Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

MISS UNIVERSE TANZANIA, WINFRIDA DOMINIC ALONGA NA VIJIMAMBO


JK mgeni rasmi mtanange wa watani wa jadi mbugani serengeti

$
0
0
Rais Kikwete akiwa mgeni rasmi katika mpambano wa soka wa ujirani Mwema kati ya mahasimu wakubwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti, hoteli za kitalii za Four Seasons Safari Lodge na Serena Serengeti Lodge ambapo mshindi aliibuka Serena kwa mabao 5-4, baada ya kupigiana penati baada ya kutoka sare ya 1-1 katika dakika za kawaida.

baba bora.....

$
0
0
Mkazi wa jiji la Dar es Salaam alietambulikwa kwa jina la Saidi Mustafa,akiendesha baiskeli huku akiwa amembeba mwanae mgongoni aitwae Bakari kama alivyokutwa maeneo ya Kinondoni B,jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Baba huyu ni mfano wa kuigwa kwa kina Baba wengine,kwani jukumu la malezi ni la pande zote.(Picha na Habari leo).

Padri apigwa risasi na watu wasiojulikana Zanzibar

$
0
0

Padri Ambros Mkenda akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akitaka kuingia ndani ya nyumba yake huko Mpendae Mjini Zanizibar. Picha na Salma Said

Padri Ambros Mkenda wa Parokia ya Mpendae katika Kanisa Katoliki Mjini Zanzibar amepigwa risasi na watu wasiojulikana nje ya nyumba yake majira ya saa 12 jioni wakati akitokea kanisani

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Aziz Juma Mohammed amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alisema Father amepigwa risasi na ameumizwa sehemu ya kichwa na amekuwa akitoka damu nyingi kichwani na tayari anapatiwa matibabu katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.

Alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wahusika walifanya uhalifu huo kwa madhumuni gani kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Sisi tunahesabu kuwa kitendo hiki ni kitendo cha kihalifu na tunawatafuta wahalifu waliofanya kitendo hiki kwa hivyo bado ni mapema kusema kwamba kitendo hiki kimefanywa na nani kwa kuwa bado uchunguzi wetu unaendelea na hadi sasa hakuna mtu tuliyemshika kuhusikana na tukio hili” alisema Kamanda.

Kamanda Aziz akisimulia tukio hilo alisema walipata taarifa majira ya saa 2 na kwenda katika eneo la tukio ambapo Father alikuwa akitokea kanisani na kutaka kuelekea nyumbani kwake wakati akiwa ndani ya gari ndipo aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kuanguka.

“Tumekuta mabaki ya risasi ndani ya gari yake na katika vioo vyake vya gari vimevunjika na tumekuta damu chini pale” alisema Kamanda.

Aidha Kamanda Azizi alisema Father Ambros yeye ni mhasibu pale kanisani na hivyo mara nyingi watu wananaamini kwamba katika siku za krismass mara nyingi sadaka hukusanywa fedha nyingi na hivyo wanamini kwamba alikuwa fedha mikononi na ndipo inawezekana waliamua kumpiga risasi wakitaka kuchukua fedha hizo.

Hata hivyo alisema uchunguzi wa awali ndio utakaoeleza ni suala gani lililopelekea kupigwa risasi lakini wanaendelea na uchunguzi huo ambapo uchunguzi ndio utakaojulikana sababu kamili ya tukio hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Askofu Michael Hafidh wa Kanisa la Anglikan la Mkunazini amesema wamesikitishwa na wamepokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo hasa kwa kuzingatia matukio kama hayo hayajawahi kutokea ya kuwahujumu viongozi wa dini.

Alisema tukio hilo ni miongoni mwa matukio ya kushtusha na yanaashiria hali mbaya ya kiusalama na kuwaomba viongozi wa serikali kuchukua hatua za tahadhari kubwa kwani matukio kama hayo yameanza kutokea kwa viongozi wa dini ambapo mwanzo ilianzia kwa Sheikh Soraga na baadae kutokea kwa Father Ambros.

“ Hii ni hali ya hatari katika nchi yetu na haipendezi lakini serikali lazima ijue sisi hatuwezi kujua wala hatuwezi kujilinda lakini serikali inapaswa kutulinda sisi ndio wananchi wake” alisema Askofu Hafidh.

Askofu Hafidh alisema hivi karibuni kumekuwepo vipeperushi vilivyosambazwa na watu vikiwatisha watu wenye imani ya kikristo ambapo alisema miongoni mwao walikuwa na khofu juu ya kusambazwa kwa vipeperushi hivyo na kuiomba serikali iongeze ulinzi.

“Tumeona hivi vipeperushi na kwa kweli tulikuwa na khofu juu ya vipeperushi hivi lakini ndio tunasema tunaelekea wapi katika maisha haya” alisema Akofu Hafidh.

“Sisi hatuamini kwamba kuna kisasi kwa viongozi wa dini lakini tunachukulia hilo ni tukio la kihalifu na pia hatuna vipeperushi vya aina yoyote vinavyoelezea kuwatisha viongozi wa dini kwa hivyo tunachukulia hayo ni matukio ya kihalifu na wala hatuamini kwamba matukio haya ni ya dini fulani” alisema Kamanda Azizi.

Akielezea kuhusiana na hilo Kamanda Aziz alisema jeshi la polisi limejipanga na kuzidisha ulinzi katika maeneo yote ya makanisa ambapo kumesambazwa polisi wa kutosha kwa kuwa wanajua wakati wa sherehe mambo ya kihalifu hujitokeza.

“Sisi kawaida huwa tunaweka ulinzi siku za sherehe zozote lakini kwanza makanisa yote yamewekwa ulinzi wa kutosha kabisa lakini wahalifu wanapotaka kufanya uhalifu huwezi kujua watatumia mbinu gani na saa ngapi na watafanya uhalifu huo wapi, lakini ulinzi upo wa kutosha” alisisitiza Kamanda Aziz.

HOJA YA MDAU: UFAHARI WA KWENYE MISIBA UONESHENI KATIKA UGONJWA WA MZEE SMALL

$
0
0

Staa wa Vichekesho na Filamu Bongo, Said Mohamed Ngamba ‘Mzee Small’ akiwa amelazwa hospitali kutokana na maradhi yanayomsumbua.

KWENU mnaohusika na sanaa ya filamu Bongo. Mnajitambua sina haja ya kuwataja mmojammoja kwa majina, nitamaliza ukurasa bure.

Mimi najua mpo poa, mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Binafsi niko poa, naendelea na majukumu yangu ya kila siku ikiwamo hili la kuwaandikia barua.

Barua yangu leo moja kwa moja nailekeza kwa nyinyi wote ambao watu sasa hivi wanawatambua kwa jina la mastaa wa filamu katika soko la Bongo, Bongo Movies.

Kikubwa ni kwamba, natambua mchango mlionao katika kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi. Natambua umuhimu wenu wa kuwatibu watu kisaikolojia kupitia filamu zenu mnazozifanya. 

Hongereni kwa hilo.Katika taaluma yangu ya uandishi wa habari, mara kadhaa nimeshuhudia uwezo wenu katika kufanikisha mambo yanayowahusu, iwe ni sherehe au misiba.

Eeeh, kwenye sherehe basi mnalipuka na kushangweka kwelikweli. Kwenye misiba, mnahakikisha mnamsindikiza mtu anayewahusu kwa hadhi anayostahili.

Hoja hapa ni kwamba, hadhi ile ambayo mnajitutumua hadi kwenye misiba, kwa nini tusioneshe kwa mkongwe wa sanaa nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’? Tunashindwa nini? Mbona pesa zipo? 

Kwa nini tusimsaidie mzee wetu ambaye tunaimani alikuwa chachu ya vijana wengi kuingia kwenye sanaa?

Mzee wetu anasumbulia na ugonjwa wa kupararazi. Anashindwa kufanya shughuli zake za sanaa ambazo ndiyo chanzo cha pato lake la kila siku.
Binafsi nilisikitishwa na kupongeza kitendo cha Rais wa Shirikisho la Filamu nchini TAFF, Saimon Mwakifwamba kuingilia kati na kuanza kutembeza ‘bakuli’ la michango kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.

Nilisikitika kwani sikuona haja ya yeye kuingilia kati suala hilo ambalo naamini lilikuwa chini ya uwezo wenu, mnaweza bwana! Kikubwa ni kipi haswa? Mbona mna ‘mauwezo’, msinifanyie hivyo bwana.

Kwani kuna tatizo gani tukiweka nukta katika starehe hata kwa siku moja, tusipige kilevi siku hiyo halafu tujichangishe fedha za kumpa sapoti mwenzetu kwenye kipindi hiki ambacho anaumwa?

Hakika hili ni dogo, tukiamua tunaweza tena haliwezi kuharibu bajeti zenu hata kidogo.

Ni yule yule,
Mkweli Daima.
Joseph Shaluwa

147 Critics:John F Kitime

FM ACADEMIA YAPAGAWISHA MASHABIKI WAKE WAKATI WA PROMOSHENI YA BIA YA WINDHOEK

$
0
0

 Wanamuziki wa bendi ya FM Academia wakitumbuiza wakati wa promosheni ya bia ya Windhoek uliofanyika katika ukumbi wa Alcade wakati wa sherehe ya Sikukuu ya Krismasi  jijini Dar es Salaam. Bendi hiyo inadhaminiwa na kampuni ya Mabibo Wine kupitia kinywaji chake cha Windhoek. (Picha na Habari Mseto Blog)
 Kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Sadati (kushoto) akiwaongoza wanamuziki wa bendi hiyo wakati wa promosheni ya bia ya Windhoek iliyofanyika katika ukumbi wa Alcade
 Wacheza shoo wa FM Academia wakifanya vitu vyao jukwaani
Baadhi ya mashabiki wa FM Academia wazee wa Ngwasuma wakiselebuka

Bilal Muslim Mission yawezesha watu 90 kuweza kuona wilayani Ruangwa

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Agness Hokororo akiwasalimia baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa macho bila malipo kwa udhamini wa Bilal Muslim Mission wilayani humo
 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa ambae pia ni Naibu waziri wa Tamisemi,Kassim Majaliwa akiwa na Bi Somoe Omary alipomtembelea katika hospital ya wilaya ya Ruangwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho na
kuweza kuona baada ya kutoona kwa miaka 10
 Bi Somoe Omary akifurahi baada ya kufanyiwa upasuaji na kuweza kuona baada ya kutoona kwa miaka 10
 Bango la matangazo
Mbunge wa Ruangwa akiwa pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ,Reubern Mfune wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wagonjwa waliotibiwa na kuweza kuona.
Picha zote na Abdulaziz Video

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AFUNGUA RASMI KITUO CHA POLISI CHA KIBOJE ZANZIBAR

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaliminana na maofisa wa Usalama wa Wilaya ya Kati, wakati alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kufungua rasmi Kituo cha Polisi cha Kiboje, kilichpo Mkoa wa Kusini Unguja leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala na Kamishina wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakifunua kwa pamoja kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho ulioanza Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika Kiboje Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja. Kush
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, Saleh Ahmed Said, kutoka Migoz Supermarket, ambaye ni mmoja kati ya watu waliochangia ujenzi wa Kituo hicho cha Polisi cha Kiboje, wakati wa hafla za ufunguzi wa kituo hicho zilizofanyika leo Desemba 26, 2012 Wilaya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje, katika Chumba cha Mawasiliano baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilala, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kamishina wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa (kulia) wakati akitembelea kukagua jengo la Kituo cha Polisi cha Kiboje katika Chumba cha Ofisi ya Polisi Jamii, baada ya kufungua rasmi jengo hilo lililoanza kujengwa Februari 14, 2012 na kuzinduliwa leo Desemba 26, 2012, wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Kikundi cha Sanaa cha Polisi kikitoa burudani ya maigizo.

Kikundi cha ngoma cha Tukulanga kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo.
Picha Zote na Ofisi ya Makamu wa Rais

Salaam za mwaka mpya toka kwa Chef Issa

$
0
0

MWAKA 2012 UMEKUA NI WAMAFANIKIO SANA, MWENYEZI MUNGU AMENIJAALIA MWANZO WA MWAKA KUANZISHA RESTAURANT NYUMBANI TANZANIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KABISA PIA MWISHO WA MWAKA MWENYEZI MUNGU AMENIJAALIA NIMEPATA MTOTO MZURI SANA WA KIKE AMEEN

HAIKUA KAZI NDOGO KUANZISHA RESTAURANT NA KUHAKIKISHA WALAJI WOTE WAWE KATIKA MIKONO SALAMA NA WAFURAHIE CHAKULA.

KWA SASA NIPO MAPUMZIKONI NITAJITAHIDI SANA NIWEZE KUWEKA RECIPE ZOOTE KATIKA PICHA PIA NIWEKE RECIPE MPYA MUWEZE FURAHIA MWAKA MPYA.

NAIMANI TUTAUANZA MWAKA 2013 KWA FURAHA, AFYA NJEMA NA MAFANIKIO

HUKU NI BARIDI SANA  





Migozi Supermarket yachangia ujenzi wa kituo cha polisi Unguja

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Mohamed Gharib Bilal akikabidhi cheti cha shukrani kwa Saleh Mohamed Said kutokana na msaada wake wa kufadhili ujenzi wa kituo cha polisi cha Kiboje mkoa wa kusini Unguja. Kampuni ya Migozi Supermarket ya mjini Zanzibar inayomilikiwa na Saleh imechangia ujenzi huo uliogharimu sh.milioni 50. Picha na Martin Kabemba

TUCHEZE SIASA NA DKT MWAMOYO HAMZA - VOA KISWAHILI

Barnaba & Suma Lee Live In London|Urban Pulse|

WATANZANIA MBWANA MATUMLA NA MADA MAUGO WATOA VICHAPO KWA WAPINZANI WAO

$
0
0
Bondia Mada Maugo (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumtwanga bondia Yiga Juma (Uganda) kwa ‘Knock Out’ raundi ya kwanza.
Bondia Mbwana Matumla (Tanzania) akitangazwa mshindi baada ya kumpa kichapo bondia David Charanga (Kenya).
Mada Maugo (kushoto) akimshushia kichapo bondia Yiga Juma (Uganda) wakati wa mpambano wao.
Bondia Mbwana Matumla (kulia) akitupiana makonde na bondia David Charanga kutoka Kenya.
Bondia David Charanga kutoka Kenya (kulia) akienda chini baada ya kupokea konde kutoka kwa Mbwana Matumla.
David Charanga kutoka Kenya (kulia) akimkabili bondia Mbwana Matumla wakati wa mpambano wao jana.
--
Mabondia wa Tanzania jana waling'ara katika mapambano yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem. Bondia maarufu nchini, Mada Maugo alimchapa Yiga Juma kutoka Uganda raundi ya kwanza kwa ‘Knock Out’. Katika hali iliyoonesha kuwa siku ya vichapo kwa wageni, pambano lingine ambalo bondia Mbwana Matumla alipambana na bondia kutoka Kenya, David Charanga lililokuwa la raundi nane, Matumla aliibuka kidedea katika raundi zote nane na kumfanya aibuke na ushindi wa kishindo.
(PICHA NA ISSA MNALLY NA RICHARD BUKOS / GPL)

leo ni hepi besdei ya kuzaliwa mdau MEGGIE IMPOSTRA (LILIAN)

$
0
0
LEO NI HEPI BESDEI YA KUZALIWA MMOJA WA WADAU WAKUBWA WA GLOBU YA JAMII MDAU MEGGIE IMPOSTRA (LILIAN) WA MOROGORO. WAKATI AKISHEREHEKEA SIKU HII MUHIMU KWAKE 
MEGGIE ANAWATAKIA WADAU WENZIE WOTE 
HERI YA MWAKA MPYA NA MAFANIKIO TELE!

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL - ENZI HIZO

$
0
0
Mkongwe James Brown alikuwa hana mpinzani wakati huo, hasa kwa ngoma yake ya 'say it loud i'm black and i'm proud'

ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mwanadada Saida Karoli na ngoma yake ya 'Maria salome' ilileta pumzi mpya katika muziki wa Tanzania kwa sauti na midundo kutoka Bukoba.Nani anabisha?

shukurani

$
0
0

Ndugu wapendwa:

 Kwa niaba ya ndugu yetu Richard Mwandemani (DJ Rich Maka) familia yake, ndugu na jamaa, tunapenda kutoa  shukran zetu za dhati kwa ushirikiano mwema mliouonyesha toka mzee wetu Edson Mwandemani alipokuwa amelazwa hospitali kwa kuja kumjulia hali hadi  kilio kilipotokea  jinsi mlivyoshughulika kwa misaada yenu ya hali na mali.

Hatuna cha kuwalipa ila Mwenyezi Mungu mwenyewe atawalipa malipo yalio stahili.

 Mwili wa marehemu mzee Mwandemani utaondoka Ijumaa tarehe 28 December, 2012 kwa safari ya kwenda nyumbani na kufika Tanzania Jumapili  jioni December 30, 2012.


Asanteni sana na shukran kwa wema na ukarimu wetu.


Isaac Kibodya, kwa niaba ya Richard Mwandemani  (DJ Rich Maka) na familia yake.

Party ya Mwaka Mpya Columbus, OHIO

$
0
0

Please, take note of the venue change from "Days Inn" to "Club Boomerang" to accomodate the Tanzanian & Kenyan community, together as we bring in the New Year 2013 in a unique way!!!!!!!!
Don't miss this year's countdown as we celebrate big on December 31! While you're remembering the best moments you had in 2012, forgetting about mishaps and looking ahead for 2013!!! Join your fellow Tanzanians and Kenyans in celebrating with our very own "DJ Mus Mus" and "DJ Slim614" on the turn tables
When: Monday, 12-31-12 from 9pm ET - 3:00am ET
Where: Club Boomerang 5736 Karl Rd. Columbus,Ohio 43229
For more information, call 614-425-1502.
See you all there!

SIKU YA WACHAGA YAFANA SANA MJINI MOSHI

$
0
0
baadhi ya wanamuziki wa serengeti band ya arusha kabla ya kutumbuiza tamasha la chagga day moshi ukumbi wa kisasa wa zumbaland.
mtoto akichorwa katika mashamsham ya chagga day ukumbini Zumba Land.
mkurugenzi uhuru museum akitoa historia ya kabila la wachagga.

Tamasha kubwa la kihistoria lililopewa jina la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Moshi lilifanyika kwenye ukumbi wa ZUMBA LAND katika manispaa ya Moshi siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 kuanzia saa sita mchana mpaka saa sita usiku na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa mji huo huku baadhi wakioongozana na familia zao.

Tamasha hilo lililotawaliwa na shangwe za mara kwa mara kutoka kwa wakazi wa mji wa Moshi waliofurika kwenye viwanja hivyo maarufu kwa michezo ya watoto, liliandaliwa na kampuni ya Myway Entertainment ya jijini Dar chini ya Mkurugenzi wake Paul Mganga na kudhaminiwa na kampuni ya bia (TBL) kupitia bia ya Safari Lager na kampuni ya vinywaji baridi (SBC) kupitia kinywaji chake murua cha Pepsi.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images