Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

UGONJWA WA DENGUE TISHIO DAR,WAGONJWA WAZIDI KUONGEZEKA,WANANCHI WASHAURIWA KUCHUKUA HATUA

$
0
0
Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wa Ugonjwa wa Dengue imeongezeka ambapo kwa sasa wamegundulika wagonjwa wapya 674 huku kata ya Ilala ikiongoza kwa kuwa na wagonjwa 235.

Akizungumza na waandishi wahabari Jijini Dar es Salaam Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi amesema kuwa Ugonjwa wa Dengue kwa sasa wameongeza vituo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Tanga hadi vituo 19 tofauti na awali ambapo vilikuwa 7.

Amezitaja  baadhi ya vituo vya Serikali vinavyopima Ugonjwa huo kuwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Amana, Temeke, Tumbi, Mkuranga  huku uhamasishaji wa upatikanaji wa vipimo zaidi vya Ugonjwa huo ukiendelea.

Aidha ameongeza kuwa dalili za ugonjwa huo ni pamoja na homa ya ghafla, Kuumwa kichwa hususani sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu ambapo dalili hizo huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu siku mtu alipoambukizwa virusi vya Ugonjwa huo.

Sambamba na hayo amewakumbusha viongozi wa mikoa, Wilaya,  Halmashauri, Kata, Tarafa, Vijiji, mitaa na vitongoji  pamoja na Maafisa wa Afya nchini kuchukua hatua kwa dhati kwani Ugonjwa huo haupo ukanda wa Pwani tu bali unaweza ukatokea pia katika maeneo yao.

Hata hivyo amesema tangu kutokea kwa Ugonjwa huo January watu 1901 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugua Ugonjwa huo ambapo kati ya hao 1809 wanatoka Dar es Salaam, 89 kutoka Tanga na mkoa wa Pwani, Singida na Kilimanjaro kukiripotiwa mgonjwa mmojammoja.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Yudas Ndungile amesema wanaendelea na jitihada ya kuangamiza mazalia ya mbu ikiwemo kufukia kupulizia dawa  na wanamkakati wa kupata mashine ya kupuliza dawa angani.

Hata hivyo wito umetolewa kwa wananchi kwenda kupima pindi wanapoona dalili za ugonjwa huo na vipimo vinatolewa bure kwenye vituo vya Afya vya  Serikali huku akisisitiza kujikinga kwa kuangamiza  mazalia ya mbu kwa kufukia madimbwi, kufyeka vichaka na kuvaa nguo ndefu kwani mbu huyo hungata majira ya asubuhi mchana na jioni.

JWTZ WATUMIA NDEGE YA ATCL KUSAFIRISHA WAPIGANAJI KUISHIRIKI ULINZI WA AMANI DARFUR

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu
Maafisa na Askari wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika  Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza  kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya  Serikali ya ATCL ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika  kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga amesema Jeshi ni Taasisi inayoongozwa na Uzalendo,uadilifu, uhodari  hivyo ni faraja kubwa kwa Jeshi  na wapiganaji kuunga mkono jitihada za Serikali katika Kuboresha Uchumi  ikiwa ni  sehemu ya mchango wao katika kuonesha  uzalendo kwa vitendo kwa  kutumia vitu vya nyumbani kwa maslahi mapana ya Taifa.

“ Tumekuwa tukitumia Ndege zetu za Jeshi lakini tumekuwa tukitumia Ndege za mataifa mengine kwa Mikataba kutoka Umoja wa Mataifa lakini sasa ni faraja kwani tumefanikiwa kuwashawishi Umoja wa Mataifa kutumia Ndege zetu” Alisema Meja Jenerali Kapinga.

Aidha,Meja Jenerali kapinga alisema   mbali na kutumia Ndege hiyo lakini aliwaasa Maafisa na Askari hao kuhakikisha wanapeperusha vema Bendera ya Nchi na kuendelea kuitangaza kwa  sifa nzuri za Utendaji Kimataifa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la la Tanzania (ATCL),  Mhandisi Ladislaus Matindi  Alisema ni Fursa Nzuri kwa ATCL na wanalishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia kwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi  kwa Mchango mkubwa   kufanikisha kupata tenda hiyo.

“ Namshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake kwa Uzalendo wake na kuhakikisha anafanikisha ATCL kupata fursa kwa mara ya kwanza na hii itakuwa mwanzo mzuri na tutahakikisha tunaitumia vizuri  fursa hii kujitangaza zaidi Kimataifa kwa maslahi  ya Nchi “ Alisema Mhandisi Matindi.

Vilevile  Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa  kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan  ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.

Naye Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT- 13,  Luteni Kanali Khalfan Kayage  anayekwenda na  Kikosi hicho  alisema kuwa  inawapa nguvu kupeperusha Bendera yetu kupitia Ndege na ameahidi kufanya kazi kwa Bidii kuendeleza jina na sifa nzuri ya Tanzania Kimataifa.
 Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga  ( Kushoto ) akiagana na Kamanda Kikosi  Kundi la 13  Luteni kanali Khalfan Kayage (Kulia ) kinachoenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan leo mei 16 wakati wakiondoka kwa Ndege ya ATCL (Haipo pichani )  katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es Salaam katikati ni Mkurugenzi wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi. Picha na Luteni Selemani Semunyu
 Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga Akiagana na  Maafisa na Askari wa  JWTZ   Kundi la 13 linalokwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan wakati wakiondoka kwa Ndege ya ATCL (haipo Pichani) leo Mei 16  katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es Salaam Picha na Luteni Selemani Semunyu
Baadhi ya Maafisa na Askari wa JWTZ  Kundi la 13 wakijiandaa  kuondoka kwa Ndege ya ATCL leo Mei 16 2019 katika Uwanja wa Ndege wa Jeshi Jijini Dar es Salaam kwenda kushiriki Ulinzi wa Amani Jimboni Darfur Nchini Sudan  . Picha  na Luteni Selemani Semunyu.

TANZANIA KUFIKIA ASILIMIA 70 YA KUONDOA UHABA WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0

waziri wa afya Ummy Mwalimu akifungua kikao cha kujadili changamoto za rasiliamali watu katika sekta ya afya kilichofanyika leo jijini Dodoma

Dkt.Dan Brun Peterson mshauri mwelekezi masuala ya afya idara ya sera ya mipango wizara ya afya akiwasilisha mada katika kikao hicho
waziri wa afya pamoja na katibu mkuu wake Dkt.Zainab Chaula(kulia)wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa
Viongozi mbalimbali wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kikao hicho ambacho kitaweka mikakati ya kuboresha uzalishaji,kuajiri watoa huduma za afya nchini
Baadhi ya viongozi wa wizara ya afya,Tamisemi pamoja wadau wa maendeleo wakifuatilia kikao hicho chenye kujadili changamoto.za.uhaba wa watumishi wa sekta ya afya ambapo pengo ni asilimia 52

Na.WAMJW,Dodoma

Tanzania imeazimia kufikia asilimia sabini kutoka arobaini na nane ya uhaba wa watoa huduma za afya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ifikapo mwaka 2022.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua kikao cha kujadili changamoto za rasilimali watu katika sekta ya afya kati ya viongozi kutoka Wizara ya Afya, Tamisemi pamoja na washirika wa maendeleo nchini.

Waziri Ummy amesema lengo la kikao hicho ni kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu rasilimali watu ikiwemo ya upungufu wa watumishi, ajira, mafunzo pamoja na mahitaji ya watumishi kuanzia ngazi za zahanati hadi hospitali za wilaya nchini.

Amesema upungufu huo umetokana na ongezeko la miundombinu ambayo imewekwa na serikali ya awamu ya tano licha ya kazi kubwa iliyofanyika ya kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

”ingawa bado ipo changamoto ya rasilimali watu katika sehemu za kutoa huduma za afya nchini ambapo pengo ni takribani asilimia 52 kwa kila watumishi wa afya mia moja tunawahitaji watumishi arobaini na mbili”. Amesisitiza Waziri Ummy.

Aidha, etaja sababu nyingine ya upungufu wa watumishi wa sekta ya afya kuwa ni pamoja na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hivyo inahitajika watoa huduma wa afya wengi katika kuwahudumia wananchi wenye matatizo hayo.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kikao hicho kitaweka mikakati ya pamoja na ya ubunifu ya kuona kunakuwa na maboresho ya uzalishaji wa wataalam wa afya na wale wanaozalishwa ni kiasi gani wanaweza kuajiriwa na kuwekwa kwenye utumishi wa umma hususan kwenye ngazi ya zahanati na hospitali za wilaya.

“Tutaweka ubunifu ambao utawawezesha mfano wauguzi kupatiwa mafunzo ya kutoa dawa za usingizi na hii ni kuona wanao uwezo wa kufanya kazi nyingine tofauti, kwa ujumla sekta ya afya nchini inaenda vizuri na nina amini kwa pamoja tunaweza kutatua uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.

WAFANYABIASHARA WATOA NENO USITISHWAJI WA MIFUKO YA PLASTIKI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAFANYABIASHARA wadogo na wauzaji wa vifungashio na mifuko mbadala wameiomba Serikali kutoa maelekezo maalumu ni wapi watapata mifuko mbadala baada ya matumizi ya mifuko ya plastiki kusitishwa kuanzia Juni mosi mwaka huu.

Wakizungumza  na Blogu ya jamii kwa nyakati tofauti wafanyabiashara katika soko la Kariakoo jijiji Dar es Salaam wamesema kuwa wamelipokea suala hilo kwa mikono miwili kwa kuwa matumizi ya mifuko ya plastiki athari zake zimeonekana hivyo ni vyema kutumia mifuko mbadala iliyoelekezwa ili kutunza mazingira.

Aidha wamesema kuwa upatikanaji wa mifuko mbadala ya kwa wafanyabiashara hao Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema tayari ametoa maelekezo ya wapi vifungashio na mifuko mbadala itapatikana kabla ya tarehe elekezi.

Aidha wameiomba serikali kuzidi kutoa elimu ya uelewa juu ya athari za mifuko ya plastiki katika mazingira ili kila mmoja awe sehemu ya utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wao akina mama wanaofanya biashara za kuuza unga wa lishe, korosho na ubuyu katika soko la Mwenge jijini humo wameiomba serikali kutoa maelekezo ya kina ni mifuko ipi haitakiwi kimatumizi, na kuiomba kuelekeza mifuko mbadala ambayo itafaa katika uhifadhi wa bidhaa hizo kwa ubora zaidi.

Vilevile kwa upande wa wauzaji wa vifungashio na mifuko mbadala wamesema kuwa mifuko na vifungashio hivyo vinapatikana Mikoani hasa katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Lindi na nchi jirani ya Kenya ambapo usafiri na kodi ni kubwa na wameiomba serikali kuangalia suala hilo hasa kwa kuhakikisha viwanda vya kutengeneza vifungashio na mifuko mbadala vinapatikana kwa wingi nchini.
 Muuzaji wa vifungashio na mifuko mbadala Benjamin Paul akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na usitishwaji wa mifuko ya plastiki ambapo ameiomba serikali kuangalia na kuwekeza katika viwanda vya ndani ambavyo vinazalisha mifuko hiyo.
Mjasiriamali wa unga wa lishe na korosho Mariam Seif akizungumza na Michuzi blogu kuhusiana na matumizi ya mifuko mbadala ambapo ameiomba serikali kutoa elimu na maelekezo zaidi juu ya mifuko iliyokatazwa. 
 Baadhi ya vifungashio mbadala ambavyo vinaruhusiwa kimatumizi kuanzia June Mosi.
Muuzaji wa mifuko ya plastiki Alawi Zeni akizungumza na blogu ya jamii kuhusiana na katazo la mifuko ya plastiki na kueleza kuwa wapo tayari katika kushiriki kukomesha matumizi ya mifuko hiyo.

SERIKALI KUJENGA KIWANDA CHA MVINYO KUPITIA MABIBO.

$
0
0


JOSEPH MPANGALA 

Serikali iko Mbioni Kujenga Kiwanda cha Mvinyo pamoja na Juise kutokana na Mabibo ya korosho ambayo yamekuwa yakitupwa mara baada ya korosho kuuzwa na hivyo Wakulima kukosa fedha za ziada kutokana na Tunda hilo.

Akiuliza swali la Nyongeza Katika Mkutano wa 15 kikao cha 29 Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe amehoji Utafiti uliokuwa ukifanywa na Chuo cha Naliendele kilichopo Mtwara kuhusu Kochoko au mabibo ya Korosho umefikia wapi Mpaka sasa kwa lengo la Kuwawezesha wakulima Kuweza kujinufaisha zaidi na zao la korosho.

“Kochoko ni zile washi zinazotokana baada ya mavuno ya korosho wakulima huwa wanazitupa na wengine huwa wanaziuza na wengine wanatengeneza Gongo na inafahamika kwamba Gongo sio pombe haramu isipokuwa namna inavyotengenezwa je Utafiti uliokuwa Ukifanywa na Chuo cha naliendele Umefikia wapi”?

Akijibu swali hilo Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema kupitia Chuo cha Utafiti cha Naliendele tayari wamefanya Utafiti na kutoa maagizo ya ujengwaji wa kinu ili kuweza kuzalisha Mvinyo pamoja na juisi itakayotokana na mabibo kwa lengo la kuongeza thamani zao la Korosho.              

“Ni kweli kabisa chuo chetu kupitia tawi letu la Naliendele tumefanya utafiti wa kina na tumebaini kwamba kuna mazao mengi tunaoweza kuzalisha kutokana na Korosho ikiwemo Juisi na ikiwemo mvinyo maalum unaotokana na mabibo ya Korosho na tumetoa maagizo kwenye tawi letu sasa hivi kujenga kinu cha kuweza kuchakata ili tuweze kuzalisha mvinyo pamoja na juisi ambayo tutaiuza hapa Nchini na hivyo itaongeza thamani na mapato yatakayotokana na zao la Korosho” amesema Hasunga Waziri wa Kilimo.
Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe

IDARA YA UHAMIAJI ARUSHA YAKANUSHA KUPOKEA MALIPO MKONONI

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani Idara ya uhamiaji imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kijamii kuwa idara hiyo inapokea malipo mkononi kutoka kwa wateja wakati inafamika malipo yote ya serikali hulipwa kwa njia za huduma za kifedha.

Kamanda wa Idara ya Uhamiaji mkoani Arusha Mratibu msaidizi Samwel Mahirani ameyasema hayo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake na kuwataka watanzania kuwaamini viongozi wao na kutoa taarifa za malalamiko bila woga

Amekemea vikali wale wote wanatumia mtandao kuichafua Idara hiyo kuacha mara moja na pia kutoa taarifa kwa uongozi pindi wanapoona hawa kuridhishwa na huduma kwani kuna vitengo mbali mbali na box la maoni haoni sababu ya kulizungumza mtandaoni.

“Taasisi zote za umma hazipokei fedha mkononi bali fedha zote za umma zinapokelewa kwa njia ya miamala ya kifedha ikiwemo benki na mitandao ya simu za mkononi” alisema Kamanda

Alisema kuwa Hapendezwi na wanaotumia mitandao ya kijamii kuichafua Idara hiyo kwa kusema wanachukuwa rushwa na kupokea fedha mkononi hilo sio sahihi walitakiwa kufika ofisini kwangu na wakiona hawawezi kuniona basi kuna taasisi za kupambana na kuzuia rushwa badala ya kukimbilia huko.

Amesema Idara hiyo mwaka 2018 wamefanya misako na doria Zaidi 234 na kukamata wahalifu 96 waliofikishwa mahakamani ambapo 128 kutoka mataifa mbali mbali waliondoshwa nchini

Amebainisha kuwa Jumla ya Pasi kubwa za kusafiria 1384 zimetolewa tokea Dec hadi mei mwaka huu sanjari na pasi ndogo 14,183 ambapo idara ya uhamiaji mkoani hapa imezitoa kwa wananchi wanaosafiri nje ya nchi.

Alieleza kuwa wahalifu 314 kati yao 38 walipandishwa mahakamani ambapo 86 waliondoshwa nchini ambapo Idara hiyo imetoa angalizo kwa askari wake wenye tabia hizo kuacha mara maja kwani.

Akatoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitendo viovu na kuacha kutumia mitandao ya kijamii ili na wao kuweza kuboresha huduma zao kwani maoni yanasaidia kuliko kutoa malalamiko kwani hayajengi.

WADAU WA MARADHI YASIYOAMBUKIZA ZANZIBAR WAJADILI HUDUMA BORA ZA MARADHI HAYO

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
Hali ya kiuchumi inayowakabili wagonjwa wengi wa maradhi yasiyoambukiza Zanzibar imetajwa kuwa ni changamoto kubwa katika kupata chakula sahihi cha kupunguza makali ya maradhi hayo.

Akitoa matokeo ya utafiti uliofanywa na Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza katika mkutano wa wadau wa maradhi hayo, Mratibu wa Kitengo hicho Omar Mwalimu alisema wagonjwa wa maradhi hayo wanatakiwa kula zaidi matunda na mboga mboga na kupunguza kutumia mafuta na vyakula vya uwanga.

Alisema katika utafiti huo wamegundua kuwa wananchi wengi wanaelewa juu ya maradhi hayo na njia za kukabiliana nayo kupitia vyombo vya habari na mikutano mbali mbali lakini hali ya kiuchumi ni kikwazo kwao.

Alieleza kuwa tabia ya wananchi kuchelewa kufanya uchunguzi wa afya zao mpaka wapate mabadiliko makubwa ya mwili ni moja ya tatizo linalowakabili wagonjwa wa maradhi yasiyoambukiza nchini.

Omar Mwalimu alisema upatikanaji wa huduma za matibabu ya maradhi yasiyoambukiza katika baadhi ya vituo vya shamba bado hairidhishi na wagonjwa huvunjika moya na kwenda katika vituo hivyo na huamua kubaki nyumbani ama kufuata huduma hizo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.

Aliongeza kuwa tatizo kubwa lipo kwa wagonjwa wenye tatizo la maradhi ya Saratani kwa vile upatikanaji wa dawa za kutibu maradhi hayo ni ghali na wagonjwa wengi hawana uwezo wa kuzinunua.

Hata hivyo Omar Mwalimu aliwashauri wagonjwa wa maradhi yasiyoambukiza kutafuta ushauri wa madaktari waliosomea kabla ya kutumia dawa mbadala ama kufuata tiba ya mitandao.

Alisema hivi sasa wamejitokeza wajanja wengi mitaani na kwenye mitandao ya kijamii wanaotoa matibabu ya maradhi yasiyoambukiza lakini hawana tiba sahihi ya maradhi hayo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Dk. Said Gharib Bilal alisema maradhi hayo yapo na yamekuwa ni sehemu ya maisha ya wananchi wengi, jambo la msingi ni kuwa na elimu ya kujua namna ya kuishi nayo.

Baadhi ya waathirika wa maradhi yasiyoambukiza walioshiriki mkutano huo uliofanyika Kitengo Shirikishi cha afya ya mama na mtoti Kidongochekundu walisema mara nyingi wanapokwenda kutafuta dawa kwenye vituo vya afya vya karibu vijiji, hawapati dawa ama hupata nusu ya kiwango kinachohitajika.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (ZNCDA) Said Gharib Bilali akizungumza katika Mkutano wa wadau wa kujadili upatikanaji huduma bora za afya kwa wagonjwa wa maradhi hayo Zanzibar.
 Mkuu wa Kitengo cha Maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Omar Mwalim akiwasilisha taarifa ya utafiti wa maradhi yasiyoambukiza katika Mkutano wa wadau uliofanyika Kitengo Shirikishi cha mama na mtoto Kidongochekundu.
 Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa kujadili upatikanaji huduma bora za afya kwa wagonjwa wa maradhi yasiyoambukiza wakifuatilia taarifa ya utafiti uliofanywa kuhusu maradhi hayo.
Mshiriki Amour Kassim kutoka Jumuiya ya ZAMWASO akitoa mchango katika mkutano huo.

ST Kids Swahili imefika hadi Makuburi Jeshini

$
0
0
StarTimes imeendelea kutembelea shule za msingi jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili. 

Alhamisi hii walitembelea shule ya Msingi Makuburi Jeshini iliyoko Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo wawakilishi wa StarTimes walikutana na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la awali hadi darasa la nne kutoka shule hiyo.

Pamoja na kuzungumza na wanafunzi wawakilishi wa StarTimes walitoa zawadi kwa ya king’amuzi na Dish kwa uongozi wa shule na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi walioweza kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa.

“Asanteni sana kwa kututembelea Shuleni kwetu na kwa zawadi mlizotuletea sisi pamoja na wanafunzi. Mmewapa changamoto wanafunzi wetu lakini pia mmetuonyesha ni wapi tunahitaji kuongeza juhudi katika ufundishaji kwa sababu hapa tumeona watoto wanaelewa zaidi kwa kutazama kama wanavyojifunza kupitia maudhui ya chaneli yenu ya ST Kids.” Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Mary Antony Manyika.

ST Kids ni chaneli ya kwanza Tanzania ya watoto ambayo vipindi vyake vinapatikana kwa lugha ya Kiswahili, lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kuburudika na katuni na maudhui mengine kwa lugha ambayo wanaifahamu vizuri ili kusaidia ukuaji wao miongoni mwa familia na jamii zao.
“Lengo letu kutembelea shule hizi ni kutambulisha maudhui mapya yanayopatikana katika chaneli ya ST Kids ambayo yako katika lugha ya Kiswahili. Vipindi ni vizuri kwa watoto kwani vinawafundisha stadi mbali mbali za maisha.” Dina Marious Balozi wa StarTimes Kids

“Kila Shule tuliyotembelea tunawasikiliza changamoto zao na sisi kama kampuni tutajaribu kuangalia ni namna gani tunaweza kusaidia. Kwa mfano hapa leo wametueleza shule ina changamoto ya maji, hivyo katika mipango yetu ya shughuli za kimaendeleo tutawafikiria pia.”
Kampeni hii ya kutembelea mashule jijini Dar es Salaam itaendelea hadi mwisho wa mwezi wa tano na itafikia jumla ya shule 7 katika Wilaya 3 za Mkoa wa Dar es Salaam.

Chaneli ya ST Kids inapatikana katika kifurushi cha UHURU kilichoboreshwa kwa watumiaji wa dikoda ya Antenna na kuanzia kifurushi cha SMART kwa watumiaji wa dikoda ya Dish.
Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kushoto) akimkabidhi zawadi ya dishi na dekoda ya Startimes Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Mary Antony Manyika wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
 Mtangazaji wa Efm radio, Dina Marios(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi ya dishi na dekoda ya Startimes kwenye Shule ya Msingi Makuburi Jeshini wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya Msingi Makuburi Jeshini Mary Antony Manyika akizungumza na waandishi wa habari mara baada mara baada ya  Shule ya Msingi Makuburi Jeshini kukabidhiwa zawadi ya dishi na dekoda ya Startimes wakati wa kutambulisha maudhui ya chaneli mpya ya watoto, ST Kids ambayo yameingiziwa sauti za Kiswahili.

USHAHIDI KESI YA ZITTO KABWE WAENDELEA KUTOLEWA

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
SHAHIDI wa pili katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa analichukia jeshi la polisi kuanzia siku alipoona video  kwenye mtandao wa kijamii wa you tube ikimuonyesha Zitto Kabwe  akielezea polisi wanavyowatendea ukatili raia.

Shahidi huyo Mashaka Juma ambaye ni msanii wa filamu, akiongozwa na Wakili wa serikali Mkuu Tumaini Kweka kutoa ushahidi wake, amedai, Oktoba 29,2018 huko Kimara Korogwe akiwa na wenzake wakicheza drafti alifika rafiki yao, Frenky Zong na kuwauliza kama wamepata habari yeyote ambapo wao hawakuwa na taarifa.

"Zong alitutolea simu yake kisha akatufungulia na tukaangalia habari kwenye yuotube ambapo tulimuona Zitto akililaumu jeshi la polisi kwa mambo mbalimbali ambayo wameyafanya wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma," amedai.

Ameendelea kudai kuwa,  kwenye video hiyo Zitto anaonekana akieleza jinsi jeshi la polisi linavyowanyanyasa wananchi, kuteka watu akiwemo  Mo wa Simba na jinsi walivyoenda hospitali kuwateka  watu waliokuwa wakitibiwa na kwenda kuwaua na pia video hiyo inamuonyesha Zitto akielezea jinsi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alivyoshindwa kuwadhibiti askari wake .

Shahidi huyo amedai kuwa, alipoona video ile na taarifa aliyotoa Ziito ambaye anamfahamu kwa muda mrefu,  aliona jeshi la polisi halina thamani kama wameshindwa kulinda raia na mali zake ndipo alipolichukia hadi leo jeshi hilo.


Katika kesi , Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anayodaiwa kutenda, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za  makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

YAJUE MAGARI YENYE GHARAMA KUBWA ZAIDI KUWAHI KUTENGENEZWA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KATIKA maisha kila mtu ana kitu anachokipenda zaidi, watu wengi hasa mashuhuri wamekuwa miongoni mwa watu wanaonunua na kubadilisha magari kama jozi za viatu huku wengi wao wakieleza kuwa ni vitu wanavyopendelea na sio kufanya maonesho kama inavyoelezwa katika mitandao ya kijamii.

Mastaa wengi wamekuwa wakionesha furaha zao kwa magari wanayomiliki akiwemo mchezaji wa Juventus Christiano Ronaldo aliyeonesha gari lake jipya la kifahari aina ya Buggati, Kanye waste pia ameonesha furaha yake baada ya kumiliki Aventador hata mtoto wa mwimbaji maarufu duniani Beyonce, Blue Ivy (3) alionekana kufurahi baada ya kumiliki Ferrari.

Kwa mujibu ya jarida la Lookers, Magari kumi ghali zaidi ni haya hapa;

10. Pagan Huayra Bc
Gari hili linauzwa Euro milioni 2.1 likiwa gari ghali zaidi zaidi kuwahi huko Italia na Horacio Pagani. Jina la gari hilo lilitolewa  a mwekezaji na rafiki wa karibu wa mtengenezaji wa gari hilo Benny Caiola, linafahamika kwa jina maarufu la "The King"

9. Ferrari Pininfarina Sergio
Gari hili linauzwa Euro milioni 2.3, na lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kijana wa mwazilishi wa kampuni hiyo Battista Pininfarina ambaye ni Sergio Pininfarina.

Gari hili limeuzwa maeneo mengi duniani na gari ya kwanza iliuzwa katika falme za nchi za kiarabu pia katika nchi za Japan, Marekani, na Uswizi.

8. Aston Martin Valkyrie
Gari hii inauzwa Euro milioni 2.4, likiwa limetengenezwa na Aston Martini na Red Bull Racing huku matumizi ya gari hilo yakilenga kutumika kama usafiri pamoja na michezo.

7. Lykan Hypersports
Hili linauzwa Euro milioni 2.6 likiwa limeundwa na kampuni ya W.Motors kutoka Lebanon kuwa gari ya kwanza na ya kipekee kutoka Uarabuni. Na moja ya gari ya aina hii imewahi kumilikiwa na Mohammed Bin zayed Al Nahyan kiongozi wa Serikali huko uarabuni kabla ya kubadilishwa na kuwa gari ya polisi.

6. Buggati Veyron
Mansory Vivere raia wa Ujerumani ndiye aliyeunda gari hii ikiwa inauzwa kwa Euro milioni 2.7.

Ilitangazwa rasmi mwaka 2005 na kuwa gari bora na lenye nguvu mara baada ya kutangazwa sokoni na linamilikiwa na kijana mdogo wa miaka 30 Houston Crosta.

5. McLaren P1 LM
Gari hili limetengenezwa na kampuni ya magari ya Uingereza chini ya McLaren's. Likiwa na gharama ya Euro milioni 2.7 limehawi kuvunja rekodi ya gari bora mwaka 2017 kwenye moja ya mashindano ya magari.

4. Lamborghini Veneno Roadster
Linauzwa kwa Euro milioni 3.4, na hadi sasa ni magari 9 pekee yamekwisha tengenezwa huku gari moja ikiwa imeuzwa kwa Euro milioni  8 zaidi ya asilimia 200 ya bei elekezi.


3. Koenigsegg CCXR Trevita
Lilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009 huku ikaielezwa limetengenezwa kwa malighafi bora zaidi ikiwemo Almasi, na linauzwa  kwa Euro milioni 3.7

2. Rolls Royce Sweptail
Gari hii imefungua milango mingi ya ubunifu wa magari bora zaidi. Inauzwa Euro milioni 9.9 likiwa limenunuliwa mwaka 2013.

1. Buggati La Voiture Noire
Ni gari ghali na bora n zaidi kwa mujibu wa jarida la Lookers likiwa linauzwa Euro milioni 14.4 hadi kufikia Machi mwaka huu lilikuwa kinara kwa kuwa gari ghali zaidi, huku tetesi zikieleza kuwa mmliki wa gari hilo ni Ferdinand Piech aliyekuwa mwenyekiti wa kampuni ya Volkswagen (kampuni ya magari Buggati.)

Tamko La Serikali Kuhusu Homa Ya Dengue Mei 16 2019

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA MKUU WA MKOA WA KATAVI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es Salaam.
. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera akila kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Kakunda Akanusha Profesa Kabudi Kuhusika na Mkataba wa Kampuni ya Indo Power Solution

$
0
0
Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda akifafanua jambo kuhusu taarifa za kumuhusisha Profesa Kabudi na sakata la Kampuni ya Indo Power Solution alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma.[/caption] 

Na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda amekanusha shutuma zilizotolewa kuhusu ushiriki wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania katika mchakato wa kumpata mzabuni wa ununuzi wa Korosho ambaye ni Kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya.

Waziri Kakunda amesema kuwa anashanga kuona Profesa Kabudi anatupiwa lawama kuwa ameingiza Serikali mkenge jambo ambalo si kweli kwani wahusika wakuu ni timu ya wataalam kutoa Ofisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kwamba upatikanaji wa zabuni hiyo ulipitia mchakato yote halali kilichotoke ni Serikali kuvunja mkataba baada ya mzabuni kutotimiza masharti yaliyomtaka kulipa ndani ya siku 10 na hata alipoongezewa muda haikutimiza.

“Kumuweka mtu ambaye hana makosa yeyote kwenye suala hili na bahati mbaya sana maagazeti karibu yote yakawa yanaandika yakimlaumu kushauri vibaya Serikalijambo ambalo halina ukweli wowote, Kabudi ambaye wakati huo alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria alikuwa mualikwa tu wa kushuhudia hafla ya utiwaji saini mkataba wa Makubaliano baina ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Kampuni ya Indo Power Solution,” Alisema Waziri Kakunda.

Kakunda alisema kuwa ni ajabu kwa kumlaumu mtu aliyealikwa na kuongeza kuwa timu ya wataalam iliyohusika inaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa anayeshughulikia Viwanda hivyo kumuhusisha Profesa Kabudi ni jambo hili si sawa ni bora hata wangemuhusisha yeye kwa kuwa ndiye Waziri mwenye dhamana na Biashara.

Aidha Waziri Kakunda amesema kuwa ni vyema Watanzania wakaelewa na kutokubali kupotoshwa juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuvunja mkataba na Kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya iliyokuwa imepewa zabuni ya kununua Korosho tani 100 kwa kutofuata masharti ya mkataba.

Alisema kuwa mchakato wa Kuipatia zabuni Kampuni hiyo ulipitia njia mbalimbali zilizohusisha wataalam kutoka pande mbili na kujiridhisha kuwa Kampuni hiyo inavigezo vyote vya vya kupewa zabuni hiyo ya kununua Korosho nchini na kuongeza kuwa pamoja na kuwa imeshindwa kutimiza masharti ya mkataba uliopelekea Serikali kusitisha mkabata bado inabaki kuwa ni Kampuni halali.

Waziri Kakunda ametoa ufafanuzi huu kufuatia kauli iliyotolewa Bungeni jana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu akimtuhumu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashari, Profesa Paramagamba Kabudi kuitia hasara Serikali kwa kumuhusisha na mkabata wa makubaliano ya ununuzi wa Korosho tani 100 na kampuni ya Indo Power Solution ya nchini Kenya ambayo baadae Serikali iliamua kusitisha mkataba wake baada ya Kampuni hiyo kutofuata masharti.

KUMBILAMOTO AWATEMBELEA WALIOPATA MAJANGA MZINGA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto Leo ameendelea na ziara yake ya kutembelea Maeneo ya Manispaa hiyo yaliyopatwa na Madhara kutokana na mvua zinazonyesha, ambapo leo ametembelea kata ya Kivule.

Akiwa katika ziara yake Kumbilamoto ametemebelea eneo lililoangukiwa na Ukuta pamoja na kuwatembelea wale wote waliopatwa na majanga kutokana na kuanguka kwa ukuta huo na kuwasihi wakazi wa Manispaa kuchukua tahadahari kabla ya kufanya ujenzi na kuepuka ujenzi holela.

Kumbilamoto mara baada ya kutembelea eneo hilo alikwenda mpaka kwenye barabara ya Kinzudi Mwanagati ambayo imeharibika na mvua hadi kushindwa kupitika kwa sasa.

Amesema kuwa licha ya barabara hiyo kuharibiwa na mvua lakini tayari Manispaa ilishatenga kiasi cha fedha Milioni 650 ambazo zitafanya ukarabati wa eneo hilo na kujenga daraja linalounganisha mitaa hiyo miwili ambayo inategemeana katika shughuli za Maendeleo.

Kumbilamoto alitoa wito kwa wakazi kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hicho cha mvua zinazonyesha kwa Mamlaka ya hali ya hewa imetangaza kuendelea kuwepo kwa mvua kubwa mpaka Mei 30  mwaka huu
 Sehemu ya Nyumba ambayo imeangukiwa na Ukuta wa nyumba ya jirani kutokana madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.
Kaimu  Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akitoa pole kwa Majeruhi waliobomokewa na Ukuta katika eneo la Mzinga kata ya kitunda jijini Dar es Salaam
 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikagua Barabara iliyoharibiwa na Mvua, barabra hiyo inayounganisha kinzudi na Mwanagati katika kata ya kitunda hivyo Manispaa ya Ilala imetenga milioni 650 kukarabati njia hiyo
 Kaimu Meye wa Manispaa ya Ilala akiwa ameongozana na Diwani wa Kata ya Kitunda wakati wa kukagua uharibifu uliofanywa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam
 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala ,Omary Kumbilamoto akipita kwenye Daraja linalounganisha Kinzudi na Mwanagati ambalo limejengwa kwa mbao na magaogogo ya Minazi lakini Manispaa ya Ilala imetenga fedha Shilingi Milioni 650 kwa ajili ya kurekebisha daraja hilo.

 Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akiangalia eneo la Nyumba iliyoangukiwa na Ukuta kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam eneo la Mzinga Manispaa ya Ilala,ambapo watu wawili wamejeruhiwa katika majanga hayo.

GAVANA SHILATU AMBANA MWENYEKITI SARUJI KUPOTEA

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Tandahimba 

Viongozi wa Serikali za vijiji na vitongoji katika Tarafa ya Mihambwe wilayani Tandahimba wametakiwa kuelewa dhana ya utumishi na uongozi ni dhamana ya wananchi si mwanya wa kujitajirisha au kuonea wengine kinyume na sheria.

Pia viongozi na wajumbe wa kamati za Serikali wametakiwa kuheshimu kanuni na sheria za nchi kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Msimamo huo umetolewa na Katibu tarafa ya mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu alipombana Mwenyekiti wa Kijiji cha Namunda (CUF) Suleiman Kazumari Mkubulu kufuata madai ya upotevu wa mifuko 24 ya saruji.

Shilatu aliwaelekeza viongozi wa serikali za vijiji na vitongoji kuelewa kiongozi asiyeheshimu taratibu za kiutawala ajiweke Kando kabla hajashitakiwa Kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Midhali Mwenyekiti umekiri kimaandishi mbele ya Serikali ya Kijiji na Kamati ya ujenzi, Nakutaka urudishe mifuko ya saruji 24 kabla ya Mei 30, 2019. Chochote kinacholetwa vijijini na Serikali Kuu au Halmashahuri ya wilaya ni mali ya umma." Alisema Gavana Shilatu

Alimtaka Mwenyekiti huyo kutimiza ahadi yake kama alivyohaidi kimaandishi kabla hatua nyingine zaidi hazijachukuliwa kisheria dhidi yake." Alisema Gavana Shilatu.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu alishangazwa na matumizi ya shilingi Milioni 12 fedha ambazo hazilingani na hali halisi ya gharama za ujenzi wa miradi ilivyo.

"Kiasi kikubwa cha fedha hapa kimetumika tofauti na miradi ilivyo. Kamati ya ujenzi ifuatilie kwa kina kujua matumizi kama yanafanana na gharama ya fedha za mradi" Alieleza.

Katika ziara hiyo Gavana huyo alikagua miradi ya maendeleo ya kijiji hicho akiambatana na Wajumbe wa kamati nzima ya Serikali ya Kijiji cha Namunda.








TAARIFA MBALIMBALI ZA UHALIFU KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA

$
0
0
 Bidhaa mbalimbali vikiwemo vipodozi na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini
 Gari aina ya Toyota Mark II iliyokamatwa ikiwa na bidhaa zilizopigwa marufuku nchini
 Watuhumiwa NASIBU JUMA na BRIGHT THOMAS
Watuhumiwa wa matukio ya wizi na utapeli, kutoka kushoto OMARY, HAMIS, ARTHA na PILI


KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WANNE KWA TUHUMA ZA WIZI NA KUGHUSHI NYARAKA MBALIMBALI.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne [04] ambao ni:-

1.     PILI OMARI [30] Mkazi wa Mbezi – Dar es Salaam

2.     M HAMIS NGOWI [40] Mkazi wa Dar es salaama na

3.     OMARY MOHAMED [41] Mwalimu na Mkazi wa Nzovwe

4.     ARTHA KASMIRI [34] Mkazi wa Dar es salaam - Mbezi kwa tuhuma ya wizi katika Benki.


Mnamo tarehe 13.05.2019 saa 14:00 mchana huko katika Benki ya Posta tawi la Mwanjelwa iliyopo Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi kwa kushirikiana na maafisa wa benki hiyo waliwakamata PILI OMARI [30] na MARTHA KASMIRI [34] wote wakazi wa Dar es salaam - Mbezi wakiwa na nyaraka ‘salary slip’ zenye majina ya watu wengine ambao ni watumishi wa idara ya elimu, vitambulisho vya mpiga kura, fomu za utambulisho kutoka Jiji, fomu za mikopo kutoka benki ya Posta na barua za uthibitisho kutoka kwa mwajiri ambazo ni za kughushi.

Watuhumiwa wengine ambao ni HAMIS NGOWI [40] mfanyabiashara na mkazi wa Dar es salaama na OMARY MOHAMED [41] mwalimu na mkazi wa Nzovwe wamekamatwa wakati mtuhumiwa HAMIS NGOWI @ OPTATI NGOWI alipopekuliwa alikutwa na:-

1.     Mihuri 6 ya idara tofauti za serikali.

2.     Laini 10 za mitandao ya simu Vodacom, Tigo na Halotel,

3.     Picha ndogo 3 za watu tofauti ya jinsia ya kike,

4.     Funguo 2 za gari,

5.     Fomu za utambulisho kutoka Jiji,

6.     Fomu za mikopo kutoka benki ya Posta,

7.     ‘Salary slip’ pamoja na barua za uthibitisho kutoka kwa waajiri. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WAWILI WANAOJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI, WIZI NA UBAKAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia vijana wawili ambao ni:-

1.     NASIBU JUMA [20] Mkazi wa Nzovwe Mbeya

2.     BRIGHT THOMAS [19] Mkazi wa Mtaa wa Ndanyella Mbeya

Kwa tuhuma ya kujihusisha na matukio ya unyang’anyi, wizi na ubakaji katika maeneo ya Nzovwe, Iyunga na Iwambi Jijini Mbeya.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 14/05/2019 huko Iyunga katika Klabu cha Pombe cha London kilichopo Jijini Mbeya na katika upekuzi watuhumiwa walikutwa na :-

1.     Mapanga mawili [02]

2.     Mizula miwili [02]

3.     Makoti meusi mawili [02]

Katika mahojiana na watuhumiwa wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 26/03/2019 saa 22:00 usiku huko Mtaa wa Inyala uliopo Kata ya Iyunga na Tarafa ya Iyunga ambapo walivamia nyumbani kwa Mwalimu wa Chuo MUST aitwaye WILLIAM MBATTA na kumjeruhi kwa mapanga sehemu ya kichwani na kisha kutoweka.

Mnamo tarehe 30/03/2019 saa 22:00 usiku katika viwanja vya MUST walimjeruhi ALLEN NYITTI kwa kumkata panga kichwani, kiunoni na tumboni na kupora simu aina ya Samsung Galaxy na pesa taslimu Shiling 21,000/=

Mnamo tarehe 05/04/2019 saa 02:00 usiku huko katika Mtaa wa Ndanyella, Kata ya Nzovwe, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya walimvamia FATUMA HAJI [21] walimbaka na kupora pesa taslimu shilingi 3,280,000/= pia waliiba TV aina ya LG na Redio Sub Woofer, Deck na simu ya mkononi aina ya Samsung J7. Mali zote zikiwa na thamani ya shilingi 4,120,000/=

Mnamo tarehe 04/05/2019 saa 02:45 usiku huko Kota za Tazara zilizopo Iyunga Mbeya walivamia nyumbani  kwa FRANK CHARLES na kumjeruhi kwa kumkata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake yeye na mke wake aitwaye VICTORIA SAMWEL pamoja na kupora TV aina ya Boss yenye ukubwa wa inchi 55.



KUKAMATA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.


Mnamo tarehe 16/05/2019 saa 05:00 Alfajiri huko maeneo ya Block “T”, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, Askari Polisi wakiwa doria katika maeneo hayo waliliona gari lenye namba ya usajili T.937 CKD aina ya Toyota Mark II Blit na kulitilia mashaka na ndipo kukuta limebeba bidhaa mbalimbali zilizopigwa marufuku nchini ambazo:-

1.     Pombe kali aina ya PRINCE katoni sita @ chupa 20 sawa na chupa 120

2.     Pombe kali aina ya Officer”s Verve katoni 24 @ chupa 20 sawa na chupa 480

3.     Condom aina ya Ultimate Assured Protection katoni 63 ambazo zilitolewa na Serikali ya Marekani kwa nchi ya Zambia.

4.     Panga moja.

5.     Carolight 120ml pcs 36

6.     Citrolight 120ml pcs 84

7.     Coco Pulp 150mls pcs 24

8.     Coco Pulp 500mls pcs 06

9.     Coco Pulp 300mls pcs 36

10.Coco Pulp Lightening oil 50mls pcs 72

11.Coco Pulp 50g pcs 06

12.Carotone Crème ndogo 65mls pcs 24

13.Cocoderm pcs 06

14.Clinic Clear pcs 06

15.Extra Clair 120mls pcs 54

16.Elle 5 Crème pcs 3

17.Diproson tube 30g pcs 74

18.Diproson lotion 30mls pcs 48

19.Top Lemon Plus 170mls pcs 84

20.Carotone black spot corrector pcs 06

21.Dermotyl tube 15g pcs 10

22.Dermotyl lotion 30mls pcs 90

23.Dodo Crème ndogo pcs 06

24.Clairmen pcs 12

25.Bronz tone crème 125ml pcs 15

26.Miki Clair 160ml pcs 48

27.Movate Cream 30g pcs 50

28.Oranvate gel 30g pcs 50

29.Beaution Cream 330mls pcs 12

30.Miss Caroline 150mls pcs 12

31.Carolight Cream 120mls pcs 78

32.Diana lotion 30mls dozen 03 sawa na pcs 36

33.Teint Clair 150mls pcs 48

34.Betasol lotion 30mls pcs 36

35.Betasol tube 15g pcs 40

36.Perfect white cream 150mls pcs 12

37.Perfect white lotion 30mls pcs 06

38.Lemon vate cream 30g pcs 40

39.Mont Claire 30g pcs 10

40.Neoprosone Gel 30g pcs 10

41.Epiderm Creme 15g pcs 41

42.Epiderm Crème 30g pcs 24

Gari hilo lilikuwa likitokea Tunduma kuja Mbeya likiwa na bidhaa hizo. Gari pamoja na vielelezo vipo kituo cha Polisi. Msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa waliokuwa wakisafirisha bidhaa hizo unaendelea.


KUPATIKANA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI.

Mnamo tarehe 13.05.2019 majira ya saa 21:00 usiku huko maeneo ya Iwambi, Kata ya Iwambi, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Polisi walimkamata kijana mmoja aitwaye ELIA MWAKALIKWE [25] Mkazi wa Iwambi akiwa na Pombe Kali zilizopigwa marufuku nchini aina ya Verve katoni 27 zikitokea nchini Zambia.


Imetolewa na;

[ULRICH O. MATEI – SACP]

   KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


JPM atengua uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wawili.

Wafanyabiashara Jijini Dodoma Waunga Mkono Katazo la Matumizi ya Mifuko ya Plastiki

$
0
0

Baadhi ya wafanyabiasha katika Jiji la Dodoma wametoa maoni yao kuhusu katazo la matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki ifikapo tarehe 1 Juni 2019 nakusema kuwa katazo hilo limekuja wakati sahihi.

Akizungumza na mwandishi wetu Katibu Mkuu wa Soko Kuu la Majengo, Jijini Dodoma, Eliamani Mollel amesema kuwa wao kama viongozi wamepokea na kuunga mkono marufuku ya kutotumia na kufanya biashara ya mifuko ya plastiki, Serikali ina nia ya dhati kabisa kukataza hii mifuko kutokana na uharibifu wa mazingira, sisi wenyewe ni mashuhuda tunaona mifuko inaleta uharibifu wa mazingira, kuziba kwa mitaro ya maji na adha zingine nyingi zinazofanana na hizo, kwa hiyo sisi kama viongozi kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji , jiji kwa ujumla tunaunga mkono hili la Wazari Mkuu la kukataza matumizi ya mifuko ya plastiki.

Akichangia maoni hayo Mfanyabiashara wa Vifungashio vya biadhaa ikiwemo mifuko ya plastiki katika Soko la Majengo Jijini Dodoma, Isack amesema kuwa licha ya mud uliotolewa kuwa mfinyu lakini yupo tayari kuhakikisha ifikapo tarehe 1 Juni 2019 anakuwa amekwisha acha kuuza mifuko ya plastiki baadala yake atakuwa anauza mifuku ambayo inakubalika kwa mujibu wa katazo hilo lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hivi karibuni.

Naye Evarist Korneli Sanzi, Mfanyabiashara wa Soko la Changombe Jijini Dodoma amesema kuwa binafsi amefurahishwa sana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililotolewa na Waziri Mkuu kwani mifuko hiyo imekuwa ikiharibu mazingiora na uchafu na kuongeza kuwa kama angekuwa na uwezo angekuwa amekemea siku nyingi sana kwa sababu imekuwa ni kero, lakini aliposikia tamko la Waziri Mkuu amefurahi sana.

Mfanyabiashara mwingine aliyechangia maoni yake, Badiliko Ally Ndudi, ambaye ni mfanyabiashara wa vifungashio katika Soko la Majengo jijini Dodoma amesema kuwa pamoja na changamoto zitakazojitokeza lakini katazo la matumizi ya plastiki amesema kuwa mifuko ya plastiki ina athari kwa afya ya binadamu kwa mujibu wa wanasayansi walivyodai.

Mfanyabiashara wa Soko Kuu la Majengo Jijini Dodoma, Urban Munishi anasema kuwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki kwake ni fursa kutokana na aina ya bidhaa anayouza ikiwa ni nafaka pamoja na vikapu. Anasema kuwa wateja wa vikapu wameongezeka na mifuko ya sandarusi wameongezeka mara baada ya tangazo la marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo Juni Mosi 2019.

Kwa upande wake mnunuzi wa bidhaa katika Soko la Majengo jijini Dodoma, Bi. Josinah Leornad amesema kuwa amefurahishwa sana na katazo hili la matumizi ya mifuko ya plastiki kwani imekuwa kero kwani ulikuwa kila ukinunua kitu kidogo unafungiwa kwenye mifuko hiyo unajikuta nyumbani unakuwa na mifuko mingi sana na baadae ukiichoma moshi wake ni hatari kwa afya kwa hiyo nimefurahi kusikia wanaleta mifuko mbadala ambayo pia itakuwa rafiki kwa mazingira kwasabubu mifuko ya plastiki imekuwa ikisababisha vyanzo vya maji kuharibika, mitaro kuziba hivyo kusitishwa kwake kuta okoa mazingira.

Mwenyekiti wa Soko la Chang’ombe jijini Dodoma anasema kuwa katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki wanaliunga mkono kwani kwao ni kama limepiga ndege wawili kwa jiwe moja kwanza kulinda mazingira ambayo mifuko imekuwa ikizagaa zagaa lakini pili linawapa ahueni wafanyabiasha kwakuwa wamekuwa wakipata hasara kutokana na kugawa mifuko bure kwa wateja wao.

Amesema kuwa vifungashio mbadala ni rafiki kwa mazingira kutokana na malighafi iliyotumika kutengenezea mifuko hiyo, ameipongeza Serikali kwa uhamasishaji mkubwa ilioufanya hasa kwa kuhakikisha wananchi wote wanapata ujumbe mfupi wa kwa njia ya simu kuhusu katazo hilo hivyo anaimani kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019 hakuna mwananchi atakayekuwa anatumia mifuko ya plastiki labda awe ameau kukaidi kwa makusudi tu.

Hassan Ramadhan Kikoro, mfanyabiashara wa nafaka na vifungashio Soko la Chang’ombe Jijini Dodoma amesema kuwa kutokana katazo hili la matumizi ya mifuko ya plastiki ameanza kuuza mifuko mbadala ambapo amesema kuwa ifikapo tarehe 31 Juni 2019 kama bado atakuwa na bidhaa ya mifuko ya plastiki ataichoma moto ili kuendana na amri iliyotolewa na Serikali, na kuongeza kuwa anafahamu athari zitokanazo na mifuko ya plastiki ila wamekuwa wakiiuza kwakuwa hakukuwa na mifuko mbadala wala katazo lolote.

Kwa upande wake mfanyabiashara wa Soko la Chang’ombe, Bibi. Elizabeth Boniphace Risasi ameishukuru Serikali kwa kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kuwa kwake binafsi imemcheleweshea maendeleo kwakuwa bidhaa zake anazouza (vikapu) kutonunuliwa kutokana na uwepo wa mifuko hiyo licha ya ukweli kwamba inachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.A

Rais Magufuli afanya kikao cha kazi na RC, RAS, DC, DAS na DED wote

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kujenga ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 16 Mei, 2019 katika kikao cha kazi kati yake na viongozi hao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu.


Mhe. Rais Magufuli amewaonya baadhi ya viongozi hao ambao wamekuwa na migogoro baina yao na hivyo kuathiri utendaji kazi na amesema endapo vitendo hivyo vitaendelea hatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa katika nyadhifa zao.


Pamoja na kuwataka kuwa waadilifu na wenye nidhamu kazini, Mhe. Rais Magufuli amewataka kusimamia kwa ukaribu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kusimamia ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali, kusimamia ulinzi na usalama na kusimamia rasimali za umma.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya zinazowezesha mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali kwenda vizuri na amewahakikishia kuwa anawaamini na anatarajia wataendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.


“Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki cha leo sote tutakwenda kwa mwelekeo mzuri zaidi, nendeni mkachape kazi, mimi ndiye niliyewaweka kwenye nafasi hizo na ninafuatilia utendaji kazi wa kila mmoja wenu, sitarajii kusikia tena hamuelewani miongoni mwenu”amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.


Katika kikao hicho Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili viongozi hao katika maeneo yao ya kazi na ameahidi kwenda kuzishughulikia.

Kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.


Mhe. Homera pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.


Baada ya kikao hicho, viongozi hao wamekula futari na Mhe. Rais Magufuli aliyoiandaa kwa ajili yao.

 

 
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

16 Mei, 2019



 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakuu wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU 


Beatrice's Night's held at Golden Memory hall at Sinza Mori in Dar es salaam

$
0
0
 Beatrice John Maroda's night held at Golden Memory hall at Sinza Mori in Dar es salaam 











Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images