Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT

0
0

VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE COMMONWEALTH SECRETARIAT


The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Adviser, Service Delivery and Reporting.


Application details can be found through the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Tuesday 18th June 2019.


“The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply”.


Issued by;

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Dodoma.

12th June 2019.




Bil. 32.5/= kuipamba bandari Kigoma, Ujenzi wa Gati la Ujiji na Kibirizi waanza kwa kasi

0
0


Na Humphrey Shai, Globu ya Jamii, Kigoma.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa Sh bilioni 32.5 kwajili ya mradi mkubwa wa ujenzi wa gati katika bandari ndogo za Ujiji na Kibirizi zilizopo Kigoma mjini.

Pia mradi huo unajumuisha ujenzi wa jengo la gorofa moja kwaajili ya ofisi za meneja wa bandari za ziwa Tanganyika.

Mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya China Railway 15 Group ulianza Februari 28, 2018 na unahusisha ujenzi wa gati la Kibirizi lenye urefu wa mita 250 na kuifanya bandari hiyo kuwa na gati refu kuliko bandari zingine katika Ziwa Tanganyika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika bandari ndogo ya Kibirizi, Afisa Bandari hiyo, Ghalib Mahyolo, alisema kwa sasa licha ya kutokuwepo kwa gati la kisasa wanahudumia tani 600,000 hadi 700,000 kwa mwezi.

Pia alisema kwa mwezi mmoja wanahudumia boti zipatazo 220 hadi 260 na boti 70 kati ya hizo ni za abiria ambazo zina uwezo wa kubeba abiria 50.
Alisema boti za abiria zinahudumia vijiji vitatu ambavyo ni Kagunga, Mwamgongo na Mtanga ambapo usafiri unapatikana siku zote za wiki isipokuwa Jumapili.

Kwa upande wa uwezo wa boti za mizigo zinazohudumiwa bandarini hapo alisema boti kubwa kabisa zina uwezo wa kubeba tani 120 na zinafanya safari katika ya Tanzania, Burundi na DRC."Mradi wa kujenga gati mpya hapa Kibirizi utaongeza biashara ya usafirishaji wa mizigo na abiria kwani itawezesha upakiaji na upakuaji kufanyika kwa urahisi zaidi tofauti na ilivyo sasa," alisema Mahyolo.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese, alisema mradi huo ni mkakati wa TPA kuboresha bandari ndogo za maziwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma pamoja na kuongeza mapato.

Msese alisema mradi huo pia unahusisha ujenzi wa uzio kuzunguka bandari ya Kibirizi ambayo imekuwa na changamoto yakuingiliwa na shughuli zingine za wananchi ambazo si za kibandari ikiwemo kuchota maji katika eneo la bandari.Alisema pia kutakuwa na ujenzi wa jengo la abiria, ghala la kuhifadhia mizigo, vyoo na kibanda cha mlinzi pamoja na uwekaji wa paving.

Akizungumzia mradi huo Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji wa Maboti, Edmond Msabaha, alimshukuru Rais John Magufuli kwa serikali kuptia TPA kuona umuhimu wa kuwajengea gati ku wa la kisasa.Alisema kwa sasa wanapakiza mizigo na abiria kwa shida tofauti na ikiwepo gati la kisasa.

"Mradi hii utakua na manufaa kwetu wasafirishaji na hata wateja wetu lakini pia utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kutokana na kazi kuwa zinafanyika kwa haraka, hivyo nimshukuru Rais Magufuli kwa kutuletea mradi huu," alisema Msabaha.
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Mseseakizungumza juu ya kazi zinazofanywa katika Bandari ya Kigoma na Miradi itakayojengwa katika bandari hiyo
Moja ya Mashine iliyopo katika Bandari ya Kigoma inayonyanyua mizigo kwa haraka ambapo bandari hiyo inaborehsw akwa gharama ya zaidi ya Milioni 30.



Halmashauri 184 Kushiriki Mashindano ya Usafi wa Mazingira Mwaka 2019

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile


Na Frank Mvungi

Mashindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kwa Mwaka 2019 kushirikisha Halmashuri zote 184 Tanzania Bara.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa tarehe ya kuanza kwa mashindano hayo itatajwa hivi karibuni ambapo Halmashauri zitakazoshinda ngazi ya mkoa zitashindanishwa Kitaifa.

Katika mashindano hayo Wizara imeongeza vipengele viwili ambavyo ni Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa na Taasisi za kibenki kwa kila mkoa ambapo benki itakayoshinda itashindanishwa na mikoa mingine ili kupata mshindi wa kitaifa

Akifafanua zaidi Dkt Ndugulile amesema kuwa lengo la kuingiza mabenki ni kukumbusha umuhimu wa kuweka miundombinu ya usafi hasa vyoo kwa ajili matumizi ya wateja ambao mara nyingi wamekua wakisahaulika.
Malengo ya Mashindano hayo ni kuongeza ufahamu na uelewa ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha Afya na Usafi wa mazingira, kupanua ushirikishwaji wa jamii katika kushughulikia masuala ya Afya na usafi wa mazingira, kuiwezesha jamii kubadili tabia na mazingira wanayoishi kwa kuzingatia usafi na kanuni za afya.

Malengo mengine ni pamoja na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika kutoa huduma za usafi wa mazingira na kuongeza uwajibikaji kwa watendaji na wadau mbalimbali katika suala la usafi wa mazingira.

Mashindano haya yataendeshwa na Kamati ya Taifa ya mashindano ya usafi wa Mazingira inayojumuisha wajumbe kutoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Wizara ya Elimu Sayansi na Tekonolojia, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

WAKULIMA WA KOROSHO WAPEWA MAFUNZO-MTWARA

0
0
Joseph Mpangala 

Wakulima wa korosho mkoani Mtwara wametakiwa kuacha Kujibweteka na badala yake wawatumie wataalamu ili kufanya kilimo cha tija kwa kutumia viuatilifu kwa usahihi na kupanda miche mipya 

kulima Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amewataka wakulima wa korosho mkoani humo kuacha kujibweteka na kuwatumia wataalamu wa kilimo Sam namba na kupanda miche mipya ya kisasa iliyofanyiwa utafiti ili kuendana na ushindani wa mikoa mipya inayoanza kuzalisha zao hilo.

Akifungua rasmi mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa baadhi ya wakulima wa korosho na maafisa ugani katika kijiji cha Mailikumi mkoani humo ambayo yatafanyika katika mikoa yote inayolima korosho amesema mikoa mipya iliyoingia katika kilimo cha korosho wanalima kisasa na matumizi sahihi ya viuatilifu.

“Tunavyojisifu na kuendelea kutamba kwamba sisi ndio wazalishaji wakubwa ip mikoa mingine ambayo imeanzisha uzalishaji, sasa tukiendelea kubweteka sisi ndio wazalishaji wakubwawenzetu huko wanalima kisasa na wana matumizi sahihi ya viuatilifu na tukibweteka tutajikuta tuko nyuma na wao watazalisha kwa wingi zaidi.

Amesema asilima 60 ya korosho inalimwa Mtwara wakiguatiwa kwa karibu na mikoa ya Lindi na Ruvuma na kwamba mikoa mingine wana maeneo mengi ya kulima.

“Wenzetu bado wana maeneo na pengine kutumia mbegu za kisasa zilizotokana na utafiti wa chuo cha Naliendele, mwisho wa siku tutapoteza ushindani, wanamtwara siku za usoni takwimu za uzalishaji zinaweza kubadilika mkajikuta nyie ni wa mwisho,”amesema Byakanwa

Kaimu mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho, Francis Alfred amesema Kama tasnia ya korosho wanaangalia kuanzia uzalishaji mpaka masoko hivyo wameanzisha mafunzo kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji.

“Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita 2017/18 uzalishaji ulipanda ukawa tani 313,000 lakini mwaka tunaomalizia 2018/19 uzalishaji umekuwa tani 244,000, sasa sisi jukumu letu ni kuhakikishana Marika kwamba uzalishaji unapanda tukaona ni lazima kuandaa mafunzo kwa wakaulima naMarika maafisa ugani yatakayofanyika katika mikoa yote inayozalisha korosho,”amesema Alfred

Akizungumza mkuu wa Teknolojia,unyunyuziaji wa viuatilifu TPRA,Mhandisi Julius Mkenda amesema baadhi ya dawa ambazo hazina lugha rafiki zimekuwaWaikiki's zikiingizwa nchini lakini kwa kupambana kwa asilimia kubwa vimepungua.
Kuliko.

Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Dk Fortunatus Kapinga amesema wamekuwa wakiendelea kutoa mafunzo kwa wakulima namna ya kutambua magonjwa na matumizi sahihi ya viuatilifu.


MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA ARINSA NA MKUTANO MKUU WA MWAKA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan(katikati) akiwa katika Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009,kutoka kulia ni Mkuu wa Mpango wa Kuzuia Utakatishaji Fedha, Michiel Van Dyk, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Augustine Mahiga, Kushoto ni Jaji Dkt.Eliezer Mbuki Feleshi, na Mshauri wa UNOC, Fitz Ray Drayton.
Washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu ARINSA, uliofanyika wakifuatilia Mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Bendera za Nchi wanachama wa ARINSA (Asset Recovery Inter-Agency
for Southern Africa), ( , 1-Uganda, 2-Tanzania, 3-Lethoto) zikipitishwa kwa
washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu ARINSA, uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , Chama hicho pia kilikuwa kinaadhimisho Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
akiwasili kufungua Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu
uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
akiwa katika Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu, ARINSA uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009, Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Augustine
Mahiga.
*************************

Kutokana na changamoto ya upungufu wa fedha za kuendesha taasisi ya ARINSA kuna ulazimu katika mali zilizotahifishwa kuwepo kwa mgawanyo wa asili,ia kadhaa ziende kwa ofisi zinazoendesha mashtaka na nyingine ziende kwa taasisi ya ARINSA.

Ameyasema hayo leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu katika maadhimisho ya miaka 10 ya ARINSA na mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Nafahamu kuwa umoja huu umetanua wigo wa ushirikiano katika masuala ya upepelezi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kiupelelezi zinazosaidia kuharakisha kukamilika kwa maombi ya ushahidi nje ya nchi na upatikanaji wa mali zinazohusiana na uhalifu”. Amesema Mh. Samia.

Kwa upande wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa ni heshima kubwa kwa nchi yetu kuwa ni mmoja wa nchi ambazo zipo katika umoja wa ushirikiano wa kudhibiti uhalifu nchini na Afrika kwa ujumla.

Pamoja na hayo Rais wa ARINSA Bw. Biswalo Mganga amesema kuwa wanataka kuhakikisha wote ambao wanajihusisha na uvunjifu wa amani wanashughulikiwa ili kuwemo na amani katika wanachama nchi.

SERIKALI YATAIFISHA MALI ZA WAHALIFU ZENYE THAMANI YA TSH BILIONI 93.16

0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO

DAR ES SALAAM

Serikali imesema kuwa kati ya kipindi cha mwaka 2013 hadi Mei 2019 imetaifisha mali za wahalifu zenye thamani ya Tsh. Bilioni 93.16 zilizokamatwa kwenye sekta za Madini, Maliasili na Sekta ya fedha (Upatu) ikiwa ni sehemu ya kudhibiti uhalifu kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Uhalifu huo unaodaiwa kukithiri katika miaka ya nyuma na ambao sasa unaendelea kudhibitwa unatajwa kuliingizia Taifa hasara ya Mabilioni ya fedha, hatua iliyoifanya Serikali kuudhibiti kwa kutaifisha mali za wahusika wa uhalifu huo.

Hayo yalibainishwa leo (Jumatano Juni 12, 2019) Jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua mkutano wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Urejeshaji wa Mali Zinazohusiana na uhalifu wenye jumla ya nchi wanachama 16.

Samia alisema hivi sasa Serikali ya Tanzania inapanga mikakati ya kuondokana kabisa na uhalifu huo kutokana na sera ya kudhibiti Rushwa pamoja na kuanzisha mahakama maalum zitakazoshughulikia ufisadi Nchini Tanzania.

“Sisi Tanzania tunaimarisha Sera zetu za kupambana na Rushwa na Ufisadi, tunaenda sambamba na umoja wetu huu wa ARINSA hivyo tunazishauri nchi zingine ambazo zipo kwenye umoja huu na bado hazijatunga Sera na Sheria ziharakishe mchakato ili twende sawa” alisema Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Augustine Mahiga alisema mkutano huo pamoja na mambo mengine utazungumzia mikakati ya pamoja ya kudhibiti uhalifu wa mipakani hasa kwenye udhibiti wa uingizwaji wa bidhaa haramu ikiwepo dawa za kulevya.

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Maganga alisema mkakati wa kutaifisha mali za wahalifu umekuja kufuatia kuona vifungo gerezani kwa wahalifu hao havitazinufaisha nchi hizo na badala yake kuchukua mali zao ili kukomesha kabisa suala hilo.

Aidha alisema tayari wataalamu kadhaa wa upelelezi wa kufuatilia mali na kuzitaifisha wameshapata mafunzo na kwamba zoezi hilo linaendelea ili kuhakikisha linafanyika kikamilifu na kwa usiri mkubwa.

ARINSA ni umoja wa urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu wenye Nchi wanachama 16 zilizopo Barani Afrika ambao kwa pamoja wanakusudia kukabiliana na uhalifu hususan kwenye mipaka ya nchi hizo.

Serikali yasema upatu ni haramu, yawaonya wanaofanya biashara hiyo

0
0
Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Serikali imewaonya wanaofanya biashara ya upatu (Pyramid Scheme) kwa kuwa sio halali na hakuna taasisi wala mtu binafsi aliyepewa leseni ya kufanya biashara hiyo.
Onyo hilo limetolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (pichani), wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Munira Mustafa Khatib, aliyetaka kujua ni lini Serikali itadhibiti biashara za upatu ambazo zimekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Taifa.
Dkt. Kijaji alisema kuwa,  kwa mujibu wa sheria ya makosa ya jinai, biashara ya upatu ni haramu na huendeshwa kinyume na sheria na taratibu za nchi hivyo Serikali huchukua hatua dhidi ya wahusika kama ilivyofanya kwa taasisi ya DECI.

“Washiriki wa biashara ya upatu na wale wanaoshawishi ufanyaji wa biashara hiyo, wote wanatenda kosa na wanatakiwa kupata adhabu na sio kusaidiwa na Serikali”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa Serikali itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya biashara ya upatu na tayari Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kushirikiana na  na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),  ilitoa taarifa kwa umma kuhusu madhara hayo na kuwahimiza wananchi kutoa taarifa ya watu au taasisi inayofanya biashara hiyo.
Dkt. Kijaji alisema kuwa,  kwa kuwa waathirika wakubwa wa biashara hiyo ni vijana na wanawake, Serikali kupitia Bunge, mwaka 2018, ilipitisha mabadiliko ya sheria ya fedha ambapo asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri  yanatakiwa kutolewa kama mikopo isiyo na riba kwa kundi hilo.
Alisema Wizara ya Fedha na Mipango kuna Taasisi ya huduma ndogo ya fedha-SELF, ambayo inatoa mikopo kwa kundi hilo kwa riba nafuu na inafanya vizuri katika maeneo mengi nchini.
Amewataka Vijana na wanawake kutojihusisha na biashara haramu bali watumie taasisi halali zinazotoa riba nafuu na zenye lengo la kujenga uchumi wa Taifa.

Aliyelazwa Mloganzila siku 210 aruhusiwa

0
0
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila Dkt. Julieth  Magandi (wapili kutoka kulia) akizungumzia kuhusu matibabu na huduma ambazo amepatiwa mtoto Hilary Plasidius ambaye alilazwa hospitalini kwa siku 210 na kuruhusiwa leo. Anayemfuatia kushoto ni Daktari Bingwa wa watoto Mwanaidi Amir.
Daktari Bingwa wa watoto kutoka Hospitali ya Mloganzila Dkt. Mwanaidi Amiri akielezea kuhusu gonjwa uliokuwa ukimsumbua mtoto Hilary.
Dkt. Julieth Magandi (kulia) akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa kiti cha kumuwezesha kutembea mtoto Hillary, ambacho kimegharimu zaidi ya shilingi laki nne.

Mtoto Hilary akiwa mwenye tabasamu mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hii leo.
Bi. Patricia Hillary (katikati) akitoa neno la shukrani kwa wauguzi, madaktari pamoja na uongozi wa hospitali kwa kwa kumpatia matibabu mjuu kuu wake na afya yake kuimarika.

DKT. KIJAJI AWATAKA WATENDAJI TRA KUWA KARIBU NA WATEJA WAO

0
0
Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amewataka Mameneja wa TRA wa mikoa na Wilaya nchini kote kusimamia vema ukusanyaji wa kodi za majengo na kuhakikisha kuwa viwango vinavyotozwa ni vile vilivyoko kisheria.
Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo mjini Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Mheshimiwa Yahaya Masare, kwamba Mamlaka ya Mapato mkoani Dodoma imempelekea ankara ya kodi ya jengo na kumtaka alipe shilingi laki moja badala ya shilingi elfu 10 zilizoainishwa kisheria kwa majengo ya kawaida.
Dkt. Kijaji ambaye alifika kwenye makazi ya Mbunge huyo, katika Mtaa wa Uzunguni Jijini Dodoma, alibaini kutokuwa na mawasiliano ya kutosha kati ya TRA  na wateja wake jambo lililosababisha malalamiko ya mteja huyo na kuagiza Mameneja wa TRA mikoa na wilaya kuhakikisha wanawafikia wateja badala ya kuwaachia kazi viongozi wa mitaa peke yao.
Awali, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mhe. Yahaya Masare  alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwamba alishitushwa na hatua ya TRA mkoa wa Dodoma kumpelekea ankara hiyo yenye kiwango kikubwa cha madai wakati anafahamu vema sheria ya kodi ya majengo iliyopitishwa bungeni imeainisha viwango vya kodi kwa kila jengo lililoko katika maeneo ya mijini na vijijini
Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma Bi. Kabula Mwemezi, amekiri kuwepo kwa kasoro ya ankara waliyompatia Mbunge huyo na kujitetea kwamba hali hiyo ilitokana na taarifa walizonazo zinazohusu wateja wote wanaomiliki majengo na kwamba suala hilo limepatiwa ufumbuzi
Bi Mwemezi aliwataka wateja wenye malalamiko kuhusu ankara walizo letewa kutoa taarifa kabla hawajalipa ili waweze kupatiwa suluhisho.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa tatu mbele) akiwasili katika nyumba ya Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare, ili kutatua malalamiko ya kodi ya Majengo katika Mtaa wa Uzunguni Jijini Dodoma
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia) akitoa ufafanuzi wa kodi ya majengo kwa Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare, alipofika kujionea hali halisi ya nyumba na bili aliyotakiwa kulipa ya Sh. 100,000, jijini Dodoma
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare (katikati) na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Dodoma Bi. Kabula Mwemezi wakizungumza jambo.
Nyumba ya Mbunge wa Manyoni Magharibi Mhe. Yahaya Masare , iliyopo jijini Dodoma ambayo TRA walimtaka alipe Sh. 100,000 badala ya Sh. 10,000 jambo liliomfanya Mbunge huyo kufikisha malalamiko kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ambaye alilipatia ufumbuzi suala hilo. 
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)

NDAYIRAGIJJE ASAINI MKATABA WA MIAKA 2 KUINOA AZAM FC

0
0

Na Mwandishi WetuUONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo umeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje, kwa ajili ya kuinoa timu hiyo kuanzia msimu ujao.Ndayiragijje, anachukua nafasi ya makocha wa wazawa, Abdul Mingange na Idd Nassor Cheche, waliokuwa makocha wa muda wa timu hiyo hadi msimu uliopita wa ligi ulipomalizika.Zoezi la kocha huyo kuingia mkataba limefanyika Ofisi za Mzizima, mbele ya waandishi wa habari, Azam FC ikiwakilishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, Mratibu Phillip Alando.

Mara baada ya kusaini mkataba huo, Ndayiragijje alikwenda makao makuu ya timu hiyo, Azam Complex na kutembezwa maeneo mbalimbali akiwa sambamba na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’.

Azam FC ikiwa na changamoto ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, imejiridhisha vilivyo hadi kumtwaa Ndayiragije, kwani ana rekodi ya kuifikisha Vital’O ya Burundi hatua ya makundi mwaka 2016.Kama ilivyo utaratibu wa Azam FC kuwapa nafasi wachezaji vijana, Kocha huyo amejipanga vilivyo kuendeleza utaratibu wa kupandisha vijana, ikiwa ndio falsafa aliyopitia pia katika timu zake za awali Mbao na KMC, alizofundisha hapa nchini.

Kocha huyo anayesifika kwa soka lake la kasi na pasi fupi fupi, anatarajia kuanza kukinoa kikosi hicho kuanzia Juni 20 mwaka huu, Azam FC itakapoanza maandalizi ya msimu mpya na kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame ikiwa kama bingwa mtetezi.

WATANO MIKONONI MWA POLISI WAKIWA NA VIFUNGASHIO VYA BIDHAA AMBAVYO SI HALISI TABORA

0
0
Na Amisa Mussa
JESHI LA POLISI MKOANI TABORA KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI MAALUMU  KUTOKA MIKOA YA SHINYANGA NA TABORA  AMBAYO IMEHUSISHA VYOMBO MBALIMBALI  VYA ULINZI NA USALAMA IKIWEMO BODI YA SUKARI ,WATAALAMU KUTOKA  KIWANDA CHA SUKARI KILOMBERO PAMOJA NA WATAALAMU WENGINE KUTOKA TAASISI ZA  TFDA, TRA, WAKALA WA VIPIMO NA OFISI YA MKURUGENZI WAMEENDESHA OPERATION  MAALUMU YA  KUKAGUA BIDHAA MBALIMBALI ZA CHAKULA HUKO MKOANI TABORA NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WAFANYABIASHARA WATANO WAKIWA NA VIFUNGASHIO  MBALIMBALI VYA BIDHAA AMBAVYO SI HALISI (FAKE) .
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Tabora Kamishna Msaidizi Wa Jeshi La Polisi  EMMANUEL NLEY Anasema Wafanyabiashara Hao  Watano Ambao Kwa Sasa Wote Wapo Mikononi Mwa Jeshi La Polisi Mkoani  Humo Wamekua Wakibadilisha  Kwenye Vifungashio Sukari Ya Kiwanda Cha Kutoka Nje Ya Nchi Na Kuiweka Kwenye Mifuko Ya Kiwanda Cha Kilombero Ili Waweze Kuuza Kwa Bie Ya Juu Huku Wakipunguza Ujazo Wa Mafuta Kwenye Bidhaa Ya Mafuta Ya Korie Lita Moja Kwa Kila Lita Ishirini Wakitafuta Faida
Wakati Huohuo KAMANDA NLEY Amesema Watu Wanne Wanashikiliwa Na Jeshi La Polisi Wakiwemo Watumishi Wawili Wa  Bohari Ya Dawa  Mkoa Wa Tabora Msd Kwa Tuhuma Za Kuiba Dawa  Aina Ya ALU Maarufu Dawa Mseto Wakidaiwa Walikua Wakisafirisha Kupeleka Nchi Jirani
Aidha KAMANDA NLEY Amebainisha Kuwa Watuhumiwa Wote Ambao Kwa Sasa Wapo Mikononi Mwa Polisi Watafikishwa Mahakamani Mara Baada Ya Upelelezi Kukamilika.
 SEHEMU YA SHEHENA YA DAWA ALMAARUFU KAMA DAWA MSETO
 KAMANDA WA POLISI MKOA TABORA ACP EMMANUEL NLEY
VIFUNGASHIO MBALIMBALI VYA BIDHAA AMBAVYO SI HALISI(FAKE)

WENYE VIWANDA WAZALISHE BIDHAA ZENYE VIPIMO SAHIHI KUMLINDA MTEJA NA UCHUMI WA NCHI-NDIKILO

0
0

NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

SERIKALI mkoani Pwani ,imewaasa wenye viwanda kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya kisheria ya vipimo, ili kumlinda mteja,uchumi wa nchi na kupata tozo stahiki.

Aidha ,mamlaka za maji na jamii zimetakiwa kupeleka mita za maji kupima kwa wakala wa vipimo ili kuondoa malalamiko mbalimbali ikiwemo ubovu wa mita ama matumizi ya maji yasiyoendana na malipo .

Akitoa rai hiyo ,wakati alipotembelea mitambo ya kituo cha upimaji wa vipimo huko Misugusugu ,Kibaha,mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Evarist Ndikilo alieleza,yapo malalamiko kutoka kwa baadhi ya viwanda wakiona wanabughudhiwa lakini ni lazima wazalishe bidhaa zinazoendana na vipimo.

“Viwanda vya saruji vizalishe saruji inayoendana na uzito sahihi na vipimo sahihi,nondo, na bidhaa zote zinazozalishwa viwandani ,kuliko kuwa na viwanda vingi vyenye bidhaa zisizo na viwango”alisisitiza Ndikilo.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ,alisema mita za maji zimekuwa kero kwa watu wakidai wanaibiwa kuwa haziingiliani na vipimo.“Mamlaka za maji na wananchi walio na kero hizo nendeni kwa wakala wa vipimo ili kuondoa kero hizo”alifafanua Ndikilo.

Awali ofisa mtendaji mkuu wa wakala wa vipimo ,dkt Ludovick Manege alisema kituo hicho kinalenga kupima vimimina vya petrol,dizel na mita za maji.Manege alibainisha kwamba, kwasasa wameunda kikosi maalum kwenda kukagua bidhaa viwandani kuangalia kama zinakidhi matakwa ya kisheria ya vipimo.

JAFO ASHANGAZWA NA KUTOKAMILIKA KWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MKONZE

0
0
Muoenekano wa baadhi ya majengo yanayoendelea kujengwa katika kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze kilichopo Jijini Dodoma.
……………………

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekasirishwa na kasi isiyoridhisha ya ujenzi wa kituo cha Afya Mkonze Jijini Dodoma ambachokwa mujibu wa ratiba za ujenzi kinatakiwa kukamilika Juni 30, 2019.

Waziri Jafo ameonyesha hali hiyo wakati alipotembelea KItuo cha Afya Mkonze kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimepokea fehda za ujenzi Tsh Mil 400 mapema mwezi Disemba, 2018
“Sikutegemea kukuta kituo cha Mkonze kikiwa katika hali hii, kituo hiki ni miongoni mwa vituo vilivyopelekewa fedha mapema tu na kiko mjini tena Makao Makuu ya Nchi mnashindwa na Halmashauri ambazo ziko pembezoni huko na zina chanagmto nyingi lakini wameshakamilisha ujenzi nini kinakwamisha ujenzi wa kituo hiki

Kituo hiki cha Mkonze kilitakiwa kiwe cha mfano, ujenzi ukamilike mapema kwa sababu kila kitu kiko karibu yenu, vifaa vya ujenzi mnavipata kwa urahisi, hakuna changamoto ya usafiri ili mfike hapa hata Ofisi ya TAMISEMI iko hapa hapa sasa endapo mmekwama kitu mna njia nyingi za kutatua nashidnwa kuelewa kwanini mpaka leo bado mnasua sua kukamilisha ujenzi wa kituo hiki” alisema Mhe. Jafo.

Waziri Jafo aliongeza kuwa Wananchi wanataka huduma za Afya hawataki hadithi Mnatakiwa kuongeza kasi ya ujenzi na kukamilisha majengo yote yanayotakiwa tena kwa ubora wa hali ya juu na ifikapo Juni, 30 kituo hiki kikwe kimeshakamilika.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema kuwa fedha walizopokea ni Tsh Mil 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho lakini kutokana na hadhi ya Jiji waliona watafute fedha zaidi ili kufanya Kituo hicho kiwe na ubora sawa na vituo vingine vilivyojengwa Jijini Dodoma.

“Tumeongeza Tsh Mil 100 kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri sasa fedha hizi zilichelewa kufanyiwa mabadiliko kwenye bajeti “Realocation” hiyo ndiyo sababu pekee iliyopelekea kuchelewa kwa baadhi ya kazi za ujenzi katika kituo hiki cha Mkonze; Lakini kwa sasa tumeshafanikiwa kuhamisha izo fedha na tumepokea maelekezo na tutasimamia kuhakikisha kituo hiki kinakamilika ndani ya muda uliopangwa” Alisema Kunambi.

Ofisi ya Rais Tamisemi inatekeleza Mpango wa Maboresho wa Huduma za Afya ambapo Vituo vya kutolea huduma za Afya 352 vipo katika hatua mbalimbali zaukarabati, ujenzi na ukamilishaji. Kazi hii imefanyika kwa awamu tano.

Kati ya hivyo 304 ni Vituo vya Afya ambavyo vitatoa huduma za dharura ya upasuaji kwa mama mjamzito.

SERIKALI KUENDELEA KUTEKELEZA MIKAKATI YA KUPIGA VITA UTUMIKISHWAJI DHIDI YA WATOTO

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama 

Serikali imekua na mikakati mikubwa ambayo imesaidia kuwatoa Watoto
katika suala zima la utumikishwaji katika kazi na mazingira mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
Bungeni kuhusu maadhimisho ya siku ya kupiga vita utumikishwaji dhidi ya
Watoto.

Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Dkt. John Pombe Magufuli imekua ikichukua hatua mbalimbali dhidi ya
tatizo hilo.

“Jamii inatakiwa kutambua maana ya utumikishwaji wa Watoto na kazi
hatarishi zinazowakabili ili kuwa walinzi wa watoto,” alisisitiza Mhagama.
Aliongeza kuwa Watoto hawatakiwi kutumikishwa bali wasaidiwe kutimiza
ndoto zao kwa kuwaandaa kuwa raia wema na wajenzi wa Taifa la kesho.

Alieleza juu ya Sheria na mikakati mbalimbali inayosimamia haki za Watoto
ikiwemo Sheria ya elimu ambayo inataka Watoto wote kupata fursa ya
elimu, Sheria Na. 1 (2009) ambayo inalinda haki na ustawi wa mtoto,
Sheria Na. 6 (2004) ya Ajira na Mahusiano Kazini inelezea mazingira
ambayo mtoto hatakiwi kutumikishwa kazi ambazo hazipo kwa mujibu wa
taratibu.

Pamoja na hilo alielezea pia juu ya mpango ya taifa wa kupiga vita ukatili
dhidi ya Wanawake na Watoto ambao umesaidia katika kuwaondoa Watoto
kwenye mazingira hatarishi na Mpango Mkakati wa taifa wa kupambana na
ajira dhidi ya Watoto.

“Ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia viwango vya kazi na imekuwa ikisisitiza
waajiri kufuata sheria za kazi kwa kutowahusisha Watoto katika
mazingingira hatarishi au kwenye kazi zisizo na staha ambazo zinafanya
Watoto waingie kwenye utumikishwaji,” alisema Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa jamii kuwapa Watoto kazi
zinazozingatia umri, ukubwa wa kazi na zinazolinda afya yao.

Introducing Brand new song from AMINI "SINA NOMA"

0
0

Social Media
Instagram @amini_tz
Twitter @aminitz
Facebook - Amini Mwinyimkuu

THE TRENDY SHOW S02 EP04 BY CYNTHIA MASASI MZIRAY AND CO.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 12.06.2019

WASHIRIKI WA MAFUNZO KUTOKA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA (NDC) WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO NCHINI INDIA

0
0

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (kushoto) akimkaribisha Ubalozini Brig. Jenerali Chestino Msola, Kiongozi wa Ujumbe wa Washiriki wa Mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea ubalozini hapo wakati wa ziara yao ya mafunzo ya siku tano nchini humo iliyoanza tarehe 10 Juni 2019. 
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akizungumza na Brid. Jenerali Msola (mwenye sare za jeshi za rangi ya kijani) pamoja na viongozi wengine wa ujumbe wa washiriki wa mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India wakati wa ziara yao ya mafunzo nchini humo. Kulia ni Comodore Michael Mumanga na Dkt. Lucy Shule, Mkurugenzi wa Mafunzo wa NDC. 
Mhe. Balozi Luvanda akizungumza na ujumbe wa washiriki wa mafunzo (hawapo pichani) kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India wakati wa ziara yao ya mafunzo nchini humo. 
Mhe. Balozi Luvanda akiendelea na mazungumzo na ujumbe huo kutoka NDC 
Mhe. Balozi Luvanda akipokea zawadi ya ukumbusho (memento) kutoka kwa Brig. Jenerali Msola 
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ujumbe wa washiriki wa mafunzo kutoka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini India wakati wa ziara yao ya mafunzo nchini humo. 
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote.

KOCHA AMUNIKE APITISHA ‘PANGA’ TAIFA STARS MISRI, AWATEMA MASTAA 9

0
0


BENCHI la Ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) likiongozwa na Kocha Mkuu, Emmanul Amunike, raia wa Nigeria limefanya mchujo wa kikosi cha wachezaji watakaoshiriki michuano ya AFCON2019 nchini Misri kutoka achezaji 32 hadi achezaji 23 huku wachezaji 9 wakitemwa.

Wakiwa Misri Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti watacheza michezo miwili ya Kirafiki na Misri, kesho Juni 13, 2019 na Zimbabwe, Juni 16,2019.

Kikosi hicho ni hiki.

Makipa
Metacha Mnata (Mbao)
Aishi Manula (Simba SC)
Aron Kalambo (Tz Prisons)

Mabeki

Kelvin Yondani (Yanga)
Hassan Kessy (Nkana, Zambia)
Vicent Philipo (Mbao)
Gadiel Michael (Yanga)
Mohamed Hussein (Simba)
Ally Mtoni(Lipuli)
Erasto Nyoni (Simba)
Agrey Moris (Azam)

Viungo
Feisal Salum (Yanga)
Mudathir Yahya (Azam)
Frank Domayo (Azam)
Himid Mao (Petrojet, Misri)
Yahya Zayd (Ismaily, Misri)
Farid Mussa (Tenerife, Hispania)

Washambuliaji
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji)
Simon Msuva (Difaa El Jadid, Morocco)
Abdilahie Abdallah Mussa (Blackpool, England)
Thomas Ulimwengu (JS Soura, Algeria)
John Bocco (Simba)
Rashid Mandawa (BDF XI,Botswana)

Walioachwa
Seleman Salula (Malindi)
Claryo Boniface (U20)
David Mwantika (Azam)
Fred Tangalu (Lipuli)
Shiza Kichuya (ENPPI, Misri)
Miraji Athumani (Lipuli)
Kelvin John (U17)
Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini)
Shaban Chilunda (Tenerife, Hispania)

WAZIRI DKT. KIGWANGALLA ATATUA MGOGORO WA ARDHI NGORONGORO

0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana kwa furaha na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akisikiliza maoni na hoja za wananchi wa Kata ya Alaitole alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo lao la Esere, wilayani Ngorongoro jijini Arusha. 
Mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na wananchi wa Kata ya Alaitole katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Mhe. Kigwangalla alifika kutatua mgogoro uliohusisha wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro


NA MWANDISHI WETU, NGORONGORO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro uwaruhusu wananchi wa Kata ya Alaitole wajenge shule ya wasichana ya bweni katika eneo la Esere lililo ndani ya Mamlaka hiyo ili waweze kupata elimu kufuatia wananchi hao kuzuiwa kwa muda mrefu kutekeleza mradi huo.

Aidha, ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo utoe kibali cha kuwawezesha wananchi kata hiyo kuanza ujenzi haraka iwezekanavyo ili fedha zilizotolewa na Serikali shilingi milioni 298 zianze kutumika.
Dkt. Kigwangalla ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi wa Kata Alaitole wilayani Ngorongoro kwenye mkutano wa hadhara uliowashirikisha viongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, viongozi serikali wa kata hiyo, viongozi wa mila wa kabila la Masai na madiwani na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha.
Amesema Serikali inaunga mkono juhudi zote za wananchi za kujiletea maendeleo akifafanua kwamba hatua ya wananchi hao kuamua kujenga shule ya Sekondari ya Bweni ni jambo la linalopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo.

“Mnacho kitaka kiko wazi, mnataka maendeleo ya watoto wenu, katika hili mmesema kila baba anatoa elfu hamsini na wanawake wanatoa elfu ishirini, hili ni jambo kubwa achilia mbali nguvu kazi mnayojitolea na tayari serikali imeshaleta milioni 298, haiingii akilini eneo linalochangia kuleta na kuingiza mapato mengi Serikalini kiasi cha bilioni 126 likose shule” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangalla ameeleza kuwa ujenzi shule hiyo utawaondolea wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu akibainisha kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono wananchi hao kwenye mipango yao ya utekelezaji miradi ya maendeleo.

Amesema jamii hiyo pamoja na mazingira wanayoishi kuwa ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro wanahitaji elimu. Aidha, amesema pia ni muhimu katika sekta ya utalii kupitia utamaduni wao akiongeza kuwa kazi ya Wizara ni kuona mafanikio ya sekta ya utalii yanakuwa kwa kuongeza mapato na sio migogoro.

Dkt. Kigwangalla amesema Hifadhi ya Ngorongoro ni hifadhi mseto inayoruhusu binadamu na wanyama kuwepo katika eneo moja na kwamba hiyo ipo kwa mujibu wa sheria akiitaka Mamlaka hiyo kuyatazama vizuri majukumu yake ya kuendeleza Utalii, Kulinda rasilimali zililizopo kwa maana ya kuhifadhi na kuhudumia jamii iliyo ndani ya hifadhi hiyo.

Katika hatua nyingine ameutaka uongozi wa Mamlaka hiyo uendelee kufanya mazungumzo na wananchi hao badala ya kujielekeza katika matumizi ya nguvu ili kupata uelewa wa pamoja akitolea mfano wa eneo la Loliondo ambalo hivi sasa lina utulivu.

“ Viongozi wa Mamlaka mnalo jukumu la kuwasikiliza wananchi na kuamua kwa pamoja, eneo la Ngorongoro ni Urithi wa dunia na litaendelea kuwa hivyo kwa kuheshimu na maslahi ya Taifa na maslahi ya walio walio wengi” Amesisitiza Dkt. Kigwangalla.

Kuhusu mahusiano baina ya wananchi na wahifdhi Dkt. Kigwangalla amesema kuwa kupitia mkutano wake na wananchi amebaini kuwepo kwa tatizo la mawasiliano na mahusiano baina ya wananchi wa eneo hilo na watumishi wa Serikali walio chini ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro akibainisha kwamba tayari serikali imeliona jambo hilo na inaendelea kulifanyia kazi.

Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe. William Ole Nasha akizungumza wakati wa mkutano huo amempongeza na kumshukuru Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za Taifa katika maeneo mbalimbali nchini.

Amemwomba aeendelee kutembelea maeneo mengine ya jimbo hilo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi wa kata za wilaya hiyo kwa lengo la kudumisha mahusiano mema.
Mhe. Ole Nasha ameeleza kuwa hatua ya Wizara kutafutia ufumbuzi mgogoro huo wa ujenzi wa shule ya wasichana ya bweni, vile vile uamuzi wa serikali kutoa eneo na fedha kiasi cha shilingi milioni 298 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo katika eneo lililokubaliwa ni ishara tosha kwamba Serikali inawalinda na kuwajali wananchi wake.

Amesema wananchi wa jimbo la Ngorongoro pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili wako ni wasikivu na wako tayari muda wote kushirikiana na Serikali ikiwemo ulinzi wa rasilimali zilizopo na kuendeleza uhifadhi katika hifadhi ya Ngorongoro.

Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Alaitole wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuamua kuwafuata na kuzungumza nao katika makazi yao wakimpongeza kwa juhudi zake za kutatua changamoto mbalimbali kwa maslahi ya wananchi na uhifadhi.
Aidha, wamemwomba kuendelea kuisimamia sekta ya uhifadhi nchi wakitoa wito wa kudumisha mahusiano mema baina ya wananchi na wahifadhi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kupitishwa na katika eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale ambalo bado taarifa zake zinaendelea kufanyiwa utafiti katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa Kata ya Alaitole ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipofika kutatua mgogoro wa wananchi wa Kata hiyo kuzuiwa kujenga shule ya Wasichana ya bweni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Hata hivyo Waziri Kigwangalla ameumaliza mgogoro huo kwa kuagiza wakazi hao wapewe kibali cha ujenzi na mamlaka hiyo katika eneo lililopendekezwa.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.William Ole Nasha akizungumza na wakazi wa Kata ya Alaitole iliyo ndani ya Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ambayo ilizuiwa kujenga shule ya bweni ya wasichana na mamlaka hiyo zuio ambalo limeondolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii aliyefika katika kata hiyo kutatua mgogoro huo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mhe.William Ole Nasha na askari wa uhifadhi wakiangalia eneo itakapojengwa shule ya wasichana ya bweni ya kata ya Alaitole.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, viongozi na wananchi wa Kata Alaitole wakitazama eneo lilipoonekana fuvu linalosadikiwa kuwa ni la binadamu wa kale lililogunduliwa na wakazi hao katika eneo la Esere, wilayani Ngorongoro. Taarifa kuhusu fuvu hilo zinaendelea kufanyiwa utafiti na watalaam. (PICHA NA WMU)
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images