Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

ASKOFU ADAIWA KUTUMIA MAMILIONI YA FEDHA ZA KANISA KWA KUFANYA ANASA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
ALIYEKUWA Askofu Kanisa Katoliki la Virginia magharibi nchini Marekani Michael J. Bransfield (75) anadaiwa kutumia fedha za Kanisa kwenye mambo ya anasa  ikiwemo pombe, kusafiri, kutoa zawadi kanisani, na kukarabati kanisa huku pia akikabiliwa na tuhuma za kuwadhalilisha kingono watu wazima wakati akiongoza kanisa hilo.

Kwa mujibu wa jarida la Newyork Post la nchini humo limeeleza kuwa askofu huyo ametumia kiasi kikubwa cha fedha za kanisa kwa matumizi binafsi na ya anasa tofauti na sheria na kanuni za kanisa hilo.

Imeelezwa kuwa Bransfield  ametumia dola za kimarekani 350,000 kwa kutoa zawadi kanisani, dola milioni 2.4 kwa kusafiri pekee pamoja na huduma za hoteli, dola 1000 kwa matumizi ya pombe, dola milioni 4.6 kwa kukarabati kanisa na matumizi ya kuleta maua ofisini kwake  kila siku yaliyogharimu dola 182, 000.

Alipohojiwa na jarida hilo kuhusiana na tuhuma dhidi yake Bransfield aliesema kuwa kila mtu anajaribu kumchafua na kueleza kuwa watu hao ni hatari sana na hakuwa wazi aliwalenga watu gani.


Uchunguzi dhidi tuhuma hizo dhidi  ya Askofu Michael Bransfield  uliongozwa na Askofu mkuu William Lori wa Baltimore.

Bransfield alikuwa Askofu wa Kanisa hilo tangu mwaka 2005 na alilazimika kuachia ngazi hiyo Septemba, 2018 baada ya Baba Mtakatifu Francis kutangaza uchunguzi dhidi yake.

Hii ndiyo miradi ya kimkakati Mwanza ,magari yanapaki chini ya ardhi

$
0
0
Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatarajia kuanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu, stendi ya mabasi Nyegesi pamoja na kituo cha maegesho ya magari makubwa Buhongwa ambapo miradi hiyo itaongeza ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo.

Hayo yalisemwa jana Juni 05, 2019 na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba wakati akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyofanyika eneo la Soko Kuu.

"Kutakuwa na "parking" ya magari zaidi ya 500 kwa wakati mmoja chini ya ardhi...ukiingia na hela unatumbukiza kwenye mashine, inakupa chenchi..." alisema Kibamba.
Tazama video hapa chini

MATAJIRI WAASWA KUSAIDIA WASIOJIWEZA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

JAMII ya watu wenye kipato na nguvu kubwa ya kiuchumi (matajiri) wametakiwa kutumia sehemu ya mapato yao kusaidia wenye mahitaji wasiojiweza,yatima na wajane.

Rai hiyo ilitolewa jana na mfanyabiashara wa madini, Zakaria Nzuki kwenye chakula alichokiandaa kwa ajili ya watoto yatima 296 wanaolelewa katika vituo vya Taqwa, Mabatini, Imamu Hapsh na misikiti tofauti tofauti jijini Mwanza.

Alisema kuwa kwenye sikukuu ya Idd el Fitri akishirikiana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoani Mwanza aliandaa hafla ya kula chakula na watoto yatima ambao baadhi yao hawana wazazi baada ya kufariki,walemavu na waliotelekezwa.

Nzuki ambaye kiimani ni Mkristo alisema matajiri na watu wengine wenye uwezo mzuri wa uchumi (kipato) wanapaswa kuangalia jamii wanayoishi nayo na kusaidia watu wasiojiweza na binafsi anafanya hivyo kwa sababu riziki anayoipata Mungu huigawa kupitia kwa watu wengine.

“Sote ni binadamu tumeumbwa na Mungu ambaye anagawa riziki za watu (yatima,wajane na wenye umaskini mkubwa wa kipato).Wakati mwingine anagawa kupitia kwetu hivyo ni vizuri kutumia sehemu ya mapato yetu kuwakumbuka watu wa namna hiyo,”alisema.

Mfanyabiashara huyo wa madini alisema ni muhimu matajiri wenye uwezo kiuchumi kurejesha kwa Mungu sehemu ya mapato yao (sadaka na zaka) kupitia kwa jamii na kusaidia watu wenye mahitaji, ingawa ni wito lakini waone na wasukumwe na utashi wa nafsi zao.

“Jambo hili kulifanya linahitaji utashi na msukumo wa nafsi, hivyo tuliojaliwa uwezo kiuchumi tuwasaidie maskini wasiojiweza ili kutimiza matakwa ya Mwenyezi Mungu ya kusaidia yatima,wajane na wenye shida mbalimbali.Binafsi nitaendelea kufanya hivyo kadiri nitakavyojaaliwa na Mungu,” Nzuki.

Alidai ni mwaka wa pili kwake kuandaa chakula na kula pamoja na watoto yatima na anafanya hayo kupitia taasisi za dini ambazo zinafahamu changamoto za jamii na makundi ya wenye mahitaji kwa karibu na hivyo kuwa rahisi kuwapata wahitaji kwa urahisi na kuwasaidia kwa pamoja, kwa wakati mmoja.

Naye Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Sheikhe Hassan Kabeke alisema, kitendo cha Nzuki kuandaa chakula na kula na yatima pamoja anatapa thawabu kubwa kutoka kwa Allah (Mwenyezi Mungu) na kuwataka wengine kujifunza kutoa robo ya mapato yao kwa ajili ya jamii.

Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula ambaye pia alishiriki chakula hicho na watoto hao alisema BAKWATA imeshiriki masuala ya kijamii bila kubagua. jambo ambalo taasisi zingine zimeiga na kushindwa si kwa uwezo bali uhusiano na bila uhusiano ni ngumu kufanikiwa.
MFANYABIASHARA wa Madini Zakaria Nzuki, akishiriki kula chakula na watoto yatima .Chakula hicho kiliandaliwa kwa ajili ya sikukuu ya Idd el Fitri na MFANYABIASHARA huyo kwa kushirikiana na BAKWATA Mkoa wa Mwanza.

NEWS ALERT: Rais Magufuli kukutana na wafanyabiashara wa Nchi nzima kesho Ijumaa

WANANCHI WAASWA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE HOFU YA MUNGU

$
0
0
.Vero Ignatus,Arusha.

WANANCHI wameaswa kuchagua viongozi wenye hofu ya Mungu katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ambao wanakuwa na nia njema ya kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja bila ya kuwa na ubaguzi wa rangi kabila au dini.

Kadhalika wananchi wametakiwa kudumisha upedo na mshikamano miongonimwao bila kubaguana kwani ndio njia pekee ya kudumisha ushirikiano ambao hautaweza kuwagawanya au kuwatenga kwa itikadi na imani zao.

Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya monaban Trading and Farming ya jijini hapa,Dkt.Philemon Mollel,aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika baraza la Eid el Fitr,lililofanyika jana katika Taasisi ya Zawiyatul Qadiriyyat iliyopo Ngarenaro jijini hapa.

“Ndugu wakae pamoja kwa amani na upendo pia wakumbuke kuwasaidia watu wenye mahitaji maluum katika jamii wakiwemo  asikini,yatima,wajane na wazee wasijiweza kwani wao hawakupenda kuwa katika hali hiyo”alisema mollel.

Alikemea baadhi ya tabia ambayo wamekuwa nayo baadhi ya watu kwa kuwa na dharau na kuwanyanyapaa watu hao na kuwataka kutowatenga na kushirikiana nao kwa hali na mali na kuacha kuwatenga kwani wao ni binadamu kama walivyo wengine.

Katika baraza hilo la Eid,Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Monaban Trading and Company limited,Dkt.Philemon Mollel,alichangia lori kumi
za mawe na fedha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kingo ya mto ngarenaro ambao umekuwa ukileta adha kubwa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.

Awali Mwenyekiti wa Taasisi ya Twarika,Mkoani hapa,Abdi Omar Bin
Said,alisema kuwa taasisi yake imejikita zaidi katika utunzaji wa mazingira na kuhakikisha kuwa wanadhibiti kingo za mto ngarenaro kwa
kupanda miti zoezi ambalo wamekwisha lianza.

Amengeza kuwa kadhalika Taasisi hiyo pia imejikita katika kutoa elimu katika fani mbalimbali kwa lengo la kuwafanya vijana kupata elimu na ujuzi wa kuweza kujiajiri ikiwa ni pamoja na kulea watoto yatima na
wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo mpaka sasa wana vituo vitano.

Kwa upande wake mlezi wa taasisi hiyo hapa nchini,Salum Darwesh,alilisitiza umoja na upendo miongoni mwa madhehebu yote ya
dini na kusema kuwa ili mtu akamilike katika kutimiza majukumu yake ya kwa jamii ni lazim awe na vitu vitatu ambavyo ni afya njema na utu.

“Ukiwa na afya njema utaweza kusimama na kutembea popote,ukiwa na kitu ni rahisi kusema chochote na kutoa msaada kwa wahitaji na endapo una utu utawajali wenzako kuwathamini na kuwapenda"alisema Darwesh.

JUMLA YA 36 KUSHIRIKI MASHINDANO YA RITTA KABATI CHALLENGE CUP 2019

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Ritta Kabati Gerald Malekela akitoa maelezo kwa viongozi wa timu shiriki kwenye mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup msimu wa tatu 2019
Baadhi ya viongozi wa timu shiriki kwenye mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup msimu wa tatu 2019 wakiwa makini kusikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa mashindano.


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Jumla ya timu thelethini na sita (36) za mkoani Iringa kushiriki mashindano ya Ritta Kabati Challenge awamu ya tatu 2019 katika viwanja mbalimbali ya mpira wa miguu mkoani Iringa ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa siku ya jumamosi tarehe 15 / 06 / 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Ritta Kabati Gerald Malekela amesema kuwa timu zilizoshiriki mashindano hayo zinatoka katika wilaya ya Mufindi,Kilolo na Iringa hivyo inajumuisha wilaya zote za mkoa wa Iringa.

“Kwa mara ya kwanza tumepata timu nyingi kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini kwa kujitokeza timu kumi na moja hiyo inaonyesha jinsi gani kila kukicha mashindano haya yanazidi kuwa na mvuto na ushindani unaongezeka” alisema Malekela

Malekela alisema msimu huu mashindano yatakuwa bora kuliko misimu iliyopita kwa kuwa kamati imejipanga kuhakikisha wanatengeneza kitu kilicho bora na kuongeza thamani ya mashindano na kuweka alama ya kuigwa kwa wapenda michezo hasa mchezo huu wa mpira wa miguu.

“Tumejipanga kwelikweli kuhakikisha kuwa mashinda haya yanakuwa ya kiwango cha hali ya juu kiasi kwamba kila mtu atakuwa anavutiwa na mfumo wetu ambao tumekuwa tunautumia kuendesha mashindano haya” alisema Malekela

Malekela alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kukuza na kuibua vipaji vya wachezaji kutoka ngazi ya chini hadi kwenda kucheza ligi ambazo ni rasmi kama vile ligi daraja la kwanza la pili pamoja na ligi kuu katika nchi mbalimbali.

“Mwaka jana tulifaulu kwa kuhakikisha kuwa vijana wengi waliocheza mashinda haya walisajiliwa kwenye vilabu mbalimbli kuanzia ligi kuu hadi madalaja ya chini hivyo hayo nayo yalikuwa mafanikio makubwa kwetu” alisema Malekela

Aidha Malekela alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto ya ubovu na uhaba wa viwanja vya mpira wa miguu,hivyo tunaiomba serikali kuhakikisha wanatusaidia kuboresha viwanja hivyo

Changamoto za usafiri kanda ya ziwa victoria

$
0
0
Mmoja wa Wakazi wa Buchosa Wilaya ya Sengerema akipanda boti kwa shida,kama alivyonaswa na mpiga picha wa Globu ya Jamii mapema leo,akitumia ngazi kutokana na kutokuwepo kwa gati ya kupaki boti hizo  ambazo zimekuwa zikisaidia suala la usafiri ndani ya ziwa victoria,hata hivyo Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imejenga gati ya kisasa katika eneo hilo ili kuondoa adha hiyo inayowakumba wakazi wa maeneo hayo.


THE TRENDY SHOW S02 EP03 BY CYNTHIA MASASI-MZIRAY


CP LIBERATES SABAS ATETA NA WANANCHI KIJIJI CHA RUNGUNGU (RUFIJI),AFANYA OPERESHENI KALI KATIKA MAKAZI YALIOTUMIWA NA WAHALIFU

$
0
0
Kamishna wa Opereshni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberates Sabas,
akiwa katika picha ya pamoja na askari wa kikosi maalum cha kupambana na wahalifu katika pori la Rungungu liliopo Kijiji cha Rungungu katika Mkoa wa Kipolisi Rufiji baada ya kumaliza kufanya Operesheni maeneo hayo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberates Sabas,
akikagua mradi wa ujenzi wa Nyumba za Askari Polisi uliofadhiliwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,
katika eneo la Ikwiriri, Mkoa wa Kipolisi Rufiji na kulidhishwa na maendeleo
mazuri ya ujenzi huo. ( PICHA NA JESHI LA POLISI)
Kamishna wa Opereshni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi CP Liberates Sabas,
akizungumza na wanakijiji cha Rungungu baada ya kuwatembelea na kutaka kujua maendelea yao na Usalama wa Kijiji hicho, hatua hiyo ya kuwatembelea wanakijiji hao kamishna CP Sabas huifanya mara kwa mara kwasababu ya kijiji hicho ndicho kilikuwa makazi makuu ya wahalifu pamoja na eneo walilokuwa wakifanyia mafunzo yao kabla ya kutimiza azima zao katika kipindi cha miaka ya 2016 na 2017. (PICHA NA JESHI LA POLISI)

UNIGLOBE SKYLINK TRAVELS & TOURS SAY ASANTE SANA FOR YOUR PRECIOUS VOTES

DC SIMANJIRO AITAKA JAMII IMUIGE MNYALU

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (wapili kushoto) akipakua chakula kilichoandaliwa na mdau wa maendeleo Charlea Manyalu (watatu kulia) kwa ajili ya watoto yatima wa mji mdogo wa Mirerani. 
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula akizungumza na mmoja kati ya watoto waliohudhuria tafrija iliyoandaliwa na mdau wa maendeleo Charles Mnyalu kwa ajili ya watoto yatima, ambapo aliwaandalia chakula na kuwagawia madaftari, kalamu na nguo. 
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima wa mji mdogo wa Mirerani katika tafrija iliyoandaliwa na mdau wa maendeleo Charles Mnyalu. 

DC SIMANJIRO AITAKA JAMII IMUIGE MNYALU 

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula ameitaka jamii kuiga mfano wa mdau wa maendeleo Charles Mnyalu kwa kuwajali yatima ambao ni viongozi wa miaka ijayo kwani jukumu hilo siyo la serikali peke yake. 

Mhandisi Chaula aliyasema hayo mji mdogo wa Mirerani kwenye chakula cha pamoja kwa yatima kilichoandaliwa na mdau wa maendeleo Charles Mnyalu, aliyewagawia kalamu, madaftari na nguo. 

Alisema jamii iige mfano wa Mnyalu ambaye amejitolea kuwasaidia watoto hao bila ubaguzi wowote ule kwani nao watajihisi faraja na kusoma kwa bidii ili miaka ijayo wawe viongozi wakubwa kwenye nchini hii. 

Alisema watoto yatima wanapaswa kusaidiwa kwa hali na mali kwani wengi wao wazazi wao wamefariki dunia hivyo watu wengine kama Mnyalu wanatakiwa kuliangalia hilo kwa jicho la kipekee. “Watoto yatima hawa ni wa kwetu ndiyo viongozi wa leo na kesho tusipowatunza sasa hatutakuwa na viongozi wazuri miaka ijayo, kila mmoja kwa namna anavyoweza aige alivyofanya Mnyalu,” alisema mhandisi Chaula. 

Hata hivyo, mdau huyo wa maendeleo, Charles Mnyalu alisema ameamua kujitolea kidogo alichojaaliwa ili kuwapa faraja watoto hao yatima. Alisema japokuwa yeye hana utajiri wa kutosha ameona ajitolee kidogo alichonacho kwani maandiko ya madhehebu ya Kikristo yanaagiza ukiwa na mashati mawili mgawie mwenzako moja. 

“Watoto wadogo nawapenda sana tuombe Mungu tutakutana tena kwenye sherehe za Christmas mwezi Desemba ninawatakia kila la heri ndugu zangu wapendwa,” alisema Mnyalu. Mmoja kati ya watoto wa eneo hilo, Hamis Ramadhan alimshukuru mdau huyo wa maendeleo Mnyalu kwa kujitolea kuwasaidia watoto hao yatima. 

“Japokuwa hatuna wazazi lakini kitendo cha kufurahi pamoja na sisi tukale, tukanunuliwa nguo, madaftari na kalamu tumepata faraja kubwa,” alisema Ramadhan.

KAZI MPYA YA JHIKOMAN "UMOJA"

$
0
0

MBUNGE MAVUNDE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI KUOMBEA AMANI,MSHIKAMANO,UMOJA NA UPENDO MIONGONI MWA WATANZANIA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde ametoa rai kwa Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa Tanzania kushamiri katika umoja,mshikamano na Upendo na pia kuiombea serikali chini ya Mh Rais Dr John Pombe Magufuli katika kutimiza wajibu wake wa kuwaletea wananchi maendeleo. 
Mbunge Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa Uzinduzi ya Albamu ya Qaswida ya MANAAZIL ATQIYAAI ISLAMIC SOCIETY katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma,ambapo aliiomba jamii ya viongozi wa Dini kuwa mstari mbele kuhakikisha misingi ya Taifa Tanzania haivunjwi na Tanzania inaendelea kuwa moja yenye Amani,Upendo na Umoja 
Wakati huo huo,Mbunge Mavunde alinunua Albamu hiyo ya Qaswida Bayana kwa kiasi cha Tsh 1,000,000 na pia kuwaahidi kupata kiwanja cha kujenga majengo ya kudumu kwa ya Taasisi yao.

RC MAKONDA AREJESHA TABASAMU KWA PASCAL CASSIAN ALIEKUWA AMEPOTEZA MATUMAINI YA KUISHI, WALIOSEMA HAWEZI KUPONA HAWAAMINI KILICHOTOKEA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametembelewa ofisini kwake na Pascal Cassian ambae amefika kwa lengo la kutoa shukrani na kumthibitishia kuwa Amepona tatizo la Mfumo wa Figo na Kibafu cha mkojo lililokuwa likimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya familia yake kupoteza matumaini. 

Itakumbukwa RC Makonda aliona taarifa ya tabu na Mateso aliyokuwa akiyapata Pascal Cassian kupitia mitandao ya kijamii na kuagiza atolewe nyumbani apelekwe Hospital ya Muhimbili ambapo alitoa ahadi ya kugharamia matibabu yake ndani na nje ya nchi na hivi karibuni alimpatia kitita cha fedha kwaajili ya Matibabu nchini India, Tiket ya Ndege kwa watu watatu waliomsindikiza pamoja na fedha ya malazi kwa siku zote walizokuwa wakipata matibabu Nchini India. 

RC Makonda amemshukuru Mungu kwa kutenda miujiza kwa Pascal ambae aliondoka nchini akiwa amebebwa huku akiwa na mifuko ya kuhifadhi haja ndogo na leo Pascal anamtembelea RC Makonda ofisini akiwa anatembea kwa miguu na akiwa anajisaidia haja ndogo kama alivyokuwa zamani. 

Aidha RC Makonda amemshukuru Mungu kwa kumponya mtu ambae baadhi ya watu walisema hawezi kupona na wengine kusema hadharani kuwa pesa alizotoa RC Makonda kwaajili ya matibabu ni sawa na kutupa pesa kwenye shimo la choo. 

RC Makonda amewashukuru watu wote waliomuunga mkono kwa kumuombea Pascal hadi ameweza kupona huku akiwataka watanzania kuwa na moyo wa upendo na kusaidiana. 

Kwa upande wake Pascal Cassian amemshukuru RC Makonda na kumuhakikishia kuwa amepona na sasa anaweza kuendelea na shughuli zake za kutafuta kipato kama alivyokuwa awali. 

Nae Mke wa Pascal Cassian na watoto wake wamesema kuwa awali hao na familia pia walikata tamaa kwa hali aliyokuwanayo Pascal lakini walipata tumaini jipya pale walipohakikishiwa na RC Makonda atasimama bega kwa bega na familia hadi kuhakikisha anapona.

BIL.8 ZA JPM KUJENGA SOKO KUBWA LA KISASA HUKO KIBAHA MJI -BYARUGABA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA 

HALMASHAURI ya Mji Kibaha ,Mkoani Pwani inajenga soko kubwa, la kisasa kwenye eneo la kitovu cha Mji 
litakalogharimu takribani sh.bilioni 7.3. 

Fedha hizo za ujenzi huo ni kati ya kiasi cha sh.bilioni 8 zilizotolewa na serikali inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Dr.John Pombe Magufuli ambazo zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi mkakati ya halmashauri mbalimbali ambapo Kibaha mji imezielekeza katika mradi wa soko la kisasa  

Ofisa mawasiliano ,habari na uhusiano wa halmashauri ya Mji huo, Innocent Byarugaba ,aliwaambia waandishi wa habari kwamba, soko hilo litakuwa na ghorofa moja, linatarajiwa kukamilika mwezi disemba, 2019. 

Aidha alieleza, miundombinu mingine itakayokuwepo ni vyumba vya maduka 43, benki mbili, ATM 12, maegesho ya magari ya kawaida 150, malori ya mizigo 15, uzio wenye urefu wa mita 
565.4, tangi la chini ya ardhi la kuhifadhia maji lenye uwezo wa kuweka lita 110,000. 

Byarugaba alimtaja, mkandarasi aliyepewa tenda ni kampuni ya Elerai ya Jijini Arusha. “Tulikuwa hatuna soko la kisasa, tunaishukuru sana serikali kwa kuidhinisha kiasi hicho cha fedha” 

“Kwani usanifu umefanyika itatumika bilioni 7.3 kwa kujenga soko hilo kubwa huko karibu kabisa na stendi ya kisasa katika kitovu cha mji wetu ,”alifafanua Byarugaba. 

Pamoja na hayo, ofisa habari huyo alieleza ,halmashauri ya Mji imeanza pia ujenzi wa machinjio ya kisasa eneo la Mtakuja itakayogharimu sh.bilioni 1,968,505,115″:, fedha hizi ni ufadhili kutoka benki ya dunia kupitia mfuko wa uboreshaji na uendelezaji miiji (ULGSP).

Songas yatoa vifaa vya usafi vyenye thamani ya mil 10, Ubungo

$
0
0

 Meneja Uhusiano wa Jamii Kampuni ya Songas, Nicodemus Chipakapaka (kulia) akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Ubungo, Kisa Makori (Kushoto) vifaa vya usafi vyenye thamani ya Shilingi milioni 10 katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Manzese Bakhresa jijini Dar es Salaam, jana. Vifaa hivyo ni sehemu ya mchango wa Kampuni ya Songas ili kutia nguvu mpango wa serikali wa kutunza na kuhifadhi mazingira, hasa hasa tukielekea maadhimisho ya wiki ya mazingira inayosherekewa duniani kote kila tarehe 6 Juni.
 Meneja uhusiano wa jamii wa Kampuni ya nishati, Songas, Bw Nicodemus Chipakapaka (kushoto) akizungumza katika hafla ya ukabidhi wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Kisa Makori katika viwanja vya Manzese Bakhresa jijini Dar es Salaam wikiendi. Vifaa hivyo ni sehemu ya mchango wa Kampuni ya Songas ili kutia nguvu mpango wa serikali wa kutunza na kuhifadhi mazingira, hasa hasa tukielekea maadhimisho ya wiki ya mazingira inayosherekewa duniani kote kila tarehe 6 Juni.

OHOOOO....NI MUHIMU KUCHUKUA TAHADHALI KABLA YA AJALI

$
0
0
 Mmoja wa wakazi wa Geita akiwa amepanda bodaboda iliyosheheni mzigo na kukaa kwa mtindo wa Kike, ambao haruhusiwi na Watu wa Usalama barabarani kwani ni hatari kwa abiria huku dereva wake akiwa hajavaa kofia ngumu hali inayohatarisha maisha yao kama ikitokea ajali .PICHA NA HUMPHREY SHAO, MICHUZI BLOG.

WAKAZI WA BUCHOSA WAANZA KUFAIDI MABORESHO YA BANDARI YA LUSHAMBA

$
0
0
Kaimu Meneja wa Bandari ya Mwanza,Geoffrey Lwesya akizungumza na waandishi wa habari leo Wilaya ya Sengerema Halmashauri ya Buchosa jijini Mwanza, ambapo mamlaka ya bandari Tanzania(TPA) inajenga gati ya kisasa katika Mwalo huo kupunguza adha ya Wanawake Watoto na Wazee kupanda kwa shida katika boti zinazo fanya safari kutokea hapo kwenda visiwani. Waandishi wa Habari wapo katika ziara ya kutembelea na kutangaza miradi ya maendeleo ya bandari zilizo katika Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasan na kujionea maboresho yaliyo fanywa na TPA Katika awamu hii ya tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Mhandisi Abraham Msina akizungumza na Waandishi wa habari  kuhusu ya Maboresho yaliyofanyika katika Bandari ya Lushamba Wilayani Sengerema ambapo Mamlaka ya Bandari imekamilisha ujenzi wa gati ya kuegeshea Boti na Meli zinazofanya safari katika ziwa victoria kutoka eneo hilo kwenda visiwa vya ukara na vinginevyo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lushamba Wilaya Sengerema akishukuru Serikali ya Awamu ya tano chini ya Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwaondolea kero ya usafiri kwa kujenga gati ya kisasa na sehemu za kupumzikia abiria na jengo la mizigo katika Bandari ya Lushamba

Mmoja wa Wakazi wa Buchosa Wilaya ya Sengerema akipanda boti kwa shida,kama alivyonaswa na mpiga picha wa Globu ya Jamii mapema leo,akitumia ngazi kutokana na kutokuwepo kwa gati ya kupaki boti hizo ambazo zimekuwa zikisaidia suala la usafiri ndani ya ziwa victoria,hata hivyo Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imejenga gati ya kisasa katika eneo hilo ili kuondoa adha hiyo inayowakumba wakazi wa maeneo hayo.

Sehemu ya gati ya kupaki boti hizo ya kisasa inayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania itakayoondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa Buchosa ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika kama inavyoonekana
Jengo la kuhifadhia Mizigo katika Bandari ya Lushamba kama linavyoonekana kwa nje ambapo kwa sasa limekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Jengo la kupumzikia abiria katika bandari ya lushamba ambalo limekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 kama linavyooenekana, Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) Imefanya maboresho katika bandari ya lushamba ili kuondoa kero walizokuwa wanapata wananchi walikouwa wakitumia Mwalo huo.

Sehemu ya geti ya Bandari ya Lushamba inavyoonekana kwa nje 

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNI 7,2019

WAJUMBE WA KAMATI MAALUM WAKAGUA MIUNDOMBINU YA BANDARI KAVI JIJINI MBEYA

$
0
0

 Wajumbe wa kamati maalumu ya kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa Malawi wanayotumia bandari ya Dar es Salaam wakikagua miundombinu katika bandari kavu ya Malawi iliyopo Jijini Mbeya, ili kuhamasisha matumizi zaidi ya bandari hiyo kupunguza siku za kusafirisha mizigo kwenda Malawi. (Picha na Iddy Mwema)





Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images