Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 7,2019


TAMBUA FURSA ZINAZOPATIKANA KWENYE TAMADUNI ZETU

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

Watanzania wametakiwa kujivunia vitu tulivyo navyo pamoja nakujijengea tabia ya kupenda tamaduni zetu na kuacha kubabaikia tamaduni zakizungu kwani tukizitumia vyema tamaduni zetu vyema zitageuka kuwa fursa na kutupatia kipato.

 Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa tamasha la utamaduni lijulikanalo kwa jina la Yakwetu Japhet Jackson  alipokuwa anaongea na waandishi wa habari jijini hapa  wakati alipouzuria katika usiku wa kumsaka mrembo wa Arusha.

Alisema kuwa Tanzania inamakabila 126 na makabila hayo yote yanatamaduni zao na vyakula vyao ambavyo tukienzi ni vivutio tosha kwa wageni hivyo ambavyo vitatuingizia kipato.

"unajua kuna fursa mbalimbali katika mila zetu na tamaduni zetu iwapo tukizienzi ,watu wanaacha asili yao wanataka kuwa wazungu ,watu wangeishi maisha yao  na kuacha kuiga watu wengine wangekuja kujifunza tamaduni zetu na tungepata pesa ,watuwangekuja kutengeneza sinema kupitia mila zetu  na tamaduni zetu "alisema Japhet 

Aidha pia alisema kuwa yeye katika kuenzi utamaduni ameaandaa tamasha ambalo linatarajiwa kufanyika Aguast 26 jijini Dodoma na itashirikisha makabila yote yaliopo hapa nchi ,ambapo watakuja katika maonyesho hayo na kuonyesha tamaduni zao ikiwemo ngoma zao,mavazi yao pamoja na vyakula vyao.

Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo lililobeba jina la Yakwetu kuona tamaduni mbalimbali za makabila pamoja na vyakula pia alisema mbali na hivyo kutakuwa na mbio zijulikanazo kama Kondoa Irangi marathon itakayofanyika siku ya kilele cha Tamasha hilo.
Mkurugenzi wa tamasha la utamaduni lijulikanalo kwa jina la Yakwetu ,Japhet Jackson  

KILA MTANZANIA ANA WAJIBU WA KULINDA NCHI-DKT BASHIRU

0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Watanzania watakiwa kutambua kuwa kazi ya kulinda uhuru wan chi yetu ni wa kila mwananchi na sio jukumu la Serikali peke yake.

Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali Kakurwa wakati akifungua na kuweka jiwe la msingi katika sherehe za uzinduzi wa boma la “Eunoto”Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja kilichopo ndani ya kata ya Sepeko wilayani Monduli Mkoani hapa ambapo alianza kwa kuwapongeza vijana wa kimasai ambao wameingia katika hatua ya makuzi na kupewa heshima ya kupewa rika na kuitwa Nyangulo.

Alisema kuwa uhuru ambao tulio nao umetokana na mapambano ya wenyeji dhidi ya wageni ambao walitutawala kwa mda mrefu na tukapata ushindi mkubwa na ndio maana nchi yetu ina uhuru na amani na ndio maana tunaheshimika duniani kote.

“ndungu zangu nchi yetu ilitawaliwa na wageni na tabia ya mtawala wa kigeni hutumia mkakati wa kuwagawa anao watawala ili asiweze kumpinga na kumuondoa katika nafasi aliopo ,mkakati mkubwa wa mtawala wa kigeni ni kuwagawa watu wenyeji hivyo tuwe makini na tusikubali kutawaliwa tena na wageni na uhuru wetu na pia tuendelee tulinde amani yetukuendelea kueneza nizamu na ”Alisema Dkt. Bashiru .

Alisema uhuru huu na amani ndio uliosababisha Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta na Rais wetu John Magufuli kuweza kukutana kwa pamoja jiji Mwanza na kuwaarifu dunia kuwa waafrika wote ni ndugu na Afrika ni moja hivyo alitumia jukwaa hilo kuwa wapongeza viongozi hao kwa hutuba walizozitoa kuwa ni nzuri kwani zimelenga kuhamazisha wananchi wao kujenga ujirani mwema ,kudumisha undugu wetu wa umoja Afrika Mashariki pia kukemea migawanyiko inatokana na wanasiasa wasiokuwa na adabu.

“mnajua mji wa Arusha , Kilimanjaro na Tanga mmepakana sana na Kenya ni majirani na mnategemeana katika shughuli mbalimbali za kibiashara ,kijamii na hata za kiutamaduni na mikoa hii pamoja na nchi jirani ya Kenya haina mipaka kwani inategemeana katika shughuli hizi mbalimbali hivyo tuendelee kudumisha umoja huu wan chi zetu pamoja na jumuiya yetu na lengo la sisi wa Afrika ni kufanya nchi zetu za Afrika kuwa moja hivyo naomba niwaambie nyie vijana wa rika la Eunoto (Nyangulo ) muendelee kudumisha umoja huu na muuende na ujumbe kuwa kazi ya kudumisha umoja wetu haija kamilika na itakamilika pale Afrika itakapokuwa moja na mahali pa kuanzia ni kudumisha umoja wa Afrika mashariki”alisema DKT Bashiru.

Akiongelea sherehe hizo kiongozi wa rika ya Eunoto( Nyangulo) Baraka Joseph alisema kuwa sherehe hizi zilizofanyika leo ni za kimila na zinalengo la kuwasimika rika vijana pia sherehe hizi ni kwa ajili ya kuhitimisha zoezi la kuwapeleka jandoni ( kutairi ) vijana wa rika la Nyangulo,alifafanua kuwa kwa mila ya kimasai zoezi hili linaendeshwa kwa kwa kipindi na huchukuwa kipindi cha miaka saba tangu kufungwa kwa zoezi hilo hadi kipindi cha kufunguliwa

“sisi wamasai tunakuwaga na kipindi cha kufungua zoezi hili tunalolifunga leo tulifungua Rasmi 2012 na tumeliendesha kwa muda wa miaka saba na sasa hivi ndio tumezinduliwa leo sherehe hizi za kufunga kwa iyo tulivyozinduliw a leo tutafanya sherehe hizi kwa muda wa miezi mitatu na ndio tuatafunga rasmi zoezi la kutairi mpaka tena miaka saba iishe ndio tuje tufungue tena upya msimu mungine”alisema Baraka

Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare alipongeza vijana hao kwa hatua waliofikia na kubainisha kuwa waendelee kudumisha yale yote ambayo wamefundishwa na wakubwa wao,alitumia mda huo kutaja changamoto zinazowakabili wananchi wa Wilaya hiyo ikiwemo ya ukosefu wa chakula hivyo aliomba serikali iwasaidie kupunguza bei ya mazao ya chakula ikiwemo maindi ambayo alisema kuwa yamepanda kwa kasi kubwa mno.

“kipindi hichi tunaukame mvua hazijanyesha huku kwetu hivyo kunaonekana kunaweza kuwa na tatizola njaa hivyo tunaomba serikali ione namna gani inaweza kutusaidi ,sio wananchi wote ni wafugaji kunawakulima kwa hiyo watateseka hivyo tunaombasana serikali itusaidie na pia mkuu wa mkoa nakupa hili uondoke nalo uone utatusaidiaje na sisi kama kamati ya siasa tutajitaidi kuangalia namna ya kuwasaida”Sanare.

Napenda kumalizia kwa kuwasihi wananchi wa jamii ya wafugaji kupeleka watoto shule kwani ,ili uweze kuongoza vyema lazima uwe na elimu ya kutosha ambayo itakuwezesha kuongoza vyema ,alimpongeza Rais magufuli kwa kutoa elimu bure kwani pia imewasaida watoto wengi wa jamii ya kifugaji ambao walikuwa hawana uwezo wa kulipa ada kuweza kwenda shule.
 Katibu  Mkuu wa chama  chama cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali Kakurwa akiwa katika picha ya pamoja 
  Katibu  Mkuu akiangalia vijana wa rika la Nyangulo wakiendelea kucheza ngoma zao za kitamaduni ya asili ya kimasai 
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare akizungumza na Wananchi waliofika kwenye sherehe hizo
 Katibu  MKuu wa chama  cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali Kakurwa akiwahutubia wananchi waliohudhuria   katika sherehe za uzinduzi wa boma la “Eunoto”Ooltwati zilizofanyika katika kijiji cha mti mmoja kilichopo ndani ya kata ya Sepeko wilayani Monduli  
Picha ya Pamoja

NMB WASISITIZA MTOTO AKAUNTI NA CHIPUKIZI AKAUNTI SABASABA

0
0

Meneja Mradi wa Uwajibikaji kwa Jamii, Bi. Lilian Kisamba akizungumza juu ya umuhimu wa kuwaandaa watoto kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo, akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Sabasaba Dar es Salaam.

Sehemu ya watoto wanaotembelea Banda la NMB wakichorwa nyuso zao baada ya kupata huduma na elimu ya masuala ya fedha.
Bi. Lilian Kisamba akifafanua jambo alipozungumzia umuhimu wa kuwaandaa watoto kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo, akiwa ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea Sabasaba Dar es Salaam.
Sehemu ya watoto wanaotembelea Banda la NMB wakichorwa nyuso zao baada ya kupata huduma.


BENKI ya NMB imewashauri wazazi na walezi kuwafungulia watoto wao akaunti za watoto pamoja na Chipukizi akaunti kwa ajili ya kuwawekea akiba na kuwajengea utamaduni wa kujifunza usimamizi wa fedha zao kwa maisha bora ya baadaye.

Kauli hiyo imetolewa leo katika viwanja vya Sabasaba ndani ya Banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Akizungumza Meneja Mradi wa Uwajibikaji kwa Jamii, Bi. Lilian Kisamba alisema akaunti hizo zinasaidia kuwaandaa watoto kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa malengo.

Alisema elimu hiyo ikitolewa vizuri na mapema kwa watoto na jamii nzima inasaidia kupunguza umasikini kwani tutakuwa nafamilia zenye uelewa na matumizi sahihi ya fedha kimalengo.

"Hizi akaunti za wajibu mzazi au mlezi anaweza kuweka kiwango chochote kwenye akaunti ya mtoto hata shilingi 1000 kwa akiba ya mtoto wake...pia hazina gharama zozote za uendeshaji kama akaunti zingine.

Aidha aliongeza kuwa jamiii kwa ujumla ina kila sababu ya kuona umuhimu wa elimu ya masuala ya fedha kuenea kwa kiasi kikubwa na hata ikiwezekana Serikali kuifanya sehemu ya mtaala ili iwe ikimfikia kila mmoja na kujifunza kwa undani wajibu na mahitaji.

MAMIA WAVUTIWA NA KIJIJI CHA MFANO KILICHOHIFADHIWA KWENDE BANDA LA WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS)

0
0
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake (pichani juu), wamefurika kwenye banda la TFS kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Undelezaji biashara nchini (Tan Trade) kwenye viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Wengi wa wananchi hao ni pamoja na wadau wa misitu na nyuki, wafanyakazi wa umma na binafsi ambao walifika kupata huduma mbalimbali lakini kubwa iliyovutia wengi ni ‘Demo’ ya Mwonekano wa Kijiji cha Mfano kilichohifadhi Mazingira kando kando ya Safu za Milima ya Maporomoko ya Maji kilichopo katika Banda la Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Mwonekano huo wa mfano umevuta hisia za watu wengi kama inavyoonekana pichani na kuinua kiu ya kutaka kujua zaidi kuhusu uhifadhi wa misitu. Sambamba na hilo TFS imetoa ofa ya safari ya kitalii katika Hifadhi ya Msitu Asilia Magamba. safari hii itafanyika tarehe 12 hadi 14 /06/2019 na zitaanzia katika viwanja vya maonesho ya kibiashara (sabasaba) jijini Dar es Salaam na kumalizikia hapo hapo.

Gharama kwa wakubwa ni tsh 171,000 na kwa watoto ni tsh 148,000 tu ikijumlisha gharama ya usafiri, malazi, chakula, tozo ya kuingia hifadhini na gharama ya waongoza wageni.

Malipo yote yatafanyika katika banda la TFS lililopo ndani ya banda la Wizara ya Maliasili na Utalii katika viwanja vya sabasaba.





MBUNGE KABATI AWAWEZESHA WANAFUNZI WA UKWATA LUNGEMBA KUREKODI ALBAMU YAO

0
0
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa(CCM) Rita Kabati msaada kwa mmoja ya wanafunzi wa chuo cha Rungemba walipofanya mahafari ya kidini. ( Picha na Denis Mlowe) 
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa(CCM) Rita Kabati akizungumza na wanafunzi wa chuo cha maendeleo ya jamii Rugby (hawapo pichani) wakati wa mahafali ya ukwata.
…………………….

NA DENIS MLOWE, IRINGA


MBUNGE viti maalum mkoa wa Iringa (CCM), Mhe. Ritta Kabati amechangia shilingi laki mbili (2) na kuahidi kununua kifaa cha muziki kwa wanafunzi wa chuo cha Maendeleo ya jamii, Lungemba, Mufindi zitakazotumika katika kurekodia albamu yao.

“Nitachangia shilingi laki 2 kwanza ili mmalize kurekodi nyimbo zenu za video. Na pia nitachangia kifaa cha muziki nitajaribu kutafuta cha aina gani kisha niwaletee”

Mhe. Kabati amechangia fedha hio wakati wa mahafali ya wanafunzi wa dhehebu la Ukwata, chuoni hapo.Pamoja na mchango huo, Kabati amewataka wanafunzi wa chuoni hapo kujikita katika mambo ya kimaendeleo ikiwepo mafunzo ya ujasiriamali yatakayoweza kunyanyua kipato chao.

“Msiache kujiingiza katika mafunzo ya ujasiriamali mtakaposikia yanafanyika kwa sababu yatainua kipato chenu”

Awali akisoma risala kwa mgeni mwanafunzi anayehitimu, Grace Mhanga amebainisha changamoto zinazowakabili wanaukwata chuoni hapo kuwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya muziki, laptop pamoja na pesa taslimu shilingi laki 2 kwa ajili ya kurekodia video.

“Sisi kama wanaukwata tunakosa pesa shilingi laki mbili pamoja na vifaa vya muziki vitakavyosaidia kuendeleza injili ya MUNGU”

RAIS MSTAAFU DK. JAKAYA KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA TIB ‘GROUP’

0
0
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametemebelea Banda la TIB ‘Group’ lililopo katika viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere na kujionea shughuli za uzalishaji na usindikaji wa nyama za kuku na mayai zinazofanywa na kampuni ya kizalendo ya Mkuza Chicks.

Mkuza Chicks ni mmoja wa wawekezaji wazalendo waliyowezeshwa na Benki ya Maendeleo ya TIB.

Akiwa katika banda hilo Dkt. Kikwete alipatiwa maelezo ya namna ambavyo kampuni hiyo inavyozalisha vifaranga pamoja na usindikaji wa nyama za kuku na kusambaza katika soko la ndani ya nchini.

Akiwa katika banda hilo, Dkt. Kikwete aliahidi kutembelea shamba la Mkuza lilipo Kwalla, Kibaha vijijini ili aweze kujifunza shughuli za ufugaji.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akizungumza na Meneja Masoko wa kampuni ya kizalendo ya Mkuza Chicks, Bw. Howard Ringo (kulia). Katikati ni Mtalaamu wa Mifugo wa Kampuni hiyo, Bw. Malambugi Ahobokile.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akifurahi jambo na wafanyakazi wa Benki ya TIB ‘Group’, ambao ni Meneja Masoko na Uhusiano, Bw. Saidi Mkabakuli (katikati) na Afisa Huduma kwa Wateja, Bi. Praise Eliya (kulia).
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini daftari la wageni wakati alipotembelea Banda la TIB ‘Group’ wakati wa Maonesho 43 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Tamasha la ZIFF 2019 - Vigogo Vya Sinema Ulimwenguni wateremka Zanzibar katika Tamasha la Filamu


Waziri Kamwelwe azindua treni ya Majaribio SGR,awamu ya kwanza Dar mpaka Moro kukamilika mwishoni mwa mwaka huu

0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa na Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa ndani ya treni  ya Wahandisi mara baada ya uzinduzi wa Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana.Picha na Michuzi Jr.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa na Wageni waalikwa mbalimbali wakishuka kwenye treni  ya Wahandisi mara baada ya uzinduzi wa Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati akizindua Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Yapi Merkezi mara baada ya kuzindua Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kufanyika katika eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk na baadhi ya Wafanyakazi wa TRC wakishuka kwenye katika trenni ya Wahandisi mara baada ya uzinduzi wa  Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kufanyika katika eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana.
Picha ya Pamoja
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akifafanua jambo kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk mara baada ya Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana,kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa
Treni ya Wahandisi kama ionekavyo pichani kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk akimkaribisha Mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa  Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Yapi Merkezi akizungumza mbele ya Mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa sambamba na wageni waalikwa mbalimali waliofika kwenye hafla fupi ya kuzindua  Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa wakifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akionesha zawadi kwa wageni waalikwa mbalimali aliopewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa wakifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Yapi Merkezi akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa kabla ya kuzindua  Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani jana



Serikali imeanza mchakato wa ununuzi wa vichwa 22 vya treni, mabehewa 1,430 ya mizigo na Mabehewa 60 ya Abiria vitakavyotumika kwenye uendeshaji wa Reli ya kisasa ya SGR ambayo ujenzi wake unaendelea.

Yapi Merkez inajenga Reli ya SGR awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam hadi Morogoro ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 56 na awamu ya pili kutoka Morogoro hadi Makutupora Mkoani Singida ikiwa imefikia asilimia 52 zote zikiwa na urefu wa zaidi ya kilomita 722 na zinajengwa kwa gharama ya fedha za ndani shilingi Trilioni 7.2.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati akizindua Safari ya kwanza ya majaribio ya Treni ya Wahandisi kwenye eneo la Soga lililopo Kibaha Mkoani Pwani.

Injinia Kamwelwe alisema mpango wa sasa wa Serikali ni kuwa na Seti tano za Treni za SGR zitakazokuwa na behewa nane za abiria, mpango ambao unalenga kuimarisha sekta ya usafirishaji wa reli.

“Ndugu zangu Watanzania, leo hii tumezindua majaribio ya njia ya reli yetu, hii inamaana kwamba tupo katika mipango ya kuhakikisha reli inakamilika kwa wakati, tumetembea kilomita 20 za majaribiop, reli ni salama kabisa, haina kikwazo,sasa tumeanza mchakato wa kununua vichwa vya treni 22 na mabehewa yake 60 ya Abiria na 1,430 ya Mizigo” alisema Waziri Kamwelwe.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema zoezi la majaribio ya awali ya treni ya wahandisi ni hatua muhimu ya kuhakikisha reli hiyo inapitika bila kikwazo kwani inakagua na kuimarisha miundombinu ya reli hiyo.

Alisema zoezi hilo la awali limekuja kufuatia kukamilika kwa baadhi ya maeneo ya kupita treni kuanzia Soga Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, kuelekea Morogoro na kuongeza kuwa treni rasmi kwa ajili ya kupita reli hiyo itawasili hivi karibuni.

Zoezi la majaribio ya uendeshaji wa Reli ya kihandisi ulishuhudiwa na Waziri Kamwelwe, Maafisa wa Shirika la Reli Tanzania TRC pamoja na Waandishi wa Habari ambao walitembea na treni hiyo kwa kilomita 20. 

NGOMA AFRIKA BAND YENYE MAKAO YAKE NCHINI UJERUMANI

Kikao cha Mheshimiwa Mwakyembe na Kocha wa Taifa Stars Amunike

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison G. Mwakyembe amesema mashindano ya kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2019 yanayoendelea kufanyika nchini Misri, yamebeba uzito wa kipekee kwa nchi ya Tanzania baada ya kukaa nje kwa miaka thelathini na tisa(39) na kufuzu kushiriki katika mashindano hayo ambayo Timu ya Taifa ya Tanzania imetupwa nje katika hatua ya makundi  baada ya kupambana na timu za Senegal, Algeria na Kenya.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari tarehe 6 Julai, 2019 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Raia wa Nigeria Emmanuel Amunike katika hotel ya Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa bado ana imani kubwa na Kocha huyo kuendelea kufanya vizuri ,kinachohitajika ni swala la muda tu, kwani amemueleza mipango mikubwa ya kiufundi aliyonayo kwa Timu ya Taifa hili iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo.
“Ndugu waandishi wa Habari kwanza kabisa niseme tu kwamba, nimefurahi sana kukutana na kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, ambapo lengo la kukutana naye ni kunieleza kilichotokea kule nchini Misri katika mashindano ya Afcon ambayo tumeshiriki baada ya miaka 39 kupita, mashindano haya yamebeba uzito wa kipekee kwa nchi yetu, na niseme tu kwamba nina imani kubwa sana na kocha Amunike kuendelea kufanya vizuri na yetu, nimeongea naye mambo mengi sana kuhusu mashindano, na tumeona kama Wizara tumpe muda zaidi kwa mipango mizuri ya kiufundi aliyonayo kwa Timu ya Taifa hili iweze kufanya vizuri katika mashindano yajayo,”.
“mimi nimefurahi sana kukaa na mwalimu, na yeye pia amefurahi kukaa na Serikali, ili tujuwe mwenzetu maoni yake ni nini kuhusu timu ya Taifa, tufanyaje kujipanga hili kesho, kesho kutwa turejee tena Afcon lakini safari hii tukirejea kila mtu awe na wasiwasi kuwa hii sio timu nzuri kukutana nayo,ametupa mfano mzuri sana, kwamba Uganda mwaka 2015 iliposhiriki mara mwisho haikufanya vizuri hata kidogo, lakini wenzetu wakarudi wakaanza kuyafanyia kazi mapungufu katika mchezo wao, badala ya kukaa mwaka mzima mnalumbana na kunyoosheana vidole, mapungufu kwenye timu ya kiufundi na sisi kwa upande wetu yamejitokeza sana, mengi sitayasema kwa sababu ni mambo ambayo tutakaa na vyombo vinavyohusika, lakini cha msingi tunafurahi sana mwalimu ana moyo chanya kwamba tunaweza, tumeonyesha watanzania kwamba tunaweza, lakini kiufundi inatakiwa na sisi tujiongeze,” alisema Mheshimiwa Mwakyembe.
Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amesema Kocha Amunike amependekeza mazoezi zaidi kwa wachezaji wa Timu ya Taifa pamoja na kucheza mechi za kirafiki kimataifa mara Tatu kwa Mwaka hili kuweza kupata uzoefu zaidi katika mashindano ya kimataifa.
“tatizo lililojitokeza ambalo mwalimu anadhani linaweza kutatuliwa ni mazoezi kwa timu ya Taifa,kwamba angalau mara tatu timu ya Taifa kila mwaka ikawa na mechi za kirafiki, wanaitwa leo wanacheza na Zambia , na Afrika Kusini, tumewakaribisha pengine Spain wanakuja na kuangalia mbuga za wanyama, tunajenga imani ya wachezaji wetu, kwenye mashindano haya yaliyopita tumeona kuna wakati wachezaji wetu walikosa kujiamini, unaona mchezo kadri unavyoendelea ndio sasa hata pasi za uwakika ndio zinapigwa, kwa hiyo ni kujiamini lakini vijana wa Tanzania walicheza vizuri sanaa,” alisema Mwakyembe.    
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison G. Mwakyembe akiongea baada ya mkutano wake na  kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Raia wa Nigeria Emmanuel Amunike katika hotel ya Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam
 Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Raia wa Nigeria Emmanuel Amunike akiongea katika hotel ya Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison G. Mwakyembe akiongea baada ya mkutano wake na  kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Raia wa Nigeria Emmanuel Amunike katika hotel ya Protea Courtyard Jijini Dar es Salaam

WALIMU NA WAZAZI SHULE YA MUYOVOZI WABUNI MIRADI KUJIKWAMUA KIELIMU

0
0
Moureen Rogath, Michuzi TV, Buhigwe. 
 Katika kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi ni unakua ,wazazi na walimu wameweza kubuni mikakati na miradi mbalimbali kwa lengo la wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki. 

 Akizungumza leo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Muyovozi, iliyopo kata ya Biharu wilayani hapa, Alfed Japhet alisema shule zimekuwa na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikijirudia, na kwamba waliazimia kupunguza au kumaliza kabisa. 

 Alisema walianza kwa kufuga mizinga ya nyuki 10 ambayo wakivuna fedha itaweza kuwasaidia katika mahitaji mbalimbali ya shuleni hapo na si kutegemea fedha kutoka serikali kuu. Mwenyekiti wa shule hiyo Mark Matini, alisema walipokea fedha kiasi cha Sh 1.5 milioni kutoka kwa Mpango wa Kuinua Elimu ya Msingi(Equip), kwa awamu ya kwanza na Sh.550,000 kwa awamu ya pili.

 “Fedha hizi zikipatikana zitatusaidia kununua mahitaji muhimu kwa shule na wanafunzi mfano, taulo za kike, kuwaboreshea miundombinu kwani kama wananfunzi atasoma kwa shida hata ufaulu wake utakuwa mbaya,”alisema mwenyekiti wa shule huyo. 

 Alisema serikali kwa kushirikiana na Equip iliweza kuleta mpango wa maendeleo ya kadi ya shule ambayo itamuwezesha mzazi kusoma taarifa mbalimbali na maendeleo ya shule ikiwemo mapato na matumizi hali iliyopunguza malalamiko kwao. 

 "Kabla ya kuwepo kwa kadi ya maendeleo ya shule kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wazazi na walezi lakini baada ya kuweka taarifa zote za shule kwenye ubao huo ushirikiano umekuwa mkubwa.  

Mzazi na mkazi wa eneo hilo Nostord Legero, alisema baada ya shule hiyo kuja na utaratibu wa kadi ya maendeleo ya shule imewasaidia wao kujua taarifa mbalimbali na kwamba wako tayari kutoa ushirikiano kwa uongozi bila kuwa na mashaka. 

 Afisa elimu na mratibu wa Equip wilaya ya Buhigwe Noel Kasaya, alisema shule 88 za wilaya zina kadi ya maendeleo ambayo lenye lengo la kuwapa taarifa za shule wazazi na walezi kupunguza maswali na malalamiko yanayoweza kujitokeza.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Muyovozi, iliyopo kata ya Biharu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma, Alfred Japhet,akionyesha kadi ya maendeleo ya shule iliyochorwa kwa lengo la wazazi na walezi kupata  taarifa za shule na kupunguza malalamiko.
Mradi wa ufugaji wa nyuki katika shule ya msingi Muyovozi ,uliobuniwa na waalimu wa shule hiyo pamoja na wazazi kwa lengo la kujipatia kipato na kutatua changamoto zinazowakabili shuleni hapo ikiwemo ununuzi wa taulo za kike kwa wanafunzi na kuboresha miundombinu kwa msaada wa fedha za Equip ikiwa ni mizinga 40 ya nyuki.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AELEKEA NCHINI UINGEREZA KWA SAFARI MAALUM

0
0

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, akiondoka Zanzibar kuelekea Nchini Uingereza kwa safari Maalum, akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi na Wananchi waliofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, wakati akiondoka kuelekea Nchi Uingereza kwa Safari Maalum.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar, wakati wa kuondoka Nchini leo kuelekea Nchini Uingereza kwa Safari Maalum, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.(Picha na Ikulu) 

WAZIRI KAMWELE AFANYA MAZUNGUMZO NA WAMILIKI WA MELI

0
0

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na wamiliki wa meli Duniani kuhusu namna watakavyofanya kazi nao ili kuongeza ufanisi kwenye bandari ya Dar es Salaam pamoja na kuangalia namna watakavyoweza kuunguza muda wa meli zenye mizigo kukaa bandarini ili kuhudumia meli nyingi wakati wa kikao hicho kilichofanyka katika ukumbi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi akizungumza na wamiliki wa meli Duniani kuhusu uhusiano uliopo kati ya Tanzania pamoja na nchi majirani katika ufanyaji wa biashara pamoja na kutoa historia ya Tanzania  kabla na baada ya ukoloni wakati wa kikao ili kuwahamasiha wamiliki hao kuweza kuleta meli zao kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga akizungumza na wamiliki wa meli pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wamiliki wa Meli wakiwasilisha changamoto kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele wanazozipata pale wanapotumia bandari ya Dar es Salaam wakati wa kikao kilichoandaliwa na Waziri huyo ili kutatua changamoto hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko(katikati) akifuatilia kwa umakini kikao cha wamiliki wa Meli kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kuweza kutatua changamoto wanazozipata katika Bandari ya Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wizara, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) na wamilii wa meli wakiwa kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kusikiliza changamoto wanazozipata wafanyabishara hao pale wanapotumia Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kikao cha wamiliki wa meli pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kilichoandaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele ili kuweza kutatua changamoto ili kuweza kuingeza ufanisi wa bandari hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizunguza na waandishi wa habari kuhusu baadhi ya changamoto wanazozipata wamiliki wa Meli kama vile tatizo la mzigo kukaa kwenye maji unakuwa na gharama kubwa  pamoja na kuondoa urasimu wowote kwenye masuala ya uendeshaji wa Bandari ili kuongezeka kwa meli zitazokuwa zinaleta mizogo kwenye bandari hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa gati nyingine ambayo itaongeza ufanisi wa bandari hiyo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha wamiliki wa meli kilichoandaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko akiwaonesha meli ya kwanza iliyotia naga kwenye gati mpya na kuweza kushusha mbolea wakati wa wamiliki wa meli walipotembelea badari ya Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza na wamiliki wa meli walipotembelea Bandari ya Dar es Salaam ili kujionea ufanisi wa bandari hiyo.

AMANA BENKI KUTATUA CHANGAMOTO YA ADA MASHULENI

0
0
  
Na Khadija Seif, Michuzi TV

BENKI ya lawapatia wanafunzi suluhisho la migogoro ya kutolipa ada kwa wakati mshuleni.

Akizungumza na Michuzi TV  kwenye Maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara viwanjwa vya Mwalimu Nyerere kwenye banda lao meneja mahusiano wa Benki ya Amana amesema wanafunzi  wengi wamekua wakikumbwa na kadhia ya kurudishwa majumbani kutokana na kukosa ada ya kuwawezesha kuendelea na masomo.

"Benki ya  Amana inatoa huduma mpya  kabisa ikiwa ni fursa kupata mkopo utakaomwezesha mzazi kumlipia ada mwanafunzi na kuendelea kulipa kidogokidogo kwa muda wa miezi 12,"

Aidha ametoa wito kwa wazazi ambao wangependa kupata fursa hiyo ya mikopo kufika katika Banda lao ili kuwawezesha wanafunzi kuanzia shule ya awali, sekondari pamoja na vyuo kupata uhakika wa elimu na kuendelea na masomo yao bila kukosa vipindi.

 "Mikopo hiyo haina liba kutokana na kufata utaratibu,sheria na misingi ya dini ya kiislam,"

Pia ameeleza  mbali na kupata fursa hiyo ya mikopo benki hiyo pia inatoa fursa kwa wananchi kujiunga na huduma za kibenki katika msimu hii ya Maonyesho



TANESCO YAMWAGIWA SIFA MAONESHO SABASABA

0
0
NA K-VIS BLOG, SABASABA
WANANCHI wanaofika kwenye banda la Shirika la Umeme nchini (TANESCO), wamesifu hali ya upatikanaji umeme kwa hivi sasa. 
Bw. Majid Omary ni mkazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, aliyefika kwenye banda la TANESCO kwenye viwanja vya Sabasaba kunakofanyika Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo Jumapili Julai 7, 2019 alisema 
“Kwakweli mnastahili pongezi, tulikuwa katika shida kubwa ya kupata umeme wa uhakika kwa muda mrefu, lakini hali kwa sasa imebadilika sana, umeme hausumbui kama ilivyokuwa hapo awali.” Alisema.
Alisema "Eneo ninakotoka Mbagala Kilungule, tulikabiliwa na tatizo la kupata umeme usiokuwa na nguvu ya kutosha kwa muda mrefu, pia ulikatika katika, tulisononeka sana lakini tunashukuru Mungu tatizo hilo sasa halipo, hali ya umeme ni nzuri sana." Alisema Bw. Omary

Kama bado kuna mtu anawalaumu basi ana sababu zake, lakini kwakweli mimi ninawapongeza sana, nimeona nipite tu hapa kuwapa pongezi, alisema Bw. Omary wakati akizungumza na wahudumu wa TANESCO waliokuwa kwenye kitengo cha huduma kwa wateja kwenye banda hilo.
Mwingine aliyepongeza huduma bora za TANESCO ni Bi. Agatha Moses, yeye anatoka Gongolamboto jijini Dar es Salaam, alisema huduma za umeme zimeimarika sana, kwani katika eneo anakoishi hawakumbuki ni lini umeme ulikatika.
“Hata ukikatika inachukua muda mfupi unarejea, sio kama zamani hali ilikuwa tete, umeme ukikatika ndio basi tena.” Alifafanua.
Aidha katika banda la TANESCO wananchi wanaalikwa kutembeela kwenye banda hilo kujipatia huduma mbalimbali kama ambazo zinazotolewa kwenye ofisi za TANESCO.
Leila Muhaji ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO alisema, wananchi wanaotaka fomu za maombi ya awali ya kuombea umeme wanaweza kufika kwenye banda hilo na wataalamu watawapatia fomu bure kabisa.
“Uje tu na picha ya passport size na kitambulisho chako utajaza fomu na itachukuliwa hapa hapa Sabasaba na kupelekwa katika mkoa husika ili maombi yashughulikiwe.” Alifafanua Bi. Leila.
Katika banda la TANESCO wananchi wanaweza kujionea mashine (mfano) ya kufua umeme wa maji, ambayo wataalamu wanaonyesha hatua zote kuanzia ufuaji umeme hadi unapomfikia mteja.
“Pia unaweza kujinunulia umeme, wapo watu wanokuja kwenye maonesho na inatokea umeme umeisha nyumbani basi TANESCO tunatoa huduma hiyo kwenye banda na unaweza mkununua umeme.” Aliongeza Bi. Leila Muhaji.
 Mtaalamu kutoka kampuni tanzu ya TANESCO ya uendelezaji jotoardhi Tanzania, (aliyechuchumaa), akiwapatia maeelzo wananchi hawa wakiwemo wanafunzi jinsi jotoardhi linavyoweza kuzalisha umeme, wakati walipotembelea banda la TANESCO Sabasaba Julai 7, 2019.
 Mtaalamu wa Mita za umeme, Bi. Matilda Cassian (wakwanza kushoto) akimfafanulia mambo mbalimbali yahusuyo huduma ya kupatiwa mita za umeme kwa mwananchi huyu aliyefika banda la TANESCO Julai 7, 2019.
Afisa Huduma kwa wateja TANESCO, Bw. Khairu Rashid, (kushoto) akimsikilzia mteja aliyefika banda la Shirika hilo Julai 7, 2019.
Mhandisi Ajuaye Jeggo (wapili kulia) na Mhandisi Esther Mushi, wote kutoka Idara ya usambazaji umeme, wakimsikiliza kwa makini mteja huyu alyetembelea banda la TANESCO Julai 7, 2019.

JINAMIZI LA NGOMA AFRICA BAND KUSUMBUA VICHWA WASHABIKI ULAYA TENA!

0
0
Jinamizi la muziki wa Ngoma Africa band limeamua kuwaganda na kuwanyima usingizi washabiki wa muziki barani ulaya !

image.jpeg

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens au

"watoto wa mbwa" ni majina ya utani walibatizwa na washabiki wao,
mzimu huo wa muziki Ngoma Africa band inayoongozwa na kiongozi
wake Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja mkuu wa viumbe
wa ajabu ,kikosi hiko kitatingisha maonyesho makubwa ya muziki kule ughaibuni baadhi tu ya maonyesho hayo ni kama yafatanyo na yote yatakuwa siku za jumamosi 
  
03 August 2018 Inter.Afrika Festival Tuebingen,Germany
10 August 2018 Rebstock Park,Frankfurt ,Germany

bendi hiyo inayodumu katika medani kwa miaka 24 sasa ndio bendi pekee ya kiafrika kufanikiwa kudumu kwa muda mrefu na kuwanasa maefu ya wwashabiki kila kona duniani. "Viumbe wa ajabu" Ngoma Africa Band sasa wanatamba na CD yao mpya "Awamu ya Tano Uwanjani" ambayo ipo katika redio mbali mbali hapa nchini.
usikose kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband









WANACHAMA PSSSF WAASWA KUJENGA UTAMADUNI WA KUFUATILIA TAARIFA ZA MICHANGO YAO

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WASTAAFU watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameaswa kujenga utamaduni wa kufuatilia taarifa za michango yao mara kwa mara ili kujipanga vema wakati wa kustaafu unapowadia, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma (CMPR), wa Mfuko huo, Bi. Eunice Chiume amesema.

Bi Chiume ameyasema hayo Julai 7, 2019 wakati akiungana na watumishi wenzake wa Mfuko kuhudumia wanachama wanaofika kupata huduma kwenye banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ambapo watu wengi hususan wale wanaotarajia kustaafu wamekuwa wakijitokeza ili kujua taarifa za michango yao.

Wanachama na wananchi wanahamasishwa kutembela banda hilo ili kupata huduma na taarifa mbalimbali kuhusu shughuli za Mfuko ambao umeundwa baada ya kuunganishwa kwa Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF. 

Huduma zitolewazo na PSSSF kwenye banda hilo namba 13 ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), ni pamoja na taarifa za Uhakiki wa wastaafu, taarifa za Pensheni ya Uzee, taarifa za Mafao ya kukosa Ajira, taarifa za Mafao ya Uzazi, taarifa za Dhamana ya Mikopo ya Nyumba na na taarifa za Uwekezaji. Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28, 2019 yanatarajiwa kufikia kilele Julai 13, 2019 ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda."
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), David Misiime ambaye ni mwanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), akipitia taarifa ya michango yake huku akipata usaidizi kutoka Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, Bi. Eunice Chiume Julai 7, 2019 wakati alipotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Julius Nyerere (Sabasaba) wakati wa maonesho ya 43 ya biashara ya Kimata ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja hivyo.
Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kushoto), akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda la PSSSF Julai 7, 2019.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Fatma Elhady, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, wakiwasilkiliza wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo Julai 7, 2019.
Hakika mama ni mama: Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akimbembeleza kichanga huyu huku mama yake akiwa karibu wakayi Nyangi alipomalzia kumuhudumia mume wa mama huyo aliyetembeela banda la PSSSF.
Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akimsikilzia Mwanachama aliyetembelea banda la Mfuko huo.
Mwnaachama wa PSSSF akimsikliza Afisa wa PSSSF wakati alipofika kwenye banda la Mfuko huo ili kuhudumiwa.
Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Fatma Elhady, akimsikiliza mwanachama huyu aliyetembelea banda la PSSSF Julai 7, 2019.
Afisa Michango PSSSF Bi. Getrude Athanas (kulia), akimsikiliza mwanachama huyu aliyefika na familia yake kupata taarifa za michango yake.
Afisa Mafao PSSSF, Bw. Salvatory Matemu akimsikiliza mwanachama huyu aliyefika kuhudumiwa.

Prof. Palamagamba John Kabudi atembelea maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)

0
0
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa kwanza kutoka kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Tagie Daisy Mwakawago Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Hassan Mnondwa akielezea picha za Mawaziri waliowahi kuiongoza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa wanafunzi waliojitokeza kwenye banda hilo. 


Bw. Joseph Mwasoto akifanunua jambo kwa wateja waliyotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba
Bi. Praxida Gasper akifanunua jambo kwa wateja waliyotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kwenye maonesho ya sabasaba


Huduma zikiendelea kutolewa kwa Wananchi mbalimbali wanaoendelea kutembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya Sabasaba
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Chuo cha Diplomasia kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akitizama Ramani ya Majengo mapya ya Chuo hicho yanayoyengwa sasa hivi, Kurasini jijini Dar Es Salaam 
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akijionea ufanisi wa utengezaji wa bidhaa mbalimbali za Nyumbani zilizotengenezwa na Jeshi la Magereza, alipotembelea banda la Jeshi la Magereza kwenye maonesho ya 43 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.


Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mahojiano na wanahabari kwenye maonesho ya biashara kimataifa maarufa sabasaba yanayofanyika jijini Dar  es Salaam


TRC kufunga Njia za Reli kwa saa 72 ili kukarabati Reli ya Kati

0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO

Shirika la Reli Tanzania TRC limeanza kukarabati njia ya Reli ya kati ya kutoka Dar Es Salaam mpaka Isaka iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga takribani kilomita 970 ili kuimarisha reli hiyo yenye kiwango cha Mitagauge zoezi ambalo lilianza Juni mwaka huu na kutarajia kukamilika mwaka 2020.

Katika Utakabati huo Shirika hilo linatarajia kufunga njia za reli hiyo kwa saa 72 kwa wiki ikiwa ni sawa na siku tatu kwa Wiki kwa muda wa miezi mitano kuanzia Julai hadi Novemba 2019, zoezi zoezi ambalo  kukamilika kwake kutaingiza faida mara dufu ya usafiri huo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Masanja Kadogosa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam na kubainisha kuwa kukamilika kwa Reli hiyo kutaongeza mapato ya usafirishaji wa Reli kwa asilimia mia moja.

“Waandishi wa Habari na Watanzania kwa ujumla, TRC sasa tunakuja kuimarisha miundombinu yenu ya Reli, tunafanya hivi kwa kuwa tunafahamu mnahitaji huduma hizi, tunaomba mtuvumilie kwa siku ambazo tutafunga njia hizi”alisema Kadogosa.

Alisema kwa treni za kawaida za mjini (Cummuter Train) za kutoka Kamata kwenda Ubungo na Pugu zitafanya kazi siku za jumatatu hadi Ijumaa huku Treni za kawaida (Ordinary Train) za kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma, Mwanza na Mpanda zitafanya kazi siku za Jumatatu na Jumatano saa tisa alasiri tu na treni za Deluxe ya kutoka Dar kwenda Kigoma zitakuwepo siku ya Jumanne pekee.

Alibainisha kuwa ukarabati mwingine wa njia ya Reli kutoka Tanga kwenda  Arusha ulianza mapema mwaka huu ambapo njia hiyo itaanza kutumika mwezi Desemba mwaka huu.

“Ndugu zangu wa mikoa ya Kaskazini mtaanza kunufaika na usafiri wa treni ya Abiria kuanzia Desemba mwaka huu, yaani Sikukuu zaKrismas na Mwaka mpya mtaenda nyumbani na Treni ya Abiria ya TRCälisema Kadogosa.

Akizungumzia ujenzi wa Reli ya Standard Gauge inayoendelea kujengwa Nchini Kadogosa alisema kwa awamu ya kwanza kutoka Dar Es Salaam kwenda Morogoro ujenzi huo umefikia asilimia 56.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images