Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Rais Tshisekedi amaliza Ziara ya Kitaifa ya siku 2 hapa nchini Tanzania

0
0
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mhe. Felix Antoine Tshisekedi amemaliza Ziara ya Kitaifa ya siku 2 aliyoifanya hapa nchini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Mhe. Tshisekedi ameagwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuelekea nchini Burundi. 

Mapema leo asubuhi Mhe. Rais Tshisekedi ametembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge Railway) katika eneo la Vingunguti Jijini Dar es Salaam na baadaye akatembelea Bandari ya Dar es Salaam ambayo hutumika kupitisha mizigo ya DRC. 

Akiwa Ikulu Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Tshisekedi amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli na baadaye viongozi hao wamezungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari. 

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Tshisekedi kwa kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na kwa dhamira yake ya kukuza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya DRC na Tanzania hususani katika uchumi. 

Mhe. Rais Magufuli amesema kiwango cha biashara kinachofanywa kati ya Tanzania na DRC ni kidogo ikilinganishwa na ukubwa wa uhusiano na fursa zilizopo kati ya nchi hizo, ambapo katika mwaka uliopita biashara kati ya Tanzania na DRC ilikuwa na thamani ya shilingi Bilioni 305.375, wafanyabiashara wa DRC walikuwa wamewekeza nchini Tanzania miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 13.144 na kukiwa na Watanzania wachache ambao wameweka nchini DRC. 

Amefafanua kuwa japo kuwa sekta ya usafirishaji inaridhisha kidogo kwa DRC kuongeza mizigo inayopita Bandari ya Dar es Salaam kutoka tani Milioni 1.176 ya mwaka 2017 hadi kufikia tani Milioni 1.78 ya mwaka 2018, kuna haja ya kuchukua hatua madhubuti zaidi za kukuza biashara na uwekezaji ikiwemo kuondoa vikwazo, kutumia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo madini, uvuvi, kilimo, ujenzi wa viwanda na kulitumia ipasavyo soko la nchi hizo lenye jumla ya watu Milioni 140. 

Kwa upande wa Tanzania, Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kujenga reli ya kati (SGR), kupanua Bandari ya Dar es Salaam, kuanzisha huduma za pamoja za bandari kwa saa 24 (siku zote 7 za wiki) na kuimarisha miundombinu ya barabara katika njia 8 za kuingia na kutoka DRC, Tanzania imeongeza muda wa kusubiri bandarini kutoka siku 24 hadi 30 kwa mizigo ya DRC, imeondoa katazo la ufunguaji makontena na kufuta tozo ya kusindikiza mizigo hadi mpakani mwa Tanzania na DRC. 

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania itaikarabati meli ya MV. Liemba inayotoa huduma kati ya Tanzania (Kigoma) na DRC, itajenga meli mpya mbili ambapo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na mizigo tani 400 na ya pili itakuwa meli ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 2,000 na ameafiki mapendekezo ya Mhe. Rais Tshisekedi ya reli ya kati ya Tanzania kujengwa kutoka Isaka – Rusumo – Kigali hadi Mashariki ya Kongo ili kufikisha mizigo moja kwa moja nchini DRC. 

Mhe. Rais Magufuli amewataka Mawaziri na Wataalamu wa Tanzania na wenzao wa DRC (watakaoteuliwa) ndani ya mwaka huu, kuitisha kikao cha Kamati ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission – JPC) ambacho hakijawahi kufanyika tangu mwaka 2002 ili kujadili na kurejesha maeneo muhimu ya ushirikiano ikiwemo ushirikiano katika usafiri wa anga kati ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) na Shirika la Ndege la Congo (Congo Airways). 

Mhe. Rais Magufuli amemtakia heri Mhe. Rais Tshisekedi katika uongozi wake na amemshauri kusimama kidete kutatua matatizo ya wananchi wa DRC huku akisisitiza kuwa kwa utajiri wa DRC, uchumi wa nchi hiyo haupaswi kukua kwa kiwango kidogo cha asilimia 4. 

Kwa upande wake, Mhe. Rais Tshisekedi amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumwalika kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na amebainisha kuwa lengo la ziara yake ni kuimarisha na kukuza zaidi udugu, urafiki na uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na DRC. 

Mhe. Tshisekedi amesema katika mazungumzo yake na Mhe. Rais Magufuli wamekubaliana kuwa bila amani jitihada za maendeleo katika eneo lote la maziwa makuu hazitafanikiwa, hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha kunakuwa na amani ya kudumu pamoja na kutumia vizuri fursa mbalimbali za kukuza uchumi ukiwemo ukanda wa ziwa Tanganyika wenye urefu wa kilometa 554. 

Amesema ana matumaini kuwa JPC itakayofanyika itatatua changamoto zote za kukuza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na DRC na ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu na Mhe. Rais Magufuli. 

Pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa ahadi yake ya kuunga mkono ombi la DRC kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Rais Tshisekedi ameahidi kuhudhuria Mkutano wa 39 Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu hapa Tanzania na amebainisha kuwa anaamini kuwa SADC ni jumuiya yenye fursa na manufaa makubwa ya kiuchumi. 


Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Dar es Salaam 
14 Juni, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo
Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa afrika Mashariki Mhe. Faraji Kasidi Mnyepe baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wakisumbiri ili kumuaga mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Profesa palagamaba Kabudi baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo anayeagana na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiagana kwa furaha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia 54 ya Congo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam baada ya kuhitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili leo Juni
14, 2019 
PICHA NA IKULU


TPSF KUANZISHA MABARAZA YA UJUZI YA KISEKTA KUKUZA UJUZI NCHINI..

0
0
Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi tanzania (tpsf) godfrey simbeye amesema kufuatia nchi kukabiliwa na changamoto ya vijana kukosa ajira kwasababu ya kukosa sifa kiushindani hivi sasa kunaanzishwa mabaraza ya ujuzi ya kisekta yenye lengo la kuhakikisha suala la ujuzi linakuzwa kiufasaha kuanzia elimu ya vyuoni pamoja na kuwezeshwa kwa vijana wabunifu nchini.

Simbeye amesema hayo mjini Morogoro wakati warsha ya kuandaa wajumbe wa mabaraza ya kisekta yenye nia ya kuwafanya kujua majukumu yao.Amesema kuwa Tpsf ni moja ya watekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kukuza ujuzi, na Tpsf ndio inayohusika na kipengele cha kuunda mabaraza ya ujuzi katika sekta sita ambazo ni muhimu kiuchumi ikiwemo Kilimo biashara, Utalii, Nishati, Ujenzi, Tehama, na Usafirishaji na zote zitakuwa na mabaraza ya ujuzi.

“mabaraza yatatakiwa kwenda na spidi ya teknolojia na mabadiliko yaliyobadilika kwenye viwanda vinavyoendelea na vinavyoanzishwa nchini, mabaraza yanatakiwa kutafanya tafiti kwa lengo la kuwafikia vijana wenye vumbuzi mbalimbali” alisema Simbeye.
Pia amesema katika mkakati huo wa kukuza ujuzi Tanzania TPSF lilidhamilia kuunda baraza la ujuzi la taifa, na nchi kama Tanzania imechukua hatua nyingine tofauti na imekuwa nchi ya pili kwa bara la Afrika ambayo imekuwa na mfumo huo wa mabaraza.
Juni 22 mwaka huu waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako anatarajiwa kuzindua mabaraza ya kisekta jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa taasisi ya sekta binafsi tanzania (tpsf) godfrey simbeye wapili kutoka kulia kwa walioketi pamoja na wadau wakati warsha ya kuandaa wajumbe wa mabaraza ya kisekta yenye nia ya kuwafanya kujua majuku

DC ASIA ABDALAH - RAIS DKT MAGUFULI AMETEKELEZA MIRADI MINGI YA MAJI AMBAYO HAIJAWAHI KUTEKELEZWA KILOLO

0
0
Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Asia Abdalah amesema kuwa toka wilaya ya Kilolo imeanzishwa na toka nchi ipate uhuru hakuna kipindi ambacho wilaya hiyo imekuwa na miradi mingi ya maji kama kipindi hiki kinachoongozwa na Rais Dkt John Magufuli, mwandishi Francis Godwin anaripoti kutoka Kilolo.

Akizungumza leo baada ya kukagua mradi wa tanki la maji kwa ajili ya kutatua kero ya maji mji wa Ilula ,mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa ujenzi wa mradi huo mkubwa wa maji utasaidia kumaliza kero ya maji ambayo wamekuwa wakiipata wananchi wa mji wa Ilula .

" Huu ni mradi mkubwa wa maji ambao utawanufaisha wananchi wa kata ya Ilula na kata nyingine za ukanda huu wa Ilula ambao walikuwa wakipata tabu ya maji " alisema Asia

Kuwa ujenzi wa mradi huo wa maji Ilula unaendelea vizuri na kuwa wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi kwa ajili ya kukagua mradi huo alikuwa ametoa maelekezo ambayo yamefanyiwa kazi na sasa mradi unaendelea vizuri .

Alisema kuwa mbali ya mradi huo utakaowanufaisha wakazi wa Ilula wilaya ya Kilolo ina miradi mingine saba na kufanya jumla kuwa na miradi mikubwa nane ya maji ambayo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa wilaya ya Kilolo.

Pia alisema pamoja na miradi hiyo kuna miradi mingine mitatu mikubwa ya maji iko mbioni kujenga hivyo iwapo miradi hiyo itakamilika uwezekano wa wananchi wa wilaya hiyo kukabiliwa na changamoto ya maji itabaki kuwa historia .

Mkuu huyo alisema kuwa mradi huo ambao unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 5 ambazo ni kodi za watanzania umefikia asilimia 45 kukamilika na kuwa ujenzi wa tanki pekee umefikia zaidi ya asilimia 90 .

Alisema kuwa mradi huo umeendeshwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ulitengewa bilioni 5 na awamu ya pili utatumia kiasi cha Tsh bilioni 4 hadi kukamilika kwake .

Akizungumzia kuhusu utunzaji wa mradi huo na miradi mingine ya maji wilayani Kilolo mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kuifanya miradi hiyo kuwa endelevu na kuwa elimu ya utunzaji mazingira imeendelea kutolewa na wilaya hiyo imezidi kupata tuzo mbali mbali za utunzaji mazingira.










MUHIMBILI YAWASHUKURU WACHANGIA DAMU- ASANTENI SANA

0
0
Muhimbili yawashukuru wachangia damu

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewaita na kuwashukuru watu waonajitolea kuchangia damu na mazao ya damu mara kwa mara ambayo imekuwa ikitumika kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji.

MNH imewaita wachangia damu na kuwashukuru ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani ambayo hufanyika Juni 14, kila mwaka.

Akizungumza leo na wachangia damu kabla ya kuwakabidhi vyeti vya kutambua mchango wao, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dkt. Praxeda Ogweyo amewashukuru kwa kujitolea damu mara kwa mara kila wanapohitajika.

“Mwenyezi Mungu awabariki sana. Pia, tunaomba muwe mabalozi wetu kwa jamii nzima ili nao waige mfano wenu wa kujitolea damu ambayo inatumika kuokoa maisha ya watu wengine. Pia, napenda kuwashukuru wafanyakazi wa kitengo cha damu kwa kutoa huduma bila kuchoka. Bila jitihada zenu, tusingeweza kuwepo hapa siku hii muhimu,” amesema Dkt. Ogweyo.

Dkt. Ogweyo amesema mahitaji ya damu ni makubwa na kwamba uhitaji wa damu MNH ni chupa 100 hadi 120 kwa siku, huku ukusanyaji wa damu kwa siku ukiwa ni chupa 70 hadi 100.

Kutokana na mahatiji makubwa ya damu na mazao ya damu, hospitali imewaomba Watanzania kujenga mazoea ya kuchangia damu na mazao ya damu ili kuboresha benki za damu na mazao ya damu.

“Watanzania wasisubiri kuuguliwa na ndugu ndio waje MNH kuchangia damu na mazao ya damu wanatakiwa kuwa na tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili itumike kuwatibu wagonjwa wakiwamo ndugu wa wagonjwa,” amesema Dkt. Ogweyo wakati akiwashukuru wachangia damu.

Amesema faida ya kuchangia damu mara kwa mara ni mchangiaji kupatiwa damu ambayo itamwezesha kupata damu katika hospitali nchini endapo amepata dharura ya uhutaji pamoja na kujua magrupu ya damu.

Mkurugenzi amesema makundi yenye uhitaji mkubwa wa damu ni wagonjwa wa saratani, watu wanaopata ajali, watoto, kina mama wajawazito na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Praxeda Ogweyo akimkabidhi Bw. Yusuph Charles cheti cha kutambua uchangiaji wa damu na mazao ya damu mara kwa mara kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji MNH. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa MNH, Bi. Martha Edward na Mtaalam wa Maabara wa MNH, Bw. John Bigambalaye.
Baadhi ya wachangiaji damu kutoka maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam wakiwa katika tafrija fupi ya kuwashukuru kutokana na mchango wao mkubwa wa kuimarisha benki ya damu na mazao ya damu MNH. 
 Bi. Khalida Ismail mkazi wa Dar es Salaam akikabidhiwa cheti cha kutambua mchango wake katika uchangiaji damu MNH na Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi, Dkt. Ogweyo.
Wachangiaji damu kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja. 
Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi wa MNH, Dkt. Ogweyo akiwa katika picha ya pamoja na wachangiaji damu kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. 

Serikali kuongeza idadi vituo vya uchangiaji damu salama

0
0
Na.WAMJW, Mwanza

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetenga Sh. bilioni tano katika mwaka wa fedha 2019/20 zitakazotumika kujenga vituo vidogo vya uchangiaji damu salama katika mikoa 12 nchini.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipozungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.

Sambamba na hilo, Waziri Ummy amezindua mashine mpya ‘full automation’ za kupima maambukizi katika damu na za kupima makundi ya damu ambapo mashine 24 zimesimikwa kwenye vituo vya kanda sita ikiwamo Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kilimanjaro, Mtwara na Mbeya.

Amesema kila kituo kimesimikwa mashine nne ikiwa mbili ni za kupima magonjwa yanayoambukizwa kupitia damu na mbili ni za kupima makundi ya damu.

Amesema hatua hiyo imelenga kuimarisha huduma ya uchangiaji damu salama pamoja na kuwezesha kusogeza karibu zaidi huduma za kuongezewa damu salama wagonjwa wenye uhitaji.“Hadi sasa kuna vituo vidogo vya damu salama nane ambavyo vimeanzishwa Mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa, Kigoma, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Mara.

“Katika mwaka wa fedha 2019/20, tunategemea kujenga vituo vya damu salama katika mikoa 12, imetengwa Sh. bilioni tano, hivi karibuni ujenzi utaanza,” amesema.Amesema kadri huduma za matibabu ya kibingwa zinavyoboreshwa ikiwamo ya moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, upandikizaji figo na upasuaji mwengine Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mloganzila, zimepanua wigo wa mahitaji ya upatikanaji wa damu salama.

“Jitihada zinafanyika ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa damu salama, kauli mbiu ya mwaka huu inasema ‘Damu Salama kwa Wote’ ni kwa sababu mkutano mkuu wa WHO mwaka huu ulihusu afya kwa wote.“Tunataka kumfikia kila mtanzania mwenye mahitaji ya damu salama popote alipo tuhakikishe anapata damu salama bila kikwazo chochote.

“WHO inakadiria katika kila idadi ya watu 1000 zipatikane chupa 10 za damu, Watanzania tunakadiriwa tupo milioni 55 tunapaswa kupata asilimia moja ya idadi hiyo, hivyo chupa 550,000 zinahitajika kila mwaka kutosheleza mahitaji,” amesema.Akitoa ulinganisho amesema mwaka 2016 zilikusanywa chupa 196,000, mwaka 2017 chupa 233,000 na 2018 idadi imeongezeka kufikia chupa 307,000.

“Kumekuwa na ongezeko la ukusanyaji damu, katika chupa 10 zinazohitajika kupatikana angalau tunapata chupa sita, hivyo nawasihi watanzania wote kujenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara ili tuweze kupata inayotosheleza,” amesema.

Aidha, amewataka waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha wanatekeleza agizo alilowapa la kuandaa kambi za wazi kwa ajili ya uchangiaji damu angalau mara tatu kila mwaka na watenge fedha katika bajeti zao kuwezesha ukusanyaji damu salama.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Steven Lalika amesema walipewa lengo la kukusanya chupa 2000, katika wiki ya uhamasishaji wamefanikiwa kukusanya chupa 3705 kufikia Juni 13 na kwamba lengo la mkoa walikusudia kukusanya chupa 4000.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa kutoka Wizara ya Afya wakiongea na moja kati ya watu waliojitokeza kuchangia damu, katika Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza, viwanja vya Furahisha.



 opo la watu waliojitokeza kushuhudia Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani yaliyofanyika  kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha, yaliyofunguliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.


 Baadhi ya picha za Kikundi cha Wasanii wa filamu Tanzania wakionesha igizo kuhusu uhamasishaji kwa jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu, tukio limefanyika kitaifa jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha.

Meya wa jiji la Dar Mwita akutana na Meya wa Zanzibar

0
0
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mstahiki Meya wa jiji la Zanzibar Khatibu A Khatibu ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana kuhusiana na namna ya uendeshaji wa majiji.

Aidha mameya hao wawili kwa pamoja wamebadilishana uzoefu wakuendesha majiji hayo hususani katika suala la ukusanyaji wa mapato, kutangaza utalii ikiwa ndio sehemu kubwa ya upatikanaji wa mapato.

Meya Mwita amesema kuwa ujio huo ni mahususi kwa wananchi kutambua kwamba viongozi waliochaguliwa wanashirikiana vizuri katika kuwaletea maendeleo.

Aidha Meya Mwita amemshauri Meya wa Zanzibar Khatibu, kwamba katika kuleta maendeleo jijini humo ,anapaswa kushirikiana vizuri na wananchi,madiwani bila kujali itikadi za vyama vyao kwani kwakufanya hivyo kutawezesha kuleta maendeleo makubwa.

Mbali na hivyo pia amemshauri kuwekeza nguvu kubwa katika sekta ya utalii kwakuwa ndio chanzo kikubwa cha mapato na kwamba Zanzibar ndio kitovu kikubwa cha utalii Tanzania Visiwani.

Kwaupande wake Meya Khatibu amemshukuru Meya Mwita kwamapokezi mazuri nakusema kuwa amejifunza uzoefu mkubwa kupitia kwakwe na kwamba ziara hiyo itamsaidia kuendesha jiji la Zanzibar.

Amesema kuwa awali Zanzibar haikuwa kama jiji, lakini kuanzia Julai mosi mwaka huu litatambulika na kwamba kwanafasi yake ataliwezesha jiji hilo kufika mbali ikiwa ni pamoja na kufahamika kimataifa.

Ameongeza kuwa ujio huo umetokana na sheria iliyounda jiji la Zanzibar inatokana na jiji la Dar es Salaam na hivyo hana budi kuja kuchukua uzoefu na mikakati ambayo inatumika kuendesha jiji hilo.

Amesema ushauri aliopewa na Meya Mwita ameupokea na kwamba itakuwa kama dira ya kumuongoza katika utendaji wake hivyo akaomba ushirikiano huo uendelee kwakuwa wote wanawatumikia wananchi.

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIMANJIRO YANUFAIKANA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Bw. Yefred Myenzi, akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake kuhusu kilimo cha umwagiliaji. pamoja na mambo mengine kinavyochangia katika pato la Halmashauri hiyo pamoja na kubadilisha Maisha ya wananchi wa Wilaya hiyo.


NA MWANDISHI MAALUM – SIMANJIRO


IMEELEZWA kuwa kilimo cha  umwagiliaji  ni chanzo kikubwa cha mapato katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kwani huingiza  shilingi Milioni mia moja  ishirini (120) hadi milioni miambili (200) kwa mwaka na kuinua  pato la wananchi  wilayani humo.


 Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi  Mtendaji  wa Halmashauri hiyo Bwana Yefred Myenzi  ambapo amesema serikali ilitoa kiasi cha takribani shilingi Bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi na maboresho ya skimu zaa umwagiliaji sambamba na kuwawezesha wakulima kupata elimu ya kilimo, uendeshaji na matunzo ya miundombinu ya  umwagiliaji jambo ambalo limepelekea wanachi kujikita zaidi kwenye kilimo  cha umwagiliaji  na kuongeza pato la Halmashauri,


“Mazao mengi yanayolimwa katika skimu za umwagiliaji ni mpunga  na mazao menginge ya Mboga mboga, lakini pia kuna mazao ambayo hayalimwi katika skimu hizo kama vile Matama, Uwele na Shayiri zao ambalo linatumika kama malighafi katika viwanda vingi vya beer nchini.” Alisema Bw. Myenzi


Bw. Myenzi alisema kuwa Skimu hizo zimesaidia kuwepo na chakula cha kutosha na Usalama wa chakula katika Wilaya hiyo, Pamoja na kwamba Kilimo hicho kinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwa na pamoja na skimu hizo kuwa mbali na masoko jambo ambalo linapelekea kupanda kwa gharama za usafishaji wa mazao kwenda kwenye masoko  na kukosekana kwa bei ya uhakika kitendo ambacho kinamuumiza mkulima pamoja na kukosekana kwa vinu vya kuchakata        nafaka jambo ambalo linapelekea kukosekana kwa chakula cha mifugo kitokanacho na mabaki ya nafaka hizo.


Awali akiongea katika kikao hicho kabla ya kutembelea skimu hizo za umwagiliaji, Mhandisi wa kanda ya Umwagiliaji Dodoma inayohusisha mikoa ya Dodoma, Singida na Simanjiro Bi Lucy Lema, alisema kuwa kutokana na kilimo cha umwagiliaji  kuwa chenye tija kwa kuongeza pato la taifa na kuwepo kwa  uhakika wa chakula nchini, Serikali ina mikakati kabambe ya kuendeleza kilimo hicho kwa kufanya upanuzi wa maeneo  na kufanya  tafiti  kabla ya ujenzi wa mabwawa, kufanyia ukarabati wa Miundombinu ya umwagiliaji na kuendeleza skimu ndogo ndogo za umwagiliaji kupitia miradi mbali mbali.

                                                                  

MKURUGENZI MTENDAJI WA DCB ALIVYOSHUHUDIA UWASILISHWAJI WA BAJETI YA SERIKALI BUNGENI DODOMA

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk, Philip Mpango (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), bungeni Dodoma mara baada ya Waziri Fedha, Dk. Philip Mpango (hayupo pichani), kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk, Ashatu Kijaji akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kulia), bungeni Dodoma mara baada ya Waziri Fedha, Dk. Philip Mpango  kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.
 Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo (kulia), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), bungeni Dodoma jana Mara baada ya waziri wa fedha kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto), bungeni Dodoma jana mara baada ya waziri wa fedha na mipango, kuwasilisha bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  DCB, Geodfey Ndalahwa (kushoto), pamoja na baadhi ya waalikwa wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa bajeti ya Serikali Bungeni, Mjini Dodoma.


MBARAWA ARIDHISHWA NA KUREJEA KWA HUDUMA YA MAJI KIJIJI CHA MPAPULA WILAYANI MTWARA

0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akikagua pampu mpya ya maji iliyofungwa katika kijiji cha Mpapula Halmashauri ya Wilaya Mtwara mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya maji.
Waziri Mbarawa akielekea eneo ilikofungwa pampu mpya ya maji katika kijiji cha Mpapula mkoani Mtwara ambapo huduma ya maji imerejea baada ya pampu hiyo kuungua kwa muda na alipofika Waziri wa Maji mwaka jana aliagiza pampu mpya inunuliwe haraka ili wananchi wapate majisafi na salama.

……………………..

Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) ameridhishwa na kurejea kwa huduma ya maji katika kijiji cha Mpapula kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara baada ya wananchi hao kufungiwa pampu mpya na kuanza kufanya kazi.

Waziri aliyasema hayo leo mara baada ya kufika katika kijiji cha Mpapula na kukuta pampu ya maji mpya iliyofungwa inafanya kazi baada ya pampu ya zamani kuungua mwaka jana.

Pampu hiyo iiliharibika mwaka jana na haikuwa katika sehemu ya Mkataba wa Mkandarasi hivyo kupelekea wananchi kukaa kwa muda mrefu bila ya kupata majisafi na salama hadi Waziri wa Maji alipokuja kujionea tatizo hilo na kuahidi kuwanunulia pampu.

“Serikali iliahidi na imetekeleza” alisema Waziri Mbarawa wakati akikagua pampu hiyo. Mradi huo wa Mpapula unahudumia kata 2 ya Mpapula na muungano na wananchi wapatao 5953 wananufaika na mradi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda alisema kununuliwa kwa pampu hiyo kutasaidia kuondoa kilio cha shida ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Mpapula, na kuwataka wananchi wa eneo hilo kutochimba katika njia ambazo mabomba yanapita. Kufanya hivyo kutasaidia kutunza mabomba hayo yasipasuke na kufanya huduma ya maji kuwa endelevu kwa wananchi.

TIMU YA WIZARA YA KILIMO YAWASILI KANDA YA ZIWA KUBAINI CHANGAMOTO ZA ZAO LA PAMBA

0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua mizani ya kupima pamba za wakulima katika Kijiji cha Imalanguzi katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 14 Juni 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba. (Picha zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akihutbia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Mwabuzo Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba, tarehe 14 Juni 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya umwagiliaji ya Igurubi iliyopo katika Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora tarehe 14 Juni 2019 wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akihutbia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Mwabuzo Wilayani Meatu, Mkoa wa Simiyu wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ufuatiliaji wa chanagmoto ya zao la Pamba, tarehe 14 Juni 2019.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo - Simiyu


Uongozi wa Wizara ya Kilimo umewasili katika mikoa ya Kanda ya ziwa ili kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la Pamba na kuzitafutia ufumbuzi.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameongoza timu hiyo ambapo amezuru katika mikoa ya Tabora na Simiyu kwenye Wilaya za Igunga na Meatu.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) anatembelea katika Mikoa ya Shinyanga na Mara huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akizuru katika Mikoa ya Geita na Mwanza.

Akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Imalanguzi Kijiji cha Igurubi Wilayani Igunga, na Kijiji cha Mwabuzo Wilayani Meatu, Mhe Hasunga amesema kuwa wizara ya Kilimo ipo katika mchakato wa kutafuta mfumo madhubuti wa ununuzi wa Pamba.

Alisema mfumo huo punde utakapoelekezwa utatumika lakini ni mfumo ambao utakuwa maalumu kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha sekta ya pamba nchini.

Amesisitiza kuwa ili kuimarisha kilimo nchini ni wazi kuwa wakulima wanapaswa kupatiwa Pembejeo za kilimo ambazo ni Mbegu, Mbolea na Viuatilifu. “Hatuwezi kuwakomboa wakulima kama tutaendelea na uagizaji wa pembejeo feki ambazo zinawarudisha nyuma wakulima” Alikaririwa Mhe Hasunga

Katika ziara hiyo yenye lengo la kutambua changamoto ya zao la Pamba, masoko yake na upatikanaji wa pembejeo, Waziri Hasunga ameeleza kuwa zao la pamba ni sehemu ya mazao makuu ya biashara nchini hivyo ni lazima litafutiwe ufumbuzi.

Aidha, Mhe Hasunga ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi katika mikutano hiyo kuwa Wizara ya Kilimo ipo katika mapitio ya sera ya Kilimo ya mwaka 2013 itakayopelekea kuwa na sheria ya kilimo itakayomnufaisha mkulima na kulinda rasilimali za kilimo ikiwemo ardhi.

Kadhalika, amesema kuwa serikali inaendelea na zoezi la usajili wa wakulima huku akisisitiza umuhimu wa sekta ya umwagiliaji ambayo ikisimamiwa vizuri itakuwa muarobaini wa kilimo pasina kutegemea msimu wa mvua kwa ajili ya kilimo.

Serikali Yawapa Motisha Wanafunzi Bora, Shule zilizofanya Vizuri 2018

0
0
Miongoni mwa wanafunzi bora wa Kidato cha Sita mwaka 2018 tokea Shule ya Sekondari Mvumi, Erick Maximilian akipokea cheti na zawadi pesa taslimu shilingi milioni 1.5 toka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Pamoja na kuwa mwanafunzi huyo kuwa ni mwenye mahitaji maalum. Meneja wa Shule ya Kaizirege and Kemebos toka Bukoba,Eulogius William akipokea cheti na tuzo toka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako kutambua mchango wa Shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mwaka 2018 wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Kumi bora wa Darasa la Saba 2018 mara baada ya kumaliza hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Kumi bora wa Kidato cha Nne mwaka 2018 mara baada ya kumaliza hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Kumi bora wa Kidato cha Sita mwaka 2018 mara baada ya kumaliza hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya hafla ya Siku ya Elimu ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 mara baada ya kumaliza hafla hiyo leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. (Picha na: Frank Shija –MAELEZO)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Avemaria Semakafu akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Bibi. Odilia Joseph Mushi akizungumza wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.Kaimu Kamishna wa Elimu Tanzania, Lyabwna Mtahabwa akielezea tuzo za Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 wakati wa hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo hizo leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato ya jijini Dodoma wakifuatilia hafla ya Siku ya Elimu iliyoambatana na utoaji tuzo kwa Wanafunzi Bora wa Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Kidato cha Sita kwa Mwaka 2018 leo jijini Dodoma. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Wasichana Msalato na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu.

VIJANA NCHINI KUNUFAIKA NA MAFUNZO YA NISHATI JUA KATIKA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA(ATC)

0
0
Mratibu wa taasisi ya Wataalamu wastaafu nchini Uholanzi(Netherlands Senior Experts),Wim Bredewold(kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ndani ya Chuo cha Ufundi Arusha. 
Kituo hicho kitaendeshwa kwa pamoja kati ya Netherlands Senior Experts(PUM), Tanzania Renewable Energy Association (TAREA) na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC).
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kituo cha mafunzo ya nishati Jua kitakachosaidia kuwapa vijana stadi za kazi na kutoa fursa ya kujiajiri.
Mwenyekiti wa Tanzania Renewable Energy Association (TAREA),Profesa Amini Kweka(kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho kitakachota mafunzo kwa vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini. 
Mwenyekiti wa Tanzania Renewable Energy Association (TAREA),Profesa Amini Kweka(kulia) na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia wakikata utepe kuzindua kituo cha mafunzo ya nishati Jua(Solar training centre) jijini Arusha. 

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 14.06.2019

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOKUTANA NA WABUNIFU WADOGO WA MITAMBO YA KUFUA UMEME IKULU DSM

Kampuni 11 za Uturuki zatafuta fursa za Uwekezaji nchini

0
0
Ujumbe wa kampuni 11  kutoka Uturuki upo nchini kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda vya dawa za binadamu, vifaa vya maabara, vyombo vya ndani,  vifaa vya umeme, ujenzi pamoja na ununuzi wa korosho.

Ziara hiyo imetokana na uratibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Ujumbe huo ambao uliwasili nchini tarehe 10 Juni 2019 ulishiriki mkutano (B2B) uliondaliwa na TPSF tarehe 11 Juni 2019. Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine,  wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda  wa Uwekezaji (EPZA) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) walitoa maelezo kuhusu kanuni, taratibu na mazingira ya kufanya biashara hapa nchini.

Ujumbe huo utatembelea Zanzibar tarehe 13 Juni 2019 na baadaye Dodoma kwa ajili ya kuangalia maonyesho ya masuala ya ujenzi. Ujumbe huo utaondoka nchini tarehe 16 Juni 2019 kurejea Uturuki.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Majadiliano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki yakiendelea katika ukumbi wa TPSF. Aliyesimama ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe Ali Davutoglu ambaye anatoa ufafanuzi kuhusu mazingira ya biashara Tanzania.

Mwenyekiti wa TPSF, Bw. Salum Shamte (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa kampuni hizo za Uturuki, Bw. Ali Engiz. Wengine ni Bw. Godfrey Simbeye (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF na Mhe. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki hapa nchini.

Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hassani Mwamweta (kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania.


UJENZI SGR-UTOBOAJI MAHANDAKI YA KUPITISHA TRENI YA UMEME MAANDALIZI YAKAMILIKA,MITAMBO YASHUSHWA

VOA SWAHILI: Zulia Jekundu Episode 228

HABARI ZA UN: Binti mwenye umri wa miaka 16 Tanzania atengeneza App ya kusaidia wajawazito kufuatilia hali zao.

USHIRIKI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

0
0

TANGAZO



Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni 2019. Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma.


Wakati wa maadhimisho hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa madawati maalum ya kutoa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya Mtumba jijini Dodoma na zile zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Huduma zitakazotolewa ni pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa hoja mbalimbali za wananchi kuhusu Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.


Madawati hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.


NYOTE MNAKARIBISHWA.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

14 Juni 2019





WAZIRI MKUU ATOA MWAKA KWA MIKOA ISIYOKAMILISHA MWONGOZO WA UWEZESHAJI

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwaka mmoja kwa viongozi wa mikoa ya Dar-es-salaam, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Rukwa, Singida na Shinyanga ihakikishe iwe imekamilisha kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji.


Pia amewataka viongozi wa mikoa na halmashauri zote nchini wahakikishe wanaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi kama kile cha Kahama ili kuharakisha nia ya Serikali katika kuwezesha wananchi kiuchumi. 

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Juni 15, 2019) wakati akifungua Kongamano la Nne la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika ukumbi wa Hazina jijini Dodoma. Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) na kauli mbiu yake ni Wezesha Watanzania Kujenga Viwanda.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuliagiza Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kuratibu mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo ya Serikali na ile ya binafsi ili kujua ipo mingapi na inamnufaisha nani na je wanufaika wanajijua na ni kweli wananufaika na kisha wampelekee taarifa.

Waziri Mkuu amesema mikoa yote iliyokamilisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji, nayo ifikapo mwakani inapaswa kuonesha hatua za utekelezaji katika kutumia fursa mbalimbali zilizoainishwa pamoja na mikakati ya kutangaza fursa hizo zilizopo katika maeneo yao.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema matokeo ya tafiti ziliyofanywa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuhusu biashara na uwekezaji nchini yanatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uandaaji wa maandiko ya miradi mikubwa inayopendekezwa na shirika hilo.

“Miradi hiyo ni pamoja na ule wa “Harmonized Innovation Solutions for Local Economic Development” ambao upo katika hatua za maandalizi. Lengo la UNDP ni kuhakikisha kuwa miradi inayohusu uwezeshaji wananchi kiuchumi inatekelezwa moja kwa moja na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambalo lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.” 

Amesema NEEC ina uwezo mkubwa katika kusimamia miradi mbalimbali ya uwezeshaji ambayo imekuwa ikifadhiliwa na Serikali pamoja na Jumuiya ya Kimataifa ikiwemo UNDP, ILO, UNCTAD, AfDB na UN-Women, hivyo ameyahakikishia mashirika hayo kuwa Serikali itasimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi yote ili kupata matokeo yaliyo tarajiwa. 

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuziagizamamlaka zote zishirikiane na NEEC kuhakikisha kuwa fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi zilizobainishwa kupitia tafiti za UNDP zinafanyiwa kazi. “Aidha, hakikisheni kuwa Miradi mikubwa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inatokana na tafiti hizo” 

Amesema anaimani kubwa kuwa kupitia utekelezaji wa miradi hiyo, malengo mbalimbali ya nchi kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi yatafikiwa. Baadhi ya malengo hayo ni pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 - 2020; Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano; Dira ya Taifa ya Miaka 25; na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya umoja wa Mataifa (SDGs).

Pia Waziri Mkuu amelitaka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi liendeleekuratibu masuala ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ikiwemo utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha 2015 - 2020 kuhusu uanzishwaji wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu.

“Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iboreshwe sambamba na kuongeza ufanisi ili iweze kuwafikia Watanzania wengi hususan wale wa vijijini. Vilevile, kamilisheni na hakikisheni mnazindua haraka mfumo wa kupima mifuko ya uwezeshaji kwa matokeo ya kiuchumi na kijamii na siyo kwa shughuli walizofanya.”

Amesema uwezeshaji wananchi kiuchumi ni suala mtambuka, sekta mbalimbali za kiuchumi na sekta binafsi zinajihusisha moja kwa moja katika kuwawezesha wananchi kiuchumi, hivyo, amesisitiza kwamba ni muhimu sana masuala ya uratibu, ufuatiliaji na tathimini ya shughuli za uwezeshaji wananchi kiuchumi, yakafanywa mara kwa mara ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images