Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

Michepuko ndio chanzo Cha kuongezeka migogoro ya kifamilia - Ripoti

$
0
0

Na Humphrey Shao, Michuzi TV



Imeelezwa Michepuko ndio chanzo Cha kuongezeka migogoro ya kifamilia ambapo kuanzia March 2018/2019 Mashauri ya ndoa 16832 yalipokelewa        
Kulinganisha na Mashauri 13,382 yaliyolipotiwa 2017/18

Hayo yamesemwa na Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr.Naftar .B. Ng'ondi Kamishna ustawi wa Jamii katika mafunzo ya agenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi /walezi katika malezi na matunzo ya familia Nchini Tanzania

Dr.Naftar Amesema changamoto za kukithiri vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto na wanawake hali ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na kukithiri kwa mmong'onyoko was maadili kwa wanafamilia.

"Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya ofisi ya kamishna wa ustawi wa Jamii kwa miezi Tisa kuanzia julai 2018 Hadi Marchi 2019 Mashauri ya migogoro ya ndoa 16832 ilipokelewa kulinganisha namashauri 13,382 mwaka 2017/18"Amesema  Dr Naftar.

Amesema migogoro hiyo inaathiri ukuaji wa Watoto , ustawi na Maendeleo ya familia,kiuchumi husababisha wanafamilia kusahau wajibu wao kwa familia .

Anataja kuwa kwa mujibu wa matokeo ya ukatili wa taharifa za jeshi la polisi nchini kwa mwaka 2018 matokeo ya ukatili 14,419 yameripotiwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.7 ya vitendo vya ukatili kwa Watoto nchini 

"ikiwemo ubakaji ,5,557,mimba 2,692,kulawiti 1,159,shambulio 965 na kujeruhi 705 huku mikoa inayoongoza ni Tanga,Mbeya , Mwanza,Arusha na Tabora"

Anasema kuwa mikoa ya kipolisi yenye takwimu kubwa ni za ukatili ni Kinondoni(2,426),Dodoma(1283),Tanga 1064,Temeke 984 na Arusha 972.

Amesema ni muhimu kujikumbusha na kujengeana uwezo juu ya malezi Bora,kuboresha mawasiliano katika familia kama njia ya kutambua changamoto zinazowakabili Watoto na wanafamilia wote ili kuzitafutia ufumbuzi mapema.

Asha Abdalla akabidhi vifaa vya kazi vyenye thamani ya Shilingi Milioni 1.5 kwa Katibu wa UWT Wilaya ya Amani

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdalla Juma pamoja na Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee wakiwa wamebeba Komputa na Printer zenye Thamani ya Shilingi Milioni 1.5 zilizotolewa na Mbunge huyo.
MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdalla Juma (kushoto),akikabidhi Vitendea kazi kwa Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee ambavyo ni Komputa Moja na Printer Moja ya kisasa ya rangi vyenye thamani ya shilingi Milioni 1.5 Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee(kushoto).
KATIBU wa CCM Wilaya ya Amani Ali Salum Suleiman akitoa shukrani kwa Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdalla Juma na kuahidi kuwa miongozo aliyotoa kupitia hotuba yake itafanyiwa kazi kwa Vitendo.

KONGAMANO LA MAOMBI MAALUM YA KUOMBEA VIONGOZI WA NCHI LAFANYIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Huduma ya maombi na maombezi ya Radio safina jijini Arusha imeongoza mamia ya watu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi ya Tanzania kushiriki katika kongamano la maombi maalum ya kuombea viongozi wa nchi ili waweze kuongoza nchi katika misingi inayompendeza Mungu.

Akizungumza na vyombo vya habari Makamu  Mkurugenzi wa huduma hiyo Bi.Hellen Lema amesema kuwa dhima kubwa ya maombi hao ni kuliweka taifa ya Tanzania katika kusudi na mpango wa Mungu utakaowafanya wananchi kunufaika na rasilimali walizonazo.

Aidha amesema kuwa maombi hayo ni maombi ya Esta ambayo yamelenga kusafisha njia kwaajili ya uchaguzi wa mwaka ujao ili uweze kufanyika kwa haki pasipo watu kugombana 

Kwa upande wake mtumishi Paschal Thomas ambaye ndiye aliyeongoza maombi hayo amesema kuwa kusudi la maombi hayo ni kuzuia mauti inayotengezwa na watu wasio na hofu na mungu hivyo wanatarajia baada ya maombi hayo kuona watanzania wa mataifa mengine kubadilika na kuenenda kama ambavyo mafundisho yao yanyofundishwa.

Naye mmoja wa wananchi Bernad ambao Kivuyo wamefika katika kongamano hilo amesema Bernard Kivuyo amesema kuwa wingi wa watu waliohudhuria katika viwanja hivyo anaamini kuwa Mungu anaenda kuwatoa sehemu moja kwenda nyingine kimafanikio.
Wananchi kutoka maeneo  mbalimbali ndani na nje ya Tanzania walio hudhuria katika kongamano la kuombea viongozi wa nchi ya Tanzania lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid Memorial Stadium Arusha

JITIHADA ZA SERIKALI KUPUNGUZA UMASIKINI ZAFANIKIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akipeana mkono na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), jijini Dodoma. 
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Jijini Dodoma, lililozinduliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia), akimkabidhi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kitabu cha matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa mwaka 2017/18, jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa sita kulia) na viongozi wengine wakiwa wamenyanyua kitabu cha matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya binafsi kwa Tanzania Bara wa mwaka 2017/18, jijini Dodoma 

******************* 

Na. Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma 

Kiwango cha umaskini nchini Tanzania kimepungua kwa asilimia mbili, ikiwa ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kupunguza umasikini kwa wananchi hasa wa hali ya chini. 

Hayo yamebainishwa wakati Waziri Mkuu Mhe. Kassimu Majaliwa, akizindua ripoti ya matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya mwaka 2017-18 na jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Mkoani Dodoma. 

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa, amewataka Watakwimu nchini kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo mbalimbali wakati wa kutekeleza majukumu yao hususan kuzalisha na kusambaza takwimu zenye viwango vya kitaifa na kimataifa ili kuisaidia Serikali kujua mahitaji yaliyopo. 

“Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, inatambua umuhimu wa takwimu zenye ubora, kwa kuwa ndiyo macho na masikio ya Serikali katika kufuatilia na kutathmini mipango ya maendeleo ya nchi”, alieleza Mhe. Majaliwa. 

Mhe. Majaliwa, alisema kuwa takwimu bora hutoa fursa kwa Serikali kufanya mapitio ya sera, mipango na mikakati kulingana na hali ilivyo kwa wakati husika na pia kupima ilikotoka, ilipo na kutabiri inakoelekea hivyo kupima mwenendo wa jitihada za Serikali. 

Aidha aliiagiza Ofisi ya Taifa ya Takwimu Nchini (NBS), kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinakuwa na Afisa Takwimu ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu kwa wakati ili kuweza kusaidia maendeleo nchini. 

Kwa upande wake Naibu wa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa Wizara yake imepewa jukumu la kusimamia Uchumi wa Taifa, lakini haiwezi kusimamia uchumi bila kuwa na takwimu rasmi na sahihi. 

“Katika kipindi cha takribani miaka mitatu na nusu tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, umaskini nchini umepungua hadi kufikia takribani asilimia 26 kutoka asilimia 28, ikiwa ni sawa na kupungua kwa asilimia mbili”, alisisitiza Dkt. Kijaji. 

Dkt. Kijaji alisema kuwa matokeo ya tafiti yaliyozinduliwa na Mhe. Kassim Majaliwa, yameonesha kupungua kwa umaskini wa watanzania waishio vijijini kwa asilimia 3.1 kati ya mwaka 2011/12 na mwaka 2017/18. 

Alieleza kuwa hayo ni matunda ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Kiongozi wake, Mhe. Rais, Dkt. Magufuli. Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa, alisema kuwa utafiti wa mwaka 2017/2018 umetumia teknolojia ya kisasa inayojulikana kama Survey Solution ambayo ni tofauti na njia ya awali ya kutumia madodoso yaliyochapishwa hivyo kupunguza gharama za kufanya tafiti za kijamii. 

Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa akiwemo Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bw. Denis Biseko, wameipongeza Serikali kwa kupunguza kiwango cha umasikini kwa takribani asilimia 2, na pia wamepongeza matokeo ya utafiti huo ambao umezingatia usawa wa kijinsia hivyo kuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa ni moja ya lengo la mashirika hayo.

GAVANA SHILATU ASHANGAZWA NA DIWANI KUTOFUATILIA UPATIKANAJI WA MIKOPO YA VIJANA, WANAWAKE NA WALEMAVU

$
0
0


Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amembana Diwani wa Chama Cha Wananchi (CUF) Kata ya Mkoreha Mhe. Ahmad Ally Ndende juu ya utolewaji wa mikopo ya Halmashauri kwa Vijana, Wanawake na Walemavu ili kuwakwamua Wananchi kiuchumi. 

Hayo yamejitokeza kwenye mkutano na Wananchi wa Kijiji cha Dinyeke kata ya Mkoreha ambapo Gavana Shilatu aliitisha ili kusikiliza na kutatua kero za Wananchi zinazowakabili. 

Gavana Shilatu alimuuliza Diwani huyo kuelezea ni vikundi vingapi mpaka sasa vimenufaika na mikopo nafuu kwa Vijana, Wanawake na Walemavu toka Halmashauri ikiwa yeye ni Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya kata. 

*_”Hakuna wanufaika wa mikopo hiyo ya 10% toka Halmashauri kwani vikundi vingi havijasajiliwa na havina miradi.”_* Alijibu Diwani Ndende. 

Gavana Shilatu alisisitiza kazi ya viongozi ni kuonyesha njia ya kuwakwamua Wananchi kiuchumi pasipo kukwepa majukumu wala kuingiza ubaguzi. 

Gavana Shilatu alisisitiza kuwa viongozi tunatakiwa kuhamasisha Vijana, wanawake na walemavu kuwatengenezea mazingira ya kuwa na vikundi vyenye katiba vilivyosajiliwa na vyenye shughuli maalumu ili waweze kupata mikopo hiyo. 

_”Sisi viongozi tunajukumu la kuwaonyesha njia Wananchi na si kutumia mwanya wa kutokuelewa kwao kama njia ya kuwakosesha *FURSA MUHIMU* kama ya Mikopo nafuu toka Halmashauri. Na mikopo hii inatolewa kwa haki pasipo ubaguzi wa kiitikadi.”_ Alisisitiza Gavana Shilatu. 

Katika mkutano huo ulihudhuliwa na Diwani kata ya Mkoreha, Mtendaji Kata ya Mkoreha, Mtendaji Kijiji cha Dinyeke, Serikali ya Kijiji cha Dinyeke pamoja na viongozi wa Vitongoji.

SEKTA BINAFSI ZAASWA KUCHANGAMKIA FURSA KATIKA MKUTANO WA SADC

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt, Faraji Kasidi Mnyepe amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa benki mbalimbali, wawakilishi wa kampuni za utalii, viongozi wa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafiri na wafanyabiashara mbalimbali jijini Dar Es Salaam. 

Katika Mkutano huo, Dkt. Mnyepe aliwasihi wawakilishi hao kujipanga vizuri ili waweze kuchangamkia fursa za Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika nchini Mwezi Agosti 2019. Aliwasihi kujipanga vizuri katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya usafiri, utalii, burdani na vyakula. Dkt. Mnyepe alisisitiza umuhimu wa Watanzania kuendeleza utamaduni wa ukarimu na kuwa waaminifu na uadilifu katika kuhudumia ugeni huo mkubwa ambapo inakadiriwa zaidi ya watu elf moja watakuja nchini. 
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya maandalizi ya Habari, Machapisho na Matangazo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi Kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Zamaradi Kawawa. 
Ujumbe ulioshiriki kikao hicho ukisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu. 
Mkutano ukiendelea. 

WAZIRI MKUU: UJENZI WA NYUMBA BORA WAONGEZEKA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kaya zinazoishi kwenye makazi bora zimeongezeka kwa asilimia 16 katika kipindi cha miaka sita ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2011/2012. 

“Kaya zinazoishi kwenye nyumba zenye paa la kisasa zilizoezekwa kwa bati zimeongezeka kutoka asilimia 68 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 84 mwaka 2017/2018 wakati kuta za kudumu zimeongezeka kutoka asilimia 46 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 79 mwaka 2017/2018,” amesema. 

Ametoa kauli hiyo leo jioni (Jumamosi, Juni 29, 2019) wakati akizungumza na viongozi na wananchi mara baada ya kuzindua Jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu lililoko Makulu, Manispaa ya Jiji la Dodoma. 

Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Dkt. John Pombe Magufuli, pia alizindua ripoti ya matokeo ya viashiria muhimu vya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara ya mwaka 2017/18. 

Waziri Mkuu alisema takwimu hizo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu na zinaonyesha jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kujenga Tanzania ya Viwanda zinaendelea kuwanufaisha wananchi kwa zinagusa moja kwa moja katika sekta ya ujenzi kama vile viwanda vya saruji, mabati, nondo, na vinginevyo. 

Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali ni kuona kila Mtanzania anaishi kwenye makazi bora kwani makazi bora huimarisha afya za wakazi na afya bora ni mtaji wa msingi kwa kila mwanadamu kwa kufanya kazi na hivyo kukuza uchumi. 

“Tuendelee kuunga mkono jitihada za Serikali kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje waje wawekeze kwenye viwanda vya saruji, mabati, na marumaru ili kuongeza uzalishaji na kuleta ushindani wa bei ambao utawanufaisha watu wengi na kuwapatia fursa za kujenga makazi bora ya kuishi,” alisema. 

Waziri Mkuu alisema mbali na makazi bora, utafiti huo umebainisha uwepo wa ongezeko la kaya zilizounganishwa kwenye umeme wa Gridi ya Taifa kutoka asilimia 18 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 29.1 mwaka 2017/2018. “Jitihada za Serikali chini ya Mpango wa Umeme Vijijini (REA), zinaendelea na utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Awamu ya Tatu wa kusambaza nishati vijijini unaojumuisha vijiji 7,873 katika wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara ambao unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ulioanza mwaka wa fedha 2016/17 na unategemewa kukamilika mwaka 2020/2021,” alisema. 

Akizungumzia hali ya umaskini barani Afrika, Waziri Mkuu alisema kiwango cha umaskini wa kipato cha Watanzania hakitofautiani sana na nchi nyingine ndani ya bara hilo. “Tukiangalia hali ya umaskini katika nchi nyingine za Bara la Afrika kwa miaka ya hivi karibuni, nikianza na Kenya kiwango cha umaskini wa mahitaji ya msingi ni asilimia 36.8 (mwaka 2015), Afrika ya Kusini asilimia 55.5 (mwaka 2015), Rwanda asilimia 38.2 (mwaka 2016), Zambia asilimia 54.4 (mwaka 2015), Ethiopia asilimia 23.5 (mwaka 2015) na Zimbabwe asilimia 72.3,” alisema. 

Alisema kupunguza umaskini kwa nchi yoyote ile kunapaswa kuhusishwa na uwekezaji kwenye sekta nyingine za kiuchumi ambazo hugusa na kuwanufaisha wananchi walio wengi. “Nitumie fursa hii kusisitiza kuwa umaskini ni changamoto kwa dunia nzima na hasa kwa nchi zinazoendelea. Nchi zilizo na hali mbaya zaidi ni zile zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara kama takwimu rasmi zinavyoonesha.” 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema ni lazima Serikali iimarishe upatikanaji wa takwimu kwa kuajiri maafisa takwimu wanaowajibika moja kwa moja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu badala ya kumtegemea mtu anayewajibika kwa Mkurugenzi wa Halmashauri. 

“Leo hii hatuna Afisa Takwimu katika kila Halmashauri, na matokeo yake hatuna mfumo mzuri wa kupata taarifa kuanzia ngazi ya chini. Tuweke utaratibu ili hawa watu wawepo na kila Afisa takwimu awajibike kupeleka taarifa yake kwa Mtakwimu Mkuu kila wakati.” 

“Nilipokuwa Naibu Waziri TAMISEMI ninayeshughulikia elimu, nikiagiza takwimu fulani, kuzipata ilikuwa inachukua zaidi ya wiki mbili, na hiyo ni kwa Halmshauri moja tu. Na wakati mwingine, taarifa inakujia wakati umeshasahau kuwa ulitoa agizo uletewe.” 

Mapema, akitoa taarifa juu ya utafiti huo, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Dkt. Albina Chuwa alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani ambazo kiwango cha umaskini kimeendelea kushuka na kufikia tarakimu moja. 

Alisema utafiti huo uliofanywa na ofisi yake kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, baadhi ya balozi na mashirika ya Umoja wa Mataifa ulilenga kupata makadirio ya viwango vya umaskini ili kufuatilia, kupima na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa. 

Alisema katika utafiti huo, walitumia teknolojia ya kisasa iitwayo survey solution ambayo imesaidia kupunguza gharama za utafiti za kupeleka madodoso na magari. “Tulitumia vishkwambi (tablets) na kupunguza mzigo wa kubeba na makaratasi au kukaa kujumlisha taarifa,” alisema,

SERIKALI YAKABIDHIWA MADINI YENYE THAMANI YA MABILIONI YA FEDHA

$
0
0
*Ni yale yaliyokuwa yanatoroshwa na kusafirishwa bila kibali
*Yamo madini ya dhahabu, Tanzanite, mawaziri watatu wafunguka


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JUMLA ya madini yenye thamani ya Sh.3,125, 704,456.12 yamekabidhiwa kwa Serikali kupitia Hazina baada ya kutaifishwa kutokana na kubainika yalikuwa yanatoroshwa nchini.

Mbali na kukabidhiwa madini na vito, pia Serikali imekabidhiwa fedha za kigeni ambazo nazo zimetaifishwa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madini, vito na fedha hizo kwa Katibu Mkuu Hazina Dotto James, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amefananua kuwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) katika vipindi tofauti kati ya mwaka 2017 na mwaka 2018 imeendesha kesi mbalimbali.

Amesema kesi hizo zilikuwa zinahusiasana na utoroshaji au kukutwa na madini bila kuwa na kibali na katika uendeshaji wa kesi hizo washtakwa walitiwa hatiani na kuamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo gerezani pamoja na amri ya kutaifishwa madini na fedha walizokutwa nazo wakati wakisafirisha madini hayo.

"Madini yaliyotaifishwa ni kilo 25.546 za dhahabu ,zaidi ya kilo 76,020.20(tani 76) za Colored gemstone, Tanzanite pamoja na fedha za kigeni za mataifa mbalimbali 15 zenye thamani ya Sh.1,023,608, 515.12.

"Kwa kuwa madini hayo yametunzwa sehemu mbalimbali kiasi kwamba uwezekano wa kupotea au kumbukumbu zake kupotea na kwa kuwa mali zote zinazotaifishwa zinakuwa mali za Serikali na Katibu Mkuu Hazina ndiye msimamizi wa mali hizo" ameeleza.

"Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) anakabidhi kilo 25.5 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani 913,954.72 sawa na Sh.bilioni 2,102,095,941,"amesema Mganga.

Akifafanua madini na vito, amesema kuna tani 76 na Carrats 2849 zenye thamani ya Dola za Marekani 2,638,349.95 sawa na Sh.bilioni 6,068,204.885 na Carrats 2,849 zenye thamani ya Dola za Marekani 3,803.32 sawa na Sh. milioni 888,409,000.

Pia Tanzanite gramu 888 zenye thamani ya Dola 3,197 sawa na Sh.bilioni 7,353,348 na fedha za kigeni za mataifa 15 ambazo ni sawa na Sh.1,023,608,515.12.

Hata hivyo Mganga baada ya kukabidhi madini hayo na fedha kwa Katibu Mkuu Hazina ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa watumishi wa madini ambao wanashindwa kutoa taarifa kwa wakati kuhusu madini na kuwataka kufanya hivyo ili awe nafasi ya kufuatilia na kuchukua hatua mapema.

Akizungumza baada ya kukadhiwa madini na fedha hizo, Katibu Mkuu Hazina Dotto James amewahakikishia Watanzania wote kuwa mali yao iko salama na itatumika kufanya maendeleo kulingana na uamuzi wa Serikali kuhusu mali hizo.

"Tunaamini Benki Kuu ya Tanzania(BoT) itatunza mali hizi bila wasiwasi wowote kama ambavyo wamekuwa wakitunza kwa siku zote na pale ambapo Serikali itaamua namna ya kuzitumia kwa lengo la kuimarisha huduma kwa wananchi wake basi itazichukua,"amesema James.

Wakati huo huo Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango amesema inasikitisha kuona watu wasiokuwa na nia njema wakitorosha madini wakati wananchi wakiendelea kuteseka."Kwa kweli inasikitisha sana kuona watu wanaendelea kutorosha madini wakati wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.Bungeni wabunge kila siku wanalalamika maji! maji! halafu kuna watu wanatorosha madini." ameeleza.

"Ni aibu Waziri wa Fedha kuendelea kuomba misaada wakati mali tunazo za kutosha...tena misaada mingine masharti yake ni magumu. Nitoe rai kwa Watanzania tuwe macho na wote ambao wanatabia ya kupora mali zetu na kuzitorosha,"amesema Waziri Mpango.

Waziri wa Madini Dotto Biteko ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wote ambao wamefanikisha kupatikana kwa madini na fedha hizo huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa wachimbaji madini ambao wenye tabia ya wizi wa kutosha madini watambue kwa sasa hawana nafasi tena.

Pia amesema kuna baadhi ya watanzania ambao wamekuwa wakifanya utapeli kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kwa kujifanya wana madini na kisha kuchukua fedha za raia wa mataifa mengine, ambapo amesema wenye tabia hiyo wajue siku zao zinahesabika kwani Serikali haiko tayari kuendelea kuwavumilia wenye tabia hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Augustino Mahiga amesema Tanzania kuna madini mengi ambayo hayawezi kuisha leo wala kesho na vema Watanzania wakawa macho kwa kuhakikisha madini hayo yanatunzwa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali sehemu ya vipande vya Madini ya Dhahabu ambayo ilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Agustine Mahiga, Waziri wa Madini Dotto Biteko pamoja na Kamishina wa Madini Profesa Abdukalim Mruma wakiwa wamishika vipande vya madini ya dhahabu ambayo Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amezikabidhi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, vito na Fedha za mataifa mbalimbali zilizokamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akionyesha juu kwa Mawaziri na Wanahabari Fedha za Kimarekani (Dollar) kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Fedha hizo pamoja na Madini na Vito ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali sehemu ya Fedha za Mataifa mbalimbali pamoja na Madini na Vito ambavyo vilikamatwa na kutaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akikagua sehemu ya fedha za mataifa mbalimbali mara baada ya kukabidhiwa kwa niaba ya Serikali Fedha na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga amabazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini vikiwemo pia Madini na vito mbalimbali, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akionyesha juu kwa Mawaziri na Wanahabari moja kipande cha madini ya Pie light kabla ya kumkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James kwa niaba ya Serikali Madini, Vito na Fedha za mataifa mbalimbali ambavyo vilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 

Masanduku yaliyoifadhiwa Madini,Vito pamoja na fedha za Mataifa mbalimbali zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi zikiingizwa Ukumbini tayari kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) Biswalo Mganga kukabidhi kwa Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BOT). 
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dotto James akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhiwa kwa niaba ya Serikali Madini, vito mbalimbali na Fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt.Agustine Mahiga akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi Madini, vito mbalimbali na Fedha kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 
Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wanahabari katika hafla ya kukabidhi Madini, vito mbalimbali na Fedha kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga ambazo zilikamatwa na kuitaifishwa kwa mujibu wa Sheria zilizotokana na Kesi mbalimbali za Uhujumu Uchumi nchini, katika ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam Juni 29, 2019 

PICHA NA IKULU

WENYEVITI WOTE WA SERIKALI ZA MTAA MNAALIKWA KUSHIRIKI NA KUSHUHUDIA UWEKAJI SAINI MIRADI MIKUBWA YA USAMBAZAJI MAJI

SERIKALI YADHAMIRIA KUIMARISHA HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Baadhi ya Viti Mwendo “Wheelchair” na Fimbo Nyeupe “White Cane” walizokabidhiwa Watu wenye Ulemavu. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Bi. Paulina Mwalimu mara baada ya kuwakabidhi vifaa saidizi hivyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TCC, Bw. Godson Killiza. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watu wenye Ulemavu waliokabidhiwa vifaa saidizi. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu wakati wa hafla ya kupokea vifaa saidizi kwa ajili ya Watu wenye Ulemavu iliyofanyika katika Viwanja wa Nyerere Square Jijini Dodoma.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bw. Derick Amahoro akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama kuhusu mradi wa ugawaji vifaa saidizi kwa watu wenye Ulemavu ikiwa ni utoaji wa huduma za kijamii.


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kuboresha huduma na upatikanaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu. 

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa saidizi kwa ajili ya watu wenye ulemavu iliyoandaliwa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC Plc), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alisema kuwa kundi la Watu wenye Ulemavu lilikosa baadhi ya fursa hapo awali kutokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo. 

“Tunafahamu watu wenye ulemavu wanauhitaji wa huduma bora na vifaa saidizi vitakavyo wawezesha kumudu mazingira ili nao waweze kujumuika katika nyanja zote,” alisema Mhagama 

Alifafanua kuwa takwimu na Sensa ya Taifa ya Watu wenye na Makazi ya mwaka 2012, imekadiria idadi ya watu Tanzania ni zaidi ya milioni 44 ambapo milioni 2.5 ni Watu wenye Ulemavu. 

Waziri Mhagama alisema, Serikali imeazima kuboresha huduma kwa Watu wenye ulemavu ikimemo kutoa elimu bure na kuimarisha elimu jumuishi, kujenga vituo vya afya na hospitali pamoja na utoaji wa matibabu bure kwa watu wenye ulemavu wasio na uwezo. 

Mbali na hayo, alihimiza wadau pamoja na makampuni kuona umuhimu wa kuhudumia kundi la watu wenye ulemavu wakiwa wanatoa huduma mbalimbali za kijamii. 

Aidha, alipongeza Kampuni ya Singara Tanzania (TCC) kwa msaada huo na kuwashauri waendelee kukumbuka kundi hilo. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TCC, Bw. Godson Killiza alisema kuwa watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa na nijukumu kama wadau kuwasaidia na kuwaunga mkono kwenye masuala mbalimbali. 

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bi. Ummy Nderiananga alieleza kuwa juhudi za Serikali katika kushirikiana na wadau itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto za Watu wenye Ulemavu katika kufanikisha masuala yao.

DIWANI YINDI AJA NA MPANGO WA KUKUZA MICHEZO DODOMA

$
0
0

Na Charles James,Globu ya jamii

Katika kukuza vipaji vya vijana katika Mkoani Dodoma, Diwani wa Kata ya Buigiri iliyopo Wilaya ya Chamwino Kenneth Yindi ameandaa mashindano ya mpira wa miguu yatakayoshirikisha tmu mane za kata hiyo.

Mashindano hayo yaliyopewa jina la Buchimwe Cup 2019, yatazinduliwa kesho na Mkurugenzi wa Michezo Nchini, Ado Komba ambapo mshindi wa kwanza atajnyakulia Kombe, Seti Moja ya Jezi na kiasi cha Sh 100,000 taslimu.

" Lengo la mashindano haya ni kukuza vipaji vya vijana wetu, Michezo imekua Ajira kubwa Duniani kote hivi sasa, hivyo kama Diwani nimeoana nianzishe mashindano haya ambayo naamini yatatumika kama fursa kwa wachezaji wetu kuweza kupata Timu kubwa zaidi ya hizi walizonazo sasa.

"Tunashukuru Wizara ya Michezo chini ya Waziri Mhe Harrison Mwakyembe kwa kutuunga mkono katika kufanikisha mashindano haya bila kuwasahau Chama Cha Soka Mkoa (DOREFA)," amesema Yindi.

Ameongeza licha ya Ligi hiyo kuchezwa pia ameandaa mafunzo ya uamuzi kwa waamuzi waliyopo ndani ya Kata yake yenye viwango vinavyotakiwa na Shirikisho la Soka nchini TFF.

" Kwa kushirikiana na wenzetu wa Dorefa tumeandaa pia mafunzo haya kwa waamuzi na watakaofuzu watakabidhiaa vyeti vya kuhitimu, lengo letu ni kukuza Michezo kwenye Mkoa wetu, " amesema Yindi.

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kuwaletea ujenzi wa uwanja wa Kisasa wa Michezo uliopo eneo la Nzuguni ni heshima kwao hivyo hawana budi kuhakikisha sasa wanaandaa vijana wazawa kukua kimichezo ili kuweza kunufaika na uwanja huo.

" Rais Magufuli tunampongeza sana kwa kutupa heshima kubwa ya uwanja wa kisasa, sasa ni jukumu letu sisi wasaidizi wake kuwaandaa vijana wetu kimichezo ili wanufaike na zawadi hii ambayo Rais ametupa sisi watu wa Dodoma," 

Yindi amesema pia kutakua na zawadi Kwa mshindi wa pili na wa tatu, mfungaji na mchezaji bora wa mashindano, kipa bora pamoja na mchezaji bora wa kila mechi.
Diwani Yindi akizungumza kuhusu namna alivyojipanga kukuza vipaji kwenye kata yake

NAIBU WAZIRI KANYASU AIPONGEZA TFS, ATAKA MATUMIZI SAHIHI YA BOTI

$
0
0

Na Ripota wetu ,wa Michuzi TV

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu amezindua boti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko.

Pia Kanyasu ameipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi misitu nchini.

Akizungumza leo Jumamosi Juni 29,2019 wakati wa uzinduzi boti hizo Kanyasu ameitaka TFS iongeze bidii kwa  kubuni matumizi  sahihi ya  boti hizo."Kumekuwa na matumizi tofauti na yaliokusudiwa hivyo inabidi kubuni matumizi na kuwa na nidhamu katika matumizi yaliyokusudiwa" amesema Kanyasu.

Amesema boti hizo zitasaidia kuthibiti  uvunaji holela wa mikoko ambayo ni muhimu kutokana na uhifadhi wa bahari.

Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TFS Meneja Kanda ya Mashariki, Caroline Malundo amesema boti hizo zitatumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko na kuongeza kumekuwa na changamoto nyingi ndani ya hifadhi ikiwemo ukataji wa mikoko na kufanya kilimo cha mpunga.

"Tumekuwa na changamoto nyingi ndani ikiwemo ukataji wa mikoko,kilimo cha mpunga ndani ya delta ya Rufiji pamoja na bandari 77 zisizo rasmi" amesema Malundo.

Kwa upande wa Mmiliki wa kampuni ya  Sam and Anzai Boat Builders iliyotengeneza boti hizo Samweli Luenje amesema wametengeneza boti tatu kwa gharama ya shilingi 600 milioni ambapo tayari moja imeshaanza kazi kati eneo la Nyamisati.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) baada ya kuzindua boti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Constantine Kanyasu akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kuzinduaboti zitakazotumika kuendeleza na kusimamia misitu ya mikoko ambapo ametumia nafasi kuipongeza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kulinda na kuhifadhi misitu.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI HOSPITAL YA BENJAMIN

$
0
0
Na Charles James wa Michuzi Tv- Dodoma

TAASISI  ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa imefungua na kuzindua Baraza jipya la wafanyakazi ikiwa ni mara ya kwanza yangu kuanzishwa kwa Hospitali hiyo kubwa nchini.

Akizungumza na wafanyakazi wa Hospital hiyo, Katibu Mkuu Wizara  ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula ametoa rai kwa Wafanyakazi wa baraza hilo kuwajibika na kufanya kazi kwa kujituma zaidi pamoja na kuonesha uzalendo kwa Wagonjwa.

“Tunajifunza kila siku,kwa hiyo nyie mlioteuliwa mtuwezeshe,haki haipo bila wajibu,na kila mmoja akijituma atatizimiza wajibu  wake,mimi sikumbuki kutumwa na napata shida kum-push mtu,na lazima tutengeneze Mechanism ya watu kufanyakazi bila kutumwa. Hakuna kazi  ya neema na ibada tunayo fanya kama hii, Mtu ana Stress zake,ana shida,hana hela lakini unamfariji,unamtibu,mwisho wa kazi saa 9 ukifanya kazi mpaka saa 11 au saa 1 jioni una dhambi gani.” Amesema Dk Chaula.

Aidha amewataka wafanyakazi kuwa Wepesi katika kutekeleza Majukumu yao na kutowakwaza wagonjwa na wananchi kwa ujumla hivyo ni jambo la busara kupeana Moyo katika kazi ngumu na yenye wito ya  utabibu na kumtegemea Mungu katika changamoto wanazokumbana nazo .

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Afya  Dokta Chaula amesema upendo na huruma ni jambo la Muhimu kwa Maisha ya Binadamu kwani ni Moja ya Kujenga Marafiki wengi  na kusema kuwa hakuna mtu mdogo katika maisha kila mtu ana mchango wake na kinachotofautisha ni Madaraka na Mamlaka tu ila  binadamu wote ni sawa..

“Kwa makusudi tu mtu anakuja  halafu anatoka analia ofisini kwako unajisikiaje,lazima tupendane tuhurumiane tukitengeneza system ya namna hii katika maisha yetu tutakuwa na marafiki wengi kuliko maadui,tusameheane”Alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Baraza la wafanyakazi mkoa wa Dodoma,ambaye pia Mjumbe Taifa wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali kanisa  la Waadventista Wasabato ,[ATAPE] Bw.Mchenya John amesema amesema wataendelea kuyafanyia kazi maelekezo yote muhimu yaliyotolewa huku akizungumzia namna  walivyofanya mchakato wa uanzishaji wa Chuo wa Chuo kikuu cha Dodoma pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa akitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa awamu ya nne Dokta.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha uanzishaji  wa Hospitali hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi  Taasisi ya Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dokta Alphonce Chandika  amesema taasisi hiyo ina takriban miaka mitatu tangu ianzishwe na walikuwa hawajaunda Baraza la Wafanyakazi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wafanyakazi lakini kwa sasa idadi imejitosheleza na wameona kuwa na umuhimu wa kuwa na Baraza ambapo tayari na  katiba na mkataba wa Baraza hilo ilishatengenezwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Zainab Chaula akizungumza na watumishi wa Hospital ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
 Watumishi wa Hospital ya Rufaa ya Benjamini Mkapa wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Zainab Chaula wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi kwenye Taasisi hiyo

WAZIRI MHAGAMA AKABIDHI VIFAA VYA KUTEMBELEA KWA WALEMAVU

$
0
0

Na Charles James wa Michuzi TV 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu na kuhakikisha wanapata huduma bora zinazowahusu bila changamoto yoyote.

Waziri Jenista ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa vya kutembelea Baiskeli 'wheelchair' na fimbo kwa watu wenye ulemavu mkoani Dodoma.

" Niwapongeze sana Kampuni ya Sigara nchini TCC kwa kuandaa tukio hili sambamba na kugawa vifaa hivi maalumu vya kutembelea kwa ndugu zetu wenye ulemavu.

" Hii ni kumuunga mkono Rais wetu Dk John Magufuli katika kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu ambapo tumeshuhudia katika Serikali yake akiteua watu wenye ulemavu kushika nafasi mbalimbali," amesema Waziri Jenista.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa amemshukuru Waziri Jenista kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la makabidhiano ya vifaa hivyo kwani imeonesha jinsi gani Serikali inathamini watu wenye ulemavu.

Nae Naibu Waziri wa Vijana, Ajira na Kazi ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameupongeza Uongozi wa TCC kwa kugawa vifaa hivyo kwa wananchi wake kwani vitawarahisishia majukumu yao.

" Niwashukuru sana TCC mmekua wadau wakubwa katika kuwashika mkono ndugu zetu wenye ulemavu, mara kwa mara mmekua mkitoa misaada ambayo imekua pia ni chachu ya kukuza vipato vyao," amesema Mavunde.

Mkurugenzi wa Sheria wa Kampuni ya TCC, Godson Kiliza ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuwasaidia watu wenye Ulemavu ikiwa ni pamoja na kuwapa vifaa hivyo vya kutembelea pamoja na nyenzo za biashara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watu wenye ulemavu baada ya kupatiwa  vifaa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Ulemavu Jenista Mhagama akizungumza Mjini Dodoma wakati akikabidhi vifaa vya kutembelea Baiskeli 'wheelchair' na fimbo kwa watu wenye ulemavu mkoani Dodoma.
 Waziri Mhagama akikabidhi fimbo kwa moja ya watu wenye ulemavu Jijini Dodoma

WAZIRI KAIRUKI AUTAKA UONGOZI WA KNAUF KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII INAYOWAZUNGUKA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia moja ya malighali zinazotumika katika kiwanda cha KNAUF (Metal Profile) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa kiwanda hicho na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo. Meneja Uzalishaji Bw. Nurdin Bofu akimuonesha jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara kuhusu namna wanavyopakia unga maalumu wa kutengeneza jasi wakati wa ujenzi wakati wa ziara yake. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalai moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kiwanda kinachotengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wakati wa ziara yake kiwandani hapo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika ziara ya kukagua kiwanda cha kutengeneza gypsum board cha KNAUF kilichopo Mkuranga Pwani. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihutubia washiriki wa mkutano wa wafanyakazi wa kiwanda cha KNAUF ili kuzungumza nao masuala ya uboreshaji wa mazingira ya wawekezaji nchini.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza Jasi (Gypsum Board) cha KNAUF kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kwa lengo la kukagua mazingira ya wawekezaji wa kiwanda hicho kwa nia ya kuendelea kuboresha mazingira yao ziara ilifanyika Juni 28, 2019.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihutubia washiriki wa mkutano wa wafanyakazi wa kiwanda cha KNAUF ili kuzungumza nao masuala ya uboreshaji wa mazingira ya wawekezaji nchini wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.Meneja wa Mradi kutoka kiwanda cha KNAUF Bw. Norbert Wagner akimuonesha michoro ya ramani ya kiwanda hicho Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipotembelea na kukagua mazingira yao Juni 28, 2019. 

Meneja Fedha wa kiwanda cha KNAUF akiwasilisha hotuba kuhusu kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki kiwandani hapo. 
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU) 
…………………. 
NA.MWANDISHI WETU – OWM 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuka ameutaka uongozi wa kiwanda kinachotengeneza bidhaa za cha za jasi (Gypsumboard) cha KNAUF kuendelea kushirikiana na jamii inayowazunguka katika kujiletee maendeleo. 
Ametoa kauli hiyo mapema mwishoni mwa wiki hii alipotembelea kiwanda hicho kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani ili kukagua shughuli za uzalishaji zinazoendela pamoja na kusikiliza changamoto za wawekezaji hao na kuweza kujadili masuala ya kuendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. 
Waziri Kairuki aliwataka kuona umuhimu wa kuchangia katika shughuli za kimaendeleo katika maeneo yanayozunguka kiwanda hicho hususan katika uboreshaji wa miundombinu na utoaji wa misaada itakayofikia jamii kwa sehemu kubwa na si mtu mmoja mmoja ili kuleta maendeleo katika eneo kubwa na kuondoa tofauti kubwa za kimaendeleo zisizoendana na maendeleo ya maeneo kiwanda hicho. 
“Ni muhimu sana, na ni busara kuona ni kwa namna gani mnashirikiana na wananchi wanaozunguka eneo hili katika kuleta maendeleo ili kuhakikisha mnakubalika , na kuleta maendeleo ya eneo husika na kuondoa tofauti za kimaendeleo kati ya ustawi wa kiwanda na jamii inayowazunguka”alieleza Waziri Kairuki 
Waziri aliutaka uongozi huo kushiriki kimalilifu katika shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia kuboresha miundombinu inayozunguka mazingira ya kiwanda ili kuendelea kushiriki kwa vitendo na kuunga mkono jitihada za kuendelea eneo hilo. 
Sambamba na hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jumaa Abeld aliomba uongozi wa kiwanda kuona namna ya kuchangia katika maendeleo ya eneo lao kwa kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa sita katika shule ya msingi ya Kitangwi pamoja na madarasa manne katika shule ya msingi ya Kisemvule zilizopo Wialya ya Mkuranga katika mkoa huo. 
“Ombi letu ni kuona namna kiwanda hiki kinavyoweza kuchangia katika maendeleo kwa kutujengea vyumba sita vya madarasa katika shule zinazotuzunguka ili kusaidia uhaba uliopo na kusaidi watoto wetu kujifunza katika mazingira mazuri,”alisema Jumaa. 
Aidha Meneja Masoko wa Kiwanda hicho Bi. Zainab Mwasara aliahidi ifikapo Julai 05 mwaka huu uongozi wa kiwanda utatoa taarifa za utekelezaji wa maombi hayo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 6. 
“Tunaahidi kukutana kama uongozi wa kiwanda ili kujadili na kutekeleza masuala ya msingi ikiwemo hili la ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuendelea kuleta tija kwa uwepo wa kiwanda katika eneo hili,”alisema Mwasara. 
Naye, Meneja Fedha wa kiwanda hicho Bi. Wema Mboga alishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya wawekezaji nchini na kumpongeza ziara ya Waziri katika kutatua na kuahidi kufanyia kazi masuala yaliyoelezwa kuwa ni changamoto kiwandani hapo ikiwemo uhaba wa upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika, kutokamili kwa leseni za uchimbaji kwa wakati, tozo kubwa za malighafi na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji kiwandani hapo. 
AWALI 
Kiwanda cha KNAUF kilianzishwa mwezi Novemba mwaka 2015 kwa lengo la kuzalisha bidhaa za jasi (Gypsum board), gundi za jasi, pamoja na chuma za jasi (metal profile) kufanya kazi na usambazaj.Kiwanda kinafanya kazi katika nchi zaidi ya 80 ambapo katika nchi za kusini mwa Janga la Sahara, Tanzania ni nchi pekee ambayo ina uwekezaji huo kutokana na sababu za mazingira mazuri ya kibiashara na uwekezaji pamoja na sababu za kijiografia.Kampuni imeajiri wazawa 150 katika Nyanja zote kwa kulenga ifikapo 2020 kiwanda kiweze kuendeshwa na wazawa pasipo kutegemea wataalam kutoka nje.

DAR ES SALAAM NA TABORA ZATWAA UBINGWA WA MPIRA WA KENGELE

$
0
0

Washiriki wa mchezo wa mpira wa Kengele na mabingwa wapya timu ya mpira wa kengele kutoka mkoa wa Tabora wasichana wakiwa katika mchezo wa fainali dhidi ya Morogoro ambapo matokeo Tabora 16- 7 
Baadhi ya wachezaji wa soka maalum wakipambana vikali kuingia hatua ya nusu fainali baina ya timu za mikoa ya Dodoma na Simiyu.
…………………………..

Na Mathew Kwembe, Mtwara
Timu ya wavulana kutoka mkoa wa Dar es salaam na timu ya wasichana kutoka mkoa wa Tabora zimefanikiwa kujishindia nafasi ya kwanza baada ya kufanikiwa kuwabwaga wapinzani wao katika kuwania ubingwa wa mpira wa kengele katika fainali za UMITASHUMTA zilizofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Timu ya wavulana kutoka mkoa wa Dar es salaam ndiyo ilikuwa ya kwanza kufanikiwa kutwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Lindi 23-13, huku mshindi wa tatu kwa upande wa wavulana ilikuwa timu ya Tanga baada ya kuifunga Tabora 14-7.

Kwa wasichana Tabora ilishika nafasi ya kwanza baada ya kuilaza Morogoro 16-7 na mshindi wa tatu kwa wasichana ilikuwa timu kutoka mkoa wa Arusha baada ya kuilaza Tanga 8-6.

Wakati huo huo matokeo ya mchezo wa robo fainali soka wasichana baina ya Mwanza na Dar es salaam matokeo ni kuwa timu ya Mwanza ilifanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuifunga Dar es salaam kwa kutumia mikwaju ya penati 3-2 baada ya kutoka sare ya goli 1-1, Manyara ilifungwa na Mara 0-1, Kagera iliitoa Simiyu kwa penati 4-1 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana, na Morogoro iliondolewa na Kilimanjaro kwa penati 5-6 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.

Katika soka maalum timu ya mkoa wa Dodoma ilifanikiwa kuilaza Kilimanjaro 1-0, Tabora ilichapwa na Ruvuma 0-5, Mtwara iliifunga Kagera 2-0, na Dar es salaam ilichabangwa na Shinyanga 1-5.

Kufuatia matokeo hayo, timu zilizofuzu hatua ya nusu fainali kwa soka wasichana ni Mwanza ambayo itacheza na Mara, huku mchezo mwingine utahusisha Kagera watakaomenyana na Kilimanjaro.

Katika soka maalum wavulana michezo ya nusu fainali itahusisha Dodoma watakaopambana na Ruvuma na mchezo mwingine utahusisha timu za Mtwara itakayopambana na Shinyanga Kwa upande wa soka wavulana timu za Dar es salaam, Manyara, Mwanza, Geita, Kagera na Tanga tayari zimefuzu hatua ya robo fainali na zinasubiri wapinzani wao wacheze ili waweze kujua timu zitakazoshindana nazo.

Katika matokeo ya mechi zilizochezwa jana Iringa ilibugizwa na Lindi 1-7, Mbeya ilifungwa na Pwani 0-1, Mwanza iliichapa Simiyu 6-1, katavi ilifungwa na Songwe 2-4, Kagera ilifungwa na Rukwa 0-1 na Arusha iligalagazwa na Tabora kwa magoli 0-9.

Taliss-IST yachangia timu za Taifa za mchezo wa kuogelea

$
0
0
Waogeleaji wa timu ya Taliss-IST wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki katika mashindano maalum ya kuzichangia fedha timu za Taifa za mchezo wa kuogelea ili zishiriki katika mashindano ya Dunia. 
 

Dar es Salaam. Mabingwa wa mchezo wa kuogelea nchini, Taliss- IST ya Upanga imechangia kiasi cha Sh1.5 millioni kwa ajili ya timu za taifa za mchezo huo zinazojiandaa na mashindano ya Dunia mjini Gwangju, Korea Kusini na mashindano ya vijana ya dunia yaliyopangwa kufanyika mjini Budapest, Hungary. 

Klabu hiyo iliwakilisha fedha hizo katika mashindano maalum yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la shule ya sekondari ya Shaaban Robert yaliyoandaliwa na Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA). 

Taliss-IST ilichangia fedha taslimu Sh1,225,000 na dola za Kimarekani 140 katika mashindano hayo maalum ambayo yalishirikisha waogeleaji wenye umri tofauti. 

Waogeleaji hao hao ni Mohameduwais Abullatif, Lara Steenkamp Aravind Raghavendran, Fallih Ahmed, Ahmed Rashid, Adam Tapya, Augustino Lucas na Hussein Ebrahim. 

Wengine ni Shivani Bhatt, Sylivia Caloiaro, Nawal Shebe, Amylia Chali, Laila Rashid, Doreen Ahmed, na Zahabiya Ebrahim. Kocha wa timu hiyo, Alex Mwaipasi na Meneja, Hadija Shebe waliongoza timu hiyo katika mashindano hayo. Waogeleaji hao waliogelea katika umbali wa kilometa 1.5 kwa mtindo wa relay, mita 400 na mita 200. 

Shebe alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kuchangia timu ya Taifa ya wakubwa na vijana ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia. TSA inahitaji jumla ya Sh 120 million kwa ajili ya kusafirisha waogeleaji wa timu ya Taifa. 

Mashindano ya dunia ya kuogelea kwa wakubwa yatafanyika kuanzia Julai 12 mpaka 28 mjini Gwangju, Korea Kusini wakati mashindano uua vijana ya dunia yamepangwa kuanza Agosti 20 mjini, Budapest, Hungary. 

Waogealeaji wa timu ya taifa ya wakubwa ni Hilal Hemed, Collins Saliboko ambao wanawakilisha upande wa wanaume na kwa upande wa wanawake ni Sylvia Caloiaro na Shivani Bhatt. Waogeleaji wa timu ya taifa ya vijana ni Dennis Mhini, Delvin Barick, Christopher Fitzpatrick, Christian Shirima, na Isam Sepetu ambao watashindana kwa upande wa wanaume wakati kwa upande wa wanawake ni Kayla Temba na Laila Rashid.

IGP SIRRO AWASILI MKOANI MTWARA

$
0
0

  Mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro leo akiwasili mkoani mtwara kwa ajili ya kujiridhisha kutokea kwa mauaji ya watanzania tisa baada ya kupigwa risasi Juni 26 mwaka huu na watu wanaodaiwa kuvalia sare aina ya jeshi katika kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pembezoni wa mto Ruvuma.
 Mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro leo akiwa katika sehemu ya kupokea paredi la heshima kutoka kwa jeshi la polisi mkoani mtwara baada ya kuwaasili mkoani humo kwa ajili ya kujiridhisha kutokea kwa mauaji ya watanzania tisa baada ya kupigwa risasi Juni 26 mwaka huu na watu wanaodaiwa kuvalia sare aina ya jeshi katika kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pembezoni wa mto Ruvuma.
 Wananchi wa kijiji cha Kihamba kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani mtwara jana wakipokea miili ya watanzania 9 waliouwa baada ya kupigwa risasi Juni 26 mwaka huu na watu wanaodaiwa kuvalia sare aina ya jeshi katika kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pembezoni wa mto Ruvuma.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Kihamba kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani mtwara Abdurahamani Saidi aliyekaa chini jana akitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari waliotembelea katika eneo hilo la tukio baada na kunusurika kifo kufutatia mauji ya watanzania 9 waliofariki kwa kupigwa risasi Juni 26 mwaka huu na watu wanaodaiwa kuvalia sare aina ya jeshi katika kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pembezoni wa mto Ruvuma.

Watanzania wakirejea hapa nchini kwao wakitokea nchi jirani ya Msumbiji baada ya kutokea kwa mauaji ya watanzania 9 waliofariki kwa kupigwa risasi Juni 26 mwaka huu na watu wanaodaiwa kuvalia sare aina ya jeshi katika kijiji cha Mtole kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji pembezoni wa mto Ruvuma. (PICHA NA FATNA MWINYIMKUU)

MJADALA YA WAZI WA SIASA ZA UCHUMI WA GMOs KWA TANZANIA

$
0
0
Na John Nditi
UTAFITI wa Teknolojia ya Uhandisi Jeni ( GMO) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Makutupora na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI ), Mikocheni unaendelea na utakapokamilika matokeo yake yatawasilishwa serikalini kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi ya kuitumia au kitoitumia.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Tafiti za bioteknolojia za kilimo nchini, Dkt. Fredy Tairo kutoka Taasisi ya Utafiti ya TARI Mikocheni wakati akiwasilisha mada ya hali ya utafiti wa GMO nchini kwenye mkutano wa mjadala wa wazi wa siasa za uchumi wa GMO nchini.

Mkutano wa mjadala huo uliofanyika Chuo Kikuu Dar es Salaam na kuandaliwa na Idara ya Sayansi ya Siasa na utawala ya Chuo Kikuu hicho.

Dk, Tairo alisema, msimamo wa Serikali ni kuendelea Utafiti wa GMOs ili uweze kukamilika katika hatua zake muhimu na kisha utakapokamilika katika hatua zote utapeleka katika Mamlaka husika kwa ajili ya kutoa maamuzi hapa nchini.

Alisema, watu na baadhi ya vyombo vya habari walielewa vibaya kauli iliyotolewa na serikali ilitaka watafiti wafuate utaratibu wa kutoa matokeo waliyokuwa wanayapata kwenye majaribio hayo ili kuondoa mkanganyiko.

Mratibu huyo wa Bioteknolojia katika mada yake alisema , sababu na umuhimu wa serikali kufanya tafiti za GMO ili kukabiliana na Changamoto sugu zinazotokana na madiliko ya tabia nchi ikiwemo ukame, wadudu na magonjwa sugu ili kuongeza tija kwa wakulima.

Amesema, kuwa majaribio yanayofanyika katika taasisi ya utafiti ya Makutupora Mkoani Dodoma unalenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya ukame na bungua wa mahindi na kwa matokeo ya awali yameonyesha kufanikiwa pia kupambana pia na Viwavi jeshi vamizi.

Kwa upande wa utafiti wa zao la Muhogo unaofanyika katika Taasisi ya utafiti ya TARI Mikocheni alisema ,unalenga kuipa kinga mihogo kupambana na magonjwa sugu ya Batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo yanaathiri zao hilo Afrika hasa kusini mwa Jangwa la Sahara.

Naye Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha Sayansi na teknolojia cha Nelson Mandela , Mashamba Philipo alisema , teknolojia hiyo ni nzuri na kwa serikali,wakulima na Watafiti ni kuona kama ni muda muafaka wa teknolojia hiyo kutumika hapa nchini.

Mtafiti huyo (plant breeder) alisema, teknolojia hiyo ina uwezo wa kuwezesha nyanya kuwekewa jeni ambayo inauwezo wa kuifanya isiharibike ndani ya mwezi mmoja hata baada ya kuichuma na hivyo kumuongezea tija mkulima.

“Hii sio teknolojia ngeni duniani maana nchi za Marekani, China, Brazil na nyingine nyingi za Afrika zinaitumia , lakini ni muhimu wadau wote wapewe elimu ili kuondoa mashaka waliyonayo kuhusu teknolojia hii” alisema Mtafiti Philipo.

Naye Mratibu wa tafiti za Bioteknolojia nchini, Dk Raphael Nduguru alisema ,walizunguka nchini nzima na kukusanya mbegu za asili na kuanzia utafiti na kuongeza jeni ili kuweza kukabilina na magonjwa yanayohusiana na mihogo.

Naye Mtafiti Emmanuel Sulle ambaye ni Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu cha Western Cape Afrika Kusini alisema , kuna haja ya Serikali ya Tanzania kuongeza bajeti kwenye tafiti za kilimo nchini ili kuwezesha watafiti wa ndani kupatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wakulima.

Alisema , mbali na fedha lakini iongeze idadi ya watafiti kwenye aina ya utafiti huo ambao unakuwa kwa kasi Duniani ili waweze kuwa na uwezo wa kufanya tafiti hizo katika viwango vinavyotakiwa kimataifa.

Sulle alisema , licha ya kufanya tafiti za GMO lazima watafiti waangalie na pia na mbinu zingine za asili wanazozitumia wakulima na kuziboresha. 
 Mratibu wa Tafiti za Bioteknolojia katika kilimo kutoka TARI Mikocheni , Dk. Fredy Tairo akizungumza na na waandishi wa habari wakati wa mjadala wa wazi wa siasa za uchumi wa GMO nchini na kuandaliwa na Idara ya Sayansi ya Siasa na utawala ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.


 Baadhi ya Washiriki kutoka idara, taasisi, mashirika na wadau wengine wa kilimo wakifuatilia mada wakati wa mjadala wa wazi wa siasa za uchumi wa GMO nchini na kuandaliwa na Idara ya Sayansi ya Siasa na utawala ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mratibu wa Tafiti za Bioteknolojia katika kilimo kutoka TARI Mikocheni , Dk. Fredy Tairo ( Kulia) , pamoja na Profesa Daudi Mukangara ( kati kati ) wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) ambaye alikuwa ni Mwongoza mada pamoja na Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela ,Mashamba Philipo ( kushoto) wakisilikiza hoja mbalimbali ziliozolewa kwenye mjadala wa wazi wa siasa za uchumi wa GMO nchini ulioandaliwa na Idara ya Sayansi ya Siasa na utawala ya chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Diaspora kusimamia ujenzi wa Daraja refu Zanzibar

$
0
0
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Waoishi Nje ya Nchi maarufu {Diaspora} uko tayari kusimamia Ujenzi wa Daraja refu la kisasa lenye uwezo wa kuunganisha Miji Miwili ya Dar es salaam na ule wa Zanzibar katika harakati za kuimarisha Uchumi na Mawasiliano.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo akiwa pia Mjumbe wa Kamati ya Biashara Tanzania Bwana Jonas Njao akiiongoza Timu ya Wanajumuiya hiyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Bwana Jonas Njao alisema Diaspora imeanza harakati za Maandalizi ya kufanya utaratibu wa kuziomba Serikali zote Mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kuuridhia Mradi huo Mkubwa wa Kimataifa utakaoweza kupunguza kundi kubwa la ajira Nchini Tanzania.

Alisema Wataalamu pamoja na Wafadhili wa ujenzi wa Mradi huo wa Kiuchumi tayari wameshajitokeza na kinachosubiriwa kwao kwa sasa ni kukubalika kwa maombi ya Mradi ambao bado umekuwa adimu ndani ya Bara la Afrika.

Bwana Jonas Njao alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba fursa wanazozipata za kuwasiliana na Taasisi na Makampuni wanamozunguuka katika Mataifa tofauti Duniani zimelenga kutafuta nafasi za ajira zitakazosaidia kuimarisha ustawi wa Wananchi kutokana na vijana wao kujikomboa katika masuala ya ajira.

Naye Afisa Muandamizi wa Kampuni ya Maxtruder yenye Mastakimu yake Nchini Ujerumani Mhandisi Felix Von Lumburg alisema Uongozi wa Taasisi yake uko tayari kuwekeza Miradi ya Ujenzi wa Nyumba zenye bei nafuu kufuatia ushawishi mkubwa walioupata kutoka Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi.

Mhandisi Lumburg alisema ujenzi wa Nyumba Moja yenye thamani ya Dola za Kimarekani Elfu 5,000 hutumia Masaa Mawili tuu kuunganisha kuta zake zilizotengenezwa kwa zege yenye kuzingatia kiwango madhubuti cha Kimataifa.

Alisema Uongozi wa Kampuni hiyo mbali ya kujikita katika Miradi tofauti kutokana na Taaluma kubwa ya Wahandisi wake lakini imeamua kulenga katika ujenzi wa Nyumba hizo ili kusaidia Jamii za Wanaadamu hasa wale wanaoishi wakiwa na kipato cha chini.

Afisa Muandamizi huyo wa Kampuni ya Maxtruder amemuhakikishia Balozi Seif kwamba nyumba zinazojengwa na Kampuni hiyo zinahimili matukio ya dharura ikiwemo mitetemeko na tayari wameshajenga moja ya Mfano Nchini Kenya na mradi kama huo kwa sasa upo Nchini Russia.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali zote Mbili Nchini Tanzania zimetoa fursa kwa Wananchi wake kutafuta Maisha mahali popote mali ilimradi wanazingatia Sheria na Taratibu za Mataifa wanaamua kuishi.

Balozi Seif alisema ni vyema kwa Watanzania hao walioko Ughaibuni wakachuma katika njia ya halali, wakala, lakini wasisahau kuweka hakiba kwa ajili ya kusaidia Familia zao pamoja na wao wenyewe.

Aliwaomba kuitumia fursa ya Uwekezaji iliyopo Nchini hivi sasa kwa kuanzisha Miradi ya uzalishaji vikiwemo viwanda vidogo na hata vikubwa ili vije kuwasaidia pale watakapoamua kurudi kumaliza maisha yao nyumbani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Watanzania hao wanaoishi Ughaibuniu kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa vile tayari imesharidhia uwepo wa Jumuiya hiyo iko tayari kuwasaidia wana Diaspora hao kwa wale watakaoamua kuwekeza Miradi yao ikiwemo Nyumba na Mashamba.

Akigusia mradi wa Ujenzi wa Nyumba za bei nafuu Balozi Seif aliipongeza Kampuni ya Maxtruder kwa uamuzi wake iliyochukuwa ya kutaka kufungua Milango ya Uwekezaji katika Mataifa machanga yanayohitaji huduma hizo muhimu kwa ustawi wa Jamii.

Balozi Seif alisema Zanzibar ni miongoni mwa Nchi zenye maeneo madogo ya Ardhi. Hivyo aliushauri Uongozi wa Kapuni hiyo kuandika maombi yake yakutaka kuanzisha Miradi ya Ujenzi wa Nyum.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Timu ya Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi {Diaspora} Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Waoishi Nje ya Nchi maarufu {Diaspora} akiwa pia Mjumbe wa Kamati ya Biashara Tanzania Bwana Jonas Njao akimkabidhi Balozi Seif Barua za maombi yakutaka kuanzisha Mradi wa Ujenzi wa Daraja kati ya Miji ya Dar es salaam na Zanzibar.
  Afisa Muandamizi wa Kampuni ya Maxtruder yenye Mastakimu yake Nchini Ujerumani Mhandisi Felix Von Lumburg akimkabidhi Balozi Seif baadhi ya michoro ya ramani ya Nyumba za bei nafuu zinazojengwa naq Kampuni hiyo.
 Balozi Seif kati kati akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi {Diaspora} mara baada ya mazungumzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.





















Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images