Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Shirika la Ndege la Tanzania ATCL laanza safari zake za kwenda Nchini Afrika Kusini Ijumaa tarehe 28/06/2019

$
0
0
 Ndege ya Abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL aina na Airbus A220-300 ikipakia abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka kuanza safari yake ya kwanza ya kuelekea nchini Afrika Kusini Ijumaa  tarehe 28/06/2019. 
 Ndege ya Abiria ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL aina na Airbus A220-300 ikiruka kuelekea nchini Afrika Kusini Ijumaa  tarehe 28/06/2019 ikiwa ni uzinduzi wa Safari yake ya kwanza kwenda nchini humo. 

RAIS DK. MAGUFULI AKUTANA NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WABUNGE WA SADC NA SPIKA JOB NDUGAI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898 
Baruapepe: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Nukushi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU, 
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ijumaa tarehe 28 Juni, 2019 amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Verónica Nataniel Macamo Dlhovo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Katibu wa Jukwaa la Wabunge la SADC Bi. Boemo Sekgoma.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Dlhovo ambaye ni Spika wa Bunge la Msumbiji amewasilisha salamu za Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi na salamu za Maspika wa SADC pamoja na kueleza kuhusu ushiriki wa jukwaa hilo katika Mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dlhovo amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na hatua kubwa ambazo Tanzania inapiga katika maendeleo na ameeleza kuwa Jukwaa la Wabunge la SADC linakusudia kujenga mazingira ambayo yataweka sheria na taratibu zitakazowezesha nchi wanachama kubadilishana uzoefu ya kupiga hatua zaidi za maendeleo.
Aidha, Mhe. Dlhovo amesema Msumbiji na nchi nyingine za Afrika zinatambua mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania tangu wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa mataifa mengi ya Afrika na uanzishaji wa nchi za mstari wa mbele na SADC.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Dlhovo kwa kufika Ikulu kumsalimu na kufikisha salamu za Mhe. Rais Nyusi na Wabunge wa SADC na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC ikiwemo Msumbiji ambayo ina uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Juni, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma ambao wameongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na wageni hao Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Tingatinga na Kinyago Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, alipokutana na na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya picha ya kuchora toka Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, huku akishuhudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Ikulu jijini Dar es salaam  Ijumaa Juni 28, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019 PICHA NA IKULU

Dar es Salaam kucheza na Mwanza Robo Fainali Soka Wasichana UMITASHUMTA

$
0
0

Lidya Daudi wa timu ya soka ya wasichana Geita (mwenye jezi ya bluu) akichuana vikali kugombea mpira na mchezaji Eneck Daud wa Mbeya (jezi nyeusi) wakati timu hizo zilipocheza hivi karibuni. 
Mshambuliaji hatari wa timu ya soka wavulana ya mkoa wa Lindi Omari Mohamed akifunga goli la pili kwa njia ya penati dhidi ya timu ya Mtwara huku golikipa wa timu hiyo Benard William akijaribu kuchupa bila mafanikio wakati timu hizo zilipokutana hivi karibuni. Lindi iliifunga Mtwara 2-0. 
………………….. 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 
Timu za soka za wasichana za mikoa ya Dar es salaam na Mwanza zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya UMITASHUMTA na zinatarajiwa kucheza leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara. 

Dar es salaam imefikia hatua hiyo baada ya kuibuka kinara katika kundi A na hivyo itachuana na mshindi wa pili kundi C Mwanza katika hatua ya robo fainali. Pambano lingine la robo fainali litazikutanisha timu za mikoa ya Manyara ambao iliibuka mshindi wa kwanza kutoka kundi B watakaochuana na mshindi wa pili kundi D timu ya soka ya wasichana kutoka mkoa wa Mara. 

Mshindi wa kwanza kutoka kundi C, timu ya soka wasichana kutoka mkoa wa Kagera imepangwa kuchuana na mshindi wa pili kundi B, Simiyu huku mshindi wa kwanza kundi D Morogoro watachuana na mshindi wa pili kundi A, Kilimanjaro. 

Kwa upande wa soka maalum wavulana, michuano hiyo pia imefikia hatua ya robo fainali na inatarajiwa kuchezwa leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara ambapo mshindi wa kwanza kundi A Kilimanjaro atachuana na mshindi wa pili kundi C Dodoma. Mshindi wa kwanza kundi B Tabora atachuana na mshindi wa pili kundi D Ruvuma. Mchuano mwingine mkali utahusisha mshindi wa kwanza kundi C, Mtwara atachuana na mshindi wa pili kundi B, Kagera huku mshindi wa kwanza kundi D, Dar es salaam atachuana na mshindi wa pili kundi A, timu ya soka maalum wavulana kutoka mkoa wa Shinyanga. 

Kwa upande wa soka wavulana, michuano hiyo bado inaendelea katika hatua ya makundi na inatarajiwa kuchezwa hatua ya robo fainali tarehe 1, julai, 2019 ambapo mshindi wa kwanza kundi A atacheza na mshindi wa pili kundi C, mshindi wa kwanza kundi B atachuana na mshindi wa pili kundi D, mshindi wa kwanza kundi C atacheza na mshindi wa pili kundi B na mshindi wa kwanza kundi D atachuana na mshindi wa pili kundi A. 

Matokeo ya michezo iliyochezwa kundi A kuanzia tarehe 24 juni hadi tarehe 28 juni, 2019 katika soka wavulana inaonyesha kuwa Tanga imeifunga Singida 4-0, Dodoma wameichapa Mara 2-1, Dar es salam imetoka sare na Kilimanjaro 1-1, Singida imetoka suluhu na Kilimanjaro 0-0, Mara imefungwa na Dar es salaam 0-1, Tanga imeifunga Dodoma 2-1, na Dodoma imefungwa pia na Dar es salaam 2-3. 

Kilimanjaro iliifunga Tanga 1-0, Singida iliichapa Mara 2-0, Dodoma nayo iliifunga singida 2-1, Mara ikaichapa Kilimanjaro 2-1, Dar es salaam ikatoka suluhu na Tanga, Tanga ikaifunga Mara 3-0, Singida ikachapwa na Dar es salaam 0-3 na Kilimanjaro pia ikachapwa na Dodoma 0-3. 

Matokeo ya kundi B soka wavulana, Mbeya ilichabangwa na mwanza 2-5, Pwani iliibugiza Iringa 4-0, Lindi nayo ikaichapa Mtwara 2-0, Mwanza ikaifunga Pwani 3-0, Simiyu ikaifunga Iringa 2-0, na Mbeya ikaichapa Mtwara 1-0, Lindi ikatoka suluhu na Simiyu, Mtwara ikafungwa na pwani 0-3, Iringa nayo ikabugizwa na Mwanza 1-5 na Mbeya ilipata kipigo kutoka Simiyu 0-1, Mwanza imeichapa Mtwara 4-0, Pwani ikatoka sare na Lindi 1-1, Iringa ikapata kipigo kutoka Mbeya 0-4, Mtwara nayo ikafungwa na Simiyu 1-3 na Mwanza ikatoka sare na Lindi 1-1. 

Matokeo ya michezo ya kundi C yanaonyesha Geita iliichapa Kigoma 1-0, Manyara iliifunga Njombe 2-1, Shinyanga ilikubali kichapo kutoka kwa Ruvuma 0-2, Kigoma iliifunga Ruvuma 1-0, na Njombe ikaifunga Shinyanga 4-1. Pia Geita ikaifunga Manyara 2-0, Manyara ilikubali kipigo kutoka kwa Shinyanga 0-5, Ruvuma nayo ilifungwa na Geita 0-2, Kigoma ikaifunga Njombe 1-0, Manyara ikaichapa Kigoma 4-0, Njombe na Ruvuma zikatoka suluhu, Shinyanga ikafungwa na Geita 0-1, Geita ikaichapa Njombe 4-0, Kigoma ikatoka sare na Shinyanga 1-1 na Ruvuma ikakubali kichapo kutoka kwa Manyara 1-3. 

Katika michezo iliyochezwa kundi D soka wavulana, matokeo yanaonyesha Katavi ilifungwa na Kagera 1-2, Morogoro ilichapwa na Tabora 1-2, Rukwa ikaifunga Songwe 3-1, Morogoro ikatoka sare na Rukwa 1-1, Kagera ikaichapa Arusha 3-0, huku Katavi na Tabora zikitoka suluhu ya bila kufungana. Matokeo mengine Songwe ilichapwa na Kagera 0-2, Tabora na Rukwa zikatoka suluhu, Arusha ikachapwa na Morogoro 1-3, Arusha pia ilibugizwa na Songwe 1-7, Katavi ilifungwa na Rukwa 0-1, Morogoro ilifungwa na kagera 1-2, Arusha ilifungwa na katavi 0-2, Tabora ilichapwa na Kagera 0-3 na Morogoro na Songwe zilitoka suluhu ya bila kufungana. 
Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea leo na kesho ili kukamilisha ratiba kwa timu za soka wavulana kutoka makundi A hadi D kwa soka wavulana ili kukamilisha ratiba ya michuano hiyo kabla ya kuchezwa hatua ya robo fainali kesho kutwa katika viwanja hivyo hivyo vya chuo cha ualimu Mtwara

Manispaa ya Sumbawanga Yatoa 115% ya Fedha za Uwezeshaji kiuchumi

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi hundi kwa moja ya kikundi cha walemavu wa ngozi katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Sumbawanga 
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi hundi kwa moja ya kikundi cha walemavu wa ngozi katika hafla fupi ya kukabidhi mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Sumbawanga 
…………………….. 

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameisifu Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kuzidisha kiwango cha asilimia 10 ya mikopo kwa Vijana, akina Mama na Watu wenye Ulemavu kwa kutoa shilingi 253,228,000/= zaidi ya lengo la awali ambapo halmashauri ilitakiwa kutoa Shilingi 2,212,104,000/= kutokana na makisio ya makusanyo yake ya ndani yaliyolenga kukusanya Shilingi 2,212,104,000/=. 

Mh. Wangabo alisema kuwa kiwango hicho cha asilimia 10 ambachoo Manispaa ya Sumbawanga wameweza kukitoa ni sawa na asilimia 115 kutokana na mapato yaliyokusanywa ya shilingi Bilioni 3.1 ambayo ni tofauti na makadirio yaliyofanyika kwa mwaka wa fedha 2018/2019. 
“Taarifa ya Mkurugenzi imeonesha kuwa kuna mafanikio ya kujivunia katika suala zima la uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwa kipindi cha Miaka sita, kiwango cha fedha kinachotolewa kama mtaji kwa wajasiriamali kimekuwa kikiongezeka kila Mwaka na kwa Mwaka huu wa fedha 2018/2019 Manispaa imevunja rekodi kwa kutoa Shilingi 253, 228,000/= jambo hili ni la kupongezwa kwa mafanikio mliyofikia ya kutoa fedha 10% ya mapato ya ndani kwa 115% haya ni mafanikio makubwa sana, hivyo Hongereni sana Manispaa ya Sumbawanga,” Alisema. 

Aidha, aliupongeza uongozi mzima wa Wilaya ya Sumbawanga pamoja na Halmashauri hiyo kwa kutekeleza sheria ya fedha ya mwaka 2018 inayoelekeza utekelezaji wa uwezeshaji wa vijana, kinamama na watu wenye ulemavu na kuzitaka halmashauri nyingine za mkoa kuiga mfano huo na hatimae kuwafaidisha wananchi kwa mikopo isiyo na riba ili waweze kujiinua kiuchumi. 

Wakati akisoma taarifa ya utoaji wa mikopo Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga Jacob Mtalitinya alisema kuwa siku ya leo (28.6.2019) Halmashauri itatoa mikopo kwa vikundi 32 ambapo kati ya hivyo vikundi vya Wanawake 13, Vijana 14 na Watu wenye Ulemavu 5 ambapo kiasi cha Tsh. 73,678,000 kitatolewa kama uwezeshaji wa Wananchi. 

“Kwa maana hiyo, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga kwa kipindi cha mwaka 2018/19 itakuwa imeweza kutoa mikopo kwa vikundi 114 vikiwemo vya Wanawake 56, Vijana 44 na watu wenye ulemavu 14 Ambapo kiasi cha jumla ya Tshs. 253,228,000.00 zitakuwa zimetolewa kwa makundi yaliyoainishwa. Hivyo itapelekea kufikiwa kwa jumla ya wanachama 1,135 kama wanufaika wa mikopo hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019,” Alieleza.

 
Pamoja na mafanikio hayo makubwa, Mtalitinya hakusita kugusia changamoto ambazo halmashauri inakumbana nazo ikiwemo Hamasa ndogo ya uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi, Uelewa mdogo wa Jamii kuhusu uanzishwaji wa vikundi vya kiuchumi, Uelewa mdogo wa fursa za kiuchumi kwa Jamii. 

Kukosekana kwa masoko ya bidhaa za vikundi. Na hivyo kuahdi kuendela kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi ngazi ya kata na mitaa. 
Katika hatua nyingine Mh. Wangabo alichukua fursa hiyo kukabidi kikombe cha ushindi wa jumla wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2018 ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga iliibuka na ushindi huo.

RC Wangabo atoa ushauri baada ya Taifa Stars kufungwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo ametoa ushauri kwa wadau wa michezo nchini kuona namna ya kuimarisha mbinu za kuibua vipaji vya wanamichezo kuanzia ngazi ya shule za msingi katika mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA ili kuweza kuwa na vijana watakaoweza kubeba jina la Tanzania katika michezo.

Amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliochelewa kulala ili kuangalia mechi baina Tanzania maarufu kama Taifa Starts na jirani zetu Kenya maarufu kama Harambee Strars ambapo hadi kumalizika kwa mchezo huo Harambee Stars iliibuka kidedea kwa kuilaza Taifa Stars mabao 3 kwa 2.

“Kuna ambao wamelala alfajiri na wengine wapo humu ambao wamelala leo, tunaomboleza kufungwa huku, tungeshinda jana tungekuwa na mwanga wa kusonga mbele, sasa ni kinyume na yalivyokuwa matarajio yetu lakini ndugu wana Rukwa tusikate tamaa, tuendelee kuiunga mkono timu yetu hii ya Taifa, Kufungwa ni kujifunza, tuendelee kujipanga vizuri hasa kwa vijana kuanzia UMISHAMTA huku mpaka UMISETA na kwenye “academy” hizi,” alieleza.

Aidha, alibainisha kasoro kadhaa zinazojitokeza katika ligi yetu ya Tanzania hasa kwa upande wa timu vinara zinazopata nafasi za kwenda kucheza makombe ya Kalbu Bingwa Afrika pamoja na Kombe la Shirikisho kuona namna ya kutoa fursa kwa wachezaji wa kitanzania ili wapate ujuzi wa kimataifa na sio kuwajenga wachezaji wa nje ambao wanakwenda kutumikia nchi zao.

“Hizi timu zetu za Yanga na Simba pamoja na Azama zinafanya vizuri kwasababu zina wachezaji wengi wa kigeni matokeo yake timu ya Taifa inapokwenda kwenye mashindano wachezaji wetu wanabaki wenyewe, angalieni Emanuel Okwi anavuma kule Uganda lakini tumemuwezesha sisi hapa Tanzania,” Alisema.

UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA MASIKINI SI HIARI NI WAJIBU-DR.NTULI

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe(kwanza kulia) akitoa maelekzo ya jumla wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika Hospital ya Wilaya ya Chato.
Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe akizungumza na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani humo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dr. Japhet Simeo akifuatilia kikao wakati Mkurugenzwa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato.
Dr. Fatuma Mrisho akizungumza wakati wa kikao na Mkurugenzi wa Afya alipokuwa akizungumza na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato
Wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakifuatilia kikao cha Mkurugenzi wa Afya a na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato 
………………………… 
Nteghenjwa Hosseah, Chato 

Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dr.Ntuli Angelile Kapologwe amesema huduma jumuishi za afya kwa wananchi masikini si jambo hiari bali ni wajibu wa kila mtoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za Afya Nchini. 

Dr. Ntuli amesema hayo wakati alipokutana na watumishi wa Hospital ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita kuzungumzia masuala mbalimbali ya kiutendaji na namna ya kuboresha utoaji wa huduma za Afya kwa Jamii. 
Dr. Ntuli amesema mwananchi masikini hapaswi kubaguliwa kwa sababu tu hawezi kuchangia huduma za Afya ni wajibu wetu kumhudumia kisha kujirdhisha kama kweli hana uwezo wa kulipa kisha kupewa msamaha kwa mujibu wa Sera ya Afya. 

“Moja kati ya haki ya msingi za kila binadamu ni kufurahia viwango vya juu vya afya viwezekanavyo na sisi kama watumishi wa Serikali tunalo jukumu la kutoa huduma bora za afya zinazofikika na zinazopatikana kwa watu wote bila ubaguzi. 

Msamaha katika huduma za Afya unahusishwa mama mjamzito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano lakini kwa mama yule ambaye ana Bima ya Matibabu inapaswa kutumika ili kuchangia na gharama hizo ambazo zitaenda kusaidia wananchi ambao hawana uwezo hivyo katika hili ni muhimu tuelimishe wananchi ili kuwa na uelewa wa pamoja” Alisema Dr Ntuli. 

Aidha Dr.Ntuli aliongeza kuwa msamaha huu pia unalenga wazee wenye zaidi ya miaka sitini na wale wenye magonjwa sugu lakini msamaha huo utatolewa pale ambapo afisa usawi wa jamii wa hospital au kituo husika atajiridhisha pasipo shaka kuwa makundi haya yote yaliyotajwa kwenye msahama hawana kabisa uwezo wa kuchangia huduma za Afya. 

“Kila mtoa huduma anapaswa kuelewa vyema kuhusu msamaha na nani analengwa kati msamaha huu, mwananchi yupi anapaswa kuchangia huduma na yupi anapaswa kupewa msamaha na mfahamu fika kuwa utaoji wa msamaha huu si kwa mujibu wa matakwa yetu bali ni Sera ndio imeelekeza hivyo kila mmojawetu atimize wajibu wake katika hili” alisema Dr, Ntuli. 

Sambamba na hilo Serikali inaendelea kupanua utoaji wa huduma za afya kila inapowezekana, kuhakikisha upatikanaji wa dawa ni wa uhakika, wataalamu wa afya wanaajiriwa na kuendelezwa kulingana na mahitaji na wanapata motisha: Tunatarajia jitihada hizi zitawezeshe utoaji wa huduma za Afya kuzidi kuimarika kuanzia ngazi ya msingi, ninachowataka ni nyinyi kujituma kwa moyo na kuhakikisha wananchi wanakuwa na Afya njema na mnaokoa maisha ya watanzania alimalizia Dr.Ntuli. 

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dr. Japhet Simeo amemshkuru Mkurugenzi wa Afya kwa kukutana na watumishi wa Afya, kuskiliza changamoto zao, kutafuta ufumbuzi wa pamoja na kutoa maelekezo ya Serikali katika kuboresha huduma za Afya. 

“Nikuhakikishie tu kuwa maelekezo uliyatoa tumeyapokea na tutayafanyia kazi kwa weledi na kufuata miiko ya Taalumu yetu ili kuhakikisha tunafanikisha ile dhana ya upatikanaji wa huduma za Afya kwa wote” alisema Dr. Japhet”

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 29,2019

UKIUKWAJI WA HAKI JINAI NCHINI UPUNGUE-KAILIMA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza na Kikosi kazi kinachofanya Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa kikosi kazi kinachofanya maboresho ya mfumo wa haki jinai .
Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Katib na Sheria Bw. Patience Ntwina akitoa maelezo mafupi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani Ndg. Ramadhani Kailima kuhusu kazi ya Maboresho ya mfumo wa haki jinai inayofanywa na kikosi kazi maalum jijini Dodoma ambapo Ndg. Kailima aliwatembelea na kuzungumza nao.


Naibu Katibu Mkuuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ndg. Ramadhani Kailima awataka wadau wa Maboresho ya mfumo wa Haki Jinai kuibua changamoto zinazokwamisha ufikiwaji wa Haki Jinai. 

Hayo ameyasema alipotembelea kikosi kazi kinachopitia Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai na kuwataka wataalam kuupitia mfumo huo kwa umakini na kufuta viashiria vyote vya ukiukwaji wa Haki Jinai nchini ikiwemo tabia ya baadhi ya viongozi kuweka watu ndani bila kufuata utaratibu wa kisheria. 

“Mnapoendelea na maboresho ya Haki Jinai mhakikishe mnatafuta namna ya kufuta ukiukwaji wa Haki jinai” amesema .Naibu Katibu Mkuu huyo amewataka wadau wa mkutano huo kuweka wazi mambo yote yenye Ushahidi wa uvunjwaji wa haki Jinai ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa ukiukwaji wa Haki Jinai. 

Akitolea mfano namna wananchi wanavyovunjiwa haki zao na polisi kwa kuwekwa ndani bila kufuata sheria hasa wanapoamria na viongozi, Kailima alisema kabla ya kumweka mtuhumiwa ndani polisi wajiridhishe kwa kufanya upelelezi juu ya tuhuma husika ndipo wamweke mtuhumiwa ndani hapo ndipo haki jinai itakuwa imetekelezwa. 

Aidha, amewataka wadau kufanya kazi ya maboresho hayo kwa bidii na wasichoke kwani maboresho hayo yatasaidia wananchi kupata haki zao. 


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATENGENEZO YA BOMBA KUU LA USAMBAZAJI MAJI

KIKUNDI CHA NGUVUKAZI CHATOA MSAADA WA CHAKULA MUSOMA VIJIJINI MKOANI MARA

$
0
0

Kikundi cha NGUVUKAZI kilichopo Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli Musoma Vijijini mkoani Mara,kilianzishwa Mwaka jana (2018) wakiwa chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Jamii (PCI, Project Concern International) lililowapa MAFUNZO ya KILIMO Wanachama wa Kikundi hicho na baadae wakaanzisha KILIMO cha MAHINDI, VIAZI LISHE, na MPUNGA.

Afisa Kilimo wa Kata, Ndugu Sevas Ngova ameeleza kwamba Kikundi cha NGUVUKAZI kilipata MAFUNZO ya ZAO JIPYA JIMBONI la ALIZETI na baada ya MAFUNZO walianza na SHAMBA DARASA kwa kutumia Mbegu walizopewa na Mbunge wa Jimbo,  Profesa Sospeter Muhongo. Mavuno ya awali ya ALIZETI yalikuwa ya MAGUNIA 10. Mbegu nyingine walizopokea kutoka kwa Mbunge wao huyo ni za MTAMA, MIHOGO na UFUTA.

Ndugu Tore Masamaki, Mwenyekiti wa Kikundi cha NGUVUKAZI ameeleza kwamba Kikundi hicho kilianza na WANACHAMA 18 na baada ya MAFANIKIO ya kuridhisha kupatikana, Wanachama wameongezeka na kufikia 30 (thelathini).

Kikundi cha nguvu kazi kinaendelea kushirikiana na Shirika la PCI ambalo moja ya malengo yake makuu ni kutoa CHAKULA mashuleni, ikiwemo Shule ya Msingi Bwenda.

"Kupitia Kikundi hiki mavuno yanayopatikana hupelekwa shuleni hapo, na mengine ni kwa manufaa yao wenyewe na familia zao , Masamaki aliyasema haya na kuongeza kwamba sasa wanatafuta vifaa vya umwagiliaji waanze Kilimo hicho.

Mwalimu Mkuu  Bwenda, Christopher Cosmas  amekiri kupokea jumla ya KILO 220  za MAHINDI kutoka Kikundi cha NGUVUKAZI  kwa ajili ya CHAKULA cha WANAFUNZI.

Mwalimu Mkuu huyo anasema CHAKULA kinachotelewa kwa WANAFUNZI wote hapo Shuleni kimefanya UTORO usiwepo na HAMASA ya Wanafunzi kupenda kupata ELIMU imeongezeka.

Aidha Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeura ameshukuru Kikundi cha NGUVUKAZI kwa jitihada zake na kupitia vikao vya hadhara ameomba VIKUNDI vingine kujitokeza kusaidia UPATIKANAJI wa CHAKULA kwa Shule nyingine ndani ya Kata yao ya Rusoli.
 Wana Kikundi cha NGUVUKAZI wakiendelea na shughuli ya kuandaa mahindi yao yakauke vizuri mara baada ya kuvunwa shambani kwa ajili ya kutoa msaada mashuleni.
 Kikundi cha NGUVUKAZI kikiwa na mavuno ya MAHINDI kutoka shambani mwao wakiwa sambamba na Diwani wao, Mhe Boaz Nyeura (aliyevaa nguo za Chama- CCM) 
 Diwani wao, Mhe Boaz Nyeura (aliyevaa nguo za Chama- CCM)  kizungumza na Kikundi cha  NGUVUKAZI  Kijijini Buanga, Kata ya Rusoli,Musoma mkoani Mara 
 Kikundi cha NGUVUKAZI kikiwa na mavuno ya MAHINDI kutoka shambani mwao. 


SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) LAANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI UMUHIMU WA BIMA KATIKA MAONESHO YA SABA SABA JIJINI DAR

$
0
0
 Afisa Bima wa Shirika la  Bima la Taifa (NIC) Honest Valence kulia akitoa maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na NIC kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao walitembelea banda hilo jana wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.


Afisa Bima wa Shirika la  Bima la Taifa (NIC) Honest Valence kulia akifurahia jambo na mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam waliotembelea banda la shirika hilo jana wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.


 Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakiwa kwenye picha ya pamoja  wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.

 Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakiwa kwenye ‘pozi’ wakati wa maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa  yaliyoanza jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.


Viongozi Kasulu watakiwa kuimarisha usalama Korongo la Bolelo

$
0
0
Baadhi ya watoto walionaswa na kamera ya BMG wakicheza katika korongo hatari la Bolelo lililopo Kata ya Kumsenga, Halmashauri ya Mji wa Kasulu mkoani Kigoma ambapo korongo hilo linaelezwa kuwa uwanja wa vitendo viovu ikiwemo ushirikina.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Pia korongo la Bolelo licha ya kwamba ni hatari kwa jinsi lilivyo, bado linapendwa na watoto wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi zilizopo jirani ambapo wamekuwa wakilitumia kwa kucheza/ kujificha wanapotoroka shuleni.
Nyakati za usiku inaelezwa korongo hili ni hatari kwa wakazi wanaokatisha hapa kwani baadhi ya wahalifu hulitumia kufanya uhalifu kama vile ukabaji.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge wilayani Kasulu, Mwl. John Edson akieleza mbele ya wanahabari namna uwepo wa korongo la Bolelo jirani na shule hiyo unavyoathiri masomo kwa wanafunzi ambao wamekuwa wakitoroka na kwenda kujifisha humo.
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Watoto na Wanawake KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge, Mwl. John Edson kuhusiana na mathara ya korongo ya Bolelo kwa wanafunzi.
Tazama BMG Online TV hapa chini
SOMA>>> Wazee wilayani Tarime wajitenga na Ukatili wa Kijinsia

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA HALI YA HEWA NCHINI OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (wanne kulia) walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Injinia. Atashasta Nditiye. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Switzerland.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Injinia. Atashasta Nditiye. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Switzerland.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) alipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Injinia. Atashasta Nditiye
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini, Dkt. Agnes Kijazi (kulia) na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Injinia. Atashasta Nditiye walipomtembelea leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Dkt. Kijazi alishinda nafasi ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la hali ya hewa Duniani (WMO) uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Juni, 2019 Geneva, Switzerland.

MISS KINONDONI TISHIO ,MINI COPPER KUSHINDANIWA

$
0
0

    Na Khadija seif,Globu ya jamii

MASHINDANO ya miss kinondoni yazinduliwa rasmi jijini Dar es salaam  

Mratibu wa mashindano hayo Nancy kikwembe ( super model) amesema mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na kufanikiwa kupata warembo takribani 18.

"Mchakato  ulianza muda mrefu taingia mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu na matangazo yalikua mengi na warembo 46 walijitokeza ,"

Super model amesema katika mchuano huo wanategemea kupata mrembo atakaewakilisha vizuri katika wilaya ya kinondoni na kufanikiwa kuingia miss Tanzania.

"Julai 13 mashindano ya kumpata miss kinondoni yatafanyika katika ukumbi wa life park jijini Dar es salaam,"

Hata hivyo mratibu huyo amesema zawadi kwa mshindi wa Kwanza atapatiwa gari aina ya Min Cooper yenye thamani ya shilingi milioni 13,huku mshindi wa pili atapata seti ya vitu vya ndani ikiwemo kitanda,godoro pamoja na viti.

"Mshindi wa tatu atapatiwa televisheni pamoja na king'amuzi huku mshindi wa nne na watano watapatiwa vifuta jasho,"

Aidha,amewaomba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha shindano hilo kwani mabalozi mbalimbali hutokea  kwenye mashindano ya mamiss kutokana na mionekano yao pamoja na akili na nidhamu.
 Mratibu wa mashindano ya miss kinondoni Nancy Joseph (super model) akizungumza na waandishi wahabari wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo life park jijini Dar es salaam.
 Gari aina ya Min copper ambayo itatolewa kwa mshindi wa Kwanza wa miss kinondoni mwaka huu jijini Dar es salaam.

AIBUKA MSHINDI MBIO ZA MITA 100 UMITASHUMTA 2019

$
0
0
Mwanariadha Makoye Bundala (501) wa Shinyanga akimaliza mbio za mita 100 wavulana mbele ya Mwanariadha aliyeshika nafasi ya pili Matiko Nyamalaga (289) wa Mara na mwanariadha Steven Stephano wa Tabora (601) wakati wa hatua ya fainali zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu mtwara. 
Wanariadha kutoka kundi la wasichana Shija Donald wa Mwanza (387) akiwaongoza wakimbiaji wenzake kumaliza fainali za mbio za mita 100 leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 
Baadhi ya wakimbiaji wa mbio za mita 400 x4 wakijiandaa kwa ajili ya mchuano wa nusu fainali wa mbio hizo zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara 
……………………….. 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 

Mwanariadha wa Shinyanga Makoye Bundala ameibuka kuwa mshindi wa kwanza katika fainali za mbio za mita 100 za mashindano ya UMITASHUMTA zilizofanyika leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara. 

Makoye alitumia muda wa sekunde 11:87, ambapo aliyemfuatia ni Matiko Nyamalaga kutoka mkoani Mara ambaye alitumia muda wa sekunde 11:94, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na mwanariadha Steven Stephano wa Tabora ambaye alitumia muda wa sekunde 12:07 kumaliza mbio hizo. 

Kwa wasichana, mshindi wa fainali za mbio za mita 100 ni Shija Donald wa Mwanza ambaye alitumia muda wa sekunde 13:16 kumaliza mbio hizo, nafasi ya pili ilichukuliwa na Paulina Pius pia wa Mwanza ambaye alitumia muda wa sekunde 13:38, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Fauzia Hamu wa Singida ambaye alitumia muda wa sekunde 13:91. 

Katika mchezo wa kurusha mkuki nafasi ya kwanza ilichukuliwa na mwanafunzi Suzan Wilson wa Mbeya ambaye alirusha mkuki umbali wa mita 33 na sentimita 94, nafasi ya pili ilichukuliwa na Vatheline Amri wa Tabora ambaye alirusha mkuki umbali wa mita 31 na sentimita 80, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na Paskalina Augustino wa Manyara aliyetumia umbali wa mita 29 na sentimita 40.

TASAC: TUNAFANYA UKAGUZI WA MELI KUHAKIKI UBORA NA KUVIONDOSHA VISIVYOKUWA NAVYO MAJINI

$
0
0
Meneja wa Usajili,Ukaguzi na Udhibiti wa Usalama wa Vyombo vya maji Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Afred Waryana wa pili kushoto akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alipotembelea banda lao wakati wa maadhimisho ya wiki ya mabaharia kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi 
Meneja wa Usajili,Ukaguzi na Udhibiti wa Usalama wa Vyombo vya maji Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Afred Waryana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa warsha hiyo
Sehemu ya mabaharia wakiwa kwenye warsha hiyo
Sehemu ya mabaharia wakiwa kwenye warsha hiyo
Sehemu ya wanafunzi wa shule za Sekondari wakiwa kwenye warsha hiyo



UKAGUZI wa kushtukiza mara kwa mara kwenye vyombo vya majini umeelezwa kwamba unaweza kusaidia kuondosha vyombo vya majini visivyokuwa na ubora na hivyo kusaidia kupunguza majanga yanayoweza kujitokeza wakati wakiendelea kutoka huduma hizo ikiwemo meli 

Hayo yalisemwa na Meneja wa Usajili,Ukaguzi na Udhibiti wa Usalama wa Vyombo vya maji Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Afred Waryana wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo mabaharia na wadau wa masuala ya usafirishaji wa majini iliyoandaliwa na shirika la hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi. 

Alisema kwamba wanafanya hivyo ili kuhakikisha meli zinazofanya kazi na kutoa huduma majini wamiliki wake wanafuata taratibu na viwango vinavyostahili ikiwemo kuwa na ubora ili kuweza kuepusha majanga ambayo yanaweza kujitokeza wakiwa wanaendelea na shughuli hizo. 

“Tumekuwa tukifanya kaguzi mbalimbali kwa lengo la kujirihidhisha na ubora wa meli husika na hili hufanyika wakati wa meli inajengwa kabla ya kuingizwa majini, ukaguzi wa kila mwaka kuhakikiwa kwamba ina ubora”Alisema 

Aidha alisema pia wamekuwa wakifanya ukaguzi wa kila baada ya miaka miwili na nusu kwa meli kutolewa kwenye maji na kuangaliwa kama bado ina viwango hiyo yote ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha vyombo vya majini vinavyotoa huduma majini vinakuwa na ubora unaotakiwa. 

Mkurugenzi hiyo alisema kwamba kaguzi hizo zipo kwa mujibu wa sheria lengo likiwa ni kuhakikisha meli hazitoi huduma bila kukaguliwa huku akieleza wanafanya za kushtukiza kuzuia watu kufanya shughuli za meli bila kukaguliwa. 

Alisema kwa sasa wanafanya ukaguzi kwa vyombo 6000 vya majini nchi nzima kwa kila mwaka huku vyombo vikubwa meli kubwa na ndogo vilivyo zaidi ya tano 50 kwenda juu wanakagua zaidi ya kaguzi 230. 

Awali akizungumza wakati akiwasilisha mada kwenye warsha hiyo Captain Hilaly Salum kutoka Chuo cha Mabaharia (DMI) Dar es Salaam akiwasilisha mada ya tatu katika Warsha hiyo alikieleza chuo hicho pekee Afrika Mashariki kilichoanzishwa miaka 42 iliyopita kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kiteknolojia na hali ya kiuchumi.

Alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali na taasisi kukisaidia chuo hicho kupata vyombo kwa ajiri ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi ambavyo vitawawezesha kufanya majaribio wasifu pamoja na kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa ngazi ya chini ambao hawana uwezo kugharamia masomo hayo.

“Endapo serikali itagharamia elimu hiyo kwa wanafunzi wa chini wasiyo na uwezo kifedha wa kulipa ada licha ya kuwafanya kupata ajira lakini pia watailipa serikali kodi na hivyo kuchangia uchumi wa taifa”alieleza Salimu.

Awali wakichangia mjadala baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waliiomba serikali kufanya uwekezaji katikamazao ya baharini kama inavyofanya kwenye sekta mbalimbali nchini na kwamba kufanya hivyo kutaongeza pato la taifa kwa madai kuwa bahari ndiyo eneo pekee lenye uwezo mkubwa wa kufanya uwekezaji Duniani. 

RAIS MSTAAFUMKAPA MGENI RASMI UZINDUZI MAADHIMISHO YA MIAKA 20 KUELEKEA MIAKA 25 TANGU KUANZISHWA KWA CHUO KIKUU SAUT

$
0
0

Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Mwanza kuhusu uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 kuelekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT) utakaofanyika Julai, 2 mwaka huu jijini Mwanza ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin. Kulia ni Mratibu wa Kamati ya Habari-Maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya miaka 20/25 ya chuo cha SAUT Padre Titus Ngapemba na Rais wa Serikali ya wanachuo Elian Rodrick (kushoto). 
……………… 

Na Eleuteri Mangi- SAUT 
Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 20 kuelekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Mt. Augustino Tanzania (SAUT). 

Kwa mujibu wa Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu amesema kuwa chuo kimemualika Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa kwa kutambua na kuthamini mchango wake katika elimu ya juu ambapo uzinduzi wa maadhimisho hayo unatarajiwa kufanyika chuoni hapo Julai, 2 mwaka huu jijini Mwanza. 

Akiongea na waandishi wa habari leo chuoni hapo makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Balozi Prof. Mahalu amesema kuwa yapo mafanikio mengi ambayo chuo kinajivunia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 204 hadi wanafunzi 11400 kwa mwaka wa masomo 2018/2019 licha ya kwamba katika mwaka wa masomo 2012/2013 udahili uliwahi kufikia wanafunzi 13121 kabla ya kuongezeka kwa matawi 13 ya chuo hicho. 

“Katika mtaala wa chuo, wanafunzi wanapata fursa ya kusoma masomo ya 
ujasiriamali na kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao na hivyo kuondokana na dhana ya kungoja kuajiriwa. Chuo kimeboresha kiwango cha elimu inayotolewa kuhakikisha wahitimu wanahimili soko la ushindani Afrika Mashariki na duniani kote pia kutokana na elimu ya dini na maadili kwa wanafunzi wote.” 

Amesema Balozi Prof. Mahalu 
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali, Balozi Prof. Mahalu amesema kuwa chuo kimefanikiwa kuanzisha kituo cha kuzalisha na kuwawezesha wajasiriamali ambapo wanafunzi wanaohitimu masomo yao wanapata fursa ya kuandika mawazo ya biashara na baada ya mawazo yao kukubalika hupatiwa mafunzo maalumu juu ya mawazo hayo na kisha wanapatiwa mtaji kati ya shilingi milioni 25 hadi 30 kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali. 

Aidha, chuo hicho kimefanikiwa kuongeza vitivo vingine vinne (4) kutoka kitivo kimoja ambacho kilikuwa cha Sayansi ya Jamii na Mawasiliano kilichokuwa na shahada moja ya Mawasiliano ya Umma na kuongezeka kwa Kitivo cha Biashara na Utawala, Kitivo cha Ualimu, Kitivo cha Sheria na Kitivo cha Uhandisi. 

Zaidi ya hayo Balozi Prof. Mahalu amesema chuo cha SAUT kina mchango mkubwa katika kutoa wanataaluma na wataalam katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wahadhiri, Wanahabari, Wanasheria, Wasimamizi katika taasisi za Fedha na Wakaguzi wa Fedha, Walimu, Wahandisi, Wafanyabiashara, Watunza amani katika majeshi ya Ulinzi na Usalama pamoja na Wanasiasa. Miongoni mwa wahitimu hao ni Mhe. Dotto Biteko Waziri wa Madini, Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, Zawadi Machibya na Sammy Awami ambao ni watangazaji wa BBC, pamoja na wataalamu mbalimbali wanaofanya kazi ndani na nje ya nchi. 

Chuo cha SAUT nje ya taaluma pia kinatoa huduma kwa jamii ambapo kimefanikiwa kuanzisha mradi mkuwa wa umeme wa kutumia nishati ya jua kwa kushirikiana na nchi ya Ujerumani ambapo mradi huo unatekelezwa katika vijiji mbalimbali katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kagera na Geita. 
Naye Mratibu wa Kamati ya Habari-Maandalizi ya kuelekea miaka 20/25 ya chuo cha SAUT Padre Titus Ngapemba amesema kuwa Rais Mtaafu Benjamin Mkapa amekuwa mdau muhimu katika sekta ya Elimu nchini katika ngazi mbalimbali za uongozi. 

Padre Ngapemba amesema kuwa Rais mstaafu Benjamin Mkapa amekuwa mdau muhimu katika sekta ya elimu nchini na kwa namna ya pekee katika chuo cha SAUT, akiwa madarakani alifanikisha ujenzi wa barabara ya kutoka jijini Mwanza kuingia chuoni hapo ambapo ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ulianza mwaka 2002 na kuzinduliwa mwaka 2004.” 

“Mzee Mkapa anakumbukwa sana kwa kuwa mwasisi wa utoaji wa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa vyuo vyote vya umma na binafsi. Uamuzi huu wa Mzee Mkapa wa kuwapatia mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu binafsi umesaidia Watanzania wengi kusoma elimu ya juu. Kwa hili utakumbukwa Mzee Mkapa” alisisitiza Padre Ngapemba. 

Padre Ngapemba aliendelea kusema “Kwa mara ya kwanza mwaka 2005 Serikali ya Awamu ya Tatu ilibadilisha Sera ya mikopo ya elimu ya juu na kuanza kutoa mikopo kwa vyuo vikuu binafsi ikiwemo SAUT baada Makamu wa Mkuu wa chuo wa wakati huo Padre Deogratius Rweyengeza kutoa ombi hilo wakati wa mahafali ya kwanza mwaka 2001 tangu kipandishwe hadhi.” 

Chuo Kikuu cha SAUT kinamilikiwa na kusimamiwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kimeanzishwa kwa mujibu wa sheria za nchi na kinafanya kazi chini ya Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) kwa mujibu wa masharti ya vyuo vikuu sheria namba 7 ya mwaka 2005 ambapo awali kilikuwa kinajulikana kama Chuo cha Maendeleo ya Jamii Nyegezi (NSTI) kilichoanzishwa tangu mwaka 1960 na wamisionari wa kanisa katoliki ambao kwa sasa wanajulikana kama Wamisionari wa Afrika wakiwa chini ya Askofu Mkuu Joseph Blomjous wa Jimbo Kuu la Mwanza.

MBUNGE VITI MAALUM MKOA MJI ASHA AWATAKA WANAWAKE NCHINI KUIPIGANIA CCM

$
0
0


Na Is-haka Omar,Zanzibar. 

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdalla Juma ‘Mshua’,amewataka Wanawake katika Nchini kuamini,kulinda na kuipigania CCM na kuhakikisha inashinda kwa kishindo mwaka 2020 kuliko Chaguzi zote zilizopita toka kuanzishwa Mfumo wa Vyama Vingi Mwaka 1992. 

Amesema Serikali za Awamu ya Saba ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini wa Marais wake ambao ni Dk.Shein na Dkt.John Pombe Magufuli, wamesimamia utekelezaji wa mambo mengi ya kimaendeleo yanayokidhi mahitaji ya Wanawake na jamii nzima kwa ujumla. 

Hayo ameyasema wakati akifungua Kikao cha Baraza la UWT Wilaya ya Amani kilichofanyika katika Ofisi za Wilaya hiyo Sebleni Amani Unguja. 
Mhe.Asha alieleza kwamba kupitia Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 Serikali imeimarisha Huduma za Afya,Miundombinu ya Barabara,Umeme,Elimu,Mikopo kwa Wanawake yenye masharti nafuu pamoja na kutoa fursa za Uongozi kwa Wanawake katika Chama na Serikali zote mbili. 

Alisema kutokana na mambo mengi ya kimaendeleo yaliyotekelezwa Nchini, Wanawake wanatakiwa kuunganisha nguvu zao bila ya kujali bila ya kujali tofauti za Vyeo,rangi na kabila wahakikishe CCM inashinda kwa ngazi zote katika Uchaguzi Mkuu ujao kwani hiyo ndio njia pekee ya kuthamini kwa vitendo juhudi zinazofanywa na Serikali. 

Kupitia Mkutano huo aliwasihi Wajumbe wa Mkutano huo na Wanawake mbali mbali kuendeleza Umoja na Mshikamano katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa ndani na nje ya UWT, kwa lengo la kuandaa mazingira rafiki ya kisiasa yatakayoimarisha CCM. 

Aliwakumbusha Akina Mama hao kwamba pamoja na majukumu waliyokuwa nayo wanatakiwa kusimamia Malezi ya Watoto katika Maadili mema na kuhakikisha wanalindwa dhidi ya Vitendo vya Udhalilishaji. 
Akizungumzia suala la uimarishaji wa Chama na Jumuiya hiyo, Mhe.Asha alisisitiza umuhimu wa kuongeza Wanachama Wapya wenye Sifa kisheria za kuipigia kura CCM kwa kila Uchaguzi wa Dola. 

“Kila Mwanachama kwa nafasi yake aanze kuwatafuta Wapiga kura Wapya wa makundi yote wenye Sifa za kupiga kura, waelezeni mazuri mengi yanayopatikana ndani ya CCM japokuwa mengi wanayaona na kuyatambua lakini bado tuna jukumu la kuwakaribisha kwa ukarimu kwani CCM ni Chama cha Wote,,,Nyumbani kumenoga.”,alisema Mhe.Asha. 

Kupitia Kikao hicho Mhe.Asha,alikabidhi Komputa Moja na Printer Moja ya Kisasa ya rangi kwa Uongozi wa UWT Wilaya hiyo ili watekeleze kwa ufanisi shughuli mbali mbali za Umoja huo. 

Naye Katibu wa UWT Wilaya hiyo Ndugu Asha Mzee Omar,akisoma taarifa ya Utendaji wa kazi za UWT, alisema Viongozi,Watendaji na Wanachama wanashirikiana vizuri huku wakijipanga vizuri kukabiliana na dalili zozote za upinzani ili CCM ishinde katika uchaguzi ujao. 

Amesema katika mikakati ya kuimarisha Jumuiya wamesimamia vizuri vikao vya ngazi za Matawi hadi Wilaya kuhakikisha vinafanyika kwa mujibu wa Katiba sambamba na kufanya ziara,vikao na mafunzo ya kuwajenge uwezo Akina Mama juu ya masuala mbali mbali ya kisiasa na kujikwamua kiuchumi.
 
Akizungumza Mjumbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma, aliupongeza Uongozi wa Wilaya hiyo kwa kutekeleza masuala ya msingi ya kiutendaji yenye dhamira ya kuimasha UWT na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla. 

Kwa upande wake Mjumbe wa Mkutano huo,ambaye pia ni Mwakilishi wa Viti Maalum Mhe.Saada Ramadhan Mwendwa, alisema kupitia kikao hicho Wanawake kutoka ngazi mbali mbali za Uongozi watajengew uwezo ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi. 

Mkutano huo wa Siku Moja ulioandaliwa na UWT Wilaya ya Amani kwa kushirikiana na Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Unguja.

WAREMBO MISS ARUSHA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA ZIWA MANYARA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

Warembo wanaowania taji la Miss Arusha 2019 wameaswa kuwa wahamasishaji na mabalozi katika kutangaza vivutio vya utalii vilivyoelekezwa hapa nchini .

Hayo yalisemwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi Ziwa Manyara, Noela Myonga ambaye alikutana na warembo 16 wanaowania taji la Miss Arusha waliofika kutembelea hifadhi hiyo ya taifa ambapo aliwasihi wawe mabalozi katika kutangaza utalii .

Akizungumza na warembo hao, Myonga alisema urembo umebebwa na vigezo vingi ikiwa ni pamoja na kuwa na ufahamu wa mazingira uliopo pamoja na kujua vivutio mbalimbali vya utalii.

"Katika hifadhi hii Kuna vivutio vya kitalii ikiwa ni pamoja na Simba
wakweao miti ,makundi makubwa ya tembo na nyati, aina mbalimbali za ndege, bwawa la viboko, chemchem za maji Moto,ukuta wa bonde la ufa,Ziwa lenye mandhari ya kupendeza ambalo ni makazi ya makundi makubwa ya ndege aina ya heroe pia wingi wa aina za wanyama,alisema Myonga.

Noela alitoa shukurani kwa Kampuni ya Function House kwa kuruhusu warembo hao kufika katika hifadhi hiyo na aliwasihi waeendelee kutangaza utalii huu wa ndani.

Naye Meneja Itifaki wa Kampuni ya Function House Basili Elias alisema
safari ya kutembelea vivutio vya utalii ilianzia katika hifadhi ya mkomazi
na wameendelea kwa kutembelea hifadhi ya ziwa Manyara lengo ikiwa ni
kuwawezesha washiriki kwa pamoja kwenda sambamba na kauli mbiu ya serikali ya kuhamasisha utalii .

"Sisi Kama waandaaji wa Miss Arusha 2919 tumeamua kuhamasisha utalii wa ndani na warembo hao ambao tunaimani watakuwa mabalozi wazuri kwani urembo si sanaa tu bali unagusa masuala mbalimbali ikiwemo uhamasishaji na kupata elimu ,"alisema Elias.

Shindano la Miss Arusha litafanyika julai 5 katika ukumbi wa Point Zone
uliopo ndani ya Jiji la Arusha,
warembo wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa uhifadhi Ziwa Manyara Noela Myonga ,na muhifadhi ujirani mwema Ibrahimu Ninga

Halmashauri Kuu ya mkoa wa Arusha CCM yapokea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020

$
0
0
Na,Vero Ignatus Arusha.

Halmashauri Kuu ya mkoa wa Arusha CCM imepokea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 Kwa kipindi cha Robo Tatu ya Mwaka wa Fedha Julai-March 2019.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao hicho Katibu mkuu wa CCM mkoa Mussa Matoroka amesema kuwa kabla ya kufanya kikao hicho walifanya ziara katika wilaya zote zilizopo mkoani humo kukagua shughuli za maendeleo na kujiridhisha.

Mrisho Gambo amesema kuwa hali halisi ya mapato katika mkoa huu ni ndogo ukilinganisha na matumizi kwa mwaka huku akisema kuwa serikali kuu imekuwa ikiibeba mkoa ili kukukidhi mishahara ya wafanyakazi mkoani humu.

Aidha amesema serikali imefanya mambo mengi Sana katika mkoa huu Kama za ujenzi wa barabara  za lami na sisizo za lami huku, kujenga madaraja ya kiwango kizuri ili kurahisha huduma za kijamii pamoja na upatikanaji  wa mkoani maji ya kutoka mkoani hapa.

Aidha amesema kuwa Serikali kwa nguvu kubwa imeweka nguvu kubwa katika kujenga barabara la lami yenye kilimita 49 Wilayani Ngorongoro jambo ambalo halijawahi kufanyika tangu uhuru wa Tanzania bara.

Katika uwasilishaji huu, Mrisho Gambo amesema kuwa Serikali pia imewezesha upatikanaji wa maji ya kutosha kwa asilimia mia moja pindi mradi utakapokamilika na wanachi wote mkoa ni watapata maji safi na salama ukilinganisha na asilimia 40 ya maji
 yanayopatikana kwa sasa.

Kuhusu huduma za afya, Mrisho Gambo amesema ametoa fedha za kujenga hospitali za Wilaya katika zote mkoani Arusha hivyo kufanya Kila wilaya kuwa na hospitali yake huku akisema kuwa bado serikali imejenga vituo vipya vya afya katika mkoa mzima wa Arusha.
 
Aidha  Gambo amewataka viongozi wa dini kuendelea kuiombea na nchi na kudumisha na kuhubiri Amani katika ibada zao kwani ikiondoka hakuna atayeweza kuirejesha Ameongeza kuwa miradi hiyo inayosimimamiwa na kutekelezwa na  Serikali haijapata msaada wowote toka nje, amesema yote ni mapato na makusanyo ya ndani.

Naye kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Arusha Jonathan Shani amesema kuwa katika kutekeleza ilani ya CCM, Jeshi la Polisi mkoani hapa wanatekeleza kwa kudumisha ulinzi na Usalama kama jina lijulikanavyo la Geneva of Africa.

Aidha ametoa onyo kali kwa watakaojaribu kuhamasisha ama kujaribu kuandama huku akisema kuwa wanaendelea kuhakikisha Arusha itakuwa mbali na madawa ya kulevya.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi lipo kuwalinda wananchi wote ila akatoa wito kwa kwa wanawake kuwa ulinzi upo kwao na Kila atakayemtesa mwanamke atachukuliwa hatua stahiki kwa wanaowanyanyasa wake zao.

Hata hivyo kamanda huyo amesema kuwa ulinzi katika mkoa wa Arusha na mipaka yake upo imara na kwamba wananchi wote wasiwe na shaka


Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images