Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

YANGA KUKINUKISHA DIAMOND JUBILEE JIJINI DAR ES SALAAM JUNI 15, 2019


VOA SWAHILI: Duniani Leo June 12th, 2019

Karigo afunguka hakuna uyanga na usimba/Taifa Stars kupeperusha bendera ya Tanzania AFCON

Masoud Kipanya:Wachora katuni hatupendwi/Magufuli ni Rais wangu nampenda...

KIPINDI MAALUM CHA RAIS DKT. MAGUFULI NCHINI AFRIKA KUSINI, NAMIBIA NA ZIMBABWE

Loss Report ya Polisi kuanza kulipiwa kwa njia ya Mtandao

$
0
0
Mtakumbuka kuwa Serikali ilitoa maelekezo kwa Taasisi zake  zinazohusika na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali waanze kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya kieletroniki yaani Government eletronic-Payment Gateway (GePG). Jeshi la Polisi nchini, katika kutekeleza maagizo hayo lilishaanza kupokea malipo kwa njia ya kieletroniki kwa malipo ya tozo ya makosa yanayotokana na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani kwa kutumia mashine za POS.  
Katika kuendelea kutekeleza maagizo hayo ya Serikali ya kupokea malipo kwa njia ya kieletroniki ili kuhakikisha pia tunaendana na muda uliotolewa,  Jeshi la Polisi kuanzia tarehe 8/05/2019 lilianzisha  mfumo wa kukusanya malipo kwa ajili ya kulipia taarifa ya kupotelewa mali ( Loss Report) kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kwa sasa mfumo huu ambao unapatikana kwenye mtandao kupitia tovuti ya  https://lormis.tpf.go.tz  umeenea nchi nzima. Lormis ni kifupi cha Loss Management Information System.  Jeshi la Polisi limeanzisha tovuti hiyo ili kurahisisha huduma ya loss report kupitia mitandao ili kutekeleza maagizo ya Serikali kuwa ifikapo mwisho wa mwezi June, 2019 ukusanyaji wa maduhuli yote ya Serikali ufanyike kwa mfumo wa kieletroniki kupitia GePG.  
Mfumo huu ulioanzishwa na Jeshi la Polisi utamwezesha mwananchi kutoa taarifa za upotevu wa mali au nyaraka kwa kupitia mtandao na kuweza kupata loss report bila kufika Kituo cha Polisi, isipokuwa kwa anayetoa taarifa ya upotevu wa kitabu cha kumiliki silaha, kadi ya gari, hati ya kiwanja au shamba, huyu itamlazimu kufika kituo cha Polisi. Mwananchi anaweza kutoa taarifa ya kupotelewa mali au nyaraka kwa kutumia kompyuta au simu yenye internet.   
Taarifa hiyo inaweza kutolewa akiwa mahali popote pale ilimradi awe na kifaa cha kieletroniki chenye internet atakachotumia kutolea taarifa. Ili kutoa taarifa bila kufika kituoni inambidi mwananchi kutembelea tovuti ambayo nimeitaja awali ambayo ni https://lormis.tpf.go.tz inayopatikana kwa lugha ya Kiswahili na Kiingeleza. Akishaingia kwenye tovuti atabonyeza kitufe cha “ S a jili M a li I li y o p o t e a ” na ataendelea kujaza fomu  atakayoipata. Baada ya kujaza fomu hiyo atatakiwa kufanya malipo.    
    
Mfumo huu wa malipo wa Loss report unaowawezesha wananchi kulipa malipo hayo kupitia mfumo wa kieletroniki yaani Government electronic Payment Gateway (GePG) unapatikana kwenye mitandao yote ya simu na  kwenye mabenki.  Mwananchi anapojaza fomu ya Loss report kwenye mtandao atapata namba ya malipo (Control number) ambayo kupitia tovuti hiyo ya Polisi inaanzia na 99108 na kuendelea / kufuatiwa na namba nyingine. Endapo mwananchi ataamua kufanya malipo kupitia benki anachotakiwa ni kwenda  na  namba ya malipo (control number) na hapo  watamsaidia kufanya malipo. Kama mwananchi atatumia mitandao ya simu za mkononi atakapo andika kodi ya namba ya kufanyia miamala ya fedha ya kampuni ya simu, baada ya hapo atachagua namba 4(lipa bili), halafu  atachagua namba 5 (Malipo ya Serikali)na kisha ataingiza namba ya malipo (Control number) yake na kulipa kiasi cha Tsh 500/=  
Kwa wale wananchi waliopoteza laini za simu, kadi za benki  au vitambulisho na kujaza maombi yao kwa kutumia kadi zao za NIDA au namba ya NIDA  hawahitajiki kwenda Kituo cha Polisi kwani mfumo huu wa Loss report umeunganishwa na mfumo wa NIDA ambao una uwezo wa kuthibitisha  taarifa za vitambulisho hivyo moja kwa moja (online).Kwa maana hiyo mwananchi mwenye kitambulisho cha NIDA au namba na akawa amepoteza laini za simu ana uwezo wa kujaza fomu online na kupata loss report yake online.  Kwa wale ambao watatumia vitambulisho vingine na kujaza fomu ya loss report watahitajika kufika Kituo cha Polisi ili kufanya uthibitisho. Kufika Kituo cha Polisi ni kwa sababu zifuatazo:- Moja ni ili Polisi waweze kuthibitisha kwamba aliyetoa taarifa ni yeye kutokana na kwamba kitambulisho alichotumia hakijaunganishwa na hakitumiwi na watoa huduma wengi kama cha NIDA.   
Aidha, wengine wanaotakiwa kufika kituoni ni wale waliopoteza mali zikiwemo  vitabu vya  kumiliki silaha, kadi za gari na hati za nyumba au mashamba hizi zinahitaji uchunguzi wa Polisi ufanyike kabla ya Loss Report haijatolewa kwa mhusika. Pia ambao wanatakiwa kuendelea kutoa taarifa zao katika vituo vya Polisi ni wale ambao hawana simu au kompyuta zenye internet itakayowezesha kutoa taarifa ya kupotelewa na mali au nyaraka kwa njia ya mtandao (online).    
Kwa wananchi wa aina hii Wakuu wa Vituo na Wahasibu wameshapata mafunzo na maelekezo ya namna ya kuwahudumia. Mfumo huu wa kulipia kwa ya njia ya mtandao (online) na kupata loss report kama nilivyosema tulianza na Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, napenda kuwajulisha kuwa mfumo huu unatumika kwa nchi nzima sasa. Hivyo ninapenda kuwapa taarifa watoa huduma za mawasiliano kuwa kuanzia sasa wawape huduma wananchi wote wanaofika kwao wakiwa na Loss report ya kieletroniki.     
    
Watoa huduma pale watakapokuwa na mashaka wanaweza kuthibitisha/ kuhakiki kama Loss report ya mwananchi ni halali au ya kugushi kwa kutumia njia mbili:- Njia ya kwanza ni kutembelea tovuti ya loss report ya Jeshi la Polisi ambayo ni https://lormis.tpf.go.tz na kwenda kwenye kitufe cha “Angalia Ripoti yako” hapo ataingiza namba ya malipo (Control Number) ambayo atapewa na mwananchi pamoja na namba ya kitambulisho chake,  ripoti ikitoka itakuwa ni sahihi na isipotoka itakuwa ni ya kughushi.  
 Njia ya pili,   kwa wale watoa huduma ambao wana mifumo ya kieletroniki na wangependa  kujiunga na mfumo huu tunatoa Application Program Interface      (API) ambayo itaweza kuwaunganisha na hapo wataweza kuwahakiki wateja wao kwa njia ya kieletroniki bila ya kufika au kutembelea tovuti yetu. Ili kupata hii API wawasiliane na Mkuu wa TEHAMA wa Jeshi la Polisi kwa barua pepe gabriel.mkungu@tpf.go.tz, au incharge wa Kitengo cha mifumo ya TEHAMA (godfrey.kapinga@tpf.go.tz). Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi wote watumie mfumo huu kwani unaokoa muda na ni wa uhakika katika kufanya malipo ya Serikali kwa njia ya kieletroniki pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma ya loss report. 

  Imetolewa na: David A. Misime - SACP 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi.  
www.policeforce.go.tz    www.twitter.com/tanpol    www.facebook.com/tanpol  

The 3rd East African Bicycle Tour (Tour d’EAC 2019) SET FOR 1ST AUGUST TO 20TH SEPTEMBER 2019

$
0
0

The 3rd East African Bicycle Tour (Tour d’EAC 2019) themed “Integrate or Perish” is set for 1st August to 20th September 2019, with over 100 cyclists taking on an epic route of over 4,300 km around East Africa over a course of 50 days.

According to the Team Leader and Director of Campfire Logs Guild of Uganda, the lead organizer of the Bicycle Tour, Mr. John Bosco Balongo, the 3rd East African Bicycle Tour will be flagged off on 1st August 2019 at the Independence Monument in Kampala, Uganda by the 2nd Deputy Prime Minister and Minister of East African Community Affairs of the Republic of Uganda, Rt. Hon. Dr. A. M. Kirunda Kivejinja.

The aim of the Annual East African Bicycle Tour, code-named Tour d’EAC, is to promote the spirit of the East Africanness among the people of East Africa, promote tourism and business potential of the Community while enhancing the awareness of social and cultural peculiarities of people and places in the East African Community. The ultimate goal of the initiative is to bring the citizens of East Africa to own the integration process.

The East African Bicycle Tour is an expression of unity, oneness, togetherness, and peace. By riding through all the East African countries, the ties that bind East Africans together is renewed and strengthened. The event welcomes every East African from whatever part of the region to take part.

The route of the 3rd Bicycle tour will cover Kampala-Jinja-Malaba on the Ugandan side. On the Kenyan side, to will pass through Malaba-Eldoret-Nakuru-Nairobi-Kajiado to Namanga.

On the Tanzanian side, the tour will connect Namanga-Longido-Arusha-Moshi-Dar es Salaam-Chalinze-Morogoro-Gairo-Dodoma-Nzega to Tabora. From Tabora, it will pass through Using and enter Burundi through Mugina-Manyonvu border.

In Burundi, the tour will connect Rumonge-Bujumbura-Ngozi-to Rwanda border then to Kigali. From Kigali, the tour will pass through Ruhengeri to Kisoro-Kihihi-Mbarara then to Kampala. The Campfire Logs Guild is partnering with several persons/or organizations in the Partner States to undertake the 3rd EAC Bicycle Tour.

The Secretary-General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko has commended the organizers of this initiative led by Campfire Logs Guild of Uganda and said that the Tour d’EAC will go a long way to promote the EAC integration agenda.

“We have endorsed this event and written to the Permanent/Principal Secretary/Undersecretary in the Ministries responsible for EAC Affairs in the Partner States notifying and requesting them to support and assist the organizers to undertake this tour successfully in their respective territories”, asserted the Secretary-General.

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAWEKA MKAKATI WA UTOAJI MAFUNZO KWA WACHUNAJI WA NGOZI NCHINI

$
0
0
SERIKALI kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza kutoa mafunzo ya wachunaji wa ngozi wa machinjio mbalimbali nchini  ili waweze kuboresha kazi zao kwa  kutoa mazao bora ya ngozi zitakazo ingiza fedha za kigeni kutokana na mauzo ya nje , na kukuza uchumi wa taifa na kuanzishwa kwa Viwanda  vya ngozi.

Mkurugenzi wa Uzalishaji  Mifugo na Masoko kutoka Wizara hiyo, Dk Felix Nandonde alisema hayo wakati akifungua mafunzo  ya wachunaji wa ngozi wa machinjio ya Manispaa ya Morogoro.

Dk Nandonde alisema , Tanzania imekuwa ikipata kiasi kidogo cha fedha za kigeni kutokana na uharibifu wa ngozi licha ya kuwa ni nchi ya pili kwa uwingi wa mifugo Barani Afrika baada Ethiopia.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ,  kwa sasa Tanzania ina  ng’ombe milioni 32.2, mbuzi milioni 20 na kondoo milioni tisa,   na kwamba ngozi zote zingeweza kusimamiwa ubora wake na kuingia katika mfumo wa biashara ya ngozi  pato la Serikali na Wananchi lingeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Mkurugenzi wa Uzalishaji  Mifugo na Masoko kutoka Wizara hiyo alisema , kwa sasa   asilimia 50 ya uharibifu wa ngozi ikifanyika katika machinjio hasa wakati wa uchunaji.

Dk Nandonde a lisema , kutokana na mapungufu hayo,Wizara  imeamua kuja na mkakati mahususi juu ya mbinu mpya ili kuikwamua sekta ndogo ya ngozi ili na kuifanya itoe mchango mkubwa zaidi kwa kuwapa mafunzo maalumu wachunaji wa ngozi katika machinjio.

Hata hivyo alisema , kuwa kwa sasa sekta hiyo ya ngozi imekuwa ikitoa mchango katika pato la Serikali na mtu mmoja mmoja ambapo  kwa mwaka 2017/18 jumla ya  Sh  5,098,846,623 zilipatikana wakati Sh 5,254,388,808 zilikusanywa na Serikali katika kipindi cha Machi 2018/19 kutokana na kusafirisha ngozi na bidhaa zake nje ya nchi.

Naye Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa mazao ya mifugo,usalama wa chakula na lishe kutoka Wizara hiyo, Gabriel Bura alisema ,wameamua kutoa mafunzo hayo kwa Wachunaji ngozi kutokana na sheria ya biashara ya ngozi namba 18 ya mwaka 2008 inawataka kufanya hivyo na kisha baada ya mafunzo watapewa leseni ya uchunaji ngozi na kuweza kutambulika na Serikali.

Alisema kuwa kupitia sheria hiyo ya ngozi mambo mengi yanatakiwa kusimamiwa ikiwemo ya machinjio yoyote wakati wa kusajiliwa kuwepo kwa watalaam wenye mafunzo ya namna ya kuchuna ngozi na  ili kuhakikisha ubora wa ngozi unasaidia kuinua sekta ndogo ya ngozi.

Naye Afisa Mifugo mkoa wa Morogoro,Dk Gasper Msimbe alisema,  zaidi ya  Wachunaji wa ngozi 200 wa Manispaa ya Morogoro watapatiwa mafunzo hayo yenye lengo la kuwapa mbinu mpya za uchunaji ili kuhakikisha wanasaidia kupatikana kwa ngozi yenye ubora.

Mmoja wa wachunaji wa ngozi katika machinjio hiyo ya Manispaa ya Morogoro, Alex Chiboyi alisema, kupitia mafunzo hayo yatawezesha kuzalisha ngozi yenye ubora na kuongeza kipato chao.

Chiboyi ambaye anauzoefu wa miaka 20 katika uchunaji wa ngozi katika machinjio aliishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango huo unaoensa sambamba na utoaji wa leseni kwani zitawasaidia kuwepo na usimamizi mzuri na kuondokana na matapeli .
 Mkurugenzi wa Uzalishaji  Mifugo na Masoko kutoka Wizara  ya Mifugo na Uvuvi , Dk Felix Nandonde ( kushoto) akisisitiza jambo  alipokuwa wakifungua wakati  mafunzo kwa wachunaji wa ngozi wa machinjio ya ngozi  Manispaa ya Morogoro  na ( kulia) ni Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa mazao ya mifugo,usalama wa chakula na lishe kutoka Wizara hiyo, Gabriel Bura , na ( kati kati ) ni Afisa Mifugo mkoa wa Morogoro,Dk Gasper Msimbe.

 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wachunaji wa ngozi wa machinjio ya Manispaa ya Morogoro wakimsililiza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo.

 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wachunaji wa ngozi wa machinjio ya Manispaa ya Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja na  mgeni rasmi  baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo mjini Morogoro.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji  Mifugo na Masoko kutoka Wizara  ya Mifugo na Uvuvi , Dk Felix Nandonde  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mpango mkakati  wa wizara hiyo kuhusu  mafunzo kwa wachunaji wa ngozi wa machinjio ya ngozi  nchini.
( Picha zote na John Nditi).

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed amewataka wananchi kuendelea kuchangia damu kwa hiari kwani mahitaji ya damu salama nchini yamekuwa makubwa.

Amesema mahitaji ya damu kwa mwezi ni wastani wa chupa 1,550 kwa matumizi ya kawaida na watumiaji wakubwa ni mama wajawazito, watoto, wahanga wa ajali na wagonjwa wa upasuaji.

Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na siku ya wachangiaji damu duniani Ofisini kwake Mnazimmoja, Waziri Hamad alisema kutokana na wananchi wengi kuhamasika kutumia hospitali na vituo vya afya mahitaji ya damu yanaongezeka kwa kiasi.

Waziri wa afya alizipongeza taasisi na vikundi vya hiari vinavyojitokeza kuchangia damu kwa hiari katika mabonanza yanayoandaliwa na kitengo cha damu salama ambapo imekuwa msaada mkubwa katika hospitali na vituo vya afya.

Aliahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi za kijamii na vikundi mbali mbali vinavyojitolea kuchangia damu ili kuondosha tatizo la damu na kuokoa maisha ya wananchi.

Alisema lengo kuu la siku ya wachangia damu ni kuwapongeza, kuwajali na kuwahamasisha wachangiaji damu na kuwashajiisha wengine wapya ambao wanaweza kujitolea damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wengine.

Waziri wa Afya alikumbusha kuwa siku ya wachangiaji damu duniani ndiyo siku aliyozaliwa mvumbuzi wa makundi ya damu, Raia wa Australi Dr. Karl Landsteiner hivyo inapaswa kuenziwa.

Meneja Uhusiano na Uhamasishaji wa Kitengo cha damu salama Hamad Bakari Magarawa alisema maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila ifikapo tarehe 14 ya mwezi Juni kila mwaka kwa Zanzibar yatafanyika Mwanakwerekwe.

Amesema maadhimisho hayo yanafuatiwa na Bonanza kubwa la kuchangia damu linalofanyika maeneo tofauti na wananchi wametakiwa kujitokeza katika mabonanza hayo na siku ya kilele kwa lengo la kuchangia damu.

Hamad Bakari Magarawa alisema Kaulimbiu ya siku ya wachangiaji damu duniani mwaka huu ni ‘’Damu kwa wote’’.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika mkutano wa Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kuhusiana na Siku ya Wachangiaji Damu Duniani (WORLD BLOOD DONOR DAY)ambayo itafanyika siku ya Ijumaa 14/06/2019.hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba yake mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na Siku ya Wachangiaji Damu Duniani (WORLD BLOOD DONOR DAY)ambayo itafanyika siku ya Ijumaa 14/06/2019.hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid mohamed akitolea ufafanuzi baadhi ya maswala yalioulizwa na Waandishi wa Habari katika mkutano kuhusiana na Siku ya Wachangiaji Damu Duniani (WORLD BLOOD DONOR DAY)ambayo itafanyika siku ya Ijumaa 14/06/2019.hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja.
Meneja Uhusiano na uhamasishaji Damu Salama Hamad Bakar Magarawa akizungumza kuhusiana na Siku ya Wachangiaji Damu Duniani (WORLD BLOOD DONOR DAY)ambayo itafanyika siku ya Ijumaa 14/06/2019.hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara hio Mnazi mmoja. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

DKT. MPANGO AWASILISHA BUNGENI HALI YA UCHUMI (2018) NA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA (2019/2020)

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma, Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa pili kulia walioketi mbele) akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, Prof. Florens Luoga (kulia kwake) wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipoiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)  baada ya  kuwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiteta jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) mara baada ya Wizara kuwasilisha Bungeni Jijini Dodoma, Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb),  (kushoto), akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Bungeni Jijini Dodoma wakati Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) alipo wasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto alieipa mgongo kamera), akiwaongoza baadhi ya Mawaziri na Wabunge kumpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020 bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (katikati), akipongezwa na baadhi ya Wabunge nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kuwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020 bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na  familia ya  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, Prof. Florens Luoga (wa pili kushoto) baada ya  kuwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2019/2020. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2019/20

RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUWAPONGEZA WABUNIFU WA UMEME WA MAJI KUTOKA MKOANI NJOMBE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kuwakabidhi kifuta jasho cha shilingi milioni 5 wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute(Mzee Pwagu)  na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO, Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam  Juni 13, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwakabidhi kifuta jasho cha shilingi milioni 5 wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO, Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasindikiza baada ya kuwakabidhi kifuta jasho cha shilingi milioni 5  kuwakabidhi wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO, Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya kumbukumbu na wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo pamoja na Mkurugenzi Mkuu na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC, Makatibu wakuu wa Wizara ya Nishat, Elimu Sayansi na teknolojia, Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu na wataalamu kutoka TANESCO, Kamishna wa Umeme na Mkurugenzi Mkuu na Wataalamu wa COSTECH Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kuwakabidhi wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu)  na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita kuwapongeza na kuongea nao pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Rioba pamoja na Waandaji wa Kipindi cha Hadubini TBC,  Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwapongeza wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita  Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kuwapongeza wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita  Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahi na wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na Bw. Jailosi Ngairo aliowaita  Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019
 Mbunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) aliyepongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapongeza na mwenzake  Bw. Jailosi Ngairo aliowaita  Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019.
 Mbunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. Jailosi Ngairo aliyepongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapongeza na mwenzake Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) aliowaita  Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019.
 Mtangazaji wa Shirika la utangazajinTanzania TBC Tatu Abdalah kutoka Njombe akifuatilia kwa umakini tukio la kuwaponeza wabunifu wa Umeme wa Maji kutoka Njombe Bw. John Akane Mwafute (Mzee Pwagu) na mwenzake  Bw. Jailosi Ngairo waliopongezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Juni 13, 2019.
PICHA NA IKULU

PRINCE AMIGO AELEZA SAFARI YAKE KIMUZIKI ASIFU MALEZI BORA KUTOKA JAHAZI NA EAST AFRICAN MELODY

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii

 MKURUGENZI wa bendi ya taarab first classic modern, Abubakari soud (Prince Amigo)  amesema muziki wa taarab hautokufa na utaendelea kuwepo.

Amigo amesema kuwa muziki wa taarab ulianza zamani na utaendelea kuwepo kutokana na uwepo  wa mashabiki na wadau wa muziki huo wa mwambao.

"Waliopotea ni baadhi ya mashabiki na sio muziki wa taarab kwani waimbaji wakali bado wapona wanaendelea kuongezeka kila siku." ameeleza Amigo.

Aidha, ameeleza kuwa utofauti wake kwa sasa kuwa yupo kwenye utawala mpya ambao anafanya kazi akiwa Kama mkurugenzi na mmiliki wa bendi hiyo ya first classic modern taarab.

"Nilikua jahazi  na nililelewa vizuri ili niweze kukua kimuziki na ndio sababu kubwa imefanya nimeweza kuwa na uthubutu na kusimama imara na bendi yangu." Ameeleza.

Pia ameeleza kuwa tabia ya baadhi ya waimbaji wakike  kuponda uongozi walipotoka pindi wanapoahamia kwenye uongozi mpya kuwa si jambo zuri kwani inajenga uhasama baina ya muimbaji na uongozi wa awali ama kati ya bendi na bendi.

"Waimbaji wakike ndio wanaongoza kwa tabia hiyo hivyo wajifunze kuheshimu uongozi walipotoka  kwani binafsi nimefanya kazi bendi tofauti kama east Africa melody na jahazi hata baada ya kuondoka sikuwahi kuongea vibaya japo wote ni binadamu hakuna mkamilifu kuna matatizo mawili matatu" ameeleza Amigo.

Pia amesema kwa sasa anategemea kuzindua albamu yake mpya "mama wa hiyari"  aliyomshirikisha malkia wa mipasho khadija kopa.

Vilevile ametoa rai kwa wamiliki wa bendi za taarab kuwapa faraja wasanii wao na kushirikiana nao kwa hali na mali. "Kuwepo kwa mahusiano mazuri kati ya viongozi hadi kwa waimbaji ndipo kazi itafanyika kwa ufanisi na kuepusha minong'ono isio na tija" ameeleza.

DPO Group launches Africa’s first B2B Virtual and card

$
0
0
New DumaCard gives businesses in Africa access to new markets by enabling online payments regionally and internationally

DPO Group, a leading Payment Service Provider (PSP) in Africa, has just launched Africa’s first business to business payment card. DPO’s DumaCard, which is offered as a plastic card as well as in virtual form, is available initially to its 10,000 business customers in Kenya and Tanzania, with plans to roll the card out across the other 14 countries in which DPO Group operates.

Eran Feinstein, CEO, DPO Group commented, “This is an extremely exciting development particularly for businesses in Africa – the growth of which is critical to economic development. Our goal is to support the growth of businesses throughout Africa by allowing them to pay and be paid securely and effortlessly throughout the continent and internationally, ensuring that more organisations in Africa are financially included and have the same opportunity to transact online as elsewhere in the world. The DumaCard is another of our innovations enabling this.”


The announcement follows DPO’s partnership with Mastercard allowing DPO Group, in collaboration with banks, to be able to issue physical and virtual cards. Last year, Mastercard also enabled DPO Group to act as a Pan-African switch via Mastercard Payments Gateway Services, (MPGS) meaning it can independently authorise transactions with no need for bank integration.


The DumaCard can be used by merchants as a single or multiple-use card and can be topped up regularly using mobile money so users do not have to have a bank account in order to be able to use the card. As a multi-currency card, it can be used across Africa as well as internationally, and in local currencies. It can also be customised to allow merchants to pay single or multiple recipients. The company expects the DumaCard to be particularly popular amongst its travel partners (tour operators & airlines) who will use the card to pay international airlines and global distribution systems.


The virtual card, which is the first of its kind in Africa, provides merchants with a 16-digit card number, expiry date and security code linked to their DPO payments system. This offers vendors in Africa and across the world a flexible and secure way to pay. DPO has developed highly sophisticated, end-to-end fraud prevention and risk management systems, and holds PCI DSS Level 1 Certification in all 16 markets in which it operates.


In future, individuals will also have access to the DumaCard to make and receive payments for everything from household bills to entertainment subscriptions. For the first time,consumers will be able to use the card for shopping on online stores such as Amazon and Netflix, bringing consumers in Africa access to e-commerce opportunities previously unavailable to them. The card will be showcased at East Africa’s largest tourism fair, the Karibu Kilifair held in Arusha, Tanzania.


DPO’s goal is to provide all businesses with the option to transact effortlessly worldwide, and to support greater financial inclusion across the continent. DPO enables merchants to accept payments from all modes of payments, including mobile money, prepaid cards, debit and credit cards, and in all major currencies. The DumaCard is an additional solution on DPO’s payment platform, through which it aims to close the gap between merchants and their customers by providing businesses with the technology to support real-time payments through a single platform and using various modes of payment, including via virtual terminals, website integration and online invoicing.

RUFANI ZA WALIOCHOMA KITUO CHA POLISI BUNJU B ZASHINDWA KUSIKILIZWA BAADA YA MAJALADA YA WARUFANI KUCHANGANYWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
RUFAA dhidi ya washtakiwa watatu kati ya wanne waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi bunju imeshindwa kuanza kusikilizwa kufuatia majalada ya warufani hao kuchanganywa.

 Hali hiyo imetokea leo Juni 13, 2019  baada ya wakili wa Serikali, Sadah Mohamed kuieleza mbele ya Naibu msajili wa Mahakama Kuu, Crecensia Kisongo kuwa, rufaa hiyo leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mwenendo wa kesi (proceedings) alionao siyo za mrufani aliyekuwa mahakani hapo, bali anayo ya mrufani Abrahamu Minga.
"Mheshimiwa, tunaomba muongozo wa mahakama ili kufahamu nini kifanyike, rufaa iliyoko mbele yako ni ya mrufani Konzo ambayo mi sijaipata na si ya mrufani Minga niliyonayo" ameeleza wakili Saada.
 Wakili wa warufani hao Profesa Abdallah Safari amedai kuwa  hati ya wito (summons) aliyonayo yeye ni ya washtakiwa watatu ambao ni, Yusuph Sungu maarufu kama Mayuku ambaye leo hakuwepo mahakamani, Juma Konzo na Abrahamu Minga.

 Rufani hiyo imeahirishwa hadi Juni 17 mwaka huu.

Mwezi Februari mwaka huu,  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupitia hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, aliwahukumu kifungo cha maisha washtakiwa wanane baada ya kutiwa hatiani katika kesi ya kuchoma moto Kituo cha Polisi cha Bunju A ambapo 10 waliachiwa huru.

Waliohukumiwa ni Yusuph Sugu (40), Juma Kozo (32), Rashid Liwima (29), Baraka Nkoko (23), Abuu Issa (36), Abraham Mninga (23), Veronica Ephraem (32) na Ramadhan Said (22).

Walioachiwa huru ni Mrisho Majaliwa (30), Hamis Ndege (37), Seleman Gwae (33), Menge’nya Anthony (28), Rehema Hussein (32) Rajabu Ally (25), Ally Athuman (24), Amina Matipwili (33), Gubila Temba (51) na Mariam Honza (44).

Wanadaiwa Julai 10, 2015. Walichoma kituo cha polisi ambacho ni mali ya umma jambo ambalo ni kosa la kisheria.
 Warufani, Juma Konzo na Abrahamu Minga wakielekea mahakamani kusikiliza rufaa yao waliyokata baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa hatia ya kuchoma moto kituo cha polisi bunju, hata hivyo Rufaa hiyo imeahirishwa kufuatia majalada yake kuchanganywa.
Ndugu wa warufani hao wakimsikiliza wakili wa warufani hao, Profesa Abdallah Safari baada ya kesi hiyo kuahirishwa

NKASI YAJA KIMKAKATI ZAIDI/DC AAHIDI MAKUBWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Nkasi
 MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda amesema kuwa Wilaya yake imekamilisha ukarabaati wa kituo cha Afya cha Nkomolo na ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika katika Wilaya ya Nkasi kuripoti habari za miradi ya Maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi Rais Dkt.John Pombe Magufuli na kueleza kuwa miradi yote hiyo imejengwa kwa gharama za  sh.Bilioni Mbili.

" Hospitali ya Wilaya inajengwa kwa gharama sh. Bilioni 1.5 na kituo cha Afya Nkomolo kimejengwa kwa gharama ya sh. Milioni 500 ambacho kimekamilika na kitatoa huduma kwa sasa "Amesema Mtanda

Amesema kuwa mara baada ya kukarabati kituo hicho cha Afya wameweza kutoa huduma ya Upasuaji kwa watu sita kwa wakati mmoja jambo ambalo halikuwepo hapo awali.

"Kwa sasa tuna chumba cha kuhifadhia maiti na majokofu sita ambayo awali hayakuwepo na wakazi wa hapa walikuwa wanalazimika kutembea hadi Sumbawanga kwa ajili ya kuhifadhi maiti" ameeleza.

Aidha amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 1979 haikuwahi kuwa na chumba cha kuhifadhia maiti, lakini kutokana na jitihada za serikali ya awamu ya tano,Nkasi imeorodheshwa kati ya wilaya ambazo zimefaulu kwa kupiga hatua kimaendeleo ikiwemo sekta ya elimu na afya.

Amesema kuwa kuwa kwa kipindi chote hicho Wilaya hiyo ilikuwa haina Hospitali ya Wilaya lakini katika awamu hii ya tano chini ya Rais Magufuli, Nkasi imepata Hospitali mpya.

Mtanda amesema licha ya mafanikio hayo, Mganga Mkuu wa kituo cha afya Nkomolo Everada Sanane amesema bado kuna uhitaji wa watumishi kutokana na idadi ya wagonjwa inavyoongezeka na ameishukuru serikali kwa hatua ilizozipiga katika kuboresha sekta mbalimbali Wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda akizungumza na Waandishi wa Habari wakati kuhusiana  na   Miradi ya Maendeleo katika Wilaya hiyo  iliyofanywa katika Serikali ya awamu ya tano.
 Kituo cha Kituo cha afya kilichojengwa katika serikali ya awamu ya Tano na kutatua changamoto ya huduma za afya
 Mganga Mkuu wa Kituo Cha Afya Nkomolo,Everanda Sanane akieleza changamoto zinazopatikana katika kituo hicho wakati waandishi wa habari walipofika kituoni hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda akionyesha majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Nkasi inayojengwa kwa gharama za Bilioni 1.5.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda akizungumza na Mmoja wa Wagonjwa waliofanikiwa kupata matibabu katika kituo cha afya Nkomolo.

Onesho la tano la Utalii la Kimataifa nchini (SITE) kufanyika Oktoba

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
ONESHO la tano la  Utalii la Kimataifa nchini (SITE) linatarajiwa kukutanisha wadau wa utalii wa Kimataifa wa ndani  ya nchi zaidi ya 400.

Onesho hilo linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mliman city kuanzia Oktoba 18 hadi 20, mwaka huu utakaowakutanisha wadau wa utalii nchini na nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari  Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii (TTB), Devota Mdachi amesema washiriki wa maonesho hayo ni mawakala wa utalii wa Kimataifa, waandishi wa habari za utalii wa kimataifa na wafanyabiashsra wa utalii kutoka Tanzania na nchi za jirani.

Amesema washiriki hao wanatarajiwa kutoka nchi zaidi ya 57 Ulimwenguni na  baadhi ya nchi mashuhuri zinazotarajiwa kuleta washiriki ni Marekani, Uingereza, Italia, Ujerumani, Urusi, China, Sweden, Afrika Kusini, Seychelles, Mauritius, Rwanda, Malaysia, Kenya, Thailand, India, Korea ya Kusini na Singapore.

Mdachi amesema maonesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwani mwaka 2014 kampuni za uoneshaji utalii zilikuwa 40 na mwaka 2018 zimekuwa 152.

Pia amesema wauza safari wakubwa wa kimataifa kwa mwaka 2014 walikuwa 24 na mwaka 2018 walikuwa 335.

"Onesho hili la Swahili Expo limeendelea kupanua wigo wa maeneo ya vivutio vya utalii vya kutembelewa na mawakala wa utalii wa kimataifa ili kuwapatia elimu pana ya vivutio vya utalii," amesema Mdachi.

Ameongeza kuwa onesho hilo limeendelea kuwavutia wafadhili wengi zaidi kutokana na fursa zinazotolewa na onesho hili za kutangaza brand za wafadhili hao.

Amesema onesho hilo pia litakuwa na programu zitakazoongeza mvuto kwa kampuni za uoneshaji na wananchi watakaotembelea onesho.

"Imeandaliwa program maalum ya kuwasaili mawakala wa utalii wa Kimataifa kupitia Balozi za Tanzania, nchi za ng'ambo. Kupitia ushirikiano tunaopata kutokana ofisi zetu za Ubalozi wakitekeleza diplomasia ya uchumi hivyo mawakala tutakaopata watakuwa wenye tija kwa biashara ya utalii Tanzania," amesema Mdachi.

Onesho hilo ni mahusus kutoa fursa za kipekee kwa wakala hao kukutana na mawakala wa utalii wakubwa  pia kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogowadogo kuonesha bidhaa zao  utamaduni wa mtanzania kama vile sanaa za mikono, mavazi, vyakula vya kitanzania na ngoma.
Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Devotha Mdachi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho la tano la Utalii la Kimataifa litakalofanyika mwezi Oktoba baadae. Kushoto kwake ni Mratibu wa Onesho hilo la SITE 2019 Joseph Sendwa na  kulia ni Afisa uhusiano wa bodi hiyo Geoffrey Tengeneza,jijini Dar es Salaam.

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Job Ndugai akiongoza Mkutano wa Kumi na Tano kikao cha Arobaini na Tano leo tarehe 13 Juni, 2019 Bungeni Jijini Dodoma. Katika Mkutano huo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mipango alitoa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

aziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mipango akitoa taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2019/2020  leo tarehe 13 Juni, 2019 katika Mkutano wa Kumi na Tano kikao cha Arobaini na Tano Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (aliekaa) akizungumza na Mbunge wa Mlalo, Mhe. Rashid Shangazi leo tarehe 13 Juni, 2019 katika Mkutano wa Kumi na Tano kikao cha Arobaini na Tano Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Cpt. Mstaafu George Mkuchika (kulia) akizungumza na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi leo tarehe 13 Juni, 2019 katika Mkutano wa Kumi na Tano kikao cha Arobaini na Tano Bungeni Jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ikuwo kutoka Makete Mkoa wa Njombe (kulia), Wanafunzi wa Shule ya Msingi St. Joseph kutoka Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mkutano wa Kumi na Tano kikao cha Arobaini na Tano Bungeni Jijini Dodoma.

Watendaji Wakuu kutoka Wizara ya Fedha, Gavana wa Benki Kuu na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya fedha wakiwa katika jukwaa la Spika wakifuatilia taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 leo tarehe 13 Juni, 2019 katika Mkutano wa Kumi na Tano kikao cha Arobaini na Tano Bungeni Jijini Dodoma. Taarifa hiyo imewasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mipango

Register Now for next week's event. 2019 IT Annual Conference.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU BINGENI JIJINI

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula, Bungeni jijini Dodoma, Juni 13.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 13.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Geita, Joseph Musukuma, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 13.2019. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 13.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Kilimo, Omar Mgumba, kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 13.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, kwenye jengo la Utawala Bungeni jijini Dodoma, Juni 13.2019. Tokea kushoto ni Mbunge Nzega mjini Hussein Bashe, Mbunge wa Mtama Nape Mnauye, Mbunge wa Kahama mjini Jumanne Kishimba.
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images