Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

NACTE YASITISHA UDAHILI KOZI YA HUDUMU YA AFYA NGAZI YA JAMII ( COMMUNITY HEALTH) KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020

$
0
0

Mkurugenzi wa uzingativu, ufuatiliaji na tathmini wa (NACTE) Jofrey Oleke akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza udahili mpya kwa wanafunzi, katika maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo Jijini Dodoma.
Mdahili wa wanafunzi kutoka Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo(NACTE) Twaha A Twaha akitoa ufafanuzi wa jambo flani kwa waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa mkutano na wanahabari wakati wa kutangazwa kufunguliwa kwa udahili kwa mwaka 2019/2020.

…………………..
Na.Mwaandishi Wetu,Dodoma
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE)limetangaza kusitisha udahili wa wanafunzi wapya wa program ya Huduma ya Afya Ngazi ya Jamii(Community Health) kwa mwaka wa masomo 2019/2020 hadi hapo itakapotangaza tena.

Akizungumza mbele ya wanahabari Jijini Dodoma leo Mkurugenzi wa uzingativu, ufuatiliaji na Tathmini wa NACTE Jofrey Oleke, amesema maombi ya udahili kwa waombaji wapya wa Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2019/2020, umesitishwa hadi hapo baraza litakapotangaza maamuzi mengine.

Kufutwa kwa udahili huo kumetokana na maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwamba kwa mwaka huu wa masomo hakutakuwa na kozi hizo.

Kuhusu kusitishwa kwa udahili, amesema baraza limepokea maagizo kutoka wizara ya afya ambao ndio wanaosimamia kozi zote za afya, kuwa katika mwaka huu wa masoma hakutakuwa na udahili katika ngazi hiyo afya ya jamii nasi tunatekeleza.

“Baraza linavitaarifu vyuo na umma kwamba udahili wa wanafunzi katika programu ya Huduma ya afya Ngazi ya Jamii umesitishwa hadi hapo itakapotangazwa tena”,amesema.

Pia baraza limetangaza kufunguliwa kwa udahili mpya kwa ngazi za Astashahada na stashahada kwa kozi zote isipokuwa kwa kozi za ualimu na utaendelea mpaka tarehe 2 mwezi wa tisa mwaka huu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo katika ngazi hizo.

Amefafanua kuwa kwa waombaji wa programu za Afya katika vyuo vya Serikali watatakiwa ama kuomba moja kwa moja kupitia vyuoni ambapo vyuo vitasawasajili kupitia baraza la chuo au wanaweza kuomba kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (www.nacte.go.tz) kubonyeza kwenye ‘apply online'(SAVS).

Kuhusu waombaji wa programu za Afya kwenye vyuo visivyo vya Serikali na waombaji wa programu nyingine zote wanatakiwa kuomba moja kwa moja kwenye vyuo husika.

“Hivyo vyuo vitapokea maombi na kufanya uchaguzi wa wanafunzi wenye sifa na kisha wawasilishe NACTE majina ya waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuyatangaza, vyuo vinaelekezwa kuzingatia utaratibu wa udahili kama ulivyotolewa na baraza katika mwaka wa masomo 2019/2020,”amesema.

Amewataka wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, kufanya maombi kwa umakini ili kuweza kupata nafasi ya kujiunga programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za kujiunga nazo kwa mwaka 2019/2020.

Pia baraza limewashauri waombaji na wazazi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye vyuo vinavyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye kitabu cha mwongozo wa udahili kwa mwaka wa masomo mwaka 2019/2020 .

Rais Magufuli awasili nchini zimbabwe kwa ziara rasmi ya kitaifa ya siku 2

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono pamoja na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe mheshimiwa Emmerson Mnangagwa wakati wakiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Robert Mugabe nchini Zimbabwe. PICHA NA IKULU

  

TANZANIA NA NAMIBIA ZATILIANA SAINI TAMKO LA PAMOJA LA MASHIRIKIANO KATIKA MASUALA MBALIMBALI

$
0
0
 Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano wakitia saini tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019.
Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano wakibadilishana nyaraka baada ya kutia saini tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019.
 Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  (Mb) pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano (Mb) wakionesha kwa waandishi wa habari nyaraka za tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia walizotia saini  Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019

Profesa Palamagamba John Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  pamoja na Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah  Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutia saini na kubadilishana nyaraka za tamko la pamoja la mashirikiano kuhusu masuala mbalimbali baina ya Tanzania na Namibia walizotia saini  Mjini Windhoek,Namibia May 28,2019. Kushoto ni kaimu balozi wa Tanzania Nchini Afrika ya Kusini anayesimamia pia Namibia Bw. Richard Lupembe na kulia ni Balozi wa Namibia nchini Tanzania Theresia Samaria.

IMEBAKI SIKU MOJA USAJILI WA MAGARI YANAYOTOA HUDUMA YA MAJITAKA

TBS Yaendelea na Ukaguzi wa Kushtukiza Sokoni

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limeendelea na ukaguzi wa bidhaa sokoni kwa kushtukiza ikiwa ni moja ya majukumu yake chini ya sheria Namba 2. Ya mwaka 2009. Bi. Gladness Kaseka, Afisa Masoko Mwandamizi (TBS), alisema Ukaguzi huo unalenga kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa na kusambazwa sokoni kwa mlaji au mtumiaji wa mwisho zinakuwa zimekidhi matakwa ya kiwango husika.

Vilevile ukaguzi huu unaenda sambamba na kuchukua sampuli ili kwenda kupima maabara ili kujihakikishia ubora wake na pia kuzitoa sokoni zile zilizozuiliwa kama nguo za ndani za mitumba na vilainishi aina ya dot 3.

Tunawahimiza wazalishaji na wasambazaji kufwata utaratibu ili kulinda soko na kuepuka hasara.

 Bwn.Medard Muna Afisa Udhibiti Ubora wa (TBS) akiangalia maelezo ya msingi yanayotakiwa kuwepo katika bidhaa ya juisi na pombe kali(ujazo,tarehe ya uzalishwaji, mzalishaji ni nani,mwisho wa matumizi, jinsi ya kuhifadhi)wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni wilayani Mikumi.Sampuli zilinunuliwa kwa ajili ya kupimwa ili kuhakiki ubora wake
 Subira Mshery Afisa Udhibiti Ubora wa (TBS) akiangalia maelezo ya msingi yanayotakiwa kuwepo katika bidhaa ya pipi (,tarehe ya uzalishwaji, mzalishaji ni nani,mwisho wa matumizi,)wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni wilayani Gairo.Sampuli zilinunuliwa kwa ajili ya kupimwa ili kuhakiki ubora wake
Venance Colman na Subira Mshery, wakaguzi wa TBS, wakiangalia maelezo ya msingi yanayotakiwa kuwepo katika taulo za watoto na za wanawake (uzito,imezalishwa lini,  mzalishaji ni nani, na mwisho wa matumizi)wakati wa ukaguzi wa bidhaa sokoni wilayani Mikumi,pia sampuli ilinunuliwa kwa ajili ya kupimwa ili  kuhakiki ubora wake.

 Bwn. Venance Colman, mkaguzi toka TBS, akitoa elimu juu ya katazo la mafuta ya breki "dot 3",kwa muuzaji wa vilainishi hivyo wilayani Kilosa, Vilainishi hivyo vilitolewa sokoni ili kuepusha madhara kwa watumiaji.

RC CHALAMILA ALITAKA BARAZA LA BIASHARA KUWA KUWA KIUNGO MUHIMU KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI.

$
0
0
Na Emanuel Madafa,Mbeya 

Serikali imeliataka baraza la biashara Mkoa wa Mbeya kuanza majadiliano ya pamoja kati ya sekta binafsi na serikali kuhusu masuala ya uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila wakati akizingumza na wajumbe baraza jipya la biashara Mkoani Mbeya .

Amesema lazima kuwepo na majadiliano ambayo yatawezesha wawekezaji wa ndani na nje ili kufahamu sera na vikwazo Mbalimbali katika hatua za uwekezaji.

“Kati ya sekta binafsi na sekta za umma inapotokea tunafanya kazi kwa pamoja kwa njia ya majadiliano kunauwezekano mkubwa tukajadili changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwa wawekezaji hasa masuala ya tozo na kodi “Amesema Chalamila 

Ameeleza kuwa sekta binafsi inaweza kuwa na mchango kubwa kwa kuishauri serikali juu ya mazingira bora ya uwekezaji.“Serikali ikiwa imenyamaza na kutumia mabavu katika kuendesha manaake itabidi sasa watu wasiwe wawekezaji wala wafanyabiashara “Amesema Mkuu wa Mkoa .

Aidha Chalamila amelitaka baraza hilo kuandaa na kutoa taarifa kwa wawekezaji kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa mbeya .

Kwa wake Mwenyekiti wa Chama Cha wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya Dkt . Lwitiko Mwakalukwa amesema baraza la biashara ni muhimu zaidi kuwepo hasa katika Maendeleo ya biashara na uwekezaji Nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Mwenye shati jeupe) katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa baraza la biashara Mkoa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la biashara Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani)katika Ukumbi wa Mkapa .

 Wajumbe wapya wa Baraza la wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya .
 Mwenyekiti wa Chama Cha wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya Dkt . Lwitiko Mwakalukwa akizungumza na wajumbe wa  baraza jipya  la biashara ambalo limeanza kazi mara baada kupatikana kwa wajumbe wapya.

Serikali ya Poland Yaonyesha Nia ya kuisaidia Sekta ya Afya Nchini

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwasilikiza wadau wa Sekta ya Afya kutoka nchini Poland kwenye kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ALVO MEDICAL nchini Poland Bw. Tadeus Olszewski ambaye anaeezea dhumuni la kuwekeza katika sekta ya afya nchini kwenye kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akipokea kitabu cha wasifu wa nchi ya Poland kwenye kikao cha kujadili masuala mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini. 

……………… 
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameishukuru Serikali ya Poland kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuisadia Tanzania katika Sekta ya Afya Nchini ili kuboresha na kupunguza changamoto katika Sekta hiyo. 

Mhe. Jafo ameyasema hayo wakati wa kikao na wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka Poland cha kujadili masuala mbalimbali yanayouhusiana na Afya na jinsi Nchi hiyo inavyoweza kusaidia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Afya nchini. 

Mhe. Jafo ameishukuru Serikali ya Poland kwa ushirikiano wanatoa katika Miradi mbalimbali ya maendeleo na kutambua umuhimu wa sekta ya afya nchini kwa kuwa bila kuimarisha Sekta ya afya hakutakuwa na maendeleo na kushindwa kufikia uchumi wa kati. 

“Sekta ya afya ni muhimu kwa jamii, jamii isipokuwa na afya bora hakutakuwa na maendeleo, hivyo ni vyema Serikali ikajikita kuwekeza katika Sekta ya afya kwa kuhakikisha inajenga miundombinu bora, uwepo wa vifaa na vifaa tiba ili kuboresha huduma za afya nchini” Amesema Mhe. Jafo 

Amesema kuwa hatuwezi kufikia uchumi wa kati endapo watu wetu hawatakuwa na afya bora, ili watu wafanyekazi kwa bidi waweze kuzalisha na kulipa kodi inavyotakiwa wanatakiwa kuwa na afya bora hivyo tunawakaribisha wadau mbalimbali wa Sekta ya afya kuwekeza katika Sekta hiyo. 

Mhe. Jafo amendelea kuishukuru Serikali ya Poland kwa kuonyesha nia ya kuisaidia Serikali mkopo wenye gharama nafuu utakaosaidia kuimarisha na kuboresha sekta ya Afya nchini lengo likiwa ni kupunguza changamoto mbalimbali katika sekta hiyo. 

Ameiomba Serikali ya Poland kujikita zaidi katika kusaidia kwenye kuimarisha huduma za msingi hasa ujenzi wa Vituo vya afya na upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba kwa kuwa ndipo kwenye changamoto kubwa katika suala zima la utoaji wa huduma na itasaidia kupunguza vifo kwa jamii 
Mhe. Jafo amefafanua kuwa katika eneo la Sekta ya Afya Serikali itapata fursa ya kusaidiwa ujenzi wa Vituo vya afya, ambavyo vitakuwa vya mfano kwa kuwa na vifaa vyake na kuwa na nyumba zaidi ya nne za madaktari na hivyo kupunguza changamoto zilizopo. 

Mhe. Jafo amelishukuru shirika la Light For Africa kwa kuunganisha nchi ya Poland na Tanzania ambao wameonyesha nia ya dhati katika kusaidia masuala ya Sekta ya Afya nchini jambo ambalo litasaidia kuleta maendeleo kwa jamii 

Aidha Wadau hao watatembelea, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hospitali ya Mirembe, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Amana na Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kuangalia ni namna Tanzania inavyotoa huduma za afya na kuangalia maeneo ambayo wanaweza kusaidia katika kutumia fursa walizonazo.

WAZIRI UMMY AIPA KIPAUMBELE HEDHI SALAMA

$
0
0
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Biashara kutoka Shirika la AFRIpads Bi. Liz McNeil wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akishika Taulo ya kike kuangalia ubora wake katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mak’s Ama Home Pharmacy. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akisoma jarida la Fema wakati alipotembelea katika Banda lao katika maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma kushoto ni Msaidizi wa Masuala ya Kihabari kutoka Shirika la Femina Hip Bi. Sekela Mwaipaja. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwa na wadau wa hedhi Salama wakati wa maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani jijini Dodoma. 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma. 
Baadhi ya wadau wa Hedhi Salama nchini wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma. 



Na.WAMJW-Dodoma 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameahidi kuweka masuala ya hedhi salama kwenye Sera mpya ya Afya ambayo iko mbioni kukamilika ili kuona kama hedhi salama imewekwa kama kipaumbele. 

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini hapa. 

Waziri Ummy amesema masuala ya hedhi salama katika jamii hususan watoto wasichana na wanawake ni muhimu katika kuweka hali ya usafi wa mazingira rafiki ambapo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama, vyoo bora hasa mashuleni na sehemu za kazi vyenye chumba cha kubadilishia wakati wa hedhi. 

“Katika ripoti za UNICEF na WHO ya mwaka 2013 zinasema kuwa katika kila msichana mmoja kati ya kumi kusini mwa jangwa la sahara anakosa kwenda shule kwa siku tatu hadi tano kwa sababu ya kuwa kwenye siku za hedhi”,Alisema Waziri Ummy. 

Hata hivyo alisema asilimia 52 ya vyoo vya wasichana mashuleni havina milango na ni asilimia 1 tu ya shule zimetenga chumba maalum kwa ajili ya wasichana kujisitiri wakiwa kwenye hedhi kikiwa na maji na vifaa vya hedhi. 

Aidha, aliwataka wadau kuweka mkazo kwenye kuongeza uelewa kwa wafanyabiashara kuzingatia upunguzaji wa bei kwani taulo za hedhi si bidhaa ya anasa ila ni bidhaa muhimu kwa mstakabali wa afya na maendeleo ya wanawake na wasichana nchini. 

Waziri Ummy ametoa rai kwa wadau wote wa hedhi salama kutenga fedha kwa ajili ya kujenga walau choo kimoja cha mfano katika halmashauri kwani jamii ipo tayari kuchangia maendeleo. Aidha, amekusudia kila taulo za kike zikatazoingizwa au kuzalishwa Tanzania ziwe na idadi maalumu za katika kila paketi angalau taulo kumi.

Wakenya wazindua usajili wa usalama kwa alama za vidole

$
0
0

 Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu, akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la usajili wa alama za vidole lenye lengo la kuimarisha usalama kwa raia wa nchi ya Kenya wanaoishi ndani na nje ya nchi mapema leo jijini Dar Es Salaam. Waliosimama nyuma ni baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi huo waliokuwa wakisamamia zoezi hilo. 
 Mary Njoroge (kushoto) raia wa Kenya anaeishi nchini Tanzania akipewa maelekezo na Balozi msaidizi, Rose Mugo, wakati wa zoezi la usajili wa alama za vidole kwa raia wa Kenya linaloendelea katika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo linalenga kuimarisha usalama kwa raia wa Kenya wanaoishi ndani na nje ya nchi hiyo.  Aliyesimama kulia ni Balozi wa Kenya nchini, Mh Dan Kazungu.
Philip Wandela Mwakimu (kushoto) raia wa Kenya anaeishi nchini Tanzania akipewa maelekezo na Balozi msaidizi, Rose Mugo wakati wa zoezi la usajili wa alama za vidole kwa raia wa Kenya linaloendelea katika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo linalenga kuimarisha usalama kwa raia wa Kenya wanaoishi ndani na nje ya nchi hiyo.  Aliyesimama kulia ni Balozi wa Kenya nchini, Mh Dan Kazungu.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS EMMERSON MNANGAGWA WA ZIMBWABWE

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa pamoja Mke wa Rais wa Zimbwabwe Amai Mnangagwa kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa Mnangagwa kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa, Mke wa Rais wa Zimbwabwe  Mhe. Amai Mnangagwa(Wapili kutoka kulia),Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi (Wapili kutoka kushoto),Waziri wa Mambo ya nje wa Zimbabwe Mhe.Sibusiso Moyo(Wakwanza kulia) pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Tanzania  Balozi Grace Martin kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa inayoonyesha baadhi ya Wanyama waliopo katika Hifadhi mbalimbali za Wanyama Tanzania pamoja kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akigonga glasi na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa wakati wa Dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais wa Zimbwabwe Ikulu ya Harare  nchini Zimbabwe. Mei 28, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa kwa Dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa Ikulu ya Harare  nchini Zimbabwe. Mei 28, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa Ikulu ya Harare  nchini Zimbabwe. Mei 28, 2019. PICHA NA IKULU

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 29,2019

RC NDIKILO AMPA WIKI MOJA DED BUTAMO KUYAFANYIA KAZI MADOKEZO,KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amempa wiki moja mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,kushughulikia madokezo ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi unaoendelea wa hospital ya wilaya ya kisasa ambapo madokezo hayo yapo mezani huku ujenzi ukiwa umesimama.

Kufuatia agizo hilo ,amemtaka katibu tawala wa mkoa (RAS) kumfuatilia ndani ya siku saba kuwe na mabadiliko ,kinyume na hapo mkurugenzi huyo atakuwa ameshindwa kufanya kazi hiyo ambayo ,waziri wa TAMISEMI ,Selemani Jafo aliagiza hospitali hizo zikabidhiwe juni 25 mwaka huu.

Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi unaondelea katika halmashauri za wilaya ya Kibaha,Ndikilo alimuelekeza mkurugenzi Butamo Ndalahwa abadilike ,afanye kazi kwa ushirikiano na watendaji wake na asiwe chanzo cha kukwamisha kila kitu.

“Maofisa ununuzi wameshamaliza kazi yao ,watendaji wameshapeleka muda mrefu taarifa za manunuzi ya vifaa vinavyohitaji lakini madokezo hayo yapo mezani hayajafanyiwa kazi ,”

Hata hivyo alisema ,katika kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa jamii serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa ,mkoani hapo ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5.

Ndikilo alifafanua, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo.

Awali mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alieleza,alitoa taarifa ya ujio wa mkuu wa mkoa lakini mkurugenzi ametoa hudhuru yupo katika kikao na madiwani kinachohusu masuala ya fedha.

Mkuu huyo wa mkoa alisema ,ni sawa yupo kwenye majukumu yake ambayo ni muhimu lakini ziara hiyo imelenga kufuatilia hatua zilipofika ujenzi huo,hivyo alipaswa kukaimisha mtu ambae angeweza kutoa majibu ya changamoto zilizojitokeza .

Katika ziara hiyo pia alitembelea ujenzi wa hospital ya wilaya inayojengwa Lulanzi ,mjini Kibaha akiwa hapo Ndikilo alikemea baadhi ya madiwani kuacha kuingiza siasa kwenye shughuli za wataalamu na kusababisha kukwama kwa utekelezaji wa mradi huo unaoendelea kujengwa .

Aliwaasa, baadhi ya wanasiasa na watendaji kutokwamisha kwa namna yoyote miradi ya kitaifa na kimkoa kwa maslahi ya matumbo yao .

SELOU MARATHON KUFANYIKA MKOANI MOROGORO AGOSTI 24 MWAKA HUU

$
0
0
Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Selou marathon,Emmanuel Kajula akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam ambapo amesema lengo la kuandaa mbio hizo ni kutaka kuchochea na kukuza maendeleo ya mbio za riadha nchini Tanzania. Amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo yatakayo fanyika Agosti 24 mwaka huu katika mkoa wa Morogoro.
Msanii wa kizazi kipya,Barnaba boy (kulia) ambaye pia mi balozi wa mbio za Selou marathon akizungumza leo Jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa website ambayo ina fomu ya kuijiunga ambayo ni www.selousmarathon.com.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Msanii wa kizazi kipya,Barnaba boy ambaye pia ni balozi wa mbio za Selou marathon akizindua website ambayo inafomu ya kuijiunga ambayo ni www.selousmarathon.com
Picha ya pamoja.

TUNDURU WAFUNGUA SOKO LA MADINI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akikata utepe kufungua soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilaya ya Tunduru kama utekelezaji wa agiza ka Rais Dkt John Magufuri aliloagiza kila wilaya na mkoa ambao una madini kufungua soko la kuuzia madini ambalo litawezesha wauzaji na wanunuzi kuuzia madini,wa pili kushoto ni MKuu wa Wilaya ya Namtumbo Mh.Sophia Kizigo.Picha na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi Christina Mndeme aliyenyoosha mkono akiongea na baadhi ya wanunuzi wa Madini  waliosimama kushoto wakati wakati wa Ufunguzi wa soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito wilayani Tunduru,kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tunduru ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo.

 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme katikati akipiga makofi jana mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa soko la kuuzia Dhahabu na madini ya vito katika wilaya ya Tunduru mkoani humo,wa kwanza kushoto  mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Mkwanda Sudi ,Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Kizigo na kulia Afisa madini Mkazi wa wilaya hiyo Juma Kapela.

KAMPUNI YA JATU KUANDAA MKUTANO MKUBWA WA WANAHISA WAKE JUNI MOSI JIJINI DAR


VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAKABIDHI ZAWADI ZA KOMPUTA MPAKATO (LAPTOP) KWA WASHINDI WA HACKTHON

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kushoto)  akimkabidhi  Kompyuta mpakato (laptop) mwanafunzi wa  mwaka wa Tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ( UDSM) Kelvin Boya  baada ya kuibuka  mshindi wa shindano la ubunifu wa Suluhisho la Teknohama ya kufikisha elimu  vijijini  (Hackathon) lililodhaminiwa na  Vodacom Tanzania Foundation kupitia mradi wa “Instant  Schools” lililofanyika  wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu ( Innovation week ) jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kushoto)  akimkabidhi  Komputa mpakato (laptop)   John Alfred  ambaye ni mwanamfunzi wa  mwaka wa Tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ( UDSM) baada ya  kuibuka  mshindi wa shindano la  ubunifu wa Suluhisho la Teknohama ya kufikisha elimu  vijijini  (Hackathon) lililothaminiwa na  Vodacom Tanzania Foundation   kupitia mradi wa “Instant  Schools” lililofanyika wakati wa maadhimisho ya  wiki ya Ubunifu ( Innovation week ) jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kushoto)  akimkabidhi  Komputa mpakato (laptop)   Essa Mohamedali   mwanafunzi wa  mwaka wa kwanza  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ( UDSM) baada ya  kuibuka  mshindi wa shindano la  ubunifu wa Suluhisho la Teknohama ya kufikisha elimu  vijijini  (Hackthon) lililodhaminiwa na  Vodacom Tanzania Foundation   kupitia mradi wa “Instant  Schools” lililofanyika  wakati wa maadhimisho  ya wiki ya Ubunifu ( Innovation week ) jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa  shindano la  ubunifu wa Suluhisho la Teknohama ya kufikisha elimu  vijijini  (Hackathon) lililodhaminiwa na  Vodacom Tanzania Foundation   kupitia mradi wa “Instant  Schools”  lililofanyika wakati wa maadhimisho ya  wiki ya Ubunifu ( Innovation week ) jijini Dar es Salaam, Essa Mohamedali (kulia) John Alfred na Kelvin Boya wote wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) wakimsikiliza mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kushoto) wakati walipotembelea ofisi za kampuni hiyo ambapo walikabidhiwa zawadi zao za Komputa mpakato (laptop ) kila mmoja.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kelvin  Boya, John Alfred na Essa Mohamedali ambao ni Washindi wa shindano la  ubunifu wa Suluhisho la Teknohama ya kufikisha elimu  vijijini  (Hackathon) lililodhaminiwa na  Vodacom Tanzania Foundation   kupitia mradi wa “Instant  Schools” lililofanyika  wakati wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu ( Innovation week ) jijini Dar es Salaam, wakifurahia Komputa zao mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Jacquiline Materu (kushoto)   wakati wa hafla iliyofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo.

DMF, TIKA watoa Sadaka ya Iftar kwa watu wasio na uwezo wilayani Bagamoyo

$
0
0
Taasisi ya Doris Mollel (DMF) kwa kushirikiana na Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA) wametoa wa chakula kwa wananchi wasiojiweza katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia muendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambao unaelekea ukingozi sasa. msaada huo ulihusisha Mchele, Mafuta, tende nk.

Wakati huohuo, Ubalozi wa Oman nchini ulishirikiana na Taasisi ya Doris Mollel katika kuwazawadia mavazi wananchi hao kwa maandalizi wa sikukuu ya Eid el Fitr, ambapo walipatia Kanzu, Vikoi na Khanga kwa wakina mama. msaada huo umegusa kaya 250 za vijiji mbalimbali vya wilaya ya Bagamoyo ikiwemo Kitopeni, Mataya, Buma Madrasa, Ramiya na Makurunge. Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa alishirikiana na Taasisi ya Doris Mollel katika kulifanikisha zoezi hilo kikamilifu. Zoezi hilo limefanyika jana Mei 28, 2019.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF), Rahma Amood (wa pili kushoto) kwa pamoja na Mratibu wa Shughuli za Kijamii wa Taasisi hiyo, Maryam Gerion wakikabidhi sehemu ya msaada kwa wakazi wa Kijiji cha Mataya, wilayani Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia muendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, vilivyotolewa kwa ushirikiano na Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA), jana Mei 28, 2019.
Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) amshukuru Mratibu Msaidizi wa Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA), Ali Ozkaya kwa kushirikiana na Taasisi ya Doris Mollel kufanikisha zoezi hilo kwa wananchi wa Bagamoyo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel (DMF), Rahma Amood.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood akishikiana na Afisa kutoka TIKA, Ibrahim Mohamed kutoa msaada wa chakula kwa wananchi wa kijiji cha Kitopeni, wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Rahma Amood na Mratibu wa Shughuli za Kijamii wa Taasisi hiyo, Maryam Gerion wakikabidhi sehemu ya msaada kwa wakazi wa Kijiji cha Buma, wilayani Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya sadaka ya iftar kufuatia muendelezo wa ibada ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, vilivyotolewa kwa ushirikiano na Shirika la Kiserekali la Uturuki nchini Tanzania (TIKA), jana Mei 28, 2019.







VIONGOZI NA WATUMISHI WA WIZARA YA MADINI WATAKIWA KUWA WAADILIFU KATIKA UTENDAJI KAZI WAO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akikabidhi cheti cha ufanyakazi bora kwa mmoja wa wafanyakazi bora wa Wizara ya Madini, Bi. Asteria Muhozya baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (Mb) (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini Bw. Issa Nchasi (kulia).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) akifungua mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) na Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko (Mb) wakifurahia jambo baada ya ufunguzi mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Wizara ya Madini Bw. Issa Nchasi.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George H. Mkuchika (Mb) (hayupopichani) katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) amewataka viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kuwa waadilifu katika utendaji kazi wao ili Tanzania iweze kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mhe. Mkuchika ametoa wito huo alipokuwa akifungua mafunzo kwa viongozi wa Wizara ya Madini katika ukumbi wa St. Gaspar jijini Dodoma.

Mhe. Mkuchika amesema kuwa, katika kulenga dira ya pamoja ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ni lazima viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kufuata misingi ya maadili kama inavyoelezwa katika Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma za mwaka 2005.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, kutozingatia viapo vya maadili ni kosa kwa mujibu wa sheria. Mhe. Mkuchika amewataka viongozi wa Wizara ya Madini kuwa mfano wa kuigwa katika kutekeleza kiapo cha uadillifu.

“Kiongozi unapaswa kuwa mfano katika kutekeleza kiapo chako cha uadilifu, na kama utakuwa umesahau kiapo chako, si vibaya ukaichukua nakala ya kiapo ofisini kwako na kujikumbusha mara kwa mara,” Mhe. Mkuchika amesisitiza.

Mhe. Mkuchika amesema kuwa ni vema watumishi wa Wizara ya Madini hasa wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya uchimbaji madini wawe waadilifu pia ili kuongeza tija na utendaji kazi mzuri.

“Watumishi mlioko kwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji, muwe waadilifu na mtangulize uzalendo wa nchi mnapotekeleza majukumu yenu” Mhe. Mkuchika amesema.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewataka viongozi na watumishi wa Wizara ya Madini kuepuka vitendo vya rushwa huku akinukuu maneno ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Hayati Koffi Annan.

“Rushwa ni ugonjwa ambao unatafuna taratibu na wenye kuleta madhara katika jamii. Unadhoofisha demokrasia na utawala wa sheria, unaleta uvunjifu wa haki za binadamu, unaharibu hali ya maisha, na kusababisha kuwepo kwa mauaji na mambo mengine yanayotishia usalama wa binadamu” Mhe. Mkuchika amesema.

Katika tukio la ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhe. Mkuchika amekabidhi vyeti vya ufanyakazi bora kwa watumishi 12 wa Wizara ya Madini. Mafunzo ya viongozi wa Wizara ya Madini yamefanyika lengo ikiwa ni kukumbushana stadi muhimu za kazi, kuwajengea uwezo wa utendaji kazi na kuongeza ari ya utekelezaji wa majukumu yao.

MBWANA SAMATTA ATETA NA MSEMAJI MKUU WA SERIKALI, DKT. HASSAN ABBASI

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi jarida la Nchi Yetu Tanzania, Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya Nchini Ublegiji Mbwana Samatta amara baada ya mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuaji wa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji (katikati) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuliaji wa Timu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuaji wa Kalbu ya KRC Genk ya Ubelgiji akifafanua jambo ka Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Samatta Tours, Hamisi Waziri akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta.

SERIKALI imesema itaendelea kumsaidia kwa hali na mali Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, anayechezea Klabu ya Genk ya Nchini Ubelgiji Mbwana Samatta ili kuhakikisha kuwa anafungua milango ya uwekezaji na kuiweka juu ramani ya Soka la Tanzania katika anga la kimataifa.

Akizungumza jana Jumanne (Mei 28, 2019) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na Nahodha huyo waTaifa Stars, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema Samatta ameonyesha njia iliyoshindwa kufikiwa na wachezaji wengi wa miaka ya nyuma waliojaribu kucheza Soka la kulipwa katika vilabu mbalimbali vya Nchi za Nje hususani Bara la Ulaya.

Dkt. Abbasi alisema Serikali ilimteua Sammatta kuwa Balozi wake wa Utalii kutokana na sifa kubwa zilizoletwa na mchezaji huyo nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa Serikali ina Imani naye kubwa katika kufungua milango ya fursa za uwekezaji hususani katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano hapa nchini.

“Mbwana Samatta ameonyesha njia ambayo ilikuwa ndoto iliyoshindwa kutimizwa na wachezaji wengi wa zamani, hatua hii aliyofikia ni kubwa na imetokana na sifa kubwa ya nidhamu na kipaji cha mchezo huu hili ni funzo kwa wachezaji wetu chipukizi” alisema Dkt. Abbasi.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema kwa sasa yapo mambo makubwa na mazuri hususani vivutio vya sekta ya utalii, hivyo kupitia nafasi yake ya Ubalozi Serikali itatoa msaada wowote unaohitajiwa na mchezaji huyo ili kuhakikisha kuwa vivutio vya Tanzania vinabainishwa na hivyo kutangaza mambo mazuri ya Tanzania.

Aidha Dkt. Abbasi alisema Ofisi yake imeandaa mikakati mbalimbali ya mawasiliano ya kitaifa katika kuisema nchi katika maeneo mbalimbali hivyo kumtaka mchezaji huyo kutumia majukwaa hayo kwa ajili ya kuona namna bora ya kutumia fursa hizo ili kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alimtaka mchezaji huyo kuwasiliana naye iwapo kutakuwepo na changamoto yoyote anayoweza kuipata katika kutekeleza majukumu yake ya nafasi ya Ubalozi kwani kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano imefungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Kwa upande wake, Nahodha huyo wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema akiwa nchini Ubelgiji tayari amefanya juhudi kubwa katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, ambapo mwanzoni mwa mwezi ujao madaktari 5 wa timu hiyo wanatarajia kuja nchini kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini.

Samatta alisema raia wengi wa kigeni wana shauku ya kutembelea Tanzania kutokana kusikia na kuona uzuri wa vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Wanyama, hivyo akiwa Balozi wa Utalii afanya kila liwezekanalo  kukaa karibu na viongozi na wachezaji wa klabu yake ya KRC Genk kuwaeleza uzuri wa Tanzania ili na wao waonesha nia ya kuitembelea Tanzania.

“Wachezaji wengi hususani wale wa kiafrika waliopo nje hususani Bara la Ulaya wanaipenda sana Tanzania, na hi inatokana na sifa tuliyonayo, na hivyo kwa kutumia nafasi yangu ya Ubalozi nitaendelea kushawishi waitembelee Tanzania” alisema Samatta.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Samatta Tours, Hamis Waziri aliishukuru Serikali kutokana na jitihada mbalimbali inazofanya kwa ajili ya kuhamasisha sekta ya utalii nchini na kusema taasisi hiyo itakuwa tayari kutangaza matukio mbalimbali kwa ajili ya kulitangaza jina la Tanzania.

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN, AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA WA MAZIZINI ZANZIBAR KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA

$
0
0
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuka na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar katika Futari Maalum aliyowaandalia jana 28-5-2019, katika makazi yao mazizini, akiwa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.
WATOTO wanaoishi katika Nyumba ya Serikali ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar wakipata futari walioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, iliofanyika katika makazi yao mazizini jana 28-5-2019.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa katika futari aliyowaandalia Watoto wa Nyumba ya Serikali ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar, kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Suleiman Iddi na kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Mauydline Castico, wakijumuika na Watoto hao katika futari hiyo iliofanyika katika makazi yao mazizini jana 28-5-2019.

WATOTO wa Nyumba ya Watoto Mazizuini Zanzibar wakiwa katika futari ilioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, iliofanyika katika makazi yao mazizini Zanzibar.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mtoto anayelelewa katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar Mtoto Nadir Abdalla mwenye umri wa mwaka moja na miezi mitano,baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari maalum aliyowaandalia katika makazi yao mazizini Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar baada ya kumalizika kwa hafla ya futari aliyowaandalia katika makazi yao Mazizini akiwa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.(Picha na Ikulu, Zanzibar)
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images