Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

NIDA YAHITIMISHA WIKI YA UTUMISHI UMMA KWA USAFI

0
0
Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutoa huduma kwa jamii. 
Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutoa huduma kwa jamii. 
…………………….. 

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wamehitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye Ufukwe wa Coco, Dar es Salaam, Juni 22, 2019. 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati, Thomas Nyakabengwe alisema NIDA imeamua kuhitimisha wiki hiyo kwa kufanya usafi ikiwa ni kuunga juhudi za Serikali za kupambana na mifuko plastiki na ugonjwa wa kipindupindu. 

Wafanyakazi hao walifagia, kufyeka na kuzoa taka mbalimbali zilizotupwa kwenye ufukwe huo na kuzikusanya kwenye jalala la kukusanyia taka lililopo karibu na vibanda vya wauza mihogo. 

Alisema ingawa jukumu la msingi la NIDA ni usajili na utambuzi wa watu ambalo matokeo yake ni kutoa Vitambulisho vya Taifa lakini ni muhimu kushiriki kwenye shughuli za kijamii na kuwa mfano kwa taasisi nyingine za Serikali na binafsi kutenga muda wa kushiriki kwenye shuguli za kijamii. 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Harrison Lukosi aliwashukuru NIDA kwa kujitolea kufanya usafi katika ufukwe huo ambao upo kwenye Mtaa wake na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano wao wa kujitolea kwenye shughuli za kijamii. 

Pamoja na kufanya usafi NIDA imeshiriki kwenye maadhimisho hayo kwa kusajili wananchi katika kanda mbalimbali nchini ili kufanikisha azma ya usajili wa laini za simu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu “Uhusiano Kati ya Uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji, Kujenga Utamaduni wa Utawala Bora, Matumizi ya Tehama na Ubunifu katika Utoaji Wa Huduma Jumuishi”

DK. SHEIN, AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA CCM ZANZIBAR AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI LEO

0
0
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua Mkutano wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afiri Kuu ya CCM Zanzibar, kushoto Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Mhe.Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Balozi Seif Ali Iddi. 
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kilichofanyika katika ukumbi wa CCM Kisiwandui Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar akisalimiana naMjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Kombo, kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,. Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Hamad Mberwa, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuhudhuria Kokao cha Kamati Maalu ya CCM Zanzibar
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi wa CCM Afisi Kuu Zanzibar, alipowasili kuhudhuria Kikoa cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM na Makamu wa Pili wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na kulia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM Mwalimu Kombo, wakiwa wamesimama baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wa Kikoa cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar uliofanyikia Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
WAJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa wamesimama wakati wa kuwasili Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuongoza Kikoa cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika Afiki Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijiandaa kufungua Mkutano wa Kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika uku 

…………… 

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. 
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar kuanzia Majira ya Saa 4:00 Asubuhi. 

Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar. 
Kikao kilikuwa cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 1977 Toleo la 2017,Ibara ya 108 (2). 

Viongozi mbali mbali wameudhuria Kikao hicho wakiwemo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. 

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. 

Aidha Chama Cha Mapinduzi kinaeleza kuwa Kikao hicho ni miongoni mwa Vikao Vyake vya Uongozi vya Kitaifa vinavyofanyika kwa Mujibu wa Kanuni na Miongozo ya CCM. 
Imetolewa na Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar.

Jukwaa la Walimu Wazalendo Kinondoni Wachangia Damu Hospitali ya Rufaa Dodoma

WIKI YA UTUMISHI WA UMA WAFANYAKAZI NEMC,AICC WAFANYA USAFI HOSPITALINI.

0
0

Na Woinde Shizz, Arusha 

Wafanyakazi wa kituo cha mikutano cha Arusha(AICC) kwakushirikiana na wafanyakazi wa baraza la utunzaji na usimamizi wa mazingira leo wamehitimisha kilele cha Wiki ya utumishi Umma kwa kufanya usafi katika baadhi ya maeneo ya jiji la Arusha ikiwepo hospital ya AICC inayomilikiwa na kituo . 

Akiongea na waandishi wa habari kaimu mkurugenzi wa mwendeshaji wa kituo hicho cha mikutano Victor Kamagenge alisema kuwa katika wiki hii ya kuazimisha wiki ya watumishi wa umma wao kama kituo wamefanya kazi mbalimbali ikiwemo uongozi wa kituo kukutana na wateja wao waliopanga katika ofisi zao pamoja na Nyumba zao, wafanyakazi wa kituo hicho na wamehitimisha leo kwakufanya usafi katika hospital hiyo inaomilikiwa na kituo. 

Alisema kuwa lengo la kuazimisha siku hii kwakufanya usafi katika hospital hii ni kusaidia kuweka mazingira mazuri ya hali ya usafi katika hospital yao ambayo pia ni moja ya sehemu inayoingizia mapato kituo 
“mnajua tumeona tuje kufanya usafi hapa hospital ili mazingira yetu yazidi kuwa rafiki kwa wateja wanaokuja hapa kupata huduma, haiwezekani mgojwa anakuja hapa kutibiwa akimaliza anaondoka na ugonjwa mungine kutokana na mazingira kuwa machafu hivyo ndio maana tumekuja kufanya usafi “alisema Kamagenge 

Alibainisha iwapo mazingira yatakuwa masafi na salama pamoja na huduma kuwa nzuri itasaidia ata wateja kuja kwa wingi na watapata fedha itakao saidia ata kupata gawiwo la serikali. 

Naye meneja baraza la utunzaji na usimamizi wa mazingira (NEMC)kanda ya kaskazini Lewis Nzari Alisema kuwa wao kama wasimamizi wamazingira wameamua kujiunga pamoja na kituo hichi kufanya usafi katika maeneo ya jamii kwani wanatambua kuwa mazingira yakiwa safi yanachangia kuhakikisha afya za watu zinakuwa nzuri. 

Aidha pia aliwapongeza wananchi wa mkoa wa Arusha na kanda ya kaskazini kwa ujumla kwa namna walivyopokea katazo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa la kuacha kutumia Mifuko ya plastiki ,kwani wananchi wamepokea kwa muitikio mkubwa. 

“mazara ya matumizi ya Mifuko ya plastick ni mengi sana kama vile uchafuzi wa mazingira, pia Mifuko hii inasababisha magonjwa mengi kama vile kansa na magonjwa ya uzazi “alisema Nzari 

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kupiga Vita matumizi haya ya Mifuko ya plasticki kwa kuwapa elimu wananchi wote ambao wanatumia pamoja na kuwakataza kutumia, maathimisho haya ya juma la utumishi wa uma yanafanyika kila mwaka na kauli mbiu ikiwa ni “kujenga Utamaduni wa utawala na matumizi ya tehama na ubunifu katika utoaji wa huduma jumuishi”.






RC MAKONDA ACHANGIA GHARAMA ZA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60

0
0
* Awaomba wadau, mashirika na makampuni kujitolea kuokoa maisha ya watoto hao, awapongeza Samaj Brotherhood kwa kusaidia watoto hao.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
ZAIDI ya  wagonjwa laki tatu wenye matatizo ya moyo wameonwa na madaktari bingwa wa moyo tangu kuanzisha kwa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) mwaka 2015 na zaidi ya wagonjwa 3000 kufanyiwa upasuaji ukilinganisha kasi ya upelekaji wa wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mwaka wagonjwa kati ya 50 hadi 100 pekee ndio waliokuwa wanafanikiwa kupelekwa nje kwa matibabu.

Akizungumza katika hafla ya kupokea fedha za matibabu takribani shilingi milioni 20 zilizotolewa na ukoo wa Samaj Brotherhood Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa mahitaji kwa watoto hao ni makubwa sana na zaidi ya watoto 500 wanahitaji kufanyiwa upasuaji hadi kufikia sasa na amewaomba watanzania, wadau na mashirika mbalimbali kuwagusa watoto hao kwa namna moja au nyingine ili kuweza kuokoa maisha yao.

Makonda amehaidi kusaidia kwa kuchangia gharama za upasuaji kwa watoto 60 kuanzia mwezi Julai hadi Desemba mwaka huu na kuahidi kuwa huduma muhimu za namna hiyo ikiwemo afya zinazidi kuletwa karibu zaidi na wananchi.

Aidha RC Makonda amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa  kuwezesha uwepo wa kituo hicho cha moyo na amewapongeza na kuwashukuru wana ukoo wa Samaj Brotherhood kwa kuendelea kuwa wadau na washiriki bora katika kusaidia jamii hasa watoto katika sekta ya afya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa ukoo wa Samaj, Harish Patel amesema kuwa serikali itoe elimu ya utambuzi hasa katika maeneo ya vijijini na Wilayani ambako kuna madaktari bingwa wachache wa matatizo hayo huku akitolea mifano wa watoto waliokuwa wanapewa tiba za magonjwa tofauti na yale waliyokuwa wanasumbuliwa nayo.

Harish amesema kuwa taasisi hiyo ya Hindu imesaidia na itaendelea kushiriki katika kusaidia watoto wasio na uwezo katika sekta ya afya pamoja na kushiriki katika sekta za madini, michezo, afya, elimu na kilimo.

Awali akieleza namna taasisi hiyo inavyofanya kazi Mkurugenzi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa. Mohamed Janabi amesema kuwa taasisi hiyo inaongoza kwa kufanya upasuaji kwa idadi kubwa barani Afrika ukiitoa Afrika kusini ambapo kwa mwaka jana pekee jumla ya idadi za upasuaji zilizofanyika ni 1352.

Janabi amesema kuwa taasisi hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa gharama na idadi  ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kwa matibabu huku akieleza kuwa kwa mwaka 2015-2018 idadi za upasuaji zilizofanywa na taasisi hiyo ni zimekuwa na matokeo chanya.

Amesema kuwa kati ya watoto 100 wanaozaliwa mtoto mmoja ana tatizo la moyo na kwa makadirio kwa mwaka watoto milioni 2 huzaliwa na wao kama taasisi wamejipanga na wataendelea kuwahudumia na kuokoa maisha ya watoto hao ambao kulingana na matatizo yao hufanyiwa upasuaji huo kwa kupasuliwa vifua na wengine hufanyiwa upasuaji wa tundu dogo.

Upasuaji kwa watoto 10 uliofadhiliwa na ukoo wa Samaj Brotherhood utaanza jumatatu wiki ijayo na kuanzia mwezi Julai hadi Disemba watoto 10 waliofadhiliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda watafanyiwa upasuaji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimpa pole mtoto Lodric Dalema (2) aliyeletwa hospitali hapo kutoka Katesh, Manyara ambapo alipewa tiba ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa zaidi ya miezi 6 kabla ya kugundulika na tatizo hilo na kuletwa JKCI kulia ni mama wa mtoto huyo bi. Paulina Saktai, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni  ishirini mmoja ya wazazi wa watoto wenye matatizo hayo bi. Agnes Mahenge pesa zilizotolewa na ukoo wa Samaj Brotherhood ili kusaidia kufanikisha  upasuaji kwa watoto 10, utakaoanza jumatatu wiki ijayo, leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni  ishirini kutoka kwa mwenyekiti wa ukoo wa Samaj Brotherhood Harish patel ambazo wamechangia kusaidia kufanikisha  upasuaji kwa watoto 10, utakaoanza jumatatu wiki ijayo, leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na watoto wenye matatizo ya moyo pamoja na ukoo wa Samaj Brotherhood na wafanyakazi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI WA UTUMISHI WA UMMA, VIJANA NA JINSIA JAMHURI YA KENYA AMSIFU RAIS MAGUFULI KWA UTHUBUTU WA UJENZI WA SGR.

0
0
Banda la Shirika la Reli Tanzania - TRC lilipo katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa umma Barani Afrika katika viwanja vya KICC jijini Nairobi nchini Kenya Limepata fursa ya kutembelewa na Waziri wa Utumishi wa Umma,Vijana na Jinsia Mheshimiwa, Dokta Margaret Kobia juni 22, 2019.

Lengo la ziara ya Waziri katika maadhimisho haya kwa nchi za bara la Afrika ni kufahamu majukumu ya taasisi za utumishi wa umma zilizoshiriki,maendeleo na ubunifu unaoleta tija katika nchi zilizoshiriki kutoka nchi tofauti barani Afrika.

Kupitia ziara hiyo Mheshimiwa Waziri alisifu uthubutu alioufanya Mh.Rais Dokta John Pombe Magufuli katika mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa-SGR.

Pia Waziri amepata fursa ya kufahamu Huduma zitolewazo na TRC pamoja na miradi mikubwa inayosimamiwa na Shirika la Reli yaani Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR,Uboreshaji wa Reli ya kati na miradi mingine kama Ufufuaji wa njia ya reli Tanga, Arusha ba Moshi pamoja na Mradi wa treni za kisada za Mijini ambazo TRC imeanza na jiji la Daresalaam na Dodoma.

Maadhimisho haya ya Utumishi wa umma barani Afrika yaliyobebwa na kauli mbiu Uhusiano kati ya uwezesha vijana na usimamizi masuala ya uhamiaji, kujenga utamaduni wa utawala Bora, matumizi ya Tehama na ubunifu katika utoaji utoaji huduma jumuishi.

Washiriki kutoka Tanzania ni taasisi zilizo chini ya serikali kuu ambapo maadhimisho haya yameandaliwa na kuongozwa na Ofisi ya Rais Utumishi, Taasisi hizo ni zilizoshiriki ni Shirika la reli Tanzania-TRC, Mamlaka ya chakula na Dawa-TFDA, Bohari ya Dawa Tanzania-MSD.

Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika yanatarajia kufungwa juni 23, 2019 katika jiji la Nairobi nchini Kenya.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari  na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk  akitoa  Maelezo na ufafanuzi  kwa Waziri wa Wizara ya Utumishi wa Umma, Vijana na Jinsia, Jamhuri ya Kenya  Dkt.Margaret Kobia  (Wa pili kushoto)kuhusu Huduma zitolewazo na TRC pamoja na miradi inayosimamiwa katika maadhimisho  ya wiki ya utumishi wa umma mjini Nairobi nchini Kenya katika viwanja vya KICC  leo juni 22, 2019.
 Mhandisi Tito Mateshi kutoka TRC akitoa  Maelezo  kwa Bi Hytham Amour kuhusu miradi inayosimamiwa na TRC pamoja na huduma zitolewazo katika maadhimisho  ya Wiki  ya wiki ya utumishi wa umma jijini Nairobi nchini katika viwanja vya KICC juni 22, 2019.
Watumishi wa  Shirika la Reli Tanzania -TRC wakimpokea mdau  Bi Lilian John, tayari kwa kumpatia maelezo kuhusu Huduma zitolewazo  pamoja na miradi inayosimamiwa na TRC katika maadhimisho  ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika  yanayoendelea  jijini Nairobi, nchini Kenya juni 22, 2019.
Baadhi ya Wadau jijini Nairobi  walipotembelea banda la Shirika la Reli  Tanzania -TRC kwa ajili ya kupata uelewa kuhusu  Huduma na Miradi inayosimamiwa na TRC katika viwanja vya KICC  jijini Nairobi  nchini Kenya juni 22, 2019.

ASKARI POLISI WANAOWASUMBUA WAFANYABIASHARA KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA WAPEWA ONYO KALI

0
0

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, mapema leo amefunga mafunzo katika Eneo la mafunzo liliopo Kilelepori wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kwa askari wanaotunza Silaha na Vielelezo vilivyopo ndani ya vituo vya polisi katika sehemu mbalimbali, katika
hatua hiyo amewataka Askari kutenda kazi kwa kuzingatia Maadili na
Weledi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi hii itasaidia
kuepuka kupotea kwa vielelezo hivyo. 

Aidha katika hatua hiyo amewaonya Askari Polisi wanaoomba na kupokea rushwa kutoka sehemu mbalimbali hasa kwa wafanyabiashara na watu wengine wenye nia njema ya kuhakikisha Uchumi wa Nchi unapanda na kufikia uchumi wa kati, Jeshi la Polisi halitamuonea muhali askari yoyote bali atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi kisha kufikishwa mahakamani kwa kufanya hivyo Jeshi la Polisi litakuwa limemuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Magufuli katika kuhakikisha nchi yetu inafikia uchumi wa kati. 

Amemalizia kwa kuwataka wale wote wanaotaka kuvunja amani au kuchezea amani ya nchi yetu watachukuliwa hatua kali ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani kama ilivyo na inavyofahamika kuwa Tanzania ni kisiwa cha amani.

BASHIRU AZINDUA UJENZI WA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO CCM PWANI

0
0


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Bashiru Ally amezindua ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mkoani Pwani,ambapo amechangisha zaidi ya milioni 25 na vifaa mbalimbali.

Katika uzinduzi huo, jumla ya mifuko ya saruji 2,861 imechangiwa ,nondo tani tano thamani ya milioni 9 ,malori ya mchanga, fedha taslimu ni sh.milioni 22.562 na ahadi ni sh.milioni 2.5 .

Alisema kati ya fedha hizo milioni tano imechangiwa na mwenyekiti wa CCM Taifa dk.John Magufuli.

Bashiru alisema, kwasasa hakuna mtindo wa kuchangia shughuli za kichama kwa fedha za mikononi ili kuweka mifumo mizuri ya kuaminiana.

Aidha alisisitiza ujenzi wa ofisi za chama ili kukijenga chama kwa maslahi ya wanaCCM.

“Uhai wetu unatokana na vikao na vikao haviwezi kufanyika chini ya miti,au kukutana gesti ,hivyo jengeni ofisi za chama kuanzia matawi na kata ili kuimarisha chama chetu”

Hata hivyo aliwasihi wananchi wasiwasikilize wale wanaokebehi Chama kilichopo madarakani na wale wanaopotosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.“Upotoshaji ni dhambi hasa kwa mtu aliyesoma chuo cha Dar es salaam na kusisitiza kwamba ,hali ya uchumi wetu ni imara” .


“Huwezi kudanganya watu na kuwaona ni wa pumbavu ,hakuna uchumi uliokufa ,hatuna deni la ndege,tunajenga vituo vya afya ,tunatundika nishati ya umeme hadi vijijini,watoto wanasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne leo mtu unaibuka anasema uchumi umekufa”alikemea Bashiru. 

Hakusita ,kuupongeza mkoa kwa kushirikiana ,kushikamana na kuwa na mahusiano mema baina ya serikali na chama. Aliweka wazi wilaya ambazo bado hazina mahusiano mazuri kati ya serikali na chama ikiwemo Bagamoyo ,Rufiji na Kibaha Vijiji ambako pale tatizo lipo kwa mkurugenzi mtendaji wa Kibaha Vijijini. 

Alimjia juu mkurugenzi huyo wa wilaya ya Kibaha kwa kufanya kazi zake kwa mazoea na kushindwa kujenga mahusiano na ushirikiano na chama na kwenye majukumu yake ya kazi. Katika hatua nyingine akielekeza juu ya muelekeo wa chaguzi zijazo ,Bashiru aliwataka viongozi wanaokaa kwenye vikao vya maamuzi waache kutembea na wagombea mifukoni na badala yake waache wabunge,madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa waliopo wafanye kazi. 

Pia aliwaasa baadhi ya wabunge kuacha kutumwa na kuwa wapiga debe kwa wawekezaji uchwara bali waelekezeni wawekezaji masharti na taratibu za nchi kwa maslahi mapana ya nchi. Awali mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani ,Ramadhani Maneno alisema siasa inayotakiwa sasa ni siasa ya uchumi ili kujiinua kiuchumi na kuimarisha chama.

Maneno aliomba pia changamoto ya tatizo la usafiri wa uhakika kwa njia ya maji utatuliwe kwani imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wa Mafia.
Katika uzinduzi huo wa ujenzi wabunge wamechangia kiasi cha sh.milioni 12 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za kufufua ujenzi wa ukumbi huo.

Pamoja na hilo kila mmoja kati yao alichangia ambapo mbunge wa jimbo la Chalinze aliahidi kuchangia mifuko ya saruji 1,200 na familia yake,mbunge wa Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa alichangia mifuko ya saruji 100 na mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega alisema atachangia vigae vya ujenzi mzima .

Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka aliahidi kuchangia tani tano za nondo zitagharimu milioni tisa,mbunge wa Kibiti Ally Ungando sh.500,000,mbunge wa Bagamoyo Shukuru Kawambwa sh.milioni moja na Amina Makilagi mifuko ya saruji 100.

Wengine ni MNEC Mkoa Hajji Jumaa amechangia 200,000,wabunge wa viti maalum mkoani hapo Subira Mgalu na Zaynab Matitu Vullu wameahidi kuchangia mabati yatakayotakiwa katika ujenzi huo na ofisi ya mkuu wa mkoa imechangia milioni mbili na mifuko ya saruji 600.#

MAJALIWA ASHIRIKI BONANZA NA BENKI YA NMB NA WABUNGE

0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira wakati lipoanzisha mechi ya mpira wa kikapu ya Bonanza na Benki ya NMB na Wabunge kati ya timu ya Bunge na NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Wachezaji wa timu ya mpira wa kikapu ya Bunge wakiwa wamejipanga kabla ya mechi kati yao na timu ya Benki ya NMB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua timu ya Mpira wa kikapu ya Benki ya NMB ambayo ilipambana na timu ya Bunge katika mechi la Bonanza la Benki ya NMB na Bunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 



WATUMISHI NI MUHIMU KUSHIRIKI MICHEZO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni muhimu kwa watumishi kushiriki katika michezo mbalimbali kwa kuwa inaimarisha afya pamoja na kudumisha mshikamano.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Juni 22, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya NMB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema mbali na kuimarisha afya kwa watumishi na wabunge, pia michezo inasaidia katika kuimarisha mshikamano baina ya benki hiyo pamoja na wateja.Akizungumzia kuhusu utendaji wa benki ya NMB, amesema imekuwa ikishirikiana na Serikali kuwaelimisha wakulima umuhimu wa kufungua akaunti na kujiwekea akiba.

“Benki ya NMB ni benki pekee iliyomudu kufungua matawi hadi maeneo ya vijijini, hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma kwa watumishi na wananchi waishio maeneo hayo.”Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya Bunge ilishinda baada ya kuifunga timu ya benki ya NMB magoli matano kwa matatu. 

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuifunga timu ya NMB magoli 25 kwa 18, huku katika mchezo wa mpira wa kikapu timu ya NMB ilishinda baada ya kuifunga Bunge vikapu 52 kwa 51.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za NMB.

Watumishi Mambo ya Ndani ‘waikosha’ Hospitali ya Mirembe, wapewa elimu

0
0
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya usafi wamazingira kwenye Hospitali ya Rufaa ya Wagonjwa wa Akili yaMirembe, iliyopo mkoani Dodoma leo. 

********* 

Na Mwandishi Wetu, MOHA 

UONGOZI wa Hospitali ya Rufaa ya Wagonjwa wa Akili ya Mirembe, mkoani Dodoma, umefurahishwa na kitendo cha watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwenda kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo. 

Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mganda Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt. Escor Tweve. Watumishi hao wakiwa na baadhi ya viongozi wa Wizara, idara zilizopo chini ya Wizara hiyo, waliadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapo. 

“Nawashukuru kwa uamuzi wa kuja kufanya usafi wa mazingira hospitalini hapa kwa kufyeka, kulima, kuchoma taka, kudeki na kufanya kazi nyingine za kijamii. “Mmeonyesha upendo mkubwa mlionao dhidi yetu, mmejitoa kwa moyo wa dhati, miaka mingi imepita hatujawahi kupata ugeni uliofanya jambo muhimu kama hili,” alisema Dkt. Tweve. 

Mbali ya kufanya usafi wa mazingira, watumishi hao walipata fursa ya kupewa elimu juu ya huduma zinazotolewa kwa wagonjwa hospitalini hapo.  Dkt. Tweve alisema changamoto kubwa waliyonayo wagonjwa wa akili huwa hawapendwi katika jamii ila ni watu wanaopaswa kupewa upendo mkubwa na jamii. 

“Wagonjwa wa akili hawana tofauti na watu wengine ambao hawana matatizo kama yao kwenye jamii, wanapoletwa hapa hospitali huwa tunawapatia matibabu, kupona, kutoa michango mizuri kwenye jamii na nchi kwa ujumla,” alisema. Aliishukuru Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa wanaowapa kwani kuna wagonjwa wengine wa akili hukamatwa, kuhitajika kufanyiwa matibabu hospitalini hapo. 

Pia wapo baadhi ya watumishi wa idara za serikali wakiwemo askari ambao hospitali hiyo huwapatia matibabu ya akili, kupona, kuendelea na majukumu yao ya kazi. “Naishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuadhimisha siku hii kwa kuja Mirembe na kufanya usafi wa mazingira, nawaomba muwe na utaratibu wa kuja mara kwa mara,” alisisitiza. 

Aliwapongeza watumishi wa Wizara hiyo na viongozi wao akiwemo Waziri Kangi Lugola, Naibu Waziri, Mhandisi Hamad  Masauni, Katibu Mkuu, Meja Jenerali Jacob Kingu, Naibu KaribuMkuu, Ramadhani kailima kwa utendaji mzuri wa kazi. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha TEHAWA katika Wizara hiyo, Jane Massawe ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu, aliushukuru uongozi wa hospitali hiyo kwa ushirikiano walioutoa kwa watumishi  hao. “Tumefurahishwa na mapokezi mliyotupa, tupatapo nafasi kwa siku nyingine tutakuja kuwatembelea na kufanya shughuli za
kijamii,” alisema Massawe. 

Wiki ya Utumishi wa umma ilianza huadhimishwa kuanzia Juni 17 hadi 22, mwaka huu. Maadhimisho hayo ni kwa mujibu wa Kalenda ya Umoja wa Afrika (AU).  Nchi mbalimbali huadhimisha siku hiyo kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu utumishi wa umma.

ALICHOZUNGVUMZA KOCHA NA NAHODHA WA TAIFA STARS LEO KUHUSIANA NA MCHEZO WAO DHIDI YA SENEGAL

0
0
Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars,amesema wana imani kubwa ya kuweza kuibuka na ushindi katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Senegal,ambao ni mchezo wa kwanza utakaofanyika,Juni 21 katika Uwanja wa 30 June,Cairo,Misri.

Amunike amesema mpaka sasa wameweza kujiandaa kimbinu na kiakili katika mchezo huo ambao anatambua wanacheza na timu kubwa Barani Afrika, lakini hawana wasiwasi kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

“Kikubwa katika mchezo huo,tumejiandaa kisaikolojia na kimbinu ili tuweze kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na tunaamini kesho utakuwa mchezo mzuri wa mashindano,na naamini wachezaji wangu wapo kamili kuweza kucheza mchezo huo na wanajua umuhimu wa mchezo huo.

Kwa upande wa nahodha wa Taifa Stars,Mbwana Samatta,alisema Kwamba wanawaheshimu Senegal kwakuwa ni timu kubwa Afrika ,lakini hawatokwenda uwanjani kinyonge.

“Kikubwa ni kwamba tutakwenda uwanjani,huku tukijua tunaenda kupambana na timu kubwa na lazima tupambane uwanjani ili tuwezee kulisogeze jina la nchi yetu,hivyo tunaamini kabla ya filimbi ya mwisho kila timu ina nafasi.”

TIMU YA WATAALAM TOKA SERIKALI YA CHINA WATUA NCHINI KUKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA CHUO CHA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL

0
0
Juni 21/2019 timu ya wataalam Saba toka Wizara ya Uchumi na Fedha ya Serikali ya China ilitembelea eneo la ujenzi wa Chuo cha Mwalimu Nyerere Leadership School, kilichopo Kibaha kwa Mfipa kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo.

Mratibu wa ujenzi huo Bi. Emmanuela Mtatifikolo Kaganda alieleza kuwa, ukaguzi huo unaotarajia kuchukua siku kumi unafanyika kwa mara ya kwanza ikiwa shughuli zote za ujenzi wa msingi, nguzo na kuta za majengo yote umekamilika. 

Pamoja na mambo mengine wakaguzi hao wanaangalia uimara na ubora wa majengo, kabla ya kutoa kibali kwa mkandarasi kampuni ya CRJE kuendelea na ujenzi. 

Aidha Bi. Kaganda alieleza kuwa ukaguzi wa pili utafanyika katika hatua za mwisho za ujenzi miezi michache ijayo huku wa mwisho ukitarajiwa kufanyika baada ya ujenzi kukamilika na kabla ya mradi kukabidhiwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mradi wa ujenzi wa chuo hicho cha mafunzo ya itikadi na uongozi chenye uwezo wa kufundisha viongozi 200 kwa wakati mmoja, kinachomilikiwa na CCM kwa kushirikiana na vyama vya ANC, Afrika Kusini; ZANU PF, Zimbabwe; FRELIMO , Msumbiji na SWAPO, Namibia, ulizinduliwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mwezi Julai 2018 na kinatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2020.

WATUMISHI WA SEKRETARIATI YA MKOA WA KATAVI WAJITOKEZA KUJENGA HOSPITALI

0
0
Baadhi ya watumishi wakihamisha matofali kwenda katika jengo la wazazi linaloendelea kujengwa 

Katikati Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Omary Sukari akinyanyua tofali kwa ajili ya ujenzi unaoendelea wa hospitali ya wilaya ya Tanganyika, kulia kwake ni Afisa Utumishi Mkoa wa katavi Bi. Cresensia Joseph 
Baadhi ya watumishi wakifanya usafi kwa kufyeka nyasi katika eneo la hospitali ya wilaya ya Tanganyika 
Jengo la maabara likiwa tayari limekwishaezekwa 



Na Mwandishi Wetu Katavi 


Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma watumishi wa sekretariati ya mkoa wa katavi wamejumuika na mafundi katika kusaidia kazi mbalimbali za ujenzi katika hospitali ya wilaya ya Tanganyika lengo likiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Afisa Utumishi wa Mkoa Bi. Cresensia Joseph amesema lengo la zoezi hilo ni kuunga mkono juhudi za serikali kutoa huduma kwa wananchi 

Amesema watumishi wanatambua azma ya serikali ya kufikisha huduma karibu na jamii hivyo nao wamejitoa kwa nguvu zao kushiriki katika ujenzi huo .Aidha baadhi ya watumishi walioshiriki katika zoezi hilo wamesema wanafanya hivyo katika kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusogeza huduma za afya kwa jamii 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Dkt. Selemani Mtenjela amesema hospitali hiyo ikikamilika itahudumia zaidi wakazi laki tatu wa wilaya hiyo 

Ameongeza kuwa hospitali hiyo ikikamilika itawaondolea adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa 130 wakazi wa wilaya hiyo kufuata huduma za afya katika hospitali ya manispaa ya Mpanda

Wabunge watembelea kambi ya Taifa Stars

0
0
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakiongozwa na Spika Job Ndugai, leo wameitembelea kambi ya timu ya taifa Taifa Stars,iliyopo nchini Misri,inayojiandaa na mashindano ya Mataifa Afrika.

Wabunge hao wamepata nafasi ya kuzungumza na wachezaji pamoja na viongozi waliopo na kambi hiyo nchini Misri,kwa leongo la kuweza kuwapa hamsa katika kuelekea mchezo wao wa kwanza wa tangulizi dhid ya Senegal na michezo mingine inayofuatia.

Mbunge wa Viti Maalumu,Mheshimiwa Salma Kikwete,akizungumza leo kwa niaba ya wabunge wengine alisema:

“Napenda kuwapongeza sana kwa kazi kubwa na nzuri kuanzia mwanzo na hatimaye kesho tunafikia kileleni,tumekuja hapa kwa ajili ya kuungana na timu kuwatia moyo na kuwatia shime na kuwaambia kwamba tumekuja Misri sio kushiriki bali kushinda,”alisema na kuongeza:

“Ushirikiano katika timu yaani ‘team work’ ndiyo itakayoleta ushindi,kwa maana hiyo Watanzania wote macho na masikio yao ni kwenu, kwahiyo,mtangulizeni Mwenyezi Mungu na Mungu atawasaidia.”

Kwa upande wa Mheshimiwa Magreth Sitta alisema, ”Nawapongeza sana vijana ambao wamechaguliwa katika hii timu,siku zote mi huwa napenda kuchukua mfano wa Leicester City ya England,wakati inachukua ubingwa haikuwa na mchezaji hata mmoja ambaye anajulikana sana,lakini waliweza kupambana kwahiyo na nyie msigope majina naamini mnaweza.”

Wabunge hao walifunga mazungumzo yao kwa sala ya pamoja na wa chezaji na viongozi,kwa sala iliyoongozwa Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa,kwa ajili ya kuiombea timu ya taifa katika mchezo wa kesho na michezo mengine miwili dhid ya Kenya na Algeria.

WATAFITI WATAKIWA KUTUMIA MBINU ZA KISAYANSI ILI KULETA TIJA KATIKA JAMII

0
0
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe, akieleza umuhimu wakuzingatia mbinu za ufanyaji wa tafiti zenye kuzingatia viwango vya kimataifa katika wakati akifungua warsha ya watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda, akitoa mada katika warsha ya watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma, ambapo alieleza mikakati ya Serikali kukuza uchumi na ajira nchini. 
Watafiti kutoka nchi ya Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda na wenyeji Tanzania, wakifuatilia mada kuhusu changamoto za kiuchumi Afrika na mikakati ya kukabiliana nayo ikiwemo kuwa na uchumi wa viwanda, iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani), katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma 
Mhandisi wa Chuo Kikuu cha Munich Ujerumani Prof. Walter Vries, akisikiliza kwamakini maelezo ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda(kushoto), wakati wa warsha ya watafiti kutoka nchi tano za Afrika, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. 
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa utafiti kutoka Ujerumani, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Rwanda, wakati wa warsha ya watafiti wanaochipukia, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. 
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa utafiti kutoka baadhi ya halmashauri nchini, na wengine kutoka nchi ya Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Rwanda wakati wa warsha ya watafiti wanaochipukia, katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. 



****************** 

Watafiti nchini wametakiwa kuweka mkazo katika mbinu za utafiti zinazokidhi viwango vya kimataifa ili kuwa na majibu ya tafiti zenye tija zilizo na lengo la kutatua changamoto katika jamii ya watanzania na duniani kwa ujumla. 

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof Davis Mwamfupe,alipokuwa akifungua warsha ya Watafiti kutoka nchi ya Kenya, Afrika Kusini, Rwanda, Uganda na wenyeji Tanzania, uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) jijini Dodoma. 

Mtahiki Meya Mwamfupe, alisema kuwa ili utafiti uwe na thamani nilazima kutumiambinu zinazoaminika bila kujali utafiti unaofanyika unahusu kitu gani, kwa lengo la kuondoa mkanganyiko wa matokeo hivyo kuwa na tija kwa jamii. 

“Utafiti wa kisayansi ni ule unaotumia njia zinazokubalika kimataifa na kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zikiwemo za kutokuwa na usawa hasa katika pande mbili za Dunia yani Kasikazini na Kusini lakini pia katika jamii moja na nyingine”, alieleza Meya Prof. Mwamfupe. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, ambaye alikua mtoa mada katika warsha hiyo alisema kuwa, katika wasilisho lake wadau kutoka nje ya nchi wamefurahishwa na uchambuzi kuhusu hali ya uchumi ambapo ilielezwa namna watu wenye kipato kikubwa kupenda kununua bidhaa nje jambo ambalo limeifanya Serikali ya Tanzania kuweka mikakati ya kutatua tatizo hilo ili kujenga uchumi wa nchi. 

Alisema kuwa tabia ya wenye kipato kikubwa kununua bidhaa nje kuna kosesha ajira, hivyo Serikali imeamua kuweka mikakati ya Ujenzi wa uchumi katika Nyanja ya viwanda, kilimo na miundombinu ikiwemo ya umeme, jambo ambalo ni ajenda ya Afrika Kwa upande wake Mratibu wa Warsha hiyo ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Cha Mipango Vijijini, Dkt. George Kanyasi, alisema kuwa lengo la Warsha hiyo ni kuwakutanisha watafiti wanaochipukia na wanasayansi kutoka nchi tano za Afrika kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kupata watafiti mahiri. 

Amesema kuwa kazi ya tafiti sio tu kuongeza maarifa lakini pia kutatua changamoto katika maeneo yaliyokosa usawa katika elimu, uchumi, siasa na masuala ya kijamii Mkutano huo pamoja na kuwashirikisha watafiti kutoka nje ya nchi, pia umewahusisha baadhi ya wadau kutoka Halmashauri ili kujua changamoto zao na kuweka mikakati ya kuzitatua, aidha warsha zinazofuata zitawakutanisha Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Mipango ili waweze kubaini matatizo ya maeneo yao na waweze kuyatatua.

WATAKAOWASUMUA WAFANYABIASHARA KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA KUKIONA.

0
0
 Kamishna wa Operesheni na Mafunzo-CP Liberatus Sabas

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKABIDHI KOMBE TIMU YA BUNGE BONANZA LA NMB

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) na wa tatu kulia Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bw. Albert Jonkergouw wakimtazama nahodha wa timu ya Soka ya Bunge, Cosato Chumi aliponyanyua kikombe cha ushindi wa mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5 - 3. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kikombe nahodha wa timu ya soka ya Bunge, Cosato Chumi baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa 5-3 dhidi ya timu ya NMB katika mchi ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 22, 2019. Kushoto ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,wa tatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bw. Albert Jonkergouw .

Martin Massawe wa NMB akimlamba chenga Abdallah Aman wa Bunge (kushoto) katika mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5-3.
Abdallah Aman wa Bunge (kushoto) akizuia mpira huku akizongwa na Martin Massawe wa Bunge katika mechi ya soka ya Bonanza la Benki ya NMB na Wabunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 22, 2019. Bunge ilishinda 5-3. 

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MISA TAKATIFU YA MAADHIMISHO YA SHEREHE EKARISTI TAKATIFU KANISA LA MTAKATIFU PETRO JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Padre Dkt. Alister Makubi, Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam baada ya kushiriki Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu kanisani hapo katika leo Jumapili Juni 23, 2019. Katikati ni Paroko Msaidizi wa kanisa hilo Padre Paul Haule na Mzee wa Kanisa Dkt. Aldehem Meru
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki katika Misa ya Maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumapili Juni 23, 2019 

MAMENEJA TANESCO TUTAWAPIMA KWA KAZI ZENU – NAIBU WAZIRI MGALU

0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza na wananchi wa wananchi wa Mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu, wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani, kabla ya kuzindua rasmi uwashaji wa umeme katika Mtaa huo, kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza, Juni 22, 2019. 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akiwa amefuatana na Mbunge wa Kibaha Mjini, Silivester Koka (wa pili-kulia), Mtendaji wa Mtaa wa Vitendo wilayani Kibaha, Juma Hamisi (wa pili-kushoto), wataalamu kutoka REA, TANESCO pamoja na wananchi; akiwa katika ziara ya kazi wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani, Juni 22 mwaka huu. 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akiwahamasisha wananchi wa Mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu, wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani, kutumia kifaa cha Umeme Tayari (UMETA), alipokuwa katika ziara ya kazi na kuwawashia umeme, Juni 22 mwaka huu. 

****************** 



*Na Veronica Simba – Pwani* 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa wito kwa Mameneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Ngazi ya Mkoa na Wilaya nchi nzima, kufanya kazi kwa bidii kwani ndicho kigezo kitakachotumiwa kuwapima iwapo wanafaa kuendelea kushikilia nyadhifa hizo. 

Ametoa wito huo leo Juni 22, 2019 wakati akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu, wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani, kabla ya kuzindua rasmi uwashaji wa umeme katika Mtaa huo, kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu, Mzunguko wa Kwanza. 

“Meneja wa TANESCO ujisikie aibu kukuta Mtaa una nyumba 300 na hauna umeme; wewe upo tu! Tuwawapima kwa kazi,” alisema Naibu Waziri. 

Akifafanua, Naibu Waziri Mgalu alisema, hakuna mantiki kuwa na Meneja wa Wilaya au Mkoa, ambaye wananchi wa eneo lake wanaomba umeme miaka minne hadi mitano mfululizo wakati yeyé mwenyewe hana andiko wala ubunifu na wala hafuatilii. “Maeneo mengine yasiyo na umeme yanahitaji ubunifu tu wa Meneja.” 

Akizungumzia mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Nishati, kuhusu upatikanaji na usambazaji wa umeme nchini, Naibu Waziri alisema iko miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa, ambayo kukamilika kwake kutawezesha nchi kuwa na umeme mwingi zaidi na wenye uhakika. 

Aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni pamoja na wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza, Mradi wa Ujazilizi (Densification) Awamu ya Pili pamoja na ule ujulikanao kama Miji Vijiji (Peri-Urban). 

Kuhusu Mradi wa Miji Vijiji, alisema upo katika hatua za mwisho ambapo mchakato wa zabuni umekamilika, wakandarasi wa kuutekeleza wamepatikana na mikataba imewasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama taratibu zinavyoelekeza. 

“Tuna matarajio hadi kufikia wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu, mikataba itakuwa imerudi na tutawakabidhi wakandarasi waanze utekelezaji,” alisema. 

Alisema takribani shilingi za kitanzania bilioni 86 zimetengwa kwa ajili ya kuwasambazia wananchi umeme kupitia mradi huo ambao utahusisha maeneo ya Ukonga, Kigamboni, Kibaha na Bagamoyo. 

Vilevile, Naibu Waziri Mgalu alisema kuhusu Mradi wa Ujazilizi Awamu ya Pili, takribani shilingi za kitanzania bilioni 169 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji. 

Akiendelea kubainisha jitihada mbalimbali za kuboresha sekta ya umeme nchini, alisema TANESCO wamebainisha maeneo 754 ambayo yamepitiwa na umeme mkubwa hususan barabarani lakini hayajashushiwa nishati hiyo kwa lengo la kutatua changamoto husika. 

“Tumewapa miezi sita, hadi Desemba 2019 wawe wamekamilisha,” alisisitiza na kuongeza kuwa jumla ya shilingi bilioni 400 zimetengwa kukamilisha kazi hiyo. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri aliuagiza uongozi wa TANESCO Mkoa wa Pwani, kuhakikisha wanatimiza pasipo kuchelewa ahadi walizotoa mbele yake, ikiwemo kuziwashia umeme Kaya 10 za Mtaa wa Vitendo, ambazo zimekwishalipia huduma hiyo, ifikapo kesho (Jumapili), Juni 23, mwaka huu. 

Nyingine ni kukamilisha kazi ya makadirio ya gharama za kuunganishiwa umeme kwa Kaya 30 za Mtaa huo, ifikapo Jumanne ijayo, Juni 25 mwaka huu ili Mkandarasi aziwashie umeme siku ya Alhamisi ya Juni 26, 2019. 

Akizungumza katika tukio hilo, Mbunge wa Kibaha Mjini, Silivester Koka, aliwasihi wananchi ambao bado hawajafikiwa na huduma ya umeme kuwa na uvumilivu kwani zoezi la kuunganisha nishati hiyo ni endelevu. 

Naye Kaimu Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Pwani, Mhandisi Kenneth Boymanda, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu kwa Ofisi yake katika eneo husika, alimweleza Naibu Waziri kuwa, vitongoji 25 vya Wilaya ya Kibaha vimenufaika kwa kupata Mradi wa umeme wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza. 

Akizungumzia hatua iliyofikiwa katika utekelezaji, alisema Mkandarasi amekwisha washa jumla ya transfoma 24 na kuunganisha wateja wapatao 554. 

Alizitaja Kata zinazonufaika na Mradi huo kuwa ni Gwata, Mlandizi, Kilangalanga, Janga, Kikongo, Kwala, Boko, Kawawa na Soga.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHANUFAISHA KIUCHUMI KIKUNDI CHA MKULIMA JEMBE CHA KATA YA BUKIMA

0
0
Na Verediana Mgoma 

KIKUNDI cha MKULIMA JEMBE kilichopo Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima kilianzishwa Mwaka 2014 kikijishughulisha na uoteshaji wa miche badaae walifanikiwa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji wakilimo cha mbogamboga, matunda pamoja na mazao ya chakula ikiwemo viazi vitamu, maharage na mahindi.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndugu Festo Obed ameeleza kuwa kupitia kilimo cha umwagiliaji wamefanikiwa kununua Mashine/Pampu ya Umwagiliaji ya SOLAR, kusomesha Watoto wao na kujikimu kwenye matumizi mengine ya kifamilia. Fedha zao zinatunzwa Benki. 

Aidha, Obed ameeleza kikundi cha MKULIMA JEMBE kimefanikia kuanzisha Kikundi kingine kiitwacho "TUMETAMBUA" ambacho kinajishughulisha na Kilimo cha Umwagiliaji na kina Mradi wa kuweka na kukopeshana.

Afisa Kilimo wa Kata ya Bukima, Ndugu Mushangi Salige ameeleza kuwa Kata hiyo ina fursa kubwa ya kupanua KILIMO cha UMWAGILIAJI kwa sababu Wakazi wengi wapo kando kando mwa Ziwa Viktoria. 

Afisa Kilimo huyo amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuwezesha Kikundi cha mkulima jembe kupata Vifaa vya Umwagiliaji (pampu na mipira) kutoka mfuko wa jimbo Kikundi hicho na vingine Jimboni viligawiwa bure mbegu za Mbogamboga na Matunda.

Vilevile Wanavijiji wa Kata hiyo ya Bukima wanamshukuru sana Mbunge wao Prof Muhongo kwa kuwagawia Mbegu za alizeti,mtama na mihogo amesema Afisa Kilimo huyo.
Wanachama wa Kikundi cha mkulima jembe wakiwa kwenye Shamba lao la matikiti katika Kijijini Kastam, Kata ya Bukima musoma vijijini.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images