Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

WAREMBO 15 WAFANIKIWA KUPITA MCHUJO WA AWALI WA MASHINDANO YA MISS TANGA.

$
0
0
  Na Khadija seif,Globu ya jamii

JUMLA ya warembo 15 wamefanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka miss Tanga mwaka huu,2019.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Tanga muandaaji wa shindano hilo Chuchu Hansy amesema warembo walijitokeza wengi kiasi kwamba wote ni wazuri na wana vigezo vya kuingia kambini.

"Warembo  mkoa wa Tanga wamejitokeza wengi kiasi imekua ngumi kwa majaji kuchagua yupi anastaili kuingia kwenye kinyang'anyiro hiki lakini tumeweza kutoa nafasi ya upendeleo na kuongeza baadhi ya washiriki na hatimae idadi kufikia 15,"

Hata hivyo Chuchu amewataka warembo watakapoingia kambini kuwa na nidhamu ya hali ya juu kuanzia kwa viongozi wao wakiwa Kama walezi wao na kwa warembo watakaoonyesha utovu wa nidhamu hatuwaonea huruma kuwaondoa.

"Sitosita kumuondoa mrembo yoyote atakaye kuwa hana nidhamu,hata Kama atakuwa ni mrembo mzuri na mwenye vigezo vyote kuanzia elimu,figa ,rangi na kipaji,"alisisitiza Chuchu.

Amesema kwa sasa sasa warembo wanatarajia kuingia kambini julai 1 mwaka huu .



DKT MABULA ATAKA KUPITIWA UPYA MKATABA MAUZIANO NYUMBA 4000 VINGUNGUTI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Uuzaji Nyumba 4000 katika eneo la Vingunguti Dar es Salaam pamoja na Kampuni ya PMM 2001 Ltd inayonunua nyumba hizo walipokutana katika ofisi za Wizara jijini Dodoma mwishoni mwa wiki wakati wa kutafuta muafaka wa ununuzi nyumba hizo. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Bona Kamoli, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati Ramadhani Pepo, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utumishi wa Kampuni ya PMM 2001 Ltd Damian Kanuti na wa tatu kushoto ni Katibu wa Kamati Ibrahim Mkumbi. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Katibu wa Kamati ya Kusimamia Uuzaji Nyumba 4000 katika eneo la Vingunguti Dar es Salaam Ramadhani Pepo alipokutana na Kampuni ya PMM 2001 Ltd inayonunua nyumba hizo pamoja na Kamati jijini Dodoma mwishoni mwa wiki wakati wa kutafuta muafaka wa ununuzi nyumba hizo. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Bona Kamoli, wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utumishi wa Kampuni ya PMM 2001 Ltd Damian Kanuti na wa tatu kushoto ni Katibu wa Kamati Ibrahim Mkumbi (PICHA NA WIZARA YA ARDHI) 


Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameagiza kupitiwa upya Mkataba wa Mauziano ya nyumba baina ya Kampuni ya PMM 2001 Ltd na Wamiliki wa nyumba 4000 wakazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam. 

Uamuzi huo unafuatiwa kutozingatiwa kwa masharti ya Mkataba ulioingiwa awali ambao umeonekana kuwa na mapungufu mengi ya kisheria na hivyo kusababisha kampuni ya PMM 2001 Ltd kushindwa kuwalipa Wamiliki wa nyumba katika eneo la Vingunguti kwa takriban miezi tisa kama walivyokubaliana jambo lililozua taharuki kwa wamiliki wa nyumba hizo. 

Dkt Mabula alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki baada ya kukutana na pande zote mbili za Kamati inayosimamia makubaliano ya uuzaji nyumba 4000 katika mitaa minne ya Vingunguti ambayo ni Mnyamani, Mtambani, Mtakuja na Faru, kampuni ya PMM 2001 Ltd na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bona Kamoli katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, baada ya kupitia Mkataba wa mauziano ya nyumba katika eneo la Vingunguti kati ya Kampuni ya PMM 2001 Ltd na Wamiliki wa nyumba katika eneo la Vingunguti wamebaini mkataba kutofuata taratibu za kisheria na kubainisha kuwa wamiliki ambao hawajalipwa fedha yoyote hawabanwi na mkataba huo na wanaweza kuzifanyia shughuli yoyote nyumba zao. 

Alisema, kwa zile nyumba themanini (80) ambazo kampuni ya PMM 2001 Ltd ilizinunua kwa wamiliki katika eneo hilo, Wizara yake itatuma timu maalum kufuatilia iwapo Kampuni hiyo imefuata taratibu zote za mauziano ikiwemo kutoa kodi ya serikali na kuongeza kwa kuitaka kuhakikisha inakamilisha taratibu za kumilikishwa nyumba hizo.. 

Akigeukia suala la Wamiliki wa nyumba 17 ambao kampuni hiyo imewalipa shilingi milioni 35 kwa kila mmoja kama fedha za awali, Naibu Waziri wa Ardhi aliagiza hatua za kisheria zifuate kwa kuwa Mkataba wa Mauziano hauoneshi kiasi kilichobaki baada ya kutolewa cha awali sambamba na muda wa ukamilishaji malipo jambo lililosababisha Wamiliki kufuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio. 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, ilichofanya kampuni ya PMM 2001 Ltd kwa Wamiliki ni udanganyifu unaoweza kutoa mwanya mkubwa kupoteza haki yao na kusisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano haiko tayari kuona wananchi wanapata tabu kufuatilia haki zao na kuiagiza kampuni hiyo kuwaeleza Wamiliki itawalipa lini kiasi kilichobaki ili kuondoa mkanganyiko. 

Hata hivyo, Dkt Mabula alisema, atamuagiza Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam kuzungumza na wananchi wanaouza nyumba kwa kampuni hiyo na yeye mwenyewe atakupokuwa mkoani humo katika ziara yake atazungumza na wakazi hao wa Vingunguti kuhusiana na sakata hilo. 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha na Utumishi wa Kapmuni ya PMM 2001 LTD Damian Kanuti alijitetea kwa kueleza kuwa kampuni yake ilishindwa kutekeleza makubaliano ya ununuzi wa nyumba katika mitaa ya Vingunguti kutokana na kuchelewa kupata mkopo ilioutarajiwa kutoka Benki ya TIB na kubainisha kuwa pamoja na sakata hilo lakini kampuni yake ilishalipa kiasi cha bilioni 1.7 ikiwa ni malipo ya nyumba 80 na fedha ya awali kwa Wamiliki 17. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Uuzaji nyumba 4000 katika eneo la Vingunguti Ramadhani Pepo ameilalamikia kapuni ya PMM 2001 Ltd kwa kutoonyesha ushirikiano kwa kamati wakati wa zoezi hilo jambo alilolieleza kuwa limesababisha Kamati kufikisha malalmiko kwa Mbunge wa Jimbo la Segerea Bona Kamoli na hatimaye kwa Naibu Waziri wa Arhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kwa lengo la kupatiwa ufumbuzi 

Pepo alisema, kutokana na Kampuni ya PMM 2001 Ltd kushindwa kutekeleza makubaliano yaliyokuwa yatekelezwe Septemba 2018 wamechoka kufuatilia suala hilo na wanachotaka kwa sasa ni wao waliolipwa fedha za awali kukamilishiwa kiasi kilichopaki na hawako tayari kuendelea na zoezi hilo tena kwa kuwa kampuni hiyo imeshindwa kuonesha ushirikiano. 

Mbunge wa jimbo la Segerea Bonna Kamoli ameitaka kampuni ya PMM 2001 Ltd kueleza bayana kiasi cha fedha kilichobaki kwa wamiliki wa nyumba 17 zitalipwa lini lakini Mkurugenzi wa Fedha na Utumishi wa PMM 2001 Ltd Kanuti alishindwa kutoa jibu na kutaka kampuni yake kupewa muda kulifanyia kazi suala hilo.

Dar yatamba mbio za mita 100 UMISSETA 2019

$
0
0
Mshindi wa kwanza hadi wa tatu kwa upande wa wavulana, wakimaliza mbio za mita 1500 leo asubuhi katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Mwanariadha Regina Deogratius kutoka mkoa wa Pwani akimaliza mbio za mita 1500 na kujinyakulia medali ya dhahabu katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara leo asubuhi
Mwanariadha Teresia Nicholaus wa Singida ambaye alishika nafasi ya pili katika mbio za mita 1500 akivuka mstari kuashiria kukamilika kwa mbio hizo. Teresia alionekana kuwa kivutio kwenye mbio hizo kutokana na kasi aliyoionyesha kulinganisha na umbo lake. 

******************* 



Na Mathew Kwembe, Mtwara 

Mkoa wa Dar es salaam umeendelea kutamba katika mashindano ya UMISSETA yanayoendelea katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara kufuatia mkoa huo kutoa mshindi wa kwanza na wa pili katika fainali za mbio za mita 100 kwa upande wa wavulana katika fainali zilifanyika leo asubuhi. 

Mwanariadha Ismail Tosil akitumia sekunde 11:49 alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mbio hizo na hivyo kujitwalia medali ya dhahabu, huku mwanariadha mwenzake Elias Silverster ambaye alitumia sekunde 11: 50 pia kutoka Dar es salaam kushika nafasi ya pili na kujinyakulia medali ya fedha, huku nafasi ya tatu ilichukuliwa na mwanariadha Geofrey Maganga kutoka mkoani Dodoma aliyetumia sekunde 11:68 na kujinyakulia medali ya shaba. 

Kwa upande wa wasichana, Mwanariadha Emmy Hosseah kutoka mkoani Singida amefanikiwa kutwaa medali ya dhahabu katika mbio za mita 100 baada ya kuwaacha nyuma wenzake, Leocadia Joho kutoka Tabora aliyeshika nafasi ya pili na Zawadi Juma wa Mara aliyeshika nafasi ya tatu. 

Emmy alifanikiwa kumaliza mbio hizo baada ya kutumia sekunde 13:16, huku Leokadia Joho akitumia sekunde 13:48 na Zawadi Juma aliyejitwalia medali ya shaba alitumia sekunde 13:70. 

Katika mbio za mita 1500, mwanariadha Japhet John kutoka mkoani Singida alitwaa medali ya dhahabu kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kutumia dakika 4:12:31, huku nafasi ya pili kwa upande wa wavulana ikishikwa na Lusengulano Faida kutoka Mwanza aliyetumia dakika 4:12:88, na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Emanuel Petro kutoka Shinyanga ambaye alitumia dakika 4:13:58. 

Katika mbio za mita 1500 wasichana, aliyetwaa medali ya dhahabu ni mwanariadha Regina Deogratius kutoka Pwani ambaye alimaliza mbio hizo baada ya kutumia dakika 4:44:67, nafasi ya pili ikichukuliwa na Teresia Nicholaus kutoka Singida ambaye alitumia dakika 4:49:25 na nafasi ya tatu ilikwenda kwa mwanariadha Yusta Ninga kutoka mkoa wa Manyara baada ya kutumia dakika 4:50:49.

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atembelea Makumbusho

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Aldof Mkenda akifurahia chungu na vibuyu vilivyotumika kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar vilivyohifadhiwa Makumbusho ya Taifa. Kulia kwake ni Dkt Agnes Gidna mtaalamu wa Akiolojia, Makumbusho ya Taifa na Mkurungezi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof audax Mabulla (wa kwanza kulia) kushoto kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi wa Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ndugu Deograsias Mdamu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Aldof Mkenda akipata maelezo kuhusu fuvu la binadamu wa kwanza kutoka kwa mtaalum wa Akiolojia Dkt. Agnes Gidna alipotembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Aldof Mkenda akionyesha kwa kidole fuvu la mwanadamu wa kwanza lijulikanalo kam Zinjanthropus alipotembelea Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Katika ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Prof. Audax Mabula na mbembeni yake ni Dkt Agnes Gidna.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof Adolf Mkenda jumamosi tarehe 15 Juni, 2019 alitembelea Makumbusho ya Taifa kujionea urithi na hazina kubwa ya Taifa la Tanzania. Urithi huu wa utamaduni na asili ni pamoja na mafuvu na masalia ya binadamu wa kale au zamadamu, kama Australopithecus afarensis, Zinjanthropus (Paranthropus) boisei, Homo habilis, Homo erectus na Homo sapiens sapiens, yenye umri wa tangu miaka milioni 3.6 had miaka 200,000 iliyopita. 

Akiwa Makumbusho ya Taifa, Pof. Mkenda alijadiliana na kuielekeza Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa hatua ambazo Wizara ya Maliasili na Utalii inachukua kuimarisha sekta ya malikale na hususan, Shirika la Makumbusho ya Taifa la Tanzania. 

“Wizara inaiimarisha na kuijengea uwezo Makumbusho ya Taifa ili itimize majukumu yake ya msingi ya kutafiti, kuhifadhi, kuonesha na kuelimisha umma juu ya urithi wa Taifa na dunia kwa ujumla”. 

Prof. Mkenda, aliyasema hayo alipotembelea chumba maalumu cha kuhifadhia mikusanyo adhimu, na kujionea masalia hayo ya binadamu wa kale, hati ya Uhuru wa Tanganyika, tai ya uhuru, kinyago maarufu cha kimakonde na chungu, mchanga na vibuyu halisi vilivyotumiwa na Baba wa Taifa Mwal. Julius K. Nyerere kuchanganya mchanga kama ishara ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Aprili, 1964. 

Prof. Mkenda alisema kuwa kufika kwake Makumbusho ya Taifa inadhihirisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imejipambanua na inajali na kuthamini urithi wa Taifa na iko tayari kuulinda urithi huu kwa gharama yoyote kwa sababu ukipotea haupatikani tena. 

“Vitu hivi ni muhimu na ni urithi wetu, hivyo tunatakiwa kuvitunza kwa gharama yoyote kwani ni utambulisho wa Taifa la Tanzania, vinaleta amani, mshikamano, uzalendo na furaha. Aidha, vinavutia watalii wa ndani na nje na hivyo kuongeza pato la Taifa”, alisema Prof. Mkenda. 

Akizungumza na menejemeti na baadhi ya wataalamu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Mkenda ameweka wazi kuridhishwa na uhifadhi na kazi iliyofanywa na Makumbusho ya Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Usalama wa Majengo ya Serikali ya kukiimarisha chumba hicho maalumu. 

Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo alimuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa na Menejimenti yake kuimarisha zaidi uhifadhi na ulinzi wa urithi huu wa nchi yetu na dunia kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. 

Fuvu la Zinjanthropus lenye umri wa miaka milioni 1.75 iliyopita liligunduliwa kwenye bonde la Olduvai, Ngorongoro tarehe 17 July, 1959 na wataalamu wa Akiolojia Dkt. Louis Leakey na mke wake Dkt. Mary Leakey. 

Uguduzi huo ulibadilisha uelewa wa wanasayansi kuhusu mchango wa bara la Afrika katika sayansi ya chimbuko la binadamu duniani. Masalia ya Zinjanthropus (Paranthropus) boisei pamoja na masalia mengine ya binadamu wa kale (kama Homo habilis, Homo erectus), zana zao za mawe na masalia ya mifupa ya wanyama waliyokula bonde la Olduvai miaka milioni 2.0-1.0 iliyopita, vinathibitishia dunia kuwa Tanzania ndiyo nchi pekee yenye taarifa bora na sahihi kuhusu chimbuko la binadamu na utamaduni wake (tabia, teknolojia, chakula na namna ya kupata chakula hicho) katika kipindi hicho; na kwamba bonde la Olduvai ndilo Chimbuko la Binadamu wote duniani (the Cradle of Humankind). 

Prof. Mkenda ameitaka Makumbusho ya Taifa kuanzisha kampeni ya kutangaza vivutio mbalimbali ambavyo vinapatikana katika makumbusho zetu yakiwemo masalia ya binadamu wa kale. 

“Elimu hii na vitu nilivyoviona leo nimefurahi sana, lakini Watanzania wangapi wanavijua? Serikali ya Awamu ya tano inajipambanua kujali na kujivunia vitu vyetu, lugha yetu ya Kiswahili, maliasili zetu, malikale zetu na utamaduni wetu, alisema Prof Mkenda.. 

Alisema matangazo kwenye luninga, redio na magazeti kuhusu vitu vinavyotunzwa Makumbusho ya Taifa, yatajenga uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa makumbusho na hivyo, kufanya watu wengi kuja kutembelea makumbusho zetu. 

“Msipotangaza hakuna anayewezea kujua kuwa vitu muhimu kama hivi viko hapa Makumbusho ya Taifa, tunatakiwa tuwaambie wananchi ili waje kuviona,” alisisitiza. 

Prof. Mkenda alisema, “tunapoelekea kwenye maadhimisho ya miaka 60 tangu kugunduliwa kwa fuvu la Zinjanthropus, fuvu hilo, halitaondolewa Makumbusho ya Taifa kwenda bonde la Olduvai, bali litaendelea kuhifadhiwa na kutunzwa vizuri Makumbusho ya Taifa na badala yake nakala itatumika pale inapohitajika. 

Aidha, amesisitiza kuwa matangazo hayo yawe ya ndani na nje ya nchi (International Promotion) kwa sababu kuna watafiti wengi nje ya Tanzania ambao wangependa kuja kufanya utafiti katika Nyanja za akiolojia na paleontolojia. 

Sambamba na hilo, aliwaagiza Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Dkt. Freddy Manongi na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabulla, kuisimamia Kamati inayohusika na maandalizi ya maadhimisho hayo kubuni na kupanga matukio mbali mbali yatakayoleta hamasa katika kuadhimisha miaka 60 ya ugunduzi wa Zinjanthropus na kutangaza vivutio mbalimbali vilivyoko Tanzania. 

Alisisitiza kuwa matukio tofauti yaandaliwe kuanzia mwezi Julai mpaka Desemba mwaka huu kama sehemu ya kumbukumbu ya ugunduzi wa fuvu la Zinjanthropus boisei.

Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru yazindua bonanza la michezo

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud, Arusha 

Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru (TICD) imezindua bonanza la michezo kwa wanafunzi na watumishi wa taasisi hiyo yakiwa na lengo la kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli pamoja na kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya katika kuelekea uchumi wa viwanda. 

Akizungumza jana wakati wa kuzindua bonanza hilo lenye jina la TICD maendeleo bonanza 2019,Kaimu mkuu wa chuo hicho, Dokta Bakari George alisema kuwa, lengo la bonanza hilo lenye kauli mbiu ya “vijana nguvu kazi ya Taifa kufikia uchumi wa kati “ni kumuunga mkono na kumpongeza Rais Magufuli katika juhudi nzuri anazofanya katika kuelekea uchumi wa viwanda . 

Dokta Bakari alisema kuwa, wamekuwa wakihamasisha michezo chuoni hapo kila mwaka kwa lengo la kuunganisha mahusiano mazuri kati ya watumishi wa taasisi hiyo pamoja na wanafunzi sambamba na kuibua vipaji mbalimbali. 

Alisema kuwa, bonanza hilo limekuja muda muafaka ambao wanafunzi wanaelekea katika mitihani ambapo itawawezesha kuwandaa vyema katika kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na maandalizi ya timu ya taasisi hiyo kujiandaa katika kushiriki mashindano ya michezo ya vyuo vikuu mwezi wa kumi yatakayofanyika jijini Mwanza. 

“bonanza hili litasaidia pia kuinua vipaji mbalimbali vya wanafunzi wetu katika kuipenda michezo wakiwa tangu wadogo ,kwani kuna wanafunzi wengi wana vipaji vizuri katika michezo mbalimbali hivyo wanahitaji kujengewa uwezo kama hivi ili waendelee kuipenda michezo hiyo. “alisema Dokta Bakari. 

Mhadhiri na Mratibu wa michezo hiyo katika taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru, Elifadhili Mpehongwa alisema kuwa, wamekuwa wakifanya Bonanza hilo kila mwaka ambapo huu ni mwaka wa tatu kufanya bonanza hilo ambapo limekuwa na manufaa makubwa hasa kujenga mahusiano mazuri kati ya watumishi na wanafunzi. 

Alisema kuwa, bonanza hilo limeshirikisha timu 6 ambapo timu 5 ni za wanafunzi huku timu moja ikiwa ya watumishi wa taasisi hiyo na imeshirikisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa Pete, mpira wa wavu, drafts na mpira wa pool table ambapo mwisho wa siku ni kuweza kupata wataalamu wazuri waliobobea katika michezo mbalimbali. 

Aliongeza kuwa, lengo la bonanza hilo pia ni kuweza kuufufua mchezo wa draft ambao umesahaulika Sana na una historia kubwa katika nchi yetu na unahitaji kuendelezwa kwa kasi kwani ni mchezo ambao hautumii nguvu na unachezwa na watu wa umri wowote. 

“katika bonanza hili mshindi wa kwanza atapatiwa mbuzi wawili, huku mshindi wa pili na wa tatu wakipatiwa mbuzi moja moja na tumefadhiliwa na kampuni ya bia ya Heineken kupitia kinywaji chake chake cha Aimstell ambao wameahidi kuendelea kutusaidia zaidi katika michezo mbalimbali. “alisema Mpehongwa. 

Mmoja wa wachezaji wa mpira wa miguu, Yohana Makala alisema kuwa, uwepo wa michezo hiyo kwenye vyuo inasaidia Sana kuweka mahusiano ya karibu kati ya watumishi na wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuwawesha wanafunzi kujiepusha na makundi mbalimbali yasiyofaa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ampa pole Mkurugenzi Uendeshaji Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas

$
0
0


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimpa pole, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas, kwa kufiwa na watoto wake wawili, Maisam na Alliazgar Tarimba Abbas, nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimpa pole, Mke wa Mkurugenzi wa Uendeshaji Sport Pesa Tanzania, Tarimba Abbas, Warda Tarimba Abbas kwa kufiwa na watoto wake wawili, Maisam na Alliazgar Tarimba Abbas, nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Juni 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Benki ya Exim Yapewa Tuzo kwa Uchangiaji wa Damu Nchini

$
0
0
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim Tanzania Bw Stanley Kafu (Kulia) akipokea tuzo maalum kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ikiwa ni utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha suala la uhamasishaji na uchangiaji wa damu salama hapa nchini katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tanzania kutoka makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo, Bw Arafat Haji (katikati) wakichangia damu katika Maadhimisho hayo.
Pamoja na wafanyakazi pia baadhi ya wateja wa benki hiyo walijitokeza kwa wingi makao makuu ya benki hiyojijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitolea damu.

  Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine Ulimwenguni katika kuadhimisha Siku ya Wachangiaji Damu Duniani, Benki ya Exim Tanzania imekabidhiwa tuzo maalum kutoka serikalini ikiwa ni utambuzi wa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha suala zima la upatikanaji wa damu salama hapa nchini.

Benki hiyo imekabidhiwa tuzo hiyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika Maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha mwishoni mwa wiki iliyopita yakiwa na kauli mbiu ‘Damu Salama Kwa Wote’

Akiipongeza benki hiyo kwa ushiriki wake mkubwa kwenye jitihada za upatikanaji wa damu salama hapa nchini, Waziri Ummy ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo pia aliihimiza benki hiyo kuendelea kuwa balozi imara wa damu salama hapa nchini sambamba na kuhamasisha taasisi nyingine na watu binafsi kuungana na benki hiyo katika kufanikisha mpango huo muhimu.

“Serikali imetenga Sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha 2019/20 zitakazotumika kujenga vituo vidogo vya uchangiaji damu salama katika mikoa 12 nchini.’’ Alisema Ummy ambae pia alizindua mashine mpya ‘full automation’ za kupima maambukizi katika damu na za kupima makundi ya damu ambazo zimesimikwa kwenye vituo vya kanda sita ikiwamo Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Mtwara na Mbeya.

“Tunataka kumfikia kila mtanzania mwenye mahitaji ya damu salama popote alipo tuhakikishe anapata damu salama bila kikwazo chochote. WHO inakadiria idadi ya watu 1000 zipatikane chupa 10 za damu, Watanzania tunakadiriwa tupo milioni 55 tunapaswa kupata asilimia moja ya idadi hiyo, hivyo chupa 550,000 zinahitajika kila mwaka kutosheleza mahitaji,” alisema.

Akizungumza kuhusiana na tuzo hiyo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema: "Benki ya Exim tumepokea tuzo na heshima hii kutoka serikalini kwa mikono miwili kwa kuwa ni sehemu ya matokeo chanya ya mkakati wa benki ya Exim ya uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’. Hivyo tuzo na heshima hii ni kama chachu ya sisi kuendelea kujitoa zaidi katika kufanikisha mpango wa damu salama hapa nchini,’’ alisema

Kwa mujibu wa Bw Kafu, mapema mwezi huu benki hiyo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) walianza utekelezaji wa pamoja wa mpango wa uchangiaji wa damu uliohusisha matawi yote ya benki hiyo hapa nchini hususani katika mikoa minane ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Tanga, Mtwara na Zanzibar.

"Sisi ni mojawapo ya taasisi ambazo zinaendesha huduma zake katika sehemu kubwa ya nchi hii na huduma yetu inagusa idadi kubwa ya watu. Tunaguswa na jamii tunayoihudumia na tunaamini jamii yenye afya ni muhimu katika kutimiza malengo yetu. Na hiyo ndio sababu tumeelekeza rasilimali zetu pamoja na maeneo ya ofisi zetu kama kambi za kukusanyia damu,’’ alisema Kafu

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii. Katika miaka minane iliyopita benki imechangia zaidi ya chupa 1000 za damu katika Benki ya damu taifa.  



KADA CCM ANENA JAMBO KUHUSU MEMBE, AMTAKA ZITTO AKAE KIMYA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ALIYEKUA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametakiwa kuachana na mawazo ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao wa Urais.

Kauli hiyo imetolewa na Kada wa CCM, Ally Mwinyi Simba jijini Dar es Salaam leo ambapo amemtaka Membe na wenzake kufuta wazo la kuwa Rais hadi hapo Rais Magufuli atakapostaafu.

" Tumeshasikia tetesi za wao kuwaza kuweka nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa 2020, Ndugu Membe na wengineo waendelee na shughuli zao nyingine watuachie Mwenyekiti na Rais wetu Magufuli amalizie kazi aliyoianza.

" Tena wakae wakijua wazi hili tutalisimamia kwa nguvu zetu zote kwa sababu tuna imani kubwa na Mwenyekiti na Rais wetu Dk John Magufuli," amesema Mwinyi Simba.

Amesema kwa kazi nzuri ambayo inafanywa na Rais Dk.John Magufuli na Watanzania kwa ujumla wanafunga mkono na kuahidi kumchagua kwenye uchaguzi mkuu mwakani na hivyo wanaoutaka urais kwa sasa hawana nafasi.

Amesema kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli imekuwa chachu kubwa ya maendeleo na kwa sasa sote tunashuhudia utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na hivyo lazima Rais apewe muhula wa pili aweze kumalizia kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa ajili ya nchi yetu.

Hata hivyo amefafanua kwa utamaduni na taratibu za CCM Rais anapochaguliwa huuchwa kwa vipindi vya mihula miwili kwa kila muhula kuwa na miaka mitano na ndio maana kuanzia Rais wa awamu ya pili na kuendelea wote wamehudumu kwa miaka 10 ,hivyo Rais Magufuli naye lazima aachwe aendelee kututumikia Watanzania.

Akizungumzia kauli iliyotolewa na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe kuhusu kauli yake ya kusema wanajiandaa kuchukua Nchi, Mwinyi Simba alimtaka kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini kuhakikisha kwanza wanaongeza idadi ya wabunge wa upinzani kabla hawajafikiria kushinda Urais.

Amesema inashangaza kuona Zitto anapiga hesabu zza Urais ilihali wabunge wa upinzani hawafiki nusu ya wale wa Chama cha Mapinduzi.

" Zitto ni mwanasiasa ambaye hana heshima, katika mkutano wake na wandishi wa habari wa Juni 11 mwaka huu alikaririwa akisema kuwa yeye hawezi kusikiliza matamko ya kisiasa bali atasikiliza yale yanayotolewa na Taasisi.

" Lakini anasahau yeye mwenyewe ni mwanasiasa na ametoa matamko ya kisiasa. Zitto anapaswa kufahamu kuwa Watanzania wa Sasa wanafahamu kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Dk John Magufuli," amesema Mwinyi Simba.

Akizungumzia ongezeko la wigo wa walipa Kodi, Mwinyi alimpongeza Rais Magufuli kwa kuimarisha urafiki uliopo kati ya wafanyabiashara na Serikali.

Ametoa rai kwa Serikali kuangalia namna ya kuanzisha Ward Tax Officer (Afisa Kodi Kara) ambao kwa kuanza wanaweza kuwafanyia majaribio katika majiji ambayo kibiashara ukusanyaji wake wa kodi upo juu.

" Afisa Kodi Kata wanaweza kukusanya taarifa kwa usahihi juu ya biashara zilizopo katika kata husika, mikataba inayoingiwa na pia wataweza kutoa elimu juu ya ulipaji kodi na kutengeneza urafiki kati ya mlipaji kodi na watoza kodi," amesema Mwinyi Simba.

Aidha amempongeza Rais Magufuli kwa kuwapa kipaumbele wabunifu wawili wa umeme ambao wamekua wakitatua changamoto ya umeme katika sehemu ambazo wametoka.

WAZIRI MPINA ATEMBELEA MAKAO MAKUU KAMPUNI YA RANCHI ZA TAIFA (NARCO), AZUNGUNGUMZA NA WATUMISHI

$
0
0
Waziri wa Mifugo naUvuvi Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na Wafanyakazi wa Kampuniya Ranchi zaTaifa (NARCO) alipotembelea Makao Makuu ya kampuni hiyo Nzuguni, Dodoma, leo Kushoto ni MenejaMkuuwa NARCO, Prof. PhilemoniWambura. Kulia ni Mratibu wa Dawati la SektaBinafsi, Steven Michael.
Mratibu wa Dawati la Sekta Binafsi Wizara ya Mifugo naUvuvi, Bw. Steven Michael akieleza nafasi ya Dawati la Sekta Binafsi katika kuboresha uwekezaji kwenye Kampuni ya Ranchi zaTaifa, NARCO (katikati) niWaziri waMifugonaUvuviMhe. Luhaga Mpina na Kaimu Meneja Mkuu wa NARCO, Profesa Philemon Wambura
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali watu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Teddy Njau akifafanua hoja mbalimbali kuhusuWatumishi wa Kampuni ya Ranchi zaTaifa katika ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alipotembea Makao Makuu ya NARCO, Nzugunijijini Dodoma.

Watumishi wa Kampuni ya Ranchi zaTaifa (NARCO) wakifuatilia kwa makini maelekezo yaWaziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani) alipotembelea makao makuuya NARCO Nzuguni, Dodoma.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiwa katika picha ya pamoja na Ma meneja wa Ranchi zote zaTaifa baada ya kumaliz akikao cha siku mbili kilichofanyika makao makuu ya NarcoNzuguni, Dodoma wengine ni Kaimu Meneja Mkuu wa NARCO naWakurugenzi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Tume ya Madini yasisitiza uuzaji wa Madini kwenye Masoko

$
0
0
Afisa Madini mkazi mkoa wa Njombe na Iringa Wilfred Machumu
katikati akiambatana na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris
Kikula wa kwanza kulia wakiingia kukagua soko la madini ya
Dhahabu na Vito mkoa wa Iringa. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa kwanza kushoto,
Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma wa nne kulia
wakiwa kwenye kikao na mwenyeji wao mkuu wa mkoa Ruvuma
Christina Mndeme kuhusu ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia
sekta ya madini. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula mwenye kofia akiwa
kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa kampuni ya Thomas G.
Masuka & Partners kwenye mgodi wa Nyakavangala Isimani mkoani
Iringa. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula na Kamishna wa
Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakiwa chini kwenye mgodi wa
kampuni ya TANCOAL inayo zalisha makaa ya mawe
walipotembelea eneo la uzalishaji mgodini hapo. 




Na Issa Mtuwa “WM” Iringa

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amekemea na kutoa onyo
kwa Wachimbaji na wanunuzi wa madini nchini kuacha tabia ya kufanya
biashara ya madini nje ya masoko yaliyoteyari na yanayoendelea
kuanzishwa mikoa yote hapa nchini. 

Prof. Kikula amesema hayo Juni 15, 2019 muda mfupi mara baada ya
kukagua soko la madini mkoani Iringa ambako hakuridhishwa na takwimu
za uuzaji wa madini ya dhahabu katika soko hilo kuwa spidi ni ndogo
akitolea mfano wa takwimu zilizotolewa na Mkaguzi wa Madini kituo cha
Iringa Severine Haule kuanzia tarehe 30 Mei, 2019 hadi tarehe 14 Juni,
2019 ni gram 92 tuu za dhahabu zimezalishwa na kupita sokoni hapo. 

Amesema serikali haina mzaha kuhusu suala hilo na yeyote atakae kutwa
anafanya biashara ya madini nje ya masoko rasmi atakumbana na mkono
wa sheria ikiwemo kutaifishwa madini na kila aina ya raslimali iliyotumika
kuwezesha ufanyikaji wa biashara hiyo, hivyo ametoa wito kwa wadau
wote kujiepusha na utoroshaji wa madini sambamba na kufanya biashara
nje ya Masoko. 

Ameongeza kuwa, jicho la serikali linaona mbali hivyo asijidanganye mtu.
Amesema kuwa ziko taarifa za ujanja ujanja kufanya biashara ya kuuziana
madini usiku wilayani Tunduru, wengine kutorosha madini kuelekea Malawi
kwa wilaya ya Songea na Mbinga, na Iringa wachimbaji wadogo, wanunuzi
wa kati (Brokers) na wanunuzi wakubwa (Dealers) kuuziana madini kwa siri
kutofikisha madini kwenye soko. Amesema taarifa zote hizo serikali inazo
hivyo amewaomba wadau wote wanaohusika na michezo hiyo waache
mara moja na kama wataendelea wajue siku zao si nyingi hivyo
wasijitafutie matatizo wakaacha familia zao bila sababu. 

Wakati huo huo Mwenyekiti ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Tume
hiyo mikoa yote nchini kuzingatia uadilifu na kwamba kamwe wasikubali
kushawishika kwa rushwa. 

Amesema laiti kama yeye angekuwa mwepesi wa kupokea rushwa pengine
asingekuwa anaendelea kumsaidia Rais Magufuli kuwatumikia Wananchi
kwani yapo majaribu mengi na majaribio ya watu kumpelekea vifurushi na
mabegi ya fedha lakini hajawahi kuingia katika mitego hiyo na hajawahi pokea rushwa hata siku moja katika miaka 46 ya maisha yake yote ya
utumishi wa umma. 

Amewambia watumishi hao kuwa wakae wakijua wale watakao waletea
fedha hiyo siri haitabaki kwa mtu mmoja lazima itavuja na huo ndio
mwanzo wa kuharibu jina lake hivyo wasikubali rusha ni hatari. 

Mwenyekiti Prof. Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini Prof.
Abdulkarim Mruma wamehitimisha ziara yao katika mikoa ya Lindi, Mtwara,Ruvuma, Njombe na Iringa ambako walikuwa wanakagua shuguli zamadini, kuhimiza ulipaji wa maduhuli ya serikali, utatuzi wa migogoro,
kusikiliza kero na kutatua, kuongea na wafanyakazi wa tume ya madini,
wachimbaji, wafanyabiashara wa madini na kuognea na viongozi wa
serikali ngazi ya mikoa na wilaya. 

Yaliyojiri kwa ujumla katika ziara hiyo ni pamoja na; kilio cha wachimbaji
wadogo katika mikoa mbalimbali kutozwa kodi zaidi na Halmashauri za
wilaya na vijiji kinyume cha sheria ya madini, ufinyu wa bajeti, uhaba wa
watumishi na vitendea kazi kwa ofisi za tume ya madini mikoani,
ucheleweshaji wa utolewaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji
wadogo, ulipaji wa maduhuli ya serikali, uuzaji wa madini kwenye masoko
rasmi, uadilifu na kuepuka rushwa.

WANUNUZI WATAKIWA KUNUNUA PAMBA KWA BEI ELEKEZI

$
0
0

Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi(kushoto) akitoa maelezo ya aina za mbegu za pamba zinazozalishwa katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(wa pili kushoto) na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019. 
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kushoto) akiangali namna taarifa za wakulima zinavyoandikwa mara baada ya pamba yao kupimwa wakati alipotembelea moja ya Chama cha Msingi Cha Ushirika (AMCOS)kilichopo kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 15, 2019 
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akiangalia baadhi ya marobota ya pamba iliyochambuliwa katika kiwanda cha NGS kilichopo Majahida wilayani Bariadi, mara baada ya kutembela kiwanda hicho wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 15, 2019. 
Mkurugenzi wa Kiwanda cha NGS kilichopo Majahida Bariadi ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kulia), na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(wa pili kushoto) akiangalia baadhi ya mashine za kuchambua pamba zinavyofanya kazi, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu Juni 15, 2019.(wa nne kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka. 
Baadhi ya viongozi na wataalam wa mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(hayupo pichani) wakati alipozungumza nao katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara yake mkoani humo, Juni 15, 2019. 
Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akiwasilisha kero za wananchi zinazohusu kilimo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kulia) katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Katika Kijiji cha Inalo Kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019 
Mjumbe wa NEC kupitia Mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akichangia hoja katika kikao cha ndani kati ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na viongozi pamoja na watendaji mbalimbali, wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019. 

****************************** 



Na Stella Kalinga, Simiyu 

Waziri wa Kilimo amewaomba wanunuzi wa pamba waliopewa leseni na Bodi ya pamba wanunue pamba kwa wakulima kwa bei elekezi ya shilingi 1200 kama ilivyopangwa na kukubaliwa katika kikao cha wadau wa pamba mwezi Mei, 2019 jijini Mwanza. 

Waziri Hasunga ameyasema hayo Juni 15, 2019 wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu wakati alipotembelea viwanda vya kuchambua pamba, vituo vya kununulia pamba na kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara. 

“Naomba nitumie nafasi kuwaomba wanunuzi wa pamba wenye nia njema na nchi hii waliopewa leseni na Bodi ya Pamba waje kununua pamba kwa wakulima, bei elekezi ya mwaka huu ni shilingi 1200”-alisema Waziri Hasunga. 

Aidha, Waziri Hasunga amevitaka vyama vya ushirika vya msingi kuzikagua mizani kwani itakapobainika kufanyika uchakachuaji wakati wa kupima hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, huku akiwahakikishia wakulima kuwa changamoto zote zilizobainishwa na wakulima katika msimu wa 2018/2019 zitafanyiwa kazi. 

Mkulima wa Pamba kutoka Luguru wilayani Itilima, Bw. Ngusa Lutenganeja ameishauri Serikali kupanga bei ya pamba wakati wa maandalizi ya msimu ili wakulima walime wakiwa wanafahamu bei na maandalizi ya fedha yafanyike mapema wakulima wasikopwe pamba yao. 

Kwa upande wake Mnunuzi wa pamba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amesema imani yake ni kwamba Serikali itasimamia na kuhakikisha pamba ya wakulima inanunuliwa kwa bei elekezi ya shilingi 1200/= na wananchi wanapata fedha zao kwa wakati. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu una viwanda vingi vya kuchambua pamba, ambapo ameshauri kuwa ili kuliongezea thamani zao la pamba Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wengine kuona uwezekano wa kujenga kiwanda cha kutengeneza nguo kwa kuwa uhakika wa soko la bidhaa zitakazotengenezwa upo. 

Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini (TCA), Bw. Boaz Ogola ametoa wito kwa Wanunuzi wa pamba kuunga mkono juhudi za Serikali katika viwanda kwa kuwekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya pamba ili tusitegemee soko nje ambalo linayumba.

WAZIRI MKUU AWASHAURI WATANZANIA KUJIWEKEA AKIBA KUPITIA HISA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ni wakati muafaka kwa Watanzania kuanza kujiwekea akiba kwa kununua hisa kupitia taasisi za kifedha nchini ikiwemo benki ya CRDB.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Juni 16, 2019) wakati wa bonanza kati ya Wabunge na watumishi wa benki ya CRDB lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema suala la wananchi kujiwekea akiba ni muhimu kwa ajili ya maendeleo yao. "Nashauri wananchi tutumie taasisi za fedha kujiwekea akiba pamoja na kukopa mikopo kwa ajili ya maendeleo yetu."

Akizungumzia kuhusu bonanza hilo lililoandaliwa na benki ya CRDB, Waziri Mkuu amesema michezo ni sehemu nzuri kujenga afya, furaha na kujenga mshikamano wa karibu baina ya benki hiyo na wananchi ambao ni wateja.

Michezo iliyochezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu ambapo timu ya CRDB ilishinda baada ya kuifunga timu ya Bunge penati tatu kwa moja na kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete timu ya Bunge iliibuka na ushindi baada ya kuibugiza CRDB magoli 35 kwa mawili.

Katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Wabunge Wanawake na Wanaume waliibuka na ushindi baada ya kuzishinda timu za CRDB. Upande wa mchezo wa basketball timu ya Bunge ilishinda vikapu 53 kwa 51.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
JUMAPILI, JUNI 16, 2019.
Waziri Mkuu Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa Timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kikombe cha ushindi wa mechi ya soka ya kirafiki kati ya timu hiyo na timu ya Bunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1. 
Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka ya benki ya CRDB wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi baada ya kuitandika timu ya Bunge 3-1 katika mechi ya kirafiki ilichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mchezaji nyota wa timu ya mpira wa pete ya Bunge, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki kati ya Bunge na CRDB iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 16, 2019. Bunge ilishinda 35-2. 

Watoto Tabora Washerehekea Siku Ya Mtoto Wa Afrika, huku Wazazi na Walezi Wakituhumiwa Kutumia Vibaya Sheria Ya Elimu

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Baadhi ya wazazi na walezi wa Mkoani Tabora  wanatuhumiwa kutumia vibaya sheria ya Elimu no, 25 Ya siku 90 zinazoweza kumfuta mtoto shule huku wengine wakitumia nafasi hiyo kuwaozesha watoto wakiwa na umri mdogo na wengine kutumikishwa katika shughuli za kiuchumi 

Ameyasema Hayo mkuu wa Wilaya John Mwaipopo katika kilele cha siku ya mtoto wa Afrika ambapo hufanyika kila ifikapa Tarehe16/6 kila mwaka 

Katika kuhakikisha mtoto anapata haki zake za msingi Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision linalopambana na kutetea haki za mtoto ikiwa ni mimba na ndoa za utotoni, John Masenza Meneja wa Shirika la World Vision amesema kila mzazi au Mlezi analo jukumu la kulea Watoto na kuwatunza katika maeneo wanayoishi na Kushirikiana kwa pamoja na shirika hilo na kutoa taarifa za unyanyasaji wanaofanyiwa Watoto 

Akisoma risala kwa niaba ya Watoto wengine katika kilele hicho cha mtoto wa Afrika James Jackob amesema anapata faraja kubwa kuona Serikali ya Tanzania na Serikali za nchi za nje zimedhamilia kuimarisha harakati za kumkomboa na kumlinda  mtoto.
 Pichani ni Watoto waliowakilisha wanafunzi wote kutoka katika wilaya ya Igunga wakisoma Risala mbele ya mkuu wa Wilaya.
Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali Wilaya Igunga wakiwa kwenye Maandamano ya kupinga Manyanyaso siku ya mtoto wa Afrika.

WAZEE ZANZIBAR WAADHIMISHA SIKU YA KUPINGA UKATILI JUU YAO

$
0
0
Na Salum Vuai
JAMII nchini imetakiwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa wazee kwa kutumia upungufu wao wa nguvu kuwatendea vitendo visivyokuwa vya kiungwana ikiwemo kuwasingizia uchawi.
Akizungumza katika kongamano la kupinga unyanyasaji dhidi ya wazee lililofanyika jana kwenye ukumbi wa ZSSF Kariakoo mjini Zanzibar, Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Shadya Mohammed Suleiman, amesema wazee wanastahili matunzo na heshima na sio kudharauliwa.
Kongamano hilo lililokuwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya kujenga uelewa na kupinga ukatili na unyanyasaji dhidi ya wazee duniani, lilihudhuriwa na wanachama kutoka jumuiya ya wazee pamoja na taasisi nyengine zinafanya kazi ya kulitetea kundi hilo muhimu kwa ustawi wa taifa.
Shadya alisema si jambo jemba kwa vijana kuwatenga wazee na kukataa kuwapa msaada wanaouhitaji, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanakuwa na afya nzuri na kuishi kwa faraja baada ya kutumia nguvu zao kuwalea vijana hao na kujenga taifa kwa jumla.
“Suala la kuwatunza wazee halina mbadala kwetu, kwani hata viongozi waasisi wa taifa letu marehemu mzee Abeid Karume na hayati Mwalimu Julius Nyerere, waliuona umuhimu wa wazee na kuwajengea mazingira mazuri ya kuishi  wanapofikia umri mkubwa na kupungua nguvu za mwili,” alisema.
Kwa hivyo alisema, wakati serikali zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar zinafanya jitihada ya kuwaenzi wazee, sio vizuri baadhi ya watu wawanyanyase na kuwatendea vitendo visivyostahili.
Alieleza kuwa, miongoni mwa mambo yanayofanywa na  serikali ni kuunda na kuyaimarisha mabaraza ya wazee ili kuwawezesha kupata haki zao za msingi ikiwemo matibabu, usafiri, na mafao ya uzeeni kwa wakati.
Alisema hakuna hata nchi moja duniani iliyopata maendeleo bila mchango wa wazee, na kuongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya kila jitihada kuhakikisha wazee 53,311 wenye umri kuanzia miaka 60 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, wanaishi kwa furaha katika uzee wao.
Alisema hatua ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kuwapatia wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea pensheni ya shilingi 70,000 ni kielelezo kwamba serikali inajali na kuthamini mchango wa wazee.
Hata hivyo, kwa upande mwengine, Naibu Waziri huyo aliwataka wazee kutokuona muhali pale wanapofanyiwa vitendo vibaya na watu wa  familia zao, majirani na wengine, akisema muhali umechangia kurejesha nyuma maendeleo  na kuiweka Zanzibar katika hali ngumu ya kupungua kwa ustawi.
Alihitimisha kwa kusema, ni matumaini yake kuwa serikali, taasisi na wadau mbalimbali wa  maendeleo, wataongeza ushirikiano ili kuhakikisha kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo; “Tuungane pamoja kwa kupaza sauti za wazee”, inasaidia kumaliza ukatili dhidi ya wazee na kulifanya jambo hilo kuwa historia.
Mapema, katika risala iliyosomwa na mjumbe wa kamati tendaji ya Jumuiya ya Wastaafu na Wazee Zanzibar (JUWAZA) Amour Haji Nassor, ilielezwa kuwa, kuna matukio mengi yanayotokea ambayo yanaonesha kuwa wazee katika sehemu mbalimbali nchini hawako salama.
Alisema wazee wa Zanzibar wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile lishe duni, huduma za matibabu zisizoridhisha, usafiri, makaazi, kupungukiwa na fedha na misaada ya hali na mali kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wa karibu.
Aliiomba serikali kuongeza jitihada katika kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo, akiitaka wizara iwawekee wazee vituo maalumu vya huduma za afya, kuwezesha uundwaji na uimarishwaji wa mabaraza ya wazee nchini na kujenga mtandao wa kuyaunganisha kupitia ngazi ya shehia.
Aisga aliwataka vijana wa sasa na watoto kutambua kwamba nao wanaelekea huko, kwani uzee na ‘kuzeeka haukwepeki’.
Katibu wa JUWAZA Dk. Yussuf Nuhu Pandu, kwa niaba ya Mweyekiti alitumia fursa hiyo kuwashajiisha wazee wasione vibaya kupaza sauti zao pale wanapotendewa vitendo vilivyo kinyume na ubinadamu.
“Unapojiona umesimama katika daladala usione shida kumuinua mtu hata kwa kumkemea, au pale unaporushiwa maneno ya ufedhuli na kijana, tumia nguvu zako zilizobaki kushika bakora umtandike ndipo atakapokuwekea heshima,“ alisema Dk. Nuhu.
Siku hiyo ilizinduliwa mwaka 2006 na Mtandao wa Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee Duniani kwa kushirikiana na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), ikilenga kuwajengea mazingira salama wazee ili waishi bila ya vitisho, ukatili, unyanyapaa, ubakaji na kukosa misaada kutoka kwa marafiki wa karibu.
 Baadhi ya wazee wakiwa wameshikilia bango lenye ujumbe Zuia unyanyasaji dhidi ya wazee kwenye maandamano ya siku ya kujenga uelewa wa uwepo wa udhalilishwaji wa wazee Duniani Juni 15 iliyofanyika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Zanzibar.
 Mkurugenzi, Kituo cha Msaada wa Kisheria na Kijamii kwa Wazee Zanzibar Maria Obel Malila akiwasilisha mada ya Udhalilishaji wa Wazee katika Sherehe ya Siku ya kujenga uwelewa wa uwepo wa udhalilishwaji wa wazee iliyoadhimishwa Juni 15 ukumbi wa ZSSF Kariakoo.
 Bi. Tatu Lisweko Mlekwa wa kijiji cha Bumbwisudi Popo akitoa ushuhuda wa namna walivyowahi kukumbwa na mambo ya unyanyasaji kabla ya kusaidiwa na Jumuiya ya Wastaafu na Wazee Zanzibar (JUWAZA).
Mzee Nassor Salum Hamad wa Dunga kiembeni akitoa ushuhuda wa namna walivyowahi kukumbwa na mambo ya unyanyasaji kabla ya kusaidiwa na Jumuiya ya Wastaafu na Wazee Zanzibar (JUWAZA).
 Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Shadya Mohammed Suleiman akiwahutubia wazee katika siku ya kujenga uelewa wa uwepo wa udhalilishwaji wa wazee Duniani iliyoadhimishwa Juni 15 katika ukumbi wa ZSSF Kariakoo Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wazee wakifuatialia hutuba ya Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto Shadya Mohammed (hayupo pichani) katika madhimisho ya siku ya kujenga uelewa wa uwepo wa udhalilishwaji wa wazee Duniani. Picha na Makame Mshenga.

Article 1


Sarah wa Harmonize alivyo pagawisha mashabiki Jamhuri Studium Dodoma...

NMB KULIPA GAWIO LA SH. BILIONI 33

$
0
0

Benki ya NMB Plc. (NMB), kulipa gawio la Shilingi 66 kwa kila Hisa.

Wanahisa wa Benki ya NMB wameidhinisha kiasi kilichopendekezwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM), uliofanyika mwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam.

Ikiwa ni matokeo ya utendaji bora na uimara wa nafasi ya mitaji, malipo ya jumla ya gawio la Shilingi Bilioni 33 (sawa na Shilingi 66 kwa kila hisa), yanafanana na sera ya benki ya kulipa moja ya tatu (asilimia 33.3) ya faida la jumla baada ya makato ya kodi (PAT) katika gawio. Hili ni ongezeko la asilimia 3 ukilinganisha na bei ya Shilingi 64 kwa kila hisa iliyolipwa mwaka uliopita. Nia ni kukuza kiwango cha gawio kwa kila hisa, kulingana na utendaji bora wa benki unavyoongezeka.

Benki iliripoti faida ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 142 kabla ya makato ya kodi (PBT), kwa mwaaka wa fedha ulioishia Desemba 31 2018; ambayo ni ongezeko la asilimia 3 kutoka faida ya Shilingi Bilioni 138 iliyopatikana mwaka uliotangulia. Licha ya mafanikio yaliyopatikana, Bodi na Uongozi wa Benki ya NMB umeridhishwa na aina ya mafanikio na mapinduzi chanya katika kipindi cha mwaka.

Mapinduzi hayo ni pamoja na uzinduzi wa NMB KLiK, mikopo ya mshahara - ambayo ni bidhaa ya kwanza ya benki kutoa mkopo kwa njia ya simu. Kuanzishwa kwa Mawakala zaidi ya 6800, wanaoshughulika – pamoja na mambo mengine, ukusanyaji na ulipaji wa kodi, ushuru na mapato ya Serikali za Mitaa katika Halmashauri 180, mapinduzi yanayochangia mzunguko wa pesa kwa mifumo ya kidijitali na kukuza amana. Pia tumeimarisha huduma za kibenki kupitia mtandao ilikuhudumia vizuri zaidi akaunti za makampuni na kuwapa suluhisho zote kamilifu na kufanya miamala ambayo imesababisha ongezeko la wateja kutoka milioni 2.2 hadi milioni 3.1 mwishoni wa mwaka 2018 .

Uimara wa NMB kama taasisi za fedha imepelekea Moody kuipa alama ya B1 ambayo vimethibitisha kuaminiwa kwa Benki ya NMB na wawekezaji wa kimataaifa. Benki imeimarishwa vema na uwiano wa mtaji kwa asilimia 16.5.Hiyo inamaanisha kwamba benki yetu iko salama kabisa kibiashara Mwenyekiti wa Benki, Prof. Joseph Semboja, anabainisha kuwa Bodi inataka kuweka sawa ongezeko la wanahisa, sambamba na kuimarisha biashara ya fedha ndani ya benki katika mpango mkakati wa kukua zaidi kiuchumi.

“Kwa miaka kadhaa sasa NMB imeendelea kuwa imara yenye afya kifedha, lengo ni kuendelea kuimarika zaidi na kubaki hivyo. Ili kufikia mafanikio haya, tunapaswa kuhakikisha tunafanya maamuzi sahihi hasa katika udhibiti wa mabadiliko kwenye mahitaji makuu ya kimtaji,” anasema Mwenyekiti.

“NMB imejipambanua katika kuendelea kusaidia harakati za maendeleo ya uchumi Tanzania na kuvuka kiwango cha sasa cha dira ya uchumi kama kichocheo cha ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi nchini. Tutaendelea kuwa vinara wa hudumaa bora kwa wateja wetu, huku tukiendelea kutimiza wajibu wetu kwa jamii,” alisema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Albert Jonkergouw.

NMB imejitolea katika kusaidia ukuaji kiuchumi wa wajasiriamali wadogo na wakati (SME's), hususani wanawake kwa kuwapa mafunzo na elimu ya uwezeshaji katika kuimarisha biashara zao kwa kutambulisha jukwaa jipya la ‘Woman in Banking’ kote nchini. Katika kilimo, NMB tumeboresha jopo la wataalamu wanaojikita zaidi katika Sekta ya KilimoBiashara, ili kuimarisha mnyororo wa thamani unaopewa usaidizi mkubwa na Taasisi ya NMB Foundation, ambayo.

"Sisi ni Benki Bora Tanzania. Ubora wetu ni katika nyanja zote, za utawala, teknolojia ya habari na mfumo mzima unaoifanya NMB kuwa benki salama nchini, huku tukihakikisha amana na akiba zako ziko salama chini yetu," aliongeza. 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  NMB  Albert Jonkergouw akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa  wanahisa wa Benki ya NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana.

 

WAZIRI KIGWANGALLA AWAFUATA MADAKTARI, WAUGUZI NA WAFANYAKAZI WA ARUSHA LUTHERAN MEDICAL CENTRE KUWASHUKURU

BAADHI YA WANANCHI WANAKOSA HAKI MAHAKAMANI KWA KUKOSA KUTUMIKA KWA KISWAHILI KWENYE HUKUMU- INJINIA MANYANYA

$
0
0

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya akitoa hotuba yake wakati wa Mahafali ya chama cha wanafunzi wa Kiswahili Afrika mashariki tawi la Makumira
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya akisaini kitabu cha wageni walipowasili kwenye Mahafali ya chama cha wanafunzi wa Kiswahili Afrika mashariki tawi la Makumira wilaya Arumeru picha zote na Ahmed Mahmoud Arumeru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akitoa nasaha zake kwenye Mahafali ya chama cha wanafunzi wa Kiswahili Afrika mashariki tawi la Makumira picha na Ahmed Mahmoud Arumeru


Na Ahmed Mahmoud Arumeru

Mahakama zimetakiwa kuangalia namna ya kukitumia Kiswahili wakati mwananchi anapokata rufaa kwenye mahakama za rufaa badala ya utaratibu unaotumika sasa.

Ambapo pia Watanzania wametakiwa kutumia fursa ya kukitangaza na kueneza Lugha adhimu kwa kukienzi Kiswahili ili kitupatie maarifa zaidi na kuzitumia lugha nyingine kukuza mawasiliano kote ulimwenguni.

Akiongea kwenye Mahafali ya 12 ya CHAWAKITUMA na Kongamano la Kiswahili kwenye Chuo cha Makumira Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Injinia Stella Manyanya alisema kuwa Kiswahili ni kidhibiti kasi katika Biashara kwani Biashara inatija na faida hivyo kujiamini ni sehemu ya Biashara kwa kuwa mawasiliano yapo kati yenu.

Amesema kuwa anahidi serikali ya awamu ya tano ni sikivu na itasikiliza kwa kushika lugha yetu kwani lugha hiyo ni bidhaa na fursa ya kiuchumi kwa kuinua mkono kukinadi Kiswahili.

Kuna changamoto kutokana na kutotumika kwa lugha ya Kiswahili kwenye Rufaa kwani eneo hilo zinaonyesha litawanyima wadawaa haki kwa kutumika lugha ya kuongeza “Lugha ya Kiswahili ni bidhaa Bora ndio maana Mh.rais kila mahali amekuwa akikinadi kwenye mataifa mbali mbali ili kuweza kutoa walimu na hivyo fursa ya Kiswahili kukua kwa kukitangaza hata kwenye bidhaa zetu”
 
Amewataka kuwa wahitimu hao kuchangamkia fursa za kufundisha Kiswahili kwani wanaweza kuitumia nafasi hiyo kueneza upendo kwenye maeneo yenye vurugu kwani lugha hiyo inamchango wa kuweza kupatanisha.
Amesema kuwa mabango ya usalama Barabarani yameboreshwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili namshukuru sana na kongole wadau wa Kiswahili kwani lugha hiyo hapa nchini ni lugha rasmi.

Kupitia viwanda tunaweza bidhaa zetu watu kununua kwa haki sehemu hii ni nafasi ya sehemu ya viwanda katika mchango wake katika kukiuza .
Akiongea kwenye Mahafali hayo yalioenda sambamba na Kongamano la Kiswahili kwenye chuo cha Makumira Makamu Mkuu wa Chuo cha Makumira Utawala Prof. Joseph Parsalaw Alisema kuwa Kiswahili ni tunu na fursa ya kuongeza mawasiliano na kuwataka watanzania kukienzi.

Naye Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro alisema kuwa aliwataka wahitimu kuangalia namna nzuri ya kukilea na kujifunza Kiswahili tujipange kwani wenzetu wanatumia nafasi na kujitangaza kiswahili kipo nchini mwao nanyi wanazuoni ndio wakuondoa ombwe hilo kwa dunia kujua asili ya Kiswahili.

“Haya yote vijana tusimame tuinuke kwani hatma ya taifa hili ipo mikononi mwetu kwa kuenda kufundisha kukitangaza na kuwa mabalozi wazuri wa kukitangaza Kiswahili chetu”


Alisema Tunamshukuru mh.rais ameendelea kujipambanua na kukitangaza Kiswahili fikra sahihi huja wakati sahihi na mkumbuke lugha hii ni ya tatu inayopendwa na kutamalaki barani Afrika kwa kufanya shughuli za mawasiliano.
Alisema kuwa Wakongo wanapoingia nchi za jumuiya ya Afrika mashariki ni fursa nzuri kuitumia kwa kutoka na kwenda kujionea fursa na kuacha kusikiliza ambayo hawajajionea kabla hawajafik

ZAINABU MAULID AZIAGIZA NGAZI ZA WADI NDANI YA MKOA WA MAGHARIBI UNGUJA KUFANYA VIKAO VYA KAWAIDA

$
0
0
KATIBU wa UWT Wadi ya Mwanakwere Ndugu Khadija Seif akisoma Taarifa ya Utendaji wa Majukumu mbali mbali ya Wadi hiyo mara baada ya kufunguliwa kwa Kikao hicho cha Baraza la UWT ngazi ya Wadi huko katika Ukumbi wa Mikutano wa Tawi la Mwanakwerekwe ‘A’. 
BAADHI ya Viongozi wa UWT Ngazi ya Mkoa na Jimbo wakiwa katika Kikao hicho cha Baraza la UWT Wadi ya Mwanakwerekwe. 
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Magharibi Unguja Ndugu Zainab Ali Maulid,akiwahutubia Wajumbe wa Baraza la UWT Wadi ya Mwanakwerekwe mara baada ya kufungua Kikao cha Baraza hilo kwa niaba ya Wadi 14 za UWT za Wilaya ya Dimani zilizofanya Vikao leo Tarehe 16/06/2019. 
MJUMBE wa Baraza la UWT Wadi ya Mwanakwerekwe ambaye pia ni Mwakilishi wa Viti Maalum Mhe.Mwanaidi Kassim Mussa akitoa maoni yake kuhusu Taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa na Wadi hiyo. 
WAJUMBE wa Baraza la UWT Wadi ya Mwanakwerekwe wakisikiliza nasaha zinazotolewa na Viongozi wao kupitia Kikao hicho. 



NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Tanzania Mkoa wa Magharibi Unguja Ndugu Zainab Ali Maulid, amezitaka Ngazi za Wadi ndani ya Mkoa huo kufanya Vikao vya Kawaida na Kikatiba kwa Mujibu wa Miongozo ya Katiba na Kanuni ya Umoja huo. 

Wito huo aliutoa wakati akiwahutubia Wajumbe wa Baraza la UWT Wadi ya Mwanakwerekwe katika Mkutano wa Baraza hilo, uliofunguliwa kwa niaba ya Mikutano yote iliyofanyika leo ya Mabaraza 14 yaliyopo katika Wilaya ya Dimani Unguja. 

Alisema ufanisi wa kiutendaji ndani ya Umoja huo inatokana na Utekelezaji wa maelekezo ya Vikao halali vinavyotoa maazimio na maelekezo ya utatuzi wa Changamoto mbali mbali zinazowakabili Wanachama,Viongozi na Watendaji wa UWT. 

Alisema Vikao ndio sehemu pekee ya kujitathimini na kupanga mikakati ya Utendaji wa shughuli mbali mbali za UWT hasa katika wakati wa sasa wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Dola wa Mwaka 2020. 

Alisema kila Mwanamke ndani ya Umoja huo anatakiwa kuwahamasisha Wanawake wengine hasa waliokuwa hawajajiunga na UWT na CCM kuweza kujiunga ili wanufaike na Siasa Bora zinazoendeshwa na Chama Cha Mapinduzi. 

Mwenyekiti huyo aliwakumbusha Akina Mama hao kwamba wanatakiwa kujipanga vizuri juu ya kuwahamasisha Wanawake kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura pindi wakati wa zoezi hilo utakapofika. 

Katika maelezo yake Mwenyekiti huyo Zainab, aliwasisitiza Wanawake hao kushiriki katika harakati za kukemea na kupambana na Vitendo vya Udhalilishaji wa Kijinsia kwani vinakwamisha malengo ya Vijana hasa wa Kike. 

Naye Mwenyekiti wa Wadi hiyo, Ndugu Amina Khalfan alisema watayafanyia kazi kwa vitendo maelekezo yote yaliyotolewa na Mwenyekiti huyo kwa lengo la kuimarisha shughuli mbali mbali za Umoja huo katika Wadi hiyo. 

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza hilo ambaye pia ni Mwakilishi wa Viti Maalum Mhe.Mwanaidi Kassim Mussa aliwashauri Viongozi wa Wadi hiyo kuendelea kuwa Wabunifu na kushirikiana na Viongozi mbali mbali wa ngazi za juu za Umoja huo ili wasaidie kutatua kwa haraka changamoto zinazowakabili.
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images