Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO


UJENZI WA TAWI LA IFM SIMIYU UTAMALIZIKA SEPTEMBA 2019: PROFESA SATTA

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof.Tadeo Satta akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( katikati) kuhusu ramani ya majengo ya tawi jipya la chuo hicho wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019 kijiji cha Sapiwi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMkinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi. 
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Prof.Tadeo Satta akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Tadeo Satta wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi. 
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi. 
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi. 
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi. 
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wakishuhudia zoezi la uchimbaji msingi wa baadhi ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kinachojengwa Kata ya Sapiwi wialayni bariadi mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019. 
…………………….. 
Na Stella Kalinga, Simiyu 
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta amewahakikisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kuwa ujenzi wa awali wa tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu ,unatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 . 

Profesa Satta ameyasema hayo Juni 17, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Simiyu katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi. 

Profesa Satta amesema kujengwa kwa kituo hicho kipya cha mafunzo kutachangia kuongeza udahili na kubainisha kuwa katika mpango mkakati wa chuo mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021, chuo kimejipanga kuongeza kutoa mafunzo kwa wateja wake hasa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Simiyu inayotarajiwa kuchukua mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Tabora. 

Ameongeza kuwa azma ya chuo ni kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia ngazi ya cheti na matarajio ni kuhamisha wanafunzi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Mwanza kuja Simiyu ili Mwanza zibaki kozi za jioni wanazosoma watu wanaotoka kazini. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amempongeza Makamu Mkuu wa Chuo IFM, Prof. Tadeo Satta kwa kuwa mtendaji wa mipango aliyoipanga na kutimiza ahadi ya kuanza kujenga tawi hilo mwaka huu, huku akitoa wito kwa wananchi wote kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hosteli, migahawa na nyumba za kupangisha watumishi. 

“Tawi la Chuo cha IFM linajengwa Sapiwi watu wote wanaalikwa kuchangamkia fursa na wachangamikiaji wa fursa wa kwanza ni wana Sapiwi wenyewe, tungehitaji kupata hosteli, migahawa ya chakula, maeneo ya watu kunywa vinywaji na tutawaambia TANROADS waone namna ya kuweka “stendi” maana hapa Sapiwi kitakuwa kituo kikubwa” alisisitiza Mtaka. 

Aidha, Mtaka amewahakikishia viongozi wa Chuo cha IFM kuwa viongozi wa Mkoa wataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha azma ya kukamilisha ujenzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwezesha mkandarasi kufanya kazi saa 24 kwa kuhakikisha kuna ulinzi na miundombinu ya umeme inakuwepo katika eneo la ujenzi. 

Naye Mayunga Juma Mkazi wa kijiji cha Sapiwi amesema wananchi wa Sapiwi wanashukuru uwepo wa ujenzi huo kwani umesaidia kutoa ajira na kuwawezesha kupata fedha za kujikimu kimaisha. 

Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Kagera, Baluye Mitinje ameahidi kusimamia na kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati. 
Ujenzi wa awali wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tawi la Sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na sabini na moja .

WANAWAKE WAFANYABIASHARA MASOKONI JIJINI MBEYA WAJIUNGA NA UMOJA WA KITAIFA

$
0
0
 Uhamasishaji ukiendelea

 Mwenyekiti wa Soko la Soweto jijini Mbeya, Fredy Mwakongano, akizungumza na Wanawake wafanyabiashara kutoka jijini Dar es Salaam waliofika katika soko hilo juzi kwa ziara ya mafuzo na kuwahamasisha wanawake wenzao kujiunga na Umoja wa Kitaifa. Kushoto ni Katibu wa Soko hilo, Atu Mwinuka.
 Mwenyekiti wa muda wa umoja huo Kitaifa kutoka  shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG) Betty Mtewele akizungumza.
 Uhamasishaji ukifanyika katika Soko la Soweto
 Wafanyabiashara wa Soko la Igawilo wakipiga makofi kufurahia umoja huo
 Mfanyabiashara Fatna Konzo akitoa ushuhuda wa mafanikio aliyopata baada ya kujiunga na EfG
 Ofisa Tathmini na ufuatiliaji wa EfG, Samora Julus akizungumza na wafanyabiasha wa Soko la Igawilo
 Maswali yakiulizwa
 Mfanyabiashara Joanitha Katunzi kutoka Dar es Salaam akihamasisha
 Katibu wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko la Soweto, Tumaini Kalinga akizunguka na wafanyabiashara wa Soko la Igawilo.
 Picha ya pamoja  na wafanyabiashara wa Soko la Igawilo.



 Mwanasheria wa EfG, Mussa Mlawa, akizungumza na wafanyabiasha wa Soko la Igawilo
 Mfanyabiashara akiwa na kipeperushi
 Wafanyabiasha wa Soko la Ilomba wakiwa kwenye mkutano wa uhamasishaji
 Ofisa Tathmini na ufuatiliaji wa EfG, Samora Julus akizungumza na wafanyabiasha wa Soko la Ilomba


 Mwenyekiti wa Soko la Mabatini Musimu Kipande akizungumza
 Picha ya pamoja  na wafanyabiashara wa Soko la Mabatini.
Wafanyabiasha kutoka Dar es Salaam wakiwa na mifuko maalumu waliobebea nyaraka za uhamasishaji 

Picha ya pamoja  na wafanyabiashara wa Soko la Ilomba.

Na Dotto Mwaibale, Mbeya

WANAWAKE Wafanyabiashara  5000 katika masoko jijini Mbeya wamejiunga na Umoja wa Wanawake Sokoni wa Kitaifa.

Akizungumza jijini Mbeya jana katika ziara ya mafunzo kwa wanawake hao Mwenyekiti wa muda wa umoja huo kitaifa kutoka  shirika lisilo la kiserikali la Equality for Growth (EfG) Betty Mtewele alisema wamepata mafanikio makubwa baada ya wanawake wafanyabiashara masokoni jijini Mbeya kuhamasika na kujiunga na umoja huo. 

Alisema mafunzo hayo ni utekelezaji wa mikakati na shughuli za programu ya Mwanamke sokoni wa kitaifa ambao umeratibiwa na hilo lenye dhima ya kuinua maendeleo ya sekta isiyo rasmi nchini Tanzania hususani kwa wanawake.

" Dhima ya shirika letu ni kuinua sekta hiyo hususani wanawake kwa kuwapunguzia umaskini kwa njia ya kutoa mafunzo ya sheria na haki za binadamu, kutoa msaada wa kisheria, kuwawezesha kuwepo kwa fursa sawa za kibiashara kwa wanawake na wanaume pàmoja na kuwashawishi utungaji wa sera zinazoinua wanawake na kujenga uwezo sawa kwa wanawake na wanaume 

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo, Penina Leveta alisema EfG ilifanya utafiti mwaka 2009 katika masoko 18 ya jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza mradi wa Sauti ya Mwanamke sokoni unaofadhiliwa na Serikali ya Uingereza ambao ulibainisha sekta isiyorasmi kama chanzo kikuu cha ajira kwa wanawake maskini na ambao hawakusoma nchini Tanzania. 

Alisema ilikadiriwa kuwa asilimia 43 ya wanawake Tanzania wanapata kipato chao kutoka sekta isiyo rasmi hata hivyo ni kwa nadra sana wameshirikishwa katika kufanya maamuzi na kuingizwa katika kamati za masoko, jambo ambalo linadhihirisha kukosa udhibiti juu ya mazingira ya biashara zao na kuwazuia kufanya mabadiliko muhimu ambapo kati ya viongozi 89 wa kamati za masoko wanawake walikuwa ni 14 tu.

Alisema kwa jijini Mbeya wamefanikiwa kuwahamasisha wanawake wafanyabiashra kujiunga na umoja huo katika masoko ya Igawilo, Ilomba, Soweto, Mabatini, Uhindini, Soko Matola, Nzovwe na Ikuti Iyunga.

" Shirika letu lilianzia kufanya kazi ya mradi wa Sauti ya Mwanamke Sokoni jijini Dar es Salaam katika masoko ya Wilaya ya Ilala na Temeke na kuendelea hadi mikoa ya Tanga, Iringa, Mbeya, Lindi, Mtwara na Shinyanga. alisema Leveta.

Katibu wa Umoja wa Wanawake Wafanyabiashara katika Soko la Soweto, Tumaini Kalinga alisema mafunzo waliyopata kutoka EfG yamewasaidia ambapo wamefanikiwa kuanzisha vikundi vya Vicoba tisa na wanamtaji wa sh.milioni 500, wamenunua bajaj na kiwanja ambacho wanatarajia kujenga hoteli kama chanzo kingine cha mapato yao ambapo katika hatua nyingine amemuomba Naibu Spika Tulia Ackson kuwa mlezi wa umoja wao huo.

TIMU YA UFUATILIAJI YAKERWA NA KUSUASUA KWA UJENZI WA ZAHANATI YA MATALE MKOANI SIMIYU

$
0
0
Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA 
Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda akikagua Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA 
Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA 
Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda akikagua Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA 
………………. 

Na.Angela Msimbira SIMIYU 
Timu ya ufuatiliaji inayoshughulika na Mradi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI imekerwa na kusuasua kwa ujenzi wa Zahanati ya Matale, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu . 

Akiongea kwa niaba ya Timu hiyo Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda amesema ujenzi wa zahanati hiyo umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya vitu vingi kutokamilika na jengo hilo kutotumika licha ya kutakiwa kuanza kutoa huduma za mama na mtoto katika jengo hilo. 

Ameyataja maeneo ambayo hayajakamilika kuwa ni uwekaji wa milango, ufungaji wa gata za kuvunia maji, uwekaji wa madirisha ya alluminium, uwekaji wa mfumo wa umeme, uwekaji wa marumaru upande wa vyooni , uchimbaji na ujenzi wa mashimo ya maji taka, uwekaji wa masinki wakati fedha zote zilitolewa kwa ajili ya ujenzi ambapo ujenzi huo ulikuwa unatakiwa kukamilika juni, 2018 

“Ni jambo la kushangaza kuona Zahanati iliyotakiwa kuanza kutumika tangu 2018 mpaka leo haijaanza kufanya kazi japokuwa Serikali imeweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo, suala hili halipendezi na linarudisha nyuma maendeleo kwa jamii” amesisitiza Bi. Atinda 

Amesema kuwa timu imegundua kuwa kuna matumizi ya fedha yasiyofuata miongozo yaliyofanywa wakati wa ujenzi wa miundombinu ya Zahanati hiyo ambapo taarifa zinaonyesha kuwa Fundi wa ujenzi amelipwa zaidi ya shilingi milioni 5 kati ya shilingi milioni 6 alizotakiwa kulipwa wakati sehemu kubwa ya ujenzi huo haujakamilika. 

Bi. Atinda ameiagiza Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa jengo hilo na kuanza kutumika ifikapo tarehe 30 juni, 2019 na kutumia fedha zilizopelekwa na TAMISEMI katika robo ya nne ya mwaka 2018/2019 kufanya usimamizi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya 38 vilivyofanyiwa maboresho chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA na kuhakikisha vituo vyote vinaanza kutoa huduma kwa jamii. 

Bi. Atinda amesema kuwa tathimini ya matumizi ya fedha iliyofanywa na mkaguzi wa ndani wa Halmashaiuri ya Mji wa Bariadi ifanyiwe kazi na kutolewa taarifa katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. 
Aidha Timu ya Ufuatiliaji kutoka OR-TAMISEMI ilifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi na matumizi ya Zahanati na Vituo vya afya vilivyojengwa Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMCH-UNFPA.

VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA TISHIO KWA WATOTO WILAYANI PANGANI

$
0
0

KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange akizungumza wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa
MKURUGENZI wa Shirika la UZIKWASA Novatus Urrasa akizungumza wakati wa wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa
AFISA Maendeleo ya Jamii wilaya ya Pangani Elias Msuya akizungumza wakati wa siku ya Mtoto wa Afrika
Mwanafunzi wa shule ya Msingi Funguni Aisha Ally akisoma risala
Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi akizungumza na vikundi mbalimbali
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange katika akizindua Mpango wa Taifa kazi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) wakati wa Tamasha la Ugawaji tuzo kwa vijiji bora katika mapambano dhidi ya Ukatili wa wanawake na watoto wilayani humo kushoto ni Mkurugenzi wa UZIKWASA Novatus Urassa
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia matukio


VITENDO vya ubakaji na Ulawiti ikiwemo wanafunzi kupewa ujauzito ni moja ya vitendo vya kikatili ambavyo vimekuwa tishio kwa watoto wilayani Pangani huku ikielezwa kwamba wanaofanyiwa vitendo hivyo wanaanzia darasa la pili na kuendelea jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wa maendeleo yao 

Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakati wa Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika kiwilaya Kata ya Pangani Mashariki iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa Mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa) wilayani Pangani ambapo Halmashauri wa wilaya hiyo ilishirikiana na Shirika la Uzikwasa

Alisema hilo limekuwa ni tatizo kubwa sana wilayani humo huku akiitaka jamii kubadilika na kuachana na vitendo vya namna hiyo kwani vimekuwa vikikwamisha watoto kushindwa kufikia ndoto zao 

“Hili ni tatizo kubwa sana OCD hapa wilayani Pangani lakini pia inaumiza sana hivyo jamii lazima ibadilike na kuhakikisha wanawafuchua watu wanaohusika na vitendo hivyo kwenye jamii lakini pia toeni ushirikiano tuweze kumaliza matukio ya ukatili wa kijinsia kiu yangu ni kuona matokeo kesi zinaendelea mahakamani yanakwisha na wahusika kuchukuliwa hatua “Alisema 

Hata hivyo aliwataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kwenda kutoa ushahidi pindi yanapotokea matukio hayo msikubali kurubuniwa kwani kufanya hivyo tunapelekea haki kushindwa kutendeka na wahusika kuchukuliwa hatua 

“Lakini kama mashauri mengi yatakuwa yanalalamikiwa na mashauri kushindwa kupata muafaka hiii pia sio taswira nzuri kwetu hivyo watu kwenye vyombo husika wananchi watajenga mashaka nao nao wabadilike “Alisema 

Naye kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilaya ya Pangani (OCD) Georgina Matagi aliwataka wanaume kuwaacha watoto wa kike wasome na kupata elimu ambayo itakuwa ndio silaha kubwa kwenye maisha yao ya sasa na baadae. 

Hata hivyo aliwataka watendaji wa Kata na Vijiji kuacha kumaliza kesi zinazohusiana na masuala hayo kwenye maeneo yao badala yake wahakikishe zinafikishwa mahakamani. 

Naye kwa upande wake Mwanafunzi wa shule ya Msingi Funguni Aisha Ally aliziomba mamlaka husika za kisheria kuhakikisha zinawachukulia hatua kali za kisheria watu wanaojihusisha na vitendo vya ubakaji, ulawiti na wanaowapa mimba wanafunzi kwani wanakatisa ndoto zao. 

Huku wakieleza kwamba watafurahi siku moja itatokea wabakaji au wanaowalawiti wakifungwa vifungo mbalimbali kwani hivi sasa kesi ni nyingi lakini matokeo ya kesi ni madogo sana. 

Siku hiyo ilikwenda sambamba na sambamba na kauli mbiu isemayo mtoto ni msingi wa Taifa endelevu tutumze, tumlinde na tumuendeleze ambapo alisema siku hizi kumekuwa na tabia ya watoto katika jamii kubakwa na kulawitiwa na watu wazima ikiwemo wengine kuwaozesha tabia ni kiyume cha sheria ya nchi. 

Alisema tabia hizo zimekuwa kikwazo kikubwa cha watoto hao na wengi kushindwa kuhitimu masomo yao na kupata mimba za utotoni na kupelekea wimbi la utegemezi kwenye familia na Taifa kwa ujumla ikiwemo kuongezeka magonjwa ya zinaa na kusababnisha kupungua nguvu kubwa ya Taifa. 

“Sisi kama watoto tuna ndoto nyingi na serikali ndio kimbilio letu baada ya wazazi na walezi na jamii kukatisha ndoto zetu ,jamii itambue kumekuwa na wimbi kubwa la kubakwa na kulawitiwa watoto wa kiume wao na watu wazima hivyo tunaimba jamii ikishiriki kikamilifu kutulinda kututunza na kutuelendeleza kufikia malengo”Alisema

KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI PROFFESA KITILA MKUMBO ATOA MAAGIZO KWA MABONDE YA MAJI KOTE NCHINI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akimtua mama ndoo wakati wa ziara yake akiwa kwenye eneo la Mashewa wilayani Muheza mara baada ya kutembelea mradi ya upandaji wa vitalu vya miti ya mitikiti.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kulia akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo namna wanavyopanda miti ya mitikiki wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
Mwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji katikati Proffesa Kitila Mkumbo na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara hiyo .
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo wakati alipotembelea mradi wa Kunusuru vyanzo vya maji na Matumizi Bora ya Ardhi (Securing Watershed through Sustainable Land Management) wilayani Muheza unaotekelezwa na Bonde la Maji la Pangani pamoja na Bonde la Wami Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga, Dar es Salaam na Morogoro (Tanga UWASA, DAWASA na MORUWASA
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akitazama mpaka wa bwawa la maji la Mabayani Jijini Tanga wakati wa ziara yake mkoani Tanga kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly 
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akitoka kutazama mpaka wa bwawa la maji la Mabayani Jijini Tanga wakati wa ziara yake mkoani Tanga
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Goefrey Hilly kulia aliyevaa koti wakati wa ziara yake 
AFISA Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga ( Tanga Uwasa) Dorrah Kilo kushoto akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga na wilayani Muheza
Muonekano wa eneo la kutirirsha maji eneo la bwawa la Mabayani Jijini Tanga mara baada ya Maji kujaa bwawani kama linavyoonekana wakati wa ziara hiyo 
Mwenyekiti wa Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa wilaya ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo anayeshuhudia katikati
Mwenyekiti wa Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly




KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo ameagiza mabonde yote tisa ya Maji nchini kuhakikisha wanafanya utafiti ili kuweza kutambua mazao rafiki ambayo wananchi wanaweza kulima bila kuathiri vyanzo vya maji vilivyopo ili viendelee kuwa endelevu.

Proffesa Mkumbo aliyasema hayo leo wakati alipotembelea mradi wa Kunusuru vyanzo vya maji na Matumizi Bora ya Ardhi (Securing Watershed through Sustainable Land Management) unaotekelezwa na Bonde la Maji la Pangani pamoja na Bonde la Wami Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga, Dar es Salaam na Morogoro (Tanga UWASA, DAWASA na MORUWASA)

Pia Katibu huyo alitembelea Umoja wa Wakulima wa Hifadhi Mazingira Kihuwi Zigi (UWAMAKIZI) huku akionyeshwa kuridhishwa na namna wanavyotunza vyanzo vya maji kwenye maeneo yao jambo ambalo alisema linapaswa kuigwa mfano na maeneo mengine hapa nchini.

Alisema katika jambo hilo wananchi wanapaswa kutambua mazao ambayo wanaweza kulima kwenye maeneo hayo ambayo yatakuwa tija kwao kuwakomboa kiuchumi bila kuleta athari za uharibifu wa vyanzo vya maji vilivyopo ili viendelee kuwepo kwa manufaa vya vizazi vya sasa na vijavyo.
"Mazao ni mengi mnaweza kulima kwenye maeneo mengine hivyo lakini ni muhimu kwamba mhakikishe mnafanya utafiti kuweza kubaini ni mazao gani mnaweza kulima bila kuathiri vyanzo vya maji "Alisema 

Aidha alisema baada ya kutembelea na kuona mafanikio yaliyopo amesema amejifunza kwamba mradi ambao wananchi wakishirikishwa na kushiriki ikiwemo kuelimishwa wanakuwa msaada mkubwa kwenye kutunza vyanzo vya maji kama alivyoona kwenye Mito hiyo aliyotembelea maji ni mazuri kabisa.

Katibu huyo alisema pia utunzaji mzuri wa maji hayo umesaidia kulinda bwawa la Mabayani na kupelekea gharama za kusafisha maji kupungua huku wananchi wakishirikishwa kutunza bwawa hilo kupitia mradi huo ambao pia umesaidia kuweka mipaka kati ya bwawa na walipo wananchi.

Hata hivyo alieleza kwamba katika maeneo hayo mradi unapotekelezwa Mto Zingi na Ruvu wananchi wameelimishwa kulima mazao ambayo ni rafiki kwa mto ambayo hayana athari hivyo Agizo la Rais Dkt John Magufuli la kutaka wananchji wasiondolee kwenye mita sitini ila waelimishwe limetekelezwa kwa asilimia kubwa Tanga kupitia Tanga Uwasa na hivyo hakuna ugomvi.

KIBESA WAIYOMBA SERIKALI KUTATUA CHANGAMOTO YA UMEME NA MIUNDOMBINU MBALIMBALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Seriklai ya Mtaa Mpiji Magohe kata ya Mbezi wilaya ya Ubungo,Said Maziku amesema kuwa Mtaa wa Kibesa umekuwa na changamoto ya umeme na maendeleo mengine yanayogusa huduma za kijamii.

Maziku aliyasema hayo wakati wa Mkutano wa Wananchi wa Mtaa huo kujadili masuala mbalimbali ya Mtaa, amesema Kibesa inakabiliwa na changamoto za Umeme , miundombinu ya Barabara , Maeneo ya Mazishi pamoja na huduma za Afya.

Amesema kuwa Kibesa ina maeneo mengi ya ardhi yanamilikiwa lakini hayaendelezwi na kutaka viongozi wa juu kuchukua hatua kwa baadhi ya maeneo kuweza kufanyia huduma za kijamii.

Maziku aliongeza kuwa Wenyeviti wa mitaa hawana madaraka ya kuchukua ardhi, hali ambayo kwao inawapa wakati mgumu pale wanapoona kuna mahitaji ya ardhi hawana mamlaka kuchukua ardhi hiyo.Amesema kuwa wananchi wanahitaji huduma za kijamii ambazo serikali inatakiwa kutoa huduma hizo huku kukiwa na ardhi ya watu ambayo wanamiliki bila kuendelezwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mpiji Magohe Said Maziku (mwenye tai) akiteta jambo na wananchi w baada ya kumaliza mkutano uliofanyika katika mtaa wa Kibesa kata ya Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dare s Salaam.
wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Seriklai ya Mtaa Mpiji Magohe Said Maziku katika mkutano uliofanyika Kibesa kata ya Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mpiji Magohe Said Maziku katika mkutano uliofanyika katika mtaa wa Kibesa kata ya Mbezi wilaya ya Ubungo jijini Dare s Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

PROF. MCHOME ATEMBELEA MKOA WA SONGWE KUKAGUA MSAADA WA SHERIA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome akisikiliza Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za msaada wa kisheria mkoani Songwe kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Songwe 
Prof. Mchome akizungumza baada ya kutembelea kituo cha msaada wa Sheria Cha Talaleca mjini Vwawa 
Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kituo cha WSCO kinachotoa msaada wa sheria wilayani Mbozi 
Prof. Mchome akitoa maelekezo baada ya kumaliza kazi ya ukaguzi wa kituo kinachotoa msaada wa sheria cha WSCO 
Prof. Mchome akikagua jalada la Taarifa mbalimbali za utekelezaji alipotembelea kituo cha msaada wa kisheria cha WSCO cha Mbozi

SAKATA LAKUONDOKA POGBA MAN UNITED, NYOTA WAWILI BARCA KUTUA OLD TRAFFORD

$
0
0
 Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Baada yakunukuliwa kutaka kuondoka Manchester United nakutafuta changamoto mpya katika timu nyingine, Kiungo Paul Labile Pogba, timu hiyo ya Uingereza imeanza maandalizi yakuishi bila Nyota wake huyo aliyenunuliwa kwa gharama kubwa zaidi iliyovunja rekodi mwaka 2016.

Kuondoka kwa Pogba Man United imetajwa sababu ya Nyota huyo wa Kimataifa wa Ufaransa kutaka kusajiliwa Real Madrid ya Kocha Zinedine Zidane Zizzou au timu yake ya zamani ya Juventus, hiyo ikiwa baada yakukabiliwa na shutma zakushuka kiwango akiwa na Mashetani Wekundu.

Pogba alinunuliwa na Man United kwa gharama ya kitta cha fedha cha £89 Milioni akitokea katika Klabu ya Juventus ya Italia, hivi karibuni akiwa katika mji wa Tokyo, Japan katika tukio lililoandaliwa na Mdhamini wake, Kampuni ya Adidas, Nyota huyo aliwaambia Waandishi wa Habari nia yake yakutaka kuondoka Old Trafford.
"Nimekuwa Manchester United kwa kipindi cha miaka mitatu, nimepata mafanikio, kulikuwa na kipindi raha na shida, kwa kila kitu kilichotokea msimu uliopita naamini nilikuwa na msimu mzuri, naamini kwangu mimi itakuwa muda mzuri kutafuta changamoto sehemu nyingine," alisema Pogba.
Licha yakuwepo taarifa hizo, Man United huenda ikaanza kukamilisha dili la uhamisho kwa Nyota wa Kimataifa wa Craotia anayechezea Klabu ya Barcelona, Ivan Rakitic na Nyota wa Kimataifa wa Brazil, Philippe Coutinho anayekipiga Camp Nou huko huko Barcelona.
Taarifa zilizoripotiwa na Jarida la Mundo Deportivo la Hispania na Spanish Daily imeeleza kuwa Man United imevutiwa siku nyingi na Nyota hao wawili.

Ujio wa Ivan Rakitic ni matamanio ya muda mrefu kwa Manchester United kutaka msaada wa Kiungo huyo Maestro licha yakuwa mtu muhimu katika Kikosi cha Kocha Ernesto Valverde, Barca kwa misimu iliyopita, lakini imeelezwa matarajio ya klabu huenda ikamuuza.
Kwa Philippe Coutinho hakuwa na msimu mzuri sana msimu uliopita, lakini Man United inahitaji msaada wake licha yakuwepo tetesi kutakiwa pia na Mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint Germain.
Yote kwa yote usajili wa Nyota hao wa Barcelona ndani ya Manchester United inategemeana nakuondoka kwa Kiungo Paul Pogba klabuni hapo. 


TAARIFA KWA UMMA: KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAWAALIKA WADAU WA MASUALA YA FEDHA KUTOA MAONI KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA FEDHA WA MWAKA 2019

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AKUTANA NA WAWEKEZAJI TOKA UTURUKI

$
0
0


Balozi wa Uturuki akimkabidhi Waziri wa Viwanda zawadi ya mojawapo yabidhaa zinazotengenezwa Uturuki kwa niaba ya ujumbe wa wafanyabiashara

Mheshimiwa Innocent Bashungwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara
pamoja na balozi wa Uturuki

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa akizungumza naujumbe wa wafanyabiashara toka nchini Uturuki. Pembeni yake ni Balozi wa Uturuki nchini Mhe Ali Davutaglu

Wafanyabiashara wakimsikiliza kwa makini akiwaeleza kuhusu faida za kuwekeza nchini

………………..
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amekutana na ujumbe wa
wafanyabiashara toka nchini Uturuki katika ofisi za Kiuo cha Uwekezaji
(TIC). 

Ujumbe huo ulioongozwa na balozi wa Uturuki nchini Mheshimiwa Ali
Davutaglu ulihusisha wafanyabiashara wa sekta za ujenzi, utalii, chakula na
viwanda mbalimbali. 

Wafanyabiashara hao walielezea sifa ya Tanzania kuwa na amani kama kivutio
cha wao kutaka kuwekeza nchini na kusema wangependa kufungua ofisi
itakayokuwa kiungo baina ya wafanyabishara wa Uturuki na wale wa Tanzania. 

Mheshimiwa Bashungwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba Tanzania ni nchi salama na yenye mazingira rafiki kwa wawekezaji akiahidi kuhakikisha Wizara ya Viwanda na Biashara ikishirikiana kwa ukaribu na taasisi nyingine za Serikali itaharakisha taratibu zote zinazotakiwa ili waanze uwekezaji wao mapema iwezekanavyo. 

Pia aliahidi kuwakutanisha na wafanyabiashara wengine nchini ili wapate kufahamiana na kubadilishana ujuzi.

SERIKALI YAIPATIA TUME YA MADINI NA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI SHI. BIL. 17 KUBORESHA MAPATO

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, wakisaini mkataba wa Sh. bilioni 10.7, utakao iwezesha Tume ya Madini, kuongeza ukusanyaji wa Maduhuli yatokanayo na madini kupitia Mkakati wa Serikali wa kuziwezesha taasisi zake mbalimbali kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi kwa kuongeza mapato, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leonard Chamriho, wakisaini mkataba wa Sh. bilioni 6, kuiwezesha Kampuni ya Huduma za Meli nchini- MSCL kujiendesha kibiashara, ikiwa ni moja ya mradi wa kimkakati wa kuongeza mapato ya Serikali, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho, wakionesha mkataba wa Sh. bilioni 6 waliousaini, wa kuiwezesha Kampuni ya Huduma za Meli nchini- MSCL, kujiendesha kibiashara ikiwa ni moja ya mradi wa kimkakati kuongeza mapato ya Serikali , hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila, wakibadilishana mkataba wa kiasi cha Sh. bilioni 10.7, utakao iwezesha Tume ya Madini, kuongeza ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na madini, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, wakionesha mkataba wa kiasi cha Sh. bilioni 10.7, kwa ajili ya kuiwezesha Tume ya Madini kuongeza ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na madini, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila (kulia), akitoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa kutoa kiasi cha Sh. bilioni 10.7, kwa ajili ya kuiwezesha Tume ya Madini, kuongeza ukusanyaji wa maduhuli yatokanayo na madini, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, akiwataka makatibu wa Wizara ya Madini na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kuhakikisha fedha walizopata kwa ajili ya miradi ya kimkakati zinaleta tija iliyokusudiwa, wakati wa hafla ya kusainiwa fedha za miradi ya kimkakati iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dodoma. 

*************************** 


Na Farida Ramadhani na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, imetoa Sh. billion 10.7, kwa Tume ya Madini nchini na Sh. billion 5.9, kwa Kampuni ya Huduma za Meli (Marine Service Company Limited -MSCL) kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya kimkakati, yenye lengo kuongeza mapato yanayotokana na madini pamoja na kuiwezesha Kampuni ya Huduma za Meli kujiendesha kibiashara.

Hafla ya utiaji saini mikataba ya fedha hizo umefanyika Jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Doto James na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamriho.

Bw. James alisema kuwa Sekta ya Madini na Kampuni ya Huduma za Meli, wajifunze kupitia miradi mingine ya kimkakati katika Halmashauri zilizopewa fedha, ili kuepuka changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa baadhi ya Halmashauri kushindwa kufikia malengo. 

“Fedha hizi sio za bure tutazifuatilia mpaka shilingi ya mwisho, ili kupata mrejesho wa kuchangia maduhuli katika Mfuko Mkuu wa Serikali, hivyo fedha hizo zinatakiwa kutumika kwa ufanisi kwa lengo lililo kusudiwa”, alisisitiza Bw. James.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeunda kikosi kazi maalum ambacho kitakuwa kinafuatilia maendeleo ya miradi hiyo na kutoa taarifa Serikalini.Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Pro. Simon Msanjila aliishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha hizo na kuahidi kuwa watazitendea haki na kuongeza mapato ya Serikali.“Tumepewa lengo la kukusanya maduhuli ya kiasi cha shilingi bilioni 475 katika mwaka huu wa fedha 2018/2019, nina kuhakikishia kuwa lengo hili tutalifikia kwasababu ya uwezeshaji huu wa Serikali na mwitikio mzuri wa wadau wa sekta ya madini katika kulipa kodi kwa hiari” alisema Prof. Msanjila

Alisema kuwa Sekta ya madini ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa nchi, uwezeshaji huo utawezesha kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiikumba Tume ya Madini kwa lengo la kuongeza ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini.Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula, alisema kuwa uwezeshaji huo utaiwezesha Tume hiyo kufikia lengo na kuahidi kuendelea na juhudi za kuhakikisha maduka ya madini nchini yanaboreshwa. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. 

Leonard Chamriho, aliishukuru Serikali kwa kuipatia Kampuni ya Meli nchini (MSCL) kiasi cha shilingi bilioni 5.9 zitakazotumika kukarabati baadhi ya meli zilizopo pamoja na kuweka mifumo ya kieletroniki ya kukusanya maduhuli ya Serikali.

Aidha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli, Bw. Eric Hamissi, aliahidi Serikali kuwa hawatoiangusha na kubainisha kuwa kampuni hiyo ni ya kimkakati na inaweza kuchangia uchumi wa nchi.

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUSAJILI BIASHARA ZAO

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

Wakala wa usajili wa biashara na leseni nchini( BRELA)  wamewakutanisha wadau mbalimbali wa biashara Mkoani Arusha,lengo likiwa ni kuwapa mwongozo wa kampuni kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao( ORS)

Akizungumza wakati wa semina inayoendelea Jijini Arusha Mkurugenzi wa fedha na utawala Tanzania Bakari Ally Mketo amesema kuwa kuna umuhimu wa kutambulisha Mfumo huo kwa wafanyabiashara ili kuweza kufanya Kazi kwa uweledi na ufanisi .

Aidha amesema kuwa mwamko wa watanzania kusajili biashara zao kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni nchini (BRELLA) umeongezeka kutoka makampuni 62 kwa mwezi hadi kufikia 700 hali inayosababisha na kuwepo kwa mfumo rafiki wa kuweza kuwafikia kupitia mtandao ambao umekuwa mkombozi kwao.

Alibainisha kuwa hatua hiyo ni mzuri kwa sababu inaonyeshwa namna watanzania hususani wafanyabiashara walivyokuwa mstari kujisajili kupitia wakala huu na kuweza kutambulika ambapo alisema idadi hiyo ilitokea makampuni hayo 62 kwenda 200 na baadae sasa kufikia 700 huku wakiweka mipango ya kuhakikisha wanazidi kuongeza wigo mpaka ili kuongeza idadi ya makampuni yatakayojisajili

" malengo yetu ni kuhakikisha tunapanua wigo mpana na kufikia idadi ya watu 1000 kwa mwezi ili kumhakikisha kila mdau wao anafikia na huduma yao kwa wakati hali itakayopelekea kumpunguzia mzigo mzito mwananchi na hivyo pia kuondoa gharama za kufuata huduma hiyo"alisema mketo

Nao baadhi Ya wafanyabiashara waliyohudhuria kwenye semina hiyo akiwemo Privanus Saimon na John Tasha wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kutatua changamoto mbalimbali walizonazo hivyo watafanya maboresho ya leseni zao ili waweze kuendesha makampuni yao kwa uhuru

Walisema kuwa kabla ya semina hiyo walikuwa Hawafahamu mambo mengi lakini tangu wapewe mafunzo hayo wameelewa na wamejua umuimu wa kusajili majina yao ya biashara pamoja na kubaini faida zakutoa taarifa Kwa mamlaka husika pindi wanapo funga biashara Zao

Alisema kuwa wafanyabiashara wengi wamekuwa hawajui faida za kutoa taarifa pindi wanapofunga biashara zao, kwani wamekuwa hawana elimu juu ya faida na hasara za kutoa elimu hivyo waliomba brela kuendelea kutoa elimu ili wananchi wengine ambao hawajui waweze kufahamu 

Waliiomba serikali kufuta madeni yote ya nyuma ambayo wananchi hao ambao ni wafanyabiashara waliokuwa wamesajili majina yao brela na teari wamefunga biashara lakini hawakutoa taarifa katika vyombo husika kitendo kilichowapelekea kuwa na mlimbikano wa madeni makubwa na mengi ili waweze kuanza upya kwani kwasasa wamepewa elimu na wataendelea kuwapa elimu wefanya biashara wengine 

"unajua unakuta mfanyabiashara kama Mimi nimesajili biashara yangu au jina la biashara brela ,nikasajili mamlaka yamapato na nimeendesha biashara mwishowe nikafunga labda kutokana nakukosa mtaji wa biashara au la nanilipofunga sikuwa najua kuwa natakiwa kutoa taarifa kitendo kinachonipelekea kulimbukiwa madeni kila siku na Mimi sijui kama nilivyofunga nilitakiwa kutoa taarifa kitu ambacho nichangamoto kubwa sana kwangu na yote hii imesababisha kutokana na awali kutokuwa na elimu "John Tasha

Kwa upande wake mmiliki ubunifu wa BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo amesema mfumo huo utasaidia kukamilisha usajili kwa haraka na kupunguza gharama kubwa ambazo wafanyabiashara walikuwa wanatumia

"Katika mfumo wa OBS wananchi haswa wa mkoani hususa ni Arusha walikuwa wanatumia mda mwingi mpaka kusajili pia walikuwa wanatumia fedha nyingi sana kwani walikuwa mpaka wasafiri ndio wasajiliwe lakini kwa mfumo huu mpya wa ORS ambao ni mfumo ambao Mwananchi ambaye ni mfanya biashara atajisajili kupitia njia ya mtandao "alisema Suzana

“Kwa kweli niwaambie wakazi wa mkoa huu wa Arusha na mikoa ya jirani wachangamkie fursa hii ya kuweza kutumia muda huu kuweza kusajili majina ya biashara zao, makampuni na nembo lakini pia leseni daraja A zililokuwa zinasajiliwa Wizara zimerudishwa kwetu na hivyo pia wanasajili iwapo walengwa watakidhi vigezo vilivyowekwa “Alisema 

Aidha alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kusajili ili kuweza kusajili kampuni lakini lazima vigezo na masharti husika vinavyohitajika kwenye upatikanaji wa leseni hiyolazimauzingatiwe 

Alisema kuwa kwakufanya hivyo kutawasaidia kuongeza kiwango cha biashara Zai kwani akiwa amesajili jina na kampuni itakuwa inatambulika kimataifa zaidi. 
Mmiliki Ubunifu wa  BRELA ambae pia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Susani Senzo akitoa Elimu kwa washiriki hao. 
 Mkurugenzi wa fedha na utawala Tanzania Bakari Ally Mketo akiongea na waandishi WA habari katika semina hiyo  
26Picha ikionyesha washiriki wakifuatilia mafunzo kwa makini

Zingatieni MabadilIko ya Maisha Baada ya Kustaafu- Mwaluko

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth 
Mwaluko akifungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma. 
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Bi
Mazoea Mwera akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi hiyo wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma. 
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bima Tanzania Kanda ya Kati Bi Maneno Adam akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma. 
Muwezeshaji kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Bw. Peter Seme
akizungumza katika mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma 
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi Doroth
Mwaluko (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa umma hivi karibuni leo June 17, 2019 Jijini Dodoma mara baada ya kufungua mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu. 


Watumishi wanaotarajia kustaafu wameaswa kuzingatia mabadiliko ya maisha kutoka katika utumishi wa umma kwenda katika mfumo wa maisha ya kawaida na kujiepusha kufanya miradi ambayo hawana ujuzi wa kutosha kuihusu. 

Akizungumza katika mafunzo kwa yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni ili wawe na mbinu za kuendana na mazingira hayo, Katibu Mkuuu wa Ofisi hiyo anayeshughulikia (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi. Doroth Mwaluko amesem kuwa Ofisi hiyo inatambua umuhimu wa wastaafu na faida za kujiandaa kustaafu. 

Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua kuwa suala la kustaafu ni la kila mmoa wetu na ni muhimu kujiandaa vyema na maisha mapya ambayo kimsingi yatakuwa tofauti na haya ya utumishi wa umma mliyo nayo kwa sasa
Akifafanua amesema kuwa kila mtumishi wa umma lazima atambue kuwa ni mstaafu matarajiwa hivyo kujiandaa kwake ni jambo muhimu. 

Kwa upande wake Muwezeshaji Kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni Jijini Dar es Salaam Bw. Peter Seme amesema kuwa watumishi hao wanaotarajia kustaafu watajifunza mambo mengi yakuwawzesha kuendelea na maisha yao kama kawaidia hata baada ya kustaafu. 

Alitaja baadhi ya mada kuwa ni pamoja na utayari wa kupokea mabadiliko baada ya kustaafu, Stadi za kuongeza kipato, Mtindo wa maisha bora baada ya kustaafu, Namna ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu. 

Kwa upande wake mmoja wa watumishi hao Bw. Esamo Sawaki amesema kuwa
wanaipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuandaa mafunzo hayo kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi hiyo ili waweze kukabiliana na changamaoto zinazoweza kujitokeza baada ya kustaafu. 

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kupata uzoefu kutoka kwa wastaafu wengine ambao tayari wana uzoefu katika kukabiliana na changamoto za kustaafu na hata kuelewa kazi ambazo ni za uzalishaji wanazoweza kuzifanya kama wastaafu ili kuwaletea tija. 

Tupata maarifa sahihi ya namna ya kutumia kiinua mgongo tutakachopewa baada ya kustaafu kutoka katika utumishi wa umma Alisisitiza Mafunzo yakuwajengea uwezo watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wanaotarajia kustaafu hivi karibuni yanafanyika Jijini Dodoma kwa siku tano yakiwashirikisha watumishi hao kutoka kada mbalimbali.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC yavitaka Vyama vya Siasa kufuata Utaratibu

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imevitaka vyama vya Siasa Nchini kufuata taratibu na sheria kwa kuwasilisha malalamiko yao kwenye tume hiyo pale inapobainika ukiukwaji wake hususan nyakati za uchaguzi.

Tume hiyo imevitaka vyama hivyo kuacha kulalamikia kwenye vyombo vya habari ambavyo vitaishia kuandika na kutangaza habari zao tu na sio kuchukua hatua stahiki za kutatua changamoto za uchaguzi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji
Semistocles Kaijage Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na Viongozi wa Dini mbalimbali Nchini kuhusiana na uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.

Awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura litafanyika nchini kote mapema mwezi Julai Mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya chaguzi za Serikali za mitaa ambapo jumla ya vituo Vituo 37,814 katika mikoa 31 vitahusika na zoezi hilo.

Kaijage alisema malalamiko mengi ya Viongozi wa vyama vya siasa hayajawafikia ofisini kwao bali wanaishia kuyaona tu kwenye vyombo vya Habari suala ambalo haliwezi kufanyiwa kazi na tume hiyo na kubainisha kuwa ni kesi moja tu ya uchaguzi iliyowafikia katika ngazi ya Taifa tangu mwaka 2006.

“Mnajua ndugu zangu viongozi wa Dini suala la malalamiko ya vyama vya siasa kuhusu uchaguzi ni suala linalohitaji kuangaliwa sana na hawa wanasiasa, mtu ana tatizo anakimbilia kwenye vyombo vya habari badala ya kuja kwetu, hatufanyi kazi hivyo,wanatakiwa kuja NEC ili tuyafanyie kazi malalamiko yao”alisema Jaji Kaijage.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt Athumani Kihamia aliwataka viongozi hao kutoa ushirikiano katika uboreshaji wa Daftari hilo ili liweze kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“Tunawategemea sana nyinyi Viongozi wa Dini katika kuhamasisha wananchi
kujiandikisha katika Daftari hili, nyinyi mna watu wengi,hivyo ni rahisi kuwashawishi kutekeleza jambo hili muhimu kwa Taifa letu”alisema Dkt Kihamia.

Nae Kamishna wa Tume hiyo Jaji Maryrose Longway aliwaomba Viongozi hao wa Dini kuwasihi wanasiasa kuepukana na lawama ambayo haitawasaidia na badala yake wafuate sharia za uchaguzi.

Mwenyekiti wa Baraza kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Mussa Kundecha na Mchungaji Charles Mzinga wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania KKKT wameiomba Tume hiyo kutoa elimu mara kwa mara kwa jamii kuhusu umuhimu wa kupiga kura pamoja na kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura.

DC SIMANJIRO AAGIZA WATAKAOWATUMIKISHA WATOTO WAKAMATWE

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akizindua chanjo ya watoto kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo kiwilaya ilifanyika katika Kata ya Naberera, Kijiji cha Landanai.
Wanafunzi wa shule ya msingi Landanai Kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiimba wimbo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika.
***********************
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula amewataka watu wote watakaohusika na kuwatumikisha watoto chini ya miaka18 kwenye maeneo ya migodini, majumbani, machungani na kwenye biashara za mama lishe wachukuliwe hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa na kushtakiwa.

Mhandisi Chaula akizungumza jana kwenye kijiji cha Landanai katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika alisema kila mwanaume yeyote atakayehusika kumpa mimba mtoto au mwanafunzi wa kike achukuliwe hatua za kisheria na endapo mtoto hatataja mwanaume aliyehusika wazazi pamoja na mtoto wachukuliwe hatua.

Alisema mangariba wanaohusika katika kuwakeketa watoto wa kike, wote wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake.

Alisema kila mtu ahakikishe anakuwa mlinzi wa mtoto kwa kushirikiana na wadau wanaohusika na masuala ya mtoto pamoja na serikali.

Alisema watoto wote wenye umri wa kwenda shule waandikishwe shule, mzazi yeyote atakaye kaidi agizo hili achukuliwe hatua za kisheri, aidha walimu wakuu wahakikishe kuwa wanafunzi wote wanavaa sare za shule (viatu na mavazi) na endapo wazazi watakwepa kuwajibika wachukuliwa hatua.

“Wazazi wahakikishe kuwa wanachangia chakula shuleni ili watoto wapate mazingira mazuri ya kujifunza, kusitisha uvamizi, uporaji na uuzaji wa ardhi ya wanachi kiholela katika maeneo ya vijiji,” alisema mhandisi Chaula.

Alisema kila kaya ihakikishe kuwa inatunza chakula cha mwaka mzima ili kuepuka janga la njaa na kila kaya ihakikishe inajiunga na bima ya afya iliyoboreshwa ili kuepuka gharama kubwa za matibabu endapo magonjwa yanapotokea na kila kijiji kihakishe kinatunza vyanzo vya maji vinavyopatikana katika maeneo yao.


Kwa upande wake, mtoto John Mollel ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba kweye shule ya msingi Landanai akisoma risala ya maadhimisho hayo alisema maadhimisho haya ya siku ya mtoto wa Afrika yalianza rasmi mwaka 1991.

Alisema chimbuko la siku hiyo ni kutokana na azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Mataifa huru ya Afrika (AU) la Juni 1991, ikiwa ni lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976.

Alisema katika azimio hilo la nchi 51 za AU, Tanzania ilijiwekea malengo mbalimbali juu ya ulinzi, haki na maendeleo ya mtoto kama vile, kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga chini ya miaka 5, kupunguza vifo vya kinamama vinavyotokana na matatizo ya uzazi, kupunguza viwango vya utapiamlo miongoni mwa watoto chini ya miaka 5, kuhakikisha watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule wanaandikishwa na kuhudhuria shule na kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto bila ubaguzi.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa mwaka huu ni “Mtoto ni Msingi wa Taifa endelevu: Tumtunze, Tumlinde na kumwendeleza.” Kauli mbiu hii ina maanisha kuwa sisi watoto tunatakiwa tulindwe na tulelewe ipasavyo kielimu, kimwili, kiroho, kisaikolojia na kimaadili ili tuwe na msingi imara kwa maendeleo ya Taifa letu.

Hata hivyo, ofisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni alimhakikishia Mkuu huyo wa wilaya kutekeleza maagizo hayo yaliyotolewa naye.

Ngalisoni alisema jamii inapaswa kutambua kuwa kila mtoto wa mwenzake ni mtoto wake ili waweze kuwa na jamii yenye upendo, maendeleo na mshikamano kwa siku za baadaye.

TANESCO WABAINI HUJUMA NA UBADHILIFU WA MIUNDO MBINU YAKE UNAOFANYWA NA WAFANYABIASHARA WA SENENE BUKOBA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus, wa Michuzi TV 

Shirika la Umeme Nchini Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera limefanya oparesheni ya kushtukiza katika Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba na kubaini ubadhilifu na wizi wa umeme unaopelekea hasara kubwa ya upotevu wa umeme, ikiwemo uhalibifu wa miundo mbinu ya shirika hilo.

Ziara hiyo ya kushtukiza ilyofanyika mnamo Juni 17, 2019 ikongozwa na Afisa Usalama wa Shirika la Tanesco Mkoa wa Kagera Bwana Steven Maganga imefanikiwa kubaini wafanyabiashara wa senene katika kijiji cha Ngarama Kata Katoro wakiwa wamejiunganishia umeme kwa njia zisizo halali hali hiyo ikiwa ni uhujumu wa Shirika la TANESCO na kurudisha nyuma Jitihada za maendeleo ya Nchi.

Wizi huo wa umeme katika kijiji hicho unasababishwa na biashara ya senene ambapo biashara hiyo hutumia umeme mkubwa ikiwa taa moja ya umeme hutumia KW 200 – 300, na kwa mfanyabiashara mmoja hufunga taa zaidi ya tano, na kupelekea mita kuzidiwa na kuungua hivyo njia pekee inayofuata kwa wafanyabiashara hao ni kujiunganishia umeme moja kwa moja kutoka kwenye nguzo za umeme wa TANESCO.

Akizungumza katika eneo la tukio Afisa Usalama wa Tanesco Bwn. Maganga amesema kuwa kufuatia wizi huo shirika limeanza kuchukua hatua za makusudi mara moja kwa kushirikiana na serikali ya kijiji kwa kuwastishia huduma wateja hao wasiokuwa waaminifu kwa kung’oa mita zao huku akitoa angalizo endapo hujuma hizo zitaendelea Shirika litakuwa tayari kung’oa hadi nguzo na kukiacha kijiji chote gizani.

Katika hali ya kushangaza wakazi wa maeneo husika wameonekana kukimbia maeneo yao na kuziacha nyumba zikiwa zimefungwa, kana kwamba hamna shughuli yoyote inayoendelea kijijini hapo, ilihali Miongoni mwa waliokamatwa katika msako huo ni pamoja na Ndugu aliyekiri kuunganishiwa umeme wa wizi na mmoja kati ya Vishoka (jina limehifadhiwa) ambaye inadaiwa aliwahi kuwa mtumishi wa Shirika la Tanesco siku za nyuma kisha kutimuliwa, huku majina ya wote waliobanika katika wizi huo yakifikishwa katika kituo kidogo cha Polisi Kijijini hapo, baada ya kusitishiwa huduma hiyo ya Umeme.

 Pichani shughuli ya kung'oa Mita na kukata huduma ya umeme ikiendelea Kwa waliobainika kuhujumu shirika la Umeme Mkoani Kagera, kijiji Cha Ngarama Kata Katoro Wilayani Bukoba.
 Pichani ni Baadhi ya Mita zilizoungua baada ya kulemewa mzigo Wa Taa za Senene ambazo hufungwa Kwa ajili ya kutega na kuvuna Senene maeneo ya Katoro Bukoba.

 Pichani ni baadhi ya nyumba za wateja Wa Tanesco ambao sio waaminifu, baada ya kugundua ujio Wa Tanesco mahala hapo walifunga nyumba zao na kuingia mitini. 
 Pichani shughuli ya kung'oa Mita na kukata huduma ya umeme ikiendelea Kwa waliobainika kuhujumu shirika la Umeme Mkoani Kagera, kijiji Cha Ngarama Kata Katoro Wilayani Bukoba.
 Pichani ni namna wafanyabiashara wanavyotumia njia hii kuvuna Senene wakati Wa usiku ambapo huwasha Umeme na kisha Senene hupumbazwa na mwanga mkali na kudondoka kiurahisi katika bati hizo

 Shughuli ya Kubaini Mita zilizofanyiwa hujuma ikiendelea chini ya Maafsa wa Tanesco na Uongozi Wa Kijiji Ngarama Kata Katoro Wilayani Bukoba.

DK.MABODI NA UGENI WA FRELIMO

$
0
0
UJUMBE wa Viongozi wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Roque Silva Samuel wakipewa maelezo katika Eneo la Kihistoria alipouawa kwa kupigwa Risasi na Wapinga Maendeleo Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume April 7, Mwaka 1972.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi(kushoto) akikabidhiwa Tisheti na Katibu Mkuu wa Chama Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO Ndugu Roque Silva Samuel(kulia) tukio hilo ikiwa ni ishara ya kuendeleza ushirikiano na Urafiki kwa Vyama hivyo vyenye Historia kubwa ya Urafiki wa Ukombozi wa Nchini mbali mbali za Afrika,ambapo Hafla hiyo imefanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo Tarehe 16/06/2019 
KATIBU Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO Ndugu Roque Silva Samuel(kulia),akimvisha Kofia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi ikiwa ni ishara ya Ushirikiano wa kiutendaji baina ya CCM na FRELIMO. 
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akivishwa Kofia ya FRELIMO na ATIBU Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji cha FRELIMO Ndugu Roque Silva Samuel, ikiwa ni ishara ya Ushirikiano wa kiutendaji baina ya CCM na FRELIMO. 
UJUMBE wa Chama Tawala cha Msumbiji FRELIMO wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Roque Silva Samuel wakiwa na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake katika eneo la Kaburi ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume wakiomba Dua. 
………………. 
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,amesema Urafiki wa Vyama vya ASP,TANU na hivi sasa CCM na Chama Cha Tawala cha Msumbiji FRELIMO ni wa Kihistoria uliodumu kwa muda mrefu. 

Alisema Urafiki huo umefikia kiwango cha kuwa na uhusiano wa Kindugu na Kidamu baina ya Wananchi wa Nchi hizo mbili,sambamba na kudumisha ushirikiano katika nyanja za Kisiasa na Kidiplomasia. 

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Ujumbe wa Chama cha FRELIMO ukiongozwa na Katibu Mkuu wake Ndugu Roque Silva Samuel, aliyefika katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kwa ajili ya mazungumzo ya kuimarisha mahusiano baina ya Taasisi hizo za Kisiasa. 

Dk.Mabodi alisema Chimbuko la Urafiki kati ya Vyama hivyo umetokana na harakati za Vyama vya ASP,TANU na FRELIMO vilivyoongoza harakati za Ukombozi Barani Afrika na baada ya Nchi mbali mbali kupata Uhuru wa kujitawala zenyewe viliendelea kuaminiwa na Wananchi wakavipa ridhaa ya kuongoza Dola. 

Alisema kuwa Wananchi wa Msumbiji wanaishi kwa Amani na Utulivu Zanzibar na wapo Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara wanaoishi Msumbiji kwa Amani masuala yanayotakiwa kuenziwa ili Mahusiano hayo yawe imara zaidi kwa maslahi ya Vizazi vya sasa na Vijavyo. 

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo alisema Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume aliongoza Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 na Zanzibar ikawa Huru za kuanza kujitawala yenyewe, ambapo kwa sasa Nchi inaendeleza Mapinduzi ya Kiuchumi kupitia Sera zake imara zilizowekwa na Chama Cha Mapinduzi. 

Dk.Mabodi alimwambia Katibu Mkuu huyo kuwa CCM itaendeleza Ushirikiano uliotukuka ulioachwa na Viongozi Wakuu wa Nchi hizo za Msumbiji na Tanzania ambao ni Marehemu Abeid Amani Karume,Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere na Hayati Samora Machel. 

Naye Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha Msumbiji Ndugu Roque Silva Samuel,alishukru kwa mapokezi mazuri aliyopata Zanzibar na kueleza kuwa lengo la ziara hiyo fupi ni kuishukru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Msaada waliotoa hivi karibu wakati Msumbiji ilipokumbwa na Maafa. 

Alisema Msumbiji ilipata Maafa ya Kimbunga mara mbili na kusababisha Vifo vya Wananchi zaidi ya 600 na kuharibika kwa miundombinu ya Maakaazi,Shule 300,Barabara,Mawasiliano na Nyumba za Umma na binafsi. 

“Tunawashukru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa msaada wao Mkubwa waliotoa kwa Msumbiji kwani wameonyesha kwa Vitendo namna wanavyojali 
Katibu Mkuu huyo wa FRELIMO alisema Chama hicho kimeendelea kufanya Siasa Huru zinazojali Hali za Watu wote bila ubaguzi wa kabila,rangi na kidini. 

Alisema kwa sasa Msumbiji wanajiandaa na Uchaguzi Mkuu wa Dola unaotarajiwa kufanyika Octoba 15,Mwaka 2019,Uchaguzi huo unatarajiwa kuwa wa huru na haki unakwenda sambamba na Matakwa ya Kidemokrasia.

HAULE, BRAISON WAJIFUNGA AZAM FC

$
0
0
NYOTA wawili wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, kipa Benedict Haule na kiungo Braison Raphael, wameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kila mmoja wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Wawili hao ambao kila mmoja alikuwa akimaliza mkataba, wanatarajia kudumu kwa matajiri hao kutoka viunga vya Azam Complex hadi 2021.

Wachezaji hao kuongeza mkataba huo, ni muendelezo wa uongozi wa Azam FC chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', kwa kushirikiana na benchi la ufundi, linaloongozwa na Kocha Mkuu mpya, Etienne Ndayiragije, kuwabakisha nyota wenye umuhimu kikosini.

Nyota hao wanatarajia kuanza maandalizi ya msimu mpya na kikosi hicho Alhamisi hii, wakianza na changamoto ya kuiongoza timu hiyo kutetea ubingwa wa michuano ya Kombe la Kagame, itakayofanyika Rwanda Julai mwaka huu.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' akiwa anapeana mkono na kiungo Braison Raphael baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili na kuendelea kusalia katika klabu hiyo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Abdulkarim Amin 'Popat' akiwa anapeana mkono na Golikipa Benedict Haule baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili na kuendelea kusalia katika klabu hiyo

WAKALA WA VIPIMO WATOA ELIMU YA VIPIMO KWA WAKULIMA ZAO LA KAHAWA, KAGERA

$
0
0
Wakulima wa Kahawa pamoja na Viongozi wa Vyama vya msingi wakiapishwa na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godrefy Muheruka (Aliyevaa Koti) kuwa hawatachakachua Mizani ya kununulia Kahawa Wilayani humo, kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa ununuzi wa zao la Kahawa.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godrefy Muheruka akifuatilia elimu na Afisa Vipimo, Jares Msalike namna ya kutambua Mizani iliyohakikiwa na Wakala wa Vipimo ili kuwalinda Wakulima kwa Vipimo sahihi.
Maafisa wa Wakala wa Vipimo wakitoa Elimu kwa wakulima wa zao Kahawa mkoani Kagera katika Wilaya ya Karagwe katika Chama cha msingi cha Nyakahanga namna ya kutambua mizani sahihi na ile isiyo sahihi.
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images