Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

WAZAZI WATAKIWA KUJITAMBUA NA KUJUA MAJUKUMU YAO

0
0
Wazazi wanapaswa kutambua kuwa bado wataendelea kuwa na jukumu la kuzaa na kulea suala ambalo kwa wakati huu wengi kati yao hujisahau hasa katika ule mfumo wa asili wa malezi ya pamoja na badala yake kila Mzazi huamua kulea Mtoto wake pekee.

Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi alitoa kauli hiyo wakati akilifungua Baraza la Wazazi la Chama cha Mapinduzi la Wilaya ya Mfenesini linalofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere uliopo Bububu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Mama Asha alisema hali ya ukosefu wa malezi ya pamoja kwa Watoto imepelekea kuporomoka kwa maadili ya Watoto walio wengi katika Jamii na matokeo yake wanashindwa kuwaheshimu Wazazi wa wenzao wakiona wa kwao ndio wanaostahiki kupata Heshima hiyo.

Alisema Watoto wa sasa wameacha maisha mazuri yanayoongozwa na Utamaduni wa Taifa na kuamua kufuata mila na Tamaduni za Ughaibuni jambo ambalo limechangia kuporomoka kwa Maadili hasa wakiangaliwa Watoto wenyewe vivazi na mienendo yao tayari imeshapoteza hadhi ya Utamaduni wa asili.

Mke huyo wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alielezea masikitiko yake kutokana na vitendo vya udhalilishaji vilivyoshamiri katika mitaa mbali mbali Nchini ambavyo kwa mtazamo wa matukio hayo, maadili tayari yameshapoteza muelekeo kutokana na jamii ya sasa kukosea njia sahihi ya kuelekea.

Mama Asha alisema tabia ya kupigwa kwa Wanawake na Watoto hadi kuumizwa na wakati mwengine kuchomwa moto Watoto kwa makosa madogo madogo pamoja na kutelekezwa ni miongoni mwa vyanzo vikuu vya udhalilishaji wa makundi hayo.

Alieleza kwamba ni ukweli usiofichika kwamba wanaoendeleza vitendo hivyo ambavyo ni vya kinyama na aibu kwa Jamii yenye kufuata mila, silka, desturi na Utamaduni wa Watu wastaarabu ni wale waliokosa malezi ingawa wanaelewa fika ubaya wanaoufanya.

Mama Asha aliwataka Wazazi na Viongozi wa ngazi na nyanja zote pamoja na Wananchi wote kuchukuwa tahadhari kwa kuwa karibu na familia zao ili kila mmoja kwa nafasi yake ailinde Jamii kwa kukemea vitendo hivyo viovu vyenye kutia aibu.

Aliwakumbusha Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kwamba bado wana jukumu kubwa la kutoa elimu, kusimamia malezi bora ya Watoto na kuhakikisha kwamba mazingira ya Mitaa yanaimarika ipasavyo ili kuwa na Jamii yenye ustawi na umakini mkubwa.

Akigusia janga la Dawa za kulevya Nchini ambalo huwakumba zaidi Vijana wanaotarajiwa kuwa Viongozi wa Taifa la kesho Mama Asha alisema jamii bado inapaswa kukemea utumiaji wa Dawa hizo ambazo ni janga linaloendelea kuikumba Dunia na hatimae kuathiri Mataifa mengi Ulimwenguni.

Mama Asha aliwanasihi Wananchi kwa kushirikiana na Viongozi wao ni vyema wakashiriki kikamilivu katika mapambano dhidi ya kupiga vita vitendo hivyo kwa kuwafichua wahalifu wanaoingiza, kusambaza na watumiaji kwa vile madhara yake huwagusa hata wale wasiohusika kwa kukumbwa na vitendo vya ajabu.

Alizikumbusha Taasisi zinazohusika na udhibiti wa Dawa za kulevya kuendelea kuimarisha mashirikiano na Serikali pamoja na wadau wengine wa Kitaifa na kimataifa ili kuona wimbi hili la Dawa za hatari linakomeshwa au kupunguzwa kwa kiasi kikubwa.

Mama Asha alishauri katika kukabiliana na janga hilo ni budi kuanzishwa kwa vituo vya Maandalizi katika kila Tawi la Chama cha Mapinduzi, kuimarisha Vijana kuwa Chipukizi na kuendeleza madarasa ya Itikadi ya Jumuiya ili kulea, kusimamia na kuwafundisha Vijana Maadili mema ya Chama cha Mapinduzi na Jumuiya zake.

Akigusia masuala ya uchumi ndani ya Jumuiya Mama Asha aliutaka Uongozi wa Jumuiya hiyo ya Wazazi kuhakikisha kwamba Wawekezaji wanaoshirikiana nao wanazingatia Maadili, Heshima na Uzalendo wa Taifa.

Alisema wapo baadhi ya Viongozi hudiriki kuiua Miradi ya Uwekezaji kwa sababu ya kukoza asilimia Kumi ya Mradi jambo ambalo ni miongoni mwa vitendo vya Ruishwa vinavyodumaza maendeleo ya Jumuiya pamoja na Taifa kwa Ujumla.

Aliwapongeza Wajumbe wa Baraza la Wazazi la Wilaya ya Mfenesini kwa umahiri wao wa kutekeleza Kanuni ya Jumuiya yao Kifungu cha 60{2} kinachotaka kufanyika Vikao kila miezi Sita ili Wajumbe wapate fursa ya kujadili masuala yao yenye mustakabal na Jumuiya pamoja na Chama chenyewe.

Alisema kwa vile Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi ni kongwe iliyoasisiwa mnamo Mwaka 1955 tokea wakati wa enzi za Vyama vya TANU na ASP ikiwa ni miongoni mwa mihimili ya Ukombozi lazima ienziwe, itunzwe na kuthaminiwa ili iendelee kulea na kupata maendeleo mema yatakayokikidhi ustawi na maeneleo ya Jamii yote Nchini.

Akitoaa Taarifa fupi ya Utekelezaji wa majukumu ya Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini, Katibu wa Jumuiya Hiyo Bibi Biubwa Jabir alisema yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kazi za Jumuiya hiyo ndani ya kipindi cha Miezi Sita iliyopita.

Bibi Biubwa alisema Viongozi wa Jumuiya hiyo bado wanaendelea kusimamia Jukumu lao la kuwajenga Vijana katika muelekeo wa kukua kimaadili wakizingatia kwamba Elimu ndio msingi imara wa kufanikisha majukumu hayo muhimu kwa Taifa.

Alisema kazi iliyopo mbele ya Viongozi hao ni kuunganisha nguvu katika kuhamasisha Wazazi waelekeze juhudi zao kwenye Utekelezaji wa Sera na Malezi bora kwa Watoto ili kuwa na Jamii iliyostawi Kimaadili.

Hata hivyo Katibu huyo wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini alisema zipo changamoto zinazokwaza ufanisi wa kazi wa Jumuiya akizitaja baadhi kuwa ni pamoja na ukosefu wa Fotokopi, Mashine, Fedha kwa ajili ya kuanzisha Mradi wa Ufugaji Nyuki, ushakavu wa Mabweni wa Skuli ya Wazazi Dole inayokwenda sambamba na ukosefu wa Gari kwa ajili ya Wanafunzi.

Naye kwa upande wake akitoa salamu Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Zanzibar Nd. Othman Ali Maulid alisema kuanzia sasa Kiongozi au Mdau ye yote anayeamua kuchangia au kusaidia shughuli za Chama na Jumuia zake lazima kuwepo kumbu kumbu kamili.

Nd. Othman alisema hatua hii ina lenga kujiepusha na vitendo vya Rushwa wakati Taifa likikaribia kuelekea katika Chaguzi za Serikali za Mitaa kwa upnade wa Tanzania Bara na Uchaguzi Mkuu Mwaka ujao.

Alisema wapo Watu wakiwemo baadhi ya Viongozi wanaoutumia udhaifu wa baadhi ya changamoto zinazokuwepo Kwenye Taasisi za Chama kwa kutoa Misaada kwa muekeo wa kujinyooshea njia ya kupata madaraka na baadae kujinufaisha kibinafsi.

Mkutano huo wa Wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi {CCM} Wilaya ya Mfenesini umejadili Utekelezaji wa Majukumu yake ndani ya Kipindi cha Miezi Sita iliyopita na kupanga Mikakati ya Utekelezaji kwa Kipindi chengine cha Miezi Sita Ijayo.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akisindikizwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Nd. Othman Ali Maulid kuingia katika Ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kufungua Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Wilaya ya Mfenesini.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akilifungua baraza la Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mfenesini.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini na Mikoa wa Magharibi na Mjini wakifuatilia ufunguzi wa baraza la Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mfenesini.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini Bibi Biubwa Jabiri akitoa Taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi ndani ya kipindi cha Miezi Sita.
 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya Wazazi Zanzibar Nd. Othman Ali Maulid akitoa salamu wakati akimkaribisha Mgeni rasmi kuufungua Mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini.
Mama Asha akimkabidhi mchango wake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini Bibi Biubwa Jabiri mara baada ya kuufungua Mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Mfenesini Ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu. Picha na – OMPR – ZNZ.


WAZIRI WA HABARI UTALII NA MAMBO YA KALE AZINDUA RIPOTI YA UTAFITI WA WATUMIAJI WA MAUDHUI YA UTANGAZAJI ZANZIBAR

0
0
 Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akifafanua jambo wakati wa kutoa hotuba ya Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watumiaji wa maudhui ya Utangazaji iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
 Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akikata Utepe wa kifurushi kuashiria Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watumiaji wa maudhui ya Utangazaji iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.Wamwanzo kulia ni Mjumbe wa Bodi wa Tume ya Utangazaji Ali Khatib Chwaya na katikati ni Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Omar Said Ameir.
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo akionesha Vitabu vya Ripoti ya Utafiti wa Watumiaji wa maudhui ya Utangazaji baada ya kuzinduliwa katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.Wamwanzo kulia Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Omar Said Ameir. na katikati ni Mjumbe wa Bodi wa Tume ya Utangazaji Ali Khatib Chwaya. 
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Omar Said Ameir akizungumza machache katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watumiaji wa maudhui ya Utangazaji iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar.
 Baadhi ya Waandishi pamoja na Wamiliki wa Vyombo vya Habari waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watumiaji wa maudhui ya Utangazaji iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Kikwajuni Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

VETA:Simu ni ajira kwa vijana katika fursa masomo

0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Teknolojia ya Mawasiliano inaweza kutumika kwa vijana katika kutatua changamoto ya ajira  pamoja na kusoma kozi mbalimbali katika Mitandao ya Simu za Mkononi.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Mradi wa VISOMO katika Chuo VETA Kipawa  Charle's Mapuli wakati Maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam amesema kupitia kusoma kwa kutumia mtandao baadhi wameweza kuhitimu katika kuunganisha mfumo wa Umeme viwandani.

Amesema baadhi ya vijana wameweza kujiunga kusoma katika mtandao na mwisho wa siku wamefanya vizuri katika kutengeneza mifumo mbalimbali ya Umeme. Mapuli amesema wanasoma katika Mitandao lakini mwisho wa siku mtihani wao ni kwa vitendo kufika chuoni na kuonyesha kile walichojifunza.

"Simu zinaweza kutumika katika kufanya maendeleo vijana wengi wanatumia simu janja lakini wanatumia kwa kufanya vitu ambavyo havina maendeleo na wale walitumia simu janja hizo wameweza kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Nae Meneja wa Mawasiliano VETA Sitta Peter amewataka wananchi kutembelea VETA kuangalia bidhaa mbalimbali wanazozalisha pamoja na kozi zinazotolewa na Vyuo vya VETA. Amesema katika kuelekea uchumi wa Viwanda VETA imejikita katika utoaji wa mafunzo kwa ajili Rasilmali itakayotumika katika Viwanda hivyo.

Peter amesema kuwa bila ya kuwa na Rasilmali yenye ujuzi malengo ya serikali yatakuwa hayajafikiwa kwa vitendo kama VETA itabaki nyuma.
 Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Sitta Peter akizungumza na mteja aliyetembelea Banda la VETA katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja Vya Makini Julius Jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mradi wa VISOMO katika Chuo VETA Kipawa Charle's Mapuli akionesha sakiti ya Umeme viwandani uliotengezwa na vijana waliosoma katika Mtandao katika Chuo hicho katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi wa Shule ya Watu Wenye Ulemavu Singida Abdi Kipara (34) akionesha umahiri wa ushonaji katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Zanura Hango (17) mwanafunzi wa Shule ya Watu Wenye Ulemavu Singida akionesha umahiri wa ufumaji vitambaa katika Banda la VETA katika Maonesho ya Sababa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

MKE, MTOTO WACHUKULIWA NA WATU WASIOJULIKANA MTWARA,IGP SIRRO ATOA NENO

0
0
JOSEPH MPANGALA , MTWARA.

“Walimuita Mke wangu nikamwambia Uende lakini mke wangu akaogopa akaenda akiwa amembeba mwanangu mmoja wa kike wakamshika kwa nguvu na kuondoka naye na mimi wakaniambia Niondoke”anasema Ahmad Msham Kijana anayejishughulisha na kilimo cha Mahindi,Mpunga na Kunde katika kijiji cha Mtole Kilichopo Nchini Msumbiji Mpakani mwa Tanzania.

Ahmad Msham Mtanzania alikuwa akiishi kijiji cha Mtole anasema Juni26 Usiku wa kuamkia alhamis Baadhia ya watu waliovalia Mavazi ya Jeshi la Msumbiji walivamia Kijiji cha Mtole kilichopo Msumbiji na kuanza kuchoma moto nyumba na baadae kuwakusanya wananchii pamoja na kuanza kuwaua kwa kuwapiga risasi ,tisa wakiwa Watanzania na wawili Raia wa msumbiji 

Mke wake Halima Hassan Lyanga pamoja na mmoja wa Mtoto wake Zarahna mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu alichukuliwa na Watu hao huku yeye akiachiwa mtoto wa kiume Zahran ambao ni mapacha mpaka sasa Hawajulikani walipo.

Msham ameiomba serikali kusaidi ili kuwezesha kupatikana kwa Mke na mtoto ambao mpaka sasa hakuna taari zozote zinazoonesha kuwa wamepelekwa wapi.

Aidha Diwani wa Kata ya KitayaJamal Kapende amesema kuwa baadhi ya wakazi wa kata yake wanashiriki shughuli za kilimo katika Kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania kwa makubaliano na serikali ya Vijiji pamoja wanakijiji Husika kutokana na kuwapo na maeneo mazuri kwa kilimo.

Kapende anasema Katika watu Tisa waliokufa ni wanakijiji Saba wanatoka Kijiji cha Kitaya na hivyo kuleta majonzi kutokana na kfahamika na wanakijiji hao.

“Sisi Tumepatwa na simanzi kubwa isitoshe kuna Watanzania watatu ambao hawajulikani kama wakufa au wapo Salama,kuna mama ambaye alikuwa na watoto mapacha wamemchukua yeye na mtoto mmoja wakamuacha mtoto mmoja na Mumewe wake na Kuna Binti amechukuliwa jambo ambalo wakazi wa kata hii wamekuwa na Huzuni Kubwa”amesema Kapende ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitaya.

Hata Hivyo Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka wakazi wa Kata Hiyo Kuhakikisha wanaonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ili kuweza kufanikisha Upatikanaji wa wananchii waliochukuliwa pamoja na Uwapo na Amani katika eneo hilo la mpakani.

“Tunadhamana kubwa ya Kuwalinda nyinyi na yoote yanawezekana tukishirikiana, sikuzote tunasema Taarifa ndio kitu cha msingi wewe ukimuona mtoto wako tatizo unamashaka naye tuambie,ukimuona mumeo tatizo unamashaka naye tuambie,ukiona mpenzi wako tatizo tuambie kwasababu usipofanya hivyo hata msikitini utashindwa kwenda hata makanisani utashindwa kwenda”IGP Sirro.

Jumapili ya wiki hii IGP Simon Sirro anatarajia kufanya mazungumzo na Mkuu wa Jeshi la Polisi kutoka Nchini Msumbiji ili kutatua tatizo hilo lililopo Mpakani.
Ahmad Msham akiwa amembeba Mtoto wake Zahran huku akimsikiliza Inspekta jenerali wa polisi IGP Simon Sirro wakati akiongea na wananchii wa kata ya Kitaya katika uwanja wa Mahakamani Mtwara Vijijini.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akiongea na wanannchii wa kijiji cha Kitaya Mkoani Mtwara Juu ya utoaji wa Taarifa kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa lengo la kuimarisha Ulinzi na Usalama.
Ahmad Msham akiongea mbele ya IGP Simon Sirro kuhusiana na kuchukuliwa kwa Mke pamoja na mtoto wake katika kijiji cha Mtole kilichopo Msumbiji mpakani mwa Tanzania ambapo mpaka sasa hawajulikani walipo.
Baadhi ya wananchiii wa kijiji cha Kitaya mkoani Mtwara wakimsikiliza IGP Saimon Sirro katika mkutano baada ya kutokea mauaji ya Watanzania Tisa katika Kijiji cha Kitole kilichopo Msumbiji Mpakani mwa Tanzania. 


WATANZANIA WASHAURIWA KUTUMIA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI

0
0

Na Mwandishi Wetu. Blog ya Jamii

WATANZANIA wameshauliwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini ili kuchochea wazawa kufanya vizuri zaidi kwenye soko la ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kampuni ya wa asili asilia Limited ambayo inatengeneza bidhaa za ngozi asilia ya Tanzania Dedan Munis katika viwanja vya maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa.

Amesema kuwa pamekuwepo nakasumba mbaya kwa watanzania kupenda bidhaa za kigeni badala ya kupenda zinazozalishwa na watanzania wezao ambao pia wanatengeneza ajira kwa vijana wa kitanzania.

Alisema iko shida kubwa kwa watanzania kwani wanapenda sana bidhaa za nje kuliko za ndani jambo ambalo linazolotesha bidhaa za ndani ukizingatia kuwa bidhaa hizi zinatengenezwa katika kiwango cha juu na cha ubora tena kwa Mali ghafi za ndani.

"Ndugu waandishi kimsingi nawakaribisha wananchi watanzania wezangu hapa sabasaba katika majengo haya ya Jakaya Kikwete Banda na 31,32waje wapate bidhaa bora zaidi zinazotengezwa na watanzania wenyewe kupitia Kampuni ya waasili asilia limited." Alisema Munisi.

Nakuongeza kuwa hapo kuna changamoto ya uwepo wa bidhaa Kutoka nje ambazo pia ni za plastiki na Mara zote watanzania ndio wanakimbilia,lakini nivema wananchi wakafika katika Banda hilo la Jakaya kikwete ili kujionea vitu vizuri vinavyozalishwa na wazawa katika kiwango cha ubora.

Amesema mwaka huu wamejipanga zaidi kushinda mwakajana kwani wanabidhaa bora zaidi kama vile viatu vya ngozi aina zote,sandles kwa akina mama na akina Baba na hata watoto mabegi kwa (handbegi) na vitu vingine vingi na tena vinapatikana kwa gharama nafuu.

Amesema katika kumuunga mkono mh.Rais katika azima yake ya viwanda basi wao wamefanya kwa vitendo na ameweza kuajiri watanzania wakutosha tu japo bado changamoto mbalimbali zipo ila wanapambana nazo.

"kama watanzania kwa sehemu yetu tumeamua kuweka kikubwa Serikali iendelee kuruboreshea Mazingira ya kufanya biashara pamoja na kuruhu taasisi za Fedha kutoa mikopo pasipo kuwa na riba kubwa." Amesema Munisi.

Amefafanua kuwa watanzania wakumbuke kuwa wakipenda bidhaa za ndani kimsingi zinaleta na kuhifadhi utamaduni halisi wa mtanzania na mwaafrika kwa ujumla hivyo wananchi wajitokeze kwenye Banda hilo la Jakaya Kikwete.
Mkurugenzi wa Kampuni ya wa asili asilia Dedan Munisi alifafanua jambo kwenye maonyesho ya 43 ya biashara yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Wilayani Temeke leo.picha na Mpiga picha wetu.

RC HOMERA AAPA KUWABANA WATOROSHA DHAHABU,WAKWEPA KODI

0
0

Na Ripota Wetu,Wa Michuzi TV 

MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera ameapa  kupambana na wanaotorosha Dhahabu na mpaka sasa na watu wawili wametiwa Mbaroni kwa kununua dhahabu kinyume cha sheria .

Homera ameyasema hayo mkoani Katavi akiwa katika ziara ya  kutembelea  migodi mbalimbali ukiwemo wa  Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi Mining.

Amesema  anachotaka nikuona  wachimbaji wadogo wanauza madini yao katika soko la madini lililopo mkoa huo .

Homera  ameanza majukumu ya ukuu wa mkoa ikiwa tayari  soko limeshafanya biashara kwa kununua dhahabu Gram 238, Mei 23 mwaka huu wa 2019 jambo ambalo lilimfanya aanze kufatilia na kubaini dhahabu nyingi inayopatikana mkoani Katavi inauzwa nje ya mkoa hali iliyonayosababisha soko hilo kusua sua.

Amesema  kutokana na hali hiyo bosi huyo wa mkoa alimua kufanya ziara ambayo ilikwenda kuyafanyia kazi mapungufu ya soko hilo ambapo hadi  sasa linaridhisha na kufuatia oparesheni mbalimbali zinazoendelea Soko linaendelea  kufanyika kwa ununuzi na uuzaji wa madini na mpaka sasa Grams 6317.2 sawa na Kg 6 na Grams 317.2 yenye thamani ya Sh. 519,155,127.56 zimenunuliwa kwa kipindi cha Mei na Juni 30/2019 na Serikali kupata mrahaba (Royality7%) Sh. 36,340,858.92 na Service levy asilimia 0.3  sawa na Sh.1,401,718.85,

Pia  amefafanua kuwa  ameimarisha mifumo ya Benk mbili katika soko hilo nakwamba  ameendelea kuwa bana mablokers na wanunuzi wenye leseni na wachimbaji mbalimbali  kuhakikisha pia wanauza madini yao kwenye soko la mkoa ili kujenga  uchumi wa Tanzania na kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli katika kuinua uchumi na miundombinu ya nchi  kwa kulipa kodi.
 Wachimbaji wadogo wadogo wakimsikiliza  MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera  akiwa katika ziara ya  kutembelea  migodi mbalimbali ukiwemo wa  Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi Mining.
 

 MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera  akiwa katia ziara ya  kutembelea  migodi mbalimbali ukiwemo wa  Dilifu ambao ni mgodi wa wachimbaji wadogo na mgodi mkubwa wa Katavi na Kapufi Mining.


WAZIRI KALEMANI ATIMIZA AHADI YAKE KUWAWASHIA UMEME WANANCHI WA MWAKITOLYO

0
0
 Na Veronica Simba - Shinyanga 

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametimiza ahadi yake aliyoitoa mwanzoni mwa mwezi huu (Juni) kwa wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, kuwa umeme utawashwa katika eneo lao kabla ya Julai, 2019.

Dkt. Kalemani alitimiza ahadi hiyo jana, Juni 29, 2019 akiwa katika ziara ya kazi mkoani Shinyanga, ambapo aliwasha rasmi umeme katika jengo la Ofisi ya Serikali, Kitongoji cha Mwakitolyo Namba Tano.

Akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara kijijini Mwakitolyo, Waziri Kalemani alisema Serikali inatambua umuhimu na kuthamini mchango wa wachimbaji wadogo wa madini katika uchumi wa nchi.

Alisema, ndiyo maana aliagiza mchakato wa kupeleka umeme eneo hilo uharakishwe; baada ya kufanya ziara katika eneo hilo awali na kushuhudia wachimbaji wadogo wa madini wakifanya kazi zao bila umeme.

Kuhusu Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini (REA) katika eneo hilo, ambaye katika ziara yake ya awali, Waziri aliagiza kushikiliwa kwa Hati za kusafiria za Wakurugenzi wa Kampuni husika; kutokana na kusuasua kwa kazi, aliruhusu mmoja kati yao arejeshewe hati hiyo baada ya kuridhishwa na maendeleo ya kazi.

“Maendeleo ya kazi yao kwa sasa yanaridhisha. Naagiza Kiongozi wao mkuu, arejeshewe Hati yake lakini wenzake watatu wataendelea kuwepo hapa hadi watakapokamilisha kazi ya kuunganisha vitongoji vyote vya Mwakitolyo,” alielekeza Waziri.

Aidha, Dkt. Kalemani alitoa maagizo kwa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi FedGrace Shuma pamoja na Mkandarasi husika, kukamilisha kazi ya kusambaza nguzo za umeme katika eneo hilo ndani ya Wiki mbili tu ili eneo lote liwashwe umeme katika kipindi hicho.

Waziri alitoa rai kwa wananchi wa Mwakitolyo kujitokeza kwa wingi na kuendelea kulipia gharama ya kuunganishiwa umeme ambayo ni shilingi 27,000/- tu. 

Aidha, aliwataka viongozi wanaosimamia Taasisi mbalimbali za Umma na Miradi ya kijamii, kutenga fedha katika bajeti zao na kulipia gharama hiyo ndogo ili Taasisi na Miradi husika iunganishiwe umeme.

Awali, akikagua maendeleo ya kazi ya kuunganisha umeme katika Kijiji cha Mahembe, Waziri Kalemani aliuagiza uongozi wa TANESCO Shinyanga, kufunga Transfoma kubwa yenye uwezo wa kilovoti 200, kwenye Kituo cha Afya katika eneo hilo, ndani ya siku Tano, ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwapelekea wananchi maendeleo, hususani umeme vijijini.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Donald Magesa, alisema uongozi na wanachama wa CCM mkoani humo, wanafurahi kuona Ilani ya Chama Tawala ikitekelezwa kwa vitendo.

“Ilani ya Chama inasema umeme uende kila nyumba. Tunatekeleza. Nawaombeni wananchi tujitokeze kwa wingi kulipia shilingi 27,000 ili kila mmoja apate umeme na tupate maendeleo kama Serikali inavyokusudia,” alisema Katibu.

Kwa upande wao, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwakitolyo, Nuhi Shomi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mwakitolyo Namba Tano, Benedict Robert, kwa nyakati tofauti, walimpongeza Waziri Kalemani, kutimiza ahadi aliyoitoa kwa wananchi wa eneo hilo kwa kuwashiwa umeme ndani ya muda mfupi.

Katika ziara hiyo, Waziri Kalemani alifuatana na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Tawala na wataalamu mbalimbali kutoka Wizarani, REA na TANESCO.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (aliyeinua mkono), akifurahi na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, Juni 29, 2019.

 Fundi kutoka Kampuni ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Kampuni ya Angelique International Limited ya India, akikamilisha zoezi la kuunganisha umeme katika Kitongoji cha Mwakitolyo Namba Tano, Shinyanga Vijijini wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani  (hayupo pichani) Juni 29, 2019. Wanaoshuhudia ni wananchi wa eneo hilo.

 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, muda mfupi kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo, Juni 29, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.

Sehemu ya umati wa wananchi wa Kata ya Mwakitolyo, Shinyanga Vijijini, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo, Juni 29, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.

BADO NNA MATUMAINI MAKUBWA NA TAIFA STARS-KOCHA AMUNEKE

0
0
Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars  Emmanuel Amuneke, ana matumaini kuwa bado timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa tatu wa mashindano ya Mataifa Afrika dhidi ya Algeria,utakaofanyika Julai 1,katika Uwanja wa Al- Salam nchini Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari,Amuneke,alisema kuwa licha ya kuwa Algeria ina kikosi kizuri,lakini bado ana matumaini makubwa na vijana wake kuwa watafanya vizuri katika mchezo huo wa mwisho wa kundi C.

“Tumecheza na Algeria mara kadhaa,nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam tuliocheza tukafungwa bao mbili kwa sifuri,na baadaye tukaja kucheza nao tukatoka nao 2-2,nakumbuka pia walikuja wakatufunga bao 7 kwa bila,lakini hiyo yote ni historia,”alisema na kuongeza:

“Kwasasa hivi tunachokitazama ni namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo miwili iliyopita,na kufanya maamuzi sahihi tunapokuwa na mpira,kwahiyo Jumatatu ni ukurasa mwingine na ni safari nyingine kwa Tanzania na Algeria,na hauwezi kutabiri nani atakuwa mshindi,kwahiyo tutaingia uwanjani kupambana na kusaka pointi tatu.”

Taifa stars,itashuka dimbani kupambana na Algeria baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa bao 2-0 na mchezo wa pili dhidi ya Kenya ulioisha kwa Kenya kuibuka na ushindi wa bao 3-2.


PSSSF YAWAALIKA WANACHAMA NA WANANCHI KUFIKA BANDA LA MFUKO HUO KUPATA ELIMU KUHUSU HIFADHI YA JAMII KWA WATUMISHI WA UMMA

0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAONESHO ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, tayari yamepamba moto ambapo Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, ametoa wito kwa Wanachama wa Mfuko huo pamoja na Wananchi kufika kwenye banda hilo ili kupata elimu kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.

Bi. Chiume amesema, banda la PSSSF liko jengo namba 13 mkabala na jengo la matangazo ndani ya viwanja vya Maonesho Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
"Mfuko wa PSSSF umeundwa baada ya kuunganishwa kwa mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya GEPF, PSPF, LAPF na PPF na kwa sababu hiyo bado ni mpya na wanachama wanahitaji kuelimishwa kuhusu majukumu mapya ya Mfuko huo kwa wanachama ambao ni watumishi wa Umma." Alifafanua Bi. Chiume.

Alisema uduma za PSSSF zitatolewa kwenye jingo moja ambalo pia linatumiwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Maonesho hayo yameanza Juni 28 na yatafikia kilele Julai 13, 2019 na kauli mbiu ya mwaka huu ni "Usindikaji wa Mazao ya Kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda."
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. William Erio (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (wapili kushoto), pamoja na Afisa Matekelezo wa NSSF, Bi.Diogi Janguo, (wapili kulia) na Mtaalamu wa mifumo ya computer, NSSF Bi.Grace Magigile wakati Bw. Erio alipofika kwenye jengo namba 13 ambalo Mifuko yote miwili ya PSSSF na NSSF inatoa huduma kwa ushirikiano katika jengo hilo. Itakumbukwa kuwa PSSSF ni Mfuko ulioundwa kuhudumia Watumishi wa Umma na NSSF kuhudumia Sekta binasi.
 Afisa Matekelezo Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Donald P. Maeda (kushoto), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko huo.
 Afisa Mwandamizi wa Malipo, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma,(PSSSF), Bi.Nyangi Masalu (kulia), akiwahudumia wanachama wa Mfuko huo waliotembelea banda la PSSSF kwenye viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam Juni 30, 2019.
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kushoto), akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda hilo.
Jengo namba 13 ambalo ndipo ilipo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSSF na NSSF.
Timu ya PSSSF ikiongozwa na Mkurugenzi wa Banda la Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ikiwa tayari kutoa huduma bora kwa wanachama na wananchi watakaofika kwenye banda hilo.

Maktaba zitumike kuongeza ufaulu na kupunguza uhalifu kwa vijana-DC Daqarro

0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Jamii imetakiwa kuhamasisha watoto wao kupenda kujisomea vitabu mbalimbali kwenye Maktaba ili kuepuka vishawishi na matendo yasiyofaa ikiwemo kuvuta bangi na ubakaji.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro wakati alipokuwa akizindua kituo kipya cha Maktaba ya Jamii cha Madecha kilichojengwa katika Kata ya Sinoni kwa thamani ya zaidi ya sh, Mil.40 chini ya ufadhili wa familia ya Mathew Hladezuk(17) kutoka nchini Marekeni.

Akizungumza katika hafla hiyo,mkuu huyo wa wilaya ,mbali na kumpongeza mwanzilishi wa kituo hicho,Profesa Richard Msomba na Mkewe Elaine Msomba alisema ipo haja kwa kila mzazi kumhamasisha mtoto wake kujisomea vitabu mbalimbali katika Maktaba hiyo jambo litakalosaidia kuongeza uelewa katika masomo yao.

"Vijana wa kata ya Sinoni watumie Maktaba hii kujiendeleza kielimu na serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ,kwani vijana wetu wakihamasika vizuri kujisomea itapunguza matukio ya uhalifu" Alisema Daqqaro

Awali mwanzilishi wa Maktaba hiyo,Prof,Richard Msomba ambaye ni mwalimu wa uchumi nchini Marekani alisema kituo hilo kitakachohudumia bure wanafunzi wa Chekechea hadi kidato cha Sita.

Alisema ameamua kujenga Maktaba hiyo yeye na mke wake,Elaine Msomba kama sehemu ya mchango wao kwa jamii katika kuendeleza sekta ya elimu baada ya kubaini kuwa Jamii haina Huduma hiyo na watoto wengi wanajisomea majumbali mwao na kukosa sehemu ya utulivu. .

"Maktaba hii itahudumia shule mbalimbali za sekondari na msingi zipatazo 17 na wanafunzi wapatao 140 wanajisomea kwa kila siku na wakati wa mitihani wanafunzi wanakuwa wengi zaidi" Alisema prof.Msomba.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa walionayo wanafunzi ni uwezo wa kununua vitabu hivyo wamewasogezea Huduma ya vitabu na watakuwa wanajisomea bure bila kulipa gharama yeyote.


Aliiomba Jamii kuwa na Moyo wa kujitolea kuisaidia Jamii isiyona uwezo kama ambavyo yeye amefanya kwa kuanzisha kituo hicho cha Maktaba ya Jamii.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo,Godfrey Simbile àliishuuru familia hiyo kwa kuwaletea karibu Maktaba hiyo katika Kata yake na kueleza kuwa jukumu lake ni kuhakikisha wananchi wake hususani vijana wanahamasika kuja kujisomea katika Maktaba hiyo.


"Maktaba hii itasaidia watoto kujiendeleza kielimu kupitia vitabu mbalimbali vinavyopatikana katika maktaba hii na itapunguza matukio ya uhalifu na vishawishi vibaya.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro(kati) akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha maktaba

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NNE WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI ZANZIBAR

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na Viongozi wa Meza Kuu wakiimba wimbo wa Solidariti Foreva wakati wa ufunguzi wa Mkutanio Mkuu wa Nne wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
MWENYEKITI wa TUCTA Dr.Yahya Msingwa, akitowa salamu za TUCTA wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Shirkisho la Wafanyakazi Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa AbdulWakili Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu Mkuu wa ZATUC Ndg. Khamis Mwinyi, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Nne wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Katibu Mkuu wa ZATUC Ndg. Khamis Mwinyi, alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Nne wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Zanzibar.
WAALIKWA wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazini Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MWAKILISHI wa ILO Ndg. Mohammed Mwamadzingo, akitowa salamu za ILO wakati wa fhafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Badulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu
WAZIRI wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe.Maudlini Castico akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kuhutubia hafla hiyo, iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

PROF KABUDI ZIARANI FALME ZA KIARABU

0
0
Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu zimekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya usalama wa eneo la Ghuba na bahari ya Hindi pia kusaidia kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi alipomtembelea na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan.

Katika Mazungumzo hayo wawili hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha udugu wa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili ikiwa ni pamoja na kufufua mazungumzo ya Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambayo kwa mara ya mwisho yalifanyika katika Mji wa Abu Dhabikatika Umoja wa Falme za Kiarabu ili kufufua na kutekeleza makubaliano ikiwa ni pamoja na kuangalia fursa za kiuchumi kwa faida ya pande zote mbili.

Akizungumza mara baada ya mazungumzo hayo Waziri Palamgamba John Kabudi amesema pamoja na masuala mbalimbali waliyokubaliana pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan ameahidi kufanya mazungumzo na Ubalozi wa Falme za Kiarabu uliopo Nchini Tanzania ili kuharakisha matayarisho ya Ubalozi huo kuhamia Dodoma baada ya serikali ya Tanzania kuupatia ubalozi huo eneo la kujenga ubalozi wa Nchi hiyo mjini Dodoma bure.

Waziri Kabudi ameongeza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa ya manufaa kwa pande zote mbili na kwamba yataendelea kuimarisha mahusiano baina ya Nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kufungua fursa za kibiashara kwa ajili ya maendeleo ya mataifa hayo.

Katika hatua nyingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi akizungumza wakati akihitimisha ziara yake Nchini China,amesema ziara hiyo imekuwa ya manufaa kiuchumi kwa Tanzania ambapo tayari wawekezaji takribani 150 wanatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa nia ya kuangalia maeneo mbalimbali ya uwekezaji mapema mwezi septemba wakitanguliwa na ujumbe wa watu 10 mwezi Julai 2019,hii ikiwa ni kipindi kifupi sana mara baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhudhuria mkutano wa kwanza wa maonesho ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika uliofanyika katika mji wa Chanshang katika jimbo la Hunan,Nchini China.

Aidha ametanabaisha kuwa tayari wamepatikana wawekezaji wanaotaka kujenga nyumba ya kulala wageni yenye vyumba mia tatu katika mji wa Karatu ulioko mkoani Manyara kwa nia ya kuhamasisha watalii hususani kutoka China ambao wanatarajiwa kuongezeka maradufu kufuatia hatua ya Tanzania kuweka msisitizo katika kutangaza vivutio vyake vya Utalii.

Pia Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Beijing kimekubali ombi la Waziri Kabudi la kutaka kuongeza idadi ya wanafunzi watakaokwenda kusoma chuoni hapo kutoka 20 hadi kufikia idadi 40 nafasi zitakazotolewa kwa ufadhili wa chuo hicho kila mwaka ili kuandaa nguvu kazi ya kutosha wakati Tanzania ikijiandaa kuingia katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan,Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu. June 30,2019. Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu zimekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala ya usalama wa eneo la Ghuba na bahari ya Hindi pia kusaidia kuimarisha hali ya usalama katika nchi za Somalia na Sudan. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi,akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Wizara ya Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi. June 30,2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Umoja wa Falme za kiarabu Sheikh Abdullah bin Zayed Al Nahyan,Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu. June 30,2019.

Wananchi wajitokeza kwa wingi katika Banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kupima afya zao na kupata ushauri

0
0

Afisa Uuguzi wa chumba cha upasuaji kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Edina Mulenda akieleza jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika kwa wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo. 

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mfunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa za shinikizo la juu la damu kwa Mbaraka Samatta wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo. 


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aisha Omary akimpima kiwango cha sukari mwilini Joseph Karumuna wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa bila malipo huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo kwa wananchi wanaotembelea banda hilo lililopo katika banda la Jakaya Kikwete. 


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Consolata Minja akimpima shinikizo la damu (BP) Erick Nestory wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo bila malipo kwaa watoto na watu wazima wanaotembelea banda hilo lililopo katika banda la Jakaya Kikwete. 


Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Swai akitoa ushauri wa jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo kwa Anna Mtui wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Katika maonyesho hayo Taasisi hiyo inatoa huduma za ushauri, vipimo na tiba za magonjwa ya moyo bila malipo kwa wananchi wanaotembelea banda hilo lililopo ndani ya banda la Jakaya Kikwete.

MASHINDANO YA JUMUIYA YA MICHEZO (NDONDO CUP) YAFUNGULIWA RASMI ARUSHA.

0
0
Mgeni Rasmi ambaye ni Mhariri Mkuu wa kampuni ya Tan Communication Media wamiliki wa Redio 5 Arusha,Bi.Ashura Mohamed akizungumza na wachezaji wakati wa uzinduzi rasmi wa michezo hiyo.
Robert Pius Afisa Michezo 977 akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Tanganyika uliopo Jijini Arusha 






Mratibu wa mashindano hayo ambaye ni mdau wa michezo Bw.Benjamini Mathayo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mashundano hayo ya Ndondo Cup
Timu mbili zilizocheza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo Timu ya Jeshi kikosi cha 977 Upendo Fc ambapo timu ya Kikosi cha Jeshi 977 iliibuka mshindi katika mechi hiyo ya Ufunguzi kwa Kuichapa Upendo Fc goli 4-0.
Mgeni rasmi Bi Ashura Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Jeshi kikosi cha 977 Upendo Fc.
Mgeni rasmi Bi Ashura Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na Timu Upendo FC


Na.Vero Ignatus,Arusha.


Mashindano ya Jumuiya ya Michezo Arusha maarufu kama (Arusha ndondo Cup) yamefunguliwa rasmi jana katika Viwanja vya Jeshi kikosi cha 977 Tanganyika pekas,ambapo Jumla ya timu 20 kuchuana hapo.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo Bi.Ashura Mohamed kutoka ya Tan Communication Media wamiliki wa Redio 5 aliwataka vijana hao kuchukulia Mashindano hayo kama chachu ya kuendeleza Vipaji vyao.

Alisema kuwa mchezo wa soka hapa nchini na duniani ni mchezo wenye mashabiki wengi hivyo waendelee kufanya mazoezi kwa bidii na kuwa na nidhamu ili kukuza vipaji na kutumia mashindano hayo Vyema kujitangaza.

Aidha aliwataka marefa ambao wanachezesha mechi zote pamoja na waratibu wa mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanatumia sheria kumi na saba za mpira wa Miguu ili kuhakikisha kuwa Mshindi halali anapatikana badala ya kubebana.

“Nimeelezwa kuwa mashindano haya yameanza mwaka 2015,yakiwa na timu 12 leo tuna timu 20 ni hatua nzuri na inaonesha wazi kuwa mmejipanga vizuri nisisitize tu sheria zifuatwe na umati huu wa watu unaonesha nia njema ya kuvutiwa na mashindano haya”Alisema Ashura.

Hata hivyo alisema kuwa ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo ataongeza zawadi ili kuongeza hamasa kwa timu zitakazoshiriki na kufanya vyema zaidi.

Naye Mratibu wa mashindano hayo ambaye ni mdau wa michezo kutoka wilaya ya Arumeru Bw.Benjamini Mathayo alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ni kukosekana kwa vifaa vya kutosha pamoja na changamoto ya fedha hali inayopelekea kukosekana kwa zawadi za washindi pamoja na kukosa mdhamini.

Bw.Mathayo alisema kuwa mafanikio katika mashindano hayo ni kupunguza Idadi ya Matukio ya Uhalifu na utumiaji mbaya wa madawa ya kulevya.

alisema kuwa Mashindano hayo yataenda sambamba na Utunzaji wa Mazingira ambapo kila Jumapili timu zote zitapata fursa ya kupanda miti,katika maeneo ya wazi.

katika mashindano hayo timu ya Jeshi kikosi cha 977 kiliibuka mshindi katika mechi hiyo ya Ufunguzi kwa Kuichapa Upendo Fc goli 4-0.

Mara yatamba mbio za mita 400 UMITASHUMTA 2019

0
0

Mwanariadha Matiko Nyamaraga (289) kutoka mkoa wa Mara akimaliza mbio za mita 400 na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza. Nyuma yake ni Dotto Mwandu wa Simiyu (533) na Steven Stephano wa Tabora aliyeshika nafasi ya tatu. 
Mkimbiaji Nyairabu Chacha kutoka mkoa wa Mara akimalizia mbio za kupokezana vijiti mita 4 x 400 na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe.Mwita Waitara akizungumza na walimu na wanafunzi wanaoshiriki michezo ya UMITASHUMTA kutoka mkoa wa Mara wakati Mhe.Waitara alipotembelea viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara kuona maendeleo ya michezo hiyo jana. 
Wanariadha kutoka mkoa wa Simiyu walioshiriki mbio za mita 400 x 4 wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wao mara baada ya kufanikiwa kushinda mbio hizo na kujinyakulia medali za dhahabu leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 

Wanariadha kutoka mkoa wa Mara wametamba katika mbio za mita 400 zilizofanyika leo asubuhi kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara baada ya kufanikiwa kuchukua medali za dhahabu kwenye mbio za mita 400 wavulana, na mbio za kupokezana kijiti mita 4 x 400 kwa wasichana, huku mkoa huo ukishika nafasi ya pili kwa mbio za mita 400 wasichana na kushika nafasi ya tatu kwenye mbio za kupokezana kijiti 4 x 400. 

Mwanariadha Matiko Nyamaraga alifanikiwa kushinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 400 baada ya kutumia muda wa sekunde 55:28, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Doto Mwandu wa Simiyu aliyetumia muda wa sekunde 55:50, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mkimbiaji Steven Stephano wa Tabora ambaye alitumia muda wa sekunde 55:72 na hivyo kufanikiwa kujishindia medali ya shaba. 

Katika mbio za kupokezana vijiti wasichana, mkoa wa Mara ulijishindia nafasi ya kwanza baada ya wanariadha wake Zainabu Chacha, Anjelina Olembe, Nyanzobe Bahi na Nyairabu Chacha kufanikiwa kukimbia kwa kupokezana vijiti na kutumia muda wa dakika 4:18:97 na kuwashinda wanariadha kutoka mikoa mingine. Nafasi ya pili ilichukuliwa na wanariadha kutoka mkoa wa Mwanza ambao kwa jumla walitumia muda wa dakika 4:20:91 na walioshika nafasi ya tatu Simiyu walitumia muda wa dakika 4:21:69. 

Mkoa wa Mara ulishika nafasi ya pili kwa upande wa mbio za mita 400 wasichana baada ya mkimbiaji wake Angelina Olembe kushika nafasi ya pili ambaye alitumia muda wa dakika 1:01:85, huku aliyeshinda mbio hizo Lucia Nestory wa Mwanza ambaye alishika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda wa dakika 1:01: 80. Nafasi ya mshindi wa tatu ilichukuliwa na mwanariadha Johari Hussein wa Tabora ambaye alitumia muda wa dakika 1:02:22. 

Kwa upande wa mbio za kupokezana vijiti wavulana mkoa wa Mara ulishika nafasi ya tatu kufuatia wanariadha wake Matiko Nyamaraga, David Paul, Josephat Maranya na Daniel Maiko kutumia muda wa dakika 3:53:45. Nafasi ya kwanza ilichukuliwa na wanariadha kutoka mkoa wa Simiyu ambao walitumia jumla ya dakika 3:51:88 huku nafasi ya pili ikienda kwa wanariadha wa mkoa wa Mwanza ambao walitumia muda wa dakika 3:52:12. 

Katika mchezo wa kurusha mkuki wavulana Pascas Qurejo wa Manyara alifanikiwa kujishindia medali ya dhahabu baada ya kurusha mkuki umbali wa mita 47 na sentimita 03, nafasi ya pili ilichukuliwa na Omary Abdallah wa Pwani ambaye alirusha umbali wa mita 38 na sentimita 93, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Bernard William wa Pwani ambaye alirusha umbali wa mita 38 na sentimita 67. 

Mashindano hayo yanatarajiwa kumalizika tarehe 3 julai, 2019 ambapo yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara

BASHUNGWA-AWAJIA JUU WANAOPOTOSHA NA KUKANDIA UBORA WA KOROSHO NCHINI,ASEMA KOROSHO YA TANZANIA INA UBORA

0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA



WAZIRI Wa Viwanda na Biashara ,Innocent Bashungwa amekemea baadhi ya Watanzania wanaopotosha na kukandia kuwa korosho ya Tanzania iliyopo kwenye maghala ,haina ubora ambapo amewapasha kuacha propaganda zisizo na tija kwa Taifa.

Aidha ameielekeza DAWASA na TANESCO kukimbilia fursa ya kutoa huduma ya maji na umeme kwa wawekezaji pasipo kuwakwamisha huduma hizi ili wazalishe zaidi na serikali ipate mapato makubwa.

Akitembelea kiwanda cha korosho Terra cashew kilichopo ,Tanita wilayani Kibaha mkoani Pwani, Bashungwa alieleza watu hao hawalitakii mema Taifa. Aliweka bayana kwamba, tayari kwa sasa kuna korosho ya kutosha na yenye ubora katika maghala 37 nchini . 

“Nchi yetu inategemea zao hili la kibiashara wakitokea watu wapotoshaji inakuwa haileti maana na kushusha sifa ya nchi katika biashara ya zao hilo”. “Nilitembelea maghala hayo na wataalamu wangu, tumejiridhisha ,korosho yetu ni nzuri kwa grade ya I na ya II na ipo katika thamani”alisisitiza Bashungwa. 

Akizungumzia suala la ubanguaji korosho ,Bashungwa alibainisha ,watu wanapata ajira katika ubanguaji na kukuza pato la Taifa,kuelekea katika uchumi wa kati. Alisisitiza ubanguaji wa viwango na ubora kwa wakati ili kuwa na korosho yenye ubora. 

Wakati huo huo ,Bashungwa alitembelea kiwanda cha KEDS ambacho kinazalisha soft care (pempas) na sabuni za unga na kutajiwa changamoto ya upungufu wa umeme na maji ya uhakika. 

“Endapo wakibaniwa huduma hizi uzalishaji unapungua tuvutie wawekezaji,hii ni biashara sio kama tunawapa msaaada mjue kama hawa hawazalishi basi na serikali inakosa mapato” . 

Nae mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Silvestry Koka alisema, mpango uliowekwa na serikali kwenye maghala na kuhakikisha wakulima hawapunjwi ni mpango mzuri kwa maslahi ya wakulima na Taifa. 

Koka alieleza ,hao wanaopotosha juu ya korosho iliyopo kwenye maghala zimeoza na kuharibika wapuuzwe. Awali Ofisa Utawala wa Terra Cashew ,Peter Christopher alitaja changamoto zinazowakabili ni ucheleweshaji wa kutolewa makontena ya mitambo na vipuri bandarini kwa takriban miezi mitatu na zaidi. 

Pia tatizo likiwa kupewa taarifa zisizo kamilika mara kwa mara kuhusu nyaraka wanazozihitaji . Peter alisema kwa sasa kiwanda hicho kina ajira rasmi 120 na ajira zisizo rasmi 300.

TUME YA MADINI YANG’ARA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

0
0
Leo tarehe 30 Juni, 2019 Tume ya Madini kwa kushirikiana na wadau wa madini imeendelea na utoaji wa elimu katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba kwa mwaka 2019 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Taasisi za Serikali zinazoshiriki katika banda la Tume ya Madini ni pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Masuala ya Madini na Gesi Asilia (TEITI) 

Kampuni za madini zinazoshiriki katika Banda la Tume ya Madini ni pamoja na Williamson Diamonds Limited, Shanta Mining Co. Limited, Geita Gold Mining Limited, TANSHEQ, Marmo & Granito Mines (T) Limited na Afro Gems Limited

Hospitali ya Benjamin Mkapa Yapongezwa kwa Kuunda Baraza la Wafanyakazi

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akikata utepe kuashiria rasmi uzinduzi rasmi wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akimkabidhi Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Bw. Maudhi Mayunga Mkataba wa Utendaji Kazi alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akimkabidhi Mwakilishi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Bi. Asha Mkataba wa Utendaji Kazi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika. Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Zainabu Chaula akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa mara baada ya kuzindua Baraza hilo mapema hivi karibuni jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO)

Tanzania na Msumbiji wakubalina Kushirikina kuondoa Wahalifu.

0
0
Joseph Mpangala,Mtwara.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saimon Sirro amekutana na Mkuu wa Polisi Kutoka Msumbiji Bernardo Rafael na kufanya Mazungumzo kuhusiana na Mauaji ya Watanzania 9 yaliyotokea tareh26 Mwezi huu katika Kijiji cha Mtole Nchini Msumbiji.

Katika Mazungumzo yao wamekubaliana Kufanya kazi pamoja ikiwepo kufanya operesheni za pamoja ili kupunguza Uhalifu.

Wakiongea Mara baada ya Kikao Hicho Mkuu wa Jeshi la Tanzania IGP Saimon Sirro amesema wahalifu hawana Mipaka hivyo ni lazima kushirikiana kwa pamoja ili kuofanikisha uwepo wa Amani kwa Nchi zote mbili.

"Tumekubaliana kimsingi ya Kwamba wahalifu hawana Mipaka kwa hiyo na Sisi mipaka Isitufanye tukashindwa  kupambana na Wahalifu na hasa haya makosa ya kuvuka Mipaka ni Lazima Tushirikiane na kikubwa zaidi ni kubadilisha taarifa na kufanya Operesheni Pamoja"IGP Sirro.

Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Msumbiji amesema kuwa Kwa ushirikiano watahakikisha wanafanya upelelezi ili kiweza kubaini watu hao wamepata wapi mavazi ya Kijeshi ya Nchini Humo.

" Tunafanya Investigation kujua nini kimetokea kwa tumekuja hapa kuhangaikia mambo yenyewe tufanyekazi pamoja tujue Wamepata wapi Uniform za jeshi la Taifa la kwetu"Bernardo IGP wa Msumbiji.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Msumbiji IGP Bernardino Rafael  akizungumza jambo mbele ya Waandishi wa Habari kufuatia mauaji ya watanzania yaliotokea Juni 26 mwaka huu katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbi,kulia ni  Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Simon Sirro 
 Picha ya Pamoja 
 Pichani ni mkuu wa jeshi la polisi nchini Msumbiji IGP Bernardino Rafael leo wakisalimiana na mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mtwara kwa ajili ya kuja kuweka mambo sawa kufuatia mauaji ya watanzania yaliotokea Junin 26 mwaka huu katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU).

 Pichani ni Mkuu wa jeshi la polisi nchini Msumbiji IGP Bernardino Rafael kushoto leo wakipeana mikono ya salamu na mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Simon Sirro kulia mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mtwara kwa ajili ya kuja kuweka mambo sawa kufuatia mauaji ya watanzania yaliotokea Junin 26 mwaka huu katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU).

VETA YAJIZATITI KWENDA NA KASI YA AWAMU YA TANO KATIKA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA

0
0
*Yajikita katika kuwanoa vijana zaidi ili waweze kujiajiri wenyewe kupitia viwanda

Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv
KATIKA kuadhimisha maonesho  ya 43 ya biashara maarufu Kama sabasaba Mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA)wamejizatiti katika kuendana na kasi ya awamu ya tano ambayo kwa kiasi kikubwa imejikita zaidi katika kujenga uchumi wa viwanda na kulipeleka taifa katika uchumi wa Kati.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Michuzi Tv mara baada ya kuwatembelea katika banda lao la maonesho katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam, wadau mbalimbali wameeleza namna VETA inavyoshiriki kwa kiasi kikubwa katika kuchangia ukuaji wa kiuchumi hasa kwa kuzalisha vijana waliobobea katika fani mbalimbali.

Akieleza namna wanavyoshiriki katika shughuli za kilimo Gema Ngoo ambaye ni mkufunzi wa masomo ya kilimo amesema kuwa wamekuwa wakitoa mafunzo mbalimbali juu ya kilimo bora na cha kisasa zaidi ili kuweza kuzalisha mazao yanayoendana na soko kwa Sasa.

"Maarifa mengi yanatolewa kwa vijana na sio katika kilimo pekee pia na namna ya kupambana na wanyama waharibifu, hapa tuna ndege aina ya tai ambaye  ametengenezwa kitaalamu na anaweza kutembea takribani katika hekta kumi kufukuza wanyama waharibifu, pia tuna mafunzo ya umeme, upishi, useremala na vingine vingi" ameeleza Ngoo.

Aidha amesema kuwa VETA wataendelea kushirikiana na serikali na taasisi nyingine ili kuhakikisha azma ya serikali ya awamu ya tano inafikiwa na amewataka vijana kutembelea katika banda lao ili waweze kupata ujuzi wa namna ya kujiajiri wenyewe.

Vilevile William Mnuo ambaye ni mkufunzi wa magari hasa magari makubwa yakiwemo mabasi ameeleza kuwa wapo makini katika kuhakikisha wataalamu hasa madereva wanaozalishwa kutoka VETA wanakuwa wa mfano na mabalozi bora kwa wenzao.

Mnuo amesema kuwa maarifa na ustadi unaotolewa na VETA kote nchini umelenga katika kuwakomboa vijana kutoka katika  mawazo ya kuajiriwa na kuweza kujiajiri wenyewe.
 William Mnuo ambaye ni mkufunzi wa magari makubwa kutoka VETA akizungumza na Michuzi Tv ambapo amesema kuwa wataendelea kutoa mafunzo wa vijana ili kuzidi kuzalisha vijana waliobobea katika fani mbalimbali zinazotolewa na vyuo hivyo vya ufundi, leo jijini Dar es Salaam.
 Gema Ngoo mkufunzi wa masuala ya kilimo akizungumza na Michuzi Tv na kueleza kuwa vijana wasitegee zaidi katika kujiajiri kwani mafunzo yanayotolewa na VETA ni mtaji tosha wa kuweza kujiajiri, leo jijini Dar es Salaam.
 Rose Mushi mwanafunzi wa VETA mwaka wa pili akitoa maelekezo ya namna mashine ya kuoka nyama waliyoibuni inavyofanya kazi, leo jijini Dar Es Salaam.
Sussack Mbulu mwalimu wa VETA kutoka Mkoa wa Ruvuma akitoa maelekezo ya namna mashine ya kubangulia kwa wakulima wadogo aliyoibuni inavyofanya kazi, leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images