Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

NDALICHAKO AMEITAKA NACTE KUVIBANA VYUO VYA UFUNDI

0
0
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mhadhiri wa Chuo Mipango Ezekiel Kanire, juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Chuo hicho wakati wa maonyesho ya kwanza ya Elimu na mafunzo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technologia Prof.Joyce Ndalichako akipokea maelekezo kutoka kwa Mkufunzi wa chuo cha Dare es saalam institute Technology juu ya kazi zinazofanyika chuoni hapo wakati wa maonyesho ya mabanda ya vyuo vya kati jijini Dodoma.
Askari wa kikosi cha zima moto na uokoaji akionyesha namna ya kuzima moto, wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Elimu ya ufundi na mafunzo ya nayofanyika Jijini Dodoma.
Msajili wa chuo cha Bandari cha Dar es Saalam wa kwanza kushoto, Jonneo Lugoye akitoa maelezo kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako juu ya kazi zinazofanywa na chuo hicho, wakati wa maonyesho kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia, Prof, Joyce Ndalichako katikati akiselebuka pamoja na msanii maarufu Mrisho Mpoto kushoto, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho ya kwanza ya Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Tanzania Adolph Rutayuga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobus Katambi akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya huduma za kijamii, ambaye ni Mbunge wa jimbo la Chemba, Mh, Juma Nkamia akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo Bw, John Kondoro akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maonyesho Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Pro, Joyce Ndalichako akihutubia mamia ya washiriki wa ufunguzi wiki ya maonyesho ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof, Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wakati ya ufunguzi wa wiki ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo yanayofanyika Jijini Dodoma.
......................
Na.Mwaandishi Wetu,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Technolojia Prof. Joyce Ndalichako amelitaka baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Tanzania, NACTE, kujenga utamaduni wa kuvitembelea mara kwa mara vyuo vilivyo chini ya baraza hilo ili kuhakikisha elimu inayotolewa na vyuo hivyo iwe ya kiwango, ili kufikia malengo ya Serikali.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akifungua maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo, yaliyoandaliwa na baraza hilo yenye lengo la kuvikutanisha vyuo vilivyochini ya balaza hilo.Amesema ni lazima NACTE ijenge utamaduni wa kuvitembelea vyuo hivyo ili viweze kutoa mafunzo bora yatakayo saidia katika mkakati wa Serikali na kufikia malengo ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

Amesema kama vyuo hivyo hazitatoa elimu na mafunzo bora lengo la kufikia nchi ya viwanda halitafanikiwa, ni wajibu wa baraza hilo kuhakikisha inasimamia utoaji wa mafunzo yaliyo bora.
“Pia niwatake ninyi baraza kama walezi wa hivi vyuo hebu mjenge utamaduni na tabia ya kuvitembelea vyuo hivyo vilivyochini yenu angalau vitoe elimu bora, kataka kufikia malengo ya serikali kufikia nchi ya viwanda, na tutafikia kwa kuhakikisha vyuo hizi vinatoa mafunzo bora” amesema Prof. Ndalichako.

Pia amesema serikali haitasita kukifungia chuo chochote kitakachokutwa kinaendeshwa kinyume na ithibati iliyotolewa na serikali, kwani itakuwa ni kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali.

Pia amevitaka vyuo hivyo kutumia maonyesho kubadilishana mawazo, na namna ya kutoa mafunzo bora na kukuza ushirikiano baina ya taasisi, wadau wa maendeleo pamoja na waajiri mbalimbali katika kuuza sekta hiyo.
Amesema katika kuhakikisha elimu hiyo inakuwa serikali kupitia wizara hiyo imetenga kiasi cha milioni kumi na nane(18,000,000) kujenga chuo kikubwa cha ufundi jijini Dodoma kitakachosaidia kukuza elimu ya ufindi, pia imetengwa bilion arobaini kujenga vyuo vingine ishirini na tano (25) maeneo mbalimbali.

Sambamba na hilo serikali imepanga kukarabati vyuo hamsini na nne(54) vya ufundi ili kufikia kutoa mafunzo yaliyobora, na kuongeza udahili wa wanafunzi wa ufundi mbalimbali hapa nchini.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa NACTE Adolph Rutayuga amesema tangu kuanzishwa kwa baraza hilo mwaka 1997 na kuanza rasmi kazi zake mwaka 2001 wamefanikiwa kudhibiti uanzishwaji wa vyuo vya ufundi kiholela.

Amesema jumla ya vyuo vyote ni mia tano arobaini(540) na kati ya hivyo mia mbili hamsini na moja ni vya umma na mia tatu kumi na tisa na vya binafsi na kati ya hivyo vyuo ishirini na moja havikukidhi matakwa na vilifutwa kabisa usajiri wake.

Maonyesho hayo yatakayo dumu kwa siku tano yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma, umebebwa na kauli mbiu isemayo “Elimu ya ufundi na mafunzo kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda Tanzania”

MADAKTARI ZAIDI YA 150 KUTOKA MATAIFA YA AFRIKA NA SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI WASHIRIKI KONGAMANO LA MADAKTARI WA MIFUPA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa mifupa linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia tarehe 26 -30 May 2019 katika ukumbi mpya wa mikutano MOI
Madaktari wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la kimataifa linalofanyika MOI
Madaktari wa Mifupa kutoka mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la kimataifa linalofanyika MOI
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) katika kongamano la kimataifa la  madaktari bingwa wa mifupa linalofanyika Tanzania (MOI) Kuanzia tarehe 26 -30 May 2019 katika ukumbi mpya wa mikutano MOI
Mratibu wa Kongamano la Kimataifa la madaktari Bingwa wa Mifupa Dkt Joseph Mwanga akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa kongamano hilo.

*****************************************

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI Dkt Respicious Boniface leo amefungua kongamano la kimataifa la madaktari wa Mifupa linalofanyika kwa siku tano hapa Tanzania ambapo madaktari zaidi ya 150 kutoka mataifa ya Afrika na sehemu mbalimbali duniani wanashiriki.

Dkt Boniface amesema Kongamano hilo limekua likifanyika hapa nchini kila mwaka kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa mbinu mpya za matibabu ya mifupa madaktari hapa nchini na nchi nyingine barani Afrika kutokana na MOI kuwa kituo cha mafunzo kutokana na huduma bora za mifupa inazotozitoa.

“Madaktari bingwa wetu hapa nchini wamekua wakinufaika sana na kongamano hili, wamekua wakipewa mbinu mpya na zakisasa za matibabu na upasuaji wa mifupa jambo ambalo limepelekea MOI kuweza kumaliza rufaa za nje ya nchi kwa wagonjwa wa mifupa ambapo kwa sasa huduma karibia zote zinapatikana hapa nchini” Alisema Dkt Boniface.

Mratibu wa Kongamano hilo Dkt Joseph Mwanga amesema mafunzo yatatolewa kwa njia ya nadharia, vitendo katika chumba cha maabara kwa kutumia mifupa bandia na kwenda kwenye chumba maalum cha kujifunzia kwa kutumia miili ya binadamu (Cadavers).

“Kongamano hili limekua na manufaa makubwa sana kwetu, tumekuwa tukipata mbinu mpya kila mwaka kutoka kwa wenzetu wa Marekani jambo ambalo limefanya huduma za mifupa hapa nchini ziendelee kuwa bora ukilinganisha na mataifa mengine barani Afrika” Alisema Dkt Mwanga.

Kwa upande wake Profesa Michael Terry ambaye ni mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Calfonia cha San Francisco amesema ushirikiano kati ya Taasisi yake na MOI umejikita katika mafunzo ya namna ya kuwahudumia majeruhi wa ajali kwa lengo la kuwapa huduma bora na za kisasa kwa wakati.

Kongamano hilo limeratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Taasisi za 
IGOT, SIGN, OTA, AO Alliance na Chuo kikuu cha Calfonia San Fransisco Marekani

Wakuu wa Idara na Vitengo Wizara ya Habari Wapigwa Msasa Kuhusu Manunuzi na Ugavi

BEI YA FUTARI IPO SHWARI SOKO LA BUGURUNI

0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

WAFANYABIASHARA na watumiaji wa soko la Buguruni jijini Dar es Salaam wameridhishwa na bei ya bidhaa sokoni humo hasa katika msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na Michuzi Tv Mwenyekiti wa soko la Buguruni,Said Habibu Kondo amesema kuwa bidhaa za kilimo zimeongezeka tofauti na kipindi cha nyuma hivyo wananchi wasiogope kupanda kwa bei za bidhaa katika msimu huu wa Ramadhani.

Amesema kuwa bidhaa zote zinanunulika kwa bei ya kawaida kabisa huku bidhaa nyingine zikishuka bei na zinapatikana kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamesema kuwa shughuli katika soko hilo zinaendelea kama kawaida na hawajapata malalamiko ya kupanda kwa bei za bidhaa sokoni humo.

Mmoja wa wateja akizungumza na blogu ya jamii amesema kuwa bidhaa nyingi za kilimo zinapatikana zikiwemo viazi, maboga, mihogo na magimbi na bei zake ni za kawaida kabisa na kila mwananchi anaweza kuzimudu.
Mwenyekiti wa soko la Buguruni,Said Habibu Kondo akizngumza na Michuzi Tv leo jijini Dar es Salaam juu ya bidhaa zote zinanunulika kwa bei ya kawaida kabisa huku bidhaa nyingine zikishuka bei na zinapatikana kwa wingi.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

wafanyabiashara wa soko la Buguruni wakiendelea na kazi kama inavyo onekana katika picha.

Rais Magufuli afanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia,afungua mtaa mkubwa uliopewa jina la Mwl. Nyerere

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Mawaziri wa Tanzania kuitisha kikao cha Kamati ya Pamoja ya Tanzania na Namibia (Joint Permanent Commission – JPC) ndani ya kipindi cha miezi 2 ili kujadiliana juu ya fursa mbalimbali za ushirikiano wenye manufaa kwa nchi hizo.


Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo leo tarehe 27 Mei, 2019 wakati wa mazungumzo rasmi kati yake na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Hage Geingob yaliyofanyika katika Ikulu ya Windhoek nchini Namibia ambako ameanza Ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku 2 nchini humo.


Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya yeye na Mhe. Rais Geingob kupokea taarifa kuwa kikao cha JPC hakijafanyika tangu mwaka 1999 na kusababisha masuala mengi yakiwemo ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kutopata msukumo wa kutosha.


Amebainisha kuwa licha ya uhusiano wa kihistoria na kidugu wa Tanzania na Namibia ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Namibia Mhe. Sam Nujoma, nchi hizo zimekuwa na kiwango cha chini cha ushirikiano wa kibiashara baina yake ambapo katika mwaka uliopita biashara iliyofanyika ilikuwa na thamani ya shilingi Bilioni 59.556 tu na kwamba nchini Tanzania kuna kampuni 2 tu za Namibia zinazofanya biashara.


Pamoja na kutoa maagizo hayo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Geingob kwa kumualika kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wowote unaohitajika ikiwemo kushirikiana katika masuala ya kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, usafiri wa anga, biashara, uwekezaji, utamaduni na kufundisha lugha ya Kiswahili ambacho baadhi ya nchi za Afrika zimeridhia kianze kufundishwa katika shule zake.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema kwa kutambua uhusiano wa kihistoria na kidugu, Tanzania inakamilisha maandalizi ya kufungua Ubalozi wake Jijini Windhoek ili kurahisisha masuala mbalimbali ya uhusiano, hususani katika uchumi ambayo yapo nyuma.


Kwa upande wake Mhe. Rais Geingob amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kufanya ziara hiyo na amesema Namibia inatambua na kuenzi mchango mkubwa wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere na Watanzania katika juhudi za ukombozi wa Namibia.


Amefafanua kuwa wakati wa kupigania uhuru wa Namibia, wapigania uhuru wa Namibia walipata nafasi ya kuweka kambi yao huko Kongwa Mkoani Dodoma ambako licha ya kupiga kambi walisaidiwa kupata mafunzo ya kijeshi na waliishi vizuri na wananchi wa eneo hilo jambo ambalo hawatasahau.


Mhe. Geingob ameungana na Mhe. Rais Magufuli kusisitiza umuhimu wa kutekeleza makubaliano yatakayowekwa katika kikao cha JPC na kwamba Namibia ipo tayari kuyatekeleza kwa maslahi ya Wanamibia na Watanzania.

Kabla ya kufanya mazungumzo rasmi, Mhe. Rais Magufuli amefanyiwa mapokezi rasmi ambapo amepigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi liliandaliwa kwa heshima yake katika viwanja vya Ikulu Jijini Windhoek.

Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli ametoa zawadi ya vitabu vya kusoma na kufundishia lugha ya Kiswahili na amemhakikishia Mhe. Rais Geingob kuwa Tanzania ipo tayari kutoa walimu na vitabu vya kufundishia Kiswahili nchini Namibia.


Nyakati za jioni Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Geingob wamefungua rasmi mtaa mkubwa uliopo katikati ya Jiji la Windhoek ambao umebadilishwa jina na kupewa jina la Julius K. Nyerere ikiwa ni kuenzi mchango wake mkubwa katika ukombozi wa Namibia na Bara zima la Afrika.


Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mtaa huo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Rais wa Namibia Mhe. Dkt. Geingob na Wanamibia wote kwa heshima hiyo na ameeleza kuwa Watanzania wanajisikia faraja kuona Namibia inatambua mchango mkubwa wa Hayati Mwl. Nyerere na Watanzania katika ukombozi wa nchi yao.


Mhe. Rais Magufuli amebainisha kuwa Hayati Mwl. Nyerere alikuwa kiongozi shupavu, aliyepambana na ukoloni, ubaguzi wa rangi na kupigania usawa, na ametoa wito kwa viongozi wa Afrika kumuenzi Hayati Mwl. Nyerere na viongozi wengine wa Afrika waliotoa mchango mkubwa wakati wa ukombozi kwa vitendo.


Meya wa Jiji la Windhoek, Mhe. Muesee Kazapua amesema Namibia imeamua kulipanga upya Jiji hilo na kubadili majina yote ya mitaa na kuyapa majina ya viongozi wa Afrika waliotoa mchango mkubwa katika ukombozi na maendeleo, na kwamba mtaa uliopewa jina la Julius K. Nyerere unaungana na mitaa mitatu yenye majina ya viongozi waliotoa mchango mkubwa katika ukombozi ambao ni Robert Mugabe, Jan Jonkerweg na Mandume Ndemufayo.


Katika hafla hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Philip Mangula na Mtoto wa Baba wa Taifa Ndg. Makongoro Nyerere ambaye katika salamu zake kwa niaba ya familia ameishukuru Namibia kwa kuendelea kumuenzi na kumpa heshima Hayati Mwl. Nyerere na kwamba wanafamilia wanapokea heshima hiyo kwa umuhimu mkubwa.


Jioni hii, Mhe. Rais Magufuli amehudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na mwenyeji wake Mhe. Rais Geingob kwa heshima yake. Hafla hiyo imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Namibia Mhe. Mama Monica Geingos, Rais Mstaafu wa Kwanza wa Namibia Mhe. Sam Nujoma na Rais Mstaafu wa Pili wa Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba.


Kesho, Mhe. Rais Magufuli atamaliza Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia ambapo atatembelea kiwanda cha Nyama kilichopo Jijini Windhoek na kisha ataondoka kwenda nchini Zimbabwe ambako atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa.

  
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Windhoek

27 Mei, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob kuashiria uzinduzi rasmi wa mtaa Julius K. Nyerere ulipo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob alipokuwa akimuonyesha Makongoro Nyerere mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mtaa mpya unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019


 Mtaa mpya wenye jina Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE ukifunuliwa rasmi mara baada ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia. Mei 27, 2019
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimweleza Mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob alichokiandika kwenye kitabu cha kumbukumbu kwa Lugha ya Kiswahili Katika kuhakikisha Kiswahili kinatangazwa kimataifa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Jijini Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob wakati wa hafla ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia. Mei 27, 2019 

Picha namba 9  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza Watanzania wanaoishi Namibia mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019.PICHA NA IKULU

Maandalizi mashindano ya umiseta kitaifa Mtwara

0
0
Mkoa wa mtwara ukiwa ni mwenyeji wa mashindano ya umisenta na umishunta kitaifa mwaka huu bado wanaendelea na maandalizi mbalimbali ambapo leo wameanza kuandaa kiwanja ambacho kinategemewa kutumika katika mashindano ya mchezo wa mbio za riadha.

Akizungumza na michuzi kaimu Afisa michezo Mkoa wa Mtwara Mack Kayombo amesema kuwa maandalizi yanakwenda vizuri na wanategemea kuwa mchezo wa mbio za riadha mwaka huu utakuwa ni mchezo wa kwaza kuchezwa ikilinganisha na miaka iliyopita. 

Kwaupande wake mkandarasi anaeandaa kiwanja hicho Johakim Makwiche amesema urefu wa kiwanja hicho ni mita 400 na anatarajia kukamilisha kazi ya kuandaa hapo kesho huku mwenyekiti wa chama cha mchezo wa mbio za riadha mkoa wa mtwara Omary NYENJE amesema wanatarajia ushindi katika mashindano ya mchezo huo.
Mkandarasi Johakim Makwiche anaeandaa kiwanja kinachotarajiwa kutumika katika mashindano ya umesenta kitaifa mchezo wa liadha chuo cha uwalimu( TTC)mkoani mtwara.(picha na Adam Juma)
kiwanja kinachotarajia kutumika katika mashindano ya umesenta kitaifa mchezo wa mbio za liadha chuo cha uwalimu (TTC) mkoani twara.(picha na Adam Juma)
shuguli za maandalizi ya uwanja unaotarajia kutumika katika mashindano ya mbio za liadha umeseta kitaifa chuo cha uwalimu mtwara (TTC).(picha na Adam Juma)

MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 28,2019

PROF. MCHOME ATOA MSAADA WA SHERIA KWA MWANANCHI MASWA

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome kulia akiwa wilayani Maswa mkoani Simiyu akiangalia nyaraka za Bibi Kang’wa Kija ambaye ni msimamizi was mirathi ya Kija Gogadi aliekuwa akihitaji msaada wa sheria baada ya suala hilo kuchukua muda mrefu bila ya kumalizika.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome alievaa tai akisikiliza suala la Bibi Kang’wa Kija kutoka kwa mwanasheria wilayani Maswa ili kumsaidia mwananchi huyo ambaye ni msimamizi wa mirathi ya Kija Gogadi ambaye suala lake limechukua muda mrefu bila ya kumalizika.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akipokea nakala ya Taarifa ya utendaji kutoka kwa Msaidizi wa Sheria kutoka wilaya ya Itilima mkoani Simiyu alipozungumza nao mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
WASAIDIZI wa sheria kutoka kituo cha msaada wa sheria wilayani Maswa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na Msajili wa Watoa msaada wa sheria nchini walipokitembelea kituo hicho wilayani Maswa mkoani Simiyu
WASAIDIZI wa sheria kutoka wilaya za Maswa,Itilima na Meatu katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome na Msajili wa Watoa Msaada wa Sheria nchini walipokutana na wasaidizi wa sheria wa Mkoa wa Simiyu mjini Bariadi.
………………………..

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome ametoa huduma ya msaada wa sheria wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Prof. Mchome amemhudumia mwananchi Kang’wa Kija aliyemkuta kaika kituo cha Msaada wa sheria wilayani Maswa. Bibi Kang’wa ambaye ni msimamizi wa mirathi ya Kija Gogadi amekuwa akishughulikia kwa muda suala lake bila ya kumalizika.

Prof Mchome amepitia nyaraka mbalimbali ambazo Bibi Kang’wa alikuwa nazo na kuzichukua kwa ajili ya kushughulikia suala lake.
Prof Mchome yuko mkoani Simiyu kwa ajili ya kukagua huduma za msaada wa sheria kwa wananchi kuona kama zinaendana na matakwa ya Sheria ya Msaada wa Sheria No.1 ya mwaka 2017.

Prof. Mchome pia amezungumza na taasisi zinazotoa msaada wa sheria na wasaidizi wa sheria mkoani Simiyu.

Kupitia mazungumzo hayo amewataka watoa msaada wa sheria kuendelea kufanya kazi hiyo kwa juhudi kubwa kwani Serikali iliwatambua kutokana na umuhimu wa huduma hiyo kwa wananchi huku ikizingatia uchache wa wanasheria nchini ili kuweza kutatua matatizo mbalimbai yanayowakabili wananchi nchini.

Amesema kutokana na uchache huo wa Wanasheria na ukubwa wa nchi ilikuwa inawawia vigumu kwa wananchi kupata huduma za kisheria nchini.

Amesema wasaidizi wa sheria watasaidia kusuluhisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi kama vile kupata haki zao, kumiliki mali na hivyo kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kuwa na jamii yenye afya na salama na kupata maendeleo.

Katika ziara hiyo Prof. Mchome ameambatana na Msajili wa Watoa huduma ya msaada wa sheria nchini na msajili masaidizi kutoka katika Ofisi ya Mkoa wa Simiyu ambapo anatembelea vituo vinavyotoa msaada wa sheria na kuzungumza na wasaidizi wa sheria katika mikoa husika.

MSAKO MKALI WA WANAUME WANAOJIPAKA OIL NA KUWAINGILIA WANAWAKE KINGONO KWA NGUVU 'TEREZA' KIGOMA WAANZA

0
0
Na Editha karlo wa blog ya jamii,Kigoma

MKUU wa Wilaya ya Kigoma Samson Hanga ametangaza msako mkali wa kuwasaka wanaume wanaojipaka oil mwilini kisha kuwaingilia kingono kinguvu akina mama sambamba na kuwajeruhi na kuwaibia mali zao maarufu 'tereza' waliopo Mkoani Kigoma.

Anga aliyasema hayo juzi kwenye viwanja vya mwanga center wakati kanisa la halisi la Mungu baba likiwa kwenye kongamano lake lake la hija ambapo Mkuu huyo wa Wilaya alimuwakilisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga kwenye hija hiyo.

Hanga aliliomba kanisa hilo kufanya maombi maalum kwaajili ya pepo hilo teleza linalowasumbua wanawake liteketezwe."Hili suala la tereza hapa Kigoma lipo muda mrefu toka mwaka 2016 ila watu walikuwa wakilizungumzia kama vile siyo tatizo kubwa nina waomba katika maombi yenu mliombee na hili la tereza ili liishe hapa kwetu"alisema

Akiongoza maombi hayo ya kumteketeza teleza baba mtakatifu wa kanisa la Mungu baba Elisha Elia alisema tatizo la teleza katika Mkoa Kigoma limekwisha hivyo kila mmoja napaswa kuomba ili tatizo hili lisiendelee.

"Hawa mapepo wachafu teleza wanaojipaka oil ili wakishikwa wateleze tunakuomba Mungu baba ukaondoe roho hii ya pepo mchafu huyo teleza atoweke na asirudi tena kuwatesa watu wako hasa wanawake wa Kigoma"aliomba baba mtakatifu

Katika kuhakikisha maombi yao yanamfikia Mungu baba aliwataka waumini wote waliokusanyika katika viwanja vya mwanga center kulala chini kifudifudi nakumuomba. Mungu kwa dakika tatu ateketeze pepo la teleza kwenye Mkoa wa Kigoma.

Mkuu wa polisi wa Wilaya ya ya Kigoma Raphael Mayunga amesema kuwa jeshi la polisi mpaka sasa tayari linawashikilia watu kadhaa kwa tuhuma hizo na kuwataka wananchi kufika kituoni waweze kuwatambua.

"Wale waliofanyiwa vitendo hivyo wanaweza kufika hapa ili waweze kuwatambua,kama mtu anaogopa anaweza kuja kunifuata kwa siri aje kuwatambua"alisema.Alisema askari polisi wanafanya misako katika mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Teleza ni jina linalotumika kuwatambulisha vijana wanaofanya vitendi vya uhalifu nyakati za usiku ambao huvunja milango na kuwabaka wanawake kinguvu,kuiba na kuwajeruhi.

Baadhi ya waumini wa kanisa la halisi la Mungu baba wakiwa wamelala chini kwaajili ya maombi maalum ya kukemea pepo la kubaka wanawake,na kujeruhi"teleza"wakati wa ibada ya hija iliyofanyika katika viwanja vya mwanga center Manispaa ya Kigoma Ujiji.

NEW ERA NEWS

WAREMBO ARUSHA WATOA ELIMU YA USAFI KWA WANAFUNZI WA KIKE WANAOSOMA SHULE ZA MSINGI

0
0
Na Woinde Shizza , Michuzi TV-Arusha 

WAREMBO 23 wanaoshiriki kinyang'anyiro cha kumpata mrembo mmoja wa Mkoa Arusha wametoa elimu ya afya na usafi kwa wanafunzi wa kike wanaosoma katika Shule ya Msingi Naurei na Sekei .

Mbali na kutoa elimu hiyo yenye leng la kuwandaa wasichana ambao wanakaribia kuvunja ungo, pia warembo hao wametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi ambao wamevunja ungo pamoja na kuwapa elimu ya kujinga na U.T.I.

Akizungumza na wanafunzi wa shule hizo mmoja wa warembo hao Anna Fanuel(23)amesema wameona kuna kila sababu ya kutoa elimu ka wanafunzi hao wakiwamo waliovunja ungo na wale ambao bado hawajavunja ungo kwani elimu hiyo wanastahili kuipata wote.
"Kwa sehemu kubwa elimu ambayo tumeitoa ni kumsaidia msichana aliyekuwa shuleni kutambua kuwa ni muhimu kuzingatia usafi muda wote.Wakiwa wasafi maana yake wanajiepusha na magonjwa ambayo msingi wake ni uchafu,"amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashindano ya Miss kwa Mkoa wa Arusha Tilly Chizenga amesema wamegawa taulo za kike zaidi ya 1000 kwa wanafunzi wa shule hizo mbili na wana mpango wa kuendelea kuzigawa sambamba na utoaji elimu kwa shule nyingine za mkoani hapa.
Kuhusu warembo hao amesema watakaa kambini kwa muda wa mwezi mmoja na kisha wataingia katika kinyanganyiro cha kumpata mrembo mmoja.Mashindano hayo yatafanyika mwishoni mwa Juni mwaka huu.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewapongeza warembo hao kwa utoaji wa elimu na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi hao.

Amesema Serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha mrembo wa Arusha anapatikana, na si Arusha tu, bali wanatoa Miss Tanzania."Tunatamani hata Mrembo wa Dunia safari hii awe anatoka Arusha."

Amewaambia warembo hao wanatakiwa kufahamu kuwa urembo unaanzia kwenye tabia, muonekano na hata sura na kwamba Serikali ya Wilaya inafuatilia hatua kwa hatua mashindano hayo.


"Wenye tabia nzuri hao watafika mbali lakini mwenye tabia mbaya na ya hovyo ni vema wakajindoa mapema kama wapo.Msione mko kambini lakini taarifa za kila mmoa wenu zipo na zinafuatiliwa kwa muda wote, hivyo hakikisheni mnalinda heshima yenu na mnabaki kuwa wenye tabia njema,"amesema Muro.

Ametumia nafasi hiyo kueleza Arusha ni ndio kitovu cha utalii, hivyo anaamini kabisa mrembo atakaepatikana atautangaza mkoa huo pamoja na vivutio vya utalii vilivyopo.Kwa upande wake Meneja Itifaki wa mashindano hayo Basil Elias amesema kuwa mpaka sasa warembo wote wako kambini na wanaendelea na mazoezi.
 Mrembo Anna  Fanuel(23) akiwa anawapa elimu wanafunzi 
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na warembo wanaowania Taji la Miss Arusha 

Rais Magufuli atembelea eneo la makaburi ya mashujaa wa Namibia,atembelea kiwanda cha nyama Jijini Windhoek Namibia

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali mbele ya Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuweka shada la maua.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre mara baada ya kuwasili katika eneo hilo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka pamoja na mwenyeji wake Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Namibia Hage Geingob mara baada ya kuweka shada la maua katika Makaburi ya Mashujaa wa Namibia yaliyopo katika eneo la Heroes’ Acre

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua kiwanda cha nyama cha Meatco kilichopo jijini katikati mwa mji wa Windhoek Namibia. PICHA NA IKULU 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Mei, 2019 ametembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa (Heros Acre) waliopigania ukombozi wa Namibia, lililopo nje kidogo ya Jiji la Windhoek nchini humo. 

Katika eneo hilo wamezikwa mashujaa wa ukombozi wa Namibia ambao baadhi yao walipata mafunzo katika kambi ya Kongwa nchini Tanzania, wengine walikuwa maafisa wa Chama cha SWAPO ambao ofisi zao zilikuwa Jijini Dar es Salaam na wengine ni viongozi wakuu walioendesha mapambano wakiwa nchini Namibia. 

Baadhi ya mashujaa waliozikwa katika eneo hilo ni Ndimo Hamaambo, Peter Nanyemba, Theo-Ben Gurirabo na Toiro ya Toire. 

Mhe. Rais Magufuli ameongozana na mwenyeji wake Mhe. Rais Hage Geingob. 

Baada ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek na kuelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Jannie Breytenbach kuwa kiwanda kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, kimeajiri wafanyakazi 650 na kwamba kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha viwanda vya nyama. 

Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika na ameikaribisha kampuni ya Meatco kuja kuwekeza nchini Tanzania. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. 

Kabla ya kuondoka nchini Namibia kwenda nchini Zimbabwe ambako anakwenda kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Pili wa Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba Jijini Windhoek. 

Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Windhoek 
28 Mei, 2019

Tigo yapeleka mtandao wa 4G Mpanda mkoani Katavi

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa Tigo ulipandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G wilayani Mpanda jana. Kushoto ni Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada. 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga (kushoto) akitembelea banda la mauzo ya bidhaa za mawasiliano kama simu muda mfupi kabla ya kuzindua mnara wa Tigo ulliopandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G. Kulia ni Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mpanda (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuzindua mnara wa Tigo ulipandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G wilayani Mpanda jana. Kulia ni Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada na wa kwanza kulia na Oliver Baltazar na Laverty Khana ambao ni wafanyakazi wa Tigo 
Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada (kushoto) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga (kati kati) muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua mnara wa Tigo uliopandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G wilayani Mpanda jana. 

………………………………………………………. 

Mji wa Mpanda, Katavi sasa umeunganishwa kwenye mtandao wa 4G baada ya kampuni ya Tigo kuzindua mnara wenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya mtandao wenye kasi.

Huduma hiyo mpya,itawezesha wateja wa Tigo wilayani Mpanda kunufaika na huduma bora za kupiga simu, intaneti, kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao huo. 

Akizindua mnara huo mjini, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga, aliipongeza Tigo na uongozi wake kwa mafanikio ya kuleta mnara huo wa kisasa, ambao utakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa wilaya hiyo. 

“Kwa niaba ya watu wa Mpanda, napenda kuwashukuru sana Tigo kwa kazi nzuri. Hakika, huu mnara ambao tunaouzindua leo utachochea kwa kasi kubwa shughuli zetu za biashara, utalii na kilimo tunazofanya hapa Mpanda,” alisema Matinga. 

Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada, alisema kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka mtandao wa 3G kwenda 4G kuna maana kwamba wateja wa Tigo Mpanda wataweza kupata huduma zao kwa uharaka na urahisi zaidi.

“Kipaumbele chetu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma za teknolojia za kisasa kama mtandao wa 4G. Pia ni muhimu kutambua kwamba, teknolojia ya 4G imeongeza idadi kubwa ya watu kuunganishwa na intanet kupitia simu, na pia imezifungulia jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Hivyo, kubadilisha kabisa namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Ndada. 

Uzinduzi wa mnara huu unaenda sambamba na ofa maalum kwa wateja wa Mpanda, ambapo wateja ambao watahudumiwa katika eneo ya mnara huo wa 4G, watazawadiwa GB 4 za intanet bure pale wanapobadilisha laini zao za simu na kuchukua za 4G. Wateja wataweza kutumia kifurushi hicho kwa muda wa siku 7. 

Ndada pia alizungumzia kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya Taifa na kuunga jitihada za serikali katika kujenga viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbali mbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali. 

Mnara wa Mpanda ni wa tatu kuzinduliwa baada ya Kilolo, Iringa na Bariadi, Simiyu. Jumla ya minara 52 itazinduliwa katika kampeni hii ya nchi nzima kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini. 
Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ni Sumbawanga, Rukwa.

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN AJUMUIKA NA WATOTO WA KIJIJI CHA SOS KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA

0
0
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar , katika Futari Maalum aliyowaandalia katika makazi yao iliofanyika jana 27-5-2019. 
WATOTO wa Kijiji cha Watoto SOS Mombasa Zanzibar wakipata futari walioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kujumuika nae katika hafla hiyo ya futari iliofanyika jana 27-5-2019, katika makazi yao Mombasa Zanzibar.) 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico, wakijumuika na Watoto wa Kijiji cha Watoto cha SOS Mombasa Zanzibar, katika futari Maalum walioandaliwa na Mama Mwanamwem,Shein, katika makaazi yao jana 27-5-2019 
WATOTO wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar,Mama Mwanamwema Shein, katika futari maalum aliyowaandalia katika makaazi yao jana 27-5-2019 (Picha na Ikulu) 
MKURUGENZI wa Kijiji cha Watoto cha SOS Mombasa Zanzibar Bi. Asha Salum Ali, akitowa neno la shukrani kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari maalum ilioandaliwa katika makaazi yao.jana 27-5-2019 
MTOTO Mohammed Ali Dausi akisoma dua baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari Maalum walioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, iliofanyika katika makaazi ya SOS Mombasa Zanzibar 
MKE wa Rais wa Zanzibaerv Mama Mama Mwanamwema Shein, akiitikia dua ikisomwa na Mtoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar Mohammed Ali Deus, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika katika ukumbi wa SOS Mombasa Zanzibar kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na kulia Waziri wa Kazi, Uwezeshaji wa Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar, Mhe Maudline Castico. 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimsalimiana mmoja wa Watoto Wanaolelewa katika Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar Wahida Abdallah, aliyebebwa na mtoto mwezake Amina Shabani, baada ya kumalizika kwa kwa hafla ya futari aliyowaandalia katika makaazi yao SOS Mombasa Zanzibar jana 27-5-2019 
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar, baada ya kumaliza hafla ya futari aliyowaandalia katika makaazi yao Mombasa Zanzibar jana, 27-5-2019.(Picha na Ikulu)

NAIBU SPIKA AONGOZA KIKAO CHA BODI YA LSP

0
0

Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ndugu Verity Nyagah kizungumza katika kikao cha Bodi ya Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II) kilichofanyika Katika Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma, kulia ni Naibu Spika, Mhe. Dkt.Tulia Ackoson 
Wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II) wakiwa katika kikao cha Bodi kilichofanyika Katika Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma. kikao hicho kiliongozwa na Naibu Spika, Mhe. Dkt.Tulia Ackoson na Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Ndugu Verity Nyagah 

WIZARA YA NISHATI YAWASILISHA BAJETI YA SH.TRILIONI 2.142

0
0

*Ni kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020 ...yaweka wazi mikakati yake
*Yataja miradi mikubwa mitatu ya kimkakati ambayo lazima itekelezwe
*Yazungumzia hali ya upatikanaji umeme nchini, hatua itakazochukua

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAZIRI wa Nishati Dk.Medrard Kalemani amesema kuwa Bajeti ya mwaka 2019/20 kwa Wizara hiyo inalenga kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuhakikisha inazalisha umeme wa kutosha, wa uhakika, unaotabirika na wenye gharama nafuu na kwamba katika mwaka 2019/20, Wizara inakadiria kutumia jumla ya Sh.trilioni 2.142 ikilinganishwa na Sh.trilioni 1.692 iliyotengwa kwa mwaka 2018/19, sawa na ongezeko la asilimia 26.6.

Kwa mujibu wa Dk.Kalemani ni kwamba ongezeko hili limetokana na kuanza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa Rufiji utakaozalisha MW 2,115. 166 huku akieleza katika bajeti hiyo pamoja na mambo mengine imelenga kuimarisha shughuli za utafutaji na biashara ya mafuta na gesi asilia pamoja na kuwezesha wananchi kunufaika na rasilimali hizo.

Akizungumza leo Bungeni wakati akiwasikilisha Bajeti ya Wizara ya Nishati, Dk.Kalemani ameliambia Bunge kuwa lengo bajeti hiyo ni kuiwezesha Serikali kufikia azma ya kujenga uchumi wa viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 na kuongeza fedha nyingi za ndani za miradi ya maendeleo zilizotengwa kwa mwaka 2019/20 zimeelekezwa katika miradi mitatu (3) ya kimkakati ambazo ni 117 Sh. trilioni 1.86, sawa na asilimia 95.1 ya bajeti yote ya ndani. 

Ameitaja miradi hiyo ni Mradi wa Kuzalisha Umeme katika Mto Rufiji, wenye Mewati 2,115 (Sh. trilioni 1.44); Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Sh.bilioni 363.11); na Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Kinyerezi I Extension Megawati 185 (Sh. bilioni 60). 

"Mheshimiwa Spika naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe bajeti ya jumla ya Sh. 2,142,793,309,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na taasisi zake. Mchanganuo wa fedhahizo ni kama ifuatavyo: (i) Sh. 2,116,454,000,000 sawa na asilimia 98.8 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. 

"Kati ya fedha hizo za maendeleo, Sh.1,956,372,000,000 ni fedha za ndani na Sh. 160,082,000,000 ni fedha za nje; na (ii) Sh. 26,339,309,000 sawa na asilimia 1.2 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Sh. 15,025,821,000 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Sh. 11,313,488,000 kwa ajili ya mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na 118 Taasisi zilizo chini yake. Naomba tena nitoe shukrani zangu za dhati kwako na kwa Wabunge wote kwa kunisikiliza,"amesema Dk.Kalemani wakati anawasilisha bajeti ya wizara hiyo.

Awali akifafanua zaidi kuhusu bajeti hiyo ambayo pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz. Dk.Kalemani amesema anaungana na Mawaziri wenzangu, Wabunge na Watanzania kwa ujumla kumpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa maelekezo yake thabiti yanayonisaidia kuisimamia vema Sekta ya Nishati na ni dhahiri kuwa Rais wetu amekuwa chachu katika kutekeleza mipango mikubwa na yenye tija katika Sekta ya Nishati hapa nchini. 

Amesema mipango hiyo ni pamoja na kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa kielelezo wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (MW 2,115) na amewaahidi Watanzania kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Bunge na wadau mbalimbali watasimamia vema mradi huo ili ukamilike kwa wakati.

"Nitumie fursa hii kuwashukuru Makamu wa Rais SamiaSuluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa miongozo mbalimbali wanayonipatia katika kusimamia Sekta ya Nishati. Nikiri kuwa maelekezo na miongozo ya viongozi wetu hawa ni msingi wa mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Sekta ya Nishati. Aidha, napenda 3kumpongeza pia Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,"amesema.

Akifafanua zaidi kuhusu bajeti ya mwaka 2019/2020,Dk.Kalemani pamoja na kuelezea utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/2019 amesema kutokana na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana ndani ya Wizara hiyo kwa bajeti iliyopita, ni matarajio kuwa TANESCO itaweza kuanza kutoa gawio Serikalini katika kipindi cha Mwaka 2019/20.

Kuhusu taarifa utekelezaji wa shughuli za wizara kwa mwaka 2018/2019 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2019/20 amesema katika mwaka 2019/20, Wizara ya Nishati itaendelea kutekeleza maeneo ya vipaumbele mbalimbali yakiwemo: kuongeza uzalishaji wa umeme nchini ili kufikia lengo la kuwa na MW 10,000 ifikapo mwaka 2025, kwa kutekeleza miradi 18 mikubwa ikiwemo: mradi wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji (MW 2,115) na mradi wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa Kinyerezi I - Extension (MW 185).

Pia mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo MW 80, Ruhudji MW 358 na Rumakali MW 222; Kuimarisha mifumo ya usafirishaji wa umeme nchini kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa North - West Grid Extension kV 400 yenye umbali wa kilomita 1,384 inayojumuisha Iringa – Mbeya – Sumbawanga – Mpanda – Kigoma hadi Nyakanazi; Singida – Arusha – Namanga kV 400, kilomita 414; Rufiji - Chalinze – Dodoma kV 400, kilomita 512; Rusumo – Nyakanazi kV 220, kilomita 98; Geita – Nyakanazi kV 220, kilomita 133; Tabora – Urambo – Kaliua – Nguruka hadi Kidahwe Mkoani Kigoma kV 132, kilomita 391; na Tabora – Ipole – Inyonga hadi Nsimbo (Katavi) kV 132, kilomita 381. 17. 

Dk.Kalemani amesema maeneo mengine ya kisekta yatakayozingatiwa na Wizara ni: kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kupeleka Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), katika vijiji takriban 1,990 vilivyobaki 19 kati ya vijiji 12,268; kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania (East African Crude Oil Pipeline - EACOP); kuimarisha shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia; kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia; kuendeleza miradi ya nishati jadidifu (jotoardhi, upepo na jua); kuvutia uwekezaji katika sekta ya nishati; na kuendelea kuimarisha utendaji wa Taasisi za TANESCO, TGDC, REA, TPDC, PURA na Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja ili kuongeza ufanisi na ushindani katika Sekta ya Nishati. 1

Ameongeza pamoja na maeneo hayo ya kisekta, Wizara itazingatia maeneo mengine ya kuboresha utendaji ambayo ni pamoja na: kuendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara na Taasisi zake katika kusimamia Sekta ya Nishati; kuendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa Wizara na Taasisi zake ili kutoa huduma bora zaidi; na kuendelea kuelimisha umma na kuboresha mawasiliano kati ya Wizara na wadau mbalimbali kuhusu masuala ya nishati. 




HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI

Wakati huo huo Dk.Kaleman wakati anawasilisha bajeti hiyo amesema kwa sasa hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika katika kipindi chote cha mwaka 2018/19. Aidha, mahitaji ya umeme nchini yameendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na kukua na kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi zinazohitaji nishati ya umeme wa kutosha, wa uhakika na wa gharama nafuu katika uzalishaji.

" Katika mwaka 2018/19 uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme (installed capacity) nchini umeongezeka na kufikia MW 1,601.90 kutoka MW 1,517.47 zilizofikiwa mwaka2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 5.6. Kati ya jumla ya MW 1,601.90 zilizopo nchini, MW 1,565.72 zimeunganishwa katika mfumo wa Gridi ya Taifa na MW 36.18 zipo nje ya mfumo wa Gridi ya Taifa. 

"Matumizi ya juu ya umeme yamefikia MW 1,116.58 ukilinganisha na MW 1,051.27 zilizofikiwa mwaka 2017/18 sawa na ongezeko la asilimia 6.2. Aidha, umeme uliozalishwa nchini uliongezeka kutoka GWh 7,114 mwaka 2017 na kufikia GWh 7,374 sawa na ongezeko la asilimia 3.7. Hadi kufikia mwaka 2015, nchi yetu ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa MW 1,204 ikilinganishwa na uwezo wa sasa wa MW 1,601.90 sawa na ongezeko la asilimia 33. Katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda, Serikali kupitia Wizara ya Nishati imelenga kuzalisha umeme wa MW 10,000 ifikapo mwaka 2025,"amesema.


MIRADI YA KUZALISHA UMEME 

Kuhusu Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Mto Rufiji (Rufiji Hydro Power Project) – MW 2,115 21, Dk.Kaleman amaesema mradi huo unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa Megawati 2,115 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji na mkataba wa ujenzi huo ulisainiwa Desemba 12 , 2018 kati ya TANESCO na Mkandarasi Kampuni ya Arab Contractors na Elsewedy Electric za nchini Misri. 

"Tukio hili lilishuhudiwa na Rais Dk.Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Misri. Mkandarasi huyo alikabidhiwa eneo la mradi tarehe 14 Februari, 2019 na kuanza utekelezaji wa kazi za awali. Katika kipindi 22 cha mwaka 2018/19, kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kukamilisha ujenzi wa miundombinu wezeshi ikijumuisha: njia ya kusafirisha umeme wa MW 8 yenye msongo wa kV 33 kutoka Msamvu, Morogoro hadi eneo la mradi yenye urefu wa kilomita 170; barabara za kiwango cha changarawe za Ubena – Zomozi na Kibiti – Mloka hadi eneo la mradi; mifumo ya maji; mawasiliano ya simu; na nyumba za kuishi Mkandarasi. 

"Vilevile, kulingana na mahitaji ya umeme wakati wa ujenzi, TANESCO imeanza ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto kupitia Kisarawe hadi eneo la mradi urefu wa kilomita 245 itakayosafirisha umeme wa MW 22.Katika kipindi cha mwaka 2019/20 Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi huu muhimu ambapo kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kuanza ujenzi wa bwawa (main dam and spillways); kuanza ujenzi wa njia za kupitisha maji (tunnels); na kukamilisha ujenzi wa njia ya pili ya umeme msongo wa kV 33 kutoka Gongo la Mboto. Fedha za ndani Shilingi trilioni 1.443 zimetengwa katika mwaka 2019/20 23 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo. 

"Utekelezaji wa mradi umeanza Desemba, 2018 na unatarajiwa kukamilika Juni, 2022. Kwa ujumla Serikali imedhamiria kwa dhati kutekeleza mradi huu bila kuyumbishwa, kucheleweshwa wala kukwamishwa na mtu yeyote kutoka ndani au nje ya nchi asiyeitakia mema nchi yetu. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rusumo – MW 80 23,"amesema.

Ameongeza kuwa mradi huu wa nchi tatu (3) za Tanzania, Burundi na Rwanda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 80 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera kwa mgawanyo sawa kwa kila nchi. Kwa upande wa Tanzania, Mradi unagharimu Dola za Marekani milioni 113 sawa na takriban Shilingi bilioni 261.75 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia. 

Amefafanua kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika kwa ujenzi wa barabara za kuingia eneo la Mradi; kukamilika kwa ujenzi wa kikinga maji (coffer dam) na kukamilika kwa uchimbaji wa eneo la kusimika mitambo (power house). Wakati kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja na kujenga miundombinu ya kukinga na kuingiza maji katika handaki (Dam and Intake); ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme (powerhouse); ufungaji wa mitambo katika kituo cha kuzalisha umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme (Switchyard);

Na kukamilisha miradi ya kijamii kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi (Local Area Development Plan – LADP na Livelihood Restoration Program - LRP). Fedha za nje Shilingi bilioni 3 zimetengwa na Serikali katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya mradi huu. Mradi huu umeanza mwaka 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2020. Pia mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Ruhudji – MW 358 25. 

"Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa MW 358 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhudji mkoani Njombe. Ujenzi wa mradi huu utahusisha njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 170 kutoka Ruhudji hadi kituo cha kupoza umeme cha Kisada mkoani Iringa. 25 Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: Serikali kuanza majadiliano ya ufadhili na Serikali ya China kwa ajili ya kutekeleza mradi; na kumpata Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu. 

"Ujenzi wa mradi unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 407.40 sawa na takriban Sh. bilioni 943.70 na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani milioni 53.2 sawa na takriban Shilingi bilioni 123. Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kukamilisha taratibu za ufadhili wa mradi; kuhuisha Upembuzi Yakinifu (Updating of feasibility study); kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa kujenga mradi. 

"Jumla ya Sh.bilioni 12.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 10.00 ni fedha za ndani na Sh.bilioni 2.50 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwezi Mei, 2020 na kukamilika mwezi Aprili, 2023. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Rumakali – MW 222 27. mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 222 kwa kutumia maji ya Mto Rumakali mkoani Njombe na njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 150 kutoka katika mitambo hadi kituo cha kupoza umeme cha Iganjo mkoani Mbeya,"amesema.

Amefafanua kuwa gharama za mradi huo kwa pamoja zinakadiriwa kuwa jumla ya Dola za Marekani milioni 344.22 sawa na takriban Shilingi bilioni 899.27. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kumtafuta Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kuhuisha Upembuzi Yakinifu wa mradi uliofanyika mwaka 1998; na kuanza usanifu wa miundombinu ya mradi. 28. 

Wakati katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kuhuisha Upembuzi Yakinifu ; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi; kufanya tathmini ya athari za mazingira na kijamii (ESIA); na kulipa fidia. Jumla ya Shilingi bilioni 3.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo.

" Kati ya 27 fedha hizo Shilingi bilioni 1.0 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.50 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2021 na kukamilika mwezi Juni, 2023. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kakono – MW 87 29. Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 87 kwa kutumia maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 220 kutoka Kakono hadi Kyaka yenye urefu wa kilomita 38.8.

" Gharama za ujenzi wa mradi ni Dola za Marekani milioni 380 zitakazotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD). Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilisha utafiti wa kijiolojia na haidrolojia; kukamilisha usanifu wa awali wa mradi; kufanya maandalizi ya zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi; kuhuisha tathmini ya athari za mazingira na kijamii (updating ESIA); na kukamilisha mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi (Resettlement Action Plan - RAP).Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kutwaa ardhi na kulipa fidia katika eneo la mradi; na kutafuta Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 220. 

"Jumla ya Sh.bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.milioni 500 ni fedha za ndani na Sh. bilioni 2 ni fedha za nje. Mradi huu unatarajiwa kuanza Desemba, 2019 na kukamilika Desemba, 2022. Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Malagarasi – MW 45 31. Mradi huu unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 45 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi mkoani Kigoma na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka Malagarasi hadi Kidahwe mkoani Kigoma,"amesema.

Dk.Kalemani amesema gharama za utekelezaji wa mradi ni Dola za Marekani milioni 150.0 sawa na takriban Sh. bilioni 346.30. Katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na kukamilisha: Upembuzi Yakinifu wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 29 132; usanifu (design) wa miundombinu ya mradi; upimaji na uthamini wa eneo la mradi na njia ya kusafirisha umeme; na mpango wa kuhamisha wananchi wanaopisha mradi. 32. 

Ameweka wazi katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na: kutwaa ardhi na kulipa fidia kwa wananchi watakaopisha mradi; kumpata Mtaalam Mshauri na Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi na njia ya umeme msongo wa kV 132. Jumla ya Shilingi bilioni 3 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 600 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2.40 ni fedha za nje. Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuanza Septemba, 2020 na kukamilika Septemba, 2023. 

Amesema Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Kikonge – MW 300 33, unahusu ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 300 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Ruhuhu mkoani Njombe na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kV 132 yenye urefu wa kilomita 53 kutoka Kikonge hadi kituo 30 cha kupoza umeme cha Madaba. Gharama za utekelezaji wa mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani Milioni 750 sawa na takriban Shilingi trilioni 1.737. Mradi huu pia unahusisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya umwagiliaji. 

"Kazi zilizotekelezwa kwa mwaka 2018/19 ni kumpata Mtaalamu Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu (Feasibility Study) na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (Strategic Environmental & Social Assessment – SESA). Kazi hizi zinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni: kukamilisha Upembuzi Yakinifu pamoja na Tathmini ya Kimkakati ya Mazingira na Kijamii (SESA); kukamilisha majadiliano ya ufadhili wa ujenzi wa mradi na kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Shilingi milioni 500 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 2 ni fedha za nje. 

"Mradi huu unatarajiwa kuanza Novemba, 2020 na kukamilika Oktoba, 2023. 31 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji wa Murongo/Kikagati – MW 14 35. Mradi huu wa nchi mbili za Tanzania na Uganda unahusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 14 kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Kagera na ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kV 33 yenye urefu wa kilomita 0.7 kutoka Kikagati (Uganda) hadi Murongo (Tanzania). 

"Mradi utagharimu Dola za Marekani milioni 58 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 134.35 na unatekelezwa na mwekezaji binafsi, Kampuni ya Kikagati Power Company Ltd (KPCL). 36. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilisha ujenzi wa kambi ya kudumu ya wafanyakazi na miundombinu ya barabara za kuingia eneo la mradi; usanifu wa mitambo na vifaa ya umeme; na ujenzi wa miundombinu ya kukinga na kuingiza maji (Dam and Intake) na njia za kupitisha maji (waterways). 

"Kazi zitakazotekelezwa kwa mwaka 2019/20 ni pamoja na: kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuzalisha umeme; na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 33. Mradi huu ulianza mwezi Novemba, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2020. 32 Matengenezo ya Mtambo wa Kuzalisha Umeme wa Hale (Rehabilitation of Hale Hydro Power Plant) – MW 21 37. Mradi huu unahusu uboreshaji wa mifumo ya uendeshaji na ukarabati wa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia maji wa Hale mkoani Tanga.

" Gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa SEK milioni 200 ambazo ni takriban Shilingi bilioni 50.96 zitakazotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Sweden kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa (Sida). Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni kukamilisha taratibu za kumpata Mkandarasi wa ukarabati wa mitambo. 38. Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni pamoja na kuanza uchimbaji wa handaki la kuingia katika kituo cha kuzalisha umeme (access tunnel). 

"Jumla ya Sh.bilioni 7.80 zimetengwa kutekeleza kazi hizo ambapo kati ya fedha hizo Shilingi milioni 300 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 7.50 ni fedha za nje. Kazi za ukarabati zinatarajiwa kuanza mwezi Agosti, 2019 na kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2021. 33 Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi II – MW 240 39. Ujenzi wa mradi huu ulianza Machi, 2016 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 344, sawa na takriban Sh.bilioni 794.12,"amesema.

Akielezea zaidi mradi huo amesema ulihusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme wa MW 240 kwa kutumia gesi asilia katika eneo la Kinyerezi Jijini Dar es Salaam. Kituo hiki chenye jumla ya mitambo nane (8), ambapo mitambo sita (6) ni ya kutumia gesi asilia (gas turbines) na mitambo miwili (2) ni ya kutumia mvuke (steam turbines) kilikamilika na kukabidhiwa rasmi kwa TANESCO mwezi Desemba, 2018. Kukamilika kwa kituo hiki kumeongeza jumla ya MW 248.22 katika Gridi ya Taifa. 




Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Kinyerezi I Extension – MW 185 na kwamba mradi huo upo katika hatua za mwisho za utekelezaji unahusu upanuzi wa kituo cha Kinyerezi I – MW 150 kwa kuongeza mitambo itakayozalisha MW 185 na kufanya kituo hicho kuzalisha jumla ya MW 335. Mradi 34 huu unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 188 sawa na takriban Shilingi bilioni 435.48. Katika mwaka 2018/19 kazi zilizofanyika ni pamoja na: kukamilika kwa utengenezwaji wa mitambo yote minne (4) 

Na kuanza kufungwa katika eneo la mradi; kukamilika kwa upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I kV 220 na kuendelea na upanuzi (upgrade) wa njia ya msongo wa kV 132 kutoka Kinyerezi I hadi kituo cha kupoza umeme cha Gongo la Mboto. Ujenzi wa mradi huu ulianza mwezi Juni, 2016 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2019. 41. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2019/20 kazi zitakazotekelezwa ni kukamilisha ufungaji wa mitambo na kuingiza jumla ya MW 185 katika Gridi ya Taifa. Fedha za ndani Shilingi bilioni 60.00 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya kutekeleza kazi hizo.

"Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Gesi Asilia wa Mtwara – MW 300, mradi huu unahusu ujenzi wa mitambo ya kuzalisha MW 300 kwa kutumia gesi asilia katika Mkoa wa Mtwara. Gharama za mradi zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 360 sawa na takriban Shilingi bilioni 833.90. Mradi huu utatekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA) kwa kushirikiana na Serikali. Kazi zilizofanyika katika mwaka 2018/19 ni pamoja na: kukamilika kwa Upembuzi Yakinifu wa kituo cha kuzalisha umeme na miundombinu wezeshi ya maji, barabara na gesi asilia. 

"43. Katika mwaka 2019/20 kazi zitakazofanyika ni pamoja na kukamilisha uthamini na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa mradi; kumpata Mtaalam Mshauri wa kusimamia ujenzi wa mradi; na kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi. Jumla ya Shilingi bilioni 4.20 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh. bilioni 1.00 ni fedha za ndani na Sh.bilioni 3.20 ni fedha za nje. Mradi 36 huu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa Machi, 2020 na kukamilika Septemba, 2022

" Miradi ya Kufua Umeme Utokanao na Jua – MW 150, Upepo – MW 200 na Makaa ya Mawe – MW 600 , Septemba 2018, Serikali kupitia TANESCO ilitangaza miradi ya nishati jadidifu (Jua – MW 150 na Upepo – MW 200) na Makaa ya Mawe – MW 600 kwa wawekezaji binafsi. Lengo ni kupata miradi ya kuzalisha umeme wa jumla ya MW 950 kwa njia ya ushindani na kuingizwa katika Gridi ya Taifa. Hadi kufikia mwezi Februari, 2019 tathmini ya zabuni kwa kampuni zilizoshiriki ilikamilika,"amesema.

Ameongeza taratibu zinazoendelea kwa sasa ni kampuni zilizopita hatua ya awali kuwasilisha mapendekezo ya namna bora ya kuendeleza miradi husika baada ya kupatiwa Request for Proposals (RFPs) na kwamba katika kipindi cha mwaka 2019/20, TANESCO itakamilisha taratibu za kuwapata wawekezaji binafsi wenye bei nafuu na kuanza utekelezaji wa miradi hiyo. Utekelezaji wa miradi hii nafuu utapunguzia Shirika gharama za uendeshaji 37 na hivyo kuwepo matarajio ya kushuka kwa bei ya umeme. Utekelezaji huo unatarajiwa kuanza mwezi Novemba, 2019 na kukamilika mwezi Oktoba, 2022. 


MIRADI YA KUSAFIRISHA UMEME 

Dk.Kalemani ametumia nafasi hiyo kuelezea Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 400 wa Singida – Arusha – Namanga ambapo amsema mradi huo unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 400 yenye urefu wa kilomita 414 kutoka Singida hadi Namanga kupitia Arusha. Pia unahusisha ujenzi wa kituo kipya cha kupoza umeme katika eneo la Kisongo mkoani Arusha, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme (bay addition) cha Singida na usambazaji wa umeme katika vijiji 22 vinavyopitiwa na mradi. Mradi unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) na Serikali ya Tanzania. Gharama ya mradi ni Dola za Marekani milioni 258.82 sawa na takriban Shilingi bilioni 599.53. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kulipa fidia na kuanza shughuli za ujenzi wa mradi. 38 47. 

"Kazi zilizopangwa kufanyika kwa mwaka 2019/20 ni: kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme. Jumla ya Shilingi bilioni 4 fedha za nje zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi, 2017 na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2020. 48. Utekelezaji wa mradi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Backbone awamu ya pili (Backbone Phase II) unaohusu kuongeza uwezo (upgrade) wa vituo vya kupoza umeme kutoka kV 220 mpaka kV 400 katika mikoa ya Iringa na Shinyanga kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na katika mikoa ya Singida na Dodoma kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA). 

"Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 kutoka Makambako hadi Songea na Kusambaza Umeme Vijijini kwa Mikoa ya Njombe na Ruvuma 49. Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa 39 kV 220, yenye urefu wa kilomita 250 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba pamoja na ujenzi wa vituo vya kupoza umeme vya Madaba na Songea na upanuzi wa kituo cha Makambako ulianza mwezi Mei, 2016 na kukamilika mwezi Septemba, 2018. 

"Mradi huu ulizinduliwa rasmi na Rais Dk. John Magufuli Aprili 6, 2019. Hadi kufikia tarehe 15 Mei, 2019 jumla ya vijiji 112 kati ya 122 vilikuwa vimeunganishwa umeme. Jumla ya wateja wapatao 22,700 wanatarajiwa kuunganishwa umeme kupitia mradi huu katika wilaya za Makambako, Njombe na Ludewa katika Mkoa wa Njombe; na Songea Vijijini, Songea Mjini, Namtumbo na Mbinga katika Mkoa wa Ruvuma. Gharama ya mradi huu ilikuwa ni Shilingi bilioni 216 chini ya ufadhili wa Serikali za Tanzania na Sweden,"amesema.

Amefafanua kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni: kuendelea kuunganisha wateja ikiwemo Vijiji vya Lutikila, Ifinga na Mbangamawe mkoani Ruvuma vilivyoongezeka pamoja na kukamilisha kazi ya kufunga Reactor na Distribution Panels katika vituo vya kupoza 40 umeme vya Makambako, Madaba na Songea. Jumla ya Shilingi bilioni 2.50 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 2 ni fedha za ndani na Sh. milioni 500 ni fedha za nje. 

"Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 Bulyanhulu – Geita 51. Mheshimiwa Spika, lengo la mradi ni kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 55 kutoka Bulyanhulu hadi Geita. Mradi huu unahusisha ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kV 220, upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu, usambazaji wa umeme katika vijiji 10 vilivyopo ndani ya eneo la mradi na kubadilisha mita za umeme za kawaida (conventional meters) 1,500 mkoani Geita. Gharama za mradi huu ni Dola za Marekani milioni 23 sawa na takriban Shilingi bilioni 53.28. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni kupatikana kwa Mkandarasi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; kuanza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme; kupatikana kwa Mkandarasi wa usambazaji umeme vijijini; na kulipa fidia kwa wananchi wanaopisha mradi,"amefafanua.

Ameeleza kuwa kazi zitakazofanyika mwaka 2019/20 ni kukamilisha: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme mkoani Geita; upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Bulyanhulu; ujenzi wa njia za kusambaza umeme za msongo wa kV 33 na kV 0.4 katika vijiji 10; na kuunganisha wateja wapya 1,500. Jumla ya Sh.bilioni 4.10 zimetengwa katika mwaka 2019/20 ili kutekeleza kazi hizo. Kati ya fedha hizo Sh.bilioni 1.50 ni fedha za ndani na Sh.bilioni 2.60 ni fedha za nje.

Dk.Kalemani amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Januari, 2019 na unatarajiwa kukamilikaMei, 2020. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa Msongo wa kV 220 Geita – Nyakanazi na kwamba unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 133, kituo cha kupoza umeme Nyakanazi na kusambaza umeme katika vijiji 32 vinavyopitiwa na mradi. 

Ambapo gharama za utekelezaji wa mradi huu ni EURO milioni 45 sawa na takriban Shilingi bilioni 117.79. Kazi zilizofanyika kwa mwaka 2018/19 ni: kukamilisha upatikanaji wa Mkandarasi; 42 kukamilisha uhakiki wa mali za wananchi watakaopisha mradi na kuanza kulipa fidia.Kazi zilizopangwa kufanyika mwaka 2019/20 ni kuanza: ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Geita hadi Nyakanazi; ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nyakanazi; upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Geita kitakachojengwa kupitia Mradi wa Bulyanhulu – Geita; na usambazaji wa umeme katika vijiji 32. Fedha za nje Shilingi bilioni 1 zimetengwa katika mwaka 2019/20 kwa ajili ya kazi hizo. 

"Ujenzi wa mradi huu utaanza Agosti, 2019 na kukamilika mwezi Julai, 2021. Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme Msongo wa kV 220 Rusumo – Nyakanazi 55. Mradi huu unahusu ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kV 220 yenye urefu wa kilomita 98.2 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Rusumo hadi Nyakanazi. Gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 35 sawa na takriban Sh. bilioni 81.07. Mradi huu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Tanzania,"amesema.Hotuba kamili inapatikana katika tovuti ya Wizara kwa anuani ya www.nishati.go.tz.
 Waziri wa Nishati Dk.Medrard Kalemani akiwasilisha makadirio ya bajeti ya fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020 bungeni Mjini Dodoma leo
 Sehamu ya viongozi wa Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake wakifuatilia hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizata ya Nishati kwa mwaka 2019/2020 ambayo imewasilisha leo Bungeni Mjini Dodoma
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza Bungeni wakati wa Wizara hiyo ikiwasilisha makadirio ya bajeti yake kwa mwaka 2019/2020
Mbunge wa Muleba Kaskazini akichangia hotuba ya bajaeti ya Wizara ya Nishati ambayo imewasilisha leo Bungeni Mjini Dodoma

Rais wa Namibia Dr. Hage Geingob amwandalia dhifa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Windhoek Namibia

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigonganisha glasi ya mvinyo laini na Rais wa Namibia Mh. Dr. Hage Geingob (kushoto) Ikulu jijini Windhoek usiku wa Jumatatu May 27, 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi kushoto na Waziri wa Kilimo na Chakula Mh. Japhet Hasunga pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina pamoja na maofisa wengine wa serikali ya Tanzania wakigonganisha glasi katika Dhifa iliyoadaliwa kwa ajili ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na RAis Mstaafu wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Dr. Hage Geingob (kushoto) Ikulu jijini Windhoek usiku wa Jumatatu May 27, 2019. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya kwanza wa Nchi hiyo Mhe. Sam Nujoma na Kulia na Makamu MWenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na RAis Mstaafu wa Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Namibia Mhe. Hifikepunye Pohamba wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Dr. Hage Geingob (kushoto) Ikulu jijini Windhoek usiku wa Jumatatu May 27, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais wa Namibia Dr. Hage Geingob Ikulu jijini Windhoek usiku wa Jumatatu May 27, 2019

Dkt. Ndumbaro aeleza mikakati ya Tanzania kunufaika na Programu ya ACP

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 109 wa Baraza la Mawaziri wa ACP na Mkutano wa 44 wa pamoja wa Mawaziri wa ACP na EU uliofanyika Brussels, Ubelgiji tarehe 20 hadi 24 Mei 2019. Kulia ni Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga. 
Waandishi wa habari wakimsikiliza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb). 





TAARIFA KUHUSU USHIRIKI WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 109 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA NCHI ZA AFRIKA, KARIBBEAN, NA PASIFIKI (ACP) NA MKUTANO WA 44 WA PAMOJA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA ACP NA UMOJA WA ULAYA, TAREHE 20 - 24 MEI 2019 BRUSSELS, UBELGIJI


1. Nilipata heshima ya kuongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa 109 wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Afrika, Karibiani, na Pasifiki (ACP) uliofanyika Brussels, Ubelgiji kuanzia tarahe 20 hadi 22 Mei 2019. Mkutano huu, ulifuatiwa na Mkutano wa 44 wa pamoja wa Mawaziri wa nchi za ACP na wenzetu wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao ulifanyika mnamo tarehe 23 na 24 Mei 2019. 

2. Katika mkutano huu, upande wa Tanzania niliongozana na Watendaji Waandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Fedha na Mipango, na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pia, Watalaam kutoka Ofisi ya Ubalozi wetu wa Tanzania Brussels, walishiriki mikutano hii. 

3. Aidha, katika mikutano yote miwili, majadiliano yetu yalijikita katika maeneo makuu matatu. Mosi, ni kupitia na kutathimini utekelezaji wa makubaliano na mipango mbalimbali tuliyonayo ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU. Pili, kuainisha, kujadili, na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ushirikiano ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU. Tatu, kutoa muongozo juu ya mustakabali wa ushirikiano tunaotarajia uwepo ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU katika kipindi kijacho. 

4. Kwa upande wa agenda ya kwanza, tulipitia utekelezaji wa makubaliano ya programu mbalimbali ndani ya nchi za ACP na baina ya nchi za ACP na EU. Programu hizo ni pamoja na zile zinazohusu masuala ya ubia wa kimaendeleo, biashara, masoko, kilimo, elimu, maendeleo ya sekta binafsi, teknolojia, mifumo ya kodi, uhifadhi wa mazingira, hifadhi ya bahari, na masuala mengine yanayofanana na hayo. Kwa ujumla tulikubaliana kuwa programu hizi ni muhimu katika kuchochea kasi ya maendeleo ya nchi zetu na zikaendelea kutekelezwa kwa kasi inayostahili, mgawanyo ulio sawa na kwa kuzingatia mahitaji ya nchi husika. 

5. Kwa mfano, katika eneo la kilimo, Tanzania ilitoa hoja ambayo baada ya majadiliano ya kina ilikubalika kuongeza mazao ya korosho, pamba, na kahawa katika orodha ya mazao yaliyopo katika mpango wa mwaka 2019 wa utekelezaji wa programu ya ACP ya kuendeleza mnyororo wa thamani katika mazao ya kilimo. Mpango huu unafadhiliwa na EU na umetengewa kiasi cha Euro milioni 125. Katika zao la korosho, nchi wanachama wa ACP iliisifu na kuipongeza Tanzania kwa uamuzi wa kishujaa uliochukuliwa na Serikali chini ya uongozi thabiti wa Mhe. Rais Magufuli kwa kuzuia mwendelezo wa mdororo wa bei ya korosho na hatua za makusudi zinazoendelea katika kuongeza mnyororo wa thamani wa zao hilo. 

6. Katika kuimarisha sekta binafsi, ujumbe wa Tanzania uliuomba Umoja wa Ulaya kupitia mkakati wa kusaidia sekta binafsi (ACP Private Sector Development Strategy), kuangalia uwezekano wa kuja na mfumo rafiki kwa nchi za ACP, na Tanzania ikiwemo, ambao utawezesha sekta binafsi ya nchi hizo kunufaika. Katika mkutadha huo, ujumbe wa Tanzania uliiomba Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank – EIB), inayosimamia mpango huo, kuanza majadiliano na serikali na kukubaliana namna ya kusaidia sekta binafsi katika utoaji wa mikopo nafuu ya maendeleo (development finance) kwa ajili ya kuchochea uzalishaji na 3 kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Umoja wa Ulaya kupitia mpango wake wa kuwezesha ufanikishaji wa utekelezaji miradi ya kibiashara na sekta binafsi imetenga kiasi cha Euro bilioni 1.1 kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2020. 

7. Wakati wa mkutano huu, ujumbe wa Tanzania ulieleza kwa kina hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano katika kujenga uchumi wa viwanda kwa lengo la kufikia uchumi wa kati. Miongoni mwa hatua tulizozieleza ni pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), mradi wa uzalishaji wa umeme wa mto Rufiji, ununuzi wa ndege na kufufuliwa kwa ATCL, ujenzi wa barabara, kupanuliwa kwa bandari, viwanja vya ndege na miradi mingine. Tulitumia nafasi hiyo kuzihakikishia nchi za ACP na Umoja wa Ulaya juu ya uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na biashara nchini Tanzania na kuwajulisha kuwa Serikali kupitia mwongozo wa BLUEPRINT inatekeleza mikakati ya kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji na biashara. Hatimaye, tuliwaomba wadau wetu wa maendeleo ndani ya ACP na Umoja wa Ulaya kuunga mkono juhudi hizi madhubuti za Serikali na kuhimiza raia wa nchi zao kuja kuwekeza nchini. 

8. Katika agenda ya kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ushirikiano wetu, tulibainisha na kujadiliana na wenzetu wa Umoja wa Ulaya juu ya changamoto hizo na umuhimu wa kupata ufumbuzi wake. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kasi ndogo ya utekelezaji wa baadhi ya programu za maendeleo, kiwango kidogo cha biashara baina ya nchi za ACP, kuendelea kuibuka kwa vikwazo vipya vya biashara visivyo vya kiforodha kwa bidhaa za ACP katika soko la Ulaya, sintofahamu inayoendelea baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya katika kusainiwa na kutekelezwa kwa Mikataba ya Ubia wa Kiuchumi (Economic Partnership Agreements – EPAs), na kuwepo kwa vikwazo kwa baadhi ya nchi wanachamaa wa ACP na kuwepo kwa maamuzi 4 yasiyozingatia misingi ya uhuru wa nchi (sovereignty), usawa (equal partnership), na kuheshimiana. Nchi za ACP, ikiwemo Tanzania, zilisisitiza changamoto hizi zipatiwe ufumbuzi haraka kwa kila upande unaohusika na tulikubaliana kuwa katika ushirikiano wetu ni muhimu kila upande ukaheshimu kanuni za ushirikiano, sheria na tamaduni za nchi husika. Kwenye hili, Tanzania ikiungwa mkono na nchi nyingine za ACP haja na umuhimu wa kuzingatia na kuheshimu matakwa ya Ibara ya 12 ya mkataba wa ubia wa sasa unaojulikana kama Cotonou Partnership Agreement. Ibara hiyo inazuia upande wowote kuchukua uamuzi wenye madhara kwa upande mwingine bila kuingia kwenye mashauriano ya kina na upande huo. 

9. Katika majadiliano yetu, juu ya mstakabali wa ubia mpya baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya baada ya ubia wa sasa kufikia ukomo wake ifikapo tarehe 29 Februari 2020, tulipokea taarifa ya majadiliano yanayoendelea. Tulisisitiza mambo makuu matatu. Kwanza, mkataba wa ubia mpya uzingatie zaidi kuziinua nchi za ACP kiuchumi, maendeleo, na biashara. Pili, tulisisitiza umuhimu wa mkataba wa ubia mpya kutohusianishwa moja kwa moja na mikataba mingine ambayo majadiliano yake bado yanaendelea baina ya nchi za ACP na Umoja wa Ulaya ikiwemo mkataba wa EPA na mikataba mingine. Tatu, kwa kuzingatia kuwa tunahitahi majadiliano ya kina na yanayozingatia maslahi mapana ya nchi za ACP, ikiwemo Tanzania, tulitoa fursa kwa majadiliano haya kuendelea hata ikibidi kwa muda wa nyongeza ili kuwezesha zoezi hilo muhimu la majadiliano kwa mstakabali wa ushirikiano wetu na EU kwa miaka mingine ijayo kukamilika kwa ufanisi unaostahiki. 

10.Katika hatua ya kuimarisha zaidi ushirikiano na nchi mbalimbali katika ngazi ya kitaifa, kikanda, na kimataifa, hususan kwenye masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, tulipata pia fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa nchi 5 zingine zilizoshiriki mkutano huo. Viongozi tulioonana nao na kufanya mazungumzo ni pamoja na kiongozi wa ujumbe wa Ethiopia, Eswatini, Chadi, Zambia, Equatorial Guinea, Commoro, na Namibia. Pia, tulipata nafasi ya kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi ya Romania na Umoja wa Ulaya. Mazungumzo haya kwa ujumla yametupa uelewa wa pamoja baina ya nchi yetu na nchi hizo kwenye agenda mbalimbali za kitaifa, kikanda, na kimataifa na pia kuimarisha zaidi ushirikiano wenye maslahi baina ya Tanzania na nchi hizo. 

11.Ndugu Waandishi wa Habari, kwa ujumla ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano huu ulikuwa muhimu na wenye manufaa. Ujumbe wa Tanzania ulitoa mchango mkubwa na kwa hakika hoja nyingi za Tanzania zilikubaliwa na kuwa sehemu ya maamuzi na maazimio ya mkutano. Tutaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa maamuzi na maazimio hayo.

Asanteni kwa kunisikiliza. NAIBU WAZIRI, WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI 28 MEI 2019, DODOMA

MHE MGUMBA AITAKA TPRI KUONGEZA JUHUDI KATIKA UDHIBITI WA VIUATILIFU

0
0
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifatilia jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.

Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI Dkt Margaret Mollel wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha. 
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha 220919


Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI imekuwa kitovu cha kuunda mifumo mizuri inayosimamia na kudhibiti Biashara ya Viuatilifu. 

Zipo baadhi ya nchi za Afika kusini mwa Jangwa la sahara ambazo bado hazijatengeneza mifumo mizuri ya Kisheria na sera za kusimamia biashara za viuatilifu. 

Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI.

Mhe Mgumba ameipongeza Taasisi hiyo ya TPRI kwa kushirikiana na wadau wengine kwa kuandaa kongamano hilo Kwani ni sehemu ya kuwajengea uwezo wadau mbalimbali ili waweze kuhakikisha kuwa Visumbufu (Pests) haviwi kikwazo katika kutimiza azma ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alisema kuwa umuhimu wa viuatilifu katika kuzalisha mazao ni jambo la wazi na muhimu katika nchi za Ukanda wa kusini mwa Afrika na maeneo mengine duniani hivyo kongamano hilo litakuwa chachu na taswira chanya katika maendeleo ya kilimo nchini.

Alisema matumizi ya viuatilifu kwa tafsiri ya wengi ni kupata mazao mengi na hivyo mapato ya kutosha na kupata uhakika wa chakula. “Suala la madhara ya viuatilifu hivi kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa mazingira wengi hawalipi kipaumbele na hawaoni kwamba ni tatizo. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo wengi wanatumia viuatilifu bila kuzingatia maelekezo ya watengenezaji” Alikaririwa Mhe Hasunga

Kadhalika alisema, Visumbufu vya mazao husababisha upotevu wa karibia ya nusu ya mazao katika Bara la Afrika na nchi zinazoendelea hivyo Bara la Afrika likiwa linakusudia kuzalisha chakula cha kutosha kwa ajili ya watu wake ambao wanaongezeka kwa kasi, hivyo ni lazima wakulima watumie mbinu mbalimbali za kupambana na visumbufu vya mazao.

“Ingawa viuatilifu vimeleta mafanikio makubwa sana duniani katika kupambana na visumbufu vya mazao, visumbufu vya mifugo na binadamu, pia vinasababisha madhara kwa binadamu na mazingira kwa upande mwingine” Alikaririwa Mhe Mgumba

Aidha, alisisitiza kuwa katika Bara la Afrika tatizo ni kubwa zaidi kuliko maeneo mengine duniani kutokana na uwepo wa matumizi ya viuatilifu hata vile ambavyo vimepigwa marufuku maeneo mengine duniani hivyo kuhisiwa kusababisha madhara kwa maelfu ya watu wengi. 

Alisema kuwa matumizi ya viuatilifu au biashara zinazohusiana na viuatilifu zinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa viuatilifu au kwa jamii na vile vile kusababisha uchafuzi wa mazingira pale ambapo viuatilifu havijatumika kwa njia zilizo sahihi na salama. 

Tanzania kuna sheria mbili zinazoongoza katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi na salama ya viuatilifu. 

Sheria hizi ni sheria ya udhibiti wa visumbufu vya mimea Namba 13 ya Mwaka 1997 (Plant Protection Act No. 13 of 1997) na kanuni zake za mwaka 1999. Na sheria ya TPRI (The TPRI Act. No. 18 of 1979).

Hata hivyo, Baadhi ya nchi za Kiafrika zinazotumia viuatilifu kwa wingi na zenye sheria hafifu za kusimamia matumizi ya viuatilifu, madhara ya viuatilifu ni mengi sana kutokana na usimamizi hafifu na pia kutokuwepo kwa huduma ya upimaji wa madhara ya viuatilifu katika afya ya binadamu.

HASUNGA AWASIMAISHA KAZI WATUMISHI WATANO WA TUME YA UMWAGILIAJI

0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amewasimamisha kazi watumishi watano wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

Watumishi hao waliosimamishwa kazi ni Mhandisi Naomi Adoncome Mcharo, Bw Robert Samson Fundi, Bi Doris Daniel Sendewa, Bw Mohamed Ally Mchemi na Bw Mujuberi Thomas Masatu.

Waziri Hasunga amesema kuwa watumishi hao wamesimamishwa kazi kufuatia taarifa ya awali ya uchunguzi iliyoundwa na ofisi ya Waziri Mkuu kubaini udhaifu wa kiutendaji ndani ya Tume ya Umwagiliaji ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za miradi, matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo na kukosa umakini katika ujenzi wa Miradi ya Umwagiliaji.

Alisema kuwa watumishi hao watano wataungana na watumishi wengine waliosimamishwa kazi hivi karibuni na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa ambao ni Wakurugenzi saba wa Tume ya Umwagiliaji akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) 
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images