Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WADAU WAHIMIZWA KUWEKEZA KWENYE ELIMU YA MTOTO WA KIKE KUINUA UFAULU WA WASICHANA

$
0
0
Moureen Rogath, Michuzi TV, Buhigwe. 
 Wadau mbalimbali wa elimu nchini wametakiwa kujitokeza kuwekeza kwenye elimu kwa mtoto wa kike kwa lengo la kuinua na kuongeza ufaulu wa wasichana ukilinganisha na ufaulu wa mtoto wa kiume ambao umekuwa mkubwa. 
 Hayo yamebainishwa  na mratibu wa Equip wilaya ya Buhigwe Bi. Noel Kasaya, wakati alipotembelea katika shule ya msingi Nyarugano iliyopo kata ya Kibwiga, kukagua miradi iliyotekelezwa na Mpango wa Kuinua Elimu ya Msingi(Equip).
Bi. Kasaya alisema wanafunzi wa kike wana haki sawa ya kupata elimu bora kama mtoto wa kiume. Alisema wadau wanamchango mkubwa katika kuinua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi ambapo kwa sasa wanafunzi wamekuwa na ufaulu mdogo kuliko watoto wa kiume hasa katika mkoa wa Kigoma. 
 Mwalimu mkuu wa shule ya Nyarugano Bw. Elias Boaz, alisema walipokea fedha kutoka Equip kiasi cha sh 550,000 kwa awamu mbili na kuanzisha mradi wa shamba la kulima ndizi pamoja na kununua sola ya kusomea wanafunzi hasa nyakati za jioni. 
 “Lengo la fedha hizi ni kuiwezesha shule kujitegemea kwa mahitaji yake na si kila kitu kutegemea kutoka serikalini. Hapa shuleni kwetu hatuna umeme tukaamua kununua sola kwa ajili ya kusomea wanafunzi wa maeneo ya karibu na shule nyakati za jioni,” alisema, 
Awali kabla ya kununua sola na kuweka taa kwaajili ya wanafunzi kujisomea hali ya ufaulu ilikuwa kwa asilimia 39 kwa darasa la saba lakini kwasasa baada ya wanafunzi kuanza kujisomea ufaulu umepanda kwa asilimia zaidi ya 55 huku watoto wa kike wakiwa wanashika namba moja. 
Bw.  Sosthenes Katunzi mwalimu wa shule hiyo ambaye alipewa mafunzo ya mbinu za kufundishia na Equip kwa ajili ya kwenda kufundisha waalimu wenzake wa madarasa ya awali pamoja na madarasa ya juu alisema kwamba mafunzo aliyoyapata ni kwa ajili ya mbinu za kufundishia wanafunzi wa madarasa ya awali, na kwa kuwa hawawezi kuchukua waalimu wote  mimi ni mwakilishi wao ambapo nakuja kufundisha waalimu wenzangu,”alisema Katunzi. 
 Mwanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo Leonia Samwel, alisema wamekuwa na klabu ya juu kwaajili ya kufundishwa usawa wa kijinsia, ambapo umeweza kumsaidia kwa kujua haki zake kama mtoto wa kike awapo darasani. 
“Katika klabu yetu nimejifunza usawa wa kijinsia kati yangu na mwanafunzi wa kiume zamani nilikuwa siwezi kumfata na kumuuliza swali lakini kwasasa naweza kukaa naye na kusoma naye bila kuogopa tofauti na awali,”alisema Samweli.
 Waalimu pamoja na wazazi wakiwa katika shamba la shule la migomba ya ndizi ambalo lengo lake ni kusaidia wanafunzi wa shule ya msingi Nyarugano iliyopo kata ya Kibwiga wilayani Buhigwe mkoani hapa,na kujitegemea ambapo walipokea kiasi cha Sh. 550 , 000 Kwa Mpango wa Kuinua Elimu ya Msingi (Equip).
 Sehemu ya shamba la shule la migomba ya ndizi la kusaidia wanafunzi wa shule ya msingi Nyarugano iliyopo kata ya Kibwiga wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Papa Francisko: Watakatifu wapya kutangazwa rasmi 13 Oktoba 2019

$
0
0
Papa Francisko, tarehe Mosi, Julai, 2019 ameongoza Baraza la Makardinali kwa njia ya sala na hatimaye, kuwapigia kura Wenyeheri watano watakaotangazwa kuwa watakatifu, tarehe 13 Oktoba 2019. Watakatifu watarajiwa ni pamoja na: Kardinali John Newman, Giuseppina Vannini; Maria Theresa Chiramel Mankidiyan, Sr. Dulce Lopes Pontes pamoja na Margarita Bays! Mifano bora ya kuigwa!
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, Kanisa ni Takatifu kwa maana Kristo Yesu, Mwana wa Mungu anayetangazwa pamoja na Baba na Roho Mtakatifu kwamba ni peke yake mtakatifu, amelipenda Kanisa kama Bibi arusi wake, akajitoa mwenyewe kwa ajili yake ili alitakatifuze, akaliunganisha naye kama mwili wake, akalijazia kipaji cha Roho Mtakatifu, kwa utukufu wa Mungu! Kumbe, watu wote wa familia ya Mungu wanaitwa kuwa ni watakatifu! Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Kristo Yesu ndiye chemchemi na utimilifu wa utakatifu wote! Waamini wanahimizwa kujivika moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu na wawe na matunda ya Roho Mtakatifu ili wafanywe watakatifu. Kutokana na udhaifu wa binadamu, waamini wanahitaji mara kwa mara kuonjeshwa huruma na upendo wa Mungu katika maisha yao!
Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican wanaendelea kudadavua kuhusu Fumbo la Kanisa kwa kusema, Wakristo wote wanaitwa na kuhamasishwa kushiriki utakatifu mmoja, kwa kumtii na kumwabudu Mwenyezi Mungu katika roho na kweli; kwa kumfuasa Kristo Yesu aliyekuwa ni: mtii, fukara na mnyenyekevu wa moyo, aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu, kwa njia hii, wastahilishwe kushiriki utukufu wa Kristo! Upendo wa dhati ni njia inayoweza kuwapeleka waamini katika utakatifu! Wanapaswa pia kusikiliza, kutafakari na kulimwilisha Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha yao; wajitahidi kushiriki mara kwa mara Sakramenti za Kanisa; kwa kujitia uthabiti katika kusali, kujinyima pamoja na kutekeleza matendo ya huruma: kiroho na kimwili kwa wahitaji zaidi. Hii ndiyo changamoto inayotolewa na Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake kitume “Gaudete et exsultate” yaani “Furahini na kushangilia, wito wa utakatifu katika ulimwengu mamboleo”.
Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe Mosi, Julai, 2019 ameongoza Baraza la Makardinali kwa njia ya sala na hatimaye, kuwapigia kura Wenyeheri watano watakaotangazwa kuwa watakatifu, tarehe 13 Oktoba 2019 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Watakatifu watarajiwa ni pamoja na Kardinali John Newman, muasisi wa Kituo cha Michezo cha Mtakatifu Filippo Neri, nchini Uingereza. Maisha ya Kardinali John Newman yalikuwa ni hija kuelekea ukweli mkamilifu. Alizaliwa kunako mwaka 1801, akawekwa wakfu kuwa Shemasi, Kanisa Anglikani. Baada ya tafakari ya kina na ya muda mrefu, akaongokea kwenye Kanisa Katoliki na Mwaka 1847 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, akateuliwa kuwa Kardinali na Papa Leo XIII na kufariki dunia kunako mwaka 1890.
Hii ni changamoto kwa waamini kuutafuta na kuuambata ukweli unaowaweka huru, ingawa una gharama zake. Ni kiongozi aliyejibidiisha kutangaza na kushuhudia Injili ya huruma na upendo kwa wagonjwa, maskini pamoja na wafungwa gerezani. Maisha na wito wa kila Mkristo ni kuambata utakatifu wa maisha. Sr. Giuseppina Vannini, Muasisi wa Shirika la Mabinti wa Mtakatifu Camillus aliyezaliwa kunako mwaka 1859 mjini Roma, akapata malezi makini kutoka katika familia ya Kikristo. Akiwa na umri wa miaka 32, kunako mwaka 1891 akajiunga na maisha ya kitawa, baada ya safari ndefu ya maisha ya kiroho, mwaka 1892 akaanzisha Shirika na kukubaliwa na Kanisa kunako mwaka 1909, baada ya changamoto nyingi. Tarehe 23 Februari 1911 akafariki dunia na kuacha Shirika lake likiwa na watawa 156. Tarehe 16 Oktoba 1994, akatangazwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa ni Mwenyeheri.
Maria Theresa Chiramel Mankidiyan, Muasisi wa Shirika la Watawa wa Familia Takatifu aliyezaliwa kunako mwaka 1876. Alipata malezi makini kutoka kwa Mama yake na katika ujana wake, akajisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya huduma kwa maskini, wagonjwa pamoja na kutoa hifadhi kwa watu ambao hawa kuwa na makazi maalum. Akajaliwa neema ya kuwa na maono, akapata mang’amuzi ya Madonda Matakatifu mwilini wake, na hatimaye, akabahatika kuanzisha Shirika la Watawa wa Familia takatifu kwa ajili ya huduma kwa wagonjwa waliokuwa kufani pamoja na elimu na majiundo makini kwa wasichana wa kizazi kipya. Akafanikiwa kuliongoza Shirika kwa kipindi cha miaka 12. Akafariki dunia kunako mwaka 1926 na kutangazwa Mwenyeheri na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 2000.
Sr. Dulce Lopes Pontes wa Shirika la Watawa Wamisionari wa Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na Mama wa Mungu, alizaliwa kunako mwaka 1914, akiwa na umri wa miaka 18 alijiunga na Shirika la Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili na Mama wa Mungu. Alivutiwa sana na maisha na wito wa Mtakatifu Theresa wa Mtoto Yesu. Akasaidia sana kuunda umoja wa wafanyakazi wa Mtakatifu Francisko, ili kuwasaidia wafanyakazi waliokuwa wanakabiliwa na matatizo pamoja na changamoto mbali mbali za maisha. Kunako mwaka 1959 akaanzisha Hospitali kama kielelezo cha huduma ya upendo. Akafariki dunia kunako mwaka 1992. Ni mtawa ambaye alikita maisha yake katika sala iliyomwilishwa kwenye huduma ya upendo kwa wagonjwa, kiasi kwamba, upendo wake, ukavunjilia mbali kuta zilizokuwa zinawatenganisha watu! Leo hii amekuwa ni mfano bora wa kuigwa katika uchaji na utakatifu wa maisha!
Margarita Bays, Bikira na mtawa wa Utawa wa tatu wa Mtakatifu Francisko wa Assisi, alizaliwa kunako mwaka 1815. Katika maisha yake alikuwa ni mshonaji, dada wa nyumbani na katekista, akabahatika kupata Madonda Matakatifu mwilini wake. Kwa muujiza, akaponeshwa saratani ya tumbo tarehe 8 Desemba 1854 wakati Papa Pio IX alipokuwa anatangaza kwamba, Mwenyeheri kabisa Bikira Maria, tangu nukta ya kutungwa kwake mimba, kwa neema na upendeleo wa pekee wa Mungu Mwenyezi, kwa kutazamia mastahili ya Kristo Yesu, Mwokozi wa wanadamu wote, alikingiwa na kila doa la dhambi ya asili. Akafariki dunia katika hali ya neema kunako mwaka 1879. Mtakatifu Yohane Paulo II akamtangaza kuwa Mwenyeheri kunako mwaka 1995.
Wenyeheri hawa wanatarajiwa kutangazwa kuwa Watakatifu tarehe 13 Oktoba 2019 wakati wa Maadhimisho ya Sinodi ya Maaskofu Ukanda wa Amazonia yatakayofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 6-27 Oktoba 2019 kwa kuongozwa na kauli mbiu "Amazonia: njia mpya ya Kanisa na kwa ajili ya ekolojia fungamani"Hati ya maandalizi ya Sinodi ya Amazonia inakazia umuhimu wa: kuona, kung'amua na kutenda! Ni Sinodi itakayopembua tema mbali mbali:kuhusu: haki jamii, malezi awali na endelevu, katekesi, liturujia na utambulisho wa Kanisa katika Ukanda wa Amazonia. Watakatifu wapya, wanawekwa mbele ya macho ya watu wa Mungu kama mfano na kielelezo cha kufuatwa katika maisha na utume wa Kanisa.


Jafo kufunga UMISSETA na UMITASHUMTA leo mjini Mtwara

$
0
0
Dar, Geita kuchuana vikali fainali ya soka wavulana UMISSETA  2019                   
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Timu za mikoa ya Dar es salaam na Geita zimetinga hatua ya fainali ya soka wavulana na zinatarajiwa kuchuana vikali katika mchezo  mkali na wa kusisimua wa fainali utakaochezwa tarehe 3 julai, 2019 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mchezo huo ambao utashuhudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaoongozwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo utahitimishwa na sherehe za kufunga mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kwa mwaka 2019 katika uwanja wa Nangwanda.
Kabla ya kufanyika kwa mchezo wa fainali, kutachezwa mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ambapo aliyekuwa bingwa mtetezi Tanga atapambana na timu ngumu ya Mwanza katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Katika michezo iliyochezwa jana, timu ya soka ya mkoa wa Dar es salaam ilifanikiwa kuingia fainali baada ya kuichapa timu ya mkoa wa Mwanza, na bingwa mtetezi Tanga alicheza na Geita katika hatua ya nusu fainali ambapo timu za Dar es salaam na Geita zilifanikiwa kusonga mbele baada ya Dar es salaam kushinda kwa 1-0, huku Geita ikiifunga Tanga kwa mikwaju ya penati  6-5 baada ya kutoka sare 1-1.
Kwa upande wa soka wasichana bingwa ni timu ya kagera amemfunga Mara magoli 3-0, mshindi wa tatu ni  Kilimanjaro baada ya kumfunga mwanza 2-1, 
Kwa upande wa soka maalum bingwa ni  Shinyanga ambaye alimfunga Ruvuma kwa magoli  3-1, huku nafasi ya mshindi wa tatu  ilichukuliwa na Mtwara baada ya kuilaza Dodoma 2-1,
Katika mchezo wa netboli bingwa wa UMISSETA 2019 ni Mwanza ambaye alimfunga Tabora, huku nafasi ya mshindi wa tatu ilichukuliwa na Tanga.
Katika fainali za mpira wa mikono zilizochezwa leo bingwa ni timu za soka za wavulana na wasichana za mkoa wa Mara baada ya kufanikiwa kuzichapa timu za wavulana na wasichana kutoka mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wa mpira wa wavu (volleyball) bingwa ni timu ya mkoa wa Mbeya kwa wavulana ambayo iliifunga timu ya mkoa wa Mtwara, na wasichana bingwa ni Mtwara baada ya kuifunga Katavi.
Wakati huo huo tukio la ugawaji medali kwa washindi mbalimbali lilifanyika leo ambao washindi mbalimbali wa riadha mbio za mita 100, 200, 400, 800 na 1500 walipewa medali zao ambapo katika tukio hilo mikoa ya Mwanza na Mara ilitia fora kwa kujizolea medali nyingi.
Tukio la ugawaji medali pia lilishuhudiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga akimpongeza baada ya kumvalisha medali ya dhahabu mmoja wa wakimbiaji wa mbio za kupokezana vijiti kutoka mkoa wa Tabora ambao walishika nafasi ya kwanza kwenye hafla ya kutoa medali kwa washindi zilizofanyika jana katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
 Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Newaho Mkisi akimpongeza mmoja wa washindi wa medali mara baada ya kumvisha medali kwenye hafla iliyofanyika jana katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Julius Nestory akitoa medali kwa washindi kwenye hafla iliyofanyika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara jana
 Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Dkt. Jilly Maleko akitoa tuzo ya medali kwa mmoja wa washindi wa mbio za mita 800 jana katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara

VOA SWAHILI: Duniani leo July 3, 2019

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

PSSSF NA NSSF WAWASOGEZEA HUDUMA WANACHAMA WA MIFUKO HIYO KATIKA JENGO NAMBA 13 VIWANJA VYA MAONESHO SABASABA 2019

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wamewasogezea karibu huduma Wanachama wa Mifuko hiyo katika msimu huu wa Maonesho ya 43 ya Bishara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Wakizungumza leo Julai 2, 2019 kwa nyakati tofauti Wakurugenzi Wakuu wa Mifuko hiyo, Bw. Hoseah E. Kashimba (PSSSF) na Bw. William Erio (NSSF) wamesema kuwa wameamua kufanya maonesho hayo kwa kushrikiana ili kuwarahisishia Wanachama kupata huduma wanazohitaji wote wakiwa kwenye banda  namba 13 lililo mkabala na jingo la matangazo ndani ya viwanja vya Sabasaba.
“Tukiwa katika banda hili kwa kushirikiana na wenzetu wa NSSF ambao wao wanashughulika na wafanyakazi kutoka Sekta Binafsi na sisi PSSSF tunahudumia wafanyakazi kutoka Sekta ya Umma.”
 Tumeona tufanye maonesho haya pamoja kwa sababu ya kutoa elimu kwa wanachama kwa urahisi zaidi hasa kwa vile hatuko katika ushindani kama ilivyokuwa hapo awali, hii itasaidia kama Mwanachama anataka kujua taarifa kuhusu Mafao yake kama anatoka Sekta binafsi ataelekezwa aende NSSF na kama anatoka Sekta ya Umma ataelekezwa aende PSSSF, amefafanua Bw. Kashimba.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Bw. William Erio alisema “Baada ya kuunganishwa Mifuko hapo mwaka jana bado watu hawajaelewa vema tofauti zilizopo kwa hiyo wanakuja hapa kama banda pekee linalotoa huduma ya Hifadhi ya Jamii na wakifika basi wanaelekezwa katika sehemu husika na kupata huduma wanayohitaji.” Alisisitiza Bw. Erio.

Alisema ni sehemu ambayo watu wanaweza kuja na kujibiwa maswali yote waliyonayo na kutatuliwa kero zao.
Maonesho hayo ya kila mwaka yamefunhguliwa rasmi leo Julai 2, 2019 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa kufikia kilele Jlai 13, 2019.
 Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hoseah E. Kashimba (wapili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. William Erio (wapili kushoto) wakiwa na Mameneja Kiongozi Uhusiano na Elimu Kwa Umma, Bi. Eunice Chiume (kushoto) ambaye yuko PSSSF na Bi. Lulu Mengele (kulia) ambaye yuko NSSF.
Bw. Erio (kushoto) na Bw. Kashimba wakibadilishana mawazo ndani ya banda hilo.

 Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hoseah E. Kashimba, (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo na ule wa NSSF.

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa PSSSF na NSSF katika banda namba 13 viwanja vya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

TAMIDA WALAANI VITENDO VYA UTOROSHWAJI MADINI VINAVYOFANYWA NA BAADHI YA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
CHAMA cha wafanyabiashara wa Madini Taifa (TAMIDA) kimelaani hatua ya vitendo vya utoroshwaji wa madini vinavyofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasiowaaminifu jambo ambalo  wameeleza ni uhujumu wa rasilimali za nchi na kuitaka serikali iwasake na kuwachukulia hatua kali ili kukomkesha matukio hayo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia tukio la hivi karibuni kukamatwa kwa madini mbalimbali yakiwemo Tanzanite yenye uzito wa  kilogram zaidi 31 yaliyokuwa yakitoroshwa na wafanyabiashara kupitia  mpaka wa Namanga ,kuelekea nchi jirani ya Kenya yakiwa yamefungwa kwenye viroba vya mchele.

Aidha Tamida imeishukuru Serikali kwa kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya kuhamasisha wachimbaji kuuza madini yao katika masoko rasimi kwa kuwaondolea baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa na urasimu kwa wafanyabiashara wa madini nchini.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa, Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiasha wa madini Taifa, Sammy Mollel (pichani)amesema kuwa Kuondolewa kwa tozo ya kodi ya zuio kwa asilimia 5 na kodi ya ongezeko la thamani  asilimia 18 na tozo hiyo kutozwa asilimia 0 ni kuhamasisha biashara kufanyika katika mazingira rahisi.
Amesema kuwa Tamida na wachimbaji wa madini nchini wanalaani kwa nguvu zao zote na watatoa ushirikiano kwa serikali kwa wale wote wenye nia ya kutorosha rasilimali za madini kwa njia za magendo nje ya nchi wakati serikali imefanya mambo makubwa chini ya Rais  Dkt.John Magufuli.
Ameeleza lengo la serikali ni kuondoa urasimu na kuhamasisha biashara ifanyike katika masoko rasimi na hivyo kuondoa ubaguzi na kudhibiti utoroshwaji wa rasilimali ya madini ili sekta hiyo iweze kutoa mchango wake katika pato la taifa na kukuza uchumi sisi tamida tunaunga mkono na kulaani utoroshwaji na hatua zichkuliwe kwa kuwasaka na kuwatia nguvuni.
“Hivyo basi tunaiomba serikali yetu ihakikishe inawasaka na kuwatia nguvuni wote waliohusika katika jaribio la utoroshaji wa madini  hayo ili sheria ifuate mkondo wake na adhabu kali itolewe kwani wanaharibu taswira ya wafanyabiashara waaminifu”
Amesema wao kama Tamida watasimama na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli kuona watanzania wananufaika na rasilimali za madini kwa kulipa mapato na kuzalisha kwa uwazi na utaratibu kwa sisi wafanyabiashara kufanya biashara kuwa wa wazi.
Akawataka wafanyabiashara kufuata utaratibu kwa kuongeza thamani ya madini na kuitaka serikali kuleta teknolojia ya kusanifu madini yetu ili wafanyabiashra waendelee kufanya biashara zao kwa uwazi kwani imeondoa urasimu mkubwa hivyo tunaishukuru serikali yetu kwa kutuandalia mazingira mazuri chini ya waziri Biteko.

GAVANA SHILATU ASISITIZA MIRADI IKAMILISHWE KWA WAKATI NA KWA UBORA

$
0
0

Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe *Emmanuel Shilatu* amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya umaliziwaji wa maboma kwa shule za msingi ambazo Serikali imetoa fedha kwa ajili ya ukamilishwaji wake yaliyopo kata za Miuta, Mkoreha na Michenjele. 

Kwenye ziara hiyo Gavana Shilatu ametoa maelekezo kwa kamati za ujenzi ya miradi hiyo wahakikishe inamalizwa kwa wakati na kwa ubora tayari kutumiwa na Wanafunzi. 

*”Nawapongeza Wanakijiji kuanzisha miradi hii na tunamshukuru Rais Magufuli kutoa fedha za kumalizia maboma haya. Nawapa maagizo uongozi wa shule na kamati ya ujenzi muhakikishe ndani ya wiki mbili kuanzia sasa miradi hii inamalizwa kwa wakati na ubora unaolingana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali. Nami mara kwa mara nitakuwa napita pita kukagua maendeleo ya ujenzi.”* Alisisitiza Gavana Shilatu. 

Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Dkt John Magufuli* kupitia mradi wa lipa kulingana na matokeo imetoa fedha Tsh. Milioni 42.5 kukamilisha maboma ya madarasa 3 na uwekaji wa Madawati yake kwa shule za Msingi Ngongolo, Shule ya Msingi Misufini na Shule ya Msingi Mmalala yaliyopo Tarafa ya Mihambwe.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU ATEMBELEA BANDA LA WAKALA WA VIPIMO MAONESHO YA SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akiangalia vipimo vinavyotumiwa na Wakala wa Vipimo alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akioneshwa kigezi (standard) kinachotumia kupimia mizani ya madini na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akipata maelezo juu ya majukumu ya WMA kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu,akioneshwa vifaa vya kitaalam vinavyotumiwa na WMA katika kutimiza majukumu yake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa vipimo Dr.Ludovick Manege alipotembelea banda la wakala wa vipimo wizara ya viwanda na biashara katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

……………….
Jumuiya ya wafanyabiashara watakiwa kutoendelea kutegemea kuuza nje bidhaa ghafi bali watumie viwanda vya nyumbani na bidhaa hizo ziongezwe thamani kwa kusindikwa na kufungashwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.
Ameyasema hay oleo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu katika sherehe za ufunguzi wa Maonesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari katika sherehe hizo Mh. Samia amesema kuwa jumuiya ya wafanyabiashara ina jukumu la kuwandaa wanachama wake kuwa na ufahamu wa kutosha, kuwa na uthubutu na kutayarisha miradi na kuwa tayari kupambana katika medani ya biashara.
“Ili Tanzania iweze kukidhi mahitaji ya fursa za masoko ya biashara zao, tunahitaji kufanya kazi kwa bidii kwa kuzalisha bidhaa zenye ushindani”. Amesema Mh. Samia.
Aidha, Mh. Samia amesema kuwa ili ujenzi wa Uchumi wa Viwanda ushike kasi ya kutosha, hakuna budi kwa sekta kama kama vile kilimo, mifugo,Uvuvi na madini kutoa malighafi za kutosheleza viwanda hivyo.


“Wakati tunahimiza ujenzi wa Uchumi wa Viwanda msukumo tunauweka pia kwenye sekta zinazozalisha malighafi.Sekta ya kilimo ikijipanga vema, viwanda vitapata malighafi hivyo hivyo kwa sekta ya mifugo, uvuvi, madini na sekta nyingine”. Ameongeza Mh. Samia.

Mawaziri Bara, Zanzibar Wasaini Makubaliano ya Ushirikiano

$
0
0



Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe(Katikati) akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za
Utalii,Habari,Utamaduni,Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma. Kushoto ni Mhe.Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale na kulia ni Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Ally Abeid Karume na Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo (Kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) wakisaini Taarifa ya Ushirikiano baina ya Serikali ya
Tanzania Bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Sekta wanazosimamia leo Julai 02,2019 Jijini Dodoma.Wanaoshuhudia ni Viongozi waandamizi wa wa Jamhuri ya Muungano katika Sekta hizo. 
3.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nicholas William akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Tanzania bara na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wanaosimamia Sekta za Habari, Utalii Utamaduni,Sanaa, Michezo na Mambo ya Kale kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika sekta hizo kilichofanyika Julai 02,2019 Jijini Dodoma. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe
(kushoto) akizungumza na Wanafunzi na wanamichezo wa shule ya Foutain Gate Academy iliyopo Jijini Dodoma ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kukuza vipaji mbalimbali vya michezo wakati akiwatambulisha Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Ally,Abeid Karume (kulia) na Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo (wa pili kulia) kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar walipoitembelea shule hiyo leo Julai 02,2019. 
Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Mahmoud Thabit Kombo kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akifurahia zawadi ya sabuni aliyopewa na Uongozi wa wa Shule ya Foutain Gate Academy mara baada ya kuitembelea shule hiyo iliyopo Jijini Dodoma leo Julai 02,2019. (PICHA NA SHAMIMU NYAKI- WHUSM). 


Na Lorietha Laurence-WHUSM 


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza sekta za Habari, Utamaduni,Sanaa na michezo ili kuongeza tija. 

Uwekaji wa saini za ushirikiano huo umefanyika leo Jijini Dodoma katika ukumbi wa chuo cha Ufundi Veta, baada ya vikao vya ngazi za wataalam na Makatibu Wakuu wa Wizara husika kuwasilisha taarifa hizo kwa Mawaziri na hatimaye kuridhia tayari kwa ajili ya utekelezaji. 

“Hatua hii ni nzuri na muhimu kwetu katika kuhakikisha tunadumisha na kuhifadhi muungano wa kihistoria ambao ulioasisiwa na waasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere na Shehe Amani Abed Karume” Alisisitiza Dkt. Mwakyembe. Aidha, Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo ameeleza kuwa katika sekta ya habari ni muhimu kwa Shirika la UtangazajiTanzania (TBC) kushirikiana na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) ili kuandaa vipindi mbalimbali ikiwemo kipindi cha utalii Safari chaneli. 

“Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya utalii nchini , vyombo hivi vya habari TBC na ZBC vinapaswa kushirikiana kuandaa vipindi vya utalii ili kuitangaza sekta hii nje na ndani ya nchi” Alisisitiza Mhe. Mahmoud Thabit Kombo . Kwa upande wake Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid Karume amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inatangazwa na kuenezwa kuna umuhimu wa kuandaa kanzi data itakayojumuisha wataalam wa Kiswahili ambao watakuwa wakifundisha wageni ndani na nje ya nchi. 

“Tanzania imechangia sana katika kukuza lugha ya Kiswahili na watu wengi
wanapenda kuja kujifunza kwetu ,hivyo naamini kwa kuwa na kanzi data hii
itasaidia sana katika kuwapata watalaam wazuri wa kufundisha lugha hii”. Balozi Ally Abeid Karume. 

Vilevile Mawaziri hao wamekubaliana kuimarisha ushirikano katika sekya ya sanaa kwa kuhakikisha kuwa ifikapo desemba 2019 wanakuwa wamesha andaa kanuni zitakazowawezesha watayarisha wa filamu kutoka nje ya nchi ili kuruhusu utumiaji wa maudhui hayo kwa vyombo vya habari vya serikali.

WACHIMABJI WADOGO WA DHAHABU KUPUNGUZA UTUMIAJI WA ZEBAKI KWA 30% IFIKAPO 2024

$
0
0
Tanzania yadhamiria kupunguza matumizi ya Zabaki kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwa asilimia 30% ifikapo 2024. 

Katika kikao cha kupitisha Mpango Kazi wa Taifa wa kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo kilichoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na kushirikisha sekta husika, leo katika Chuo cha Biashara (CBE) jijini Dodoma, Ikiwa sehemu ya Maandalizi ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Minamata ambao Tanzania ipo kwenye mchakato wa kuridhia. 

Zebaki imetajwa kuwa moja kati ya kemikali kumi hatarishi zilizo orodheshwa na Shirika la Afya Duniani na ina madhara makubwa haswa kwenye magonjwa ya mfumo wa fahamu. 

Tanzania inakadiriwa kuwa na wachimbaji wadogo milioni 1.2, asilimia 20-30 ni wachimbaji wanawake ambapo sehemu kubwa ya wachimbaji hawa hutumia zebaki huku kukiwa na makisio ya mwaka ambapo tani 13 mpaka 24 hutumika na huingizwa nchini kinyemela. 

Zaidi ya 25-33% ya wachimbaji wadogo wadogo wameathirika na matumizi ya zebaki,hivyo Serikali imedhamiria kupunguza ama kuondosha matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo. 

Wakizungumza mara baada ya kumaliza kikao hicho Bi. Noela R. Magoche ambaye ni mdau wa Madini alisema kuwa zifikiriwe mbinu mbadala kunusuru watoto wanaofanya kazi migodini kwani ndio waathirika wakubwa wa zebaki huku akisisitiza sheria inayokataza ajira kwa watoto 

Kwa upande wake mdau wa Mazingira Bw. Haji Rehani amesema zebaki imetambulika kimataifa kwa madhara makubwa ya kiafya.
Wadau walioshiriki Kikao cha Kupitisha Mpango Kazi wa Taifa wa Kupunguza matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo jijini Dodoma leo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
………………. 

LEMA AWATAKA WAKAZI WA JIJI LA ARUSHA KUTOKUWA NA HOFU

$
0
0
Na,Jusline Marco -Arusha

Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema amewataka wakazi wa jiji la Arusha kutokuwa na hofu katikati mwao kwani hofu lazima ishindwe kwa vitendo.

Lema aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko kuu  jijini Arusha ambapo alisema hofu imepandikizwa katika nchi na kuwafanya watu kuwa waoga na wengi wao kukata tamaa  ya kupiga kura katika uchaguzi ujao.

Kufuatia hali hiyo aliwaondoa hofu wananchi wake na kuwataka wafahamu kuwa hao wanaowatisha na kuwafanya waogope kushiriki zoezi la upigaji kura mwaka ujao wanaweza wasiwakute kwasababu mungu ana nguvu kuliko wao.

Alisema shauku yake ya kupigania haki inazidi maumivu ya mauti hivyo amewataka wananchi hao kuendelea kuimarika katika umoja wao na kuimarisha imani zao pindi wasikiapo maneno ya kuwatia hofu katika mapambano ya kudai haki.

"Safari ya wana wa israel kufika kanani haikuwa rahisi lakini walifika,tunamjua mungu tunaye muamini".Alisema Mbunge Lema

Aliongeza  kuwa madiwani wengi wa chama cha demokrasia na maendeleo wamenunuliwa kwasababu ya hofu iliyotanda mioyoni mwao."Kuliko nijiunge na chama cha mapinduzi nitaenda kuwa Mwalimu wa madrasa au Sunday school hiyo pia ni kazi ya utume"Alisema Lema

Naye katibu wa Wilaya wa chama hicho Innocent Kisanyage alisema kuwa nchi ya Tanzania inaongozwa kwa mujibu wa katiba,taratibu na kanuni ambapo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 kifungu cha (D)kikielezea ni haki ya Kila mmoja  kupataji wa taarifa za matukio mbalimbali yahusuyo jamii wakati wote.

Sambamba na hayo amewakata wananchi walio na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uandikishwaji katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Julai 18 hadi 24 mwaka huu ambapo ametoa wito kwa wananchi wote wa jiji la Arusha walio katika kata zote 25 na vituo 185 kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo litakalowawezesha kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2020.
 Mbunge Lema akiweka msisitizo kwa wakazi wa Arusha akiwataka kutumia akili kwenye kuchuja mambo na kuondoa hofu katika utafutaji wa haki
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na wakazi wa jijini Arusha kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika  viwanja vya soko kuu.

BILIONI 114.1 KUWAPA NEEMA YA MAJISAFI WAKAZI WA DAR NA PWANI

$
0
0
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya utiaji saini wa DAWASA na wakandarasi juu ya ujenzi na uendeshaji wa miradi sita mikubwa ya usambazaji wa maji yenye thamani ya Bilion 114.5 iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi TV. 
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Prof Mbarawa. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwasilisha taarifa fupi ya miradi sita mikubwa yenye thamani ya Bilion 114.5 kwa Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa wakati wa halfa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Miradi hiyo itahudumia maeneo ambayo hayana kabisa mtandao wa DAWASA pamoja na Mkoa wa Pwani. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akibadilishana mkataba wa utekelezaji wa miradi ya majisafi toka kwa wawakilishi wa makampuni ya ukandarasi ya Watanzania na Wachina yatakayotekeleza ujenzi wa miradi itakayojengwa Dar es Salaam na Pwani. Wengine wanaoshuhudia ni Mawaziri, Naibu Waziri, Mwakilishi wa benki ya Dunia na viongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi TV. 
Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA waliohudhuria hafla hiyo. Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo akitoa machache. Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akifafanua jambo. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akielezea furaha yake juu ya DAWASA kupeleka wa maji katika jimbo lake la Mkuranga na vitongoji vyake kupitia miradi hiyo. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi DAWASA Jenarali Mstaafu Davis Mwamunyange akielezea chagamoto zinazoikabili mamlaka hiyo.

Wageni waalikwa na wafanyakazi wa DAWASA waliohudhuria hafla hiyo. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Assumpta Mshama ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha akitoa salamu. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sophia Mjema ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ilala akitoa salamu. 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba akielezea furaha yake jinsi DAWASA inavyotekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi kumtua mama ndoo kichwani. Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jaffo (kushoto) akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia). 

Na Zainab Nyamka na Cathbert Kajuna, Michuzi TV. 

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wametia saini mikataba wa miradi mikubwa sita ya usambazaji maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wenye thamani ya Bilion 114.5. Utiaji huo wa saini umefanyika leo Julai 2, 2019 katika ofisi za Mamlaka hiyo huku ukishuhudiwa na Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso, Waziri wa TAMISEMI Selemani Jaffo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Bodi ya DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na Wakuu wa Wilaya kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. 

Kabla ya utiaji saini, Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa amewataka Mamlaka hiyo kusimamia vizuri miradi yote na kutafuta wakandarasi watakaofanya kazi kwa uweledi na kumaliza kwa wakati na muda mfupi ili wananchi wapate majisafi na salama. "Mamlaka mnaposimamia vizuri miradi ya maji, na kupata mkandarasi atakayefanya kazi kwa weledi na kumaliza ujenzi wa mradi kwa muda mfupi basi wananchi watapata majisafi na salama," amesema Prof. Mbarawa. 

Profesa Mbarawa amesema, li kufikia lengo la serikali la kumtua mama ndoo kichwani kwa asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 kwa vijijini na hilo linawezekana iwapo miradi midogo na mikubwa kusimamiwa vizuri na wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati. Akitoa taarifa fupi ya miradi hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kwa sasa mkoa wa Dar es Salaam unapata maji kwa asilimia 85 na kukamilika kwa miradi hiyo mikubwa itafikia malengo ya serikali ya asilimia 95 kufikia mwaka 2020. 

Amesema, katika kutekeleza miradi hiyo fedha zinazotumika ni za ndani zinazotokana na makusanyo ya mapato ya kila mwezi ambapo ndani ya miaka nne wameweza kuongeza ukusanyaji kutoka bilioni 3.2 hadi 11.2 kwa mwezi na asilimia 35 za mapato zinatumika kwenye ujenzi wa miradi ya maji. Nae Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenarali Mstaafu Davis Mwamunyange ameeleza changamoto mbalimbali ndani ya mamlaka hiyo ila ameahidi kushirikiana na menejimenti kukabiliana nazo ikiwemo upotevu wa maji na wateja kupewa ankara za maji tofauti na matumizi yao. 

Miradi iliyowekewa saini ni mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Jeti hadi Buza wenye wenye urefu wa Km 7.5 na litahudumia maeneo ya Kiwalani Vituka, Buza, Mashine namba 5 - Tandika na Mwanagati na wakazi 173,810 wa kata za Vituka na Buza watapata huduma ya maji kwenye awamu ya kwanza. 

Mradi mwingine ni mradi wa usambazaji maji utakaoanzia matanki ya Chuo Kikuu mpaka Bagamoyo awamu ya pili, mradi wa kuchimba visima 20 vya Kimbiji Mpera, mradi wa usambazaji maji Kisarawe hadi Pugu, mradi wa maji katika mji wa Mkuranga na mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Mlandizi (Ruvu juu) hadi Kijiji cha Mboga Chalinze. Viongozi mbalimbali hususani wawakilishi wa wananchi wameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwezesha miradi mikubwa kama hiyo kwenda katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Serikali kushirikiana na TMRC katika ukopeshaji wa mikopo katika sekta ya nyumba.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Serikali imesema kuwa litaendelea kushirikiana na Kampuni ya mikopo ya nyumba (TMRC) ambayo imeorodheshwa katika awamu ya pili katika hatifungani ya soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khatib Kazungu katika hafla ya TMRC kuorodhoshwa hatifungani ya soko hilo iliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa ni asilimia moja ya mikopo ya nyumba ikilinganishwa na nyingine hivyo wadau lazima waongeze jitihada ya kutoka hiyo asilimia moja na kuongeza zaidi ili wananchi kupata mikopo nyumba zenye riba nafuu.Amesema mpango wa ukopeshaji wa nyumba ulikuwa ukifanywa na Benki ya nyumba ambayo ilifisika na serikali kukopa katika benki ya Dunia na kuikopesha TMRC dola za kimarekani milioni 70.

"Serikali itaendelea kushirikiana wadau wote katika kukuza sekta ya nyumba nchi ikizingatiwa umuhimu wa umiliki wa nyumba" amesema Kazungu.Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Dhamana na Mitaji (CMSA) Nicodemus Mkama amesema mauzo ya toleo la kwanza yalikamilika Juni 8 mwaka jana ambapo TMRC ilifanikiwa kukusanya billion 12 ikiwa ni asilimia 4.3 ambayo ni zaidi ya lengo lililokuwa limetarajiwa.

Amesema toleo la pili ya TMRC yamekuwa na mafanikio kwa sh.bilioni bilioni 9.2 ikilinganishwa na sh.bilioni nane zilizotarajiwa kukusanywa.

"Ongezeko hili linaonesha imani walionayo wawekezaji kwa Kampuni ya TMRC na CMSA na fedha zilizopatikana katika mauzo ya toleo la pili zitatumika kugharamia shughuli za maendeleo pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa benki zinazotoa mikopo ya nyumba"amesema Mkama.

Ametoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na Taasisi za Fedha yatumie njia ya Masoko ya Mitaji ili kuongeza Ukwasi na uhakika zaidi.Kwa ipande wa Mwnyekiti wa Bodi ya TMRC Theobald Sabi amesema kuwa kwa imeshatoa mikopo kwenye benki 15 yenye thamani ya sh.bilioni 122.

TMRC iko katika mazungumzo na Taasisi za Kimataifa kwa ajili ya kupata mikopo nafuu ili mraji apate mikopo nafuu na riba.
 Mwenyikiti wa Bodi ya TMRC Theobald Sabi akitoa maelezo namna TMRC ilipopata mafanikio katika ukopeshaji wa mikopo ya nyumba katika Taasisi za Fedha na kuingia katika hatifungani ya kuorodhoshwa katika Soko la Hisa Dar es salaam awamu ya pili katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watendaji wakishuhudia kuorodhoshwa kwa TMRC  hatifungani awamu ya pili katika Soko la Hisa Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khatib Kazungu akifungua Mnada katika Soko la His Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khatib Kazungu akizungumza wakati wa kuorodhoshwa kwa hatifungani ya kwa Kampuni ya mikopo ya nyumba TMRC katika Soko la Hisa Dar es Salaam awamu ya Pili hafla iliofanyika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Dhamana na Mitaji (CMSA)   Nicodemus Mkama akitoa maelezo namna soko linavyopanda kwa Kampuni katika kuorodhoshwa kwa Hatifungani katika Soko la Hisa Dar es salaam  katika hafla ya TMRC kuorodhoshwa hatifungani awamu ya Pili katika Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 3,2019


Mantrac yawazawadia wateja wake kwa mafunzo maalumu

$
0
0
Kampuni ya Mantrac, ambayo ina idhini ya kuingiza nchini mashine za uchimbaji maarufu kama caterpillar, imewazawadia wateja wake kwa namna ya kipekee kwa kutoa mafunzo kwa wateja wake ili waweze kuelewa namna ya kuendesha mashine zao mpya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Mauzo wa Mantrac Tanzania, Butwa Sanga, alisema mafunzo hayo ya siku tatu yaliyojulikana kama ‘The Operator Challenge’, yaliandaliwa mahususi kwa waendeshaji hao ili kuwaongezea ujuzi hasa wanapotumia mashine mpya zinazojulikana kama New Generation Hydraulic Excavator (NGH).
Alisema mashine hiyo mpya ya NGH inalenga kuongeza ufanisi wa hali ya juu, kupunguza gharama na kupunguza muda wa kufanya kazi na hivi kuongeza uzalishaji.
“Makatapila haya mapya ya NHG yanapunguza muda wa kazi kwa nusu na wakati huo huo kupunguza matumizi ya mafuta kwa kati ya asilimia 25 na kuongeza ufanisi kwa hadi asilimia 45,” alisema.
Alisema mafunzo hayo ya siku tatu yalidhaminiwa na Mantrac Tanzania na kuendeshwa na mtaalamu wa mafunzo Ehab Abdelfatah Mohamed kutoka Misri.
“Tunataka waendeshaji hawa wapate ujuzi zaidi kuhusu makatapila haya mapya kwani yana teknolojia ya juu zaidi ukilinganisha na mengine ya nyuma,” alisema na kuongeza kuwa uzinduzi rasmi wa katapila hiyo mpya ya NHG utafanyika Julai 17 mwaka huu Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo pia yalienda pamoja na zoezi maalumu lijulikanalo kama ‘The Operator Challenge’ ambapo waliofanya vizuri zaidi walipokea zawadi na vyeti.
Mmoja wa wahudhuriaji wa mafunzo hayo, Samuel Leonard, ambaye alipokea moja ya tuzo za juu  alisema mafunzo hayo yalikuwa muhimu katika kuhakikisha wanaweza kuendesha mashine hizo mpya bila matatizo.
“Tunajifunza kila siku na hasa ukizingatia makatapila haya mapya yana teknolojia ya juu sana, mafunzo haya ni muhimu sana kwetu,” alisema.

 Mkufunzi kutoka Kampuni ya Mantrac, Ehab Abdelfatah Mohamed, (mwenye miwani) akitoa maelezo kwa baadhi ya waendeshaji kutoka makampuni tofauti  kuhusu mashine mpya za uchimbaji aina ya Caterpillar,  zinazosambazwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Waendeshaji hao wanahudhuria mafunzo ya siku tatu yaiyoandaliwa na kampuni ya Mantrac Tanzania. 
Mmoja wa washindi wa shindano lililoandaliwa na Mantrac Tanzania lijulikanalo kama ‘The Operator Challenge’ ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya siku tatu kwa waendeshaji wa makatapila, Samwel Leonard (kushoto) akipokea zawadi yake kutoka kwa Mkufunzi kutoka Kampuni ya Mantrac, Ehab Abdelfatah Mohamed.

Vodacom, Robotech waendesha maonesho kuinua teknolojia kwa vijana

$
0
0

  Mkurugenzi Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia, akizungumza na wanafunzi waliohudhuria maonyesho ya Techfest yaliyoandaliwa na kampuni ya Robotech kwa ajili ya kuinua vijana kwenye fani ya technolojia, jijini Dar es Salaam, wikiendi hii . Kampuni ya vodacom Kupitia mpango wake wa instant schools inaendelea kuinua na kuhimiza vijana kujiingiza katika fani ya teknolojia ili kutanua uelewa wao na kupanua fursa zao kupata ajira kwenye masoko ya dunia.
 Mkurugenzi Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia akitazama bunifu mbali mbali zilizofanywa na wanafunzi katika maonyesho ya Techfest yaliyoandaliwa na kampuni ya Robotech kwa ajili ya kuinua vijana kwenye fani ya teknolojia, jijini Dar es Salaam, wikiendi hii. Kampuni ya vodacom Kupitia mpango wake wa Instant schools inaendelea kuinua na kuhimiza vijana kujiingiza katika fani ya technologia ili kutanua uelewa wao na kupanua fursa zao kupata ajira kwenye masoko ya dunia. Alieambatana naye ni muandaaji wa maonyesho hayo Shaukatal Zahir.

WIZARA YA VIWANDA YAJIPANGA KUKUZA MASOKO NDANI NA NJE YA NCHI

$
0
0
*Yatakiwa kuwa karibu na balozi zilizopo nchini ili kuweza kupata masoko ya bidhaa za ndani

*TANTRADE wapongezwa kwa kuyatendea haki maonesho hayo kila mwaka

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAONESHO ya 43 ya biashara maarufu kama sabasaba yenye  kauli mbiu ya usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo ya viwanda yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam huku masuala ya utafutaji wa masoko pamoja na kuelimimisha wafanyabiashara kuhusiana na kliniki ya biashara yakitiliwa mkazo.

Akizungumza katika ufunguzi huo makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa maonesho hayo ni kwa kutoa kipaumbele kwa bidhaa zinazozalishwa nchini Kama Rais anavyosisitiza.

Suluhu amesema kuwa maonesho ya sabasaba ni makubwa katika ukanda wa Afrika na katika maonesho hayo zaidi ya nchi 35 zimeshiriki katika hali inayoashiria ubora na utulivu unaovutia uwekezaji katika nchi yetu.

Amesema kuwa serikali itaviwezesha viwanda vidogo na Kati katika masoko pamoja na kuendelea kushiriki katika maonesho hayo ili waweze kutangaza bidhaa zao zaidi.

Pia amesema kuwa kukua kwa uchumi kwa asilimia 7 kunachagizwa na maendeleo ya viwanda na kasi zaidi pamoja na wasimamizi wa sekta hiyo utapelekea wananchi kufanana na kasi ya ukuaji wa uchumi.

Aidha amezitaka mamlaka za TFDA, TBS, mamlaka za uvuvi na kilimo kufanya kazi kwa uadilifu na utii na wao kama Serikali watasimamia na kuhakikisha hakuna urasimu katika hilo, na amewahimiza tantrade ambao ndio wasimamizi na waandaaji wa maonesho hayo kutafuta masoko na kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na ubora na kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazozalishwa nchini.

Kuhusiana na ujenzi wa viwanda Suluhu amesema kuwa azma ya serikali katika ujenzi wa viwanda bado ipo palepale na hiyo ni pamoja na utafutaji wa masoko ya ndani na nje.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa chama Cha mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewapongeza bodi, baraza na wafanyakazi wa tantrade kwa kuyatendea haki maonesho hayo mwaka hadi mwaka.

Amesema kuwa maonesho ya namna hayo ni kisiwa Cha kuboresha nyaraka za kisera zinazosaidia katika maendeleo.

Pia Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa gurudumu la maendeleo linaenda vyema na hiyo ni kutokana na uongozi Bora wa serikali ya awamu ya tano na kusema kuwa wizara za biashara na viwanda pamoja na uvuvi na kilimo  zinategemewa na watanzania wengi hivyo zitazidi kusimamiwa ili kuongea kipato zaidi.

Bashungwa amehaidi ushirikiano baina yao na wawekezaji na ndani na nje ya nchi na kuwahimiza watanzania kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa kujihusisha na viwanda hasa vidogo na vya Kati.

Aidha amezitaka halmashauri zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na wao Kama wizara watahakikisha uwepo wamaeneo ya usindikaji.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa Wilaya, wabunge pamoja na wajumbe wa baraza la wawakilishi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa uzindua rasmi wa maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam leo Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizindua rasmi kwa kubonyeza kitufe maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa zawadi kwa washindi wakati wa uzinduzi rasmi na kutembelea maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,  akitembelea mabanda mablimbali mara baada ya kuzindua rasmi maonesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara katika Viwanja vya Sabasaba Barabara ya kilwarod jijini Dar es salaam Julai 02, 2019. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WANANCHI WAFIKA MFUKO WA SELF-SELF KUJUA KAZI ZAO

$
0
0
 Meneja wa Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa SELF- SELF MF, Linda Mshana kulia akimpa maelekezo Mkurugenzi Mkuu wa Star Natural Products LTD, George Buchafwe namna mfuko huo unavyotoa huduma zake kwa wananchi katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam na kushoto ni Meneja Mikopo Ufuatiliaji wa mfuko huo,Bw. Lucas Mlelwa.
Meneja wa Masoko na Uhamasishaji wa Mfuko wa SELF- SELF MF, Linda Mshana kulia na Meneja Mikopo Ufuatiliaji wa mfuko huo, Lucas Mlelwa kushoto wakitoa maelekezo kwa wananchi waliofika kujionea huduma zinazotolewa na mfuko huo katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. (Picha na Mpiga Picha wetu, Dar es Salaam).

NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU ATOA NAFASI KWA WADAU WA UTALII WA UTALII NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa nafasi kwa Wadau wa Utalii nchini kuwa Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii upo tayari kupokea ushauri, mapendekezo pamoja na mawazo mapya yatakayosaidia kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani.

Pia, Amewataka watu binafsi, mashirika pamoja na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye sekta ya utalii wasisite ofisi yake ipo wazi kwa mtu yeyote.

"Kwa yeyote atakayetaka kuniona kwa ajili ya kukuza na kuendeleza utalii hasa utalii wa ndani kwangu Mimi pamoja Waziri milango ipo wazi muda wote" alisisitiza Kanyasu.

Hayo ameyasema wakati alipokuwa akizungumza na Watalii wa ndani wapatao 200 kutoka jijini Dar es Salaam ambao walitembelea katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya kutalii ndani ya msitu wenye kila aina ya vivutio vya utalii likiwemo ziwa la kutengenezwa.

Kundi hilo la watalii wa ndani liliratibiwa na Kampuni ya Dalida Tours and Travel Agency kupitia chini ya Usimamizi wa Mratibu wa safari hiyo , Emma David.

Mhe. Kanyasu amesema moja ya mkakati wa Wizara ni kutaka watalii wa ndani wawe namba moja kwa kutembelea vivutio vya utalii badala ya kutegemea Watalii wa kutoka nje kama ilivyo sasa.

Aidha, Mhe.Kanyasu amesema pia Wizara yake ipo tayari kupokea na kutoa msaada wa hali na mali kwa mtu au kikundi cha watu kitakacholenga kuhamasisha utalii wa ndani.

''Tunataka akili mpya na mawazo mapya ya namna ya kusukuma na kujenga utamaduni wa watu wetu Wawe wa kwanza kutalii kama ilivyo kwa China'' Alisisitiza Kanyasu

Ameongeza kuwa Idadi ya watalii wa ndani hairidhishi hivyo kunahitajika mkakati wa pamoja katika kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania ili waweze kutembelea vivutio hivyo.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amesema kama nchi haiwezi kuifanya sekta ya utalii kama injini ya uchumi endapo Wazawa wenyewe wataendelea kuwa nyuma huku utalii wa ndani ukiwa na mwitikio mdogo.

" Kama taifa na kwa Mwananchi mmoja mmoja bado hatujaitendea hali sekta ya Utalii ni sekta ambayo haijaguswa hata kidogo ni lazima wananchi wawekeze na wakati huo huo wananchi watembelee vivutio vya Utalii.Amesisitiza Kanyasu

Naye, Emma David ambaye ni Mratibu wa kundi hilo la watalii wa ndani amesema wamejipanga kuhamasisha idadi kubwa zaidi ya watalii wa ndani kwa kupitia mitandao ya kijamii ili waweze kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoppo nchini.

''Sisi tumejipanga kutembelea mikoa yote lengo letu ni kuunga mkono jitihada za Wizara katika kuhamasisha Utalii wa ndani, Alisisitiza Emma.

Aidha, Ameishukuru Wizara kwa jitihada inazozifanya za kutengeneza mazingira rafiki kwa watu wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye utalii wa ndani.

Naye, Meneja wa Magoroto, Jeremia Mchechu amesema mwitikio wa wa watalii kutoka ndani na nje ya nchi umekuwa mkubwa tangu walipoanzisha eneo hilo kama kivutio cha Utalii na eneo la ziwa ambalo ni la kutengeneza limekuwa kivutio kikubwa cha Utalii.

Amesema watalii wengi wanaofaika katika eneo hilo wamekuwa wakipendelea kupanda milima, kuapnda baiskeli milimani pamoja na kutembelea vijijini kwa ajili ya kujifunza tamaduni ya wakazi wa Tanga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Dayna Saimoni ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti Mratibu wa safari ya Utalii wa ndani, Esta Satta ikiwa ni ishara ya shukrani kwa kuunga mkono jitihada za Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuchochea na kuinua idadi ya watalii wa ndani katika Msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nhe, Constantine Kanyasu akizungumza na watalii wa ndani walitembelea Msitu asilia wa Magoroto ambao ni kivutio kikubwa cha Utalii wakati walipokusanyika usiku kufurahia ngoma za kabila la wadigo.
 Kundi la watalii wa ndani kutoka jijini Dar es Salaam walioungana kwa pamoja na kwenda kutembelea msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na watalii wa nje mara baada ya kuwasili katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na watalii wa ndani mara baada ya chakula cha jioni katika msitu Asilia wa Magoroto katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Baadhi ya watalii wa ndani na wa nje nyakati za usiku wakifurahia ngoma ya kabila wasambaa iliyokuwa ikitumbuizwa kwa watalii hao. (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images