Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

WAKULIMA LEMKUNA WAIOMBA SEREKALI KUWAONGEZEA ENEO LA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

$
0
0

Shamba la zao la mpunga katika skimu ya umwagiliaji ya Lemkuna Iliyopo wilayani Manyara mkoani simanjiro, ambapo Mpunga huo upo tayari kwa ajili ya mavuno. 
Banio linaloruhusu maji kwenda katika mashamba yaliyopo katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Lemkuna Wilayani Simanjiro, ambapo imelezwa na wakulima ambao niyo watumiaji kuwa maji hayo yametoka katika mto ruvu na bwawa la maji la mto wa mungu. 
…………………. 

NA MWANDISHI MAALUM –SIMANJIRO 
Wakulima katika skimu ya Umwagiliaji ya Lemkuna iliyopo katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba serikali kuwaongeazea eneo linalotumika katika kilimo cha umwagiliaji kwa sasa lenye ukubwa wa Hekta mia tatu (300) mbali na zaidi ya hekta elfu kumi (10,000) zilizoendelezwa kwa kilimo cha Hicho. 

Akiongea na waandishi wa Habari kwa niaba ya wakulima katika katika skimu hiyo, Mwenyekiti wa chama cha wakuliwa Lemkuna Uwale Bw. Stanley Msuya amesema kuwa kutokana na kilimo hicho kuwa na mafaniko na faida kubwa katika jamii inayozunguka maeneo jirani, kumekuwa na mwamko mkubwa wa vijana wa kizazi kipya katika maeneo hayo kuwa na hari ya kujiajiri kupitia sekta ya kilimo, lakini maeneo mengi yamekuwa yakimilikiwa na watangulizi au wazazi wao jambo ambalo limepelekea vijana hao kukosa maeneo ya kufanya shunguli za kilimo. 

“kilimo hiki cha umwagiliaji kimekuwa na faida kubwa kwetu sisi wakulima hasa baada ya serikali kupitia tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutujengea miundo mbinu ya umwagialia, kipato cha mkulima mmoja kabla ya maboresho na kupatiwa mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, mkulima aliweza kupata gunia za Mpunga kwa mfano kuanzia kumi na tano (15) mpaka ishirini (20) kwa heka moja, lakini kwa sasa mkulima anaweza kupata hata gunia thelathini na tano (35) mpaka hamsini (50) unaweza kuona namna ambavyo kilimo hiki kina faida, Hivyo tunaiomba serikali kufanya upanuzi wa eneo hili kwani vijana wanahitaji sana kufanya shughuli za kilimo.” Alisisitiza Bwana Msuya. 

Akiongelea baadhi ya Changamoto wanazokabiliana nazo wakulima katika Skimu hiyo, Bw. Msuya alisema kuwa Chama hicho kimekuwa hakina kifaa za kuvunia zao la mpunga na ili kukabiliana na changamoto hiyo kipo kwenye mchakato wa kupata mkopo kupitia Bank ya kilimo na Bank ya NMB nchini ili kuweza kununua mashine hiyo na kuweza kuinua wakulima wadogowadogo kwa kuchangia katika upatikanaji wa pembejeo za kilimo na kuongeza mtaji. 

Skimu ya kilimo cha umwagiliaji Lemkuna ipo katika kanda ya umwagiliaji ya Dodoma, inayohusisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 16,2019

BITEKO:WATANZANIA FICHUENI WANAOKWEPA KODI NA KUTOROSHA MADINI

$
0
0
Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko akipokea zawadi ya picha kutoka kwa moja wa wafanyabiashara wa madini 
Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha lililozinduliwa rasmi jana.
Baadhi ya wafanyabiashara wa vito vya madini wakifatilia kwa makini 
waziri Biteko akiangalia baadhi ya vito vilivyopo katika soko hilo
baadhi ya wafanyabiashara wakiangalia vito vilivyopo katika soko hilo 
Mwenyekiti wa TAMIDA, Sammy Mollel akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alishukuru kwa kuanzishwa kwa soko la madini pia alipongeza serikali kwa bajeti ya mwaka 2019/20 kwani imeondoa kilio cha muda mrefu cha wachimbaji na wauzaji wa madini nchini.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea katika uzinduzi huo
Mbunge wa viti maalumu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge nishati na madini Catherine Magige akiongea katika uzinduzi huo 


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko,amewataka wafanyabishara wa madini wadogo pamoja na wakubwa kuwafichua wafanyabiashara wote wanaojaribu kutorosha madini pamoja na wale ambao wanaokwepa kulipa kodi ya serikali ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao

Hayo ameyasema leo wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha ,ambapo alisema kuwa Iwapo wafanya biashara watakuwa wawazi na watafichua watu wote ambao wanakwepa kodi na kutorosha madini hitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi yetu.

Alisema kuwa ili kuweza kuinua uchumi wan chi yetu ni lazima kila mwananchi kutimiza wajibu wake kwa kulipa kodi kwa uaminifu ili kusaidia kukuza uchumi wan chi yetu aidha alisisitiza kuwa heshima kubwa ya mtanzania ni kulipa kodi na sio kufanya mambo ya kijanja janja na alibainisha kuwa ni lazima watanzania tuhame katika taifa la watu wajanja wajanja tuwe wananchi wa taifa la watu waaminifu .

“mlilalamika kuhusiana na kodi tumefanyia kazi na yale ambayo bado tutafanyia kazi lakini kwa kuwa tumefanyia kazi na nyie rudisheni fadhila kwa kulipa kodi ,na pia napenda kuwasihi wenyeviti wa mabroka kuwakusanya mabroka ambao hawajalipa kodi kulipa kodi wakate leseni ili nao wawe katika orodha ya walipa kodi”alisema Biteko

Alibainisha kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususani wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.

Alibainisha kuwa kuwekwa kwa soko hili hapa Arusha kunasaida kuwepo kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 na pia soko hili litasaidia kuondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.“napenda kuwasihi wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali” alisema Biteko .

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa manufaa ya soko jipya la madini litasaidia kuziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.

Aliongeza kuwa soko hili litasaidia kuwezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoani Arusha ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu Bunge nishati na madini Catherine Magige alisema kuwa Soko hili litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana.Alitumia mda huo kuwasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiongea katika uzinduzi wa kituo cha uuzaji madini mkoa hapa 

BEN "KUN" AGUERO(10): A STRIKER WITH UNIQUE FOOTBALL GENES!!!

$
0
0

1. Usuli:

HAJI MANARA ni  mwanamichezo aliyetokea kwenye damu ya gozi la n'gombe. Baba yake, SUNDAY MANARA "COMPUTER" ndiye Mchezaji Bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania huku baba yake mkubwa, KITWANA MANARA "POPAT" ndiye mchezaji anaeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ya ligi, kupiga Hat-trick nyingi kuliko wachezaji wote Tanzania na aliyechezea Taifa Stars kwa muda mrefu kuliko wachezaji wote(miaka 16 toka 1960-1976) na baba yake mdogo, KASSIM MANARA, alikuwa mshambuliaji mahiri wa Taifa Stars hadi ligi kuu ya Austria.

Hata hivyo, kwa dogo wa miaka 10 aitwaye BENJAMIN "KUN" AGUERO, HAJI MANARA anasubiri sana!,  BEN aliwaacha hoi waandishi wa habari waliofurika Etihad Stadium tarehe 12 Mei 2019 siku MAN CITY ilipotwaa ubingwa wa England alipotoboa ukweli huu:

"Sergio Aguero is MY FATHER, Lionel Messi is MY GODFATHER and Diego Maradona is MY GRANDFATHER".

2. AGUERO, MARADONA & MESSI:

BEN alizaliwa tarehe 12 Februari 2009. Baba yake ni SERGIO "KUN" AGUERO, Mnyama wa MAN CITY, Mabingwa wa kabumbu England.

Mwaka 2008, SERGIO alimuoa GIANNINA, mtoto wa  DIEGO ARMANDO MARADONA, Mnyama ambaye mwaka 2000 alitunukiwa "The FIFA Player of the Century Award" pamoja na Mnyama mwingine, EDSON ARANTES D'ASCIMENTO "PELE".

SERGIO na GIANNINA wakamzaa BEN mwaka 2009. 

BEN alibatizwa mwaka 2010 ambapo baba yake wa ubatizo "Godfather" akawa ni Mnyama LIONEL ANDRES MESSI CUCCITINI wa BARCELONA.

3. BEN Akimbiza watoto wenzake:

BEN alizaliwa na kipaji cha ajabu cha kabumbu na baba yake alianza kucheza nae ndani ya nyumba akiwa na miaka miwili tu huku akionesha nguvu kubwa ya kupiga mashuti tofauti na watoto wenzake wa rika lake. Akiwa na miaka mitano akaanza kucheza na baba yake na marafiki wa baba yake kwenye garden nyuma ya nyumba ambapo aliwashangaza kwa "control" yake ya hali ya juu.

BEN alisajiliwa Man City Academy na mara moja akawa akiwakimbiza vilivyo watoto wake wa umri huo na kuwa maarufu kuliko watoto wote!.

4. SERGIO Ammwagwa na GIANNINA:

Mwaka 2012, SERGIO "KUN" AGUERO ambaye anaaminika ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuwa na mademu wengi kuliko wachezaji wote kwenye ligi ya Uingereza, alimwagwa na mkewe, GIANNINA, kutokana na kuwa na pepo la ngono!.

GIANNINA alikuwa akifumania vimeseji kwenye simu ya SERGIO na mara kwa mara akawa anashtaki kwa DAVID SILVA ambaye alikuwa akiwasuruhisha na SERGIO akiishia kuomba msamaha kwa kudai "Shetani alinipitia". Hata hivyo, mwaka 2012, GIANNINA aliporudi ghafla toka Argentina na kumfuma SERGIO akiwa na milupo miwili kwenye garden yao, MERCY TUNCAFUTZ na YACINTA FALCUM, akalianzisha vagi la kufa mtu na kusepa jumla. MARADONA alimlaani sana SERGIO kwa jinsi alivyomuumiza mwanae.

Baada ya kumwagwa, SERGIO aliendeleza weledi wake wa kutupia magoli kambani akiwa na Man City na Timu ya Taifa ya Argentina na nje ya uwanja akaendelea kufunga magoli kama kawa na akawa akibadilisha milupo kutoka mataifa mbalimbali. 

Kutokana na hulka hiyo ya kupenda ngono, SERGIO alipoulizwa na Jack Milmall, mwandishi wa "The Mirror", ni kwanini anapenda sana vidosho, alijibu kuwa akifanya ngono siku moja kabla ya mechi, kesho yake anakuwa kwenye kuwango bora kabisa na huwa na utulivu wa aina yake alikaribiapo goli!.

Hata hivyo kama inavyowatokeaga watu wengi wapenda Totoz kwamba fedheha huwa haichezi nao mbali, SERGIO alipata fedheha kubwa tarehe 28 Septemba 2017, siku mbili kabla ya mechi ngumu ya ligi dhidi ya CHELSEA.

SERGIO alikuwa amekwea pipa na kwenda jiji la maraha la Amsterdam ambako alikwenda Pub maarufu ya mabilionea jijini humo, Cancula Pub, ambako alijirusha na vimwana hadi usiku wa manani.

Ilipofika saa 8.30, SERGIO aliondoka na vishtobe watano na kwa gari jeusi kwenda nao hotelini kwake. Hata hivyo, kutokana na kuwa alikuwa "bwaksi" kwani alikuwa "amepiga vyombo" kisawasawa, SERGIO aliuvaa mstimu na kuvunjika mbavu mbili huku kidosho GRACE JUDAKGIK akichanika sikio na mwingine JANE PINKPALL akivunjika bega!.

Kuna kila aina ya dalili kuwa BEN atarithi si tu kipaji cha soka toka kwa baba yake, SERGIO AGUERO, bali pia mambo ya kupenda vimwana. Hii ni kwasababu mara kwa mara BEN huonekana akifurahia kukumbatiwa na vitoto visichana ambavyo wazazi wao huenda navyo kushuhudia mechi kwenye Academy ya Man City ambako BEN daima hutakata vilivyo!.

Aidha, BEN anatarajiwa kurithi si tu kipaji cha mpira bali pia cha kupenda mademu toka kwa babu yake, DIEGO MARADONA. MARADONA amezaa na michepuko nane watoto nane nchini Italy, Agentina na Cuba akiwemo GIANNINA! Tarehe 8 Machi 2019, MARADONA aliumbuka na alilazimika kuwakubali watoto watatu baada ya DNA kumuumbua kwa watoto aliozaa na michepuko mitatu tofauti ya Cuba ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matumizi ya ngada toka 2000 hadi 2005!.

5. BEN Amkubali KYLIAN MBAPPE:

Ungetazamia mtoto wa magwiji hao wa kabumbu angemtaja mmoja wapo kati ya MARADONA, AGUERO au MESSI kuwa ndiye 'Idol" wake lakini BEN amewashangaza wengi kwa kusema ye hawamaindi wote hao ila anamuhusudu sana Mnyama KYLIAN MBAPPE!!.

KILA LA KHERI DOGO BEN "KUN" AGUERO!

UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTECOSTE SHINYANGA WAFANYA MAZOEZI, WACHANGIA DAMU SALAMA

$
0
0
Umoja wa makanisa ya Kipentecoste Mkoani Shinyanga wamefanya mazoezi na kuchangia damu salama, ili kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha afya za wananchi, pamoja na kuokoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi kwa sababu ya kumwaga damu nyingi.

Mazoezi hayo yamefanyika leo Juni 15, 2019 kwenye uwanja wa wamichezo wa Sabasaba, na kuongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga, mhe. Jasinta Mboneko, ambayo yalianza kwa matembezi na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga na kuhitimishwa kwa kuchangia damu salama. Akizungumza kwenye mazoezi hayo, mwenyekiti wa umoja wa makanisa hayo ya Kipentecoste mkoa wa Shinyanga,Askofu Elias Madoshi, amesema wao kama viongozi wa kidini wameona ni vyema kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kuchangia damu salama. 

Amesema juhudi za serikali ya awamu ya tano zinapaswa kuungwa mkono, ambapo wananchi wakiwa na afya mgogoro kamwe hawataweza kufaya shughuli za uzalishaji mali, na hatimaye nchi kushindwa kukua kimaendeleo na kufikia kwenye uchumi wa kati. “Sisi kama Umoja wa makanisa ya Kipentecoste mkoani Shinyanga CPCT kwa kushirikiana na umoja wa makanisa ya Kiinjili CCT, Tumeamua kuungana na Serikali kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ili wawe na afya imara, pamoja na kuchagia damu salama ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vikonavyo na uzazi kwa kumwaga damu nyingi wakati wa kujifungua”amesema Madoshi. 

“Hivyo tunatoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga wajikite kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao pamoja na kujitoa kuchangia damu salama, ambayo itaokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu ikiwamo na kumaliza vifo vya uzazi vitokanavyo na umwagaji damu nyingi,”ameongeza. Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amepongeza Umoja huo wa makanisa ya Kipentecoste kwa kutoa hamasa ya wananchi kushiriki kufanya mazoezi pamoja na uchagiaji wa damu salama. 

Amesema mazoezi hayo yalizinduliwa na makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo yatafanyika kila Jumamosi ya pili ya mwisho wa mwezi, na kuwasihi watumishi wa serikali kuwa mfano wa kuigwa kushiriki kwenye mazoezi hayo na siyo kuwa wategeaji, ambapo ataanza kuwa anapitisha daftari la ukaguzi wa majina ya watumishi. 

Kwa upande wake mratibu wa Damu salama mkoani Shinyanga,Dkt. Joel Mdale, ametoa shukrani kwa umoja huo wa makanisa ya kipentecoste kwa hamasa hiyo ya uchangiaji wa damu salama, jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa damu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa, na hatimaye kuokoa vifo vya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwamo wajawazito. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiwataka wananchi kuendelea kufanya mazoezi ambayo yatawasidia kuimarisha afya zao. Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog. Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentecoste mkoani Shinyanga Askofu, Elias Madoshi, akielezea namna walivyohamasika kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano, kwa kufanya mazoezi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchagia damu salama kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko katikati mwenye kofia akiongoza mazoezi kwa kutembea kwa miguu pamoja na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga. Mazoezi yakiendelea kwenye uwanja wa Sabasaba mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kutembea na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga. Viongozi wa dini kutoka makanisa ya kipentecoste mkoani Shinyanga wakiwa na wananchi pamoja na watumishi wa Serikali kwenye mstari kwa ajili ya kuchangia damu salama kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Mratibu wa damu salama mkoani Shinyanga Joeli Mdale akimtoa damu Askofu Josephat Msila kutoka kanisa la Kipentecoste (TMRC) Ndembezi mjini Shinyanga. Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea. Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) Shinyanga, akiombea amani mkoani Shinyanga katika kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

WAZIRI KIGWANGALLA AHAMASISHA WASANII, WAFANYABIASHARA NA WANASIASA MAARUFU KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

MLIMA KILIMANJARO WATUMIKA KATIKA MAPAMBANO VITA DHIDI YA UKIMWI

MABODI AWATAKA WANACHAMA KUHAKIKISHA WANASHINDA MAJIMBO YOTE YA UCHAGUZI WILAYANI MFENESINI

$
0
0

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi,akipokea Heshima ya Utii kutoka kwa Vijana Maalum wa UVCCM Wilaya ya Mfenesini mara baada ya kukagua Gwaride la Kikundi hicho alipowasili katika ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Kawaida wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mfenesini Unguja.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi,akivishwa Skafu na Kijana wa UVCCM wa Wilaya ya Mfenesini Unguja mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharibi ”A” Unguja, kwa ajili ya kufungua Mkutano wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Mfenesini Unguja.


MWENYEKITI wa CCM Wilaya Mfenesini Ndugu Kesi Mashaka Ngusa akizungumza katika Mkutano wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya Wilaya hiyo uliofanyika leo huko katika ukumbi wa Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja

MWENYEKITI wa CCM Mkoa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud akizungumza katika Mkutano wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya Wilaya hiyo uliofanyika leo huko katika ukumbi wa Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.
*****************************
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,amewataka Wanachama,Viongozi na Watendaji wa CCM Wilaya ya Mfenesini kuhakikisha Taasisi hiyo inashinda Majimbo yote ya Uchaguzi ndani ya Wilaya hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Dola Mwaka 2020.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua Mkutano wa kawaida wa Halmashauri Kuu ya Wilaya hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza la Manispaa ya Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja.
Alisema Viongozi na Watendaji hao kwa kushirikiana na Wanachama na Makada  mbali mbali wanatakiwa kuendelea kufanya kazi mbali mbali zikiwemo kuelezea kwa kina namna Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 inavyotekelezwa katika maeneo yao.
Aliwataka viongozi hao kuendeleza mikakati ya kuongeza Wanachama wapya waliotimiza umri wa kupiga kura kwa mujibu wa Sheria za Nchi, ambao ndio Mtaji wa kudumu wa CCM watakaoleta ushindi wa Chama katika Uchaguzi Mkuu wa Dola Mwaka 2020.
Katika maelezo yake Dk.Mabodi,alisema Serikali ya Awamu ya Saba chini ya Uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amekuwa ni kinara wa kuenzi na kudumisha Amani na Utulivu wa Nchi hali inayochochea Maendeleo Endelevu.
Alieleza kuwa Tunu hiyo ya Amani inatakiwa kulindwa kwa gharama yoyote na kila Mwananchi bila kujali tofauti za Kidini,Kisiasa na Kikabila kwani ndio chimbuko la mafanikio katika Nyanja mbali mbali za Kiuchumi,Kijamii na Kisiasa.
“CCM tunaendelea kusimamia Serikali yetu itekeleze kwa kasi Ilani ya Uchaguzi kama tulivyoahidi wakati wa Kampeni za kuomba ridhaa za Uongozi kutoka kwa Wananchi,tumepiga hatua kubwa ya maendeleo katika Sekta mbali mbali za Kilimo,Uvuvi,Afya,Mawasiliano,Usafiri wa Anga,Baharini na Nchi kavu,Elimu na Barabara”,alisema Dk.Mabodi.
Dk.Mabodi alieleza kwamba Chama Cha Mapinduzi kinawathamini Wananchi Wote bila kujali tofauti zao za Kisiasa ndio maana kinasimamia Sera zake zitekelezwe kila eneo linalohitaji huduma za Kijamii na Kiuchumi.
Sambamba na hayo aliwasihi Viongozi hao kuendeleza Utamaduni wa kufanya Vikao vya Kikatiba kwa Wakati husika ili kutoa fursa pana ya ngazi mbali mbali za Uongozi kujadili na kufanya Maamuzi ya kuimarisha Chama.
Aliwakumbusha kwamba CCM haitovumilia Mwanachama yeyote atayetumika kufanya ama kufanyiwa kampeni za kugombea nafasi za Uongozi mwaka 2020,kabla ya Chama kutangaza kufanyika kwa mchakato huo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Magharibi Ndugu Mohamed Rajab Soud,alisema kufanyika kwa Mkutano huo kunatoa nafasi pana kwa Ngazi ya Mkoa ya Kichama kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Alisema kuwa Hali ya Kisiasa ndani ya Mkoa huo kwa sasa ipo vizuri na inaimarika zaidi kutoka na juhudi za Viongozi wa Majimbo ambao ni Wabunge na Wawakilishi kutekeleza Wajibu wao kwa Jamii.
Kwa upande Wake Mwenyekiti wa Wilaya ya Mfenesini Ndugu Kesi Mashaka Ngusa,alisema Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo imeendelea kutekeleza kwa ufanisi masuala mbali mbali ya kuleta Maendeleo ndani ya Wilaya sambamba na kuwajenga Kiitikadi na Kiuongozi Wanachama wa CCM hasa Vijana na Wanawake.

YANGA KUWA NA WIKI YA MWANANCHI KILA MWEZI WA NANE

$
0
0
Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga imetoa mapendekezo kadhaa kwa Uongozi wa Klabu ya Yanga ikiwemo kuanzisha wiki ya mwananchi itakayokuwa inafanyika mwezi wa nane kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga Anthony Mavunde wakati wa hafla ya KUBWA KULIKO inayoendelea kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mavunde amesema katika ripoti yao wapendekeza kuanzishwa kwa wiki maalum itakayojulikana kama ‘Wiki ya Mwananchi’, ambayo ni maalum kwaajili ya wapenzi na wanachama wa Yanga kuitumikia jamii.

Amesema wiki hiyo itakuwa ikifanyika mwezi Agosti kila mwaka na siku ya kilele chake kutafanyika tukio kubwa litakalofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam likiambatana na utambulisho wa wachezaji wao wapya.

“Tumepanga tuwe na Wiki ya Mwananchi’, ambapo wanachama wa Yanga watafanya usafi maeneo katika hospitali, masoko na kutoa misaada mbalimbali. Wiki hiyo ikikamilika tutakutana Uwanja wa Taifa”, amesema Mavunde.

Amesema wamemuomba Rais Magufuli na endapo ataridhia tukio hilo litafanyika mwaka huu ambapo miongoni mwa mambo yatakayofanyika ni kutambulisha wachezaji wao wapya wanane ambao wamesajiliwa kutoka nje ya Tanzania kwaajili ya msimu ujao.

SOKO LA MADINI LAFUNGULIWA RASMI ARUSHA

$
0
0
Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Waziri wa Madini Dotto Mashaka Biteko amezindua soko la madini mkoani Arusha ambalo litawarahisishia wafanyabiashara na kuruhusu mzunguko wa fedha jambo ambalo serikali imeamua kusimamia rasilimali za nchi 

Akizungumza katika ufunguzi  wa soko hilo Biteko amesema hakuna serikali inayoweza kujiendesha bila kulipa kodi ambapo maendeleo ya nchi yanaletwa kwa kulipa kodi pesa hizo zipatikana kwenye madini na watu wa kufanya hivyo ni watanzania wenyewe.

 Mhe. Biteko amesema jambo hilo ni la kwanza kutokea  kihistoria tangia kupata uhuru kuwa na soko la madini katika mkoa wa Arusha,kwani Tanzania ni nchi ambayo imejaliwa kuwa na madini ambapo mengine hayawezi kupatikana  nchi nyingine zaidi isipokuwa nchi ya Tanzania.

Amewataka wafanyabiashara wa madini kupambana kuondoa rushwa kwenye sekta ya madini na kuwasihi kutokutumia muda mwingi kuwashawishi kuchukua zawadi kwani kwa kufanya hivyo hakusaidii kuondoa rushwa kwenye sekta ya madini,ametoa tahadhari kwa watu wote ambao wanadhania soko hilo wanaweza wakalihujumu

 "WanaArusha wachukieni watu wanaokwepa kulipa kodi,wachukienu wanaotorosha madini na tumpende mtu anayelipa kodi  na sisi serikali mtu anayelipa kodi tumpe heshima akija kwenye ofisi yako mpe na maji ya kunywa.amesema Biteko" alisema Biteko

Mrisho Gambo ni mkuu wa mkoa wa Arusha amewataka wafanyabiashara hao kulitumia soko hilo kwa faida na amewajakikishia kuwa hakuna mfanyabiashara atakayenyang'anywa madini yake kama baadhi ya watu wanavyozusha,amesema yeye yupo tayari kushirikiana na Waziri katika wizara husika ,kuhakikisha hakuna mfanyabiashara wa madini ananyanyaswa.

" Wapo baadhi ya watu wanakujakuja wanajifanya wao sijui nani sijui nini wanafanya mambo ya ajabu ajabu namba zetu mnazo malengo wa serikali siyo kunyanyasa wafanyabiashara ,lengo la serikali nikuwatengenezea mazingira mazuri ili ipate haki yake na nyie mpate haki yenu"alisema Gambo

Aidha amemuomba mhe.Waziri kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani hapo, waruhusiwe kuwa na senta ya kisasa ya madini,waendelee kufanya maonyesho ya madini kwani mkoa huo ni wa kimataifa na unapata wageni wengi kutoka nchi za nje na Taasisi nyingi za Kimataifa,zipo mkoani hapo ambapo mkoa huo ni  soko la kimataifa

"Lengo la serikali ni kuona wafanyabiashara wanapata soko la madini ili waweze kuliingizia Taifa kipato,kulipa kodi halali na wao kunufaika kinaisha ma siyo kuzusha na kubambikiana mambo yasiyofaa ya uongo uongo"alisema Gambo.

Kwa upande wake Afisa madini mkazi Richard Robert mkoani Arusha akitoa taarifa amesema hadi sasa mkoa unakaribia kuwa na madini mbalimbalimbali kutokana na hali ya kijiolojia.

Amesema takwimu za madini mkoa wa Arusha kwa mwaka 2018-2019 zinaonyesha kuwa madini yenye thamani ya jumla ya shilingi 21,074,505,883.43,yaliuzwa na mrahaba ulipatikana zaidi ya shilingi764, 385,283.88 tzs,ambapo ada ya ukaguzi ni 208,653, 073.56,.

Amesema takwimu hizo zinadhihirisha kuwa mapato yanayokusanywa kutokana na madini 40% ya maduhuli yote,ambapo  hadi sasa mkoa wa Arusha umeshavuka lengo lililowekewa la kukusanya shilingi 2,500,000,000 kwa kiasi cha 102,419,194.95Tzs

Umaarufu wa mkoa wa Arusha umejijenga zaidi miaka 30  iliyopita kwa kipindi cha  mwaka wa serikali 2018-19 Hadi sasa wapo wafanyabiashara 97 wafanyabiashara wadogo wa madini 291,ARUGEBA783 na TASGEDO 500.

Mkoa wa Arusha una ukubwa wa kilometa za mraba 37,576 una jumla ya leseni 784 za uchimbaji mdogo,leseni 4 za uchimbaji wa kati,leseni 42 za utafiti na leseni 1 ya uchenjuaji ambapo pamoja na utalii umekuwa kivutio cha biashara ya  madini
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akimsikiliza mmoja wawafanyabiashara wa madini ambao wanaongeza thamani na kutengeneza vito vya thamani alipokuwa anatembelea maonyesho ya bidhaa za madini katika ufunguzi wa soko la Madini mkoani Arusha.

 Waziri wa Madini Dotto Biteko akisalimiana na wafanyabiashara wa madini Mkoani Arusha katika ufunguzi wa soko la madini mkoani hapo.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wafanyabiashara na wa madini na wakazi wa Arusha kaika uzinduzi wa soko la Madini mkoani Hapo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akitangulisha wageni meza kuu katika ufunguzi wa Soko la Madini .
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akizungumza na wafanyabiashara ,mabroka wa madini na wakazi wa mkaoa wa Arusha wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha
Waziri Biteko akisalimiana na moja wawananchi wa mkoa wa Arusha ambae pia ni mfanyabiashara wa madini

Waziri wa Madini akisalimiana na Mzee Elishilia Kaaya mkurugenzi wa AICC walipokutana kwenye ufunguzi wa soko la madini ,wakiwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Mkurugenzi wa AICC Elishilia Kaaya akitoa salamu kwa wafanyabiashara wa madini.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake ambapo ametilia mkazo kwa wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo vizuri kwa manufaa ya watanzania.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia jambo wakati wa ufunguzi wa soko la madini
Wafanyabiashara wamadini wakiwa katika viwanja vya eneo la AICC ambapo ndipo ofisi za wauzaji wa madini zilipo
Wafanyabiashara wa madini wakifuatilia hotuba ya Waziri Biteko kwa makini kabla ya ufunguzi wa soko la madini
Wafanyabiashara wa madini

Waziri wa Madini Dotto Biteko akiangalia Madini ya Tanzanite katika maonyesho katika moja ya ofisi ya wauza madini,kushoto kwake ni mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa madini mara baada ya ufunguzi rasmi qa soko la madini mkoani Arusha.
Waziri wa Madini Mhe.Dotto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikalikatika mkoa wa Arusha na baadhi ya viongozi wawafanyabiashara ya madini .




Bonde la Wami/ Ruvu lazuia uchimbaji mchanga Mto Mbezi

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Wakazi wa Kawe Mkwamani wanaokaa pembezoni mwa Mto mbezi watakiwa kuacha kuendelea kuchimba mchanga katika mto huo.

Kuchimba kwa mchanga huo kunasababisha madhara kwa wakazi wa eneo kwa kuongeza kingo  na kufanya wakati wa mvua baadhi nyumba kuanguka.

Akizungumza na Wananchi Kawe Ukwamani Afisa wa maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema zuio hilo ni kwa mujibu wa sheria ikiwa ni kulinda mazingira ya Mto  Mbezi na hakuna kibali cha uchimbaji wa mchanga katika Mto huo.

"Nyumba za watu zinabomoka, watu wanachimba wanaenda hadi kwenye kuta za nyumba na kuanguka, hivyo haiwezekani uchimbaji huo ukiendelea katika eneo hili”. Amesema Mhandisi Ngonyani.

Aidha Mhandisi Ngonyani amesema kuwa sheria za rasilimali za maji ya mwaka 2009 namba 11 mwenye mamlaka ya kutoa vibali kwaajili ya watu kuingia mtoni kwaajili ya shughuli yoyote ile ni bonde hasa wao Wami-Ruvu sio halmashauri kwasasa.

Kwa upande wa Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kawe ASP. Dkt. Ezekiel Kyogo amewataka wachimbaji wamchanga wa maeneo hayo  kufuata sheria na taratibu zilizowekwa ili wasiweze kuingia katika matatizo.

 “Kama wanataka kuchimba mchanga wanatakiwa kufuata sheria kwani kila kitu kina utaratibu wake zilizowekwa na kama wakiamua kutofuata sheria basi sheria itachukua mkondo wake”. Amesema ASP. Dkt. Kyogo.
 Baadhi ya nyumba zilizolika kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanywa katika Mto Mbezi Kawe Mkwamani.
 Mkuu wa Operesheni wa Polisi Wilaya ya Kawe Dkt.Ezekiel Kayogo akizungumza na waandishi habari namna walioyapokea maagizo ya zuio la uchimbaji wa mchanga katika Mto Mbezi,jijini Dar es Salaam.
 Gari lililokutwa katika Mto Mbezi eneo la Kawe Mkwamani likiwa limebeba mchanga ambapo walilikamata Jeshi la Polisi.
 Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akitoa maelezo kwa wananchi Madhara ya uchimbaji mchanga katika Mto Mbezi.
 Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kupiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika Mto Mbezi jijini Dar es Salaam.

Shilingi Milioni 150 zategwa kukarabati Miundombinu Chuo cha Michezo Malya.

$
0
0

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
akizungumza na Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali,wanafunzi na wazazi (hawapo katika picha) katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo cha Maendeleo ya Micheo Malya kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Maganga na Kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw.Jeremiah John. 
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw.Richard Maganga akitoa taarifa fupi ya chuo hicho wakati wa mahafali ya 08 ya Stashahada za Michezo mbalimbali 8 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo hicho kilichopo Wilaya yaKwimba Jijini Mwanza.Kulia ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza. 

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw.Jeremiah John akitoa salam za Wilaya wakati wa mahafali ya 08 ya Stashahada za Michezo mbalimbali yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika cha Maendeleo ya Michezo Malya Chuo kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza na kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Maganga 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Bw.Jeremiah John akimkabidhi zawadi
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza aliyopewa na uongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya wakati wa mahafali ya 08 ya Stashahada za Michezo mbalimbali yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza. 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
akikabidhi vyeti kwa baadhi ya Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali,katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo cha Maendeleo yaMicheo Malya kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza. 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, Viongozi wa Wilaya ya Kwimba pamoja na baadhi ya Wahitimu wa Stashahada za Michezo mbalimbali, katika mahafali ya 08 yaliyofanyika Juni 15, 2019 katika Chuo hicho kilichopo Wilaya ya Kwimba Jijini Mwanza. 

******************** 




Na Shamimu Nyaki –WHUSM

Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Milioni mia moja hamsini (150,000,000/=) kwa ajili ya kukarabati viwanja pamoja na kuchimba kisima cha maji katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ili kuondoa kero hiyo iliyodumu kwa muda mrefu chuoni hapo. 

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza katika mahafali ya na ne ya Chuo hicho ambapo amewataka wahitimu hao kutumia taaluma waliyoipata kuendeleza michezo hapa nchini. 

“Fedha hizi ni kwa ajili ya kukarabati miundombinu ambayo Serikali imeelekeza nawaomba sana viongozi mtumie pesa hizi kwa uangalifu na kuzingatia makusudi ya yaliyowekwa ili changamoto zilizopo ziishe na wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki” Mhe.Shonza. 

Aidha Mhe.Naibu Waziri ameongeza kuwa Wizara inaendelea kushughulikia andiko lililowasilishwa na chuo hicho la kutaka Chuo kuwa Wakala wa Serikali ili kusaidia kuongeza tija na ufanisi wa chuo hicho ambacho ndio chuo pekee kinachotoa taaluma ya michezo hapa nchini. 

Mhe.Shonza pia amewataka viongozi na wakufunzi wa chuo hicho kuongeza ubunifu na kutafuta njia mbadala kwa ajili ya kupata fedha za kukabiliana na changamoto mbalimbali pamoja na kukitangaza chuo hicho ili kipate wanafunzi wengi zaidi. 

Vilevile amewataka Viongozi wa Halmsahuri ambazo wahitimu wametoka kuwatumia vizuri watalaam hao katika shughuli zote za kimichezo katika maeneo wanayotoka,lakini pia kuongeza idadi ya watumishi kujifunza katika chuo hicho. 

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Bw.Richard Maganga amesema kuwa chuo kinatoa mafunzo mbalimbali ikiwemo ya muda mfupi kwa ajili ya kujenga uwezo kwa walimu wa Michezo ambapo mpaka sasa zaidi ya walimu 557 wameshapata mafunzo katika mikoa ya  ingida,Mwanza,Dodoma,Iringa,Mbeya na Tabora. 

“Zoezi hili linafanyika ili kuhamasisha michezo pamoja na kutoa elimu ya awali kwa ajili ya waalimu wanaofundisha Michezo, Na masomo yanayofundishwa Chuoni hapa yanazingatia mitaala ambayo imepitishwa na NACTE”Bw.Maganga. 

Bw.Maganga ameongeza kuwa tangu Chuo kianze kutoa Stashahada tayari
kimeshadahili wanachuo 531 na kimeshatoa wahitimu takriban 280 ambao wengi ni watumishi wa Halmashauri mbalimbali nchini. 

Naye Mhitimu Daniel Manala amesema kuwa taaluma aliyopata kwa kipindi cha Miaka miwili itamsaidia katika kufundisha michezo kwa wanafunzi ambao ndio wenye ari kubwa ya kujifunza michezo mbalimbali. 

Jumla ya wahitimu 115 wamehitimu mafunzo mbalimbali ikiwemo Stashahada ya ufundishaji michezo,Stashahada ya elimu ya viungo vya mwili katika michezo pamoja na Stashahada ya uongozi na Utawala katika Michezo

OLE MILLYA AFAGILIA MIRADI YA KIMKAKATI YA MAGUFULI

$
0
0

Mbunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya amesema miradi mikubwa mitano ya kimkakati inayotekelezwa na iliyoahidiwa na Serikali ya Rais John Magufuli Wilayani Simanjiro ndiyo imesababisha yeye aondoke Chadema na kuhamia CCM.

Ole Millya akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet alisema aliamua kuhama kama shukrani na kumuunga mkono Rais Magufuli kutokana na maendeleo hayo. 

Alitaja miradi hiyo ya maendeleo ni baada ya kusoma ilani ya CCM chini ya serikali ya Rais John Magufuli juu ya ujenzi wa barabara ya lami ya Arusha, Komolo, Terrat na Mirerani, Orkesumet, Kiteto hadi Kongwa mkoani Dodoma. 

Alisema mradi mkubwa wa maji wa mto Pangani (Ruvu) hadi Orkesumet wenye thamani ya sh41 bilioni unaoendelea, ukuta wa madini ya Tanzanite ambapo badala ya kukusanya sh70 milioni kwa mwaka sasa inakusanywa sh2.1 bilioni na wananchi wanafaidika nayo. 

"Mradi mwingine ni katika hospitali mpya 60 nchi nzima zinazojengwa na sisi Simanjiro tumepata hospitali ya wilaya tukitengewa sh1.5 bilioni, na ujenzi unaendelea kwa kasi kwenye kata ya Langai kwani hatukuwa na hospitali tangu wilaya igawanywe kutoka Kiteto," alisema Ole Millya. 

Alitaja sababu nyingine ni mgogoro baina ya wafugaji wa kata ya Loiborsiret na hifadhi ya Taifa ya Tarangire na pori la akiba la Mkungunero ulisababisha waishi kwa hofu na manyanyaso ila Rais Magufuli akaingilia kati na kuwasaidia wafugaji nchini. 

"Kilio cha wafugaji kupatiwa ufumbuzi baada ya Rais John Pombe Magufuli kuunda Tume ya Mawaziri nane wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kufuatilia kero za wafugaji wa Kimotorok," alisema Ole Millya. 

Alisema kutokana na maemdeleo hayo yanayofanyika Simanjiro aliamua kuhama Chadema na kurudi CCM chama ambacho alikuwepo na kuwahi kuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya UVCCM mkoani Arusha.

"Baada ya kuona ubabaishaji na ubaguzi unafanyika CCM wilayani Simanjiro niliamua kuhamia Chadema na ninawashukuru mkanichagua mimi mtoto wa masikini ambaye sikuwapa hata shilingi moja," alisema Ole Millya.

Diwani wa kata ya Orkesumet, Sendeu Laizer alimshukuru Ole Millya kwa kuwasemea bungeni hadi wakapata sh200 milioni za kituo cha afya na Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo ameahidi kuwapatia kilomita mbili za barabara ya lami.

Laizer alisema pia sekondari ya Simanjiro imeboreshwa na mwaka huu itapokea wanafunzi wapya wa kidato cha tano kwani mabweni na bwalo la kulia chakula yameshakamilika.

Alisema mwaka 2015 baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mapinduzi walikuwa wanasoma chini ya miti lakini serikali ya Rais John Magufuli ikawajengea madarasa saba na kumaliza changamoto hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya (kushoto) akimsikiliza Ofisa mtendaji wa kata ya Orkesumet, Edmond Tibiita (kulia) akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika eneo hilo, katikati ni Diwani wa kata hiyo Sendeu Laizer.

 Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, James Ole Millya akifurahi baada ya wananchi wa Kata ya Edonyoengijape kumkabidhi zawadi ya kondoo kama shukurani kwa kutetea maslahi ya jamii ya wafugaji akiwa bungeni.

Wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet wakimpokea mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara, James Ole Millya ambaye kwa muda wa zaidi ya wiki moja alikuwa kwenye ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, kuzungumza na jamii na kusikiliza kero, malalamiko na changamoto zao.

PROF KABUDI AKUTANA NA WAMILIKI NA WAFANYABIASHARA WA HOTELI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na baadhi ya wamiliki na wafanyabiashara wa Hoteli baada ya kumalizika mkutano baina yao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Mb) Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli baada ya kumalizika mkutano baina yao uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019. Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Bi. Agnes Kayola.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe akifafanua jambo wakati wa mkutano wa wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli (hawapo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Hoteli wakifuatilia kwa ukaribu mkutano baina yao na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraji Mnyepe wakati wa Mkutano wa wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli (hawapo pichani) Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Sehemu ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Hoteli waliohudhuria mkutano wa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani). Mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.
Baadhi ya Wafanyabiashara na Wamiliki wa Hoteli wakisubiri kupiga picha ya pamoja na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa mkutano baina yao katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. June 15, 2019.

GAVANA SHILATU ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0

Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu Leo Jumamosi Juni 15, 2019 ameshiriki zoezi la usafi wa mazingira akishirikiana na viongozi pamoja na Wananchi wa kata ya Kitama. 

Gavana Shilatu aliwasihi Wananchi wote kuhakikisha wanasafisha na kuyatunza mazingira ili nayo yawatunze ikiwemo kila iitwapo jumamosi kuwa ni siku ya usafi wa mazingira. 

*”Nimetoa maelekezo kwa Watendaji kata na Vijiji kuhakikisha kila iitwapo jumamosi ndani ya Tarafa ya Mihambwe wanashiriki na kusimamia zoezi la kitaifa la usafi wa mazingira na wakati wote wanahakikisha maeneo yao ni safi. Nami nimekuja hapa kuonyesha kwa vitendo kwamba suala la usafi wa mazingira ni jukumu letu sote.”* Alisema Gavana Shilatu. 

Usafi wa mazingira wa kila jumamosi ni agizo na kampeni ya kitaifa ambayo kila Mtu anapaswa kuitii kwa kufanya usafi na kuyatunza mazingira yawe safi nyakati zote. 

Katika zoezi hilo la usafi wa mazingira Gavana Shilatu aliambata na Watendaji kata na Vijiji wakishirikiana na Serikali za Vijiji pamoja na Wananchi.

SADC KUTENGENEZA AJIRA ZAIDI YA 5000 KUINGIZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amewataka wamiliki na wafanyabiashara wa Hoteli Jijini Dar es salaam kutumia fursa ya kibiashara itakayotokana na ujio wa wageni takribani 1000 watakaoshiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuanzia mwezi August 2019. 

Waziri Prof Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli na kuongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itafanya kazi kwa ukaribu na wadau hao wa Hoteli na kuwataka kutoa huduma bora,bidi,weledi na kwa uzalendo usiotiliwa mashaka ili waweze kunufaika na uwepo wa ugeni huo mkubwa wa SADC. 

“Ninyi ni watu muhimu sana katika ugeni huu wa SADC,tushirikiane kuufanya mkutano huu kuwa wa mafanikio makubwa kwa ukarimu na uzalendo wetu na hivyo kutufanya pia kuingiza kipato katika biashara zetu kwa kuwa tukifanya vizuri kila watakapokuwa wanakuja Tanzania kwa mikutano mingine ya mawaziri watafikia katika hoteli zetu kutokana na ukweli kuwa tutakuwa na mfululizo wa mikutano ya SADC kuanzia August 2019 hadi August 2020 Tanzania itakapokoma kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo” 

Ameongeza kuwa ataendelea kukutana na wadau mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wa Sekta binafsi ili kuhakikisha fursa ya kufanyika kwa mkutano wa SADC hapa nchini inawanufaisha pia wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara. 

Katika Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi ameongozana pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo kwa upande wake amesema kutokana na Mkutano huo wa SADC serikali inatarajia kuingiza zaidi ya shilingi bilioni kumi pamoja na kutengeneza ajira zaidi ya elfu tano na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo. 

Pia amewataka wamiliki na wafanyabiashara hao wa hoteli kuzingatia muongozo wa serikali uliotolewa na Gavana wa benki kuu ya Tanzania kuhusiana na suala la ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa kuwataka kuwaelekeza wageni kubadilishia fedha zao benki na pia katika hoteli ambazo zimeidhinishwa kubadilisha fedha za kigeni.

MABADILIKO YA MAAFISA UHAMIAJI WA MIKOA

WAOKAJI VITAFUNWA WAPEWA ELIMU YA KUJITANGAZA KWENYE MITANDAO

$
0
0
Na.Khadija seif,Globu ya jamii

*Washiriki wapewa fursa kushiriki mashindano ya keki juni 26

Tamasha la waokaji  kufanyika rasmi jijini Dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi ambao walijitokeza kwenye tamasha hilo Muandaaji Laura Mkula amesema imekua ni mara ya kwanza kuandaa shindano hilo na muitikio umekua mkubwa kiasi chake kuanzia mchakato wa fomu hadi kushiriki kikamilifu.

" Imekua ni fursa ya kipekee kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo hasa waokaji wa vitafunwa kushindanishwa na kupata ujuzi mpya kuboresha biashara zao,"

Aidha,Mkula ametoa ushauri kwa washiriki wote kuboresha biashara zao huku swala la kujitangaza likipewa kipaumbele na kutengeneza mitandao ya kijamii Kama njia pekee ya kuwasiliana na wateja wao na kuwafikia kwa haraka zaidi.

"Mitandao ya kijamii ifanye biashara yako ya kwanza ili iweze kukupatia wateja wengi zaidi na kupika vitu mbali mbali kutokana na idadi ya wateja wako,"

Pia amepongeza washiriki wote ambao wameweza kujitokeza kwenye tamasha hilo kwani wote ni washindi na wamefanya uthubutu wa kushiriki japo washindi ni watatu ambao wameweza kushinda zawadi.

"Waliochukua fomu walikua 15 lakini tumeweza kupata washindi watatu , Diana bakery ambae mshindi wa kwanza aliyejishindia jiko la kuoka keki ,hakim Bakery, huku mshindi wa pili fatna production alipewa vifaa vya upishi pamoja na jastin makeki ambae alifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu alizawadiwa vifaa vya upishi wa keki,"

Kwa upande wake mshindi wa kwanza edina cake amepongeza washiriki wote pamoja na muandaaji wa shindano hilo huku akiwataka wakina kuacha kujibweteka nakusubiri kuajiriwa.

"Kwa mara ya kwanza nilitamani kushiriki shindano hilo na Leo nimeibuka mshindi japo kuna wakati nilikata tamaa nakuona ni vitu vya ubabaishaji ,"
Aidha, jaji wa tamasha hilo Alexander vitalis amewahimiza washiriki wote kuchukua ujuzi zaidi ili kushiriki mashindano makubwa zaidi.

"Wote wamefanya vizuri japo hakuna vitu ambavyo vimekua tofauti sana kuanzia ladha na baadhi ya mionekano ya keki,"

Pia vitalis ametoa nafasi ya upendeleo kwa washiriki wote kushiriki shindano la keki bure linaloandaliwa na zena Sharif (Anezliytta) juni 26 mwaka katika ukumbi wa kingsolomon jijini Dar es salaam .
Majaji wakipita kila meza ya mshiriki kuonja keki kwenye tamasha la waokaji lilofanyika katika ukumbi wa little threate jijini Dar es salaam 

TCRA Kanda ya Mashariki yakutana kujadili huduma za mawasiliano

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa changamoto ya mawasiliano ni watumiaji wenyewe kwa kutojua namna ya kutumia mitandao.

Odiero aliyasema hayo jana wakati akifungua mkutano wa Kanda ya Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mkutano wa wadau ni kutaka kupata ushauri na changamoto ya mawasiliano katika utoaji huduma unaofanywa na TCRA Kanda ya Mashariki.

Mhandisi Odiero amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wadau ikiwa ni utoaji wa maoni pamoja na changamoto zinazowakabili ambazo baada ya mkutano huo zitashugulikiwa.  Aidha amesema kuwa mkutano huo ni pamoja na kujua mkataba wa TCRA katika utoaji huduma ikiwa na watoa huduma kutoa mkataba kwa wateja wao kwa bidhaa wanazozipata.

Odiero amesema kuwa malalamiko walioyapokea ni 57 ambapo wanashughulikia  yanayohusiana na matumizi ya simu. Mmoja wa wadau meneja wa Abood Media Abeid Dogori amesema  kuwa mkutano wadau ni mhimu kwani unatatua changamoto kwao kwa kutoa yaliyomoyoni na kuwa tofauti na kupeleka taarifa kwa maandishi.

Amesema kuwa TCRA imejapambanua katika utoaji huduma kwa wateja wao ikiwa ni kutatua changamoto kutokana na kushirikisha baadhi vyombo vingine vya serikali ikiwemo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na Jeshi la Polisi.

Meneja wa Radio Okoa FM ya mkoani Morogoro Gelard Nyabinyili amesema kuwa TCRA iendelee kuwa karibu ili changamoto zinazowakabili kama watoa huduma kuweza kutatuliwa kwa wakati.

Amesema jambo la kuleta mkataba kwa  mteja wa TCRA ni muhimu kwani wangeweza kukaa nao lakini wameona ushirikishaji ni bora kwa wateja kuelewa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza katika kukaa cha wadau wa sekta ya mawasiliano Kanda hiyo kujadili changamoto za Kihuduma na kiudhibiti kwa lengo la kuboresha sekta kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Radio ya Okoa FM ya mkoani Morogoro Gelard Nyabinyili akitoa maelezo mara baada ya kupata leseni katika kikao cha wadau wa mawasiliano kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero (katikati) akiwa na watendaji wa TCRA wakisiliza ushauri unaotolewa na wadau wa mawasiliano katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi  Lawi Odiero akimkabidhi Leseni Meneja wa Radio ya Okoa FM Gelard Nyabinyili  katika kikao cha wadau kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi wadau wa mawasiliano wakiwa katika kikao kilichoratibiwa na Kanda ya Mashariki ya TCRA na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Ubao wa taarifa ya huduma ya Majisafi toka Dawasa

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images