Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110117 articles
Browse latest View live

AZAM YAENDELEA NA USAJILI WAKE KIMYA KIMYA

$
0
0
Uongozi wa Klabu ya Azam umewaongezea mikataba wachezaji wake mshambuliaji Obrey Chirwa kwa na Kiungo Salmin Hoza pamoja na kusajili mchezaji mpya.

Chirwa aliyefunga goli muhimu katika fainali ya kombe la Shirikisho ameongeza mkataba wa mwaka mmoja na Hoza akiongeza miaka miwili ya kuendelea kuwatumikia matajiri hao wa Dar es Salaam.

Mbali na kuwaongezea kandarasi wachezaji hao, Azam wamemsajili pia Kiungo mshambuliaji Emmanuel Mvuyekure, kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMC.

Wachezaji hao wote kwa pamoja wamesaini kandarasi mpya mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' na mmoja wa maofisa wa timu hiyo, Abubakar Mapwisa.

Mvuyekure anayemudu nafasi zote za ushambuliaji, anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Azam FC kuelekea msimu ujao baada ya ule wa kwanza wa winga idd 'Nado'. Mbali na kusaidia pasi za mwisho za mabao akiwa KMC msimu uliopita, nyota huyo raia wa Burundi alimaliza msimu akiwa na mabao 10.

Nyota huyo aliyewahi kucheza Mbao na KMC, tayari ameshatua nchini leo alfajiri na leo usiku anatarajia kuanza rasmi mazoezi na kikosi hicho kilichoanza maandalizi ya msimu mpya jana jioni.

Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Etienne Ndayiragije, ndiye aliyependekeza usajili wa nyota huyo, ambapo hadi sasa katika mapendekzo ya usajili wa nyota wapya wanne, amebakisha nafasi mbili, mmoja akiwa wa ndani na mwingine wa nje.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' akiwa anapeana mkono na Mshambuliaji Obrey Chirwa baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja na kuendelea kusalia katika klabu hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' akiwa anapeana mkono na kumkabidhi jezi Kiungo Mshambuliaji Emanuel Mvuyekure baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja na kuanza kibarua cha kuwatumia matajiri wa Chamazi.

DK.SHEIN AMUAPISHA MKUU WA KVZ ZANZIBAR MAJOR SAID ALI JUMA SHAMUHUNA IKULU LEO.

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mkuu wa Kikosi cha Valantia Zanzibar Major Said Ali Juma Shamuhuna, hafla hiyo imefanylia leo katika Ukumbi wa Ikulu Zanzibar.21-6-2019.(Picha na Ikulu

MKUU Mpya wa Kikosi cha Valantia Zanzibar KVZ Major Said Ali Juma Shamuhuna akipitia Hati ya kiapo kabla ya kuaza kwa hafla hiyo.(Picha na Ikulu)
WAKUU wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Mkuu Mpya wa Kikosi cha Valantia Zanzibar KVZ Major Said Ali Juma Shamuhuna, hafla hiyo imefanyila leo Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)
MAKAMU wac Pili wa Rais wa Zanziubar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Bara la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zuberi Ali Maulid na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe. Said Hassan Said na Viongozi wengine wa Sereikali wakihudhuria hafla ya kuapishwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia Zanzibar KVZ Major Said Ali Juma Shamuhuna, hafla hiyo imefanyika leo 21-6-2019 Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)

ZIWA NATRON KUPANDISHWA HADHI KUWA PORI LA AKIBA

$
0
0

 Wajumbe wa Bodi ya TAWA wakiangalia baadhi ya viumbe na Samaki aina ya Alcolapia wanaopatikana Ziwa Natron RAMSAR SITE lilipo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.
Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Dk. James Wakibara akijambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jeneral Mstaafu Hamis Semfuko, Bodi hiyo ilitembelea eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.
 Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Frank Mwaisumbe mwenye (Kaunda suti) akiwa na Wajumbe wa Bodi ya TAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko kulia. Bodi hiyo ilitembelea eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori la Akiba.

 Muikolojia wa eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE John Sule akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko kushoto, wajumbe wa bodi hiyo wametembelea eneo hilo linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori Tengefu ili kuliongezea thamani ya kiutalii. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko akiruka maji kwenye eneo chepechep la Ziwa Natron RAMSAR SITE lilipo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha, linalotarajiwa kupandishwa hadhi kuwa Pori Tengefu.

Na Ripota Wetu, ARUSHA

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imejipanga kulipandisha hadhi eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE kutoka aneo la ardhi owevu na kuwa eneo maalumu la Uhifadhi.

Hatua hiyo imelenga kunusuru hatari ya kutoweka kwa ndege maarufu duniani aina ya flamingo kutokana na shughuli mbalimbali za kibinaadamu zinazoendelea kufanywa pembezoni mwa Ziwa hilo.

Bodi ya TAWA ikiongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali Mstaafu Hamis Semfuko imetembelea eneo hilo na kujionea hali halisi ya mazingira na maisha ya viumbe hai wanaopatikana eneo hilo maarufu duniani.

Eneo hilo ni maarufu duniani kwa kuwa na makazi Heroe wadogo kwa asilimia 100 wanaopatikana Afrika Mashariki na mazalia ya asilimia 80 ya Heroe wadogo wanaopatikana eneo hilo pamoja na aina tatu ya za Samaki aina ya Alcolapia.

Aidha eneo la Ziwa Natron RAMSAR SITE pia limekuwa muhimu kwa utalii wa ndege aina ya Heroe Afrika Mashariki.



WATOTO 7,935 KUPATA MATONE YA VITAMIN A

$
0
0

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Omary Sukari akitoa matone ya Vitamini A kwa mtoto 
Watumishi wa halmashauri wakitumia usafiri wa pikipiki katika kufuatilia zoezi la chanjo linavyoendelea katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma

Baadhi ya watoto waliofika kupata chanjo katika zahanati ya kijiji cha Kikonko katika halmashauri ya Mpimbwe 
Baadhi ya kinamama na watoto wao wakisubiri chanjo katika zahanati ya Kikonko 
********************* 

21.06.2019 

Na Mwandishi wetu, Katavi 

Jumla ya watoto 7,935 wa Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi watarajiwa kupata matone ya Vitamini A na dawa za minyoo katika zoezi la utoaji chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano linatalotarajiwa kukamilika juni 30 mwaka huu 

Akizungumzia zoezi hilo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe dk. Sebastian Siwale amesema zoezi hilo litahusisha vituo 15 vya kutolea huduma za afya katika halmashauri hiyo 

Aidha ameongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto ya uchache wa vyombo vya usafiri hali inayopelekea wakati mwingine kushindwa kufuatilia kwa karibu jinsi zoezi hilo linavyoendelea katika vituo mbalimbali 

“Tuna gari moja kwahiyo inapotokea kuna mgonjwa inabidi atumie gari hilo kupelekwa hospitali na ufuatiliaji unaahirishwa mpaka gari litakaporejea” alisema dk. Siwale 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi dk. Omary Sukari ambaye alikuwa ameambatana na kamati ya usimamizi wa huduma za afya mkoa wameshiriki katika zoezi hilo ambapo amesisitiza umuhimu wa watoto kupata chanjo 

Dk Sukari amesema matone ya Vitamin A yanasaidia kinga ya mwili wa mtoto dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumwezesha mtoto kuona vizuri .Pia ametoa wito kwa wazazi waliowafikisha watoto wao kupata chanjo kuwa mabalozi wazuri kwa majirani zao ili watoto waote wapate chanjo hiyo 

Nao baadhi ya kinamama waliokutwa katika vituo vya kutolea huduma ya afya wameeleza umuhimu wa chanjo hiyo ikiwa ni pamoja na kumpa mtoto kutibu minyoo inayoshambulia katika tumbo la mtoto

SERIKALI YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUWASILISHA KERO ZAO.

$
0
0
SERIKALI imewataka wafanyabiashara kuwasilisha kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi badala ya kubaki wakinung’unika kwani hazitatatuliwa na lengo ni kuwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru ili waweze kulipa kodi.

Kauli hiyo imetolewa Juni 20 na mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro,kwenye kikao cha pamoja cha siku moja cha wafanyabiashara,mamlaka ya mapato,halmashauri ya jiji pamoja na taasisi zingine za serikali wilayani Arusha kilichofanyika ukumbi wa Katibu tawala mkoa kwa ajili ya kusikiliza kero zao.

Daqarrop,amesema wapo baadhi ya wafanyabiashara wana kero zao lakini hawako tayari kuziwasilisha TRA kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi badala yake wamekuwa wakinung’unika hivyo wahakikishe wanaziwasilisha TRA ili waweze kukaa pamoja na kuzipatia ufumbuzi.

Kuhusu maegesho yasiyo sahihi(wrongparking)mkuu wa wilaya,amesema utaratibu wa kufunga cheni kwenye magari yaliyoegeshwa unaofanywa na Longparking, ni uhuni huwa wanavizia magari na kuyafunga cheni kwa lengo la kujipatia rushwa baada ya majadiliano na mwenyegari na fedha wanazolipwa huwa hazipelekwi kunakotakiwa.

Ameiagiza wakala wa bara bara Vijijini Tarura, kuiondoa wakala wa Long parking ,kuanzia Juni 21 eneo hilo kwa kuwa imekuwa ni kero na vikwazo kwa wafanyabiashara na wateja wao akawashauri wenye magari wakiombwa fedha wasitoe bali wampigie simu kwani ni wasumbufu wanalazimisha rushwa .

Kikao kimeagiza magari yaegeshwe kwenye eneo hilo kuanzia makutano ya bara bara ya Masijid Kubha na mpaka Miami beachi hotel na yalipe ushuru wa kawaida ili halmashauri ipate mapato yake kupitia kwa wakal wake.

Kwa upande wao wamiliki wa maduka ya rejareja jijini Arusha wameiomba serikali kuwatafutia Machinga maeneo ya kufanyia shughuli zao kutokana na kodi wanazolipa wakati Machinga hawalipi hivyo wanashindwa kufanya biashara .

Kwenye kikao hicho cha pamoja na wamiliki wa maduka wamesema kuwa wenye maduka wanalipa kodi mbalimbali lakini mbele ya maduka yao Machinga nao wanaweka bidhaa zao hivyo wakaiomba serikali kuwatafutia maeneo mengine .

Mwenyekiti wa wafanyabiashara stand ndogo Joan Minja, pia wamelalamikia Wakala wa maegesho ya magari maarufu (wrongparking) kuwa ni kero wanawakosesha wateja wanaoenda kununua bidhaa kwenye maduka yao.

Minja,amesema utaratibu unaotumiwa na maegesho yasiyo sahihi ni kuwatoza faini ya shilingi 50,000 watu wanaoegesha magari hayo na kuingia ndani ya stand hiyo kwa kisingizio cha maegesho hayo kero na usumbufu unazosababisha kukosa wateja.

Mamlaka ya mapato TRA,mkoa wa Arusha ,imesema itafanyakazi hata siku za mapumziko na siku kuu wakati wa kupokea retun za VAT kutoka kwa wafanyabiashara.

Meneja wa TRA Faustini Mdesa, ameyasema hayo alipokuwa akitolea ufafanuzi hoja za wafanyabiashara ikiwemo kulalama kurejesha retun za VAT siku ambazo sio za kazi lengo ni kuwahudumia walipa kodi.

Akawaonya wafanyabiashara kutokufanya udanganyifu kwenye taarifa za biashara zao kwa kufanya hivyo ni kuikosesha mapato serikali hivyo ambao watagundulika kuwasilisha taarifa zisizo sahihi TRA itawarejea kufanya upya ukaguzi wa hesabu .

Amesema kuwa lengo la TRA ni kuwakuza wafanyabiashara na sio kuwadidimiza hivyo wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni waende TRA ili kutafuta ufumbuzi wa kulipa madeni yao.

Mdesa,ameema TRA inatoa motisha kwa mwananchi yeyote atakaewezesha kutoa taarifa za kukamatwa kwa wakwepa kodi ,ambapo motisha hiyo itatoa asilimia 3% ya bidhaa itakayokamatwa na kuuzwa kutokana na ukwepaji kodi au shilingi milioni 20 .

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya ya Arusha Adolf Lokeni ,amesema mkutano wa rais Magufuli na wafanyabiashara hivi karibuni uliofanyika Ikulu, umezaa matunda na akawasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi.

Amesema ni kweli wapo baadhi ya wafanyabiasha wana malimbikizo ya kodi na wengine hali zao za kibiashara ni mbaya hivyo akaiomba mamlaka ya mapato TRA mkoa wa Arusha kukaa nao ili wajenge mazingira rafiki yatakayowezesha kulipwa kodi na malimbikizo yaliyopo.

Aidha ,Lokeni, ameitaka halmashauri ya jiji kutokuwafungia wafanyabiashara kuna maduka 50 yamefungwa wiki iliyopita stand ndogo kwa sababu wanadaiwa na akasema rais akishatoa maelekezo hakutoa kwa TRA pekee bali na mamlaka zingine zikiwemo halmashauri kutokufunga biashara.
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro.

ATHARI YA UTANDAWAZI NA SIASA YA TANZANIA NA MAENDELEO YAKE (SEHEMU YA KWANZA).

$
0
0
Rais wa Jamhuri ua Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli

UTANGULIZI 

HIVI karibuni, kumekuwa na mfumko mkubwa wa wananchi kuwa na hamu ya kuijua siasa ya nchi yao nchini Tanzania. Hamu hii imetokana na 
matukio mbalimbali ya mabadiliko yaliyoletwa na kimbunga cha serikali
ya awamu ya tano ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli katika sekta 
mbalimbali ikiwemo maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo
yamewagusa wananchi wengi. 

Kutokana na mabadiliko haya nchini, wananchi wengi wamebaki kujiuliza ni nini kinachoendelea nchini, tupo wapi, tunatoka wapi na tunaelekea wapi. Wakati huohuo, wazee kwa vijana, wanalalamika mmomonyoko wa maadili katika jamii, uchumi ‘kukaza kwa vyuma’ na hali ya kisiasa nchini.

Kwa hivyo, ni vyema kwa wanafunzi, walimu, na wananchi ambao siyo wanasiasa na wanasiasa kwa ujumla wao – kujikumbusha itikadi zao za kisiasa zinazowaongoza ili waweze kubaini na kupambanua mambo yanayowagusa katika jamii zao nakatika uchumi wa taifa lao kutokana na itikadi za siasa. 

Makala hii nimeigawa sehemu tatu: sehemu ya kwanza nitafafanua na
kudadavua maana ya itikadi ya siasa; sehemu ya pili nitaelezea itikadi 
za vyama vya siasa vilivyomo nchini na vyama vinavyofuata itikadi
hizo; na sehemu ya tatu nayo nimeigawa katika sehemu tatu kwenye kila 
itikadi ya siasa: nitachambua na kudadavua mtazamo wa uchumi, siasa na
jamii. 

Madhumuni ni kutoa mchango wangu kwa taifa, na siyo kwa nia ya
kukebehi wengine wenye elimu zaidi yangu au wasio na elimu. Mheshimiwa 
Rais John Pombe Magufuli amesema: “Definition ya mtu aliyepata
education, ni yule aliyepata education… iwe ni formal au informal, 
akaitumia kwenye different environment, ku-solve matatizo ya pale“
(Magufuli, 2019). Nami nitaendelea kujielimisha ‘kwa kadiri ya uwezo 
wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote’.


Matarajio ni kwamba mwisho wa makala hii, wananchi wataelewa na wataweza kupambanua  tofauti za itikadi za kisiasa na mambo yanayohusu siasa kwa kutumialenzi ya itikadi za siasa. Na hatimaye, wananchi wa kawaida, viongozi, walimu na wanafunzi ambao ndiyo taifa la kesho wataendelea kufanyamaamuzi sahihi katika kuisaidia nchi na kuisaidia jamii iliyowazunguka. “…bila ya kuwa na mtazamo sahihi, taasisi zinaweza kupotezwa muelekeo wa madhumuni yake ya kweli”. Mwalimu Nyerere, 1968 

ITIKADI ZA KISIASA

Neno ‘itikadi’, limetokana na mwanazuoni wa Kifaransa aliyetambulika
kwa jina la Antoine Destutt de Tracy (1754-1836), ambaye mwishoni mwa 
karne ya 18 mpaka mwanzoni mwa karne ya 19 alikuwa akifanya utafiti wa
kutaka kujua chanzo cha ‘fikra’ za watu katika maisha yao. 

Yaani, kwanini watu wanakuwa na mawazo ya kufanya maamuzi juu ya mambo mbalimbali. Na hapo ndipo neno ideology (itikadi) lilipozaliwa. Kwa
maana hiyo, neno itikadi (ideology) linamaanisha kuwa ni somo la 
kisayansi linalosomea mawazo (ya kifikra) ya watu (Ball & Dagger,
1991, uk. 4). 

Ufafanuzi wa neno itikadi kama linavyofafanuliwa na bwana Ball &
Dagger (1991), linamaanisha kuwa ni mawazo na fikra ambayo yanaelezea 
na yanatathmini hali ya kijamii, na kuisaidia jamii ijitambue ilipo na
kuipangia mpango bora wa utekelezaji wa sera za kijamii na za kisiasa: 
“An ideology is a… set of ideas that explains and evaluates social
conditions, helps people understand their place in society, and 
provides a program for social and political action.” (Ball & Dagger,
1991, uk. 8). 

Kwa maana hiyo, itikadi ni mkusanyiko wa mawazo ya kifikra
yanayotokana na imani ya dhati inayoitazama hali ya kijamii ilivyo na 
jinsi inavyotakiwa iwe kwa kutoa muongozo na muelekeo maalum wa
kisiasa na wa kijamii ili kufikia malengo ya kuiona jamii hiyo 
inavyotakiwa iwe katika hali zao za kimaisha. Muongozo na muelekeo huo
ndiyo unaotengeneza itikadi ya watu, na itikadi ya watu ndiyo inawapa 
watu muongozo na muelekeo wa kuufuata.

Itikadi zinaweza kufanya watu wawe wamoja na itikadi zinaweza kuwagawa
watu katika makundi. Tofauti za kiitikadi zinaweza kuleta madhara na 
pia zinaweza kuleta umoja, upendo, mshikamano na amani.

Kwa kuwa sera za itikadi zinachukua hatua za kuifanyia kazi jamii, na kwa kuwa itikadi mbalimbali zinatofautiana kifikra, siyo ajabu tukiona itikadi
zikigongana mara kwa mara na hata mara nyingine hupelekea mpaka watu 
wanaotoka sehemu moja au wa taifa moja kufanyiana uhasama, fitna,
chuki na uadui. 

Sifa za uhasama, fitna, chuki na uadui zikitumika kama
ndiyo nyenzo katika kujenga jamii, jamii hiyo itakuja kuchuma 
ilichokipanda. Kwasababu sifa hizo zitajifinyanga kwenye itikadi zao.

Kuijenga jamii iliyogawika na kuiweka kwenye jamii yenye umoja,
upendo, mshikamano na amani, inategemea sana msingi wa historia ya 
watu walipotoka na siyo historia ya machimbuko ya pale walipogawanyika
kifikra. Taifa letu lipo njia panda. Ni muhimu kufanya maamuzi sahihi 
ya kuamua wapi tunataka kwenda kwa kuangalia itikadi ipi itaweza
kutufikisha huko kama taifa – na kwa kuangalia wapi tulipo na wapi 
tunatoka.

Kwa mfano, Tanzania msingi wa historia yake ni nchi ya
itikadi ya ujamaa. Hapa tulipo taifa letu la Tanzania limegawika 
katika itikadi za kisiasa kuu tatu tangu kuanzishwa kwa siasa ya vyama
vingi mwaka 1992 – baada ya kuingiliwa na sera za kimagharibi miaka ya 
‘80.

Zaidi ya miaka ishirini imepita tangu siasa ya vyama vingi ianze. Watu
wa nchi yetu wamekuwa bado wapo katika hali duni, na usawa wa kipato 
unazidi kudidimia. Hii ukitoa miaka ya serikali ya awamu ya tano ya
Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ambaye bado hajatimiza hata miaka minne madarakani.

Na ninamaanisha kwamba athari za sera za kimagharibi
zilizoingia miaka ya ‘80 ndizo zilizoathiri awamu zilizopita kuanzia 
awamu ya Alhajj Ali Hassan Mwinyi rais wa awamu ya pili, Mheshimiwa
Benjamin Mkapa rais wa awamu ya tatu na Mheshimiwa Jakaya Mrisho 
Kikwete rais wa awamu ya nne.

Halikadhalika, simaanishi kwamba matokeo
ya watu wetu wengi kuendelea kuwa na hali duni yametokana na viongozi 
wetu waliopita, bali namaanisha kwamba yametokana na sera za
kimagharibi ambazo ‘kwa upande mwingine’ tunaweza kusema zilikuwa nje 
ya uwezo wao kuzikabili. Tutakuja kuona huko mbele tunamaanisha nini.

Siamini kwamba taifa kuwa na vyama vingi ndiyo maendeleo ya nchi. Kuna
baadhi ya nchi barani Afrika zina vyama zaidi ya hamsini kwenye nchi 
moja lakini watu wetu katika bara la Afrika ndiyo kwanza wanaendelea
kuwa maskini na hata matarajio ya kuwa na mustakbali wa ustawi ni 
mdogo sana.

Pamoja na hayo, mara kwa mara hutokea matukio ya
changamoto ya vyama kwa kupoteza malengo ya maendeleo ya miradi ya 
wananchi, kupiga majungu, na kuwa na mdomo mpana – kuliko muda huo
kutumika kwenye kuleta ustawi na maendeleo ya nchi na wananchi. 

Kwa upande mwingine, ukiangalia nchi mfano wa Marekani (USA) tangu
ipate uhuru wake zaidi ya miaka mia mbili iliyopita mpaka hii leo 
imeendeshwa na vyama viwili tu (Republicans na Democrats).
Halikadhalika, nchi ya China tangu ijipatie uhuru wake takriban miaka 
sabini iliyopita mpaka hii leo imejiendesha yenyewe mpaka kufikia
malengo yake ya kimaendeleo kwa kupitia chama kimoja tu (Communist 
Party of China).

Hii leo, nchi mbili hizi ndiyo nchi katika nchi
tajiri duniani, na ndiyo nchi katika nchi zenye nguvu duniani. Ingawa 
ufafanuzi wa neno ‘maendeleo’ baina ya nchi na nchi unaweza
ukatofautiana, lakini hatuwezi kusema kwamba hawajapiga hatua kubwa 
sana duniani pamoja na kuwa na vyama vichache au chama kimoja katika
kufikia malengo yao ya maendeleo. 

Na la zaidi, vyama vya kisiasa vya
nchi zote hizi mbili, Marekani na China, vina itikadi mbili tofauti, 
na kijiografia nchi zao zipo katika pande mbili tofauti za dunia,
lakini zote zimeweza kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Kwa maelezo 
haya nakusudia kusema kwamba, kuwa na vyama vingi siyo hoja. Hoja ni
kujitambua wapi tulipo, wapi tunatoka, wapi tunataka kuelekea, na 
‘itikadi’ ipi itakayotuwezesha kufika huko kama taifa.

Kutokana na ufafanuzi wa neno itikadi hapo juu, tumeona kwamba ili
jamii iweze kujitambua wapi inaelekea, lazima itambue inafuata itikadi 
ipi katika kufikia maendeleo yake. Itikadi ni imani, na itikadi ni
msingi wa maendeleo, bila ya kuwa na msingi madhubuti wa itikadi jamii 
yetu itayumba, na kuyumba kwa jamii “…nchi yetu itayumba” (Nyerere,
1990). 

Kwa mfano, chama cha siasa, hakiwezi kuwa chama madhubuti iwapo
msingi wake ni itikadi ya kijamaa kisha kiwe kinatekeleza sera za 
itikadi ya kiliberali. Halikadhalika, chama chenye kufuata itikadi ya
kiliberali hakiwezi kuwa madhubuti iwapo msingi wake ni itikadi ya 
kiliberali kisha kigeuke kiwe kinatekeleza sera za itikadi ya kijamaa.

Itikadi ni roho ya chama, itikadi ni chombo cha safari, lakini pia 
itikadi ni mfano wa moyo, bila ya kuwa na moyo wenye afya madhubuti,
mwili utakumbwa na maradhi ya mara kwa mara. Chama cha siasa na 
uongozi wa chama cha siasa hauwezi kuwa na itikadi mbili kwa wakati
mmoja. Waswahili wamesema “Mwenda tezi na omo, marejeo ngamani”. 

Itikadi ya kisiasa haiendeshwi kwa muongozo wa nje ya itikadi yenyewe.
Chama au nchi isiyofuata itikadi inaweza ikaelekea pabaya. Wanasayansi 
bwana Ball & Dagger (1991) kwenye maandishi yao wamesema, kama
tunataka kutenda mambo yetu kwa ufanisi na kuishi kwa amani, lazima 
tujue maana ya itikadi za kisiasa ambazo zimetushawishi sisi na
zimeshawishi wengine fikra zao na matendo yao: “If we wish to act 
effectively and live peacefully, then, we need to know something about
the political ideologies that have influenced so profoundly our own 
and other people’s political attitudes and actions” (Ball & Dagger,
1991, uk. 3). 

Siasa ni sayansi: ni njia ya kufikia malengo. Siasa siyo sayansi ya
moja na moja ni mbili. Siasa ni kukabiliana na hali na changamoto za 
kila siku zinazojitokeza ambazo za jana huwa siyo sawa na za leo
katika masuala ya wananchi na taifa. Siasa ni kupinduka na siyo 
kupindukia.

Chama cha siasa na uongozi wa chama cha siasa hauwezi
ukalala leo na imani ya itikadi moja, kisha kesho kuamka na itikadi 
nyingine. Kwasababu hatari yake ni kwamba hatujui kesho kutwa wataamka
na itikadi ipi. Na hii siyo afya kwa uongozi wa nchi na siyo afya kwa 
wananchi wanaoongozwa.

Ni muhimu kuwa wawazi katika maslahi ya taifa ili tuweze kusaidiana
kama watu wa taifa moja. Kwasababu sisi Watanzania kiasili tunapendana 
kama ndugu na tunalipenda taifa letu. Mheshimiwa Rais Magufuli (2018)
kwenye hotuba yake alipokuwa jijini Mwanza katika utiaji wa saini wa 
mkataba wa meli mpya, chelezo na ukarabati wa meli ya MV BUTIAMA na MV
VICTORIA, alisema: “…tunatakiwa tuzivae challenge …kwa wakati huu 
nitawaambia ukweli …na ukweli saa nyingine unauma, lakini baadaye
ukweli hufurahisha” (Magufuli, 2018). 

Pamoja na kuwepo kwa itikadi mbalimbali za kisiasa duniani, lakini
itikadi kuu tatu ndiyo zinazotawala dunia hivi sasa: Ujamaa 
(Socialism), Uliberali (Liberalism), na Uhafidhina (Conservatism).
Katika sehemu hii ya makala, tutaangalia kwa kuchambua, kudadavua na 
kukosoa hitilafu za itikadi za vyama vya siasa viliopo nchini. Vyama
vinavyofuata itikadi hizo ni kama ifuatavyo: 

Chama cha CUF, kinafuata itikadi ya Uliberali (Liberalism);
Chama cha CHADEMA, kinafuata itikadi ya Uhafidhina (Conservatism); 
Chama Cha Mapinduzi (CCM), NCCR na ACT, vinafuata itikadi ya Ujamaa (Socialism).

“Msipotambua historia yenu, mtaingiliwa na wanafiki, waongo,
watawapoteza muelekeo – mwenye kusikia na asikie”. Rais John Pombe Magufuli, 2019 


Imeandikwa na: 

Saleh J. Katundu

20/06/2019

Itaendelea…

HABARI- MAHAKAMA YATUPILIA MBALI KESI YA MBOWE NA WENZAKE

$
0
0

Na Dennis Buyekwa


Mahakama ya Afrika ya Mashariki imetupilia mbali maombi ya dharura katika Shauri namba 2 la mwaka 2019 lililofunguliwa na Viongozi waandamizi wa vyama vya siasa vya upinzani nchini katika Mahakama hiyo iliyopo jijini Arusha.


 Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya upande wa walalamikaji kumuomba Jaji anayesikiliza kesi hiyo Mhe. Monica Mungenyi kusikiliza upande mmoja wa walalamikaji kitendo kilichopingwa na mawakili wa Serikali.



Baada ya kusikiliza shauri hilo kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa na upande wa waleta maombi, Jopo la waheshimiwa Majaji liliamua kutupilia mbali shauri hilo kwa kile walichokieleza kuwa upande wa waleta maombi wameshindwa kuthibitisha kwa Mahakama hiyo umuhimu wa kusikiliza shauri upande mmoja kwani masuala yaliyopo katika shauri hilo ni muhimu hivyo ili haki itendeke ni vyema upande wa pili usikilizwe ndipo Mahakama itoe maamuzi.


Kesi hiyo iliyosikilizwa na Majaji watano wa Mahakama hiyo ambao ni Mhe. Jaji Monica Mugenyi, Mhe Jaji Faustine Ntezyilyayo, Mhe Jaji Fakihi Jundu, Mhe. Jaji Audace Ngiye, na Mhe. Jaji Charles Nyachae, ilifunguliwa na viongozi wa vyama vya siasa wakiongozwa na Mhe. Freeman Mbowe, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe, Mhe.Hashimu Rungwe, Mhe.Seif Sharif Hamad na Mhe.Salum Mwalim kupinga utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019.


Kufuatia hatua hiyo waheshimiwa Majaji wameutaka upande wa waleta maombi kuipatia nakala ya maombi hayo Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ili kujibu, na tarehe ya kusikiliza maombi hayo itapangwa hapo baadae.


Katika shauri hilo upande wa Serikali uliwakilishwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kupitia Mawakili wa Serikali Ndg. Evarist M. Mashiba, na Bw. Kombe wakati upande wa Mashtaka uliwakilishwa na Bi. Fatma Karume, Bw. Jebra Kambole na Ndg, John Malya.

Wakili Mkuu wa Serikali


MBUNGE KOKA AUNGA MKONO UJENZI WA MAKAZI YA ASKARI POLISI PWANI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

MBUNGE wa jimbo la Mji wa Kibaha,mkoani Pwani Silvestry Koka amechangia malumali zenye thamani ya sh.milioni mbili kwa jeshi la polisi mkoani hapo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kujenga makazi ya askari polisi.

Akikabidhi malumalu hizo kwa kamanda wa polisi mkoni humo ,Wankyo Nyigesa ,Mbunge Koka alipongeza serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa makazi hayo ya askari.

Alisema askari wanafanya kubwa lakini makazi yao ni duni na mradi huo una manufaa na ni ukombozi kwao.
 
Koka alieleza ameamua kulisaidia jeshi hilo ili kukamilisha ujenzi huo ambapo Rais Dk John Magufuli alilipatia jeshi hilo mkoa kasi cha shilingi milioni 500.

"Tujitoleeni katika miradi kama hii,kutoa ni moyo ili kushirikiana na serikali kutimiza malengo yake na kufikia uchumi wa kati"alifafanua .

Nae Kamanda wa  Polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa  alimshukuru Mbunge huyo.

Alisema askari wengi hawana nyumba za kuishi  hivyo kulazimika kuishi uraiani ambapo inakuwa ngumu kuwapata pale inapotokea dharura ya kikazi.


WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi Utawala wa Wizara ya Katiba na Sheria Edith Simtengu (mwenye kofia) akiongoza watumishi wa Wizara hiyo kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2019.
 Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakifanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2019.
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2019.

TRA YAENDESHA SEMINA KWA MAKAMPUNI YA WATEMBEZA WATALII ZANZIBAR

$
0
0
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Ofisi ya Zanzibar imezitaka Kampuni za utembezaji Watalii Zanzibar kusajili Kampuni zao na kulipa Kodi kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. Kwa kufanya hivyo kutawarahisishia kufanya kazi zao na kuwaondoshea usumbufu ikiwemo kulipa faini ya kuchelewesha Kodi hizo.

Wito huo umetolewa na Afisa mwandamizi Elimu ya mlipa kodi TRA Shuweikha S. Khalfan wakati akiwasilisha mada katika Semina ya utozaji wa Kodi na uwasilishaji wa Taarifa za Mapato kwa Kampuni za utembezaji Watalii Zanzibar iliyofanyika Raha leo mjini Zanzibar.

Amesema Sheria ya Kodi ya mapato ya mwaka 2004 ibara 4(1) inamtaka kila mtu ambaye anapata kipato kulipa kodi kwa mujibu wa sheria. Amesema lengo la Semina hiyo ni kuendelea kutoa elimu kwa kila kundi ambalo lina wajibu wa kulipa Kodi ili kuziba mianya ya upoteaji wa mapato nchini.

Shuweikha amesema TRA inategemea sana wafanyabiashara katika kufanikisha malengo yaliyowekwa ili kuindeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na huduma za kijamii nchini.

Wakichangia katika Semina hiyo Wawakilishi wa Kampuni hizo waliiomba TRA kufanya utafiti wa kina kubaini mapato wanayoingiza kabla ya maamuzi ya kutakiwa kulipa Kodi.

“Hakuna ambaye anakataa kulipa Kodi lakini lazima TRA wafanye Research ya kina hasa maeneo tunayofanyia kazi ili wabaini kipato chetu maana ukweli biashara ya kutembeza watalii imekuwa ngumu sana” Alisema Mwakilishi wa Kampuni ya Coral Tour Khamis Makame

Khamis amesema Kampuni za kuendesha utalii zinapitia wakati mgumu hivyo ni vyema kuwe na mikutano ya kuelimishana mara kwa mara kwa lengo la kuongeza uelewa kwa wadau.

“Tunahitaji pia kila mtu kujua Kampuni yake inanufaika vipi na Kodi inayoitoa hasa ikizingatiwa kuwa Kampuni inaweza kupita hata miezi sita bila hata kupata mgeni wa kufanya naye kazi” Alisema Khamis.

Kwa upande wake Salim Salim amesema biashara hiyo imekuwa ngumu kutokana na kuwepo kwa Tozo nyingi zinazotolewa bila kuangalia kipato halisi wanachoingiza kwa mwaka.

Hivyo alishauri Semina zinazofuata TRA wawashirikishe Wadau wengine wa Kodi kama vile ZRB na Halmashauri ili kuwa na msimamo wa pamoja kuhusu ulipaji wa Kodi.

Kwa upande wake Afisa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka TRA Abd Seif amesema maoni yaliyotolewa yatafanyiwa kazi ili kuhakikisha Makampuni hayo ya kiutalii yanashirikiana vyema kulipa kodi bila tatizo. Amesema wataendelea kutoa elimu kwa makundi yote ili kuziba mianya ya ulipaji Kodi nchini.
 Afisa Elimu ya mlipa kodi TRA Ofisi ya Zanzibar Abdallah Seif akionesha Kitabu cha Makadirio ya Bajet ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka 2019-20 kwa washiriki wa Semina iliyohusu utozaji wa Kodi na uwasilishaji waTaarifa za Mapato kwa Kampuni za utembezaji Watalii Zanzibar iliyofanyika Raha leo mjini Zanzibar. Kulia ni Afisa mwandamizi Elimu ya mlipa kodi TRA Shuweikha S. Khalfan.
 Mmoja wa wawakilishi wa Kampuni za utembezaji Watalii Zanzibar Salim Salim akihangia katika Semina iliyoendeshwa na TRA Ofisi ya Zanzibar huko Raha leo mjini Zanzibar kuhusu utozaji wa Kodi na uwasilishaji waTaarifa za Mapato kwa Kampuni za utembezaji Watalii Zanzibar.
Mwakilishi wa Kampuni ya Coral Tour Khamis Makame akichangia katika Semina ya utozaji wa Kodi na uwasilishaji wa Taarifa za Mapato kwa Kampuni za utembezaji Watalii Zanzibar iliyofanyika Raha leo mjini Zanzibar.

ZANZIBAR YAPIGA HATUA KWENYE KUDHIBITI MAAMBUKIZO YA VIRUSI

$
0
0
Zanzibar imepiga hatua katika kudhibiti maambukizo ya virusi vinavyosababisha kutokana na takwimu zinazoonesha mambukizi ya virusi hivyo kuwa chini ya asilimia moja (1%) ambapo kwa upande wa unguja ni 0.5% wakati kisiwa cha pemba kufikia 0.2%.

Mkurugenzi Mtendaji wa tume ya Ukimwi Zanzibar Dk. Ahmed Momahed Khatib alieleza hayo katika ziara ya kushtukiza iliofanywa na katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed kupitia Idara mbali mbali zilizo chini ya Ofisi hiyo.

Dk. Ahmed alisema Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2016/2017 ambapo kwa sasa tume hiyo bado inaendelea na jukumu la kutoa elimu kwa wananchi dhidi ya hatua za kuchukua katika kujikinga na virusi vinavyosababisha maradhi hayo.

Alifafanua kuwa kwa sasa bajeti ya tume hiyo imefanikiwa kutegemea bajeti ya ndani kwa asilimia kubwa kutokana na serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuongeza nguvu katika bajeti ya tume hiyo kila mwaka mpya wa fedha hali iliyopelekea kupunguza kutegemea Mataifa na Taasisi wahisani.

Nae Afisa kitengo cha sera , mipango na mwiitiko wa kijamii wa tume hiyo Bibi Jogha Bakari Mohamed alisema uwepo wa changamoto ya wananchi wengi nchini hususani vijana kwa kulichukulia tatizo la maambukizi ya ukimwi kama jambo la kawaida na kufanya mambo yao bila ya kujali kuchukua tahadhari yoyote jambo linalopelekea kuenea kwa maambukizi.

Mkuu huyo wa kitengo alisema ni jambo linalosikitisha kuona kesi mpya nyingi zinawahusu vijana wengi wanaoripotiwa kuwepo katika hali hatarishi inayosikitisha na kuhuzunisha ikizingatiwa kuwa wao ndio nguvu kazi na tegemeo la Taifa katika masuala ya Maendeleo ya nchi.

Katika ziara hiyo ya kushtukiza watendaji wa tume ya ukimwi walipata fursa ya kuelezea faraja yao pamoja na changamoto zinazowakabili kwa Katibu Mkuu ikiwemo changamoto ya kuchelewa kukamilika kwa mfumo maalum wa kutunzia kumbukumbu zao. {Data Base System}.

Wakati huo huo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizitembelea ofisi za idara ya watu wenye ulemavu na kumtaka mkurugenzi wa idara hiyo kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa mujibu wa mahitaji yao ambao wanatarajiwa kupangwa katika ofisi za wilaya.

Nd. Mkuu Shaaban amewaeleza watendaji wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa uwadilifu kwa kuzitunza vyema nyaraka za ofisi zao sambamba na kuziwasilisha barua zinazoingia idarani mwao kwa wakati badala ya kusubiri mrindikano wa barua hizo, kwani kufanya hivyo kutasaidia mambo muhimu na ya msingi kuchukuliwa hatua bila ya kuchelewa.

Pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Shaaban amelezea kukerwa kwakwe na mpangilio mbaya ya utunzaji wa baadhi ya kumbukumbu na nyaraka katika idara ya watu wenye ulemavu na kuagiza hatua za haraka kuchukuliwa ili kuzinusuru nyaraka hizo kupotea.

Mapema Katibu Mkuu akibadilishana mawazo na watendaji wa tume ya uchaguzi Zanzibar wakimueleza kuwa kwa sasa tume ipo katika mchakato wa kuimarisha kitengo chake cha mfumo wa teknolojia kwa ajili ya kukamilisha zoezi la usajili linalotarajia kuanza hivi karibuni.

Watendaji hao walimueleza katibu mkuu uwepo wa changamoto kwa wapiga kura wengi kutokana na kutokuwa na elimu ya upigaji kura ingawaje tume ya uchaguzi inaendelea na utowaji wa elimu hiyo hali inayosababishwa na ukubwa wa Maeneo ya Zanzibar ikilinganishwa na idadi ya watendaji wa tume hiyo.

Ziara hiyo ya kushtukiza ya Katibu Mkuu imejumuisha tume ya ukimwi Zanzibar, Idara ya watu wenye ulemavu pamoja na tume ya uchaguzi ziara ambayo ina lenga kuimarisha utendaji kazi wa idara zilizo chini ya ofisi ya makamu wa Pili wa Rais.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif Mohamed akizungumza na Wafanyakazi wa Idara ya Watu wenye ulemavu katika ziara ya kushtukizia.
 Mkurugenzi wa Idara ya Watu wenye ulemavu Abeda Rashid Abdulla akimuelezea Nd. Shaaban majukumu ya Idara hiyo lipofanya ziara ya kushtukizia.
 Mkuu wa Utawala wa Tume ya Uchaguzi Nd. Saadon Ahmed Khamis akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Shaaban Seif.
 Katibu Mkuu Shaaban akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Nd. Thabit Idarous Faina alipotembelea Ofisi hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa tume ya Ukimwi Zanzibar Dk. Ahmed Momahed Khatib akimueleze Katibu Mkuu Shaaban hali halisi ya Ukimwi ilivyo Zanzibar.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Tume ya Ukimwi Zanzibar wakimsikiliza Katibu Mkuu wakatialipofanya ziara ya Ghafla kwenye Ofisi yao.
 Mtendaji wa Tume ya Ukimwi Zanzibar akimuelezea Ndugu Shaaban changamoto wanazopambana nazo katika kuwapatia elimu Wananchi hasa Vijana.
Nd. Shaaban akisisitiza umuhimu wa kutunzwa kumbukumbu alipozungumza na Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofiosi yake. Picha na – OMPR – ZNZ.

RAIA WA NIGERIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30 BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA YA KUSAFIRISHA PIPI 56 ZA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi, maarufu kama mahakama ya mafisadi imemuhukumu raia wa Nigeria Christian Ugbechi (28) kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha pipi 56 za dawa za kulevya aina ya heroin hydrochloride.
Hukumu hiyo, imesomwa leo, Juni 21,2019 na Jaji Sirrilius Matupa ambae amesema upande wa mashitaka katika kesi hiyo umeweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kupitia mashahidi wake 11 na vielelezo 22 waliofika mahakamani hapo kuthibitisha mashitaka hayo, kuwa mshitakiwa ametenda kosa hilo.
Aidha Mahakama imeamuru dawa za kulevya alizokutwa nazo mshtakiwa ziteketezwe kwa mujibu wa sheria.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Matupa amesema Mahakama imemuhukumu mshtakiwa kutumikia miaka 30 gerezani na siyo kifungo cha maisha  kwa sababu imeona inayomamlaka ya kumpa mshtakiwa adhabu kwa jinsi yenyewe inavyoona kutokana na mkanganyiko uliopo kwenye kifungu cha sheria cha 15(1)(a) na 15(1).
Amesema sheria hizo mbili zilikuwa na madhimuni tofauti kutokana na matumizi ya maneno hayo shall be liable ambayo yako kwenye kifungu cha 25(1)(a) na shall be sentenced kifungu cha 15(1). 
Mshtakiwa Ogbechi alitiwa hatiani juzi, Juni 19 na leo amesomewa adhabu yake ambapo upande wa mashtaka uliwakilishwa na wakili wa serikali Batilida Mushi huku utetezi ukiwakilishwa na wakili Nashon Nkungu.
Hata hivyo kabla ya kuahirishwa kutolewa kwa adhabu hiyo, wakili anayentetea Ogbechi, Jeremiah Mtobesya mbali na maombi mengine pia aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu mshtakiwa licha ya  kwamba kifungu cha sheria cha 15(1) kinaamuru mshtakiwa kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini siyo lazima, itolewe adhabu hiyo, mahakama inaweza kuamua vinginevyo kutokana na Maneno yaliyopo kwenye kifungu cha 15(1)(a).
Mapema juzi, mahakama hiyo, ilimtia hatiani mshtakiwa huyo na kusema, pamoja na mshtakiwa kujitetea kwamba alifanyiwa upekuzi mara tatu na hakukutwa na kitu chochote na hivyo upande wa mashitaka ulipaswa kuleta ushahidi wa CCTV, haikuwa lazima kuwapangia upande wa mashitaka mashahidi wa kuwaleta na kwamba walikuwepo mashahidi wengine waliothibitisha mashitaka.
Amesema mkemia mkuu wa serikali katika uchunguzi wake, amethibitisha dawa za kulevya alizozichunguza ndizo alizokutwa nazo mshitakiwa huyo.
Mapema katika ushahidi wake, askari wa upelelezi kutoka Kituo cha  Uwanja wa ndege namba G 1782 D/C Peter alidai kuwa aliandika maelezo ya mshitakiwa huyo na katika mahojiano alimueleza kuwa amemeza pipi za dawa za kulevya.
Alidai baada ya kueleza hayo alimuweka mahabusu ili aweze kuzitoa na kwamba hadi  Januari 30,2018 saa 10:30  jioni alitoa pipi 23 alizomeza.Pia alidai walichukua kielelezo hicho na pipi nyingine zilizokutwa kwenye begi na kuzipeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali ambapo kwa pamoja zilikutwa na uzito wa gramu 947.17.
"Matokeo ya uchunguzi yalionesha kuwa pipi zote zilikuwa ni dawa za kulevya ambazo ni heroin hydrochloride zilizochanganywa na paracetamol metronidazole na papavirine," alidai Peter.
Mkuu wa Kituo cha Uwanja wa ndege, Inspekta Dickson Haule alidai siku ya tukio majira ya saa 14:00 mchana akiwa ofisini alijulishwa na askari huyo wa upelelezi kuwa kuna mtuhumiwa amekamatwa na dawa za kulevya.
Haule alidai baada ya taarifa hiyo alienda Ofisi ya Polisi Interpol walipokuwa na alishuhudia mtuhumiwa akipekuliwa  ndipo aliona begi dogo la mgongoni kuna pipi 56 zikiwa zimeviringishwa ndani ya soksi mbili nyeusi.
Katika kesi hiyo, inadaiwa Januari 28, mwaka jana maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa akisafirisha sha dawa za kulevya aina ya  Heroine hydrochloride zenye uzito wa grbamu 947.57.


DC MURO AWATAKA WAFANYABIASHARA MERU KUWASILISHA KERO ZAO ILI ZIPATIWE UFUMBUZI

$
0
0
Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha 

SERIKALI imewataka wafanyabiashara kuwasilisha kero zao ili zipatiwe ufumbuzi badala ya kubaki wakinung’unika kwani hazitatatuliwa na lengo ni kuwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru ili waweze kulipa kodi.

Kauli hiyo imetolewa Juni 20 mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Jerry Muro wakati wa kikao cha pamoja cha siku moja cha wafanyabiashara, Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Halmashauri ya Meru pamoja na taasisi zingine za Serikali wilayani.

Amesema wapo baadhi ya wafanyabiashara wana kero zao lakini hawako tayari kuziwasilisha TRA kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi badala yake wamekuwa wakinung’unika hivyo wahakikishe wanaziwasilisha TRA ili waweze kukaa pamoja na kuzipatia ufumbuzi na kuongeza Serikali inaamini wafanya biashara na wawekezaji ndio msingi pekee wa mandeleo ya Wilaya, mkoa naTaifa kwa ujumla hivyo niwajibu wao kuwasikila na kutatua kero zao 

Kuhusu kuegesha magari maeneo yasiyoruhusiwa pamoja kukata ushuru wa magari ,Muro amesema utaratibu wa kufunga cheni kwenye magari yaliyoegeshwa unaofanywa na Longparking pamoja na kuchaji ushuru wa magari katika sehemu za biashara za watu kama maofisi , ni uhuni huwa wanavizia magari na kuyafunga cheni kwa lengo la kujipatia rushwa baada ya majadiliano na mwenyegari na fedha wanazolipwa huwa hazipelekwi kunakotakiwa.

Amewataka wakala wa bara bara Vijijini Tarura, kufuatilia swala hili na ikishindikana watawaondoa wakala wa Long parking ,katika eneo hilo kwa kuwa imekuwa ni kero na vikwazo kwa wafanyabiashara na wateja wao akawashauri wenye magari wakiombwa fedha wasitoe bali wampigie simu kwani ni wasumbufu wanalazimisha rushwa .

Mmoja wa wawafanya biashara hao Profesa Justin Maeda amesema utaratibu unaotumiwa na Longparking,ni kuwatoza faini ya Sh.50,000 watu wanaoegesha magari hayo na kuingia ndani ya maduka hiyo kwa kisingizio cha Longpark ni kero na usumbufu unazosababisha kukosa wateja.

Mamlaka ya mapato TRA,wilaya ya Arumeru ,imesema itafanyakazi hata siku za mapumziko na siku kuu wakati wa kupokea retun za VAT kutoka kwa wafanyabiashara.

Meneja wa TRA Severini Wilbardy, ameyasema hayo alipokuwa akitolea ufafanuzi hoja za wafanyabiashara ikiwemo kulalama kurejesha retun za VAT siku ambazo sio za kazi lengo ni kuwahudumia walipa kodi.

Amewaonya wafanyabiashara kutokufanya udanganyifu kwenye taarifa za biashara zao kwa kufanya hivyo ni kuikosesha mapato serikali hivyo ambao watagundulika kuwasilisha taarifa zisizo sahihi TRA itawarejea kufanya upya ukaguzi wa hesabu .

Amesema kuwa lengo la TRA ni kuwakuza wafanyabiashara na sio kuwadidimiza hivyo wafanyabiashara wenye malimbikizo ya madeni waende TRA ili kutafuta ufumbuzi wa kulipa madeni yao.

Severini,ameema TRA inatoa motisha kwa mwananchi yeyote atakaewezesha kutoa taarifa za kukamatwa kwa wakwepa kodi ,ambapo motisha hiyo itatoa asilimia 3% ya bidhaa itakayokamatwa na kuuzwa kutokana na ukwepaji kodi au shilingi milioni 20 .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani Arumeru Furahini Mungure amesema mkutano wa Rais Magufuli na wafanyabiashara hivi karibuni uliofanyika Ikulu, umezaa matunda na akawasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi.

Amesema ni kweli wapo baadhi ya wafanyabiasha wana malimbikizo ya kodi na wengine hali zao za kibiashara ni mbaya hivyo akaiomba mamlaka ya mapato TRA kukaa nao ili wajenge mazingira rafiki yatakayowezesha kulipwa kodi na malimbikizo yaliyopo.

Aidha ,Mungure , ameitaka halmashauri ya Meru kutokuwafungia wafanyabiashara kwa sababu wanadaiwa na akasema rais akishatoa maelekezo hakutoa kwa TRA pekee bali na mamlaka zingine zikiwemo halmashauri kutokufunga biashara.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akiongea na wafanyabiashara na wawekezaji waliopo ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Meru

RC MAKONDA ATIMIZA AHADI YA ENEO KWA TIMU YA YANGA, AWAKABIDHI HEKARI 7 NA HATI MCHANA KWEUPEEE!.

$
0
0
kuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 21 amekabidhi eneo lenye ukubwa wa hekari 7 pamoja na hati ya umiliki kwa Klabu ya Yanga kwaajili ya ujenzi wa Uwanja na matumizi mengine ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa Hafla ya harambee ya Uchangiaji wa Timu hiyo.

RC Makonda amesema eneo hilo lina thamani ya Shilingi Milioni 700 ambapo lipo umbali wa Km 14 kutoka Daraja la Mwalimu Nyerere na umbali wa Mita 200 kutoka Barabara kubwa.

Akikabidhi eneo hilo RC Makonda ametaka uongozi wa Yanga kuanza kuliendeleza eneo hilo kwa kujenga Uwanja na miundombinu yote inayohitajika.

Wakipokea Eneo hilo, Viongozi wa Yanga,Bodi ya Wazamini na Mashabik wa Timu hiyo wamemshukuru RC Makonda kwa kuwapa eneo ambalo lipo kwenye mazingira mazuri ya tambarare na kuwatimizia ndoto waliyoishi nayo kwa miaka mingi bila mafanikio.

Dar es Salaam Bingwa UMISSETTA 2019

$
0
0
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mashindano ya 40 ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania UMISSETA yamefungwa rasmi leo katika uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Profesa Joyce Ndalichako kwa mkoa wa Dar es salaam kutangazwa kuwa mshindi wa jumla wa UMISSETA 2019.

Katika mashindano ya mwaka huu jumla ya mikoa 28 ikiwemo miwili ya Unguja na pemba ilishiriki mashindano hayo.

Mkoa wa Dar es salaam ulishika nafasi ya kwanza baada ya washiriki wake kufanya vizuri kwenye michezo ya mpira wa kikapu wasichana ambapo walishika nafasi ya kwanza, wavu walishika nafasi ya pili wasichana na wavulana, soka walishika nafasi ya tatu wasichana.

Pia washiriki kutoka mkoa wa Dar es salaam walifanya vizuri katika mchezo wa mpira wa meza ambapo wasichana walishika nafasi ya kwanza, netiboli pia walishika nafasi ya kwanza, na riadha wavulana walishika nafasi ya pili.

 Nafasi ya pili ilichukuliwa na Morogoro,nafasi ya tatu ilienda  Mwanza, nafasi ya nne ilichukuliwa na Tabora na Mbeya ulishika nafasi ya tano.

Kabla ya kutoa hotuba yake, Mhe. Ndalichako na wageni waalikwa walipata fursa ya kushuhudia pambano kali la fainali soka wavulana kati ya Songwe na Ruvuma ambapo mshindi ilibidi apatikane kwa njia ya penati baada ya timu hizo kufungana goli 1-1.

Katika hatua ya penati Ruvuma ilifanikiwa kuchukua ubingwa  wa UMISSETA wavulana baada ya kuifunga timu ngumu ya Songwe kwa penati 10-9.

Mshindi wa tatu Soka wavulana ni Mwanza ambapo golikipa bora kwa upande wa soka wavulana ni Nice kahemele wa Ruvuma na kwa wasichana ni Safina Haule pia kutoka mkoa wa Ruvuma.

Mfungaji bora kwa upande wa soka wavulana ni Paul Nyerere wa Mwanza ambaye alifanikiwa kupata magoli 6 huku mfungaji bora kwa upande wa soka wasichana ni Aisha Hamisi wa Mwanza ambaye alifunga magoli 13.

Mchezaji bora wa mashindano ya UMISSETA 2019 ni John Chinguku kwa upande wa soka wavulana kutoka Ruvuma na kwa upande wa soka wasichana mchezaji bora ni Ester Daniel kutoka Mwanza.

Kwa upande wa wachezaji walioonyesha mchezo mzuri (fair play) kwa soka wavulana ni Jackson Simba wa Ruvuma na kwa soka wasichana ni Lucy Mwenda pia kutoka mkoa wa Ruvuma.

Mapema kabla  ya kugawa zawadi kwa washindi mbalimbali, Waziri Ndalichako alisema kuwa serikali inayathamini sana mashindano ya UMISSETA kama sehemu sahihi ya kupata wanamichezo wenye vipaji watakaoweza kutumika kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Hivyo akataka wizara yake ihakikishe kuwa pindi wanapofanya ukaguzi shuleni wahakikishe pia somo la michezo linakuwemo.

Pia akataka kila shule inayosajiliwa ihakikishe kuwa inakuwa na viwanja vya michezo ili kuwawezesha watoto watakaosoma katika shule hizo kupata fursa ya kucheza michezo mbalimbali.

Waziri Ndalichako amesema kuwa michezo ni sehemu nuhimu sana kwa wanafunzi kwani inawajengea afya ya akili pindi wanaposhiriki michezo mbalimbali na hivyo kuwawezesha kusoma vizuri.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Mhe.Mwita Waitara amesema kuwa Ofisi yake itaendelea kuhakikisha kuwa michezo ya UMISSETA inafanyika ili kuwawezesha vijana wengi wenye vipaji kuonyesha uwezo wao na hivyo kupata fursa ya kujiendeleza kimichezo.
 Mgeni Rasmi Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (katikati aliyevaa tracksuit ya bluu) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa  na kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu. Mhe. Mwita Waitara wakienda kutoa zawadi kwa washindi wa UMISSETA 2019 katika uwanja wa Nangwanda, mjini Mtwara  
 Mabingwa wapya soka wavulana wa UMISSETA 2019 timu ya mkoa wa Ruvuma mara baada kukabidhiwa kombe lao na  Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Profesa Joyce Ndalichako. Ruvuma iliifunga timu ya mkoa wa Songwe kwa penati 10-9
Mchezaji bora wa mashindano ya UMISSETA 2019 John Chinguku kutoka Mkoa wa Ruvuma akipokea tuzo yake kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI Benjamin Oganga jana.

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa ofisi yake mara baada ya watumishi hao kukamilisha zoezi la usafi wa mazingira eneo la Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019.
 Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakifanya usafi katika ofisi yao iliyopo Mji wa Serikali, eneo la Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Fabian Pokela akimwagilia maji moja ya mti uliopandwa katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora eneo la Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2019.

YALE YALEEE...... DEREVA WA DALADALA AKI "CHAT"

$
0
0


Dereva wa daladala yenye namba za usajili T 457 DMF ambaye jina lake halikufahamika mara moja, ambayo ilikuwa inatoka Mbezi kuelekea Makumbosho jijini Dar es Salaam akionekana kufanya mawasiliano ya kutuma ujumbe mfupi (sms) kwa kutumia simu huku akiendelesha gari hilo lililokuwa na abiria wengi tu ndani yake. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)







TFDA YAFUNGUA OFISI YA KANDA MPYA YA ZIWA MASHARIKI SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imefungua rasmi Ofisi ya Kanda mpya ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ambapo makao makuu ya kanda hiyo yatakuwa Mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama amesema mamlaka hiyo imeanzisha Kanda Mpya ya Ziwa Mashariki inayojumuisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga ili kusogeza huduma kwa wananchi na kuharakisha ukuaji wa uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Amesema ofisi hii itajishughulisha na usajili wa maeneo yanayo jihusisha na uzalishaji na uuzaji wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba, kupokea maombi ya usajili wa bidhaa za vyakula vinavyofungashwa, kufanya ukaguzi wa bidhaa za vyakula katika soko kuwalinda walaji na kudhibiti usindikaji wa chakula dawa na vipodozi.

Kazi nyingine zitakazofanywa na kanda hii ni kutoa vibali vya uingizaji nchini na usafirishaji wa chakula nje ya nchi, kufanya ufuatiliaji wa bidhaa za vyakula katika soko, kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa, vipodozi na vifaa tiba pamoja na kuelimisha na kutoa taarifa kwa wadau na wananchi kwa ujumla kuhusu bidhaa zinazothibitiwa na mamlaka.

Aidha, Mwasulama amesema Ofisi ya kanda hii itatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambapo wataalam waliopo kwenye wilaya, manispaa, miji na majiji watasimamia sheria ya chakula na dawa kwa mujibu wa kanuni ya kukasimu baadhi ya majukumu na madaraka ya TFDA katika Halmashauri.

Akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa wa Simiyu na TFDA katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema Taasisi nyingine zinazohitajika katika uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zikaiga mfano wa TFDA kwa kusogeza huduma karibu na wananchi ili waweze kupata huduma kwa wakati.

“Hiki kilichofanywa na TFDA ni vizuri taasisi nyingine nazo ziige, kama leo TFDA ipo Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki ningetamani kuwaona TBS, NEMC, OSHA wako Simiyu kama Kanda ya Ziwa Mashariki na Taasisi zote ambazo kwenye uwekezaji wa viwanda na maeneo mengine ya uwekezaji zinakuwa karibu na maeneo ya kutolea huduma” alisisitiza Mtaka.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanaotekeleza majukumu waliyokasimiwa na TFDA kufanya majukumu hayo kwa mujibu sheria huku akiwaasa kuacha tabia ya kufungia biashara za wananchi bila kuwaelimisha badala yake wawasaidie kuwapa elimu ili wazalishe bidhaa bora kwa walaji.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Dkt. Mike Mabimbi akizungumza kwa niaba ya waganga wakuu wa wilaya ambao ni Makatibu wa kamati za ukaguzi wa chakula na dawa amesema watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa majukumu wanayokasimiwa na TFDA kwa mujibu wa sheria na akashukuru TFDA kusogeza huduma karibu na wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama akitoa taarifa fupi ya uanzishwaji wa Kanda hiyo itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, katika uzinduzi waa kanda hiyo uliofanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) wakifuatilia masuala mbalimbali ambayo yaliyokuwa yanaendelea katika Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Kanda ya Ziwa Mashariki, Bi. Nuru Mwasulama mara baada ya kuzindua rasmi Kanda ya Ziwa Mashariki ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa, Dkt. Mugune Maeka akitoa neno la shukrani mra baada ya kuhitishwa kwa uzinduzi wa Kanda ya Ziwa Mashariki ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga, Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wataalam wa mkoa wa Simiyu na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) mara baada ya Uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya wataalam wa Mkoa huo Mamlaka ya Chakula na Dawa, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Mashariki itakayohudumia mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na makao makuu yake yakiwa Bariadi Mjini, Uzinduzi umefanyika Juni 20, 2019 Mjini Bariadi.

Wahitimu wa Vyuo Vikuu washauriwa kuzingatia mambo haya kupambana na suala la ukosefu wa ajira mara baada ya kuhitimu masomo

$
0
0
Na Charles James, Dodoma.

WAZIRI Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewashauri wahitimu wa vyuo vikuu kuzingatia mambo makuu matano muhimu ili waweze kupambana na suala la ukosefu wa ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Hayo ameyasema leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo jijini humo ambapo amewataka wanafunzi hao kutumia maarifa wanayoyapata katika kutatua changamoto hiyo hasa kwa kutengeneza ajira zao wenyewe. 

Pinda amesema  kuwa serikali haiwezi kuwaajiri vijana wote wanaohitimu elimu ya juu kila mwaka hivyo amewashauri  wawe na njia  mbadala ambayo itawapa mtaji ili waweze kuwekeza katika sekta mbalimbali ambazo zitawaingizia kipato.

“Nchi haiwezi kuajiri wasomi wote wanaohitimu elimu ya juu kila mwaka, ili nieleweke wazi  tulipaswa kutengeneza mfumo ambao utawafanya wahitimu kuwa na muelekeo wa kutumia fursa zilizopo'' amesema Pinda.

Pinda amesema kuwa jambo la kwanza la kuzingatia ni kuweka mfumo wa elimu utakaowawezesha wanafunzi kupata elimu ya ujasiriamali katika kila ngazi ya masomo wanayoifikia.

“Kama mwaka wa kwanza hadi mwaka wa tatu kwenye masomo kila mwanafunzi akipatiwa mbinu mbalimbali zitakazomwezesha kubaini fursa za ujasiriamali zilizopo, kwa kiasi kikubwa tutaweza kukabiliana na ukosefu wa ajira''ameeleza.

 Pili amewataka wasomi  kubadili mtizamo wa kifikra kuhusu kuajiriwa  pindi wanapohitimu masomo yao, amewataka kubadili maarifa waliyojifunza kuwa fursa ya kujikwamua.

Aidha ameeleza kuwa alifanya ziara ya kuongea na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo mmoja wa wasomi wa masomo ya sheria, alieleza jinsi alivyopata tabu pindi alipoambiwa  afuge kuku, wakati amejifunza masuala ya sheria, suala ambalo amewataka wasomi kutoliweka akili.

Jambo la  tatu ambalo Waziri Pinda amewashauri wanafunzi hao ni kufahamu uhalisia wa dunia ya sasa hasa kwa kuangalia maendeleo ya sayansi na teknolojia na kutumia fursa zilizopo katika kuleta matokeo chanya katika jamii.

 “Itawalazimu mshindane na watu kutoka mataifa mengine ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) au maeneo mengine duniani hivyo ni lazima mkaangalia soko la sasa linahitaji nini na mkachangamkia fursa hizo''ameeleza.

Jambo la nne ambalo Pinda ameshauri ni uthubutu katika kufanya maamuzi jambo ambalo litawasaidia kufikia malengo yao huku akieleza kuwa wasikatishwe tamaa  kuhusu ndoto na malengo yao ya kujiajiri.

Mwisho amewataka  wanafunzi hao kufahamu tofauti kati yao na wale ambao hawakubahatika kupata nafasi ya kusoma na watumie maarifa yao kama fursa ambayo itawatoa sehemu moja hadi nyingine na kuweza kuwasaidia vijana wengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma mjini, Winifrida Kaliyo amesema kuwa; semina hiyo imelenga kuwawezesha wanafunzi kutambua fursa na kuzitumia ili kujenga uchumi wao binafsi na taifa kwa ujumla.

Awali Katibu wa umoja huo Wilaya ya Dodoma mjini, Diana Madukwa amesema kuwa, tangu Januari hadi Juni mwaka huu, umoja huo umeongeza wanachama wapya 1500 na kusema kuwa kuwa wametoa mafunzo kwa viongozi ngazi ya kata hadi wilaya pamoja na kuhamasisha wanawake kugombea ngazi za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

BENKI YA MAENDELEO TIB YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUINGIA MKATABA WA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati) akimkabishi mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Charles Singili (kulia) mara baada ya kuuzindua mkataba huo. Uzinduzi huo umefanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya TIB.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto) akimkabidhi nakala ya mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) Bw.Joseph Kidaha (katikati) mwakilishi wa wateja waliohudhuria uzinduzi rasmi wa Mkataba huo. 
 Mkurugenzi, Mkakati na Mahusiano ya Kibiashara, Bw. Patrick Mongella (kulia) akipokea nakala za Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili (katikati) akionesha mfano wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter) mara ya kukakidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (kushoto). Anayeshuhudia ni mmoja wa wateja wa benki hiyo, Bw.Joseph Kidaha (kulia).
 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakifuatilia uzinduzi Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customer Service Charter).
Baadhi ya wateja wa Benki ya Maendeleo ya TIB wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Dkt. Mary Mashingo (katikati waliokaa) pamoja na menejimenti ya benki hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Charles Singili (wapili kulia waliokaa).

Na Mwandishi wetu
Benki ya Maendeleo TIB (TIB Development Bank) imeadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza kuadhimishwa tarehe 16 Juni, 2019 kwa kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Wateja (Customers’ Service Charter) ili kuendeleza kutoa huduma bora na zenye viwango kwa wateja wake.
Akizungumza wakati wa unzinduzi wa Mkataba huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo, Dkt. Mary Mashingo amesema kuwa malengo ya Mkataba huo ni kuendeleza kutoa huduma bora bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka.
“Huu ni Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unaakisi dhamira ya dhati ya Benki ya kuwahudumia wateja bila ya upendeleo, kwa heshima na kwa haraka. Mkataba huu una ahadi za huduma mahsusi na za hiari.
Aliongeza kuwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja wa Benki ya Maendeleo TIB unatambua wateja wetu wana haki ya kuelewa kiwango cha huduma kinachotolewa na Benki yao kwa wakati wote.
Kwa mujibu wa Dkt. Mashingoo, Benki iko tayari kupokea maoni ya namna ya kurekebisha na kuboresha zaidi huduma zake.
“Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo TIB, tumejipanga kusimamia kwa dhati utekelezaji wa mkataba huu katika kutekeleza dhamira  ya Mheshimiwa  Rais ya  kuwa  na  taasisi za umma zinazowahudumia  wadau wake. Watumishi  wa  Benki mnatakiwa kufanya kazi  kwa weledi,  juhudi,  maarifa  na uadilifu  mkubwa.  Pamoja na utoaji wa huduma bora, kwa haraka na kwa staha ili kuwaondolea wananchi usumbufu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Bw. Charles Singili alisema kuwa TIB imejidhatiti katika kuimarisha mahusiano nawateja wake, hivyo kuzinduliwa kwa Mkataba huu kutachochea utendaji kazi wake ikizingatiwa kuwa benki hiyo muhimili muhimu katika kuunganisha Serikali na Sekta Binafsi.
“Zipo Benki za biashara lakini hii ya TIB ni tofauti kabisa kwa kuwa yenyewe imejikita katika kuleta maendeleo kwa wateja na watanzania kwa ujumla. Hivyo, mkataba huu utaimarisha mahusiano na wateja wetu,” amesema.
Ameongeza kuwa TIB ni benki kiunganishi muhimu kati ya Serikali na Sekta Binafsi, kwa kuchagiza uchangiaji kwa kiasi kikubwa katika masuala ya uwekezaji.
Akizungumzia kaulimbiu ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019, isemayo “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi.” Bw. Singili ametoa wito kwa vijana kutumia uwepo wa taasisi wezeshi ili waweze kujikwamua katika kuinua vipato vyao na taifa kwa ujumla.
“TIB tumejikita katika kuwasidia vijana waweze kusimamia misingi ya utawala bora lakini pia kuangalia kwa namna ambavyo wanaweza kuzalisha mazao mbalimbali hali inayoweza kuwasaida kutimia malengo yao binafsi na ya serikali kwa ujumla hasa kupitia mkakati wa Tanzania ya viwanda,’’ alifafanua.
Kwa upande wa wateja wa benki hiyo waliowakilishwa na Bwa. Joseph Kidaha amesema kuwa, mkataba huo una maana kubwa kwa wateja wa benki hiyo huku akisisitiza kuwa,  ukisimamiwa vizuri utaleta manufaa makubwa kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.
“Ni jambo zuri kuona mahusiano mazuri yanatengenezwa kati ya benki na wateja wake, hiyo itaamsha ari kwa watu katika kuitafuta hudumu ya benki hii na tulio wengi kutimiza matarajio tuliyojiwekea ,’’ alisema.
Bwana Kidaha aliwataka wadau kuja kukopa katika benki ya TIB na kufanya marejesho kwa muda unaostahili ili kuwafanya watanzania wengi waendelee kunufaika na mikopo ya benki ya maendeleo (TIB)
Viewing all 110117 articles
Browse latest View live




Latest Images