Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live

KAMATI YA SIASA MKOA WA DAR ES SALAAM YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI KUTOKA JIMBO LA ILALA NA SEGEREA

$
0
0
Kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam comred Mama Ketty Silvia Kamba leo hii tarehe 26.05.2019 wamepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2018/2019 kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Ilala Muheshimiwa Mussa Azzan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Segerea Muheshimiwa Bonnah Kamoli

Mwenyekiti wa Mkoa aliongozana na Ndugu Yusuph Nassor (MNEC MKOA), Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Zakaria Mwansasu, Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Simon Mwakifwamba  na Ndugu Iddi Azzan

Katika taarifa ya utekelezaji wa Ilani katika majimbo haya wawili mambo mengi yamefanyika katika miradi mbalimbali (Afya,Elimu,Miundombinu,Maji) ambapo asilimia kubwa ya miradi mmetekeleza na kumalizaka kwa kiwango kukubwa sana.

Kamati ya siasa ya mkoa wa Dar es Salaam inampongeza kwa dhati Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Muheshimiwa DKT John Pombe Magufuli kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani katika ngazi ya Taifa lakini pia kuhakikisha pesa za maendeleo   zinakuja katika majimbo na halmshauri nchini kote.

Pili, kamati ya siasa ya mkoa inawapongeza wabunge wote wa wawili kwa kazi kubwa wanayoifanya lakini pia kuhakikisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa mwaka 2018/2019 inasomwa na kuwasilishwa.

Mwisho, kamati ya siasa inaipongeza kamati ya siasa ya wilaya ya Ilala ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM wilaya Ndugu Ubaya Chuma kwa kufatilia kwa ukaribu utekelezaji wa Ilani ya CCM ndani ya wilaya ya Ilala

Viva Muheshimiwa John Pombe Magufuli

TUMEAHIDI,TUMETEKEZA

Imetolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam

26.05.2019

WAZIRI WA MAJI AHIMIZA USIMAMIZI MZURI MIRADI YA MAJI

$
0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye Mradi wa Maji wa Manga katika Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi pamoja na viongozi wa mkoa wa Katavi na wataalam wa Sekta ya Maji mkoani Katavi.Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye Mradi wa Maji wa Manga katika Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi pamoja na viongozi wa mkoa wa Katavi na wataalam wa Sekta ya Maji mkoani Katavi. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi kuhusu mgao wa fedha katika wilaya mbalimbali za mkoa huo. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera wakitoka kuangalia chanzo cha maji cha Mradi wa Maji wa Iklongo II, Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi.Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera wakitoka kuangalia chanzo cha maji cha Mradi wa Maji wa Iklongo II, Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mpanda (MUWASA), Mhandisi Zacharia Nyanda akitoa maelezo kuhusu Mradi wa Maji wa Ikolongo II uliopo Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi. 

……………………………………………………………. 


Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesisitiza umuhimu wa Wataalam wa Sekta ya Maji kusimamia miradi ya maji kwa ufanisi ili kuweza kuwa na miradi yenye tija inayolingana na thamani ya fedha zinazowekezwa na Serikali kwenye miradi yote nchini.

Profesa Mbarawa amesema ni lazima kuwe na usimamizi mzuri kwa kila hatua ya utekelezaji wa miradi ya maji, ili kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa baada ya kukamilika kwa miradi hiyo, ambayo ni kumaliza tatizo la maji nchini kote.

Akitoa majibu kwa mkandarasi aliyekuwa akilalamika kucheleweshewa malipo na Serikali, Profesa Mbarawa amesema jambo hilo linatokana na tabia ya wakandarasi kuweka makisio makubwa ya gharama za miradi ya maji kwa dhumuni la kupata faida kubwa, kulinganisha na gharama halisi za ujenzi wa miradi hiyo. Wakandarasi wengi wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya wahandisi wasio waaminifu kuihujumu Serikali na kusababisha kushindwa kulipa fedha hizo kwa wakati kutokana na gharama kuwa kubwa kupita kiasi.

“Tumegundua tulikuwa tukiibiwa fedha nyingi, hivi sasa tumeweka utaratibu wa kujiridhisha na makisio ya gharama za kila mradi kwa kila kipengele, kabla ya kuingia mkataba. Hatua hii imetusaidia kupunguza gharama kwa kulipa gharama zinazostahili. Hivyo, kutuwezesha kulipa wakandarasi kwa wakati na kuwa na miradi yenye viwango bora inayokamilika kwa wakati’’, Profesa Mbarawa amesema.

Akiwa wilayani Mpanda, Profesa Mbarawa amekagua mradi wa maji wa Manga-Kasokola ulioanza kutekelezwa Februari, 2018 chini ya Mkandarasi Monmar & Sons Co. Ltd Building and Civil Engineering na utakamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2019. Lengo la mradi huu ni kufikisha huduma karibu na wananchi wa Manga na Kasokola wapatao 7,560 kwa umbali usiozidi mita 400.

‘‘Kwa ujumla nimeridhishwa na maendeleo ya miradi ya maji katika mkoa wa Katavi, kikubwa ni kuweka msukumo mkubwa ili miradi hii iweze kukamilika mapema zaidi ili matokeo ya miradi hii iweze kuonekana kwa wananchi wa mkoa huu’’, Profesa Mbarawa amesema.

Profesa Mbarawa ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Katavi kwa kutembelea miradi ya maji ya Manga, Ikolongo II, Igagala, Ngomalusambo na Kabungu katika Wilaya za Mpanda, Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Tanganyika.

Masoko Mapya ya Madini Yaingiza Bilioni 34.3 Kwa Mwezi Mmoja

$
0
0
Na Frank Mvungi- MAELEZO 

Dhahabu ya Bilioni 34.3 imeuzwa katika Kipindi cha mwezi mmoja kupitia katika masoko 21 yaliyoanzishwa kwa ajili ya kuuza madini katika mikoa mbalimbali hapa nchini. 

Akizungumza katika mahojiano maalum na idara ya habari MAELEZO, Bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko amesema kuwa kuanzishwa kwa masoko hayo kumekuwa chachu ya kuongeza mchango wa sekta ya madini katika kukuza uchumi na pato la Taifa kwa ujumla. 

“ Katika kipindi cha mwezi mmoja tu yaani Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu,jumla ya kilo 409.3 za dhahabu pekee zenye thamani ya shiilingi bilioni 34.3 imeuzwa kupitia katika maduka yaliyoanzishwa katika mikoa mbalimbali” Alisisitiza Biteko. 

“katika kilo hizo,Mkoa wa Geita umeongoza kwa kufanya biashara ya jumla ya kilo 289,Kahama kilo 44,Mara kilo 13,lakini cha kufurahisha zaidi ni kwa Wilaya ya Chunya ambako jumla ya kilo 52 zimeuzwa katika soko hilo zikiwa nia siku chache toka kufunguliwa kwake ,”,aliongeza, mheshimiwa Biteko. 

Aidha mheshimiwa Biteko, katika mahojiano hayo maalum,ameeleza kuridhishwa na biashara inayofanyika katika maduka hayo ya madini kote nchini na kueleza kuwa licha ya mafanikio hayo yaliyofikiwa katika kipindi kifupi,serikali inashughulikia changamoto ndogondogo ikiwemo wafanyakazi,mashine za XRF na idadi ya watoa vibali. 

Akifafanua amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuona sekta hiyo inatoa mchango stahiki katika kujenga uchumi na kuchangia maendeleo hapa nchini ndio sababu mkazo umewekwa katika kusimamia sekta hii. 

Pia aliwataka wachimbaji wadogo na madalali wa madini kuhakikisha kuwa wanatumia masoko hayo kikamilifu na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufutiwa leseni jambo alilosema serikali haipendi, 

Akizungumzia mikakati ya kusimamia sekta hiyo Mhe. Biteko amesema kuwa ni pamoja na kushirikisha wachimbaji wadogo katika kuhakikisha kuwa vitendo vya utoroshaji wa madini unakomeshwa ili kulinda mapato ya Serikali. 

Aliongeza kuwa hatua nyingine ni usimamizi wa karibu katika maeneo yote ya uzalishaji wa madini ya aina mbalimbali na kuchukua hatua za kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo. 

Katika mwaka wa fedha 2019/2020 Waziri Biteko amebainisha kuwa masoko mengine 7 yanatarajiwa kufunguliwa. 

Baadhi ya Mikoa ambayo imeshafungua masoko ya kuuza madini ni pamoja na Geita, Dodoma, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Morogoro, Mbeya, ambapo tayari mikoa 21 imeshafungua maduka hayo hadi sasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alilolitoa kwa wakuu wa mikoa wote hapa nchini.

NEWS ARLET: BUKOBA TENA

$
0
0
Barabara zimefungwa Magari hayaendi Barbara kuu ya Kuingia mjini mawasliano yamekatika, maji yanapita juu ya daraja la kanoni

Tunaendelea kuleta taarifa

DullaUwezo - MichuziTv


JPM BODABODA CUP YAHITIMISHWA KAITABA

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus, Michuzi TV - Bukoba.

Hatimae Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyozikutanisha Timu za waendesha Pikipiki Manispaa ya Bukoba, maarufu kama JPM BODABODA CUP 2019 - KAGERA, Yamehitimishwa Mei 25, 2019 katika Uwanja wa Nyasi bandia wa Kaitaba.

Michuano hiyo iliyobeba hisia za wanasoka pamoja na wadau mbalimbali, imeratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera, ikiwashirikisha baadhi ya wadau wachache likiwemo Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera Kitengo cha Usalama Barabarani.

Katika fainali iliyozikutanisha Timu za Rwabizi Fc na Kasoma Fc, iliyohudhuriwa na mashabiki wengi wapenda soka kutoka Viunga mbalimbali vya Manispaa ya Bukoba, Rwabizi FC wameibuka wababe kwa kuichachafya bao 5 - 1Timu ya Kasoma.

Baada ya Mchezo huo kukamilishwa na mwamuzi Ahmada Simba, Uongozi wa Mkoa pamoja na Timu ya Maandalizi chini ya RC Marco Gaguti, wakakabidhi zawadi kwa washindi na washiriki licha ya Kiongozi huyo kukabidhi hati za Mamilioni ya Mikopo kwa Vikundi sita vya Bodaboda kwa ajili ya kujiendeleza kiujasiliamali.

Miongoni mwa Zawadi zilizotolewa kwa washindi ni pamoja na pesa Taslimu Milioni 3 kwa mshindi wa kwanza, Milioni 2 mshindi wa pili, Milioni moja  mshindi wa 3, Laki 2 mbili mshindi wa Nne, laki 2 Mfungaji bora, laki 2 mchezaji bora ambae pia aliongezwa shilingi Laki moja kutoka kwa Balozi wa kampeni ya Nyumba ni Choo Mrisho Mpoto. Sambamba na Zawadi hizo Timu nyingine zilizoshiriki zimepewa kifuta jasho shilingi elfu 50, kwa kila Timu pamoja na Zawadi ya Mpira mmoja mmoja kutoka CCM Mkoa wa Kagera kupitia Umoja wa Vijana Karagwe Saccos (UVIKASA).
 Hatimae Kikombe kikakabidhiwa kwa Washindi wa Mashindano hayo Rwabizi Fc 
 Maafisa usalama barabarani wakileta mwali uwanjani
 Mgeni rasmi wa Fainali hizo RC Gaguti akikagua Timu akisindikizwa na Viongozi wengine, nyuma yake ni Msanii Mrisho Mpoto.
 Picha ya pamoja waamuzi pamoja na manahodha wa Timu zote mbili.
 Sehemu ya mashabiki wengi waliohudhuria, wakiendelea kufuatilia mtanange huo wa Fainali ya JPM CUP
 Chama cha Mapinduzi kikikabidhi Zawadi za Mipira kwa RC Gaguti wakati wa mapunziko ya Mchezo wa fainali
 Wachezaji wa Timu ya Rwabizi Fc wakishangilia moja wapo ya Magoli kwa mtindo wa kulala chali
 Pichani Mgeni rasmi RC Gaguti akikabidhi hati ya Mkopo wa Shilingi Milioni sita kwa Kikundi cha Boda boda kwa ajili ya kujiendeleza katika mradi wao.

 Moja kati ya shughuli pevu iliyokuwa ikiendelea uwanjani
 Timu za Rwabizi FC na Kasoma FC zikiwa uwanjani Kaitaba tayari kwa ukaguzi kabla ya kuanza Mchezo wao Fainali ya JPM Bodaboda Cup
 Pichani Msanii na Balozi wa Kampeni ya Nyumba ni Choo akikabidhi Zawadi yao kwa mchezaji bora Bensoni, Shilingi laki Moja, Tisheti kumi na Kanga Kumi.
 Kikosi cha Kasoma Fc kilichoingia Fainali na kuibuka nafasi ya pili katika mashindano
Wababe wa Mashindano ya JPM Cup Kikosi cha Rwabizi Fc

UKARABATI BUKOBA SEKONDARI UMEFIKIA HAPA.

$
0
0

Kufuatia Dhoruba ya Upepo mkali uliombatana na Mvua kubwa kuikumba Shule ya Sekondari Bukoba, na Kusababisha madhara makubwa katika Shule hiyo na kufungwa kwa Muda, sasa ukarabati umeanza na hizi ndiyoo picha mbalimbali zikionesha ujenzi wa shule hiyo unavyoendelea na hatua iliyofikiwa.

BENKI YA EXIM YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Idara ya Mikopo wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Issa Hamis (kushoto) sambamba na Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo Bw Shrikant Ganduri (katikati) wakizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria  hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wakubwa wa benki hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
 Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo Bw Shrikant Ganduri akizungumza wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wakubwa wa  benki hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki
 Mmoja wa wateja wakubwa wa benki ya Exim Tanzania akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa wateja  wa benki ya Exim Tanzania  akiongoza ibada wakati hafla hiyo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim wakitoa neno la shukrani pamoja na utambulisho mbele ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wakubwa wa  benki hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
 Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo (kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo pamoja na wageni waalikwa wakiwemo Waziri wa Habari, Michezo, Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar  Bw Mahamoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Bw Issa Haji Ussi wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wateja wa benki hiyo Zanzibar.
 Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo pamoja na wageni waalikwa akiwemo Waziri wa Habari, Michezo, Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar  Bw Mahamoud Thabit Kombo (kulia kwake) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wateja wa benki hiyo Zanzibar
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo Waziri wa Habari, Michezo, Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar  Bw Mahamoud Thabit Kombo (katikati) pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Bw Issa Haji Ussi (Kulia) wakijadili jambo walipokutana kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo Zanzibar iliyofanyika visiwani humo mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo kutoka Dar es Salaam na Zanzibar kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo Zanzibar iliyofanyika visiwani humo mwishoni mwa wiki.

Serikali yaahidi kuisaidia Tembo Worries

$
0
0
SERIKALI imesema itatoa ushirikiano wa kila aina kwa timu ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu (Tembo Worries) katika mashindano yatakayoshirikisha nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yameswa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu, Stella Ikupa wakati akizungumza na viongozi na wachezaji wa timu hiyo katika Ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Ikupa alisema Serikali itashirikisha wadau wote pamoja na wabunge ili kuhakikisha mahitaji yote muhimu yanakuwepo kwa timu hiyo.Alisema wabunge wameanza kwa kukubali kuchangia Shilingi 100,000 sawa na shilingi milioni 40 huku wakiendelea kushirikisha wadau wengine.

"Ninawahakikishia serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mnachukua kombe hilo naomba msituangushe," alisema.Alisema awali walikuwa hawaamini kuwa kuna uwezekano wa watu wenye ulemavu kucheza mpira wa kiwango hicho ila amejionea mwenyewe na kwamba atawapa ushirikiano.

Ikupa alisema katika kuonesha Serikali imedhamiria kukuza michezo ofisi ya Waziri Mkuu itatoa seti tano za fimbo za kuchezea na baiskeli ya walemavu moja ili ziweze kusaidia katika mashindano.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu nchini (TAFF), Rizik Lulida alisema anaishukuru serikali na Spika wa Bunge kukubali kila mbunge kuchangia mashindano hayo.

Lulida ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF) alisema pia TAFF inawaomba wadau mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro kufadhili mashindano hayo."Tumetumia nembo tembo kama jina la timu tukiamini tutawalinda, kuwatangaza wanyama wetu na kuhifadhi vivutio vyetu," alisema Lulida.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo kwa Watu Wenye Afrika Mashariki kwa Waawake na Watoto (CECAAF), Nuru Awadhi alisema mashindano hayo ni muhimu katika kutangaza nchi kimataifa.Awadhi alisema Tembo Worries, watafanya vizuri katika mashindano hayo na kuipongeza serikali kuunga mkono mchezo huo.

Rais wa TAFF, Peter Sarungi, alisema kwa sasa wana program tatu ambazo zipo mbele yao kuhakikisha wanaibuka washindi."Program ya kuingia kambini, mafunzo ya marefa na mkakati wa ushindi hivyo ni imani yangu tukifanikisha haya kila kitu kitaenda sawa," alisema.

Katika wa CECAAF, Moses Mabula alisema alisema shirikisho limejipanga vizuri kusimamia mashindano hayo na kwamba itapendeza kombe likibaki nyumbani.Kwa upande wake Mchezaji Athuman Lubandani alisema wamejiandaa vizuri kuibuka na ushindi katika mash kinda hayo.

"Tunakushuru Mheshimiwa Naibu Waziri na Mama Lulida kwa mchango mnaotupatia hatutawaangusha," alisema
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Stella Ikupa, akizungumza na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu Walemavu pichani hawapo, kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu ya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (TAFF), Riziki Lulida na Kulia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Walemavu Afrika Mashariki (CECAAF), Nuru Awadhi

KUELEKEA SIKUKUU YA EID EL FITR, HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYO KATIKA SOKO LA DARAJANI, ZANZIBAR

$
0
0
 Sehemu ya wakaazi wa maeneo mbalimbali ya mji wa Unguja, Zanzibar wakiwa wamefurika kwa wingi katika soko la Darajani ili kujipatia mahitaji mbalimbali kuelekea sikukuu ya Eid El Fitr, inayotazamiwa kuwa tarehe za mwanzoni mwa mwezi ujao, kufuatana na mwandamo wa mwezi baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhan.








SPIKA NDUGAI ASHIRIKI SHEREHE ZA JUBILEE YA MIAKA 25 YA SHULE, MIAKA 20 YA MVUMI TRUST NA MAHAFALI YA 13 YA KIDATO CHA SITA MKOANI DODOM

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wahitimu wa kidato cha sita na wageni waalikwa wakati wa mahafali ya 13 ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Mvumi yaliyofanyika leo Mvumi Mkoani Dodoma.
Wahitimu wa kidato cha sita wamsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) wakati mahafali ya 13 ya shule ya sekondari Mvumi yaliyofanyika leo Mvumi Mkoani Dodoma.
Wageni Mbali mbali wakiwa katika mahafali ya 13 ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Mvumi tukio lililofanyika leo Mvumi Mkoani Dodoma.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Dickson Chilongani akiongoza ibada ya shukrani iliyofanyika leo katika Shule ya Sekondari Mvumi iliyopo Mvumi Mkoani Dodoma. Katikati mbele waliokaa ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya sekondari Mvumi baada ya mahafali ya 13 ya kidato cha sita yaliyofanyika leo katika shule hiyo, Mvumi Mkoani Dodoma.

WANAFUNZI WAWILI SHULE SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WATEULIWA KULIWAKILISHA TAIFA KONGAMANO LA DUNIA

$
0
0
Na Francis Godwin, Iringa 

Uongozi wa serikali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umesema umepokea kwa heshima kubwa mwaliko wa wanafunzi wawili wa shule ya msingi Southern Highlands Mafinga ambao wamepata mwaliko wa kuliwakilisha Taifa nchini Finland katika kongamano la wanafunzi dunia wanaojali mazingira .

Akizungumza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa wanafunzi hao na kiongozi wao jana kwa niba ya serikali ya wilaya ya wilaya ya Mufindi mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi Festo Mgina alisema kuwa heshima ambayo shule hiyo ya Southern Highnalnds Mafinga imepata ni kubwa kwa wilaya ,mkoa na Taifa kwa ujumla .

“ Huu ni mwaliko wa heshima kubwa kwa wilaya yetu na mkoa lakini kwa Taifa letu kualikwa katika kongamano kubwa kama hili la kujadili masuala ya mazingira duniani heshima hii sisi kama viongozi tunajivunia na tunapongeza shule kwa kuteuliwa kuwakilisha Taifa “ alisema Mgina

Kuwa mwaliko huo umekuja wakati Taifa liko katika harakati ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hata kuanza mchakato wa kuondoa sokoni mifuko ya rambo ambayo ni moja ya vikwazo vya mazingira .

HIvyo aliagiza wakuu wa shule za msingi katika wilaya ya Mufindi kuhakikisha wanafika katika shule ya Southern Highnalnds Mafinga ili kujifunza yale ambayo wanafunzi hao wawili watarudi nayo kutoka katika mkutano huo mkubwa nchini Finland.

“tunataka elimu na aagizo ambayo yatatolewa katika mkutano huo wa dunia nchini Finland vijana hao wakirudi basi kuweza kusambaza kwa wenzao kwenye shule zetu zote za MUfindi ikiwa ni pamoja na wakuu wa shule kufika kujifunza ili kila shule kuweza kujifunza elimu hiyo kwa faida ya mazingira ya maeneo yao “ alisema Mgina .

KIongozi wa wanafunzi hao nchini Finland ,mkurugenzi wa shule hiyo ya Southern Highnalnds Mafinga Kitova Mungai alisema kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule wanachama wa Klabu za mazingira duniani na kuteuliwa kwa wanafunzi hao kumetokana na ziara ya waratibu wa kongamano hilo ambao walifika kupema uwezo wa klabu zote nchini .

Hivyo baada ya kuvutiwa na jitihada zinazofanywa na klabu ya shule yake katika utoaji wa elimu ya mazingira na ufundishaji wa masomo ya ujasiliamali kwa wanafunzi ndipo wameweza kutuma mwaliko kwa wanafunzi wawili na kiongozi mmoja ambao watakwenda kushiriki kongamano hilo kwa muda wa siku 10 safari ambayo itaanza jumanne wiki hii.

‘’ Tunategemea kukutana na wawakilishi kutoka nchi mbali mbali duniani kama china ,Japan, Brazil ,Marekani ,China ,Uganda , Kenya na nchi nyingine nyingi ila tunaimani kubwa ya kuwakilisha vema Tanzania kwani watoto ambao wamechaguliwa kwenda katika kongamano hilo wanauwezo mkubwa sana katika elimu ya mazingira “ alisema Mungai

Alisema watoto hao na wenzao wamekuwa mbele kuhifadhi mazingira ya Shule ikiwa ni pamoja na uoteshaji wa miche ya miti na kuipata shuleni hapo na majumbani kwao na kwao suala la uhifadhi wa mazingira ni shughuli yao ambao hata wakipewa nafasi ya kufundisha wenzao wamekuwa wakifanya vizuri.

Mungai alisema kuwa Tnzania ni imekuwa mbele katika vita dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi na kuwa hata mkakati wa serikali wa kuzuia mifuko ya rambo ni mkakati ambao wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa namna ya kutunza mazingira pasipo kutumia mifuko hatarishi ya mazingira na kuwa kupitia kongamano hilo watapata kuwasilisha mbinu mbali mbali za utunzaji wa mazingira .

Kwa upandev wao wanafunzi watakaowakilisha Taifa katika kongamano hilo Maria Wambura na Stephen Sanga ambao ni wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo walisema kuwa kuteuliwa kwao katika kongamano hilo si nafasi ya bahati mbaya kwani wanauhakika wa kuliwakilisha vizuri Taifa katika kongamano hilo na kile ambacho watakipata watakuja kutumia kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao nchini .
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Festo Mgina (kulia) akiwakabidhi bendera ya Taifa jana wanafunzi wa shule ya msingi Southern Highlands Mafinga kwa ajili ya wenzao wawili walioteuliwa kuliwakilisha Taifa katika kongamano la mazingira duniani linalofanyika nchini Finland nkushoto kwake ni mkurugenzi wa shule hiyo ambae ni mkuu wa msafara wa wanafunzi hao Kitova Mungai

MAMENEJA TEMESA WAHIMIZWA KUBORESHA UTENDAJI KAZI WA KARAKANA

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akizungumza wakati akifungua kikao kwa mamemeja wa Wakala huo kuhusu namna ya kuboresha utendaji kazi na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa karakana katika vituo vyao vya kazi. Kikao hicho cha siku mbili kilifanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa chuo cha Ufundi VETA mkoani Iringa. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akisisitiza jambo wakati akiwakaribisha mameneja wa mikoa wa Wakala huo (hawapo pichani) katika kikao cha siku mbili kuhusu namna ya kuboresha utendaji kazi na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa karakana katika vituo wanavyovisimamia kilichofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa chuo cha Ufundi VETA mkoani Iringa. 
Mameneja wa mikoa wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakisikiliza kwa umakini mada mbali mbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao cha siku mbili kuhusu jinsi ya kuboresha utendaji kazi wao na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa karakana kilichofanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa chuo cha Ufundi VETA mkoani Iringa. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akifurahia jambo na meneja wa TEMESA mkoa wa Iringa Mhandisi Ian Makule mara baada ya kuteuliwa na mameneja wenzake kuwa Mwenyekiti wao ambaye atahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Julai mwaka huu. Kikao hicho cha mameneja kilifanyika mwishoni mwa wikii hii katika ukumbi wa chuo cha Ufundi VETA mkoani Iringa. 

***************************************** 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amewataka mameneja wa Wakala huo wa mikoa yote nchini kuboresha utendaji kazi wa karakana za mikoa wanayoisimamia kwa kujifunza na kuiga uzoefu wa kazi miongoni mwao ili kuweza kupata ufumbuzi sahihi wa changamoto zinazowakabili katika karakana za mikoa yao. 

Mhandisi Maselle ameyasema hayo mwishoni mwa wiki hii wakati akifungua kikao cha siku mbili kwa mameneja wa mikoa wa Wakala huo kuhusu utendaji kazi na namna ya kuboresha uendeshaji wa karakana za mikoa wanayoisimamia. 

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Ufundi VETA Iringa kilihudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa Wakala huo wakiwemo wakurugenzi wa vitengo mbalimbali, mameneja wa vitengo na wakuu wa idara mbalimbali. 

“Ni Imani yangu kuwa mapungufu yaliyobainika yatapatiwa suluhu katika kikao hiki kwani kimelenga kutoa mbinu kwa watendaji kupitia mawasilisho ambayo yatatolewa na wataalamu walioandaliwa na maelekezo mbalimbali yatakayotolewa na viongozi nilioambatana nao kutoka makao makuu’’, alisema Mhandisi Maselle. 

Aidha Mhandisi Maselle aliongeza kuwa madhumuni ya kikao hiko ni kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mapitio ya utendaji kazi wa nusu mwaka wa mwaka wa fedha wa 2018/2019 katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mt. Depot jijini Dar es Salaam ambapo katika kikao hicho ilibainika kuwa utendaji kazi wa vituo vya uzalishaji unatofautiana kutokana na kukosekana kwa uzoefu
wa kazi, mbinu za kibiashara na usimamizi wa karakana kwa ujumla. 

Vilevile Mhandisi Maselle alisisitiza kuwa kikao hicho kimefanyika mkoani Iringa kwasababu karakana ya mkoa huo ni kati ya karakana chache zinazofanya vizuri sana katika kutekeleza kazi zake kwa ubunifu mkubwa. 

Aliongeza, ”Naelewa kila mkoa una changamoto zake tofauti lakini huu ndio wakati sahihi wa kujadiliana kuhusu namna kila meneja anatatua changamoto zake hivyo tukijadili hapa inawezekana tukatoa ufumbuzi sahihi kwa wengine ambao huenda hawakuwa wakijua namna ya kutatua changamoto zinazowakabili na hilo ndilo jambo kuu ambalo tumekuja kujifunza hapa leo’’. 

Naye mkuu wa chuo cha Ufundi VETA mkoa wa Iringa Ndg. Ng’wandu Luhende, awali alitoa mada kuhusu namna ya kupangilia na kuendesha karakana na namna ya kusimamia na kuendesha biashara kwa upande wa karakana ambapo alitoa wito kwa mameneja hao kuongeza tija katika uzalishaji ili kuviinua vituo vyao. 

Vilevile alimpongeza mtendaji mkuu kwa kuamua kuanza kupima utendaji kazi wa mameneja hao kila mwezi ili kuona tija ya kikao hicho na aliwaomba kutumia muda wao vizuri ili kuboresha mazingira ya kazi kwa wafanyakazi wanaowasimamia katika vituo vyao. 

Awali katika kikao hicho mameneja hao walimchagua Mhandisi Ian Makule, meneja wa TEMESA mkoa wa Iringa kuwa Mwenyekiti wa mameneja hao ambapo atahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo atakua akiendesha vikao vinavyofuata vya mameneja hao.

WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA WAPEWA WIKI MBILI KUBORESHA MAGODORO YA HOSPITALI

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima akiangalia mojawapo ya magodoro ambayo yamewekewa kitambaa cha mpira ili yasiharibike kwa haraka.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na uongozi wa halmashauri ya Kigamboni wakati walipokagua hali ya utoaji huduma katika Hospitali ya Vijibweni ambayo ndiyo inayotoa huduma kama hospitali ya wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa hospitali ya Vijibweni wilayani Kigamboni.
Mashine mpya ya Xray yenye thamani ya shilingi milioni 153 ambayo imenunuliwa kwa mkopo na Hospitali ya Vijibweni kwa ajili ya kutoa huduma ya kipimo hicho kwa wakazi wa wilaya ya Kigamboni ambao wamekuwa wakilazimika kufuata huduma hiyo katika hospitali za wilaya nyingine za mkoa wa Dar es salaam.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es saaam Dkt Yudas Ndungile akielezea mikakati ya mkoa wake katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za afya zinazoukabili mkoa wa Dar es salaam jana wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima katika Hospitali ya Vijibweni


Na Mathew Kwembe, Dar es Salaam

Serikali imewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na wa Halmashauri kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuanzia sasa wawe wamekwishanunua vitambaa vigumu vya mpira ambavyo hutumika kuyafunika magodoro yanayotumiwa na wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili yasiweze kuharibika kwa haraka.

Agizo hilo limetolewa jana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima wakati alipofanya ziara kutembelea hospitali ya Vijibweni iliyopo eneo la Kigamboni jijini Dar es salaam.

Amesema anatoa siku 14 kuanzia sasa kwa waganga wakuu wa mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa magodoro yaliyopo kwenye Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwenye mikoa yao yanashonwa na kuwekea mifuko maalum ya mpira ili kuyafanya yarudi katika ubora wake. 

Ameongeza kuwa kumekuwa na mtindo kwa baadhi ya watendaji wa halmashauri kusingizia uchakavu wa magodoro na vitanda kwa vile tu Bohari kuu ya Dawa ilileta magodoro yenye vitambaa laini vya mpira na ni siku nyingi tangu magodoro hayo yaletwe.

“Watendaji wengine wamekuwa wakidai kuwa MSD wametuuzia magodoro haya siku nyingi na kitambaa chake laini hivyo yameanza kuchoka,”amesema na kuongeza: 

“Wakati inawezekana kununua kitambaa cha mpira, kwenye maduka yaliyopo yanayouza vitambaa vya mpira, mafundi wapo na kwa kuwatumia mafundi wenyeji wakashona magodoro haya yakarudi kuwa mapya,” amesema.

Dkt Gwajima ameongeza kuwa hakuna sababu kwa watendaji hao kutumia visingizio vyao kwani bei ya kununulia mita kadhaa za vitambaa vigumu vya mpira na za mashono ni ndogo na ni gharama zilizo ndani ya uwezo wa vituo vyetu vya kutolea huduma za afya.

Wakati huo huo, Dkt Gwajima amesifu hatua ya uongozi wa hospitali ya Vijibweni iliyopo wilayani Kigamboni kwa kuamua kukopa mashine ya Xray kutoka MSD ili waweze kuwahudumia wananchi walio wengi.

Amesema hatua hiyo ni nzuri kwani itawaondolea kero wananchi wengi waliokuwa wanalazimika kufuata huduma hiyo mbali na eneo hilo hivyo Dkt Gwajima amezitaka halmashauri nyingine za wilaya nchini kuiga mfano wa hospitali hiyo kwa kuhakikisha kuwa wanatumia vyanzo vyao vya mapato ya ndani kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

“Tunazo hospitali zetu nyingi ambazo zinasubiri mgao wa serikali, hii haiwezekani, tunachosema ni kwamba kila hospitali itasimama yenyewe kupitia timu yake ya usimamizi huduma za afya ya halmashauri kwa kupanua wigo wa huduma na kuvutia wateja wengi zaidi kutumia huduma hizo badala ya kuzifuata mbali na makazi yao kwa gharama kubwa,” amesisitiza Dkt Gwajima.

Naibu katibu Mkuu ameongeza kuwa kupitia uchangiaji wa huduma hizo kama walivyofanya Vijibweni ni dhahiri kuwa, vituo husika vitaweza kumudu gharama za kununua mahitaji mbalimbali ya kuboresha huduma za afya badala ya kutegemea serikali tu.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa misongamano ya wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, Dkt Gwajima amesema pamoja na ukweli kuwa baadhi ya maeneo kumekuwa na upungufu wa watumishi, yapo baadhi ya maeneo ambayo upungufu huo unachangiwa na uzembe wa baadhi ya watoa huduma katika kuwajibika.

“Baadhi ya wataalam huwa wanachelewa kufika kazini na wakifika wanaishia kuona idadi ndogo ya wateja chini ya kiwango cha walau wateja 30 hadi 40 kwa siku kilichopo kwenye miongozo,” amesisitiza Dkt Gwajima

Aidha, amesema kuwa yapo baadhi ya maeneo ambayo yana watoa huduma wengi zaidi kuliko ilivyotakiwa nayo haya yanahitaji kupanguliwa wapelekwe waliko wachache.

Dkt Gwajima ameeleza kuwa ni kweli upungufu upo ila, upungufu huo hauwezi tu kupimwa kwa maneno ya mazoea bali kwa kupima uwingi wa kazi kwa kila mtoa huduma kwa wakati huo.

“Kupitia utaratibu wa kupima uwingi wa kazi kwa wakati wa sasa (workload) inawezekana kuchochea uwajibikaji wa mtumishi mmoja mmoja na kuleta uwiano sawa wa kazi miongoni mwa watumishi wa vituo mbalimbali na siyo baadhi wanasema kuna upungufu wa watumishi akiulizwa amehudumia wateja wangapi unakuta hata kumi hawafiki,” amesema.

Dkt. Gwajima amesema, lazima hoja ipimwe kwa takwimu ndipo tutaweza kujiridhisha kwani maeneo yote hayafanani.

Pamoja na kutembelea hospitali ya Vijibweni, Dkt Gwajima alipata fursa pia ya kutembelea na kushuhudia ujenzi wa hospitali za wilaya za kigamboni na Ilala ambapo kwa upande wa hospitali ya Kigamboni Naibu Katibu Mkuu aliusifu uongozi wa halmashauri hiyo kwa usimamizi thabiti uliopelekea majengo ya hospitali kuwa katika hatua ya kupaua tofauti na wenzao wa Manispaa ya Ilala ambao wao majengo matatu kati ya saba yapo katika hatua za msingi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Yudas Ndungile amesema kuwa wao wameyapokea maagizo ya Naibu Katibu Mkuu na kwamba maagizo hayo yanatekelezeka kwa vile yapo ndani ya uwezo wa mkoa wake.

Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi kutembelea mikoa ya Dar es salaam na Pwani ambapo kabla ya hapo alitembelea mikoa ya Morogoro, Dodoma, Njombe, Ruvuma, Iringa na Manyara.

VIKOSI MAALUM VIKIONGOZWA NA KAMISHNA OPERESHENI NA MAFUNZO YA JESHI LA POLISI CP LIBERATUS SABAS, WAFANYA OPERESHENI MAPANGO YA AMBONI MKOANI TANGA.

$
0
0
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi La Polisi CP Liberatus Sabas, ameongoza Vikosi Maalum ya Kupambana na Uhalifu katika Operesheni iliyofanyika maeneo yote ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga siku ya jana baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kumeonekana baadhi ya watu wasiofahamika na baadhi yao ni wahalifu waliokuwepo kipindi cha nyuma ambao wengi wao walishakaatwa na Jeshi la Polisi na mwisho amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na taarifa katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama. (Picha na Jeshi la Polisi).
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi La Polisi CP Liberatus Sabas, ameongoza Vikosi Maalum ya Kupambana na Uhalifu katika Operesheni iliyofanyika maeneo yote ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga siku ya jana baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kumeonekana baadhi ya watu wasiofahamika na baadhi yao ni wahalifu waliokuwepo kipindi cha nyuma ambao wengi wao walishakaatwa na Jeshi la Polisi na mwisho amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na taarifa katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama. (Picha na Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi La Polisi CP Liberatus Sabas, ameongoza Vikosi Maalum ya Kupambana na Uhalifu katika Operesheni iliyofanyika maeneo yote ya Mapango ya Amboni Jijini Tanga siku ya jana baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kumeonekana baadhi ya watu wasiofahamika na baadhi yao ni wahalifu waliokuwepo kipindi cha nyuma ambao wengi wao walishakaatwa na Jeshi la Polisi na mwisho amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na taarifa katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama. (Picha na Jeshi la Polisi).

DK.MABODI AONGOZA MAELFU YA WANANCHI MAZISHI YA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA AMANI NDG.MROPE

$
0
0
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiweka udongo katika Kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Abdi Ali Mzee ‘Mrope’ aliyezikwa leo Kijijini kwao Jumbi Unguja. 
VIJANA Maalum wa UVCCM wakiwa na Jeneza la Marehemu Abdi Ali Mzee kwa ajili ya Mazishi huko Jumbi Unguja. 
…………………… 

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR. 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, leo ameongoza Maelfu ya Wananchi katika Mazishi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Amani Unguja Marehemu Abdi Ali Mzee ‘Mrope’ aliyefariki jana akiwa katika Matibabu huko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es saalam na amezikwa leo kijijini kwao Jumbi Mkoa wa Kusini Unguja. 

Viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wameshiriki mazishi hayo wakiwemo Katibu wa NEC,Idara ya Organazasheni Makao Makuu Ndugu Pereira Ame Silima,Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Mwl.Kombo Hassan Juma pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid. 
Wengine ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Wabunge na Wawakilishi,Wakurugenzi wa Idara mbali mbali za SMZ,Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa ngazi mbali mbali, Wana CCM na Wananchi kwa ujumla. 

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Amani Ndugu Mohamed Ali Mohamed,akisoma wasifu wa marehemu amesema CCM na Jumuiya zake wamepokea kwa Huzuni na Masikitiko Taarifa ya Kifo cha Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Amani Unguja. 

Alisema Mwenyekiti Abdi Ali Mzee alizaliwa mwaka 1964 katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na kupata Elimu yake ya Msingi kuanzia mwaka 1978 katika Skuli ya Msingi Kidongo Chekundu pamoja na kupata Elimu ya Sekondari katika Skuli ya Shangani mwaka 1981. 

Pia alieleza kwamba Abdi mwaka 1984 alijiunga na Chuo cha Ufundi wa Chuma huko Chang’ombe Dar es saalam na kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi mwaka 1983 katika Tawi la CCM Sogea. 

Katika maelezo yake Katibu huyo, ameeleza kuwa Marehemu Enzi za Uhai wake alishika nyadhifa mbali mbali katika Chama mwaka 1992 hadi 2007 alikuwa Balozi wa Nyumba 10 Shina namba 7 katika Tawi la CCM la Sogea,mwaka 1997 hadi 2007 alikuwa Mwenyekiti wa CCM Tawi la Sogea,mwaka 2007 hadi mwaka 2012 alikuwa ni Mwenyekiti wa Jimbo la Magombeni. 

Alieleza kuwa mwaka 2012 hadi mwaka 2019 alikukuwa ndiye Mwenyekiti wa mwanzo toka kuanzishwa kwa Wilaya Mpya ya Amani na pia alikuwa Mkufunzi wa Makada katika Chuo cha Itikadi cha CCM,Mjumbe wa Bodi ya kudhibiti kodi za Nyumba Zanzibar. 

Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo licha ya kuwa Mwanasiasa pia alikuwa ni Mwanamichezo Mstaafu wa Mpira wa Miguu aliyewahi kuchezea Timu za African Kids,Wazee Sports Club hadi umauti unamkuta alikuwa ni Mwalimu wa Timu ya New Boko kutoka Mtaa wa Boko Zanzibar. 

Sambamba na hayo Chama Cha Mapinduzi Taifa kupitia Mwenyekiti wake Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wanatoa Salamu za Pole kwa Wafiwa Ndugu,Jamaa,Marafiki na Watu wote walioguswa na Msiba huo na kuwaomba waendelee kuwa na subra katika kipindi hiki cha Maombolezo. 

Marehemu ameacha Vizuka wawili na Watoto Saba. 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala Pema Peponi Amin.

DKT. BASHIRU: UWEZO WA KUHIFADHI VITABU VITAKATIFU UWE CHACHU YA UBUNIFU KATIKA NYANJA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Dkt. Bashiru Ally, akieleza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM, Dkt. Bashiru Ally, akieleza umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally (katikati), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shaaban (kushoto) na baadhi ya wadau wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akimkabidhi zawadi Mtoto Summayya Juma, aliyeshiriki mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Baba Mzazi wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Mzee Abdalah Kijaji (katikati) na baadhi ya viongozi wa Dini Wilayani Kondoa wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, wakizungumza jambo wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa dodoma Mustapher Shaaban, akieleza umuhimu wa elimu ya Dini katika kuleta umoja wa kitaifa, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (kulia), kwa jitihada za kuhamasisha elimu Jimboni kwake, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 
Baadhi ya wanamashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wakisikiliza wito wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally (hayupo pichani), kuhusu kuwa wabunifu katika Nyanja ya Sayansi na teknolojia ili kuisaidia jamii inayowazunguka. 
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Pahi Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma wakishuhudia mashindano ya kuhifadhi Qur’an Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. 



***************************************** 



Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dkt. Bashiru Ally, amewataka watanzania kutumia uwezo wa kuhifadhi Vitabu vitakatifu kuongeza ubunifu katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia na nyingine ili kuendeleza jamii kwa kuipatia maendeleo stahiki. 

Dkt. Bashiru ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, wakati wa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyowashirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali nchini. 

Alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa katika kuwekeza kwenye elimu kwa watoto, kwa kuwa watoto wakisoma si tu wanajengewa maarifa lakini pia wanaunganishwa na hivyo kuwa chachu ya kuweza kuisaidia jamii inayowazunguka. 

Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuibua vipaji vya watoto vya kusoma Kitabu Kitukufu cha Quran na kuwajengea vijana uwezo wa kuwa na ujasili katika kueleza wanayo yaamini yakiwemo mambo mazuri ambayo yanafanywa na Serikali. 

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, alisema kuwa kazi zinazofanywa na Dkt. Ashatu Kijaji, ni zakupigiwa mfano hasa kwa wanawake na akawataka wazazi katika Wilaya ya Kondoa kumuunga mkono kwa kushiriki kikamilifu katika mikakati ya kuinua elimu katika eneo hilo, kwa kuhakikisha wanawapeleka watoto katika makambi yaliyo na lengo la kuongeza ufaulu wa wanafunzi. 

Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shabaan, amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi Quran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.

CHUO CHA TANGANYIKA POLYTECHNIC ARUSHA CHAWAPA WAJASIRIAMALI MAFUNZO YA KUTENGENEZA MIFUKO YA KARATASI

$
0
0



Wanakikundi kutoka eneo la Lemara jijini Arusha waliopata mafunzo ya muda mfupi ya kutengeneza mifuko ya karatasi ili kuendana na sera ya serikali kuondoa matumizi ya mifuko ya nailoni,mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic jijini Arusha.
Wanakikundi kutoka eneo la Lemara jijini Arusha waliopata mafunzo ya muda mfupi ya kutengeneza mifuko ya karatasi ili kuendana na sera ya serikali kuondoa matumizi ya mifuko ya nailoni,mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic jijini Arusha. 
Mmoja wa walionufaika na mafunzo ya kutengeneza mifuko ya karatasi katika Chuo cha Tanganyika Polytechnic ,Bakari Juma akitoa ushuhuda namna inavyomwingizia kipato kutokana na mahitaji kuongezeka. 
Meneja wa shirika la Sido mkoa wa Arusha,Nina Nchimbi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali wa kutengeneza mifuko ya karatasi ,kushoto ni Mkurugenzi wa ubunifu wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic kilichota mafunzo hayo,Dk Richard Masika na Mkuu wa Chuo,Abdul Semvua. 
Mkurugenzi wa ubunifu wa Chuo cha Tanganyika Polytechnic kilichopo Njiro,Dk Richard Masika akizungumza katika hafla hiyo. 

Meneja wa Sido mkoa wa Arusha,Uongozi wa Chuo pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kutengeneza mifuko ya karatasi wakiwa katika picha ya pamoja.

DAR YA KIJANA YAWANG’OA DIWANI,KATIBU WA MNYIKA

$
0
0
Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akikambidhi kadi ya CCM aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kwembe Manispaa ya Ubungo, Dweza Horace Kolimba (Chadema) leo jijini Dar es Salaam. 
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kwembe Manispaa ya Ubuongo, Dweza Horace Kolimba (Chadema) na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Liberata Samson, wakionyesha kadi zao chama chao kipya cha CCM leo. 
Naibu Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde, akizungumza na vijana wa CCM Wilaya ya Ubungo, wakati wa uzinduzi wa Ubungo ya Kijani Dar es Salaam leo. 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala akizingumza katika mkutano wa Kampeni ya Dar ya Kijani, jijini Dar es Salaam leo 
Vijana wa hamasa wa Manispaa ya Ubuongo, wakishangilia jijini Dar es Salaam leo. 
……………… 
 
Na Ripota Wetu-Michuzi TV 
 
KAMPENI ya Dar es Salaam ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), imewang’oa Diwani wa Kata ya Kwembe Dweza Horace Kolimba (Chadema) na Katibu wa Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Liberata Samson kwa kujiunga na CCM. 

Akiwapokea wanachama hao leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde, amesema mwaka 2020 ni lazima majimbo mawili la Ubungo na Kibamba yarudi ndani ya mikono ya CCM. 

Mavunde amesema kuwa hiyo ni dalili tosha kwamba CCM watachukua majimbo hayo na ni aibu kuyaacha majimbo hayo mawili yakiwa upinzani. 
Amesema kama makosa yalifanyika hapo awali hategemei tena kurudia tena na majimbo hayo yakaachwa chini ya John Mnyika (Kibamba ) na Saed Kubenea (Ubungo), kwa kuwa hakuna wanachokifanya zaidi utekelezaji wa ilani ya CCM unafanywa na wao. 

“Kama kuna uhitaji wa maji, barabara nzuri vyote vinafanyika sasa kuna haja gani ya kubakia upande wa pili wa upinzani ni lazima vijana kufanya kazi kuhakikisha majimbo yanarudi CCM na katika uchaguzi wa serikali za mitaa kata zote ziwe chini ya chama hicho. 

“Jitahidi hapa viongozi hii ni aibu anzeni na mitaa yote 91 kuhakikisha inarudi CCM mana hapa nikiangalia hakuna hata pa kupita Mnyika wala Kubenea watapitia wapi,” amesema Mavunde na kuhoji. 

Amesema jukumu la chama cha siasa ni ushindi na kushika dola na ili ushinde ni lazima kuishi matatizo ya wanajamii sasa kwa serikali ya sasa imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za wananchi wake. 
Hata hivyo amesisitiza kuwa Rais Dk. John Magufuli anakubalika ndani na nje ya nchi huku akitolea mfano, alipokuwa Afrika Kusini juzi wakati wa kuapishwa Rais Cyril Ramaphosa, ambapo alishangiliwa na wananchi wananchi wan chi hiyo. 

Katika hatua nyingine Mavunde amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii, kujiajiri wakati wakisubiri mchakato wa serikali katika kuongeza ajira kwa vijana hao. 

Amewataka kuhakikisha wanakuwa katika vikundi vya ujasiriamali vya kukopeshana ili waweze kupata fedha kwani Ubungo ina fedha nyingi ambazo zimetengwa kwa ajili yao waweze kukopeshwa na kujiendeleza. 

Katika hatua nyingine aliwapongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha kampeni ya Dar ya Kijani kwa kupandisha bendera ya CCM kila kata. 
Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, amesema wanashirikiana vizuri na viongozi wa majimbo ya Ubungo lakini bado watahakikisha kata zote 14 na majimbo ya Wilaya ya Ubungo zinarejea CCM kwani ziliazimishwa kwa muda. 

“Jimbo la Ubungo na Kibamba lazima yachukuliwe na CCM mwaka 2020, hakuna sababu ya kubaki upinzani kwani Rais Magufuli anafanya mambo makubwa ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla. 

“Na hii kampeni ya Dar ya Kijani itaambatana na kazi ya kutundika bendera, ufunguzi wa matawi kwa kila kata za Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020. Hivyo ni jukumu letu vijana kujipanga na kuhakikisha tunarejeasha heshima ya chama chetu CCM,” amesema Kilakala.

POLEPOLE ATAKA MSHIKAMANO KWA WANA CCM WILAYA YA TANGA KUPATA USHINDI CHAGUZI ZIJAZO

$
0
0
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole kulia akipokea tisheti ya umoja wetu ni ushindi wetu ya CCM kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu kushoto wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge huyo katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima ambaye ameshikilia fedha zilizochangishwa kwenye semina hiyo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba
MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa kwenye semina hiyo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima akiwa anahesabu fedha zilizotolewa 
Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole akizungumza wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee 
Sehemu ya wanachama wa CCM wilaya ya Tanga wakifuaatilia kwa umakini hotuba ya Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu

WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanga wametakiwa kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao ili kuweza kuhakikisha wanakiwezesha chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Hayo yalisemwa na Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu.

Alisema lazima kuwepo mshikamano ambao utaawasaidia kuweza kuhakikisha wana kuwa wamoja kuelekea kwenye chaguzi zijazo ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwatumikia watanzania kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Aidha pia katika semina hiyo Katibu huyo alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Tanga ambapo jumla ya shilingi milioni 18 ziliweza kupatikana papo kwa papo huku Mbunge wa Viti Malumu (CCM) Mkoani Tanga ambaye pia Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akichangia shilingi milioni 5.

Sambamba na uchangiaji huyo lakini Waziri Ummy alitoa pia bendera za mashina 1000 na sare za chama ili kuimarisha chama ngazi za chini huku bendera 1000 za mabalozi na tisheti 800 ambazo watazitumia kwenye shughuli mbalimbali za kichama .

WAMILIKI TANZANITE WAPEWA MIEZI SITA KUBORESHA MIUNDOMBINU

$
0
0

OFISA madini Mkazi wa Mkoa wa kimadini wa Simanjiro, Daudi Ntalima amewapa miezi sita wamiliki na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani, kuboresha miundombinu ya migodi yao la sivyo itafutiwa leseni. 

Ntalima aliyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na mameneja, wachimbaji na wamiliki wa migodi ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani. 

Alisema ametoa miezi sita hadi mwezi Septemba kwani ikifika mwezi Octoba wataanza kuchukua hatua na wanaanza kuhesabu miezi sita hiyo kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba. 

Alisema hawezi kutoa muda wa mwaka mmoja kwani ni muda mrefu hivyo wamiliki wa migodi hiyo zaidi ya 800 wajitahidi kuboresha miundombinu yao kabla ya miezi sita kumalizika. 

“Migodi yote inapaswa kuwekewa uzio wa ukuta wa matofali au mabati ili kuimarisha ulinzi na usalama mgodini na siyo senyenge mmiliki akishindwa hilo mgodi utafutiwa leseni,” alisema Ntalima. 

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoani Manyara (Marema) Tawi la Mirerani, Shwaibu Mushi alisema wachimbaji hao wanaiomba Serikali kuwapa muda mwaka mmoja ili waboreshe miundombinu ya migodi yao ikiwemo kuweka uzio. 

Mushi alisema wengi wao uchumi wao ni mdogo hivyo wanaomba muda huo ili kutekeleza hilo kwani agizo hilo limekuja kipindi ambacho wengi wao wana hali ngumu. 

“Wachimbaji wadogo bado wanahitaji kuwa wachimbaji wakubwa baada ya kupata madini, tuliomba tuongezewe muda wa mwaka mmoja ili tutekeleze hilo japo tunashukuru kwa kutuongezea miezi sita,” alisema. 

Mwenyekiti wa kamati ya Tanzanite, Money Yousuph alisema wachimbaji wamegawanyika kwenye matabaka tofauti kiuchumi hivyo wanaomba mwaka mmoja wa kutekeleza hilo. 

“Ofisa madini mkazi Ntalima wewe ni mlezi wetu na mchimbaji asiyekuwa rasmi mnamtambua na hamchukulii hatua kali na pia ukuta siyo kero ni tija tunaomba busara na hekima zako kwani sisi ni wasikivu,” alisema Yousuph. 

Mchimbaji mwingine Fatuma Kikuyu alisema ofisa madini mkazi Ntalima ni msikivu kwani amekuwa akiwajali wachimbaji madini hasa wadogo. 

“Hata suala la mishahara ya wachimbaji madini alitutetea kuwa haliwezekani hivyo utaratibu wa kulipana kupitia asilimia 10 pindi madini yakipatikana uendelee,” alisema Kikuyu.
Viewing all 110150 articles
Browse latest View live




Latest Images