Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Article 1

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Madaktari na Wauguzi mara baada ya kutembelea chumba cha upasuaji cha hospitali ya Arusha Lutherani Medical Centre (ALMC) alipokwenda katika hospitali hiyo kuwashukuru kwa huduma na matibabu waliyoyatoa kwake alipopata ajali ya gari mwaka jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari,Wauguzi na wafanyakazi wa Arusha Lutherani Medical Centre (ALMC) mara baada ya kutembelea hospitali hiyo kuwashukuru kwa huduma ya matibabu waliyoitoa kwake na kwa wasidizi wake alipopata ajali ya gari mwaka jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura cha Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) Dk. Peter Mabula mara baada ya ya kuwasili katika hospitali hiyo jijini Arusha leo (16 Juni, 2019) kuwashukuru Madaktari,Wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa huduma na matibabu waliyoyatoa kwake na kwa wasaidizi wake alipopata ajali ya gari mwaka jana.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Madaktari,Wauguzi na wafanyakazi wa Arusha Lutherani Medical Centre (ALMC) alipokwenda katika hospitali hiyo kuwashukuru kwa huduma ya matibabu waliyoitoa kwake na kwa wasaidizi wake alipopata ajali ya gari mwaka jana.
………………….

WMU – Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amewashukuru Madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ya jijini Arusha kwa huduma na matibabu waliyoyatoa kwake na kwa wasaidizi wake alipopata ajali mbaya ya gari Agosti 4, 2018 katika eneo la Magugu mkoani Manyara.

Dk. Kigwangalla ametoa shukrani hizo wakati akizungumza na Madaktari, Wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre, jijini Arusha.

Akiwa ameambatana na mkewe Dk. Bayoum Awadh, amewashukuru na kuwapongeza madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo kwa matibabu waliyompatia kwa kipindi chote alichokuwa hospitalini hapo na kuwaomba waendelee kuwahudumia wananchi wenye shida.Amesema kazi ya udaktari, uuguzi na fani zote zilizo katika sekta ya afya ni za wito na kila anayezifanya inampasa azifanye kwa wito kutoka ndani ya moyo wake.

“Kazi ya udaktari, uuguzi na fani zote zilizo katika sekta ya afya kwa kiasi kikubwa ni kazi ambazo mtu anazifanya kutoka ndani ya moyo wake kuwahudumia wengine ambao wako katika madhira mbalimbali ya kiafya” Amesema Dkt. Kigwangalla.

Amesisitiza kuwa hakuna namna ambayo Daktari au Muuguzi anayetoa huduma ya kumtibu mtu, kumwondolea maumivu, au kumpa faraja mgonjwa anaweza kulipwa na malipo hayo yakalingana na kazi aliyoifanya.
Amesema kazi ya Udaktari na Uuguzi inafanywa na watu wachache ambao kwa kiasi kikubwa wanakua wameitika wito ama wametumwa na Mungu na kwamba mtu yeyote hawezi kusema kuna kipato au kitu utakachoweza kumlipwa kikamtosheleza au kukidhi umuhimu na ugumu wa kazi anayoifanya.

“Kwa dhati ya moyo wangu ninatoa shukrani zangu za dhati lakini pia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye kwa muda wote toka tulipopata ajali alikua akifuatilia afya zetu, ninaomba nifikishe kwenu shukrani za Serikali anayoiongoza ya kwamba tunatambua mchango wenu mkubwa” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla

Ameeleza kuwa yeye na wasaidizi wake waliopata ajali Agosti 4, 2018 walipita katika hospitali hiyo wakiwa na hali ngumu kiafya lakini kutokana na juhudi na upendo uliooneshwa na madaktari wa hospitali hiyo wakishirikiana na madaktari wa hospitali ya mkoa wa Arusha na KCMC waliweza kushughulika afya zao na kuokoa maisha yao.

“Tunawashukuru sana kwa yote mliyotenda, tunawaombea dua madaktari, wauguzi na watumishi wa kada zote zilizo katika sekta hii ya tiba hatuna cha kuwalipa zaidi ya kusema Mungu awabariki katika maisha yenu, awape mafanikio makubwa na ujuzi zaidi ili muendelee kuwasaidia wengine” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharura cha Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC), Dk. Peter Mabula akizungumza kwa niaba ya uongozi wa hospitali hiyo amesema kuwa kitendo cha Dkt. Kigwangalla kupanga muda wa kwenda kuwashukuru kimewapa nguvu na moyo wa kuendelea kufanya kazi vizuri zaidi.

Dk. Mabula amemwomba Mhe. Kigwangalla atenge muda mwingine wa kuitembelea hospitali hiyo pia afikishe salam zao kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwamba wataendelea kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wananchi.

WAKULIMA MBULU WAIOMBA SERIKALI KUWALETA WATAALAM WA KILIMO

$
0
0
Na Mwandishi Maalum; Mbulu 

Wakulima Wilayani Mbulu wameiomba serikali iwapelekee wataalamu wa kilimo na pembejeo za kutosha ili kuwawezesha kuwa na kilimo chenye tija zaidi. 

Ombi hilo lilitolewa na umoja wa Wamwagiliaji wa Skimu ya umwagiliaji ya Mangisa iliyopo katika kata ya Dongpbeshi, Wilayani Mbulu Mkoani Manyara walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji jana walipoitembelea skimu hiyo. 

Akizungumza kwa niaba ya umoja wa Wamwagiliaji katibu wa umoja huo Damiano Sulle alisema serikali kwa kushirikiana na wafadhili ilifanya jambo la msingi kuleta skimu ya umwagiliaji katika eneo hilo ambapo ameeleza kuwa imeleta tija kwani ndio ajira pekee iliyo badilisha maisha ya wakazi wengi katika kata ya Dongobeshii. 

“Kabla ya kuwepo kwa skimu hii mkulima aliweza kuvuna chini ya gunia kumi (10) kwa tani au kumi na tano (15) za kitunguu saumu kwa hekta na baada ya kuboreshwa kwa miundombiu ya kisasa ya umwagiliaji mkulima anaweza kupata hata gunia hamsini (50) ya zao hio kwa hekta” Alisema Bwana Sulle. 

Sulle ameiomba serikali kuwasaidia kusakafia mfereji ambao haujasakafiwa wenye urefu wa mita 50 ambao utawasaidia wakulima kujipanga vizuri hasa katika matumizi sahihi ya maji na kuongeza uzalishaji zaidi wa mazao. 

Sambamba na hilo wakulima wameomba serikali kuwatafutia soko la uhakika hususan la zao la kitunguu swaumu ili waweze kuuza zao hilo kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani kwani wana maghala makubwa ya kutosha ambapo wangeweza kuhifadhi mazao hayo na kuuyauza wakati ambao bei za mazao hayo zikiwa juu. 

Wilaya hiyo ya Mbulu ina eneo la Hekta 2400 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na hekta 1250 ndizo zinazotumika kwa kilimo hicho ambapo kuna skimu saba ambazo ni Mangisa, Dongobeshi,Tumati,Diyomati,Dirm, Ari na Bashay skimu ambazo zinatumika kwa kilimo cha zao la mahindi, Viazi, Shayiri na mazao mengine ya mbogamboga.
 Moja ya mfereji unaopeleka maji katika mashamba ya mazao ya mboga mboga na mahindi katika skimu ya Mangisa iliyopo wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
 sehemu ya miundombinu iliyojengwa na Serikali kupitika shirika la kimataifa  la maendeleo laJapan JICA chini ya uasimamizi wa Tume ya Taifa ya uwagiliaji  katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji Mangisa inayopokea maji kutoka kwenye mabwawa kupeleka katika mashamba ya mazao mbalimbali
 shamba linaloonyesha zao la kitunguu swaum zao ambalo limekuwa likiwangizia wakulima kipato kikubwa katika skimu ya umwagiliaji Mangisa iliyopo Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

MDAU ATOA MAONI KUHUSU KURUDISHWA KODI KWENYE PEDI

$
0
0
Mwaka jana wakati wa Bunge la bajeti serikali ilipiga hatua kubwa yenye mwelekeo sahihi wa kupunguza gharama anazoingia msichana na mwanamke kwenye kununua bidhaa za kujihifadhi wakati wa hedhi. Serikali ilitoa msamaha wa kodi (VAT 18%) kwa bidhaa za pedi, uamuzi ambao wengi tuliufurahia. 

Lakini mwaka mmoja baada ya kutolewa kwa kodi, serikali imeirudisha tena kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kutokana na kudai kuwa wafanyabiashara hawajapunguza bei kama ilivyokusudiwa.

Maoni yangu

Katika sera yoyote ambayo serikali inapitisha ni lazima serikali iwe mbele kwenye kuweka mikakati ya ufuatiliaji ili sera husika iweze kuzaa matunda na kuwanufaisha walengwa. Tumeona kwa mfano hata serikali ilipotaka kila mfanyabiashara awe na EFD mashine, wote hawakukubali kutekeleza kwa wakati mmoja. 

Lakini serikali ilikuwa na mikakati ikiwemo elimu kwa wafanyabiashara ya kwa nini ni muhimu kuwa na EFD mashine, na leo tunaona wafanyabiashara wengi wana EFD mashine, ingawa pia inawezekana wakawa sio wote. Je, serikali ilirudisha utaratibu wa wafanyabiashara kutokuwa na mashine kwa sababu tu ndani ya muda mfupi hawakutii sheria na kuinufaisha nchi na mapato? Hapana. 

Haya tumeona hata kwenye masuala mengine ambayo serikali imeyaanzisha kwa lengo la kunufaisha nchi kwa mapato na kusaidia walaji kama vitambulisho vya wafanyabiashara (na hapa mnufaika akiwa ni mfanyabiashara yeye mwenyewe) lakini bado wafanyabiashara walichukua muda kuitia wito.Serikali iliweka mikakati ya kufuatilia utekelezaji na kuhusisha viongozi kuanzia ngazi ya taifa (Waziri), mkoa na wilaya. Tumewahi kuona wakati mwingine serikali ikiweka hata bei elekezi mfano kwenye bidhaa kama mafuta n.k. 

Katika hili la kurudisha kodi kwenye bidhaa ya pedi, mimi naona serikali imetumia tathmini ya muda mfupi sana kuhitimisha kuwa kutolewa kwa kodi hii hakuwanufaishi walengwa. 

Mwaka mmoja ni muda mfupi sana, hasa pia kama hakukuwa na mikakati madhubuti kutoka ngazi ya taifa mpaka vijijini ya kuweka mpango kazi na washika dau wa kusimamia utekelezaji wa sera badala yake tukawaachia wafanyabiashara wenyewe wafuate agizo wakati inafahamika kuwa siku zote mfanyabiashara lengo lake la kwanza ni kutengeneza faida na si kunufaisha watu. 

Serikali ilikuwa na jukumu kubwa hapa kama mlinzi wa maslahi ya wananchi.Ilikuwa ni muhimu serikali iweze kushirikiana na washika dau kama ambavyo tumeona imefanya vizuri kwenye kusimamia utekelezaji wa marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki.

Kuna wengine wanasema kodi iliyoshushwa katika viwanda kutoka asilimia 30 kwenda 25 itasaidia kwa sasa. Naomba niseme, Hapana. Tunahitaji misamaha yote ili kupata unafuu mkubwa zaidi. Ingawa kodi katika uzalishaji imeshushwa kwa asilimia tano (5) ijimradi kodi ya ongezeko la thamani (VAT 18%) bado itakuwepo, bado mlaji wa mwisho hatapata unafuu. Siku zote mlaji wa mwisho ndio hulipa kodi inayoongezwa kwa wafanyabiashara na hiyo itakuwa hivyo hivyo kwa kodi hii ambayo imerudishwa kwenye bidhaa za hedhi. Bei zitapanda maradufu

Bidhaa ya pedi haikutakiwa hata kuuzwa in the first place,hasa kwa watu kama wanafunzi. Pedi ni essential need, wanawake hawachagui kupata hedhi,kututoza kodi kwa kupata hedhi kila mwezi, kwa kweli sio jambo la kibinadamu. Kwa hiyo tukisema tuweke lense ya Jinsia, bidhaa hii haikutakiwa hata kuuzwa, sema kwa sababu ya choices, ni muhimu soko liwe na bidhaa nyingi tofauti ili walaji wachague wenyewe chapa wanazopenda. Ila kwa watu kama wanafunzi hasa wa vijijini, bado si sawa kwanza kwa hii bidhaa kupatikana kwa kununua. Walitakiwa wapate BURE. 

Utafiti uliofanywa na UNICEF unaonesha kuwa wasichana hukosa siku nne (4) hadi tano (5) kwa mwezi kutokana na hedhi na msichana mmoja (1) kati ya kumi (10) huacha shule kila mwaka kutokana na kukosa vifaa vya kujihifadhia wakati wa hedhi. 

Suluhisho la muda mrefu hapa ilikuwa zipatikane bure, na kutolewa kodi kulikuwa kunaanza kutupeleka kwenye unafuu huo. Niseme, wafanyabiashara wana jukumu la kimaadili (moral obligation) la kuhakikisha hawajinufaishi na jitihada za kupunguza makali kwa walaji wa mwisho. Ubepari umekuwa ni sababu kubwa pia inayomdidimiza mwanamke na mtoto wa kike, sababu wenyewe umejikita zaidi kwenye kupata faida na sio maendeleo ya watu.


Mapendekezo

1. Serikali ifute pendekezo la kurudisha kodi kwenye pedi, msamaha wa kodi uendelee kubaki kama ulivyopitishwa mwaka jana. Kurudisha kodi kwenye pedi ni kuendelea kumtoza msichana na mwanamke kodi kwa kupata hedhi ambayo si sawa kiubinadamu. 

2. Serikali na washika dau waweke mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kuhakikisha bei inashuka kwa kuandaa mikutano na wafanyabiashara katika eneo hili na ikiwezekana kuwepo na muda elekezi wa namna ambavyo mpango kazi utafanyiwa kazi ili kuleta unafuu kwa walengwa

3. Serikali iangalie uwezekano wa kuweka bidhaa ya pedi kwenye list ya essential needs kwenye sheria ya kodi ili kuhakikisha unafuu wa bei ni endelevu na hautabadilika badilika kila wakati

4. Kuwepo na mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha pedi inakuwa ni bidhaa inayopatikana bure hasa kwa wanafunzi ili kuhakikisha wanabaki shule na kusoma na kupunguza mdondoko kwa watoto wa kike kwenye kupata elimu.


By Rebeca Gyumi

NGOMA AFRICA BAND TO ROCK 9th INTERNATIONAL AFRICAN FESTIVAL TUBINGEN,GERMANY 2019

$
0
0
The popular Ngoma Africa band will be among many acts expected to thrill fans at the 9th International African Festival in Tübingen, Germany. The extravanganza will take place from 29 July - 4th August 2019.

.Ngoma africa band will appear live on stage on the Saturday 3rd Augost 2019

Ngoma Africa, based in Germany, founded 1993 by bandleader Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja, is home to a number of talented musicians, including soloist Christian Bakotessa aka Chris-B. Others are Jo Souza, Matondo Benda, Aj Nbongo, Flora William, Jessicha Ouyah, Vially Nbongo, and others.

The band, followed by millions worldwide, is famous for driving audience crazy with “Extraordinary Rhythm” Bongo dance from East Africa.

Ngoma Africa has released numbers of CDs, including latest “BONGO TAMBARARE” , "Mapenzi ya Pesa" and "Hapa Kazi Tu 2019" which you can listen to at www.reverbnation.com/ngomaafricaband

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 17,2019

SERIKALI YAITAKA MIKOA KUANZISHA MABARAZA YA WATOTO

$
0
0
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Akizindua kitini cha Ajenda ya wajibu wa wazazi wa Malezi na matunzo ya familia Nchini Tanzania   wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisoma kitini cha  kitini cha Ajenda ya wajibu wa wazazi wa Malezi na matunzo ya familia Nchini Tanzania wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu Akizindua Kijarida cha Kisura chenye lengo la kutoa elimu juu ya madhara ya mimba za  utotoniwakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita. 
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Geita Muhandisi Robert Gabriel  wakiangalia viatu vya katika banda la Kikundi cha Vijana Cluster cha Shirati Rolya Mkoani Mara wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.
 Watoto mbalimbali kutoka Shule zilizoko Mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita wakiwa katika maandamano  wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.

Na Ripota Wetu GEITA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  ameiagiza mikoa ambayo haijaanzisha mabaraza ya watoto Ncini kufanya hivyo mara moja kama hatua muhimu ya kutekeleza haki ushiriki watoto katika maamuzi mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wao.

Waziri Mwalimu amesema hayo leo  Mkoani Geita wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoitimishwa leo katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa iliyo  katika mji mdogo wa Katoro Mkoani Geita.

Ameitaja mikoa ambayo haijaanzisha Mabaraza ya Watoto kuwa ni mikoa ya Tanga, Mbeya, Mtwara, Simiyu Kigoma Mara na Manyara kuitaka kufanya hivyo mara moja ili kutekeleza haki ya ushirikishwaji watoto lakini pia kuimarisha ulinzi wa mtoto hapa Nchini.
Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa   katika kuimarisha haki ya ushiriki wa mtoto, Serikali kwa kushirikiana na wadau imeendelea kuhimiza Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuongeza bajeti ya kuwezesha mabaraza ya watoto. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu Mabaraza hayo Waziri Mwalimu alisema mabaraza hayo  yanatoa fursa kwa watoto kujadili masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wao na pia kuishauri Serikali kuhusu masuala hayo. 

Aidha Waziri Ummy aliongeza kuwa mpaka kufikia mwezi Machi, 2019 serikali ilianzisha mabaraza ya watoto 19 katika ngazi ya mikoa, mabaraza 121 katika ngazi ya Halmashauri za  Manispaa,Wilaya,Miji, mabaraza 733 katika ngazi ya Kata na mabaraza 795 katika ngazi ya kijiji,Mtaa akiyataja mabaraza hayo kuwa mchango mkubwa katika kuwajengea watoto uwezo wa kujieleza na kujiamini ambayo ni silaha muhimu katika kujilinda na vitendo vya ukatili.

Waziri Mwalimu ameongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa nchini, watoto wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukatishwa masomo kwa kupewa mimba, kuolewa katika umri mdogo na kutopewa fursa zaidi ya kuendelea kimasomo kwa sababu mbalimbali.

Wzairi Ummy alisisitiza kuwa takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Vishiria vya Malaria ya mwaka 2016 inaonyesha kuwepo kwa ongezeko la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hapa nchini hususan wasichana akizitaja takwimu hizi kuonesha  kuwa kiwango cha kitaifa kwa ndoa za utotoni ni 37% wakati mimba za utotoni  zikiwa 27% na ukeketaji 10%.

Aidha, Takwimu za Jeshi la Polisi za mwaka 2018 zinaonyesha kuwepo kwa matukio 14,419 yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali vya polisi hapa nchini ikilinganishwa na matukio 13,457 kwa mwaka 2017 ambalo ni ongezeko la matukio 1034 sawa na 7.7%.

Waziri Mwalimu ameitaja Mikoa 5 inayoongoza kwa ukatili dhidi ya watoto nchini kuwa  ni Tanga (1039), Mbeya (1001), Mwanza (809), Arusha (792) na Tabora (618) huku akiyataja matukio yanayoongoza kwa ukatili kuwa  ni Ubakaji (5557), Mimba (2692), Kulawiti (1159), Shambulio (965) na Kujeruhi (705).
Kuhusu ulinzi wa motto Waziri Ummy aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya matoto hapa nchini imeratibu uanzishwaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto katika mikoa 26, Halmashauri za Wilaya,Manispaa.Miji na Majiji 176, Kata 1,640 na Vijiji,Mitaa 5,609 akiongeza kuwa kamati hizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanawake na watoto.

Aidha  Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali imeshatoa maelekezo ya kuanzishwa kwa madawati ya ulinzi wa watoto shuleni ili kuboresha mfumo wa upatikanaji wa huduma kwa wahanga wa ukatili na kuimarisha ulinzi wa watoto wawapo shuleni.

Akiongea na Wakati wa Kilele cha Maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Geita  Mhandisi Robert Gabriel  amewaambia wananchi Mkoani mwake kuwa sifa ya mwanaume siyo tu kuzaa watoto bali ni kulinda mke pamoja na watoto kwa kuwapatia mahitaji muhimu  na kufanya kazi kwa bidii.

Aidha Mhandisi Gabriel amewataka wanaume kote Nchini kuacha kutafuta heshima baa na badala yake watumie muda mwingi na familia zao ili kuweza kuchangia katika malezi ya watoto ili waweze kufikia ndoto zao.  

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika uadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16, Juni na tayari yameitimishwa leo Mkoani Geita katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkapa katika Mji wa mdogo wa Katolo na kuitimishwa rasmi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Ummy Ally Mwalimu.


KANISA la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT), limfungulia kesi mwenyekiti wao wa udhamini

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

KANISA la Evangelistic Assemblies Of God Tanzania (EAGT), limemfungulia kesi katika baraza la ardhi mtoto wa marehemu, Mchungaji John Mfuko aliyekuwa Mwenyekiti wa wadhamini wa kanisa hilo, Frida Mfuko kwa madai kuwa amevamia eneo lililopo katika kiwanja namba 154 Kitalu II kilichopo Temeke.

Kesi hiyo yenye namba 127/2019, imefunguliwa na kanisa hilo katika Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Temeke mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Amina, ambapo mdai namba moja ni EAGT.

Mbali na dhehebu hilo, wadai wengine waliofungua kesi hiyo ni Mchungaji Sara Samson, Wilbroad Adebe na Enosi Ndembeta ambao ni wazee wa kanisa liliko katika eneo linalogombaniwa, ambapo wote wanadai kuwa Frida amevamia eneo hilo.

Kesi hiyo, inatarajiwa kuanza kusikilizwa Julai 19,2019 ambapo Sara na wenzake waliwasilisha zuio wakiomba isikilizwe chini ya hati ya dharura huku Frida akiomba apewe muda wa kuwasilisha utetezi wake.

Aidha, kabla ya kesi hiyo kupelekwa mahakamani, viongozi wa jimbo wa EAGT walifika katika eneo hilo linalogombaniwa na kumtangaza Mchungaji Samson kuwa mchungaji katika kanisa aliloliacha Marehemu Mchungaji John, jambo ambalo limekataliwa na waumini wa kanisa hilo.

Akizungumza hivi karibuni, Frida amesema baba yake ni mmoja wa waanzilishi wa kanisa hilo tangu 1993, baada ya kutokea kwa mgogoro katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) ambapo baba yake, Marehemu Mchungaji Mfuko alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa EAGT hadi pale kifo kilipomkuta Agosti Mosi, 2018.

Amesema Mei 5,2013 wajumbe watatu wa bodi ya wadhamini walikaa kikao na kuidhinisha kuwa kiwanja hicho si mali ya EAGT bali ni mali ya Marehemu Mchungaji John Mfuko na hivyo,wadhamini waliaamua kumilikisha kiwanja hicho. 

"Baraza la wadhamini lilifanikiwa kuandaa nyaraka za kubadilisha hati ya kiwanja hicho na kumilikisha rasimi marehemu na hivyo hati ya kiwanja ikabadilishwa kutoka jina la The Registered Board of Trustees Of EAGT, na kuwekwa jina la Rev John Henry Mfuko mmiliki halali wa kiwanja hichi na shule iliyopo katika kiwanja hicho ambayo pia imesajiliwa kwa jina la marehemu", alisema Frida 

Ameongeza, kabla ya kufariki baba yake alikuwa akihoji viongozi wakuu wa kanisa la EAGT kuhusu tuhuma za kuingiza magari nchini kwa kutumia jina la EAGT ikiwa magari hayo hayapo ndani ya umiliki wa EAGT na ukiwa kuna ukwepaji wa kodi ya Serikali

Aidha, watoto wa marehemu wamelaani kitendo hicho cha kutaka kuwafukuza na kuwanyanganya mali ya baba yao ikiwa viongozi wa EAGT wanajua fika kuwa kiwanja kile pamoja na majengo yaliyopo na shule ni mali ya marehemu Mchungaji Mfuko.

Dk. Kigwangalla kuchangisha fedha za kutokomeza VVU kupitia Mlima Kilimanjaro

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Khamis Kigwangala amesema anatarajia kuandaa utaratibu wa makundi ya watu mbalimbali wakiwamo viongozi mashuhuri na wasanii kupanda mlima Kilimanjaro ili kuchngisha fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi

Dk. Kigwangala ametoa kauli hivi karibuni mkoani Kilimanjaro wakati akizindua zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro lililoshirikisha zaidi ya watu 80 kutoka nchi mbalimbali kwa lengo la kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kupitia kampeni ya ‘Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019’.

Kampeni hiyo ambayo iliyoratibiwa na Mgodi wa dhahabu ya Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kudhibiti Ukimwi nchi (TACAIDS) pia imelenga kutunisha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF)

Alisema wizara ya maliasili na utalii itaanda utaratibu wa kuhamasisha makundi ya watu mbalimbali ikiwemo wasanii na watu mashuhuri duniani kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi kwani mapambano ya virusi hivyo ni ya watu wote na sio ya serikali pekee.

“Takwimu za maambukizi mapya hususan katika kundi la vijana yanatisha na kwamba zinahitajika jitihada za makusudi kutoka Katika kundi hilo kudhibiti ugonjwa huo.

“Hali ya maambukizi mapya ya VVU yanatisha ni lazima sisi Kama vijana tuwe msitari wa mbele kupambana na hali hii, kwa mwaka nimepanga kupanda Mlima huu na watu mashuhuri ikiwemo wanasiasa na wasanii ili kuchangisha fedha kwaajili ya kudhibiti ugonjwa huu.

“Lakini pia nimefurahi kuona kuwa miongoni mwa wanufaika wa kampeni hii ni wapagazi takribani 150 waliopatiwa mafunzo ya kujilinda na VVU na masuala mbalimbali kuhusu udhibiti wa Ukimwi. Kundi hilo pia limepatiwa mafunzo ya ujasiriamali kwa lengo la kuwasaidia wawe na kipato endelevu,” alisema.

Aidha, Mkurugenzi wa Tacaids, Dk. Leonard Maboko, alisema kila siku watu zaidi ya 200 huambukizwa VVU ambapo Kati yao asilimia 80 ni vijana kwanzia miaka 15-24.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) Richard Jordinson, kampeni hiyo imewezesha ukusanyaji wa zaidi ya Sh bilioni 13 tangu ilipoanzishwa miaka 17 iliyopita.

Alisema kampeni ya mwaka huu zaidi ya watu 80 wameshiriki ambapo kati yao 32 watapanda mlima, 28 watauzunguka kwa kutumia baiskeli na watu 17 kutoka nchi mbalimbali wameshiriki kampeni hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro.

“Upandaji huo utachukua siku saba ambapo wameanza kupanda Juni 15 na kushuka Juni 22 mwaka huu,” alisema Alisema tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo miaka 17 iliyopita zaidi ya taasisi binafsi na mashirika 50 yanayotoa misaada na elimu ya Ukimwi nchini yamenufaika na kampeni hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii. Dk. Hamis Kigwangalla (wa pili kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi na washiriki wa kampeni ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za kutomomeza VVU nchini. Kampeni hiyo iliyodumu kwa miaka 17 sasa imeratibiwa na Mgodi wa dhahabu GGM na Tacaids
Waziri wa Maliasili na Utalii. Dk. Hamis Kigwangalla (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Richard Jordinson katika hafla ya uzinduzi wa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kukusanya fedha za kutomomeza maambukizi ya VVU nchini. Zaidi wa wapandaji 80 wameshiriki kampeni hiyo inayoratibiwa na GGM kwa kushirikiana na Tacaids.
Baadhi ya washiriki wa kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro 'Kili challenge 2019' inayoratibiwa na GGM kwa kushirikiana na TACAIDS kwa lengo la kukusanya fedha za kutokomeza maambukizi ya VVU na Ukimwi nchini. Zoezi la upandaji mlima huo limezinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangalla.

TAARIFA YA KUZIMWA KW AMTAMBO WA UZALISHAJI MAJI RUVU JUU

BREAKING NEWZZZZZ:Wema Kukaa Mahabusu siku nane

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru aliyekuwa Miss Tanzania 2006  na Msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu kukaa mahabusu hadi Juni 24.2019 wakati akisubiri maamuzi ya dhamana, baada ya kukiuka masharti.

WANAFUNZI WA KIKE WANATAKIWA KUZINGATIA MASOMO

$
0
0
NA DENIS MLOWE, IRINGA

WANAFUNZI wa vyuo vikuu mkoani Iringa wametakiwa kuzingatia zaidi masomo kuliko kujihusisha na maisha ya starehe ambayo yamekuwa yakiwagharimu wengi wao kutotimiza ndoto walizojiwekea pindi wafikapo vyuoni.

Akizungumza katika kongamano kubwa la wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu vilivyoko mkoani hapa makada wa Chama cha Mapinduzi, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jeska Mbogo amewataka wanafunzi hao kuzingatia zaidi masomo kuliko kupoteza muda kwenda katika kumbi za disco na kuwa na mahusiano na wanaume na kusisitiza kuelekeza akili katika masomo kwa mambo ya kidunia watayakuta .

Mbogo alisema kuwa imekuwa kasumba ya wanafunzi wengi wa kike kuanzisha mahusiano ambayo hayana faida yoyote katika maisha yao ambapo baadhi yao wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kujiingiza katika mapenzi katika umri mdogo ama kwa kudanganywa na makundi rika au kudanganywa kwamba wakijihusha na mapenzi na walimu watafanya vyema katika mitihani yao.

Alisema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakijiingiza kwenye mambo ya anasa na starehe badala ya masomo huku wakisahau kuwa wazazi wao wanatumia nguvu nyingi katika kuwasomesha kwa gharama kubwa katika kulipia ada ya masomo na kuja kushawishika na wanaume wasiokuwa na malengo nao.

Aliongeza kuwa katika maisha ya kila siku endapo unataka kufanikiwa mwanamke unatakiwa kujitambua nini lengo la kufika chuoni, kujithamini utu wako, kujielewa na kujiamini kutakuletea mafanikio ambayo unayataka katika kutimiza ndoto za maisha yako hapo mbeleni.

Mbogo aliwataka wanafunzi hao kujikubali jinsi walivyo kwani ndivyo Mungu ndivyo alivyowaumba na kuachana na tabia ya kujibadilisha maumbile kwa kutumia dawa za kachina ili kubadili muonekano wa maumbo yao ili kuonekana wazuri wakati ni bora kujikubali ulivyo kuliko kutaka kuisha maisha ya kuwaonyesha watu bila kutambua madhara ya mbele yatakuwaje.

Katika kongamano hilo, Mbogo alikabidhi kadi zaidi ya 100 kwa wanafunzi hao kujiunga na Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) wa CCM mkoa wa Iringa ambapo wanafunzi hao waliomba kupatiwa mafunzo ya ujasiriamali katika vyuo wanavyotoka kuweza kujikomboa kiuchumi na kuwaahidi kuwapatia mafunzo hayo.

Alitoa wito kwa wazazi kutenga muda wa kuwa karibu na Watoto wao na kuzungumza nao kwani wazazi wengi wamekuwa wako bize kutafuta hela na kusahau kukaa na kuzungumza na Watoto wao jambo ambalo linazidi kuendeleza mmomonyoko wa maadili kwa Watoto wao.

Naye Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Iringa, Rose Tweve aliwataka wanafunzi wa kike kujiamini katika Maisha yao kwani hakuna kitu kinachoweza kumkomboa mwanadamu kama kujiamini kwani watu wote waliofanikiwa duniani walijiamini na kuthubutu na ndio maana wamefanikiwa.

Rose aliwataka vijana hao kutokuwa watu wakulaumu au kulalamika bali wawe ni watu wa kufanya kazi kwa vitendo kulisaidia Taifa lao kwani ni fahari sana kusema wewe nimelifanyia nini Taifa lako kuliko kusema kusema Taifa lako limekufanyia nini .
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jeska Mbogo akisalimiana na mmoja ya wanawake wa UWT mkoa wa iringa wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Iringa.
 Katibu wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Iringa, Chiku Masanja akiwatambulisha baadhi ya wajumbe wa kamati ya uwt mkoa wa Iringa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jeska Mbogo .
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jeska Mbogo akizungumza na wajumbe na viongozi wa UWT mkoa wa Iringa.
 Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Jeska Mbogo , akikabidhi kadi kwa mmoja wa wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu mkoani Iringa kujiunga na UWT.

WIZARA YA MADINI, FEDHA ZASAINI MAKUBALIANO YA MKAKATI WA UKUSANYAJI WA MADUHULI

$
0
0
Leo tarehe 17 Juni, 2019, Wizara ya Madini na Wizara ya Fedha na Mipango zimesaini makubaliano ya mkakati wa ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya shilingi bilioni 475.

Hafla ya utiaji wa saini wa makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dodoma, ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ya Madini na Tume ya Madini ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Kamishna wa Madini, David Mulabwa, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi,  Mhasibu Mkuu kutoka Wizara ya Madini, Athony Tarimo na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini, Augustine Ollal.

Viongozi kutoka Tume ya Madini waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Dk. Venance Mwase, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tume, William Mtinya, Mwanasheria wa Tume ya Madini, Salome Makange, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma aliyewakilisha Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, Jonas Mwano na watendaji wengine.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Doto James alisema kuwa mbali na kusaini makubaliano hayo, Wizara yake itatoa kiasi cha shilingi bilioni 10.7 kama fedha zitakazotumika kwenye mradi wa kimkakati wa ukusanyaji wa maduhuli kulingana na vigezo vilivyotolewa.

Aliendelea kusema kuwa, lengo la kutoa fedha hizo ni kuiwezesha Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kufikia lengo la ukusanyaji wa maduhuli lililowekwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 la shilingi bilioni 475.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akizungumza kwenye hafla hiyo aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kuongeza kuwa Wizara ya Madini pamoja na Tume ya Madini imejipanga kuhakikisha lengo lililowekwa la ukusanyaji wa maduhuli limetimia.

Alisema kuwa, fedha zinazotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango zitatumika kuboresha ukusanyaji wa maduhuli kupitia ununuzi wa vifaa vya kupimia madini pamoja na magari yatakayotumika kufika sehemu zote zenye shughuli za uchimbaji wa madini na kukusanya maduhuli.
Katika hatua nyingine, Profesa Msanjila alisema kuwa ili kuongeza usimamizi kwenye ukusanyaji wa maduhuli, hivi karibuni Wizara kupitia Tume ya Madini ilitangaza ajira kwa vibarua na kuongeza kuwa kwa sasa mchakato wa ajira unafanyika ili kuwapata wenye vigezo.

Aidha, Profesa Msanjila aliwashukuru wadau wote wa madini nchini kwa ushirikiano walioonyesha na kusisitiza kuwa Serikali ipo tayari kuwasaidia ili waweze kunufaika na Sekta ya Madini.
Aliipongeza Tume ya Madini kwa kufanya kazi kwa kujituma pamoja na changamoto zote zilizokuwepo hivyo kuwezesha Serikali kufikia lengo la ukusanyaji wa maduhuli kutokana na Sekta ya Madini kwa mwaka 2018/2019.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula mbali na kuishukuru Serikali kwa fedha hizo, alisema Tume ya Madini ina nia ya dhati ya kuisaidia Serikali kwenye  ukusanyaji wa maduhuli.
Alisisitiza kuwa, Tume ya Madini inaendelea kusimamia kwa karibu zaidi masoko ya madini yaliyoanzishwa hivi karibuni nchini kote, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya madini.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Simon Msanjila (kushoto) akisaini makubaliano ya mkakati wa ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019/2020  kati ya  Wizara ya Madini na Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma tarehe 17 Juni, 2019. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Simon Msanjila (kushoto) na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kulia) wakibadilishana nyaraka mara baada ya utiaji saini wa makubaliano ya mkakati wa ukusanyaji wa maduhuli kwa mwaka wa fedha 2019/2020  kati ya  Wizara ya Madini na Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma tarehe 17 Juni, 2019
Viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Madini na Tume ya Madini wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (mbele)

MILLYA AWASHUKURU SUKURO NA KITIANGARE KUKALIZA MGOGORO WA MIAKA 202

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya amewashukuru wananchi wa Vijiji vya Sukuro na Kitiangare waliomaliza mgogoro wao uliodumu zaidi ya miaka 20 wakigombea Kitongoji cha Katikati.

Mgogoro huo ulishasababisha mtafaruku mkubwa baina ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Henry Shekifu na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Christopher Ole Sendeka mwaka 2010.

Ole Millya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sukuro na Kitiangare aliwapongeza wananchi wa vijiji hivyo viwili kwa kuridhia kwa pamoja na kuachana na malumbano na mgogoro usiokuwa na tija kwao.

Alisema katika mgogoro huo yeye binafsi alikaa pembeni bila kupendelea kijiji chochote kwani vyote viwili ni vya kwake hivyo hakupaswa kupendelea kimoja aliwaachia wataalamu wagawe vitongoji kama sheria inavyoelekeza.

"Nawapongeza sana wananchi wa vijiji vya Kitiangare na Sukuro kwani hali ya amani haikuwepo lakini sasa mmemaliza mgogoro wenu na kuridhia kwa pamoja kuishi kama ndugu kwani mlikuwa kijiji kimoja kabla ya kugawanywa," alisema Ole Millya.

Alisema hivi sasa hali ya amani na upendo imerejea baina ya vijiji hivyo viwili kama awali na wananchi wanasalimiana kwa furaha, wanaoleana na kunywa maji pamoja.

Alisema kupitia mfuko wa jimbo anatoa sh6 milioni kwa vikundi vya wanawake wa vijiji vyote viwili na sh4 kwa mradi wa maji kijiji cha Sukuro na darasa la shule ya kijiji cha Kitiangare.

Mkazi wa kijiji cha Sukuro, Lengai Ole Makoo alipongeza hatua ya kumalizika kwa mgogoro huo usiokuwa na tija uliosababishwa na baadhi ya wanasiasa wa wilaya hiyo.

Ole Makoo alisema kijiji cha Sukuro kimebakiwa na vitongoji vyake vitano na kijiji cha Kitiangare kimebaki na vitongoji vyake viwili kama ambavyo kanuni, taratibu na sheria zilivyofuatwa wakati kijiji mama cha Sukuro kilipogawanywa.

"Kijiji cha Sukuro kimebaki na vitongoji vya Katikati, Lembutwa, Lenjani, Mouwara na Lasepa na Kitiangare imebaki na vitongoji vya Loongung na Kitiangare," alisema.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alimpa onyo Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Awadhi Omary na baadhi ya wanasiasa juu ya kutumika kwa maslahi yao katika mgogoro huo.
 Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Sukuro alipotembelea eneo hilo.
 Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Kitiangare.
Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Millya akizungumza juu ya upendo na kuondokana na makundi na ubaguzi ili lengo la kuwa na Simanjiro moja yenye amani na kutobaguana itimie

Wizara ya Nishati, TANESCO NA REA wajadili mipango ya usambazaji umeme kwa mwaka 2019/20

$
0
0
Ili kuhakikisha kuwa kazi ya usambazaji umeme mijini na vijijini inafanyika kwa kasi na ufanisi katika mwaka wa fedha 2019/20, viongozi wa Wizara ya Nishati wakiongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani wamefanya Mkutano wa siku moja na watendaji wa TANESCO na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ili kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha lengo hilo linafanikiwa.

Mkutano huo, uliofanyika tarehe 16 Juni, 2019, ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Menejimenti ya TANESCO, REA na Bodi ya REA, ulijadili kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 na kujipanga katika utekelezaji wa majukumu kwa mwaka wa fedha wa 2019/20 unaoanza mwezi Julai.

Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho ni upelekaji umeme viwandani, kuimarisha hali ya umeme katika maeneo yaliyounganishwa na gridi, kuunganishia umeme Taasisi za umma, kuunganishia umeme maeneo yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme, bei ya kupeleka umeme vijijini, ununuzi vifaa vya umeme, utambuzi wa wateja wanaohitaji umeme viwandani na utambuzi wa wazalishaji wadogo wa umeme.

“ Kimsingi lazima tuhakikishe tunaimarisha huduma za umeme kwa kutatua kero mbalimbali kama za kukatika kwa umeme na kutowaunganishia umeme wateja ndani ya muda uliopangwa hivyo lazima tujipange sasa kukamilisha shughuli zetu kwa ukamilifu ili kuwezesha nchi kuingia kwenye uchumi wa viwanda.” Alisema Dkt Kalemani

Suala la upelekaji umeme viwandani, Waziri wa Nishati, amesema kuwa ni la kipaumbele na ametoa miezi mitatu kwa Mameneja wa TANESCO wa Wilaya kuwasilisha takwimu ya viwanda walivyoviunganishia umeme kwenye maeneo yao.

Aidha, amewaagiza kuhakikisha kuwa, wanafanya jitihada za kuunganishia umeme viwanda vinavyoanzishwa kwenye maeneo yao kabla havijakamilika kwa kupeleka bili stahiki kwa wenye viwanda ili waweze kufanya malipo mapema hivyo TANESCO kutoonekana kuwa ni chanzo cha kukwamisha ufanyaji kazi wa kiwanda.

Kuhusu upelekaji umeme vijijini, Dkt Kalemani amesema kuwa kila mtumishi wa Wizara, TANESCO na REA lazima atambue kuwa, lengo la Serikali ni kupeleka umeme katika Vijiji vyote ifikapo Juni 2021 hivyo ni lazima kila mmoja ahakikishe kuwa hilo linafanikiwa na bei ya kuunganisha umeme ni 27,000 na Meneja asiyetaka kutekeleza hilo aachie ngazi.

Aidha, kuhusu Wazalishaji wadogo wa umeme ameelekeza Mameneja wa TANESCO wilayani kuhakikisha kuwa, wanawatambua wazalishaji hao, wanawapa elimu, miongozo, wanawasimamia na kuwaingiza katika programu za uzalishaji umeme.

Suala jingine lililojadiliwa ni ununuzi wa vifaa vya umeme, ambapo Dkt Kalemani amesema kuwa mtendaji anapaswa kusimamia utekelezaji wa agizo la Serikali la kutonunua nje vifaa vya umeme vinavyopatikana nchini ili kurahisisha ufuatiliaji wa vifaa hivyo pia kuokoa muda mrefu ambao ungetumika kusafirisha vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

Suala la uunganishaji umeme kwa wateja wa muda mrefu pia lilijadiliwa ambapo Waziri wa Nishati ametoa mwezi mmoja kwa TANESCO kuunganishia umeme wateja wote waliolipia umeme kwa muda mrefu na bado hawajaunganishwa na umeme.

Kazi ya kushusha umeme kwenye maeneo yaliyopitiwa na miundombinu ya umeme ameagiza kuwa, kazi hiyo ianze mwezi wa Saba mwaka huu na ikamilike ndani ya miezi Sita.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesisitiza kuhusu upelekaji umeme kwenye Taasisi za umma kama vile Shule, Zahanati na Visima vya Maji kutokana na umuhimu wake kwa jamii zinazozunguka maeneo hayo na kuagiza kuwa suala hilo liwekewe mkakati maalum.

Vilevile amempongeza Waziri wa Nishati kwa kuwa na utaratibu wa vikao kazi ambavyo vimekuwa na tija katika uendelezaji wa Sekta ya Nishati nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua amempongeza Waziri wa Nishati kwa Mkutano huo na kuahidi kuwa changamoto mbalimbali zilizojadiliwa kwenye Mkutano zitafanyiwa kazi.

Aidha, amegiza watendaji wa Taasisi zilizohudhuria Mkutano huo kutekeleza ipasavyo maagizo yaliyotolewa na Waziri wa Nishati na kuendelea kufanya kazi kwa bidii.

Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amemshukuru Waziri wa Nishati kwa kufanya Mkutano huo ambao unasaidia kuboresha utendaji kazi na kutoa wito kwa TANESCO kuendelea kutatua changamoto mbalimbali kama za kukatika umeme na kutounganishia umeme wateja ndani ya muda mfupi.
 Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO wakiwa katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizungumza wakati wakati wa kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
 Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO wakiwa katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
 Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TANESCO wakiwa katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua akizungumza katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na TANESCO wakiwa katika kikao baina ya Wizara ya Nishati, TANESCO na REA kilichofanyika jijini Dodoma na kuongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani.

TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KUHAKIKIWA KUANZIA JUNI 23 HADI JULAI 02, 2019


TFS KUFANYA MAONESHO KWA SIKU SABA MFULULIZO KUELEZEA SHUGHULI WANAZOFANYA KWA WATANZANIA

$
0
0
 Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inafanya maonesho ya Utumishi wa Umma-siku saba mfululizo ambayo yatafanyika ndani ya makao makuu ya wakala huo kuanzia Juni 17 hadi 23,mwaka huu wa  2019. 

Maonesho hayo ambayo yatazinduliwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  Profesa Dos Santos Silayo yamebeba kaulimbiu inayosema “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi,”.

Akizungumza  leo  jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi TFS,  Emanuel Wilfred amesema TFS itafanya maonesho hayo kwa kipindi cha siku saba kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa 12 jioni ili wananchi waone shughuli zinazofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. 

“Wananchi watajionea na kuelimika na mambo mbalimbali yanahohusu uhifadhi wa misitu,ufugaji nyuki, na biashara ya mazao ya misitu na utalii na pia kuwapa fursa wananchi kutoa maoni na malalamiko juu ya huduma tunazotoa,’’amesema Emanuel. 

Kupitia kauli mbiu hiyo amesema TFS itaeleza ni namna gani wanapambana na vitendo vya uharibifu wa misitu na udhibiti wa ukusanyaji mapato katika utoaji wa huduma kwa wananchi na pia kuwaeleza wananchi mipango iliyopo katika kuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu ya mazao ya misitu na nyuki. 

Katika maonesho hayo watalaam waliobobea kutoka maeneo mbalimbali ya Wakala watakuwepo ambao ni maafisa misitu, maafisa nyuki, maofisa masoko, watoa leseni, na wataalamu wa Tehama ili kukutana na wananchi watakaojitokeza. 

Maadhimisho hayo ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kufanya maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi zake na pia kongamano kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma. 

Pi maonesho hayo huratibiwa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Umma na Utwala Bora ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia 16 hadi 23 Juni.

SERIKALI YANUNUA MASHINE 62 ZA KUSAFISHIA DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO

$
0
0
Na WAMJW- DSM 

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kusogeza huduma za matibabu ya figo kwa kununua mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo na kuzisambaza katika Hospitali za Rufaa za mikoa nchini.

Hayo yamejiri mapema leo katika tukio la kupokea mashine hizo kutoka kwa kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief wakiongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini zenye jumla ya shilingi Bilion 1.55, lililoongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Dkt Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kusambaza na kuboresha huduma hizi na kwa sasa zinapatikana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi.

"Sisi kama Serikali tumeendelea kuboresha hizi huduma, kwa sasahivi zinapatikana Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi" alisema Dkt. Ndugulile 

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaendelea kuboresha huduma hizi licha ya kuwepo changamoto ya idadi kubwa ya wahitaji wa huduma hizi huku akidai kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuna mashine 42 huku zikifanyika sesheni tatu kwa siku, na zinafanyika kwa siku 6 katika kila wiki, 

Aidha, Dkt Ndugulile amesema kuwa, msaada huo wa vifaa vitavyosambazwa katika mikoa tisa nchini ikiweko mikoa ya Tanga, Mwanza, Kigoma, Kagera, Arusha, Iringa, Mtwara, Unguja na Zanzibar, hali itayosaidia kupunguza gharama kwa kuwasogezea wagonjwa huduma hizo.

Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ndani ya miaka mitatu Serikali imefanikiwa kupunguza magonjwa yakuambukiza kwa asilimia 50%, huku akikiri kuwa bado kuna changamoto kubwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo yakuambukiza kama vile kisukari, presha na figo ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mitindo ya maisha.

"Timepiga hatua kubwa sana katika magonjwa yakuambukiza, ambayo tumeyapunguza kwa asilimia 50% ndani ya miaka mitatu, tumepunguza vifo na maambukizi ya Malaria, lakini tumepunguza vile vile maambukizi ya Ukimwi, sasa changamoto inayotukabili ni magonjwa yasiyo yakuambukiza kama, kisukari, presha na magonjwa ya figo"alisema Dkt Ndugulile. 

Akiongea kwa niaba ya kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Naibu Balozi wa Saudia Arabia nchini Ahmed Bin Saleh Alghamdi ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada inayoendelea kuchukua katika kutatua changamoto kwenye Sekta ya Afya na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo baina ya nchi hizo mbili.
 Baadhi ya mashine za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zilizotolewa na kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief kwa kuongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini, zilizopokelewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akimshukuru Naibu Balozi wa Saudi Arabia baada ya makabidhiano ya mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo, tukio limefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile akiteta jambo na Naibu Balozi wa Saudi Arabia Bw. Ahmed Bin Saleh Alghamdi wakati wa makabidhiano wa mashine 62  za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zilizotolewa na kituo cha King Salman  Humanitarian and Relief, tukio  limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Balozi wa Saudi Arabia nchini Bw. Ahmed Bin Saleh Alghamdi akisaini mkataba wa makabidhiano wa mashine 62  za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zenye thamani ya shilingi Bilion 1.55 zilizopokelewa Leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa tukio la kupokea mashine 62  zakusafishia damu kwa wagonjwa wa figo, tukio limefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Serengeti Breweries yatangaza mabadiliko ya uongozi wa juu

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa uzalishaji wa bia nchini, Serengeti Breweries Limited (SBL) imemteua Mark Ocitti kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya kuchukua nafasi ya Helene Weesie anayeondoka.

Helene amekuwa na SBL kwa miaka minne kuanzia mwaka 2015, kipindi ambacho kampuni imeweza kuzindua bidhaa muhimu zilizosababisha ukuaji wa biashara kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kampuni kupata tuzo za ubunifu na kuongezeka kwa uwekezaji. 
Helene anaondoka kwenda kuchukua nafasi nyingine ndani ya Diageo barani Ulaya. Akiwa nchini Tanzania atakumbukwa, bali na mambo mengine, kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya ndani ya nchi.

Mkurugenzi mtendaji mpya, Mark Ocitti, kwa sasa anahudumu katika nafasi sawa na hiyo katika kampuni ya Uganda Breweries Limited (UBL) ambayo pia ni sehemu ya kampuni mama ya East Africa Breweries Limited (EABL) inayoongoza kwa uzalishaji wa vinywaji katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ocitti, chini ya uongozi wake, UBL imeweza kupiga hatua kubwa katika utendaji wake na kupelekea kukua kwa biashara.

Akizungumzia uteuzi wa Ocitti, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa EABL, Andrew Cowan amesema: “Mark amefanya mageuzi makubwa katika biashara yetu nchini Uganda; ameongeza nafasi yetu kiushindani na kukuza faida ya UBL kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Sina shaka kwamba kutokana na uzoefu wa uongozi wa Mark, maono, pamoja na mipango mikakati yake shupavu, itaifanya biashara ya SBL, inayokua kwa kasi kukua hata zaidi.”

SERIKALI YAPOKEA MSAADA WA MASHINE 62 ZA KUSAFISHIA DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO

$
0
0
SERIKALI YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA FIGO KWA WANANCHI 

Na WAMJW- DSM 
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yaendelea kusogeza huduma za matibabu ya figo kwa kupokea jumla ya mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo na kuzisambaza katika Hospitali za Rufaa za mikoa nchini.

Hayo yamejiri mapema leo katika tukio la kupokea mashine hizo kutoka kwa kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief wakiongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini zenye jumla ya shilingi Bilion 1.55, lililoongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Dkt Ndugulile amesema kuwa Serikali inaendelea kusambaza na kuboresha huduma hizi na kwa sasa zinapatikana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi.

"Sisi kama Serikali tumeendelea kuboresha hizi huduma, kwa sasahivi zinapatikana Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, Hospitali ya Bugando, Hospitali ya KCMC na baadhi ya Hospitali binafsi" alisema   Dkt. Ndugulile 

Aliendelea kusema kuwa, Serikali inaendelea kuboresha huduma hizi licha ya kuwepo changamoto ya idadi kubwa ya wahitaji wa huduma hizi huku akidai kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuna mashine 42 huku zikifanyika sesheni tatu kwa siku, na zinafanyika kwa siku 6 katika kila wiki, 

Aidha, Dkt Ndugulile amesema kuwa, msaada huo wa vifaa vitavyosambazwa katika mikoa tisa nchini ikiweko mikoa ya Tanga, Mwanza, Kigoma, Kagera, Arusha, Iringa, Mtwara, Unguja na Zanzibar, hali itayosaidia kupunguza gharama kwa kuwasogezea wagonjwa huduma hizo.

Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema kuwa ndani ya miaka mitatu Serikali imefanikiwa kupunguza magonjwa yakuambukiza kwa asilimia 50%, huku akikiri kuwa bado kuna changamoto kubwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo yakuambukiza kama vile kisukari, presha na figo ambayo kwa kiasi kikubwa yanatokana na mitindo ya maisha.

"Timepiga hatua kubwa sana katika magonjwa yakuambukiza, ambayo tumeyapunguza kwa asilimia 50% ndani ya miaka mitatu, tumepunguza vifo na maambukizi ya Malaria, lakini tumepunguza vile vile maambukizi ya Ukimwi, sasa changamoto inayotukabili ni magonjwa yasiyo yakuambukiza kama, kisukari, presha na magonjwa ya figo"alisema Dkt Ndugulile. 

Akiongea kwa niaba ya kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief Naibu Balozi wa Saudia Arabia nchini Ahmed Bin Saleh Alghamdi ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa jitihada inayoendelea kuchukua katika kutatua changamoto kwenye Sekta ya Afya na ameahidi kuendeleza ushirikiano huo baina ya nchi hizo mbili.
 Baadhi ya mashine za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zilizotolewa na kituo cha King Salman Humanitarian Aid and Relief kwa kuongozwa na ubalozi wa Saudia Arabia nchini, zilizopokelewa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akimshukuru Naibu Balozi wa Saudi Arabia baada ya makabidhiano ya mashine 62 za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo, tukio limefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile akiteta jambo na Naibu Balozi wa Saudi Arabia Bw. Ahmed Bin Saleh Alghamdi wakati wa makabidhiano wa mashine 62  za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zilizotolewa na kituo cha King Salman  Humanitarian and Relief, tukio  limefanyika katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Naibu Balozi wa Saudi Arabia nchini Bw. Ahmed Bin Saleh Alghamdi akisaini mkataba wa makabidhiano wa mashine 62  za kusafishia damu kwa wagonjwa wa figo zenye thamani ya shilingi Bilion 1.55 zilizopokelewa Leo na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndugulile katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) wakati wa tukio la kupokea mashine 62  zakusafishia damu kwa wagonjwa wa figo, tukio limefanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.

Tigo yawapeleka washindi watatu Misri kushuhudia AFCON

$
0
0

Washindi wa promosheni ya Soka la Afrika inayoendeshwa na kampuni ya Tigo wakiwa na nyuso za furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa tiketi za kwenda nchini Misri kushuhudia michuona ya mataifa ya Afrika. Wa kwanza kulia ni Kalaghe Rashid akifuatiwa na Rehema Kassim pamoja na Godfrey Muta. 


Mtaalamu wa Huduma za ziada kutoka Tigo Ikunda Ngowi(wa pili kulia)akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kukwakabidhi washindi wa promosheni ya Soka la Afrika tiketi za kwenda kushuhudia mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri. Kulia ni mshindi kutoka Tanga Rehema Kassim na wa kwanza kushoto ni Godfrey Muta akifuatiwa na Kalaghe Rashidi wote kutoka Dar es Salaam
Mtaalamu wa Huduma za ziada kutoka Tigo Ikunda Ngowi aimkabidhi Godfrey Muta ambaye ni mmoja kati ya washindi watatu wa droo ya kwanza ya Promosheni ya Soka la Afrika tiketi ya kwenda nchini Misri kushuhudia michuona ya mataifa ya Afrika.

Mtaalamu wa Huduma za ziada kutoka Tigo Ikunda Ngowi aimkabidhi Rehema Kassim ambaye ni mmoja kati ya washindi watatu wa droo ya kwanza ya Promosheni ya Soka la Afrika tiketi ya kwenda nchini Misri kushuhudia michuona ya mataifa ya Afrika.
Mtaalamu wa Huduma za ziada kutoka Tigo Ikunda Ngowi aimkabidhi Kalaghe Rashid ambaye ni mmoja kati ya washindi watatu wa droo ya kwanza ya Promosheni ya Soka la Afrika tiketi ya kwenda nchini Misri kushuhudia michuona ya mataifa ya Afrika.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images