Shirika la Reli Tanzania-TRC limepata fursa ya kushiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika, yaliyozinduliwa rasmi na Mh.Rais Uhuru Kenyata katika viwanja vya KICC nchini Kenya, Nairobi leo Juni 21 2019.
Lengo la maadhimisho haya kwa nchi za bara la Afrika ni kubadilishana ujuzi, kujifunza katika ufanisi wa kazi katika sekta za Umma ili kuleta tija na ubunifu zaidi katika maeneo ya kazi kutoka nchi tofauti barani Afrika.
Maadhimisho haya ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika yamesisitizwa na kauli mbiu wa Uhusiano kati uwezeshaji vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji, kujenga utamaduni wa utawala Bora, matumizi ya Tehama na ubunifu katika utoaji huduma jumuishi.
Kupitia maadhimisho haya TRC imepata fursa ya kuelezea ubunifu na matumizi ya Tehama katika kutoa huduma.
Huduma zitolewazo na TRC, yaani kutoa huduma za Usafiri wa Abiria, Mizigo na kukodisha nafasi kwa kampuni za serikali na sekta binafsi ndani ya Tanzania na Nje katika behewa za TRC nje na ndani kwa ajili ya matangazo kwa kua Treni za TRC zina masafa marefu na mafupi,Hivyo fursa ya kutangaza na kuongeza uelewa kuongezeka kwa umma endapo kama wadau watapenda kupata huduma hiyo.
Pia TRC iliendelea kutoa Elimu zaidi kuhusu miradi mikubwa miwili yaani Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ambao mpaka sasa umefikia zaidi ya 51% Kwa awamu ya kwanza Daresalaam-Mwanza katika kipande cha Daresalaam-Morogoro na Kipande cha pili Morogoro-Makutopola mradi huu umefika zaidi ya asilimia 12% katika usanifu na ujenzi.
Mradi wa uboreshaji wa Reli ya kati mpaka sasa umefikia zaidi ya 12% kwa ukarabati wa njia na madaja, na miradi mingine midogo kama ufufuaji wa njia ya Reli , Tanga, Arusha, Moshi ambao unatarajia kuanza rasmi huduma ya treni za abiria mwezi wa 9, 2019 na treni za mizigo kuanza mwezi wa 7, 2019.
Vile vile TRC inaendelea na maandalizi ya mradi wa huduma ya treni za mijini za kisasa kwa jiji la Daresalaam na Dodoma.
Katika maadhimisho haya ya Wiki ya Utumishi wa barani Afrika yaliyofanyika nchini Kenya, Nairobi waafrika kutoka nchi tofauti kama Kenya, Afrika kusini, Nigeria walipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedali Rais Dr.John Pombe Magufuli kwa uthubutu Alioufanya kwa kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia pesa ya ndani ambayo inapatikana kwa walipa kodi Tanzania na kusisitiza Rais Magufuli kuwa mfano Bora wa kuigwa katika utendeji kwa maslahi ya Nchi na Taifa kwa ujumla.
Maadhimisho haya ya Utumishi wa umma barani Afrika kwa upande wa Tanzania yaliwakilishwa na taasisi 3 zilizo chini ya serikali kuu ambapo maadhimisho haya yameandaliwa na kuongozwa na Ofisi ya Rais Utumishi, Taasisi zilizoshiriki ni Shirika la reli Tanzania-TRC, Mamlaka ya chakula na Dawa-TFDA, Bohari ya Dawa Tanzania-MSD.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Habari na Uhusiano TRC Bi Jamila Mbarouk akitoa Maelezo na ufafanuzi kwa mdau Denis Alphonse kuhusu miradi inayosimamiwa na TRC pamoja na huduma zitolewazo katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya KICC leo juni 21, 2019 jijini Nairobi,nchini Kenya.
Mhandisi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC),Tito Mateshi akitoa akifafanua jambo kwa Bi Catherine Erasto kuhusu miradi inayosimamiwa na TRC pamoja na huduma zitolewazo katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma katika viwanja vya KICC jijini Nairobi nchini Kenya, leo Juni 21, 2019.
Pichani ni watumishi kutoka taasisi tatu tofauti, Shirika la Reli Tanzania -TRC, Mamlaka ya chakula na Dawa-TFDA,Bohari ya dawa Tanzania -MSD zilizoshiriki katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dkt.Pindi Chana (wanne kulia) wakiwa mbele ya banda la Tanzania katika viwanja vya KICC, jijini Nairobi ,nchini Kenya leo Juni 21,2019.
Picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka ofisi ya Rais Utumishi Tanzania walipotembelea banda la Shirika la Reli Tanzania-TRC siku ya ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa barani Afrika katika viwanja vya KICC jijini Nairobi nchini Kenya, leo Juni 21, 2019.