema DAWASA bado wanaendelea na kusajili wamiliki wa Visima na kuhakiki ubora wa maji na kuwajua kutokana na sheria mpya kuwaondolea kodi ya kila mwaka. Ametoa rai kwa wananchi kufika kwenye banda lao lilipo ndani ya maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam ili kufahamu miradi ya maji inayoendelea kujengwa na mipya itakayoondoa changamoto ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Watanzania wamekuwa na mwamko mkubwa katika Michezo-Dkt.Mwakyembe.

0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akizungumza na wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon (hawapo
pichani) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.Kulia ni mratibu wa mbio hizo Bw.Nsolo Mlozi na Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Mhe.Antony Mavunde.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
(aliyeshika filimbi nyekundu) akionyesha ishara ya kuanza kwa mbio za Capital City Marathon kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma. 
Baadhi ya wanariadha walioshiriki mbio za Capital City Marathon wakijiandaa
kuanza mbio zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi zawadi Bw.Rashid Ally baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio za Baiskeli Km.22 za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi zawadi Bw.Godlisten Mmmary baada ya kuibuka mshindi wa kwanza
katika mbio za walemavu za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019
Jijini Dodoma. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe
akimkabidhi zawadi Bi.Fabiola John baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mbio
za Km. 10 kwa wanawake za Capital City Marathon zilizofanyika leo Julai 07,2019
Jijini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye
ulemavu Mhe.Antony Mavunde. 
Mratibu wa Mbio za Capital City Marathon Bw.Nsolo Mlozi akitoa neon la
shukrani kwa washiriki wa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini
Dodoma.Kulia ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison
Mwakyembe. 

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.Harrison
Mwakyembe(Katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa mbio za Capital City Marathon kwa upande wa walemavu pamoja na viongozi wa Mkoa,Chama na Serikali baada ya kumalizika kwa mbio hizo zilizofanyika leo Julai 07,2019 Jijini Dodoma. 

************* 

Na Shamimu Nyaki –WHUSM 

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametoa pongezi kwa watanzania kwa kuwa na mwamko mkubwa wa kupenda michezo kuanzia kushiriki,kushangilia pamoja na uhamasishaji ambao umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio na maendeleo ya michezo hapa nchini na uwakilishi mzuri nje ya nchi. 

Dkt.Mwakyembe ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa anamuwakilisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluh Hassan katika mashindano ya riadha ya Capital City Marathon ambapo amesema kuwa kwa sasa nchi yetu imeanza kurudi katika ramani ya michezo kutokana na watanzania kushriki kwa wingi katika michezo mbalimbali. 

“Nawapongeza sana Watanzania wamekuwa na ari kubwa sana ya kushirikiki michezo hasa riadha ambayo imetutangaza vyema nje ya nchi,ni matuamini yangu mtaendelea kufanya vizuri zaidi lakini pia na michezo mingine vijana endeleeni kuchezakwa bidii zaidi kwakua michezo sasa ni chanzo kikubwa cha kipato”amesema Dkt.Mwakyembe. 

Aidha Dkt.Mwakyembe ameongeza kuwa Taifa limekuwa na uwakilishi mzuri katika mchezo wa Soka kwani limepata nafasi ya kushiriki AFCON 2019,kuongezeka kwa timu zitakazoshiriki Klabu Bingwa Afrika ambayo ni Simba na Yanga pamoja na Klabu Mbili zitakazoshiriki Kombe la Shirikisho ambazo ni Azam FC na KMC. 

Katika hatua nyingine Mhe.Waziri Mwakyembe ameiagiza Idara ya Maendeleo ya
Michezo kushirikiana na wadau kuwa na utaratibu wa kuandaa orodha ya wadhamini wanaojitokeza na namna wanavyodhamini mashindano mbalimbali ili kuweka kumbukumbuku vizuri na kutoa ushauri panapowezekana katika kuimarisha Sekta hiyo. 

Kwa upande wake Mratibu wa Mbio hizo Bw.Nsolo Mlozi mbali na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyotoa pamoja na washiriki waliojitokeza ameishauri jamii kuwa na
utaratibu wa kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ili
kujenga miili yao kwa kuimarisha afya lakini pia kujikinga na magonjwa
yasiyoambukiza ambayo kwa sasa yamekuwa yakiwatesa wananchi wengi. 

Vilevile Bw.Nsolo ameongeza kuwa Capital City Marathon ilianza na kuwa na idadi
ndogo ya washiriki lakini mwaka huu idadi imeongezeka na kufikia washiriki 2,200
ambao kulingana na miundombinu imara ya Jiji la Dodoma wameweza kukimbia bila kupata changamoto yoyote. 

Naye mshindi wa km 21 kwa upande wa wanaume Bw.Emmanuel Giniki amesema
kuwa mchezo wa riadha ni mchezo ambao unahitaji kuwa na mazoezi ya mara kwa mara ili kuweza kufanya vizuri ambapo amewashauri vijana wengi kujitokeza katika mashindano mbalimbali ya riadha yanayotokea ili kupata kipato pamoja na kupata ajira. 

Mbio za Capital City Marathon zinafanyika kwa mara ya pili Jijini Dodoma ambapo
mwaka huu zimehusisha mbio za KM 22 Baiskeli,km.21wanawake na wanaume,km 10 wanawake na wanaume pamoja na km 5.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AWATAKA WANANCHI KUTUNZA VYANZO VYA MAJI,ARIDHISHWA NA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA VYANZO VYA MAJI MUHEZA

0
0

MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Mkinga Mark Yona
 KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally akivishwa skafu na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili wilayani Muheza.
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akiwa na viongozi mbalimbali mara baada ya mwenge kuwasili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza Like Gugu na Mbunge wa Jimbo la Muheza( CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni  KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akihamasisha kushiriki kuimba kwa pamoja nyingi mbalimbali za mwenge wakati wakiiusubiri
 MMOJA kati ya wakimbiza Mwenge Kitaifa akiweka mwenge mara baada ya kukimbizwa kwenye miradi mbalimbali
 Mwenge wa Uhuru 2019 ukikimbizwa wilayani Muheza
 MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri Bakari Mhando
 KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally katikati akionyeshwa namna ya utunzaji wa mazingira unavyoifanyika wakati alipotembelea na kukagua mradi wa shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji Kijiji cha Shembekeza.
 KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally kushoto akimkabidhi cheki ya Sh.Milioni moja Mwenyekiti wa Kijiji cha Mbaramo Mussa Salimu ikiwa ni mchango uliotoka Halmashauri kuunga mkono ujenzi wa Hosteli kwenye shule ya Msingi Mbaramo kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
 MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwakabidhi zawadi mbalimbali wakimbiza Mwenge wa Uhuru 2019

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 Mzee Ally amewataka wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wilayani Muheza mkoani Tanga kuhakikisha wanavitunza ili viweze kuwa endelevu.

Alitoa kauli hiyo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua mradi wa shughuli za uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo kukagua mabanda ya wadau wa mazingira na kupanda miti eneo maalumu lillotengwa Kijiji cha Shembekeza.

Akiwa kwenye eneo hilo kiongozi huyo alionyeshwa kuridhishwa na namna mradi wa uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa vyanzo vya maji.

Alisema kwani Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutekeleza miradi hiyo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni muhimu kulindwa na kuendelezwa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kiongozi huyo alisema suala la upatikanaji wa maji limekubwa na changamoto nyingi ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za serikali huku baadhi ya waka ndarasi wamekuwa wakichukua muda mrefu kukamilika miradi hiyo na hata wengine kukamilisha chini ya kiwango.

“Lakini pia niwaambie kwamba sio jambo jema kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ikiwemo ukulima, ufugaji na kujenga karibu na vyanzo hivyo tushirikiane kuhakikiha tunatunza vyanzo vya maji ili vielendee kumudu kwqa vizazi vya sasa na vijazo”Alisema Kiongozi huyo.

Awali amkizungumza wakati akisoma taarifa ya miradi itakayozinduliwa na mwenge ikiwemo kukaguliwa Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kwamba miradi yenye thamani ya Bilioni 29.471.7 huku akieleza kwamba mwenge huo umekimbizwa kwenye miradi na shughuli mbalimbali.

Alisema wakati wa mkesha wa mwenge huo huduma mbalimbali zilitolewa ikiwemo upimaji vvu ambapo walipimwa watu 448 ambapo kati yao wanaume 307 na wanawake 141 na waliokutwa na maambukizi ni wanaume wawili na wanawake wawili

Wakati huo huo Mpiga picha wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Muka Sabuni amepongeza na viongozi wa mbio hizo kutokana na namna aliyoweza kutengeneza mabango yenye picha zao wakati ulipoongia wilayani Muheza.

Hatua ya mmoja ya wakimbiza Mwenge ni kushangazwa na ubinfu uliotumiwa na mpiga picha huyo kwa kuweka picha zao kwenye mabango yaliyokuwa yamebeba ujumbe wa mwenge wilayani humo.

Kutokana na hali hiyo mmoja wa wakimbiza Mwenge hao Kenon alitumia muda wa makabidhiano baina ya Muheza na Pangani ndipo aliposimama na kumtambulisha huku akionyeshwa kufurahishwa na utendaji wake na kuiwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kumtumia kwenye shughuli mbalimbali.

RAIS BINA ALAANI UTOROSHWAJI MADINI

0
0

Rais wa shirikisho la wachimba madini nchini (Femata) John Bina akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni.

Rais wa shirikisho la wachimba madini nchini (Femata) John Bina akizungumza na wadau wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, hivi karibuni. 

*************** 

RAIS wa shirikisho la wachimbaji madini nchini (Femata) John Bina amelaani vikali tukio la utoroshwaji wa madini ya Tanzanite, Ruby na Green Tourmarine, lililotokea Wilayani Longido Mkoani Arusha na polisi kufanikisha ukamataji wa madini hayo. 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari ya ofisa habari wa Femata, Dk Bernard Joseph iliyotolewa jana, Bina aliiomba serikali kuwachukulia hatua kali wahusika hao kwani kitendo hicho cha 
utoroshwaji wa madini hakikubaliki kabisa. 

Bina alisema vitendo vya utoroshwaji madini ni kinyume cha maadili na utapeli unaofanywa na wageni unachafua taswira ya uchimbaji wa madini nchini. “Tunawapongeza askari polisi kwa kukamata madini hayo na kukataa rushwa na pia mzalendo halisi aliyetoa taarifa pamoja na Waziri wa Madini Dotto Biteko kwa kuagiza wapewe zawadi ya sh5 milioni kila mmoja kwa maslahi ya Taifa,” alisema Bina. 

Mwenyekiti wa kamati ya madini ya Tanzanite nchini, Money Yousuph alisema tukio hilo limewasikitisha mno kwani bado kuna baadhi ya watu wana hila chafu ya kutorosha madini. 

Money alisema wahusika wa tukio hilo wanapaswa kupata adhabu kali kwani hawakubaliani na wizi wa madini uliofanyika kwa kutaka kusafirisha kwa wizi madini hayo. “Hivi karibuni Rais John Magufuli aliondoa kodi zilizokuwa zinalalamikiwa lakini bado watu wengine wanafanya vitendo vya utoroshwaji wa madini,” alisema. 

Mwanamke mchimbaji wa madini ya Tanzanite, ambaye hakupenda kutaja jina lake alisikitishwa na utoroshaji madini huo kwani wamekuwa wakipekuliwa hadi sehemu za siri lakini madini hayo yameibiwa. 

“Wanawake tumekuwa tukidhalilishwa kwa kupekuliwa hadi sehemu za siri lakini mbona madini hayo yameibiwa na kutaka kutoroshwa hadi nje ya nchi jirani ya Kenya,” alisema. 

Hivi karibuni madini aina ya Tanzanite, Green Tourmarine, Saphure, Aquamarine, Crossulite, Tsavorte, Ruby na Spiwel yenye thamani ya sh958 milioni yaliyokuwa yanasafirishwa kwenda nje ya nchi yalikamatwa na polisi wilayani Longido mkoani Arusha.

TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO MICHAEL STEVEN


UJENZI WA OFISI ZA UTHIBITI UBORA WA SHULE WAANZA KWA KASI WILAYANI MISUNGWI

0
0

Naibu Waziri wa Elimu, Saysnia na Teknolojia William Ole Nasha akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Uthibiti ubora wa shule Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo ya namna mradi wa ujenzi wa ofisi ya uthibiti ubora wa shule wilaya ya Misungwi unavyotekelezwa kutoka kwa Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Shule wa Wilaya ya Misungwi Faustin Salala. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na baadhi ya Walimu pamoja na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za Uthibiti ubora Wilaya ya Misungwi. Amewataka kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu kwani inalenga kuboresha elimu ya watoto wetu. 
Muonekano wa sasa wa hatua ya ujenzi wa ofisi ya Uthibiti ubora wa shule wa wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza. 
………………… 


Naibu Waziri Ole Nasha afanya ziara kukagua asisitiza viwango katika utekelezaji wa mradi huo. 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kwa usimamizi mzuri wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya uthibiti ubora wa shule wa wilaya hiyo inayojengwa katika kata ya Igokelo kijiji cha Mapilinga mkoani humo. 

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa pongezi hizo alipofanya ziara katika Wilaya hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo ambapo amesema ameridhishwa na hatua ambayo ujenzi umefikia huku mkazo ukiwa kuzingatia ubora wa ujenzi wa jengo hilo. 

“Kwa kweli mnakwenda vizuri, kama fedha mmepokea mwezi Mei mwaka huu tokea ujenzi uanze michakato yote ni kama mmetumia mwezi mmoja na tayari mmeshapaua ni jambo jema. Lakini niwapongeze zaidi kwa kuwa ujenzi huu miundombinu yake imezingatia watu wenye mahitaji maalum zingatieni ubora wa jengo katika kukamilisha kazi hii,” alisema Naibu Waziri Ole Nasha 

Alisema ujenzi wa Ofisi za Uthibiti ubora wa shule ni mwendelezo wa nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuamua kuimarisha Idara ya Uthibiti Ubora wa shule ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa lengo la kuinua ubora wa elimu nchini. 

Ole Nasha ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuboresha Sekta ya Elimu kwa kuwa zina lengo la kuimarisha elimu ya watoto wetu lakini pia kutumia fursa zinazokuja na miradi hiyo kujiingizia kipato kwani kwa sasa Serikali imeamua kutumia utaratibu wa Force Akaunti katika utekelezaji wa miradi yake kwani utaratibu huo umeonesha kuwa na mafanikio lakini pia unawanufaisha wananchi walio karibu na mradi unapotekelezwa. 

“Wanamisungwi 34 wamefaidika na ujio wa mradi wa ujenzi wa ofisi hii ya Uthibiti ubora wa shule wapo waliopata nafasi ya kufanya kazi za ujenzi na wale waliofanya bishara ya chakula na vinywaji na hili ndilo lengo la Serikali,’aliongeza Naibu Waziri ole Nasha 

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa Ofisi hiyo Mthibiti Mkuu wa ubora wa Shule Wilaya ya Misungwi Faustini Salala alisema ujenzi wa ofisi hizo umeanza mwishoni mwa mwezi Mei 2019 na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti, 2019 na utatumia zaidi ya shilingi milioni 150. 

Mradi wa Ujenzi wa ofisi ya Uthibiti Ubora wa shule katika wilaya ya Misungwi ni moja ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa ofisi 100 za aina hiyo zinazojengwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchi nzima ili kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watendaji wa Idara hiyo.

VOA @ AFCON 2019 MISRI : Uganda Yaishukuru Afrika Mashariki Kwa Kuiunga Mkono

Tamasha la bring your Kid to work lafana jijini Dar.

0
0
 Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc wakifurahia michezo mbali mbali katika tamasha la "Bring your Kid to work" lililofanyika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Kampuni ya Vodacom ni ya kwanza nchini kuandaa tamasha la namna hiyo ambapo watoto wamepata nafasi kuona jinsi wazazi wao wanavyotekeleza majukumu yao ofisini hapo 
 Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc wakifurahia michezo mbali mbali katika tamasha la "Bring your Kid to work" lililofanyika makao makuu ya ofisi za kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Kampuni ya Vodacom ni ya kwanza nchini kuandaa tamasha la namna hiyo ambapo watoto wamepata nafasi kuona jinsi wazazi wao wanavyotekeleza majukumu yao ofisini hapo
 Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc wakifundishwa jinsi ya kutumia platform ya instant School ambayo inawawezesha wanafunzi kupata vitabu vya masomo mbali mbali, katika tamasha la "Bring your Kid to work" lililofanyika makao makuu ya ofisi za Vodacom mwishoni mwa wiki. 

KAMPUNI YA UUZAJI MAGARI KWA NJIA YA MTANDAO YA NIKKYO YATUA RASMI TANZANIA

0
0
Mkurungezi Mkuu wa Kampuni ya Nikkyo Japanese Leon Sera(kulia) inayojihusisha na uuzaji wa magari kwa njia ya mtandao akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo nchini Tanzania.Lengo ni kurahisisha watanzania kuagiza magari kupitia kampuni hiyo kwa gharama nafuu kwa magari yenye ubora.Katikati ni Meneja mkazi nchini Tanzania wa kampuni hiyo Abbas Mussa na kushoto ni mmoja wa maofisa wa Nikkyo barani Afrika KentaroIkezawa.. Mkurugenzi Mkaazi wa kampuni ya Nikkyo nchini Tanzania Pili Mkufunzi akizungumza ujio wa kampuni hiyo ambayo ilishaingia nchini mwaka mmoja uliopita na sasa imetangazwa rasmi na kuomba Watanzania kuitumia katika kuagiza magari ya aina mbalimbali kutoka Japan. 
Meneja Usafirishaji wa NIkkyo nchini Tanzania Aaliyah Abdulrhman akifafanua kwa kina kwa wageni waalikwa kuhusu ambavyo wamejipanga kuhakikisha wateja wao wanapata magari yaliyo bora.Ametoa ombi kwa Watanzania kuitumia Nikkyo kuagiza magari pindi. 
Viongozi wa kampuni ya Nikkyo wa nchini Tanzania na Japan wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuizindua rasmi kampuni hiyo ambayo inajihusisha na uuzaji wa magari kwa njia ya mtandao.Utambulisho umefanyika jijini Dar es Sala na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali. Meneja Masoko mkaazi wa kampuni ya Nikkyo nchini Tanzania Abbas Muusa akizungumza wakati wa sherehe za kuitambulisha kampuni hiyo kwa Watanzania ambayo ina uzoefu katika biashara hiyo kwa miaka 24 na kwa Tanzania imeingia mwaka jana. 

KAMPUNI ya uagizaji, usafirishaji na uuzaji magari ya nchini Japan ‘Nikkyo’ imeingia na kuwekeza katika biashara hiyo nchini huku ikiahidi kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali katika kukuza uchumi kupitia mpango wake wa maendeleo ya viwanda. 

Aidha katika kutekeleza adhma hiyo, Kampuni hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1995 na kufanya uwekezaji katika nchi mbalimbali zikiwemo za Uganda na Kenya imewahikikishia wananchi kuwapa huduma bora na zinazokidhi viwango ili kuendana na malengo iliyoyakusudia. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shughuli za kampuni hiyo hapa nchini Mkurugenzi Mtendaji wa Nikkyo Leon Sera alisema kuzinduliwa kwa kampuni hiyo hapa nchini ni mkakati unaolenga kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo wananchi kupitia sekta ya usafirishaji. 
Alisema katika kutekeleza mkakati huo Nikkyo ambayo ina ubobezi wa zaidi ya miaka 20 katika sekta ya uuzaji magari, imejipanga kuwafikia wananchi wenye mahitaji ya ununuzi wa magari ya aina mbalimbali kutoka nchini Japan na kuwafikishia pasipo usumbufu wowote. 

“Tumeingia kuwekeza hapa nchini kutokana na uwepo wa mazingira mazuri na kuvutia uwekezaji, kwetu ni fahari kubwa kuja kuwekeza katika Taifa hili ambalo kwa sasa limejielekeza katika kukuza uchumi wake kupitia viwanda, tuna ahidi kuwa tutafanya shughuli zetu kwa uaminifu mkubwa” alisema Sera 
Alisema kampuni hiyo ambayo inauza magari hayo kupitia mtandao kwa mteja kuchagua aina ya gari anayoihitaji, inampa uhahika mteja wa kupata gari analolihitaji likiwa salama na lenye ubora kwa lengo la kutimiza matakwa ya mteja huyo. 

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni hiyo tawi la Tanzania Abbas Ally, alisema ujio wa kampuni hiyo hapa nchini kutawawezesha watu wenye mahitaji kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata katika uagizaji magari. 

Alisema ukitifautisha na kampuni nyingine zinazojishughulisha na uuzaji wa magari, Nikko imejiwekea utaratibu mzuri wa kutuma mtu kwenda hadi nchini Japan kulikagua gari linalopendekezwa na mteja kabla ya kumletea hapa nchini hatua iliyolenga kumpatia gari iliyo na ubora. 

Wakati huo huo Meneja Usafirishaji wa Nikkyo nchini Tanzania Aaliyah Abdulrhman alisema wao wanachoangalia zaidi ni kuhakikisha mteja anayehitaji kuagiza gari kupitiakwao anapata gari yenye uhakika na iliyobora kwani kabla ya kuagiza gari wanatuma maofisa wao kwa ajili ya kufanya uchunguzi na baada ya kuridhika ndipo sasa wanamletea mteja wao. 

“Hatuangalii fedha bali kwetu cha kwanza ni ubora wa gari, tunataka kuhakikisha gari inayoagizwa kupitia kampuni yetu inakuwa katika mazingira mazuri na iwapo tutaona kuna tatizo tunamshauri mteja na sio tu kuchukua fedha yake.Tunaomba Watanzania wote wanapotaka kuagiza magari watuitumie Nikkyo kwani inayo uzoefu wa kutosha na kwa Tanzania ndio imeingia lakini katika nchi nyingine barani Afrika na Ulaya imekuwa ikifahamika na maarufu kwa uagizaji magari kutoka Japan,”amesema.

Taarifa ya kuwasili kwa Ujumble wa Wafanyabiashara kutoka nchini Brazil leo

0
0
Ubalozi wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Zanzibar unapenda kuwatarifu wote kuwa ujumbe wa Tanzania uliojumuisha wafanyabiashara 12 kutoka sekta binafsi na baadhi ya wakuu wa mashirika ya umma waliokwenda kwenye ziara ya kibiashara nchini Brazil kwa siku kumi unatarajiwa kurudi nchini Tanzania kesho Jumatatu saa tisa kamili mchana kupitia uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Airport na ndege ya South African Aiways ukitokea nchini Brazil.

Ziara hii ilianza tarehe 28 Juni hadi 08 Julai,2019 yenye lengo la kutafuta fursa za kibiashara, uwekezaji na masoko kwa bidhaa zinozalishwa Tanzania ukiongozwa na Balozi wa Heshima wa Shirikisho la Jamuhuri ya Brazil Zanzibar Mhe. Abdulsamad Abdulrahim

The Consulate of Brazil Zanzibar avails itself the assurances of its highest consideration.

The Honorary Consulate of the Federative Republic of Brazil, Zanzibar

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAONESHO YA 43 SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Picha mabalimbali za wananchi waliofika kununua bidhaa mbalimbali katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

VIJANA MIKOA SABA TANZANIA WAKUTANA KWENYE KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAISLAM WA AHMADIYYA

0
0
Vijana hapa nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na vitendo vinavyomchukiza Mwenyezi Mungu ambavyo ni pamoja matumizi ya dawa za kulevya, wizi, na uasherati, ambavyo vinaweza kubabisha wakapoteza mwelekeo na kutotimiza malengo yao.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumapili Julai 7,2019 na Kiongozi wa Vijana wa Kitaifa wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya, Sheikh Ramadhan Hassan Nauja katika kongamano la siku tatu lijulikanalo kama Ijtemaa ya Khuddam Kanda ya Kaskazini la Mwaka 2019 linalojumuisha washiriki kutoka mikoa saba lililofanyika katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Sheikh Nauja amesema ipo haja kwa viongozi wa dini kuhakikisha wanawalea vijana katika misingi ya kiimani ambayo itawasaidia kupata thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu pamoja na kuwa raia wema katika maeneo wanayoishi.

Amesema vijana ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo ni budi kwa viongozi wa dini wakawajengea misingi mizuri ya kumjua Mwenyezi Mungu na kuondokana na vitendo viovu kwani ndiyo kundi pekee ambalo lipo katika hatari kubwa ya kukumbwa na vishawishi katika ulimwengu huu.

Naye Sheikh Musa Issa kutoka Visiwani Zanzibar amesema viongozi wa dini wanapaswa kujikita kutoa elimu ya dini kwa wananchi waliopo vijijini ili kuwasaidia kumjua Mungu na kuondokana na matukio ya mauaji ya vikongwe na ulawiti na watu wenye ualbino.

Kwa upande wake, Sheikh Yusuph Mgeleka kutoka Kahama amesema Kongamano hilo litasaidia kuwabadili vijana kifikra na kuwa raia wema kwa kufanya kazi halali ambazo zitaweza kuwapatia vipato na kuongeza nguvu kazi katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Mahdilah Issa na Musa Saidi ambao ni miongoni mwa washiriki kongamano hilo kutoka mikoa ya Tabora na Kagera,wamesema mafunzo waliyoyapata yatawawezesha kuwa mabalozi kwa vijana wenzao katika maeneo yao wanayoishi ili kutoa fursa ya vijana wengine.

Kongamano hilo limejumuisha vijana zaidi ya 200 kutoka katika mikoa ya Tabora, Mwanza, Kagera, Geita, Simiyu na Mara limeenda sambamba na mashindano ya Kusoma Quran Tukufu,mashindano ya mpira wa miguu na shughuli mbalimbali za kijamii katika mji wa kahama na lilianza rasimi siku ya Ijumaa na limehitimishwa leo Jumapili.Na Salvatori Cevin - Malunde1 blog
Viongozi wa kitaifa wa Jumuiya ya kiislama ya Ahmadiya wakiomba dua kabla ya kuanza kwa kongamano hilo. Picha zote na Salvatori Cevin - Malunde1 blog
Kiongozi wa Vijana wa Kitaifa wa Jumuiya ya Waislam wa (Ahmadiya) Shekh, Ramadhan Hassani Nauja kushoto akisoma dua katikati ni Sheikh, Musa Issa kutoka Visiwani Zanzibar kulia ni Sheikh Yusuph Mgeleka.
Viongozi mbalimbali wa Kongamano hilo wakiwa wanasikiliza kwa makini mada zinavyowasilishwa.
Shekh Yusuph Mgeleka akiwasilisha mada mbalimbali katika kongamano hilo.
Shekh, Musa Issa kutoka Zanzibar akisoma Quan Tukufu katika kongamano hilo ambalo lilikuwa na mashindano ya kusoma kitabu hicho.
Washiriki wa kongamano hilo la siku tatu liliofanyika mjini Kahama.
Viongozi mbalimbali wa jumuiya ya kiislam ya ahmadiya kutoka mkoa wa shinyanga wakiwa na viogozi wa kitaifa wa jumuiya hiyo.

WALEMAVU 300 MOROGORO WAPEWA VIFAA WEZESHI NA SHIVYAWATA..

0
0
Chama cha watu wenye ulemavu nchini shivyawata kimegawa vifaa wezeshi zaidi ya 300 kwa walemavu kutoka wilaya 4 za mkoa wa Morogoro, lengo likiwa ni kuwaepusha dhidi ya changamoto zinazowakabili na kuwaepusha na utegemezi.

Katika makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo amesema wazazi na walezi wa watu wenye ulemavu waachane na tabia ya kuwaficha watu hao hasa katika nyanja ya elimu jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma maendeleo yao binafsi huku pia akishukuru wadau waliojitokeza kusaidia ufanikishaji wa zoezi la kupatikana kwa vifaa hivyo ikiwemo shirika la sigara tanzania tcc na shirika la kimataifa la tumbaku kutoka japan jti...

Mwenyekiti wa shivyawata Taifa Ummy Nderiananga ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuonesha dhamira ya kujenga haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwani wameshuhudui wakipatiwa nyadhifa kubwa kama mawaziri jambo ambalo limeiweka serikali ya tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache zinazothamini mchango wa viongozi kutoka watu wenye ulemavu..

Mkurugenzi wa mauzo wa TCC Victor Mashobe  aliyemuwakilisha Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo amesema wameshirikiana na shivyawata kutoa msaada huo kwani watu wenye ulemavu wanauhitaji mkubwa kwani watu hao wanastahili kuwezeshwa ili waweze kujikwamua kiuchumi..

ugawaji wa vifaa hivyo umehusisha watu wenye ulemavu kutoka wilaya za kilosa 101, mvomero 66, ifakara 77 na morogoro mjini 73.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro katikati Regina  Chonjo,Mkurugenzi wa mauzo wa TCC Victor Mashobe,Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Azizi Abood wa kwanza kulia pamoja na wadau mbalimbali wakimkabidhi muhitaji baiskeli.

 baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa kwa watu wenye ulemavu mkoani morogor
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mh Regina Chonjo katika picha ya pamoja na baadhi ya watu wenye ulemavu na viongozi wengine mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo.

RITA YAENDELEA KUTOA VYETI VYA KUZALIWA MAONESHO SABASABA

0
0
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), inatoa huduma mbalimbali ikiwamo vyeti vya kuzaliwa katika Maonyesho 43 ya biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa RITA, Josephat Kimaro amesema mbali na kusajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa pia wakala utatoa ushauri wa kisheria bure kuhusu masuala ya kuandika wosia na mirathi.

“Pia tutapokea maoni, maswali, ushauri na mapendekezo kuhusu huduma za Wakala,” amesema.Kimaro amesema RITA imekuwa ikishiriki maonesho hayo kila mwaka ambapo amewaomba wananchi wakifika sabasaba watahudumiwa kwa bora kwa wakati. 
Baadhi ya wananchi wakipata huduma ya vyeti vya kuzaliwa katika banda la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa RITA, Josephat Kimaro (kushoto) akizungumza kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo ikiwamo vyeti vya kuzaliwa katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.Watumishi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), wakiwaelekeza wananchi namna ya kujaza fom za cheti cha kuzaliwa leo katika maonesho ya 43 ya Kimataifa Sabasaba jijini Dar es Salaam.

MZUMBE WAAHIDI KUMSHIKA MKONO MBUNIFU ATAKAE TOA WAZO ZURI LA KIBIASHARA

0
0
Na.Khadija seif, Michuzi tv

CHUO kikuu cha Mzumbe cha wanufaisha wajasiriamali wadogo na wakubwa kwa kuwapatia mafunzo na elimu jinsi ya kuboresha na kujiajiri katika biashara ili kufikia uchumi wa viwanda.

Akizungumza na Michuzi tv Makamu Mkuu wa chuo kikuu Mzumbe Pro.Lughano Kusiluka katika Maonyesho ya 43 ya kimataifa ya kibiashara (7'7 ) jijini Dar es salaam amesema wananchi watakaofika katika banda lao wataweza kupatiwa elimu ya ujasiriamali, namna ya kutafuta masoko pamoja na kuboresha 
biashara zao.

Hata hivyo Kusiluka ameeleza kuwa chuo hicho kinatoa mafunzo mbalimbali ambapo kimebobea kwenye utawala wa rasilimali watu,utawala wa kiuchumi ,utawala wa kibiashara, utawala wa umma.

"Wataalam mbalimbali katika kila eneo wapo kwenye banda kwa ajili ya kutoa elimu na ujuzi, maarifa pamoja na elimu ambavyo wameshapatiwa chuoni kwa vitendo,"

Pia ametoa wito kwa wale ambao watahitaji kujiunga na mwaka ujao wa masomo katika chuo hicho watapatiwa maelezo kwa kina jinsi ya kujiandikisha,kupata fomu pamoja na vigezo na masharti ya kujiunga.

Makamu Mkuu wa chuo hicho amesema imekua ni fursa ya kipekee kuwepo katika Maonyesho hayo kutokana na kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wa elimu pamoja na biashara na kutoa maelezo kwakina.


Kusiluka amefafanua kwa wahitimu ambao wameshapata mafunzo chuo cha hawajutii kupoteza miaka yao chuoni kwa sababu ya kupata faida katika kambi iliyopo chuoni hapo kwa wahitimum

"Tumeamua wanafunzi wanaohitimu waweze kukaa kambi ya ujasiriamali ili waweza kupata ujuzi na maarifa ya kujiajiri wao wenyewe na pia kutoa mawazo ya kiubunifu yatakayowawezesha watu kupata ajira kiurahisi zaidina kuboresha biashara kwani kwa sasa wahitimu wanapitia changamoto kubwa kuajiriwa kwenye makampuni ,"

Pia ametoa wito kwa wale ambao watahitaji kujiunga na mwaka mpya wa masomo katika chuo hicho watapatiwa maelezo kwa kina jinsi ya kujiandikisha pamoja na kupata fomu katika mikoa ya Dar es salaam, Morogoro na mikoa mingine.
Makamu Mkuu wa chuo cha Mzumbe prof.Lughano Kusiluka akishika bidhaa iliyotengenezwa na mwanafunzi wa chuo hicho aliyenufaika na mafunzo ya elimu ya ujasiriamali

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 8,2019

Wabunge,Madiwani wasiokwenda majimboni wasahau uteuzi wa CCM-Katibu Mkuu CCM.

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images