Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

RC NDIKILO AKEMEA BAADHI YA MADIWANI KUACHA KUINGIZA SIASA KATIKA KAZI ZA WATAALAMU NA KUSABABISHA MIRADI KUSUASUA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amekemea baadhi ya  madiwani kuacha kuingiza siasa kwenye shughuli za wataalamu ,katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa hospital za wilaya unaoendelea kujengwa kwenye halmashauri tatu za mkoa huo .

Aidha amezitaka, halmashauri zinazojengwa hospital hizo ikiwemo Kibaha Mji,Kibiti na halmashauri ya wilaya ya Kibaha kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo ifikapo juni 25 mwaka huu .

Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi unaondelea katika halmashauri za wilaya ya Kibaha,Ndikilo aliwataka baadhi ya wanasiasa na watendaji kukwamisha kwa namna yoyote miradi ya kitaifa na kimkoa kwa maslahi ya matumbo yao .

Alisema ,katika kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa jamii serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa ,mkoani hapo ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5. 
Ndikilo alielekeza, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo.

"Uzoefu tulioupata kwamba kwanini tunachelewa chelewa sana ni baadhi yetu kutaka fedha hizi ,hii hii bilioni 1.5 kwa kila halmashauri wanajiwekea nipate asilimia 10, fundi wangu ,mjomba wangu apate tenda ya ufundi ,ndugu yangu alete matofali na kutusababishia kuchelewa malengo yetu"alifafanua Ndikilo.

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alieleza changamoto kubwa iliyosababisha kuchelewa kidogo kwa ujenzi ni hali ya mvua hivyo wanaomba kuongezwa muda japo siku 20 badala ya juni 25 mwaka huu.

Awali kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Suzan Chaula ,alielezea wanajenga majengo saba ambapo ujenzi wa majengo yote umefikia asilimia 55.

Suzan aliiomba serikali iwaongezee fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo awamu ya pili na ununuzi wa vifaa kwenye majengo hayo

BOB MARLEY ALIGOMA KWENDA VITANI VIETNAM

$
0
0
Na  Moshy Kiyungi
Licha ya kufariki miaka 38 iliyopita, muziki wa hayati Robert Nesta Marley ‘Bob Marley’ bado unapendwa na idadi kubwa wapenzi mashabiki wa muziki wa reggae duniani.

Bob Marley alionesha ujasiri mkubwa wa kugoma kwenda kupigana vita nchini Vietnam, baada ya akijiuliza ni kwanini aende kupigana vita au kushiriki katika suala la mauaji ya watu wasio na makosa, akaamua kurudi nchini kwake Jamaica.

Historia ya gwiji hilo unaonesha kuwa alizaliwa Februari 6, 1945 katika kijiji cha Nine Miles kwenye Parishi ya mtakatifu Ann, nchini Jamaica.

Baba yake Norval Sinclair Marley, alikuwa mzungu na mama yake Cedelia Booker alikuwa Mjamaica mweusi ambaye alikuwa mwimbaji wa kwaya Kanisani.

Kwake Bob Marley ilikuwa ni majonzi na huzuni baada ya kuachwa chini ya mzazi mmoja (mama yake), akiwa na umri wa miaka kumi, pale alipofiwa na baba yake Norval Sinclair, Sinclair kufariki dunia mwaka 1995 akiwa safarini, wakati huo alikiwa na umri wa miaka 60.

Marley alimalizia udogo wake akiwa huko shamba kwenye mazingira ya wakulima wa ndizi na minazi, akinywa madafu. Huko alikuwa akikamua ng’ombe maziwa na mbuzi, pia alikuwa akienda kuogelea kwenye vijito na Bahari.

Mama yake Cedella Booker hakutaka mwanaye aishie kutanga tanga na kuzurura, akihofu kuwa mwanaye Bob angeliharibika kama ilivyo kwa watoto wa familia zingine zenye tabaka la chini.

Alitamani sana mwanaye ajifunze kazi yoyote ya ufundi ambayo ingeweza ingeweza kumudu maisha yake hapo baadaye.
Booker akapata wazo ya kuhamishia makazi yao na kwenda mji wa Kingstone nchini Jamaica.

 Wakiwa Kingstone, Bob akaanza kujifunza ufundi wa kuchomelea vyuma (Welding). Katika ufundi huo alikuwa akishirikiana na kijana mwenzake Desmond Dekker.

Bob na Desmond wakawa vibarua waliokuwa wakilipwa ujira kwa siku, huku wakiendelea na shughuli za uchomeleaji. Vijana hao wakaanza kujifundisha kutunga na kuimba nyimbo.

Shughuli hiyo waliifanya mara nyingi wakiwa kazini hapo walionekana kutingwa na kazi, lakini waliendelea kuimba huku wakichapa kazi.

Siku moja kipande cha chuma chenye moto kiliingia jichoni kwa Desmond. Hapo mambo ndipo yalianza kubadilika, Desmond aliamua kurudi nyumbani kwao kwa kuwa alikuwa na ujira wa kutwa. Wakati akiuguza jicho lake akaamua kuanza kile kilichokuwa kwenye damu yake (muziki).

Desmond Dekker hakuchuka kipindi kirefu, akatoa kibao chake kilichoitwa ‘Honour Thy Father and Thy Mother’, akimaanisha ‘waheshimu Baba na Mama’. Wimbo huu ulipendwa sana na katika mafanikio hayo ilikuwa ni kijana huyo kusaidiwa na studio za Beverleys.

Mambo yalipo mnyookea katika muziki, Desmond hakufanya uchoyo, alimshawishi Bob Marley kujaribu kuupa kipaumbele muziki.
Bob alikubaliana na ushauri wa rafiki yake huyo, wote wakaenda kwenye studio za Beverley’s. Huko Bob akakutana na mwanamuziki maarufu Jimmy Cliff.

Cliff mbali ya umaarufu aliokuwanao, pia alikuwa na moyo wa huruma wa kupenda kusaidia watu. Alimsaidia Bobo Marley kwa vifaa na ushauri mpaka hapo Bob alipofanikiwa kuipua wa ‘ngoma’ yake ya kwanza ya ‘Judge Not’.
Baadae Bob aliishi maisha ya Gheto huko Trench Town kwenye nyumba ya baba wa Bonny Livingstone, ikiwa ni muda mfupi tu tangu alipounda urafiki na Bonny.

Siku moja alionekana mwanamuziki Peter Tosh akipitapita mitaani akiwa na Gitaa lake. Alikuwa akipiga na kuimba, akicheka, akitania, akitukana na kuchokoza na ubishi kama jadi yake.

Ndipo walipojenga urafiki wa watu hao watatu Bonny Livingstone, Bob Marley na Peter Tosh. Wakaunganisha nguvu na kuanzisha kundi zima la The Wailers ambayo mwanzoni waliita The Wailing Wailers.

Vijana hao Bob, Bonny na Tosh wakatokea kuwa tishio waliyapanda majukwaa ya Kingstone wakiimba nyimbo zenye mtazamo wa Kibiblia pamoja na nyimbo za mapenzi kama vile wimbo wa ‘Do It Twice’. Aidha waliimba nyimbo za kuchangamsha na kuliwaza vijana wa Gheto.

Kujulikana kwa vijana hawa kuliongezeka zaidi hasa pale walipo chukuliwa na ‘Studio one’ ya jamaa aliyeitwa Coxsone Dodd. Huyo alikuwa maarufu sana hasa katika utengenezaji wa Santuri,lakini mambo hayakuwa mazuri kwa ‘wapiganaji’ hao kuhusiana na kipato.

Mnamo mwaka 1966, Wailers waliipua kibao kama vile Put It On, Rude Boy, I’m still waiting na Rule them Rudie. Vibao hivyo vilimwingizia kipato kikubwa Coxsone Dodd. Ilipofika wakati wa sikukuu ya Krismasi, vijana hao walidai haki yao ili wakafurahi na wenzi wao Trench Town.

Dodd akawapatia Paund 60 Bob hakuweza kuvumilia akazichukua pesa hizo akamtupia usoni Dodd. Bob akaamua kuanza safari ya kumfuata mama yake huko Marekani huko akaendelea kutunga nyimbo kama vile wimbo uitwao ‘Bend Down Low’.

Akiwa huko Marekani Bob akapata kibarua katika kiwanda cha kutengeneza magari aina ya Cryster kilichopo mjini Delaware,lakini huko Amerika hakukaa sana aliamua kuondoka nchini humo baada ya kupata barua .

Barua aliyoipata Bob ilimtaka akapigane vita huko Vietnam, wazo hilo Bob hakuafikiana nalo huku akijiuliza ni kwa nini aende kupigana vita au kushiriki katika suala la mauaji ya watu wasio na makosa, akaamua kurudi nchini kwake Jamaica.

Ulimwengu wa kibepari bado uliendelea kumtupa huku na kule, aligundua kuwa kila mahali wanataka kumtumia au kukitumia kipaji chake cha muziki ili wajitajirishe wao au kumtumia kama kibarua mchomeaji kisha kumlipa ujira mdogo ama kutumia ujana wake katika vita huko Vietnam kwa manufaa ya mabeberu.

Bob Marley alibaini kwamba watu wale walijifanya ni marafiki kumbe walitaka kumtumia kama ilivyokuwa kwa Coxsone Dodd ambaye alijifanya rafiki kipenzi.
Fikra hizo zilionyesha hali halisi jinsi Bob alivyo itameibua jamii ya Kibepari. Ndipo alipoamua kuifikishia ujumbe huu Dunia nzima kupitia kibao chake cha ‘Who The Cape Fit’katika Santuri ya Rastaman Vibration.

Bob Marley alimuoa kimwana Rita Anderson Februari 10, 1966 na kwenda kuishi kwa muda na mama yake huko Wilmington, Delaware nchini Marekani. Huko wakaibuka na imani kali ya Kirastafari na kuja na mtindo wa kufuga nywele uitwao "Dreadlocks".

Rita aliyezaliwa Julai 25, 1946, huko Santiago de Cuba, jina lake halisi ni Alpharita Constantia Anderson. Katika maisha ya ndoa yao walifanikiwa kupata watoto watatu.

Hata hivyo Bob Marley aliwahi kukiri kuwa alikuwa na watoto wengine watatu kutoka katika mahusiano yake mengine.
Bob Marley na kundi lake la The wailers, baadaye walitoa vibao vingi vilivyoitikisa Dunia. Kati ya vibao hivyo ni pamoja na “Africa unit”, “Zimbabwe”, “Could you loved?”, “Iron lion zion”, “Is this love”, “Buffalo soldier” na vingine vingi..

Vyombo vya habari vikiwemo Redio, Matangazo, Magazeti ya Kibepari hayakutaka kabisa kukubali mafanikio ya The Wailers kwamba yalitokana na bidii za pamoja za wahusika wote.

Vyote hivyo viliamini kwamba kila kitu kilifanyika na Bob Marley na hao wengine walifanywa kama vijana wake tu kitendo ambacho kiliwaudhi Bunny na Tosh, hizo zilikuwa hisia ,mbinu za mabepari ili kuhakikisha  wanawatenganisha.

Peter Tosh aliiacha bendi ya The Wailers mnamo mwaka 1974 baada yeye na Livingstone kukataa kufanya ziara hiyo.
Baada ya Peter kuondoka Bob alianza kutafuta wanamuziki wengine, akawapata Al Andason Rasta, Junior Marvin ‘Rasta bitoz’ na Tyrone Downie kijana ambaye kwa muda mrefu alikuwa anawahusudu sana The Wailers.

 wakajiunga pia wale I Threes, wanawake weusi watatu waliokuwa na sauti nzuri Rita Marley, Juddy Mowatt na Marcia Griffiths walimsaidia Marley katika uimbaji. Hapo ndipo hapo Bob Marley akabadilisha jina la bendi na kuwa ‘Bob Marley & The Wailers’ akiwa yeye mwenyewe mpiga gitaa, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji mkuu.

Ujio wa wanadada hao ulikuwa ‘mtaji’ mkubwa kwa kundi la The Wailers kwa kuwa Rita alionyesha umahiri wake kwa kuipua albam iliyoitwa ‘Who Feels It Knows It’. Mwanadada Marcia alithibitisha dhahiri kwamba yeye ni mwimbaji bora huenda kuwazidi wenzie Juddy na Rita, aliposhirikiana vyema na Bob Marley katika santuri yake iitwayo ‘Young Giftted and Black’.

Ni ukweli usiopingika kwamba Bob Marley alitoa mchango mkubwa wa kuuza na kuusambaza muziki wa Regae Duniani kote hata kuwepo kwa gumzo kubwa kuhusiana na kundi zima la The Wailers. Kwa hakika kundi hilo lilijituma sana katika kuboresha muziki wa Regae na ndilo lilikuwa jipya lililounda nguvu ya The Wailers. Walitoa albam iliyowatia moyo ma-Rasta iliyoitwa ‘Natty Dread’ ambayo iliwaongezea hamasa vijana weusi wa Ulaya na Duniani kote.

Ilifika wakati Bob Marley na kundi lake la The Wailers, walivamiwa na kushambuliwa kwa risasi, ambapo watu wengi walihisi kuwa walishambuliwa kwa sababu ya mawazo yao hasa yaliyotokana na albam yao ya Natty Dread. Ilikuwa mwaka 1976, The Wailers walifikiria kufanya onesho la amani ambalo mada yake kubwa ingekuwa kuwaunganisha watu wa Jamaica, kuwasihi waache uhasama na ghasia, wafungue macho.

Jioni moja siku tatu kabla ya onyesho hilo, watu wenye bunduki waliwashambulia The Wailers ambao walikuwa wanafanya mazoezi ya muziki, ghafla wakasikia milio ya bunduki mlango ukafunguliwa huku mitutu ikitangulia na kutoa milipuko kadhaa, Bob Marley na Rita Marley walijeruhiwa.

Sababu ya mashambulizi hayo haikujulikana lakini hilo haikuwa kikwazo kwa Bob na The Wailers kusitisha onesho hilo. Mara baada ya onesho, Bob akaondoka zake kuelekea Miami, Marekani. Aidha Bob Marley alikuwa mwanaharakati wa kupigania Uhuru na haki kupitia muziki aliokuwa akiupiga katika staili ya midundo ya Regae.

Mfalme huyo wa muziki wa reggae alipinga ubaguzi kwa kiasi kikubwa kwa kusema kuwa: “wananiita chotara, lakini mimi siegamii upande wowote bali nipo upande wa Mungu aliye niumba kutoka kwa weusi na weupe…" Robert Nesta Marley alikuwa na kipaji pia alipendwa na wengi, si mashabiki tu hata baadhi ya wanamziki wenzie ambao ni mashuhuri katika ulimwengu wa muziki, walimkubali na kumheshimu kama vile Jimmy Cliff.

Marley aliwapenda wanawake, hasa wanawake wa matabaka la chini, la wakulima na wafanya kazi wa kipato cha chini, wanawake wa tabaka hizo aliwafahamu zaidi hasa wanawake weusi. Ndio maana katika wimbo wake wa ‘No Woman No Cry’ utusikia msimamo wa kisiasa wa Marley.

Bob Marley alifanya mambo mengi wakati wa uhai wake ikiwa ni pamoja na kujihusiha pia na michezo kama vile mpira miguu. Walipokuwa ziarani huko ulaya, Bob alikuwa na bendeji mguuni lakini hakuonesha wasiwasi tokana na jeraha alilolipata siku alipocheza mpira wa miguu.

Marley alipokuwa jukwaani akipiga muziki, alikuwa akirukaruka huku na kule kama mtu asiye na jeraha mwilini. Alikuwa akifanya mazoezi ya viungo kama kawaida, alikimbia kutoka studio na kuingia uwanjani kusakata kabumbu na mara kadhaa alionekana akikimbia mchaka mchaka.

Baadaye uvumi wa kutisha ukazuka kwamba mguu wa Bob Marley ulikuwa ukioza na ingebidi ukatwe. Baadae wataalamu wakitamka kuwa asingehitajika kuukata na wakasisitiza kwamba Marley angeendelea kuwa yule yule mwenye mwili mkakamavu, mcheshi, mchangamfu, mchezaji, mwanamuziki aliyeyumba na kutamba. Alikuwa akirukaruka jukwaa zima kama kawaida yake siku zote.

 Kumbe kulikuwa na ukweli wa kutisha kwamba tayari alikwisha patwa na Kansa ya Melanoma ambayo iliendelea kumtafuna ikiyaharibu maini pamoja na mapafu yake. Bob Marely ilifikia kuanguka wakati akikimbia mchaka mchaka, baada ya kupiga muziki maeneo ya Midson Sqare Gardens New York, nchini Marekani. Bob Marley akalazwa katika hospitali iliyoitwa Sloan Carttering ya jijini New York. Uchunguzi wa kina ulifanywa na matokeo ya uchunguzi huo, yalithibitisha ukweli wa kusikitisha juu ya afya yake.

Baada ya kutoonekana hadharani, uvumi ukaenea kuwa amekwenda Sheshamane nchini Ethiopia. Huko Sheshame ni sehemu maalumu kwa ajili ya wenye imani za Kirasta, japo hakuwa huko. Yeye alikuwa amekwenda Bad Wiese, nchini Ujerumani Magharibi ambako alilazwa kwa ajili ya matibabu katika hospitali mashuhuri kwa magonjwa ya Kansa ya Sun shine House Cancer Clinic.

Bob alipofika hospitalini hapo tayari alikuwa na uvimbe katika ubongo na alikuwa hawezi kutembea, alikuwa hoi bin taabani. Siku zilivyokuwa zikienda hali yake ikazidi kuzorota. Ukafikia wakati ambao yeye na daktari wake wabaini kuwa alikuwa mtu wa kuaga dunia wakati wowote.

Alipotambua kuwa mauti yake yamekaribia, Bob akaamua kufunga safari ya kurejea Jamaica ili akafie huko. Kinyume na alivyopanga kufika Jamaica akiwa hai, badala yake Bob Marley alifika huko akiwa ni marehemu.

Bob Marley alifariki dunia katika hospitali ya Florida, nchini Marekani Mei 11, 1981 kutokana na ugonjwa wa Kansa alioupata akiwa na miaka 36.
Mapema Bob alikataa kuandika urithi akiamini kuwa marastafari huwa hawafi.

BALOZI SEIF ALI IDD AWAONGOZA WATEJA WA BENKI YA CRDB KATIKA IFTAR ILIYOANDALIWA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) wakati alipowasili katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wake, iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akimtambulisha kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dkt. Joseph Witts wakati alipowasili katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wake, iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud na kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Mkurugenzi wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB, Philip Alfred (kushoto) wakati alipowasili katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wake, iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakielekea sehemu maalum iliyokuwa imetengwa kwaajili ya ibada ya Magharibi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kabla ya kufanyika kwa ibada ya Magharibi, katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wake, iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar.
Swala ya Magharibi.
Dua baada ya Swalat Magharibi.
Ifrar.





Picha ya pamoja kwa baadhi ya Wafanyabiashara na Wateja wa Benki ya CRDB Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa Wateja wake, iliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Velde, Unguja Zanzibar.




MIAKA MITATU TOKA KIFO CHA PAPA WEMBA

$
0
0
 Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam.

Miaka mitatu imetimia tokea mwanamuziki nguli Papa Wemba, kufariki dunia. Ilikuwa mithiri ya simulizi za ‘Alinacha’ asubuhi ya Jumapili Aprili 24 2016, kuzagaa kwa taarifa za kifo cha cha mtunzi na mwimbaji mkongwe Papa Wemba kwamba amefariki dunia. Taarifa hizo zilieleza kwamba nguli huyo alianguka jukwaani akiwa anatumbuiza jijini Abdjan, nchini Ivory Coast katika tamasha la muziki la FEMUA.

Baadhi ya Wanabendi wake waliokuwa jukwaani, waliendelea kupiga dansi kabla ya mmoja wao kukimbia kumuokoa baada ya kuona kasalia chini kwa sekunde kadhaa akiwa anatetemeka kisha akazirai. Msemaji wake Henry Christmas Mbuta Vokia, alikaririwa akisema ’’marehemu Papa Wemba alikuwa ameingia muda mchache tu jukwaani kisha akacheza wimbo wa kwanza, mashabiki wakamuomba awaimbie tena wimbo mwengine akakubali. Lakini dakika chache tu baada ya kuanza kupiga wimbo wake wa tatu Papa Wemba alianguka na kuzirai ghafla jukwaani. Watu wa Shirika la Msalaba Mwekundu walijaribu kumsaidia lakini hakuonesha dalili nzuri kwa hivyo wakampeleka hospitali, lakini baada ya dakika karibu thelathini hivi tukaambiwa kuwa Papa Wemba ametuacha''

Watu walishuhudia kipande cha video kinachomuonesha jamaa mmoja akichukua microphone, halafu akairudisha kwenye steji.

Baada ya Pamba Wemba kuanguka, inadaiwa jamaa yuleyule badala ya kumsaidia alikimbilia kwenye ile microphone ili isijulikane kwamba alibadilisha.

Baadhi ya watu wakazagaza taarifa kwamba microphone hiyo ilikuwa imewekewa sumu. Taarifa za kifo chake ziliendelea kuwafikia watu mbalimbali akiwemo mwimbaji mkongwe wa Kongo DRC Koffi Olomide, ambaye aliandika maneno machache kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema ‘kwaheri Kaka, asante‘ na kuambatanisha picha yao ya pamoja ya siku nyingi kwenye hayo maneno.

Koffi Olomide amekuwa akitajwa kuwa mpiga gitaa wa zamani na mtunzi wa nyimbo kadhaa zilizoimbwa na Papa Wemba.

Baada ya miezi kadhaa kupita tangu mumewe afariki, Marie Rose Lozolo, au kwa jina jingine mama Amazone, mke wa marehemu Papa Wemba, alikutana na waandishi wa habari na kufunguka mengi kuhusiana na mpendwa wake huyo. Alianza kwa kusema kuwa katika maisha yake ya miaka 45 ya ndoa na mumewe walipitia mambo mengi.

“Bado naona ugumu kuishi bila mume wangu kipenzi ambaye alikuwa ni mwanamuziki kamili, mpole sana. Awapo nyumbani ni nadra sana kumsikia akiongea hovyo, lakini awapo jukwaani ni mtu mwingine tofauti kabisa, kwani huko ndiko ilikuwa dunia yake…” alisema Marie Rose Lozolo.

Aliendelea kusimulia kuwa, sehemu nyingine ambayo alikuwa akionesha uchangamfu wa hali ya juu ni pale anapokuwa na jamaa zake. Mama Amazone alifahamiana na Papa Wemba akiwa na umri wa miaka 15 tu, wakati marehemu mumewe alikuwa na miaka 20.

Katika kipindi chote alichoishi na mumewe hakuwahi kujua kama mumewe alikuwa na hadhi kubwa hadi pale alipofariki. “Wakati akiwa hai alikuwa akipenda kunitania mara kwa mara, akisema siku atakayokufa ndiyo nitajua hadhi yake, pia aliniambia angependa kifo chake kimkute akiwa kazini (Jukwaani ), kwa kweli utabiri wake ulitimia…” anasimulia Marie Rose Lozolo. Alitamka kuwa hakuwahi kuambiwa na Papa kama ana mke mwingine au watoto zaidi ya binti mmoja ambaye alimlea yeye aitwaye Kukuna. Mama Amazone alisema ataendelea kupigania haki miliki ya marehemu mumewe, kwani ameacha kazi nyingi na kubwa.

“Mume wangu alikuwa na nyimbo nyingi sana, kuna nyingine alishawahi kunitungia akinitamkia maneno haya; “Nasali nini Mpo, Nakoma Mopaya, Na Motema nayo yebisa Nga, Yebaka bolingo Emata Nzete, Boni lelo tokomi Separer, Ngai Naleli Ngo, Show me the Way, Maboko ezangi Amazone, Wemba alingaka, Ngai Naleli, Maboko ezangi Amazone, Jules Alingaka na nyuingine nyingi.

Tafsiri yake: Hebu niambie inakuwaje, najikuta kama mgeni moyoni mwako, fahamu kwamba penzi lina nguvu ya kuupanda mti hadi juu, vipi leo twafikia hadi kuachana! Nalia mie nalia kweli nammiss Amazone nimpendaye, mie Wemba nalia mie Jules, naimiss mikono niipendayo ya Amazone.

Marie Rose Lozolo alisema kabla ya kifo cha mumewe, walikuwa jijini Paris nchini Ufaransa ambako alipatwa na homa akalazwa hospitali kwa muda wa siku 10.

Iligundulika kuwa alikuwa na Malaria, baada ya kupata matibabu aliruhusiwa, lakini madaktari walimshauri apumzike kwa muda wa wiki nne.

Baada ya wiki nne kumalizika wakiwa Paris, waliamua kuongeza wiki mbili zaidi za mapumziko. Baadaye kuingia studio kurekebisha kazi ya albamu yake mpya ambayo tayari imeshatoka, kisha kurejea jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC).

Kwa ujasiri mkubwa mama huyo aliendelea kusimulia kuwa, waliwasili Kinshasa akiwa na afya njema kabisa na alikuwa akihudhuria mazoezini na vijana wake kama kawaida. “Siku moja kabla ya safari ya Abidjan, tulikuwa na wageni nyumbani kwetu, baada ya wageni kuondoka majira ya saa nne usiku, nilimuona mume wangu anapanga nguo zake kwenye begi, nikamuuliza kulikoni?

Akaniambia anajitayarisha kwenda mazoezini usiku huo, kwani asingeweza kurudi nyumbani kwakuwa asubuhi alitarajia kusafiri na vijana wake kwenda nchini Ivory Coast ambako angefanya onesho…” alisimulia mjane huyo.


Mama Amazone alisema hakufurahishwa na utaratibu huo, kwa vile alihofia hatua ya mumewe kulala mazoezini kungeweza kumsababishia matatizo ya kiafya, hivyo alimshauri kuachana na mpango huo, lakini Wemba alikataa. Alisema kuwa mazingira waliyokuwa wanafanyia mazoezi hayakuwa rafiki, yalikuwa na mbu wengi, ndiyo sababu hakuafiki uamuzi wake, akamshauri alale nyumbani, lakini aligoma.

“Nakumbuka siku mume wangu anasafiri ilikuwa Jumanne, ilipofika Ijumaa nikaenda kwenye ibada ya maombi, nikakaa huko mpaka Jumapili alfajiri ndio nikarudi nyumbani.

Ilipofika saa mbili asubuhi walikuja watu kuniamsha, huku wengine wakilia, nikajiuliza kuna nini? Wakaniambia mume wangu amefariki,” alisimulia kwa uchungu mama Amazone.

Papa Wemba aliyekuwa nguli aliyezikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa Soukus nchini DRC na kote duniani kwa kipaji chake cha kipekee na sauti isiyokuwa na mfano.

Wasifu wake unaeleza kuwa alizaliwa Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu - Wilaya ya Sankuru nchini Congo. Majina yake halisi alikuwa akiitwa Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, aliyeanza kazi ya muziki akiwa na umri mdogo mno.

Wemba alikuwa akimfuata mama yake katika matanga na hivyo akaibukia kuwa mtunzi wa nyimbo za kuomboleza. Shungu Wembadio alijiunga na kundi la ''Stukas'' kabla ya kuliacha, akajiunga katika kundi kubwa la Zaiko Lana Langa mwaka huohuo wa 1969.

Akiwa na bendi hiyo, sauti yake ya kipekee na uweledi wake uliisaidia kundi hilo katika utunzi wa nyimbo za "Pauline", "Chouchouna" na "Liwa is somo".

Wemba wakati huo aliungana na wanamuziki wenzanke akina Nyoka Longo Jossart, Manuaku Pepe Felly, Evoloko Lay Lay, Bimi Ombale, Teddy Sukami, Zamuangana Enock, Mavuela Simeon, Clan Petrole na wengine kadhaa.

Wakati Papa Wemba anaanza kupiga, jukwaa la muziki nchini humo lilikuwa limetawaliwa na vigogo wa muziki Franco Luambo Luanzo Makiadi wa T.P.OK. Jazz, Tabu Ley Rochereau wa Afrisa Internationale, na makundi mengine mapya kama vile Les Grands Maquisards, Le Trio Madjesi, Bella-Bella na Thu Zaina na Empire Bakuba.

Hata hivyo sauti ya kipekee ya Papa Wemba akijulikana wakati huo kwa majina yake kamili yakawa Jules Presley Shungu Wembadio, aliyezikonga mioyo ya wapenzi wa Soukus.

Kilele cha ufanisi wa kundi la Zaiko Langa Langa ulikuja miaka ya mapema ya mwaka 1973. Shungu ndipo alipobadili jina lake na kuanza kuitwa jina la utani ''Papa Wemba''.

Baada ya miaka mitano alilihama kundi hilo na kujiunga na kundi la Isifi Lokole. Hapo alitunga wimbo maarufu wa "Amazon", aliokiri kuwa alimtungia mkewe.

Hata hivyo Papa Wemba aliamua kuliacha kundi hilo akaenda kujiunga na kundi lingine la Yoka Lokole, kabla yake kuunda kundi lake la Viva La Musica" mapema mwaka wa 1977.

Vibao vyake ni kama Mwasi, Show me the way, Yolele, Mama, Proclamation "Chouchouna" alizotunga yeye Papa Wemba, "Eluzam" na " Mbeya Mbeya", utunzi wake Evoloko Lay Lay, "BP ya Munu" uliotungwa na Efonge Gina, "Mwana Wabi" na "Mizou" zilizotungwa na Bimi Ombale.

Wimbo wa "Zania" ulikuwa utunzi wake Mavuela Somo, Emotion, Wake Up, Maria Valencia, Le Voyageur,Rail On, Kaokokokorobo, Legend tunzi zake nguli Papa Wemba.

Wembadio Papa Wemba aliwahi kukamatwa kwa madai ya ulanguzi wa binadamu. Aidha Februari 18, 2003, maafisa wa idara ya upelelezi nchini Ufaransa walimkamata Papa Wemba kwa tuhuma za kuwaingiza raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Zaire wakati huo) barani Ulaya kinyume cha sheria.

Mahakama ya ubelgiji ilimpata na hatia mwezi Juni mwaka wa 2003, ikamhukumu kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitatu jela. Aidha mahakama hiyo ya Brussels ilimpiga faini ya Euro 22, 000. Hata hivyo alitumikia kifungo cha miezi mitatu na nusu gerezani baada ya mdhamini kulipia dhamana ya Euro 30,000.

Papa Wemba alipoachiwa huru aliwaambia mashabiki wake kuwa aliyokumbana nayo akiwa gerezani yamemfunza mengi tu. Katika utunzi wa wimbo wake "Numéro d'écrou" (2003), Papa Wemba alisimulia kukutana na mwenyezi Mungu akiwa gerezani.

Huyo na ndiye Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba ‘Papa Wemba’ aliyeiaga dunia akiwa na umri wa miaka 67. Mungu aipumzishe roho yake pahala pema peponi, Amina.

Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba: 0784331200, 0713331200, 0736331200 na 0767331200.

BINTI HUYU NI MGONJWA ANAHITAJI MSAADA WAKO

$
0
0
Happiness Stephen Makala,mkazi wa mtaa wa Busulwa kata ya Kitangili Manispaa ya Shinyanga anaomba msaada wa matibabu kwa mtoto wake aitwaye Rogathe Cyprian Makala mwenye umri wa miaka 18, ambaye anayesumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa ngozi kwa muda wa miaka 16 sasa.

Anasema amehanghaika katika hospitali mbalimbali hapa nchini, lakini siku moja alikutana na Daktari Bingwa kutoka Apolo India katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ndipo akampima na kumgundua kuwa homoni zake ziko kwenye njia ya mkojo, hivyo anatakiwa apatiwe matibabu ndani ya miezi tisa kwa kupatiwa dawa kutoka India, ambapo kila mwezi inatakiwa shilingi 504,000 ambapo kwa miezi hiyo tisa ni sawa na shilingi milioni 4.5 (4,536,000/-).

Kwa mujibu wa Daktari huyo,binti huyo akifikisha umri wa miaka 20 ugonjwa huo wa ngozi utaweza kugeuka na kuwa kansa, na ataweza pia kuwa anazaa watoto wenye kisukari, na kichwa kikubwa na hata kuambukiza watu wengine kwa njia ya kuchangia choo.

Daktari huyo huwa anakuja kila baada ya mwezi hapa mkoani Shinyanga ambapo dozi ya dawa hiyo anatakiwa aanze Juni 2 mwaka huu ambapo itakuja na daktari huyo.
Mama wa binti huyo anasema yeye hana uwezo wa kumtibu binti yake, mume wake alishafariki kwenye ajali mwaka (2007) ambaye alikuwa Mhasibu wa shirika la umeme TANESCO mkoani Shinyanga.

Mama wa mtoto anasema mwanae huwa halali usiku kucha anashinda anajikuna tu na hata wakati wa jua kali huku vipele vikimtoka mwili mzima, na anatarajia kujiunga na kidato cha tano kwani amefaulu kidato cha nne.

Kwa yeyote atakayeguswa kumsaidia awasiliane kwa namba zifuatazo:


Vodacom : 0764206669 ukitaka kutuma kwa m-pesa jina litasoma Happines Makala

Halotel: 0626845953 jina litasoma Eliud Makala

BUKOBA HALI IMEZIDI KUIMARIKA BAADA YA MVUA KUBWA KUNYESHA.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Kagera.

Hali ya Miundo mbinu na maeneo korofi ndani ya Manispaa ya Bukoba, imeanza kuimarika baada ya Mvua kubwa iliyonyesha Mei 26, 2019 na kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo mengi Mjini humo.

Mvua hiyo iliyoanza kunyesha majira ya Asubuhi saa mbili, na kisha kukatika baada ya muda wa lisaa moja, mpaka sasa inasubiriwa ripoti rasmi kufahamu ni athari kiasi gani na madhara yaliyotokana na mafuriko hayo, ingawa duru zinaeleza kuwepo kwa kifo cha mtoto mmoja, upotevu na uharibifu wa Mali nyingi kufuatia mafuriko hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Gen Marco E. Gaguti amekaririwa katika ukurasa wake wa Twitter akiandika kuwa " Hali imeendelea kumarika baada ya Mafuriko ya Jana Tarehe 26 MRI 2019. Tuendelee kuchukua tahadhari kwani Mvua bado zipo. Aidha tuzingatie kanuni muhimu za Afya kuepuka magonjwa ya Mlipuko".

Katika ujumbe huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Uslama Mkoa Mhe. Gaguti Ameweka baadhi ya Picha zikionesha maeneo yaliyokuwa korofi na kushindwa kupitika Jana kufuatia wingi wa Maji na sasa yanapitika vizuri na shughuli nyingine za kijamii zinaendelea kama kawaida.
 Muonekano wa hali ilivyokuwa Jana na Leo, katika Daraja eneo la Lina's Hotel  baada ya hali kuimarika.
 Daraja la Kanoni maarufu kwa wauza senene muonekano wa Jana na Leo.
 Pichani Rc Gaguti akionekana kukatiza  viunga mbalimbali Manispaa ya Bukoba kujionea hali ilivyo kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha Tarehe 26, Mei 2019 na kusababisha Mafuriko.
Moja kati ya madaraja mengi ya watembea kwa miguu, linalopatikana maeneo ya Rwamishenye Machinjioni, kuelekea Kyebitembe hali iko hivyo.

WAZIRI UMMY AKABIDHI SHEHENA YA FUTARI KWA TAASISI NNE KUBWA ZA KIISLAMU JIJINI TANGA

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani Futari hiyo kushoto ambapo vitu viliyotolewa kwa kila taasisi ni Mchele kilo 100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo 50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo walikabidhiwa 
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani Futari kushoto ambapo vvitu viliyotolewa na Mchele kilo 100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo 50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo walikabidhiwa 
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimkabidhi sehemu ya shehena ya futari mmoja wa wanafunzi wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa Imamu Abdallah
Sehemu ya Shehena ya futari ilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa ajili ya Taasisi kubwa nne za Kiislamu Jijini Tanga 
Sehemu ya Shehena ya Futari iliyotolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) kwa Taasisi nne kubwa za Kiislamu Jijini Tanga 
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimsikiliza Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa ya Jijini Tanga Omari Athumani kulia mara baada ya kufanya makabidhiano ya shehena ya futari 


MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ametoa shehena ya futari kwa Taasisi kubwa za nne za Kiislamu Jijini hapa kwa ajili ya matumizi kwenye mwezi mtukufu wa ramadhani

Taasisi ambazo zimepata futari hiyo iliyotolewa na Mbunge Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ni Shamsi Maarifa ,Zaharau,Maawal na Tamta ambapo halfa ya makabidhiano hayo yalifanywa na kwenye taasisi zao.

Futari iliyotolewa kwa kila taasisi ni Mchele kilo 100, Maharage kilo 100, Tambi mifuko miwili, Sukari kilo 25, Unga wa Ngano kilo 50, Unga wa Sembe kg 25, Mafuta ya kula lita 20 na majani ya chai ambazo walikabidhiwa 

Akizungumza baada ya kukabidhi futari hiyo Waziri Ummy alisema ameona atoe futari hiyo kwa taasisi hizo kubwa kwa niaba ya wakazi wa mkoa wa Tanga akiwa kama kiongozi wa mkoa huo kwenye kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Nikiwa kama mwana jamii na kiongozi wa mkoa wa Tanga nimeona nitoe futari kwa taasisi hizo kubwa nne kwa niaba ya wakazi wa Tanga ambazo zinafundisha vijana wetu kutoka maeneo mbalimbali elimu ya dini na mambo yanayohimizwa kwenye dini kwani shamsi maarifa ina wanafunzi 600,zaharau wanafunzi 200“Alisema.

Aidha pia aliwataka waislamu mkoani Tanga kuendelea kutenda mambo mema kwenye mwezi mtukufu wa ramadahani na kuendelea kuyatenda hata baada ya kumalizika mwezi huo ikiwemo kufanya ibada kila wakati. 

Awali akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Katibu wa Taasisi ya Kiislamu ya Shamsi Maarifa iliyopo Duga Jijini humo Omari Athumani alimshukuru Waziri Ummy huku wakieleza wamepata mtu wa pekee Tanga kutokana na kuwa karibu na wananchi kila wakati kwa kutoa misaada.

Alisema kwamba hii sio mara ya kwanza kutokana na kwamba amekuwa akiwajali wananchi kwa kujitolea vitu mbalimbali wakati wa mwezi mtukufu wa ramadani na hivyo ni wazi kwamba tumepata mtu wetu sahihi kwa mkoa wa Tanga.

“Tuna mshukuru Mwenyezi Mungu akuongoze kwenye kazi zako na aendelee kukupa afya njema wewe a kubwa wataendelea kuliombea Taifa Amani na kumuombea Afya njema Rais wetu Dkt John Magufuli na kumtakia mafanikio katika kuliongoza Taifa”Alisema 

Mafunzo ya Ununuzi wa Umma Kuondoa Utata wa Mwenye Mamlaka ya Kusimamia Manunuzi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Nicholas William amesema kuwa mafunzo ya ununuzi wa umma kwa Wakuu wa Idara na Vitengo yatasaidia kuondoa utata uliopo kuhusu suala la kusimamia mikataba ya ununuzi wa umma kati ya Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB).

“Kumekua na utata kuhusu suala la yupi mwenye mamlaka ya kusimamia mikataba ya ununuzi wa umma kati ya Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi hivyo natoa rai kwa watoa mafunzo kuondoa utata huo,”alisema Bw. William.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yanahitajika hasa kwa viongozi wa umma kwani ndio wahusika wakuu katika kupitisha mikataba mbalimbali ya ununuzi.

Aidha, amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupunguza muda unaotumika kufanya ukaguzi kwa kuwa mikataba ya ununuzi wa umma haitakuwa na changamoto nyingi kwani wahusika watakuwa na uelewa mpana katika maandalizi ya mikataba hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, Bw. Godfrey Mbanyi amesema kuwa lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuwafanya wanaohusika na kutoa maamuzi juu ya manunuzi ya umma kuwa na uelewa wa pamoja ili kuhakikisha mikataba wanayoingia haileti kasoro yoyote.

“Kumekua na changamoto kwa wakuu hawa wanapoteuliwa kuwa Wajumbe wa Bodi za Zabuni wanakuwa hawajui chochote kuhusu taratibu za ununuzi wa umma hivyo semina hii itawasaidia kufahamu taratibu hizo,” alisema Bw. Mbanyi.

Bw. Mbanyi ameongeza kuwa kutokujua taratibu za manunuzi ya umma zinawasababishia matatizo viongozi wa juu kwani vitu visiponunuliwa kwa wakati au visipokuwa na ubora hatua zikianza kuchukuliwa zinaanzia kwa viongozi hao hivyo tukiwa na uelewa wa pamoja utasaidia viongozi wetu wasiwajibishwe.

Vile vile Bw. Mbanyi amefafanua kuwa Wakuu wa Idara na Vitengo wana wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba taratibu za manunuzi ya umma na thamani ya fedha katika michakato wa manunuzi hayo inapatikana kwani si lengo la Serikali kupata bidhaa na huduma kwa fedha ambazo hazina thamani halisi.

Hata hivyo Bw. Mbanyi ametoa rai kwa waajiri kuhakikisha wanaohusika na manunuzi ya umma katika ofisi zao wawe wamesajiliwa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani kutokufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Nicholas William akifungua mafunzo kuhusu Manunuzi ya Umma yanayoendeshwa na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) kwa Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo kuanzia Mei 27 -28 Jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Tanzania Bw.Godfrey Mbanyi na Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo Bw.Orest Mushi.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw.Godfrey Mbanyi akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati Bodi hiyo ilipoendesha mafunzo ya siku mbili kuhusu Manunuzi ya Umma kuanzia Mei 27- 28, 2019 Jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo Bw.Orest Mushi, na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi wa Wizara hiyo Bibi Cecilia Kasonga.
  Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Orest Mushi akizungumza wakati wa mafunzo ya Ununuzi na Ugavi yanayotolewa na Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Tanzania (PSPTB) kwa Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo kuanzia Mei 27- 28 2019 Jijini Dodoma.Katikati ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bw.Nicholas William na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi Bw.Godfrey Mbanyi.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw.Nicholas William (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Bw.Godfrey Mbanyi (wa pili kushoto) na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo baada ya kufungua mafunzo kuhusu Sheria ya Manunuzi ya Umma yanayoendeshwa na Bodi hiyo kuanzia Mei 27 -28,2019 Jijini Dodoma.



AFANYA MAUAJI YA WATU WATATU NA KUJIMALIZA MWENYEWE KWA WIVU WA MAPENZI HUKO DUMILA MKOANI MOROGORO

$
0
0
Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Michael John Mwandu mwenye umri wa miaka 54 mkazi wa Dumila wilaya ya Kilosa amejiua mwenyewe kwa kunywa sumu baada yakufanya mauji ya kumuua mke wake Leonola Ernest mwenye miaka 37 akiwa na ujauzito wa miezi Kati ya 7 hadi 8,

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro ASCP Wilbrod Mutafungwa amewataja marehemu wengine kuwa ni mama mkwe wa muuji Magreth Yohana mwenye umri wa miaka 59,Salma Iddi jirani yao mwenye umri wa miaka 52 na pamoja yeye mwenyewe marehemu Michael John ambaye amejiua baada yakufanya mauji hayo chanzo Cha vifo hivyo ni wivu wa kimapenzi alioubaini akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine huku akidai hao wengine walikuwa wakifahamu Jambo hilo.

Marehe ametumia panga kumuua mama yake mkwe huku yeye na marehemu wengine wakinywa sumu aina ya Carbon Furan ambayo ni dawa yakuua wadudu kwenye mimea

Tukio hilo limetokea tarehe 24/5/2019 usiku huko Dumila mkoani Morogoro.
Baadhi ya waandishiwa habari wakimsikiliza Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro ASCP Wilbrod Mutafungwa wakati akizungumzia mauaji hayo.
Baadhi ya ushahidi ulioonyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Wilbrod Mutafungwa.

Madereva fuateni sheria za usalama barabarani kupunguza ajali - Samwix

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Blog ya Jamii
Ajali za barabarani zinaweza kupungua au kuisha   kutokana na madereva kukubali katika kufuata kanuni pamoja na sheria za usalama barabarani katika uendeshaji wa mabasi ya mikoani na nje ya nchi jirani.

Akizungumza na Madereva wa Mabasi ya Mikoani na nchi jirani Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi wa Mabasi na Magari cha Ubungo jijini Dar es Salaam Ibrahim Samwix wakati akitoa mafunzo kwa medereva wa mabasi ya mikoani na nchi jirani  yaliyofanyika katika kituo cha Ofisi za Ukaguzi  majira ya saa 11 alfajiri jijini Dar es Salaam.

Samwix amesema kuwa madereva wakifata kanuni za kidereva  kwa kufuata matakwa yaliyowekwa basi ajali zitapungua au kuisha kabisa.

Samwix amesema kuwa taratibu zilizowekwa kwa mabasi yanayokwenda zaidi ya masaa nane kuwa na madereva wawili lakini kuna watu wanakuwa na madereva wasio na sifa 'Bosheni' ambapo ni kosa la sheria kwa dereva kuwa na dereva asiokuwa na sifa za udereva.

Amesema kuwa madereva waonyeshe ushirikiano  mara baada ya kuona dereva mwenzao hana mtu wa pili kutoa taarifa katika kituo cha  ukaguzi Ubungo ili kuweza kuwachukulia sheria kwa dereva kuruhusu kukaa na dereva wa pili asiyekuwa na sifa bosheni.

Aidha amesema kuwa mafunzo wanayoyatoa kwa madereva ni endelevu ii kufanya kazi hiyo kwa kujitambua pamoja na kuepuka na ajali ambazo zinauwezekano kukwepeka kutokana na ustadi wa udereva.

Amesema kuwa mafunzo hayo wakijua wataweza kuwa mabalozi wa madereva wengine kwa kueleza mbinu mbalimbali za uendeshaji wa mabasi kwa kuangalia masilahi ya abiria.

"Teknolojia  ya mabasi inabadilika hivyo lazima madereva wa mabasi wa wabadilike ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo ya namna ya kuendesha magari kwa kisasa na sio mazoea ya udereva wa mwaka 1940"amesema Samwix.
 Mkuu wa  Kituo cha Ukaguzi Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo INSP. Ibrahim Samwix akiwafundisha madereva wa mabasi ya mikoani na nchi jirani mamna ya kuepuka ajali wakati gurudumu limepasuka katika mafunzo ya madereva Katika kituo hicho.
 Mkuu wa Kituo cha Ukaguzi cha Ubungo Ibrahimu Samwix akitoa mafunzo madereva wa mabasi ya mikoani na nje ya nchi kwa ajili ya kujitambua katika kazi yao ya Udereva.
Madereva wakiwa katika mafunzo  katika kituo kikuu cha mabasi.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKELEWA NA MWENYEJI WAKE, RAIS HAGE GEINGOB WA NAMIBIA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Mwenyeji wake Rais Hage Geingob wa Namibia alipowasili katika Ikulu ya nchi hiyo, Jijini Windhoek leo Mei 27, 2019. Rais Dkt. Magufuli amewasili nchini Namibia kwa Ziara Rasmi ya Kikazi ya Siku mbili.





VEN ROSSY; CHIPUKIZI WA BONGO FLEVA ALIYEDHAMIRIA KUFANYA MAMBO MAKUBWA...

$
0
0
*Miondoko yake haina tofauti na staili za Sam wa Ukweli

Na Ripota,Globu ya jamii

KADRI siku zinavyokwenda ndivyo sanaa ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini unazidi kukua siku hadi siku huku vijana mbalimbali wakija kwa kasi na ubunifu wa hali ya juu katika utunzi wa mashairi yanayokonga nyoyo.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Ronald Nnko ‘Ven Rossy’, mzaliwa wa Mkoa wa Arusha aliyeingia hivi karibuni katika sanaa ya muziki huo maarufu hapa nchini kama ‘Bongofleva’

Ven Rossy anayetamba na wimbo wake wa ‘Nakupenda’ ambao ndiyo uliomtambulisha kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa muziki nia yake ni kufika mbali kupitia sanaa hiyo hapa nchini na pengine Duniani kwa ujumla.

Akizungumzia ujio wake katika sanaa hiyo Ven Rossy anasema kwake muziki ni kitu kilichopo katika damu yake tangu akiwa mtoto akianza kuimba kwa kujifunza kupitia nyimbo mbalimbali walizokuwa wakiimba shuleni huku pia akifuatilia mashairi yaliyokuwa yakiimbwa na wasanii mbalimbali redioni

Ven Rossy ambaye unaweza kumfananisha na msanii Sam wa Ukweli ambaye kwa sasa ni marehemu, ujio wake katika sanaa hii ya muziki wa `BongoFleva’ ni kama vile utawafuta machozi mashabiki wa msanii huo kutokana na style ya uimbaji wake unaendana kwa kiasi kikubwa.

Anasema ujio wa ‘Nakupenda’ uliotengenezwa na Producer ‘Napoli’ kupitia Studio aliyoipa jina lake ‘Napoli’ ni kisa cha ukweli kinachohusu maisha yake ya uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja ambaye anakiri kuwa hakuwahi kupenda kama ilivyo kwa msichana huyo katika ulimwengu huu.

Ameimba mambo mengi katika wimbo huo uliotawaliwa na ufundi mzuri wa vinanda kutoka kwa ‘Napoli’ Producer aliyefanya makubwa katika sanaa ya muziki huo baada ya kufanya kazi mbalimbali zinazotamba katika vituo mbalimbali.

Video ya Nakupenda ambayo kama ilivyo kwa wimbo huo pia imeanza kutamba kupitia Channel ya ‘You-Tube’ na Televisheni mbalimbali hapa nchini imefanywa na Director ‘Diddy’ kiasi cha kuifanya video ‘kichupa’ hicho kuonekana kama moto wa kuotea mbali.

Anasema mbali na wimbo huo wa ‘Nakupenda’ kwa sasa yupo Studio akiendelea kurekodi nyimbo zingine mbili ambazo ujio wake utawahusisha ‘Corrabo’ wasanii mbalimbali wanaotamba katika sanaa hiyo.

Kuhusu wasanii waliopo katika sanaa hiyo ya muziki wa kizazi kipya Ven Rossy anasema wengi wanafanya vizuri hivyo anaamini atapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwao na mashabiki wote wa muziki wakati huu ambao ameingia rasmi katika ‘Game’ hiyo.

Anasema hadi alipofikia ni kutokana na nguvu na jitihada zake binafsi akiwa hana Meneja kwa ajili ya kumsimamia huku akisisitiza kuwa yupo tayari kufanya kazi na Menegment yoyote itakayokuwa na malengo na dhamira ya kweli katika kazi.

Unaweza kumfollow Ven Rossy kupitia kurasa zake za Kijamii kwa account zifuatazo

SHULE YA MSINGI HAZINA WATIA FORA MASHINDANO YA KITAALUMA

$
0
0
Na Ripota wa Michuzi TV 

WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Hazina ya Magomeni wametia fora katika mashindano ya kitaaluma kwa shule za msingi katika Jiji la Dar es Salaam. 

Mashindano hayo ya kitaaluma yameandaliwa na Shule za Feza kwa kushirikisha shule mbalimbali za msingi za umma na za binafsi jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa Taaluma wa shule ya Hazina Dennis Nyakerandi amesema mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kwenye mashindano hayo Salma Sadiki Mushi ametoka katika shule yao. 

Amewataja wanafunzi wengine wa Hazina walioingia 10 bora kwenye mashindano hayo ni Ibrahim Sharif aliyeshika nafasi ya pili na nafasi ya nne ilichukuliwa na Patricia Benatus wa shule hiyo. 

Wengine ni Sahill Imam aliyeshika nafasi ya nne, Maliki Yassin nafasi ya sita na nafasi ya nane kwenye mashindano hayo ilichukuliwa na Khaulat Majid wa shule hiyo ya Hazina. Hivyo amesema matokeo hayo yamewapa motisha kuwa wanaendelea kufanya viziuri kwenye taaluma na wanatarajia kufanya vizuri zaidi kwenye mitihani inayokuja. 

Ameongeza ushindi huo haukuja tu bali umetokana na jitihada za walimu kuwaandaa wanafunzi kwaajili ya mitihani. "Hivyo sisi imetupa moyo kazi tunayofanya inazaa matunda." 

Pia amesema kwenye mashindano hayo wanafunzi wamefanya mtihani wa Hisabati na Sayansi ambapo wanafunzi walipaswa kumaliza ndani ya saa mbili na kwamba wao walipeleka wanafunzi 10 na sita wakaingia 10 bora tena kwenye nafasi za kwanza. 

"Tunajivunia mafanikio haya kwani wanafunzi walikuwa wengi sana lakini wamefanya vizuri.Tunawapongeza walimu wetu kwa mafanikio haya,"amesema na kusisitiza wataendelea kufanya vizuri siku hadi siku. 
Mkuu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Hazina, Dennis Nyakerandi akimpa zawadi ya vitabu mwanafunzi wa shule hiyo, Salma Mushi kwa kuwa wa kwanza kwenye mashindano ya Hisabati na Sayansi yaliyoshirikisha zaidi ya wanafunzi 350, yaliyoandaliwa na shule za Feza jijini Dar es Salaam. Wengine nyuma ni wanafunzi wa shule hiyo waliofanikiwa kuingia 10 bora kwenye mashindano hayo. 
Wanafunzi wa shule ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Slaam, wakiwa na vyeti vyao walivyokabidhiwa baada ya kushinda na kuingia 10 bora kwenye mashindano ya Hisabati na Sayansi shindano lililowashirikisha zaidi ya wanafunzi 350 kutoka shule mbalimbali. Shindano hilo limefanyika katika shule ya Feza. Wanafunzi wengine wa shule hiyo wanaoshuhudia nao walifanikiwa kuingia 10 bora.

WATOTO 20 KUFANYIWA UPASUAJI WA MOYO KWA TUNDU DOGO NA WATAALAMU KUTOKA ISRAEL

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete imepokea wataalamu wa moyo kutoka Canada na Israel ambao watafanya upasuaji kwa  wa moyo kwa watoto 20 ndani ya wiki moja na hiyo ni kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete profesa Mohamed Janabi amesema kuwa taasisi ya Save a Chil's h Heart   kutoka Canada imekuja nchini zaidi ya mara tano kuanzia mwaka 2015 na ujio wao umekuwa na manufaa kwa kuwa walifundisha namna ya kufanya upasuaji kwa tundu dogo na safari hii wamewaalika wenzao kutoka nchini Israel nchi ambayo imetoa mafunzo kwa manesi wa uangalizi maalumu kutoka taasisi hiyo ya JKCI.

Janabi amesema ikiwa ni mara ya pili ya wataalamu hao kufanya upasuaji wa namna hiyo, wamelenga kuokoa maisha ya watoto huku akieleza kuwa upasuaji huo unatumia gharama nafuu na muda wa kulazwa ni mchache zaidi, (takribani siku 2 pekee.)

Amesema kuwa ushirikiano baina ya nchi hizo umekuwa na manufaa hasa katika kubadilishana ujuzi na kukutana kwa madaktari bingwa hao kwa muda wa wiki moja kutakuwa ni kwa kujifunza baina ya pande zote mbili.

Awali akieleza historia na majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo Profesa Janabi amesema kuwa mikakati ya taasisi hiyo ni kuzidi kuwahudumia watoto wenye matatizo hayo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Amesema kuwa Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa ushirikiano katika kuhakikisha matibabu ya watoto hao yanafanikiwa na tayari mwezi uliopita manesi 2 wamepelekwa Nairobi, Kenya kwa ajili ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi ya Save a Child's Heart kutoka Canada Marni Brinder Byk amesema kuwa taasisi hiyo imedhamiria kuokoa maisha ya watoto pamoja na kudumidha mahusiano bora yenye tija kwa sasa na baadaye.

Brinder amesema kuwa wamefurahi sana kuja Tanzania na wanataraji kujifunza mengi kutoka taasisi hiyo pamoja na kudumisha mahusiano bora hapo mbeleni

Vilevile wakili na Mkurugenzi wa taasisi ya Save a Child's Heart kutoka Israel Simon Fisher amesema kuwa Tanzania ni nyumbani na wanaamini wataendelea kusaidia watoto Tanzania na kote duniani katika kuokoa maisha yao.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Janabi Mohamedi akizungumza wakati kutambulisha ugeni wa madaktari bingwa kutoka Israel ambao watafanya upasuaji kwa watoto 20 ndani ya wiki moja, leo jijiji Dar es Salaam.
 Wakili na Mkurugenzi wa Taasisi ya Save a Child's  Heart kutoka Israel Simon Fisher akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa wamedhamiria kuokoa maisha ya watoto hao pamoja na kudumisha mahusiano bora ya sasa na baadaye, leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi na madaktari wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.
Wataalamu na madaktari bingwa kutoka Israel na Canada (walioketi mstari wa mbele) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa Mohamed Janabi wakati wa kikao kazi kitakachowakutanisha madaktari hao katika kufanya upasuaji wa moyo kwa watoto 20, leo jijini Dar es Salaam

RAIS WA SOMALIA ATUA NCHINI KWA DHARURA, APOKELEWA NA WAZIRI LUGOLA UWANJA WA NDEGE, AMPONGEZA JPM KWA KUKUZA UCHUMI, UONGOZI MADHUBUTI

$
0
0


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimpokea Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini akielekea nchini Somalia. Katikati ni Balozi wa Somalia nchini, Mohamed Hassan Abdi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini akielekea nchini Somalia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wa pili kulia) akimuaga Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini akielekea nchini Somalia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kulia) akimpokea Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, wakati Rais huyo alipokua amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa dharura akitoka nchini Afrika Kusini kuelekea nchini Somalia. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


Na Felix Mwagara, MOHA 

RAIS wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam kwa dharura akitokea nchini Afrika Kusini kuelekea Somalia. 

Akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, katika ukumbi wa mikutano wa Wageni Mashuhuri (VIP) uwanjani hapo, mara baada ya kupokelewa na Waziri huyo, Rais Farmajo alimpongeza Rais John Magufuli kwa kukuza uchumi na kuwa na uongozi imara katika nchi yake. 

“Nina furaha kuingia Tanzania japo kwa dharura, kwa kuwa nchi hii ni Rafiki na Somalia, naomba mpelekee ujumbe huu mheshimiwa Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, na pia mpe pongezi kwa kukuza uchumi,” alisema Rais Farmajo. 

Rais Farmajo ambaye alitua nchini ajili ya ndege anayoitumia kuwekwa mafuta, pia alimuomba Rais Magufuli, nchi yake iweze kupata idadi kamili ya wazuiwa na wafungwa wote ambao wanakesi zinazohusiana na Uhamiaji waliopo magerezani hapa nchini, ili Serikali ya Somalia iweze kuwasafirisha kwa mujibu wa sheria. 

“Serikali ya Somalia inatambua kuwa na uhusiano madhubuti na Tanzania, Somalia ipo tayari kufanya utaratibu wa kisheria ili kuweza kuwarudisha nyumbani wafungwa wote ambao wanakesi zinazohusiana na uhamiaji,” alisema Rais Farmajo. 

Pia Rais Farmajo ameishukuru Tanzania kuwapa mazingira mazuri ya biashara, wafanayabiashara na Wawekezaji wenye asili ya Somalia walipo nchini. 

Rais Farmajo aliwasili saa 8:38 mchana, jijini Dar es Salaam, na kufanya mazungumzo na Waziri Lugola kwa muda wa dakika 30, na baadaye aliondoka nchini kuelekea Somalia. 

MJUE SAMBA MAPANGALA ‘MZEE WA VUNJA MIFUPA’

$
0
0
Na Moshy Kiyungi
SAMBA MAPANGALA ni mtunzi na mwimbaji maarufu wa kimataifa aliyejizolea sifa tele Afrika ya Mashariki na Kati hususani katika nyimbo zake za ‘Vunja Mifupa’ na ‘Dunia tunapita’

Ni mwanamuziki mwenye kipaji cha aina yake, anaye kula ‘Kuku’ katika jiji la Washington DC nchini Marekani. Alimfanyia kampeni rais Barack Obama wa Marekani mwaka 2008.

Alizaliwa huko Matadi katika mkoa uliojulikana kama Bas-Congo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Miaka ya 1970 alipiga muziki na bendi nyingi katika jiji la Kinshasa wakati akiwa katika masomo ya Sekondari.

Kipaji cha Mapangala kigundulika kupitia tungo zake ambazo kila wimbo una ujumbe mzito masikioni mwa msikilizaji. Mfano wa karibu ni wimbo wa ‘ Dunia tunapita’ Wimbo huu unaelezea juu ya jamaa ambaye hawezi kufanya chochote kile bila kupita kwa waganga.

Kunyooka kwa Safari ya Samba Mapangala katika masuala ya muziki kulianza kuonekana mapema miaka ya 1970 alipoondoka Matadi kwenda katika Jiji la Kinshasha kwa ajili ya masomo ya Sekondari.

Sifa kubwa aliyonayo Mapangala ni ya kuweza kutunga, kuimba nyimbo kwa lugha za Lingala na Kiswahili pia uwezo mkubwa alionao wa kumiliki Jukwaa.

‘Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza’ Usemi huu ulijidhihirisha kwa Mapangala baada ya kuonyesha umahiri mkubwa kupitia sauti yake nyororo kulipelekea kupata kazi ya kupiga muziki kwenye bendi za Bariza, Super Tukina, Bella Bella na Saka Saka katika jiji la Kinsahasa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Juhudi zake katika muziki zilimfikisha kusafiri na wanamuziki wenzake kwenda Mashariki mwa Kongo mwaka 1975. Mwaka iliofuatia wa 1976 walivuka mpaka kwenda Kampala nchini Uganda hako wakaunda bendi ya Le Kinois.

Akiwa mwimbaji Kiongozi Samba Mapangala na bendi yake ya Les Kinois ilihamisha makazi toka Kampala na kwenda jiji la Nairobi nchini Kenya mwaka 1977.

Licha ya kuwa na ushindani mkali toka bendi zingine kubwa katika jiji katika hilo la Nairobi, bado Les Kinois walifanikiwa kuliteka jiji hilo kwa kasi kubwa.

Wakati huo jiji la Nairobi kulikuwa na bendi za Super Mazembe, Orchestra Les Mangelepa, Les Wanyika, Orchestra Moja One , Baba Gaston na nyingine nyingi.

Ili kuonyesha ukomavu katika muziki, Samba aliamua kujitegemea mwenyewe kwa kuunda bendi yake na kuipa jina la Orchestra Virunga mwaka 1981 bendi ambayo kwa kipindi kifupi ikakubalika na wapenzi wa muziki na kuwa moja kati ya bendi maarufu Afrika Mashariki.

Samba Mapangala hupiga muziki wake ukiwa na mchanganyiko wa staili za rumba na Soukous kutoka Kongo. Ili kuwaridhisha wapenzi wa muziki wa Nairobi na vitongoji vyake walipiga muziki kwa staili za watu wa Kenya. Rekodi ya kwanza ya Virunga iliyoitwa ‘It's Disco Time with’ ilitoka mwaka 1982.

Mapangala na bendi yake ya Virunga walisafiri kwenda nchini Uingereza mwezi Aprili 1991 na huko walifanya maonyesho makubwa takribani 23. Baada ya kufurahia mafanikio ya safari yao, walifanya safari nyingine ya mwisho mwaka 1997 wakipitia nchi za Afrika hadi Marekani ya Kaskazini.

Album za Samba Mapangala zilizopo ni pamoja na Virunga Volcano ya mwaka 1990, Evasion ya 1983, Feet on Fireya ya 1991, na Karibu Kenya iliyofyatuliwa mwaka 1995 zilizorekodiwa katika jiji la Paris nchini Ufaransa akiwashirikishwa wanamuziki toka bendi ya Les Quarters Etoiles na wanamuziki wengine nguli waliokuwa hapo Paris.

Album ya Vunja Mifupa iliyotoka mwaka 1997 ilichukua soko kubwa la mauzo hususani Afrika ya Mashariki ikizingatiwa Ujumbe unatolewa kwa lugha ya Kiswahili. Virunga Roots Volume 1, ulijumisha nyimbo zilizo katika kumbukumbu Virunga na kutolewa mwaka 2005.

Samba kwa kawaida ni mpole na mcheshi, mwaka 2000, alialikwa kwenye Sherehe ya siku ya Jamhuri ya watu wa Kenya katika jiji la London, ambapo muziki waliopiga ‘uliwachengua’ watu wote waliofika katika sherehe hiyo. Mzee wa ‘Vunja Mifupa’ Samba Mapangala alikuja Tanzania mwezi Mei 2004 kwa ziara ya wiki mbili na kufanya maonyesho kadhaa.

Nguli huyu hupenda kushirikina na wanamuziki wengine ili kubadilishana ujuzi na uzoefu. Aliwahi kupiga muziki akiwa na safu ya wanamuziki nyota toka nchi za Kenya na Tanzania.

Album yake mpya ya Song and Dance iliyorekodiwa mwaka 2006 katika Studio za Virunga reocords, wakimshirikisha mwanamuziki Bopol na wangine wakali toka bendi yake ya Orchestra Virunga. Abum hiyo iliyokuwa na nyimbo nyingi ilizinduliwa rasmi walipokuwa kwenye ziara nchi za Ulaya mwezi March 2006.

Mwezi Juni 4 2006 Samba alikuwa nchini Kenya kawa ajili shughuli maalumu ya Ecofest, Wakati wa Kampeni ya Urais wa Marekani mwaka 2008, Samba Mapangala alionyesha ni jinsi gani wananchi wa Kenya wanavyomshabikia mgombea wa kiti hicho Barack Obama. Alifyatua wimbo maalumu wa kumtakia heri Obama ulioitwa 'Obama Ubarikiwe'

SambaMapangala na bendi yake ya Orchestra Virunga walirejea Afrika ya Mashariki mapema mwaka 2009, na kutoa burudani katika jiji la Nairobi na Zanzibar ambako alialikwa katika tamasha la Sauti za Busara .

Mwishioni mwa mwaka 2009 Samba aliuongezea nguvu mfuko wa World Wildlife Fund kwa kutunga na kutoa bure wimbo wa ‘ Mlima wa Magorila’ uliokuwa ukitoa wito kusaidia kuwalinda magorila waliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori ya Virunga ya nchini Kenya ambako wanyama hao adimu hupatikana.

Mangwana anakumbukwa na wapenzi wa muziki wa dansi katika nchi za Afrika ya mashariki na Kati pale wasikiapo nyimbo za Hadija, Marina Nyama Choma, Alimasi, Dunia haina mwisho na Dunia tunapita. Nyingine ni Jaffar, Mapenzi hayana macho, Muniache, Virunga, Vijana, Ufunguo, Vunja mifupa, Siri na Vidonge uliopigwa kwa staili ya mduwara. Nyimbo zote zimeimbwa kwa lugha ya Kiswahili.

Samba Mapangala na familia yake wanaishi katika jiji la Washington DC nchini Marekani. 

 Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200 na 0713331200

Wakuu wa Idara na Vitengo Wizara ya Habari Wapigwa Msasa Kuhusu Manunuzi na Ugavi

LAZARO NYALANDU MIKONONI MWA TAKUKURU , ASHIKILIWA KWA MAHOJIANO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blogu ya jamii

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamshikilia aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu kwa tuhuma za vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.

Nyalandu ambaye kwa sasa ni Kada wa Chadema amekamatwa leo saa tisa Alasiri mkoani Singida ambapo baada ya kukamatwa amechukuliwa na kwenda kuhojiwa na TAKUKURU.

Akizungumza na Michuzi Blog kwa njia ya simu jioni hii, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Mkoa wa Singida Joshua Msuya amesema Nyalandu wamemkamata leo kutokana na kufanya vitendo vinavyoashiria uwepo wa rushwa.

"Ni kweli tumemkamata Nyalandu kwa ajili ya kufanya naye mahojiano, kuna mikutano ya kisiasa ambayo wanaifanya na kuna viashiria vya vitendo vya rushwa.Hivyo tumemkamata kwa ajili ya kumhoji.Tunaomba ifahamike tunamhoji kwasababu ya kuwepo viashiria vya vitendo vya rushwa na si kwamba tumemkamata akitoa rushwa,"amesema Msuya.

Alipoulizwa kama bado wanamshikilia au laa ,Msuya amejibu wao baada ya kumhoji wamemkabidhi kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa mahojiano zaidi.

Taarifa za kwamba amevamiwa na watu wasiojulikana wakia na silaha, Joshua amejibu sio kweli kwani Nyalandu kabla ya kuchukuliwa kwa ajili ya kuhojiwa alipewa taarifa na hivyo alikuwa anajua kuwa anahitajika TAKUKURU.

MIFUKO YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI YA ZAMBIA NA TANZANIA YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

TANZANIA na Zambia kupitia Mifuko ya Fidia kwa Wafanyakazi, wamesaini mkataba wa ushirikiano utakaosaidia kubadilishana uzoefu kati ya mifuko hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutiliana saini mkataba huo, kwenye ofisi za WCF jijini Dodoma Jumatatu Mei 27, 2019, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba alisema, Zambia inauzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika sekta ya hifadhi ya jamii katika kulipa mafao ya Fidia kwa Wfanyakazi kwa hivyo makubaliano hayo yana manufaa makubwa.

Alisema makubaliano hayo ni ya kawaida kati ya mifuko na kwamba WCF na WCFCB watabadilishana uzoefu katika masuala ya namna ya ulipaji mafao, namna ya kuzuia ajali na magonjwa kazini kwa sababu mambo hayo ni muhimu sana katika mifuko ya fidia.

“Nguvu kazi ya taifa inapolindwa tija huongezeka makazini na jambo hili hudhihirika pale pato la taifa linaongezeka hususan kwetu sisi ambao tunajenga uchumi wa viwanda jambo hilo ni muhimu sana.”Alisema Bw. Mshomba.

Alisema kwa uzoefu ambao Zambia watakuwa wameupata kutoka kwao wataweza kuboresha huduma zao, na tayari Dkt. Nkumbula amethibitisha kuwa serikali ya Zambia inautegemea Mfuko huo katika kusaidia nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Zambia (WCFCB), Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula alisema, imekuwa ni siku njema kwao kwa kujenga ushirikiano wa pamoja katika eneo la hifadhi ya jamii.

“Zambai na Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. Keneth Kaunda na Mwalimu Nyerere, waliweza kujenga reli ya TAZARA na bomba la mafuta TAZAMA kwa hivyo ushirikiano huu wa leo ni kumbukumbu ya ushirikiano uliojengwa kwa muda mrefu na viongozi hao wa mataifa hayo mawili.” Alifafanua.

Alsema ushirikiano huu utasaidia pande mbili kubadilishana uzoefu katika kutoa huduma za ulipaji fidia na mbinu za kuzuia majanga yatokanayo na kazi na hivyo kusaidia mataifa hayo kukuza uchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (kulia) na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kutoka Zambia, (WCFCB) Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula, wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya ushirikiano baina ya mifuko hiyo, huku maafisa wa juu kutoka pande hizo mbili wakishuhudia katika hafla iliyofanyika ofisi za WCF Dodoma Jumatatu Mei 27, 2019.Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (waliokaa kulia) na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa Wfanyakazi kutoka Zambia, Dkt. Elizabeth Lunhgu Nkumbula, wakitia saini makubaliano ya ushirikiano baina ya mifuko hiyo, huku maafisa kutoka pande hizo mbili wakishuhudia katika hafla iliuofanyika ofisi za WCF Dodoma Jumatatu Mei 27, 2019.
Bw. Masha Mshomba akisaini
Dkt. Elizabeth Lunhgu Nkumbula, akiweka saini yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni mgeni wake, Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbulu.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kutoka Zambia, (WCFCB), Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula akizungumza katika hafla hiyo. 
Bw. Mshomba akimkabidhi zawadi ya picha mgeni wake, Dkt. Elizabeth Lungu Nkumbula.

RC TELACK AFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO YA UMISSETA 2019 SHINYANGA

$
0
0
 Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa kwa shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2019) yamefunguliwa rasmi mkoani Shinyanga, ambapo wanafunzi wataonyesha vipaji vyao kwa kushiriki katika michezo mbalimbali.


Mashindano ya (UMISSETA 2019) yamefunguliwa leo Mei 27,2019 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainabu Telack kwenye viwanja vya michezo vya CCM Kambarage Shinyanga Mjini na kuhudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari kutoka halmashauri sita za mkoa huo sambamba na kusindikizwa na wadogo zao wa shule za msingi. 

Michezo ambayo itashindaniwa ni mpira wa miguu, mpira wa pete, kikapu, wavu, riadha, mpira wa meza, kucheza ngoma, pamoja na kuimba kwaya, ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu, ambapo washindi watakwenda kushindana kitaifa. Akifungua mashindano hayo,Telack aliwataka wanafunzi hao kudumisha nidhamu kwenye mashindano hayo hata wale ambao watachaguliwa kwenda Mtwara kushiriki kitaifa wakaonyeshe nidhamu ya hali ya juu. 

Alisema michezo ni afya, humjenga mtoto kiakili,kinidhamu, kuibua vipaji na hivyo kusikitishwa na shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao kushiriki kwenye michezo hiyo na kuwataka waiche tabia hiyo mara moja, ikiwa huko ni kumnyima mtoto kuonyesha kipaji chake na kuweza kupata ajira hapo baadae. 

“Kuna taarifa tunazo eti baadhi ya shule binafsi zimezuia wanafunzi wao kutoshiriki michezo hii ya UMISSETA, ni jambo la ajabu sana, mfano baba yake na Mbwana Samatta angekuwa wakimzuai mtoto wake kushiriki kwenye michezo leo asingekuwa mchezaji wa kimataifa, hebu waruhusuni watoto wenu waonyeshe vipaji vyao kwani michezo ni ajira pia,”aLIsema Telack. 

“Na niye wanafunzi ambao mnashiriki michezo hii ya UMMISSETA naombeni muonyeshe vipaji vyenu ambavyo mmepewa na Mungu, pamoja na kudumisha nidhamu ya hali ya juu hata huko mtakapokwenda Mtwara na siyo kwenda kuendekeza mapenzi, nataka muje na makombe hapa ya ushindi likiwEmo la nidhamu,”aliongeza. Pia aliziagiza halmshauri zote za mkoani humo kutenga bajeti ya kila mwaka wa fedha shilingi Milioni 2 kwa ajili ya kufanikisha michezo hiyo ya UMISSETA licha ya kupata fedha zingine kutoka wahisani ili kuwa rahisishia maisha wanafunzi wakaokuwa kambini. 

Kwa upande wake Afisa Elimu mkoa Shinyanga Mohamed Kahundi akisoma risala ya ufunguzi wa michezo hiyo ya UMMISSETA, alisema changamo ambayo wanakabiliana nayo kuendesha mashindano hayo hadi ngazi ya taifa ni ukata wa fedha na hivyo kuomba wahisani waendelee kujitokeza kufadhili michezo hiyo. Alisema kwa mwaka jana (2018) mkoa ulifanikiwa kupeleka timu kwenye mashindano ya kitaifa, lakini haukufanya vizuri kwani ulishika nafasi ya 20 kati ya 28 sababu ya maandalizi kuwa mabaya kutokana na upungufu wa rasilimali fedha ambapo hata baadhi ya timu zilishindwa kuzipeleka kushiriki kwenye mashindano hayo. Kauli mbiu ya (UMISSETA) mwaka huu inasema "michezo na sanaa kwa elimu bora na ajira".
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akizungumza kwenye ufunguzi wa michezo ya UMISSETA kwa shule za Sekondari mkoani Shinyangana kuwataka wanafunzi waitumie michezo hiyo kuonyesha vipaji vyao, ikiwa michezo ni afya pamoja na ajira na kukemea shule binafsi ambazo zimezuia wanafunzi wao wasishiriki michezo hiyo.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Afisa Elimu mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi akisoma risala kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya UMISSETA na kumuomba mgeni rasmi mkuu wa mkoa kuwatafutia wafadhili ambao watakuwa wakifadhili michezo hiyo kila mwaka pamoja na halmashauri kutenga fedha za mapato ya ndani, ili kuondoa changamoto ya ukata wa Fedha na kusababisha kufanya vibaya kwenye mashindo ya kitaifa kama ilivyotokea mwaka jana. Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkaribisha mkuu wa mkoa huo wa Shinyanga Zainab Telack kufungua michezo hiyo ya UMISSETA kwa shule za sekondari ambayo itadumu kwa muda wa siku tatu. Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa mashindano ya michezo ya UMISSETA Mwaka (2019) mkoani Shinyanga yaliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kambarage. Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga. Wanafunzi wakiwa kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga. Awali wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga. Wanafunzi wakiingia kwa maandamano kwenye ufunguzi huo wa michezo ya UMMISETA. Wanafunzi wakionyesha jumbe za mabango kwenye ufunguzi wa michezo ya (UMISSETA) Mkoani Shinyanga. Awali mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufungua michezo hiyo ya shule za sekondari UMISSETA. Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack katikati akiwasili kwenye uwanja wa CCM Kambarage Shinyanga Mjini kwa ajili ya kufungua michezo hiyo ya UMISSETA. Wanafunzi wakiimba nyimbo ya taifa kwa ajili ya kuwa tayari kufungua michezo hiyo ya shule za Sekondari (UMISSETA) Mkoani Shinyanga. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images