Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

MATUKIO BUNGENI WAKATI BUNGE LIKIPITISHA BAJETI YA TRILIONI 11.94 YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020

0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za wabunge wakati wa kuhitimishwa kwa hoja za Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akieleza kuhusu makusanyo ya kodi kuongezeka, wakati wa kuhitimisha hoja za wabunge kuhusu Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja za wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wabunge na Mawaziri wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), baada ya kupitishwa kwa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.94 ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa tano kushoto), akiwa na watumishi wengine wa Wizara hiyo, wakifuatilia mijadala ya wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma, ambayo ilipitishwa kwa kishindo.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) (kushoto), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kushoto), kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, Bungeni jijini Dodoma.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb) (kulia), akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, baada ya Bunge kupitisha bajeti ya sh. trilioni 11.94 ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020, Bungeni Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya  Fedha na Mipango Bw. Doto James (wa kwanza kulia), akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Francis Mwakapalila, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaabani na viongozi mbalimbali wa Wizara wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipongezwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji baada ya  kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipongezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James baada ya  kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akipongezwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako baada ya  kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya  Fedha na Mipango Bw. Doto James, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti   Mhe. George Simbachawene, nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo Jiijni Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (wa pili kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara hiyo Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

Benki ya Exim Sasa Mdau Rasmi Uchangiaji Wa Damu Nchini

0
0
Benki ya Exim Sasa Mdau Rasmi Uchangiaji Wa Damu Nchini
Kilimanjaro; Juni 3, 2019: Benki ya Exim Tanzania pamoja na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) wameingi kwenye makubaliano rasmi ya utekelezaji wa pamoja wa mpango wa uchangiaji wa damu utakaohusisha matawi yote ya benki hiyo hapa nchini. 

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo ya uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’ 

Ushirikino huo umezinduliwa rasmi leo katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na benki hiyo kwenye tawi lake lililopo barabara ya Old Moshi katika Manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni urasmishaji wa jitihada za benki hiyo kwa kipindi cha miaka minane mfululizo katika uchangiaji wa damu hapa nchini,. 

Akizungumzia mpango huo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Staniley Kafu alisema unaenda sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” na kwamba unalenga kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa.
“Kampeni hii ni sehemu ya uthibitisho kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashiriki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.’’ Alisema Kafu. 

Akizungumzia kuhusu makubaliano hayo na NBTS, Kafu alisema benki hiyo itawezesha mpango na utekelezaji wa uchangiaji damu kwenye kambi nane (8) za uchangiaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Tanga, Mtwara na Zanzibar huku ofisi ya Mpango wa Taifa Damu Salama wakisimamia masuala yote ya kitabibu katika mpango huo. 

“Zaidi benki ya Exim kwa kushirikiana wadau wote wa mpango huu wakiwemo Mpango wa Taifa Damu Salama , Wizara ya Afya na wadau wa habari tutahusika na kuratibu mikakati ya uelemishaji na uhamasishaji wa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika suala hili muhimu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Duniani.’’ Alisema Kafu 

Kwa upande wake Menaja wa NBTS Kanda ya Kaskazini Dk Edson Mollel alisema ofisi hiyo inahitaji kukusanya chupa (units) 526,000 za damu ili kukidhi mahitaji ya kila mwaka kwa nchi nzima ambapo kiasi kilichpatikana mwaka jana ilikuwa ni chupa 307,835 sawa na asilimia 58 ya mahitaji. 

“Mwaka huu lengo nikukusanya chupa 357,000 za damu na kupitia maadhimisho ya mwaka huu pekee tumejipanga kukusanya chupa 41,920 na ndio maana tunaridhishwa sana wanapojitokeza wadau kama benki ya Exim ili kutuunga mkono…uhitaji wa damu ni mkubwa.” 

“Hatua hii ni mfano wa kuigwa kwa kuwa benki ya Exim na wafanyakazi wake wanakuwa sehemu ya jamii wanayoihudumia kwa ukaribu zaidi na pia wanathibitisha rasmi mioyo yao ya kujitolea kwa hali na mali kwa jamii wanayoihudumia,’’ alisema 

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii. Katika miaka minane iliyopita benki imechangia zaidi ya lita 100 za damu katika Benki ya damu taifa

Meneja wa Benki ya Exim Kanda ya Kaskazini Bw Amos Lyimo (Kushoto) pamoja na Meneja wa benki hiyo tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro Bw Masood Abutwalib (Kulia) wakichangia damu ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uchangiaji damu kila mwaka kupitia matawi yake yote hapa nchini kwa ushirikiano na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).Anaewahudumia ni mtaalamu wa afya kutoka NBTS Bi Marygoreth LaswaiTaarifa kwa vyombo vya habari

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tawi la Moshi pamoja na wateja wa benki hiyo wakiendelea taratibu za uchangiaji wa damu uliofanyika kwenye kwenye viunga vya tawi la benki hiyo Manispaa ya Moshi leo.

WAZIRI HASUNGA AIAGIZA COASCO KUKAGUA VYAMA VOTE VYA USHIRIKA

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za COASCO makao makuu Jijini Dodoma leo tarehe 3 Juni 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za COASCO makao makuu Jijini Dodoma leo tarehe 3 Juni 2019.
Sehemu ya watumishi wa COASCO wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za COASCO makao makuu Jijini Dodoma leo tarehe 3 Juni 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Uongozi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limetakiwa kukagua vyama vote vya Ushirika na kuwasilisha taarifa ya ukaguzi huo ofisi ya Waziri wa Kilimo kwa ajili ya hatua stahiki.

Mhe Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo ametoa agizo hilo leo tarehe 3 Juni 2019 wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa COASCO makao makuu sambamba na wakaguzi wa mikoa kwenye kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za COASCO makao makuu Jijini Dodoma.

Alisema kuwa lengo kuu la COASCO ni kuhakikisha kuwa vyama vya ushirika vinakidhi matakwa ya kisheria na misingi ya kuanzishwa kwake ili wanaushirika na vyombo vyao vinakuwa salama kulingana na makubaliano, katiba na sheria zilizopo vile vile kusimamia sheria za ushirika na sheria za biashara wanazofanya ikiwa ni pamoja na sheria na sera za nchi na utawala bora.

“Nakuagiza Kaimu Mtendaji Mkuu kuhakikisha kuwa unakagua vyama vyote vya ushirika, mimi nisingependa nikikuomba ripoti ya ukaguzi uniambie eti kuna vyama vingine hujakagua na taarifa ya ukaguzi iwasilishwe katika ofisi yangu” Alisisitiza Mhe Hasunga

Aliongeza kuwa huduma za ukaguzi zinazotolewa na Shirika zinasaidia kuimarisha utawala bora katika vyama vya ushirika, kuwajengea imani wanachama wa vyama vya ushirika juu ya shughuli zinazofanywa na vyama vyao na hivyo kuongeza uzalishaji na kuboresha huduma zinazotolewa na vyama vya Ushirika.

Mhe Hasunga pia alimuagiza kaimu Mtendaji mkuu huyo kuhakikisha kuwa anapeleka mapendekezo ya viongozi waliopo katika vyeo vyao ili kuweza kuthibitishwa kwa wale wanaostahili.

Kwa kutambua mchango wa ushirika katika mageuzi ya kiuchumi hasa kwa wakati huu ambao serikali ya awamu ya tano inakusudia kuingia katika uchumi wa kati (kupitia agenda ya Tanzania ya Viwanda), Hivyo ili kufanikisha agenda hiyo wametakiwa kutafuta vyanzo vipya vya mapato.

Aliongeza kuwa Vyama vya ushirika vina nafasi kubwa kuinua uchumi ikiwa tu usimamizi wa sheria na kanuni utaimarishwa kama inavyojidhihirisha katika serikali ya awamu ya tano.

Alibainisha pia kuwa, udhaifu katika usimamizi wa mifumo ya ufatiliaji ni moja ya changamoto zilizosababisha vyama vingi vya ushirika kutumbukia katika matatizo na kupelekea vyama vingi kufilisika.

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) ni Shirika la Umma lililoanzishwa kwa Sheria Na. 15 ya mwaka 1982 kwa lengo la kutoa huduma za ukaguzi na Usimamizi kwa Vyama vya Ushirika Tanzania.

Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2005 ili kupanua wigo wa huduma za Shirika za Ukaguzi na Ushauri kutolewa kwa vyama vya ushirika pamoja na taasisi za Umma, makampuni binafsi, mabenki na wateja wengine.

MKURUGENZI RASILIMALI ZA MAJI WIZARA YA MAJI ARIDHISHWA NA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA TANGA UWASA PAMOJA NA MRADI WA SLM

0
0
 MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera katikati akitazama kikundi cha utunzaji wa mazingira cha Uwamakizi wakati ametembelea vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM) kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Wizara Maji Obadia Kibona.
 Mratibu wa mradi wa kunusuru vyanzo vya maji kupitia matumizi bora ya ardhi (SLM) Mhandisi Maximilian Sereka ambapo  alisema mradi huo ulianza mwaka 2016 sasa wapo ndani ya mwaka wanne kwenye utekelezaji wa mradi huo.
 MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera kulia akiangalia miti aina ya mitiki iliyopandwa kwenye Kijiji cha Sembekeza wilayani Muheza wakati alipotembela vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM).
 MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera katikati akionyeshwa namna miti ya mitiki inavyopandwa wakati alipotembela  vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM).
 Mtaalamu wa Mazingiwa Tanga Uwasa Ramadhani Nyambuka kushoto akisisitiza jambo kwa MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera
 Mhandisi Rashid kutoka Tanga Uwasa kushoto akiwaongoza wataalamu mbalimbali
 MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera akitazama namna miche ya mitikiti inavyopandwa
 Wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufika kwenye ofisi za Umoja wa Wakulima Wahifadhi wa Mazingira Kihuhwi Zigi

 Kikundi cha Uwamakizi kikitoa burudani
 Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali
MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera kwenye shuti nyeusi katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na kikundi cha Uwamakizi

MKURUGENZI wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji George Mvomera ametembelea vikundi vya uwamakizi na kuona namna wanavyotunza vyanzo vya maji katika eneo dogo la Bonde la Mto Zigi wilayani Muheza huku akiridhishwa na juhudu zilizofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) pamoja na mradi wa kunusuru vyanzo vya maji (SLM).

Mradi huo unasimamiwa na Wizara ya Maji chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambao umeweza kusaidia utunzaji wa vyanzo vya maji ikiwemo upandaji wa miti kwenye maeneo husika na hivyo kufanya maeneo hayo maji kutiririka mwaka mzima.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo ikiwa ni kusheherekea wiki ya mazingira, Mvomera alioneshwa kuridhishwa na utunzaji wa mazingira unaofanywa na Uwamakizi huku akiwataka wananchi kote nchi kujiunga kwenye vikundi vinavyojihusisha na namna ya kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji ikiwemo kupanda miti rafiki inayotunza maji katika kipindi cha kiangazi.

Alisema wameona kazi kubwa na nzuri inayofanyika kwenye eneo hilo kwani miaka ya nyuma mito hiyo ilikuwa haititirishi maji lakini sasa hivi kutokana na uwepo wa utunzaji wa mazingira maji yameanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida na hilo ndio lengo lao nchi nzima wananchi wajiunge kwenye vikundi na kujihusisha na namna ya kutunza mazingira leo.

“Lakini katika kusheherekea wiki ya mazingira lengo la mwaka huu ni kuhamasisha wananchi kmuacha kutumia mifuko ya plastic lakini pia tumejifunza mengi zaidi miti inayopandwa lazima iweze rafiki kwenye utunzani wa vyanzo vya maji kwani inachangia uwepo wa maji kwenye mito kipindi cha kiangazi”Alisema.

Mkurugenzi huyo alisema miti hiyo inasaidia kufanya mito kutiririsha maji mwaka mzima kwenye maeneo ya vyanzo hizyo huku akikipongeza kikundi cha Uwamakizi kwa kuhifadhi mazingira na Mto Zigi na mito mingine midogo inayoingiza maji kwenye mto huo.

Aidha alisema pia wanategemea kuanzisha mfuko wa maji (Water Fund) kwenye eneo la Uwamakizi kwa kushirikiana na Tanga Uwasa na wadau wengine kuunda mfuko huo ili mradi huo uwe endelevu uhifadhi wa mazingira uendelea kwenye maeneo mengi zaidi ya bonde dogo la mto Zigi ambayo ni sehemu ya bonde la Mto Pangani.

“Niwapongeza uwamakizi kwa kazi nzuri wanayoifanya lakini nitoe wito maeneo mengine Tanzania waende kujifunza uwamakizi namna ya kutunza vyan zo vya maji namna inavyoileta faida kwa wananchi wanalima kokoa mitiki inayowezesha kujiongeza kipato na kutunza maji kwa kupanda mazao mbadala ya mahindi na maharage ambayo yangewezea kuharibu vyanzo hivyo”Alisema.

Hata hivyo alisema Wizara ya Maji imekuwa ikisaidia maeneo mengi kuanzisha vyama vya watumiaji wa maji kwa nguvu ya wizara maeneo mengine wa usafiri na ofisi faida za jumuiya za watumiaji maji zinasaidia kutatua changamoto za utunzaji wa maji na mazingiea eneo la uwamakizi watafanya kila njia kuwatafutua usafiri wa pikipiki kwa sababu ni eneo kubwa kupitia mradi wa kunusuru.

Naye kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kunusuru vyanzo vya maji kupitia matumizi bora ya ardhi (SLM) Mhandisi Maximilian Sereka alisema mradi huo ulianza mwaka 2016 sasa wapo ndani ya mwaka wanne kwenye utekelezaji wa mradi huo.

Alisema mradi huo unatekelezwa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Maendeleo Dunia (UNDP) pamoja na Mfuko wa Mazingira (GF) kwa kipindi cha miaka minne ya utekelezaji kwa kushirikiana na sekta mbalimbali wamepata mafanikio mengi ikiwemo utoaji wa elimu kwenye maeneo yote mawili Ruvu na Zigi hivyo kuwafanya wananchi kuwa na uelewa mkubwa ukilinganisha na kipindi wanaanza mradi.

Mratibu huyo alisema pia kumekuwepo na ushirikianao kwenye sekta mbalimbali wakati wa utekelezaji wa mradi huo ambao unaratibiwa na sekta ya maji kwa kushirikiana ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Wizara ya Kilimo,Mifugo,

“Lakini pia sekta za serikali mbalimbali ikiwemo mamlaka za maji ya Tanga Uwasa,Moruwasa na Dawasa lakini pia wilaya mbalimbali wanazoshirikiana nazo kwa ukaribu zaidi wilaya za Tanga na Morogoro”Alisema

JAMII YATAKIWA KUACHA KUWANYANYAPAA NA KUWAFICHA WATOTO WENYE MATATIZO YA MGUU KIFUNDO

0
0
Baadhi ya Viongozi wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa wamebeba mabango katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Madaktari wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania wakiwa katika matembezi ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Daktari bingwa Upasuaji Mifupa na Majeruhi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina,akizungumza na baadhi ya akina mama wenye watoto wenye ulemavu wa mguu Kifundo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe ,akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe,akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Bw.Emmanuel Kowero katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe,akitoa maelezo kwa Mratibu Miguu Kifundo kanda ya Kaskazini Bw.Goodluck Pallanayo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.
Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, akikata utepe mara baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma
Daktari bingwa Upasuaji Mifupa na Majeruhi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa wadau wanaojihusisha na matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina akiagana na Mganga Mkuu Mkoa wa Dodoma Dkt.James Kiologwe, baada ya kuzindua Cliniki ya Kutibu watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma
Daktari Bingwa Upasuaji Mifupa Hospitali ya Bugando akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo sambamba na ufunguzi wa Cliniki kitaifa yamefanyika jijini Dodoma.

...................................

Na.Mwaandishi Wetu,Dodoma
Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa Mkoa, Dodoma Dkt.James Kiologwe amewaomba wazazi /walezi pamoja na wananchi kutowafungia ndani watoto wenye matatizo ya mguu kifundo.

Watanzania wameungana na mataifa mengine Duniani katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo ambapo zaidi ya watoto elfu mbili mia tano nchi nzima hugundulika kuwa na tatizo la ulemavu wa mguu kifundo kila mwaka hapa nchini.

Akizungumza katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mtoto mwenye matatizo ya Mguu Kifundo yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma Sambamba na Ufunguzi wa Cliniki ya kutibu Dkt.Kiologwe amesema kuwa jamii inatakiwa kubadilika na kuacha tabia ya kuwaficha na kuwanyanyapaa watoto wenye Ulemavu huo.

Aidha amewapongeza wakina mama walioitikia wito na kupeleka watoto wao wenye changamoto ya mguu kifundo, pamoja na wadau waliodhamini maadhimisho hayo ikiwemo TCCO kwa kuchagua mkoa wa Dodoma kama sehemu yakwanza kuadhimisha maadhimisho ya watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo.

Pamoja na hayo amepongeza taasisi mbalimbali kwa kushirikiana na TCCO, kwani wamesaidia kuwaondolea adha watoto pamoja na vijana ambao walikuwa wanaishi kwenye mazingira ya unyanyapaa lakini wafadhili kwa kushirikiana na TCCO pamoja na wadau mbalimbali wamerejesha heshima ya utu wa mwanadamu.

Ameongeza kuwa TCCO imeshahudumia watu zaidi ya elf nne, ambao wamefanyiwa marekebisho ambapo ni watanzania wengi wamerejeshewa heshima yao ya utu pamoja na mwonekano.
“ Pongezi nyingi ni kwaajili ya nia iliyomo mioyoni mwetu lakini nilikuwa nawaambia watu kazi ya utabibu ni zaidi ya kazi ya uaskofu na nizaidi ya kazi ya upadre sisi tunamwangalia mtu kwa ujumla wake” amesema Dkt. Kiologwe

Pia Dkt. Kiologwe ameeleza kuwa thamana waliopewa matatibu ni kubwa kwani kuanzia kuzaliwa mpaka kufa kwa mwanadamu Daktari pekee ndiyo mwenye kutekeleza shughuli zote hizo hata pale inapohitajika kumrekebisha madaktari hufanya hivyo pia wanawashukuru wote waliojitokeza kushiriki maadhimisho hayo.

Aidha amesema kuwa TCCO wanajumla ya matawi 35 kote nchini (kliniki), ambapo Dkt. Kiologwe ameomba taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali kuanzisha kliniki kwenye kila mkoa na wilaya kwani takribani katika kila watoto elf moja wanaozaliwa mtoto mmoja anazaliwa na mguu kifundo.

Awali akizungumza amesema kuwa changamoto ya ufanisi imekuwa tatizo kubwa sana kwa watoto wenye ulemavu wa mguu kifundo hasa kwenye utendaji wa kazi, elimu, kushiriki kwenye masuala ya uchumi pia adha ya kuishi kwenye jamii.

Ambapo ni wastani wa watoto 120, kwa mwaka wanazaliwa kwenye mkoa wa Dodoma peke yake wakiwa na ulemavu wa mguu kifundo ikiwa ni pamoja na kukumbana na adha ya kwenda kwenye matibabu ambapo watu wengi wamezoea masuala yote yanayohitaji marekebisho yanafanyika kwenye hospitali ya CCBRT, ambayo pia ni msaada mkubwa katika nchi kwani elimu kuhusu wapi matibabu ya ulemavu wa mguu kifundo yanapatikana hivyo elimu yakutosha inatakiwa kutolewa kwa umma ili kujua ni wapi matibabu ya ulemavu wa mguu kifundo yanapatikana.

Pia ameeleza changamoto ambazo zinapelekea watu kushindwa kupata matibabu hayo ni pamoja na kipato, ambapo kwa uzinduzi wa kliniki hiyo ya marekebisho ya mguu kifundo yatakuwa yanafanyika kila alhamisi na kwa watoto wote chini ya umri wa miaka mitano matibabu yatakuwa bure.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Muungano wa Wadau wanaojihusisha na Matibabu ya Mguu Kifundo Tanzania Dkt.Robert Mhina amesema kuwa bado kuna changamoto miongoni mwa jamii wakihusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina ambapo amesema wanaendelea kutoa Elimu kwa jamii ili iache kuwanyanyapaa watoto wenye matatizo ya Mguu Kifundo.

''Rai yangu kwa wazazi/walezi pamoja na wananchi kiujumla waache kuwafungia na kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani tatizo hilo linaponyeka hivyo jamii iache tabia ya kuwanyanyapaa pamoja na kuhusisha ugonjwa huu kwa imani za kishirikina''amesema Dkt.Mhina
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya Wazazi wenye watoto wenye matatizo ya mguu Kifundo wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo unyanyapaa miongoni mwa jamii hivyo wameiomba Serikali kufanya msko na kuwachukulia hatua baadhi ya wazazi wanaowaficha watoto wenye matatizo hayo ya Ulemavu


MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 4,2019

'WASANII WA NANDY' WAPATA AJALI BAADA YA GARI YAO KUPINDUKA ENEO LA MIKUMI

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

GARI aina ya Coaster iliyokuwa imebeba wasanii ambao wapo kwenye msafara Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy imepata ajali eneo la Mikumi mkoani Morogoro.

Hata hivyo inaelezwa hadi sasa hakuna aliyepoteza maisha kutokana na ajali hiyo ila baadhi ya wasanii wamepata majeraha.Ajali hiyo imetokea mapema leo katika eneo hilo na inaelezwa wasanii hao walikuwa wanaelekea Sumbawanga.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu ya mkononi, Meneja wa Msanii Nandy amesema ni kweli kuna ajali imetokea na wao wamepata taarifa na kwa sasa wanafuatilia na kisha watatoa taarifa kamili.

"Tumepata taarifa kuwa Coaster iliyokuwa imebeba wasanii imepata ajali eneo la Mikumi.Kwa sasa tunafuatili ili kujua kinachoendelea na hali za watu wetu na baada ya hapo ndio tutakuwa na taarifa rasmi ya kueleza kuhusua ajali hiyo"amesema Meneja huyo.

Chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika ingawa baadhi ya mashuhuda wanadai eneo hilo kulikuwa a gari aina ya roli iliyokuwa imeharibika barabarani.

Hivyo dereva wa Coaster wakati anataka kuipita akaona kuna gari nyingine inakuja mbele yake na wakati anataka kukwepa ndipo akapoteza muelekeo.

Hata hivyo inaelezwa Nandy hakuwa kwenye gari iliopata ajali hiyo kwani alikuwa kwenye gari nyingine lakini naye alikuwepo eneo ambalo Coaster hiyo imepata ajali.Michuzi Blog itaendelea kukupa taarifa zaidi ya kinachoendelea.

TANZANIAN FOOTBALL FANS TREATED TO AN EXCLUSIVE HEINEKEN EXPERIANCE DURING THE UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINALS

0
0
Heineken Tanzania over the weekend engaged and excited over 1000 Tanzanian football fans at the culmination of 2019 UEFA Champions League (UCL) final between Tottenham Hotspur, and Liverpool. Liverpool thrashed Tottenham 2 -0 and were crowned 2019 UCL champions.

Heineken Tanzania is all set to engage and excite throngs of Tanzanian football fans at the culmination of 2019 UEFA Champions League (UCL) final between Tottenham Hotspur, and Liverpool to see who will emerge with bragging rights at being crowned 2019 UCL champions.

Madrid was the venue for the second all-English UEFA Champions League final as Tottenham Hotspur, at this stage for the first time in their history and a Liverpool side bidding to put aside the pain of their defeat by Real Madrid in the 2018 showpiece.

And, Tanzanian Football fans shared in the moment, at various outlets across the country, where Heineken presented the biggest viewing parties ever. The Heineken viewing parties, besides the main showpiece which is the UEFA Champions League Final, will also featured chances to win awesome Heineken merchandize and a surprise live performance from Ray Vanny From Wasafi records

The core focus for Heineken is to bring unique experiences to fans of UEFA Champions League in Tanzania. As the most prestigious platform for European football stars, this premier-sporting event has become global and fits perfectly with the Heineken brand,” said Lungisa Adams, Heineken Tanzania Country Manager.

Both these great clubs played an excellent game, Lungisa said. Both almost went out in the group stage and now one emerged victorious. It was truly an epic match.”

Heineken has been a big part of football for the last 25 years, particularly by sponsoring the UEFA Champions League. During this time, we have been giving our fans the opportunity to connect with club football’s biggest competition, while also rewarding their passion by taking some lucky few to Europe in the past. The #ShareUnmissableMoments consumer campaign in Tanzania is just another way for us to delivering on the brand promise.”

Through the course of the UEFA Champions League season, Heineken has continued its remarkable tradition of celebrating the beautiful game with fans, bringing all the action from Europe to Tanzanians more than 5,000 miles away with its premium viewing experiences. 

Heineken, has been a long-standing sponsor of the UEFA Champions League since 1994. This illustrious collaboration with club football’s biggest and most watched competition has seen Heineken become one of the most recognizable brands in the world of football.

Over the Last 25 years, we’ve seen the brand share the passion of the beautiful game while bringing all the most remarkable and Unmissable Moments from the competition to fans around the world.
The Dutch brewer is a keen sponsor of global sports tournaments and unlike other industry players steers clear from sponsoring specific teams.  


Benki ya Stanbic yatoa msaada wa TZS 20 mill kusaidia ujenzi wa darasa kituo cha watoto wetu.

0
0
 Meneja wa Data wa Benki ya Stanbic Tanzania, Ally Masoud (wa tatu kushoto), akimkabidhi Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Evans Tegete mfano wa hundi ya thamani ya Sh. Milioni 20, ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kusaidia ujenzi wa madarasa kwenye kituo hicho kilichopo kijiji cha Mazizi kata ya Msata mkoani Pwani hivi karibuni. Benki ya Stanbic imekuwa ikisaidia kituo hicho kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalumu wanapata elimu bora. Wengine ni wafanyakazi wa benki ya Stanbic pamoja na wafanyakazi na watoto wa kituo hicho.

Wabunifu VETA wapata ufadhili wa milioni 85 kutoka COSTECH

0
0
Wabunifu wa Ufundi Stadi, chini ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), wamepata ufadhili wa jumla ya Shilingi 85 milioni kutoka kwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ajili ya kuendeleza ubunifu wao. 

Mkataba kwa ajili ya ufadhili huo umesainiwa leo tarehe 3 Juni 2019 katika ofisi za COSTECH jijini Dar es Salaam, kati ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu, na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu.

Ubunifu utakaopatiwa ruzuku ni “Pikipiki Salama” ya Mwl. Aneth Mganga wa Chuo cha VETA Kipawa, “Mashine ya Kufukuza Ndege Waharibifu Mashambani” ya Mwl. Emmanuel Bukuku wa Chuo cha VETA Dar es Salaam (Chang’ombe) na “Kifaa cha Kufundishia Elimu ya Mfumo wa Jua na Sayansi ya Anga” cha Ndg. Ernest Maranya, Mbunifu na Mhitimu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu, amesema VETA imebeba jukumu la kuwasimamia na kuwadhamini wabunifu hao na kwamba Mamlaka hiyo itahakikisha ubunifu huo unakamilika na kuingia sokoni kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Baada ya kupokea ufadhili huo, mmoja wa wabunifu hao, Mwl. Emmanuel Bukuku, amesema kuwa anaamini ruzuku hiyo itamsaidia kuboresha ubunifu wake na kuhakikisha kifaa chake cha kufukuza ndege waharibifu mashambani kinaingia sokoni na kuwasaidia wakulima kulinda mazao yao mashambani na hatimaye kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.

Naye Mwl Aneth Mganga alisema kuwa ruzuku hiyo imekuja wakati mwafaka ambapo anatamani kuboresha ubunifu wake wa “Pikipiki Salama” ili kusaidia kupunguza athari za ajali za barabarani kwa watumiaji wa pikipiki na wizi wa pikipiki, hasa zile zinazotoa huduma ya usafiri wa kibiashara (maarufu kama bodaboda). Ajali hizo zimekuwa zikisababisha vifo au ulemavu kwa vijana wengi nchini.

Kwa upande wake Ndg. Ernest Maranya ameishukuru COSTECH na VETA na kusema kuwa ruzuku hiyo itamsaidia kwa kiasi kikubwa kufanya maboresho muhimu kwenye kifaa chake na kutatua changamoto iliyokuwa ikimkabili ya gharama za uagizaji wa malighafi nje ya nchi iliyosababishwa na ufinyu wa fedha.


 Amesema kuwa kifaa hicho kikikamilika kitakuwa msaada mkubwa katika kufundisha elimu ya mfumo wa jua na sayansi ya anga, hasa kwa elimu ya msingi na sekondari. Ametoa wito kwa wabunifu wengine kujitokeza na kusajili bunifu zao ili wale watakaokidhi vigezo waweze kunufaika na ufadhili kama huo wa Serikali ya Awamu ya Tano kupitia COSTECH.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt.Pancras Bujulu(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu(kushoto) wakitia saini mkataba wa ufadhili kwa wabunifu wa VETA
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt.Pancras Bunjulu akipeana mkona na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Amos Nungu mara baada ya kusainiana mkataba
Picha mbalimbali wakati wa kusainiana mkataba.

TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA

0
0

TANGAZO KWA UMMA


TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kwamba, kuanzia tarehe 20 Mei, 2019 malipo yoyote Kwa Wizara yanafanyika kwa njia ya Kielektroniki kupitia mfumo wa GOVERNMENT ELECTRONIC PAYMENT GATEWAY (GePG).

Hivyo, wateja wote watakao hitaji kufanya malipo ya uthibitisho wa nyaraka mbalimbali zikiwemo; vyeti vya talaka, ndoa, kuzaliwa, Kifo n.k wanapaswa kabla ya kufanya malipo yoyote kuwasiliana na ofisi za Wizara kupitia vituo vyake vilivyopo Dodoma, Dar es salaam na Zanzibar ili kupatiwa ‘Control Number’ ili kufanikisha malipo husika kupitia Akaunti ya Benki ya CRDB. 

Wateja wanaoleta nyaraka hizo kwa uthibitisho, wanaendelea kukumbushwa pia kukamilisha hatua muhimu kabla ya kupatiwa ‘Control Number’ ikiwemo kupelekwa kwanza katika Mamlaka na Taasisi husika zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitishwa. 

UMMA WOTE UNAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA, MALIPO YOYOTE YATAKAYOFANYIKA KINYUME NA MAELEKEZO BAADA YA TANGAZO HILI, HAYATOPOKELEWA 

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 

TCRA yatoa Msaada vyakula Katika Mkoa wa Mtwara na Lindi

0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii,Mtwara na Lindi

Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki (TCRA) imetoa Msaada wa Vitu mbalimbali katika Kituo cha Raha Leo mkoani Mtwara, Shule ya Sekondari WAMA Sharaf mkoani Lindi pamoja Kituo cha Wazee Wasiojiweza mkoa huo wa Lindi kwa ya ajili ya kushiriki Idd inayotarajiwa kufanyika kesho.

Msaada huo waliotoa TCRA ni Mchele,Unga wa Ngano, Mbuzi pamoja na mafuta ya kula ikiwa kwa sikukuu na kuendelea baada ya sikukuu. 

Akizungumza wakati wa Kukabidhi misaada hiyo Kaimu Mkuu wa Kanda ya TCRA Mhandisi Ikuja Jumanne amesema kuwa Msaada huo ni kuajili ya watoto hao kushiriki sikukuu ya Idd kwani hakuna sababu Kama mamlaka kuacha jamii isiokuwa na uwezo kushindwa kushiriki sikukuu ya Idd.

Jumanne amesema kuwa wao wameandaa vitu huku wakitambua vituo na shule mahitaji mengi hivyo watafanyia Kazi changamoto zingine wakati mwingine. Aidha amesema kuwa watoto na wazee watambue wanaangaliwa kwa ukaribu ndio maana wamejitoa katika misaada hiyo. 

Akipokea msaada Msimamizi wa Kituo cha EAGT Raha Leo mkoani Mtwara Caroline Mkuwele amesema kuwa msaada huo umekuja kwa muda mwafaka na kufanya watoto washiriki sikukuu ya Idd na muda mfupi kutokana na msaada huo. 

Mkuwele amesema kuwa TCRA wamejitoa kwa nguvu zote ikiwa na kuona raha Leo wana uhitaji wa msaada. "Mmetoka mbali hadi kutufikia sisi wana Mtwara kwa kweli mmeonyesha moyo wenu unajali jamii katika utatuzi wa baadhi ya changamoto licha ya kuwepo kwa sikukuu ya Idd"amesema Mkuwele.

Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea Wazee Wasiojiweza Simon Mnnimbo amesema kuwa TCRA inatambua watu wenye changamoto na kutaka wadau wengine waige hasa wa watu waliopembezoni.

Kwa upande wa Mwalimu wa Sekondari ya WAMA Sharaf Samson Massawa amesema kuwa TCRA amewaongoza kwa kuona Shule ya WAMA wanauhitaji wa Chakula kwa ajili ya Watoto hao kwani wapo shule na wametoka katika familia zisizo na uwezo pamoja wengine kuwa wajane.
 Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa TCRA Kanda ya Mashariki  wakiwa picha ya pamoja na watoto wa Kituo cha EAGT Raha Leo mkoani Mtwara.
 Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Ikuja Jumanne akikabidhi msaada kwa msimamizi wa Kituo cha EAGT Raha Leo mkoani Caroline Mkuwele kwa ajili sikukuu ya Idd.
 Msimamizi wa Kituo cha EAGT Raha Leo mkoani Mtwara Caroline Mkuwele akitoa neno la Shukurani mara baada y ya kupokea msaada kutoka TCRA Kanda ya Mashariki.
 Vyakula Vya Msaada katika Kituo cha EAGT Raha Leo mkoani Mtwara.
 Msimamzi wa Kituo cha EAGT Raha Leo mkoani Mtwara Caroline Mkuwele akiomba na watoto Mara baada ya kupokea Msaada kutoka Kanda ya Mashariki ya TCRA
 Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Ikuja Jumanne akitoa msaada wa vyakula katika Shule ya Sekondari ya WAMA Sharaf kwa ajili ya Sikukuu ya Idd.
 Wanafunzi wa WAMA Sharaf wakisikiliza neno kutoka TCRA
 Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Ikuja Jumanne akizungumza katika Kituo cha EAGT Raha Leo  mkoani Mtwara.
 Shule ya Sekondari WAMA Sharaf Lindi wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa TCRA Kanda ya Mashariki

taarifa kwa wamiliki na watumiaji wa vyanzo vya mionzi nchini

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR AISHAURI KAMPUNI YA BIMA YA UAP KUENDELEA KUWA KARIBU NA WATEJA WAKEWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR AISHAURI KAMPUNI YA BIMA YA UAP KUENDELEA KUWA KARIBU NA WATEJA WAKE

0
0
Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

 WAZIRI wa Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Mohammed Ramia Abdiwawa ameishauri Kampuni ya Bima ya UAP kuendeleza utaratibu wake wa kuwa karibu na wateja wake ambao wanaopatikana Zanzibar.
Waziri Abdiwawa ametoa ushauri huo wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na kampuni hiyo ya bima ndani ya HotelVerde mjini hapo ambapo amesema wanaishukuru  kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake kwa lengo la kuendelea kudumisha mshikamano uliopo baina yao.

 "Na ningeomba kwa hili niwapigie debe kwani ni Kampuni ambayo imekuwa na utamaduni huu kila mwaka na ninawaomba waendelee hivi hivi,"amesema Waziri Abdiwawa.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Biashara na Masoko Jabir Kigoda ameelezea  umuhimu wa soko la Zanzibar kwa kampuni ya bima ya UAP na kusisitiza utaratibu huo wa kuwa karibu na wateja utaendelezwa kwani kwao wateja ni sehemu ya familia ya kampuni hiyo. "Hivyo basi wanastahili kukutana ili kudumisha familia yao hiyo kubwa inayozidi kukua siku hadi siku."

Wakati huo huo Mkuu wa kitengo cha fedha ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nelson Rwihula ameishukuru Mamlaka ya bima Tanzania kwa kuendelea kuliendesha vizuri soko la bima hapa nchini.

Ghafla hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Kamishina wa Bima Tanzania Khadija Said ambaye amesema kwa utaratibu huo wa UAP na kuitaka pia iweze kushiriki katika masuala mengine pia ya kijamii pale inapowezekana

UAP ni kampuni ya bima yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam. UAP ina matawi 9 yanayopatikana katika mikoa mbalimbali hapa nchini kama vile Dar Es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Kahama, Zanzibar, Morogoro na Mtwara.

 kiongozi wa tawi la Kampuni ya UAP Zanziba Farirah Saleh akisalimia wateja waliokuja kujumuika na kampuni hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji Biashara na Masoko Jabir Kigoda baada ya kutoa hotuba ya kuwakaribisha wageni waalikwa pamoja na wateja wa kampuni hiyo ndani ya Hotel Verde Zanzibar.

 Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji Biashara na Masoko Jabir Kigoda akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wateja baada ya kufuturu nao pamoja katika ghafla iliyoandaliwa katika Hotel Verde Zanzibar

 Naibu Kamishina wa Bima Khadija Said akiwasilisha hotuba yake katika hafla hiyo.
Menejimenti ya kampuni ya bima ya UAP ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mawakala wa kampuni hiyo waliopo Zanzibar. 






WATANZANIA WASHAURIWA KUWAASILI WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU

0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

WATANZANIA wametakiwa kuwa na tabia ya kuwaasili watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto wanaoishi mazingira magumu ili waweze kuwasaidia watoto hao. 

Hayo yameelezwa jana na Mkurugenzi wa Kituo cha Samaritan ambacho kinajuhusisha na kulelea watoto yatima na wale waliotelekezwa na wazazi wao Father Josephaty Mmanyi wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea zawadi za ya vyakula kwa Sikukuu ya Iddi kutoka Kampuni ya Promasidor wanaotengeneza maziwa ya Cowbell. 

Father Mmanyi amesema kuwa ni vema Watanzania wakajenga tabia ya kusaidia kwa kuwaasili watoto (kuwadapti) wanaoishi vituoni ili nao wajisikie vyema na wajione wanandugu na wazazi kama walivyo watoto wengine. 

"Unajua hawa watoto ni binadamu na wao wanahitaji malezi ya wazazi kama vile wengine wanavyohitaji, hivyo tunawaomba wananchi kwa ujumla tujitokeze kuwaasili watoto hawa ili nao wasikae vituoni muda mrefu ,maana pia jinsi wanavyokaa mda wanazidi kuwa wapweke zaidi,"amesema. 

Aidha amebainisha hadi sasa jumla ya watoto watano wameshaasiliwa ambapo kati ya hao watatu wameasiliwa nje ya nchi ya nchi na wawili ndani ya nchini ambapo sheria zote za Serikali zimefuatwa. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo pamoja na chakula ,Meneja Masoko wa Kampuni ya Promasidor Vitus Mpanda amesema kuwa hiyo si mara yao ya kwanza kutoa msaada wa aina hiyo kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara pamoja na kufanya shughuli za kijamii.Wametoa msaada wa mchele, sukari, unga na mafuta ya kula. 

Amesema nia ya kutoa vitu hivyo ni kurudisha fadhila kwa wananchi na jamii kwa ujumla kwani wananchi wamekuwa wakinunua maziwa yao na bidhaa zao, hivyo wameona warudishe fadhila kwa kuwapatia watoto msaada wa vyakula na zawadi nyingine. 

"Tunataka watoto hawa washerekee iddi vizuri kama watoto wengine, pia tunaamini kuwa kwenye kutoa ndipo mungu anatubariki vyema,"amesema na kutoa mwito kwa wananchi kuendelea kuendelea kusaidia yatima,"amesema.  
 Meneja masoko wa kampuni ya Promasidor kampuni inayozalisha maziwa ya cowbell  Vitus Mpanda akimkabidhi mkurugenzi wa wa kituo cha Samaritan zawadi za iddi
 Mkurugenzi wa kituo chakulelea watoto yatima pamoja na Wale waliotelekezwa na wazazi wao Samaritan  father, Josephaty Mmanyi akizungumza na Waandishi wa Habari. 

MALALAMIKO YA WANANCHI KUHUSU HUDUMA MBOVU, LUGHA CHAFU YAMNG'OA MGANGA MKUU , MUUGUZI MKUU MKOANI MOROGORO

0
0
Hussein Stambuli, Morogoro

SERIKALI mkoani morogoro imewachukulia hatua baadhi ya watumishi wa sekta ya afya kwa kuwahamisha vituo baada ya kukithiri kwa malalamiko ya tuhuma za rushwa, lugha chafu na utendaji mbovu akiwemo Mganga Mkuu na Muuguzi Mkuu wa Mkoa huo.
  
 Akizungumza na waandishi wa habari,Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro  Cliford Tandari amesema uhamisho huo utahusisha Mganga mkuu wa mkoa, Muuguzi Mkuu wa mkoa, Mganga Mkuu wa meno wa Mkoa pamoja na watumishi wa idara mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo.

"Kufuatia ziara ya Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Dk.Gwajima baada ya kufanya ukaguzi katika halmashauri zote mkoani hapa sasa imebainika kumekuwa na viashiria vya rushwa, hali mbaya ya utoaji huduma kwa wagonjwa, majibu mabovu yanayotolewa na wauguzi.

"Sisi kama Serikali tumeamua kuingia kati suala hili na kuhakikisha huduma za afya mkoani hapa zinatolewa kwa usawa, haki na uboraa,"amesema Katibu Tawala huyo.


Watumishi hao watapangiwa maeneo mengine ya kazi nchini huku Serikali ikiahidi kufuatilia mwenendo wao wa kazi mahali popote watakapokuwa kwani lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanakuwa msaada mkubwa kutatua kero za wananchi.
Katibu tawala mkoa wa morogoro, Cliford Tandari akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro kuhusu watendaji wa sekta ya afya ya mkoa huo.

WAZIRI MKUU AKISALIMIANA NA WAZEE KATIKA KIJIJI CHA MANDAWA WILAYANI RUANGWA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mandawa wilayani Ruangwa, Juni 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TATIZO LA MAJI NANDAGALA LAWA HISTORIA

0
0
*Wananchi washangilia, waishukuru Serikali kwa kuwasogezea huduma

CHANGAMOTO ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama iliyokuwa inawakabili wananchi wa vijiji vya Nandagala ‘B’ na Ingawali wilayani Ruangwa imekuwa historia baada ya Ubalozi wa Uturiki kupitia taasisi yake ya Diyanet kuwachimbia visima virefu.

Visima hivyo viwili vimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo (Jumatatu, Juni 3, 2019) na Muambata wa Ubalozi wa Uturuki anayeshughulikia masuala ya jamii nchini, Muhammed Cicek. Hafla hiyo imefanyika katika kijiji cha Nandagala ‘B’.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu amesema Tanzania na Uturuki ni nchi rafiki na kwamba Serikali ya Uturuki imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania katika uboreshaji wa huduma za jamii zikiwemo za afya, elimu na maji.

Waziri Mkuu baada ya kuvipokea visima hivyo amewataka wananchi wa vijiji hivyo kupitia kamati zao za maji zihakikishe zinaisimamia vizuri miradi hiyo na pia wawe wanatoa taarifa za mapato na matumizi ya kila mwezi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Ruangwa, Samwel Pyuza ahakikishe huduma ya umeme inafikishwa katika mradi huo kwa ajili ya kusukuma maji badala ya kutumia jenereta.

Kwa upande wake, Muambata wa Ubalozi wa Uturuki anayeshughulikia masuala za jamii nchini, Muhammed Cicek amesema Watanzania na Waturuki ni ndugu, hivyo amefurahi baada ya wananchi wa vijiji hivyo kupokea zawadi ya visima hivyo walivyowakabidhi.

Wakizungumza baada ya makabidhiano hayo, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nandagala ‘B’ wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwasogezea huduma ya maji karibu na makazi yao.

Mmoja wa wakazi hao Safina Angulupele (63) amesema awali kabla ya kisima hicho walikuwa wanapata maji kutoka katika kijiji kingine na pia hayakuwa na uhakika, hivyo uwepo wa kisima kwenye kijiji chao ni mkombozi kwao.

Naye mkazi mwingine wa kijiji hicho Zainab Issa amesema huduma ya maji safi na salama ni muhimu kwa maendeleo ya jamii, hivyo anaipongeza Serikali kwa kuwafikishia huduma karibu na makazi. “Sasa hata sisi wazee tunaweza kwenda kisimani na kuchota maji.”

Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo, imedhamiria kuwafikishia wananchi wote huduma ya maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua maji baada ya kukabidhiwa kisima cha maji cha kijiji cha Nandagala ‘B’ kilichojengwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Uturuki nchini Juni 3, 2019. Kulia ni Muambata wa Ubalozi wa Uturuki anayeshughulikia masuala ya jamii nchini, Muhammed Cicek na kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Turkish Maarif Foundation, Oguz Hamza Yilmaz. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KUMBUSHENI VIONGOZI, WATUMISHI KUTIMIZA WAJIBU WAO: RC MTAKA

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali.

Mtaka ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.

Amesema ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake jamii na nchi kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali kwa wakati.

“Ni vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, nchi, mkoa na kwa namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa wakati” alisema Mtaka.

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa wakati.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.

Ameongeza kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili sheria itachukua mkondo wake.

Kwa upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Afisa Maadili kutoka Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
 Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.

SIMANJIRO YATOA MKOPO WA SH. 230.8 MILIONI KWA VIKUNDI 71

0
0
HALMASHAURI ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, imevipatia vikundi 71 vya wanawake, vijana na walemavu, sh230.8 milioni ya mikopo kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ili kuwanyanyua kiuchumi.

Ofisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Asia Ngalisoni akizungumza jana alisema vikundi hivyo ni vya kata 14 vilivyonufaika na mkopo huo.

Ngalisoni alisema mkopo huo umenufaisha vikundi 71, ambapo 59 ni vya wanawake 1,531, vikundi tisa vya vijana 238 na vikundi vitatu vya walemavu 57.

Alisema hadi mwezi Mei mwaka huu halmashauri hiyo imekusanya sh1.7 bilioni ikiwemo mapato ya ndani na marejesho ya fedha za vikundi vilivyokopeshwa awali.

"Mfuko huu unawanufaisha wananchi waliojiunga katika vikundi vyenye shughuli za ujasiriamali au vinavyokusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati," alisema Ngalisoni.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula alisema fedha hizo zinazotolewa hazina riba hivyo vikundi hivyo vinapaswa kuchukua mikopo hiyo na kurejesha kiasi kile kile walichokopa.

"Nitoe wito kwa vikundi vyote vilivyokopeshwa na halmashauri virejeshe fedha hizo kwa wakati ili wengine nao waweze kukopa na kujikwamua kiuchumi," alisema Chaula.

"Mfuko huu unawanufaisha wananchi waliojiunga katika vikundi vyenye shughuli za ujasiriamali au kinakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati," alisema Chaula.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Jackson Sipitieck alimpongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri yake Yefred Myenzi kwa kusimamia ipasavyo mapato hadi kufanikisha utolewaji wa mikopo hiyo.

"Wakati halmashauri nyingine zikisuasua kufanikisha mikopo sisi Simanjiro tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani tunatoa mikopo hadi fedha nyingine zimebaki," alisema Sipitieck.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi alitoa wito kwa vijana wa eneo hilo kuchangamkia fursa hiyo kwani mwitikio wao bado ni mdogo.

"Zile fedha zenu vijana za asilimia nne mnazopaswa kupewa hamjazichukua hivyo vijana wa Simanjiro mnapaswa kubadilika ili mnufaike kupitia mikopo hii tunayoitoa," alisema Myenzi.

Katibu wa walemavu mji mdogo wa Mirerani, William Orata alisema kupitia mkopo waliopata wamefanikisha uanzishwaji wa mashine ya kusaga nafaka.

Mmoja kati ya wanawake walionufaika na mkopo huo, Susan Alanyamuna alisema wameweza kutengeneza sabuni aina ya Sidai.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (kushoto) akipokea mfano wa hundi kutoka benki ya NMB.
 Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula (kushoto) akipeana mkono na viongozi wa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu baada ya kupokea mkopo uliotolewa na Halmashauri ya Wilaya hiyo
 Baadhi ya vikundi vya wajasiriamali, wanawake, vijana na walemavu waliopatiwa mkopo wa sh 230.8 milioni na Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images