Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Tanzania yawa mwenyeji wa Kongamano la Kikristo Afrika Mashariki

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Ubalozi wa Kimataifa wa Kikristo- Jerusalem (ICEJ) tawi la Tanzania, Stanton Newton Kanyiki akizungumza kwenye kongamano la Kikristo Afrika Mashariki lililofanyika jijini Mwanza kuanzia Juni 18-23, 2019 katika Kanisa la KKT Usharika wa Imani.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa shirika la ICEJ Tanzania, Stanton Newton Kanyiki (kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusiana na Kongamano la Kikristo Afruka Mashariki. Kulia ni mkarimani kwenye kongamano hilo.
Washiriki kutoka nchi mbalimbali Afrika Mashariki zikiongozwa na mwenyeji Tanzania, wakifuatilia kongamano hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa jijini Mwanza, Askofu Amos Hulilo (kulia) akizungumza kwenye kongamano hilo kwa niaba ya Mwenyekiti.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akizungumza kwenye ufunguzi rasmi wa kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
Viongozi wa dini kutoka mataifa mbalimbali Afrika Mashariki na Israel wakifuatilia kongamano hilo.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt.Philis Nyingi aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwasili katika viunga vya Kanisa la KKT Usharika wa Imani kufungua rasmi kongamano hilo.
Mgeni rasmi akilakiwa kwenye viunga vya Kanisa la KKT Usharika wa Imani jijini Mwanza kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa kongamano hilo.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyingi (wa pili kulia)akisalimiana na Mkurugenzi wa ICEJ Tanzania, Stanton Newton Kanyiki (wa tatu kushoto)
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyingi (wa pili kulia)akisalimiana na Makamu wa Rais wa ICEJ Israel, Dkt. Mojmir Kallus (wa tatu kushoto).
Viongozi wa ICEJ Tanzania na Israel wakiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari jijini Mwanza.
Tazama Video hapa chini

APL YA KIGOMBE MABINGWA WA LIGI YA AWESO CUP PANGANI

$
0
0
 KAIMU Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe kushoto akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya APL ya Kigombe ambao ni Mabingwa wa Ligi ya wilaya ya Pangani Maarufu kama Aweso Cup kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso (CCM) Ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
 NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa ameshika kitita cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wa mashindano hayo kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Handeni
  NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza kwenye fainali ya Ligi ya Aweso Cup
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif akizungumza wakati wa fainali hizo.
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akiwa amebebwa na baadhi ya wapenzi na mashabiki wa soka wilayani Pangani mara baada ya kumalizika Ligi ya Aweso Cup
Katibu wa Kamati ya Mipango na fedha wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri kushoto akizungumza wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso
   NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) wa pili kutoka kushoto  akiwa kwenye jukwaa kuu na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Pangani Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni kulia ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gipson George wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Ligi hiyo

 Kikosi cha timu ya Wa2020 wakiwa kwenye Picha ya Pamoja
 Kikosi cha timu ya APL ya Kigombe
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria fainali hiyo
 Sehemu ya mashabiki wa soka wilayani Pangani wakifuatilia mashindano hayo
 Wapenzi na mashabiki wa timu ya APL ya Kigombe wakishangia ushindi huo
 Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Ligi hiyo




NA MWANDISHI WETU, PANGANI.

TIMU ya APL FC ya Kigombe wilayani Muheza mkoani Tanga imetawazwa mabingwa wapya wa Ligi ya wilaya ya Pangani maarufu kama Aweso Cup baada ya kuifunga Wa 2020 FC mabao 2-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa soka Kumba.

Kutokana na Ubingwa huo APL Kigombe walifanikiwa kukabidhiwa Kombe la Mashindano hayo, Kitita cha Sh.Milioni moja na Ngom’be huku mshindi wa pili wa 2020 FC akipata kitita cha sh.laki sita na elfu sabini ya mbuzi na medali za dhahabu.

Mshindi wa pili kwenye Mashindano hayo timu ya Wa 2020 FC walikabidhiwa medali, kitita cha laki sita, mbuzi na medali ya dhahabu kwa wachezaji wake huku mshindi wa tatu naye akipata kitita cha sh.laki nne na mbuzi.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji huchezwa kila mwaka yakiwa na lengo la kuibua na kukuza viwango vya soka mkoani humo ambayo yalishirikisha timu 16.

Mchezo huo wa fainali ya Ligi hiyo ulichezwa kwenye viwanja vya Kumba mjini Pangani uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wasanii wa bongo movie.

Katika mchezo huo mabao ya APL ya Kigombe ambao ndio mabingwa wapya yalifungwa na Malimo Magembe kwenye dakika ya 35 baada ya kutumia uzembe wa mabeki wa timu pinzani kupachika wavuni bao hilo.

Baada ya kuingia bao hiloWa 2020 FC waliweza kurudi kujipan ga na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa APL ya Kigombe bila mafanikio kutokana na mashuti waliokuwa wakijipa wachezaji wao kugonga mwamba na kutoka nje.

Shambulio hilo liliweza kuwaamsha APL Kigombe ambao baada waliweza kurudi kujipanga na kupelekea mashambulizi langoni

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi Naibu Waziri Aweso alisema kwamba Ligi hiyo imekuwa na mafanikio makubwa kwani imewezesha kupandisha timu nne kwenye Ligi ya mkoa na baadae anaamini zitafika Ligi Daraja la kwanza na hatimaye Ligi kuu

Alisema kupitia michezo wilaya ya Pangani inaweza kutoa wachezaji nguli kwenye soko kama vile Mbwana Samata na Thomas Ulimwengi ambao wanaweza kuitangaza nchi kupitia soka

Aidha aliwataka kuendelea kushikamana na kupendana huku akikitaka Chama cha mpira wilayani Pangani kianzishe mashindanbo kwa upande wa wanawake ikiwemo rede na mpira wa miguu atadhamini.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Mipango na fedha wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawaziri alisema kwamba kupitia mashindano ya Aweso Cup wameona vipaji vya wachezaji huku akieleza watachukua wachezaji 10 ambao watawatumia kwenye Ligi kuu.

Mwisho.

WATUMISHI WANAOTARAJIA KUSTAAFU OFISI YA WAZIRI MKUU WAASWA KUENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WELEDI

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akimkabidhi cheti cha mafunzo ya maandalizi ya kustaafu Mtunza Kumbukumbu Mkuu wa ofisi hiyo Bi. Amina Simbaulanga ambaye anatarajia kustaafu mwezi mwishoni mwa mwaka huu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akizungumza na watumishi wa ofisi yake wanaotarajia kustaafu hivi karibuni wakati wa mafunzo ya maandalizi ya kustaafu yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma.Mafunzo hayo yalifanyika Juni 21, 2019 Jijini Dodoma.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Bi. Ziada Sadick akizungumza jambo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni wakati wa mafunzo ya ya maandalizi ya kustaafu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bi.Maimuna Tarishi amewaasa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajia kustaafu hivi karibuni kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi hadi siku zao za kuhitimisha utumishi wao katika Ofisi hiyo zitakapofika.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kujiandaa kustaafu yaliyoandaliwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea aliwaeleza umuhimu wa kuendelea kuwajibika kulingana na taratibu na kanuni zinazoongoza utendaji kazi wa kika siku.

“ Hatutarajii kuona kati yenu hata mmoja wenu akianza kuchelewa kazini au kuanza kuzembea katika kutekeleza majukumu yake kwa kuwa anatarajia kustaafu mwaka huu, tunatarajia kuwa sasa mtaendelea kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuwarithisha utamaduni wa kupenda kufanya kazi kwa bidii wale wanaobaki” Alisisitiza Bi Maimuna
Akifafanua amesema kila mtumishi wa umma anayetarajia kustaafu anapaswa kuhakikisha kuwa anaendelea kuonesha mfano bora katika sehemu yake ya kazi kwa kutekeleza yale anayotakiwa kwa weledi na kwa wakati akizingatia maslahi ya nchi.

Aliwaasa watumishi hao kutumia vizuri elimu waliyopatiwa kupitia mafunzo yakuwaandaa kustaafu yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili hatimaye wanapostaafu waweze kuanzisha na kuendeleza shughuli za uzalishaji katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkufunzi kutoka chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Bi. Ziada Sadick amesema kuwa Chuo hicho kinaipongeza Ofisi yan Waziri mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa watumishi wake wanaotarajia kustaafu hivi karibuni.Aliongeza kuwa mafunzo haya yanawapa uwezo watumishi hao katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza zikawakabili baada ya kustaafu.

Katika mafunzo hayo watumishi wanaotarajia kustaafu waliweza kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuanzisha miradi ya uzalishaji, mbinu za kukabilina na msongo wa mawazo na mada nyingine mbalimbali.Mafunzo hayo yalishirikisha watumishi takribani ishirini wa kada mbalimbali.

VIJANA HALMASHAURI WILAYA YA SIMANJIRO WASHAURIWA KUTUMIA VYEMA FEDHA ZA MIKOPO

$
0
0
Afisa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Bi. Amina Sanga (Mbele Kulia) akizungumza na wanachama wa Kikundi cha MVG kinachojishughulisha na Mradi wa ufugaji samaki katika bwawa walilochimba wenyewe ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro. Kwa Mbele Katikati ni Afisa Maendeleo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya Hai, Bi. Chima na nyuma yake ni Afisa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Godfrey Chacha.
Mfanyakazi wa Kikundi cha Vijana cha AGROP, Bi. Clara Traiphon akielezea namna ya kuweka ‘lebal’ kwenye chupa ya mvinyo (Wine) inayotetengezwa kwa matunda ya Rosella. Kikundi hiki kipo katika Halmashauri ya Wilaya Hai Mkoani Kilimanjaro kinajishughulisha na kiwanda cha kusindika mbogamboga na matunda pamoja na kutengeneza Chill source na Vinegar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Simanjiro, Bw. Yefred Mnyenzi (katikati) akiwa Ofisini kwake pamoja na Maafisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Bw. Godfrey N. Chacha (kushoto) na Bi. Amina Sanga walipofanya ziara wilayani humo ili kukagua shughuli mbalimbali za uwezeshaji Vijana Kiuchumi.
Afisa Maendeleo ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Godfrey Chacha (mwenye tisheti ya njano) akiongea na baadhi ya vijana wa kikundi cha KIWAMA wakati wa ziara yao ya kukagua maendeleo ya vikundi vilivyowezeshwa kupitia Mkopo wa Vijana. Kikundi hicho kinaendesha kiwanda kidogo cha kutengeneza samani pamoja na ushonaji “cover sit” za viti vya magari na pikipiki.

SIKU YA WAJANE DUNIANI 2019

Mkapa akumbuka alikosoma

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Umoja wa Wahitimu wa Shule ya Sekondari Ndanda (UWAHISSENDA) ya Masasi, Mtwara waliokwenda kujitambulisha ofisini kwake Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Eric Mkuti, Yohana Kasawala (Mwenyekiti), Dk Jeniffer Sesabo na Domician Mmassy. Mzee Mkapa ambaye pia amesoma Ndanda, ameridhia kuwa mwanachama mpya wa umoja huo na pia kuahidi kushiriki katika Siku ya Wahitimu wa shule hiyo itakayofanyika shuleni Ndanda Septemba 27, Mwaka huu.
Na Mwandishi Wetu
KATIKA kuonesha anathamini alikotoka kielimu, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa anatarajiwa kuungana na wahitimu wengine wa shule kongwe ya Sekondari Ndanda ya Masasi, Mtwara kuitembelea shule yao Septemba 27, mwaka huu kwa ajili ya Siku ya Wahitimu wa shule hiyo iliyoanzishwa miaka 91 iliyopita.
Mkapa aliyesoma Ndanda katika miaka ya 1950, alithibitisha kuungana na wahitimu wengine wa shule hiyo alipokutana na kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Wahitimu wa Shule ya Sekondari Ndanda (UWAHISSENDA) waliokwenda kuutambulisha umoja wao ofisini  kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Alisema, kama mmoja wa waliobahatika kusoma Ndanda, anajiona ana wajibu wa kuungana na wana umoja wengine walioanzisha wazo la kuitembelea shule yao ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa shule katika maisha yao.
“Hili ni wazo la kupongezwa sana. Hongereni kwa ubunifu na uthubutu wa kutambua umuhimu wa kule mlikopata elimu. Ni wachache sana wanaokumbuka mambo kama haya,” alisema Mkapa huku akiahidi mwaka huu ataungana nao.
Kwa wahitimu hao, hii Hii itakuwa mara ya pili kurejea Ndanda, kwani mwaka jana walikwenda kwa mara ya kwanza na kuzindua umoja wao wakiwa shuleni hapo na kukabidhi vitabu vyenye thamani ya takribani Sh milioni 5, kupanda miti, kuzungumza na wanafunzi wa sasa na pia kushiriki katika shughuli mbalimbali shuleni hapo, ikiwa ni pamoja na kufyatua matofali.
Mwenyekiti wa umoja huo, Yohana Kasawala alimshukuru Rais Mstaafu kwa kuridhia kuwa mwanachama mpya, lakini kipekee kwa kukubali kuungana na wanafunzi wengine wa zamani kwa safari ya shuleni Ndanda. Aliwataka wahitimu wengine kuona fahari ya kusoma Ndanda na hivyo wajitokeze kufanikisha Siku ya Wahitimu Ndanda.
Umoja huo uliasisiwa mwaka 2015 kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp na tayari una wanachama hao zaidi ya 150, wakiwa na malengo ya kutanua wigo wa ukaribu hata baada ya kuhitimu masomo yao, kuinuana kiuchumi na pia kushiriki katika kuijengea uwezo shule yao.
 “Daima umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu, nasi tumeona ni vyema tukatumia mshikamano huu kama fursa ya kujiimarisha kiuchumi. Tuna ndoto nyingi…ni suala la muda tu, lakini mwelekeo wetu ni mzuri na kwa sasa tunafikiria kuanzisha kampuni ya mikopo midogomidogo yaani Microfince company. Siku za usoni tunaweza kufikiria hata kuanzisha benki…,” alisema Kasawala.
Ndanda, shule yenye historia ndefu kielimu, iliaoanzishwa mwaka 1928 na imeshatoa wahitimu zaidi ya 15,000 waliobahatika kushika nyadhifa mbalimbali katika nchi, akiwemo Mzee Mkapa. Hawa Ghasia, mmoja wa mawaziri waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Utawala wa Rais Jakaya Kikwete pia ni matunda ya Ndanda kama ilivyo kwa Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Nishati katika Serikali ya Rais, Dk John Magufuli na wengine wengi.

TIMU YA WATAALAM TOKA SERIKALI YA CHINA WATUA NCHINI KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA CHUO CHA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL

$
0
0
Juni 21/2019 timu ya wataalam Saba toka Wizara ya Uchumi na Fedha ya Serikali ya China ilitembelea eneo la ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Leadership School, kilichopo Kibaha kwa Mfipa kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Mratibu wa ujenzi huo Bi. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda alieleza kuwa, ukaguzi huo unaotarajia kuchukua siku kumi unafanyika kwa mara ya kwanza ikiwa shughuli zote za ujenzi wa msingi, nguzo na kuta za majengo yote umekamilika. 

Pamoja na mambo mengine wakaguzi hao wanaangalia uimara na ubora wa majengo, kabla ya kutoa kibali kwa mkandarasi kampuni ya CRJE kuendelea na ujenzi. 

Aidha Bi. Kaganda alieleza kuwa ukaguzi wa pili utafanyika katika hatua za mwisho za ujenzi miezi michache ijayo huku wa mwisho ukitarajiwa kufanyika baada ya ujenzi kukamilika na kabla ya mradi kukabidhiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mradi wa ujenzi wa chuo hicho cha mafunzo ya itikadi na uongozi chenye uwezo wa kufundisha viongozi 200 kwa wakati mmoja, kinachomilikiwa na CCM kwa kushirikiana na vyama vya ANC, Afrika Kusini; ZANU PF, Zimbabwe; FRELIMO , Msumbiji na SWAPO, Namibia, ulizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mwezi Julai 2018 na kinatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2020.

CLARIFICATIONS ON THE DEBATE BY THE EAST AFRICAN LEGISLATIVE ASSEMBLY ON THE AUDITED FINANCIAL STATEMENTS OF THE COMMUNITY FOR THE FINANCIAL YEAR ENDED 30/6/2017

$
0
0


EAC SECRETARIAT
 OFFICE OF THE SECRETARY-GENERAL
  23RD JUNE, 2019

During its ongoing session of June 2019, the East African Legislative Assembly (EALA) has debated on the report from its Committee on Accounts, arising from the report of the EAC Audit Commission on the Audited Financial Statements for the financial year ended 30th June 2017. After the report was adopted by the Assembly, a section of the media has engaged in partial reporting of some issues in a manner that does not reflect the conclusions made by the EAC Audit Commission, hence negatively impacting on the reputation of the EAC Secretariat, as well as its current and former officials named in the EALA report unlawfully. A wrong impression was created that money was lost, and funds mismanaged.

A section of the media in the region erroneously reported that more than 1,000 assets worth US$1.88 million belonging to the Community cannot be traced and that more than US$1 million in cash cannot be accounted for.

The EAC Secretariat wishes to clarify that the issues highlighted two years ago for the year ended 30th June 2017 as reported by the Audit Commission were of a procedural nature rather than financial, and have since then been fully acted upon. Indeed, the same Audit Commission verified the available evidence provided during the audit for the year ended 30th June 2018 (yet to be debated by EALA) and confirmed the successful implementation of its recommendation and issued a clean audit report signed on 12th December 2018. There was no money reported as stolen or mismanaged as reported by some media houses.

The purpose of this Press Statement is to provide clarifications on the issues raised in the previous audit report for the year ended 30th June 2017 that EALA members debated and media reported on, so that EAC Citizens and other stakeholders are properly informed.

The clarifications are summarized as follows:

1.The alleged loss of funds on fixed assets valued at US$829,058 was rather reported by the Audit Commission as “Assets captured in various assets classes in block figures which were not individually identified” in November 2017.  The Secretariat thereafter engaged a professional valuer to break down the figures which later on were restated in the financial statements for the year ended 30thJune, 2018, and the Audit Commission verified and cleared the matter.
2. The matter of assets amounting US$64,816 reported as work in progress as at 30th June, 2017: the assets were later on delivered and put into use, verified by the EAC audit Commission. This matter was as well cleared in the audit report signed on 12th December, 2018.
3. The matter of six vehicles valued at US$236,808 distributed to the Partner States that could not be verified in November 2017: the vehicles were purchased under the framework of implementation of Avian Influenza Project, with the support from the European Union and transferred, in 2011, to the Ministries responsible for Livestock in the Partner States. In November 2017, the Audit Commission did not manage to go and verify the existence of the vehicles in the Partner States. The Secretariat has since then received letters from Partner States indicating the state of the vehicles which have subsequently been removed from our books as ownership was transferred to the Partner States. The matter was also cleared by the same Audit Commission in its report signed on 12th December, 2018.The matter of alleged unsupported expenditure and transfer of funds.
4. The EAC Secretariat also received a grant disbursement of US$356,000 in March 2016 for the implementation of Action for Reinforcing Veterinary Governance in Africa from the African Union Commission – Inter-African Bureau for Animal Resources (AU-IBAR). In November 2017, the Audit Commission could not confirm the propriety and validity of the reported expenditure and transfer of US$178,761 and US$117,000 respectively as at 30 June, 2017 since the original supporting documents were not provided for audit review. The grant agreement clearly stated that original copies are a property of AU-IBAR which has its offices in Nairobi. AU-IBAR made copies of the original documents and certified them and availed the certified copies for the expenditure of US$178,761 and a receipt acknowledging receipt of US$116,949 from the project Headquarters. After a physical visit to the AU-IBAR offices, the matter was also cleared by the same Audit Commission in the audit for the year ended June 2018.
5. Payroll variances noted between the interface file and the general ledger for Secretariat: during the period under review, the short term (temporary) staff were paid using an Excel template and reflected in the accounting software (Sun systems). Further, annual allowances such as Education and Spouse Allowances which are paid only once per year were not paid through the monthly payroll. The Audit Commission did not report this as a loss of money, but a recommendation to capture all staff, permanent and temporary, in the personnel management software. This has since been implemented and confirmed by the EAC Audit Commission.
6. Reallocation of funds within the Staff Emoluments Budget of the EAC Secretariat: The 35th meeting of the Council of Ministers directed the EAC Secretariat to reallocate funds within its current budget to cater for the recruitment exercise (EAC/CM 35/Directive 62). This approval of reallocating the US$1,342,550 constitutes a one off waiver from application of said provision on restriction by the Financial Rules and Regulations.
7. Kitchen equipment worth US$212,987 procured and delivered to the EAC Secretariat in 2014: The Audit Commission performed a physical verification of the assets of the community and saw kitchen equipment delivered and valued at US$212,987. At the time of audit in October 2017, these equipment had not been put to use, due to the fact that, through the procurement process, EAC had not been able to find a provider of catering services to run the kitchen and restaurant. The current status is that during a recent procurement process, EAC Management had managed to procure a service provider to operate the cafeteria and in so doing utilize the kitchen equipment. The service provider has been provided a Letter of Award and a contract is being drafted by the Office of Counsel to the Community, the EAC’s chief legal adviser, for the selected service provider. With this, the EAC management will ensure full utilization of the kitchen equipment.
8. In 2012, a contract was entered into between EAC and M/s. Avtech Systems Ltd for a sum of US$582,485.93 for the supply, delivery and installation of security equipment. As provided for in the agreement, 50% of the payment be made on the signing of the contract and supplier providing a valid Bank Guarantee, and 30% paid based on proof of shipment and/or delivery/installation of equipment. Due to deficiencies in the equipment, to date the Secretariat has not paid 20% of the contract, i.e. US$116,497.18.  As of May, 2019, the matter is under Arbitration (Arbitration No. 1 of 2018) at the East African Court of Justice.
9. Alleged shrinking support from Development Partners: Two years ago, the Audit Commission Report described a slight decrease in direct funding from Development Partners to the EAC Organs and Institutions. The EAC Management would like to clarify that the mode of support provided to Secretariats of Regional Economic Communities (RECs) to coordinate regional projects is changing towards Development Partners’ preference for Indirect Funding to Partner States Institutions implementing the projects.  That notwithstanding, the EAC Secretariat registered an increase of 15% in Direct Funding from its Development Partners during the financial year 2017/2018. Records on funds mobilized by the Secretariat (US$298,584,305 from USAID, African Development Bank, the World Bank, the Swedish International Development Agency, etc., plus Euro 131,686,466 from the European Union, KfW, etc.) and transferred by Development Partners to implementers in the Partner States (indirect funding) reflect a significant increase in Donors support.
We wish to assure East Africans that, contrary to what has been reported in a section of the media, the Secretariat has and will always endeavor to uphold the integrity and prudent management of all funds and resources at its disposal.

We applaud the work being done by the East African Legislative Assembly in its legislative, representative and oversight functions as enshrined in the Treaty. We further appreciate efforts by the media in the region to sensitize EAC Citizens on the integration process and appeal to them to report on matters handled by the EAC Audit Commission with accuracy, fairness, and objectivity.  

Kipeperushi Cha Viambato Vya Passport Mpya ya Tanzania

WAZIRI KABUDI ZIARANI NCHINI CHINA,AELEZEA MIRADI ITAKAYOJADILIWA BAINA YA TANZANIA NA CHINA

Vodacom watunukiwa tuzo ya NEEC

$
0
0


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Kassim Majaliwa (Kulia) akimpongeza na kumkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Rosalynn Mworia (kushoto) kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kuinua wananchi kiuchumi wakati wa semina ya uwezeshaji wananchi kiuchumi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosalynn Mworia akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya kiuchumi katika semina ya uwezeshaji wananchi kiuchumi iliyofanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Dkt Mwakyembe Afungua UMITASHUMATA na kuagiza Halmashauri Zipeleke Walimu Malya

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe akisalimiana na Waamuzi wa mchezo wa mpira wa miguu kati ya Mtwara na Lindi ambapo matokeo yanaonyesha kuwa Lindi imeifunga Mtwara kwa magoli 2-0. 
Misukosuko kwenye lango la Lindi, kufuatia mashambuzi makali yaliolekezwa langoni mwaka na washambuliaji kutoka timu ya mkoa wa Mtwara. 
…………………….. 

Na Mathew Kwembe, Mtwara 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo Sanaa na Michezo, Mh. Harrison George Mwakyembe ameitaka halmashauri za wilaya nchini kupeleka walimu wa michezo kwenye chuo cha michezo cha Malya kilichopo Mwanza ili kuboresha weledi wa walimu hao katika michezo nchini. 

Mhe.Dkt Mwakyembe ameyasema hayo jana wakati akifungua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara. 

Amesema kila akitembelea chuo cha Malya, hukuta walimu wengi wanaosoma pale hujilipia wenyewe badala ya kulipiwa na serikali jambo alilosema kuwa siyo sawa kwani walimu wanaosoma Malya siyo kwa faida yao pekee bali ni kwa ajili ya maendeleo ya michezo ya halmashauri wanakotoka. 

Hivyo Mhe Mwakyembe amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanatenga fedha kwa ajili ya kusomesha walimu wake wanaotaka kujiendeleza katika chuo cha maendeleo ya michezo Malya kwa ajili ya kuboresha weledi wao katika fani ya michezo. 

“Nitakapotembelea tena chuo cha Malya nikikuta wapo walimu ambao wanajilipia wenyewe kwa fedha zao nitahakikisha kuwa halmashauri wanakotoka walimu hao tunazitangaza ili nao wapate aibu,” amesema. 
Dkt Mwakyembe amesema kuwa halmashauri zinatenga fedha kwa ajili ya shughuli nyinginezo mfano fedha za chai lakini zinaona ugumu kutenga fedha kwa ajili ya kupeleka walimu Malya kusomea fani ya michezo. 

Akizungumzia kuhusu ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Mhe. Mwakyembe ameelezea furaha yake kuona kuwa katika mashindano ya mwaka huu kuona vipengele vya burudani ya ngoma vitashindanishwa na kuongeza kuwa fani hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa kwani katika bajeti ya mwaka huu sanaa na burudani vimechangia kwa asilimia kubwa pato la taifa. 

Aidha Mhe. Mwakyembe ameagiza kuwa kila kila shule iliyosajiliwa nchini kuanzia ile ya chekechea ihakikishe kuwa inazingatia kuimbwa kwa wimbo wa taifa kila siku asubuhi. 

Akizungumzia kuhusu mashindano ya UMITASHUMTA Dkt Mwakyembe amesema kuwa mashindano hayo ni muhimu sana katika kuibua vipaji vya wanafunzi ambao siku za usoni watakuja kuliletea heshima taifa letu. 
Ameongeza kuwa ni muhimu kwa vipaji hivyo kuviibua, na kuvilea ili vije kuleta matunda yanayokusudiwa kwa taifa letu. 

Amesema kuwa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ni muhimu sana kwa ukuaji wa sekta ya michezo katika taifa huku akitolea mfano jinsi vijana walioibuliwa na kuandaliwa vyema baada ya michezo ya UMISSETA iliyofanyika Mwanza walivyoweza kuliletea heshima kubwa taifa letui katika mchezo wa riadha baada ya kuibuka na medali 13 na hivyo kushika nafasi ya kwanza miongoni mwa nchi 11 zilizoshiriki mashindano ya ukanda wa tano wa mchezo wa riadha duniani. 

Aidha Dkt Mwakyembe ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kuanzisha shule maalum ya michezo ambayo itakuwa shule ya kwanza ya umma itakayokuwa na jukumu la kuendeleza michezo na elimu nchini. 
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu bwana Jumanne Sagini amesema kuwa mkoa wa Simiyu uliamua kuja na wazo la kuanzisha shule ya michezo kwa lengo la kulea vipaji vya michezo shuleni. 

Amesema kuwa shule hiyo inatarajiwa kuanza mwaka ujao wa masomo ambapo wataanza kwa kuchukua watoto 120 katika mwaka wa kwanza na baada ya hapo watakuwa wakichukua wanafunzi 80 kila mwaka. 

“Shule hii zamani ilikuwa ni ya kutwa tumeigeuza kuwa ya bweni na inaitwa shule ya sekondari Simiyu, na tunatarajia kuwa na jumla ya wanafunzi 320 ambapo vijana watakaokuwa wakifaulu mitihani yao ya darasa la saba na wenhye vipaji vya michezo wataletwa moja kwa moja katika shule hii,” amesema. 

Naye Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Benjamin Oganga amesema kuwa Mashindano ya Michezo ya UMITASHUMTA Taifa kwa mwaka 2019 yameshirikisha Mikoa yote 26 ya Tanzania Bara ambapo jumla ya wanafunzi 2600, walimu na viongozi 675 wanashiriki michezo hii. 

“Michezo wanayoshiriki wanafunzi hawa ni mpira wa Miguu, Netiboli, Mpira wa Mikono, Mpira wa Wavu, Riadha Jumuishi na mpira wa goli (kwa wasioona na wenye uoni hafifu)na fani za ndani zitakazohusisha Kwaya na Ngoma,” amesema. 

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara bwana Gelasius Byakanwa amesema kuwa mkoa wake umejiandaa kuwapokea na kuwakarimu watoto na wageni wote waliofika Mtwara huku akiamini kuwa watoto wanahitaji upendo, ukarimu na kuelekezwa. 

Mara baada ya ufunguzi wa mashindano hayo kulichezwa mchezo wa mpira wa miguu baina ya timu ya soka wavulana kutoka mkoa wa Lindi dhidi ya majirani zao timu ya mkoa wa Mtwara ambapo mechi hiyo baada ya dakika 60 kuchezwa timu ya soka kutoka mkoa wa Lindi ilifanikiwa kuinyuka timu ya soka ya mkoa wa Mtwara kwa magoli 2-0. 

Magoli ya washindi yalifungwa na Arid Raamadhani na Omary Mohamed ambaye alifunga goli la pili kwa njia ya penati. Mashindano ya UMITASHUMTA yatafanyika kwa muda wa wiki mbili na yameshirikisha mikoa yote 26 ya Tanzania bara na yanatarajiwa kufungwa tarehe 3 julai, 2019 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara

GGM WAKUSANYA BIL 13 KUPITIA KILI CHALLENGE

$
0
0
Washiriki wa Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kwa jina la Kili Challenge 2019 wakishuka wakiwa na Bendera ya Taifa huku wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa mara baada ya kuhitimisha safari ya siku saba ya kupanda mlima huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Anna Mghwira pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita ,Robert Gabriel wakiwa wamepokea Bendera ya Taifa kutoka kwa washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Milima Kilimanjaro ambapowashiriki hao waliipandisha bendera hiyo kileleni.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya mapokezi ya washiriki 64 wa tukio la Kili Challenge 2019 akizungumza mara baada ya kuwapokea.
Mkuu wa Mkoa wa Geita ulipo Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Robert Gabriel akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.
Baadhi ya Washiriki.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti wamiliki wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Simon Shayo akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Baaadhi ya Washiriki wa Changamoto ya Kili Challenge 2019.
Kaimu mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini,(TACAIDS),Jumanne Isango akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akitoa burudani kwa kuimba nyimbo wakati wa mapokezi ya Washiriki 64 wa Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kii Challenge 2019 .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghira akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Robert Gabriel ,Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Mhandisi Aisha Amour pamoja na Makamu w Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti,Simon Shayo wakielekea kutembelea mabanda ya maonesho yaliyokuwepo katika lango la mlima Kilimanjaro la Mweka .
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjao ,Dkt Anna Mghwira akimkabidhi Mkuu wa mko wa Geita ,Robert Gabriel kumbukumbu ya kishika Funguo ( Key Holder) wakati akitembelea moja ya mabanda ya maonesho yaliyokuwa katika lango la Mweka wakati washiriki wa Changamoto ya Kupanda Mlima Kilimanjaro (Kili Challenge 2019 ) wakishuka kutoka kilele cha Uhuru.Nyuma ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ni Makamu wa Raisi wa Kampuni ya AngloGold Ashanti wamilki wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita.Simon Shayo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro pamoja na kuuzunguka kwa Baiskeli kwa lengo la kuchangisha fedha za Mapambano dhidi ya Ukimwi mara bada ya kuwasili katika lango la Mweka .
Mgeni rasmi katika hafla ya kuwapokea Washiriki 64 wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa Baiskeli kwa lengo la kuchangisha fedha za Mapambano dhidi ya Ukimwi ,Mkuu wa Mkoawa Kilimanjaro akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wenzake na wadau .


Na Dixon Busagaga.

.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira,amewataka wageni kutoka Nje ya nchi, kwa ajili ya shughuli za kijamii, Katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, kuepuka kuingilia shughuli za mlima huo.

Mbali na hilo, Mkuu huyo pia aliutaka Uongozi wa Wilaya zinazozunguka Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA, kumaliza migogoro inayohusu eneo la hifadhi hiyo,ikiwemo ya Nusu Mail,ambayo imekuwa ikihusisha wananchi wanaozunguka eneo hilo.

Mghwira ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye hafla ya kuwapokea wanaharakati 64,waliopanda Mlima kilimanjaro,kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi,Kampeni ambayo imeandaliwa na Mgodi wa madini ya Dhahabu Geita (GGM).

"Ipo migogoro ya Nusu maili,ambayo imekuwa ikizungumzwa kila wakati lakini haiishi,niombe viongozi wa Wilaya na Tanapa,waimalize.Niombe pia wageni kutoka nje ya nchi,ambao wanakuja kwetu,kwa shughuli hasa za kijamii,kujifunza kutoka kwetu,na wasituingilie sana kwenye eneo hili"amesema Mghwira

Aliongeza kuwa"Kila wakati tumekutana na mazingira ya wageni kujiingiza kwenye masuala ya mlima na shughuli zinazofanyika hapa na kutuletea utata mgumu,sababu tunaposhughulika na Wageni kutoka nje ya nchi,mahusiano yake yanakuwa tofauti kidogo na namna ya kufanya maamuzi"

Mkuu huyo alitumia pia nafasi hiyo, kueleza kuwa,Ukimwi bado ni Tishio mtambuka na umegusa na kuathiri kila nyanja ya maendeleo na kuwataka wadau kushirikiana na serikali,kumaluza tatizo hilo.Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel,alisema katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa ukimwi,watoto wa Kike wameonekana kuwa wahanga wakubwa,na kuitaka jamii na wadau,kushiriki kulinda kundi hilo.

Kaimu mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Nchini,(TACAIDS),Jumanne Isango, amesema kunahitajika ubunifu,ili kuongeza hamasa zaidi,katika kuupanda Mlima Kilimanjaro,kwa ajili ya kuchangisha Fedha za Mapambano dhidi ya Ukimwi.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya AngloGold Ashanti kupitia mgodi wa Dhahabu Wa Geita,Simon Shayo alisema zadi ya Bil 13 zimekusanywa katika kampeni hiyo tangu ianze na kuungwa mkono na zaidi ya mashirika yasiyo ya kiserikali 40.

“Tunafurahi kweli na tunashukuru kwa washirika wetu wote na tutaendelea kushirikiana kufanya kila liwezekanalo na kwa ambao pia wangependa kujiunga katika vita hivi hii inamaanisha wakihamsika wapandaji zaidi itasababisha watu binafsi na jamii zaidi kuunga mkono na mpango wa Kili Challenge.”alisema Shayo.

Shayo aliwashukuru wafadhili wa changamoto hiyo na wote walishiriki kupanda na kwamba jitihada walizoonesha ni muhimu katika kuchochea tukio hilo wakiwemo waendesha baiskeli ambao waliamua kuweka roho zao juu ili kuhakikisha Tanzania kupitia Kili Challenge inafikia sifuri 3 mwaka 2030.

Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Rufiji washika kasi/Wadau waunga mkono Juhudi

Watanzania watakiwa kuchangamkia udhamini wa Unesco

$
0
0
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo amewataka Watanzania kuchangamkia ufadhili wa masomo unaotolewa na shirika hilo ili kutanua uwezo wa rasilimali watu katika nyanja mbalimbali.
Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati wa kutangazwa kwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kwa Mtanzania, Doreen Richard Mushi kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship .

Mtanzania huyo kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania atakwenda Japan na Canada kwa miezi minne kufanikisha utafiti wake juu ya menejimenti ya ufahamu wa data katika Tehama unavyoweza kusaidia mfumo wa kujifunza wa wanafunzi.
Doreen ameibuka mshindi kati ya watu 280 walioomba nafasi hiyo.
Profesa Malebo aliwataka watanzania kutumia nafasi mbalimbali zinazotangazwa kushindaniwa na taasisi yake kutafuta masomo na kwamba taasisi hiyo huchagua kwa haki kwa kuzingatia vigezo na ushindani uliopo.

Alisema kwa sasa watu wengi hawajitokezi kuomba nafasi hizo za ufadhili kupitia Unesco, na kuwataka waombe kwa kuwa nafasi hizo huenda yule anayestahili kwenda kutokana na vigezo vilivyopo ambavyo ni vya kishindani.
“Natoa wito kwa watanzania kutumia nafasi tunazopewa na Unesco kwani ni msaada mkubwa katika kuimarisha na kuboresha elimu na kuwezesha watanzania hasa vijana kupata elimu ya kusaidia kusogeza mbele maisha” alisema Profesa Malabo.

Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameishukuru serikali ya Japan kwa kuwezesha Unesco kutoa ufadhili huo muhimu kwa taifa hili.
Akimwakilisha Waziri Ndalichako, Naibu Makamu Mkuu  wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof Cuthbert Kimambo  alisema kwamba serikali ya Tanzania pamoja na kushukuru Japan kwa kumwezesha Mtanzania huyo, pia inaamini wale waliomaliza mafunzo yao watarejea nchini na kuyafanyia kazi yale waliojifunza na kuleta maendeleo.

Alisema pamoja na kuleta ufanisi katika ubadilishanaji wa maarifa kupitia mafunzo hayo ni matarajio ya serikali kwamba wanaopewa mafunzo hayo watahamisha elimu hiyo kwa wenzao na kulisogeza mbele zaidi gurudumu la maendeleo.

Mpango wa masomo wa kutanua uwezo wa utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship ulianzishwa mwaka 2000 na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Koichiro Matsura kwa kutafakari maono ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan wakati huo , Keizo Obuchi ambaye aliamini katika uwezo wa watu katika kuibadili na kuijenga dunia hivyo haja ya kujiongezea maarifa zaidi ili kuwepo na maendeleo.

Lengo la programu hiyo ni kuwezesha kuwa na uhakika katika utunzaji wa mazingira, kuleta mazungumzo ya kimataifa na kuendeleza suala la mawasiliano na teknolojia. Programu hii ni matokeo ya ushirikiano kati ya serikali ya Japan na UNESCO katika kuendeleza rasilimali watu kwa nchi zinazoendelea.
Programu hii ambayo ilianzishwa mwaka 2001, imeshawezesha watu 290 hasa vijana watafiti, ambapo 82 wametoka Afrika, kutanua uwezo wao katika nyanja wanazozifanyiakazi.

Miongoni mwa nchi ambazo zimeshanufaika ni Tanzania ambapo katika programu ya mwaka 2014 na 2015, Fatuma Ubwa na Juliana Samuel Kamaghe, walipata nafasi ya kujiimarisha katika sekta ya habari na teknolojia ya mawasiliano.
Doreen Richard Mushi ambaye amekuwa mshindi wa UNESCO/Keizo Obuchi Research Fellowships ya mwaka 2018 alikuwa anashindana na watu wengine 280 na ameshinda katika nyanya ya habari na tekniolojia ya mawasiliano (Tehama).

Tuzo hiyo itamwezesha Doreen Mushi kufanyakazi kwa miezi miwili na watafiti wa taasisi ya Learning Analytics Centre ya Chuo Kikuu cha Kyushu nchini Japan, na miezi mingine miwili na watafiti wa kitivo cha elimu, Chuo Kikuu cha British Columbia mjini Vancouver, Canada.
Katika vyuo vyote viwili  Doreen Richard Mushi, aliyezaliwa Agosti 27, 1983 atafanya utafiti kuhusu takwimu na uchambuzi utakaosaidia mifumo ya kusoma kwa wanafunzi.
 Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Shinichi Goto akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangazwa kwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti Bi.Doreen Richard Mushi kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. 
 Bi. Doreen Richard Mushi kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT) mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship  akisalimia wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Shinichi Goto, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Utafiti (UDSM), Prof Cuthbert Kimambo pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Utafiti (UDSM), Prof Cuthbert Kimambo akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa hafla ya kutangazwa kwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti Bi. Doreen Richard Mushi kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akitoa salamu za Unesco wakati wa hafla ya kutangazwa kwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti Bi. Doreen Richard Mushi kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Bi. Doreen Richard Mushi kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT) akizungumza jambo mara baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria hafla ya kutangazwa kwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti Bi. Doreen Richard Mushi kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Shinichi Goto akimpongeza Bi. Doreen Richard Mushi kutoka Chuo Kikuu Huria (OUT) kwa kushinda tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (katikati) akimpongeza Bi. Doreen Richard Mushi mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Shinichi Goto na kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Utafiti (UDSM), Prof Cuthbert Kimambo aliyemwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
 Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Utafiti (UDSM), Prof Cuthbert Kimambo akimpongeza Bi. Doreen Richard Mushi mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo na kulia ni Naibu Katibu Mtendaji – Utawala na Fedha wa Tume ya Taifa ya UNESCO (NATCOM), Bw. Francis Msungu.
 Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla fupi ya kutangazwa kwa mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti Bi.Doreen Richard Mushi kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos, Bi. Doreen Richard Mushi pamoja na mume wake, Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Shinichi Goto pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Utafiti (UDSM), Prof Cuthbert Kimambo wakiwa katika picha pamoja mara baada ya tuhitimisha hafla ya kumtangaza mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Bi. Doreen Richard Mushi (katikati) mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship akiwa kwenye picha ya pamoja Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (NATCOM-Unesco), Profesa Hamisi Malebo (kushoto), Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Shinichi Goto (wa pili kushoto),Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos (wa pili kulia), pamoja na na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam-Utafiti (UDSM), Prof Cuthbert Kimambo (kulia) katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
 Bi. Doreen Richard Mushi (katikati) mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship akiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu pamoja na sekretarieti iliyoshiriki mchakato huo.
 Bi. Doreen Richard Mushi (katikati) mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa na maafisa wa Ubalozi wa Japan katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan jijini Dar es Salaam.
 Bi. Doreen Richard Mushi (katikati) mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Balozi wa Japan jijini Dar es Salaam.
Bi. Doreen Richard Mushi mshindi wa tuzo ya kwenda kujinoa zaidi katika utafiti kupitia Mpango wa Masomo wa Kutanua Uwezo wa Utafiti kwa udhamini wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) inayojulikana kama The Unesco/Keizo Obuchi Research Fellowship akiwa kwenye picha ya pamoja na Afisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Regina Monyemangene (kushoto).

Wema Sepetu arejeshewa dhamana, Mahakama yamuonya.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

BAADA ya kusota Mahabusu kwa siku saba hatimae leo Juni 24, 2019 Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemrudishia  msanii wa Bongo Movie nchini Wema Isack Sepetu  dhamana na kumuonya kutorudia tena kukiuka masharti ya dhamana ama sivyo mahakama haitasita kumfutia kabisa dhamana hiyo.

Uamuzi huo umesomwa leo Juni 24, 2019 na Hakimu Mkazi Maira Kasonde kufuatia Wema kutokuhudhuria mahakamani hapo Mara mbili bila kuwepo kwa  taarifa yoyote kutoka kwake wala kwa mdhamini wake.

Kufuatia ukiukwaji huo wa msharti, mahakama ilitoa hati ya kumkata Wema ambapo Julai 17 mwaka huu, alijisalimisha mahakamani hapo na Hakimu Kasonde akatoa amri kuwa mshtakiwa aende Mahabusu ambapo amekaa mahabusu katika gereza la Segerea mpaka leo
Akisoma uamuzi huo, amesema Juni 17, mwaka mshtakiwa Wema alifika mahakamani hapo chino ya hati ya kukamatwa  ili kuonyesha kwa nini dhamanana yake isifutwe . msando alifaili mahakamani hapo kiapo kikionyesha sababu za mshtakiwa kutokufika mahakamani Juni 11, mwaka huu ambapo alieleza kuwa mshtakiwa aliugua ghafla akiwa katika viunga vya mahakama na akashindwa kuingia ndani na kuamua kuondoka.
"Baada ya kufikiria kwa makini sababu za mahakama zilizotolewa na mshtakiwa katika hati ya Kiapo mahakama inaona kuwa kweli mshtakiwa alikiuka masharti ya dhamana, lakini kama binadamu hali inaweza kumtokea mtu yeyote lakini kwa nini hakuitaarifu mahakama wakati akiwa katika eneo hili?, amehoji Hakimu Kasonde.
Amesema, pale ambapo mshtakiwa haupo mahakamani unatakiwa kuijulisha mahakama kupitia mdhamini wako na kwa ba siyo kupitia wakili kwani wakili hachukui jukumu la mdhamini na kama mdhamini anashindwa kutoa taarifa mahakamani, inamaana mdhanini hiyo hafai na dhamana ya mshtakiwa inatakiwa kufutwa kabisa.
Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza  video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani ambapo anadaiwa  kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

AFISA TARAFA ITISO AAGIZA KUSOMWA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI KATA ZOTE KABLA YA JULAI 30 MWAKA HUU

$
0
0
KATIKA kushiriki shughuli za kimaendeleo Afisa tarafa wa Itiso ameitisha mkutano wa kimkakati uliolenga kuboresha shughuli za maendeleo katika kata zote za tarafa hiyo.

Akizungumza  katika kikao hicho Afisa tarafa wa Itiso Remidius Emmanuel amesema kuwa kufanyika kikao hicho kilichowakutanisha wataalamu wote kuanzia ngazi ya vijiji kimelenga kutoa mwelekeo mpya wa Tarafa hiyo  na kuwataka viongozi wote kuwa na sauti moja katika safari ya kuelekea Itiso mpya.

Afisa huyo amehimiza suala la uwajibikaji  na mshikamano kwa viongozi wote  kama msingi namba moja wa kuifikia "Itiso Mpya"

"Nafahamu kila mmoja wetu anafurahishwa na kazi kazi kubwa  inayofanywa  Rais wetu  Dkt.John Pombe Joseph Magufuli, lakini naomba niwakumbushe jambo moja, tutahesabika tunamuunga mkono Mhe.Rais sio kwa maneno ya vinywa vyetu tu, bali ni kwa kutimiza wajibu wetu kupitia maeneo yetu,ikiwa tutafanya hivyo hapo tutakuwa tumemuunga mkono Mhe. Rais."  Ameeleza.

Pia amesema kuwa Kilimo na Ufugaji vipewe kipaumbele katika tarafa hiyo.
 "Shughuli kubwa ya uchumi wa tarafa yetu ni kilimo na ufugaji ndio maana nimehitaji uwepo wa Maafisa Ugani na Maafisa mifugo wa tarafa ya Itiso katika kikao hiki, nataka muone dhamira yangu,tunahitaji kubadili uchumi wa tarafa hii kupitia sekta hizo na hii itasaidia kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kuchochea sekta nyingine, tutaelekeza nguvu na mikakati katika eneo hili, na kwa kweli nimedhamiria" ameeleza.

Amesema maendeleo ya Itiso yanategemea Ushirikiano wa pamoja na amewataka viongozi wote kuwa waadilifu, kusimama na kufuatilia miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kuhakikisha viongozi wote wanawafikia wananchi na kutatua migogoro na kero za wananchi pamoja na kuendelea kutekeleza mipango na maelekezo ya Serikali kwa ngazi zote.

Kuhusu kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Afisa tarafa huyo ameeleza kuchukizwa na baadhi ya Serikali za vijiji ambazo zimeendelea kutoitisha mikutano mikuu ya vijiji na  kushindwa kusoma mapato na matumizi kwa visingizio kadhaa na kuagiza ifikapo Julai 30 mwaka huu vijiji vyote viwe vimeitisha mikutano hiyo na kusoma mapato na matumizi  na kuahidi kufuatilia hatua hiyo.

"Nina taarifa baadhi ya vijiji kutoitisha mikutano mikuu ya vijiji na mnakwepa kusoma mapato na matumizi, kila mara mnajizungusha na kusingizia kwamba watu hawaji mikutanoni, jambo hili nitalisimamia" amesisitiza.

Hata hivyo amehimiza viongozi wote kuendelea kutumia elimu, maarifa na uzoefu wao kuleta tija katika maeneo yao na kuwa wabunifu, aidha  amefungua milango ya kupokea ushauri,maoni na mapendekezo ambayo yatalenga kuiletea maendeleo tarafa ya Itiso.

Baadhi ya Viongozi waliopata nafasi ya kutoa maoni yao wamefurahishwa na mipango hiyo huku wakimpongeza kiongozi huyo na kuahidi ushirikiano mkubwa na baadhi yao wakionekana kufurahishwa zaidi na hatua ya  kurejeshwa kwa mashindano ya sanaa za  utamaduni na mpango wa  kuinua vipaji mbalimbali kupitia michezo na burudani Sambamba na utoaji wa Motisha kwa watumishi wote wanaofanya vizuri katika utendaji wao wa kazi na kuweka  utaratibu wa  kuwapa zawadi Wanafunzi wote katika shule za msingi na sekondari wanaofanya vizuri kitaaluma.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Polisi Tarafa ya Itiso Inspekta Misana Makweba pamoja na mambo mengine amewataka viongozi hao kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kueleza  kwamba Ulinzi na Usalama wa Tarafa ya Itiso uko mikononi mwa wana Itiso wenyewe na kuongeza kuwa wapo baadhi ya Viongozi wamekuwa wakishindwa kutoa taarifa za kuwafichua wahalifu  kwa  matukio kadhaa.

 Diwani wa Kata ya Dabalo Elisha  Matewa  amesema  tarafa ya Itiso kupitia kata ya Dabalo ina matukio makubwa ya  kihistoria ambayo yameanza kusahaulika, hivyo mkakati wa kuanzisha utaratibu wa kuhifadhi historia na kumbukumbu za Tarafa ya Itiso ni jambo jema sana na kupongeza sana suala la kutambua na kuenzi utamaduni wetu hatua itakayo anza kurejesha maadili yanayoporomoka kwa kasi.

Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya viongozi wote waliohudhuria  kikao hicho Diwani wa kata ya Haneti Peter Chidawali  amempongeza  Afisa Tarafa huyo kwa kutoa taswira mpya kwa tarafa hiyo  na wao kama Madiwani wanahaidi     ushirikano kwa kiongozi huyo.

Tarafa ya Itiso ni miongoni mwa Tarafa Tano (5) za Wilaya ya Chamwino zinazipatikana katika mkoa wa Dodoma.
 Afisa Tarafa Itiso Bw. Remidius Emmanuel akizungumza na viongozi mbalimbali wa Tarafa hiyo kupitia  kikao maalum kilichohitishwa na kiongozi huy uliolenga kuboresha shughuli za maendeleo katika kata zote za Wilaya ya Chamwino.
 Diwani wa Viti maalum Tarafa ya Itiso  Mhe. Hajira Mdimu akizungumza kupitia kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria kikao hicho

Mkutano ukiendelea

Dkt. Migiro apokea vifaa vya mafunzo ya utabibu vyenye thamani ya Tsh. milioni 130

$
0
0
Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ulipokea kifaa muhimu cha kufundishia madaktari, wauguzi na wataalamu wengine wa sekta ya afya, pamoja na vitabu vya kitabibu kutoka katika Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza wanaofanya kazi katika sekta ya afya (Tanzania United Kingdom Health Diaspora Association - TUHEDA). 

Kifaa hicho ni sanamu ya binadamu ambayo inaendeshwa na programu maalumu za kompyuta zinazowezesha wataalamu mbalimbali wa afya kupata uhalisia wa hali ya magonjwa kama ambavyo wangeupata kutoka kwa mgonjwa aliye hai. 

Sanamu hiyo iliyopewa jina la ‘Msafiri’ na Ubalozi, ina uwezo wa kupumua, kutoa sauti ya mapafu kama mtu mwenye pumu, homa ya mapafu, au mapigo ya moyo yanayoweza kuashiria shinikizo la juu au la chini la damu, sawa na mgonjwa halisi. Upatikanaji wa sanamu hiyo umefanikishwa na mwanachama wa TUHEDA, Dkt. Nasibu Mwande, mtaalamu wa masuala ya ajali na magonjwa ya dharura (Accidents and Emergency), anayefanya kazi ya udaktari hapa Uingereza. 

‘Msafiri’ ana thamani ya pauni za Uingereza zisizopungua 30,000 (sawa na shilingi za Tanzania zipatazo milioni mia moja), ana umbo la kawaida la binadamu na uzito wa kilo 60. Ubalozi umetaarifiwa kuwa sanamu hiyo ni ya kwanza nchini Tanzania katika ufundishaji wa kitabibu. 

Kupatikana kwa ‘Msafiri’ kutasaidia sana kupunguza makosa ya kibinadamu yanayoweza kufanywa na madaktari, wauguzi na wataalamu wengine kwani ‘Msafiri’ anaweza kutumika kutoa mafunzo ya kitabibu kwa mfano halisi wa magonjwa mbalimbali bila ya madhara ambayo yangetokea kama wataalamu wa utabibu wangetegemea kujifunza kupitia mgonjwa aliye hai. 

TUHEDA pia wamekabidhi vitabu muhimu mia tatu vinavyotumika kama rejea kwa madaktari wakati wa kuamua mgonjwa apewe dawa gani, dawa zipi zinaweza kutumika kwa pamoja bila madhara, na zitolewe kwa kiwango gani. Vitabu hivyo vina thamani inayokaribia pauni 9,000 sawa na shilingi za Tanzania zipatazo milioni 30. 

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akisikiliza mkoromo wa kifua cha ‘Msafiri’ kama mgonjwa halisi mwenye maambukizi kwenye mapafu. ‘Msafiri’ na vitabu hivi ni mchango mkubwa katika kazi za kitabibu nchini Tanzania. 
Watanzania waishio Uingereza waliohudhuria mapokezi ya Msafiri na vitabu vya utabibu vilivyokabidhiwa na TUHEDA. 

MGALU-KASI IONGEZWE ILI 2021 VIJIJI VYOTE VIWE VIMEUNGANISHWA UMEME

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, ametoa rai kwa wakandarasi katika wilaya mbalimbali kuongeza kasi ili kuhakikisha wananchi wanapata nishati vijijini ,kama ilivyo maagizo ya Rais Dk.John Magufuli mpaka 2021 vijiji vyote kuunganishiwa umeme .

Aidha ametoa rai kwa wanyakazi wa TANESCO katika Ofisi za Wilaya nchi nzima, hususan kada ya maofisa uhusiano na huduma kwa wateja, kufanya kazi kwa kujituma kwa kutoka maofisini kwenda kutafuta wateja ili kuliongezea shirika mapato.

Alisema hayo wakati akiwasha rasmi umeme kijijini hapo kwenye duka la Abdul Abdulrahman, ikiwa ni ishara ya kukiwashia kijiji kizima.Subira alieleza, mikakati ya serikali kufikisha umeme katika maeneo yote nchini.

Alisema kuwa ,matarajio ni kuvifikishia nishati hiyo vijiji 10,268 nchi nzima ifikapo Juni 2020, vikiwemo vijiji vipya 60 vya Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumzia uwajibikaji kwa wafanyakazi wa TANESCO Subira,alisema hasa kada ya maofisa uhusiano na huduma kwa wateja, ijitume, kuhakikisha wanawafuata wateja mahala waliko kwa ajili ya kuwapelekea taarifa mbalimbali pamoja na kupokea kero zao.

Pia aliuelekeza,uongozi wa shirika hilo,kuhakikisha wanafikisha umeme katika mradi wa maji kijiji cha Njopeka,Mkuranga ili kutatua changamoto hiyo kwa manufaa ya wakazi wake.


Subira alieleza,hilo siyo jambo la wizara ya Maji; ni la wizara ya nishati. 
"Nishati tumepewa dhamana ya kuboresha na kuhakikisha huduma nyingine za kijamii zinatolewa katika viwango vyenye ubora,” alisema naibu waziri huyo.

Taarifa ya TANESCO kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme wilayani humo inaeleza kuwa, mpaka sasa kazi ya kusambaza umeme imekamilika katika vijiji vyote 15 na kwamba kazi inayoendelea hivi sasa ni kuunganisha wateja.

Vijiji hivyo ni Kinyanya, Jaribu Magharibi, Lumionzi, Mjawa, Ngodai, Mangombela, Bungu A na Bungu B. Vingine ni Motomoto, Tomoni, Kingwila, Mtunda, Kinyamale, Mtawanya kwa Mkengelwa, Bungu Mwongozo na Njopeka.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
Wananchi

GGM, TACAIDS wafanikiwa kuanzisha vituo vya kutoa huduma za VVU/Ukimwi

$
0
0
TUME ya Kudhibiti Ukimwi nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) imefanikiwa kuanzisha vituo vinne vya utoaji huduma za Ukimwi na maarifa kwa lengo la kupunguza kasi ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) hasa kwa madreva wa masafa marefu.

Vituo hivyo vimeanzishwa kwa kupitia kampeni ya Kilimanjaro Challenge ambayo imelenga kukusanya fedha za kutunisha mfuko wa Ukimwi (ATF) na kutokomeza VVU na Ukimwi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwapokea watu zaidi ya 80 walioshuka Mlima Kilimanjaro baada ya kupanda kwa muda wa siku saba, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Jumanne Issango alisema kampeni hiyo pia imesaidia baadhi ya vikundi vya akina mama wanaoishi na VVU kupewa mafunzo ya ujasiriamali.

Aidha, alivitaji vituo hivyo vilivyojengwa kwa kupitia kampeni hiyo ya Kilimanjaro Challenge kuwa ni Michungwani Handeni- Tanga, Manyoni Singida, Geita – Geita na Dumila- Kilosa Morogoro ambako ujenzi wake unaendelea.

Alisema vituo hivyo vitasaidia kuongeza kasi ya upimaji, upatikanaji wa matumizi sahihi ya dawa ni muhimu katika kufikia malengo ya kufikia 90 -90-90 ifikapo mwaka 2020.

“Tatizo la UKIMWI kwa Tanzania bado ni kubwa kwani kutokana na takwimu zilizopo zinaonyesha kwa kila mwaka takribanii watu 72,000 hupata maambukizi mapya ya VVU kila mwaka ambapo takriban watu milioni 1.5 wameambukizwa na VVU huku wastani wa hali ya maambukizi ikiwa ni asilimia 4.7 kwa Tanzania bara,” alisema.

Aidha, alisema wakati maambukizo hayo yakipungua kwa ujumla wake kwa watanzania yapo makundi ambayo maambukizi yamekuwa yakiongezeka hususan kwa vijana kati ya miaka 15 hadi 24. 

“Makundi mengine yaliyoko kwenye mazingira hatarishi ni kama vile Wasafirishaji wa masafa marefu, watu wanaotumia dawa za kulevya, wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile, wanawake wanaofanya biashara ya ngono, wafanyakazi kwenye migodi, wavuvi, wafanyakazi kwenye mashamba makubwa.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alisema jukumu lilopo ni kuwepo kwa ushiriki mpana wa wadau katika sekta zote ikiwemo sekta binafsi ndiyo maana serikali ikaanzisha Mfuko wa UKIMWI.

“Mfuko huo unalenga kuokoa kizazi chetu, kulihakikishia Taifa upatikanaji wa dawa za kufubaza VVU na kuweka mkazo ili watu wote wapime na wanaobainika kuwa wameambukizwa waanze kutumia dawa mapema na kuwa na ufuasi mzuri ili kuendelea kuishi maisha ya kawaida na kutumikia taifa,” alisema.

Aidha Makamu wa Rais wa GGM, Simoan Shayo alisema GGM itaendelea kushirikiana na TACAIDS kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ili washiriki kikamilifu kwenye afua mbalimbali za udhibiti wa UKIMWI zikiwemo za Kinga, kufanya tafiti mbalimbali, matunzo kwa wagonjwa UKIMWI, WaVIU, watoto yatima na kuweka mazigira wenzeshi.

“Ndiyo maana GGM tulianzisha programu ya Kilimanjaro Challenge Against HIV and AIDS miaka 17 iliyopita ambayo sasa imekusanya zaidi ya Sh bilioni 13 ambazo zimenufaisha taasisi mbalimbali 40 zinatoa huduma za VVU na Ukimwi pamoja na Mfuko wa Ukimwi (ATF).

”Pia imesaidia uendelezaji na uendeshaji wa Kituo cha Watoto yatima Geita (Moyo wa Huruma Orphanage Centre), Utoaji huduma za UKIMWI kwa wasafirishaji wa masafa marefu na Jamii zinazoishi kwenye maegesho hatarishi na misaada kwa kupunguza athari za UKIMWI kwa Wajane na Watoto yatima kuwapatia vifaa vya elimu,” alisema.

Timu ya wapandaji 31 wa Kili Challenge iliyoongozwa na Kapteni Moses Rusasa ilifika kileleni, 32 walitumia baiskeli waliongoza na Kapteni Masolwa Bukelebe kupitia milima na mabonde.
 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira (wa tatu kushoto) akimsikiliza mmoja wa wajasiriamali waliowezeshwa na GGM kwa kupitia kampeni ya Kilimanjaro Chalenge, anayefuata ni Makamu wa GGM, Simon Shayo. Zaidi ya watu 65 walishuka mlima Kilimanjaro baada ya kupanda mlima huo Juni 15 mwaka huu.
 Baadhi ya washiriki 65 waliopanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za kutokomeza VVU na Ukimwi, kampeni hiyo imeandaliwa na GGM kwa kushirikiana na Tacaids
  • Makamu Rais wa GGM, Simon Shayo akizungumza katika hafla ya kuwapokea wapanda mlima 65 walioshuka Mlima Kilimanjaro Juni 22 mwaka huu baada ya kuupanda kwa siku saba kwa lengo la kukusanya fedha za kutokomeza VVU/Ukimwi.


  • Viewing all 110091 articles
    Browse latest View live




    Latest Images