Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MAONYESHO YA MADINI KATIKA VIWANJA VYA BUNGE JIJINI DODOMA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019 
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo,akizungumza kwenye maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019 
Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini,Prof. Shukran Manya,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM), Ndg. Simon Shayo wakati alipotembelea banda ilo katika maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo, Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya K TanzGraphite, Ndg. Sauda Simba akimuonyesha na kumuelezea umuhimu wa madini ya graphite (kinywe) alisema utumika kutengenezea betri za simu, kompyuta mpakato ‘lap top’ na penseli wakati alipotembelea banda hilo katika maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Yohana Msanjila na Meneja Maendeleo ya Jamii kutoka Kampuni ya K TanzGraphite, Ndg, Bernard Mihayo 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Utafiti ya madini ya Urani (MANTRA Tanzania), Ndg. Khadija Pallangyo akimuelezea kuhusu shughuli mbali mbali zilizofanywa na kampuni hiyo ikiwemo utengenezaji wa maktaba na uchimbaji wa visima wakati wa maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. 
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Uhusiano wa kampuni ya Shanta Gold Mine, Ndg. Christabella Hakili baada ya kufungua maonyesho ya Madini yaliyoanza leo katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Yohana Msanjila, Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 26 Mei, 2019 nakutegemea kumalizika kesho tarehe 27 Mei, 2019, 
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA KUAPISHWA KWA RAIS WA COMORO

$
0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais Azali wa Comoro na viongozi wa Serikali ya Commoro baada ya kuapishwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumpongeza Rais Azali Assouman wa Comoro baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Visiwa vya Comoro leo May 26,20219 katika wa Uwanja Mpya wa Ominisport Malouzini Stadium Comoro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Spika wa Bunge la Comoro Mhe. Ousseini Abdou kwenye uwanja Mpya wa Comoro wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Azali Assouman leo May 26,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mke wa Rais wa moro Bibi Ambari Azali kwenye uwanja Mpya wa Ominisport Malouzini Stadium Comoro wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Azali Assouman leo May 26,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Comoro Mhe. Souef Mohammed Al Amine kwenye Uwanja wa Mpya wa wa Ominisport Malouzini Stadium Comoro wakati wa sherehe ya kuapishwa Rais Azali Assouman leo May 6,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Azali Assouman wa Comoro baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Visiwa vya Comoro leo May 26,20219.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA IKULU YA PRETORIA NCHINI AFRIKA KUSINI SIKU MOJA MARA BAADA YA KUAPISHWA NA KABLA YA KUTEUA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi ya picha ya wanyama Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa baada ya kuwasili katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili na Kingereza pamoja na Vitabu vya Kiswahili Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa kwa ajili ya kujifunza lugha hio ya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa akisikiliza maelezo yaliokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi kuhusu vitabu hivyo vya Kiswahili leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wakati akizungumza na wanahabari Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa wakifurahia jambo katika mazungumzo yao Pretoria nchini Afrika Kusini leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa mara baada ya kumaliza mazungumzo yao leo Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri. PICHA NA IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26 Mei, 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa, Ikulu Jijini Pretoria. 

Katika Mazungumzo hayo, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Rais Ramaphosa kwa kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amemhakikishia kuwa Tanzania itadumisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria na nchi hiyo ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Nelson Mandela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ANC (African National Congress). 

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru, Mhe. Rais Ramaphosa kwa kumkaribisha kufanya nae mazungumzo siku moja baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Afrika Kusini na amebainisha kuwa anatarajia uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini utaimarishwa zaidi katika masuala ya uchumi na kukuza lugha ya Kiswahili. 

Kwa upande wake, Mhe. Rais Ramaphosa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwake, na amemhakikishia kuwa Afrika Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika ukombozi wa Taifa hilo na kwamba katika kipindi chake cha uongozi wake atauendeleza na kuuza zaidi uhusiano huo. 

Mhe. Rais Ramaphosa amesema kufuatia uamuzi wa Afrika Kusini kuanza kufundisha lugha ya Kiswahili, nchi yake itachukua walimu wa Kiswahili kutoka Tanzania ili watumike kufundisha somo hilo katika shule za msingi na sekondari. 

Aidha, Mhe. Rais Ramaphosa ameahidi kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Tanzania kabla ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliopangwa kufanyika mwezi Agosti 2019 nchini Tanzania. Na pia atahudhuria mkutano huo. 

Kabla ya mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amemkabidhi Mhe. Rais Ramaphosa zawadi ya vitabu vya kusoma na kufundishia lugha ya Kiswahili kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). 

Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Rais Ramaphosa wamefanya mazungumzo hayo ikiwa ni kabla Mhe. Rais Ramaphosa hajatangaza Baraza lake la Mawaziri. 

Mhe. Rais Magufuli kesho ataondoka nchini Afrika Kusini na kuelekea nchini Namibia ambako atafanya Ziara Rasmi ya Kitaifa kwa mwaliko wa Rais wa Namibia Mhe. Hage Geingob. 

Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Pretoria 
26 Mei, 2019

CHANGAMKIA OFA MAALUMU KABLA HAIJAISHA,WAKATI NI SASA.

WAZIRI MKUCHIKA AZINDUA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF.

$
0
0
NA ESTOM SANGA-DSM 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteini Mstaafu George Huruma Mkuchika (MB) amezindua Kamati yaTaifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF na kuagiza kamati hiyo kuendelea kutilia mkazo suala la utendaji kazi kwa kuzingatia misingi ya uadilifu na uwajibikaji. 

Akizindua Kamati hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya TASAF jijini Dar es Salaam, Mhe. Mkuchika amesema Mfuko huo umetekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kujenga jina zuri na hivyo ameagiza sifa hiyo iendelezwe kwa maslahi ya taifa. 

Amesema majukumu ambayo TASAF imekabidhiwa yanagusa kwa kiwango kikubwa maisha ya wananchi ambao wanakabiliwa na umaskini na hivyo kutaka Kamati hiyo mpya ya Uongozi ya TASAF kushirikiana na watumishi wa Mfuko huo kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla. 

“mnalo jukumu kubwa mlilokabidhiwa na taifa la kusaidia serikali kupambana na adha ya umaskini na kuboresha maisha ya wananchi,jukumu ambalo ni lazima litekelezwe kwa nguvu na ufanisi zaidi” amesisitiza Mhe. Mkuchika. 

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Uongozi iliyomaliza muda wake Dr. Florens Turuka akizungumza kwenye hafla hiyo amepongeza hatua ya serikali ya kuendelea kuuamini Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF kama njia mojawapo ya kuhamasisha wananchi kupambana na umaskini,na kuwapongeza Watumishi wa Mfuko huo kwa kufanyakazi kwa kujituma kwa manufaa ya taifa . 

Naye Mwenyekiti Mpya wa Kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF ,Dr. Moses Kusiluka amesema msingi imara uliowekwa na kamati iliyomaliza muda wake utaendelezwa kwa nguvu zaidi ili kukidhi matakwa ya serikali na wananchi wanaotegemea huduma za Mfuko huo unaogusa maisha ya wananchi wengi. 

Dr. Kusiluka pia ametumia fursa hiyo kuagiza uongozi wa TASAF na watumishi wake kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili mfuko huo unaohudumia wananchi wanaokabiliwa na kero ya umaskini waendelee kunufaika na huduma za Serikali kupitia Mfuko huo. 

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF ,bw Ladislaus Mwamanga , ameelezea mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2000 hususani katika sekta za elimu, afya, maji, miundobinu , kilimo,mifugo, uchumi na mapambano dhidi ya umaskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao amesema umefanikiwa kuhudumia zaidi ya kaya milioni Moja na Laki Moja katika awamu yake ya kwanza ya utekelezaji kwa aslimia 70 ya mitaa/vijiji na shehia nchini kote.

 Waziri Mkuchika akimkabidhi zawadi ya saa yenye picha za wajumbe wa kamati ya uongozi ya TASAF iliyomaliza muda wake Dr. Florens Turuka,wa kwanza kulia ni mwenyekiti mpya Dr. Moses Kusiluka na kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw.Ladislaus Mwamanga. 

 Waziri Mkuchika akizindua Kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Mfuko huo jijini Dar es salaam, kulia kwake ni mwenyekiti mpya wa Kamati Dr. Moses Kusiluka akifuatiwa na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Dr. Florens Turuka . Kushoto kwa Mhe. Mkuchika ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga.

 Waziri Mkuchika (aliyeketi katikati)  katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati mpya ya uongozi ya TASAF na menejimenti ya Mfuko huob aada ya kuizindua Kulia kwake ni mwenyekiti mpya wa kamati hiyo Dr. Moses Kusiluka na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 

 Waziri Mkuchika (aliketi katikati ) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya TASAF waliomaliza muda wao baada ya kuzindua rasmi kamati Mpya kwenye Ofisi ndogo ya TASAF jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya menejimenti ya TASAF wakimsikiliza Waziri Mkuchika wakati wa uzindizi wa Kamati ya Taifa mpya kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Mfuko huo  jijini Dar es Salaam.


 Waziri Mkuchika (wa pili kushoto) akizungumza na Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uongozi ya TASAF,  Dr. Moses Kusiluka (kulia )na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake  Dr. Florens Turuka) wa kwanza kulia ,na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto ) baada ya kuzindua  kamati ya taifa ya uongozi ya TASAF jijini Dar es Salaam.

MKURUGENZI ILEJE ASHIRIKI UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA KWA VITENDO.

$
0
0
 Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine
 Mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje akiwa sambamba na mafundi wengine

NA FREDY MGUNDA,ILEJE

MKURUGENZI wa wilaya ya Ileje Haji Mnasi ameshiriki ujenzi na upanuzi wa hospitali ya wilaya ya ileje baada ya kupokea kisai cha shilingi bilioni 1.5 kutoka serikalini ili kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwenye ubora unaotakiwa na wananchi wanapata huduma bora za kiafya.

Akizungumza wakati wa ujenzi huo Mnasi alisema kuwa lengo la kushiriki ujenzi huo ni kuhakikisha anaweka hamasa kwa mafundi na wananchi kusimamia vilivyo kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa na serikali kuu.

“Mimi kama kiongozi lazima niwe mfano wa kuigwa kwa kufanya kazi kwa vitendo hivyo kuja kwangu kushiriki ujenzi huu ni kuonyesha jinsi gani tunatakiwa kufanya kazi tuliyoagizwa na Rais wetu” alisema Mnasi

Mnasi  alisema kuwa atahakikisha bega kwa bega katika usimamizi na ushiriki wa karibu kuhakikisha ujenzi unakamilika  na thamani ya fedha(value for money) kwa wakati ili kutimiza malengo ya serikali yanayokusudiwa.

“Nikija mara kwa mara kuangalia ujenzi huu nitahakikisha ujenzi ulio bora wa kuzingatia ujenzi unaofaata hatua zote za msingi na kupata majengo yaliyobora ya hospitali hii ya wilaya” alisema Mnasi

Lakini pia mkurugenzi Haji Mnasi aliishukuru na kuipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuwajali wananchi kwa kutoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya wilaya.

Vodacom join hands with Amana bank to launch an Islamic mobile saving product- Halal Pesa

$
0
0
 Vodacom Tanzania Director of M-Commerce, Epimack Mbeteni (L) and Amana Bank Managing Director, Dr. Muhsin Masoud launching Halal Pesa, a new and innovative M-Pesa mobile service that adheres to Islamic laws on earning profits in Dar es Salaam, over the weekend. The product is the first-to-market innovative product that ensures all citizens have access to formal micro-savings and investment solutions which adheres to Islamic laws.
Vodacom Tanzania Director of M-Commerce, Epimack Mbeteni (C) and Amana Bank Managing Director, Dr. Muhsin Masoud (2nd R) launching Halal Pesa, a new and innovative M-Pesa mobile service that adheres to Islamic laws on earning profits in Dar es Salaam, over the weekend. \

 Vodacom Tanzania in partnership with Amana Bank has launched a new M-Pesa mobile service dubbed “Halal Pesa”.  ‘Halal’, which means ‘lawful’ is a fitting statement to this first-to- market innovative saving product that ensures all citizens and Muslims have access to a formal micro-savings and investment solution which adheres to Islamic laws on earning halal profits. The launch ceremony took place at Serena hotel, Dar es Salaam and was attended by Muslims and other Telco’s customers.

The launch of Halal Pesa plays a key role in Vodacom’s strategy to become a key contributor in the rapidly growing Islamic Finance sector, as the product targets to service more than three quarter of the total Muslim population in the country through M-Pesa, where they will be able to save money and gain profit with incurring interest.

Speaking during the launch ceremony, Vodacom Head of M-Pesa department, Tulisindo Rashid said “Our decision to launch Halal-Pesa is a direct response to feedback from our customers that they want their digital financial services needs met within Shariah principles. For a long time, the Muslim population has been in need of a mobile financial saving system which is tied to the pillars of Islamic faith, and hence this is a solution that will allow Muslim customers to achieve their financial goals while cementing their faith by abiding to sharia laws”.

Vodacom continues to create innovative financial solutions for all by using digital technology at an affordable cost.  “Halal Pesa is a user friendly and distinct service that is in line with Islamic principles. The service has diverse choices including saving money for Hajj, children or long-term savings ranging from 3 to 12 months. Also, customers can use halal-Pesa to offer their contributions to the Mosque and Zakat”, added Tulisindo.  

Speaking during an interview with the media, Vodacom’s customer Hajjat Hawa Hilal said; “This service comes at the right time as we are in the holy month of Ramadhan. I have been using M-Pesa for quite a long time, but these new services have motivated me to save money for Hajj, Zakat and other plans in harmony with our Islamic sharia”, 

The Managing Director of Amana Bank, Dr Muhsin Masoud, said that their partnership with Vodacom is expected to have a positive impact on Tanzania’s Islamic banking sector. “As an Islamic Bank, we have ventured into enabling believers in Islamic faith to deposit savings through formal means. It is our joy to collaborate with Vodacom because, now, we are bringing our bank services closer to our customer’s through Halal-Pesa on mobile money” added Dr Muhsin. 

These efforts are in hand with the government’s National Financial Inclusion Framework strategy (2018-2022) that focuses on enabling citizens to have access to formal financial services. “We are supporting the government by innovating and developing services that suit the needs of the population. Halal-Pesa is for all M-Pesa users - Muslims and non-Muslims - who would like to save their money while adhering to Islamic sharia, and we remain firm in our commitment - to be the right partner to our customers in fulfilling their evolving demands; and to the Government’s agenda in increasing accessibility to financial services”, Tulisindo concluded.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 27,2019


RC NJOMBE AKAGUA MAENDELEO YA STENDI MPYA NA UJENZI WA SOKO

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akisoma jina la nchi inayozalisha vitasa vilivyotumika kwenye milango ya jengo la utawala 
Mmoja wa Wajasiriamali anayefanya shughuli zake katika eneo la stendi kuu mpya Njombe akionesha kitambulisho cha Wajasiriamali kilichotolewa na Mhe. Rais kwa Wajasiriamali wadogo 
Mkuu wa Mkoa Njombe akionesha utaalamu wake kwenye kusonga ugali wakati alipotembelea mabanda ya muda ya mama lishe katika eneo la stendi kuu mpya 
Mkuu wa Mkoa Njombe akiangalia zege iliyomiminwa katika meza za kuuzia mbogamboga kwenye eneo la ujenzi wa soko kuula kisasa Njombe 
Ujenzi wa Soko la Kisasa ukiendelea katika Mtaa wa Gwivaha Halmashauri ya Mji Njombe ujenzi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya Tsh. Bilioni tisa mpaka kukamilika kwake. 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe akikagua kitabu cha kukata risiti kwa abiria kwenye mojawapo ya basi ikiwa ni sehemu ya ziara yake alipotembelea stendi kuu mpya ya mabasi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi . Ruth Msafiri 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe akikata nyama za kuchoma 

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga (kushoto), Wahandisi (kulia),Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama na Wataalamu mbalimbali wakati wa ziara yake katika stendi kuu mpya 
Mhandisi Mkazi wa ujenzi wa stendi Didasi Joseph akionesha shughuli za ujenzi zinazoendelea katika eneo la maegesho ya mabasi madogo kwenye stendi kuu mpya Njombe 
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka akiwa ameshikilia kipande cha marumaru ili kujirithisha ubora wa marumaru hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri
…………………….. 

Hyasinta Kissiama-Afisa Habari H/Mji Njombe 

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka amefanya ziara na kukagua shughuli za umaliziaji wa ujenzi stendi kuu mpya iliyoanza kazi rasmi 11 Mei 2019 na kukagua shughuli za ujenzi wa mradi wa soko kuu la kisasa na kuridhishwa na kasi na viwango vya ujenzi wa soko hilo. 

Ziara hiyo iliyolenga kutambua na kupatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili wananchi mara baada ya kuanza rasmi kwa stendi kuu mpya, na kuangalia thamani ya pesa iliyotumika katika hatua zinazoendelea za ujenzi wa soko kuu Njombe, ilijumuisha wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe. 

Akizungumza na Wasafiri, Wajasiriamali wadogo, Mama Ntilie na Wadau mbalimbali wa usafirishaji na Wananchi kwa ujumla waliokuwepo katika eneo hilo la stendi, ambao wengi walipongeza jitihada za Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuonekana kufurahishwa kuhamia katika stendi hiyo mpya, Sendeka amewataka Wananchi hao kuendelea kuiunga mkono na kuipongeza Serikali ya Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambayo imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa miradi mikubwa na yenye tija kwa wananchi wa hali ya chini na wanyonge. 

Mmoja wa Wajasiriamali wa bidhaa za vinywaji Mjini hapo John Msemwa alisema kuwa kero yake kubwa ni kuzuiwa kwa wao kuingia katika stendi hiyo kufanya biashara licha ya kuwa na kitambulisho cha Mhe. Rais jambo ambalo halikuwepo katika stendi ya zamani na linawakosesha wao kupata riziki. 

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo Sendeka amewataka Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo stendi ipo katika hatua za mwisho za umaliziaji na kwamba utaratibu rasmi utaandaliwa kwa ajili ya matumizi ya stendi hiyo. 

“Tupo katika hatua za mwisho za umaliziaji wa stendi. Ninachotaka niwahakikishieni ni kwamba Vitambulisho vya Mhe. Rais vitaheshimiwa kama ambavyo mwenyewe ameelekeza.Tutakaa na Halmashauri, Mkuu wa Wilaya na baadaye tutakaa na ninyi ili kuweka utaratibu ambao utakuwa, rafiki, shirikishi na wa uwazi kwa Wafanyabiashara, Wajasiriamali, Wadau wa usafirishaji na watumiaji wote wa stendi. Tukumbuke pia hatuwezi kuingiza Mji Mzima stendi kufanya shughuli zao. Alisema Sendeka. 

Akitoa ufafanuzi kuhusu taratibu za upatikanaji wa vibanda kwa ajili ya shughuli za biashara katika stendi kuu mpya, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Thadei Luoga amemuhakikishai Mkuu wa Mkoa na kumtoa hofu kuwa Halmashauri ilifuata na inaendelea kufuata taratibu zote za manunuzi katika ukodishaji wa rasilimali za stendi mpya na mchakato wa manunuzi unaendelea kulingana na sheria kanuni na taratibu na kumthibitishia kupeleka nyaraka zote za masuala ya manunuzi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kama alivyoagiza kwa ajili ya kwenda kuzipitia na kujiridhisha na vyombo vya usalama kama taratibu zote za manunuzi zimefuatwa ipasavyo. 

Katika hatu nyingine Ole Sendeka ameipongeza Halmashauri na Mkandarasi Nandra Construction kwa kazi nzuri yenye kasi na ubora ya ujenzi wa soko la kisasa Njombe na amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha kuwa anamaliza kazi hiyo kufikia Octoba 2019 kwa mujibu wa muda wa nyongeza waliiomba na amesema kuwa kwa kasi na shughuli zilizosalia ana imani kubwa muda uliobaki unatosha kumaliza shughuli zilizobaki na soko kuanza kazi mara moja. 

Halmashauri ya Mji Njombe inatekeleza mradi wa Ujenzi wa stendi ya kisasa ambayo imeanza kutumika na mradi wa ujenzi wa soko la kisasa kupitia programu ya uboreshaji na uimarisha Miji ULGSP ambapo kila mradi unatarajiwa kugharimu zaidi ya Bilioni 9 mpaka kukamilika kwake.

launching of bancassurance regulations

$
0
0
Financial Stability and Financial Deepening (FSD) Deputy Governor, Dr. Yamungu Kayandabila, (M) handing over a certificate of appreciation to Stanbic Bank Tanzania’s Head of Bancassurance and Home Loans, Moureen Majaliwa at the launch event of Bancassurance regulations in Dar Es Salaam recently. The Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) and Bank of Tanzania (BoT) has launched Bancassurance regulations to widen the scope of insurance services in Tanzania. On the right is BOT Deputy Governor Dr. Bernard Kibesse, while on the left is Mr. Michale Nyagoga - Assistant Commissioner of policy from Ministry of Finance and Planning and the Commissioner for Insurance Dr. Baghayo A. Saqware (2nd Left).

BIASHARA KIDIGITALI KUKUA KWA WAJASIRIAMALI

$
0
0

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo, akifungua mafunzo ya ujasiriamali yaliyofanyika Chuo hapo Mei 25, 2019. Mafunzo hayo yalitolewa na wanafunzi wanaosomea chuoni hapo kwa wajasiriamali wadogo.

Mratibu wa mafunzo ya wajasiriamali, Yusuph Zuberi.

Dk. Godbertha Kinyondo (kulia), akifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa kwa wajasiriamali wadogo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Washiriki.

Zuberi Kopwe akitoa mada kuhusu Masoko na Mkakati wa Kimasoko.
Raphia Kimaro, akitoa mada kuhusu Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo, Huduma kwa Wateja na Utunzaji Kumbukumbu.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Wajasiriamali Malkia Wajane, Sophia Samfundo, akielezea namna alivyonufaika na mafunzo hayo hasa suala la kufanya biashara mtandaoni.

Mfanyabiashara wa bidhaa za ngozi akizungumzia changamoto anazokutananazo katika biashara yake.

Mjasiriamali akiuliza swali.

Mjasiriamali akiuliza swali.

Brenda akijibu maswali ya baadhi ya wajasiriamali.

Ben Shine, akitoa mada kuhusu Masoko Kidigitali 'Digital Marketing'.

Hozza Mbura akitoa mada kuhusu Fursa.

Washiriki.

Hozza Mbura akijibu maswali.

Baadhi ya washirikia wakifuatilia mafunzo hayo.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Nela Alam, akifunga mafunzo hayo.

Washiriki wa mafunzo ya ujasriamali wakiwa katika picha ya kumbukumbu na wakufunzi wao.
Picha ya kumbukumbu ya washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali.

Picha ya kumbukumbu ya wakufunzi wa mafunzo hayo.



Na John Marwa


WAJASIRIAMALI wadogo nchini wameaswa kutobaki nyuma katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kukuza biashara zao na kuongeza faida.

Hayo yalibainishwa na watafiti wa Sayansi ya Jamii na Masoko kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, katika Semina ya Mafunzo ya Masoko kwa wajasiriamali wadogo iliyofanyika jijini Dar es Salam mwishoni mwa wiki.

Semina hiyo ilibeba dhima ya kuwajengea uwezo na kukuza uelewa wa wajasiriamali wadogo katika kulifikia soko na kupata faida.

Miongoni mwa mada zilizotolewa na Wandaaji wa Semina hiyo ambao ni wanafunzi wa chuo hicho ni matumizi ya mitandao katika kuwafikia wateja, Digital Marketing,

Akizungumza katika Semina hiyo mtoa mada wa Masoko Kidigitali Ben Shine aliwaomba wajasiriamali wadogo kuchangamkia fursa ya kidigitali ili kukuza biashara zao na kuweza kuwafikia wateja ili kutengeneza faida.

"Katika kukuza biashara zetu ama huduma kama wajasiriamali wadogo hatupaswi kubaki nyuma katika Masoko Kigitali (Digital Marketing) ili kuwafikia wateja.


"Sababu kubwa ya kutumia Masoko Kidigitali ni kutangaza bidhaa au huduma ili watu waweze kuzifahamu, kutoa taarifa juu ya biashara na huduma zako katika jamii,, alisema Ben na kuongeza kuwa.

"Jambo lingine baada ya kutangaza biashara zetu na kupata wateja ni kuweza kuziuza ili kutengeneza faida.


Bena alisema kuna mitandao ya kijamii mingi hapa nchini hivyo kila mjasiriamali anapaswa kujiunga huko ili kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi katika kukuza Biashara.


Kwa mfano kupitia Barua pepe, Blog, Kurasa za Kijamii, Facebook, Instagram, WhatsApp pamoja na Twitter ni moja ya mitandao ya kijamii inayotumiwa na watu wengi zaidi hivyo kuwa njia rahisi ya kuwafikia wateja na kutengeneza wapya.

Mada nyingine iliyofundishwa katika Semina hiyo ni Masoko au Soko ikiwa ni shughuli yoyote anayoifanya mfanyabiashara ili kukizi mahitaji ya mteja na kupata faida.


Akidadavua mada hiyo mtoa mada Zuberi Kopwe alisema katika soko Mfanya Biashara ama Mjasiriamali ni kutambua uhitaji wa mteja ili kutengeneza faida.


,,Ili kulifikia soko inatupasa kutekeleza malengo ya biashara au huduma husika kisha kufanya tathimini ya kila jambo lililoko mbele ya biashara ama huduma yako.


"Utaratibu wa kumfikia mteja kwanza ni kufanya tafiti ili kumfahamu mteja, pili mteja anataka nini, pia kuuliza kujua mahitaji ya mteja" alisema.


Kopwe aliongeza kuwa katika Biashara kuna Bidhaa au Huduma, bei ya kuuzia, njia bora ya kuwasiliana, mwonekana wa Mazingira, watu au wafanya kazi wenye kuvutia wateja na mwisho vyote humjengea mteja Imani ya Bidhaa zinazozalishwa au huduma.


Katika hatua nyingine wajasiriamali walipata nafasi ya kujifunza jinsi gani ya kukua katika biashara mada iliyotolewa na Raphia Kimaro.


Kimaro aliwataka wajasiriamali kufahamu sifa na tabia ya kuwa mjasiriamali. Moja ni kutafuta mwanya au nafasi ya kufanyia biashara.

"Miongoni mwa sifa na tabia za mjasiriamali ni kujiamini, utashi wa kutambua ubora wa bidhaa au huduma, uthubutu wa kufanya mambo, ushawishi kwa wateja, malengo yenye kutafsiri muelekeo wa biashara".


Zingine ni uwezo wa kusimamia biashara, kutafuta taarifa au habari juu ya biashara au huduma ili kujifunza jambo jipya, lakini pia ubunifu ni sehemu pekee ambayo humuongezea mjasiriamali ubora wa bidhaa au huduma katika ushindani wa soko" alisema Kimaro na kuongeza kuwa.


"Mjasiriamali ni Mfugaji na sio Mwindaji kwa maana ya tabia, kwani mfugaji huweza kukuza mifungo vivyo hivyo mjasiriamali anapaswa kukuza biashara yake, lakini Mwindaji yeye hutumia kilichopo chote na sio mkuzaji.


Nao wajasiriamali waliohudhuria Semina hiyo walitoa kongore zao kwa wandaaji na kutoa rai ya kuendelea kupewa fursa ya kupata mafunzo juu mambo mbali mbali yanayoendana na sekta ya ujasiriamali.


"Kiukweli tuna kila sababu ya kuwashukuru hawa vijana wetu kwa kuweza kutujali hasa sisi wajasiriamali wadogo".



"Kuna mengi tumejifunza hasa suala la kufanya biashara mtandaoni ni jambo ambalo binafsi nimelifurahia sana na naimani kama tutalitumia vema basi tutaweza kupiga hatua" alisema Sophia Samfundo Mwenyekiti wa kikundi cha Wajasiriamali Malkia Wajane kutoka Pugu Kajungeni.


Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi Dk. Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Godbertha Kinyondo, alisema Wajasiriamali ndio nguzo ya uchumi hivyo wanapaswa kutambua nafasi yao katika kukua kwa uchumi wa nchi "Tanzania ya Viwanda ni nchi ya Wajasiriamali, tunaweza kufanya mambo makubwa tukiwa wabunifu, weledi wenye kujituma huku tukimtanguliza Mungu kwa kila jambo" alisema Kinyondo.

MOTO MIFUKO YA PLASTIKI WAKOLEA

$
0
0
Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Wakati Serikali ikiwataka Wananchi wote kusalimisha kwa hiari mifuko ya plastiki waliyonayo kabla ya Juni mosi mwaka huu, Ofisi ya Tarafa ya Mihambwe imesema hakutakuwa na mzaha kwa watakaopuuza kutii agizo hilo. 

Msimamo huo umetolewa na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu kwenye mkutano wa Kijiji cha Namunda kilichopo kata ya Kitama akiwataka kuonyesha ushirikiano kwa kusalimisha mifuko ya plastiki kwa hiari kabla ya msako haujaanza. 

Gavana Shilatu alisema kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na mifuko ya plasitiki iliyotapakaa kila kona na kuathiri sana makazi na maeneo ya viumbe hai . 

*”Onyesheni ushirikiano kutokomeza mifuko ya plasitiki. Mwenye akiba ya mifuko hiyo aisalimishe ofisi ya Kijiji au ofisi ya kata. Watendaji na viongozi hakikisheni agizo hilo la Serikali linatekelezwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.”* Alisema Gavana Shilatu. 

Gavana Shilatu alisema plasitiki zinaathari kubwa kwa maisha ya binadamu na viumbe hai vyote hivyo uamuzi wa Serikali unahitaji kuungwa mkono na kutekelezwa kwa wakati muafaka. 

Kwenye mkutano huo wa siku ya pili, Mwenyekiti wa Kijiji Cha Namunda (CUF) Suleiman Mkubulu aliwaomba radhi wanakijiji kutokana na uzembe uliojitokeza kwenye miradi ya maendeleo tangu achaguliwe kushika wadhifa huo 

“Nimekubali makosa na lawama dhidi yangu .Nataka tusameheane.” alisema Mkubulu huku baadhi ya Wanakijiji wakipokea ombi lake shingo upande na wengine wakitaka ajiuzulu nafasi yake.

WANANCHI WILAYANI MPIMBWE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUTIMIZA AHADI YA MAJI

$
0
0
Ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji Chamalendi ukiendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi.
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kashishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi akitoa shukrani zake kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa baada ya kukamilika Mradi wa Maji wa Kashishi na kuanza kunufaika na huduma ya majisafi na salama. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Monmar & Sons Building Civil Engineers (haonekani pichani) anayetekeleza Mradi wa Maji Chamalendi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiteta na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi Wolfgang Mizengo Pinda alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
………………..
Wakazi wa Kijiji cha Kijiji cha Kashishi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi wameishukuru Serikali kwa kutimiza ahadi ya kuwapatia huduma ya majisafi na salama haraka na kumaliza tatizo la miaka mingi na kusababisha wananchi hao kutumia muda mwingi kutafuta maji baada ya kufanya kazi za uzalishaji.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo mbele ya Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa alipokuwa kijijini hapo kuona utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwa wananchi hao mwishoni mwa mwaka jana, alipotembelea kijiji hicho na kukutana na malalamiko mengi kuhusu tatizo sugu la maji la muda mrefu.

Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa amewashukuru wananchi hao kwa uvumilivu wao na kuwataka wawe walinzi wa miundombinu na kuutunza vizuri mradi huo uweze kutoa huduma kwa muda mrefu. Akisisitiza Serikali kuendelea kuwekeza fedha zaidi kwenye miradi mingine ili huduma hiyo iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi katika Wilaya ya Mpimbwe, mkoani Katavi.

‘‘Ni wajibu wetu kama Wizara ya Maji kumaliza tatizo la maji kwa wananchi, tumepanga kufikia lengo hilo kwa kufuatilia utekelezaji ya miradi yote nchi nzima kwa ukaribu. Bila kutoa nafasi kwa mkandarasi yeyote kutukwamisha, niwaambie ukweli tutawachukulia hatua na hatutakuwa na mchezo katika jambo hili’’, Profesa Mbarawa ameonya.

Akizungumza mbele ya Waziri wa Maji, Bi. Elizabeth Jonathan amesema wanawake wa kijiji walikuwa ni waathirika wakubwa wa tatizo la maji kutokana na kutembea mwendo mrefu kutafuta maji siku nzima, huku wakiacha kufanya kazi nyingine na kuziacha familia zao. Akisisitiza mradi huo mkubwa umeleta faraja kubwa kijijini hapo.

Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kashishi ulianza mwezi Februari, 2018 na kukamilika mwezi Aprili, 2019 ukihusisha kazi za ujenzi wa tenki la ujazo wa lita 100,000, vituo 9 vya kuchotea maji, ulazaji wa mtandao wa mabomba wenye urefu wa mita 12,500 na nyinginezo.

Mradi huo unahudumia wananchi wapatao 5,230 umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 500 na kazi ya ujenzi imefanywa na Mkandarasi Dan General Construction Co. Ltd.

Waziri Mkuu Aifagilia NMB kwa kutoa Huduma Bora Tanzania

$
0
0
Mkurugenzi wa NMB Bank – Albert Jonkergouw akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Kassim Majaliwa kwenye futari maalumu iliyoandaliwa na NMB jijini Dodoma kwaajili ya wateja na wadau mbalimbali.Pembeni ni Spika wa Bunge – Job Ndugai
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Kassim Majaliwa akihutubia wageni mbalimbali waliohudhuria Futari iliyoandaliwa na NMB.

Picha ya pamoja.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaja benki ya NMB kuwa ni taasisi inayopaswa kuigwa kwa ubora wa huduma akisifia namna walivyoweka mizizi katika maeneo ya vijijini ambako wengi hawajafika.

Majaliwa alitoa kauli hiyo juzi katika hoteli ya New Dodoma wakati benki ya NMB ilipowakutanisha wadau kutoka mkoani hapa kwenye futari maalum kwaajili ya Mwezi Mtukufu.

Waziri Mkuu alisema benki hiyo inaisaidia serikali katika juhudi za maendeleo hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linaelekea katika uchumi wa kati hivyo anaomba Watanzania kwa Umoja wao kudumisha, amani, upendo na mshikamano ili kufikia malengo.

Alisema serikali ambayo ina hisa ndani ya benki hiyo, itaendelea kushirikiana nao pale wanapoona inafaa kufanya hivyo lakini akawataka waendelee kuboresha zaidi huduma zao katika maeneo ambayo hawajafika.

“Siyo dhambi nikisema mnaongoza kwa kutoa huduma bora, nawashukuru kwa kujikita katika taasisi kama mashule ambako mmesaidia kupeleka madawati na vitabu, lakini nafurahi kusikia mmeanza kufadhili hadi kwenye michezo, nawapeni hongera, tutaendelea kuwatia moyo na popote mlipo,” alisema Majaliwa.

Katika ukaribisho wake, Mkurugenzi wa benki ya NMB Albert Jonkergouw alisema benki hiyo inajishusha kwa kuwakumbuka waumini katika kipindi hiki ambacho wanahitaji kuwa karibu na muumba wao hivyo wanaungana katika tendo hilo jema.

Jonkergouw alisema wataendelea kufanya hivyo na kufuata taratibu za huduma za fedha nyingi ikiwemo kuwasogezea zaidi huduma watu ambao wamekuwa wakizitafuta kwa gharama lakini akasema katika futari watahitimisha Mei 31 mkoani Tabora lakini kila mkoa wanatumia nafasi hiyo kuwaalika na wawakilishi kutoka maeneo ya jirani.

WAZIRI MKUU AWAONYA WAMILIKI WA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa makao ya watoto wasiofuata taratibu za usajili wa watoto, wanaowatumia watoto kama mitaji au kwa maslahi binafsi na wanaoendesha makao hayo kwa minajili ya kidini na kikabila.

Amewataka pia wamiliki hao waache mara moja kuwalea watoto hao katika maadili yasiyofaa na yasiyo ya Kitanzania na kwamba maofisa ustawi wa jamii wahusike moja kwa moja katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha kuwa ni watoto wanaostahili tu kuwekwa kwenye makao ndiyo wanasajiliwa.

Alikuwa akizungumza jana usiku (Jumapili, Mei 26, 2019) kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam alikokuwa mgeni wa heshima wakati wa futari yapamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea watoto yatima vya jijini humo.

“Nitoe rai kwamba watu mmoja mmoja, taasisi na makao wazingatie baadhi ya taratibu za msingi za uendeshaji wa makao kama vile mtoto kukuzwa katika mazingira ya familia, kuzingatia misingi ya kitaifa badala ya misingi ya tamaduni za kigeni.

“Mtoto kukuzwa kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto; kuzingatia umuhimu wa kuwa na mwendelezo katika dini ya mtoto na utamuduni wake; kutotenganisha watoto na ndugu na kuhakikisha watoto wote wanapata huduma stahiki, kulindwa dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji; na kutunzwa na  kuendelezwa hadi kufikia kimo cha utimilifu wao,” alisema.

Waziri Mkuu alitumia hadhara hiyo pia kutoa maelekezo mahsusi kwa waendeshaji wa makao pamoja na wasimamizi wa sheria na taratibu za uendeshaji wa makao ya watoto yatima.

“Afisa Ustawi wa Jamii katika eneo yanakoanzishwa makao, ahusike moja kwa moja katika usajili wa mtoto ili kuhakikisha kuwa ni watoto wanaostahili tu kuwekwa kwenye makao ndio wanasajiliwa.

“Taasisi na makao zihakikishe kuwa kila mtoto anawekewa mpango maalumu wa kuondoka kwenye makao na namna ya kumuunganisha mtoto huyo na familia yake.

“Wamiliki wa taasisi na makao, waruhusuni maafisa ustawi wa jamii na maafisa wengine wa Serikali wafanye ukaguzi kwa mujibu wa sheria na wekeni utaratibu wa kuandaa taarifa za kila mwezi za watoto na taarifa ya mwaka wa fedha,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia alionya dhidi ya wale “wanaowabadili watoto dini kinyume cha sheria; wanaofanya vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto; wasiowaruhusu watendaji wa Serikali kufanya ufuatiliaji na usimamizi; wasioandaa mpango wa kuwaunganisha watoto na familia zao na hivyo, kusababisha watoto kukaa kwa muda mrefu kwenye makao na wale wote wanaondesha makao bila kuwa na leseni ya uendeshaji.”

Alisema Serikali haitowafumbia macho watu wa namna hiyo, na mara tu watakapogundulika kuanzisha au kuendesha makao bila kufuata taratibu, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Alisema tangu mwaka 2016 hadi sasa, kuna jumla ya watoto 24,067 wanaolelewa katika makao yaliyosajiliwa nchini yakiwemo makao 140 yanayoendeshwa na kumilikiwa na watu au taasisi binafsi. Kati yao wavulana ni 11,925 na wasichana ni 12,142. 

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaratibu upatikanaji wa huduma za msingi kwenye makao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali. Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa Bima ya Afya kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. “Hadi sasa, watoto 900 kutoka Dar es Salaam, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha wamepatiwa kadi hizo na zoezi hilo linaendelea,” alisema.

Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu uendeshaji wa makao ya watoto sambamba na kutoa elimu kuhusu malezi, makuzi, haki, ulinzi na usalama wa mtoto kwa mujibu wa sheria zinazosimamia haki na ustawi wa mtoto.

Mapema, akielezea azma ya kuandaa futari hiyo, Mkurugenzi wa Chocolate Princess na mwandaaji wa kipindi cha televisheni maarufu cha The Mboni Talk Show, Bi. Mboni Masimba alisema jumla ya watoto yatima 325 walikuwa wamealikwa kushiriki futari hiyo.

Watoto hao wanatoka vituo vya Ijango Zaida Orphanage Centre kilichopo Sinza, Alzama Orphanage Centre (Mbagala), Ashura Foundation (Vingunguti), Madina Orphanage Centre (Tandale), Hiyari Orphanage Centre (Mbagala) na Hisani Orphanage Centre (Mwasonga).

Futari hiyo iliandaliwa na Mboni Masimba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Asure Yetim Vafki, United Bank of Africa (UBA), Junaco, Mo Dewji Foundation, Lake Oil, ASAS, AZAM, Uncle K Catering, Zurii, Simply Special Decor na State Oil na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo Balozi wa Uturuki nchini, Bw. Ali Davutoğlu, Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Taifa, Sheikh Issa Othman, masheikh, maimamu wa misikiti na viongozi wa taasisi zinazojihusisha na malezi ya watoto yatima.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,        
JUMATATU, MEI 27, 2019.

MIJADALA SULUHU YA BIASHARA KUKUA KUPITIA SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Albert Chalamila akizungumza  wakati wa kongamano lililoandaliwa na Programu ya kuendeleza mifumo ya kimasoko ya kilimo (AMDT),lililowakutanisha wataalamu kutoka sekta binafsi na sekta ya umma wakiwemo Wakuu wa wilaya,Makatibu tawala,Wenyeviti wa Halmashauri ,Wakurugenzi na Maafisa Biashara kutoka mikoa ya Nyanda za juu kusini .
Baadhi ya Wakuu wa wilaya kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika mkoani Mbeya.
 Mkuu wa kitengo cha uboreshaji Mazingira ya Biashara wa Programu ya kuendeleza mifumo ya kimasoko ya kilimo nchini (ADMT) , Tertula Swai akizungumza wakati wa kongamano hilo. 
Baadhi ya washiriki katika kongamano hilo kutoka taasisi za Binafsi na zile za umma.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ,Asia Juma Abdalah akichangia jambo wakati wa kongamano hilo.
Kaimu katibu tawala Mkoa wa Mbeya ,Said Madito akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Washiriki katika Kongammano hilo wakifuatilia mijadala.
Baadhi ya Wakuu wa wilaya walioshiriki kongamao hilo wakichangia hoja mbalimbali zilizowasilishwa kwa lengo la kusaidia sekta ya Kilimo nchini.

  Washiriki wa Kongamano lililolenga majadiliano ya namna ya kuboresha biashara kupitia mijadala ya pamoja baina ya sekta binafsi na watendaji wa vyombo  vya Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Albert Chalamila

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Mbeya.


BAADHI ya Changamoto zinazotajwa kuwakabili wafanyabiashara waliopo kwenye Mnyororo wa thamani unatokanana Kilimo ni pamoja na kukosekana kwa mijadala baina ya sekta Binafsi na sekta ya umma kujadili sera,kanuni na miongozo inayoweza kuleta maendeleo katika Biashara kupitia Kilimo.


Katika kuondoa changamaoto hiyo ,Programu ya kuendeleza mifumo ya kimasoko ya kilimo (AMDT) umezikutanisha pande hizi mbili jijini Mbeya ,sekta binafsi na sekta ya umma wakiwemo Wakuu wa wilaya,Makatibu tawala,Wenyeviti wa Halmashauri ,Wakurugenzi na Maafisa Biashara kutoka mikoa ya Nyanda za juu kusini .


Lengo la kukutanishwa kwa watendaji hawa wa serikali na wale wa sekta binafsi ni pamoja kuinua maisha ya Mtu ,kina Mama kina Baba, Vijana ambao ni maskini kupitia uboreshaji wa mazao ya biashara kwa wakulima,wasindikaji,wasafirishaji wanaofanya kazi katika maeneo ya vijijini.


Mkuu wa kitengo cha uboreshaji Mazingira ya Biashara wa Programu ya kuendeleza mifumo ya kimasoko ya kilimo nchini (ADMT) , Tertula Swai alisema kupitia mijadala kwa kiasi kikubwa itachangia kuboresha mazingira ya Biashara.


“Kuna namna mbalimbali ya kuboresha mazingira ya biashara moja wapo ni namna ambavyo sekta binafsi na sekta ya Umma wanakaa kwa pamoja wanajadili zile sera mbalimbali ,kanuni ,miongozo ambayo inaweza kuleteleza maendeleo katika biashara ambazo zinafanyika katika sekta hiyo ya Kilimo” alisema Swai.


“Kwa nini mjadala ni muhimu,mjadala ni muhimu kwa sababu inawezekana kabisa kwamba katika kufanya biashara aidha ya Kulima ,Kuzalisha ,Kusafirisha ama Kusindika kuna changamoto ambazo ni kikwazo kwa zile biashara kukua”aliongeza Swai.


Alisema Serikali wajibu wake ni kuweka mazingira mazuri ya biashara  na kwamba  pale ambapo kuna changamoto au kuna kikwazo ni wajibu wa serikali kuboresha yale mazingira ili wahusika iwe rashisi kufikia malengo.


“Lakini haya mazingira hayawezi kutokea tu hivi hivi ni lazima sekta binafsi wajadili, wakae pamoja na sekta ya umma kuangalia ni sera zipi hizo ,kwa nini ni kikwazo ,ni watu wangapi wanaathirika ama wanaumizwa na hizo sera na je zitarekekebishwa vipi .”alisema Swai.



“Yaani sekta binafsi washirikiane na serikali kuja na namna ya kuboresha  na mwisho wa siku wafanyabiashara watafaidika na biashara zao zitakuwa lakini pia serikali itafaidika kwa maana ya kwamba itaongeza mapato”aliomgeza Swai .


Swai alisema Lengo kuu kwa AMDT ni kuongeza kipato  na fursa za ajira kwa Watanzania wa rika lote hususani walioko maeneo ya vijijini na kwamba kupitia program hiyo AMDT inatengeneza mifumo ya masoko. 


“Tunazungumzia mfumo wa uzalishaji mbegu au mfumo wa uuzaji pembejeo au mfumo wa utoaji huduma lakini pia kwenda kuboresha pale ambako kuna upungufu ,tukilenga zaidi kwenye mazao ya Mahindi ,Mikunde na Alizeti”alisema Swai


Katika kongamano hilo lililofanyika katika Hoteli ya Usungulo jijini Mbeya,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ,Albert Chalamila alisema ipo haja kwa Serikali  kufanya marekebisho ya sheria za tozo za kodi  ili kuwa na tija na rafiki  kwa wakulima na wafanyabiashara.



Kauli ya Chalamila inatokana na uwepo wa changamoto katika eneo la tozo katika ununuzi na usafirishaji wa mazao zinazotajwa kama kero kwa wakulima kupitia mnyororo wa thamani kwa mazao ya Mahindi, Alizeti na Mikunde.



 “Maboresho ya mifumo ya kodi haikwepeki, tusikwepe kuzungumzia maboresho ya mifumo ya kodi,nina amini tukifanya maboresho ya mifumo ya sheria za kodi zetu  maana mifumo yetu ya kodi ya sasa ni ile ya tangu miaka 1990 .



Alisema endapo maboresho yatafanyika kwa kiasi itawezesha mifumo kuwa rafiki kwa wafanyabiashara na wakulima kufanya biashara nchini hatua itakayochangia kuondoa udanganyifu .



Mbali na hilo, Chalamila alisema bado kuna kasumba watu kuzungumza zaidi kuliko vitendo kwenye masuala ya msingi jambo ambalo linakwamisha juhudi za wananchi kama vile wakulima kuhamasisha kulima kwa wingi lakini mwisho wa siku wanakosa masoko na mazao yao kuharibika.



Alisema ‘Tunapohamasisha kitu fulani , ili wenzetu walioko kwenye hali ya kawaida ambao ndio walengwa wakuu maana tunapozungumzia mahindi, alizeti au maharage, utagundua kwamba Watanzania kuna baadhi ya vitu tunavizungumza sana lakini ukienda ngazi za chini havitekelezeki’.



Alisema Watanzania wakiwamo viongozi walianza miaka mingi kuimba wimbo wa ‘Kilimo ni uti wa mgongo’ lakini ukweli ni kwamba hata hao wanaohamasisha wananchi kujikita kwenye kilimo ndani yake hawana hata kitengo cha masoko  na wakiulizwa wanakuwa hawana majibu ya moja kwa moja.



Kongamano hili la siku moja lililoandaliwa na Programu ya kuendeleza mifumo ya kimasoko ya kilimo (AMDT) lilitnguliwa na Mkutano wa siku tatu uliowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo  Wakulima,wasambazaji wa mbegu,wasindikaji na vyama vya msingi kujadili mnyoro wa thamani kupitia zao la Alizeti.

Upande wa mashtaka waombwa kuharakisha upelelezi katika kesi ya Shamimu na Mmewe

$
0
0
   Na Karama Kenyuko, Michuzi Tv
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride inayomkabili Mmiliki wa Blog 8020 Fashion, Shamim Mwasha (41) na Mumewe, Abdul Nsembo(45) umedai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina alidai kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine.

 Baada ya kueleza hayo Wakili utetezi, Charles Kisoka na mwenzake Hajra Mungula walidai kuwa shauri hilo halina dhamana hivyo wanauomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi.

Wakili Wankyo alieleza kuwa amesikia kilichozungumzwa na upande wa utetezi, hivyo  watawahimiza wenzao wa upelelezi wafanye haraka na tarehe ijayo wataeleza upelelezi ulipofikia.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 10, 2019, washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu kesi yao haina dhamana.

Washtakiwa hao ambao ni wakazi wa Mbezi Beach, wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya.

Shamim na Mumewe wanatuhumiwa kusafirisha dawa hizo za kulevya, Mei 1,2019 wakiwa eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini  Dar es Salaam kinyume na sheria ya uhujumu uchumi.

Mitandao ya Kijamii haikwepeki kupiga vita dhidi Ufisadi, Rushwa pamoja na wizi wa rasilimali za Taifa.

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha

Imebainika kuwa ili vita dhidi ya ufisadi, rushwa pamoja na wizi wa rasilimali za taifa ziweze kuisha ni lazima kushirikisha makomandoo saba ambao niwazoefu. 

Hayo yamebainishwa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT)dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza wakati akizungumza katika kongamano la vijana lililoandaliwa na Taasisi ya Change Tanzania lililofanyika jijini hapa. 

Aidha alitaja makomandoo hao saba kuwa ni mitandao ya kijamii, vyombo Huru vya Habari, Asasi za Kiraia, Taasisi zisizokuwa za Kiserikali, Vyama vya Vafanyakazi, Vyama vya Upinzani, Bunge Huru pamoja na Katiba Huru. 

Alisema kuwa matumizi chanya ya mitandao ya kijamii ni nyenzo nzuri ya utetezi katika jamii ila wasioliona hili ni Wale wanaothani kuwa nafasi zao ni msaada tosha na hawaitaji watetezi. 

"Taifa la Tanzania chini ya serikali ya awamu ya tano imetangaza Vita dhidi ya mafisadi, rushwa pamoja na wizi wa rasilimali za taifa na ili kushinda vita hii Serikali yetu inaitaji Msaada wa makomandoo wazoefu katika Vita hii "Alisema Bagonza

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Change Tanzania Forum  Maria Sarungi Alisema kuwa licha ya kuwa na sheria  juu ya uhuru wa kujieleza katika Mitandao lakini bado mitandao ya kijamii haikwepeki. 

Alibainisha kuwa wao kama Change Tanzania wanaendelea kusaidia uwepo wa uhuru wa kujieleza lakini wanataka badala ya kuchukuliwa hatua watumiaji hawa wa mitandao wapewe elimu Kwanza.
Askofu wa Kanisa la kiinjili na kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza akiongea katika kongamano la vijana
Rais wa zamani wa Chama cha Wanasheria Fatma Karume akizungumza katika kongamano hilo ambapo aliwataka waandishi wa habari kutoogopa na kuwaeleza ukweli viongozi wao, pamoja na kufukua uwovu wote unaofanywa na viongozi wao. 
 Mkurugenzi wa Taasisi ya Change Tanzania Forum  Maria Sarungi akizungumza na waandishi wa habari walivojipanga katika utoaji wa elimu katika masuala mbalimbali.


WAZIRI MKUU AWAONYA WAMILIKI WA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA

$
0
0
 Waziri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi, wakati wa futari ya pamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea watoto yatima vya jijini Dar es Salaam, iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Mei 26.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watoto yatima, kwenye futari ya pamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea watoto yatima vya jijini Dar es Salaam, iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Mei 26.2019. 
Waziri Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Chocolate Princess na mwandaaji wa kipindi cha televisheni maarufu cha The Mboni Talk Show, Bi. Mboni Masimba, wakati wa futari ya pamoja na watoto yatima kutoka kwenye vituo sita vya kulea watoto yatima vya jijini Dar es Salaam, iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee Mei 26.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MRADI WA RELI YA KISASA (SGR), MWAMBA WA CHANGAMOTO ZA USAFIRISHAJI NCHINI

$
0
0
Na Paschal Dotto-MAELEZO
Ni Takribani Miaka 120 ambapo historia iliandikwa, mwaka 1912, Serikali ya Kikoloni nchini iliamua kuimarisha sekta ya usafirishaji Kwa kujenga Reli, ambapo njia zake ziliunganisha Miji hasa maeneo ya kilimo, uzalishaji na kibiashara, reli kuu kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza, hatimaye Kigoma na Tanga.

Ni dhahiri sasa tunaona Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mageuzi makubwa Kwa kujenga reli ya kisasa, maarufu SGR (Standard Gauge Railway) ambapo kwa vyovyote tutasogeza nyuma zaidi kuhusu historia ya reli nchini, kwani Rais anatakeleza Ujenzi wa Reli ya Kisasa, Standard Gauge Railway (SGR) kwa maslahi makubwa kiuchumi.

Katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya SGR awamu ya pili, Morogoro-Makutupola, iliyofanyika 14, Machi, 2018, Rais Magufuli aliwakumbusha Watanzania kuwa Tanzania imekuwa nchi ya pekee Barani Afrika katika kutekeleza mradi huo mkubwa kwa pesa za walipa kodi wake.

“Kwa bahati nzuri, hivi karibuni tulitembelewa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, na alishuhudia kwamba Tanzania tumetayarisha fedha zetu wenyewe, kwa nguvu zetu wenyewe, na walipa kodi ni watanzania wenyewe, Tsh Trilioni 2.8 na kutangaza tenda zilizokuwa wazi, makampuni zaidi ya 40 yalijitokeza kuwania tenda, na bahati nzuri kampuni kutoka Uturuki ikashinda tenda hii,” alisema Rais Magufuli na kuongeza kuwa Uturuki itatupa mkopo wa masharti nafuu kwa awamu zingine za ujenzi, Rais akaongeza, “ kwa hiyo Tanzania tunaweza”, 

Rais Magufuli aliwataka watanzania kutambua fursa za upitapo mradi wa SGR na kuwataka wafanyabiashara wakubwa, wadogowadogo, mama ntilie, kunufaika wakati wa ujenzi na mara baada ya ujenzi, na kwamba itakuwa nguzo kubwa kwa usafarishaji kwenye maeneo hayo na nchi nzima.
“Katika uchumi wa nchi yoyote duniani, Sekta ya Usafirishaji ni muhimu sana, kwa hiyo Serikali kuchukua hatua madhubuti ya kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa kujenga reli ya kisasa, SGR, ni moja ya Mwarobaini wa kutatua changamoto ya usafirishaji mizigo na kulinda usalama wa barabara”. Alisikika mmoja wa wahandisi akiwaeleza waliowatembelea.

Mageuzi ya Rais Magufuli yanalenga kuwaimarisha wananchi, si tu wafanyabiashara bali hata wasafiri kwa utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya kisasa, SGR yenye kasi ya 160km/saa utakuwa na faida kuwabwa kwani masaa 2.5 Dar es Salaam-Morogoro na masaa tisa kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza, ni dhahiri kutakuwa na Furaha kubwa kwa watu kuwahi kufika Mwanza mapema badala ya saa saba usiku au kulala Shinyanga.

“Ujenzi wa Reli hii (SGR), kwa Tanzania siyo chaguo bali ni lazima, kwani hatua hii ilitakiwa ifikiwe zamani, lakini sasa Rais Magufuli ameamua kutufikisha kwenye teknolojia mpya katika sekta ya usafirishaji, kwani matatizo mengi ya barabara yanatokea kwababu ya mizigo mizito, hakuna reli imara ya kubeba mizigo hiyo, kwa hiyo ujenzi wa Reli hii ni maamuzi sahihi kwa Serikali yetu.”, Anaeleza Mkurugenzi TRC, Masanja Kadogosa.

Kadogosa anasema, Reli hiyo ambayo inatumia nishati ya umeme imekuja wakati mwafaka ikiwa Serikali inatekeleza mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa Mto Rufiji (Rufiji Hydroelectric Power), wenye kutoa Megawati 2,115, kwa hiyo treni hiyo itapata umeme wa kutosha.
“SGR, Ni mradi mkubwa ambao unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufulu kwa kutumia fedha za walipa kodi wake kwahiyo ni vyema watu wakafahamu kuwa kodi yao inaenda wapi Trilioni 7 siyo mchezo”, alisema Kadogosa.

Ili kutekeleza adhima ya kuutangaza mradi huo kwa wananchi, Mei 17, 2019, Jopo la Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Makatibu Tawala takribani 400 wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Seleman Jafo walitembelea kuona mradi huo ili kupeleka ujumbe kwa wananchi.

Kabla ya Safari hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa aliwapitisha kidogo wageni wake katika shule ndogo kuhusu mradi ili kutambua umuhimu wa Mradi huo kwenye sekta ya usafirishaji na kwa wananchi.

Masanja alieleza kuwa Reli hiyo inayojengwa inaenda kufuta zana mbalimbaliikiwemo ile historia ya kikoloni, kuwa reli iliyopo ilijengwa na wakoloni, lakini pia ujenzi wa Reli hiyo sasa unaenda kuimarisha sekta ya usafirishaji. Serikali inatekeleza ujenzi huo Kwa Kipande cha Dar es Salaam-Morogoro, Morogoro-Makutupola na badae kutekeleza ujenzi huo hadi Mwanza, kilometa 1,219.

Kadogosa alisema kuwa Reli hiyo, SGR inauwezo wa kubeba tani milioni, 10,000, kwa mkupuo sawa na malori 500 yenye tani 20, Treni tano zenye tani 10,000 na kuwa na kasi kubwa ya 160km/saa, tofauti na ya sasa ambayo inakasi ya 30km/saa, kwa Afrika itakuwa ni Reli pekee yenye uwezo mkubwa kama huo, tani Miliomi 10-17 zitasafirishwa kwa mwaka, kwa hiyo SGR ni mwamba sekta ya usafirishaji nchini.

Aidha, Kadogosa alieleza kuwa ujenzi wa Reli (SGR), Dar es Salaam-Morogoro unatekelezwa na Kampuni kutoka Uturuki, Yapi Merkezi takribani Trilioni 2.7, lakini kwa sehemu nyingine ni Yapi Merkezi na Portuguese Construction Group Motel-Engil.

kukamilika kwa mradi huo kutakuwa na ufanisi mkubwa kwenye sekta ya usafirishaji nchini kwa kubeba mizigo tani nyingi lakini pia kasi yake katika kusafirisha abiria, kutoka Dar es Salaam- Dodoma treni itakuwa inafanya safari mara nane kwa siku, kwa hiyo ni hatua kubwa kwa sekta ya usafirishaji.

Kadogosa alizitaja baadhi ya Faida za Mradi huo Kwa sasa kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla kwani kwa sasa watanzania walioko sehemu za ujenzi wanafaidika na kupeleka malighafi za ujenzi, mama ntilie kupika chakula na biashara zingine.

“Takribani mifuko ya simenti milioni, 9,200,000 ambayo ni sawa na tani 600, nondo kilo milioni 115 sawa na tani 1500 na mataluma 1,400,000, kutoka kwa wasambazaji wa malighafi hizo takribani 500, wafanyakazi 10, 000, huku asilimia 94 ya wafanyakzi hao ni watanzania, pia asilimia 48 ya wataalam ni watanzania, kwa hiyo pamoja na mradi huu  kuwa nguzo imara ya usafirishaji nchini, SGR imekuja kutoa Fursa za ajira kwa watanzania”, Alisema Kadogosa.
Kadogosa alisema kuwa mradi huo ni mkubwa na uwezo wake ni wa juu, na sasa matatizo ya usafarishaji nchini yatapata suluhu kubwa, kuimarisha na kulinda barabara nchini.

Katika sekta ya usafirishaji wa mizigo hasa ile mikubwa inayotoka bandarini kwenda sehemu zingine za nchi na mengine nje ya nchi, kwani kuwepo kwa Reli imara itasababisha utendaji kazi wa bandari kuwa na ufanisi mkubwa, “Bandari inategemea kuwepo kwa miundombinu imara kwa upande wa nchi kavu, hakuna ufanisi wa Bandari bila kuwa na Reli imara, Serikali imeliona hilo ndiyo maana ikaamua kutekeleza haraka ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Reli yetu hii inabeba mizigo mingi Takribani Tani Milioni 17 kwa mwaka, hakuna Reli kama hii Barani Afrika” Kadogosa.
 Moja ya Kifaa cha kampuni inayojenga Reli ya Kisasa, SGR ya Yapi Merkez kikiunganisha Reli hiyo katika moja ya zaiara ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makataibu tawala  takribani 400, Mei 14, 2019.
Baadhi ya Watalaam wanaoshirika ujenzi wa Reli ya Kisasa, SGR kutoka Tanzania na Kampuni ya Ujenzi  ya Yapi Merkezi wakishuhudia  zoezi la uunganishwaji wa reli ya Kisasa katika ziara ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Makataibu tawala takribani 400, Mei 14, 2019.

Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images