Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109591 articles
Browse latest View live

TASAF KUVINOA VIKUNDI VYA WANUFAIKA KUHUSU KUWEKA AKIBA NA KUKUZA UCHUMI

0
0

Wataalamu kutoka TASAF wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji kutoka Halmashauri ya Mji Njombe
Sehemu ya Wawezeshaji wakifuatilia kwa makini mada zinazotolewa juu ya uwekaji akiba na ukuzaji uchumi kwa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini
Kaimu Meneja wa Miradi kutoka TASAF Ndg. Abdulmalik akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo wawezeshaji kuhusu mpango wa kuhamasisha jamii kuweka akiba na kukuza uchumi
Wawezeshaji wakifuatilia mada
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Thadei Luoga akifungua mafunzo kwa wawezeshaji kuhusu kuhamasisha wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini TASAF III kuweka akiba na kukuza uchumi.Kushoto kwakwe ni Mratibu wa TASAF ngazi ya Halmashauri Peter Magehema akifuatiwa na Afisa Ufuatiliaji wa TASAF ngazi ya Halmashauri Revocatus Rugeiyamu

……………………
Hyasinta Kissima-Afisa Habari H/Mji Njombe
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini TASAF umeendelea kuwawezesha wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia mpango wa kuweka akiba na kukuza uchumi lengo ikiwa ni kuhamasisha walengwa kuunda vikundi na kuimarisha uchumi wa kaya zao.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwajengea uwezo wawezeshaji ngazi ya Halmashauri kuhusu uhamasishaji wa uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndg. Thadei Luoga amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na ni vyema washiriki wakaelewa na kwenda kuwafundisha wanufaika ipasavyo ili waweze kuondokana na wimbi la umaskini.

“Wapo ambao wamekuwa wakibeza kuwa programu hii haichangii chochote. Hii sio kweli. Wananchi wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali za maendeleo lakini wakati mwingine kwa kukosa uelewa wa namna ya kuweka akiba na kutunza kumbukumbu zao wamekuwa wakiishia kwenye wimbi la umaskini wa kipato au lishe. 

TASAF wanatujengea uwezo ili tuweze kuwapelekea wanufaika na waweze kufanyia kazi.”Alisema Luoga
Thomas Mwakagali ambaye ni Mwezeshaji ngazi ya Halmashauri kutoka Kata ya Makowo amesema kuwa TASAF imekuwa ikitoa mafunzo hayo mara kwa mara lengo ikiwa ni kuwakumbusha wanufaika wa mpango wa TASAF kutengeneza vikundi ambavyo kupitia fedha za ruzuku wanazopokea kuweza kuweka akiba kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

“Tumekuwa tukitoa elimu hii kwa wanufaika. Kupitia fedha za ruzuku tumekuwa tukiwahamasisha juu ya uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba na kukuza uchumi. Kupitia fedha ambazo wamekuwa wakipokea kila baada ya miezi miwili ambapo wapo walengwa wanaopokea kiasi cha Shilingi elfu ishirini, wengine thelathini ni kiasi kidogo lakini elimu hii imewajenge nidhamu ya kutunza na kuweka akiba ambapo mpaka sasa tunavikundi vyenye milioni tano, milioni mbili. Haya yote ni manufaa ya elimu hii ya akiba.”Alisema Mwakagali.

Halmashauri ya Mji Njombe ina jumla ya wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini 3381 ambapo jumla ya vikundi 123 vya akiba vimeshaundwa na kupatiwa masanduku ya kuhifadhia hela na shajara mbalimbali.

HOTELI YA HYATT REGENCY YATOA SEMINA YA UELEWA WA BIASHARA NA UCHUMI

0
0

* Yawakutanisha wajasiriamali, wanafunzi na wafanyabiashara na kuwajengea ujuzi kuhusiana na masuala ya mauzo, masoko pamoja na teknolojia.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UWEZESHAJI wa kiuchumi kwa wananchi kwa kuwapa maarifa mapya na namna bora ya kufanya biashara yameelezwa kuwa ni nyenzo muhimu ya kujenga uchumi imara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya mafunzo yaliyowakutanisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wadau na wanafunzi Mkurugenzi wa mauzo na masoko Afrika Mashariki kutoka hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam Denis Glibiv Cluster amesema semina hiyo iliyowakutanisha wanajamii na wataalamu imelenga  vitu 4 muhimu katika biashara ikiwemo mauzo, na masoko na namna bora ya kutumia teknolojia.

Ameeleza kuwa wamewaleta wataalamu kutoa nje (Dubai na Afrika Kusini) na wataalamu wa ndani ya nchi  kwa malengo ya kujenga jamii ya kibiashara na kueleza kuwa wamepata matokeo chanya kutoka kwa washiriki 70 na mkutano ujao utakaofanyika mwezi Novemba wataongeza idadi kubwa ya washiriki ili ujumbe kuhusiana na biashara na uchumi uweze kufika kwa wananchi kote nchini.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano na masoko wa hoteli hiyo Lilian Kisasa amesema kuwa semina hiyo imefanywa kwa majadiliano na vitendo na hiyo ni baada ya kuona kuna tofauti kubwa kati ya teknolojia na wafanyabiashara hivyo wakaona ni vyema kuwaalika wadau hao ili kutoa fursa kuhusiana na maarifa ya kiuchumi.

Amesema kuwa watu wengi hawajawa na uelewa juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa ndio njia bora kukuza biashara na sio kwa burudani pekee na wana imani kuwa baada ya mafunzo hayo washiriki watakuwa mabalozi kwa wengine.

"Ni mkutano wa kwanza kuufanya na umelenga kuwekeza katika biashara, uchumi na teknolojia kwa wajasiriamali, wanafunzi na wafanyabiashara  na wataalamu waliotoa mafunzo hayo kwa kada mbalimbali wametoka hapa nchini na nje ya nchi na hiyo yote ni kwa malengo ya kujifunza mambo mapya kwa wakati huu wa mapinduzi ya kiteknolojia" ameeleza Lilian. 

Pia amesema kuwa  kitu cha tofauti walichoona kutoka kwa washiriki ni  kufurahia kwa kushiriki na kujifunza vitu vipya huku
 akisema kuwa watakutana tena na wadau hao mwezi Novemba mwaka huu ili kuendelea kujenga uelewa zaidi kuhusiana na biashara ukuaji wa uchumi.
 Mkurugenzi wa mauzo na masoko Afrika Mashariki kutoka hoteli ya Hyatt Regency Denis Glibic Cluster akizungunza wakati wa semina hiyo iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa biashara na uchumi pamoja na wanafunzi,  jijini Dar es Salaam.
 Washiriki mbalimbali wakisikiliza mafunzo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa semina hiyo,  jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa semina hiyo jijini Dar es Salaam.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTOA TAARIFA PINDI WANAPOFUNGA BIASHARA ZAO KUPUNGUZA MLUNDIKANO WA MADENI

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 
Imebainika kuwa ilikukwepa mdeni mbalimbali ya kodi pamoja na Tozo wananchi wanatakiwa kutoa taarifa katika vyombo husika pindi tu wanapo funga biashara Zao Hayo yamesemwa wakati Wakala wa usajili wa biashara na leseni nchini( BRELA) walipowakutanisha wadau mbalimbali wa biashara Mkoani Arusha, lengo likiwa ni kuwapa mwongozo wa kampuni kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao( ORS) 
Akizungumza wakati wa semina inayoendelea Jijini Arusha Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Tanzania Bakari Ally Mketo amesema kuwa kuna umuhimu wa kutambulisha Mfumo huo kwa wafanyabiashara ili kuweza kufanya Kazi kwa uweledi na ufanisi 
Aidha amesema kuwa mwamko wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao. 
 Alibainisha kuwa hatua hiyo ni mzuri kwa sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani wafanyabiashara walivyokuwa mstari kujisajili kupitia wakala huu na kuweza kutambulika ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni hayo 62 kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni yatakayojisajili 
 "Malengo yetu ni kuhakikisha tunapanua wigo mpana na kufikia idadi ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha kila mdau wao anafikia na huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia mzigo mzito mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo"alisema Mketo 
 Nao baadhi Ya wafanyabiashara waliyohudhuria kwenye semina hiyo akiwemo Privanus Saimon na John Tasha wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizonazo hivyo watafanya maboresho ya leseni zao ili waweze kuendesha makampuni yao kwa uhuru 
 Walisema kuwa kabla ya semina hiyo walikuwa hawafahamu mambo mengi lakini tangu wapewe mafunzo hayo wameelewa na wamejua umuimu wa kusajili majina yao ya biashara pamoja na kubaini faida zakutoa taarifa Kwa mamlaka husika pindi wanapo funga biashara Zao 
 Alisema kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa hawajui faida za kutoa taarifa pindi wanapofunga biashara zao, kwani wamekuwa hawana elimu juu ya faida na hasara za kutoa elimu hivyo waliomba brela kuendelea kutoa elimu ili wananchi wengine ambao hawajui waweze kufahamu Waliiomba serikali kufuta madeni yote ya nyuma ambayo wananchi hao ambao ni wafanyabiashara waliokuwa wamesajili majina yao brela na teari wamefunga biashara lakini hawakutoa taarifa katika vyombo husika kitendo kilichowapelekea kuwa na mlimbikano wa madeni makubwa na mengi ili waweze kuanza upya kwani kwasasa wamepewa elimu na wataendelea kuwapa elimu wefanya biashara wengine 
"Unajua unakuta mfanyabiashara kama Mimi nimesajili biashara yangu au jina la biashara brela ,nikasajili mamlaka yamapato na nimeendesha biashara mwishowe nikafunga labda kutokana nakukosa mtaji wa biashara au la nanilipofunga sikuwa najua kuwa natakiwa kutoa taarifa kitendo kinachonipelekea kulimbukiwa madeni kila siku na Mimi sijui kama nilivyofunga nilitakiwa kutoa taarifa kitu ambacho nichangamoto kubwa sana kwangu na yote hii imesababisha kutokana na awali kutokuwa na elimu "John Tasha 
Kwa upande wake mmiliki ubunifu wa BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo amesema mfumo huo utasaidia kukamilisha usajili kwa haraka na kupunguza gharama kubwa ambazo wafanyabiashara walikuwa wanatumia 
"Katika mfumo wa OBS wananchi haswa wa mkoani hususa ni Arusha walikuwa wanatumia mda mwingi mpaka kusajili pia walikuwa wanatumia fedha nyingi sana kwani walikuwa mpaka wasafiri ndio wasajiliwe lakini kwa mfumo huu mpya wa ORS ambao ni mfumo ambao Mwananchi ambaye ni mfanya biashara atajisajili kupitia njia ya mtandao "alisema Suzana 
“Kwa kweli niwaambie wakazi wa mkoa huu wa Arusha na mikoa ya jirani wachangamkie fursa hii ya kuweza kutumia muda huu kuweza kusajili majina ya biashara zao, makampuni na nembo lakini pia leseni daraja A zililokuwa zinasajiliwa Wizara zimerudishwa kwetu na hivyo pia wanasajili iwapo walengwa watakidhi vigezo vilivyowekwa 
“Alisema Aidha alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kusajili ili kuweza kusajili kampuni lakini lazima vigezo na masharti husika vinavyohitajika kwenye upatikanaji wa leseni hiyolazimauzingatiwe Alisema kuwa kwakufanya hivyo kutawasaidia kuongeza kiwango cha biashara Zai kwani akiwa amesajili jina na kampuni itakuwa inatambulika kimataifa zaidi.

 Mmiliki ubunifu wa  BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo akitoa Elimu kwa washiriki hao. 

Mmiliki ubunifu wa  BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo akitoa Elimu kwa washiriki hao. 

  Washiriki wakifuatilia mafunzo kwa makini
 Mkurugenzi wa fedha na utawala Tanzania Bakari Ally Mketo akiongea na waandishi WA habari katika semina hiyo

MAHAKAMA YASHINDWA KUENDELEA NA KESI YA UCHOCHEZI YA ZITTO KABWE

0
0

Na Karama Kenyunko, Blobu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa sababu upande wa mashitaka umekosa kibali cha kuita mashahidi kutoka mkoani Kigoma.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga  amebainisha hayo leo Juni 17, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokija kwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, wakili Katuga akadai, shauri hilo lilipangwa kusikilizwa na walishaanza utaratibu wa kupata mashahidi kutokea mkoani Kigoma lakini wamekosa kibali kutoka kwa Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu.

Kufuatia hivyo, Wakili Katuga ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo wakati wakifatilia kibali hicho ili wawapate mashahidi hao ambao ni takribani sita kutokea mkoani Kigoma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 16 na 17, 2019.

Katika kesi ya msingi, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

JESHI LA POLISI PWANI LAWASHIKILIA WATUMISHI SABA WA NIDA KWA TUHUMA ZA WIZI WA VIFAA NA VITAMBULISHO.

0
0

NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

WATUMISHI Saba wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Pwani, wakidaiwa kuiba raslimali vifaa vyenye thamani ya sh.mil.15 ambavyo walikuwa wakivichepusha ,kisha kuuza kwa maslahi yao binafsi.

Kati ya watumishi hao walipopekuliwa kwenye makazi yao ,pia walikutwa na vitambulisho vya Taifa boksi moja ambalo ndani vimo vitambulisho 15,000 pamoja na komputa mpakato mbili na nyaya za komputa.

Akielezea juu ya tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP) Wankyo Nyigesa alisema ,kati ya watuhumiwa hao wanaodaiwa kufanya tuhuma hizo sita ni wanaume na mmoja mwanamke ambapo majina yao yanehifadhiwa kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo,kamanda huyo alibainisha,taarifa za tukio hilo zilipokelewa kutoka kwa uongozi wa juu wa NIDA kwenda jeshi la polisi mkoa Juni 14 mwaka huu na mara moja lilifuatilia na kuwakamata watuhumiwa saba na gari T.365 DFS aina ya Toyota spacio rangi ya silver ambayo ilikuwa imebeba jenereta moja mali ya NIDA.

“Awali watumishi wa NIDA waliokuwa wanafanya kazi mkoani hapo walikuwa wanatumia ofisi za kilipokuwa kiwanda cha kubangua korosho TANITA KwaMatias Kibaha na baadae serikali iliwajengea ofisi mpya za kisasa eneo la Machinjioni huko Loliondo Mjini Kibaha.”

“:Baaada ya majengo kukamilika walitakiwa kuhamia katika ofisi hizo mpya wao wenyewe na vitendea kazi vyao kama komputa,meza,scanner,camera,stationaries,BVR kits na vingine”alifafanua Wankyo.

Wankyo alielezea,watumishi wanaoshikiliwa na polisi waliteuliwa na uongozi wa mamlaka hiyo kuhamisha raslimali vifaa kutoka TANITA kwenda Loliondo ambapo wakiwa njiani walikosa uaminifu na kuanza kuvichepusha ,kuviuza na kujipatia pesa kwa manufaa yao binafsi .

Wankyo alitoa rai kwa watumishi wa umma , taasisi na mashirika ya watu binafsi wanapokabidhiwa madaraka na mali za serikali wawe waaminifu ,watiifu kwa kuzilinda kama mboni ya jicho lao na amekemea kuacha ubadhilifu wa mali za umma kwa maslahi ya matumbo yao.





OFISI YA MAKAMU WA RAIS KUSHIRIKI MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais imeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16 hadi Juni 23 mwaka huu kwa kutoa elimu kwa wananchi na kushiriki shughuli za kijamii. 

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Samuel Mwashambwa amesema shughuli mbalimbali za kutoa elimu kuhusu masuala ya Muungano na Mazingira zimeanza kufanyika kupitia vyombo vya habari. 

Mwashambwa alisema tathmini ya kampeni ya marufuku ya mifuko ya plastiki na masuala yanayotakiwa kufanyika baada ya hatua hiyo pamoja na kuendeleza kampeni ya matumizi ya mifuko mbadala imeanza kufanyika. 

Aliongeza kuwa wananchi wataelimishwa kuhusu aina za mifuko mbadala yenye ubora unaotakiwa kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa miongozo. 

"Katika kwenda sambamba na sera ya viwanda wananchi watapata wasaa wa kufahamu tathmini ya athari kwa mazingira ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafanikiwa na pia wataelimishwa kuhusu wajibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa pamoja na bidhaa au viumbe watokanao na teknolojia hii," alisema. 

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo, Wiki ya Utumishi wa Umma itatumika katika kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano kwa ujumla ikiwemo mafanikio katika kuondoa changamoto zake. 

Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma hivyo aliwataka wananchi waendelee kufuatilia vyombo mbalimbali vya habai kupata elimu. 

Kwa mwaka huu kauli mbiu ni Uhusiano kati ya Uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji; Kujemga Utamadni wa Utawala Bora, Matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utaoaji Huudma Jumuishi.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Samuel Mwashambwa 

Article 1

0
0
Serikali ya Tanzania imehimizwa kuridhia mkataba wa shirika la kazi duniani (ILO) namba 189 uliosainiwa Juni 16, 2011 kwa lengo la kuhimiza maslahi na kazi zenye staha kwa wafanyakazi wa nyumbani duniani.


Kwa mantiki hiyo, nchi zilizoridhia mkataba huo zinaingia kwenye utekelezaji wa maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani duniani na hivyo kutoa fursa ya kuihamasisha jamii kulinda na kuheshimu nafasi ya mfanyakazi huyo muhimu katika jamii.


Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, shirika la kutetea haki za wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) lenye makazi yake jijini Mwanza, limeadhimisha maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani yaliyofanyika katika viunga vya Kishimba jumapili Juni 16, 2019.


Akizungumzia maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa shirika hilo, Angel Benedicto alisema ni wakati mwafaka sasa Serikali ya Tanzania kuridhia mkataba huo ili kuitambua rasmi Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani na kuiadhimisha ili kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kulinda maslahi ya kada hiyo tofauti na ilivyo kwa baadhi ya maeneo ambapo bado wafanyakazi wa nyumbani wanakumbana na changamoto kadhaa ikiwemo maslahi duni.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiingia kwenye viunga vya Kishimba kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani Duniani 2019.
Wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakionyesha jumbe mbalimbali kupitia mabango.
Wageni waalikwa meza kuu wakisoma jumbe mbalimbali kupitia mabango ya wafanyakazi wanyumbaji jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza walihimiza kulipwa ujira wao kwa wakati na kwa mujibu wa sheria ambapo kima cha chini ni shilingi elfu 40 kwa mwezi.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa nyumbani wakifuatilia maadhimisho hayo.
Jamii inahimizwa kutowaajiri watoto kufanya kazi za nyumbani na badala yake kuwapa fursa ya kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu.
Baadhi ya wazazi na walezi (waajiri) wa watoto wafanyakazi wa nyumbani jijini Mwanza wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za watoto wafanyakazi wa nyumbani (WoteSawa), Angel Benedicto akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mfanyakazi wa Nyumbani yaliyoandaliwa na shirika hilo jijini Mwanza.
Tazama Vidio hapa chini

Wafanyakazi wa Nyumbani Mwanza wasisitiza maslahi yao kuzingatiwa
Waajiri wajitokeza kuhimiza haki za wafanyakazi wa nyumbani

NAIBU KAMISHNA MKUU TRA ATEMBELEA BANDARI KAVU

0
0
Na Veronica Kazimoto

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo ametembelea bandari kavu ya Said Bakhresa (SSB-ICD) na African ICD ambapo amewataka Maofisa Forodha wa Mamlaka hiyo kuzingatia uwajibikaji, weledi na uadilifu wakati wote wanapotimiza majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza na maofisa hao kabla ya kukagua mizigo iliyopo katika bandari hizo, Naibu Kamishna Mkuu huyo amesema kwamba, uzingatiaji wa maadili katika sehemu za kazi utasaidia kuondoa malalamiko na kero kwa walipakodi ambao ni wadau wakuu wa TRA.

“Jukumu la kujenga taswira ya mamlaka ni la kila mtumishi wa TRA. Hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anafanya kazi bila upendeleo, anawajali wateja ikiwa ni pamoja na kutumia lugha yenye staha, alisema Naibu Kaimshna Mkuu Mbibo.

Kwa upande wake Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje amewasisitiza watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaichafua Mamlaka ya Mapato Tanzania.

“Sote humu ndani tunajua kuwa, kupokea au kutoa rushwa ni kinyume cha sheria ya nchi yetu na yeyote atakayebainika akifanya hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Hivyo, hakikisheni mnaepuka kabisa vitendo hivyo vya rushwa kwani vitawasababishia kupoteza kazi na kufikishwa mahakamani”, alisema Usaje. 

Baadhi ya majukumu ya Ofisi za Forodha zilizopo katika bandari kavu hapa nchini ni kuhakikisha kuwa taratibu zote za kuingiza mizigo ndani ya nchi zinafuatwa pamoja na kuhakikisha kwamba kodi stahiki inalipwa na wenye mizigo kabla ya kutoa mizigo yao katika bandari hizo.
 Meneja wa Bandari Kavu ya African ICD, Abeid Said (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu bandari hiyo kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo (wa pili kushoto aliyevaa tai ya mistali) wakati alipotembelea bandarini hapo.
 Afisa Forodha Mfawidhi wa Bandari Kavu ya African ICD, Brian Japheth akitoa maelezo juu ya mizigo iliyopo bandarini hapo kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo (wa pili kulia) wakati alipoitembelea bandari hiyo. Kushoto kwake ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje.
 Afisa Forodha Mfawidhi wa Bandari Kavu ya Said Bakhresa (SSB-ICD), Caleb Mwangalaba akitoa maelezo mafupi kuhusu bandari hiyo kwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo (kushoto) wakati alipoitembelea bandari hiyo kuona jinsi inavyofanya kazi.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Msafiri Mbibo (aliyevaa tai ya mistali) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Forodha waliopo katika bandari kavu ya African ICD wakati alipoitembelea bandari hiyo. Kushoto kwa Naibu Kamishna Mkuu ni Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa, Ben Usaje na kulia kwake ni Naibu Kamishna wa Biashara na Uwezeshaji, Godfrey Kitundu.  

Waziri Mohamed akagua eneo mbadala la Kuzika watu lililopo Kijiji cha Kama

0
0
 Eneo la kuzikia Watu liliyopo katika Kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi “A”. ambalo litachukuwa nafasi mbadala ya lile lililozoeleka la Mwanakwerekwe.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed Kati kati pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi yake Nd. Abdulla Hassan Mitawi kulia yake na Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Khatib wakilikagua eneo hilo.

   Waziri Aboud akiuagiza Uongozi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar kumalizia kulisafisha eneo hilo la makaburi liliopo Kama.

 Baadhi ya Makaburi ya Watu waliokufa kutokana na Maafa ya kuzama kwa Meli za M.V Spice Islander na M.V Skagit yaliyopo katika Kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi “A”.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Khatibu Makame akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri Aboud kulikagua eneo la Makaburi la Kama. Picha na – OMPR – ZNZ.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed amefanya ziara ya kulikagua eneo mbadala la kuzikia Watu liliyopo katika Kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi “A”.

Eneo hilo la Makaburi ya Watu waliofariki kutokana na Maafa ya kuzama kwa Meli ya M.V. Spice Islander mnamo Tarehe 10 Septemba Mwaka 2011 na M.V Skagit Mnamo Tarehe 18 Julai Mwaka 2012 limetengwa maalum kufuatia lile lililozoeleka la Mwanakwerekwe kujaa Makaburi.

Mh. Mohamed Aboud Mohamed akiambatana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdullah Hassan Mitawi alisema Uongozi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar unapaswa kusimamia usafishaji wa eneo hilo pamoja na kukamilisha kazi zilizobakia.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshatoa maelekezo ya kutumiwa eneo hilo la kama kwa vile Mwanakwerekwe hivi sasa kumekuwa na msongamano mkubwa wa Makaburi hali inayoweza kusababisha baadae kuharibika kwa yale yaliyopo.

Waziri Aboud hata hivyo alifahamisha kwamba bado upo umuhimu wa mahitaji ya kuongezwa kwa ukubwa zaidi wa eneo la kuzikia ili liweze kukidhi mahitaji kwa kipindi kirefu kama ilivyokuwa Mwanakwerekwe.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Makame Khatibu Makame alisema eneo hilo tayari limeshatumika kuzikiwa Watu 80 waliokufa kutokana na Maafa ya kuzama kwa Meli za M.V Spice Islander na M.V Skagit.

Ndugu Makame alisema uzikwaji wa Watu hao ambao wapo waliotambuliwa na jamaa zao na kutoa idhini pamoja na wale wasiotambulika umefanywa kwa kuzingatia tofauti ya Imani za Dini zao.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar alifahamisha kwamba katika kukamilisha vyema eneo hilo yapo mambo ya muhimu yanayostahiki kujengwa kama Msikiti na sehemu ya kuoshea Maiti.

TAMUFO yampongeza Dk Ritta Kabati

0
0
TAASISI ya Sanaa na Utamaduni ya Tanzania Music Foundations (TAMUFO) imempongeza mlezi wake Ritta Kabati kutunukiwa udaktari wa heshima kutoka Chuo Kikuu cha Afrika. Kwa mujibu wa Rais wa Tamufo, Dk Donald Kisanga wanatoa shukrani za pekee kwa mlezi wao huyo ambaye mchango wake katika maendeleo ya jamii ikiwemo Tamufo ni wa kupigiwa mfano.

Kisanga alisema umahiri wa Dk Kabati umesababisha kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum, hivyo wanatoa wito kwa jamii ya Tanzania kuitumia ipasavyo heshima aliyoipata mwanamama huyo. "Sisi Tamufo tunapongeza uteuzi wa Dk. Kabati kwani unaendana na anayoyafanya katika jamii hususani sisi wasanii ambao tumejipanga kukua na kuendeleza kazi zetu," alisema Dk Kisanga.

Aidha Dk Kisanga alisema kutokana na ushirikiano ulio bora kati ya Tamufo na Dk Kabati, nyanja ya sanaa hapa nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla itapiga hatua zaidi ya ilivyo sasa. Mahafali ya kutunukiwa tuzo hiyo ya Udaktari yalifanyika Juni 15 jijini Lusaka Zambia ambako mahafali yake yalipambwa na bendi mahiri zilizokuwa zikiimba nyimbo mbalimbali ukiwemo wimbo wa Taifa la Tanzania.

Ritta Kabati alipata tuzo hiyo kutokana na mchango wake katika jamii ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa.
 Rais wa Tamufo, Dk Donald Kisanga akimpongeza Ritta Kabati baada ya kutunukiwa udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Afrika.
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akipongezwa na Katibu Mkuu wa Tamufo, Stella Joel.

Dar, Mwanza zatinga nusu fainali UMISSETA 2019 soka wasichana

0
0
Na Mathew Kwembe, Mtwara,
Timu za soka wasichana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Iringa na Ruvuma zimetinga hatua ya nusu fainali baada ya jana kufanikiwa kuwalaza wapinzani wao katika hatua ya robo fainali iliyofanyika katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa saa 8 mchana jana, timu ya soka ya wasichana ya mkoa wa Dar es salaam iliifunga timu ya mkoa wa Lindi kwa magoli 5 kwa 0, Iringa iliichapa timu ya Morogoro 3 kwa 1, Mwanza waliitoa Tabora kupitia mikwaju ya penati 3 kwa 2 baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja, huku Kilimanjaro pia nayo ilitolewa kwa penati 4 kwa 3 baada ya kutoka suluhu ya kutofungana ndani ya dakika 90 za mchezo.

Kufuatia matokeo hayo timu ya mkoa wa Dar es salaam wasichana itamenyana na Iringa katika hatua ya nusu fainali inayotarajiwa kuchezwa kesho  saa 2 asubuhi na kufuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali ambao utawakutanisha Mwanza watakaochuana na Ruvuma.

Kwa upande wa mpira wa kikapu wasichana, mechi za robo fainali zilitarajiwa kuchezwa leo ambapo timu nane zilizotinga nusu fainali ni Morogoro ambayo itachuana na Singida, Dar es salaam wamepangwa kukutana na Dodoma, Mwanza wamepangwa kucheza na Tabora na Arusha watamenyana na jirani zao Kilimanjaro

Timu zilizofuzu hatua ya robo fainali na ambazo zinatarajiwa kuchuana leo kwa upande wa mpira wa kikapu wavulana ni pamoja na timu kutoka mkoa wa Pwani ambao wamepangwa kucheza na Mbeya, Unguja watacheza na Arusha, Dar es salaam watachuana na Tanga na Morogoro wamepangwa kucheza na timu kutoka mkoa wa Shinyanga.

Washindi wa mechi za leo katika mpira wa kikapu kwa wavulana na wasichana wanatarajiwa kucheza kesho katika hatua ya nusu fainali ambapo mechi za kutafuta mshindi wa tatu na fainali zenyewe zinatarajiwa kuchezwa tarehe 21 juni, 2019.
Wachezaji wa timu ya soka wasichana kutoka mkoa wa Kilimanjaro wakipambana na wapinzani wao timu ya soka wasichana ya mkoa wa Morogoro.

Vodacom yazindua duka jipya jijini Tanga

0
0


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Kampuni ya Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. . Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martin Shigella (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen (mkono wa kulia wa mkuu wa mkoa) wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Vodacom shop, Micheal Mtawali.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella (Kushoto) akisimkiliza Meneja wa Vodacom Mkoa wa Tanga, Fadhili Linga, (kulia) wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Aliyesimama katikati ni Meneja wa Vodacom Kanda ya kaskazini, Brigita Stephen. Uzinduzi wa duka hilo umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja wake katika mikoa mbalimbali nchini.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Vodacom na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella (Wanne kutoka kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom jijini Tanga hivi karibuni. Watatu kutoka kulia ni Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Brigita Stephen. Uzinduzi wa duka hilo ni miongoni umelenga kurahisisha upatikanaji wa huduma za simu katika mkoa ikiwa ni sehemu ya jitihada za kampuni hiyo kuwafikia zaidi wateja katika mikoa mbalimbali nchini.

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA RAFIKI YA UWEKEZAJI NCHINI

0
0
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na waandishi wa habari masuala ua uwekezaji walipokutana nao wakati wa kongamano la kujadili masuala hayo kwa wawekezaji wa Kimarekani, kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.na kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji kutoka Marekani waliopo nchini alipokutana nao 17 Juni, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe akiwasilisha mada ya masuala ya Uwekezaji nchini wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (katikati mwenye kitenge cha kijani) pamoja na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson (mwenye koti jeupe) wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa kongamano hilo.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (mb) akizungumza na Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam walipokutana kujadili masuala ya uwekezaji nchini wa kwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akizungumza na waandishi wa habari masuala ua uwekezaji walipokutana nao wakati wa kongamano la kujadili masuala hayo kwa wawekezaji wa Kimarekani, kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi na kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akihutubia wakati wa kufunga Kongamano hilo.Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo, wa pili kutoka kushoto waliokaa ni Kaimu Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
………………………

NA.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki amewahakikishia wawekezaji kutoka Marekani uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji nchini kwa kuzingatia mchango wao katika masuala ya uwekezaji.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la siku moja la kujadili masuala ya kuboresha mazingira ya biashara pamoja na uwekezaji nchini lililofanyika tarehe 17 Juni, 2019 katika Ukumbi wa mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yaliyolenga kujadili changamoto zinazowakabili na kujadili namna bora ya kukabiliana nazo na hatua mahsusi ambazo Serikali imeendelea kuzichukua ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.
Kongamano hilo limeandaliwa na Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania na kuhusisha wawakilishi wa Kampuni 47 kati ya 238 za Kimarekani na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, Maafisa Waandamizi wa Serikali ya Tanzania, Wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani pamoja na Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kimarekani.

Waziri Kairuki alieeleza nia ya Serikali ni kuendelea kuwa na mazingira wezeshi yanayowavutia wawekezaji nchini katika kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo na kupokea maoni yao ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo.

“Serikali itaendelea kuweka mkazo mkubwa wa maboresho katika maeneo mbalimbali yatakayo kuvutia wawekezaji ikiwani pamoja na uboreshwaji wa sekta ya mawasilino, miundombiu ya barabara na usafirishaji ili kuwa na mazingira mazuri ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini,”alisema Waziri Kairuki.

Aliongeza kuwa ifikapo mwezi Julai mwaka huu, serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambao tayari umefanyiwa maboresho na utekelezaji wake utaanza mapema mwaka ujao wa fedha wa 2019/ 2020.

Aidha waziri aliahidi kuendelea kusimamia maeneo muhimu ikiwemo ushiriki wa sekta binafsi katika maeneo ya uwekezaji na kueleza maboresho haya yatatekeleza hasa katika kuboresha mifumo na kuwa na maziringa mazuri yanayotabirika kwa wawekezaji.

“Kwa kutambua umuhimu wa Sekta binafsi, tutaendelea kusimamia ushiriki wao kikamilifu ili kuleta tija pasipo kubagua sekta hiyo na kuendelea kuwa na mifumo inayotabirika kwa ajili ya wawekezaji.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alifafanua kuwa, jitihada za Serikali ni kuhakikisha kunakuwa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia zote zinategemeana katika masuala hayo ya uwekezaji.

“Kimsingi tunapaswa kuwa na uelewa wa pamoja kuwa, Tanzania na Marekani zinategemeana katika masuala haya ya uwekezaji kwani mnatuhijai na sisi tunawahitaji hivyo lazima tukae meza moja na kuyajenga endapo tunaona kuna maeneo ya kuboresha yenye tija ya kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo ni vyema tukayafanyia kazi pamoja”, Alisistiza Profesa Kabudi.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dkt. Inmi Patterson katika hotuba yake ya ufunguzi alieleza kuwa, majadiliano hayo ni mwanzo mzuri wa kuendelea kutekeleza mabadiliko ya kisera yatakayosaidia kuongeza uwazi na mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara nchini.

“Majadiliano ya leo ni mwanzo wa utekelezaji wa mabadiliko ya kisera yatakayoongeza uwazi na kuboresha mazingira ya kufanya biashara na tunaunga mkono jitihada hizi za Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo sasa,”Alieleza Kaimu Balozi Patterson.
Aliongezea kuwa Serikali ya Marekani itaendelea kuunga mkono ushiriki wa sekta binafsi katika jitihada za maendeleo nchini humo kupitia ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma (Public private partnerships) ambao utaimarisha mazingira ya kibiashara na ubunifu ambao utanufaisha Wananchi wa Tanzania.

Aidha alieleza kuwa nchi yake imeendelea kuwa mstari wa mbele katika uwekezaji, kwa kuzingatia Takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Wafanyabiashara wa Kimarekani wamewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.7 nchini Tanzania na kuzalisha takriban nafasi za ajira 52,000 katika kipindi cha miaka 28 nchini kote Tanzania.

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE YAKUTANA KUPITIA SHUGHULI ZILOZOBAKI KATIKA MKUTANO WA BUNGE UNAOENDELEA JIJINI DODOMA

0
0
 Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Bunge ya Uongozi kilichokutana kupitia shughuli zilizobaki za Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Bunge ya Uongozi kilichokutana kupitia shughuli zilizobaki za Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Uongozi kilichokutana kupitia shughuli zilizobaki za Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma.
  Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Uongozi kilichokutana kupitia shughuli zilizobaki za Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma.
PICHA NA BUNGE

Kwandikwa Awataka Watanzania Kuzingatia Alama za Usalama Barabarani


MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Bungeni jijini Dodoma Juni 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mbunge wa Kijitoupele, Shamsi Vuai Nahodha, Bungeni jijini Dodoma Juni 18.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MOHAMED MORSI AZIKWA MBALI NA MAKAZI YAKE

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
HATIMA ya aliyekuwa Rais wa Misri Mohamed Morsi (68) imehitimishwa kwa kuzikwa leo huko Mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Cairo kijana wake amethibitisha.

Morsi amezikwa na ndugu zake wa karibu baada ya kukutwa na umauti kwa kuanguka ghafla akiwa mahakamani.
 Kituo cha habari Aljazeera kimeeleza kuwa Morsi amezikwa leo asubuhi na waumini wa Muslim Brotherhood pamoja na ndugu wa karibu na kupitia ukurasa wake wa Facebook kijana wa marehemu Ahmed Morsi amethibitisha.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na ndugu na waumini hao wa Brotherhood Muslim huko Mashariki mwa mji huo kwa kile kilichoelezwa kuwa mamlaka nchini humo kuzuia mazishi hayo yasifanyike nyumbani kwa Morsi huko Sharqiya.

"Tuliosha mwili wake katika hospitali ya gereza la Tora, tukamswalia katika msikiti wa magereza na amezikwa katika misingi ya kiislamu" ameandika Ahmed.

Wakili wa Morsi Abdel Moneim amethibitisha kuwa mazishi yamefanyika Al- wafaa wa al- Amal.

Morsi alikuwa Rais wa kwanza kuchanguliwa kidemokrasia nchini humo mwaka 2012 baada ya  kuondolewa kwa Hosni Mubarak aliyetawala kwa miaka 30.

Hata hivyo hakudumu madarakani kwani aliondolewa kwa jeshi na maandamano yakiongozwa na Rais wa sasa wa nchi hiyo Abdel Fattah el- Sisi mwaka 2013 na baadaye kushikiliwa hadi umauti ulipomkuta.

Serikali Yaokoa Mabilioni Uendeshaji Mashauri Ya Madai

0
0
Serikali imesema mabadiliko kwenye sekta ya sheria nchini hususani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu yameanza kuleta tija baada ya kuongeza ufanisi na kuokoa fedha ambazo hapo awali zilikuwa zikitumika kuwalipa mawakili binafsi.  

Akijibu swali la Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kuebenea ambae alitaka kujua kiasi cha fedha ambacho serikali imeokoa tangu maboresho kwenye sekta hiyo yaanze kutekelezwa, ambapo pamoja na mambo mengine yalianzisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ambayo imepewa mamlaka ya kusimamia, kuendesha na kuratibu mashauri yote ya madai kwa niaba ya Serikali nchini.

Kwenye majibu yake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga alimueleza mbunge hyo kuwa kwenye Mwaka wa Fedha 2018/19 pekee Serikali imeweza kuokoa zadi ya shilingi bilioni tisa (9,018,957,011), ambazo kama sio maboresho kwenye sekta hiyo zingetumika kulipa makampuni binafsi ya uwakili. 

Aidha, Dkt. Mahiga aliendelea kulieleza Bunge kuwa Serikali itaendelea kutumia Mawakili binafsi kwa kibali cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali pale itakapothibitika kuwa ni lazima kufanya hivyo. Alitoa mfano wa vigezo vinavyotumika kutumia mawakili binafsi ni shauri kufunguliwa kwenye mahakama ambazo sio za kimataifa na sheria za nchi husika haziruhusu uwakilishi wa mwanasheria kutoka nje ya nchi hiyo. 

Kuhakikisha maslahi ya taifa yanalindwa Dkt. Mahiga ameliambia bunge kuwa uendeshaji wa mashauri hayo utendelea kuishirikisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye kila hatua ya mwenendo wake tofauti na hapo awali. 

Kuhusu baadhi ya mashirika ya umma kuendelea kutumia mawakili binafsi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amelieleza Bunge kuwa mashirika hayo ni yale ambayo mashauri yake yalianza kabla ya maboresho kwenye sekta hiyo hayajaanza kutekelezwa na uendeshaji wa mashauri utatekelezwa kwa kushirikiana na Wakili Mkuu wa Serikali.

IGP SIRRO AMETETA NA MAOFISA NA WAKAGUZI WA POLISI KATIKA VIWANJA VYA BWALO LA MAAFISA WA POLISI OYSTERBAY

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akisalimiana na kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, wakati alipowasili katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay  jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na Maofisa na Wakaguzi wa Jeshi hilo. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimsikiliza Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi DCP Lucas Mkondya (aliyesimama) wakati akitoa hotuba mbele ya maofisa na wakaguzi (hawapo Pichani) kwenye kikao cha kuwajengea uwezo wa kiutendaji na kuwakumbusha wajibu wao. 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na makamishna wa jeshi hilo baada ya kumaliza mkutano uliowahusisha maofisa na wakaguzi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji, kutoka kulia kwake ni Kamishna wa kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii CP Mussa A. Mussa na kushoto kwake ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas. (Picha na Jeshi la Polisi).

KIJIJI CHA UTURO MKOANI MBEYA CHAFANIKIWA KUZUIA VIFO VYA MAMA NA MTOTO KWA ZAIDI YA MIAKA 20

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya jamiI,Jinsia,Wazee,na Watoto,Dkt .Zainab Chaula amewasili katika Kijiji Utoro kilichopo katika Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kujifunza jinsi ambavyo Kijiji hicho kimeweza kuzuia vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kufungua zaidi ya miaka 20 hakuna kifo kilichotokea .

Juhudi hizo zimetokana na aliekuwa Mganga mfawidhi zahanati ya Uturo kuanzia mwaka 1993 mpaka 2017 Bw. Wilson Chotamganga ,ambaye baada ya kufika kijijini hapo alikuta vifo vingi vilivyotokana na uzazi kwa wakina mama na watoto waliozaliwa ,na watoto hao wachanga walikuwa wakizikwa na wakinamama kwa siri pembeni ya nyumba zao ,ndipo alipoamua kuwatafuta wahudumu wa afya ngazi ya Jamii ambao ni wakinamama maarufu kama Makomandoo ambao hutoa huduma za afya ya uzazi katika jamii toka mama anapogundulika na ujauzito hufatiliwa na kushauriwa kwenye kituo cha afya mpaka atakapojifungua.

Dkt Chaula amesema baada ya kutoka kijijini hapo Wizara yake itaandaa mkakati wa kutoa elimu hiyo kwa kuisambaza Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt .Zainab Chaula amewahakikishia wananchi wa Kijiji cha Uturo Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya, ya kuwa Wizara yake itahakikisha inafanya maboresho katika Zahanati ya Uturo ili waweze kupata huduma zote za afya na sio huduma za Uzazi pekee.

Viewing all 109591 articles
Browse latest View live




Latest Images