Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

0
0

TANGAZO


            MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni 2019. Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma.


Wakati wa maadhimisho hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa madawati maalum ya kutoa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya Mtumba jijini Dodoma na zile zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Huduma zitakazotolewa ni pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa hoja mbalimbali za wananchi kuhusu Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.


Madawati hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.



NYOTE MNAKARIBISHWA.



Imetolewa na:


Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

14 Juni 2019






RAIS WA JAMHURI YA DEMOKRASIA YA CONGO (DRC) MHE. FELIX TSHISEKEDI AMALIZA ZIARA YAKE RASMI YA SIKU MBILI NCHIN

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na vyombo vya habari vya ndani na nye ya nchi baada ya mazungumzo rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kabla ya kumsindikiza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo kwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakatia aikondoka Ikulu kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019

Mkandarasi wa Mradi wa umeme wa Rufiji (MW 2115) kuanza ujenzi rasmi leo

0
0

Imeelezwa kuwa, Mkandarasi wa mradi wa umeme wa Rufiji, kampuni ya JV Arab Contractors na Elsewedy Electric anaanza rasmi kazi za ujenzi wa mradi huo leo tarehe 15/6/2019.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani baada ya ziara ya kukagua kazi za maandalizi ya awali ya ujenzi wa mradi huo akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Regina Chonjo, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na watendaji wengine kutoka Kampuni ya Mkandarasi, Wizara ya Nishati na TANESCO.

Mkandarasi huyo anaanza ujenzi ikiwa ni baada ya kufanya matayarisho mbalimbali ikiwemo upelekaji wa vifaa vitakavyotumika katika shughuli za ujenzi, uwepo wa kambi za Wafanyakazi, Ofisi na kukamilisha kazi nyingine za awali ambapo kwa mujibu wa mkataba.

Alipewa miezi Sita ya kufanya kazi hizo ambayo ukomo wake ulikuwa Juni 14, 2019.Dkt Kalemani alisema kuwa, kazi anazoanza nazo leo ni upasuaji wa miamba ili kuruhusu maji kupita kwenda kwenye mitambo ya kufua umeme.

Alisema kazi nyingine za awali zitakazofanywa ni kujenga daraja la muda litakaloruhusu upitishaji wa vifaa kwenda kwenye eneo jingine la kazi pamoja na ujenzi wa daraja la kudumu.Dkt Kalemani alieleza kuwa, Mkandarasi ameahidi kukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Juni, mwaka 2022 na mradi utatekelezwa kwa kasi na ikiwezekana, megawati zote 2115 zitapatikana kwa wakati mmoja.

Kuhusu vifaa vitakavyotumika kwenye mradi huo, Dkt Kalemani aliwataka kutumia vifaa vinavyopatikana nchini na kwa vifaa visivyopatikana nchini, vitanunuliwa baada ya kupata kibali maalum.

Pia aliagiza Wataalam wa ndani kupewa kipaumbele katika ujenzi wa mradi huo, ili waweze kusimamia mradi huo mara baada ya mkandarasi kukamilisha kazi.

Aidha, aliwapongeza TANESCO na TANROADS kwa kusimamia mradi huo ipasavyo, na kuwaagiza kuendelea kuwasimamia wakandarasi usiku na mchana. 



KUBWA KULIKO YA YANGA: FULL SHANGWE!! WAWEKA HISTORIA..

0
0
<iframe width="660" height="390" src="https://www.youtube.com/embed/a47OeJ1J5Hs" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture" allowfullscreen></iframe>

WATUMIA JINA LA MKURUGENZI WA NEC KUFANYA UTAPELI, MWENYEWE AWATAHADHARISHA WANANCHI

0
0
Na Ripota wetu,Michuzi TV

KUNDI la matapeli linadaiwa kutumia jina la Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) Dk.Athumani Kihamia na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kututoka na utapeli huo Dk.Kihamia ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini na utapeli unaoendelea kwenye mitandaoni wa kutumia jina lake.


Akizungumza  kwa njia ya simu, Dk.Kihamia amesema kuna watu wamefungua akaunti feki ya face book na  kuwatapeli watu kwa kuwatumia ujumbe kwa njia ya messenger.

"Kuna baadhi ya watu wamefungua akaunti kwa jina langu na kulitumia kwa kujipatia fedha kwa njia hiyo ya utapeli huku wakijua ni kosa kisheria ,"amesema.

Baadhi ya jumbe hizo ambazo zinatumika kufanyia utepeli zinasema kwamba Dk.Kihamia anauwezo wa kuwatafutia kazi katika mbuga ya Hifadhi ya Serengeti .

"Yaani tayari kuna watu wameliwa fedha na matapeli hao .Sehemu ya ujumbe huo unasema hivi "angalia kama kuna mtu amemaliza chuo na hajapata kazi uniambie maana kuna kazi shirika la Marekani la Thomson Zoology  kule Serengeti National Park na wanahitajika watu wawili wenye diploma au degree kwa ajili ya kazi ya reservations na mshahara milioni moja na laki nane kama kuna mtu aniambie mapema nimoe namba ya huyo mzungu ahsante,"amefafanua wakati anaelezea utapeli huo .

Hivyo Dk. Kihamia amewataka wananchi kuwa makini na kwamba ujumbe uliko kwenye mitandao ya kijamii  si wake ni wa matapeli.

"Nilishawahi kukanusha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii lakini naona hali inazidi kuendelea hivyo wananchi wanatakiwa kuupuuza ujumbe huo,"alisema Dk.Kihamia.

Agizo la Jaffo Lawaamsha Usingizini Viongozi Arusha ,Watekeleza kwa kasi

0
0

Na Ahmed Mahmoud,Arusha 

Serikali ya wilaya ya Arusha kwa kushirikiana na jiji la Arusha imeanza kutekeleza agizo la waziri wa nchi ofisi ya Rais, TAMISEMI,Suleiman Jaffo alilotaka jengo la hospitali mpya ya Wilaya,ambalo ujenzi wake umekamikija ,kuanza kutoa Huduma Mara Moja kwa wananchi. 

Mei 25,mwaka huu waziri Jaffo alitembelea mradi wa jengo hilo uliopo eneo la Njiro Kontena jijini hapa na kukuta limekamilika muda mrefu lakini halifanyi Kazi ,ambapo alitoa wiki mbili kwa uongozi wa wilaya na halmashauri ya Jiji la Arusha kuhakikisha hospital hiyo inafunguliwa Mara Moja na kutoa Huduma kwa wananchi. 

Akiongea na vyombo vya habari katika hospital hiyo Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqqar alisema hospitali hiyo tayari imeshaanza kutoa Huduma za chanjo na inatarajiwa kuanza kutoa Huduma zingine za matibabu muda mfupi ujao baada ya vifaa Tiba kuwasili. 

Katika hatua nyingine Dagarro alisema wilaya hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Jiji la Arusha ,imeingia mkataba wa ujenzi wa jengo lingine la Mama na Mtoto linalojengwa katika hospitali hiyo na kampuni ya ukandarasi ya BQ Contractors LTD ya jijini Dar as salaam . 

Alisema mradi huo utagharimu kiasi cha sh,Bilioni 1.36 fedha ambazo ni za ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha na utakamilika katika kipindi cha miezi saba kuanzia sasa. 

“Leo tumekuja kumkabidhi ukandarasi ujenzi wa jengo la Matenet ambalo utenzi wake utachukua miezi saba kukamikika” alisema Daqqar 

Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya BQ ,Mhandisi John Bura alisema kuwa katika kipindi cha miezi saba ya Mkataba watahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati katika kiwango kinachotakiwa. 

“Tutahakikisha tunatekeleza mradi huu kwa viwango vya hali ya juu katika muda tuliokubaliana “Alisema Mhandisi Bura. 

Awali Mkurugenzi wa jjji la Arusha,Dkt Maulid Madeni alisema kuwa kuchelewa kufunguliwa kwa hospital ya wilaya ambayo ujenzi wake umekamilika kumetokana na kubadilika kwa matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba kiasi cha sh,milioni 100. 

Alisema sehemu ya fedha hizo,sh,milioni 70 zilitumika kujenga eneo la X Ray katika kituo cha Afya cha Muriet,huku fedha zingine kiasi cha sh, milioni 30 zikielekezwa katika umaliziaji wa ujenzi katika kituo cha Afya cha Kaloleni. 

Aliongeza kuwa halmashauri hiyo tayari imeagiza vifaa Tiba kwa ajili ya hospital hiyo ya wilaya kutoka bohari kuu ya dawa (MCD) na vinatarajiwa kufika Arusha mwezi ujao ,julai mwaka huu. 

Naye Meya wa jiji la Arusha,Kalist Lazaro amesema kuwa halmashauri hiyo imeelekeza ujenzi wa majengo ya juu (Gorofa) na wanatarajia kujenga majengo 10 katika hospital hiyo ya wilaya kwa ajili ya vitengo mbalimbali vya Tiba na Afya. 

Alisema hatua hiyo ni kutokana na ufinyu wa maeneo ya wazi katika Jiji la Arusha na kupelekea halmashauri hiyo kujiwekea mkakati wa ujenzi wanyumba za gorofa.

WAZIRI MKUU ATOA MWAKA KWA MIKOA ISIYOKAMILISHA MWONGOZO WA UWEZESHAJI

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwaka mmoja kwa viongozi wa mikoa ya Dar-es-salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga ihakikishe iwe imekamilisha kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji.

Pia amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini wahakikishe wanaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama kile cha Kahama ili kuharakisha nia ya Serikali katika kuwezesha wananchi kiuchumi.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Juni 15, 2019) wakati akifungua Kongamano la Nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) na kauli mbiu yake ni Wezesha Watanzania Kujenga Viwanda.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo ya Serikali na ile ya binafsi ili kujua ipo mingapi na inamnufaisha nani na je wanufaika wanajijua na ni kweli wananufaika na kisha wampelekee taarifa.

Waziri Mkuu amesema mikoa yote iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji, nayo ifikapo mwakani inapaswa kuonesha hatua za utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo zilizopo katika maeneo yao.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema matokeo ya tafiti ziliyofanywa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuhusu biashara na uwekezaji nchini yanatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uandaaji wa maandiko ya miradi mikubwa inayopendekezwa na shirika hilo.

“Miradi hiyo ni pamoja na ule wa “Harmonized Innovation Solutions for Local Economic Development” ambao upo katika hatua za maandalizi. Lengo la UNDP ni kuhakikisha kuwa miradi inayohusu uwezeshaji wananchi kiuchumi inatekelezwa moja kwa moja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.”

Amesema NEEC ina uwezo mkubwa katika kusimamia miradi mbalimbali ya uwezeshaji ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo UNDP, ILO, UNCTAD, AfDB na UN-Women, hivyo ameyahakikishia mashirika hayo kuwa Serikali itasimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote ili kupata matokeo yaliyo tarajiwa.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuziagizamamlaka zote zishirikiane na NEEC kuhakikisha kuwa fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizobainishwa kupitia tafiti za UNDP zinafanyiwa kazi. “Aidha, hakikisheni kuwa Miradi mikubwa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inatokana na tafiti hizo”

Amesema anaimani kubwa kuwa kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, malengo mbalimbali ya nchi kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi yatafikiwa. Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 – 2020; Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano; Dira ya Taifa ya Miaka 25; na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya umoja wa Mataifa (SDGs).

Pia Waziri Mkuu amelitaka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi liendeleekuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha 2015 – 2020 kuhusu uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.

“Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iboreshwe sambamba na kuongeza ufanisi ili iweze kuwafikia Watanzania wengi hususan wale wa vijijini. Vilevile, kamilisheni na hakikisheni mnazindua haraka mfumo wa kupima mifuko ya uwezeshaji kwa matokeo ya kiuchumi na kijamii na siyo kwa shughuli walizofanya.”

Amesema uwezeshaji wananchi kiuchumi ni suala mtambuka, sekta mbalimbali za kiuchumi na sekta binafsi zinajihusisha moja kwa moja katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, hivyo, amesisitiza kwamba ni muhimu sana masuala ya uratibu, ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi, yakafanywa mara kwa mara ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.

BENKI YA CRDB YATOA GAWIO LA TZS 9.9 BILIONI KWA SERIKALI

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (katikati) akiwa ameshikilia mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi na Shilingi 6.7 bilioni ikiwa ni Gawio la Serikali kutoka Benki ya CRDB, Jumla ya Gawio ni TZS 9.9 bilioni kwa Serikali Kuu, Halmashauri, Taasisi na Mashirika ya umma ambayo ni Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSF, NSSF, GEPF na ZSSF) - TZS 2.6 bilioni, TAMISEMI (Halmashauri za Mbinga, Lindi, Shinyanga) - TZS 133.7 milioni, Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) - TZS 243.5 milioni Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Tabora - TZS 228 milioni. wengine pichani kutoka kushoto ni Balozi wa Denmark nchini, Einar Jensen, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu. hafla hiyo imefanyika leo juni 15, 2019 katika ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwakabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi na Shilingi 2.5 bilioni kwa wawakilishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSF, NSSF, GEPF na ZSSF), ilililotolewa na Benki ya CRDB.
Muwakilishi wa TAMISEMI (Halmashauri za Mbinga, Lindi, Shinyanga).
Muwakilizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimkabidhi mfano wa hundi muwakilishi wa Chama cha Ushirika cha Wakulima wa Tumbaku Tabora.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya kupokea Gawio la TZS 9.9 bilioni kwa Serikali Kuu, Halmashauri, Taasisi na Mashirika ya umma, lililotolewa na Benki ya CRDB, leo juni 15, 2019 katika ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela. 

















Fedha za Biko kumalizia ujenzi wa nyumba ya mshindi Dodoma

0
0


Mshindi wa Biko jijini Dodoma, Hamad Ibrahim Ramadhan, amesema kwamba ameamua fedha zake za ushindi sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko kumalizia ujenzi wa nyumba yake ili kuepuka adha alizokuwa anakutana nazo. 

Mshindi huyo alisema kwamba kabla ya fedha hizo, aliamua kuhamia kwenye nyumba yake yenye chumba kimoja akiishi na familia yake, jambo lililotatuliwa na ujio wa fedha za Biko nchini Tanzania. 

Naye mke wa mahindi huyo, Mwashabani Bakari Mwingi, aliishukuru Biko kwa kupunguza makali ya maisha yao kwa sababu nyumba yao itakamilika na wataanza kuishi maisha bora. 

Mama huyo alisema kuwa maisha ni magumu, hivyo mumewe kushinda Biko ni jambo la kumshukuru Mungu, maana hakuna aliyetarajia kwamba kuna siku watapata suluhu ya changamoto zao za kimaisha katika familia yao. 

Biko mchezo unaochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi unachezwa kwa kufanya miamala kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba ni 2456, huku washindi wa papo kwa hapo wakiibuka na kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja. 

Mbali na zawadi za papo kwa hapo, Biko inatoa ushindi mnono katika droo zake kubwa za Jumatano na Jumapili, ambapo washindi wake huibuka na mamilioni pamoja na bodaboda Ikiwa na lengo kubwa la kugawa utajiri kwa Watanzania wote.

JESHI LA MAGAREZA LAISHUKURU NMB KWA USHIRIKIANO KIMICHEZO

0
0
JESHI la Magereza limekabidhi cheti maalum cha kuishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa fulana ambao iliutoa kwa wanamichezo walioshiriki tamasha la michezo kati ya Magereza Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.

Cheti hicho maalum kimekabidhiwa leo na Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa kwa Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite ikiwa ni kutambua mchango wa benki hiyo mara kwa mara.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Magereza kabla ya kukabidhi cheti hicho, afisa huyo alisema wataendelea kujenga ushirikiano mzuri na benki hiyo kwa kuwa inawathamini hata maeneo mengine ya kijamii.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite alilishukuru Jeshi la Magereza kwa kutambua mchango na mahusiano mazuri kati ya pande hizo na kusema NMB itaendeleza ushirikiano huo. Aliongeza kwa sasa Benki hiyo imekuja na bidhaa bora zaidi ambazo wateja wao hasa taasisi zinazofanya biashara nao itafurahiya bidhaa hizo.
 Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa (wa pili kulia) kwa kutambua mchango wa benki hiyo ambao imekuwa ikiutoa kwa wanamichezo wa Magereza. Wa kwanza kulia ni Ofisa Michezo Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu waMagereza, Joseph Siwale pamoja na maofisa wa NMB wakishuhudia tukio hilo.

 Maofisa washiriki katika tukio hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo fupi.
 Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha shukrani Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite kwa kutambua mchango wa benki hiyo ambao imekuwa ikiutoa kwa wanamichezo wa Magereza. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Michezo Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu waMagereza, Joseph Siwale pamoja na maofisa wa NMB (kulia) wakishuhudia tukio hilo.

CCM DODOMA WAPONGEZWA MBELE YA KATIBU WA FRELIMO

0
0
Chama Cha Mapinduzi(CCM), kimewapongeza wanachama wake wa mkoa wa Dodoma kwa utulivu walionao kutokana na kutembea na wagombea makwapani.

Pongezi hizo zilitolewa na Katibu Mkuu wa CCM Dk.Bashiru Ally wakati wa hafla ya kumpokea Katibu Mkuu wa Chama cha Frelimo kutoka Msumbiji Samwel Roque ambaye kuja nchini kujifunza Tanzania inavyojishughulisha na siasa za kimapinduzi Barani Afrika.

Akizungumza na wanachama wa CCM Dodoma mara baada ya kumpokea kiongozi huyo, Katibu Mkuu huyo amesema wanaCCM Dodoma katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wapo kwenye hali ya utulivu na hawatembei na wagombea makwapani.








DKT. KIKWETE: UKIWA KIONGOZI KILA TIMU INAKUHUSU

0
0
Rais Mstaafu wa awamu nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete


Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV

Rais Mstaafu wa awamu nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa katika mchezo wa Soka ukiwa Kiongozi kwa madaraka yeyote ya Serikali kila timu inakuhusu. 

Akizungumza katika harambee ya hamasa yakuichangia timu ya Yanga SC ijulikanayo kama 'KUBWA KULIKO', Dkt Kikwete amesema utakuwa Kiongozi mwenye dhamana mpuuzi kukandamiza timu nyingine kwa madaraka yako.

"Kuna Wakati mtu kama Juma Kapuya alikuwa Kiongzi katika Serikali lakini alikuwa Simba kindakindaki hawakutumia nafasi ile kukandamiza timu ya Yanga basi kama angefanya hivyo ingebidi tutafute Waziri mwengine ashughulike na Yanga SC ", amesema Dkt Kikwete.

Katika shughuli hiyo pia, Dkt. Kikwete ameuliza: "Waziri Mkuu sijui timu yako?lakini umekubali mwaliko huu, umefanya jambo la maana sana, tushukuru suala hili, tumpomgeze sana, tusitumie nafasi hii kupiga vijembe Viongozi, ngonjeni watoke madarakani".

KUHUSU SUALA LA KLABU YA SIMBA KUJENGA UWANJA WA BUNJU


Dkt. kikwete amesema kuwa Klabu ya Simba walipokuwa wanataka kujenga Uwanja wa Mabwepande amedai walihitaji kiasi cha pesa Shilingi Milioni 30 ambapo timu hiyo ilimtumtumia Rais wa Klabu hiyo wakati huo, Ismail aden Rage kuomba pesa hizo.

"Na kweli Simba SC walipata uwanja kipindi hicho, na mimi nasema hayo kukumbushia kuwa huu ni wajibu wa Viongozi", amesema Dkt. kikwete.

Hata hivyo, Dkt. Kikwete amemuomba Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kuichangia Yanga SC kwa kutoa chochote, pamoja nakumfikishia ujumbe Rais Dkt. John Pombe Magufuli na yeye kuchangia Yanga SC.

"Nilichangia Simba kupata Milioni 30 Simba Wakapata Uwanja, sisemi mrudishe zile hela ila nawaombea Yanga mchango kutoka kwenu," alieleza Dkt. Kikwete.

Pia amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu zote kuwa na hisia za timu zao sambamba na pale zinapokuwa uwanjani zinacheza, amesema kuwa huwa hapendi kwenda uwanjani lakini amesema Simba wanachangamka,  Yanga SC hawachangamki kama Simba SC.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kikwete amewataka Yanga SC kuwa na Mipango, Mifumo yakuendesha Klabu hiyo kisasa pamoja nakuwekeza katika Soka la Vijana.


Dkt. Kikwete ametolea mfano Kocha wa zamani wa Yanga SC kutoka Romania, Victor Stanslaus kuwa aliwekeza zaidi katika Soka la Vijana ambapo vipaji kadhaa vilizaliwa mfano kina Sunday Manara, Mohammed Rishard, Kassim Manara.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga,Anthony Mavunde akizungumza na vingozi mbalimbali na mashabiki wa tumi ya Yanga leo wakati wa hafla ya KUBWA KULIKO katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa wakati alipowasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.





 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanzana kulia) akiteta jambo na viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya KUBWA KULIKO katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam.




MSEMAJI MKUU WA SERIKALI DKT. HASSAN ABBASI AIPONGEZA PSSSF KWA KUANZA VIZURI KUTEKELEZA MAJUKU YAKE

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MSEMAJI Mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuanza vizuri kutekeleza majukumu yake katika kipindi kifupi tangu kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 15, 2019 ofisini kwake jijini Dar es Salaam wakati alipotembelewa na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, aliyefuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi.

Kwa takriban wiki nzima, Meneja huyo amekuwa kwenye ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ili kujenga mahusiano ikiwa ni pamoja na kueleza malengo ya Mfuko huo ambao ni mpya baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.

“Tunaposikia kuwa watu wameanza kupata mafao yao tena kwa wakati kwakweli ni jambo la faraja kwa serikali kwa hiyo mpeleke salamu zangu kwa watendaji wote, akiwemo mtendaji mkuu wa Mfuko, tunafarijika sana tunapoona kwamba yale malengo ya serikali kuu kuunganisha hii mifuko ili kutoa huduma bora yametimia.” Alisema.

Dkt, Abbasi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Malezeo, pia amempongeza Meneja huyo kwa uamuzi wa kuvitembelea vyombo vya habari kwa lengo la kuelimisha umma na kueleza shughuli za Mfuko kwani hii itasaidia wanachama kujua kinachoendelea kwenye Mfuko wao.

“Huu ni Mfuko mpya, yako maswali mengi yanayozua tashtiti na tashwishwi ambavyo kwa pamoja vinafanya kitu kinaitwa jakamoyo ambayo ni vile mtu anaumia moyoni kumbe anakuwa tu hana taarifa sahihi, hili nalo niwapongeze baada ya kukamilisha zile taratibu za ndani na kuhakikisha wale wastaafu wanapata kile kilicho chao sasa kazi kubwa ni kutoa elimu.” Amefafanua Dkt, Abassi

Aidha Dkt. Abbasi alitoa wito kwa wastaafu na wale wastaafu watarajiwa kutambua kuwa msingi wa pensheni ni kumuhudumia mfanyakazi anapokosa nguvu ya kufanya kazi, ama uzeeni au kutokana na kupata madhara mengine ambayo yatafanya akose nguvu ya kufanya kazi.

“Niwakumbushe watanzia kuwa tuweke pesa benki zile tunazohitaji kutumia leo, kesho au katika kipindi kifupi, lakini mafao ni kwa ajili ya kukusaidia katika maisha ya baadaye, si vema umetumikia nchi, jamii halafu baada ya kustaafu ukaishi maisha ya mashaka.” Aliasa.

Awali Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume alimweleza Dkt. Abassi kuwa amepata fursa ya kutembelea vyombo vya habari ili kujenga na kuendeleza mahusiano ikiwa ni pamoja na kuutambulisha Mfuko huo mpya kwa wadau wa sekta ya habari.

Alisema Mfuko ulianza kutekelez amajukumu yake Agosti 1, 2018 na ndani ya miezi 6 tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu hayo umeweza kulipa malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ile ya kila mwezi kiasi cha shilingi bilioni 880, lakini pia Mfuko unaendelea na zoezi la kuhakiki taarifa za wanachama (wastaafu) ambapo kati ya wastaafu 120,000, elfu 10,000 bado hawajahakikiwa.

“Kwa hiyo tumeeleza kuwa Mfuko umefungua ofisi nchi nzima bara na visiwani na kwa kila mstaafu ambaye bado hajahakiki taarifa zake afike kwenye ofisi ya PSSSF iliyo karibu naye ili atekeleze wajibu huo wa kisheria.” Alifafanua Bi. Chiume.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume baada ya mazungumzo yao ofisini kwa Dkt. Abassi jijini Dar es Salaam leo Juni 15, 2019. Bi. Chiume ambaye alikuwa katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii jijini Dar es Salaam, amehitimisha ziara hiyo kwa kufanya mazungumzo na Dkt. Abassi.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kulia), akizungumza na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, wakati Bi, Chiume alipomtembeleka Dkt. Abassi ofisini kwake jijini Dar es Salaam Juni 15, 2019. 
Dkt. Abbasi (kulia), akimsikiliza mgeni wake. Bi. Eunice Chiume ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Bi. Chiume akiziungumza.
Dkt. Abassi (kulia), akijadiliana jambo na Bi. Eunice Chiume, (katikati), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi ,mara baada ya mazungumzo yao.
Msemaji Mkuu wa serikali ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbasi, (kushoto), akipeana mikono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF bw. Abdul Njaidi.
Dkt. Abbasi akiwa na wageni wake, Bi. Eunice Chiume (katikati) na Bw. Abdul Njaidi kutoka PSSSF.

TUMIENI MASHABIKI KUJIJENGA KIUCHUMI-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amevitaka vilabu vya soka nchini kutumia vema fursa ya kuwa na mashabiki wengi katika kuvifanya viweze kujitegemea kiuchumi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Juni 15, 2019) katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.Ameichangia klabu hiyo sh. milioni 10.

“Natambua kwamba Yanga ni klabu kubwa na kongwe nchini ikiwemo Simba Sport Club ambazo ndizo zina wanachama na mashabiki wasiopungua milioni 20 au zaidi.” 

Hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuvitaka vilabu vya soka nchini kutafuta njia nzuri na endelevu ya kupata mapato ili kuendesha timu zao na kujiimarisha kiuchumi. 

Amesema kwamba, kuimarika kwa vilabu hivyo vyenye ushawishi mkubwa katika soka nchini ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Taifa letu. Waziri Mkuu amesema kufanya vizuri kwa vilabu hivyo kuna uhusiano wa mkubwa na wa moja kwa moja na mafanikio ya timu ya soka ya Taifa.

“Nampongeza kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kwa kazi nzuri aliyoifanya msimu ulioisha na kuiwezesha timu ya Yanga kufanya vizuri ingawa haikupata ubingwa.” Pia, Waziri Mkuu amesema yeye ni mpenzi wa timu zote zinazoshinda na zinazoshindwa. “Kama kuna timu naipenda sana ni siri yangu, hata nyie hamuijui.”

Waziri Mkuu amesema soka ni mchezo maarufu na una wapenzi wengi duniani na hapa nchini na umejipambanua kwa fursa nyingi ikiwemo biashara, uwekezaji na ajira. Amesema Serikali imeendelea kusimamia maendeleo ya michezo, ukiwemo mchezo wa soka ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2015-2020.

“Mhe. Rais Dkt. John Magufuli amekuwa akiungana na wanamichezo kuhamasisha kuendeleza michezo na anatamani kuona mkishinda hadi katika ngazi ya Afrika.”Kadhalika, Waziri Mkuu amezipongeza timu zote za soka zinazofanya vizuri katika ngazi mbalimbali. “Tumeshuhudia Polisi na Namungo FC zikipanda hadi ligi kuu.”

Ameipongeza timu ya Simba kuwa klabu bingwa, Azam kuwa bingwa wa FA, Serengeti boys na Twiga kuliwakilisha Taifa na Taifa Stars inashiriki AFCON – Misri.“Kitendo cha Azam kushinda FA na Simba kushiriki vizuri AFCON sasa kumewezesha timu zetu mbili zaidi, Yanga na KMC kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya CAF.”

Kuhusu harambee ya Kubwa Kuliko, Waziri Mkuu amesema ni mwanzo mzuri kuelekea kwenye mabadiliko yatakayoiwezesha Yanga kujitegemea na kujiendesha bila kutarajia michango kama ilivyo sasa. 

Naye, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa Yanga warudishe hisia na mapenzi kwa timu yao kama ilivyo kwa timu ya Simba, pia wawe na ubunifu wa kutengeneza mfumo mzuri wa mapato.” Siku hizi Yanga imekuwa baridi sana, viongozi wa Yanga lazima mbadishe hali hii.”

Amesema viongozi wa sasa wa klabu ya Yanga chini ya Uwenyekiti wa Dkt. Mshindo Msolla ni wazuri na wanaujua mpira vizuri, hivyo watengeze mifumo mizuri itakayoinufaisha klabu. Wahakikishe wanawekeza kwenye timu ya watoto badala ya kuangalia wachezaji wa kutoka nje ya nchi pekee.

Amesema wasipowekeza kwenye timu ya watoto siku zote watakua mafahari wa kuwa na wachezaji kutoka nchi za nje jambo ambalo ni sawa na kuwafundishia wenzao. “Leo mnajisifia na akina Makambo, Kagere siku ikicheza timu ya Taifa inakuwaje. Oneni fahari ya kuwa na wachezaji wa ndani hivyo waendelezeni Tanzania kuna vijana wana vipaji.” 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dkt. Mosolla amesema yeye pamoja na viongozi wenzake watahakikisha wanajenga umoja ndani ya klabu na kuipeleka jirani na wananchi kwa kufufua matawi na kuwa na wanachama wapya wengi.

Pia watawatumia wachezaji wa zamani katika kupata wanachama wengi na pia watakuwa na wiki ya klabu hiyo ambayo wataitumia kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kurudisha utaratibu wa kwenda mikoani baada ya ligi kuisha kwa ajili ya kutembelea wananchi na kujiongezea wsanachama.

Kuhusu suala la mabadiliko ya katiba amesema watalifanya kwa kufuata utaratibu wa kisheria. Pia Dkt. Msolla amesema uongozi wake utahakikisha unazingatia utawala bora na tayari wametoa matangazo ya nafasi za ajira.

Akizungumza kuhusu hali ya usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu, amesema hadi sasa tayari wamekamilisha kwa asilimia 90 kuwasajili wachezaji wote aliowataka kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera kutoka nje ya nchi na wa ndani ya nchi.

Dkt. Msolla ametumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu awasaidie ili Serikali iweze kuwapunguzia changamoto mbalimbali zinazoikabili klabu hiyo ya Yanga ikiwemo ya madeni.

Awali,Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa wa klabu ya Yanga, Anthony Mavunde, alisema kamati hiyo ilikuwa na wajumbe 27 waliofanikisha kupatikana kwa fedha ambazo zimetumika katika kusajili wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Ajira na Vijana alisema walisambaza kadi kwa ajili ya kukusanya fedha za kuimarisha klabu yao ili iweze kujiendesha na kutatua changamoto za wachezaji.Alisema mbali na kukusanya michango pia kamati yao imependekeza kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ili kutengeneza mfumo mzuri utakaoisaidia timu hiyo kuweza kujiendesha na kuweka mfumo mzuri wa kutumia vifaa vya klabu kukuza uchumi.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga na Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume amewataka wananchi wasitumie vilabu vya soka kama njia ya kutaka kujipatia nafasi za kisiasa. Pia amewataka wanachama wampe ushirikiano Mwenyekiti wao mpya.

Naye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alisema hakuna kipindi kigumu kilichompa tabu katika kuongoza wizara hiyo kama kipindi ambacho timu ya Yanga ilipokuwa katika mgogoro wa kiuongozi.

Pia, Dkt. Mwakyembe alionesha kutoridhishwa na upangwaji wa ratiba za michezo mbalimbali ya ligi kuu msimu uliopita, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wapenzi wa soka nchini kwamba mambo hayo hayatajirudia tena katika msimu ujao.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JUNI 15, 2019
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea jezi ya Yanga, kutoka kwa Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwiguru Nchemba,katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikabidhi mchango wa shilingi milioni 10, kwa Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Msolla katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019. 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019. 
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga na Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mama Fatma Karume, katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019. Katikati ni Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, akizungumza na Wanachama na wapenzi wa Yanga katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wanachama na wapenzi wa Yanga katika hafla ya kuchangia klabu ya Yanga, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Juni 15.2019

MLIMA KILIMANJARO WATUMIKA KATIKA MAPAMBANO VITA DHIDI YA UKIMWI.

0
0
WMU – Arusha

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amepongeza juhudi zinazofanywa na wadau mbalimbali kutangaza utalii na uanzishwaji wa kampeni zinazohamasisha mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi kupitia vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini.

Dkt. Kigwangalla ametoa pongezi hizo leo mkoani Kilimanjaro wakati wa hafla fupi ya kuwaaga Wapanda mlima 32 na Waendesha Baskeli 28 kutoka nchi mbalimbali walioshiriki kupanda mlima Kilimanjaro kupitia Kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019 inayolenga kukusanya fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na kuwasaidia watoto yatima.

Amesema kampeni hiyo itawawezesha wapanda mlima hao kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak) na waendesha Baiskeli kuzunguka mlima Kilimanjaro takribani Kilometa 500 ikiwa ni sehemu ya kushiriki katika changamoto ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika mwitikio dhidi ya VVU na Ukimwi.

“Ugonjwa wa UKIMWI umeendelea kuwa suala la kipaumbele kwa Serikali, athari zake zinagusa sekta zote ikiwemo wizara ninayoiongoza ya Maliasili na Utalii, bila shaka sote tumeona jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kupambana na janga hili” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla

Amesema kuwa pamoja na takwimu kuonesha kupungua kwa maambukizo mapya bado jitihada zaidi zinahitajika ili kuutokomeza ugonjwa huo akifafanua kwamba kila mwananchi ni lazima awe macho kuhakikisha anashiriki kutokomeza ongezeko la maambukizo mapya.

Aidha, amefafanua kuwa programu hiyo imetoa mchango mkubwa katika kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea Mlima Kilimanjaro wakati na baada ya msimu wa Kill Challenge kumalizika kwani wageni kutoka ndani nan je ya Tanzania huwataarifu wenzao pindi wanaporudi makwao ili waweze kuja kupanda mlima Kilimanjaro.

“Huu ni uthibitisho tosha kwamba programu hii siyo tu inachangia kudhibiti Ukimwi bali pia inachangia kukuza uchumi wa nchi yetu kupitia mapato ya utalii ya Mlima Kilimanjaro” Amesema.

Dkt. Kigwangalla ameipongeza kampuni ya GGL na wawekezaji wote ambao wamekua wakijitoa kuchangia ustawi wa jamii ya watanzania akitoa wito kwa makampuni mengine kuendelea kujitolea kuchangia program hiyo pamoja na Mfuko wa hisani wa UKIMWI ulioanzishwa na Serikali wa AIDS Trust Fund (ATF).

Amesema hatua ya GGL kushirikiana na Serikali kupitia TACAIDS ni ya kupigiwa mfano na kwamba inaonesha namna sekta binafsi hususani wafanyabiashara wanavyoendelea kujitokeza kuchangia mwaka hadi mwaka.

Ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa program hiyo takribani shilingi bilioni 13 za Kitanzania zimekusanywa kupitia jitihada hizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amewapongeza wadau wote kwa kuendelea kuchangia kwenye Mfuko wa kupambana na Ukimwi.

Amesema kuwa mujibu wa takwimu zilizopo TACAIDS ugonjwa wa UKIMWI bado ni tatizo nchini kutokana na kuwepo kwa maambukizi mapya ya watu 200 kila siku.

Amesema kazi kubwa inayofanywa na TACAIDS kwa sasa ni kuendeleza kampeni ya kuzuia maambukizi yasitokee ili kuendana na makubaliano ya umoja wa Mataifa ya kufikia maambukizo 0 ifikapo mwaka 2030.

“ Bado tunayo kazi kubwa sana ya kuzuia maambukizi haya, watu 200 kwa siku kuambukizwa VVU ni wengi, tunaendelea kujitahidi na kufanya kazi kubwa ya kuelimisha wananchi na kama ingekua ni ajali ingekua ni watu 200 wanaumia kila siku, tunazungumza hizi takwimu kujikumbusha kwamba Ukimwi bado upo” Amesisitiza Dkt. Maboko.

Ameeleza kuwa kiwango cha maambukizi hayo kinazidi kuongezeka miongoni mwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 akifafanua kwamba kwamba kati ya watu 200 waliopata maambukizi , watu 80 ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24.

“ Kwa ujumla maambukizi mapya yanazidi kushuka isipokuwa kwa vijana yanazidi kupanda juu, sisi kama Tume kwa kushirikiana na wadau tunaliona na tunaendelea kulifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kunusuru kizazi cha vijana ambao ndilo tegemeo la Taifa na viongozi wa baadae” Amesisitiza Dk. Maboko.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI Mhe. Oscar Mukasa amesema kuwa kazi yao kama Kamati ni kushirikiana na wadau wote katika masuala ya Sera, Sheria na usimamizi na kufafanua kuwa mfuko wa Ukimwi tangu kuanzishwa kwake umekuwa na changamoto ya kupata fedha akiupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kuendelea kuchangia fedha katika mfuko huo.

Amesema Bunge itaendelea kuishauri Serikali kwa lengo la kupata vyanzo vingine vya mapato vya uhakika ili Serikali iweze kushirikiana na wadau wa ndani wa Sekta binafsi kwa lengo la kujitegemea.

Amesema tukio hilo la wapanda mlima kuchangisha fedha linapeleka ujumbe kwa jamii kwamba kazi ya kupambana na UKIMWI bado ni kubwa na endelevu hivyo jamii yote inapswa kushiriki kikamilifu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwaongoza wapanda  mlima Kilimanjaro 32 walioanza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa siku 7 kupitia kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019. Kampeni hiyo ina  lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, leo mkoani Kilimanjaro.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na waendesha baiskeli wanaopanda mlima Kilimanjaro kupitia kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019 yenye lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, leo kwenye lango la Machame wilayani Hai , Kilimanjaro.
 Waendesha baiskeli wakijiandaa kupanda mlima Kilimanjaro kuelekea kilele cha Uhuru kiupitia Kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge mwaka 2019 yenye lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, leo mkoani Kilimanjaro.PICHA/ WIZARA YA MALIASILI NA UTALII.

 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.  Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Bendera ya Taifa kiongozi wa timu ya waendesha baiskeli 28, Bw. Paul Pulson wakati wa kuwaaga waendesha baiskeli hao kutoka nchi mbalimbali kupitia kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019 yenye lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na kuchangisha kwa ajili ya watoto yatima na wanaoishi na VVU, leo mkoani Kilimanjaro.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Bendera ya Taifa kiongozi wa timu ya wapanda mlima Kilimanjaro 32 Bw. Moses Rusasa wakati wa kuwaaga wapanda mlima hao kutoka nchi mbalimbali kupitia kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge 2019 yenye lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, leo mkoani Kilimanjaro.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Mhe. Anna Mgwira wakati wa kuwaaga  waendesha baiskeli na  wapanda mlima na waendesha baiskeli 60 wanaoshiriki  kampeni ya Geita Gold Mining Kilimanjaro Challenge  2019 yenye lengo la kuendeleza mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi, leo mkoani Kilimanjaro.

UZINDUZI WA KITINI CHA MABARAZA YA WATOTO TANZANIA

Tume ya Madini ipo teyari kukusanya bilioni 475

0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula akisisitiza ulipaji wa tozo za serikali kwa wachimbaji wadogo wakati wa mkutano wake na wachimbaji hao wa madini uliofanyika kwenye machimbo ya Shaba Mbesa Wilayani Tunduru
1. Sehemu ya Wanunuzi wa Madini ya Vito wilayani Tunduru wakiwa kwenye kikao na viongozi wa juu wa tume ya madini wilayani humo. Mwenye kofia ni Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma.
 Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa tatu kushoto akiwa kwenye mgodi wa kampuni ya TANCOAL unaozalisha makaa ya mawe, kukagua shuguli za uzalishaji na ulipaji wa maduhuli ya serikali. Wa tatu kushoto ni Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma na wa kwanza kushoto ni Afisa Madini Mkazi mkoa wa Ruvuma Jumanne Mohamed.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa tatu kushoto akiongea na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Happiness Seneda wakati wa kikao chake mara baada ya kumtembelea ofisi kwake mjini Iringa. Kutoka kushoto ni Mhandisi kutoka tume ya Madini Fadhili Kitivai, Afisa Madini Mkazi Njombe na Iringa Wilfred Machumu na wakwanza kulia ni Severine Haule mkaguzi wa Madini Iringa.



Na Issa Mtuwa “WM” – Tunduru, Mbinga na Iringa


Tume ya madini imesema ipo teyari kukusanya bilioni 475 katika mwaka wa fedha 2019/20 kama walivyopangiwa na serikali na kufikia malengo ya ukusanyaji kama ilivyofikia mwaka 2018/2019 ya kukusanya billion 310 ambapo malengo hayo ilivuka. 

Akiongea kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Tunduru, Songea na Mbinga na Iringa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amesema hayo wakati wa vikao vyake na viongozi wa mikoa, wilaya, maafisa madini wa kaazi, viongozi na wachimbaji wadogo na wanunuzi wa madini kwenye maeneo yao akisisitiza kila mmojja kwa nafasi yake kuwajibika katika suala la usimamizi na ulipaji wa maduhuli ya serikali ili wafikie lengo hilo. 

Amesema serikali imeipangia Wizara ya Madini kukusanya jumla ya Tshs. bilioni 475 na wakusanyaji wa fedha hizo ni Tume ya madini na ili ifikie lengo la kukusanya kiwango hicho lazima wajipange kwa kila mdau anae husika kwa namna moja au nyinge awajibike kutimiza wajibu wake. 

“Ndugu zangu mkisoma jukumu namba moja la Tume ya madini ni kukusanya maduhuli ya serikali, pili kutatua migogoro ambayo ikiachwa inaathiri ukusanyaji wa maduhuli, pamoja na majukumu mengine lakini haya mawili ndio hasa yanayotufanya tuzunguke nchi nzima kuhimiza haya masuala. 

Tume tumesema, ili tufikie haya malengo kila ofisi ya Afisa Madini mkazi iseme imejiwekea malengo ya kukusanya kiasi gani na kila baada ya kipindi gani atakuwa amekusanya kiasi gani, na lazima kila ofisi ifikie hayo malengo. Pamoja na ofisi zetu ofisi zetu kusimamia makusanyo naombeni viongozi wa mikoa na wilaya wasaidieni watu wetu wanapo hitaji msaada wenu kwani tunajenga taifa moja. amesema Prof. Kikula. 

Akisisitizia hoja hiyo mwenyekiti amesema haya yote yanaweza kufikiwa kirahisi kwa kuunganisha nguvu zetu sote na kuzingatia mambo matatu, uwajibikaji, uadilifu hasa kuepuka rushwa na kufuata sheria. Ameongeza kuwa endapo kila mdau kwa nafasi yake atazingatia haya itakuwa rahisi kufikia lengo walilopewa. 

Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma ameongeza kuwa jambo lingine la msingi ni lazima kila ofisi ya tume ya madini mikoa yote lazima iwe na mpango kazi unao onesha utaratibu wa utekelezaji wa majukumu kipindi kwa kipindi ili isaidie kujifanyia tathmini kuona ulikotoka, ulipo na unako elekea na muda uliobaki nao katika kufanikisha malengo ya mwaka 

Amesema bila kuwa na mpango kazi inaweza kuwa ngumu kufikia malengo yoyote hata haya ya ukusanyaji wa maduhuli, kwa hiyo amewasisitiza watumishi wa tume kuwa na mpango kazi ambao utawaonyesha kipindi hadi kipindi atakusanya kiasi gani cha maduhuli na kwamba hicho kinaweza kuwa kigezo kikubwa cha upimaji wa utendaji kazi kwa Maafisa Madini wakazi wa Mikoa.

SADC KUTENGENEZA AJIRA ZAIDI YA 5000 KUINGIZA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 10

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amewataka wamiliki na wafanyabiashara wa Hoteli Jijini Dar es salaam kutumia fursa ya kibiashara itakayotokana na ujio wa wageni takribani 1000 watakaoshiriki katika mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuanzia mwezi August 2019.

Waziri Prof Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na wamiliki na wafanyabiashara wa hoteli na kuongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itafanya kazi kwa ukaribu na wadau hao wa Hoteli na kuwataka kutoa huduma bora,bidi,weledi na kwa uzalendo usiotiliwa mashaka ili waweze kunufaika na uwepo wa ugeni huo mkubwa wa SADC.

“Ninyi ni watu muhimu sana katika ugeni huu wa SADC,tushirikiane kuufanya mkutano huu kuwa wa mafanikio makubwa kwa ukarimu na uzalendo wetu na hivyo kutufanya pia kuingiza kipato katika biashara zetu kwa kuwa tukifanya vizuri kila watakapokuwa wanakuja Tanzania kwa mikutano mingine ya mawaziri watafikia katika hoteli zetu kutokana na ukweli kuwa tutakuwa na mfululizo wa mikutano ya SADC kuanzia August 2019 hadi August 2020 Tanzania itakapokoma kuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo”

Ameongeza kuwa ataendelea kukutana na wadau mbalimbali pamoja na wafanyabiashara wa Sekta binafsi ili kuhakikisha fursa ya kufanyika kwa mkutano wa SADC hapa nchini inawanufaisha pia wadau mbalimbali wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara.

Katika Mkutano huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba John Kabudi ameongozana pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo kwa upande wake amesema kutokana na Mkutano huo wa SADC serikali inatarajia kuingiza zaidi ya shilingi bilioni kumi pamoja na kutengeneza ajira zaidi ya elfu tano na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo.

Pia amewataka wamiliki na wafanyabiashara hao wa hoteli kuzingatia muongozo wa serikali uliotolewa na Gavana wa benki kuu ya Tanzania kuhusiana na suala la ubadilishaji wa fedha za kigeni kwa kuwataka kuwaelekeza wageni kubadilishia fedha zao benki na pia katika hoteli ambazo zimeidhinishwa kubadilisha fedha za kigeni.

Wadudu waharibifu wakiwemo funza wavamia mashamba ya wakulima Kwimba

0
0
Wakulima katika Kata Fukalo Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, wamemweleza Mkuu wa Wilaya hiyo, Senyi Ngaga (katikati) kwamba wako hatarini kukumbwa na baa la njaa baada ya wadudu waharibifu wakiwemo funza na panya kuvamia mazao yao shambani na hivyo kuomba Serikali iwasaidie kupambana na wadudu hao.
Tazama vidio hapa chini

WIZARA YA AFYA YATOA TAHADHARI KWA UMMA KUHUSU TISHIO LA UGONJWA WA EBOLA

0
0
Kituo cha kuwatenga wahisiwa wa magonjwa ya mlipuko ikiwamo ugonjwa wa Ebola, kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.


*Waziri Ummy Mwalimu atoa tamko rasmi,aelezea hatua ambazo Serikali inachukua 

*Ataja mikoa ambayo iko hatarini zaidi na tishio la ugonjwa wa Ebola nchini

*Aelezea namna ambavyo wamesambaza vifaa tiba nchini,utolewaji wa mafunzo ya kukabiliana na Ebola


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetoa tahadhari kwa umma kuhusu uwepo wa tishio la mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini unaoendelea kuripotiwa nchini DRC Congo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani ni kwamba hadi Juni 14 mwaka huu tayari imeripotiwa watu 2108 wameugua ugonjwa wa Ebola na kati ya hao  vifo vilivyotokea ni  1,411 na kwamba uwiano wa wagonjwa na vifo katika kila wagonjwa 100 watu 67 wamefariki.

Akizungumza leo Juni 15,2019 akiwa Mkoa wa Mwanza na taarifa kutuma kwa vyombo vya habari nchini, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kutokana na tishio la uwepo wa ugonjwa huo tayari Wizara ya afya imechukua hatua kadhaa ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola.

"Ugonjwa huu pia uneripotiwa kutokea katika nchi jirani ya Uganda katika Wilaya ya Kasese iliyopo upande mwa Kusini Magharibi mwa Uganda.Kwa upa nde wa  Tanzania imepaka na Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ambapo Juni 11,2019 mtoto mwe nye umri wa miaka mitano amethibitika kuugua ugonjwa huo na kwa bahati mbaya amefariki dunia na katika familia hiyo ndugu wengine wawili wamefariki katika nchi ya Uganda," amesema.

Waziri Mwalimu amesema kutokana na tishio la ugonjwa huo nchini Uganda utaona mikoa ya Kanda Ziwa na hasa Kagera,Kigoma na Mwanza iko hatarini zaidi na hivyo Wizara ya Afya imechukua tahadhari ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola nchini.

"Kwangu naona ugonjwa huu unaua watu wengi zaidi na kwa haraka.Sio kwamba Dengue na Kipindupindu haviuwi lakini Ebola kasi yake ya kuua ni kubwa," amesema Waziri Mwalimu wakati anatoa tamko la tahadhari kuhusu tishio la ugonjwa huo.

Akizungumzia zaidi kuhusu Ebola amesema dalili kuu za ugonjwa ni homa kali inayoambatana na kutokwa na damu katika matundu ya mwili yaani pua,njia ya haja kubwa na ndogo,mdomoni,masikioni na machoni hali inayosababisha kifo kwa muda mfupi.

Waziri Mwalim amesema kipindi cha kuonekana kwa dalil za ugonjwa ni kati ya siku mbili hadi 21 baada ya kupata maambukizi na kwamba ugonjwa huo unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka kwa mtu mmoja had mwingine iwapo mtu atakuwa karibu na mgonjwa na kugusana na mate ,damu,mkojo,machozi,kamasi,majimaji mengine ya mwilini ikiwa pamoja na jasho au kugumsa mtu aliyekufa kwa ebola.

 Pia amesema ugonjwa huo unaweza kuenezwa iwapo mtu atagusa nguo au mashuka ya mgonjwa ya ebola na kueleza kuwa tangu ugonjwa wa Ebola ulipotaarifa kuwapo nchini  DRC Congo ,Wizara imechukua na inaendelea kuchukua hatua katika kukabiliana na tishio la ugonjwa huo nchini kwa kuchukua hatua mbalimbali.

Ametaja baadhi ya hatua inazochukua ni kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huo kupitia kwa makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania Bara.Aidha taarifa hiyo imejumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa(ainisho la ugonjwa)" Fact sheet" ya ugonjwa.

Amesema Dodoso la kujima utayari wa mikoa na wilaya kukubaliana na ugonjwa huu ,muongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli na vipeperushi vinavyoelezea ugonjwa huu.

Pia kuimarisha utaratibu na ufuatiliaji wa ugonjwa huo kupitia kwa wataalam wa afya katika mikoa,wilaya na maeneo ya mipakani na kuimarisha uchunguzi wa wageni wanaoingia nchini kupitia mipaka yetu,ikiwemo kwa kipima joto, 

Ameongeza wamefanya tathimini ya kupima utayari wa mikoa na halmashauri katika maeneo iliyoanishwa kuwa hatari zaidi ya kupata ugonjwa Ebola kutoka nchi jirani.Maeneo yanayotakiwa kufanyiwa kazi yameanishwa na jitihada za kuyaondoa mapungufu hayo zinaendelea.

Waziri Mwalim amesema tayari wamepeleka jumla ya seti 3500 za vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa afya kupitia ofisi za kanda za Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) na kutokana na tishio la sasa wataongeza seti 4000 na kuzipeleka karibu zaidi na wananchi ikiwa ni pamoja na kwenye hospitali zote za mikoa na wilaya kwa ajili ya kujiandaa.Aidha idadi hiyo itaongezeka kutokana na uhitaji .

"Tumeandaa kitini chenye maelezo muhimu ya kukabiliana na Ebola ambapo nakala tete(softy Copy)zimetumwa kwa waganga wakuu wa mikoa na pia tumeendelea kudurufu nakala zaidi ili kuzisambaza kwenye mikoa,wilaya na vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

" Pia tumeendelea kushirikiana na wadau katika kuimarisha sehemu za kuwatenga na kuwahudumia wagonjwa wa Ebola katika  Hospitali ya Temeke,Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Ilemela Mwanza ,hospitali ya Rufaa ya Mawezi kilimanjaro na utaratibu huo unafanyika kwenye mikoa mingine,"amesema.

Amefafanua pia  wametoa mafunzo namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa watumishi zaidi ya 460 wa sekta ya afya,na 264 kutoka ngazi ya jamii(viongozi wa dini, wanahabari,bodaboda pamoja na watendaji wa vijiji).katika mikoa iliyo na hatari kubwa zaidi ya maambukizi ya ebola hapa nchini.

Amesisitiza mpango huo ni endelevu na idadi itazidi kuongezeka na tayari wameimarisha utambuzi wa ugonjwa Ebola kwa kujenga uwezo hapa nchini hususani katika Maabara Kuu ya Taifa jijini Dar es Salaam ,Hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya na Kilimanjaro Clinical Reseach Institute(KCRI) kilichopo Moshi.

Pia amesema usafirishaji wa sampuli kutoka maeneo mbalimbali kwenda kwenye maabara hizo umeimarishwa. Aidha kwa kushirikiana na wadau kutakuwa na maabara zinazohamishika.

"Tumeendelea kutoa taarifa na elimu kwa umma kuhusu kujikinga na maambukizi ya Ebola nchini kupitia vyombo vya habari ikiwa pamoja na kutambua dalili za ugonjwa huo ili endapo ugonjwa utatokea uweze kutolewa taarifa mapema.Pia Wizara inaimarisha ushirikishwaji wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini na inapobidi ili kuongeza tija ya kukabiliana na tishio hili," amesema Mwalimu.

Wakati huo huo amesema Wizara inatoa maagizo kwa mikoa na halmashauri nchini kwa kuhakikisha zinaimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa ya mlipuko , na kutoa taarifa za wiki kwa wakati na zile za kila siku pale inapobidi.

Pia imeagiza kuwepo na utaratibu mzuri wa ushirikishwaji wa wadaumbalimbalo wa mikoa na halmashauri na kuwepo mikakati thabiti ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko katika maeneo hayo.

Amesema ili kujikinga na Ebola ni vema kila mmoja wetu akaepuka kugusa damu,mkojo,jasho ,kinyesi,machozi na maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.

"Epuka kushughulikia maiti ya mtu aliyefariki kwa ugonjwa ebola : Aidha tunatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa kituo cha kutolea huduma za afya kwa ushauri .Epuka mila na desturi zinazoweza kuchelewesha mgonjwa kupatiwa huduma muhimu za afya na kupelekea kueneza ugonjwa wa ebola.Pia kuzingatia kanuni za afya na usafi wa mwili

"Kutoa taarifa mapema kwa uongozi wa Serikali na kwa wahudumu wa afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola.Kuwahi katika vituo vya huduma za afya pale unapoona dalili za ugonjwa huo ," amesema.

Waziri Mwalimu ameeleza kuwa ni muhimu kuhusisha viongozi wa kata ,mitaa ,vijiji na vitongoji katika kubaini na kutoa taarifa katika vyombo husika pindi abapoonekana kuna mtu ameingia nchini bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria.

"Kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Wizara na kuepuka kutengeneza taarifa zisizo rasmi na kuzipeleka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu ugonjwa .Wizara ya Afya inatoa tahadhari kwa umma kuhusu tishio la ugonjwa wa Ebola ambalo unaendelea kuripotiwa katika nchi ya DRC Congo," amesema Waziri Mwalimu
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images