Shindano la Miss Utalii Tanzania, nimoja ya mashindano yenye mafanikio makubwa katika medani za kimataifa barani Afrika, tangu kuanzishwa kwake na kufanyika kwake kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2004, hadi lilipo sitishwa na bodi ya mashindano haya Julai 2013,na kufungiwa kwa muda na Baraza la Sanaa la Taifa Oktoba 2013.
Ubora wa shindano hili unatokana na kuwa ndilo shindano pekee nchini ambalo limetwaa mataji katika mashindano yoyote ya dunia na kimataifa tuliyo shiriki kuanzia mwaka 2005 hadi 2013 tulipo shiriki kwa mara ya mwisho. Ni shindano hili pekee ambalo mafanikio yake kimataifa yaliipa Tanzania heshima ya kihistoria ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia ,za Miss Utalii Dunia 2006,zilizo fanyika 11, Machi 2006 katika ukumbi wa Ubungo Plaza, ambapo zaidi ya nchi 100 zilishiriki huku fainali hizo zikionyweshwa LIVE duniani kote kutokea Tanzania.
Kubwa zaidi ni kuwa shindano la kwanza na kwa mara ya kwanza Tanzania kabla na baada ya uhuru kutwaa taji la Dunia la urembo, hivyo kuingiza Tanzania katika ramani ya Dunia ya nchi zenye mafanikio makubwa katika tasnia ya urembo, pale Miss Utalii Tanzania 2004, Witness Manwingi alipo twaa taji la Dunia la Miss Tourism World 2005 – Africa, katika shindano lililo shirikisha nchi 118, huko Harare Zimbabwe.
Na sasa baada ya mabadiliko ya mfumo wa uongozi na mfumo wa shindano, shindano hili linaandika historia nyingine kubwa ya kuwa shindano la kwanza la kimataifa Tanzania, likishirikisha washirikiki zaidi ya 140,40 wakiwakilisha kanda na mikoa ya Tanzania kuwania taji la taifa la Miss Utalii Tanzania na 100 wakiwakilisha nchi mbalimbali Duniani kuwania taji la kimataifa la Miss Tourism Tanzania International.
Kwa miaka zaidi ya mitano, tangu shindano hili lilipo fanyika kwa mara ya mwisho, uongozi na bodi ya shindano hili kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za kitaifa na kimataifa, ikiwemo Baraza la Sanaa la taifa (BASATA) na taasisi ya kimataifa ya World Beauty Pageant Association (WBPA) tume kuwa tukifanya marekebisho na maboresho mbalimbali ya mfumo wa uongozi, mfumo wa mashindano, kanuni na taratibu za mashindano, kwa kuzingatia vigezo na maelekezo ya BASATA na WBPA,lakini pia kufikia Viwango vya kimataifa vya mashindano ya urembo na mitindo.
Matokeo ya juhudi hizo ni mabadiliko ya kihistoria ambayo yamelifanya shindano hili sasa kuwa pekee nchini lenye mfumo wa kitaasisi wa uongozi, mfumo wa kimataifa wa mashindano, kanuni na taratibu za mashindano zinazo kidhi viwango vya kimataifa na kitaifa, yenye kuzingatia tamaduni, mila na desturi za kitanzania na kiafrika, hivyo shindano hili kuwa la kimataifa la Miss Tourism Tanzania International Pageant. Mabadiliko ambayo yamekidhi masharti na vigezo vyote vya Baraza la Sanaa la taifa (BASATA),ikiwemo ya kuboresha mfumo wa uongozi na wa mashindano, hivyo kulifanya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kubariki mabadiliko na maboresho hayo ,na kulifungulia na kuruhusu kuendeleza kufanyika shindano hili kwa barua yake tarehe 22 Januari,2019 yenye kumbukumbu namba BST/PR/MT784/27. Kufuatia Baraza la Sanaa la Taifa kubariki maboresho na mabadiliko hayo:
Shindano hili sasa ni shindano la kimataifa la Miss Utalii Tanzania (Miss Tourism Tanzania International Pageant), litakuwa na washiriki wa kitaifa na wa kimataifa wakiwakilisha nchi zao. Fainali za kimataifa za Miss Utalii Tanzania, (Miss Tourism Tanzania International Pageant), zitafanyika Tanzania kila mwaka, na kushirikisha zaidi ya washiriki miamoja (100) kutoka nchi miamoja (100) duniani kote, hii ni fulsa nyingine kwa Tanzania kujitangaza kimataifa na katika nchi zote ambazo zita shiriki shindano hili, ikiwa ni faida zaidi kwa Tanzania kuliko kupeleka washiriki kushiriki mashindano katika nchi nyingine.
Shindano hili sasa limekuwa na kalenda ya kudumu ya mashindano, likiwa ni sehemu ya maazimisho ya kitaifa ya sherehe za uhuru wa Tanzania, ambapo fainali za kanda zitafanyika kati ya Julai na Novemba,za kitaifa na kimataifa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe za uhuru tarehe 8 Disemba kila mwaka. Kalenda hii ya mashindano imezingatia uwepo wa mashindano mengine nchini na kimataifa kila mwaka.
Washiriki wa fainali za kanda ni wawakilishi wa mikoa katika kila kanda, ambao ni washindi wa 1-5 wa kila mkoa, ambao wata patikana kwa njia ya udahili mahususi utakao fanyika chini ya bodi za kanda za mashindano haya, ambazo zinaundwa na wakurugenzi wa mashindano wa kanda, maafisa utamaduni, maafisa ustawi wa jamii, maafisa Maliasili na Misitu wa mikoa iliyopo katika kanda husika. Washiriki wa fainali za kitaifa na kimataifa ni washindi 1-5 wa kanda, na washindi wa 1,2 au wa tatu wa shindano lolote la kitaifa kutoka nchi zote duniani.
Mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani imegawanywa katika kanda maalum nane (8) za mashindano haya, kwa kuzingatia uwiano wa kijiografia, kitamaduni na uwepo wa vivutio vya utalii katika mikoa husika kama ifuatavyo: Miss Tourism Northern Zone (Manyara, Arusha, Kilimanjaro), Miss Tourism Southern Zone (Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro), Miss Tourism Swahili Coast Zone (Coast, Dar es Salaam, Tanga), Miss Tourism Western Zone(Kigoma, Tabora, Katavi), Miss Tourism Lake Zone (Kagera, Mwanza, Mara, Geita, Simiyu), Miss Tourism Central Zone (Dodoma, Singida, Shinyanga), Miss Tourism Southern Highlands (Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe), Miss Tourism Eastern Zone (Unguja na Pemba).
Fainali zote za kanda zita rushwa mbashara (LIVE) kupitia Televisheni na mitandao ya kijamii kitaifa na kimataifa, huku ikitangaza vivutio vya utalii, Utamaduni, Uwekezaji, Wanyamapori, Mazingira na kuhamasisha utalii wa ndani, kitamaduni, kimichezo na kimikutano ya kanda na mikoa yote ya kanda husika. Fainali za taifa na kimataifa zitarushwa mbashara (LIVE) kimataifa na kuangaliwa LIVE na watazamaji zaidi ya milioni 750 duniani kote, huku vivutio vya Tanzania vya utalii, utamaduni, uwekezaji, Mazingira, Misitu, Wanyama pori na fukwe vikitangazwa kitaifa na kimataifa duniani kote. Fainali za ngazi zote za kanda, Taifa na kimataifa, zitafanyika katika awamu mbili, ya Fainali za Tuzo za Utalii, Hifadhi za taifa, Hifadhi za Bahari, Mapori ya akiba, Utalii wa ndani, Utamaduni, Vipaji ,Jamii, Wanyamapori, Mazingira, Uwekezaji, Mitindo, Michezo, Wadhamini, Biashara, Viwanda na Uchumi.
Tofauti na mashindano mengine ya urembo nchini, shindano hili ni la urembo wa kitalii na kitamaduni ambalo ni zaidi ya shindano la urembo kwani ni tafsiri ya vitendo ya sera za Taifa za Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, Mazingira, Misitu, Wanyama Pori, Michezo na Mazingira, ambalo lina lenga katika kuhamasisha na kutangaza Utalii, Utamaduni na Utalii wa Kitamaduni, Uwekezaji na Mianya ya Uwekezaji, Wanyamapori na Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu, Mazingira na Uharibifu wa Mazingira, Michezo na Utalii wa Michezo, Kumbi za Mikutano na Utalii wa Mikutano, Hifadhi za Bahari na utalii wa Bahari, Vita dhidi ya Tamaduni kongwe na Potofu, Ujasiliamali na Ujasiliamali wa Kitalii ,vita dhidi ya Ujinga, Umasikini na Maradhi, Viwanda na Bidhaa za Tanzania.
Mavazi ya mashindano haya ni yale yaliyo buniwa na wabunifu wa Kitanzania kwa malighafi zinazo zalishwa na kupatikana Tanzania tu, ambayo haya mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yenye kuzingatia mila ,desturi na tamaduni za kitanzania. Sifa kuu za washiriki wa shindano hili ni pamoja na kuwa msichana kwa asili mwenye Elimu isiyo pungua kidato cha sita, cheti cha chuo au zaidi, mwenye ngozi ya asili, uraia wa nchi yake kwa mujibu wa sheria, urefu wa angalau sentimita 168 japo ni vyema zaidi ikiwa ni sentimita 174 au zaidi, afya njema ya akili na mwili, tabia njema, tegemeo na mfano wa kuigwa katika jamii, dira, dhamira na mguso nafsi kwa jamii na Taifa ya kushiriki shindano hili (Vision, Mission and Platform).
Bodi mpya ya mashindano inaundwa na Erasto Gideon- Mwenyekiti Mtendaji, Georgina Saulo- Mkurugenzi wa Mashindano na Matukio, Wakili Msomi Noel Shani- Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano ya Kimataifa, Wakili Msomi Jonson Kaijage- Mkurugenzi wa Protokali, Mahusiano na mawasiliano ya Umma , Wakili Msomi Anna Marealle-Mkurugenzi wa Ufundi,Utafiti na Ushauri, na Judith Masawe-Mkurugenzi wa Mafunzo, Viwango na Ukuzaji Vipaji. Shindano hili kuanzia mwaka huu, litaratibiwa na Taasisi ya Africa Tourism Promotion Centre (ATPC), ambayo ina uzoefu mkubwa wa uratibu wa matamasha na matukio ya promosheni za utalii kitaifa na kimataifa, ikiwemo ya World Tourism Awards, Tanzania Tourism Awards, Miss Tourism University World, National Parks International Marathon, World Great Safari Tour, Tanzania Great Safari Tour, Wildlife International Marathon, World Tourism Music Awards, Tanzania Tourism Music Awards, na Ant Poaching International Marathon, Cultural , Conference and Sports Tourism International Life Party. Kabla ya hapo shindano hilo lilikuwa likiratibiwa na Miss Tourism Tanzania Organisation moja kwa moja, kabala ya kuanza mfumo mpya wa mashindano haya ya kipekee nchini.
Miss Utalii Tanzania Alama ya Urithi wa Taifa, Utalii ni Maisha – Utamaduni ni Uhai