Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAIS TSHISEKEDI WA DRC ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM, AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR)

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akipewa maelezo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isaack Kamwelwe kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR na njia itamopita wakati mgeni huyo alipotembelea sehemu ya mradi huo eneo la Vingunguti ‘Mahakama ya Mbuzi’ jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akisalimia wananchi wakati mgeni huyo alipotembelea sehemu ya mradi wa Reli ya Kisasa eneo la Vingunguti ‘Mahakama ya Mbuzi’ jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa kongo (DRC)
Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isaack Kamwelwe akikagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR na njia itamopita wakati mgeni huyo alipotembelea sehemu ya mradi huo eneo la Vingunguti ‘Mahakama ya Mbuzi’ jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa
kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akitambulishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isaack Kamwelwe kwa viongozi wa kampuni ya upakuaji Makontena ya Tanzania International Containers Terminal Services (TICTS) alipotembelea Bandari ya Dar es salaam jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019. 
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akitambulishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isaack Kamwelwe Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isaack Kamwelwe kwa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR na njia itamopita wakati mgeni huyo alipotembelea sehemu ya mradi huo eneo la Vingunguti ‘Mahakama ya Mbuzi’ jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019 
PICHA NA IKULU

WAFANYABIASHARA WAILALAMIKIA HALMASHAURI YA JIJI

$
0
0


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

WAFANYABIASHARA ndogondogo zaidi ya 17 waliopo Soko kuu la mjini
hapa,wameulalamikia uongozi wa Halimashauri ya jiji la Arusha,kwa
kutowarejesha katika maeneo yao waliyokuwa wanafanyia biashara awali
ambapo kwa sasa wanataka kuyagawa kwa wafanyabiashara wengine.


Wakizungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao,Nelson
Alfayo,Gilbert Fransis,Joseph Mungaya,juma Zuberi na Gasper
Ngowi,wamesema kuwa wameshangazwa na uamuzi wa uongozi wa halimashauri ya jiji kwa uamuzi huo kwani wao wamekuwa wakifanya biashara katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Wamesema kuwa uongozi wa jiji la Arusha uliwaamuru wapishe eneo hilo
ili waweze kujenga mabanda ya kisasa ndani ya soko hilo kwa ahadi kuwa
mara baada ya kukamilika wao watapewa kipaumbele kurejeshwa katika
eneo hilo jambo ambalo halijafanyika.

Mmoja wa wafanyabiashara hao,Nelson Alfayo,alisema kuwa uongozi wa
jiji uliwaambia waandike barua ya kuomba kugawiwa maeneo hayo jambo
ambalo walilifanya kwa kuandika barua hiyo mei 13, lakini cha
kushangaza hadi leo hii wamekuwa wakipigwa danadana ikiwa ni pamoja na kupewa vitisho vya mara kwa mara.

“Baada ya kuandika barua tumekuwa tukifuatilia na kwa mara ya mwisho
tuliambiwa turudi tarehe 29 Mei ambapo tulifanikiwa kukutana na
mkurugenzi Mtendaji wa Jiji Dk.Ahmad Madeni lakini tulishangazwa na
kitendo chake cha kuamuru Mwenyekiti wetu Fredy Eliphace na baadhi ya
wenzetu watatu kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi”alisema
Alfayo.

Aliongeza kuwa wenzao walipopelekwa polisi walifunguliwa jalada la
kufanya biashara bila leseni jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote
kwani walikuwa nazo pamoja na vitambulisho vya mjasirimali ambapo
walilazimika kulala katika kituo kikuu cha polisi hadi kesho yake
walipotoka kwa dhamana.

Amesema kuwa kitendo cha kutishiwa maisha na wenzao kukamatwa kimekuwa kikiwapa hofu kubwa sana kuendelea kufuatilia majibu ya barua yao ambapo wameziomba mamlaka za juu kuliangalia suala hilo na kuhakikisha linapatiwa ufumbuzi.

Akizungumzia suala hilo Mstahiki Meya wa jiji la Arusha,Kalist
Lazaro,alisema kuwa wafanyabiashara hao wanatakiwa kufuata taratibu
stahiki za kuomba kupatiwa eneo la kufanyia biashara ambapo baada ya
kutuma maombi wanatakiwa wasubiri vikao husika vikae kwa ajili ya
kuwajadili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Arusha.Dkt Ahmad Madeni
alinukuliwa aakiwaambia wafanyabiashara hao kuwa endapo wanataka
kuomba maeneo ya kufanyia biashara ndani ya jiji wanatakiwa kuomba mtu
moja moja na sio kuomba kama kundi kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na
fujo.

Naye Afisa Biashara wa jiji la Arusha,Godfrey Edward ameliambia gazeti
hili kuwa ni kweli wafanyabiashara hao walifika katika ofisi za
halimashauri hiyo kuomba wapatiwe maeneo hayo,lakini halimashauri
imetenga maeneo hayo kuwapatia wafanyabiasha ambao walikuwa na
migogoro ya vibanda vya biashara kwa muda mrefu katika maeneo ya
biashara yanayomilikiwa na halimashauri ya jiji hilo.

SERIKALI YAWABANA WAINGIZA 'MAWIGI' NCHINI, WAPANDISHIWA USHURU WA KODI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Fedha Dk. Philip Mpango wakati anawasilisha bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 pamoja na mambo mengine amezungumzia kutoza ushuru kwenye nywele bandia(Mawigi).

Dk.Mpango akizungumza Bungeni Mjini Dodoma amesema Serikali itatoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye nywele bandia zinazotengenezwa ndani ya nchi na asilimia 25 kwenye nywele zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.

Amesema lengo likiwa kuongeza mapato ya serikali."Nywele bandia ambazo zinatengenezwa nje ya nchini ushuru utakaotozwa ni asilimia 25,"amesema Waziri Mpango wakati anawasilisha bajeti hiyo.

Hata hivyo wakati anazungumzia kwenye nywele hizo bandia, baadhi ya wabunge walisikika wakisema kuwa Serikali pia iongeze ushuru wa kodi kwa kucha bandia ambazo nazo zimekuwa zikiingizwa nchini kwa wingi.

Mbali na ushuru kwenye nywele bandia,Waziri Mpango amesema Serikali imesamehe ushuru wa bidhaa kwenye vilainishi vya ndege vinavyoingizwa nchini na Shirika la Ndege la Tanzania au mashirika ya kimataifa ya huduma za anga.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kuiwezesha nchi kusaini mikataba ya kimataifa ambayo ilishindikana kusainiwa awali kutokana na kutokuwepo kwa msamaha huo.

Amezungumzia pia kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 10 kwenye bidhaa za mabomba na vifaa vya plastiki vinavyotumika kwenye ujenzi wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya maji kwa kuwa hivi sasa kuna viwanda vingi vyenye uwezo wa kuzalisha bidhaa hizo.

Waziri Mpango amesema hatua hiyo itahusisha bidhaa za mabomba ya plasitiki zinazotambuliwa na kwamba lengo la kuanzisha ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa hizo ni kulinda viwanda na kuongeza fursa za kazi, ajira na mapato ya Serikali.

Ameongeza kwa ushuru wa bidhaa kwenye bishaa zisizo za petroli kwa ujumla wake azinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh.bilioni 2. 9.

NI BAJETI YA KIMKAKATI...YAFUTA UTITIRI WA KODI

$
0
0

*Yaondoa msamaha wa kodi kwenye taulo za kike kisa...

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BAJETI ya Serikali ambayo imewasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk.Philip Mpango imeonesha namna ambavyo imefuta msururu wa kodi ambazo nyingine zilikuwa kero ka Watanzania.

Mbali ya kufuta utitiri huo wa kodi,Waziri Mpango amesema ni marufuku kwa watumishi wa TRA kufunga biashara kwa madai ya kudai kodi.

Akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni Mjini Dodoma,Waziri Mpango amesisitiza kwa watumishi wa TRA kuwa hairuhusiwi kufunga biashara ili kushinikiza mfanyabiashara alipe kodi au malimbikizo ya kodi isipokuwa kwa kibali cha kamishina Mkuu wa TRA.

Amefafanua alipendekeza kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi ikiwemo baadhi ya viwango vya kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya sheria mbalimbali na pia taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya serikali.

Dk.Mpango amesema marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwa na mfumo wa kodi ambao ni tulivu na wakutabirika.

Amesema kwamba marekebisho hayo yanalenga kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi hususan katika sekta ya kilimo,viwanda,kukuza ajira, na kuongeza mapato ya serikali.

Wakati huo huo ameeleza kuwa Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa biashara (BluePrint) ulioidhinishwa mwaka 2017/18 kwa kupitia mfumo wa tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na mamlaka za udhibiti kwa lengo la kupunguza na kuondoa muingiliano katika kutoza tozo hizo.

"Marekebisho yanayopendekezwa yanahusu Sheria ya Kodi ya Ongezeko la thamani, Sura 148, Sheria ya kodi ya mapato, Sura 332 na Sheria ya ushuru wa bidhaa, Sura 147.

"Pia yatahusu Sheria ya usimamizi wa kodi, Sura 438, Sheria ya Usalama Barabarani, Sura 168, Sheria ya forodha ya jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004, Sheria ya bajeti Sura 439, na marekebisho madogo katika baadhi ya sheria za kodi na sheria nyingine mbalimbali,"amesema.

Ameweka wazi kuanza utekelezaji wa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa biashara kwa kurekebisha ada na tozo mbalimbali, kuchukua hatua za kisera na kiutawala katika kuboresha ukusanyaji wa mapato.

Kuhusu sheria ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT) Waziri huyo wa fedha amesema marekebisho yanayopendekezwa yanahusu sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya VAT, Sura ya 148, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura 332, Sheria ya Ushuru wa Bidhaa Sura ya 147.Pia amependekeza kufanya marekebisho kwenye sheria hiyo ambayo inasamehe VAT kwenye makasha yenye majokofu yanayotumika kwenye kilimo cha Kisasa cha mboga mboga kwa wakulima wanaoingiza makasha hayo kutoka nje ya nchi.

"Lengo la hatua hiyo ni kupunguza gharama na kutoa unafuu katika uzalishaji na kuhamasisha kilimo cha kisasa cha mboga mboga nchini.Pia kufanyika marekebisho kwenye kifungu cha 68(3)(d) ili kisihusishe uuzaji wa mazao ghafi ya kilimo nje ya nchi."Lengo la hatua hii ni kuwawezesha wauzaji wa mazao ghafi ya kilimo nje ya nchi kuendelea kufanya biashara hiyo kwa kadri ya kibali kitakavyotolewa na serikali,,"amesema Wazriri Mpaango.

Amesema msamaha huo unatarajiwa kutoa unafuu kwenye gharama za kukausha nafaka kwa ajili ya kuzihifadhi na kwamba hatua hiyo itachochea ukuaji wa kilimo cha mazao ya nafaka.

Amesema kupunguza kiwango cha VAT kutoka asilimia 18 hadi sifuri kwenye huduma ya umeme unaouzwa kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar ili kuwapunguzia gharama za maisha wananchi wa Tanzania Zanzibar.

Amesema kuwa "Serikali iliridhia na kuelekeza kuwa umeme unaouzwa kutoka Tanzania Bara kwenda Tanzania visiwani utozwe VAT kwa kiwango cha asilimia sifuri."

Kwa upande mwingine ,Waziri Mpango amesema Serikali imeamua kufuta msamaha wa VAT uliokuwa umetolewa kwenye taulo za kike kwa kuwa haujawezesha kupatikana kwa bidhaa hiyo muhimu kwa bei nafuu kwa walengwa na badala yake unawanufaisha wafanyabiashara.
Amefafanua kuwa Serikali ilipoweka msamaha kwenye taulo za kike ilitarajia wazalishaji wa taulo za kike wataziuza kwa bei nafuu baada ya kusamehewa kodi.

Hata hivyo amesema hatua hiyo ya VAT zinatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh.Milioni 1,646.7.

Kuhusu sheria ya kodi ya mapato,Waziri Mpango amesema katika sheria hiyo ya mapato inapendekezwa kufanyika kwa marekebisho ya kupunguza kiwango cha kodi ya mapato kwa makampuni kutoka asilimia 30 hadi asilimia 25 kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2019/20 hadi 2020/21 kwa wawekezaji wapya wa viwanda vya kuzlaisha taulo za kike.

Amesema kuwa Serikali itaingia mkataba wa makubaliano na kila mwekezaji ambao utaainisha wajibu wa kila upande na lengo la hatua hiyo ni kuvutia uwekezaji katika uzalishaji wa bidhaa hiyo muhimu, kuongeza ajira na mapato.

"Pia hatua hii itapunguza matumizi ya fedha za kigeni zinazotumika kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje na kuhamasisha uzalishaji wake ndani ya nchi,"amesema Waziri Mpango wakati anawasilisha bajeti hiyo yenye kurasa 74.

MARIAM HAMDUN KUUPAMBA USIKU WA NASAHA CREW

$
0
0
Na.Khadija seif,Globu ya jamii

WANAMUZIKI wa bongofleva waasa kuacha kufanya mzaa na dini ya kiislam.

Akizungumza na michuzi tv muimbaji wa qaswida Masoud ferouz amesema si vizuri kwa wasanii kuamua kuimba qaswida na baadae kurudi kwenye miziki ya kidunia (bongofleva).

"Wapo wasanii ambao wanafanya miziki ya aina nyingi hasa ya kidunia ,ni sawa kutokana na wote tunatafuta ridhiki ni kheri ukafanya muziki wa aina moja na kujua shabiki zako kwa urahisi,"

Aidha ,ameweka wazi kuwa kundi la qaswida la nasaha lipo kwa ajili ya kuburudisha, kufundisha na kuwa mchamungu kutokana na tungo na uimbaji wake wa kipekee."Kundi hili linabeba waimbaji takribani 11 akiwemo Mariam hamdun ambae anafanya vizuri katika soko la muziki wa qaswida nje na ndani ya nchi,"

Pia amewaomba wapenzi na mashabiki wa nasaha kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la pili la usiku wa furaha (laylatul helwa) juni 16 katika ukumbi wa Daimond jubilee jijini Dar es salaam."Siku hiyo ya tamasha utakua ni usiku wa kitofauti kwani waimbaji wengine wapya watatambulishwa ambao tayari wapo kwenye muziki wa mwambao,"

Kwa upande wake Mariam hamdun amesema sababu inayopelekea kupata mashabiki wengi ni sauti yake ya kipekee sana huku nidhamu ikiwa ndio nguzo kubwa kwa Msanii yoyote yule.

"Vyombo tunavotumia katika qaswida zetu ni vya kiasili kama zumari,kinanda na filimbi na hata video zetu tunatumia mandhari ya kiasili bahari,makumbusho ya kale na vitu mbali mbali ambavyo vilitumika kwenye qaswida ya utu,algenani mahaba ya mtume.

BAJETI YA FEDHA YA 2019/2020 YAWABEBA SEKTA YA MIFUGO...KODI LUNDO ZAFUTWA

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MAPENDEKEZO ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2019,2020 imeonesha namna ambavyo Serikali imedhamiria kuboresha sekta ya mifugo nchini.

Akizungumza Bungeni Mjini Dodoma wakati anawasilisha makadirio ya bejeti ya Serikali,Waziri wa Fedha Dk.Philip Mpango pamoja na mambo mengine amesma Serikali imependekeza kufuta tozo mbalimbali kwenye sekta ya mifugo.

Amesema wamefuta tozo ya sh. 5000 ya vibali vya vyombo vya kusafirisha maziwa chini ya lita 51, pia kufuta tozo ya Sh. 50,000 ya usajili wa vituo vya kukusanyia maziwa lita 201 kwa siku.Pia imefuta tozo ya Sh.5000 ya usajili wa wazalishaji wa maziwa chini ya lita 51 kwa siku pamoja na kufuta tozo ya Sh.500,000 ya usajili wa wasambazaji wa pembejeo za maziwa.

Waziri Mpango amefafanua pia wamefuta tozo ya sh. 15,000 ya usajili wafugaji wadogo wa mifugo ya nyama na kufuta tozo ya Sh. 50,000 ya usajili wa wafgaji wadogo wa mifugo ya nyama.

"Tumefuta tozo ya Sh. 50,000 ya usajili wa wafugaji wa kati wa mifugo ya nyama, kufuta tozo ya Sh. 75,000 ya usajili wafugaji wakubwa wa mifugo ya nyama na kufuta tozo ya Sh. 20,000 ya usajili wasimamiziwa minada ya awali,"amesema.

Ameongeza kuwa Serikali imependekeza kufuta tozo ya Sh. 30,000 ya usajili wasimamizi wa minada ya upili na mipakani pamoja na kufuta tozo ya sh. 50,000 ya usajili wa minada ya upili na mpakani.

Pia kufuta tozo ya Sh. 30,000 ya usajili wafanyabiashara wa minada ya awali na kufuta tozo ya Sh. 60,000 ya usajili wafanyabiashara wa minada ya upili na mipakani.Aidha, Waziri Mpango amesema Serikali imefuta tozo ya Sh. 100,000 ya usajili wa wafanyabiashara wa nyama na bidhaa zake za nje ya nchi pamoja na kufuta tozo ya Sh. 1000 ya kibali cha kusafirisha kuku nchini ya vifaranga 100 kwa siku.

Wakati huo huo amesema amependekeza kufuta tozo ya Sh. 200 ya kibali cha kusafirisha kuku mkubwa nchini na kwamba hatua hiyo inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa sh. bilioni 16.6.

TPA yasikia kilio Bandari Cha Wakazi wa Kabwe Nkasi

$
0
0

Na Humphrey Sha, Globu ya Jamii Nkasi.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesikia kilio cha muda mrefu cha watumiaji wa bandari ndogo ya Kabwe iliyopo wilayani Nkasi mkoani Rukwa, kwa kuanza ujenzi wa bandari kubwa ya kisasa itakayomaliza changamoto zilizopo hivi sasa.

Bandari ya sasa ya Kabwe iliyopo katika mwambao wa Ziwa Tanganyika ina gati dogo ambalo limelalamikiwa na wasafirishaji kuwa wakati wa kiangazi maji yanapungua hadi kufikia kina cha mita moja na hivyo kulazimika kupakia mizigo ndani ya maji kwa kutumia boti ndogo.

Akizungumza na waandishi wa habari bandarini hapo Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, amesema Bandari ya Kabwe ni kitovu cha biashara kati ya mkoa wa Rukwa na mikoa mingine na kati ya Tanzania na nchi jirani hivyo ina umuhimu mkubwa kwa ustawi wa uchumi.

Amesema kutokana na umuhimu huo sambamba na changamoto za bandari ndogo ya sasa Serikali kupitia TPA ilitoa fedha Sh bilioni 7.49 kwaajili ya ujenzi wa bandari mpya ya kisasa itakayoendana na mahitaji ya sasa na ya baadae.

Amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa mita 74 kuingia majini, ujenzi wa jengo la abiria, ghala, nyumba za watumishi, jengo la mgahawa na uzio utakaozunguka eneo lote la bandari.

Ametaja kuwa mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi M/S Sumry's Enterprises Ltd ulianza Aprili Mosi 2018 na unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 24 sawa na miaka miwili na kwamba hadi sasa umefikia asilimia 40.

Meneja huyo amesema mradi huo ukikamilika utaongeza ufanisi wa huduma za bandari hiyo na kuingiza mapato zaidi.

Kwa mujibu wa Afisa Bandari ya Kabwe, Mohamed Mahyoro bandari hiyo licha ya changamoto zilizopo meli na shehena zimekuwa zikiongekeza mwaka hadi mwaka na kwamba hiyo ni ishara kwamba kuna biashara kubwa katika bandari hiyo.

"Kuanzia Julai 2017 hadi Juni 2018 tulihudumia tani 14,550 na kuanzia Julai 2018 hadi Mei mwaka huu bandari hiyo ndogo imehudumia tani 19, 591 na kwa upande wa maboti yaliyohudumiwa katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 yalikua 259 na Julai 2018 hadi Mei mwaka huu imeshahudumia meli 319," alisema Mahyoro.

Mahyoro alisema changamoto iliyopo ni kina cha maji kupungua hadi mita moja na wakati wa mvua huongezeka na kifikia mita 1.5.Mfanyabiashara Mohamed Shabib ambaye anatumia bandari hiyo kusafirisha mizigo yake alisema ujio wa bandari mpya utamaliza changamoto ya ufupi wa kina cha maji.

"Hapa kuna shida ya kina cha maji na tunalazimika kujaza mzigo kwenye maboti makubwa ndani ya maji kwa kutumia boti ndogo hivyo tunashkuru mradi huu mpya utatuondolea kero hii ambayo inaongeza gharama," alisema Shabib.
 Meneja Bandari za Ziwa Tanganyika Ajuaye Msese akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika katika bandari ya Kabwe Mkoani Rukwa Wilaya ya Nkasi kujionea shughuliA ujenzi wa gati mpya inavyoendelea.
 Moja ya Mafundi wa Gati ya Bandari ya Kabwe Ziwa Tanganyika akiwa ameibuka kutoka kwenye maji ambapo anazamia kwa ajili ya kupanga mawe.
 Mafundi was kufuma nguzo zinazo zamishwa kwenye maji wakiendelea na shughuli yao katika mradi huo unaogharimu zaidi ya Bilioni 7.
 Afisa Bandari ya Kabwe Mohamed Mahyoro akizungumza na Waandishi wa Habari
Sehemu ya majahazi yanayopakilia mzigo ndani ya Maji kwa sasa kutokana na changamoto ya kutokuwey kwa gati yenue kina kizuti na Cha kutosha.

DKT. KIJAZI ASHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA UMAKAMU WA TATU WA RAIS WA WMO

$
0
0

Mkurugennzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na mwakilishi wa kudumu Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) 

​​
Na: Monica Mutoni. Geneva

Kwa mara nyingine Tanzania imeingia katika historia ya kimataifa kwa Mkurugennzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania na mwakilishi wa kudumu Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) kuibuka mshindi wa nafasi ya umakamu wa tatu wa Rais wa WMO. Dkt. Kijazi anachukua nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2019-2022 akiwa mwanamke wa kwanza na mjumbe wa kwanza kutoka nchi zinazoendelea kushika nafasi hiyo. Dkt. Kijazi atakuwa na majukumu makubwa ya kumsaidia Rais kuongoza shirika hilo katika kutekeleza majukumu yenye tija kwa wanachama wake ikiwemo Tanzania 

Akizungumzia ushindi wake mbele ya wapiga kura wa mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na wajumbe waalikwa, Dkt. Kijazi alitoa shukrani zake za dhati kwa wote waliomwamini na kumuunga mkono hadi kufika kupata nafasi hiyo na kuahidi kuitumika nafasi hiyo kwa weledi wa hali ya juu ili kufikia malengo ya shirika hilo.
‘ Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote waliokuwa pamoja na mimi kwa kuniunga mkono na kunichagua kwa kura zote, naahidi kuitumikia nafasi hii kwa weledi mkubwa na kuhakikisha WMO inafikia malengo yake’. Alisema Dkt Kijazi 

Akizungumzia ushundi huo, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Atashasta Nditiye alisema ni heshima kubwa sana kwa nchi, Wizara inampongeza sana Dkt. Kijazi na kuamini kuwa ataiwakilisha nchi vizuri, aidha alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano aliouonesha kwa kukubali Tanzania kuwakilishwa na Dkt. Kijazi ambapo kwa jitihada zake katika kuboresha sekta ya hali ya hewa kumeendelea kuiletea sifa nchi kwa ujumla 

Kwa upande wa Kaimu Balozi, Ubalozi wa Kuduma Umoja wa Mataifa, Geneva Ndugu. Robert Kahendaguza alisema kuwa ushindi wa Dkt. Kijazi ni kielelezo cha umadhubuti wa kidiplomasia ya Tanzania na sifa zake binafsi ikiwemo uzoefu wa muda mrefu na elimu ya ngazi ya juu katika nyanja ya sayansi ya hali ya hewa, aidha aliongeza kuwa sababu za sifa hizo ziliupunguzia ubalozi kazi ya kumnadi na hata kuwa rahisi kuishawishi nchi ya Sudan kuondoa mgombea wao na hivyo kumfanya Dkt. Kijazi kuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo. 

Uchaguzi wa viongozi wa WMO hufanyika kila baada ya miaka minne kwa kuchagua viongozi mbali mbali wakiwemo Katibu Mkuu, Rais, Makamu wa Rais wa kwanza, wapili na watatu, ambapo kwa mwaka huu umefanyika katika mkutano wa 18 wa shirika hilo baada ya muda wa viongozi hao kuisha. Uchaguzi huo ulifanyika kwa haki na kwa mani na kuwapata viongozi hao ambao ni Prof. Petteri Taalas kutoka Finland (Katibu Mkuu), Prof. Dk. Gerhard Adrian kutoka Ujerumani (Rais), Prof. Celeste Saulo kutoka Argentina (Makamu wa kwanza wa Rais), Dr. Albert Martis kutoka Curacao (Makamu wa Pili wa Rais) na Dkt. Agnes Kijazi kutoka Tanzania (makamu wa tatu wa Rais).

KAMISHINA WA OPERESHENI NA MAFUNZO CP LIBERATUS SABAS, AFANYA ZIARA YA UKAGUZI KATIKA UWANJA WA MBINU ZA MEDANI KILELEPORI – KILIMANJARO

$
0
0
Kamishina wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas wa pili kutoka kulia akiwa ameongozana na sacp Gemini S. Mushy ambaye ni Chief Instructor katika Chuo cha Polisi Moshi pamoja na wakufunzi wa mbinu za Medani baada ya kuwasili katika eneo la mafunzo liliopo Kilelepori wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. 
Kamishina wa Opereshni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, akisalimiana na wakufunzi wa kozi mbalimbali za Jeshi la Polisi waliopo eneo la kilelepori wilayani Hai mkoani Kilimanjaro baada ya kuwasili kwa ajili ya kuongea na wanafunzi walioko hapo. 
Kamishina wa Opereshni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, akizungumza na wanafunzi wa kozi ya utunzaji wa silaha baada ya kuwasili eneo la kilelepori wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. (PICHA NA JESHI LA POLISI).

WATOTO, WAZAZI/WALEZI WAJADILIANA CHANGAMATO ZA MALEZI NA UKATILI KUELEKA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Sebastian Kitiku akifungua mdahalo uliwakutanisha watoto, wadau wa maendeleo ya mtoto, wazazi/walezi na viongozi wa dini uliofanyika mkoani Geita. 
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Christopher Mushi akitoa mada kuhusu haki za watoto wakati wa mdahalo uliwakutanisha watoto, wadau wa maendeleo ya mtoto, wazazi/walezi na viongozi wa dini uliofanyika mkoani Geita. 
Mwakilishi wa Shirika la Campassion Bi. Zinath Sylvester akitoa mada kuhusu hali ya ukatili katika mkoa wa Geita wakati wa mdahalo uliwakutanisha watoto, wadau wa maendeleo ya mtoto, wazazi/walezi na viongozi wa dini uliofanyika mkoani Geita. 
Mhamasishaji Dkt. Katanta Semwinza akitoa mada kuhusu hali ya ukatili katika mkoa wa Geita wakati wa mdahalo uliwakutanisha watoto, wadau wa maendeleo ya mtoto, wazazi/walezi na viongozi wa dini uliofanyika mkoani Geita. 
Baadhi ya watoto wakifuatilia mada wakati wa mdahalo uliwakutanisha watoto, wadau wa maendeleo ya mtoto, wazazi/walezi na viongozi wa dini uliofanyika mkoani Geita. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

MARIAM HAMDUN KUUPAMBA USIKU WA LAYLATUL HELWA WA NASAHA CREW

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya jamii
WANAMUZIKI wa bongofleva wameaswa kuacha kufanya mzaha na dini ya kiislam.

Akizungumza na michuzi tv muimbaji wa qaswida Masoud ferouz amesema si vizuri kwa wasanii kuamua kuimba Qaswida na baadaye kurudi kwenye muziki ya kidunia (bongofleva).

" Wote tunatafuta ridhiki ila ni kheri ukafanya muziki wa aina moja na kujua shabiki zako kwa urahisi," ameeleza.

Aidha ,ameweka wazi kuwa kundi la Qaswida la nasaha lipo kwa ajili ya kuburudisha, kufundisha na kuwa mchamungu kutokana na tungo na  uimbaji wake wa kipekee.

"Kundi hili linabeba waimbaji takribani 11 akiwemo Mariam hamdun ambae anafanya vizuri katika soko la muziki wa Qaswida nje na ndani ya nchi." ameeleza.

Pia amewaomba wapenzi na mashabiki wa nasaha kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha la pili la usiku wa furaha (laylatul helwa) juni 16 katika ukumbi wa Daimond jubilee jijini Dar es salaam.

"Siku hiyo ya tamasha utakua ni usiku wa kitofauti kwani waimbaji wengine wapya watatambulishwa ambao tayari wapo kwenye muziki wa mwambao" amesema.

Kwa upande wake Mariam hamdun amesema sababu inayopelekea kupata mashabiki wengi ni sauti yake ya kipekee sana huku nidhamu ikiwa ndio nguzo kubwa kwa Msanii yoyote yule.

"Vyombo tunavotumia katika Qaswida zetu ni vya kiasili kama zumari,kinanda na filimbi na hata video zetu tunatumia mandhari ya kiasili bahari, makumbusho ya kale na vitu mbali mbali ambavyo vilitumika kwenye Qaswida ya utu naalgenani mahaba ya mtume.

Mwisho.

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMED AHUTUBIA SIKU YA WACHANGIAJI DAMU DUNIANI MWANAKWEREKWE ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akimkabidhi zawadi Mchangiaji Bora wa Damu Rashid Adam Mtawa ambae anadamu Group ‘O’Nagative katika siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD BLOOD DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini Zanzibar.
Wafanyakazi wa Kitengo cha Damu Salama Hasina Khamis Masoud na Ussi Bakar Mohamed wakiwa katika kazi ya kuwapima Damu wananchi mbalimbali waliojitokeza katika siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD BLOOD DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini Zanzibar. 
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa hotuba katika hafla ya siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD BLOOD DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini Zanzibar. 
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kuchangia Damu katika siku ya Wachangia Damu Duniani(WORLD BLOOD DONOR DAY)iliofanyika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni mjini Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR. 
…………………… 
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 

Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amewataka wananchi waongeze juhudi ya kuchangia damu ili kuokoa maisha kwa wagonjwa aliokuwa hatarini ambao wanahitajika kusaidiwa damu kutokana na matatizo mbali mbali. 

Hayo aliyasema huko katika Uwanja wa Mwanakwerekwe Sokoni Wilaya ya Magharibi B Unguja wakati wa Sherehe ya Kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani . 

Alisema wananchi wenye moyo wa kuchangia damu kwa hiyari huokoa maisha ya watu wengi ambao wanahitaji huduma ya kusaidiwa damu wakiwemo mama wajawazito na waliojifungua ni zaidi ya asilimia 75 ,wahanga wa ajali pamoja na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji . 
“Damu ni uhai bila ya damu huna uhai huwezi kufanya kazi kama huna damu ya kutosha pia huwezi juwa wakati gani utapata tatizo. “alisema Waziri wa Afya 

Aidha alisema ukaguzi unahitajika katika sehemu zote zinazohifadhiwa damu ili kuhakikisha damu iliyopo ipo katika hali ya usalama na inatumika ipasavyo bila ya kukaa hadi kuharibika. 

Alifahamisha kuwa utowaji wa damu kwa wananchi kumesaidia kuepua matatizo mbali mbali ya Maradhi hasa magonjwa ya ini ambayo yameonekana kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa bado hawajajibaini na kuweza kupatiwa huduma za tiba mapema . 
Alisema takwimu zinahitajika kwa kila wilaya kuweza kujuwa kiasi gani cha mahitaji ya damu ambayo yanahitajika ili kuweza kujipanga kwa mujibu wa mahitaji yaliopo. 

Pia aliwashukuru wananchi kwa uwelewa wa kujitokeza katika kuchangia damu kwani kila siku mahitaji ya damu yanahitajika kuongezeka kutokana na ongezeko la idadi ya watu . 

Hata hivyo alitoa shukurani kwa wananchi mbali mbali Jumuiya pamoja na Taasisi za Serikali ikiwemo Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Vikosi vya ulinzi na usalama,sehemu za ibada Msikitini pamoja na Kanisani. 
Nae Mkuu wa Wilaya Magharibi B Kapteni Silima Haji Haji alipongeza jitihada zilizochukuliwa za uhamasishaji wananchi pamoja na jumuiya mbali mbali ili kujitokeza kwa wingi kwa kuitika wito huo wa kuchangia damu zao . 

Aidha alisema kufanya hivyo ni kusaidia kuokoa maisha ya watu wengi ambao wanapata matatizo mbali mbali ya kiafya ikiwemo wahanga wa ajali . 
Kaimu Meneja wa mpango wa damu salama Uchangiaji Omar Juma Kidawa alisema wataendelea kuwahamasisha wananchi katika sehemu mbali mbali ili hakikisha uchangiaji unaongezeka kulingana na mahitaji ya wananchi . 
Alisema kila siku idadi ya wachangiaji inazidi kuongezeka kuanzia Januari mosi hadi sasa imeshapatikana damu unit 6954 jambo ambalo linatia moyo sana kila siku idadi inaengezeka ya uchangiaji kwa wananchi. 

Meneja Mstaafu wa kuchangiaji damu Mwanakheir Mahamoud aliahidi kuwa sambamba katika kuhamasisha watu kuchangia damu kwani ni suala muhimu ambalo linaokoa wengi kwa kuweza kuchangiwa damu salama . 
Katika Sherehe hiyo ya Uchangiaji Damu Duniani zawadi mbali mbali zimetolewa kwa Wananchi Jumuiya, Taasisi pamoja na Nyumba za Ibada kwa kuwa wachangiaji bora

TBA WAASWA KUTEKELEZA MIRADI KWA WAKATI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisisitiza jambo katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dodoma. Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), ambaye pia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daud Kondoro, akisoma taarifa ya utekelezaji wa Wakala huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, katika kikao cha Baraza la wafanyakazi jijini Dodoma, leo. Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala huo jijini Dodoma, leo. Kaimu Mkurugenzi wa Miliki kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Kileo Hamis, akichangia mada katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala huo jijini Dodoma, leo. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), jijini Dodoma.
PICHA NA WUUM 
……………….. 
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umetakiwa kutekeleza miradi wanayoisimamia kwa wakati na kuzingatia weledi ili kuongeza tija na uzalishaji katika Wakala huo. 
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, wakati akifungua kikao cha siku mbili cha Baraza la wafanyakazi wa Wakala huo, jijini Dodoma. 
Agizo la Katibu Mkuu huyo limefuatia baada ya kupata malalamiko kutoka kwa baadhi ya wateja wa Wakala huo amabapo wamesema kuwa Wakala huo umekuwa ukichelewesha miradi, hivyo amewataka kupitia Baraza hilo kujiwekea malengo na mpango mkakati wa kutekeleza miradi hiyo na kuikamilisha kwa wakati. 
“Nina uhakiaka suala hili lipo chini ya uwezo wenu endapo mtajipanga vizuri na kufanya kazi kwa mshikamano na weledi huku mkithamini mchango wa kila mmoja wenu katika eneo la kazi, basi mtafanikiwa,” amesema Mwakalinga. 
Aidha, ameutaka Wakala huo kujiwekea maazimio yatakayowasilishwa Wizarani ambayo yatajikita katika uboreshaji wa maslahi ya watumishi, ikiwemo kuwajengea uwezo utakaowafanya kutimiza majukumu yao kwa wakati na ufanisi zaidi. 
Kuhusu madai ambayo Wakala unadai Taasisi nyingine za umma, Katibu Mkuu Mwakalinga ameutoa hofu Wakala huo kwa kusema kuwa suala hilo halitafumbiwa macho na atahakikisha kuwa madeni yote yanalipwa baada ya kuhakikiwa. 
“Wekeni kumbukumbu zenu za madai vizuri ili ziweze kuhakikiwa kabla ya kuwasilishwa kwa wahusika, nami naahidi kufuatilia madeni haya na kuhakikisha kuwa yatalipwa,” amesisitiza Katibu Mkuu. 
Ameongeza kuwa Serikali inathamini mchango wa Wakala huo katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ambapo amefafanua kuwa Wizara yake pamoja na Taasisi zilizo chini yake imejiwekea agenda madhubuti ambazo anaamini zikitekelezwa basi Sekta ya Ujenzi nchini itakuwa kwa kasi. 
Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA Arch. Daudi Kondoro amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kuwa atatekeleza maagizo yote na pia atahakikisha maazimio watakayo jiwekea yanatekelezwa kwa wakati. 
Alisema kuwa taratibu za kupandisha watumishi vyeo zinaendelea ambapo tayari watumishi 64 waliokidhi vigezo wamepandishwa vyeo katika madaraja mbalimbali na watumishi 17 wamebadilishwa kada kulingana na taaluma zao. 
Kikao hicho kimejumuisha zaidi ya wajumbe 62 ambao baadhi yao ni wakuu wa idara na vitengo, mameneja kutoka mikoa yote, wawakilishi wa wafanya kazi kutoka idara na vitengo pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi vilivyomo ndani ya Wakala.

MELI ZA MAFUTA ZASHAMBULIWA, NCHI YA IRAN YATILIA SHAKA

$
0
0
Na Ripota ,Kimataifa 

MELI mbili za mafuta zimeharibiwa ambapo meli moja imeshika moto na nyingine ikiwa inaelea hali iliyosababisha wafanyakazi kuondolewa kutoka meli hizo. 

Matukio hayo ya kutia shaka yametokea hivi karibuni na yanahusu meli hizo za mafuta, huku kukiwa na hali ya wasi wasi mkubwa kati ya Marekani na Iran. 

Taarifa iliyopo kwenye Mtandao wa DW umeeleza kuwa Jeshi la majini la Marekani, limechukua hatua za haraka kutoa msaada kwa meli hizo, na wamiliki wa meli hizo hawakutoa ufafanuzi mara moja wa silaha zilizosababisha uharibifu katika meli zao katika ghuba ya Oman nje ya pwani ya Iran. 

Kwa mujibu wa Wamiliki hao wamesema hata hivyo kuwa meli hizo zimelengwa katika mashambulizi hayo huku Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif amesema mashambulizi hayo yaliyoripotiwa wakati Waziri Mkuu wa Japan anafanya ziara nchini humo kwa kiasi kikubwa yanatia shaka. 

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe alikutana na Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, akitafuta kupunguza hali ya wasi wasi kati ya Iran na Marekani. 


TFDA yakabiliana na Sumukuvu kupitia Maabara ya Kisasa ya uchunguzi wa chakula

$
0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema inayo maabara ya kisasa ya upimaji wa usalama wa mazao ya Chakula ili kuondokana madhara yatokanayo na ulaji wa vyakula vizivyopimwa yakiwepo magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula vyenye Sumu kuvu.


Aidha Mamlaka hiyo imejipanga kupambana na magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa vyakula hivyo ambayo yana athari kubwa kwa afya za binaadamu ikiwepo udumavu na vifo.


 Hayo yalibainishwa na Mkaguzi wa chakula Mwandamizi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA Dkt Analice Kamala wakati akiwasilisha mada juu ya uchafuzi wa Sumukuvu madhara yake kwa afya na jinsi ya kudhibiti katika Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi na Wahariri wa Habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Dkt Kamala alisema alisema maabara za kisasa za upimaji wa vyakula zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zina uwezo wa kisasa wa kubaini magonjwa au vimelea vya fangas ambavyo huathiri vyakula hususa vilivyohifadhiwa kwenye maeneo yasiyo salama ikiwepo sehemu ya  unyevu unyevu,joto na wadudu wa nafaka.


“ Niwahakikishie tu watanzania wenzangu kuwa vyakula vinavyopimwa kwenye maabara hii ni salama, hakuna kinachopita hapa kikiwa na madhara, kitatupwa tu, tuzingatie usalama wa vyakula na tutumie vyakula vilivyopimwa alisema Dkt Kamala.


Aidha katika hatua nyingine Dkt Kamala aliwataka Wanawake wanaonyoshesha nchini kuwa waangalifu katika uandaaji na matumizi ya vyakula wanavyotumia ili kuepukana na madhara ya Sumukuvu iliyopo kwenye baadhi ya vyakula vya nafaka ambayo inadaiwa kuwa na madhara kwa binaadamu na wakati mwingine husababisha vifo.


Dkt Kamala alisema iwapo Mama anayenyonyesha atatumia vyakula vyenye sumukuvu anasababisha madhara makubwa kwa Mtoto ikiwepo Udumavu, Vifo na Magonjwa ambayo yanaathiri ukuaji wa mtoto.


“Wanawake wanaonyonyesha ni muhimu kuzingatia uandaaji wa vyakula kwani watoto hula vyakula hivyo kupitia kwenye Maziwa ya Mama na hivyo kuathiri mfumo mzima wa ukuajiälisema Dkt Kamala.


Aidha pia Dkt Kamala alisema ulaji wa mazao ya mifugo iliyotumia vyakula vilivyoathiriwa na sumu kuvu pia inaweza kuathiri afya za binaadamu.


Alisema Sumu kuvu inaathiri ini na Figo na kusababisha ugonjwa wa manjano na wakati mwingine kuvuja damu kwenye maeneo ya wazi,kuharisha na kuhisi kichefuchefu na dalili zake huanza kuonekana baada ya wiki mbili.


Ugonjwa huo kwa Nchini Tanzania ulilipotiwa na Wizara ya Afya Juni 13 mwaka 2016 Mkoani Dodoma ambapo ilibainika kuwepo kwa watu 68 kwenye familia 42 kuugua magonjwa yatokanayo na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu na kati yao watu 20 sawa na asilimia 30 walipoteza maisha.
Ofisa Mwandamizi wa Uchanganuzi wa Hatari zitokanazo na Chakula kutoka (TFDA) Dkt. Analice Kamara akifafanua moja ya Mada kuhusu Madhara ya Sumu kuvu mbele ya Waandishi wa Habari katika kikao kazi  cha  kuwajengea uwezo waandishi na wahariri wa Habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula ,iliyofanyika  leo katika ukumbi wa  Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 

Meneja Mawasiliano na  Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) , Bi. Gaudensia  Simwanza akifafanua jambo katika kikao kazi cha kuwajengea uwezo waandishi  wa habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika katika ukumbi wa   Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa  Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

TIBA RADIOLOJIA YAWAFIKIA WAGONJWA WA FIGO,KINA MAMA WENYE UVIMBE KWENYE KIZAZI

$
0
0

Mtaalam wa Tiba Radiolojia (Interventional Radiology) wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Erick Mbuguje (mwenye kofia ya bluu) na wenzake wa MNH wakifuatilia jinsi mtaalam wa Tiba Radiolojia kutoka Marekani, Dkt. Michelle Maneevese anavyomwekea mgonjwa wa figo mpira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) ambao unamsaidia mgonjwa kusafisha damu (renal dialysis). Wataalam wa Tiba Raidolojia (Interventional Radiology) MNH wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Tiba Ridolojia kutoka vyuo vikuu vya Emory na Yale Marekani na hospitali iliyopo Buffalo New York. Wataalam hao kutoka Marekani wanaongozwa na Dkt. Janice Newsome wa Chuo Kikuu cha Emory.Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Flora Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanzishwa kwa huduma mpya ya kutibu uvimbe kwenye kizazi (uterine fibroids) kwa kutumia njia ya kisasa ya Tiba Radiolojia (interventional radiology) na kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) kwa wagonjwa wa figo ambao wapo kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au kwa wagonjwa wanaopatiwa tiba ya saratani. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani, Dkt. Dkt. Janice Newsome na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo wa MNH, Dkt. Jonathan Mngumi.Baadhi ya wataalam wa MNH na Chuo Kikuu cha Yale na vyuo shiriki vya Emory na Dartmouth) nchini Marekani wakimsikiliza Dkt. Lwakatare wa MNH.Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani, Dkt. Janice Newsome akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kutoa huduma ya tiba radiolojia kwa wagonjwa mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wataalam wa MNH. 
………………… 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanzisha huduma mpya ya kutibu uvimbe kwenye kizazi (uterine fibroids) kwa kutumia njia ya kisasa yaTiba Radiolojia (interventional radiology). 

Pia, MNH imeanzisha huduma mpya nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu (permanent catheter insertions) kwa wagonjwa wa figo ambao wapo kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au kwa wagonjwa wanaopatiwa tiba ya saratani. 

Wataalam wa MNH kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Yale na vyuo shiriki (kama Emory, Dartmouth) vya nchini Marekani wako kwenye programu maalum ya mafunzo ya tiba Radiolojia tangu Octoba mwaka 2018 hospitalini hapa. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa MNH, Dkt. Flora Lwakatare amesema mgonjwa mwenye uvimbe kwenye kizazi anaingiziwa mpira wenye chembechembe maalum kwenye mishipa ya damu na kwenda kuziba mishipa inayopeleka damu kwenye uvimbe. 

“Baada ya mishipa kuziba uvimbe unakosa damu au chakula chake na hivyo kusinyaa na kufa kabisa. Hivyo basi mama mwenye uvimbe kwenye kizazi endapo anapatiwa tiba hii hakuna haja ya kumfanyia upasuaji kubwa wa kuondoa uvimbe,” amesema Dkt. Lwakatare. 

Dkt Lwakatare amesema faida ya kutumia njia hii ya kisasa, inamsaidia mgonjwa kutofanyiwa upasuaji mkubwa na pia inampunguzia gharama za matibabu na kuondoa hatari yoyote kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji mkubwa. 

Akizungumzia huduma nyingine ya kuweka mipira maalum kwenye mshipa mkubwa wa damu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na figo, Dkt Lwakatare amesema huduma hii inawanufaisha wagonjwa wa figo ambao wako kwenye mfumo wa kusafisha damu (renal dialysis) au wanaopatiwa tiba ya saratani. 

Amesema tiba hii inaondoa usumbufu wa kutumia mishipa midogo ya mikononi ambayo mara nyingi ni ngumu kupatikana hasa kama inatumika mara kwa mara na kwa muda mrefu. 

“Tiba hii inafaida kubwa kwa kuwa inawezesha kuepeuka upasuaji mkubwa ambao una vihatarishi (risk), kuepeuka mgonjwa kukaa hopsitali kwa muda mrefu na wanaofanyiwa tiba radiolojia mara nyingi wanaweza kurudi nyumbani siku hiyo hiyo, hivyo inapunguza gharama kwa mgonjwa na Hospitali kwa ujumla,” amesema. 

Hivyo kujengewa uwezo kwa watalaam wa ndani itasadia kwa kiwango kikubwa kukuza huduma hii hapa nchini ambapo watalaam kutoka Hospitali za hapa nchini watapata fursa ya kujifunza kwa gharama nafuu na kuongeza idadi ya watoa huduma mikoani. 

Naye Daktari Bingwa wa Tiba Radiolojia wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani, Dkt. Janice Newsome amesema tiba radiolojia inahitaji ubunifu na kutoa huduma kwa kushirikiana. Dkt. Janice Newsome amesema wametoa mafunzo ya kutoa huduma ya tiba radiolojia kwa wataalam wa MNH na kwamba wao wamejifunza mambo mbalimbali kupitia wataalam wetu. 

“Kuwekeza kwa wataalam ni jambo muhimu na zuri kwa kuwa kazi ya kutoa huduma inahitaji kushirikiana,” amesema Dkt. Newsome. Katika mafunzo haya ya awamu ya nne, wataalam 13 wa MNH wakiwamo madaktari, wauguzi na mafundi sanifu wamepatiwa mafunzo sambamba na kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa mbalimbali. 

Mafunzo na huduma za tiba radiolojia zinazotolewa MNH ni mfululizo wa programu mbalimbali za tiba radiolojia yayolianza Novemba 2017 ili kujenga uwezo kwa wataalam wa MNH. Tangu kuanzishwa kwa huduma hii, wagonjwa 339 wamepatiwa huduma ya kibingwa ya tiba radiolojia na wengi ni wagonjwa wenye uvimbe kinywani.

BRAC YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAKUTANISHA WATOTO ZAIDI YA 600 WILAYANI TEMEKE

$
0
0

* Jamii yashauriwa watoto wanakuwa salama kwa kupiga vita vitendo vya unyanyasaji

Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii
KATIKA kuelekea kilele cha siku ya mtoto wa Afrika inayofanyika kila tarehe 16 Juni kila mwaka shirika la maendeleo la  BRAC Tanzania limeadhimisha siku hiyo kupitia mradi wake wa elimu ya makuzi na malezi kwa watoto unaojulikana BRAC Play Lab.

Akizungumza katika hafla hiyo Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Temeke Eva Komba amesema kuwa shirika hilo limekuwa msaada mkubwa sana katika suala zima la malezi na kuwataka wazazi wahudhurie semina za mafunzo kuhusiana na malezi ya watoto.

Amesema kuwa Play Lab zilizoanzishwa kwa ajili ya malezi wazazi wazitumie kwa kuwapeleka wao ili wapate kujifunza kupitia  huku akihaidi kuwa serikali itazidi kutoa ushirikiano kwa mashirika hayo.

Aidha amewataka wadau mbalimbali wa namna hiyo kushiriki katika shughuli za kijamii hasa elimu na afya.

Kwa upande wake wake Meneja programu ya elimu Suzan Bipa amesema kuwa  mradi huo wa BRAC unaotumia michezo unafadhiliwa  na mfuko wa maendeleo wa LEGO na ni moja ya miradi bunifu ya maendeleo ambayo unahudumia watoto wa umri wa miaka 3 hadi 5 kutoka familia maskini kwa kuhakikisha wanapata elimu ya awali.

"Sisi kama BARC kila siku ni sherehe ya mtoto wa Afrika kwa sababu programu mbalimbali ambazo sisi tunazitekeleza nchini ni endelevu na siku zote tunalenga kuhakikisha watoto wanalindwa, wanatunzwa na kuendelezwa" ameeleza Suzan.

Amesema kuwa mipango yao inalenga kuwawezesha wanawake ambao ni walezi wakuu wa watoto na wao wataendelea kuchangia majukumu muhimu ya maendeleo ya watoto.

Aidha amesema kuwa mafanikio ya mradi huo umetokana na ushirikiano bora  toka kwa wazazi na walezi katika suala zima la malezi ikiwemo utunzaji wa usalama kwa watoto pamoja na haki zao.

Vilevile ameeleza kuwa mradi huo wa Play Lab BRAC ulichaguliwa kutumika kutokana na mtindo wake uliokuwa wa ubunifu wa kujifunza ambao unatoa fursa ya mafunzo kwa watoto walio katika mazingira magumu kwa kuwapa mafunzo bora yenye gharama nafuu.

Kuhusu rasilimali zitumikazo kwa watoto hao Suzan ameeleza kuwa wazazi wamekuwa wakishiriki kwa karibu katika kutengeneza vifaa vinavyotumika katika Play Lab hizo na pia kusaidia walimu wakati wa darasa.

BRAC nchini inatekeleza mradi wa Play Lab katika Mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam na hadi sasa watoto 1200 wanapata mafunzo hayo na tangu kuanza kwake zaidi ya watoto 2400 wamemaliza mafunzo hayo kupitia vituo 80 vya Play Lab.

Imeelezwa kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006 zaidi ya watu milioni 4.13 katika Mikoa 25 wamefikiwa ikiwa ni pamoja na uwezeshaji wa mipango mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu, biashara ndogondogo, kilimo na chakula na hiyo yote ni kwa malengo ya kupunguza umaskini.

Licha ya miradi hiyo kwa watoto BRAC inasaidia watoto wa kike walioacha shule kwa sababu za mimba za utotoni na kukosekana kwa ada kwa ajili ya masomo yao kwa kuwapa mitaji na mafunzo mbalimbali.
 Meneja wa programu ya elimu BRAC Suzan Bipa akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambapo ameeleza kuwa wataendelea kuwa karibu na wazazi ili azma ya kuwasaidia watoto itimie, leo jijini Dar es Salaam.
Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Temeke Eva Komba akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambapo amesema kuwa serikali ipo pamoja na itaendelea kushirikiana na mashirika ya namna hiyo, leo jijini Dar es Salaam.


 Watoto wakionesha shughuli mbalimbali ambazo ni zao la waliofundishwa kupitia Play Lab ya BRAC, leo jijini Dar es Salaam.

 Watoto wakiwa na uongozi wa BRAC wakikata keki wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Afrika yaliyofanyika katika viwanja vya Bandari, leo jijini Dar ea Salaam.
Uongozi wa BRAC wakiwalishwa keki na watoto wakati wa maadhimisho hayo, leo jijini Dar es Salaam.

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, itashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 17 hadi 22 Juni 2019. Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma.


Wakati wa maadhimisho hayo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeandaa madawati maalum ya kutoa huduma kwa wananchi katika Ofisi za Wizara zilizopo Kata ya Mtumba jijini Dodoma na zile zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).


Huduma zitakazotolewa ni pamoja na kusikiliza na kutoa ufafafanuzi wa hoja mbalimbali za wananchi kuhusu Wizara pamoja na kutoa elimu kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika.


Madawati hayo yatakuwa wazi kuanzia saa 1.30 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.



NYOTE MNAKARIBISHWA.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

14 Juni 2019





TAARIFA MUHIMU KWA UMMA KUHUSU KUPIGA MARUFUKU MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha Umma wa Watanzania kuwa Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko ya Plastiki za Mwaka 2019 zimeanza kutekelezwa kuanzia tarehe Mosi Juni 2019.

Baada ya kuanza kwa utekelezaji wa Katazo la Kutumia mifuko ya Plastiki baadhi ya wazalishaji na wasambazaji wamebadilisha mifuko laini ya plastiki isiyokuwa na mishikio na kuitumia kama vibebeo vya bidhaa. Hii ni kinyume na kanuni ya 8 ya Kanuni tajwa hapo juu.

Kanuni ya 9 inatoa msamaha kwa baadhi ya vifungashio vya plastiki kwa ajili ya huduma za afya au ambavyo vinatumika kwenye kufungashia bidhaa za viwandani au sekta ya ujenzi au sekta ya kilimo au vyakula au usafi na udhibiti wa taka. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaandaa viwango vya Vifungashio hivi ambavyo vitaainisha kiwango cha unene na uwekwaji wa lakiri na kutambulisha bidhaa iliyofungashwa kabla ya kuuzwa.

Ofisi ya Makamu wa Rais inautahadharisha Umma kuwa ni makosa kisheria kubadili matumizi ya vifungashio hivyo kuwa mifuko ya kubebea bidhaa. Adhabu stahiki zitatolewa kwa watengenezaji, waingizaji, wasambazaji na watumiaji wa vifungashio vya plastiki vilivyozalishwa ama kuingizwa nchini na kutumika kama vibebeo vya bidhaa.

Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira ni jukumu letu sote.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

14/06/2019

PROF. KABUDI AMUAGA BALOZI WA INDIA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimpa zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro na Mbuga ya Wanyama Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sandeep Arya. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sandeep Arya (wa pili baada ya aliyevaa tai nyekundu) jijini Dar Es Salaam. Mhe. Waziri alimuandalia chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mhe. Balozi. Katika chakula hicho, Prof. Kabudi alishukuru misaada ya maendeleo inayotolewa na Serikali ya India katika sekta mbalimbali zikiwemo za maji, elimu, nishati na afya. Mhe. Waziri pia alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa Serikali itatoa ushirikiano kwa Balozi mpya atakayekuja kuchukua nafasi yake nchini. 
Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini (wa pili kutoka kulia) akiwa na ujumbe wake wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Prof. Kabudi akiwa na ujumbe wake wakati wa chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini. 
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images