Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

CHRISTIN BELLA ASIFU UWEZO WA HAMISA MOBETTO KUKARIRI MASHAIRI NDANI YA KIBAO CHA BOSS

$
0
0

Na.Khadija seif,Globu ya jamii

MWAMITINDO Hamisa Mobeto ambae pia ni mwanamuziki chipukizi kwa sasa ameweka wazi kuwa hatoruhusu kukatishwa tamaa kwenye sanaa yake .
Mobeto ambae ameshafanya vibao mbali mbali Kama madam hero na kibao chake kipya alichomshirikisha msanii Christian Bella "Boss" anasema ataendelea kusimama na kukiamini kipaji chake cha kuimba.

" Sitazuia mtu kuongea kile anachokifiria na nitaendelea kusimama kwenye kile ninachokiamini siku zote na maoni yao kwa namna moja au nyingine zinani imarisha na kufanya niendelee kurekebisha baadhi ya makosa madogo madogo kwani bado sijawa na uzoefu wa kutosha Kama nilivo na uzoefu kwenye tasnia ya urembo na maigizo,"

Hata hivyo Mobeto ameeleza kuwa kufanya kazi na Msanii mkubwa Kama Bella ni nafasi kubwa Licha yakuwa mwanamuziki mzuri pia ni mwalimu mzuri katika muziki.Pia amesema ni mwanzo mzuri kufanya kazi na bella hivyo mashabiki zake wategemee vitu vingi vizuri.

Huku Msanii wa miondoko ya dansi nchini christin Bella amesema wazo la kufanya kazi pamoja lilitokea baada ya kukutana nchini Marekani ."Wakati nipo kwenye jukwaa nilimuita ili atumbuize wimbo wake wa madam hero ,"

Hata hivyo bella amesema amepokea baadhi ya maoni ya watu ambayo yamekua mengi ya kumkatisha tamaa mobetto." Hakuna mashindano wala bifu ni kazi tu tumeifanya kwa ajili ya mashabiki zetu waipokee nimeshaimba na watu tofauti Kama alikiba ,ommy dimpoz hivyo kufanya kazi na hamisa sio kitu kibaya japo wengi wamebeza sana ,"

Pia amemsifia mobetto kwa uwezo wake mzuri wa kushika mashairi kwa haraka zaidi .Hata hivyo Bella ameweka wazi kuwa mbali na kuachia kazi hiyo , mashabiki wasubiri vibao vingine vizuri kutoka kwa wawili hao.


KABUDI AMPOKEA WAZIRI WA VIWANDA NA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI WA SUDAN KUSINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech kabla ya kuanza mazungumzo yao. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech, akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya mazungumzo kati yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi (katikati) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo kati yake na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Paul Mayom Akech (kushoto). Kulia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Mayom Akech,Waziri wa Viwanda,Biashara na Masuala ya Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Sudan Kusini. Kushoto kwa Profesa Kabudi ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe. Mazungumzo ya viongozi hao yalifanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 11 Juni 2019. 

WADAU WAKUTANA KUJADILI NISHATI NA MAZINGIRA YANAYOWAZUNGUKA WAKIMBIZI,WAISHUKURU SERIKALI KWA USHIRIKIANO

Uvivu wa Vijana wa Kiume Mkoani Rukwa wamkasirisha RC Wangabo

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akikagua ujenzi wa jengo la Wazazi katika hospitali mpya ya wilaya ya Nkasi 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) akiongea mawili amatatu na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda (kulia) wakati wakiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi. 

************************************* 



Mkuu wa mkoa wa Rukwa mh. Joachim Wangabo amesikitishwa na uvivu wa kutofanya kazi kwa vijana wa kiume katika mkoa hali inayopelekea miradi mingi inayotekelezwa na serikali katika mkoa huo kwa kutumia force account inafanywa na vijana wanaotoka nje ya mkoa huo jambo ambalo sio madhumuni ya serikali ya awamu tano. 

Amesema kuwa lengo la ujenzi kwa kutumia force account ni kuhakikisha kwamba wananchi wa maeneo husika wanapata manufaa ya ujenzi ule na kufanya ujenzi huo kuwa ni wa kwao na kujivunia kwamba walishiriki tangu mwanzo wa ujenzi huo kuanzia ngazi ya songambele ya kuchimba msingi hadi kumalizika kwa majengo hayo 

“Watu wameshiriki kweny songambele hapa lakini baadae tunapotafuta vibarua wa kufanya kazi, mtu anafanya siku mbili, siku tatu akipewa malipo yake anapotea, Uvivu, sasa hii tabia ya uvivu hii ndio ambayo ningependa kutoa wito kwa wananchi wangu ndani ya mkoa wa Rukwa kuwa waache uvivu, mbona kuna mabinti na kina mama wanachapa kazi kule, hawakimbii wanapiga kokoto na wako wengi, lakini vijana wa kiume wanataka kupiga draft, kufanya vitu vyepesi vyepesi, hii tabia ningewaasa waiache,” alisema 

Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo miradi hivyo wanakosa umiliki wa miradi hiyo na kuiona ni miradi isiyowahusu na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza katika ufundi na vibarua ili kufanye kazi na kujipatia kipato na kuacha uvivu. 

Ameyasema hayo alipotembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi inayojengwa katika mji mdogo wa Namanyere wilayani humo akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na wataalamu kutoka katika ofisi ya mkuu wa mkoa. 

Katika ziara hiyo Mh. Wangabo amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo unaoendelea huku majengo yote saba ya hospitali hiyo yakiwa yamefikia katika hatua ya kupaua na kuzingatia ubora katika ujenzi huo huku vifaa vyote kwaajili ya ujenzi huo vikiwa tayari vimeshanunuliwa na kuwaasa kuwa hadi kufikia tarehe 30.6.2019 wahakikishe mafundi wanakabidhi majengo hayo kwaajili ya kuanza kutumika. 

Mmoja wa vibarua anaetokea mkoa wa shinyanga Joseph James kwa niaba ya wenzie alisema kuwa tangu wafike hapo wamekuwa wakilipwa vizuri na wanaona kuwa kazi zinakwenda sawa na hawana malalamiko yoyote huku fundi wao mkuu katika jengo la maabara alikiri kuwa vibarua wake anawatoa mkoa wa shinyanga na kuwa vijana waliopo katika wilaya ya Nkasi ni wavivu na walikuwa wakirudisha nyuma kasi ya kazi. 

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda alisema kuwa ujenzi huo unakwenda kwa awamu tatu na hadi kufikia tarehe 15.6.2019 awamu ya kwanza itakuwa imeisha na awamu ya pili ya kupaka majengo rangi pamoja na kuweka fremu za milango na madirisha tayari imeshaanza kufanyika na awamu ya mwisho ni kuweka marumaru kwenye majengo yote hivyo hadi kufikia tarehe 30.6.2019 ujenzi huo utakuwa umekamilika. 

“Kwa zote hadi sasa tumeshatumia kama shilingi bilioni 1.15 na mpaka jana kweny akaunti tuna kama shilingi milioni 351 ambazo matarajio yetu ni kwamba zitakidhi shughuli za mradi kwasababu kwa upande wa mafundi wote wameshalipwa haki zao kitu ambaco kimebakia katika kununua ni masuala ya marumaru na kulipia aluminiam ya vioo na kumalizia kuwalipa mafundi wakaofanya kazi awamu ya pili, matarajio yetu fedha hiyo itakidhi mahitaji hayo,” Alimalizia.

TANZANIA KUTUMIA ZOEZI LA KUPIMA UTAYARI KUKABILI MAGONJWA YA MLIPUKO MIPAKANI, KUCHAGIZA UTEKELEZAJI WA DHANA YA AFYA MOJA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, akisisitiza umuhimu wa Sekta za Afya kutumia Dhana ya Afya moja, wakati akifungua zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, tarehe 11 Juni, 2019. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akitoa hotuba wakati wa mkutano wa kufungua zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, tarehe 11 Juni, 2019. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, akisisitiza umuhimu wa Sekta za Afya kutumia Dhana ya Afya moja, wakati akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, tarehe 11 Juni, 2019. 
Mratibu wa Dawati la Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka (wa kwanza kulia) akiwa katika chumba maalum cha Menejimenti ya Taarifa za zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, tarehe 11 Juni, 2019. 

************************************* 



Kufuatia nchi za Kanda ya Afrika Mashariki kuwa katika hatari ya kuathirika na magonjwa ya mlipuko kama Homa ya Bonde la Ufa, Mafua Makali ya Ndege na Ebola, na kwa kuwa magonjwa hayo husambaa kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, Tanzania kwa kushirikiana na Kenya wameanza kutekeleza zoezi la Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, lilofunguliwa leo mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, kuanzia tarehe 11 hadi 14 Juni mwaka huu. 

Zoezi hilo, linazingatia Dhana ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. Jumla ya washiriki 150 ambao wanatoka Sekretarieti ya Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania washiriki 130 kutoka ngazi ya taifa, mkoa na wilaya katika mpaka wa Namanga; pamoja na nchi nyingine wanachama ambapo watakuwa watazamaji ikiwa ni Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani Kusini wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo. 

Akiongea leo tarehe 11 Juni, 2019, wakati wa Kufungua rasmi zoezi hilo la siku nne, mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu, amefafanua kuwa, serikali kupitia Wizara hiyo inatumia zoezi hilo kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji na kuwapa washiriki fursa ya kujifunza namna sekta zingine zinavyotekeleza majukumu katika kuzuia na kupunguza madhara pamoja na kujiandaa kukabiliana na maafa ya magonjwa ya mlipuko. 

“Hapa nchini Tanzania tunalo Dawati la Kuratibu masuala ya Afya Moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati hilo sisi kama wizara ya Afya tunasubiri tu ripoti ya zoezi hili na tutaitekeleza mara moja. Utekelezaji wa ripoti hiyo tutahakikisha unakuwa wa ufanisi na tija kwa nchi ili tuweze kusaidia kuimarisha ushirikiano wa sekta za Afya hapa nchini kwa kuzingatia dhana ya Afya moja.” Amesisitiza Waziri Ummy. 

Aidha, Waziri Ummy, ameongeza kuwa zoezi hilo linalenga kutathmini utaratibu wa kutumia kikosi cha taifa cha dharura cha kukabili lakini pia kuhakiki matumizi ya maabara zinazohamishika, kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa magonjwa ya mlipuko kwa vituo vilivyopo mpakani kwa magonjwa ya mifugo na binadamu; kupima hatua za kujiandaa kukabiliana katika viwanja vya kimataifa vya Jomo Kenyatta na Kilimanjaro. 

Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akiongea kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, ameeleza kuwa Serikali kupitia ofisi hiyo, itaendelea kuratibu sekta zote za Afya nchini kwa kutumia Dhana ya Afya moja, ili kuhakikisha Afya za wananchi zinakuwa imara na salama kwa kudhibiti magonjwa ya mlipuko ambayo yanaweza kusababisha maafa. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, akiongea kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina, amebainisha kuwa, kwa kutambua umuhimu wa Dhana ya Afya moja, Wizara inafahamu kuwa mifugo huwa ni chanzo cha vimelea vya magonjwa ambayohuambukizwa binadamu,hivyo serikali imeendelea kuboresha maabara za Mifugo nchini ili kuweza kutambua vimelea kwa haraka na wakati ili visisababishe magonjwa ya mlipuko kwa binadamu. 

Naye, Waziri wa Afya wa Kenya, Mhe. Sicily Kariuki, amebainisha kuwa zoezi hilo ambalo linahusisha mlipuko wa virusi vinavyo shabihiana na Homa ya Bonde la Ufa katika eneo la mpakani, ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa sekta za Afya, kwa kuwa washiriki watahitajika kuonesha utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo kwakuzingatia Dhana ya Afya Moja. 

Zoezi hilo linafanyika nchini Tanzania kufuatia Kikao cha 11 cha Kawaida cha Mawaziri wa Sekta ya Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika mwezi Machi, 2015, ambapo kilielekeza Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuandaa Zoezi la Nadharia la kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika mpaka wa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga. 

Zoezi hilo ambalo linafanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya, kwenye eneo la Namanga, linaratibiwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na nchi wanachama kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani la GIZ na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa.

JUMLA YA WASTAAFU ELFU 10, 500 BADO HAWAJAFIKA PSSSF KUHAKIKI TAARIFA ZAO

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

JUMLA ya wastaafu elfu 10,500 bado hawajafika kwenye ofisi za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ili kuhakiki taarifa zao hadi sasa, Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko huo Bi. Eunice Chiume ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akitembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Juni 11, 2019.

Vyombo vya habari alivyotembelea leo Juni 11, 2019 kwa lengo la kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni Mpya ni pamoja na magazeti ya serikali yanayomilikiwa na kampuni ya Tanzania Standard News Papers (TSN), Azam Media, wamiliki wa Azam TV na Uhai FM, Mwananchi Communications Limited, wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, Citizen na Mwanaspoti na Clouds Media Group, wamiliki wa Clouds TV na Clouds FM.

Alisema, zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu huwa linafanyika kila mwaka na huu ni utaratibu wa taasisi za hifadhi ya jamii na kwa upande wa PSSSF zoezi lilianza Desemba mwaka jana (2018).

”Tangu Mfuko huu uanze shughuli zake Agosti 1, 2018 PSSSF ilifungua ofisi nchi nzima Bara na Visiwani na hivyo tunatoa wito kwa wastaafu wote ambao bado hawajahakiki taarifa zao kufanya hivyo kupitia ofisi zetu zilizoenea nchi nzima na wala hawalazimiki kuja makao makuu Dodoma kupatiwa huduma hiyo. “Alifafanua Bi. Eunice Chiume.

Zoezi la kuhakiki taarifa hufanyika kila mwaka kwa upande wetu tulianza zoezi hili Desemba mwaka jana (2018) na liliendelea hadi Machi 2019 na tumeanza tena na zoezi hilo nab ado linaendelea.

“kuhakiki taarifa ni muhimu kwani kunasaidia kujiridhisha na taarifa za wastaafu wetu kwa sababu huwa kunakuwa na mabadiliko mbalimbali ikiwa ni pamoaja na kujua kama bado wapo, au taarifa zao za kibenki zimebadilika au la nah ii inasaidia kufanya malipo sahihi na kwa mtu sahihi.” Alibainisha.

Meneja huyo Kiongozi alitoa wito kwa wastaafu na jamii kwa ujumla kuwa PSSSF iko imara katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wastaafu na wanachama wake wote popote pale nchini. “Mafao yenu yapo wastaafu wote, nendeni mkahakik taarifai, na hata ndugu ambao ndugu zao wastaafu ni wagonjwa wafike kwenye ofisi zetu na sisi tutakwenda kufanya uhakiki huko huko aliko.” Alifafanua Bi. Enice Chiume ambaye anaendelea na ziara yake Alhamisi Juni 12, 2019.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga(wapili kulia), akizungumza jambo na Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), wakati alipotembelea kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, ikiwa ni ziara ya kujenga mahusiano lakini pia kueleza shughuli za Mfuko huo ambao umeanza kutekeelza majukumu yake Agosti 2018 baada ya serikali kuiunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, (wakwanza kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi (wapili kushoto), wakiwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN), chini ya Kaimu Mhariri Mtendaji, Bw. Januarius Maganga (wakwanza kulia), ikiwa ni muendelezo wa ziara ya meneja huyo kiongzi kutembeela vyombo vya habari kwa nia ya kujenga mahusiano na kueleza shughuli za Mfuko huo mpya.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akifafanua masuala mbalimbali kuhusu shughuli na majukumu ya Mfuko huo.
Kaimu Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali (TSN), ambaye pia ni Meneja Masoko na Mauzo, Bw, Januarius Maganga, akizungumza mbele ya mgeni wake Bi. Eunice Chiume wakati wa mazungumzo yao
Picha ya pamoja na uongozi wa TSN.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume, akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, wakati alipotem,belea vyombo vya habari vya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, (kushoto), akisalimiana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi wakati wa ziara ya kutembelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. 
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume(wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, wakiwa katika mazungumzo na Afisa Mtednaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando (wapili kushoto) na Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Bw. John Mbele wakati wa ziara ya meneja huyo kwenye vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo vya Azam TV na Uhai FM.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Bw. Tido Mhando, akizungumza kwenye mkutano huo. 
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Eunice Chiume(wapili kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji mashuhuri wa luninga ya Azam TV, Charles Hillary na Ivona Kamuntu. 
Picha ya pamoja 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communications, Bw. Francis Nanai (kulia), akisalimiana na Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) huku Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bw. Bakari Machumu akishuhudia wakati wa ziara ya meneja huyo ikiwa ni muendelezo wa kutembelea vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019. 
Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Bw. Frank Sanga (kulia), akiongozana na Bi. Eunice Chiume, wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni ya Mwananchi Communications Tabata jijini Dar es Salaam Juni 11, 2019.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa PSSSF, Bi. Eunice Chiume, (wapili kushoto) na Bw. Abdul Njaidi (watatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi cha XXL, cha Clouds FM, kutoka kushoto, B12, Kennedy the Remedy, na DJ
Picha ya pamoja na uongozi wa Clouds Media

RAS MSOVELA AFUNGA MASHINDANO YA UMITASHUMTA 2019 SHINYANGA

$
0
0
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela amefunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA – 2019) mkoa wa Shinyanga ambapo shule kutoka halmashauri sita za wilaya mkoa huo zimeshiriki. 

Akifunga Mashindano hayo leo Jumanne June 11,2019,katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga Msovela alisema hataki kuona wanafunzi kutoka Shinyanga wanashiriki mashindano ya UMITASHUMTA 2019 kitaifa mkoani Mtwara,bali anataka vijana hao wakarudi na makombe ya kutosha. 

“Nataka mkalete makombe badala tu ya kuwa washiriki wa mashindano ya UMITASHUMTA kitaifa,naamini kabisa vijana wetu wameandaliwa vya kutosha na tutachagua kikosi imara kitakachotuletea ushindi katika mkoa wetu”,alisema Msovela. 

Aidha aliwataka wanafunzi watakaokwenda kushiriki mashindano hayo kitaifa kuwa na nidhamu ya kutosha na wakaoneshe vipaji vyao huku akiwakumbusha kuwa michezo ni ajira. Kwa upande wake,Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika alisema ili kuleta ushindi wa kishindo,wataunda timu ya ushindi yenye vipaji maalum. 

Rutazika aliitaja miongoni mwa michezo iliyokuwepo wakati wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 yaliyofunguliwa mkoani Shinyanga Mei 27,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack kuwa ni mpira wa miguu kwa wasichana na wavulana,netiboli,riadha,riadha maalumu iliyohusisha watoto wasiosikia (viziwi),Goalball (kwa wasioona),ngoma na kwaya. 

Aliongeza kuwa washindi katika michezo yote wamejipatia zawadi ya makombe huku akiwataja washindi wa jumla kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Msalala,Usafi Manispaa ya Shinyanga,Riadha Shinyanga,pete/netiboli Manispaa ya Shinyanga.

Kauli mbiu ya Mashindano ya UMITASHUMTA mwaka 2019 ni 'Michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira'.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela (katikati) akizungumza wakati wa kufunga Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA – 2019) mkoa wa Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage leo Juni 11,2019. Kulia ni Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika,kushoto ni Afisa Michezo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Joseph Bihemo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizitakia mchezo mwema timu zilizofuzu fainali mashindano ya UMITASHUMITA 2019 mkoa wa Shinyanga ambazo ni Halmashauri ya Msalala (jezi rangi ya machungwa) na Halmashauri ya wilaya ya Kishapu (jezi za bluu).
Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya UMITASHUMTA 2019 mkoa wa Shinyanga.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akisalimiana na kuwakagua wachezaji wa timu ya Kishapu.
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akisalimiana na kuwakagua wachezaji wa timu ya Msalala.
Mtanange kati ya Msalala na Kishapu ukiendelea ambapo mpaka dakika 90 zinamalizika hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenzake wakalazimika kwenda kwenye matuta na timu ya Msalala kuibuka na ushindi wa magoli 5 -4.
Vijana wakishangilia uwanjani.
Mchezaji wa timu ya Kishapu akiipatia goli timu yake.
Mbwembwe zikiendelea uwanjani.
Golikipa wa timu ya Kishapu akitapatapa na shuti kali lilisukumwa na mchezaji wa Msalala.
Walimu na wanafunzi wa Msalala wakishangilia baada ya kuichapa Kishapu magoli 5 -4.
Mchezo wa fainali kati ya timu ya wasichana ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi nyeupe) na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (jezi za bluu) ukiendelea.
Mchezo wa fainali kati ya timu ya wasichana ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi nyeupe) na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga (jezi za bluu) ukiendelea ambapo Manispaa ya Shinyanga waliibuka washindi kwa kuifunga Kishapu magoli 18 - 11.
Mchezo wa mpira wa netiboli kati ya timu ya wasichana halmashauri ya Kahama Mji na Msalala ukiendelea. Kahama Mji walipata magoli 20 huku Msalala ikipata magoli 19.
Mchezo kati ya timu ya Halmashauri ya Kishapu (wenye jezi za bluu) na Halmashauri ya Shinyanga ukiendelea ambapo Halmashauri ya Shinyanga waliichapa Kishapu bao 1-0.
Shangwe zikiendelea uwanjani.
Vijana wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa uwanjani.
Meza kuu wakiwa wamesimama tayari kwa kugawa zawadi kwa washindi wa mashindano ya UMITASHUMTA 2019 mkoa wa Shinyanga.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea : Kaimu Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga,Dedan Rutazika akikabidhi zawadi ya makombe kwa washindi katika michezo yote. Washindi wa jumla kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na washindi mpira wa miguu kuwa ni halmashauri ya wilaya ya Msalala,Usafi Manispaa ya Shinyanga,Riadha Shinyanga,pete/netiboli Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea 
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi ya makombe likiendelea. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

NABII ANAETILIWA SHAKA ATAKIWA ASAKWE ILI AHOJIWE-RC NDIKILO

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na usalama mkoani Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemuelekeza kamanda wa polisi mkoa,kumtafuta nabii Elia (shehe Hamza Issa) huko Misugusugu ,Kibaha ili ahojiwe kuhusiana na shughuli hiyo anayoifanya kwa waumini ambao ni wanawake pekee.

Aidha nabii huyo anadaiwa kuishi na mke wa mdogo wake ,Halima Hajji bila ridhaa ya mdogo wake huku akidai anampa maombi .

Akielezea juu ya tukio hilo Ndikilo alibainisha,endapo atabainika kufanya shughuli hizo nje ya imani ya dini ya kiislamu asitishiwe kazi hiyo na sheria ichukuliwe. 

"Taarifa zilizotoka kwa mdogo wake ,mkewe aliondoka na mtoto wa kiume Abdillah Chande ,ila tangu mkewe achukuliwe na kaka yake hataki kurudi Moshi na akipiga simu hawapokei wakidai wapo kwenye maombi"

Nae shehe wa wilaya ya Kibaha ,Saidi Mtonda alisema, mwaka uliopita mtu huyo alifika BAKWATA wilaya ya Kibaha kuomba kujitangaza na kupewa fursa ya kuhubiri baadhi ya maeneo.

Alisema, walipokuja kufanya utafiti waligundua uhubiri wake hauhashirii imani na maelekezo ya dini ya kiislamu ambapo walimpiga marufuku.

"Mufti wa Tanzania nae tulimfikishia taarifa hizi na alitoa tamko la kutomruhusu na aache shughuli hizo ,sasa kama amerudia atafuatilia ili sheria ichukue mkondo wake kwani hawawezi kufumbia macho mambo yaliyo nje na imani ya dini hiyo"alisisitiza Mponda.

Rc Hapi apiga marufuko vifungashio vya mifuko ya Plastiki visivyo na TBS

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamahuri Wiliam ( kulia) akimkabidhi jana mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi mifuko kilo 344 ya Plastiki ambayo imesalimishwa na wafanyabiashara wa Mufindi kwa ajili ya kuteketezwa ,mwenye sare za kijani ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Daud Yassin (picha na Francis Godwin) 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Mufindi katika viwanja vya mashujaa jana wakati wa kilele cha siku ya mazingira duniani ,maadhimisho yaliyofanyika kimkoa katika mji wa Mafinga wilaya ya Mufindi 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi akionyesha jana wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mjini Mafinga aina nyingine ya mifuko ya plastiki ambayo inatumiwa na wafanyabiashara ndogo ndogo mkoani Iringa kuwa vifungashio badala ya rambo ,mifuko ambayo pia ameipiga marufuku kuendelea kutumika (picha na Francis Godwin) 



NA Francis Godwin, Iringa 

Wafanyabiashara mbali mbali wilayani Mufindi mkoani Iringa wamesalimisha jumla ya kilo 344 za mifuko ya Plasitiki kwa ajili ya kuteketezwa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la serikali la upigaji marufuku matumizi ya mifuko hiyo . 

Akikabidhi mifuko hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi jana wakati wa madhimisho ya siku ya mazingira duniani iliyofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini Mafinga wilani Mufindi kwa mkoa wa Iringa, mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam alisema kuwa mifuko hiyo imesalimishwa katika ofisi za Halmashauri na wafanyabiashara hao kabla kuanza kwa utekelezaji wa agizo la serikali na uzuiaji wa matumizi ya mifuko hiyo . 

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa wilaya ya Mufindi iliweza kutoa elimu kwa wananchi wake juu ya zuio la matumizi ya mifuko hiyo na hadi sasa wananchi wameanza matumizi ya mifuko mbadala inayotengenezwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka ndani ya wilaya hiyo kwa kutumia karatasi kutoka kiwanda cha Mgololo kilichopo wilayani hapo . 

” WAnanchi wetu wa Mufindi wameheshimu sana na kupokea maelekezo ya serikali ya kuanza matumizi ya mifuko mbadala lakini mkuu wa suala hili la mazingira ni pana sana na linagusa maisha ya wananchi wetu tunajua suala la kutunza vyanzo vya maji tumekuwa tukilipigia kelele na suala hili bado lipo na tumekuwa tukiwapigia kelele wananchi wetu kuhakikisha wanaacha hatua tano kutoka mito pindi wanapofanya shughuli za kilimo ” 

Aidha alisema kuwa wilaya ya Mufindi wananchi wanatumia sana mkaa na kwa sasa kupitia viwanda mbali mbali vilivyopo wilayani Mufindi wameanza utengenezaji wa mkaa mbadala ambao tayari unauzwa kwenye maduka na maeneo mbali mbali ya wilaya ya Mufindi na nje ya wilaya hiyo japo bado kasi ya uzalishaji wa mkaa huo ni ndogo na haujaweza kuwatosheleza wananchi wengi. 

Hivyo alisema wananchi wengi wameendelea kutumia mkaa wa miti ya porini na kuwa serikali haijapiga marufuku matumizi ya mkaa wa porini na kuwa wananchi wanaruhusiwa kuendelea kutumia mkaa wa porini na mkaa mbadala unaotengenezwa viwandani ila kinachotakiwa ni kufuata taratibu za ufanyaji wa biashara ya mkaa huo wa porini pasipo kuvunja sheria. 

Aidha mkuu huyo wa wilaya aliwataka wafanyabiashara na wananchi wa wilaya ya Mufindi kuendelea kutekeleza agizo la serikali la utumiaji wa mifuko mbadala na kuepuka matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo tayari imepigwa marufuku huku akiwataka wale ambao bado hawajasalimisha mifuko ya plastiki katika ofisi za Halmashauri ama ofisi za watendaji wa mitaa na kata kufanya hivyo kwani kukutwa na mifuko hiyo ni kosa kisheria na mtumiaji anaweza kufungwa jela siku saba ama faini . 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi mbali ya kupongeza hatua iliyochukuliwa na wafanyabiashara na watumiaji wa mifuko ya plastiki wilayani Mufindi kwa kukabidhi kilo 344 za mifuko hiyo kwa ajili ya kuteketezwa bado aliziagiza halmashauri zote za mkoa wa Iringa kuendelea kutoa elimu na kuwachukulia hatua wale wote ambao wanatumia mifuko ya plastiki mweupe kwa kufungashia bidhaa ambazo hazijawekewa nembo ya ubora na TBS . 

Kuwa baada ya serikali kuzuia matumizi ya mikofo ya rambo na mingine ya plastiki yenye rangi baadhi ya wananchi wameanza kutumia mifuko ya plastiki mweupe kwa kugeuza kama kifungashio kuwa kufanya hivyo ni kosa na mifuko hiyo nayo haitakiwi ila vifungashio vinavyoruhusiwa ni vile ambavyo vimewekewa alama ya ubora na TBS pekee . 

Alisema kutokana na na wajasiriamali wanawake katika wilaya ya Mufindi wameanzisha vikundi vya utengenezaji wa mifuko mbadala kwa matumizi ya kubebea bidhaa mbali mbali ni vizuri halmashauri za wilaya ya Mufindi kuwasaidia mikopo isiyo na riba ili kuongeza mitaji na kutafuta mashine za kutengenezea mifuko hiyo na ikiwezekana waweze kuisambaza wilaya nzima mkoa na nje ya mkoa wa Iringa .

WASANII WASHAURIWA KUWA NA UTHUBUTU,KUFANYA KAZI KWA BIDII

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

MSANII wa filamu na vichekesho nchini Tabu Mtingita amewashauri wasanii kuwa na uthubutu katika kazi zao ili waweze kufikia malengo yao na hiyo ni pamoja na kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii.

Akizungumza na blogu ya jamii Tabu amesema kuwa kupitia sanaa ya uigizaji aliyoifanya wa muda mrefu amejifunza zaidi kuthamini kile anachokifaanya na kujenga maudhui ambayo yanasaidia jamii kitu ambacho kimempa umaarufu zaidi.

Amesema kuwa kabla ya kuanza kufanya sanaa ya uigizaji Ndumbagwe Misayo maarufu kama Thea alimvutia sana kupitia uigizaji wake wa kubadilika na kujenga uhalisia na kufanya sanaa ya uigizaji kabla ya kuanza kujihusisha na sanaa ya vichekesho ambayo imezidi kumpa umaarufu.

Tabu amewataka wasanii kuwa na subira na uvumilivu pamoja na kufanya kazi zenye manufaa na zenye kubadilisha na kujenga zaidi jamii zao huku akisisitiza wazazi na walezi kuichukulia sanaa kama kazi nyingine.
Msanii wa filamu na vichekesho nchini,Tabu Mtingita akizungumza na Michuzi Tv leo jijini Dare es Salaam kuhusu soko la filamu ambapo amesema wasanii watengeneze kazi zenye tija kwa jamii.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNI 12,2019

WAZIRI JAFO AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI KITUO CHA AFYA MKUNWA MKOANI MTWARA

$
0
0
 Pichani ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani humo Omari Kipanga wa tatu kulia hivi karibuni akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya kinachojengwa kijiji cha Mkunwa kwenye halmashauri hiyo kwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wa tano kushoto wakati alipotembelea  na kukagua maendeleo ya ujenzi kijijini humo wengine ni viongozi na wananchi wa kijiji hicho.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU)

 Pichani ni wananchi wa kijiji cha Mkunwa kwenye halmashauri hiyo hivi karibuni wakimsikiliza waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wakati alipotembelea  na kukagua maendeleo ya ujenzi  huo kijijini humo.
  waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo wa pili kushoto hivi karibuni akitoa agizo kwa viongozi mkoani mtwara kuhusu kusua sua kwa ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa katika Kata ya Nanguruwe halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani humo wakati alipotembelea  na kukagua maendeleo ya ujenzi  huo katani humo wengine ni viongozi na wananchi wa kata hiyo
waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo kati kati hivi karibuni akielekea na kukagua eneo la ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa katika Kata ya Nanguruwe halmashauri ya wilaya ya mtwara mkoani humo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi  huo katani humo wengine ni viongozi na wananchi wa kata hiyo.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU).

RC Homera: Marufuku kufanya kampeni kabla ya muda

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Katavi

MKUU wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amesema ni marufuku kwa wanachama wa chama chochote cha siasa kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba kwasababu ni kosa kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu huyo wa mkoa amesema aligundua uwepo wa baadhi ya wanasiasa wanaopita nyumba kwa nyumba kufanya kampeni na kuandikisha kadi za wapiga kura jambo ambalo ni kosa.

Pasipo kutaja chama hicho alisema vyama vyote vinapaswa kusubiri hadi Septemba katika uchaguzi wa serikali za mtaa ndipo waanze kampeni zao kwa mujibu wa sheria.

"Tunatambua kwamba kampeni za siasa zina muda wake hivyo ni kosa kwa chama chochote iwe CCM, TLP, ACT-Wazalendo au Chadema kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kabla ya muda wa kampeni na atakayekamatwa anafanya hivyo atashughulikiwa," amesema RC Homera.

Alifafanua kuwa mikutano ya hadhara ya kisiasa ilipigwa marufuku na Msajili wa Vyama vya Siasa na wanaruhusiwa kufanya mikutano ya ndani.

Katika hatua nyingi pia Homera alipiga marufuku wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya wajasiriamali kusumbuliwa katika maeneo yao wqnayoyofanyia biashara.

Akieleza mafanikio katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho katika mkoa wake Mkuu huyo wa Mkoa alisema alipoingia katika nafasi hiyo alikuta zoezi hilo likiwa limefikia asilimia 5 tu lakini hadi kufikia jana lilikua limefikia asilimia 29.

"Niliingia ofisini Mei 23 mwaka huu na nilikuta ugawaji umefikia asilimia tano lakini hadi sasa tumeshafika asilimia 29 na tunaelekea asilimia 30," amesema Homera.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Juma Homera akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea ofisini kwake kusikiliza juu ya Miradi ya Maendeleo inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Pombe Magufuli.
Wanahabari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Juma Homera alipokuwa akizungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ndani ya mkoa wake

TPA kurasimisha bandari bubu Kigoma

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Kigoma

MAMLAKA ya Bandari Tanzania Kanda ya Ziwa Tanganyika, iko kwenye mchakato wa kurasimisha na kufunga bandari ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Mkuu wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese alisema lengo la hatua hiyo ni kuzifanya bandari hizo zifanye kazi kulingana na kanuni na taratibu za kisheria na hivyo kuimarisha ulinzi na usalama.

"Utaratibu wa urasimishaji na kuzifunga bandari hizo bubu unaendelea na ukishamalizika tutazitangaza," alisema.

Pamoja na mambo mengine Msese alisema katika Bandari ya Kigoma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji lakini wamejipanga kukabiliana nazo kwa kuzitatua kimkakati.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kupungua kwa shehena iendayo Nchi jirani za Congo na Burundi ambapo mkakati wa kutatua changamoto hiyo no kuendelea na juhudi za kutafuta masoko mapya na kuvutia yaliyopo.

"Changamoto nyingine ni ufanisi mdogo wa Shirika la Reli nchini (TRC), lakini mazungumzo ya pamoja kati ya Bandari ya Kigoma na TRC ili kuweza kuboresha miundombinu ya Reli kwa nia ya kuboresha huduma za usafirishaji," alisema Msese.

Akizungumzia huduma zinazotolewa na Bandari ya Kigoma, Msese alisema inatoa huduma kwa wateja aina mbili yaani wenye meli na wenye mizigo na nchi zinazohudumiwa na bandari hiyo ni Congo na Burundi.

Alisema bandari hiyo pia inahudumia shehena mchanganyiko, mafuta na makasha ambapo shehena hiyo imekuwa ikiongezeka licha ya matatizo ya njia ya usafirishaji hususani reli.

"Lakini pia katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi, mamlaka imeendelea kuboresha Bandari ya Kigoma kwa kufanya maboresho ya gati la abiria na upembuzi yakinifu ulishafanywa Kampuni ya M/S Royal Haskoning ya Uholanzi katika gati la mizigo umeshakamilika.

"Shirika la Misaada la Japan (JICA), litatekeleza mradi wa uboreshaji wa gati la abiria na ghala la kuhifadhia mizigo ambapo ujenzi huo utaanza Julai mwaka huu," alisema.
 Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Ajuaye Msese akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kigoma.
 Waandishi wa Habari  wakimsikiliza Meneja Bandari  Ziwa Tanganyika Ajuaye Msese.

RPC KILIMANJARO AELEZA WASAFIRISHAJI WA MIRUNGI WALIVYOPAMBANA NA ASKARI.

$
0
0


Anaripoti dixonbusagaga


Baadhi ya wasafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi wamepambana na askari Polisi katika eneo la Sadala wilayani Hai wakigombea  Gunia la kilogramu 50 za dawa hizo zilizokamatwa wakati zikisafirishwa kuelekea Arusha.


Tukio hilo limetokea majira ya saa nane za usiku katika eneo hilo ambapo pikipiki iliyokuwa imebeba mzigo wa Mirungi  ikiendeshwa na mmoja ya vijana hao ilipata ajali  kisha mhusika  alikimbia na kutelekeza  pikipiki na gunia hilo la Mirungi


Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,ACP Hamisi Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akieleza kuwa katika tukio hilo Polisi wamefanikiwa kukamata mtuhumiwa mmoja aliyemtaja kwa jina la Stephano John (17) mkazi wa Bomang’ombe ,kilogramu 50 za Dawa za kulevya aina ya Mirungi pamoja na pikipiki mbili.



MAPRO WATATU WAKATWA KIKOSI CHA MWISHO CHA AMUNIKE

$
0
0
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha Tanzania kwenye fainali za mataifa Afrika (Afcon 2019) nchini Misri.

Kikosi hicho kimetangazwa rasmi jana na Kocha Amunike kimewaacha nyota kadhaa wanaochezw soka la kulipwa nje ya nchi.

Wachezaji walioachwa ni pamoja na Beki Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Shiza Kichuya wa ENNPI ya Misri na Shaaban Iddi Chilunda wa Tenerife ya Hispania.

Wengine ni magolikipa Suleiman Salula wa Malindi SC ya Zanzibar na Claryo Boniface wa u20, David Mwantika wa Azam, Freddy Tangalu na Miraj Athumani wa Lipuli na kinda wa Serengeti Boys (U17), Kelvin John ‘Mbappe’.

Akitangaza kikosi kamili cha mwisho cha  wachezaji 23  wa Taifa Stars kwa ajili ya AFCON, Amunike amewataja ni   makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC) na Aaron Kalambo (Tanzania Prisons).

Mabeki ni Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Mohamed Hussein, Erasto Nyoni (Simba SC), Kelvin Yondan, Gardiel Michael (Yanga SC), Ally Mtoni Sonso (Lipuli FC) na Aggrey Morris (Azam FC).

Kwa upande wa safu ya Kiungo ni Feisal Salum (Yanga SC), Himid Mao (Petrojet, Misri), Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi Morocco) na Farid Mussa (Tenerife, Hispania).

Safu ya ushambuliaji ni Yahya Zayd (Ismailia, Misri), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Adi Yussuf (Blackpool, England), John Bocco (Simba SC), Thomas Ulimwengu (JS Saoura, Algeria) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).

Kikosi hicho kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri utakaopigwa kesho katika Jiji la Alexandria na baadae kucheza na Zimbabwe kabla ya kuanza kwa michuano ya AFCON.

Taifa Stars wapo kundi C na Timu ya Senegal, Algeria na Kenya na mchezo wa kwanza utakuwa dhidi ya Senegal.

CALL FOR APPLICATIONS TO VARIOUS ACADEMIC PROGRAMMES FOR THE 2019/20 ACADEMIC YEAR

$
0
0
The Institute of Social Work (ISW) invites applications from qualified candidates for admission into various Programmes offered for the academic year 2019/2020. 
Basic Technician Certificate Programmes – (NTA Level 4) in: - 
1.Social Work 
2.Business Administration 
3.Labour Relations and Public Management 
4.Human Resource Management 
5.Community Work with Children and Youth 
Minimum Entry Qualifications 
(i) The applicant must have at least four (4) passes at Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) - excluding religious subjects 
OR
(ii) The applicant who hold at least six (6) months certificate from any institution recognized 
by NACTE or NVA Level 3. 
   
1 Ordinary Diploma Programmes – (NTA Level 5&6) in: - 

1.Social Work 
2.Business Administration 
3.Labour Relations and Public Management 
4.Human Resource Management 
Minimum Entry Qualifications 

Direct Entry: 
(i) The applicant must have at least a minimum of one (1) principal pass and a subsidiary at Advanced Certificate of Secondary Education Examination (ACSEE) in appropriate subjects that will amount to a minimum of 1.5 points (i.e. at least one E and S). In addition, the applicant must have four (4) credits from Certificate of Secondary Education Examination (CSEE) - excluding religious subjects 

Equivalent Entry: 

1.(i)  Basic Technician Certificate from an institution recognized by NACTE with a GPA of 2.0. In addition, the applicant must have Four (4) passes from Certificate of Secondary Education Examination (CSEE)- excluding religious subjects 
OR 
2.(ii)  Certificate in Nursing/Midwifery and related courses, and Certificate in Education (Grade 
III A) with an average of C from institutions recognized by NACTE. In addition, the applicant must have at least four (4) passes from Certificate of Secondary Education Examination (CSEE)- excluding religious subjects 

Postgraduate Diploma Programmes in: - 

1.Law, Mediation and Arbitration (Evening Session) 
2.Strategic Human Resource Management (Evening Session) 
3.Health System Management (Evening Session) 
Minimum Entry Qualifications 
(i) The applicant must have a Bachelor Degree or Advanced Diploma in relevant fields or its equivalent in Social Science with PASS grade. 

2 Master Degree Programme (NTA Level 9) in: - 1. Social Work 
Minimum Entry Qualifications One-year Programme 
(i) Advanced Diploma / Bachelor degree in Social Work with 2.7 GPA or Postgraduate Diploma in Social Work. The applicants in this category will only be required to undertake the Advanced Modules that carry 120 credits. 

Two-year programme 
(i) Advanced Diploma / Bachelor Degree in Social Sciences preferably, Community Development, Sociology, Health Sciences, Psychology, Education, and any other related discipline with 2.7 GPA. In addition, Applicants in this category (Without Social Work background) will be required to undertake both Foundation and Advanced Modules that carry 260 credits. 

MODE OF APPLICATION 

Applicants are required to apply through the Online Application System (OAS) link: https://oas.isw.ac.tz/OAS/ or via the Institute’s website www.isw.ac.tz, and pay a non-refundable fee of Tshs. 10,000/= for Tanzanians or USD 30.00 for non-Tanzanians. 
For more information, please visit the Institute’s website at “www.isw.ac.tz” or Call: 0677 111200 or 0735 509090. 

NOTE: Deadline for receiving applications is 02nd September, 2019 for Certificate & Diploma Programs and 30th September, 2019 for Postgraduate Degree programs. 
Applications for Bachelor Degree programs will be open from 24th June, 2019. You are welcome! 

Rector 

Institute of Social work 
P.O. Box 3375
Dar es Salaam 
Tel: +255 22 2774443 
Fax: +255 22 2701375 
Email: info@isw.ac.tz 

Tigo yaunganisha wateja wa Sumbawanga na mtandao wa 4G

$
0
0
Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa 4G wilayani humo. Wanaoshangilia ni baadhi ya wafanyakazi wa Tigo waliohudhuria uzinduzi huo jana.
Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena akionyeshwa baadhi ya bidhaa za mawsiliano kama simu zenye uwezo wa G4 muda mfupi kabla ya uzinduzi wa mnara wa 4G uliofanyika jana. Anayemuelekeza ni Meneja Mauzo wa Tigo Rukwa Francis Ndada 
Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini Ladislaus Karlo (kushoto) akiongea na wananchi wa Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa mnara wa 4G mjini Sumbawanga. Wa pili Kulia ni Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena akifuatiwa na Meneja Mauzo wa Tigo Rukwa Francis Ndada
Katibu Tawala wa Manispaa ya Sumbawanga Christina Mzena (kati kati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnara wa Tigo 4G wilayani Sumbawanga jana. Kushoto ni Meneja wa Tigo Kanda ya Kusini Ladislaus Karlo na kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Rukwa, Francis Ndada .


Kampuni ya Tigo imezindua mtandao wenye kasi wa 4G mjini Sumbawanga, utakaowawezesha wateja wake kupata huduma bora ya intanet, kupiga na kupokea simu, pamoja na ujumbe mfupi wa maneno (SMS). 


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mnara wa 4G mjini Sumbawanga, Meneja Tigo wa Kanda ya KusinI Ladislaus Karlo alisema mnara huo ulioongezwa ufanisi kutoka 3G kwenda 4G umeimarishwa ili kuweza kupitisha mfumo wa data kwa haraka zaidi, hivyo kuwezesha miamala ya fedha na huduma ya intanet kuwa ya kasi zaidi.

“Kama mnavyofahamu, Sumbawanga ni makao makuu ya mkoa wa Rukwa, hivyo kupelekea mji huu kuwa kiungo muhimu wa shughuli za kiuchumi…hapa ndipo faida ya mtandao huu wa 4G unapoweza kudhihirika, katika kuwezesha biashara na kurahisisha upatikanaji wa taarifa na habari kwa kasi zaidi,” alisema Karlo wakati wa uzinduzi wa mnara huo mpya wa 4G.

Katika hotuba yake, Karlo alisisitiza pia kwamba wateja wa Tigo sasa wataweza kutumia mtandao ulioimara, usiokuwa na vikwazo, ambao utawawezesha kufanya shughuli zinazotumia kiwango kikubwa cha intanet, kama kutazama video, kusikiliza muziki, na kutuma na kupokea habari mtandaoni bila wasiwasi wowote.

“Wateja wetu wa hapa Sumbawanga ambao watahudumiwa katika eneo la mnara huu wa 4G watapata ofa maalum, watazawadiwa GB 4 za intanet bure pale wanapobadilisha laini zao za simu kuingia 4G. Wateja wataweza kutumia kifurushi hichi cha intanet kwa muda wa siku 7,” alisema Karlo.

Karlo pia aliwakumbusha wateja wa Tigo Sumbawanga kuwa wanaweza wakapata ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ ambayo inamwezesha kila mteja kupata ofa bora ya kupiga, kupokea simu, intanet na SMS iliyo mahususi na kuendana na mahitaji yao binafsi. Kujiunga na ofa hiyo, piga *147*00# or *148*00#.”

“Kipaumbele chetu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma za teknolojia za kisasa kama vile mtandao wa 4G. Pia ni muhimu kutambua kwamba, teknolojia ya 4G imeongeza idadi kubwa ya watu kuunganishwa na intanet kupitia simu na pia imefungulia jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma,” alisema Karlo. 

Mnara wa Sumbawanga ni wa nne kuzinduliwa baada ya uzinduzi wa minara iliyopo Mpanda, Katavi; Kilolo, Iringa na Bariadi. Jumla ya minara 52 itazinduliwa katika kampeni hii ya nchi nzima kwenye maeneo mbali mbali ikiwa ni pamoja na kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini.

Uvivu wa Vijana wa Kiume Mkoani Rukwa wamkasirisha RC Wangabo

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesikitishwa na uvivu wa kutofanya kazi kwa vijana wa kiume katika mkoa hali inayopelekea miradi mingi inayotekelezwa na serikali katika mkoa huo kwa kutumia force account inafanywa na vijana wanaotoka nje ya mkoa huo jambo ambalo sio madhumuni ya serikali ya awamu tano.

Amesema kuwa lengo la ujenzi kwa kutumia force account ni kuhakikisha kwamba wananchi wa maeneo husika wanapata manufaa ya ujenzi ule na kufanya ujenzi huo kuwa ni wa kwao na kujivunia kwamba walishiriki tangu mwanzo wa ujenzi huo kuanzia ngazi ya songambele ya kuchimba msingi hadi kumalizika kwa majengo hayo

“Watu wameshiriki kweny songambele hapa lakini baadae tunapotafuta vibarua wa kufanya kazi, mtu anafanya siku mbili, siku tatu akipewa malipo yake anapotea, Uvivu, sasa hii tabia ya uvivu hii ndio ambayo ningependa kutoa wito kwa wananchi wangu ndani ya mkoa wa Rukwa kuwa waache uvivu, mbona kuna mabinti na kina mama wanachapa kazi kule, hawakimbii wanapiga kokoto na wako wengi, lakini vijana wa kiume wanataka kupiga draft, kufanya vitu vyepesi vyepesi, hii tabia ningewaasa waiache,” alisema

Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo miradi hivyo wanakosa umiliki wa miradi hiyo na kuiona ni miradi isiyowahusu na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza katika ufundi na vibarua ili kufanye kazi na kujipatia kipato na kuacha uvivu.

Ameyasema hayo alipotembelea ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi inayojengwa katika mji mdogo wa Namanyere wilayani humo akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na wataalamu kutoka katika ofisi ya mkuu wa mkoa.

Katika ziara hiyo Mh. Wangabo amepongeza hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo unaoendelea huku majengo yote saba ya hospitali hiyo yakiwa yamefikia katika hatua ya kupaua na kuzingatia ubora katika ujenzi huo huku vifaa vyote kwaajili ya ujenzi huo vikiwa tayari vimeshanunuliwa na kuwaasa kuwa hadi kufikia tarehe 30.6.2019 wahakikishe mafundi wanakabidhi majengo hayo kwaajili ya kuanza kutumika.

Mmoja wa vibarua anaetokea mkoa wa shinyanga Joseph James kwa niaba ya wenzie alisema kuwa tangu wafike hapo wamekuwa wakilipwa vizuri na wanaona kuwa kazi zinakwenda sawa na hawana malalamiko yoyote huku fundi wao mkuu katika jengo la maabara alikiri kuwa vibarua wake anawatoa mkoa wa shinyanga na kuwa vijana waliopo katika wilaya ya Nkasi ni wavivu na walikuwa wakirudisha nyuma kasi ya kazi.

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Said Mtanda alisema kuwa ujenzi huo unakwenda kwa awamu tatu na hadi kufikia tarehe 15.6.2019 awamu ya kwanza itakuwa imeisha na awamu ya pili ya kupaka majengo rangi pamoja na kuweka fremu za milango na madirisha tayari imeshaanza kufanyika na awamu ya mwisho ni kuweka marumaru kwenye majengo yote hivyo hadi kufikia tarehe 30.6.2019 ujenzi huo utakuwa umekamilika.

“Kwa zote hadi sasa tumeshatumia kama shilingi bilioni 1.15 na mpaka jana kweny akaunti tuna kama shilingi milioni 351 ambazo matarajio yetu ni kwamba zitakidhi shughuli za mradi kwasababu kwa upande wa mafundi wote wameshalipwa haki zao kitu ambaco kimebakia katika kununua ni masuala ya marumaru na kulipia aluminiam ya vioo na kumalizia kuwalipa mafundi wakaofanya kazi awamu ya pili, matarajio yetu fedha hiyo itakidhi mahitaji hayo,” Alimalizia.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (mbele) akikagua ujenzi wa jengo la Wazazi katika hospitali mpya ya wilaya ya Nkasi 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Wazazi katika hospitali mpya ya wilaya ya Nkasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda (kulia) wakati wakiendelea na ukaguzi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Nkasi. 

SERIKALI KUWAJENGEA UWEZO MAKANDARASI WA NDANI

$
0
0
Na Siti Said
Serikali kuptia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) imesema kuwa ina mpango wa kuwajengea uwezo makandarasi wa ndani ili waweze kutekeleza kazi zao na kuongeza ushindani katika soko la ajira.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Arch. Elius Mwakalinga, jijini Dodoma wakati akifungua kikao kilichoshirikisha wakurugenzi wa Wizara na Taasisi zake pamoja na makandarasi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.
Katibu Mkuu huyo, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake itaanza kuwawezesha makandarasi hao kwa kuwashirikisha kwenya miradi michache mikubwa ya Wizara inayojengwa na makandarasi wa nje ili kupata taaluma na ujuzi kutoka kwao. 

“Nimeamua kuitisha kikao hiki ili kuwaeleza mikakati ya Serikali ya kuwajengea uwezo na kujadili kwa pamoja changamoto zenu na hatimae kuzitafutia ufumbuzi”, amesema Katibu Mkuu Mwakalinga.
Aidha, amefafafanua kuwa mkakati huo umeanza ndani ya Wizara kwa kuwapeleka watumishi 44 kwenye miradi nane ya ujenzi inayotekelezwa nchini ikiwemo mradi wa daraja la Selander ambapo watumishi hao watashiriki mwanzo hadi mwisho wa utekelezaji wa miradi hiyo. 

Ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata wataalamu wazalendo katika miaka ijayo ili nao kutoa elimu walioipata kwa wenzao na hatimaye kupata wataalamu wengi wazalendo watakaosaidia kukuza uchumi wa nchi na kulinda maslahi mapana ya Taifa.
Kwa upande wake, Mhandisi Oscar Lisi kutoka mkoani Mwanza, amemuomba Katibu Mkuu Mwakalinga kuwa mkali na kuchukua hatua katika suala la rushwa kwani amesema kuwa sekta hiyo haiendelei na haikui kutoka na kuingiliwa na rushwa.

Pia mkandarasi huyo ameiomba Serikali kulegeza masharti yaliyomo kwenye mikataba ya zabuni kwani masharti mengi yanaonekana kumnyima fursa mkandarasi wa ndani katika zabuni zinazotangazwa na Serikali.
Naye, Mhandisi kutoka Mbeya, Shakira Kiwanga, amemuomba Katibu Mkuu Mwakalinga, kuwasaidia kuzungumza na mabenki ili kuweza kupata mikopo ambayo itasaidia kuinua na kukuza mitaji yao kwani wengi wao wana hali duni.

Mkutano huo umeshirikisha Makandarasi kutoka mikoa mbalimbali nchini lengo likiwa ni kupata taarifa na mikakati ya Serikali kuhusu taaluma yao.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, akisikiliza na kunukuu hoja za Makandarasi wa ndani katika kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao kilichofanyika jijini Dodoma.
 Makandarasi wa ndani kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, katika kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao kilichofanyika jijini Dodoma.
 Mkandarasi wa ndani Valiana Pascal kutoka Mkoa wa Iringa akitoa hoja kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga, katika kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao kilichofanyika jijini Dodoma.
Makandarasi wa ndani kutoka katika mikoa mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi), Arch. Elius Mwakalinga mara baada ya kumaliza kikao cha Katibu Mkuu huyo na makandarasi hao kilichofanyika jijini Dodoma. PICHA NA WUUM
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images