Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

Introducing "BOSS" Official Video by Christian Bella feat Hamisa mobetto


SHUKURANI

0
0

Sisi, familia ya marehemu Prof. Robert B.M. Mabele, tunatoa shukurani za dhati kwa wote walioshiriki nasi tangu kumuuguza, kutwaliwa, maombolezo, na hatimaye kumpumzisha mpendwa wetu Prof. Robert B. Mabelle, “Kaka Bob” au “Uncle Bob” kama alivyojulikana na watu wake wa karibu, katika nyumba yake ya milele, makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.  
Tunathamini ushiriki wenu wa hali na mali katika kufanikisha kumpumzisha mpendwa wetu kwa heshima zote alizostahili.
Tunatoa shukurani maalum kwa wafanyakazi hospitali ya serikali Iringa, hospitali aliyokuwa akitibiwa huko India, na hospitali za TMJ na Muhimbili (Mloganzila), Dar es Salaam kwa juhudi walizozifanya kujaribu kuokoa Maisha ya mpendwa wetu. Pia tunawashukuru jamii ya vyuo vikuu vya Ruaha (RUCU) na Dar es Salaam (UDSM) kwa ujumla wao, Uongozi wa kanisa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, marafiki na wote waliosoma na kufanya kazi na mpendwa wetu katika maeneo mbali mbali, pia ndugu, marafiki na majirani wa ukoo wa Mabele katika ujumla wao kwa kujitoa kwenu kwa moyo katika kufanikisha yote kwa ajili ya safari ya mwisho ya mpendwa wetu, MUNGU awabariki sana.
Hatuwezi tumshukuru mtu mmoja mmoja, lakini kwa heshima kubwa tunawaomba wote mtambue shukurani hii kwenu.
Tutafarijika sana kwa uwepo wenu katika MISA YA SHUKURANI itakayofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Anna, Hananasif Kinondoni, siku ya Jumamosi, Juni 15, 2019 saa nne kamili asubuhi na kufuatiwa na chakula cha mchana nyumbani kwa Bw. na Bibi Charles Yanga, Tabata Chang’ombe, Dar es Salaam.
"BWANA akubariki, na kukulinda; BWANA akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; BWANA akuinulie uso wake, na kukupa amani.”
 Hesabu 6:24-26
"Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake." 
Zaburi 116:15

 FAMILIA YA MABELE

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 13.06.2019

Matukio Katika Picha Uwasilishwaji Mapendekezo Bajeti Kuu ya Serikali

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akionyesha Mkoba unaowakilisha Bajeti Kuu ya Serikali alipowasili katika viwanja vya Bunge leo jijini Dodoma tayari kwa ajili ya kuwasilisha Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Dotto James (kulia) wakifuatiliana Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Katibu Mkuu Kiongozi (kushoto) na Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mizengo Pinda wakisoma vitabu vya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 wakati ikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (hayupo pichani) leo Bungeni jijini Dodoma. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akipitia kitabu cha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 wakatiikiwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango leo Bungeni jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba na Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. Baadhi ya Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatiliana Hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango akiwasilisha Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo jijini Dodoma. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Dktt. Phillip Mpango (kulia) mara baada ya kuwasilisha Hotuba yake ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 leo Bungeni jijini Dodoma.Anayeshuhudia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji. Serikali imewasilisha mapendekezo ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020. (Picha na: Frank Shija)

HAPPY BITHDAY PRESIDENT FELIX TSHISEKEDI

0
0
Rais Dkt.Magufuli amumwandalia mgeni wake Rais Felix Tshisekedi keki ya Birthday ampongeza kwa kusherekea miaka 57 ya kuzaliwa akiwa nchinimTanzania Wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia Ikulu Jijini Dar es salaam. June 13, 2019 
Rais Dkt.Magufuli akimtumbuiza mgeni wake Rais Felix Tshisekedi akiwa na Wanamuziki Christian Bella, King Kikii na Christina Shusho mara baada ya kumpa keki ya Birthday na kumpongeza kwa kusherekea miaka 57 ya kuzaliwa akiwa nchinimTanzania Wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia Ikulu Jijini Dar es salaam. June 13, 2019

NMB YAZIPIGA TAFU S/M LIWITI, KITUO CHA AFYA GAIRO

0
0


Mkuu wa wilaya ya Urambo,Angelina Kwingwa akipokea madawati na vifaa vya afya kwa naiba ya shule ya msingi ya Vumila kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Magharibi,Sospeter Magesse. Benki ya NMB izipiga tafu shule na vituo vya afya kwa wiki hii ikiunga mkono jitihada za Serikali kuboresha Sekta za Elimu na Afya. 


……………………….

KATIKA kuunga mkono jitihada za Serikali kuboresha Sekta za Elimu na Afya, Benki ya NMB imekabidhi mabati 180 kwa Shule ya Msingi Liwiti, iliyoko Tabata, Dar es Salaam, huku ikitoa msaada wa vifaa katika Kituo cha Afya Gairo, mkoani Morogoro vyote vikiwa na thamani ya Sh. Mil. 20. 

Hafla za makabidhiano hayo zimefanyika kwa nyakati tofauti jana, ambako Shule ya Msingi Liwiti imekabidhiwa mabati ya kuezekea madarasa matatu, yakiwa na tahamni ya Sh. Mil. 5, wakati Kituo cha Afya Gairo kikipokea mashuka 62, vitanda vya kulala wagonjwa vitano na magodoro yake. Pia benki hiyo wilayani Urambo imekabidhi Kituo cha afya cha Uyoga vifaa vyenye thamani ya millioni tano pamoja na madawati kwa ajili shule ya msingi ya Vumila. 

Wakati msaada wa mabati kwa Shule ya Liwiti ukipokelewa na Mkuru
genzi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri, katika hafla iliyofanyika Liwiti shuleni, msaada mashuka, vitanda na magodoro vyenye thamani ya Sh. Mil. 5 kwa Kituo cha Afya Gairo, vilipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Seriel Mchemba.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mabati Liwiti Shuleni, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, alisema misaada wanayotoa katika Sekta za Elimu, Afya na Majanga, inaongeza chachu ya benki hiyo kujiweka karibu na jamii, na kubaki kuwa kinara miongoni mwa taasisi zinazosapoti Serikali.
Badru aliongeza ya kwanza, misaada yao inatokana na utaratibu wa benki hiyo kupitia Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) kutoa asilimia moja ya faida yao ya mwaka baada ya kodi na kwamba mwaka huu wametenga kiasi cha Sh. Bilioni 1, ambako hadi sasa wametoa misaada inaayofikia Sh. Mil. 500. 

Kwa upande wake, Shauri aliishukuru NMB kwa namna inavyosaidia utatuzi wa changamoto za elimu na afya wilayani Ilala, huku akisema misaada ya hiyo katika mashule wilayani humo, imesaidia kukuza kiwango cha ufaulu, ambako mwaka uliopita ilikuwa ya nne kati ya wilaya 185, ikifaulisha wanafunzzi 21,000. 

Alibainisha ya kwamba, kupita misaada ya wadau muhimu kama NMB na ruzuku ya Mpango wa Elimu Bure wa Serikali ya Awamu ya Tano – unaowaingizia kiasi cha Sh. Mil. 70 kwa mwezzi (sawa na zaidi ya Sh. Mil. 800 kwa mwaka), matumaini yao ni kupandisha zaidi kiwango cha ufaulu wa sasa wilayani humo. 

Shauri aliongeza ya kwamba, ukiondoa misaada ya wadau kama NMB na ruzuku ya Elimu Bure, eneo lingine wanalotegemea kupata pesa za kutatuzi changamoto za elimu na kukuza ufaulu, ni pamoja na asilimia 30 ya mapato ya ndani ya wilaya hiyo, iliyokamilisha ujenzi wa shule mpya 10 (tano za Msingi na tano za Sekondari). 

Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mchemba, alisema kuwa kwa sasa wananachi wa wilaya hiyo wamepunguza kasi ya kupiga simu kwake na kutoa malalamiko juu ya huduma mbovu zilizokuwa zinatolewa na wahudumu wa Kituo cha Afya Gairo, tuhuma walizokuwa wakipata kwa miaka mitatu sasa kutoka kwa jamii. 

Akizungumza wakati wa kupokea msaada kutoka NMB, Mchemba alisema ku
wa, kwa sasa baada ya kukaa na watumishi hao hali imeadilika na inaweza kupita mwezi mmoja bila kupigiwa simu na wananchi kutoa malalamiko juu ya huduma zisizo bora na bila shaka mambo yamebadiliko kituoni hapo. 

Aidha, Meneja Mahusiano na Biashara za Serikali, Kanda ya Mashariki wa Benki ya NMB, Anneth Kwayu, alisema kuwa Kituo cha Afya Gairo kimekuwa kikipokea vifaa mbalimbali kutoka NMB kwa miaka mitatu mfulilizo, katika jitihada za benki hiyo kusaidia kupunguza changamoto za afya. 




Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Urambo, Angelina Kwingwa, akizungumza mapema jana kabla ya kupokea vitanda saba na mashuka ishirini na tano vyote vikiwa na jumla ya shilingi milioni tano kutoka benki ya NMB,ameipongeza benki hiyo kwa kupunguza adha za wagonjwa hasa wajawazito na watoto waliokuwa wakilala wawili hadi wanne kitanda kimoja.

WAZIRI WA VIWANDA NA UWEKEZAJI SUDAN KUSINI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA - SGR.

0
0
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Sudan Kusini  Ndugu Paul Mayomu atembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR kipande cha Daresalaam  - Morogoro, Ziara hiyo imefanyika hivi karibuniJune , 2019. 

Aidha, katika  ziara hiyo iliongozwa na mwenyeji wake  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, walipata fursa ya kuona maendeleo na hatua tofauti za ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR ukiwemo ujenzi wa stesheni kuu ya Daresalaam, madaraja, na utandikaji wa reli unao endelea maeneo  ya vingunguti jijini Dar Es Salaam. 

Waziri Mayomu ameipongeza Tanzania kwa kuamua kujenga Reli ya Kisasa - SGR ambayo ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi, viwanda na biashara katika Taifa na nchi jirani. 

Hata hivyo, Waziri Mayomu ameeleza kuwa reli hii itakapo kamilika itakuwa chachu ya maendeleo kwa nchi zote mbili pia itadumisha uhusiano katika sekta ya uchukuzi, viwanda na biashara kati ya Tanzania na Sudan ya Kusini.

Kwa upande wake, Waziri  Kamwelwe amempongeza waziri Mayomu kwa kuja Tanzania ambayo ni heshima kwa Taifa na kujionea maendeleo yanayofanyika katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi katika ujenzi wa reli ya kisasa ambayo ni chachu ya maendeleo baina ya nchi hizo mbili.

Waziri  Kamwelwe ameahidi kudumisha uhusiano kupitia reli ya kisasa hasa katika sekta ya viwanda, biashara na uchumi.
  

Washirika wa Maendeleo Kuchangia Asilimia 8 Tu ya Bajeti – Dkt. Mpango


MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 14,2019

WASTAAFU 10,000 WA PSSSF WALIOKUWA WANADAI MALIMBIKIZO YA PENSHENI YA MKUPUO NA ILE YA KILA MWEZI WALIPWA BILIONI 880

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) umefanya malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 880 kwa wastaafu elfu 10,000 ambao walikuwa wanadai malimbikizo ya pensheni ya mkupuo na ya kila mwezi, Meneja Kiongozi wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume amesema.

Amesema malipo hayo yamefanyika katika kipindi cha mpito kilichotolewa na serikali kuanzia Agosti 2018 hadi Februari 2019 hii ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu Mfuko huo uanze kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.

“Ili kuhakikisha PSSSF inatoa huduma bora na za haraka, imefungua ofisi mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na tunatoa wito sasa, kwa wale wastaafu takriban elfu 10,500 ambao bado taarifa zao hazijahakikiwa wafike kwenye ofisi zilizo karibu nao ili kukamilisha zoezi hilo muhimu linalofanyika kila mwaka.” Alisema Meneja huyo kiongozi wakati akizungumza na waendesha bloggers na waendesha mitandao ya kijamii kwenye ofisi za PSSSF, barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.

Alisema uhakiki wa wastaafu sio kitu kipya ingawa mwaka huu zoezi hilo lilionekana kama ni geni.

“Lengo la uhakiki ni kuupa Mfuko fursa ya kufanya malipo kwa wakati, usahihi na kwa mtu anayepaswa kulipwa kwani taarifa zinaweza kubadilika ikiwa ni pamoja na zile za kibenki huenda muhusika akahama kutoka benki moja kwenda nyingine, mabadiliko ya wategemezi lakini haka kifo pia.” Alifafanua Bi. Chiume.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (katikati), akisikilzia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mmoja wa bloggers katika kikao baina ya meneja huyo na wamiliki na waendeshaji wa blogu hapa nchini. Kikao hicho kilicholenga kujenga mahusiano na kuutambulisha Mfuko huo Mpya kwa wamiliki hao wa mitandao ya kijamii kilifanyika ofisi za PSSSF jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam Juni 13, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akizungumza.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, akizungumza.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi(kulia), akitoa maoni yake wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi. 
Bi. Eunice Chiume (kushoto), akimsikilzia Mwenyekiti wa Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN), Bw. Joachim Mushi (watatu kushoto), wakati wa kikao hicho.
Bi. Eunice Chiume, akisalimiana na Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network, (TBN) Bw. Joachim Mushi, wakati wa kikao hicho.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (watatu kushoto) na Afisa Uhusiano Mewandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wakwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Bloggers mara baada ya kikao hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Aipongeza Wilaya ya Nyasa kwa Kupata Hati Safi Miaka Mitano Mfululizo

0
0
Mkuu wa Mkoawa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme akihutubia Kikao cha Baraza La Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma jana akiwa katika ziara ya kikazi ya Siku moja Wilayani Nyasa 
(Picha na Ofisi ya DED Nyasa) 
…………….. 
Na Neto Credo- Nyasa 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Kwa kupata hati safi kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo. 

Akizungumza wakati akihutubia baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya hiyo lililofanyika jana katika Ukumbi wa Kepten John Komba uliopo mjini Mbamba-Bay ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya Siku moja. 

“Ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Za Serikali ni matakwa ya Kikatiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya mwaka 1977 na kufanyiwa marekebisho ya mwaka 2005 kanuni namba 10 ya sheria ya ukaguzi namba 11 ya mwaka 2008”. Alisisitiza Mhe Mndeme 

Aliongeza kuwa ukaguzi huo upo kisheria na ni haki ya Halmashuri kukaguliwa na isipokaguliwa ina haki ya kuhoji kwa nini hamjakaguliwa, kwani hoja zinawahusu wote yaani Madiwani na 
watendaji kwa vile Halmashauri ina undwa na pande zote mbili. 

Aidha alimpongeza Mhe. Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mhandisi Stella Martin Manyanya, Madiwani na Wataalam wote wa Wilaya ya Nyasa kwa kusimamia vema matumizi ya fedha za miradi na kupata Hati safi katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2017/2018, na kwa miaka mitano mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2017/2018. 

“Halmashauri hii imeshakaguliwa na CAG kwa miaka mitano kuanzia mwaka wa Fedha 2013/2014-2017/2018 katika kipindi hiki chote Halmashauri imepata Hati safi mara nne (4)na kupata hati yenye mashaka mara moja Hongereni sana kwa hati mnazoendelea kupata.haya ni matokeo ya utendaji kazi mzuri wenye mshikamano na ushirikiano.

Inapotokea mmefanya vizuri hata sisi viongozi katika ngazi ya Mkoa tunafarijika sana kuona Halmashauri zetu zinafanya vizuri. Pia niwakumbushe pia msibweteke na kuona mmefika mwisho bali kwa mwaka unaofuata mzuie hoja sio kuzalisha hoja”.Alisisitiza Mhe. Mndeme 

Katika Hatua nyingine Alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa Jimson Mhagama kwa kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyasa na kumtaka ashirikiane na Madiwani, Wataalumu na Wananchi ili Wilaya iweze kuwa na Maendeleo. 

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mh. Alto Komba alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kwa kufanya ziara ya siku moja Wilayani Nyasa na kuhudhuria Baraza la Madiwani na kusema kuwa wananyasa wamefarijika sana kwa ujio wake na wanamkaribisha siku nyingine akipata nafasi. 

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme alifanya ziara ya siku moja wilayani hapa na kuhudhuria kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa na kukagua Miradi Mitatu ya Maendeleo .Miradi hiyo ni Jengo Ofisi na nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Jengo la Hosteli ya wasichana katika shule ya Sekondari Limbo ,na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.

TAARIFA YA HALI YA UCHUMI WA TAIFA MWAKA 2018 NA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2019/20

MAKATIBU WA MAWAZIRI NA MAKATIBU WA NAIBU MAWAZIRI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUWAJENGEA UWEZO KIUTENDAJI

0
0
Mratibu wa Wasaidizi wa Viongozi, Bw. John Kiswaga akiwasilisha hoja kwa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
  Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akifungua mafunzo ya Makatibu wa Mawaziri na wa Naibu Mawaziri ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
 Baadhi ya Makatibu wa Mawaziri na wa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo yao ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wa Mawaziri na wa Naibu Mawaziri baada ya kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji yaliyofanyika jijini Dodoma leo. 

Makatibu wa Mawaziri na wa Naibu Mawaziri wamepatiwa mafunzo ya siku moja na Serikali ili kuwajengea uwezo kiutendaji.
Akifungua mafunzo hayo leo jijini Dodoma, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael amesema, watumishi hao wanapaswa kuzielewa vema Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo ya Utumishi wa Umma pamoja na mipaka ya kazi zao ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao.

“Mafunzo hayo yatawaongeza upeo na uelewa wa majukumu yao katika utendaji kazi.” Dkt. Michael amesisitiza.
Dkt. Michael ameongeza kuwa, serikali inaandaa utaratibu wa kuwa na mafunzo endelevu ya namna hiyo kwa Makatibu hao.
Aidha, Dkt. Michael amefafanua kuwa, serikali imeona kuna umuhimu wa kuandaa waraka na mwongozo utakaoonyesha stahili na majukumu ya Makatibu hao katika mizania moja kutokana na utofauti wa kiutendaji katika Wizara.

Naye, Mratibu wa Wasaidizi wa Viongozi, Bw. John Kiswaga amesema, mafunzo hayo yatasaidia kuwakumbusha umuhimu wa utekelezaji wa miongozo ya serikali ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya viongozi.
Mafunzo ya Makatibu wa Mawaziri na Makatibu wa Naibu Mawaziri yameandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa.

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAKABIDHI RIPOTI YA MAPENDEKEZO SHERIA YA UFILISI

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Balozi Augustine Mahiga amepokea ripoti ya mapendekezo ya sheria yaliyowasilishwa na Tume ya Kurekebisha Sheria hii leo Jijini Dodoma.

Akipokea taarifa hiyo Dkt Balozi Mahiga amefurahishwa kwa kazi nzuri iliyofanywa na Tume hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha kukamilika kwa mapendekezo ya sheria ya Ufilisi na nyingine zilizowasilishwa katika tume hiyo  ambazo ni sheria ya Ushahidi na ile ya Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro.

‘’Nimeridhishwa kwa kazi nzuri iliyofanyika kwani tunakwenda kupata sheria madhubuti itakayoendana na hali ya sasa na kusimamia kikamilifu misingi ya utawala bora’’. Alisema Balozi Mahiga.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe, Januari  Msofe amesema kuwa tume yake imefanya mapitio na utafiti wa kina kuhusu mifumo ya  Sheria zinazosimamia Ufilisi na kubaini mapungufu ya kisheria na kiutendaji ambao umeathili utekelezaji wa masuala ya hayo hapa Nchini.

Ameendelea kubainisha mapungufu hayo ni pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali za kisekta kama vile sheria ya Makampuni sura ya 212, sheria ya mabenki na taasisi za kifedha sura ya 342 , sheria ya vyama vya ushirika sura ya 211, Sheria ya bima sura ya 394, sheria ya mashirika ya umma Sura ya 57  na sheria ya usajili wa wadhamini sura ya 318 na hivyo kukosekana kwa sheria mahsusi inayosimamia jukumu la ufilisi pekee na kusababisha mkanganyiko kwa watumiaji kufanya maamuzi ya sheria ipi inaweza kutatua matatizo yanayowakabili.

Hata hivyo kuwepo kwa sheria hizo kumesababisha matatizo kwa wadai kutojua taratibu za kupata haki zao kwa wakati pamoja na kuwepo kwa taratibu ndefu zinazochelewesha mashauri ya ufilisi kumalizika kwa wakati mara baada ya taasisi au kampuni husika kufilisika.

Ameongeza kuwa Sheria zinazotumika hivi sasa zimepitwa  na wakati ambazo baadhi yake zinatoa adhabu na faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za ufilisi kwa mfano faini ya shilingi 200 kiasi ambacho hakiendani na kiwango cha uchumi na maisha ya sasa huku zikitambua njia moja tu ya mawasiliano ambayo ni  posta pekee huku ikiacha nyuma maendeleo makubwa upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Vilevile Ugumu wa taratibu za kisheria katika ufilisi wa makampuni ya nje yenye kampuni tanzu Tanzania na hivyo kuziachia kampuni hizo kutumia sheria za nchi zao na kusababisha tatizo la kiuchumi katika nchi yetu kutokana na sheria zetu kukosa nguvu ya kuyadhibiti makampuni hayo tofauti na nchi jirani ya Kenya na Uganda ambazo zimeweka sheria na taratibu nzuri za kufuata kwa makampuni ya nje yenye kampuni tanzu kwenye nchi zao.

Mapungufu ya sheria hizo pia kumesababisha Kuwepo kwa mamlaka na vyombo mbalimbali vinavyosimamia masuala ya ufilisi kama vile kuangalia mali za kampuni pale inapofikia hatua ya kufilisika na mahakama kuteua chombo au taasisi yoyote inayoshughulika na ufilisi badala ya Taasisi ya RITA ambayo kisheria ndiyo yenye mamlaka kisheria ya kuwa msimamizi na mratibu wa masuala yote ya ufilisi.

Hafla ya kukabidhi ripoti hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Watumishi wa Wizara ya katiba na sheria, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja Wizara ya Ardhi.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt,  Balozi Augustine Mahige akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya RITA Prof. Hamisi Dihenga ripoti  ya Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria hii leo Jijini Dodoma, wengine katika picha ni Katibu Mkuu  wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome (wa tatu kutoka kulia) na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA Emmy Hudson (wapili kutoka kulia).
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt,  Balozi Augustine Mahige akikabidhiwa ripoti kuhusu Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Januari Msofe hii leo Jijini Dodoma.
Kikao cha uzinduzi wa bodi kikiwa kinaendelea

Mawakala wa Tigo Pesa wajishindia mamilioni

0
0


Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Katikati) akiwa na washindi wa ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani Vicky Ibrahim (kulia) na Suleiman Hussein (kushoto) muda mfupi baada ya kuwakabidhi zawadi zao za fedha baada ya kuibuka washindi.

Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa mawakala wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni inayojulikana ‘Wakala Cash In Promotion’. Kushoto ni Suleiman Hussein na kulia ni Vicky Ibrahim wote wakiwa ni washindi wakubwa kutoka kanda ya Pwani. 
Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3.5 Suleiman Hussein ambaye ni mmoja kati ya washindi wakubwa wawili wa promosheni ya ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani. 
Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2.5 Vicky Ibrahim ambaye ni mmoja kati ya washindi wakubwa wawili wa promosheni ya ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani. 


==========  =========  ======== = =======

Zaidi ya mawakala 200 wa huduma ya Tigo Pesa, wamejishindia zawadi za fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 160 kwenye promosheni ya mwezi mmoja inayojulikana kama ‘Wakala Cash In Promotion’.

Promosheni hiyo ya nchi nzima iliyozinduliwa mwezi Mei mwaka huu, ililenga kuwahimiza Mawakala wa Tigo Pesa nchini kufanya miamala kwa wingi ili kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu.

Akiwakabidhi zawadi washindi wa promosheni hiyo, kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha alisema, kampuni ya Tigo inathamini juhudi kubwa zinazofanywa na mawakala na kuongeza kuwa promosheni hiyo ililenga kuwazadia mawakala kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.

“Kampeni hii siyo tu inaonyesha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye biashara lakini pia adhma yetu ya kugawana tunachokipata kutokana na biashara tunayofanya pamoja na wadau wetu. Promosheni hii ni fursa nyingine ya kuwazawadia mawakala wetu fedha taslimu na bonasi ambazo tunawaamini zitawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuendelea kufikisha huduma jumuifu za kifedha kwa wananchi wengi zaidi,” alisema

Kwa mujibu wa Pesha, pamoja na washindi wengine, washindi wawili wakubwa kutoka kila kanda walipatikana ambao ni Suleiman Hussein na Vicky Ibrahim kutoka Kanda ya Pwani, Peter Myovela na Stivin Katoto kutoka kanda ya Kusini, Anton Masawe na Athuman Mbwana kutoka kanda ya Kaskazini pamona na Harry Lwila na Joseph Kabeba kutoka Kanda ya Ziwa.

“Pamoja na washindi 2000 ambao wamejinyakulia zawadi mbali mbali za fedha taslimu kutokana na juhudi zao, tumepata washindi wengine wawili wakubwa kutoka katika kila kanda ambao kwa jumla wao ni 8 ambao wameweza kujishindia shilingi milioni 12 zaidi kutokana na jitihada zao. Tunawapongeza sana Mawakala wote ambao wamefanya vizuri na kujishindia zawadi na kwa wale ambao wahakuweza kushinda waongeze bidii ili waweze kuwa washindi katika promosheni zijazo,” alisema.

Akipokea zawadi ya shilingi milioni 3.5, Suleiman Hussein ambaye ni Wakala kutoka Kanda ya Pwani alisema “Napenda kuishukuru sana kampuni ya Tigo. Promosheni hii inaonyesha ni kwa kiasi gani sisi mawakala ni kiungo muhimu kwenye huduma nzima ya Tigo Pesa. Kuibuka mshindi kwenye promosheni hii ni rahisi sana kwa kuwa unahitajika kufanya kazi kwa bidii tu. Nawashauri Mawakala wenzangu wafanye kazi kwa bidi kwani Tigo Pesa inalipa,”

Vicky Ibrahim, Wakala aliyejishindia shilingi milioni 2.5 alisema amefurahi kuwa mshindi wa zawadi hiyo na kuwataka wanawake kuwa mawakala wa Tigo Pesa na wale ambao tayari ni mawakala kuwekeza zaidi na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa Tigo Pesa.

“Tigo Pesa imetuwezesha sisi wanawake kujiajiri na kuboresha maisha yetu. Nawashauri wanawake wenzangu kujiajiri au kujiongezea vipato vyao kupitia Tigo Pesa. Kwa kuwa Mawakala pia wanaweza kujishindia zawadi kupitia promoshei hii kama ambavyo mimi nilivyojishi,” alisema


TUME YA KUREKEBISHA SHERIA YAKABIDHI RIPOTI YA MAPENDEKEZO SHERIA YA UFILISI

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt, Balozi Augustine Mahige akikabidhiwa ripoti kuhusu Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe Januari Msofe hii leo Jijini Dodom 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt, Balozi Augustine Mahige akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya RITA Prof. Hamisi Dihenga ripoti ya Mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria hii leo Jijini Dodoma, wengine katika picha ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Sifuni Mchome (wa tatu kutoka kulia) na Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson (wapili kutoka kulia). 

****************************** 



Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Dkt Balozi Augustine Mahiga amepokea ripoti ya mapendekezo ya sheria yaliyowasilishwa na Tume ya Kurekebisha Sheria hii leo Jijini Dodoma. 

Akipokea taarifa hiyo Mhe, Dkt Balozi Mahiga amefurahishwa kwa kazi nzuri iliyofanywa na Tume hiyo pamoja na wadau mbalimbali waliofanikisha kukamilika kwa mapendekezo ya sheria ya Ufilisi na nyingine zilizowasilishwa katika tume hiyo ambazo ni sheria ya Ushahidi na ile ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. 

“Nimeridhishwa kwa kazi nzuri iliyofanyika kwani tunakwenda kupata sheria madhubuti itakayoendana na hali ya sasa na kusimamia kikamilifu misingi ya utawala bora’’. Alisema Balozi Mahiga. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe, Januari Msofe amesema kuwa tume yake imefanya mapitio na utafiti wa kina kuhusu mifumo ya Sheria zinazosimamia Ufilisi na kubaini mapungufu ya kisheria na kiutendaji ambao umeathili utekelezaji wa masuala ya hayo hapa Nchini. 

Ameendelea kubainisha mapungufu hayo ni pamoja na kuwepo kwa sheria mbalimbali za kisekta kama vile sheria ya Makampuni sura ya 212, sheria ya mabenki na taasisi za kifedha sura ya 342 , sheria ya vyama vya ushirika sura ya 211, Sheria ya bima sura ya 394, sheria ya mashirika ya umma Sura ya 57 na sheria ya usajili wa wadhamini sura ya 318 na hivyo kukosekana kwa sheria mahsusi inayosimamia jukumu la ufilisi pekee na kusababisha mkanganyiko kwa watumiaji kufanya maamuzi ya sheria ipi inaweza kutatua matatizo yanayowakabili. 

Hata hivyo kuwepo kwa sheria hizo kumesababisha matatizo kwa wadai kutojua taratibu za kupata haki zao kwa wakati pamoja na kuwepo kwa taratibu ndefu zinazochelewesha mashauri ya ufilisi kumalizika kwa wakati mara baada ya taasisi au kampuni husika kufilisika. 

Ameongeza kuwa Sheria zinazotumika hivi sasa zimepitwa na wakati ambazo baadhi yake zinatoa adhabu na faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za ufilisi kwa mfano faini ya shilingi 200 kiasi ambacho hakiendani na kiwango cha uchumi na maisha ya sasa huku zikitambua njia moja tu ya mawasiliano ambayo ni posta pekee huku ikiacha nyuma maendeleo makubwa upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano. 

Vilevile Ugumu wa taratibu za kisheria katika ufilisi wa makampuni ya nje yenye kampuni tanzu Tanzania na hivyo kuziachia kampuni hizo kutumia sheria za nchi zao na kusababisha tatizo la kiuchumi katika nchi yetu kutokana na sheria zetu kukosa nguvu ya kuyadhibiti makampuni hayo tofauti na nchi jirani ya Kenya na Uganda ambazo zimeweka sheria na taratibu nzuri za kufuata kwa makampuni ya nje yenye kampuni tanzu kwenye nchi zao. 

Mapungufu ya sheria hizo pia kumesababisha Kuwepo kwa mamlaka na vyombo mbalimbali vinavyosimamia masuala ya ufilisi kama vile kuangalia mali za kampuni pale inapofikia hatua ya kufilisika na mahakama kuteua chombo au taasisi yoyote inayoshughulika na ufilisi badala ya Taasisi ya RITA ambayo kisheria ndiyo yenye mamlaka kisheria ya kuwa msimamizi na mratibu wa masuala yote ya ufilisi. 

Hafla ya kukabidhi ripoti hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Taasisi, Watumishi wa Wizara ya katiba na sheria, Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja Wizara ya Ardhi.

ZAIDI YA ASKARI 300 WA JWTZ WAPATA MAFUNZO YA UCHUNGUZI WA KISAYANSI POLISI MAKAO MAKUU

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Silaha na Milipuko wa jeshi la Polisi Mrakibu Msaidizi wa Polisi John Mayunga akitoa elimuu kuhusu silaha na milipuko kwa askari wa Chuo cha Kijeshi Pangawe Morogoro walipofanya ziara ya mafunzo katika Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi iliyopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Zaidi ya askari 300 walipata mafunzo hayo hivi karibuni. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Hati wa jeshi la Polisi, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Maria Njenga akitoa elimu ya uchunguzi wa hati na maandishi kwa askari wa Chuo cha Kijeshi Pangawe Morogoro walipofanya ziara ya mafunzo katika Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi iliyopo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi. Zaidi ya askari 300 walipata mafunzo hayo hivi karibuni. Picha na Jeshi la Polisi.

WAFUGAJI KIMOTOROK WALIA NA HUJUMA

0
0
Baadhi ya wafugaji wa Mkoa wa Manyara, wanaolalamikia wafugaji kunyanyaswa sababu ya mifugo yao.

Diwani wa Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ezekiel Lesenga (Mardad) akizungumzia manyanyaso wanayopata wafugaji wa Kijiji cha Kimotorok.

……………….
WAFUGAJI wa Kijiji cha Kimotorok Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamelalamikia kitendo cha maofisa wa pori la akiba la Mkungunero kukusanya ng’ombe zaidi ya 2,000 na kuchukua picha ili ionekane wamekiuka agizo la kuingiza mifugo kwenye pori hilo.

Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Mardad) akizungumza na waandishi wa habari alisema wanalaani vikali kitendo hicho cha watumishi wa Mkungunero.

Lesenga alisema japokuwa ng’ombe hizo zaidi ya 2,000 hazikuchukuliwa na Mkungunero lakini vijana wanaochunga mifugo hiyo walipata hofu na kulikimbia eneo hilo.

Alisema kitendo cha baadhi ya watumishi wa Mkungunero kukusanya mifugo yao mbugani katika sehemu ambayo siyo hifadhi ni kosa kubwa kwani wanahofia kufanyiwa hujuma.

Alisema kitendo hicho kinataka kiwachonganishe wafugaji kwa serikali ili waonekane wanakiuka utaratibu wa agizo la Wizari ya Mifugo la kutoingiza mifugo hifadhini.

“Sisi tunamuunga mkono Rais John Magufuli ambaye amekuwa akiwasemea na kuwatetea wafugaji hivyo hatuwezi kuingiza mifugo yetu hifadhini kwa hiyo tunalaani vikali kitendo hicho,” alisema Lesenga.

Alisema wanatoa tahadhari kwa serikali kwani wao hawahusiki japo watu wachache wa Mkungunero wamekusanya mifugo hiyo ili wafugaji waonekane wamekiuka agizo la serikali.

“Tunamuomba mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti asikie kilio hiki cha wafugaji kwani tunataka kuhujumiwa na watumishi wachache wa Mkungunero wenye nia ovu,” alisema Lesenga.

Hata hivyo, meneja wa pori la akiba la Mkungunero, Khadija Malongo alikanusha vikali kutaka kufanyika hujuma kwa wafugaji wa eneo hilo la Kimotorok.

Malongo alisema bado wafugaji wa eneo hilo wanaingiza mifugo yao na kuchungia kwenye pori la akiba la Mkungunero.

Alisema wao wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria, ila wafugaji wa kijiji cha Kimotorok bado wanaingiza mifugo yao kwenye pori la akiba la Mkungunero, japokuwa wamekuwa wakiwapa elimu ya kuzingatia hilo.

Kampuni 11 za Uturuki zatafuta fursa za Uwekezaji

0
0



Ujumbe wa kampuni 11 kutoka Uturuki upo nchini kwa ajili ya kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji, hususan kwenye sekta ya viwanda vya dawa za binadamu, vifaa vya maabara, vyombo vya ndani, vifaa vya umeme, ujenzi pamoja na ununuzi wa korosho.

Ziara hiyo imetokana na uratibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF).

Ujumbe huo ambao uliwasili nchini tarehe 10 Juni 2019 ulishiriki mkutano (B2B) uliondaliwa na TPSF tarehe 11 Juni 2019. Katika mkutano huo pamoja na mambo mengine, wawakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda wa Uwekezaji (EPZA) na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) walitoa maelezo kuhusu kanuni, taratibu na mazingira ya kufanya biashara hapa nchini.

Ujumbe huo utatembelea Zanzibar tarehe 13 Juni 2019 na baadaye Dodoma kwa ajili ya kuangalia maonyesho ya masuala ya ujenzi. Ujumbe huo utaondoka nchini tarehe 16 Juni 2019 kurejea Uturuki.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Majadiliano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki yakiendelea katika ukumbi wa TPSF. Aliyesimama ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe Ali Davutoglu ambaye anatoa ufafanuzi kuhusu mazingira ya biashara Tanzania. 
Mwenyekiti wa TPSF, Bw. Salum Shamte (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa kampuni hizo za Uturuki, Bw. Ali Engiz. Wengine ni Bw. Godfrey Simbeye (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF na Mhe. Ali Davutoglu, Balozi wa Uturuki hapa nchini. 
Mwakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hassani Mwamweta (kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania. 

AWAMU YA TANO YA RAIS DKT MAGUFULI IPO KAZINI,YAFUFUA MRADI WA MAJI ULIOACHWA TANGU 1990,GEZAULOLE WILAYANI KIGAMBONI

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images