Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 28 | 29 | (Page 30) | 31 | 32 | .... | 3278 | newer

  0 0
 • 01/25/13--08:41: Article 12


 • 0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipunga mkono kuaga baada ya kupanda treni stesheni ya Dar es alaam tayari kuelekea  Kigoma ambako sherehe za miaka 36 ya chama hicho tawala zitafanyika kitaifa mwaka huu
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipanda treni kuongoza msafara wa Sektretarieti  kwenda Kigoma kutoka Dar es salaam jioni hii
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dkt Asha-Rose Migiro akipunga mkono baada ya kupanda treni kutoka Dar kwenda Kigoma leo
  Ndugu Kinana, Dkt Migiro na Ndugu Nape Nnauye  wakiwaaga wana-CCM na wananchi akwa jumla katika stesheni ya Dar es salaam kabla ya kupanda treni mjini Dar es salaam kwenda Kigoma leo
  WanaCCM wakimuaga Ndugu Kinana na msafara wake kutoka stesheni ya reli Dar es salaam kwenda Kigoma. Picha zote na Bashir Nkoromo

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkesha wa sherehe za Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhamad (S.A.W). 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumin wa dini ya Kiislamu, katika mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013. Kushoto kwake ni ,Sheikh Mohamed Ismail. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa, wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana Januari 24, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za mkesha wa maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W.).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh Mohamed Ismail, wakati akiondoka kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013, baada ya kuhudhuria sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
   Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakia Bilal, akijumuika na waumini wa dini ya kiislamu katika mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Sheikh Mohamed Ismail, wakati alipokuwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku Januari 24, 2013, kwenye sherehe za mkesha wa Sikukuu ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W).
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu zake za mkesha wa sherehe za Maulid, ya Maulid za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), wakati wa sherehe hizo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jana usiku.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba na waumin wa dini ya kiislamu wakijumuika kwa pamoja katika sherehe za mkesha wa Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W), zilizofanyika jana usiku katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.. Picha Zote na Muhidin Sufiani-OMR

  0 0

  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia Wakazi wa wa mji wa Morogoro Stesheni usiku huu,walipokuwa wakielekea mkoani Kigoma kwa njia ya treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka leo jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Ndg Abdulrahman Kinana akizungumza Wakazi wa wa mji wa Morogoro Stesheni usiku huu,walipokuwa wakielekea mkoani Kigoma kwa njia ya treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka leo jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Ndg Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC itikaji na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia Wakazi wa wa mji wa Morogoro Stesheni usiku huu,walipokuwa wakielekea mkoani Kigoma kwa njia ya treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka leo jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.

  0 0

  Mwanamama wa Sauzi Yvonne Chaka Chaka alitupa raha si haba na ngoma zake kibao ezi hizo, mmoja ukiwa huu wa 'Thank You Mr DJ'

  0 0  Japo mwenyewe hayupo nasi kimweili lakini ngoma ya VULINDLELA ya BRENDA FASSIE itatamba  daima.

  0 0

  Kaka Michuzi,
  Pole na kazi,
  Ninaomba kama kuna anayefahamu anifahamishe nini cha kufanya kuhusiana na DAWASCO kinondoni.
  Mimi ni mteja wao Account 00505204, na ninaishi kwenye nyumba ya kawaida yenye idadi ya watu 7 na niliwekewa mita ya maji kama ilivyo wateja wengine.

  Tangu mita ya maji ilipowekwa imekuwa inaleta matatizo kwa mwezi inaonyesha tunapaswa kulipa kati ya TZS 97,000 - 214,511, tumehangaika kuripoti ofisi za Dawasco kinondoni (ofisi iliyoko nyuma ya Airtel HQ) kwa muda mrefu sana na 2010 alikuwepo meneja mwanamke(sikumbuki jina) akaahidi kwa maandishi kwamba tungefungiwa test meter lakini haikufanyika na tulipozidi kufuatilia tukaambiwa amehama na sasa akawepo meneja (Bw. Mtowela) ikabidi tuanze upya story yetu ikachukuwa tena muda mrefu lakini test meter ikafungwa na wakagundua kwamba ni kweli mita  ina matatizo hivyo wakatwambia wataweka mita mpya hapo ilikuwa 2012.

  Tukapewa maagizo kwamba wakati suala letu linashughulikiwa tuwe tunalipa angalau TZS 50,000 (elf 50).

  Tulianza kulipahiyo elf 50 lakini bado walikuwa wakifika kukata maji wakisema tunadaiwa mamilioni ya pesa na wakishakata inabidi twende tena kwa meneja kujieleza ndipo turudishiwe maji.

  25 October, 2012 tulifuatilia Meneja akasema mita ziliwaishia lakini zimeshawasili hivyo Jumatatu 29 October, 2012 watakuja kutubadilishia mita na tutakapopata ankara ya mwezi Novemba 2012 itaonyesha ni kiasi gani tunapaswa kulipa. Ankara ikaendelea kuletwa ikionyesha bado tunadaiwa mamilioni ya pesa (3,789,225.80).

  Leo 25 January, 2013 tatizo bado linaendelea na baada ya kuona tumekatiwa maji kwa sababu tunadaiwa 3,789,225.80 (bill ya December 2012)  tumefika Dawasco kinondoni na tumeambiwa kwamba MENEJA AMEBADILISHWAna hayupo hivyo tufike kesho TUKAANZE TENA STORY UPYAAA!!!

  Na aliyetupa jibu hilo billing officer nae ni mgeni anasema katika kazi alizokabidhiwa hii ya kwetu haipo.
  Kama mteja kwa kweli nimechoka na sielewi nifanye nini maana nimeshakwenda sana kwenye hiyo ofisi lakini hakuna kinachofanyika.
  Naomba kufahamishwa nifanye nini?? kwa sababu mpaka sasa sijui haswa napaswa kulipa kiasi gani ?? na pia wanapokuja kukata maji wananisumbua kwa sababu tatizo sio kulipa bali kama mteja nina haki ya kujua matumizi yangu halisi ni kiasi gani (najua haifikii hiyo elf 50)

  Asante
  Mdau Kinondoni

  0 0

  Kutoka Kushoto - Mh. Balozi Tuvako Manongi, Dr. Aleck Che-Mponda, Mh. Balozi Ramadhani M. Mwinyi
  Kutoka Kushoto - Mh. Noel Kaganda, Mh. Balozi Tuvako Manongi, Dr. Aleck Che-Mponda, Mh. Balozi Ramadhani M. Mwinyi, na shemeji yangu Stanley Harris.


  Dr. Aleck Che-Mponda alikutana na Balozi Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Mh. Tuvako N. Manongi na Naibu Mwakilishi wa kudumu, Mh. Ramadhani M. Mwinyi, jana, Alhamisi, January 24, 2013 mjini New York.

  Dr. Che-Mponda alifanya utafiti muhimu kuhusu mgogoro katika ya Malawi na Tanzania kuhusu Ziwa Nyasa mwaka 1971 kwa ajili ya Ph.D yake kutoka Chuo Kikuu cha Howard (Howard University). Dissertation inaitwa, ''The Malawi-Tanzania Border and Territorial Disputes, 1968: A case study of Boundary and Territorial Imperatives in the new Africa". Dr. Che-Mponda alimkabidhi Mh. Balozi Manongi, nakala la andiko (dissertation) lake.  Kwa wasiofahamu, Dr. Che-Mponda ni baba yangu mzazi.

  Utafiti aliyofanya zaidi ya miaka 40 uliyopita umekuwa muhimu sana sasa kutokana na Rais wa Malawi, Mh. Joyce Banda kuruhusu makampuni kuchimba mafuta (oil exploration) katika Ziwa Nyasa, akidai kuwa Ziwa yote ni mali/ardhi ya Malawi.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiongoza mapokezi ya ujumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma mapema asubuhi hii kwa usafiri wa treni,ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayo adhimishwa mkoani humo.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.Kushoto kwake ni Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro na kulia kwake ni Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye 
   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiagana na baadhi ya WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM,Wajumbe wa Sekretarieti ya NEC wameondoka jana jijini Dar kwenda Mkoani Kigoma kuadhimisha miaka 36 ya Chama hicho.

   Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwaaga Wanachama wa CCM mkoani Dodoma waliokuwa wamefika Stesheni ya Dodoma asubuhi hii kuwalaki Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM
  Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika stesheni ya treni Mkoani Dodoma Mapema leo asubuhi.
  Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro  akiwa ndani ya treni asubuhi hii akiwapungia mkono WanaCCM wa Mkoani Dodoma waliofika kuwalaki na kuwatakia safari njema Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,wanaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM

  0 0

  Na. Lemmy Hipolite-Mo Blog.
  Kofia ngumu za kusaidia kuokoa kichwa dhidi ya majanga mbalimbali iwe ni katika maeneo ya ujenzi au katika vyombo vya usafiri ni muhimu sana kwetu tunapokuwa katika mazingira hayo.
  Tunaishukuru serikali kwa kutumia idara zake husika kuhimiza matumizi ya kofia hizi hasa kwa madereva wa usafiri wa pikipiki maarufu kama Bodaboda.
  Kama inavyojulikana mtu ni afya na pia tunafahamu kuna baadhi ya magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kugusana, kutumia kitu kimoja watu wawili au zaidi na mengine kwa njia ya maji, hewa, mbu, kujamiiana na kadhalika.
  Hapa kwenye hili la kofia ngumu bado hainiingii akilini vizuri jinsi gani twaweza kukwepa magonjwa ya ngozi na mba japo sio lazima tuyapate wala hatuyaombei ila tunaangalia uhalisia wa matumizi ya kofia hizi.
  Ndugu zangu wataalamu wa magonjwa ya ngozi na tiba hili likoje katika uhalisia wake? Sichokonoi ila naomba kufahamu tu kwamba tuwe tunazifua? Au hakuna neno? Mzingatie pia je zitakauka?.
  Wadau sijasema msivae helmet la hasha nimeulizia tu ili woote tupate fahamu.
  Karibu uchangie maoni yako kwa kubofya hapa

  0 0


  0 0

  Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamepanga kufanya ziara ya kihistoria mkoani Morogoro mwezi wa tatu. Ziara hiyo ya siku tatu waliyoipa jina la Dom mpaka Moro (bata kwenda bata kurudi) inatarajiwa kufanyika sehemu mbalilmbali za mkoa wa Morogoro. 
  Mratibu wa ziara hiyo Mr AMANI KIZUGUTO ameuambia Mtandao huu  ya kwamba taratibu za awali za maandalizi kwa upande mmoja zimekamilika kwani tayari wameshazungumza na mshauri wa wanafunzi (dean of students) katika maandalizi ya awali.
  Alisema wanatarajia katika ziara hiyo kutembelea mbuga ya wanyama mikumi,maporomoko ya maji katika milima ya udizungwa huku mazungumzo ya kupitia katika vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo Mkoani Morogoro yakiendelea ili kwenda kufanya nao matukio mbalimbali ya kijamii.
  Pamoja na kujadili mambo ya kielimu. haya sasa kazi kwenu wana udom kwa wale mtakaopenda kwenda wasilianeni na mratibu kwa simu namba 0717 3767350769 081122

  0 0
 • 01/25/13--23:48: MDAU WA TWANGA ALA NONDOZZZZ
 •  Mdau  Lusivya wa Twanga Pepeta amekula nondozzz yake ya pili ya Accounting and Finance kutoka kwenye  Chuo Kikuu cha De Monfort University  kilichopo UK. Hapa akiwa na marafiki zake.
   La Familia Msiilwa Baraka, Omary Baraka na Baraka Baraka wakisheherekea na Lusivya
  Wahitimu Mo,Lusivya na Rashid wakisherehekea nondozzzzz

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Tabora waliofika kwenye Stesheni ya treni ya mkoa huo kuupokea ujumbe wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana sambamba na Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye wakiwaaga Wanachama wa CCM maeneno ya Stesheni ya Seranda,wilaya ya Manyoni mkoani Singida.wakati ujumbe wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM,unaoelekea mkoani Kigoma kwa usafiri wa treni kwenye maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM ulipopita eneo hilo mchana wa leo.
   Vijana wa Chipukizi Wilaya ya Manyoni,Mkoani Singida wakimvisha skafu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana wakati alipofika kwenye Kituo cha Treni cha Saranda mkoani humo na kuzungumza na WanaCCM wa Manyoni.Mh. Kinana na Ujumbe wa Sekretarieti ya CCM wako safarini kuelekea Mkoani Kigoma kwenye Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM.
  "Bai Baii.........!! "hivi ndivyo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana sambamba na Katibu wa NEC,Itikaji na Uenezi CCM,Nape Nnauye walivyokuwa wakiwaaga wanaCCM wa mji wa Saranda,Wilayani Manyoni.
  Dkt. Asha-Rose Migiro akisalimiana na WanaCCM wa Manyoni.
  Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt. Asha-Rose Migiro akiwasalimia wanaCCM wa Manyoni,Mkoani Singida wakati waliposiama katika kituo cha Saranda.
  Mbunge wa Jimbo Manyoni,Mh. John Chiligati akizungumza.
  Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza na WanaCCM wa Manyoni leo.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza na WanaCCM wa Manyoni leo.

  0 0

  Katibu wa Bunge ambae pia ni Katibu wa Afrika wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA), Dr Thomas Kashililah akipokelewa katika Bunge la Nigeria na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kibunge Mhe.Daniel Reyeneiju.Dr.Kashililah na ujumbe wake wako Abuja, Nigeria kutathmini hatua za maandalizi ya Mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CPA unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi ujao.
  Meneja wa Mikutano ktk Bunge la Nigeria Bw.Kayode, akielezea hatua za maandalizi na maeneo ya mikutano Katibu wa CPA Afrika, Dr Thomas Kashililah (kwanza kushoto).
  Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Mhe Msuya Waldi Mangachi (katikati) akifafanua kuhusu kitabu chake Regional Integration in Africa kilichotokw hivi karibuni.Balozi Mangachi ambae amemaliza muda wake nchini Nigeria alikutana na Dr Kashililah ambae yuko katiks ziara ya kikazi nchini humo.Kulia ni Nd.Demetrius Mgalami, Katibu Msaidizi wa CPA Afrika na Mkuu wa Itifaki katika Bunge la Tanzania. PICHA NA SAIDI YAKUBU WA OFISI YA BUNGE.

  0 0

  Bondia Antony Mathias (kushoto) akitunishiana misuri na Fadhili Majia baada ya kupima uzito,leo jijini Dar es salaam  kwa ajili ya mpambo wao kesho utakaofanyika katika ukumbi wa CCM Tandale.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, (kushoto) Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akibadilishana mawazo na Katibu Mtendaji (kulia) wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) walipokutana nchini Ethiopia katika mkutano wa AU.

  Mhe. Membe anasisitiza jambo wakati alipokuwa anafanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa SADC, anayefuata baada ya Mhe. Waziri ni Mhe. Joram Biswaro, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Mhe. Waziri Bernard Membe (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Mhe. Joram Biswaro, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia nje ya ukumbi wa mkutano mjini Addis Ababa. mwingine katika picha ni mmoja wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa AU.

  0 0

  • Jumla ya Shilingi milioni 438 kushindaniwa kwa siku tisini(90).

  Wateja wa Vodacom Tanzania mnakumbushwa kushiriki katika Promosheni kabambe ya”Mega SMS Promo” ambayo itamuwezesha mteja kujishindia hadi shilingi milioni moja papo hapo kila siku.

  Aidha, mbali ya kujishindia kiasi hicho cha fedha kupitia kampeni hiyo kubwa na ya aina yake,pia kampeni ya Mega Promo inatoa fursa kwa wateja wawili kujishindia hadi shilingi milioni 5 kila mmoja katika kipindi cha siku saba.

  Jumla ya shilingi milioni 438 zinaendelea kushindaniwa ndani ya siku 90 nchi nzima,na wateja wote watakaoibuka washindi watajulishwa kwa njia ya simu sambamba na kupewa utaratibu maalumu wa kuchukua fedha zao zitakazotolewa kwa njia ya M-Pesa.

  Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Rukia Mtingwa, amesema ili mteja aweze kuingia kwenye nafasi ya kushinda fedha hizo atalazimika kutuma ujumbe wa neno ‘Mahela’ kwenda 15544.

  “Ili kujiweka katika nafasi kubwa ya kushinda unapaswa kutuma neno mahela kwenda 15544, baadaye utaulizwa maswali tofauti tofauti kupitia ujumbe mfupi na ukifanikiwa kujibu utajinyakulia shilingi milioni moja,” anasema Mtingwa.

  Anafafanua kuwa kupitia kampeni hiyo wateja watatu watakaoshinda kwa kujibu maswali vizuri waliyoulizwa kupitia SMS watajinyakulia shilingi milioni moja kila mmoja kila siku. Wakati wengine wawili watakaojibu vizuri zaidi watajipatia hadi shilingi milioni 5 kila mmoja ndani ya siku saba.

  0 0

  Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi kilichoko manispaa ya Mtwara/Mikindani yakoswa koswa kuchomwa moto hii leo kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia pamoja na kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara.

  Vurugu hizo zilizoanza jana,leo zimehamia wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo Inasemekana Askari mmoja wa Upelelezi wa jeshi la Polisi Ameuawa baada ya kujiingiza katika kundi na kubainika akiwapiga picha ambapo pia alikutwa na bastola 2 huku Nyumba ya Mbunge wa Masasi(Mama Kasembe),Vifaa vya Mahakama ya mwanzo pamoja na magari ya Halmashauri nayo yateketezwa kwa Moto mchana wa leo katika vurugu za waandamanaji zilizoanzishwa na watu wa Bodaboda.

  POLISI walianza kutuliza ghasia hizo na baadae wakazidiwa na kulazimika kupiga mabomu ya machozi na risasi za moto.

  Taarifa ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa kufuatia simu za mkono za viongozi wa polisi kutopokelewa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa katika mji huo ambapo Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki.

  Na wameshateketeza nyumba ya mama Kassembe,Mbunge wa Masasi

  Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu. Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.

  Maandamano hayo ya Vurugu yalioongozwa na Madereva wa boda boda. Risasi za moto na mabomu ya machozi yanapigwa kutawanya watu na tayari nyumba moja imechomwa moto na baadhi ya magari huku Vijana wakizidi kusonga mbele

  0 0


  Ngoma ya Eddy Grant ya 'Hello Hello Africa' bado inatikisa hii leo

older | 1 | .... | 28 | 29 | (Page 30) | 31 | 32 | .... | 3278 | newer