Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU AVUTIWA NA UWEKEZAJI WA BENKI YA MAENDELEO YA TIB

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amevutiwa na uwekezaji wa unaofanywa na Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kuyakopesha makampuni ya wazawa hivyo kuchochea ajira nchini.

Waziri Mkuu alionyeshwa kufurahishwa kwake na bidhaa zilizokuwa zikionyeshwa katika banda la Benki hiyo wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Tamasha la Uwekezaji Dodoma, yanayoendelea jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Waziri Mkuu Majaliwa, Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki hiyo, Bw. Patrick Mongella alisema kuwa Benki ya Maendeleo ya TIB inaendelea kutekeleza kwa vitendo juhudi za serikali kwa kuwezesha uwekezaji wa viwanda nchini ili kuongeza ajira na kuondoa umaskini kwa Watanzania.

“Tumeshiriki Tamasha ili kutangaza fursa zilipo kwenye benki yetu ili kuongeza ufanisi katika kugharamia miradi ya maendeleo ya kiuchumi hasa ile ya kimikakati inayotoa ajira kwa Watanzania,” alisema.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Patrick Mongella (kulia). Kushoto ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Bw. Joseph Chilambo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya vipeperushi vilivyokuwa vikioneshwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya TIB. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki hiyo, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Chilambo (wapili kushoto) na Meneja Masoko na Uhusiano, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia).
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Patrick Mongella (wapili kulia) akimuonesha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa kutokana na mkopo uliotolewa na benki hiyo. Wengine pichani ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo Bw. Joseph Chilambo (wapili kushoto) na Meneja Masoko na Uhusiano, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia).

KENYA IS FULLY COMMITTED TO EAC INTEGRATION PROCESS - EAC CS DECLARES

$
0
0

cid:5cc40b6c-53ac-4312-8698-e2bfa635d25b
East African Legislative Assembly


…dissociates Government/citizens & clears the air over remarks made by Starehe legislator

East African Legislative Assembly, Arusha, Tanzania: 27 June, 2019: The Government of Kenya has clarified the matter over the recent offensive utterances made by a Member of Parliament of Starehe Constituency in Nairobi.

Kenya’s Cabinet Secretary, Ministry of East African Community and Regional Development, Hon Adan Mohammed, informed the Sitting of the East African Legislative Assembly this morning that the Republic of Kenya was “duly and fully” committed to the EAC integration process.

In addition, Hon Mohammed, while dissociating the Government of the Republic of Kenya from the utterances of the MP, sounded a stern warning to other like-minded leaders in the country and region who may be harboring similar agenda.

And in a show of unity, the Cabinet Secretary, Hon Adan Mohammed, re-echoed the statement by the Prime Minister of the United Republic of Tanzania, Rt Hon Kassim Majaliwa Majaliwa to the Parliament of Tanzania in Dodoma on Tuesday, 25th June 2019, reiterating commitment to integration process and never to allow situations that “sow of seeds of discord” between the Tanzanian and Kenyan people, and with the brothers and sisters in the East African Community.

“I would like to reiterate the Kenya Government’s unwavering commitment to EAC integration, the EAC Treaty and all the protocols that we have signed and ratified”, Hon Mohammed told an attentive House.  The Cabinet Secretary emphasized that Kenya’s commitment to integration stemmed from the top – led by none other than the President – H.E. Uhuru Kenyatta.

“Mr. Speaker, Members of this Assembly are aware that the Kenyan President, H.E. Uhuru Kenyatta is on record on several occasions in his public addresses, making it abundantly clear that East Africans are welcome to visit Kenya, to invest, to visit for pleasure and even marry and settle in Kenya so long as they do so in accordance with the local laws. That position has not changed. Kenya is at the forefront in the implementation of the various provisions of the Common Market Protocol, including the one on free movement of people and labour”, Hon Mohammed remarked.

“Kenyans and indeed all East Africans, must get used to the idea of the EAC Common Market that provides for non-discrimination of citizens of other EAC Partner States on the basis of their nationality and guarantees protection of EAC citizens and their property as provided for under Article 7(2) of the EAC Common Market Protocol”, Hon Mohammed added.

Two days ago (June 25th, 2019), a video clip of Hon Charles Njagua Kanyi (Jaguar) emanated in his Starehe constituency, calling for the expulsion of foreign nationals including East Africans from the Republic of Uganda and the United Republic of Tanzania, from Kenya within 24 hours or to be forcefully removed. 

The utterances did not sit easily in Kenya and across the borders. The Country’s Foreign Affairs Permanent Secretary, Macharia Kamau said Kenya regrets the careless and inciteful remarks while Government Spokesperson, Col (Rtd) Cyrus Oguna assured foreign investors of their security terming the remarks ‘unfortunate’. The MP has since been arraigned in Court and is facing charges of inciting voters against foreigners. The Court is to rule on his bail application tomorrow.

In his address to the House today, Hon Mohammed was categorical that such acts that contravene the EAC Treaty would not be tolerated. “This incident is indeed a wake - up call to all of us to keep our eyes and ears open across the region, to safeguard against leaders advocating for policies that are inconsistent with our East African integration agenda. We must not allow certain leaders to incite EAC citizens against one another on the one hand, and yet still urge our people to embrace our motto and spirit of One People One Destiny, on the other”, the Cabinet Secretary stated.

Following the Cabinet Secretary’s statement and in the spirit of co-operation, Hon Abdullah Makame, Chair of the EALA Chapter, United Republic of Tanzania, swiftly moved to withdraw his notice to table a motion urging the EAC Partner States to ensure that freedoms, rights, and treatments of East Africans as guaranteed under the EAC Treaty are adhered to.  

Hon Makame thanked the Government of Kenya, for the assurances that it would defend the integration process to a hilt.“I thank Hon Mohammed and the High Commissioner of Kenya in the United Republic of Tanzania, Hon Dan Kazungu for the swift action taken”, Hon Makame remarked.
 A section of the Members of EALA earlier today.
 Hon Dr Abdulla Hasnu Makame; withdrew his motion urging Partner States to ensure freedoms, rights, and treatments of East Africans as guaranteed under the EAC Treaty is adhered to
Hon Adan Mohammed ,  Kenya's Cabinet Secretary, Ministry of EAC and Regional Development makes his statement in the Assembly.

ASSEMBLY ADJOURNS BUDGET DEBATE, DEMANDS PRESENCE OF COUNCIL OF MINISTERS

$
0
0

cid:5cc40b6c-53ac-4312-8698-e2bfa635d25b
East African Legislative Assembly

…Only Burundi’s EAC Minister was on front-bench

 The debate and approval of the EAC Budget proposals for the Financial Year 2019/20, will now be delayed for another day following the adjournment of debate this afternoon. EALA Member, Hon Rose Akol, this afternoon moved a motion for adjournment, (under Rule 30 (c) of the Rules of Procedure of the EALA), citing the absence of the majority of the Members of the Council of Ministers, with only Burundi’s EAC Minister, Hon Isabelle Ndahayo in attendance.

In her submissions, Hon Akol lamented over the absence of the Members of the Council of Ministers who occupy the front-bench. “Ideally, in the respective EAC ministries, for every Minister, there is a deputy minister. It is absurd just to have one in attendance. We must, therefore, adjourn until such time when the Council of Ministers is represented and prepared to come and address issues on the budget. We cannot talk much when the front bench is empty”, the legislator said.

Hon Abdikadir Aden noted the absence of the front bench was not a good sign given the fact that the budget is a critical matter. Hon Susan Nakawuki on her part called for more attention by the EAC Council of Ministers. “We are not ready to proceed with the debate”, the legislator said

Hon Noor Mohammed termed the budget session as too critical for the Assembly to be seen to be ‘talking to itself’. Hon Kim Gai however, said the Council of Ministers and the General-Purpose Committee had agreed in principle during the Committee level and that it was therefore in order for the House to continue with its business, a move that was defeated.

While guiding the House, Speaker, Rt Hon Ngoga Martin said in terms of legality, the Assembly was duly constituted since nothing in the Rules of Procedure bars it for conducting business in absence of Ministers. The rules he said did not specify about quorum issues when it comes to the attendance of the Members of the front bench.

The House unanimously decided to adjourn the business to tomorrow afternoon (June 26th, 2019).  As per the Order Paper, the House was expected at the session to resolve itself into a Committee of Ways and Means and a Committee of Supply to consider and approve the Financial Statement and approve the estimates of expenditure and revenue for the next Financial Year.

Last week, the Assembly received the EAC Budget speech presented to the House by the Deputy Minister for Foreign Affairs and East African Co-operation, United Republic of Tanzania, Hon Dr. Damas Ndumbaro, on behalf of the Chairperson of the EAC Council of Ministers. The estimates for the Financial Year 2019/20 amounts to $111,450,529.

The Chair of Council while presenting the speech had proposed that the 2019/2020 Budget be allocated to the Organs and Institutions of the EAC as follows; East African Community Secretariat ($53,296,404), East African Legislative Assembly ($18,973,845) and the East African Court of Justice ($4,225,241). The Inter-University Council for East Africa shall receive ($9,586,426), Lake Victoria Basin Commission ($13,193,849) while $ 4,061,145 is earmarked for the Lake Victoria Fisheries Organization.   On their part, the East African Science and Technology Commission shall receive ($ 1,915,073), East African Kiswahili Commission ($ 1,474,775) and the East African Health Research Commission ($ 3,996,270). The East African Competition Authority is to benefit from an amount of $727,501 in the Financial Year 2019/20.
 Hon Rose Akol, mover of the Motion that adjourned the House citing the absence of EAC Ministers during the budget debate


 Hon Noor Mohammed supported the motion to adjourn the House
A section of Members, moments after the Speaker adjourned the Sitting.  The House is expected to resume tomorrow




MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA (NEC) YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM- Zanzibar, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein , Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Phillip Mangula wakiimba wimbo wa Chama mara baada ya kuwasili ukumbini katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM- Zanzibar, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein , Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Phillip Mangula wakiimba wimbo wa Chama mara baada ya kuwasili ukumbini katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha halimashauri kuu ya Chama hicho (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019
 Wajumbe wa halimashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wakiimba wimbo wa Chama mara baada ya kuwasili ukumbini Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha halimashauri kuu ya Chama hicho (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019


 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Ccm Taifa  (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019



 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao cha halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Ccm Taifa  (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019



 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM- Zanzibar Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohhamed Shein wakati wa kikao cha halimashauri kuu ya Chama hicho (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM- Zanzibar Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohhamed Shein wakati wa kikao cha halimashauri kuu ya Chama hicho (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam.  
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo katika cha halimashauri kuu ya Chama hicho (NEC) kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na mjumbe  halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Taifa Mhe. Zuberi Ali Maulid katika kikao cha NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27, 2019
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Arusha na mjumbe  halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Taifa Loata Sanare katika kikao cha NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri mkuu mstaafu na mjumbe wa halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Taifa Mizengo Pinda mara baada ya kikao cha  NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe wa kamati kuu mpya aliyeteuliwa katika kikao cha NEC ambaye pia ni mjumbe wa halimashauri kuu ya Chama Mapinduzi Taifa Munde Tambwe mara baada ya kikao cha  NEC kilichofanyika jijini Dar es Salaam.June 27,2019




MISA TANZANIA, ICNL WAJADILI NA WADAU CHANGAMOTO ZA KISHERIA KWA VYOMBO VYA HABARI

$
0
0
Mkurugenzi wa MISA Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akichangia mada katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari. Geline Fuko (kushoto) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Network of Legal Aid Provider Christina Kamili (kulia) akiwasilisha mada wakati wa siku ya pili ya warsha hiyo. Na Mwandishi Wetu Katika kuendeleza hamasa na kutetea uhuru wa kujieleza katika jamii, MISA Tanzania na shirika la utetezi wa sheria na haki za kijamii la ICNL zimewakutanisha wadau mbali mbali katika warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari. Warsha hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya habari,asasi za utetezi wa haki za binadamu, wanasheria pamoja na wahadhiri wa vyuo vikuu. Warsha hiyo ya siku tatu iliyofanyika mjini Bagamoyo ambayo ni muendelezo wa warsha iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu ililenga kuwakutanisha wadau hao kwa lengo la kujadili zaidi namna sheria za vyombo vya habari zinavyo athiri mazingira ya kazi za kiuandishi pamoja na uhuru wa kujieleza. Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akiendesha warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL. Kadhalika akielezea umuhimu wa uwepo wa sheria rafiki katika kufanya mazingira yawe salama kwa tasnia ya habari,Bw.Aloys Habimana kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL lenye makao makuu yake nchini Marekani amesema changamoto ya sheria zisizo rafiki kwa taaluma ya habari na uhuru wa kujieleza ni changamoto sehemu nyingi duniani Afrika ikiwa na mifano halisi. "Pamoja na mazingira haya nawasihi msivunjike moyo wala kukata tamaa, masuala ya kisheria hayabadiliki kwa siku moja yanahitaji kupitia hatua kadhaa na kila jambo linaweza kupatiwa ufumbuzi hasa wadau wote watakaposhirikiana na kujenga hoja zenye ushawishi na tija kwa pande zote", alisisitiza Bw.Aloys. Bi.Lily Liu kutoka shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL akijadili jambo pamoja na wadau walioshiriki warsha hiyo. Sambamba na hilo Bi.Lily Liu mjumbe kutoka ICNL aliahidi kuwa shirika lao litaendelea kushirikiana na wadau husika katika nyanja zote ili kufanikisha na kutimiza adhma ya kuwa na jamii isiyo na sheria kandamizi zinazoathiri dhana nzima ya uhuru wa kujieleza na vyombo vya habari. Warsha hiyo iliyojikita zaidi katika mfumo wa washiriki kubadilishana mawazo na uzoefu wao wa mazingira ya kazi pamoja na namna hali inavyobadilika na kubanwa kwa uwepo wa sheria zisizojitosheleza. Washiriki warsha hiyo wakijadili baadhi ya sheria na kanuni katika makundi. Mkurugenzi wa Highlands Fm Radio ya Mbeya Bi. Jacqueline Lawrence akiwasilisha mada kwa niaba ya washiriki wenzake Washiriki wa warsha ya utetezi wa sheria za vyombo vya habari iliyoandaliwa na kuendeshwa na MISA kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la utetezi wa haki za kijamii la ICNL wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungwa kwa warsha hiyo.

INTRODUCING "MIDADI" NY IZZO BIZNESS feat. ASLAY

KASI YA RAIS MAGUFULI YAWAKUNA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA CCM

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kasi ya Ujenzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari, Rais Dkt. John Pombe Magufuli imewavutia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza Ilani yake ya Chama kama ilivyoahidi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Uwanja wa Ndege (Terminal 3), Ujenzi wa Barabara (Daraja la Mfugale, Ubungo Interchange), pamona na Bandari Kavu. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wajumbe hao wakati wakitembelea miradi hiyo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Pwani wakiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM),Humphrey Polepole, Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo, Livingstone Lusinde amesema wanampongeza Mhe. Rais na Serikali yake yote kwa kasi anayoionyesha.

"Wale ambao hawajaona maendeleo haya wasubiri kuona, anayebeza mambo haya sio mzalendo, ni mtu ambaye hajui maana ya maendeleo", amesema Lusinde.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba amesema maendeleo yanayoonekana sasa hivi ni jambo lakujivunia kwa Taifa zima kwa Mhe. Rais chini ya Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo yote yakimaendeleo.

"Kwa nchi za Afrika Mashariki tunajivunia Uwanja mkubwa wa Ndege, tunayaona maendeleo kwa kweli wale waliokuwa wanasema hakuna maendeleo wana sababu zao, siku zote mwenye macho haambiwi tazama", amesema Kate Kamba.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika picha ya moja mara baada ya kukaguwa  ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.      

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM)   wakati alipotembelea ujenzi wa reli ya kisasa ya standarge gaurge  katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali jana juni 26,2019.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa juu ya daraja Mfugale, katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali leo juni 26,2019.
 Msimamizi wa jengo la tatu la abiria kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere,Mhandisi Barton  Komba akitoa  maelezo kwa wajumbe wa Halmashauri kuu Taifa  katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali jana juni 26,2019.
 Mataaluma yakiwa tayari kwenye kiwanda cha kilichopo Soga mkoa wa Pwani kwaajili ya kwenda kuwekwa kwenye maeneo ambayo reli ya kisasa itapita.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kiwanda Mataaluma Soga mkoa wa Pwani.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Mchuzi Tv)

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakikaguwa ujenzi wa shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoa wa Pwani.
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea na ukaguzi wa jengo la tatu la abiria  kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere jana  juni 26,2019  katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Mchuzi Tv)

Mafundi wakiendelea na kazi katika mradi wa reli ya kisasa ya standarge gaurge
Muonekano wa jengo la tatu la abiria kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere.

'WE FARM' WAJA NA HUDUMA ZA KIDIGITALI KUWASAIDIA WAKULIMA TANZANIA

$
0
0
 Na Cathbert Kajuna - Kajunason/Michuzi TV
Katika kuhakikisha wakuliwa mbalimbali nchini wanapata taarifa za kilimo na kukifanya kiwe na tija, taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo ‘We Farm’ imenzisha mradi unaowaunganisha wakulima kuwasiliana moja kwa moja na kupeana taarifa zitakazowawezesha kutimiza mahitaji yao ya kilimo. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa taasisi hiyo Nicholus John amesema ujio wa ‘We Farm’ zaidi umelenga kutatua changamoto zinazowakabili wakulima ikiwemo kukosa taarifa sahihi zinazohusiana na masuala ya kilimo hicho na kuwafanya wapate hasara kwa kukosa au mazao wanayoyalima kutokidhi makusudio yao. 

Amesema mradi huo uliolenga kuwafikia wakuliza 400,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu, zaidi utawaunganisha wakulima hao lupitia simu zao za mikononi huku ukitumia mwanya huo pia kupata majibu ya maswali mbalimbali yanayohusiana na kilimo wanachokifanya. Nicholus amesema katika utekelezaji wa majukumu yake, ‘We Farm’ pia itafanya kazi kwa karibu na maafisa wa ugani waliopo katika halmashauri zote nchini ili kuleta tija zaidi katika kilimo hicho na hivyo kukuza uchumi wao pamoja na wa taifa kwa ujumla. 

“Huduma hii inawawezesha wakulima kuwasiliana wao kwa wao na kuelezana changamoto zilizopo katika kilimo na kupaena majibu juu ya maswali mbalimbali yanayojitokeza, kikubwa ‘we farm’ ni ukumbi wa majadiliano kwa wakulima” aliongeza Nicholus. 

Aidha amesema utafiti walioufanya hivi karibuni walibaini uwepo wa changamoto ya ukosefu wa taarifa kwa wakulima hao na hivyo kuwafanya washindwe kupata majibu katika masuala mbalimbali yanayohusiana na kilimo hicho. Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi hiyo Cyrila Anton amesema kupitia huduma hiyo, wakulima wataweza kupiga hatua katika kilimo wanachokifanya na hivyo kuwawezesha kupata mafanikio yanayotokana kilimo wanachokifanya.
Meneja Mkuu wa taasisi ya 'We Farm' Bw. Nicholus John akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam waliofika katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuijua taasisi hiyo na malengo yake katika kutoka huduma kwa wakulima nchini Tanzania. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.
Mkuu wa Idara ya ufuatiliaji wa taasisi ya We Farm Bi. Cyrila Anton akitoa ufafanuzi zaidi masuala mbalimbali ya wakulima.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakisikiliza mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo.
Mmoja ya viongozi akiuliza maswali.
Viongozi wa taasisi ya We Farm wakiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajenga uwezo.

INTRODUCING Diamond Platnumz's "Kanyaga" Official Music Video

TIC YAMJIBU ZITTO KABWE KUHUSU TAARIFA YAKE YA MIRADI YA UWEKEZAJI

INTRODUCING NEW SONG BY EVELYNE GIDEON "ANAFANYA"

KIKAO CHA AJENDA YA KITAIFA YA WAJIBU WA WAZAZI /WALEZI WA MALEZI NA MATUNZO YA FAMILIA KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA OFISI NDOGO YA WIZARA JIJINI DAR ES SALAAM

VOA SWAHILI KATIKA AFCON MISRI

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK

BI. HALIMA SALUM AMEWATAKA WATENDAJI WA TAASISI KUWA NA USHIRIKIANO

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa  Zanzibar Zahran Ali Hamad  akizungumza na Washiriki wa Mkutano wa Tathmin  ya Dawa huko  Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi nje kidogo ya Mji wa Zanzibar (Kulia) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya  Halima Salum na Mratibu wa Huduma za Ushaurinasaha na Uchunguzi wa Virusi vya Ukumwi Tatu Bilali
Afisa kutoka Ofisi ya Mfamasia Mkuu wa Serikali Said Mohamed akieleza mpango mkakati wa dawa katika mkutano wa tathmini uliyofanyika Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi nje kidogo ya Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa  Zanzibar Zahran Ali Hamad akiwatembeza washiriki wa mkutano wa tathmini ya dawa baada ya kumaliza mkutano wao wa siku moja maelezo. (Kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar  Halima Salum.
Meneja Bohari Kuu ya Dawa  Zanzibar Lydia Zungufya  akiongoza washiriki wa mkutano wa tathmini ya kuangalia uhifadhi wa dawa kabla ya kupelekwa hospitali na vituo vya afya.
*****************
Na Ramadhani Ali – Maelezo                        27.6.2019
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Maulid Salum ameshauri kuongeza ushirikiano baina ya watendaji wa Taasisi zilizomo ndani ya Wizara hiyo na Halmashauri za Wilaya katika kufanikisha usambazaji wa dawa kwenye vituo vya afya baada ya Serikali kufanya ugatuzi katika huduma za afya ya msingi.

Amesema suala la ugatuzi ni kitu kipya kwa Zanzibar, na watendaji wengi bado hawajauelewa vizuri, hivyo suala la ushirikiano na ufuatiliaji wa mara kwa mara ni jambo la msingi katika kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.
Naibu Katibu Mkuu alitoa ushauri huo Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi katika mkutano wa kutathmini utaratibu mzima wa uagiziaji, uhifadhi na usambazaji wa dawa katika hospitali na vituo afya.

Alisema kumejitokeza malalamiko kwa baadhi ya Halmashauri za Wilaya, hawatoi ushirikiano mzuri kwa Wafamasia wa Wilaya zao na hatimae baadhi ya vituo hukosa dawa na vyengine kuwa na mrundikano mkubwa wa dawa bila kuwa na matumizi na hatimae kumaliza muda wa matumizi.
Alisema upatikanaji wa dawa Zanzibar hivi sasa upo vizuri kufuatia Wizara ya Afya  kuongezewa bajeti ya kununulia dawa na jambo la msingi ni kuhakikisha zinatunzwa vizuri zinapofika kwenye vituo vya afya.

Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad amewahakikishia wadau wa Dawa walioshiriki mkutano huo kwamba wataendelea kutoa huduma bora kwa wakati kwenye hospitali na vituo vyote vya afya Unguja na Pemba.

Hata hivyo aliwataka wananchi wanapopata tatizo la afya kufika hospitali na vituo vya afya na kuhakikisha dawa wanazopewa wanazitumia kwa usahihi.Alisema baadhi ya wananchi huchukuwa dawa na kuzitumia kwa muda mfupi na baada ya kupata nafuu huzitupa bila ya kujua kwamba Serikali imetumia fedha nyingi kuziagiza. 

Aidha aliwataka wafanyakazi wa Bohari Kuu kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuhudumia jamii ya Zanzibar kwa uadilifu na mapenzi makubwa.
Mkutano huo wa siku moja wa wadau wa dawa uliangalia mafanikio yaliyofikiwa katika mfumo mzima wa dawa, changamoto na njia za kupunguza changamoto zilizojitokeza na njia za kuzitafutia ufumbuzi changamto hizo.

WANAUME WATAJWA KUONGOZA KWA KUFANYA VITENDO VYA UKATILI

$
0
0

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akizungumza na viongozi wa dini wakati wa kikao baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kikao cha kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akichangia jambo katika kikao baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na viongozi wa dini chenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akielezea athari za ukatili wa kijinsia na Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia katika kikao baina ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na viongozi wa dini chenye lengo la kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambaye ni Kamishana wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na viongozi wa dini mara baada ya kikao kilichowakutanisha viongozi hao kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

******************

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam

Jinsi ya kiume imetajwa kuwa ni moja kati ya watendaji wakubwa wa vitendo vingi vya ukatili dhidi ya Mwanamke na Mtoto katika jamii ambavyo vimekuwa vikiathiri malezi ya watoto na ustawi wa familia.

Hayo yamebainika leo jijini Dar es Salaam katika kikao katika ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Viongozi wa dini katika kujengewa uelewa kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia.

Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu, Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi amesema kuwa kwa mujibu wa Utafiti wa hali ya ukatili dhidi ya watoto uliofanyika na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na UNICEF wa mwaka 2011 unaonesha kuwa mtoto 1 kati ya watoto 3 wa kike na 1 kati ya 7 wa kiume walifanyiwa vitendo vya ukatili kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

Dkt. Ng’ondi ameongeza kuwa asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana walifanyiwa ukatili wa kimwili na vilevile robo ya watoto walifanyiwa ukatili wa kiakili.

“Uandaji wa Ajenda hii umetokana na hali halisi ya ongezeko la changamoto zinazomkabili mtoto hasa zinzaoanzia katika ngazi ya familia” alisema

Kamishna Ng’ondi ameeleza kuwa vitendo vya ukatili pia vimekuwa vikisababishwa na ongezeko la migogoro ya ndoa ambapo imesababisha watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili ambapo amesema kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Ustawi wa Jamii inaonesha kwa muda wa miezi tisa kuanzia Julai, 2018 hadi Marchi 2019 jumla ya mashauri ya ndoa 16,832 ukilinganisha na mashauri 13,382 kwa mwaka 2017/2018.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Manendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Mwajuma Magwiza ameeleza kuwa jamii ya kitanzania inakumbwa na changamoto nyingi zikiwemo ukatili dhidi ya wanawake na watoto na Serikali imekuwa ikiandaa mikakati mbalimbali katika kukabiliana na changamoto hzio ikiwemo Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi/Walezi katika malezi na matunzo ya familia.

Naye Mwakilishi wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Sheikh Hassan Said Chizenga amesema kuwa Ajenga hii inatakiwa kushirikisha Sekta nyingine kama vile utamaduni na michezo ili iweke misingi bora katika kujenga maadili ya watoto wetu katika malezi na makuzi yao.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Jamii kutoka Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) John Riziki amesema kuwa Baraza hilo limejidhatiti katika kuhakikisha wanasaidia na wazazi/walezi katika malezi kwa kufanya somo la dini kufundishwa katika shule za Msingi na Sekondari ili kuhakikisha watoto wanakuwa katika maadili mema.

Kikao hiki cha kuwajengea uelewa viongozi wa dini kuhusu Ajenda ya Kitaifa ya Wajibu wa Wazazi /Walezi wa Malezi na Matunzo ya Familia ambayo kinakuja mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(Mb) katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika mkoani Geita Juni, 16.

MADINI YENYE THAMANI YA SH.MILIONI 958 YAKAMATWA MPAKANI KWA TANZANIA NA KENYA...WATUHUMIWA WATATU WASHIKILIWA

$
0
0
Na Jusline Marco:Arusha

JESHI la Polisi mkoani Arusha limefanyika kukamata madini aina nane yenye thamani ya Sh. milioni 958 yaliyokuwa yakitoroshwa mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Kenya katika eneo la Namang.

Akizungumza leo na vyombo vya habari wakati akikabidhi madini hayo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)kwa ajili ya kuhifadhiwa,Waziri wa Madini Dotto Biteko ameliagiza Jeshi la polisi kuwafikisha watuhumiwa wote kwenye mikono ya dola.

Aidha Waziri Biteko ameagiza vyombo vyote ambavyo  vinasimamia haki  sheria ichukukuwe mkondo wake ili iwe mfano kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Pia ameongeza wajibu wake na wajibu wa Serikali ni kumlinda mwananchi ambaye anafanyakazi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha yule ambaye hatekelezi sheria,sheria iwezekuchukua mkondo wake dhidi. 

Awali akizungumza,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema utokewaji wa vibali kwa wafanyabiashara wa madini nchini na uwepo wa masoko ya uhakika ni ili kuwapa unafuu na kuondoa urasimu katika ufanyaji wa biashara zao.

Amesema pamoja na uondolewaji wa tozo hizo katika sekta ya madini anashangazwa kuwepo kwa baadhi ya watu wasio waaminifu katika sekta hiyo na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ambapo amesema kuwa ni lazima mahakama ziungane na serikali kulinda rasilimali za umma kwa kuhakikisha inatolewa adhabu kali kwa wa watu hao ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wenye tabia kama hizo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Jonathan Shanna amesema kuwa ukamatwaji wa utoroshwaji wa madini hayo ni kutokana na taarifa iliyotolewa na raia mwema ambapo saa tisa ya usiku wa kuamkia leo Jeshi la Polisi walifanikiwa kuwakamata watu watatu waliokuwa wakisafirisha madini hayo.

Amewataka watuhumiwa hao ni Joseph Abdallah(41), aliyekuwa dereva wa basi  la abiria la Perfect namba T 716 AAC ,Kondokta Mohamed Madume (36) na Latifa Abdallah(42) mkazi wa Sakina ambaye ndio mwenye mzigo huo na wote ni wakazi wa Arusha.
 Waziri wa madini Dotto Biteko wa kwanza kulia akikagua madini yaliyokuwa yamehifadhiwa benki kuu Mkoani Arusha baada  ya kukamatwa jana mpakani mwa longido na nchi jirani ya Kenya
Waziri Biteko akihakikisha madini hayo tayari kwa kuhifadhiwa katika ghala maalum la Benki kuu,wa kwanza kulia ni Gavana Mkazi Benki Kuu tawi la Arusha Charles Yamo

WAFANYABIASHARA WA MADINI WATAKIWA KUHUISHA LESENI

$
0
0

Ofisa madini Mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima (mwenye suti nyeusi) akizungumza na madalali na wafanyabiashara wa magonga ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani. 
Ofisa wa Tume ya madini Mirerani, Selemani Hassan akizungumzia juhudi za serikali za kuongeza wataalam na muda wa kufanya tathmini kwenye madini ya Tanzanite. 

WAFANYABIASHARA wa udalali wa madini ambao leseni zao zimemaliza muda wake wametakiwa kuhuisha na kuomba upya katika shughuli itakayotumia muda wa mwezi mmoja. 

Ofisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima akizungumza jana mji mdogo wa Mirerani alisema zoezi hilo litaanza Julai mosi hadi Julai 25 mwaka huu. 

Ntalima alisema anayedaiwa malipo ya mrabaha na ada ya ukaguzi anapaswa kukamilisha malipo yake kabla ya mwisho wa mwezi huu na hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kuzuiwa kuingia ndani ya ukuta. 

Alisema kila mfanyabiashara wa madini ili apate leseni mpya anapaswa kuwa na jalada la taarifa getini lenye nakala ya leseni na taarifa za ununuzi na mauzo na zionyeshe mfanyabiashara mkubwa anayenunua madini hayo 

“Vigezo vya kuhuisha leseni kwa wafanyabiashara wa madini ni kuwa na tin namba, kitambukisho cha mpiga kura, vielelezo vya ununuzi na uuzaji, wanunuzi wakubwa wawe na ofisi Mirerani, leseni iliyotolewa Mirerani na picha ndogo mbili,” alisema Ntalima. 

Mwenyekiti wa kamati ya maadili ya wanunuzi na madalali wa madini, Victor Kunyara alisema wamelipokea agizo hilo na watalifanyia kazi kwa maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla. 

Kunyara alisema wafanyabiashara wa madini ya Tanzanite hivi sasa wamepata elimu ya ulipaji kodi na wanalipa kodi pindi wakishauza madini yao. Dalali wa madini Hussein Msokoto alitoa ombi kwa serikali kuhakikisha wanatoa leseni inayolingana nao ili waweze kulipa kodi na wao kujiwezesha kiuchumi na familia zao. 

Msokoto alisema pia suala la wafanyabiashara kukusanyika pamoja na kutumia leseni moja linapaswa kutazamwa ili waweze kulipia na kufanya shughuli zao. 

Raphael Riaga alisema changamoto ya madalali kuendelea kulipia baadhi ya kodi ikiwemo kiwango sawa cha anayelipia leseni upya na anayekata leseni upya bado inawasumbua

NGOs nyingine zinasajiiliwa BRELA,Nyingine RITA,kuna Ubaya zikisajiliwa Dirisha Moja''? - Wabunge.

VIJANA WA KAMBI YA ARIEL WATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI VYA IPP ,MAKUMBUSHO YA TAIFA

$
0
0


Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Simiyu,Mwanza,Mara na Shinyanga wanaoshiriki Kambi ya Ariel 2019 leo Juni 27,2019 wametembelea Vyombo vya Habari vinavyomilikiwa na Kampuni ya IPP Media ambavyo ni ITV,Radio One, Capital Radio,Capital Tv,East Africa Tv ili kujifunza namna wanavyoendesha vipindi na kurusha matangazo.

Vijana na watoto hao pia wametembelea Makumbusho ya Taifa ili kujifunza historia ya mwanadamu na nchi ya Tanzania pamoja na kiwanda cha kutengeneza juisi kinachomilikiwa na Kampuni ya Bakhresa ili kujionea namna uzalishaji unavyofanyika. 

Ziara hiyo inakuja baada ya watoto hao wanaoshiriki kambi ya Ariel 2019 ya wiki moja iliyoanza Juni 23,2019 jijini Dar es salaam, kujifunza darasani masuala ya VVU/UKIMWI, kukua, ujinsia,ujasiriamali na kujengewa ujasiri na kujiamini ili waweze kutimiza ndoto zao. 

Kambi ya Ariel 'Ariel Camp' inasimamiwa na asasi inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) ambayo inafanya shughuli zake katika mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara. 
Kulia ni Mkurugenzi wa Radio One Stereo na Capital Radio ,Deogratius Rweyunga akiwaelezea vijana na watoto kutoka mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza na Mara wanaoshiri Ariel Camp 2019 namna wanavyoendesha vipindi vya radio. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mtangazaji wa kipindi cha Yaliyomo Yamo, Hatya Omary akiendelea na kipindi wakati vijana na watoto wa Ariel Camp 2019 walipotembelea studio ya Radio One. 
Meneja Mawasiliano wa asasi ya AGPAHI,Agnes Kabigi akizungumza 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'. Kabigi alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi kukaa na watoto na kuwaeleza kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI. 
Kijana akielezea kuhusu VVU na UKIMWI 'Live katika kipindi cha Yaliyomo Yamo cha Radio One Stereo'. 
Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Capital Radio, Abdallah Mwaipaya akitoa ufafanuzi namna wanavyoendesha vipindi vya radio. 
Hapa ni Control Room ITV: Kulia Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyoandaa vipindi vya Televisheni. 
Ndani ya chumba cha kurushia matangazo ITV na East Africa Tv: Mtaalamu wa IT wa ITV,Martine Kwalazi akiwaelezea vijana na watoto wanaoshiriki Ariel Camp 2019 namna wanavyorusha vipindi vya Televisheni. 
Hapa ni chumba cha kusomea taarifa ya habari ITV: Kulia ni Fundi wa ITV, Paul Urio akiwaonesha vijana na watoto namna wanavyoendesha vipindi vya habari. 
Vijana na watoto wakipiga picha na Mtangazaji wa Kipindi cha Habari za saa, Richard Stephen. 
Afisa Elimu Mwandamizi katika Makumbusho ya taifa,Anamery Bagenyi (aliyevaa nguo nyeupe) akielezea historia ya Makumbusho ya taifa yaliyoanzishwa mwaka 1940. Alisema katika Makumbusho hayo kuna maeneo matano ya kujifunza ambayo ni Chimbuko la Mwanadamu,jumba la maonesho ya kihistoria,jumba la michoro ya mapangoni na miamba,jumba la sanaa za kisasa,jumba la kumbukumbu ya ubalozi wa Marekani na Jumba la Baiolojia.
Kushoto aliyenyoosha mkono ni Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana akionesha gari (la kijani) la kwanza kutumiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya Taifa,Samson Yohana akionesha moja ya nyumba za kihistoria.

Vijana na watoto wakipiga picha ya pamoja nje ya jumba la makumbusho lililojengwa mwaka 1940 na Waingereza. 
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Samson Yohana simba aliyekaushwa. 
Vijana na watoto wakiwa katika jumba la makumbusho ya kihistoria. 
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha michoro iliyochorwa mapangoni. 
Vijana na watoto wakifurahia kinyago cha mwanamke anayetwanga vitu huku kabeba mtoto na kashikilia mtoto. 
Mwongoza watalii katika Makumbusho ya taifa,Robert Yami akionesha picha ya binadamu aliyejitambua. 
Watoto wakisoma vitabu na kuangalia katuni kwenye vifaa vya kisasa katika Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa. 
Watoto wakisoma vitabu kwenye Maktaba ya watoto katika makumbusho ya taifa. 
Vijana wakisaga unga wa ulezi kwa kutumia mawe katika makumbusho ya taifa. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images