Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUGOLA, LUKUVI WAKUTANA MJINI MOROGORO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati), akifafanua jambo katika Kikao cha kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi Mjini Mrogoro, ambacho pia kilichohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu). Kikao hicho pia kilihudhuriwa na maafisa wa Magereza na Manispaa ya Morogoro. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe (katikati). 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsalimia Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), Phaustine Kasike, wakati alipokua anawasili Makao Makuu ya Magereza Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akifurahia jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, wakati walipokua wanatoka ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe (katikati). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KORTI YATAKA KUFAHAMU UPEPELEZI KESI YA UTAKATISHAJI FEDHA, KUKWEPA KODI DOLA ZA MAREKANI MIL 112 UMEFIKIA HATUA GANI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya dola za Marekani milioni 112 dhidi ya aliyekuwa rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na wenzake waeleze upelelezi wa kesi hiyo, umefikia hatua gani.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina amesema hayo leo Mei 17,2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili  ya kutajwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon kudai upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika wanasubiri taarifa kutoka nje ya nchi ambako wameomba msaada.

Kutokana na taarifa hiyo, Wakili Wa utetezi Nyika  ameomba upande wa mashtaka waeleze bado muda gani upelelezi huo utakamilika kwani mara kwa mara wamekuwa wakisema upelezi bado kuna maeneo bado hawajakamilisha lakini hawasemo ni maeneo gani.

Hata hivyo baada ya maelezo hayo kutolewa  Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 30, mwaka huu na ameutaka upande wa mashtaka siku hiyo kueleza upelelezi umefikia hatua gani
Mbali na Mwanyika washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo,  Mkurugenzi mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhuku Assa Mwaipopo,kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.Wanakabiliwa na tuhuma za mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya dola za Marekani milioni 112.

Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama , mashtaka saba ya kughushi , mashtaka 17 ya Utakatishaji wa fedha, Kuwasilisha nyaraka  za uongo  kwa  Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa, mashtaka nane ya kukwepa kodi na shtaka moja la kutoa Rushwa.

Wanadaiwa, kutenda makosa hayo kati ya Aprili 11, 2008 na Juni 30,2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maeneo mengine ambayo washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo ni katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.
Aidha mshtakiwa Mwanyika  na Lugendo, wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutoa tamko la uongo kwa kamishna Generali wa TRA huko Biharamulo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi ya dola 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Pia Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kati ya Desemba 2009 na Desemba 31 2018 katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi ya Tanzania kwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani, walisaidia mgodi wa North Mara kuhamisha fedha kiasi cha dola 374,243,943,45 huku wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kughushi na kukwepa kodi.

Wanadaiwa kati ya Novemba 2,  2012 na Novemba 27, 2015 huko Shinyanga walitoa rushwa ya Sh. 718,520,001.76 kwa Hussein Kashindye aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi makosa ya jinai wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kumshawishi ili aweze kuachana na uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyokuwa yametendwa na Mgodi wa Bulyanhulu.

Katika shtaka la kughushi washtakiwa hao wakiwa na nia ya ulaghai waligushi mkataba wa mkopo wakitaka kuonyesha kwamba Aprili 30, 2014 Kampuni ya Pangea limited ilikubali kukopa dola za Marekani 90,000,000 ikiwa na riba kutoka benki ya kimataifa ya barrick huku wakijua kuwa siyo kweli.

Wakati katika shtaka la kutoa nyaraka ya uongo, mshtakiwa Mwanyika anadaiwa Aprili 30, 2018 huko BOT iliyopo wilaya ya ilala, kwa makusudi aliwasilisha  nyaraka ya uongo ya mkopo baina ya kampuni mgodi wa Bulyanhulu na Barrick international bank Corp kwa madhumuni ya kuonesha kuwa, kati ya June 2001 na Desemba 13, 2007 Bulyanhulu walijipatia mkopo usio na faida wa dola za Marekani 416,100,000 kutoka Barrick.

SERIKALI KUPITIA UPYA MASHAMBA YALIYOFUTWA NA RAIS KILOSA

$
0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema wizara yake itapitia upya mashamba yote yaliyofutwa na Raisi katika wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro.

Lukuvi amesema hayo leo tarehe 16 Mei 2019 katika kata ya Chanzulu tarafa ya Kimamba wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro alipozungumza na wananchi wa kata hiyo wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa Ardhi katika wilaya hiyo ikiwa ni jitihada za wizara kumaliza migogoro ya ardhi nchini.

Waziri Lukuvi alisema, katika maeneo mbalimbali yapo mashamba yaliyofutwa na Raisi lakini hayajawekewa utaratibu wa kuyatumia na hivyo kutoa fursa kwa wajanja wachache kujigawiwa na mengine kuyauza kwa wananchi bila kufuata utaratibu.

Alisema katika kuhakikisha mashamba yote yaliyofutwa na Rais katika wilaya ya Kilosa na kuzua mgogoro baina ya wananchi na wamiliki wizara yake imeamua kupeleka timu kutoka wizarani kwa ajili ya kuyafanyia uhakiki mashamba yote yaliyofutwa katika wilaya ya Kilosa.

Kwa mujibu wa Lukuvi timu hiyo inajumuisha Kamishna wa ardhi nchini Mary Makondo, Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Samweli Katambi, Mthamini Mkuu wa Serikali Evalyne Mugasha, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Kati Ezekiel Kitlya na Wataalamu kutoka idara za Mipango Miji Wizarani.

Alisema, uamuzi wa kwenda na timu kutoka Wizarani unalenga kumaliza kabisa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo hasa baada ya kubaini ofisi za wilaya na mkoa wa Morogoro kushindwa kutatua mgogoro huku viongozi wa wake wakituhumiwa.

Waziri wa Ardhi alitaja kazi kubwa itakayofanya timu hiyo kuwa ni kupitia mashamba 15 yaliyofutwa na raisi sambamba na kufufua mipaka ya mashamba hayo na kazi hiyo itafanywa kwa na ushirikiano wa ngazi za wilaya.

" tutayapitia mashamba yote yaliyofutwa na raisi na kujua kilichomo ndani yake na timu ya uhakiki niliyokuja nayo itanilitea mapendekezo ya namna ya kutumia mashamba na mengine watapewa wanaostahili na si kila mtu atapewa" alisema Lukuvi

Huku akishangiliwa na wananchi wa Chanzulu Lukuvi alisema, wale wote waliojimilikisha mashamba yaliyofutwa na Rais watanyang'anywa na kupatiwa wanaostahili na mengine yatatolewa kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa ajili ya kupatiwa wawekezaji.

Mkuu wa Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira katika halmashauri ya Kilosa Ibrahim Mndembo alisema, Jumla ya mashamba 25 yenye ukubwa wa ekari 23,596 kwenye maeneo ya Msowero, Magole na Chanzulu katika wilaya ya Iringa Kilosa yamebatilishwa umiliki baada ya wamiliki wake kushindwa kuyaendeleza ambapo kati ya mashamba hayo mashamba 15 yalibatilishwa miliki zake katika kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya tano.

Mashamba yenye mgogoro na wananchi katika wilaya ya Kilosa ni Noble Agriculture Enterprises, Magereza dhidi ya wananchi wa Mabane, Mbigiri na Mabwegere, Chadulu Estate, Shamba la Swai dhidi ya wananchi wa Ilonga na shamba la Mauzi Estate Malangali.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati), akifafanua jambo katika Kikao cha kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi Mjini Mrogoro, ambacho pia kilichohudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu). Kikao hicho pia kilihudhuriwa na maafisa wa Magereza na Manispaa ya Morogoro. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephen Kebwe (katikati). 

MAKAMBO KUTIMKIA NCHINI GUINEA.

$
0
0
MSHAMBULIAJI na nyota wa klabu ya Yanga sc Heritier Makambo inasemekana kuna tetezi za sintofahamu kuwa ametimkia nchini Guinea ambapo amesaini kandarasi ya miaka 3 na klabu ya Horoya  Athletic inayocheza ligi kuu nchini humo kwa ada ya 230,000,000 za kitanzania. 

Kwa mujibu wa ukurasa wa Instagram wa Yanga  umesema kuwa Makambo mwenye  umri wa miaka 25 amesaini  mkataba wa kuitumikia klabu hiyo miaka 3 na kupewa nafasi  kubwa ya kufanya makubwa  kwenye ligi kuu ya nchi hiyo hasa baada ya kuonyesha mafanikio makubwa akiwa kwenye kikosi cha Yanga. 

Makambo aliebakiza mkataba mmoja wa kuitumikia Yanga  uliokuwa umalizike mwakani 2020.

Hata hivyo  mwenyekiti wa  klabu ya Yanga  Mshindo Msolla ameweka wazi kwa   taarifa hizo zinazoleta sintofahamu kwa kueleza kuwa mshambuliaji huyo aliondoka na kocha Mwinyi Zahera  Mwinyi nchini Guinea  kuonana na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya  na ambapo angefaulu vipimo hivyo alipaswa kurudi nchini kuja kufanya mazungumzo na uongozi. 

"Ni kweli Makambo aliondoka juzi na mwalimu Zahera  kuelekea nchini humo kwa ajili ya vipimo vya afya kwa klabu ya Horoya, hivyo basi tunawasubiri warudi tuitazame ofa yao kisha tufanye biashara"amesema Mwenyekiti huyo. 

Aidha Msolla amesisitiza  kuwa "hizo taarifa za kutambulishwa rasmi sizielewi ila mwalimu akirudi tutatizama ofa yao na kulingana na klabu nyingine nyingi  zinazomtaka mchezaji huyo kisha tufanye maamuzi"

Nyota  huyoa ambaye ni  raia wa Congo alisajiliwa na klabu ya Yanga  ya Tanzania akitokea  Fc Lupopo ya nchi kwao kwa dau lisilopungua milioni 60 za kitanzanzania.
Mshabuliaji Herieter Makambo akiwa katika uzi wa Horoya Athletic klabu ya Guinea na viongozi wa timu hiyo amabapo inasemekana ameshasaini mkataba wa miaka 3 na klabu hiyo. 

Zaidi ya watoto 100 wafanyiwa uchunguzi wa macho Mloganzila.

$
0
0
Daktari wa macho wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Geofrey Josephat akitumia kifaa maalum kumfanyia uchunguzi mtoto sehemu ya nyuma ya jicho ili kubaini kama ana tatizo. Hospitali ya Mloganzila imefanya zoezi la uchunguzi wa macho bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya saratani ya jicho kwa watoto (Retinoblastoma). 
Mtaalam wa miwani Nestory Massawe akimpima uwezo wa kuona mbali mtoto Shamsa Mbegu.

Daktari Bingwa wa macho Suzan Mosenene (kulia) akimfanyia uchunguzi wa macho mtoto, huduma ya uchunguzi wa macho bure kwa watoto imefanyika Mei 16 hadi Mei 17, 2019.

Baadhi ya wazazi ambao wamewaleta watoto wao katika Hospitali ya Mloganzila kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa macho.






Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imefanya zoezi la uchunguzi wa macho bure kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya saratani ya jicho kwa watoto (Retinoblastoma).


Katika zoezi hilo ambalo limefanyika Mei 16 hadi Mei 17, 2019 zaidi ya watoto 100 wamehudumiwa ambapo baadhi yao wamekutwa na matatizo ya uoni hafifu, mzio na kovu kwenye macho.


Daktari Bingwa wa macho kutoka Muhimbili Judith Mwende amesema ugonjwa wa saratani ya jicho kwa watoto ni hatari na husababisha upofu na kifo endapo usipotibiwa mapema na wakati mwingine hulazimu kuliondoa jicho ili kuokoa  maisha ya mtoto.


Akifafanua Dkt. Mwende amesema takwimu za miaka mitatu za kutibu na kufuatilia ugonjwa wa saratani ya jicho  kwa watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) takribani asilimia 60-70 ya watoto hao huwa wako kwenye hatua mbaya za ugonjwa.


Hali hiyo husababisha asilimia 50-60 kupoteza maisha kwa sababu ya kuchelewa kufika kupata huduma inayostahili na kwa wakati.


Ametaja  sababu za kucheleweshwa hospitalini ni familia kutokufahamu dalili za  ugonjwa  na hatari zake, wahudumu wa afya ya msingi kuchelewesha rufaa kwa kutofahamu dalili za ugonjwa, familia kukosa nauli kufuata matibabu pindi wakipewa rufaa , familia kutafuta matibabu mbadala mpaka wakiona hatua za mwisho za ugonjwa na kukataa mapendekezo ya wataalam hasa kuliondoa jicho pale inapohitajika ili kunusuru maisha ya mtoto


Dalili za mwanzoni za saratani ya jicho kwa watoto ni weupe kwenye mboni ya jicho ambao unaonekana kirahisi kwenye giza au mtoto akipigwa picha na flush, kengeza, jicho kuvilia damu kuwa jekundu, kubadilika rangi au kuuma.

STARS KUANZA NA SENEGAL AFCON.

$
0
0
Na Agness Francis, Michuzi Tv

UONGOZI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) umetangaza rasmi gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali ya Africa (AFCON) inayotarajia kuanza juni mwaka huu zitakazofanyika  nchini Misri.

Ambapo shirikisho hilo limetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali.

Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la 1 ni dola za kimarekani 29,tiketi za daraja la 2  ni 18 na tiketi za daraja la 3  kwa dola za kimarekani 6.

Hatua hiyo (Taifa Stars)  itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria. 

Hatua ya robo fainali kwa gharama ya tiketi daraja 1 kwa dola za kimarekani  35  kwa daraja la 2 ni 24 na  la 3  ni 12, ikiwa hatua ya nusu fainali dalaja  la 1 ni  dola 59, la 2 ni 29 na la 3  kwa dola  18.

Wakati mchezo wa mshindi wa 3  itakua   daraja la 1 kwa dola 24 za kimarekani,  la 2 na la 3 kwa  12,ambapo  kwa mchezo wa fainali daraja la 1 n dola 106,la 2 44, na  la 3 ni 24.

Aidha Afisa habari na mawasiano TFF Cliffold Ndimbo amesema kuwa kwa yeyote mwenye nia ya kununua tiketi hizo za AFCON awasiliane na TFF mapema kabla ya kufungwa kwa muda wa maombi hayo. 

WALIPA KODI KAGERA, ZINGATIENI ELIMU MLIYOIPATA ILI KUTIMIZA WAJIBU WENU.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi Tv - Kagera.

Wananchi na walipa kodi Mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia Elimu ya kodi waliyoipata katika wiki ya Elimu kwa mlipa kodi, na kuwa tayari kupokea mabadiliko mbalimbali ya kodi na usimamizi wake Kwa masilahi ya Taifa.

Wito huo umetolewa  Wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipa Kodi, ambapo Mkoani Kagera yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru Manispaa ya Bukoba, Mei, 17 yakihudhuriwa na wananchi, wafanyabiashara, wanafunzi na wadau mbalimbali.

Katika hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera, iliyosomwa kwa niaba yake na Mwakilishi katika maadhimisho hayo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Ndg. Projestus Rubanzibwa ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera  kuendelea kutoa Elimu na Hamasa kwa Umma ili walipa kodi waendelea kulipia kodi zao sahihi na Kwa wakati, bila shurti, kutoa Elimu ya Ufahamu ya mabadiliko mbalimbali ulipaji kodi kupitia simu, matumizi ya mashine za Efds hii itachangia kwa mlipa kodi kwa mzalendo na kutimiza wajibu wake kwa maendeleo ya Taifa.

Awali akitoa salaam zake kwa niaba ya Meneja Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoani Kagera, amesema changamoto kubwa miongoni mwazo ni pamoja na mwitikio mdogo wa wafanyabiashara katika Elimu ya ulipaji kodi, matumizi kidogo ya EFDs, wananchi kutoomba lisiti wanaponunua bidhaa.

Maadhimisho hayo yaliyoanza Mei 13, 2019 yenye kauli mbiu ya "Karibu Tukuhudumie" yameambatana na usikilizwaji wa kero, ushauri na maoni kutoka kwa wananchi na walipa kodi, huku yakipambwa na burudani safi kutoka kikundi cha KAKAU BAND.
 Mwakilishi wa Mgeni Rasmi, Kaimu RAS-Kagera, Ndg. Projestus Rubanzibwa akionesha Risti yake aliyonunulia bidhaa, wakati akizungumza na Wananchi, wadau na walipa Kodi, kabla ya kusoma hotuba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria kilele cha Wiki ya Elimu kwa Mlipa kodi wakiendelea kufuatilia maadhimisho hayo katika Viwanja vya Uhuru Platform Bukoba Manispaa.
 Pichani ni maafisa Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera kutoka Wilaya mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.
 Pichani ni mfanyabiashara Ndg. John Jackson Nkwama, akiendelea kupata ufafanuzi juu ya masuala ya ulipaji Kodi kutoka kwa Afisa Kodi Mkoa wa Kagera Ndg. Fravian Mgore katika maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa mlipa kodi.
 Baadhi ya wananchi, wafanyabiashara na wadau wakiendelea kuhudumiwa mapema Mei 17, katika viwanja vya Uhuru Platform mjini Bukoba katika maadhimishobya Wiki ya Elimu kwa mlipa kodi.
 Pichani ni Bwn. Frank Mbeikya akitoa ushauri wake kwa Mamlaka ya Mapato Nchini juu ya kuangalia upya Kodi ya uingizwaji bidhaa nchini hasa maeneo ya Mpakani.
Kikundi cha burudani KAKAU BAND wakinogesha maadhimisho hayo kwa wimbo maalum juu ya Elimu kwa mlipa kodi. 

Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Sarahawi awasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Waziri Kabudi.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akipokea nakala za hati za utambulisho za Mhe. Mahayub Buyema Mahafud, Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sarahawi nchini Tanzania. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Bwana. Mahayub Buyema Mahafud, Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Sarahawi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA SEMINA YA WANAHISA WA BENKI YA CRDB, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay pamoja na Mkurugenzi  mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, kwa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa Simba, AICC jijini Arusha leo. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Ally Laay.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha. Katikati ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichele aliyemuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa wakati alipowasili katika ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichele akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango, wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.





















































































Profesa Kabudi akutana na mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mikel Kafando ambaye ni Rais Mstaafu wa Burkina Faso na Mjumbe Maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi. 
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Mikel Kafando ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Burkina Faso na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NDANI AFUNGUA KIKAO KAZI CHA WAKUU WA MAGEREZA YOTE TANZANIA BARA

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kushoto) akiwasili katika Viwanja vya NaneNane, Mkoani Morogoro tayari kwa Ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 – 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu akihutubia katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 – 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro.  Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Mei 17 – 18, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro.
 Baadhi ya Wakuu wa Magereza wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu(hayupo pichani).
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Usalama, Mhe. Salum Rehani(vazi la kiraia) akiongea katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, leo Mei 17, 2019 katika Ukumbi wa Magereza Mkoani Morogoro. Kushoto kwake ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Meja Jenerali, Jacob Kingu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Magereza toka katika vituo mbalimbali nchini (waliosimama) baada ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, leo Mei 17, 2019. Wa pili toka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Phaustine Kasike(Picha na Jeshi la Magereza).
                                                 

BALOZI SEIF AWAASA WANANCHI KUWATUNZA WAZEE WAASISI WA ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wazee Waasisi wa Zanzibar wataendelea kuwa ngao ya Taifa ambayo Viongozi wa sasa pamoja na Wananchi na Kizazi Kipya wana wajibu wa kuwatunza katika maisha yao ya kila siku.

Alisema ngao hiyo inatokana na kazi kubwa waliyoifanya wakati wa harakati za kupigania Ukombozi wa Taifa hili ambapo kwa sasa Viongozi waliopo madarakani pamoja na Wananchi wanaendelea kula matunda ya Uhuru uliotokana na Wazee hao.

Balozi Seif alitoa kauli hiyo iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed kwenye Futari ya pamoja iliyoandaliwa kwa ajili ya Wazee wanaohifadhiwa katika Nyumba za Serikali zilizopo Welezo Wilaya ya Magharibi “A”.

Alisema Kizazi cha sasa wakati kikiendelea kufaidika na matunda hayo lakini kwa upande mengine wana wajibu wa kulinda na kuendeleza Uhuru huo utakaokuwa kielelezo cha Heshima ya muda wote wa Wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba.

Mapema Mchana Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikabidhi msaada wa Tangi la kuhifadhia Maji, Mashine yake pamoja na Luva ya kusafishia Msikiti wa Ijumaa wa Umbuji uliopo Wilaya ya Kati Mkoa Kusini Unguja.

Msaada huo unafuatia ahadi aliyoitoa wakati wa ufunguzi Rasmi wa Msikiti huo alipomuwakilkisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein kwenye Ufunguzi wakeMiaka michache iliyopita nyuma.

Akizungumza na Uongozi wa Msikiti huo Balozi Seif alisema ahadi ni deni kitu ambacho alilazimika kukitekeleza ingawa kimechukuwa muda mrefu kutokana na sababu mbali mbali yakiwemo majukumu yaliyotangulia ya ahadi nyengine za awali.

Akipokea msaada huo kwa Niaba ya Uongozi wa Msikiti huo Sheha wa Shehia ya Umbuji Bwana Muhamad Mrisho Juma alisema Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Umbuji walilazimika kuwa na subra kutokana na ahadi hiyo kutokana na kazi kubwa inayomkabili Balozi Seif ya kulitumikia Taifa kila siku .

Sheha Mrisho alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba msaada huo muhimu kwao utatumika kwa lengo lililokusudiwa la kuombwa kwake ili uendelee kutoa huduma katika kipindi kirefu kijacho.

Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alikutana kwa mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi Watatu wa Kampuni ya Kimataifa ya Huduma za Afya na Uwekezaji kutoka Nchini Uturuki hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Katika mazungumzo yao Kiongozi wa Ujumbe huo Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya huduma za Afya na Uwekezaji {KAYI} Bwana Batur Engin alimueleza balozi Seif kwamba Taasisi hiyo yenye Wafanyakazi 600 inatoa huduma katika Mataifa 200 Duniani.

Bwana Batur alisema Wahandisi wa Kampuni hiyo huendeleza kazi za Miundombinu ya Ujenzi wa Hospitali kubwa za kisasa zenye vifaa vya Teknolojia mpya unaofanywa katika mfumo wa ubia.

Alisema zipo Hospitali kubwa zilizojengwa katika Miji ya Paris Nchini Ufaransa, Istambul Uturuki yenyewe pamoja na Hospiatli Kubwa zilizopo Nchini Kenya zinazotarajiwa kukamilika Ujenzi wake hivi karibuni.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Huduma za Afya na Uwekezaji alieleza pia Kampuni yake huendesha Miradi mengine ya Miundombinu katika Sekta ya Mawasiliano kwa ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Bara bara Kubwa za Kisasa pamoja na Mahoteli Makubwa.

Alifahamisha kwamba mtazamo wa Kampuni yake kwa sasa umezingatia kuwekeza katika Visiwa vya Zanzibar Miradi zitakayoweza kutoa huduma katika Mwambao wa Afrika Mashariki pamoja na Ukanda Mzima wa Nchi za Sahara.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari inaendeleza Miradi mikubwa ya Ujenzi wa Hospitali ya Kisasa katika eneo la Binguni pamoja na mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Mizigo katika eneo la Mpiga Duri.

Balozi Seif aliueleza Ujumbe wa Viongozi hao kutoka Uturuki kwamba Kampuni yao ina fursa ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uimarishaji wa Ujenzi wa Hospitali hiyo inayotarajiwa pia kuwa na Kitengo cha Mafunzo ya Afya.

“ Inapendeza kuona Ujenzi wa Hospitali Kubwa ya Binguni inafanana na mtazamo wa Kampuni hiyo katika uimarishaji wa Miradi yake katika Huduma za Afya na Uwekezaji Vitega Uchumi”. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba Serikali hivi sasa ina mtazamo wa uwepo wa Hospitali ya Kimataifa itakayolenga kutoa huduma kwa Watalii pamoja na wageni wanaoingia Nchini kwa safari za kimatembezi.

Balozi Seif alisema mtazamo huo umekuja kutokana na Zanzibar kwa sasa kuimarika katika Sekta ya Utalii inayoweza kuchukuwa nafasi ya kwanza ya Uchumi wake.

Alisema kuimarika kwa huduma za Afya katika Sekta ya Utalii kutaipa hadhi Zanzibar kurejea katika hadhi yake ya kutoa huduma mbali mbali za kibiashara ndani ya Bahari ya Hindi kama ilivyokuwa ikifanya karne nyingi zilizopita kutokana na mazingira yake ya kuwa kituo cha Biashara enzi hizo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi msaada wa Tangi la kuhifadhia Maji safi, Mashine ya kusukumuia Maji pamoja na Luva ya kusafishia Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji akitekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa Ufunguzi rasmi wa Msikiti huo Miaka michache iliyopia.
 Sheha wa Shehia ya Umbuji Wilaya ya Kati Bwana Muhamad Mrisho Juma akitoa shukrani kwa niaba ya Ungozi wa Msikiti huo kutokana na msaada huo adhimu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa shukrani kwa niaba ya Balozi Seif mara baada ya futari ya pamoja na Wazee wanaohifadhiwa Nyumba za Serikali Welezo.
Balozi Seif akiagana na Wazee wanaohifadhiwa katika Nyumba za Serikali zilizopo Welezo mara baada ya kufutari nao pamoja akiendeleza utaratibu wake aliojipangia ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Picha na – OMPR – ZNZ.

NAFASI ZA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.

$
0
0



Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa kuomba nafasi ya ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.

Ajira hizo ni :-

Afisa Msaidizi Programu ya Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (Assistant Programmes Officer – Monitoring and Evaluation Unit) na

Meneja Utafiti wa masuala ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Research Manager-Economic, Youth and Sustainable Development).

Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hizo za ajira zinapatikana kwa kupitia tovuti http://thecommonwealth.org.jobs.

Mwisho wa kutuma maombi ya nafasi hizo ni tarehe 23 Mei, 2019.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

MEMBE AMTOLEA UVIVU ROSTAM AZIZ , AMWAMBIA WAMEKATWA MIKIA

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amesema yeye na Kada wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rostam Aziz wamekatwa mikia huku akimshauri ajikite katika kujadili masuala ya uchumi wa nchi.

Membe amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waaandishi wa habari ambapo ametumia nafasi hiyo kumjibu Rostam baada ya siku za karibuni kumshambulia.

"Kwanza niseme hivi, napata kigugumizi kumjibu rafiki yangu Rostam , lakini Rostam ni mchumi na nikikutana naye nitamshauri kwamba anafanya vizuri katika jamii ya Watanzania anapozungumzia uchumi.

"Rostam inabidi awe anazungumzia masuala ya nchi na sio kujikita kuzungumza mambo binafsi. Kwa levo yetu tunatakiwa kuzungumzia masuala ya kitaifa. "Kwa kuwa Rostam ni mchumi mzuri sana , tunapaswa kujadili kwanini uchumi wetu uko hapa ulipo.Kwanini wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanafunga biashara zao,"amesema Membe.

Amesisitiza kuwa "Rostam ni mchumi, sasa huu ndio ushauri wangu kwake, ajielekeze kwenye uchumi. Rostam wewe ni mwenzetu, sisi tumekatwa mikia, hata ukijitahidi vipi mkia wako ni mfupi". Ameongeza anamshauri wawe wanazungumza vitu ambavyo wakizungumza binadamu wanawaheshimu.

"Asijifanye mtoto mzawa badala ya kukubali Rostam na mimi ni watoto wakambo,"amesema Membe huku akimsisitiza ajikite kwenye masuala ya uchumi.

Inadaiwa kuwa Rostam alitoa kauli ya kumzungumzia Membe kuhusu uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwakani huku akimhusisha na masuala ya kugombea urais.
Mh,Rostam Aziz

WAZIRI LUGOLA AWA MBOGO KWA POLISI WALIOWAFANYIA VURUGU WAWEKEZAJI KIWANDA CHA TUMBAKU MOROGORO

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa (kulia), wakati Waziri huyo alipofika Kiwandani hapo mjini Morogoro, kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya Viongozi Wakuu wa Kampuni hiyo ambao wanadaiwa kufanyiwa vurugu na Polisi wane waliofika ofisini hapo kwa lengo la kuwakamata kwa nguvu bila kufuata utaratibu. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa, wakati alipokua anatoa malalamiko yake akidai Polisi Mkoani Morogoro kuingia ndani Kiwanda chake na kufanya vurugu kwa kulazimisha kuwakamata kwa nguvu bila kufuata utaratibu viongozi wa Kampuni hiyo. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa, alipokua anashirikiana na Mkurugenzi mwenzake wa Kampuni hiyo, kutoa malalamiko yao kwa Waziri huyo kuhusu Polisi Mjini Morogoro kuingia ndani Kiwanda chao na kufanya vurugu kwa kulazimisha kuwakamata kwa nguvu bila kuwa na kosa lolote.  Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


MOI YATOA VYETI KWA WAHITIM WA KUTOA DAWA ZA USINGIZI

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na wahitimu 100 wa mafunzo ya kutoa dawa za usingizi ( Anaesthesia) kutoka katika Hospitali za Mikoa mbalimbali ambao walikua wakipata mafunzo Taasisi ya Mifupa MOI pamoja Hospitali ya Muhimbili.
Muwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Mtemi Buriani (kushoto) akimkabidhi mhitimu cheti cha kuhitimu mafunzo maalum ya kutoa dawa za usingizi yaliyohitimishwa leo.
Mkurugenzi wa Tiba wa MOI Dkt Samuel Swai akimkabidhi mhitimu cheti cha kuhitimu mafunzo maalum ya kutoa dawa za usingizi yaliyohitimishwa leo.
Ibrahim Mwita ambaye ni kiongozi wa wahitimu akitoa neno la shukrani kwa Serikali, Taasisi ya MOI pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuwawezesha kupata mafunzo maalum ya kutoa dawa za usingizi.
Wahitimu wa mafunzo maalum ya kutoa dawa za usingizi wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao pamoja na viongozi wa juu wa Taasisi ya Mifupa MOI na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Watendaji lazima wawajibike katika ukusanyaji wa kodi -Kaimu Mkurugenzi Temeke

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imesema kuwa katika kupata maendeleo ya nchi lazima Watendaji wawajibike katika ukusanyaji wa mapato.

Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Rugambwa Banyikila wakati mafunzo kazi kwa Watendaji Kata na Mitaa yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato nchini Mkoa wa Temeke kwa ajili ya uhakiki wa nyumba kwa Mkoa huo.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano katika miradi inayotekeleza asilimia kubwa inatokana na hivyo hakuna sababu ya kumuangusha Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Banyikila amesema Watendaji wa Kata na Mitaa wametakiwa kuorodhesha nyumba ili kuweka takwimu na kurahisisha katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na nyumba hizo.

Amesema TRA iko imara hivyo Manispaa itatoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki nyumba kurahisisha ukusanyaji wa kodi ya majengo.

Nae Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke Gamaliel Mafie amesema kuwa maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa watarahisha katika ukusanyaji kodi ya majengo kutokana na kuwa takwimu za nyumba.

Amesema kuwa serikali imeacha utegemezi wa misaada kwa asilimia kubwa kutokana na ukusanyaji mapato ya ndani.Mafie amesema kuwa nyumba ambazo wameuziana na kuhamisha umiliki nyumba hizo na kusomeka majina ya umiliki mpya.

Aidha amesema kodi ndio zinaendesha nchi katika miradi pamoja na utoaji wa huduma za kijamii."Kodi ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi kila mtu anawajibu wa kulipa kodi ili zitumike kuleta maendeleo hayo katika huduma za kijamii"amesema Mafie.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke  Rugambwa Banyikila akizungumza na Watendaji wa Kata na Mitaa wa Halmashauri za Temeke na Kigamboni kuhusiana na Watendaji hao kuorodhesha nyumba katika maeneo hayo.
Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke Gamaliel Mafie akizungumza na Watendaji wa Kata na Mitaa kuhusiana na uhakiki wa nyumba katika kurahisisha ukusanyaji kodi za majengo.
 Baadhi ya maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa katika mafunzo namna ya uhakiki wa Nyumba.

JAFFO AWAONGOZA WAKUU WA MIKOA, WILAYA NA WAKURUGENZI KUTEMBELEA MRADI WA SGR, WAMPIGIA SALUTI JPM

UFAFANUZI- Mgodi wa Nyamongo kupigwa faini ya Bilioni 5.6

$
0
0
Serikali kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), imeupiga faini ya shilini bilioni 5.6 mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, kwa kushindwa kudhibiti bwawa la maji yenye sumu na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wanaozunguka mgodi huo.
Maamuzi hayo yalitolewa jana baada ya Waziri wa Madini, Doto Biteko pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kufanya ziara mgodini hapo, wakiambatana na Watendaji mbalimbali.
Faini hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Samuel Gwamaka baada ya ripoti ya Kamati Huru iliyoundwa kwa ushirikiano wa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) pamoja na Wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam kubaini mgodi huo umekuwa ukitiririsha maji yenye sumu kwa zaidi ya miaka 10 huku ukitoa taarifa zenye udanganyifu kuhusiana na maji hayo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba (kushoto), pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati) wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa Kamati Huru iliyoundwa kuchunguza malalamiko ya utirishaji wa maji yenye sumu kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Sehemu ya eneo linalokusanya maji yenye sumu kwa ajili ya kuyasukuma kwa mashine kuyarudisha kwenye bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu katika mgodi wa Acacia North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba pamoja na Waziri wa Madini Doto Biteko wakiwa wameambataba na viongozi mbalimbali kukagua mazingira mbalimbali yanayozunguka mgodi wa Acacia North Mara.
Viongozi hao wakijionea mtaro uliochimbwa na mgodi wa Acacia North Mara kwa ajili ya kunasa maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa la kuhifadhia maji/ tope sumu.
Sehemu ya maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa la maji yenye sumu kutoka mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Sehemu ya dimbwi la maji yenye sumu yanayotiririka kutoka kwenye bwawa (TFS) la kuhifadhia maji hayo.
Baadhi ya askari wanaoimarisha ulinzi katika mgodi wa Acacia North Mara wilayani Tarime.
Tazama Video hapa chini

LIBENEKE LA YANGA TV

Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images