Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

SAADANI NATIONAL PARK TRIP ON IDDI PILI


RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA JUMA ZUBERI HOMERA KUWA MKUU WA MKOA WA KATAVI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt. John Pom be Magufuli akimuapisha Mhe. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Mei 16, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera akila kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMIS 16/05/2019

SAVE THE CHILDREN,KIWOHEDE WAENDESHA TAMASHA LA MWANAUME JASIRI KAHAMA

0
0
Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Shinyanga Save The Children na KIWOHEDE, yameendesha Tamasha Mwanaume Jasiri la Kupinga Mila na Desturi kandamizi katika Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama, kwa lengo la kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.

Tamasha hilo limefanyika Alhamis Mei 16, 2019 katika kijiji cha Kangeme Kata ya Ulowa, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Afisa Maendeleo Jamii wa halmashauri ya Ushetu Aminael John akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha. Tamasha hilo liliambatana na kauli mbiu isemayo “Mwanaume Jasiri ana mlinda mtoto wa kike dhidi ya mimba na ndoa za utoton”.

 Akizungumza kwenye Tamasha hilo mgeni rasmi Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Ushetu Aminael John, amewataka wanaume kuacha kuendekeza mila na desturi kandamizi zilizopitwa na wakati, ambazo zimekuwa zikichangia kuendelea kuwepo kwa tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Amesema wanaume wanatakiwa kubadilika na kutambua umuhimu wa elimu, kwa kumlinda mtoto wa kike dhidi ya matukio hayo ya kupewa ujauzito na kuolewa ndoa za utotoni, ili waweze kutimiza malengo yao na kuja kuwasaidia hapo baadae.

 “Natoa wito kwa wanaume wa kata hii ya Ulowa na Ushetu kwa ujumla, acheni kuendekeza mila na desturi kandamizi ambazo zimekuwa zikiwanyima haki watoto wa kike kuweza kutimiza malengo yao, na kuishia kupewa ujauzito ama kuolewa ndoa za utotoni na kuacha shule,”amesema John.

 “Tambueni kuwa mtoto anapopata elimu ataweza kuja kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini au kupata ajira yake nzuri, ambapo atawasaidia katika maisha yenu kuliko hata hao ng’ombe mnawategemea na kuona wa thamani sana, na kuamua kuwaozesha ndoa hizo za utotoni kwa tamaa ya kupata mifugo,”ameongeza.

 Naye Mtendaji wa kata ya Ulowa Geofrey Philip, ametaja takwimu za wanafunzi ambao walikatishwa masomo mwaka jana (2018) kwa sababu ya kupewa ujauzito kuwa walikuwa 10, ambapo kwa mwaka huu (2019) tayari wameshapewa mimba wanafunzi wawili. Aidha Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga Alex Enock, amesema wameanzisha mradi huo katika kata nane za halmashauri hiyo ya Ushetu, kwa lengo la kutokomeza mila na desturi kandamizi, ambazo zimekuwa kikwazo katika kumaliza tatizo la mimba na ndoa za utotoni. 

Amezitaja kata hizo kuwa ni Ulowa, Ushetu, Ukune, Kisuke, Uyogo,Kimampula, Bulungwa, na Ulewe, kwa kutoa elimu mbalimbali ambazo zinahusu malezi bora kwa watoto, kwa kushiriki wazazi wa pande zote mbili baba na mama na siyo kumwachia mzazi mmoja, likiwamo pia na suala la kutokomeza mila na desturi kandamizi.

 Kwa upande wake, Mratibu wa mradi huo wa kupinga mila na desturi kandamizi kutoka Shirika la KIWOHEDE Victor Reveta, ambao ndiyo wanatekeleza mradi huo kwenye kata nane za halmashauri ya Ushetu, amesema ulianza mwaka 2017 na unatarajiwa kukoma mwaka huu 2019, ambapo pia wamewajengea uwezo wanaume 25 kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa wanaume wenzao dhidi ya kutokomeza tamaduni hizo ambazo zimeshapitwa na wakati. TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI


Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Aminael John akizungumza kwenye Tamasha la Mwanaume Jasiri la Kupinga Mila na Desturi Kandamizi ambazo zimekuwa zikichangia mimba na ndoa za utotoni kuendelea kuwepo kwenye kata ya Ulowa na kuwaasa wanaume waachane na mila hizo. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Afisa maendeleo wa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Aminael John, akielezea madhara ya mimba na ndoa za utotoni kuwa athari zake kuwa ni ongezeko la vifo vitokanavyo na uzazi, kuugua fistula, pamoja na magonjwa mengine ya ikiwa via vyao vya uzazi vinakuwa bado havijakomaa. Kaimu Mkurugenzi kutoka shirika la Save The Children mkoani Shinyanga Alex Enock akielezea malengo ya mradi huo wa kutokomeza mila na desturi kandamizi kwenye halmashauri hiyo ya Ushetu wilayani Kahama, kuwa ni kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi kutoka Shirika la KIWOHEDE wilayani Kahama Victor Reveta akielezea namna wanavyoutekeleza mradi huo katika halmashauri ya Ushetu katika kata nane, kuwa ni utoaji wa elimu wa kupinga mila hizo, elimu ya malezi pamoja na kuunda vikundi vya Wanaume Jasiri ambao watakuwa mabalozi wa kutoa elimu ya kutokomeza mila kwa wanaume wenzao. Lenard Mboje akisoma risala kwa niaba ya Wanaume Jasiri 25 ambao wamejengewa uwezo wa kutoa elimu ya kupinga mila na desturi kandamizi kwa wanaume wenzao ,amebainisha kuwa kwa sasa kumeibuka mbinu mpya ya kuozesha wanafunzi ndoa za utotoni kwa kuweka ma Bibi harusi bandia ambao wemetimiza umri wa miaka 18, lakini kumbe muolewaji ni chini ya umri huo. Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga mila na desturi kandamizi ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni na kuweza kutimiza ndoto za mtoto wa kike kielimu. Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya kupinga mila na desturi Kandamizi, ili kumuokoa mtoto wa kike kielimu kwa kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Burudani ya uvutaji kamba ikitolewa kwenye tamasha hilo la mwanaume jasiri la kupinga mila na desturi kandamizi ili kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Burudani ikiendelea kutolewa kwenye Tamasha hilo kwa kukimbia mbio za kwenye magunia. Burudani ya kukimbia mbio na mayayi nayo ikitolewa kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri katika kata ya Ulowa. Mchezo wa kukimbiza kuku nao ulikuwepo ambao washindi walipewa zawadi zao. Mchezo wa kukimbiza kuku ukiendelea. Wasanii nao walikuwepo kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri la kupinga mila na desrturi Kandamizi, ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. Washindi walioshiriki michezo mbalimbali kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri wakiondoka na zawadi zao. Washindi walioshiriki michezo mbalimbali kwenye Tamasha hilo la Mwanaume Jasiri wakiondoka na zawadi zao. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU USAJILI WA MAGARI YANAYOSAMBAZA MAJISAFI

UONGOZI WA LIPULI WAKANA TAARIFA ZA KIHWELO KUIHUJUMU TIMU YAO

0
0
Uongozi wa klabu ya Lipuli unapenda kutumia nafasi hii kukanusha vikali ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaosambaa katika vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ukidai Makamu M/Kiti wa klabu hiyo Ayoub Kihwelo amekili kuwa baadhi ya viongozi wa klabu  wamejihusisha na njama za kuihujumu klabu katika michezo yake ya hivi karibuni ikiwemo mchezo dhidi ya Simba SC, Biashara United na Mbeya City. 

Ujumbe huo unadai Ayoub Kihwelo alikiri hayo katika moja ya mohojiano yao na vyombo vya habari ikiwemo redio Ebony Fm ya mkoani Iringa. 

Uongozi unapenda kusema taarifa iliyopo katika ujumbe huo ni uzushi wenye lengo la kuharibu mahusiano ya klabu na wadau wake ikiwemo wanachama na mashabiki wake na kwa muktadha huo uongozi unaomba ujumbe huo upuuzwe.

Uongozi pia unatoa tahadhari kwa wanaoendelea kusambaza ujumbe huo kwani umekwisha wasilisha suala hilo kwa mamlaka husika za makosa ya kimtandao ikiwemo jeshi la Polisi.

Kwa hali hiyo uongozi unaomba radhi kwa wanachama na mashabiki wake kutokana na kuzagaa kwa taarifa hiyo ya uzushi.

Asanteni kwa ushirikiano.

Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Lipuli, Clement Sanga

DKT. ABBASI- SERIKALI INAENDELEA NA MAJADILIANO BANDARI YA BAGAMOYO

0
0
Na Grace Semfuko, MAELEZO, DAR ES SALAAM


MKURUGENZI wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi  (pichani) amesema Serikali inaendelea na majadiliano kuhusu kuendelea na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani ili kuona kama inaweza kuwa na tija kiuchumi kwa upande wa Tanzania.

Dkt. Abbasi alisema Serikali ina uwezo wa kujenga bandari nyingi na kwa kuwa Tanzania ina ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari na kwamba bado majadiliano yenye tija kwa Taifa yanaendelea kufanywa baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.
“Serikali haijasema kuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari, tunaendelea na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, nchi yetu imejaliwa ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari kwa hiyo tuna uwezo wa kujenga Bandari nyingi tu, hii ya Bagamoyo si kweli kuwa imeachwa kuna mambo ya msingi tunayajadili na tusipofikia maamuzi tutaachana nayo” alisema Dkt Abbasi.
Kuhusu suala la uwekezaji wa vitu aliloulizwa kwenye kipindi hicho Dr Abbasi alisema Serikali haitaacha kuwekeza kwenye vitu kwa sababu vitu husaidia maendeleo ya watu, mfano afya, elimu na miundombinu mingine.
“Kwenye sekta ya madini tumekuachia fedha, dawa hospitalini tumeongeza na bei zimepungua, tumekuletea yote hayo lakini bado unasema huna pesa mfukoni, Serikali inafanya yote haya kuhakikisha kuwa uchumi wetu unaleta manufaa mapana kwa Taifa” alisema Dkt. Abbasi.
Kuhusu uhuru wa Habari na kufungia magazeti yasiyofuata sheria za uchapishaji Msemaji huyo wa Serikali alisema kuwa ofisi yake haikurupuki  kufungia magazeti, na kusema kuwa  ni magazeti  mitatu tu yalifungiwa kati ya 266 yaliyosajiliwa nchini na kuwataka wamiliki wa magazeti hayo kufuata sheria.
Kuhusu malamiko ya wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini ya kufunga biashara hizo kwa kisingizio cha kodi na tozo mbalimbali, Dkt. Abbasi alisema ni muhimu wakaelewa kwamba kwa sasa Serikali inapita katika kipindi cha mabadiliko na hakuna siku serikali haitadai kodi huku akieleza kuwa kodi nyingi zimepunguzwa hususan kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na uvuvi.
“kwanza tukubali tunapita kwenye kipindi cha mabadiliko, hakuna siku serikali haitadai kodi kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi hii, kuna dhana ilijengeka kuwa unaweza kufanya biashara bila kulipa kodi hiyo sasa haipo, lazima tuangalie changamoto ambazo zinakumba sekta mbalimbali mfano sekta ya kilimo, miufgo na uvubvi kulikuwa na kodi zaidi ya 150, serikali imefuta zaidi ya kodi 80 hadi 100” alisema Dkt Abbasi.

DKT. ABBASI- SERIKALI INAENDELEA NA MAJADILIANO BANDARI YA BAGAMOYO

0
0
Na Grace Semfuko,MAELEZO,
DAR ES SALAAM,

MKURUGENZI na Msemaji Mkuu wa, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali inaendelea na majadiliano kuhusu kuendelea na ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo Mkoani Pwani ili kuona kama inaweza kuwa na tija kiuchumi kwa upande wa Tanzania.

Dkt. Abbasi alisema Serikali ina uwezo wa kujenga bandari nyingi na kwa kuwa Tanzania ina ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari na kwamba bado majadiliano yenye tija kwa Taifa yanaendelea kufanywa baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji wa mradi huo.

“Serikali haijasema kuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni hatari, tunaendelea na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, nchi yetu imejaliwa ukanda mkubwa wa ufukwe wa bahari kwa hiyo tuna uwezo wa kujenga Bandari nyingi tu, hii ya Bagamoyo si kweli kuwa imeachwa kuna mambo ya msingi tunayajadili na tusipofikia maamuzi tutaachana nayo” alisema Dkt Abbasi.

Kuhusu suala la uwekezaji wa vitu aliloulizwa kwenye kipindi hicho Dr Abbasi alisema Serikali haitaacha kuwekeza kwenye vitu kwa sababu vitu husaidia maendeleo ya watu, mfano afya, elimu na miundombinu mingine.

“Kwenye sekta ya madini tumekuachia fedha, dawa hospitalini tumeongeza na bei zimepungua, tumekuletea yote hayo lakini bado unasema huna pesa mfukoni, Serikali inafanya yote haya kuhakikisha kuwa uchumi wetu unaleta manufaa mapana kwa Taifa” alisema Dkt. Abbasi.

Kuhusu uhuru wa Habari na kufungia magazeti yasiyofuata sheria za uchapishaji Msemaji huyo wa Serikali alisema kuwa ofisi yake haikurupuki kufungia magazeti, na kusema kuwa ni magazeti mitatu tu yalifungiwa kati ya 266 yaliyosajiliwa nchini na kuwataka wamiliki wa magazeti hayo kufuata sheria.

Kuhusu malamiko ya wafanyabiashara kwenye maeneo mbalimbali nchini ya kufunga biashara hizo kwa kisingizio cha kodi na tozo mbalimbali, Dkt. Abbasi alisema ni muhimu wakaelewa kwamba kwa sasa Serikali inapita katika kipindi cha mabadiliko na hakuna siku serikali haitadai kodi huku akieleza kuwa kodi nyingi zimepunguzwa hususan kwenye sekta za Kilimo, Mifugo na uvuvi.

“kwanza tukubali tunapita kwenye kipindi cha mabadiliko, hakuna siku serikali haitadai kodi kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi hii, kuna dhana ilijengeka kuwa unaweza kufanya biashara bila kulipa kodi hiyo sasa haipo, lazima tuangalie changamoto ambazo zinakumba sekta mbalimbali mfano sekta ya kilimo, miufgo na uvubvi kulikuwa na kodi zaidi ya 150, serikali imefuta zaidi ya kodi 80 hadi 100” alisema Dkt Abbasi.


WANANCHI WA NAMIUNGO TUNDURU WAJIPONGEZA KWA UFYATUAJI MATOFALI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

0
0


Pichani ni wakazi wa Kijiji na Kata ya Namiungo wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma hivi karibuni wakiangalia na kujipongeza kwa kazi mzuri ya ufyatuaji matoli iliyofanywa na wakazi hao kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa kituo cha afya katani hapo ambapo hilo ni eneo maalum  lililotengwa kwa ajili ya ujenzi huo.(PICHA NA FATNA MWINYIMKUU)

RAIS DKT.SHEIN AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKOA WA KUSINI PEMBA KATIKA FUTARI ALIOWAANDALIA IKULU CHAKECHAKE

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein amefutari pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba na kuwataka kuendeleza amani na utulivu uliopo nchini ili maendeleo zaidi yazidi kupatikana.

Hafla hiyo ya futari iliyoandaliwa na Rais Dk. Shein kwa ajili ya wananchi wa Mkoa wa Kusini  Pemba ilifanyika katika viwanja vya Ikulu ndogo Chake Chake, na kuhudhuriwa  na viongozi mbali mbali wa Serikali, dini, vyama vya siasa pamoja na wananchi wa Mkoa huo.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Rais Dk. Shein, Mkuu wa Mkoa huo Hemed Suleiman alieleza kuwa amani na utulivu ndio msingi wa maendeleo hivyo kila mmoja anapaswa kuilinda na kuiendeleza kwa nguvu zake zote.

Alisisitiza kuwa maendeleo yote yaliopatikana nchini yametokana na kuwepo kwa amani na utulivu mkubwa ambayo ndio chachu ya mafanikio hayo na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuyakuza maendeleo hayo kwa kadri uwezo utakapopatikana.

Alhaj Dk. Shein aliwatakia Ramadhani njema wananchi wa Mkoa huo na kuwasisitiza kuutukuza mwezi huo mtukufu kwa kusoma sana Qur-an kwani ndio mwezi ulioshuka kitabu hicho kitakatifu.

Alhaj Dk. Shein aliwataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kushirikiana na kupendana sambamba na kuwa wamoja huku akiwataka kuachama na mambo yote yaliyokatazwa ndani ya mwezi huu na miezi mengineyo ili waendelee kupata neema za Allah.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa kupambana na vitendo na matukio yanayovunja maadili ya dini ya kiislamu na ambayo hayapaswi kufanyika katika jamii ukiwemo udhalilishaji wa wanawake na watoto pamoja na matumizi ya dawa za kulevya ambayo hayaleti taswira nzuri katika jamii.

Pia, Alhaj Dk. Shein alisisitiza haja ya kuendelezwa na kudumishwa kwa usafi hasa katika kipindi hichi cha msimu wa mvua huku akieleza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupambana na athari za mvua kwa Unguja na Pemba. 

Pamoja na hayo, Alhaj Dk. Shein aliwashukuru wananchi wote waliohudhuria katika futari hiyo aliyowaandalia na kupongeza jinsi walivyoonesha upendo mkubwa kwake wa kukubali muwaliko wake huo.

Nao wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba wakitoa neno la shukurani kwa upande wao ambalo lililotolewa na Sheikh Mohamed Suleiman ambaye pia, ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Istiqama Pemba walieleza kufarajika kwao na futari hiyo maalum waliyoandaliwa na Rais wao na kueleza jinsi walivyoifurahia.

Wananchi wa Mkoa huo walieleza kuridhishwa kwao na juhudi kubwa anazozichukua Rais Dk. Shein kwa kuwapelekea maendeleo makubwa wananchi wa Zanzibar wakiwemo wa kisiwa cha Pemba ukiwemo Mkoa wao wa Kusini.

Sheikh Mohamed alieleza kuwa Rais Dk. Shein amekuwa akifuata sunna na fadhila za Mtume Mohammad (S.A.W) ya kuwafutarisha watu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan jambo ambalo limesisitizwa katika mwezi huu kutokana na fadhila zake.

Aidha, wananchi hao walitumia fursa hiyo kumuombea dua Rais Dk. Shein kwa ukarimu na upendo wake mkubwa aliyowaonesha wananchi hao pamoja na ukarimu anaoendelea kuwaonesha wananchi wote wa Zanzibar katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na katika kipindi chote cha uongozi wake.

Wakati huohuo, nae Mama Mwanamwema Shein kwa upande wake alishirikiana kikamilifu na viongozi wanawake wa kitaifa pamoja na wananchi wa Mkoa huo wa Kusini katika futari hiyo maalum aliyoianda Rais Dk. Shein.

Akitoa neno la shukurani Mshauri wa Rais Pemba Dk. Mauwa Abeid Daftari alitoa shukurani kwa Rais Dk. Shein kwa ukarimu wake anaoendelea kuuonesha kwa wananchi wake sambamba na kusisitiza umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi. 

Leo Alhaj Dk. Shein anatarajiwa kuungana pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba katika futari maalum aliyowaandalia. 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar kushoto Sheikh Saleh Omar Kabi na Mkuu wa Wilaya ya Chakechake  Rashid Hadid Rashid  katika Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari maalum aliyowaandalia  katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.(Picha na Ikulu)

 WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Pemba wakijumuika katika Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, kwa Wananchi wa Mkoa wac Kusini Pemba iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akijumuika na Wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba kulia Mshauri wa Rais Afisi ya Rais Pemba Mhe. Maua Abeid Daftari na kushoto Mshauri wa Rais Masuala ya Kijamii  Mhe. Zainab Omar.
 WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Pemba wakijumuika na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, katika futari maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu)  
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman akitowa neno la shukrani baada kumaliza hafla ya Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Kisiwani Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,na kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na kulia Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, wakiitikia dua ikisomwa na Sheikh Mohammed Suleiman,baada ya kumalizika hafla ya Futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba.(Picha na Ikulu)
 WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Pembe wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa hafla ya futari Maalum ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Sheikh Mohammed Suleiman, baada ya kumaliza kusoma dua na kutowa mawaidha ya fadhila ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani, wakati wa hafla ya futari maalum iliofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo Chakechake Pemba, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi. (Picha na Ikulu)

WAZIRI MKUU AFUTURISHA WAHESHIMIWA WABUNGE JIJINI DODOMA

0
0

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai wakiwaongoza Waheshimiwa Wabunge kupata futari aliyowaandalia katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi, Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Joseph Selasini wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakwanza kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenknlojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Waziri Mkuu)-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu wa Ofisi ya Bunge Bi. Jane Kajiru (wakwanza kushoto) wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. PICHA NA BUNGE

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI UTALII NA MAMBO YA KALE IKULU NDOGO KIBWENI

0
0


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni, wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyokwa mwezi Julai 2018 hadi March 2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, kushoto Mhe,. Mahmoud Thabit Kombo akisoma Utelelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March2019, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar na kushoto Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Chuom Kombo Khamis.
KATIBU Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akizungumza wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
 MAOFISA wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yao kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019.uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmaoud Thabit Kombo, akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

 WAKUU wa Idara mbalimbali za Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar wakifuatilia mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 MKURUGENZI Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Aiman Osmond Duwe, akichangia wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bi. Khadija Bakari, akisoma na Ripoti ya Matumizi na Mapato ya Idara mbalimbali za Wizara hiyo wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 MHARIRI Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, Zanzibar Leo, Ndh. Yussuf Khamis, akichangia wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar. (Picha na Ikulu)

Job Announcement at the African Union Commission

0
0
Dodoma, 17 May 2019



The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commission of African Union inviting qualified Tanzanians to apply for the posts available at the Commission.


The vacant positions currently available in the commission are as follows:

Position

Department

location

Deadline

DESKTOP-PUBLISHER

DIRECTORATE OF Conference & Publication Management

Ethiopia

30/5/2019

DIRECTOR-INTER-AFRICAN BUREAU FOR ANIMAL RESOURCES ((IBAR)

Department of Rural Economy & Agriculture.

Kenya

27/5/2019

DIRECTOR-INTER-AFRICAN BUREAU FOR ANIMAL RESOURCES ((IBAR)

Department of Rural Economy & Agriculture

Kenya

30/5/2019


Details of the positions are available on the Union career website http://aucareers.org/.


Issued by;

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,


HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO, MHESHIMIWA JAPHET NGAILONGA HASUNGA (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO KWA MWAKA 2019/2020

0
0


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2019/2020 Bungeni Jijini Dodoma, leo tarehe 17 Mei 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2019/2020 Bungeni Jijini Dodoma, leo tarehe 17 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2019/2020 Bungeni Jijini Dodoma, leo tarehe 17 Mei 2019.

1.0             UTANGULIZI


1.  Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji, Bunge lako Tukufu sasa lipokee na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha 2018/2019.  Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu lipitishe Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.
2.   Mheshimiwa Spika, awali ya yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kufikia siku ya leo tukiwa wazima wa afya njema na kuendelea kuijalia nchi yetu amani na mshikamano na kujadili bajeti hii inayolenga kusukuma mbele kasi ya maendeleo ya Sekta ya Kilimo na wakulima kwa ujumla wao.
3.  Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuniteua kuwa Waziri wa Kilimo. Pia, niwashukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu kwa kazi kubwa wanayofanya kusukuma maendeleo ya nchi hii, ikiwemo Sekta ya Kilimo. Napenda kuwaahidi kwamba nitafanya kazi ya kuongoza Wizara ya Kilimo kwa uaminifu, juhudi na maarifa ili kuhakikisha kuwa rasilimali zinazotengwa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo zinawafikia walengwa ili kuongeza tija na kuinua kipato chao.
4.  Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) kwa hotuba  yake ambayo iligusa maeneo mengi ikiwemo Sekta ya Kilimo. Aidha, nimpongeze tena Mhe. Waziri Mkuu kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kuhamasisha na kusimamia kilimo pamoja na maendeleo ya Vyama vya Ushirika.
5.  Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe na Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) pamoja na Wenyeviti wa Bunge kwa jinsi mnavyoliongoza Bunge kwa umahiri mkubwa.
 Aidha, nitumie nafasi hii kuwapongeza Wabunge wote kwa umahiri wao mkubwa katika mijadala inayoendelea katika Bunge hili la Bajeti.
6.  Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwapongeza na kuwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji chini ya Uenyekiti wa Mhe. Mahmoud Mgimwa, Mbunge wa Mufindi Kaskazini na Makamu Mwenyekiti Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma (Mb). Kamati ilipata fursa ya kukutana na Wizara na kutembelea baadhi ya maeneo kuona utekelezaji wa kazi za kilimo na kushauri namna ya kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara, Bodi na Taasisi zake. Naomba kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba, ushauri wao umezingatiwa na tutaendelea kushirikiana na Kamati ili kuleta mageuzi ya kilimo nchini.

2.0             MWELEKEO WA SEKTA YA KILIMO

7.  Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa kilimo cha kibiashara kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Aidha, Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo umesisitizia mapinduzi ya viwanda na umeitambua Sekta ya Kilimo kuwa mhimili imara kwa ajili ya upatikanaji wa malighafi za viwanda.  Miongozo hiyo ya Kitaifa, pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na Sera ya Kilimo ya mwaka 2013, inatekelezwa na Wizara kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ambayo inalenga kuleta mageuzi katika Sekta ya Kilimo. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa kuongeza mitaji, teknolojia na ubunifu, Sekta Binafsi inashirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa ASDP II.
8.  Mheshimiwa Spika, ASDP II iliyozinduliwa rasmi tarehe 4 Juni, 2018 na Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inalenga kubadilisha maisha ya mkulima kwa kufanya mageuzi makubwa kwenye kilimo kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kulingana na ikolojia za kilimo. 

3.0             MCHANGO WA KILIMO KATIKA UCHUMI

9.  Mheshimiwa Spika, kilimo ni sekta kubwa na muhimu kwa maendeleo kutokana na mchango wake katika uchumi. Katika mwaka 2017, sekta hiyo imetoa ajira kwa Watanzania kwa asilimia 65.5, ikichangia takriban asilimia 28.7 ya Pato la Taifa ambapo sekta ndogo ya mazao ilichangia asilimia 16.58.  Vilevile, Sekta ya Kilimo inachangia asilimia 65 ya malighafi za viwanda. Takwimu zinaonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka 2018, ukuaji wa Sekta ya Kilimo ulifikia asilimia 7.1. Ukuaji huo ulichangiwa na jitihada za Serikali za kuhakikisha upatikanaji na matumizi ya  pembejeo bora, hali nzuri ya mvua na uboreshaji wa miundombinu ya uzalishaji.

3.1  Upatikanaji wa Chakula

10. Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa  chakula kwa mwaka 2018/2019 ulifikia tani milioni 16.89 zikiwemo tani milioni 9.53 za mazao ya nafaka na tani milioni 7.35 za mazao yasiyo nafaka. Kiwango hicho cha uzalishaji kimeiwezesha nchi kujitosheleza kwa mahitaji yake ya chakula ya tani milioni 13.56 na hivyo kuwa na ziada ya tani milioni 3.32 za chakula kwa kiwango cha utoshelevu cha asilimia 124. Niwahakikishie watanzania kwamba, tunacho chakula cha kutosha nchini.  Hata hivyo, tuendelee kuweka akiba katika kaya zetu hadi tutakapovuna tena kwani inaonekana kwamba huenda tusiwe na mavuno mazuri sana msimu huu kutokana na uhaba wa mvua kwenye maeneo ya Kanda ya Ziwa, Kati na Kaskazini mwa nchi yetu.(Maelezo ya kina yanapatikana uk.5 wa kitabu cha Hotuba ya bajeti).

3.2   Umwagiliaji

11. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekamilisha mapitio ya Mpango Kabambe wa Taifa wa Umwagiliaji wa mwaka 2002 ili kubaini maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji kwa kuzingatia Mipango Shirikishi ya Maendeleo ya Rasilimali za Maji. Katika mpango huo, hekta 560,880 zimepangwa kuendelezwa kwa lengo la kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 475,052 mwaka 2018/2019 hadi hekta 1,000,000 ifikapo mwaka 2035. (Maelezo ya kina yanapatikana uk.6 wa kitabu cha Hotuba ya bajeti)

3.3   Maendeleo ya Ushirika

12. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeendelea kuimarisha Sekta ya Ushirika kwa kusimamia na kuhamasisha maendeleo yake. Vyama vya Ushirika vimeongezeka kutoka vyama 10,990 Desemba 2017 hadi vyama 11,331 kufikia Desemba 2018. Vilevile, idadi ya wanachama wa vyama vya ushirika imeongezeka kutoka 2,619,311 mwaka 2017 hadi 3,998,193 Februari, 2019 sawa na ongezeko la asilimia 53.
Hadi Desemba 2018, mikopo yenye thamani ya Shilingi trilioni 1.3 imetolewa kwa wanachama ikilinganishwa na Shilingi bilioni 902 iliyotolewa kufikia Desemba 2017.

 Aidha, Akiba na Amana za wanachama katika SACCOS zimefikia Shilingi bilioni 575 na hisa Shilingi bilioni 79. (Maelezo ya kina yanapatikana uk.7 wa kitabu cha Hotuba ya bajeti)

4.0             UTEKELEZAJI WA MAENEO YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2018/2019

13. Mheshimiwa Spika,  katika mwaka 2018/2019, Wizara imetekeleza  maeneo ya kipaumbele ya kuongeza tija kwa kuimarisha upatikanaji wa pembejeo za kilimo, udhibiti wa visumbufu, matumizi ya zana bora za kilimo na huduma za ugani; ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji; ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhi mazao ya kilimo na masoko; kufanya utafiti wa kilimo na kuzalisha teknolojia kwa mazao ya mahindi, muhogo, ngano, michikichi, ufuta, alizeti, pamba na mpunga.
14.  Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ya kipaumbele ni kuimarisha uzalishaji na upatikanaji wa mbegu bora za mazao na kusambaza kwa wakulima; kuboresha maarifa na ujuzi kwa watafiti; kuimarisha huduma za upimaji wa matabaka na ubora wa udongo kuendana na mahitaji ya mazao ya kilimo ki-ikolojia; mafunzo na usambazaji taarifa za kilimo na sayansi shirikishi; kusajili na kuandaa kanzidata ya wakulima na kuimarisha ushirika. (masuala yote ya utekelezaji wa maeneo ya kipaubele yapo kwa kina kwenye ukurasa 10-61  katika kitabu cha Hotuba ya bajeti)
15. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza vipaumbele hivyo, Shilingi bilioni 204.07 ziliidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Kati ya fedha hizo, Fungu 43 – Wizara ya Kilimo iliidhinishiwa Shilingi bilioni 166.26zikiwemo Shilingi bilioni 68.14 za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 98.12 za matumizi ya maendeleo; Tume ya Taifa ya Umwagiliaji - Fungu 05 iliidhinishiwa Shilingi bilioni 29.77 zikiwemo Shilingi bilioni 3.95 za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 25.82fedha za maendeleo; na Tume ya Maendeleo ya Ushirika - Fungu 24 iliidhinishiwa Shilingi bilioni 8.05 zikiwa ni fedha za matumizi ya kawaida.

4.1  Kuongeza Tija katika Kilimo

Upatikanaji wa mbegu bora za mazao
16. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019,  upatikanaji wa mbegu bora umefikia tani 49,040.66. Kati ya kiasi hicho, tani 38,507.87 zimezalishwa hapa nchini, tani 8,361.46 zimeagizwa toka nje ya nchi na tani 2,171.33 ni bakaa ya msimu wa 2017/2018. Vilevile, miche 1,507 ya miwa, vipando 121,805 vya muhogo na vikonyo 520,000 vya viazi lishe vimezalishwa. Aidha, aina mpya 13 za mbegu bora zimeidhinishwa na zitaanza kuzalishwa msimu wa 2019/2020.
Upatikanaji na udhibiti wa ubora wa Mbolea
17. Mheshimiwa Spika, hadi Machi 2019, upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini ulikuwa tani 492,394 ikilinganishwa na mahitaji ya tani 514,138 katika msimu wa 2018/2019. Aidha, Wizara kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imefanya ukaguzi kwa wauzaji wa mbolea 1,350 na wafanyabiashara 496 wapya wa mbolea  wamesajiliwa.

Upatikanaji wa Viuatilifu na Udhibiti wa Visumbufu
18. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imenunua lita 296,000 na kilo 3,000 za viuatilifu vyenye thamani ya Shilingi bilioni tisa (9) kwa ajili ya kukabiliana na milipuko ya visumbufu vya mazao. Hadi kufikia Machi 2019, ndege waharibifu wa nafaka walidhibitiwa katika skimu za umwagiliaji za Kahe, Lekitatu na Misenyi kwa mazao ya mpunga na mtama.  Aidha, lita 119,000 kwa ajili ya kudhibiti Viwavijeshi Vamizi zimesambazwa katika Kanda ya Ziwa, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Mashariki na kutoa mafunzo kwa maafisa ugani na wakulima 350.

Zana za Kilimo
19. Mheshimiwa Spika, takwimu zinaonesha kwamba wastani wa kitaifa wa matumizi ya zana bora za kilimo umeongezeka hadi kufikia asilimia 20 kwa matrekta na asilimia 27 kwa wanyama kazi ikilinganishwa na asilimia 14 ya  matrekta na asilimia 24 ya wanyama kazi mwaka 2013. Kutokana na ongezeko hilo, matumizi ya jembe la mkono yamepungua na kufikia asilimia 53 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na asilimia 62 kwa mwaka 2013.  Aidha, kupitia Mfuko wa Taifa wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) Wizara imendelea kutoa mikopo ya pembejeo na zana za kilimo. Katika kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019, mikopo 33 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.50imetolewa.

4.2  Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji

20.  Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya Maendeleo ya Umwagiliaji imeendelea kusimamia utekelezaji wa Mradi wa  Skimu za Umwagiliaji za Wakulima Wadogo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan. Mradi umekarabati skimu za umwagiliaji 129 katika Halmashauri 68 nchini pamoja na ununuzi wa mitambo ya ujenzi. 

4.3   Utafiti wa Kilimo na Uhaulishaji wa Teknolojia

21.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia TARI imegundua mbegu bora mpya aina nne (4) za mahindi. Mbegu hizo zina uwezo wa kutoa mavuno kwa wastani wa tani 5.8 kwa hekta kwenye mashamba ya wakulima katika ukanda wa chini na kati, zinahimili ukame na zina ukinzani wa magonjwa ya majani ya mahindi na michirizi na ukungu. Vilevile, kwa kushirikiana na kampuni binafsi, TARI imezalisha aina sita (6) ya miche ya mbegu bora ya migomba na kugundua aina 62 za  mbegu za mazao ya mikunde.

4.4  Maendeleo ya Mazao

22.  Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya  mazao mbalimbali  kwa kuimarisha huduma za utafiti, upatikanaji na utumiaji wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu vya mazao, huduma za ugani, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko. Aidha, Wizara imeandaa mkakati wa miaka minne (2018/2019 – 2021/2022) wa  kuendeleza zao la michikichi.
Mazao Makuu ya Asili ya Biashara
23.  Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa mazao makuu ya biashara uliongezeka kutoka tani 901,641 msimu wa  2016/2017 hadi tani 967,184 msimu wa 2017/2018 ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.2. Katika msimu wa 2018/2019, Wizara ililenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara hadi kufikia tani 1,356,368 na hadi kufikia Machi 2019, tani 667,631.77 sawa na asilimia 49.2 ya lengo zilikuwa zimezalishwa na uzalishaji unaendelea.
24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2017/2018, uzalishaji wa mazao ya bustani ulikuwa tani milioni 5.33 na matarajio ya uzalishaji kwa mwaka 2018/2019 ni tani milioni 5.96. Hadi Machi 2019, uzalishaji umefikia tani milioni 4.36 sawa na asilimia 73.17 ya lengo na msimu wa uzalishaji unaendelea.

4.5  Ujenzi wa Miundombinu ya Kuhifadhi Mazao ya Kilimo na Masoko

Miundombinu ya Kuhifadhi Mazao ya Kilimo
25. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea kutekeleza Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka. Hadi kufikia mwezi Machi 2019, asilimia 83 ya vifaa  vilikuwa vimeingizwa nchini kwa ajili ya ujenzi wa ghala katika vituo vya Makambako, Mbozi, Songea, Shinyanga na Dodoma.
Masoko ya Mazao ya Kilimo
26. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imeanzisha kitengo cha masoko ya mazao ya kilimo ambacho kinahusika na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi. Katika kutekeleza jukumu hilo, Wizara imeingia makubaliano ya Itifaki ya Usafi baina ya Tanzania na Serikali ya China kuwezesha kuuza muhogo nchini China ambapo hadi mwezi Machi 2019, kampuni tano zimesajiliwa kwa ajili ya kuuza zao hilo nchini China.


Hifadhi na Usalama wa Chakula
27. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, NFRA imenunua tani 46,236.035 za mahindi kwa ajili hifadhi na imeliuzia Shirika la Mpango wa Chakula Duniani tani 36,000 za mahindi zenye thamani ya Shilingi bilioni 21.  Aidha, Wizara imeanza kutekeleza Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu katika mazao unaolenga kudhibiti tatizo la sumukuvu katika mazao ya mahindi na karanga.

4.6  Huduma za Ushauri Kuhusu Utafiti, Mafunzo na Usambazaji Taarifa za Kilimo na Sayansi Shirikishi

Huduma za Ugani
28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imeandaa rasimu ya  Mwongozo wa Utoaji na usimamizi wa huduma za ugani utakaotumiwa na Sekta ya Umma na Binafsi. Aidha, elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji wa mazao, kuongeza thamani mazao ya kilimo, upatikanaji wa masoko, mitaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo, pembejeo na zana bora za kilimo imetolewa kupitia maonesho na vyombo vya habari.






Vyuo na Vituo vya Mafunzo ya Kilimo
29. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara kupitia Vyuo vyake vya Kilimo  imedahili na kufundisha wanafunzi 2,389 ambapo wanafunzi 2,051 wamefadhiliwa na Serikali  na 338 wanajilipia wenyewe.  Kati ya  wanafunzi waliodahiliwa, wanafunzi 1,537 ni ngazi ya Astashahada na 852 ni  ngazi ya Stashahada. Jumla ya wanafunzi 1,026 wakiwemo 263 wa Stashahada na 763 wa Astashahada watahitimu masomo yao mwezi Juni, 2019.

4.7  Kuimarisha Ushirika

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Tume ya Maendeleo ya Ushirika kupitia Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limefanya ukaguzi wa nje kwa vyama vya ushirika 2,297. Kati ya Vyama vilivyokaguliwa, asilimia 4.6 vilipata hati inayoridhisha, asilimia 64.6 vilipata hati yenye shaka, asilimia 21.6 vilipata hati isiyoridhisha na asilimia 9.2 vilipata hati mbaya. Hali hiyo ya Vyama vya Ushirika siyo nzuri na hatuwezi kuifumbia macho. Natoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge katika maeneo yetu tuendelee kushirikiana na Halmashauri zetu kuvisaidia vyama hivi ambavyo ni mkombozi wa mkulima.

4.8   Usajili wa Wakulima

31. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza usajili wakulima wote kwa mazao ambayo yanasimamiwa na Bodi.  Mazao hayo ni, kahawa, korosho, miwa, pamba, chai, mkonge, tumbaku na pareto. Hadi kufikia mwezi Machi 2019, wakulima 1,464,827 wametambuliwa na kusajiliwa katika maeneo mbalimbali nchini.

4.9  Masuala Mtambuka


32.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2018/2019, Wizara imeendelea kuzingatia masuala mtambuka katika kutekeleza majukumu yake. Masuala hayo ni pamoja na ushiriki wa vijana katika kilimo, lishe, jinsia, hifadhi ya mazingira na VVU na UKIMWI.

5.0             MPANGO NA MAENEO YA KIPAUMBELE KWA MWAKA 2019/2020

5.1  Kuongeza Tija katika Kilimo

    Upatikanaji wa mbegu bora za mazao
33.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Serikali kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, imejipanga kuzalisha jumla ya tani 53,608.2 za mbegu mbalimbali. Wazalishaji hao ni pamoja na ASA, Vituo vya Utafiti, Magereza na Sekta binafsi. Vilevile, ASA itazalisha vipando bora vya mihogo pingili 7,000,000 na miche bora ya matunda 20,000. Ili kufikia malengo hayo, miundombinu ya umwagiliaji itaboreshwa katika mashamba yanayomilikiwa na ASA na eneo la uzalishaji wa mbegu litaongezwa hadi kufikia hekta 811 katika mashamba mbalimbali.
Upatikanaji na udhibiti wa ubora wa Mbolea
34. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itasimamia uagizaji na usambazaji wa tani 625,000 za mbolea zinazokadiriwa kutumika nchini. Aidha, Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) itaongeza mauzo ya mbolea kutoka tani 10,000 hadi tani 100,000. Vilevile, ghala moja (1) lenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za mbolea litakarabatiwa katika wilaya ya Tabora pamoja na kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuchanganya mbolea kwa uwiano (blending plant) katika Mkoa wa Dar es Salaam. 
Upatikanaji wa Viuatilifu na Udhibiti wa Visumbufu
35. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itanunua na kusambaza lita 300,000 na kilo 3,000 za viuatilifu kwa ajili ya kukabiliana na milipuko ya visumbufu vya mazao.  Aidha, Wizara itaendelea kuimarisha kituo cha kudhibiti milipuko cha Kilimo Anga (Arusha) ili kutoa huduma bora. Vilevile, Wizara itaendelea kuvijengea uwezo na kukarabati vituo 10 kati ya 36 vya ukaguzi wa mazao mipakani.
Zana za Kilimo
36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itaanzisha kituo kimoja (1) cha zana za kilimo kwa ajili ya kutoa huduma za kiufundi na mafunzo kwa watoa huduma binafsi  wamiliki na watumiaji wa zana za kilimo kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wakulima katika Kanda ya Ziwa. Vilevile, Wizara kupitia AGITF, imepanga kutoa mikopo 250 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.12.

5.2  Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umwagiliaji

37. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itafanya tathmini ya miradi ya umwagiliaji ambayo ujenzi wake haujakamilika ili miradi hiyo iweze kukamilishwa kwa awamu.
Aidha, kupitia Mradi wa Kuendeleza Skimu za Wamwagiliaji Wadogo, Wizara itakamilisha ujenzi wa skimu 16 za umwagiliaji katika maeneo mbalimbali.

5.3  Utafiti wa Kilimo na Uhaulishaji wa Teknolojia

38. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia TARI imepanga kutafiti, kugundua na kusambaza aina 15 za mbegu bora za mazao ya nafaka, mizizi, mbegu za mafuta, mikunde, migomba na mazao ya bustani. Vilevile, Wizara itasafisha aina tisa (9) za mbegu ya mpunga na kuzalisha tani 10 za mbegu za awali katika Kituo cha Utafiti cha KATRINI. Aidha, kupitia kituo cha TARI Naliendele, Serikali itajenga kinu cha kubangua korosho chenye uwezo wa kubangua tani 1,800 kwa mwaka na kusindika tani 1,000 za mvinyo na sharubati (juice).

5.4  Maendeleo ya Mazao

39. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara imepanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kipaumbele kwa kuendelea kuratibu utekelezaji wa mikakati ya maendeleo ya  mazao hayo ikiwemo kuimarisha utafiti, upatikanaji na utumiaji wa pembejeo na zana za kilimo, udhibiti wa visumbufu, huduma za ugani, kuongeza maeneo ya uzalishaji, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko.
Zao la Korosho
40. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Korosho itaendelea kutekeleza programu ya kuzalisha miche bora milioni 10 ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.
Aidha, Bodi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango itahakiki na kulipa vikundi vya wazalisha miche ya mikorosho kwa msimu wa 2017/2018 ambao hawajalipwa katika mikoa saba (7). Vilevile, Wizara itaratibu upatikanaji na usambazaji wa tani 30,000 na lita 500,000 za salfa kwa ajili ya kudhibiti visumbufu vya zao la korosho.
Zao la Miwa na Uzalishaji wa Sukari
41. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Sukari itaratibu uzalishaji wa tani 403,786  za sukari kwa kuongeza eneo la uzalishaji wa kilimo cha miwa kutoka hekta 52,000 hadi hekta 97,000.  Wizara, kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) itawezesha upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji wa miradi mipya ya sukari katika Wilaya za Kasulu, Kibondo, Rufiji, Geita, Kilombero, Karagwe, Pangani, Bagamoyo na Morogoro. 
Zao la Kahawa
42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya kahawa itaongeza uzalishaji wa kahawa kutoka tani 65,000 hadi tani 80,000. Aidha Bodi imepanga kuzalisha na kusambaza miche milioni 10 ya kahawa katika Wilaya 42.
Zao la Mkonge
43. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Mkonge imepanga kuongeza uzalishaji wa mkonge kutoka tani 38,506 hadi tani 113,506 kwa kuongeza eneo la uzalishaji kutoka hekta 42,426.11 hadi 114,915.08, kusimamia uendeshaji wa mfumo wa kilimo cha wakulima wadogo cha mkataba na kuimarisha vyama vya ushirika na masoko ya mkonge.

Zao la Pamba
44. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Pamba imepanga kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka tani 222,000 hadi tani 700,000 na tija kutoka tani 300 hadi tani 600 kwa ekari. Aidha, upatikanaji wa mbegu za pamba utaongezeka kutoka tani 22,000 hadi 40,000 na upatikanaji wa viuatilifu utaongezeka kutoka lita milioni 7 hadi milioni 10.
Zao la Tumbaku
45. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Tumbaku imepanga kuongeza uzalishaji kutoka tani 55,000 hadi tani 60,000; kuimarisha vituo 1,972 vya kufungia na kuchambulia tumbaku; itaimarisha mfumo wa upatikanaji wa pembejeo za zao la tumbaku kwa kuwaunganisha watoa huduma wa pembejeo na Vyama vya Ushirika ili ziwafikie kwa wakati.
Zao la Chai
46. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia Bodi ya Chai imepanga kuongeza uzalishaji wa chai kavu kutoka tani 34,000 hadi tani 40,000 ambazo ni sawa na tani 182,000 za majani mabichi ya chai. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSSSF) itafufua kiwanda cha chai cha Mponde ili kuimarisha upatikanaji wa soko la majani mabichi ya chai kwa wakulima na kuongeza ajira.

5.5  Miundombinu ya Hifadhi na Uongezaji Thamani Mazao ya Kilimo

47. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kupitia NFRA itakamilisha awamu ya kwanza ya Mradi wa Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi ambapo ujenzi wa maghala matano (5) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 60,000 na vihenge  nane (8) vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 190,000 za nafaka utakamilika na hivyo kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000.

5.6  Vituo vya Utafiti huduma za Ugani na Mafunzo

Kuimarisha Vituo vya Utafiti
48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itakarabati ofisi na kuvipatia vifaa muhimu vituo vya utafiti vya Ukiliguru, Ilonga na Tumbi. Aidha, miundombinu ya umwagiliaji ya vituo vya utafiti vya Ilonga, Naliendele, Ukiliguru na miundombinu ya uhifadhi wa mbegu katika vituo vya Uyole, Ilonga na Seliani itaboreshwa. 
Huduma za Ugani
49. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI na Sekta binafsi itakamilisha Mwongozo wa Utoaji na Usimamizi wa Huduma za Ugani Kilimo ili kuendana na mahitaji ya sasa ya utoaji wa huduma za ugani nchini.
Vyuo na Vituo vya Mafunzo ya Kilimo
50. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itadahili wanafunzi 2,500 ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa ufadhili wa Serikali. Vilevile, itakarabati miundombinu ikiwa ni pamoja na madarasa sita (6), ofisi 12, mabweni 12, maktaba sita (6) na mabwalo ya chakula sita (6) katika vyuo vya mafunzo ya kilimo vya Mtwara, Igurusi, HORTI Tengeru, Tumbi, Mlingano na Maruku.

5.7  Kuimarisha Ushirika

51. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Tume ya Maendeleo ya Ushirika itaimarisha udhibiti na usimamizi wa vyama vya ushirika; itahamasisha wanachama wa Vyama vya Ushirika vya Mazao kuanzisha SACCOS 1,500 kwenye maeneo yao; na itahuisha Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 na kuipitia upya sheria za ushirika.

5.8  Uratibu, Takwimu, Ufuatiliaji na Tathmini

52. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar itafanya Sensa ya kilimo. 

5.9  Masuala Mtambuka

53.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itaendelea kuzingatia masuala mtambuka yakiwemo ushiriki wa vijana katika kilimo, lishe, jinsia, VVU na UKIMWI na mazingira katika utekelezaji wa majukumu yake.

5.10     Maeneo Maalum ya Maboresho katika Kilimo

54. Mheshimiwa Spika, naomba nizungumzie maeneo machache ya kimkakati ambayo kama Wizara tumeona ni muhimu kuyafanyia maboresho ili kuimarisha usimamizi wa kilimo na kuwapatia wakulima huduma kwa urahisi zaidi. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:

 Mapitio ya Sera na Sheria 

55. Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza na itaendelea kuipitia Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2013 na sheria mbalimbali kwa lengo la kubaini maeneo ambayo yatapaswa kuhuishwa ili kwenda na hali halisi ya sasa na mwelekeo wa Serikali wa kubadili kilimo chetu kuwa kilimo cha kibiashara.  Mtazamo wa Wizara ni kuwa na Sheria moja itakayosimamia rasilimaliwatu, matumizi bora ya pembejeo, ardhi ya kilimo na maeneo mengine muhimu. 
Bima ya Mazao
56.  Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau imeanza mchakato wa kuanzisha Bima ya Mazao hapa nchini ili kumwezesha mkulima kulipwa fidia pale anapopata hasara. Maandalizi yanaendelea kufanyika ili katika mwaka 2019/2020 tuwe angalau na aina mbili za mifumo ya Bima ya mazao inayoweza kutumika hapa nchini. Hata hivyo, ili utaratibu huu uwezekane, kutahitajika takwimu sahihi za hali ya hewa pamoja na uzingatiaji wa kanuni bora za Kilimo.

Usajili wa wakulima
57.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara itaimarisha kanzidata ya wakulima na kuendelea na usajili wa wakulima wa mazao mchanganyiko kwa kushirikiana kwa karibu sana na Vyama vya Ushirika na Taasisi nyingine kilele za wakulima kama vile Tanganyika Farmers Association (TFA). Ninawaomba Waheshimiwa Wabunge tusaidiane kuhamasisha wakulima katika maeneo yetu ili watakapofikiwa na zoezi la uandikishaji watoe ushirikiano na waelewe kwamba zoezi hili ni la kuwasaidia kupata huduma bora za Kilimo.
Masoko ya Mazao ya Kilimo
58.  Mheshimiwa Spika, Wizara imeamua kuimarisha utafutaji wa masoko ya mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi. Katika mwaka 2019/2020, Wizara itakiimarisha kitengo cha masoko kwa kukijengea uwezo wa kufanya uchambuzi na utafutaji wa masoko ndani na nje ya nchi.
 Aidha, elimu itaendelea kutolewa kwa wakulima ili wazalishe kulingana na mahitaji ya soko. Vilevile, tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi nyingine zinazohusika na masoko nchini ikiwemo TANTRADE na Soko la Bidhaa (TMX).
Mfumo wa upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo
59.  Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza zoezi la kupitia kwa kina mifumo iliyopo ya uzalishaji, uagizaji na usambazaji wa mbegu, mbolea na viuatilifu. Mifumo iliyopo kwa sasa inatofautiana kwani kuna baadhi ya Bodi za Mazao zinazojihusisha na uagizaji  na usambazaji wa pembejeo, wakati mwingine Vyama vya Ushirika vinaagiza na kusambaza pembejeo kwa wanachama wao, wakulima pia hununua pembejeo moja kwa moja kutoka kwa wafanyabiashara na pia mbolea kwa sasa inaagizwa kwa mfumo wa pamoja (Bulk Procurement).
60.  Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa pembejeo za kilimo na tofuati ya mifumo hiyo, tumeamua kuipitia yote ili kuona mfumo bora unaoweza kutumika kuhakikisha pembejeo zenye ubora zinapatikana na kusambazwa kwa wakulima kwa wakati. Malengo yetu ni kukamilisha mapitio hayo na kupata majawabu ya mfumo bora ifikapo Juni 2019, ili mwaka 2019/2020 tuwe na mfumo madhubuti utakaokuwa na tija kwetu sote. Nina uhakika kwamba, mfumo mzuri wa upatikanaji na usambazaji wa pembejeo utawezesha uwepo wa pembejeo bora kwa bei nafuu na hivyo kuongeza matumizi kwa wakulima wetu.
61.  Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina ya hotuba yangu hususan mpango na maeneo ya kipaumbele kwa mwaka 2019/2020 yanapatikana ukurasa wa 61 hadi 91 katika kitabu cha hotuba cha Wizara ya Kilimo kwa mwaka 2019/2020 kilichowasilishwa Bungeni.

6.0              SHUKRANI

62. Mheshimiwa Spika, kabla sijamaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa watu, taasisi, makundi na wadau mbalimbali ambao tunashirikiana kuendeleza kilimo. Kwanza, nawashukuru sana, Naibu Mawaziri wa Kilimo, Mhe. Omary Tebweta Mgumba (Mb.) na Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb.) kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu yangu. Napenda pia, kuwashukuru  Katibu Mkuu, Mhandisi Mathew John Mtigumwe; Naibu Katibu Mkuu, Prof. Siza D. Tumbo; Wakurugenzi wa Idara na Wakuu wa Vitengo; Taasisi na Asasi zilizo chini ya Wizara; watumishi wote wa Wizara; na wadau wa Sekta ya Kilimo kwa juhudi, ushirikiano na ushauri uliowezesha kutekelezwa kwa majukumu ya Wizara kwa mwaka 2018/2019 pamoja na kuandaa Hotuba hii. Ni matarajio yangu kwamba, nitaendelea kupata ushirikiano wao katika mwaka 2019/2020.
63. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie fursa hii kuzishukuru Nchi na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa ambayo yamesaidia Wizara katika juhudi za kuendeleza kilimo. Nachukua fursa hii kutaja baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali za Japan, Marekani, Uingereza, Ireland, Malaysia, China, Indonesia, Korea ya Kusini, India, Misri, Israel, Ubelgiji, Ujerumani, Finland, Norway, Brazil, Uholanzi, Vietnam, Canada na Poland.  Ninayashukuru pia Mashirika na Taasisi za Kimataifa zifuatazo: Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, AU, IFAD, DFID, UNDP, FAO, JICA, EU, UNICEF, WFP, CIMMYT, ICRISAT, ASARECA, USAID, KOICA, ICRAF, IITA, IRRI, ILRI na CABI. Nyingine ni CFC, AVRDC, AGRA, CIP, CIAT/PABRA, UNEP, WARDA, Shirika la Kudhibiti Nzige wa Jangwani na HELVETAS.  Wadau wengine ni Shirika la Kudhibiti Nzige Wekundu, Bill and Melinda Gates Foundation, Gatsby TrustRockfeller Foundation, Aga Khan Foundation, Unilever na Asasi zisizo za kiserikali nyingi ambazo hatuwezi kuzitaja zote hapa.
64. Mheshimiwa Spika, natoa shukrani za pekee kwa wananchi wa Jimbo langu la Vwawa kwa ushirikiano wanaoendelea kunipa katika kipindi chote cha kuwawakilisha hapa Bungeni. Aidha, napenda kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya jimbo letu na Taifa kwa ujumla. Kwa umuhimu wa kipekee ninatoa shukrani za dhati, kwa wakulima wa nchi hii kwa kazi kubwa wanayofanya katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

7.0             MAOMBI YA FEDHA MWAKA 2019/2020

65.  Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2019/2020, Wizara inaomba idhini ya kukusanya maduhuli ya Shilingi 3,472,515,000yatokanayo na vyanzo mbalimbali vya mapato.
66. Mheshimiwa Spika,  katika mwaka 2019/2020, Wizara ya Kilimo inaomba kutumia jumla ya Shilingi 253,856,943,970 kupitia Fungu 43, Fungu 05 na Fungu 24 kama ifuatavyo;
FUNGU 43 – Wizara ya Kilimo
67. Mheshimiwa Spika, jumla ya Shilingi 208,044,783,140zinaombwaKati ya fedha hizo, Shilingi 143,577,036,140 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ambapo Shilingi 82,000,000,000ni fedha za ndani na Shilingi 61,577,036,140 ni fedha za nje. Aidha, Shilingi 64,467,747,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapoShilingi 13,214,159,060 ni kwa ajili ya mishahara ya Wizara, Shilingi29,621,801,490 ni kwa ajili ya mishahara ya Bodi na Taasisi, Shilingi11,453,309,490 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa Wizara naShilingi 10,178,476,510 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo kwa Bodi na Taasisi.
FUNGU 05 – Tume ya Umwagiliaji
68. Mheshimiwa Spika,  jumla ya Shilingi 37,485,090,830zinaombwaKati ya fedha hizo, Shilingi 32,501,462,613 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 3,000,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 29,501,462,613 ni fedha za nje.
 Aidha, Shilingi 4,983,628,217 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Shilingi 4,098,444,217 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Tume na Shilingi 885,184,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.
FUNGU 24 – TUME YA USHIRIKA
69. Mheshimiwa Spika,  jumla ya Shilingi 8,327,070,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Shilingi6,127,370,000 kwa ajili ya mishahara na Shilingi 2,199,700,000kwa ajili ya matumizi mengineyo.
Maelezo ya sehemu ya maombi ya fedha mwaka 2019/2020 kwa fungu 43, 65 na fungu 24 yanapatikana ukurasa wa 93 hadi 95 katika kitabu cha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo.

HITIMISHO

70. Mheshimiwa Spika, Pamoja na hotuba hii, vipo viambatisho vinavyotoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo.  Hotuba hii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara ya Kilimo, www.kilimo.go.tz. Ninaomba kuhitimisha kwa kukushukuru wewe binafsi na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.
71. Mheshimiwa Spika,  NAOMBA KUTOA HOJA

JAJI MKUU ASHAURI CHAMA CHA WANASHERIA KUSHIRIKIANA NA MAHAKAMA

0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amekishauri chama cha wanasheria cha Tanganyika Law Society (TLS) kushirikiana na Mahakama katika kutekeleza majukumu yake.

Akizungumza na Rais wa TLS pamoja na ujumbe wake walipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es salaam, Jaji Mkuu amesema Mahakama pamoja na chama hicho wanayo maeneo mengi ya kushirikiana pasipo kuingiliana katika majukumu yao.

Aidha, Jaji Mkuu pia amekishauri chama hicho kuwa na mpango kazi wa muda mrefu ili kuongeza ufanisi ndani ya chama hicho kwa kuwa kwa mujibu wa Sheria, viongozi wa chama hicho hukaa madarakani kwa kipindi cha mwaka moja kabla ya uchaguzi kufanyika tena.

Akizungumzia mapambano dhidi ya rushwa katika utoaji wa haki, Jaji Mkuu amewataka Mawakili nao kupambana na rushwa kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kufuata maadili.

“Zifanyieni kazi changamoto za rushwa na shirikianeni na Mahakama ya Tanzania kwa kuwa Mahakama ni mfumo wa kukosoana, alisema Jaji Mkuu.

Kwa upande wake, Rais wa TLS Mhe. Dkt. Rugemeleza Nshala ameiomba Mahakama ya Tanzania kushughulikia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo Mawakili wanapotekeleza majukumu yao ya kisheria Mahakamani ikiwemo kuchelewa kuanza kwa kesi mahakamani.

Rais huyo pia aliishukuru Mahakama kwa ushirikiano inaoutoa kwa chama chake na kuahidi kufanya kazi zake kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania.

Naye Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezar Feleshi amewapongeza viongozi wapya wa TLS waliochaguliwa hivi karibuni na kuwashauri kufanya kazi kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania.

“Mifumo yetu iko wazi nasi tuko tayari kufanya kazi nanyi kwa kuwa wote tunayo nia moja ya kumtumikia mwananchi”, alisema Jaji Kiongozi.

Wakati huo huo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bwn. Hussein Kattanga amewashauri viongozi wa TLS kushirikiana na Mahakama katika kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa haki na kuwataka kuwasilisha hoja na malalamiko kwa kuwa Mahakama kwa sasa inapokea hoja, maoni na malalamiko ili kuboresha huduma zake.
 Jaji Mkuu wa Tanzania,  Prof. Ibrahim Hamis Juma akizunzumza na viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walipomtembelea mapema Mei 16, 2019 ofisini kwake Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia kwake ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, anaefuata ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga, kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dkt. Rugemeleza Nshala, anaefuata ni Makamu wa Rais wa Chama hicho Bw. Mpale Mpoki , pamoja na wajumbe wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo.
  Jaji Mkuu wa Tanzania,  Prof. ibrahim Hamis Juma akisisitiza jambo wakati akizungumza na ujumbe kutoka Chama cha Wnasheria Tanganyika, ukiongozwa na Rais wa chama hicho, Dkt. Rugemeleza Nshala.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria nchini (TLS) Dkt. Rugemeleza Nshala (kushoto kwa Jaji Mkuu) pamoja na wajumbe wengine.

MATUKIO YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE ALIPOKUTANA NA VIONGOZI MBALIMBALI

0
0
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia.
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia na baadhi ya wajumbe aliombatana nao.
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia.
  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia,wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe.
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (mb) akiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina alipokwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (mb)  akiwa katika mazungumzo na Mhe. Mikel Kafando ambaye ni Rais Mstaafu wa Burkinafaso ambaye pia ni mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (mb) (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mikel Kafando ambaye nui Rais Mstaafu wa Burkinafaso ambaye pia ni mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi 
 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (mb) akipokea hati ya utambulisho ya Mahayub Buyema Mahafud, Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Sarahawi.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (mb) akiwa katika mazungumzo na Bwana. Mahayub Buyema Mahafud, Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Sarahawi.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA OFISI KUU YA KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA MPWAPWA NA SHULE YA QUEEN ESTHER

0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Watumishi wa Ofisi kuu ya wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa alipowatembelea leo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akipatiwa zawadi ya Biblia na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya alipomtembelea leo katika Ofisi kuu ya wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akipatiwa zawadi ya Mbuzi wawili na Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya alipomtembelea leo nyumbani kwake Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mke wa Askofu ambae ni Mshauri wa Wanawake ndani ya Dayosisi katika Malezi ya Kikristo, Ndg. Mwezwa Chimeledya
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akipatiwa maelezo na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther, Mwl. Angelina Kashangaki (kushoto) alipoitembelea Shule hiyo inayomilika na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kulia ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akikagua darasa la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Wa pili kushoto ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Angelina Kashangaki
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akikagua ujenzi wa darasa la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kulia ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (hayupo kwenye picha) akizungumza wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kuanzia kushoto ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther, Mwl. Angelina Kashangaki na Katibu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Ndg. Charles Makuyu
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimpatia zawadi ya vitabu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther, Mwl. Angelina Kashangaki wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilika na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha nne (4) Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Queen Esther wakati alipoitembelea Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa iliyopo Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma. Kuanzia kushoto waliokaa ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mwl. Angelina Kashangaki  na Katibu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa, Ndg. Charles Makuyu

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

CAF YATANGAZA GHARAMA ZA TIKETI KUTAZAMA MECHI ZA AFCON

0
0

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza gharama za tiketi za kutazama mechi za Fainali ya Africa (AFCON) inayotarajia kuanza mwezi ujao nchini Misri.

CAF imetangaza gharama hizo kwa madaraja mbalimbali.

Kwenye michezo ya hatua ya makundi ambayo itahusisha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” tiketi za daraja la 1 USD 29,tiketi za daraja la 2 USD 18 na tiketi za daraja la 3 USD 6

Hatua hiyo Taifa Stars itacheza michezo mitatu ambapo itaanza dhidi ya Senegal ikifuatiwa na mchezo dhidi ya Kenya na kumalizia hatua hiyo kwa kucheza na Algeria 

Kwenye hatua ya robo fainali gharama ya tiketi daraja 1 USD 35 kwa daraja la 2 USD 24 na daraja la 3 USD 12 

Hatua ya nusu fainali daraja la 1 USD 59,daraja la 2 USD 29 na daraja la 3 USD 18

Wakati mchezo wa mshindi wa 3  itakua USD 35 daraja la 1,USD 24 daraja la 2 na USD 12 daraja la 3.

Mchezo wa fainali daraja la 1 USD 106,daraja la 2 USD 44 na daraja la 3 USD 24.

Yeyote mwenye nia ya kununua tiketi hizo za AFCON awasiliane na TFF mapema kabla ya kufungwa kwa muda wa maombi.

UMOJA WA MASHABIKI WAIFUTURISHA TIMU YAO NA KUTOA UJUMBE MZITO KWA UONGOZI WA TIMU

0
0
Bukoba na Allawi Kaboyo.
Umoja wa mashabiki wa timu ya soka ya  Kagera Sugar inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara wameiandalia timu hiyo futari iliyowajumuisha wachezaji wote wa timu hiyo,benchi la ufundi, viongozi wa timu pamoja na mashabiki ikiwa ni ishara ya kuonesha umoja na upendo kwa timu yao.

Futari hiyo iliandaliwa jana tarehe 16 mwezi machi mwaka huu  katika ukumbi wa Red Cross Bukoba mkoani Kagera na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na dini katika kuonesha mshikamano baina ya mashabiki na timu.

Akiongea mmoja wa viongozi wa umoja wa mashabiki ambaye ni katibu  wa jumuiya hiyo ndugu Alex Xavery aliutaka uongozi wa timu ya Kagera sugar kuonesha ushirikiano na mashabiki ili kuweza kuijenga timu lakini pia kuwafanya mashabiki kuwa karibu zaidi na timu yao.
 Katibu huyo aliongeza kuwa timu kwa sasa ina hali mbaya katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara kutokana na kutofanya vizuri katika msimu huu ambapo alimuomba mwalimu wa timu hiyo Meck Maxime kuwa na malengo ya kuchukua taji hilo kwa msimu ujao endapo wataweza kubakia kwenye ligi kutokana na nafasi ya timu iliyopo kwa sasa.
 “Timu yetu tunajua hali iliyonayo na sasa tunamuomba mungu tubakie kwenye ligi, tukuombe mwalimu uanze kuwa na malengo ya kuchukua ubingwa msimu ujao. Zipo tetesi za kuwa mashabiki tukiwa na nguvu tutaichukua timu irudi kwa wananchi mimic niseme tu hilo sio lengo letu kwanza tunajua hatuna uwezo wa kuiendesha timu,ila tunachotaka kwenu ni ushirikiano na kitu kikubwa ambayo mnaweza kutulipa ninyi kama benchi la ufundi na wachezaji ni matokeo mazuri.” Alisema Alex.

Alex alisisitiza kuwa wao kama wachezaji wa 12 ambao hukaa nje ya uwanja kwaajili ya kuwahamasisha wachezaji hujisikia vibaya pale mchango wao unaposhindwa kuthaminiwa nap engine kuonekana wanajipendekeza.
 Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Meck Maxime aliwaomba radhi mashabiki hao kwa mwenendo mbaya wa timu kwa sasa katika msimu huu ambapo alisema kufungwa ni sehemu ya mchezo na kukili mbele ya mashabiki hao kuwa hali ya timu kwa sasa sio nzuri na kuomba waombewe dua ili waweze kubakia katika ligi kuu Tanzania Bara.

Maxime alisema kuwa mashabiki wasipende sana kulalamikia uongozi bila hata kuwauliza uongozi husika juu ya jambo linalowakera ambapo aliuueleza umma uliojitokeza katika futari hiyo kuwa wao wanawapenda sana mashabiki wao.
“Ninachojua mashabiki mnapenda kuiona timu ikifanya vizuri na hatimaye kuleta matokeo yaliyo mazuri, lakini tambueni mchezo una kufunga,kufungwa na kutoka suruhu hivyo tunaomba matokeo yote ambayo timu itayapata tuyapokee sote isiwe timu ikifungwa ni timu ya kocha lakini ikishinda ni yetu sote.” Alisema Maxime.

Aidha Maxime alisema kuwa wamefurahishwa na upendo ulioneshwa na umoja wa mashabiki kwa kuwaandalia Futari na kuongeza kuwa kwa shabiki yeyote atakayeona jambo ambalo anahisi hakulielewa basi asianze kulalamika awafate viongozi watamueleza juu ya jambo hilo.

Timu ya Kagera Sugar jana ilicheza mchezo wake wa 36 wa ligi kuu Tanzania Bara na timu ya soka ya Stand Utd kutoka Mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na kukubali kichapo kitakatifu cha goli 3 kwa 1(3-1) na kuifanya timu hiyo kushuka kutoka nafasi ya 13 hadi nafasi ya 15 ya msimamo wa ligi hiyo ikiwa imecheza michezo 36 ikiwa na alama 43 huku vinala wa ligi hiyo wakiwa ni mabingwa watetezi wenye alama 85 baada ya kucheza michezo 34.

IGP SIMON SIRRO AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke, wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, na kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo kuendeleza ushirikiano. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (kulia), akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam, na kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo kuendeleza ushirikiano. Picha na Jeshi la Polisi.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images