Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Vodacom kupeleka mashabiki wa Taifa Stars Misri.

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Vodacom Tanzania, Jackline Materu akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Data na AFCON kupitia huduma ya Soka Letu, hapo jana, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Afisa kitengo cha digitali na huduma za ziada, Furaha Limu na Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Vijana Abdi Zagar.

: Tukielekea msimu wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AfCON), kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC, leo imezindua kampeni ya Data na AfCON kupitia huduma ya Soka Letu na itawazawadia wateja kumi wa Kampuni hiyo tiketi za kwenda kushuhudia timu ya Taifa Stars ikicheza huko Misri. Kampeni hiyo ilizinduliwa katika ofisi za makao makuu ya Vodacom jijini Dar es Salaam. 

Kampeni hii itaendeshwa nchi nzima ili kutoa fursa kwa kila mtanzania na shabiki wa Taifa Stars kushinda. 

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara wa Vodacom, Bi. Linda Riwa, alisema huu ni wakati wa kusapoti vya nyumbani. “Tunafuraha kubwa kuona timu yetu ya taifa imefuzu kuwania kombe hili la AfCON, na tunasambaza furaha yetu kwa wateja wetu. Kama mnavyojua kwa takribani miaka 39 timu ya taifa haikupata fursa ya kuwania mashindano haya, hivyo inabidi tuipe nguvu na kuishabikia. kupitia huduma ya Soka letu kutoka Vodacom Tanzania tutawazawadia wateja wetu 10 ambao ni mashabiki wa Taifa Stars tiketi za ndege pamoja na malazi huko Misri ili wakaishangilie timu yetu ya taifa” 

Alitaja kuwa kampeni hiyo inaanza rasmi leo, tarehe 7 Juni na kufungwa tarehe 21 Julai ambapo washindi watatangazwa. “Kuna zawadi kemkem katika msimu huu wa kombe la mataifa ya Africa kupitia Data na AfCON, hivyo ili ushinde inabidi ujiunge na huduma ya Soka Letu kwa kubonyeza *149*84# na utapokea jumbe mbali mbali kuhusiana na mechi zinazoendelea. Na si hayo tu, kutazama mechi mbashara unahitaji kuwa na intaneti ya uhakika hivyo endelea kujiunga na vifurushi vya intaneti upate hadi mara mbili ya kifurushi unachonunua “Data Datani” Aliongeza Bi Riwa. 

Kwa Wateja wapya, watapata dakika tano bure za kupiga papo hapo, lakini pia Wateja wote wanaweza kujishindia Dk 10,000 za kupiga kutoka Vodacom Tanzania PLC, na pia watapata nafasi ya kujibu maswali na kujishindia point nyingi zaidi, point hizi zitawawezesha kuingia katika droo ambayo washindi watapata tiketi za kwenda Misri huku gharama zote zikiwa zimelipiwa na kampuni hiyo 

Wateja wa Vodacom pia wanaaswa kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, kila Taifa Stars itakapocheza na kushinda, kutatolewa namba maalum ambazo mteja akiingiza katika simu yake atajishindia zawadi mbalimbali. 

“Tuna Zawadi nyingi na za aina mbalimbali, nawaomba wateja wetu waendelee kufuatilia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, hiii itawawezesha kujishindia kila tutakapokuwa tunatoa zawadi,” alisema Riwa huku akiongeza kwamba kwa kila goli litakalofungwa wateja wa Vodacom watajipatia dakika za bure na kuwaasa watembelee kurasa hizo ili kujua namna watakavyojishindia dakika hizo. 

Nao washabiki wa Taifa Stars Juma Hamisi wa Mbagala na Christian John wa Mwenge wameipongeza kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC kwa kuwa wadau wakubwa wa soka nchini. “Tunafurahi sana kuona Vodacom wakitusapoti kwa hili, nina imani washindi watakaopatikana wataongeza ushabiki kule Misri na kututia nguvu ya kufanya vizuri katika msimu huu,” alisema bwana Hamisi. 

“Vodacom Tanzania PLC tunajivunia muitikio mkubwa tunaoupata kutoka kwa wateja wetu mbali mbali, ndio maana tunaendelea kuleta huduma na bidhaa nyingi zaidi. Huduma ya Soka letu ilizinduliwa mwaka 2018 na mpaka sasa kuna wateja wetu wengi wanatumia huduma hii kupata taarifa mbalimbali zinazohusu soka, hivyo nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga ili wapate dondoo za AfCON,” alihitimisha bi. Riwa. 

CCM YAZOA 883 WA CHADEMA SIMANJIRO

$
0
0
Wanachama 883 wa Chadema wa kata ya Naberera Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wamehama chama hicho na kujiunga na CCM wakimfuata mbunge wa jimbo hilo James Ole Millya. Wanachama hao walirudisha kadi zao jana kwenye kijiji cha Namaluli na kupokewa na katibu wa CCM wilayani Simanjiro Ally Kidunda.

Akizungumza baada ya wanachama hao kupokelewa Ole Millya alisema anawashukuru kwa kuamua kumfuata CCM kwani awali walikuwa wote Chadema. Alisema yale mambo waliyokuwa wanalalamika awali hivi sasa hayafanyiki hivyo wamuunge mkono Rais John Magufuli ili wapatiwe maendeleo zaidi.

"Ninawashukuru mno kwa ninyi kuja CCM kama mimi kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Magufuli mwenye maamuzi na moyo kama ya baba wa Taifa hayati mwalimu Julius Nyerere wa kusimamia maendeleo," Katibu wa CCM wa wilaya ya Simanjiro, Ally Kidunda aliwashukia vikali wanasiasa wanaoanza kujipitishapitisha kwa wanachama wa chama hicho kufanya kampeni kabla ya muda wa uchaguzi kufika. 

Kidunda alisema watawachukulia hatua kali wanachama hao kupitia vikao vyao kwani yeye ndiye mtendaji wa chama hicho kwenye wilaya hiyo. Alisema yeye ndiye mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho hivyo hatakubali kuona viongozi wa CCM waliopo madarakani wanafanyiwa fitina na wanachama wa chama hicho kabla ya muda kufika. 

Alisema mbunge wa jimbo hilo ni James Ole Millya hadi mwaka 2020 hivyo wanaohitaji kugombea nafasi hiyo wasubiri hadi kipindi hicho kwani wanaojipitisha hivi sasa watakuwa wanafanya makosa. "Wanachama wa CCM mnapaswa kuanza kufanya fitina na kupitapita kwenye kata, vijiji au vitongoji vinavyoongozwa na viongozi wanaotokana na CCM," alisema Kidunda. 

Alisema hata nafasi za udiwani na wenyeviti wa vijiji na vitongoji wanaotokana na CCM wanapaswa kuachwa wamalize nafasi zao na siyo baadhi ya wanachama kuanza kampeni mapema. Mmoja kati ya wanachama waliojiunga na CCM Raphael Mollel alisema ubabaishaji uliokuwa CCM awali ndiyo uliwakimbiza Chadema ndiyo sababu wamerejea CCM.

"CCM ya Simanjiro ilikuwa inakata majina ya watu na kuendeshwa kindugu tukahama ila sasa tumerudi kwenye chama chetu kumfuata mbunge wetu Millya ambaye tulikuwa naye Chadema," alisema Mollel.

MKURUGENZI TEMEKE AWATAKA WANANCHI KUJIHADHARI NA MLIPUKO WA KIPINDIPINDU

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Lusubilo Mwakabibi  awatahadharisha wakazi wote wa Manispaa na viunga vyake kuchukua tahadhari ya mlipuko wa  ugonjwa wa Kipindupindu .

Alibainisha kuwa kukithiri kwa uchafu katika maeneo mengi ni sababu mojawapo inayopelekea mlipuko wa magonjwa ikiambatana na matumizi ya maji yasiyo safi na salama iwapo yatatumiwa katika chakula au mtu kunywa bila ya kuchemshwa kwa kiwango kinachohitajika,alibainisha kwamba usafi wa mazingira ni wa msingi zaidi ili kujilinda na magonjwa ya mlipuko.

“Manispaa ya Temeke imejipanga kwa kutoa elimu ya uhamasishaji  na tayari wadau wa Afya wameanza kutembelea nyumba kwa nyumba katika maeneo yote yaliyoathirika sambamba na  ugawaji wa dawa za usafi ili kuangamiza mazalia”.Alibainisha zaidi

Tangu ugonjwa wa kipindupindu uliporipotiwa kwa Manispa ya Temeke tarehe 20/04/2019 wagonjwa 48 wamehisiwa mpaka sasa, na kati yao vipimo 10 vimeonesha uwepo wa ugonjwa huo na vifo vilivyoripotiwa ni 2 tu.

Nae Mratibu wa ufuatiliaji magonjwa wa Manispaa ya Temeke Prisca Uswege alibainisha kuwa mpaka sasa nyumba 400 zimetembelewa  na wakazi 123 wamepatiwa  elimu ya namna ya kujikinga na mlipuko huo sambamba  na ugawaji wa water guard pamoja na dawa ya Chlorine.

Nae Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dr.Gwamaka Mwabulambo alisema “tayari kuna kambi maalumu iliyopo katika Hospitali ya Temeke kwaajili ya magonjwa ya mlipuko ambapo  matibabu na uangalizi kwa wagonjwa hao hufanyika kwa urahisi zaidi”.

Dr. Mwabulambo alibainisha zaidi kwamba dalili za ugonjwa wa kipindupindu ni pamoja na kuharisha mfululizo, kutapika,macho kudidimia ndani, kinyesi na matapishi yenye rangi kama ya maji ya mchele, pamoja na ngozi kusinyaa.

Pamoja na hayo ameeleza  namna ya kujikinga na mlipuko huo kwa kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa sabuni kabla ya kuandaa chakula ama kumlisha mtoto,kunawa mikono kwa maji safi na salama baada ya kutoka chooni au kumsafisha mtoto aliyejisaidia,kusafisha matunda  ama vyakula vibichi kama matunda na mbogamboga, kuhakikisha unatumia choo kwa usahihi,kula chakula cha moto,kufunika chakula kilichoandaliwa tayari kwa  kula,na ukiona mtu anatiririsha au kutapisha choo,toa taarifa haraka kwenye ofisi za serikali ya mtaa au kata zilizokaribu na nawe.

Kipindupindu kitakwisha iwapo mazingira bora ya kukiepuka yatakuwepo huku jamii nzima ikipewa elimu ya namna ya kujilinda na magonjwa ya mlipuko sambamba na kuhaikisha kanuni za Afya zinazingatiwa.

SPIKA NDUGAI AONGOZA WAHESHIMIWA WABUNGE KATIKA HAFLA YA CHAKULA CHA JIONI NA SPIKA WA BUNGE LA RWANDA NYUMBANI KWAKE KISASA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiongozana na Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille wakati wakiingia katika hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma. Kulia nyuma ni Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura na Mbunge ni Mbunge wa kasulu Mhe. Daniel Nswanzugwako.
 Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille akizungumza na Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa (hawapo kwenye picha) katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma. Lengo likiwa ni kuboresha mahusiano baina ya Mabunge na nchini hizi mbili.

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na ugeni kutoka Bunge la Rwanda ulioongozwa na  Spika wa Bunge hilo, Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Watumishi wa Ofisi ya Bunge na wageni waalikwa waliofika katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwake kisasa Jijini Dodoma. Wageni hao kutoka Bunge la Rwanda walifika nchini Tanzania kwa ajili ya kuboresha mahusiano baina ya Mabunge na nchini hizi mbili.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa tatu kulia), Spika wa Bunge la Rwanda, Mhe. Mukabalisa Donatille (wanne kulia), Balozi wa Rwanda nchini, Mhe. Eugene Kayihura (wa pili kulia), Mbunge wa Kasulu, Mhe. Daniel Nswanzugwako (kulia), Mbunge wa Ngara, Mhe. Alex Gashaza (kushoto) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Bahi, Dkt. Fatma Mganga wakiwa katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma.
Mawaziri, Manaibu Waziri na Wabunge wakiwa katika hafla ya chakula jioni nyumbani kwake kisasa Jijini Dodoma. Hafla ikiwa ni baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Rwanda uku dhumuni likiwa kuboresha mahusiano baina ya Mabunge na nchini hizi mbili

 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akishuhudia Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akipatiwa zawadi na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge la Rwanda ya Masuala ya Siasa na Jinsia, Mhe. Rubagumya Emma wakati wa hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akishuhudia Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (katikati) akipatiwa zawadi na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura wakati wa hafla ya chakula cha jioni nyumbani kwa Spika Ndugai kisasa Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WARAKA WANGU KWA WATANZANIA...TAIFA STARS NI YETU TUIAMINI NA KUISAPOTI...

$
0
0
Na Dominick Salamba
Zimebaki siku chake kabla ya Fainal za mataifa ya Afrika zianze nchini Misri na miongoni mwa mataifa machache ambayo yamepata bahati ya kushiriki katika michuano hiyo ni Taifa letu pendwa la Tanzania..

Imepita takribani miaka 39 tukiwa washuhudiaji wa michuano hii kwa kuangalia mataifa ya wenzetu na kufikia hatua ya kujibatiza ushabiki wa kudumu kwa baadhi ya nchi masalani wapo ambao wanasema wao ni mashabiki wa Nigeria,Cameron,Ghana,Misri,Senagal na mengine mengi hii yote ilitokana na kitendo cha kua mashabiki wa mda mrefu kwa kushuhudia mataifa mengine yakishiriki..

Wakati wetu umefika na nitakua mchoyo wa fadhila kama sito pongeza juhudi za Serikali yetu,Tff,na wadau mbalimbali ambao walisimama kidete kwa nguvu,hali na mali hili tu kuona tunaingia kwenye historia ya soka la Afrika kwa mara nyingine..

Shukrani za pekee kama sio maalumu lazima nizitoe kwa benchi la ufundi likiongozwa na Emanuel Amunike na Wachezaji wote walioshiriki kuanzia mwanzo wa kuitafuta nafasi hii na kweli wakafanikisha hili..

Katika mchakato huu toka mwanzo wametumika wachezaji wengi hati imefika mahali imepatikana Timu ya wachezaji 23 ambao ndio watatuwakilisha kwenye michuano hiyo tukiwa kwenye kundi moja na Senagal,Algeria na majirani zetu Kenya na katika hao wachezaji 23 wapo 11 ambao ndio watatufungulia pazia katika mechi ya ufunguzi na kutoa picha kamili ya soka letu..

Nirejee nyuma kidogo kwanini imenisukuma kuandika waraka huu sababu moja kubwa ni kutokana na maneno mengi ambayo yameibuka na kupewa nafasi bila kujua madhara yake na ni kinyume na matamanio yetu kwani kila mtu amekua mwalimu kila mtu amekua na kikosi chake kila mtu amekua na mipango yake kuhusu namna ya timu inatakiwa iwe na wachezaji gani watumike,Si dhambi kutoa maoni lakini tukumbuke kua maoni na ushauri ni ziada sio kitu halisi na uamuzi wa wale wanaoshauriwa na tumekwenda mbali mpaka kuanza kutaja majina ya wachezaji ambao tunaona hawafai kuwepo na wanaofaa wakati timu imeshatangazwa hii si sawa tena si sawa..

Tukumbuke kua soka ni taaluma tena taaluma kamili mbinu na mikakati inapangwa na jopo la benchi la ufundi na mtazamo wao ndio silaha yetu kuu na maneno ya dhihaka tunayoyasambaza juu ya timu yetu hayawachafui tunaowataja bali tunajichafua wenyewe ni sawa kutoka nje na kueleza madhaifu ya mzazi wako kwa watu wengine..

Tumeanza kuikataa Timu yetu kabla ya michuano kuanza hivi wakifanya vema kule tutafanyeje tutaendelea kua hivi hadi lini?

Ifike mahali tuheshimu taaluma na sio kila jambo ni lazima kutafuta ubaya hata pasipo na sababu mbona wenzetu hawana haya,timu imekwenda inahitaji sapoti yetu kubwa na kama kuna marekebisho baada ya mashindano kuna jopo ambalo litatoa tathimini ya mashindano yote mapungufu na nini tufanye katika michuano ijayo..

Tujue kuwa kuna idadi maalumu hata tungekua na wakina messi na ronaldo 50 wanaotakiwa ni 23 tu kwa mujibu wa mahitaji ya mwalimu kulingana na mbinu halizoziandaa..

Mwalimu yupo na timu kambini anakaa na wachezaji anajua mienendo na mtazamo wao juu ya michuano husika inafika mahali anatangaza kikosi cha mwisho unaibuka kutoka sijui Vikindu unaanza kwanini kamuacha fulani wakati anauwezo hivi unadhani mchezaji ni uwezo tu?kuna tofauti kati ya mchezaji na timu unaweza kua mchezaji mzuri ila ukashindwa kutengeneza timu nzuri..

Tuachane na kujimaliza wenyewe tujikite katika kuwatia moyo wa ujasiri tuzungumze mazuri yao tuoneshe tunawaamini na tupo nyuma yao waone upendo na shauku zetu juu ya uwajibikaji wao ndio njia nzuri ya kuwatia shime kinyume na hapo inaonesha kua basi hatuka na nia ya dhati kuona tunashiriki..

Ombi langu mitandao ya kijamii,waandishi wa habari,wachambuzi,walimu,na,wadau wengine tutumie vinywa vyetu,kalamu zetu na chochote tukitumiacho kuona tunaandika mazuri ya Timu yetu tuache chuki na kutafuta umaarufu binafsi kwa kutumia njia hasi ili tujizolee umaarufu kwa urahis hapana hili swala la kitaifa linawaunganisha Watanzania popote pale walipo..

Timu ni yetu na tuiamini na wanaweza kutupatia furaha na naimani watafanya vizuri kwa kadri ya uwezo wao wote tuanze wote ili tumalize wote kama Taifa..
Asante...@dominicksalamba

TDLI yaomba wananchi kuchangia watoto wenye uhitaji wapate mahitaji ya shuleni

$
0
0

Asasi ya kiraia inayojihusisha na kuwasaidia watoto wa shule nchini, Tanzania Development Lightening Initiative (TDLI) imeanzisha kampeni ya kukusanya viatu jozi (pairs) 100 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa shule za msingi wenye uhitaji.

Heri Ayubu, mwenyekiti wa TDLI amesema sio wanafunzi wote wanaoweza kumudu sehemu ya gharama ya kununua sare za shule, vikiwemo viatu, hivyo katika utafiti wao walifanya kwa shule wanazozisaidia katika mikoa ya Mwanza na Dodoma, kuna uhitaji wa viatu jozi 100, ambazo zitavaliwa na wanafunzi 50, kwa wastani wa jozi mbili kwa mwanafunzi mmoja.

“Wanafunzi wanaotoka katika familia za kimaskini wana mahitaji mengi, tunadhani jamii ikitusaidia katika kampeni hii itaongeza chachu ya ufaulu wao,” amesema Ayubu. Amesema tangu waanze kuzisaidia shule hizo miaka miwili iliyopita, ufaulu wa wanafunzi hao umeongezeka na wamekuwa wakijiona sehemu ya wanafunzi wengi.

“Mwanafunzi anaweza kukosa raha na hata wakati mwingine anaweza kushindwa mitihani yake kwa sababu anakwenda shule bila viatu au sketi yake imechanika, akijilinganishana wanafunzi wenzake anajiona tofauti,” anasema Ayubu.

Amesema nchi za Ulaya zina utaratibu wa kuwasaidia watu wasiojiweza, lakini kwa nchi nyingi za Kiafrika, jukumu hili bado linabaki katika jamii. Amesema kuna haja ya jamii ya Kitanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watoto wenye uhitaji na  kuchangia mahitaji yao, kama wanavyochangia katika sherehe za harusi, misiba na siku za kuzaliwa.

Pia amesema kuna baadhi ya mashirika na watu binafsi wenye utamaduni wa kujumuika na kula pamoja na watoto wenye uhitaji likiwa ni jambo zuri, lakini TDLI inadhani kula nao pekee haitoshi, bali msaada ya kimkakati yenye lengo la kuwajengea misingi watoto maskini kukabiliana na maisha na kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa, akitolea mfano misaada inayokusidia kuwapa Elimu bora na huduma za Afya.

Mshauri wa  TDLI, Lilian Simule amesema wanachama  wa asasi yao wamekuwa na utamaduni wa kuchangia fedha au vifaa wakati wanaadhimisha siku zao za kuzaliwa. Akiadhimisha sherehe za kuzaliwa kwake, Simule aliendesha harambee yakuchangia sehemu ya hitaji la viatu v, ambapo waalikwa walichangia pesa taslimu na wengine kuweka ahadi, pesa zote vikifikia zaidi ya 450,000.

“Kiasi hiki kidogo tulichopata kitatuwezesha kupata walau jozi 30 kwa kuanzia, hivyo tunaomba wengine watusaidie, kwa kutoa pesa au kutuletea viatu na vitu vingine kwa ajili ya mahitaji yao ya shule,” amesema.
“Watoto hawahitaji mahitaji makubwa na mengi yapo ndani ya uwezo wetu tukiamua kutoa kile kidogo tunachokipata;”

“Sisi, TDLI sio matajiri, bali tuna moyo, hivyo ikiwa watu watachangia japo shilingi elfu kumi kila mmoja au kiasi chochote tutafanikiwa kuwasaidia watoto kutoka kaya maskini wenye mahitaji ya kielimu ili baadae wawe na ushindani katika soko la ajira,”amesema Simule.
“Lakini hata mtu akichangia kalamu, vitabu na madaftari pia tutapokea misaada hiyo,” amesema Simule.

Asasi ya TDLI inaendesha shughuli zake kwa kutumia michango ya wanachama wake na wadau mbalimbali pamoja na shughuli za kuingiza kipato kwa ajili ya kazi zake, hivyo kupunguza utegemezi wa ufadhili wa wahisani pekee tofauti na Asasi nyingine nyingi hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TDLI, Asasi ya TDLI inawakutanisha vijana kutoka katika kada mbalimbali ili kuunganisha nguvu zao katika kurudisha fadhila kwa jamii ya Tanzania wakiunganishwa na Imani kuwa maendeleo endelevu yatapatikana endapo wanajamii watachangia kuondoa tofauti ya mahitaji ya msingi kama vile Elimu bora na huduma za afya kwa wanajamii walio na changamoto za kiuchumi.

Ayubu amesema wale watakaoguswa wanaweza kutuma walichojaaliwa kupitia MPESA namba 0744333344 kwa jina la Tanzania Devt Lightening Initiative. Ameongeza kuwa TDLI wanao utaratibu wa kuhakikisha mrejesho unatolewa kwa mchangiaji kuhusu utekelezwaji wa malengo yaliyokusudiwa.
 Mshauri wa TDLI, Lilian Simile akitoa wito wa watu kuchangia wakati wa kuanzisha kampeni ya kukusanya viatu jozi (pairs) 100 kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa shule za msingi wenye uhitaji hafla fupi iliyofanyika wikiendi Dar es Salaam.
Lilian Simile ( Wa pili kutoka kushoto) akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuhamasisha wenzao waliochangia sehemu ya mahitaji ya viatu jozi 1,500,000 Kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa shule maskini wenye uhitaji.

NDITIYE: WMO INAMCHANGO MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA TANZANIA.

$
0
0
Na Christopher Philemon, Monica Mutoni. Geneva
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye ameeleza namna ambavyo Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) linavyochangia katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa Tanzania.Amezungumza hayo wakati akihutubia mkutano wa 18 wa WMO, unaoendelea jijini Geneva, Uswisi.

‘WMO ina mchango mkubwa katika huduma za hali ya hewa nchini kama vile miongozo maalum iliyowekwa kwa ajili ya uandaaji na utoaji wa tahadhari za hali mbaya ya hewa kwa maeneo ya ziwa Viktoria ambapo TMA inatoa miongozo ya tahadhari kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utekelezaji wa Mfumo wa Kidunia wa Huduma za Hali ya Hewa (Global Framework for Climate Services-GFCS) ambao ndani yake Tanzania kupitia TMA inanufaika masuala mbalimbali kama vile mafunzo ya muda mrefu na mfupi, upatikanaji wa baadhi ya vifaa vya hali ya hewa  alisema’ Alisema  Nditiye. 

Aidha, katika hotuba yake, naibu waziri  Nditiye aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuelezea namna Serikali inavyoweka jitihada kubwa kuhakikisha huduma za hali ya hewa nchini zinakuwa za kisasa kwa kufanikisha ununuzi wa rada tatu za hali ya hewa pamoja na kuifanya TMA iweze kukidhi zaidi matakwa ya watumiaji kwa kuibadilisha TMA kutoka kuwa Wakala na kuwa Mamlaka kamili.

Wakati akimalizia hotuba yake, Naibu waziri  Nditiye alitumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kumnadi mgombea wa nafasi ya makamu wa tatu wa Rais wa WMO Dkt. Agnes Kijazi kutokana na uwezo na uzoefu alionao WMO akiwa mjumbe wa kamati kuu wa shirika hilo kwa miaka saba.   
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye akihutubia mkutano wa 18 wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) mbele ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali waliodhuria mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka 4(Picha Christopher Philemon)

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawsailiano Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa na kaimu Balozi  Bw. Robert Kahendaguza , mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na baadhi ya waumbe kutoka Tanzania kwenye mkutano wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) unaofanyika Geniva (Picha na Christopher Philemon)

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AMEFANYA UTEUZI


WATU WAWILI WANAODHANIWA MAJAMBAZI WAUAWA NGORONGORO

$
0
0
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akionyesha bunduki aina ya Ak -47  pamoja na risasi 20 zilizokamatwa jana katika misitu ya milima ya Digodigo  Tarafa ya Sale wilaya ya Ngoronroro.



Na Vero Ignatus,Arusha

Watu wawili wanaosadikiwa  kuwa majambazi wameuwawa katika majibizano na polisi eneo la Digodigo ,Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro

Akizungumza na waandishi wa habari jana , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana alisema ,majambazi hayo yalikuwa na bunduki aina ya Ak -47  pamoja na risasi 20

Amesema majibizano hayo yalichukua zaidi ya dakika 75 huku wenyeji wakishuhudia mirindimo ya risasi ambapo tukio hilo liketokea jana saa 3:00 asubuhi kwenye msitu wa Digodigo Tarafa ya Sale Wilayani Ngorongoro

Aliwataja waliokufa  kuwa ni Kulima Albart (35) mkazi wa kijiji cha Mholo  na Hashim Nginodya(28)mkazi wa Digodigo ambapo miili yao umehifadhiwa hospitali ya Digodigo

Amesema watu hao wanaosadikiwa ni majambazi walikuwa wakitafutwa muda mrefu kwa matukio ya unyang'anyi na kuteka watalii

"Majibizano ya risasi yalichukua dakika 75 pia baada ya majibizano walikutwa na risasi 20  pamoja na bunduki aina ya Ak-47"

Sambamba na hayo Kamanda  Shana amesisitiza kuwalinda wafanyabishara wote wa Mkoa wa Arusha na kutoa rai walipe kodi ikiwemo kufuata taratibu za kisheria zilizopo katika kufanya shuguli zao

Natoa onyo kali kwa wale wote wakwepa kodi kuhakikisha wanaliodi ili wasije kukumbana na mkono wa serikali.

ZOEZI LA UTAYARI WA KUPAMBANA NA MGONJWA YA BONDE LA UFA WAZINDULIWA MPAKA WA NAMANGA

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha
Nchi za Tanzania na Kenya wamezindua zoezi rasmi la kupima utayari kama nchi za Afrika ya Mashariki wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza kama homa ya bonde la Ufa na Ebola.

Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema jambo kubwa watakaloliangalia katika zoezi hilo ni pamoja na kuona kama vipo vifaa tiba vya kutosha endapo umetokea mlipuko wa magonjwa hayo.

Tunaangalia kama wataalamu wetu wanaao ujuzi wa kuwahudumia wagonjwa au kuzuia ugonjwa usienee kwa watu na kwa wanyama wengi zaidi ikianguka ebola Tanzania Kenya haitakuwa salama.ikianguka leo Ebola Tanzania ,Kenya haipo salama kwasababu tunapakana na nchi ambayo sasahivi inamlipuko wa ugonjwaa wa EBOLA ambayo ni Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Waziri Mwalimu amesema serikali inayo mikakati na mipango ya kuweza kukabiliana na magonjwa hayo ya bonde la ufa ambapo zoezi hili litatoa picha halisi kuwa kama upo utayari kiasi gani kupambana au kukabiliana na magonjwa hayo ya bonde la Ufa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema Wizara ipo makini katika jambo kutokana na swala la kiasili kwamba magonjwa yanayotoka kwa wanyama pori kwa mifugo ambayo inafugwa majumbani.

Amesema kupitia vituo vya vilivyopo katika mipaka na vile vilivyopo katika mikoa ya mipakani vina wataalam wa kutosha ambao wanaweA kushughulika na kutambua linapoibuka tatizo.

Mathalani ugonjwa wa kimeta na kwa bahati njema sana ugonjwa kama huu sisi wenyewe kama nchi tunao uwezo tunatengeneza dawa za kukinga na magonjwa haya kupitia taasisi yetu ya TVLA iliyopo Kibaha.

Amesema Wizara ya mifugo ni sehemu ya mkakati huo wa Afya moja ambao unasimamiwa na ofisi ya waziri mkuu , na wamekumuika ya Sekretarieti ya EAC kwaajili ya kuhakikisha kuwa mradi huo wa kusimamia magonjwa yanayoweza kuambukiza binadamu na wanyama kutoka eneo moja kwenda jingine tunashiriki kikamikifu kuyazuia.

Amesema wanachohangaikia kwa sasa ni utayari wa mataifa haya katika kupambana na maradhi ya bonde la ufa.

Amewatoa hofu wananchi na kusema kuwa wataalamu katika nchini ya Tanzania wapo tayari wanashirikiana na wafugaji ambapo mifugo inakaguliwa mara kwa mara na itakapogundulika tatizo kwamba.
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto  Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Bonde la Ufa.

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Bonde la Ufa.
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na Adan Mohamed Naibu Katibu mkuu wa EAC anayeshughulikia sekta ya huduma na uzalishaji wakifuatilia maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari wa nchiji Kenya na Tanzania.
Baadhi ya viongozi kutoka Jumuiya ya Afrika ya Mashariki akiongozwa na Adan Mohamed Naibu Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki anayeshughulikia sekta ya huduma za uzalishaji Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu, Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi  Abdallah Ulega akizungumza katika uzinduzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Bonde la Ufa.

MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (UWEKEZAJI), Angela Kairuki (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Anne Kilango, Bungeni jijini Dodoma, Juni 12, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana na Ajira, Anthony Mavunde, Bungeni jijini Dodoma Juni 12, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Babati Vijijini, Vrajilal Jituson, Bungeni jijini Dodoma, Juni 12, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Peace House ya jijini Arusha  kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 12, 2019. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi  wa Shule ya Sekondari ya Peace House ya jijini Arusha kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 12, 2019.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi na washiriki wa Mashindano ya Miss TANZANITE  Dodoma kwenye viwanja vya Bunge , Juni 12, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia Walimu na Maafisa Elimu kutoka jiji la Mbeya kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma Juni 12, 2019. Kulia ni mwenyeji wa walimu hao, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Walimu na  Maafisa Elimu  wa jiji la Mbeya pamoja na baadhi ya wabunge kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Juni 12, 2019. Walimu na Maafisa Elimu hao walikwenda Bungeni kwa mwaliko wa Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (kulia kwa Waziri Mkuu) ili kujifunza. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Taasisi ya  Mwalimu Julius  Nyerere, Joseph Butiku kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma Juni 12, 2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MGOGORO WA UENDESHAJI KINU CHA NAFAKA CHA ARUSHA WAMALIZIKA

$
0
0
HATIMAYE mgogoro wa muda mrefu wa uendeshaji wa kinu cha kusagisha nafaka kilichopo Arusha kati ya Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Kampuni ya Monaban Trading and Farming ya jijini Arusha umemalizika baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuingilia kati.

Kufuatia kumalizika kwa mgogoro huo na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kukabidhiwa uendeshaji wa kinu hicho, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri Kilimo, Japhet Hasunga aisimamie Bodi hiyo na kuhakikisha inaendeleza kinu hicho ili kiwe na tija kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Jumatano, Juni 12, 2019) wakati alipokutana na Waziri wa Kilimo pamoja na Viongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma. Awali kinu hicho kilikuwa kinamilikiwa na Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).

Amesema Waziri wa Kilimo ahakikishe kuwa kinu hicho kinasagisha nafaka kwa wingi kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi na ziada ya unga utakaozalishwa kuuzwa nje ya nchi ili nchi iweze kupata faida zaidi kwa kuuza unga utaotokana na kinu hicho.

Uamuzi wa kukabidhi kinu hicho cha kusagisha nafaka kilichokuwa kikiendeshwa na Kampuni ya Monaban Trading and Farmning kwa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ulitolewa na Baraza la Mawaziri katika kikao kilichofanyika mwaka 2008. 

Mgogoro huo wa uendeshaji wa kinu hicho ulitokea baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Monaban Trading and Farming, Dkt. Philemon Mollel kutoelewana na uongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kuhusu uendeshaji wa kinu hicho hali iliyosababisha Waziri Mkuu kuingilia kati.

Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inamiliki vinu vinne vilivyopo Arusha, Dodoma, Iringa na Mwanza. Kinu cha Arusha pekee ndicho kilichokuwa na migogoro ya mara kwa mara ambayo haikuwa na utatuzi kwa muda mrefu licha ya jitihada za Serikali kutatua mgogoro huo. 

“Viongozi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko waliwahi kufungiwa milango na mwekezaji aliyesaini mikataba ambayo haieleweki na akawa anaonekana anataka kukirasimisha Kinu cha Arusha kiwe mali yake na ndipo tukalazimika kuunda Timu ya uchunguzi ili kubaini uhalali wake na kuchukua hatua stahiki”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ripoti ya uchunguzi wa kinu cha kisagisha nafaka cha jijini Arusha kilichokuwa kikiendeshwa na kampuni ya Monaban Trading and Farming, ambacho sasa kitaendeshwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma Juni 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RC CHALAMILA AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MBEYA

$
0
0
Na Emanuel Madafa, Mbeya .
Dhamira ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwapatia wananchi huduma nzuri, itafanikiwa endapo viongozi wenye dhamana ya kuisimamia Serikali hawatakuwa wasanii wa kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya inayojengwa Inyala kwa gharama ya Sh1.5 bilioni na kuonekana kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

Chalamila amesema Rais Magufuli ana nia njema kwa Watanzania lakini baadhi ya wasaidizi wake ndio wanaomuangusha na ndio sababu inayomfanya kupangua pangua safu ya uongozi wake.

Amesema endapo viongozi walioaminiwa wakiwa ni wasanii katika kusimamia na kutekeleza maazimio ya Rais Magufuli hawatakuwa wamembeba wala kumuwakilisha vyema.

“Tukiacha usanii na kuweka kando rushwa na ufisadi…tutakuwa tumembeba vizuri Rais katika kuwatumia Watanzania.  Kwa hiyo hospitali hizi zote za mkoa wetu wa Mbeya zinaenda vizuri sana na hii inadhihirisha sisi viongozi wake ni wasafi na tunasimamia vyema fedha na hatujawa wasanii  na ndio maana majengo yanaonekana lakini kama tungekuwa wasanii nina amini  tungekuwa tumefukuzwa kabisa”.

Amesema Serikali imetoa zaidi ya Shilingi 6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za wilaya tatu ambazo ni Mbarali, Busokelo na Mbeya na vituo vya afya 14 kwa mkoa mzima wa Mbeya 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Steven Katemba amesema fedha hizo Sh1.5 bilioni zimewezesha kujenga majengo saba  ya kutolea huduma  zote muhimu katika hospitali hiyo.

Amesema pia halmashauri yake  imetoa Sh60 milioni ambazo zitasaidia kujenga nyumba mbili za watumishi lakini wananchi wametoa ushirikiano mzuri kwenye ujenzi huo ikiwamo kutoa eneo la ardhi ili ijengwe hospitali hiyo.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Stephan Katemba (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila leo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbeya inayojengwa eneo la Inyala ,kwa gharama shilingi Bilioni 1.5
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (mwenye kofia), Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika,Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Stephan Katemba(Katikati) na Mganga Mkuu Wilaya ya Mbeya Dkt  Yahaya Msuya ,wakikagua Maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbeya ambayo inajengwa eneo la Inyala kwa gharama ya shilingi Bil 1.5
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (katikati) ,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (Kushoto) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbeya Stephan Katemba wakiwa katika eneo la ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbeya ambayo inajengwa kwa shilingi Bilioni 1.5.

TFF YAMUONDOA AMMY NINJE KATIKA NAFASI YAKE

$
0
0
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limemfuta kazi mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo Ammy Ninje  kutokana na sababu mbalimbali za kifamilia na kimasomo. 

Pia TFF imelivunja bechi lote la ufundi la Serengeti Boys ambalo lilikuwa chini ya Kocha Oscar Milambo na nafasi hizo zitajazwa hapo baadae.

Afisa habari na Mawasiliano wa TFF Clifford Ndimbo amesema,Ninje hajafukuzwa ila matatizo na majukumu ya kifamilia yamefanya Tff wachukue maamuzi hayo ila ataendelea kutumika katika masuala mbalimbali ya kisoka.

  "Sio kwamba tumemfukuza Kutokana na masuala ya kifamilia Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Ammy Ninje bali Rais Wallace Karia amesema kutokana na masuala ya kifamilia yanayomtinga basi atarudi Uingereza lakini tutaendelea kumtumia katika masuala ya soka na atakayeshika nafasi yake tutamtangaza hivi karibuni. Kwa upande wa Benchi la ufundi pia ni kweli tumelivunja na tutatangaza hapo baadaye pia benchi jipya la ufundi," amesema Ndimbo.

KWESI APPIAH ATAJA SILAHA 23 ZA AFCON 2019

$
0
0
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana James Kwesi Appiah ameweka wazi kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya Mataifa Afrika AFCON 2019 yanayotarajiwa kuanza June 19 huko nchini Misri.

Kikosi kilichotangazwa ni Makipa  watatu ambao ni Richard Ofori (Maritzburg United, South Africa), Lawrence Ati-Zigi (Sochaux, France), Felix Annan (Asante Kotoko, Ghana)

Safu ya ulinzi itaongozwa na Andy Yiadom (Reading, England), Abdul Rahman Baba (Reims, France), Lumor Agbenyenu (Goztepe, Turkey), Kasim Nuhu Adams (Hoffenheim, Germany) John Boye (Metz, France), Jonathan Mensah (Columbus Crew SC, USA) Joseph Aidoo (Genk, Belguim) na Joseph Attamah (Istanbul Basaksehir, Turkey)

Kwa upande wa safu ya kiungo itakuwa na Mubarak Wakaso (Deportivo Alaves, Spain), Thomas Teye Partey (Atletico Madrid, Spain), Kwadwo Asamoah (Internazionale, Italy), Afriyie Acquah (Empoli, Italy), Andre Ayew (Fenerbahce, Turkey), Christian Atsu (Newcastle United, England), Samuel Owusu (Cukaricki, Serbia) na Thomas Agyepong (Hibernian, Scotland)

Washambuliaji ni  Asamoah Gyan (Kayserispor, Turkey) Jordan Ayew (Crystal Palace, England) Caleb Ekuban (Trabzonspor, Turkey) na Kwabena Owusu (Leganes, Spain)

Ghana wapo Kundi F wakiwa na timu za Cameroon, Benin na Guinea Bissau

BENKI YA KCB KUTOA RUZUKU YA MILIONI 85 /-KWA WAKINA MAMA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
BENKI ya KCB Tanzania imezindua awamu ya pili ya programu ya 2jiajiri katika kuonesha dhamira ya dhati ya kumnyanyua mwanamke wa Kitanzania kujikwamua kiuchumi.

Warsha ya uzinduzi huo, iliyofanyika leo Juni 12, 2019 katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam imehudhuriwa na baadhi ya walengwa wa programu ya 2jiajiri, wafanyakazi wa Benki ya KCB, waandishi wa habari na wadau mbali mbali.

 Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Christine Manyenye amesema  benki hiyo inatarajia kutoa ruzuku ya jumla ya Sh. milioni 85 kwa jumla ya washiriki 17 watakaokuwa wamekamilisha na kufuzu awamu ya kwanza ya programu hiyo.

Amesema kuwa walengwa wanaotarajiwa kupata ruzuku hizo   watapitia mchujo ili kuhakikisha ustahili wa na matumizi sahihi ya ruzuku hiyo ili kukuza biashara zao na kuongeza ingawa ruzuku hiyo haina marejesho, benki ya KCB itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wapokeaji ili kuhakikisha wanawake hao wanafikia malengo yao ya kibiashara.

Aidha  Manyeye ameanisha vigezo ambavyo wapokeaji wanatakiwa kukidhi vikiwemo kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya Benki ya KCB na matawi yake nchi nzima.Pia  mpokeaji lazima awe amekamilisha mafunzo ya kinadharia na vitendo katika awamu ya kwanza na vie vile awe anaakaunti ya 2jiajiri iliyo hai na awe mwenye cheti na leseni halali ya usajili wa biashara. 

"Tangu kuzinduliwa kwa programu  hii mwaka 2016, benki imewawezesha wanawake 256 wa Tanzania katika sekta ya biashara na  kuwapa mafunzo mbali mbali na kuwapanulia wigo wa masoko ili kukuza mitaji na uwezo wa kibiashara ambapo kayi yao ni wanawake 115 ndio walipitia mafunzo kwa vitendo katika nyanja mbali mbali. 

Kwa upande wake, mnufaika wa programu hiyo,  Bhoke Mhini, Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya East Coast iliyoko Kibaha ambaye pia ni mmoja wa walengwa wa programu ya 2jiajiri amesema hajawahi kuona dhamira ya dhati katika kumuwezesha mwanawake wa Kitanzania. 

 Amesema kwamba  Benki ya KCB na 2jiajiri ni mfano wa kuigwa na taasisi nyingine kwani umenyanyua ufito wa uwekezaji kwa jamii. 
Mkuu Wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya  KCB, Christine Manyenye akizungumza na waaandishi wa habari wakati uzinduzi wa programu ya 2jiajiri ambapo jumla ya sh.milioni 85 zinatarajiwa kutolewa kwa wanawake 17 ili kukuza biashara zao, aliyekaa kushoto kwake ni Bhoke Mhini, mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya East Coast ya Kibaha, kulia kwake ni Rojas Mdoe, Mkuu wa kitengo cha uendeshaji na technology na mwishoni mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa

THAMANI YA MALI ZILIZOTOKANA NA UHALIFU ZAFIKIA SHILINGI BILIONI 93.16

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
THAMANI ya mali  zilizotaifishwa kutokana na uhalifu zimefikia shilingi bilioni 93.16, mali hizo zilizotaifishwa na kufikia thamani hiyo ni pamoja na madini, nyumba, magari, fedha za upatu, mbao na maliasili kwa kipindi cha mwaka 2013 hadi 2019 zilizotokana na uhalifu wa kupangwa, utakatishaji fedha, kughushi na wanyamapori.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan  wakati  akifungua maadhimisho ya miaka 10 ya Umoja wa taasisi zinazokabiliana na uhalifu kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (ARINSA) ambapo amesema kuwa miongoni mwa mali walizotaifisha ni madini yenye thamani ya Shilingi bilioni 32.

Amesema kuwa mafanikio yaliyopatikana yametokana na marekebisho makubwa katika sheria za nchi ikiwemo Sheria ya Utakatishaji wa mali zinazotokana na Uhalifu na Sheria ya Kuzuia Utakatishafi wa Fedha Haramu ili kuhakikisha zinakuwa na ufanisi unaotakiwa katika kupambana na mbinu mpya za kihalifu hasa unaovuka mipaka.

Samia ameeleza kuwa  kuwepo wapelelezi na waendesha mashitaka wachache waliopata mafunzo kupitia umoja huo, wamechangia kutaifishwa kwa mali hizo kutokana na ujuzi walioupata.

Makamu wa Rais amesema kuwa utekelezaji na kasi ya Rais Magufuli unaendana sana na malengo ya ARINSA hasa katika kukemea masuala ya rushwa, ufisadi na kujilimbikizia mali.

Amesema kuwa umoja huo umetanua wigo wa ushirikiano katika masuala ya upelelezi na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za kiupelelezi zinazosaidia kuharakisha kukamilika kwa maombi ya ushahidi nje ya nchi na upatikanaji wa mali zinazohusiana na uhalifu.

Makamu wa Rais amesema kuwa makosa mengi ya kupangwa na mbinu za utendekaji wake wa kisasa kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia hususani Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kueleza kuwa programu za wapelelezi na waendesha mashitaka wameweza kujengewa uwezo kwenye makosa ya kifedha, wanyamapori na misitu na ufadhili wa ugaidi ikiwa ni pamoja na kufuatilia mali walizozipata wahalifu au kuzitumia kutenda uhalifu ili kuzitaifisha.

Aidha amesema kuwa  nchi wanachama zimefaidika kupitia programu za mafunzo kwa kurekebisha sheria  mbalimbali zilizokuwepo na kutunga sheria mpya ili kurahisisha utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazohusiana na uhalifu na kuhakikisha nchi zinaendelea kuwa salama.

Vilevile amezishauri nchi wanachama kuwa kila nchi itakapotaifisha mali asilimia fulani ya fedha ipelekwe kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka na baadaye kuja katika taasisi hiyo ili iweze kujitegemea kifedha.

Kwa upande wake, Rais wa ARINSA, Biswalo Mganga ambaye pia ni Mkurugenzi wa mashtaka nchini (DPP) amesema kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2019 umoja huo umeweza kutaifisha mali zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.406. amesema kiwa mwaka huu pekee mali zilizotaifishwa zina thamani ya Dola za Maarekani milioni 700 na kwamba mali zinazoshikiliwa zinathamani ya Dola za Marekani 594.23 na maombi ya kutaifisha mali ni 142.

Amesema changamoto wanazokabiliana nazo ni kupoteza thamani ya mali zinazokamatwa na kukaa muda mrefu kwenye vituo vya polisi  na baadhi zinaharibiwa na wahalifu wenyewe zikiachwa mikononi mwao.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametumia wasaa huo kutangaza utalii wa ndani hasa mlima kilimanjaro na kusema kuwa ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii hauwezi kutimia endapo hakuna amani kwa watu na mali zao kwenye nchi wanachama.

Mkutano huo umehudhuriwa na nchi wanachama 16 ambazo ni; Tanzania, Lesotho, Malawi, zambia, Botswana, Afrika kusini, Eswatini, Zimbabwe, Uganda, Kenya, Angola, Madagascar, Msumbiji, Mauritus, Namibia na Shelisheli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa katika Mkutano wa Umoja wa Urejeshaji wa Mali zinazohusu uhalifu uliofanyika Jijini Dar es Salaam leo , ARINSA pia walifanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake 2009,kutoka kulia ni Mkuu wa Mpango wa Kuzuia Utakatishaji Fedha, Michiel Van Dyk, Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP) Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Augustine Mahiga, Kushoto ni Jaji Dkt.Eliezer Mbuki Feleshi, na Mshauri wa UNOC, Fitz Ray Drayton.

NEMC kuingia mtaani kuangalia vvifungashio kutumika vibebesheo

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Baraza la Uhifadhi na Usimamizi  wa Mazingira (NEMC)  limepiga marufuku matumizi  ya vifungashio  vinavyotumika kuwa vibebesheo vya bidhaa mbalimbali.

Akizungumza na waandishi  wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka amesema vifungashio vimeingia kwa kasi kutumika kwa ajili ya kubebea bidhaa mbalimbali ambapo hakuna tofauti  na mifuko ya plastiki ya Rambo na Mifuko laini Soft (Rambo).

Amesema kuwa NEMC inaingia mtaani kwa nchi nzima kuangalia mifuko hiyo na atakayekutwa na mifuko hiyo ashike faini ya sh.30,000 na kuendelea.
"Serikali  imepiga marufuku mifuko ya plastiki  hivyo hakuna njia mbadala ya kutumia mifuko hiyo plastiki  kwa kudai mifuko  ya vifungashio imeruhusiwa"amesema Gwamaka. 

Gwamaka  amesema watu wakiingia  mtaani mifuko  yeyote ile  kwani mifuko mbadala ipo lakini mingine ina ghafi ya plastiki  itaondolewa katika soko. Aidha amesema kuwa wananchi watoe ushirikiano  ikiwa ni kuacha kutumia mifuko ya plastiki wanayodai vifungashio.
 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt Samuel Gwamaka akizungumza na waandishi habari  kuhusiana na watumiaji wa vifungashio vinavyotumika Kama vibebesheo ambapo ni kosa kisheria iliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt Samuel Gwamaka akionesha vifungashio kutumika kama vibebesheo

PSSSF YAWAHAKIKISHIA WANACHAMA NA WASTAAFU WA MFUKO HUO HUDUMA BORA NA ZA HARAKA

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Ryoba (kushoto), akiwa kwenye mazungumzo na Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, wakati meneja huyo alipotembelea studio za TBC Mikocheni jijini Dar es Salaam Juni 12, 2019. Ziara hiyo ilikuwa ni muendelezo wa ziara ya Bi. Chiume kutembelea vyombo vya habari jijini ili kuimarisha mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni mpya. PSSSF iliundwa baada ya kuunganishwa kwa Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF. Vyombo vingine ambavyo PSSSF ilivitembelea katika ziara ya Juni 12, 2019 ni pamoja na Kampuni ya Uhuru Publications Limited (UPL), Kampuni ya African Media Group, wamiliki wa Channel Ten na Magic FM, kampuni inayochapisha gazeti la Jamhuri, Kampuni ya New Habari (2006) wachapishaji wa magazeti la Mtanzania, Rai, na Dimba. Pamoja na mambo mengine, Meneja huyo kiongozi amesema Mfuko umeanza kutekeleza majukumu yake Agosti 1, 2018 na kwamba uko imara na kuwahimiza wastaafu wajitokeze kwa wingi katika zoezi la kuhakiki taarifa zao ili kuondoa usumbufu wakati wa kufanya malipo ya pensheni na kutoa hakikisho la kupata huduma bora na za haraka.
Bi. Eunice Chiume akiwa na Mkurugenzi wa Chaneli ya kitalii ya TBC Safari Channel, Bw. Gabriel Nderumaki (wapili kulia), wakati akiangalia studio inayotembea yaani OB VAN ya kisasa kabisa ya shirika hilo. Gari hilo maalum ambalo limefungwa mitambo na kufanyab studio kamili huwezesha matangazo ya moja kwa moja na lina uweso wa kusafiri mahapa popote hapa nchini. Anayetoa maelezo ni mtaalamu wa ufundi na mitambo wa TBC Bw. K.A Chitenda.
Studio ya kusomea taarifa ya habari TBC.
Picha ya pamoja na uongozi wa TBC
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume akizungumza wakati alipotembelea ofisi za New Habari Sinza jijini Dar es Salaam
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume akizungumza na uongozi wa kampuni ya New Habari Sinza jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Afisa Uhusiano Mwanzamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi na kulia kwake ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Denis Msacky.
Picha ya pamoja na uongozi wa New Habari(2006) 
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications wachapishaji wa magazeti ya Cham cha Mapinduzi (CCM), Uhuru na Mzalendo, Bw. Kiondo Mshana (kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja Kingozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, wa PSSSF Bi. Eunice Chiume, (kulia) na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, wakati Meneja huyo alipofanya ziara kwenye ofisi za kampuni hiyo Juni 12, 2019.
Mhariri wa gzeti la Uhuru, Bw. Ramadhan Mbwaduke, akisalimiana na Bi. Eunice Chiume alipotembelea ofisi za gazeti hilo Juni 12, 2019
Bi Eunice Chiume akipo ngozana na Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Bw.

Picha ya pamoja na wafanyakazi wa gazeti la Jamhuri.
Bi. Enice Chiume akisalimiana na Mhariri wa Channel Ten, Bi. Dina Chahali.
Bi. Eunice Chiume akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSS, Bw. Abdul Njaidi, wakisalimiana na Meneja Uendeshaji wa AMG, Bw.Elias Shamte.

PROF. KABUDI AVIOMBA VYOMBO VYA HABARI KUELIMISHA UMMA KUHUSU SADC

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere leo. Prof. Kabudi aliwaeleza Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utakaofanyika nchini mwezi Agosti 2019. Prof. Kabudi aliwasihi Wakuu hao kushirikiana na Serikali huusan katika kuelimisha umma kuhusu SADC pamoja na kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kuhusu fursa za mkutano huo na zile zinazopatikana katika nchi wanachama wa SADC. 
Msemaji wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbas akitoa neno katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Prof. Kabudi azungumze na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Dkt. Abbas alimuhakikishia Mhe. Waziri kuwa namna anavyovijua vyombo vya habari vya hapa nchini vinavyofanya kazi hana shaka yoyote kuhusu kutoa ushirikiano wao. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisisitiza jambo kwa Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiongea na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. Mhe. Makonda alisema kuwa mkoa wa Dar Es Salam umejipanga kupokea ugeni mkubwa wa mkutano wa SADC ambao unakadiriwa utahudhuriwa na watu zaidi ya 1000 kutoka nchi 16 wanachama wa SADC. 
Meza Kuu kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini, Bw. Henry Mwanika, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bi. Agnes Kayola, Waziri Prof. Kabudi, na Dkt. Abbas. 
Baadhi ya Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini walioshiriki katika kikao cha Waziri. Mwenye tai nyekundu ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania, Dkt. Ayoub Rioba. 
Mkutano wa Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya habari na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukiendelea 
Wakongwe wa tasnia ya Habari nchini ambao walikuwa walimu wa Mhe. Waziri katika fani hiyo. 
Picha ya Pamoja kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wamiliki na Wakuu wa Vyombo vya Habari nchini. 
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images