Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

YANGA SC HAIHITAJI MFADHILI-ROSTAM


NAIBU WAZIRI MGALU AZURU KONDOA KUJIRIDHISHA NA ELFU 27 YA UMEME VIJIJINI

$
0
0
Na Veronica Simba - Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya ziara wilayani Kondoa, Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa agizo la Serikali kuhusu kuwezesha wananchi wote wanaopitiwa na miradi ya umeme vijijini (REA), kulipia shilingi 27,000 tu bila kujali ni vijijini au katika Halmashauri za Wilaya.

Alifanya ziara hiyo jana, Juni 20, 2019 ambapo pia aliwasha rasmi umeme katika Taasisi mbalimbali za Umma zikiwemo Shule na Zahanati.

Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Bicha, Kolo na Kwayondu, Naibu Waziri alimpongeza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wilayani humo, Emily Ntanzimila, kutokana na kutekeleza kwa haraka agizo hilo lilitolewa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati.

“Hongera sana maana nimeona hapa kwenye orodha majina ya wananchi ikiambatishwa na risiti za malipo waliyofanya ambazo zinasomeka wamelipia shilingi 27,000 tu kama tulivyoelekeza.”

Akifafanua kuhusu agizo hilo la Serikali, Naibu Waziri alisema kuwa, awali, gharama iliyokuwa ikitozwa ilikuwa inatofautiana kwani miradi ya REA ilikuwa shilingi 27,000 lakini ilipokamilika na kukabidhiwa kwa TANESCO, wateja walilazimika kuunganishiwa umeme kwa shilingi 177,000.

“Naipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kutoa maelekezo kwamba, umeme unaletwa kwa ajili ya kutumiwa na wananchi, hivyo bei iwe moja tu yaani shilingi 27,000.”

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika eneo lake, Meneja wa TANESCO Kondoa, alimweleza Naibu Waziri kuwa vijiji vyenye umeme wilayani humo ni 29 kati ya 84 vilivyopo, ambavyo ni sawa na asilimia 34.

Alisema, kupitia Mradi wa REA Awamu ya Tatu ambayo inaendelea kutekelezwa, vijiji vingine 23 vinatarajiwa kuunganishwa hivyo kufikia 52, sawa na asilimia 62.

Aliongeza kuwa, asilimia 38 ya vijiji vilivyobaki (vijiji 32), vimependekezwa kwenye miradi ya REA ya Ujazilizi, REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili na kwenye Bajeti ya TANESCO mwaka 2019/2020.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alimwagiza Meneja huyo kufika eneo la Itundwi wilayani humo siku ya Jumatatu, Juni 24, mwaka huu, ili apokee malipo ya umeme ya wananchi ambao awali aliwarudisha.

Naibu Waziri alitoa maagizo hayo baada ya wananchi wa eneo husika kusimamisha msafara wake na kutoa malalamiko kadhaa ikiwemo hilo la kukataliwa kupokelewa malipo yao ya kuunganishiwa umeme.

“Tumeshatoa maelekezo kwa Mameneja wote wa TANESCO nchi nzima kuwa ni marufuku kukataa kupokea malipo ya umeme kutoka kwa wananchi kwa kisingizio chochote kile. Naamini wakati akiwarudisha tulikuwa bado hatujatoa maelekezo, hivyo namwagiza arudi kupokea malipo yenu.”

Aidha, alimtaka Meneja huyo kufanyia kazi utaratibu wa kuwaunganishia umeme wananchi wa eneo hilo ambao wamepitiwa na miundombinu lakini hawana nishati hiyo, kupitia Mradi wa Ujazilizi.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri alifuatana na viongozi mbalimbali pamoja na wataalamu kutoka wizarani, TANESCO na REA.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye ushungi), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Shule ya Sekondari Bicha iliyopo wilayani Kondoa, Juni 20, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (aliyenyanyua mkono-kushoto), akizungumza na wananchi wa eneo la Itundwi, wilayani Kondoa, waliosimamisha msafara wake akiwa katika ziara ya kazi, Juni 20, 2019. Naibu Waziri alitoa majibu ya changamoto zote walizomwasilishia.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akifurahi pamoja na wananchi wa Kijiji cha Kolo wilayani Kondoa, baada ya kuwasha rasmi umeme katika Zahanati ya Kijiji hicho, Juni 20, 2019.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bicha, wilayani Kondoa, baada ya kuiwashia rasmi umeme, Juni 20, 2019 akiwa katika ziara ya kazi. Naibu Waziri alitoa hamasa kwao kuongeza ufaulu kutokana na uwepo wa nishati hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwayondu wilayani Kondoa, muda mfupi kabla ya kuwasha umeme katika Shule ya Msingi kijijini hapo, akiwa katika ziara ya kazi Juni 20, 2019.
Sehemu ya viongozi wa Serikali na wataalamu kutoka wizarani, TANESCO na REA, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwayondu, wilayani Kondoa, Juni 20, 2019 akiwa katika ziara ya kazi.

Tumepokea Maombi Mapya ya kuuza Mahindi Tani Milioni Moja kwenda Kenya – Naibu Waziri Mgumba

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba akipata amelezo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa kwa upande wa ndani kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao Makuu Bwana Iman Nzobonaliba kulia kwake na wengine ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Bwana Mikalu Mapunda na kushoto kwake ni Mhandisi Mgole Chambili Msimamizi kutoka Kampuni ya Feruum 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba akipata amelezo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa kutoka Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao Makuu Bwana Iman Nzobonaliba kulia kwake na wengine ni Mtendaji Mkuu wa NFRA Bwana Milton Lupa 
Mafunsi wa Kampuni ya Feruum wakiendelea na kazi ya kuunganisha vyuma vya ujenzi wa vihenge vya kisasa eneo la Kizota Jijini Dodoma wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba alasiri ya leo 
………………………… 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali ya Tanzania imepokea maombi mapya ya kuuza mahindi kwenda nchini Kenya yenye jumla ya Tani milioni 1. 

Mhe. Mgumba ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya gafla kwenye Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA – Makao Makuu) Jijini, Dodoma alipotembelea leo alasiri ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa vya kuhifadhia chakula katika eneo la Kizota, Jijini Dodoma. 

Naibu Waziri Mgumba amesema wakati Serikali ikiwa kwenye hatua ya kuiuzia Zimbabwe kiasi cha mahindi Tani laki saba (700,000) na tani laki moja (100,000) kwa mazao mengine ya nafaka, Serikali ya Kenya imewasilisha ombi rasmi la kununua kiasi hicho kutoka Tanzania. 

Naibu Waziri Mgumba amesema huu ni wakati muhafaka kwa Wakulima wa Tanzania kuchangamkia fursa ya kuuza chakula cha ziada nje ya nchi na kwa bei nzuri ambayo italeta tija na maendeleo na uchumi wao. 

Aidha Mhe. Mgumba alidokeza kuwa amefanya ziara hiyo lengo lake likiwa ni kujionea maendeleo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) vya kuhifadhia mazao kwa lengo la kuongeza akiba ya taifa ya chakula kwa Kanda ya Kati yenye kuhudumia mikoa ya Dodoma, Singida kutoka uwezo wake wa sasa wa kuhifadhi, tani elfu thelasini na tisa (39,000) hadi kufikia tani elfu hamsini na tisa (59,000). 

Mradi wa ujenzi wa vihenge hivyo vya kisasa, ulizinduliwa rasmi tarehe 24 Aprili, 2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na ulianza rasmi Mwezi Juni 2018 huku Kampuni ya Feruum kutoka nchini Poland ndiyo iliyoshinda zabuni ya ujenzi huo. 

Akijibu swali la Mhe. Mgumba, Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bwana Iman Nzobonaliba amesema Mradi unataraji kuisha kwa wakati mnamo Mwezi Disemba 2019. 

Akijibu swali la Naibu Waziri Mgumba ambaye alitaka kufaham namna Wakala ilivyojianda kununua mazao ya Wakulima katika msimu wa kilimo wa 2019/2020 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bwana Milton Lupa amemwambia Naibu Waziri Mgumba kuwa NFRA imeanza zoezi la kununua chakula cha ziada kutoka kwa Wakulima tangu tarehe 17 Juni 2019 katika Kanda ya Makambako na Sumbawanga na kwamba kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kitatumika kwa sasa. 

Bwana Lupa amesema NFRA imejipanga kutumia bajeti ya kiasi cha bilioni 15 pamoja na kuomba mkopo kutoka Benki ya Kilimo wenye riba nafuu na kuongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 62.6 zitatumika kwa ununuzi wa nafaka kwa msimu wa kilimo wa 2019/2020. 

Akizungumzia bei ya kununulia mahindi kwa kilo, Mtendaji Mkuu amesema bei ya ununuzi itakuwa ikitofautiana kutoka eneo moja na eneo linguine. 

“Niseme tu kuwa tutaanza na bei ya shilingi 400 hadi 500 kwa kila kilo moja ya mahindi lakini bei hii pia itakuwa ikibadilika kutokana na sababu mbalimbali” Amekaririwa Bwana Milton Lupa. 

Naibu Waziri Mgumba ameongeza kuwa NFRA ni Taasisi ya Serikali na imeaminiwa kusimamia jukumu la uhifadhi wa chakula na kuwa Taifa linatarajia makubwa katika kuhakikisha Taifa linakuwa na akiba ya chakula ya kutosha. 

“Sisi kama Viongozi wenu, hatuna shaka na uzoefu wenu na umahiri wenu katika nyanja ya uhifadhi wa chakula hususan nafaka kama mahindi, endeleeni mbele na sisi tutahakikisha mnapata mahitaji yenu, nawahakiki kuwa fedha za ununuzi mtazipata kwa kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imetuahidi kuwa zitakuja mapema kama mlivyopanga” Amekaririwa Mhe. Mgumba

MAKAMU WA TATU WA RAIS SHIRIKA LA HALI YA HEWA DUNIANI AWASILI TANZANIA

$
0
0
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akiwasili nchini Tanzania akipokea zawadi ya uwa kutoka kwa wafanyakazi wa TMA ikiwa ni ishara ya kumpongeza na kumkaribisha nyumbani akitokea nchini Uswisi – Geneva alipokuwa akishiriki Mkutano wa 18 wa WMO ambapo alichaguliwa kushika nafasi hiyo. Kushoto ni mumewe Bw. Mwara Anande Shoo akishiriki mapokezi hayo. 
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Pascal Waniha (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili Tanzania akitokea nchini Uswisi – Geneva alipokuwa akishiriki Mkutano wa 18 wa WMO ambapo alichaguliwa kushika nafasi hiyo. Wengine ni viongozi waandamizi wa TMA wakishiriki mapokezi. 
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Utabiri TMA, Dk. Hamza Kaberwa (wa tatu kushoto). 
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (kushoto) akisalimiana na Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri – TMA, Bw. Samwel Mbuya (kulia) mara baada ya kuwasili. 
Wafanyakazi na viongozi wa TMA wakimlaki Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi. 
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akiongozana na wafanyakazi na viongozi wa TMA kuelekea ukumbi wa mkutano kuzungumza. 
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi (katikati) akizungumza machache na wafanyakazi na viongozi wa TMA mara baada ya kuwasili. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Pascal Waniha pamoja na mume wa Dk. Kijazi, Bw. Mwara Anande Shoo (kushoto). 
Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akizungumza na kutoa shukrani kwa waliompokea. 
Picha ya pamoja ya Makamu wa Tatu wa Rais wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agnes Kijazi akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa TMA walioshiriki mapokezi.

WAANDISHI WA NURU FM WAPIGWA MSASA KUANDIKA HABARI ZA KIJINSIA

$
0
0


Gerald Malekela ambaye ni program meneja wa radio akiwasilisha mada walizojadiliana kwenye kundi lao walipopata wakiwa darasani wakati wa mafunzo yanayodhaminiwa na mradi wa Boresha Habari unaoendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID.
Baadhi ya waandishi wa Radio Nuru fm wakiwa wanasikiliza kwa umakini elimu inayotolewa na mkufunzi Temigunga Mahondo kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Waandishi wa habari wa kituo cha radio cha Nuru Fm Iringa wamepigwa msasa juu ya kuandika habari za kijinsia kupitia Mradi wa Boresha Habari unaoendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID.

Akitoa mafunzo hayo mkufunzi kutoka Mradi wa Boresha Habari ukiendeshwa chini ya uratibu wa mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Internews na FHI 360 unaofadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID),Temigunga Mahondo alisema kuwa waandishi wengi wamekuwa wakiandika habari bila kuangalia kwa kina juu ya habari za kijinsia.

“Niwaombe waandishi wa habari hakikisheni mnaandika habari za kijinsia ili kutengeneza usawa katika jamii zetu na kuwa na kizazi ambacho kitakuwa kinaishi kwa usawa” alisem Mahondo

Mahondo alisema kuwa ni vyema waandishi wa habari wakajikita kuandika habari zinazogusa maisha ya wananchi wote bila kujali jinsia

Aidha Mahondo amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanajukumu la kuandika habari ambazo zitakuwa zinaelimisha maswala ya jinsia ili kujenga na kizazi cha kuwa na usawa.

Akichangia mada wakati wa semina mhariri wa radio Nuru fm Hafidh Ally alisema kuwa mafunzo kuwa mafunzo hayo yatawaongezea waandishi wa habari wa radio hiyo kuandika habari za kuelimisha jamii kuhusu jinsia

“Hii kwetu ni moja ya mafunzo bora ambayo yatatusaidia kuongeza uelewa wa kuandika habari za kijinsia na kukuelimisha jamii kwa kuandika habari za aina hiyo ambazo zitakuwa na mguso kwa jamii husika” alisema Ally

Ally alisema atahakikisha waandishi wa habari wa kituo cha NURU FM wanayafanyia kazi kwa vitendo mafunzo hayo ili waweze kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa sugu katika jamii.

Lengo la mafunzo hayo ni kuondoa mfumo dume ambao umekuwa kwenye jamii zetu na umekukuwa ukilalamikiwa na taasisi mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi

Songas yawekeza kuwawezesha wakazi wa fukwe

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songas Tanzania, Nigel Whitaker (Watatu kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 108 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sea Sense, Joana Trindade (watatu kulia), kwa ajili ya wa kuchangia TZS 108 milioni kudhamini programu ya mafunzo ya mwaka mmoja kuwawezesha wananchi katika kisiwa cha Kilwa kupata elimu ya utunzaji wa fukwe na uvuaji salama mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Songas imetoa msaada wa shilingi huo kama jitihada za kudumisha viumbe hai na kuchochea ukuwaji wa sekta ya uvuvi nchini. Wa mwisho upande wa kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara na ufuatiliaji, Sebastian Kastuli na Mshauri wa masuala ya kiufundi, Bi. Lindsey West. (wamwisho kushoto).
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songas Tanzania, Nigel Whitaker (wapili kushoto aliekaa) akisaini mkataba na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sea Sense, Joana Trindade (wa kati aliekaa), kwa ajili ya wa kuchangia TZS 108 milioni kudhamini programu ya mafunzo ya mwaka mmoja kuwawezesha wananchi katika kisiwa cha Kilwa kupata elimu ya utunzaji wa fukwe na uvuaji salama mapema leo katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Songas imetoa msaada wa shilingi huo kama jitihada za kudumisha viumbe hai na kuchochea ukuwaji wa sekta ya uvuvi nchini. Wa mwisho upande wa kushoto alieketi ni Afisa Mkuu wa Biashara na  ufuatiliaji, Sebastian Kastuli na Mshauri wa masuala ya kiufundi, Bi. Lindsey West (wapili kulia), wengineo ni wafanyakazi wa kampuni ya songas .

MWENYEKITI AREJESHA SARUJI ALIYOICHUKUA BILA UTARATIBU

$
0
0

Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Suleiman Mkubulu amerejesha mifuko 24 aliyoitumia kinyume na utaratibu kama alivyohaidi kuirudisha baada ya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kugundua upotevu wa mifuko hiyo alipokuwa akifuatilia kwa makini ujenzi wa miradi ya maendeleo kijijini hapo. 

Tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Diwani kata ya Kitama, Mtendaji kata Kitama, Mtendaji Kijiji Namunda, Wajumbe Serikali ya Kijiji pamoja na kamati ya ujenzi. 

Akizungumza mara baada ya mifuko hiyo kukabidhiwa kimaandishi kwa Mtendaji wa Kijiji na kamati ya ujenzi, Gavana Shilatu aliwasihi sana viongozi kuelewa dhana ya utumishi na uongozi ni dhamana ya Wananchi na si mwanya wa kujitajirisha, kudhulumu au kuonea wengine kinyume na sheria. 

*”Pasipo usimamizi imara, hii mifuko 24 ya saruji ingepotea. Ni lazima tutambue uongozi ni dhamana na si fursa ya kujitajirisha au kuonea wengine.” Alisema Gavana Shilatu 

Tangu awali alipopata taarifa ya upotevu, Gavana Shilatu alisimama kidete hadi saruji hiyo kurejeshwa kwa ajili ujenzi wa miradi ya maendeleo ya ofisi ya Kijiji na Madarasa mawili na ofisi moja ya Walimu ya Shule ya msingi Namunda.

MAANDALIZI YA TAIFA STARS-MISRI

$
0
0


Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars,inaendelea vizuri na matayarisho yake kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa michuano ya Mataifa Afrika dhidi ya Senegal,Juni 23 mwaka huu katika Uwanja wa 3o June Cairo.

Kutokana na maandalizi yanayoendelea hadi sasa katika kikosi hicho,benchi la ufundi lina imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa ufunguzi na michezo mingine dhidi ya Kenya na Algeria.

Pamoja na wachezaji hao kufanya mazoezi ya uwanjani,pia wamekuwa wanafundishwa mbinu mbalimbali nje ya uwanja kwa kutumia mikanda mbalimbali ya video kuwasoma wapinzani wao,kabla ya kuanza kutupa karata yake rasmi katika mashindano hayo.

Kwa upande wa majeruhi,hadi sasa mchezaji ambaye hatoweza kushiriki mashindano hayo ni Aggrey Morris,ambaye nafasi yake imechukuliwa na David Mwantika,ambaye tayari ashawasili ndani ya kambi tayari kwa ajili ya mashindano.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Emmamuel Amuneke,kimeweka kambi nchini Misri tangu Juni 7,kwa ajili ya kuweza kupata nafasi ya kufanya maandalizi ya kina kabla ya kuanza kwa mashindano hayo

TanFootball






HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA WAJASIRIAMALI WADOGO

$
0
0
Na.Khadija seif,Globu ya jamii

HALMASHAURI ya jiji la Dar es salaam lameadhimisha siku ya wiki ya utumishi wa umma kwa kutembelea viwanda vya wajasiliamali wadogo jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji Herman amesema Serikali Ina nia ya dhati kuwanyanyua wajasiLiamali hao kibiashara ili kukuza pato la taifa.

Wiki hii ya utumishi wa umma imeanza juni 17 na unatarajiwa kufika kilele juni 23 mwaka huu.Aidha, ameeleza WajasiLiamali hao wadogo na wanafanya shughul hizi katika mazingira shirikishi na halmashauri ikaamua kuwatengea wajasiriamali hao sehemu ya kuuza biashara hizo.

" Mpaka sasa vikundi 15 katika kata ya mwanayamala wamekua wanufaika wa mikopo iliyotengwa na serikali na million 853 imeshatolewa ,"Hata hivyo Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikikasha 10% ya mapato ya ndani zinatengwa kwa ajili ya kusaidia kundi maalum wakiwemo walemavu na wakina"

WajasiLiamali wameanzisha shughulI za uzalishaji wa usindikaji chakula ,sabuni. Mafuta,viatu , batik ushonaji na uchoraji.Kaimu Muhandisi wa halmashauri ya jiji Jumanne Manish amesema ujenzi ulizingatia maeneo ambayo ni rahisi kufikiwa kwa wahitajika. 

Pia Manish ameeleza kuwa ujenzi unaendelea kwenye jengo hilo kufatia wajasiriamali kuomba kuanza shughul zao kabla ya kukamilika matengenezo makubwa Kama kuleta umeme mahali hapo kwa wajasiriamali ambao shughuli zao zintegemea sana umeme.

"Uboreshwaji wa majengo utaendelea na tutegemee kuwepo kwa majengo ili kupanua wigo wa kibiashara na kutakuwepo jengo la utawala pamoja na wataalam watakaowezesha wajasiriamali kuhifadhi fedha ,"

Kwa upande wake mjasiriamali mdogo wa kiwanda cha batiki amewashukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John pombe Magufuli kwa kuona ipo haja ya kutenga fedha kwa ajili ya kundi maalum .

"Mimi ni mmoja wa wanufaika wa mikopo ya Serikali na imeniwezesha kununua vifaa vipya vinavonisaidia kushona kwa haraka zaidi tofauti na hapo awali nilikua natumia mashine ya kushonea ya kizamani,"

Amewaomba wakina mama kuchukua mikopo hiyo kwa ajili ya biashara na si vingine kutokana na ipo kwa ajili ya kunyanyua wakina mama na kupanua wigo wa kibiashara zaidi.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 21,2019

WAKIMBIZI KIGOMA WAIOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA NAFASI ZA MASOMO ELIMU YA JUU WANAFUNZI WANAOMALIZA KIDATO CHA SITA

$
0
0
Moureen Rogath, Kibondo 

Wakimbizi kambi ya wakimbizi Nduta iliyopo wilayani hapa mkoani Kigoma wameiomba serikali ya Tanzania kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Duniani(UNHCR), kuwatafutia nafasi za kusoma elimu ya chuo kikuu kwa wanafunzi wakimbizi wanaomaliza kidato cha sita.

Wakizungumza  jana kambini hapo katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani ambayo hufanyika Juni 20, kila mwaka, wamesema watoto wao wengi wanamaliza kidato cha sita lakini wameshindwa kuendelea na elimu ya juu. 

"Hakuna chuo hapa Tanzania ambacho watoto wakimbizi watamaliza kidato cha sita na kwenda kusoma huko,tunaomba serikali itusaidie kwani tunatamani kuona watoto wetu wanafika mbali na kutimiza ndoto walizonazo katika maisha yao,”alisema Mkimbizi Paulo Bandondee, 

Mwenyekiti wa kambi ya Nduta, Habarugira Godasi alisema wanatamani kurudi nchini kwao lakini kutokana na kupata taarifa ya kutokuwepo kwa amani wanashindwa kurudi. 

“Tunatamani kurudi nyumbani na kwenda kutumikia nchi yetu lakini hatuwezi kurudi mpaka tutakapo hakikishiwa kuwa kumetulia kwani vyombo vya habari vya nchini kwetu vinatangaza bado hali sio nzuri,”alisema Godasi.

Aidha Shimiriamana Erick ameiyomba serikali ya Tanzania kuwavumilia na kuwapa huduma kwa kipindi ambacho wanakaa katika nchi yao huku akidai kuwa kuna siku amani itapatikana nchini mwao na watarejea.

Mkuu wa kambi ya wakimbizi Nduta kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani (MHA), Barnabas Kipii , amewataka wakimbizi kufuata sheria zilizowekwa na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu. 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kibondo Luis Bula , Katibu tawala wa wilaya hiyo Ayubu Sebabili, amewataka wakimbizi wa Burundi kuwa tayari kurejea kwao kwa hiyari kwani wanazo taarifa kuwa ya kuwepo kwa amani."Niwaombe mashirika yanayohudumia wakimbizi kambini hapa kuangalia upya swala la kuwabadilishia chakula, kutoakana na kulalamika kuwa mmechoka kula ugali na njegele kila siku,”alisema Bula.

wakilishi wa UNHCR Barb Wigley alisema wanaishukuru serikali ya Tanzania na mkoa wa Kigoma kukubali kuwapokea na kuwapa hifadhi wakimbizi wa kutoka Burundi na Demokrasia ya Congo (DRC).

“Asilimia 80 ya ya wakimbizi wanaishi katika nchi za jirani na nchi zao, ni kazi kubwa ambayo nchi hizo zinazo wasaidia ikiwemo Tanzania ambayo imehifadhi wakimbizi 300,000 kutoka Burundi na DRC,”alisema Wigley.

 Wakimbizi kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma , wakiwa katika maandamano ya Maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani, yanayofanyika june 20 kila mwaka.picha zote na Moureen Rogath.
 

IGP SIRRO AZUNGUMZIA TAARIFA ZA KUWEPO HALI YA HATARI DAR ES SALAAM

ROSTAM AZIZI AFUNGUKA KUHUSU KLABU ZA MICHEZO KUMILIKIWA NA MTU BINAFSI

RC CHALAMILA AINGILIA KATI MGOGORO WA MADIWANI NA MKURUGENZI KYELA, ATAMKA MAZITO

MBUNGE KISHIMBA AIBANA SERIKALI 'MAITI KUTOZWA FEDHA' HOSPITALI

$
0
0
*Ataja sababu za wagonjwa kukimbilia kwa waganga wa kienyeji , aomba uwepo msamaha 

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MBUNGE wa Kahama Mjini, kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Jumanne Kishimba ameliambia Bunge anasikitishwa na tabia iliyopo kwenye hospitali za Serikali na zile za misheni ya mgonjwa anapofariki duniani kudaiwa deni la matibabu ndipo mwili uchukuliwe na ndugu.

Amefafanua kibaya zaidi ndugu wanapokuwa hawana fedha hizo, mwili wa marehemu unazuiliwa hadi deni lilipwe, hali ambayo ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Fedha kuangalia na ikiwezekana kufuta msamaha wa madeni ya matibabu.

Kishimba ameyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati anachangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ambapo amesema kuwa imefikia hatua ya miili ya marehemu kuzikwa na hospitali na kusababisha ndugu kutofahamu ilipozikwa maiti na wakati mwingine inazikwa kama mbwa.

Ameliambia Bunge kuwa wabunge walioko bungeni wote ni maiti na marehemu watarajiwa ila haijulikani muda wala saa.

 Wakati Kishimba anazungumza kuhusu hja yake, Naibu Spika Dk.Tulia Ackson alimtaka mbunge huyo kukaa chini na kisha akatangaza kumuongeza muda wa kuzungumza.

"Waheshimiwa wabunge kwa mujibu wa Kanuni ya 28 fasili ya tano naongeza muda wa 

nusu saa ili mheshimiwa Kishimba aweze kumaliza mchango wake,"alisema Dk.Tulia.

Hivyo wakati Kishimba anazungumza amesema kuwa "Ukiangalia kwenye bajeti yetu tumesamehe unga  wa keki, lakini tunatoza tozo la maiti kwenye mochwari. Nakuomba Waziri wa Fedha au Naibu Waziri wa Fedha, ebu rudisha hiyo kodi ya unga wa keki  ili tufute tozo la mochwari kwa maiti."

Amefafanua asilimia 95 ya vifo vinatokana na kuumwa na kuumwa kwenyewe mara nyingi 
kunakuwa ni kwa muda mrefu. Alisema mtu akiugua muda mrefu, anakuwa amedhoofika kiuchumi  na kiafya.

Ameongeza kwa kueleza kuwa leo hii mgonjwa anafariki hospitali inatoa bili ya Sh.500,000, anazipata wapi mheshimiwa 

Spika? Ameisha kufa na wachangiaji wengi humu wamesema, Watanzania wote wanalipa kodi, wanakunywa bia, wanavuta sigara...wanafanya shughuli zote.

Amehoji kwa nini Serikali isimsamehe bili mtu aliyefariki halafu hizo fedha zipelekwe katika keki na kwamba ni hatari na inaonekana  wanaotengeneza bajeti ni vijana waliopo 
Oysterbay."Nadhani walifikiri keki ni kitu cha maana sana wakashindwa kuelewa kuwa kuna shida nyingi kule kijijini.

"Naibu Spika alikuwa Kahama hivi karibuni na zile nyumba za nyasi ulizoziona ukiwa njiani ni za waganga wa kienyeji. Kwa waganga wa kienyeji ukipeleka mgonjwa na kwa bahati mbaya akafariki, hawaombi fedha. 

"Badala yake wanakusaidia kabisa na sanda. Inawezekanaje sisi Serikali tumdai mtu aliyefariki, halafu tukatalie maiti?" Amehoji na kuongeza; 

"Bahati mzuri Msigwa (Pater) ni mchungaji na Mama Rwakatare (Getrude)  wangetusaidia sana, maana yake turuhusu watu wakafanye maombi huko kwenye makaburi ya Serikali, watu wajue makaburi ya ndugu zao, baada ya miaka 10 watoto wakipata hela wakachukue mifupa ya wazazi wao wakazike upya."

Hivyo amesema hicho ni vizuri kikaangaliwa na Serikali kama ikiwezekana warudishe kodi ya unga wa keki. "Wanasema unga wa ngano unaotengeneza vyakula. Vyakula gani  mheshimiwa Naibu Spika? Ni keki na biskuti," amesema.

Mbunge huyo alichangia kuhusu mashine za X-ray na kusafisha figo ambapo amesema  daladala inauzwa kati ya Sh.milioni 50 hadi 100 kwa siku inaleta Sh. 50,000, Mashine ya X-ray  inauzwa Sh. milioni 40 hadi 100 mashine hiyo ikifanyakazi  kwa mgonjwa  kwa mgonjwa mmoja anatozwa kati ya sh. 100,000 hadi 200,000 kwa mtu mmoja.

Amehoji kama ni hivyo kwa nini Serikali isiruhusu watu binafsi wanunue X-Ray ili wazipeleke hospitali  ili gharama za X-Ray ipungue? Alisema anajua wataalamu wataleta maneno mengi ambayo yanahusu afya , lakini ni uongo kwani hata waganga wa kienyeji wanapewa kibali na Wizara ya Afya kuendesha shughuli zao na hawana elimu yoyote ya hospitali.

"Kule kwetu kanda ya ziwa, mgonjwa mahututi ndiye anapelekwa kwa mganga wa kienyeji 

ambapo hakuna choo, sasa iweje Serikali ikatae watu wanunue X-Ray wapeleke kwenye  hospitali?" Amehoji Kishimba.

Ameongeza kwenye nchi nyingine bili ya maji na umeme inamdhamini mtu hospitali na kwamba ikija bili ya maji na umeme, mamlaka husuka zinakaa  hospitali na kujadiliana namna ya kulipa deni la matibabu, hivyo watu wa hospitali wanaigiza madai yao humo na mtu anaanza kulipa kidogo kidogo.

"Mtu akilipa bili ya maji au umeme kinachukuliwa kiasi kidogo cha fedha kama ni  4,000 kinapelekwa hospitali, lakini mtu anakuwa amepona, kuliko sasa hivi kama hauna fedha ni tatizo sana,"amesema.

Hivyo amemtaka Waziri wa fedha kuliangalia hilo na kuhusu watu wasiokuwa na kadi za bima kukosa matibabu, Kishimba ameshaui hospitali zikubali hata kupokea kuku kutoka kwa wagonjwa ili mtu akishatibiwa zinauzwa ili kufidia gharama za matibabu.

"Wakati wakati wa mkutano wa Rais na wafanyabiashara kikubwa kilichokuwa kikilalamikiwa ilikuwa ni suala la uchunguzi baada ya mtu kuwa amemaliza kulipa kodi. Suala la kutafuta watu watakatifu yeye haliamini.

"Kwani hata dini ina miaka 2000 tangu Yesu aje, lakini watu hawajashika dini. Ili kumaliza mgogoro  unaosababisha matatizo TRA wanayo sheria inayohusu mtu ambaye  hakufanya mahesabu wamtoze kwa gharama ya mauzo, inawaruhusu wao kumchunguza yeye,"amesema.

Ameongeza Sheria hiyo iliachwa na mkoloni kwamba kama mtu hana vitabu analipa asilimia 2 ya mauzo yake, kwa hiyo kama mtu ameuza Sh. bilioni 1, asilimia mbili ni Sh. milioni 20.

"Hivyo kwa sababu asilimia 90 ya wafanyabiashara wa Tanzania elimu yao ni darasa la saba. wengine hawakusoma kabisa, inakuwa kazi ngumu sana utunze stoo ya mali, utunze stoo za karatasi na bado karatasi hizo hizo ukipeleka (TRA) unaambiwa hazifai,"amesema.

UBALOZI WA MAREKANI WAITWA WIZARA YA MAMBO YA NJE

Wengine wawili wajishindia tiketi za Tigo kushuhudia michuano AFCON

$
0
0

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael (kati kati) akiwa na washindi wa promosheni ya Soka la Afrika Emmanue Mushi kushoto na Sanga Massawe (kulia) muda mfupi baada ya kukabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya kwenda kuishangia timu ya Taifa, Taifa Starts kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri.

Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisae,l akimkabidhi Sanga Massawe ambaye ni mshindi wa droo ya pili ya promosheni ya Soka la Afrika stakabadhi ya kusafiria (boarding pass) kwa ajili ya kwenda kushuhudia michuoano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni hiyo inayoendelea.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisael (kati kati) akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuwakabidhi stakabadhi ya kusafiria (boarding pass) washindi wa droo ya pili ya promosheni ya Soka la Afrika watakaokwenda Misri kushuhudia michuano ya mataifa ya Afrika. Kushoto ni Sanga Massawe ambaye ni mshindi kutoka Moshi na kulia ni Emmanuel Mushi mshindi kutoka Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Tigo Woinde Shisae,l akimkabidhi Emmanuel Mushi ambaye ni mshindi wa droo ya pili ya promosheni ya Soka la Afrika stakabadhi ya kusafiria (boarding pass) kwa ajili ya kwenda kushuhudia michuoano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni hiyo inayoendelea.
 




Kupitia droo ya pili ya promosheni ya SOKA LA AFRIKA, kampuni ya Tigo imewatangaza washindi wengine wawili na kuwakabidhi tiketi za kwenda kushuhudia michuano ya Mataifa ya Afrika yanayofanyika nchini Misri na kufanya idadi ya washindi kuwa watano.

Washindi walioshinda tiketi katika droo ya pili ni Sanga Massawe kutoka Moshi Kilimanjaro na Emmanuel Mushi kutoka Dar es Salaam.

Mapema wiki iliyopita, Tigo iliwakabidhi tiketi washindi watatu katika droo ya kwanza ya promosheni hiyo. Washindi wa droo ya kwanza ni Kalaghe Rashid na Godfrey Muta kutoka Dar es Salaam na Rehema Kassim kutoka Tanga.

Kupitia Promosheni ya Soka la Afrika, wateja wa Tigo wanayo nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Misri kushuhudia michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika pamoja na fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 50.

Kupitia promosheni hii, wateja 10 wa Tigo wataweza kujishindia tiketi za kwenda kushuhudia mashindano haya makubwa barani Afrika, ambapo timu ya taifa, Taifa Stars nayo itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.

Ili wateja waweze kushiriki katika promosheni hii ya SOKA LA AFRIKA na kujipatia nafasi ya kuwa mamilionea pamoja na kushinda tiketi, watatakiwa kutuma neno SOKA kwenda 15670 au kutembelea tovuti ya www.tigosports.co.tz ili kuweza kujibu maswali yanayoihusu mashindano hayo yanayofanyika nchini Misri.

SOKA LA AFRIKA ipo mahususi kwa ajili ya kuwazawadia wateja waaminifu wa Tigo ambao siku zote wamekuwa mstari wa mbele kutumia bidhaa na huduma za kampuni hiyo.

Fainali za Mataifa ya Afrika, ni mashindano makubwa kuliko yote barani Afrika ambayo yanawaleta pamoja wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki ligi kubwa na zenye ushindani ndani na nje ya bara la Afrika.

Zaidi ya wateja mia moja watashinda fedha kila siku, kila wiki na kila mwezi kwa muda wa miezi mitatu na kadiri mteja anapojibu maswali, ndivyo anavyozidi kujiongezea pointi na nafasi kubwa zaidi ya kushinda tiketi kwenda Misri au mamilioni ya pesa.

PSPTB YAJIZATITI KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA KWA KUZINGATIA MISINGI YA UFANISI NA MAADILI

$
0
0
* Washauriwa utumiaji wa dawati la ushauri na maoni kuwa endelevu ili kujenga uadilifu na ufanisi kwa wafanyakazi

KATIKA kuadhimisha wiki ya utumishi kwa Umma bodi ya wataalamu wa manunuzi na ugavi nchini (PSPTB) imeendelea kuadhimisha wiki hiyo kwa kutoa huduma na kusikiliza maoni na kero mbalimbali kutoka kwa wateja wao.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wateja, Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa wiki ya utumishi kwa Umma  mwaka huu imeanza tarehe 17 na itafikia kikomo tarehe 23 mwezi huu, na taasisi zote za serikali zimepata nafasi ya kusikiliza changamoto za wateja ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa ukaribu zaidi.

Amesema kuwa kupitia nafasi yake ya kaimu mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo wameandaa dawati maaalumu ambalo maafisa wa sekta husika za ununuzi na ugavi watakuwepo na baada ya kuhudumiwa watapita katika dawati na kueleza namna walivyohudumiwa na changamoto wanazozipata ili ziweze kutatuliwa.

Amesema kuwa maoni yote yatakayotolewa na wananchi na wateja yatafanyiwa kazi na bodi ya wataalamu ya ununuzi na ugavi na watahakikisha maeneo yote ya ununuzi na ugavi yanafanyiwa kazi kwa umakini na kuhakikisha uaminifu na uadilifu kwa wafanyakazi unazingatiwa.

Kuhusiana na namna huduma zinavyotolewa katika bodi hiyo Mbanyi amesema kuwa; wakati wote wa utoaji huduma wamekuwa na kitengo maalumu cha usiri ambacho wateja hupita mara baada ya kupata huduma na kutoa maoni na kero zao.

Aidha amesema kuwa wamedhamiria na watahakikisha wanafanya kazi kwa manufaa ya taifa na kusema kuwa watashirikiana na wizara washirika katika kuhakikisha azma ya taifa inafanikiwa.

Vilevile amesema kuwa wataalamu wanaosomea fani hiyo ya manunuzi na ugavi wanawatambua kupitia usajili na na kwa kushirikiana na wizara ya fedha na mipango na ofisi ya Rais utumishi katika kuhakikisha suala la ajira kwa wataalamu wa fani hiyo linatekelezwa kwa urahisi.

Kwa upande wake Eliakim Paul ambaye pia ni mteja wa bodi hiyo amesema kuwa dawati hilo la maoni na ushauri lisiwe kwa kipindi cha wiki ya utumishi kwa Umma bali liwe endelevu ili waweze kupokea maoni ya wateja na kuyafanyia kazi kwa wakati.

Na ameeleza kuwa uwepo wa dawati hilo kila siku pia utaongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa wafanyakazi wa bodi hiyo.
 Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi (kushoto) akizungumza na wateja waliofika katika ofisi ya Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi kwa ajili ya kupewa huduma wakati wa wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza terehe  Juni 17 hadi  juni 23 mwaka huu.
 Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya wataalumu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi  akiwaonesha wateja wao namna wanavyofanya kazi katika ofisi hiyo wakati wa wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza terehe  Juni 17 hadi  Juni 23 mwaka huu. 
Afisa mwandamiza Masoko na mahusiano kwa Umma wa Bodi ya wataalamu wa Manunuzi na Ugavi (PSPTB), Shamim Ally Mdee(katikati) akimsikiliza mteja alipofika kwenye dawati la ushauri na maoni ili kusikiliza kero na changamoto wanazozipata wanapopewa huduma wakati wa wiki ya Utumishi wa Umma. Kulia ni Afisa Mipango ( PSPTB), James Maghori 

Katibu Mkuu: Kampeni ya marufuku ya mifuko ya plastiki inaenda vizuri

$
0
0
Serikali imesema kampeni ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki inakwenda vizuri na kusisitiza ni makosa kisheria kubadili matumizi ya vifungashio vya bidhaa maalumu na kutumika kama mifuko ya kubebea bidhaa mbalimbali huku.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amebainisha hayo leo  jijini Dodoma alipozungumzia azma ya Serikali ya kuendesha operesheni maalumu nchi nzima ya uzingatiaji wa sheria ya usimamizi wa mazingira juu ya marufuku ya mifuko ya plastiki na matumizi endelevu ya mifuko mbadala.

Alisema adhabu stahiki zitatolewa kwa watengenezaji, waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa vifungashio vya plastiki vilivyozalishwa ama kuingizwa nchini na kutumika kama vibebeo vya bidhaa.

"Baada ya kuanza kwa utekelezaji wa Katazo la Kutumia mifuko ya Plastiki imebainika kuwa baadhi ya wazalishaji na wasambazaji wamebadilisha matumizi ya mifuko laini ya plastiki isiyokuwa na mishikio na kuitumia kama vibebeo vya bidhaa," alisema Mhandisi Malongo.
Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na kikosi kazi inaendelea na zoezi la kuelimisha umma juu ya jambo hili pamoja na kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala.

Kwa mujibu wa Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki za Mwaka 2019, ni marufuku kuzalisha, kuingiza nchini, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki iliyotajwa katika Katazo hili. 

Alisema Kanuni ya 9 inatoa msamaha kwa baadhi ya vifungashio vya plastiki kwa ajili ya huduma za afya au ambavyo vinatumika kwenye kufungashia bidhaa za viwandani, sekta ya ujenzi, sekta ya kilimo, vyakula au usafi na udhibiti wa taka. 
"Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaanda viwango kwa vifungashio hivi ambavyo vitalazimisha kiwango cha unene, uwekwaji lakiri na kutambulisha bidhaa iliyofungashwa kabla ya kuuzwa," alisema.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (katikati) akifafanua kuhusu vifungashio alipozungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)jijini Dodoma. Wengine pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine na Mkurugenzi Mkuu Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akionesha baadhi ya viungashio vinavyotumika kwa matumizi ya kubebea bidhaa nyingine tofauti na inayotakiwa.
 Naibu Katibu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akionesha mfuko mbadala unaoruhusiwa kubebea.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akionesha kifungashio kilichofungwa nyama bila kukidhi vigezo vinavyotwakiwa.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais kufafanua nkuhusu vifungashio. 

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angela Kairuki, Bungeni jijini Dodoma Juni 20, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, Bungeni jijini Dodoma Juni 20, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, Bungeni jijini Dodoma Juni 20, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Bungeni jijini Dodoma, Juni 20, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images