Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 16,2019


DAWASA WAANZA USAJILI MAGARI YANAYOTOA HUDUMA YA KUUZA MAJISAFI DAR NA PWANI

$
0
0
 Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akibandika moja ya magari ambayo yaliletwa kwenye usajili ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limefanyika kituo cha Chuo Kikuu Ardhi nyenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal. Anayeshuhudia ni dereva wa gari hilo. 
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo kwa dereva mara baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. 
Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi (kulia) akitoa maelekezo cheti cha utambuzi kwa kwa dereva mara baada ya kumaliza zoezi la ubandikaji wa stika ili kuweza kuendelea kutoa huduma ya kuuza majisafi jijini Dar es Salaam. 
Magari yakipata yakijaziwa maji tayari kwenda kuuza. Picha zote na Cathbert Kajuna - 

Kajunason/MMG. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

 Mamlaka ya Majisafi na MajiTaka Dar es Salaam (DAWASA) limeanza kutekeleza zoezi la usajili na utoaji wa vibali kwa magari ya kusambaza majisafi (water Bowsers) katika jiji la Dar es Salaam na Pwani. Zoezi hilo la Usajili litaendeshwa kwa wiki mbili kuanzia Mei 15 litadumu kwa wiki mbili mpaka Mei 29, 2019 eneo la kituo cha Chuo Kikuu Ardhi nyenye matanki ya DAWASA maarufu kama Terminal, Tegeta na Bagamoyo.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akisimamia zoezi hilo Afisa Mawasiliano wa DAWASA Joseph Mkonyi amesema kuwa zoezi hilo linalengo la kuwatambua wauzaji wote wa majisafi ikiwa na kuangalia usalama wa vyombo wanavyotumia kuwauzia maji wananchi.

 "Niwaombe wote wenye kufanyabiashara ya majisafi kujitokeza ili tuweze kuwatambua na kuwapa leseni na kuwapa mikakati yenye lengo la kujenga ili watoe huduma salama," amesema Mkonyi. Zoezi hilo la usajili linamtaka mwenye gari kuja na vielelezo ikiwemo picha moja ya rangi ya mmiliki wa gari na nakala ya kitambulisho chake (KURA, UTAIFA au HATI YA KUSAFIRIA). Kingine ni Nakala ya kasi ya gari, nakala ya bima ya gari na nakala ya leseni ya dereva vyote viwe vimethibitishwa na mwanasheria.

Amesema kuwa matenki yatakayokuwa yamekidhi vigezo vya kupata usajili yatasafishwa na dawa maalumu ya kuua wadudu kwenye mantenki na kubandikwa stika ya DAWASA. Amesisitiza kuwa baada ya zoezi hilo kuisha Mei 29, 2019 gari litakalokuwa halijasajiliwa halitaruhusiwa kuendesha biashara ya kutoa huduma ya kuuza maji na wananchi wanashauriwa kutoa taarifa kwa endapo watayaona magari hayo yakitoa huduma bila kuwa na vibali ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.

BEI YA VYAKULA SOKO LA KINYEREZI JIJINI DAR

$
0
0
Bei ya fungu la Magimbi ni kati ya  sh.1000/= mpaka 2000/= katika soko la Kinyerezi wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kama inavyo onekana katika picha.
Baadhi ya wananchi wa maneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam wakiwa katika soko la Kinyerezi wilaya ya Ilala wakijipatia mahitaji yao mbalimbali ambapo na Maboga moja ni sh. 1000 mpaka 4000 Magimbi ni sh.1000 mpka 2000 (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
pichani ni Maboga moja ni sh. 1000 mpaka 4000 (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Bei za fungu la viazi katika soko la Kinyerezi wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kama inavyo onekana katika picha.
 

BEI YA VITOWEO NDANI YA SOKO LA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Mfanyabiashara wa Kuku katika soko la Kinyerezi wilaya ya Ilala akimhudumia mteja wake leo jijini Dar es Salaam,ambapo bei ya kipande cha kuku ni kati ya sh. 1000/= mpaka 3500/=.
Sehemu ya kukaangia kuku katika soko la Kinyerezi wilaya Ilala kama inavyoonekana katika picha. 



Wafanyabiashara wa Samaki katika soko la Kinyerezi wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam,wakiendelea na shughuli zao mbalimbali katika soko hilo leo ambapo bei ya samaki wanauzwa kati ya sh. 2000/= mpaka 35,000/= (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv).

Wafanyabiashara wa Samaki katika soko la Kinyerezi wilaya ya Ilala akimhudumia mteja wake leo jijini Dar es Salaam.

NEWZ ALERT: SPIKA NDUGAI ASITISHA UWAKILISHI MAKAMU WA KWANZA WA RAIS BUNGELA AFRIKA,STEPHEN MASELE

$
0
0
SPIKA wa Bunge Mhe. Job Ndugai, amesitisha uwakilishi wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Stephen Masele katika bunge hilo kuanzia leo Mei 16, 2019.

Sababu za hatua hiyo, Mhe. Ndugai amesema ni kutokana na utovu mkubwa wa kinidhamu ulioonyeshwa na Mhe. Masele ikiwemo kukaidi kurejea nyumbani kutokana na vitendo hivyo ili ahojiwe na Kamati ya Bunge ya Haki maadili na madaraka ya bunge.

Kwa sasa Mhe. Masele hyuko nchini Afrika Kusini akiongoza vikao vya bunge la Afrika (PAP).

Akitoa taarifa ya Spika bungeni jijini Dodoma leo Mei 16, 2019, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai aliliambia bunge kuwa, “Kuna matatizo mkubwa sana ya kinidhamu yanayofanywa na Mhe. Stephene Masele, tuliagiza arudi nyumbani kuanzia Jumatatu iliyopita lakini amegoma, hata jana clips zinaonyesha akihutubia bunge la PAP japo ameitwa na spika lakini amedai kuwa ameagizwa na Waziri Mkuu a disregard (akaidi) wito wa spika aendelee tu na mambo yake kule kitu ambacho ni uongo na kudhalilisha nchi,” Alisema Spika Ndugai, na kuendelea.

“Ni kiongozi ambaye amekuwa akifanya mambo ya hovyo hovyo ndio maana tumemuita ili ahudhurie kwenye kamati ya maadili atufafanulie huenda yuko sahihi lakini kwa mtazamo wetu amekuwa akifanya mambo ambayo ni hatari kubwa ikiwemo kugonganisha mihimili amekuwa akipeleka kwenye mhimili wa serikali juu kabisa maneno mengi ya uongo na ushahidi upo, kulidhalilisha bunge, ni kiongozi ambaye amejisahau hajui hata anatafuta kitu gani.” Alisema Spika Ndugai.

“Sasa kwakuwa tumekuwa tukimuita tangu Jumatatu na hataki kurudi ningependa kulifahamisha bunge hili kwamba kwa niaba yenu na mamlaka niliyonayo basi nimemuandikia barua Rais wa PAP ya kusitisha uwakilishi tuliompatia Mhe. Masele katika bunge la PAP hadi hapo kamati ya haki maadili na madaraka ya bunge itakapokamilisha uchunguzi dhidi yake na kukamilisha taarifa yake, kwahiyo kwamuda temporarily suspension ya Mhe. Masele kuwa mbunge wa bunge la Afrika hadi hapo tutakapomalizana naye hapa.” Alifafanua Spika Ndugai.
Pichani shoto ni SPIKA wa Bunge Mhe. Job Ndugai akipeana mkono na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Stephen Masele.kwa hisani ya K-VIS BLOG

BENKI NIC TANZANIA YAFTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume akiowaongoza baadhi ya wageni na wateja wa benki hiyo katika iftar iliyoandiliwa kwa ajili ya wateja wao katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wageni na wateja wa NIC Bank wakipata iftar kwa pamoja iliyoandalia na benki hiyo katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Tanzania, Margaret Karume (kulia) akizungumza na wateja wa benki hiyo baada ya iftar iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wake, katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana.

WAZIRI MKUU AFUTURISHA WAHESHIMIWA WABUNGE JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakiwaongoza Waheshimiwa Wabunge kupata futari aliyowaandalia katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi, Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Joseph Selasini wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakwanza kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenknlojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Waziri Mkuu)-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu wa Ofisi ya Bunge Bi. Jane Kajiru (wakwanza kushoto) wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. PICHA NA BUNGE

WAKULIMA KISARAWE WAANZA KUPATA MAFUNZO YA KILIMO MKATABA

$
0
0

Afisa wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA), Veronica Kilango, akisoma risala mbele ya Afisa Mtendaji Kata ya Mzenga, Godfrey Ambelle kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya kilimo cha mkataba na ufugaji kwa vikundi 27 vilivyopo katika Tarafa ya Mzenga.
Wawakilishi wa wakulima ambao ni viongozi wa vikundi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mratibu wa Mradi wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA), Saidi Simkonda, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya kilimo cha mkataba na ufugaji kwa vikundi 27 vilivyopo katika Tarafa ya Mzenga vyenye wanachama 850 wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mzenga, Godfrey Ambelle na Diwani wa Kata hiyo, Mohammed Rubondo.
Afisa wa Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association (TWCHA), Veronica Kilango (kulia), akimkabidhi risala, Afisa Mtendaji Kata ya Mzenga, Godfrey Ambelle kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya kilimo cha mkataba na ufugaji kwa vikundi 27 vilivyopo katika Tarafa ya Mzenga.
Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Mzenga, Agness Msanya akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwalimu Willbroad Rosper kutoka Taasisi ya Family Hope Foundation Tanzania (FAHOT), akiwa pamoja na Afisa Kilimo, Fatuma Kipingu katika hafla hiyo.
Afisa Mtendaji Kata ya Mzenga, Godfrey Ambelle kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, akizungumza.
Diwani wa Kata ya Mzenga, Mohammed Rubondo akizungumza.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, ambaye ni Afisa Tarafa ya Mzenga, Mulael Angelo akizungumza.
Afisa Ugani kutoka Kampuni ya Kilimo Joint, Joel Nchimbi akizungumza.
Mkulima wa Kata hiyo, Salum Kiame, akichangia jambo kwenye uzinduzi huo.




Na Dotto Mwaibale, Kisarawe

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Shirika la The Winamwanga Cultural Heritage Association wameanza kutoa mafunzo ya kilimo cha mkataba na ufugaji kwa vikundi 27 vilivyopo katika Tarafa ya Mzenga vyenye wanachama 850.

Mafunzo hayo ya mwezi mmoja ambayo yameanza jana yatafanyika katika Kituo cha Agricuture Resouce Center kilichopo Kata ya Mzenga ambayo yatawakutanisha wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakiwemo wawakilishi wa vikundi vya wakulima, watengenezaji na wasambazaji wa pembejeo za kilimo, Taasisi za kifedha pamoja na wanunuzi wakubwa wa mazao.

Akizungumza juzi wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Mratibu wa Mradi wa shirika hilo, Saidi Simkonda alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wakulima wa kujua mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na kilimo ili kufanya kilimo chenye tija.

Simkonda aliongeza kuwa pamoja na mambo mengine Bodi ya shirika hilo ilikaa na kuona ni bora kuwa na leseni ya biashara ili shirika liweze kuanza kununua mazao ya wakulima wake kwa wakati ili kufanya kilimo cha mkataba kiwe cha moja kwa moja ambapo Halmashauri ya wilaya hiyo imetoa leseni ya biashara kwa shirika hilo yenye namba B.2874206.

Mratibu huyo alitaja mafanikio waliyopata katika kufanikisha kilimo hicho cha mkataba kuwa ni kupata ardhi yenye ekari 50 toka Serikali ya Kijiji cha Gwata kwa ajili ya kuwekeza kiwanda cha kusindika nafaka na kutoa unga wa mahindi chenye uwezo wa kusindika tani 20 kwa masaa 24 kupitia mtambo wenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni mia moja na kumi na mbili za kitanzania kutoka Kampuni ya Shijia Nhuang Hongdefa Machinery Comp Ltd ya Nchini China.

Afisa Mtendaji Kata ya Mzenga, Godfrey Ambelle akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, alisema elimu watakayoipata ndiyo itakayopelekea kuwatoa katika dimbwi la umaskini kupitia kilimo hicho cha mkataba na kuwa kinachohitajika ni soko la uhakika wa mazao ya wakulima.

SERIKALI KUFANYA UKAGUZI NA TATHMINI YA KINA YA MIRADI YOTE YA UMWAGILIAJI NCHINI-MHE MGUMBA Inbox x

$
0
0

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 16 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 16 Mei 2019 wakati wa mkutano wa kumi na tano wa Bunge la Bajeti Jijini Dodoma.




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo, Dodoma

Serikali iko katika mchakato wa kufanya ukaguzi na tathmini ya kina ya miradi yote ya umwagiliaji nchini ili kufanya uhakiki wa eneo la umwagiliaji kwa lengo la kubaini ubora wa miradi, thamani ya fedha, gharama za mradi na mahitaji halisi ya sasa ya kuboresha, kuendeleza na kuongeza miradi mipya ya umwagiliaji.

Aidha, baada ya tathmini hiyo Serikali itaendelea kutafuta fedha ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha mabwawa na skimu za umwagiliaji nchini ikiwemo mradi wa umwagiliaji katika bonde la Mkomazi zinaendelezwa na kuwanufaisha wananchi wa Mombo na taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 16 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Mhe Timotheo Mnzava aliyetaka kufahamu mpango wa Serikali katika utekelezaji wa mradi wa Umwagiliaji katika Bonde la mto Mkomazi.

Alisema kuwa katika miaka ya 1980 Serikali kupitia washirika wa maendeleo, Wakala wa Ushirikiano wa Kitalaam wa kimataifa wa Serikali ya Ujerumani (Germany Agency for Technical Cooperation Ltd) ulifanya upembuzi yakinifu (Feasibility studies) kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Mkomazi katika tarafa ya Mombo, Halmashauri ya Korogwe. Hata hivyo taarifa za upembuzi yakinifu na usanifu zilibaini kuwa ujenzi wa bwawa hilo ungesababisha kuongezeka kwa maji katika ziwa Manga na kupelekea kuzama kwa Kijiji cha Manga Mikocheni pamoja na mashamba ya wakulima.

Mhe Mgumba alisema kuwa kutokana na changamoto hiyo katika mwaka 2014/2015, wataalam wa ofisi ya kanda ya umwagiliaji ya Kilimanjaro walifanya mapitio ya upembuzi yakinifu na usanifu uliofanywa katika eneo hilo kwa lengo kuepusha uwezekano wa kufurika kwa Ziwa Manga, kuzama kwa Kijiji cha Manga Mikocheni na Mashamba ya wakulima kutokana na ujenzi wa bwawa. Mapitio hayo yalibaini uwezekano wa ujenzi wa bwawa na mradi wa umwagiliaji katika eneo hilo bila kuathiri wakazi wa eneo hilo. Mapitio ya usanifu huo yalibaini kuwa ujenzi wa bwawa pekee utagharimu Shilingi 1,543,736,877.

Aidha, akijibu swali la Mbunge wa Kondoa Mjini Mhe Edwin Mgate Dannda aliyetaka kufahamu ni lini andiko la mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji katika Kijiji cha Mongoroma, Kata ya Serya wenye eneo la ekari 3000 utaanza utekelezaji wake, Mhe Mgumba alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2010/2011 Serikali kupitia Idara ya Umwagiliaji ilituma Shilingi milioni 300 kwa ajili kuendeleza miradi ya umwagiliaji ya Kisese, Kidoka na Mongoroma Serya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wakati huo.

Alisema Kati ya fedha hizo Shilingi 143,265,000 zilitumika kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu katika mradi wa Mongoroma Serya uliopo katika Kata ya Serya. Kazi zilizofanyika ni pamoja na upimaji wa sura ya ardhi (Topographical Survey), usanifu wa kina (detail design), matayarisho ya gharama za ujenzi, tathmini ya rasilimali maji (Hydrological survey), tathmini ya awali ya mazingira, utafiti wa udongo (Soil analysis) na masuala ya jamii.

Aliongeza kuwa Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa bwawa la Mongoroma Serya ulibaini kuwa bwawa hilo lingegharimu Shilingi bilioni 4 kwa wakati huo. Aidha, bwawa hilo lingekuwa na uwezo wa kumwagilia zaidi ya hekta 3,000 na kunufaisha zaidi ya wakulima 12,000 kwa ajiili ya kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya binadamu, unyweshaji wa mifugo na wanyama pori pamoja na ufugaji wa samaki katika vijiji vya Mongoroma, Serya na Munguri.

Mgumba alisema Serikali iko katika mchakato wa kufanya tathmini ya kina kwa miradi yote ya umwagiliaji nchini ili kubaini thamani ya fedha, ubora wa miradi na mahitaji halisi ya uboreshwaji, uendelezwaji na kuchagua miradi michache kwa utekelezaji wa ujenzi kwa miradi yenye TIJA, matokeo na manufaa makubwa kwa wakulima na Taifa kwa ujumla. Aidha, baada ya tathmini hiyo na kutegemea upatikanaji wa fedha serikali itahakikisha bwawa hilo na skimu zingine zitajengwa.

PANAFRICAN ENERGY TANZANIA YASAINI MKATABA WA KUFADHILI UJENZI MIRADI YA AFYA WILAYA YA KILWA

$
0
0
Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imesaini mkataba wa ujenzi wa Kituo cha Afya Somanga na upanuzi wa hospitali ya Wilaya Kinyonga.

Mkataba huo wenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia mbili (1.2bilion) umesainiwa kati viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kampuni ya Pan African Energy ambao ni wadau wa maendeleo katika Wilaya ya Kilwa. Utiaji saini huo umeshuhudiwa na wawakilishi wa kampuni ya Pan African na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Mkurugenzi wa Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo uliokuja kwa wakati na kueleza kuwa kwa muda mrefu Wilaya ya kilwa ilikuwa na changamoto katika sekta ya Afya lakini kwa sasa changamoto hizo zinakaribia kwisha kutokana na halamshauri yake kuweka nguvu katika kuzitatu.

‘ Tangu mwaka 2017 tumepokea zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni mia nane kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI katika mpango wa uboreshaji wa Miundo mbinu ya sekta ya Afya ambapo vituo vinne vya Afya vya Masoko, Tingi, Pande na Nanjilinji, na sasa mchango wa hawa wadau wametuongezea nguvu nyingine katika kuendeleza sekta ya Afya.

Alisema msaada huo wa Pan African utaongeza idadi ya vituo vya Afya kutoka vitano vya sasa hadi sita ambapo kati ya hivyo vituo vinne vitakuwa na uwezo wa kufanya upasuaji na kuongeza damu kwa wanawake wajawazito.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe.Abuu Mjaka amewashukuru kwa mara nyingine kampuni hiyo kwa msaada huo kwani ni mara ya pili wanatoa msaada mkubwa baada ya ujenzi wa awali wa kituo cha Afya cha Nangurukuru. ‘Nyie sasa tunawatambua rasmi si kama wadau tu bali familia ya Kilwa’’ aliongeza Mhe.Mjaka.

Ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga ulianza kwa Mchango wa nguvu za wananchi ambapo mpaka sasa jengo la mapokezi lipo katika hatua ya linta ambapo zaidi ya shilingi milioni sabini kutokana na mchango wa wananchi , halmashauri pamoja mchango binafsi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli wa shiingi milioni ishirini(20,000,000) aliyoitoa mwaka 2017 akiwa katika ziara mkoani Lindi. Mhe.Rais alitoa msaada huo baada ya kuombwa na wananchi waliomsimamisha katika kata ya Somanga, msaada huo ulikuwa chachu kwa wanachi wa kata hiyo na hivyo wakaanda kuchangia nguvu zao.

Upanuzi huo utahusisha ujenzi wa Jengo la mapokezi,Jengo la wazazi, Upasuaji , chumba cha kuhifadhia maiti na chumba cha kufulia nguo vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya milioni mia nane na thelathini.

Katika hospitali ya Wilaya ya Kinyonga upanuzi utahusisha chumba cha kuhifadhia maiti na Bohari ya dawa thamani ya shilingi milioni mia nne.

Baada ya kukamilika kwa ujenzi Kituo cha Afya cha Somanga, Wilaya ya Kilwa itakuwa na vituo vya Afya sita ambavyo ni Somanga, Tingi, Masoko,Nanjilinji , Pande na Njinjo..
Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Ritha Mohele na Meneja uwajibikaji kwa jamii wa Kampuni hiyo, Andrew Kashangaki, wakiwapa mkataba uliotiwa saini kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kilwa Abuu Mjaka na DED wa halmashauri ya wilaya hiyo Renatus Mchau.
Mwanasheria wa kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania, Ritha Mohele akisaini mkataba kwa niaba ya kampuni hiyo,kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga.
Baadhi ya mashuhuda walio hudhuria kushuhudia mkataba uliotiwa saini kwa ajili ya ufadhili wa ujenzi wa miradi ya afya itakayo gharimu zaidi ya billion moja za kitanzania.miradi hiyo sehemu ya kuhifadhia maiti, duka la dawa la wilaya na marekebisho ya hospital ya Somanga kwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya kilwa Abuu Mjaka,na DED wa halmashauri ya wilaya hiyo Renatus Mchau.

Tigo yasajili laini za watumishi wa Umma Dodoma

$
0
0
 Afisa usajili laini za simu kutoka kampuni ya  Tigo Regan  Emmanuel (wa kwanza kulia), akisajili laini ya mteja wa kampuni hiyo kupitia utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana. Kushoto ni afisa mwingine wa Tigo Jackson Jerry akimsajili mteja.
 Afisa usajili laini za simu kutoka kampuni ya  Tigo Regan  Emmanuel (wa kwanza kulia), akisajili laini ya mteja wa kampuni hiyo kupitia utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana. Kulia kwake ni afisa  mwingine wa Tigo Jackson Jerry.
 Afisa usajili laini za simu kutoka kampuni ya  Tigo Regan  Emmanuel (kushoto), akisajili laini ya mteja wa kampuni hiyo kupitia utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana. Kulia ni afisa mwingine wa Tigo Placida Jamson 
Maafisa wa Kampuni ya Tigo wakisajili laini za simu za watumishi wa Umma kupitia  utaratibu mpya ya usajili wa laini za simu kwa njia ya alama za vidole katika mji wa Kiserikali wa Mtumba mjijini Dodoma jana.

JIJI LA TANGA LAELEZA NAMNA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI VILIVYOSABABISHA KUKOSA MAPATO Inbox x

$
0
0
  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi akisisitiza jambo wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kulia niKaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi
 Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi akizungumza wakati wa kikao hicho
 Diwani wa Kata ya Maweni Jijini Tanga Calvas akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe Mbaraka Sadi
 DIWANI wa Kata ya Mswambweni (CUF) Abdulrahamani  akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CCM) Saida Gadafi
 Baadhi ya madiwani wakipitia makabrasha wakati wa kikao hicho
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imeeleza namna vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais John Magufuli vilivyowasababishia kukosa mapato huku vyanzo vyake vya mapato 15 kufutika na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ya maendeleo.
Kauli hiyo aliitoa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mustapha Selebosi wakati wa kikao cha baraza la Madiwani cha kuwasilisha taarifa ya utendaji wa kata kilichofanyika Jijini hapa na kusema hali ya Halmashauri imekuwa mbaya kutokana na vitambulisho hivyo kugawiwa kwa wafanyabiashara wasi walengwa.
Alisema kuwa Jiji hilo lilikuwa na jumla ya vyanzo vya mapato 38 ambavyo vilikuwa vinatarajiwa kuliingiza Halimashauri hiyo bajeti ya Bil 15 lakini ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wasio stahiki imesababisha kasoro hiyo.
Alidai chanzo cha kupelekea hali hiyo kimesababishwa na Watendaji wa kata na Mitaa kwa kushindwa kusimamia kwa ukaribu ugawaji wa vitambulishi hivyo kwa watu wanaostahili na badala yake wamewagawiwa hata wafanyabiashara wasihusika.
“Watendaji mmetuangusha mmegawa vitambulisho hata kwa wafanyabiashara wasiostahili na mmefanya hivyo ili kuvimaliza lakini ni athari kwetu hasa Halmashauri hatuna fedha na miradi mingi itakwama”Alisema Seleboss.
Aidha alisema watendaji  wamechangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato ambapo yamefikia asilimia 65% huku ikiwa bado mwezi mmoja kumalizika kwa mwaka wa serikali uishe ilihali angalau ukusanyaji huo ulitakiwa ufikie 80%.
Alisema kuwa ukosefu huo wa mapato umesababisha Halimashauri hiyo kushindwa kutekeleza shughuli za kijamii kama usafi wa masoko pamoja na marekebisho ya taa za barabarani.
“Watendaji wameshindwa kutafsiri nia ya Rais kwani vitambulisho vimetolewa hadi kwa wavuvi pamoja na wafanyabiashara wakubwa wenye maduka sasa wote wamegeuka na kuwa wajasiriamali”alisema Mustafa.
Hata hivyo akiongelea upande wa leseni za biashara Meya Mustafa alisema kuwa wamepoteza mapato ya kiasi cha sh Mil 700 zilizokuwa zikusanywe kutokana na maombi ya leseni hizo lakini sasa wafanyabiashara wengi wamerudisha leseni hizo na kukata vitambulisho vya wajasiriamali.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Ramadhani Possi alisema kuwa ufinyu wa bajeti umesababisha miradi mingi ambayo walikuwa wamepanga kuitekeleza kushindwa kutekelezwa kwa wakati .
“Kwa sasa tunajipanga kuboresha miundombinu ya shule zetu kwa kujenga madarasa mapya ukarabati ya vyoo pamoja na madawati ambapo tunafanya kila pale tunapopata fedha japo kidogo”alisema Possi.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Tanga Selemani Zumo aliwataka watendaji wa Jiji kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na kujituma pamoja na kujua mipaka ya kazi zao.
Alisema kuwa haiwezekani watendaji hao wakawa ni sehemu ya migogoro baina yao na viongozi wa kisiasa ambao wao wapo kwa ajili ya kuhakikisha wanasimami maslahi ya wananchi ambao ni wapiga kura wao.
Awali akichangia mada katika baraza hilo Diwani wa kata ya Mabawa Mwasabu Ngare alisema baadhi ya taa za barabarani haziwaki na hali hiyo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la vibaka na wananchi kupoteza mali zao.
Mwisho.

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI UTALII NA MAMBO YA KALE IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni, wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyokwa mwezi Julai 2018 hadi March2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, kushoto Mhe,. Mahmoud Thabit Kombo akisoma Utelelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March2019, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar na kushoto Naibu Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Chuom Kombo Khamis.
KATIBU Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee akizungumza wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayuko pichani, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
 MAOFISA wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, wakifuatilia mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara yao kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019.uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmaoud Thabit Kombo, akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.

 WAKUU wa Idara mbalimbali za Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar wakifuatilia mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 MKURUGENZI Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Aiman Osmond Duwe, akichangia wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bi. Khadija Bakari, akisoma na Ripoti ya Matumizi na Mapato ya Idara mbalimbali za Wizara hiyo wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi, uliofanyika Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 MHARIRI Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar, Zanzibar Leo, Ndh. Yussuf Khamis, akichangia wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar. (Picha na Ikulu)

MWONEKANO WA BARABARA YA JANGWANI BAADA MVUA KUKATA

WAZIRI MKUU AFUTURISHA WAHESHIMIWA WABUNGE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai wakiwaongoza Waheshimiwa Wabunge kupata futari aliyowaandalia katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi, Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Joseph Selasini wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakwanza kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenknlojia Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Nchi (Ofisi ya Waziri Mkuu)-Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Raslimaliwatu wa Ofisi ya Bunge Bi. Jane Kajiru (wakwanza kushoto) wakipata futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. PICHA NA BUNGE

Airtel yaendeleza usajili jijini Dodoma

$
0
0

Watumishi mbalimbali kutoka Wizara na taasisi zake zilizopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambao ni wateja wa Airtel wakisajili laini zao kwa alama za vidole jana. Airtel inaendelea na usajili huo pia katika maduka yake zaidi ya 650 nchini. (Picha na Airtel).


Watumishi mbalimbali kutoka Wizara na taasisi zake zilizopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambao ni wateja wa Airtel wakisajili laini zao kwa alama za vidole jana. Airtel inaendelea na usajili huo pia katika maduka yake zaidi ya 650 nchini. (Picha na Airtel).

NYOSHI AMVULIA KOFIA DIAMOND,ATAMANI KUFANYA NAE 'KOLLABO'

$
0
0
Na.Khadija seif,Globu ya jamii

RAIS wa muziki wa dance nchini Nyoshi El Sadat anatamani kufanya kazi na msanii wa bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond.

Nyoshi amempongeza Diamond baada ya kuachia ngoma yake mpya "inama" aliomshirikisha msanii kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Fally Ipupa na kupokelewa vizuri na mashabiki wa Kongo.

"Diamond ni mwanamuziki mkubwa kama mimi na ana uwezo mkubwa wa kufanya kazi na msanii yoyote yule nitamtafuta ili tufanye kazi pamoja,"

Nyoshi ameweka wazi hayo alipokuwa akizungumza na Globu ya Jamii,ameongeza kusema kuwa wanamuziki wote ni vizuri kushirikiana katika kazi bila kujali upande mmoja hasa likitokea swala la matamasha na kushirikishana kwenye wimbo.

"Likija swala la matamasha wanamuziki wa bongofleva wanaonekana peke yao ,sio vibaya wanamuziki wa dance wakashirikishwa ili kusiwepo tafsiri ya ubaguzi wa aina yoyote ile,"
 
Akifafanua zaidi katika lafudhi yake ile ile ya Kikongo,licha ya kuishi nchini kwa miaka mingi,Nyoshi amegusia swala la mavazi Kwa msanii ni moja ya kivutio Kwa mashabiki hata kama inatokea msanii haeleweki anachokiimba lakini muonekano wake unachukua nafasi mkubwa Kwa kile anachokifanya.

"Jux,daimond ,Irene uwoya, jackline wolper wanavaa vizuri nawapenda ", alisema nyoshi

Hata hivyo Nyoshi amesema muziki wa live bado upo na mashabiki wake bado wapo, Ila kwa sasa ndio unarudi kutokana na kipindi cha mwanzo kutengewa muda wa kufunga kumbi za starehe zinazopiga miziki, hasa ikifika saa 6 usiku na kupelekea kukosa mashabiki wengi.

"Mkuu wa mkoa amesikia kilio chetu kwani muziki ni ajira na tunatafuta riziki kupitia muziki,hivyo ameruhusu muziki kwenye kumbi za starehe mpaka saa 8 usiku,tunamshukuru sana kwa kuliona hilo"

Sanjari na hilo amewaomba mashabiki zake wampokee mtoto wake wa kike "brand" ambae anatarajia kuingia rasmi kwenye soko la muziki wa bongofleva .

PROFESA MCHOME AKUTANA NA WATOA MSAADA WA KISHERIA JIJINI ARUSHA

$
0
0
KATIBU Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amekutana na watoa huduma ya msaada wa kisheria jijini Arusha na kuwataka kuleta matokeo kupitia huduma ya msaada wa kisheria.

Prof Mchome alikutana na watoa huduma ya msaada wa kisheria jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa shughuli za msaada wa kisheria zinazotolewa kwa wananchi  ili  kuboresha huduma hizo kwa wananchi.

“Msaada wa kisheria unalenga kumsaidia mwananchi ilia pate matokeo fulani, nakama mkishindwa kupata matokeo mtakuwa hamjatimiza lengo la kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria,” amesema Prof. Mchome.

Amesema Sheria ya Msaada wa Kisheria No.1 ya 2017 imelenga kupata matokeo kama ya kusaidia mwananchi-1 kupata haki yake na kama  kumaliza kesi bila ya kuzipeleka Mahakamani basi hayo ni matokeo chanya kwani inawezesha Serikali na mwananchi husika kuokoa fedha ambazo zingetumika kufungua na kuendesha kesi kutumika kwa shughuli nyingine za maendeleo.

Prof. Mchome pia amewataka watoa huduma hao kupitia wasaidizi wa sheria kuhakikisha huduma ya msaada wa kisheria inatolewa kwa wananchi wenye uhitaji ambao wanakidhi vigezo ambavyo vipo kwa mujibu wa sheria.

Amesema sheria ni chombo cha maendeleo na zinakuwepo ili kutengeneza njia sahihi ili wananchi kupita na hivyo kupata haki zao na maendeleo kwa ujumla.

“Sheria zipo ili kuleta aina fulani ya utaratibu na maendeleo ya nchi, sio wote wanayajua hayo, sheria inafanya kazi hiyo inakuelekeza kwa kuanzia na msaada wa kisheria ni pamoja na kufanya kazi ya kuelekeza njia ya kufuata kupata haki na kutatua kero ya wananchi,” alisema.

Wizara ya Katiba na Sheria iko katika ziara ya kuwatembelea watoa huduma za msaada wa kisheria nchini kwa ajili ya kukagua wanavyotoa huduma zao na  kujua changamaoto zinazowakabili ili kuboresha huduma za msaada wa kisheria nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na watoa huduma ya msaada wa sheria kwa wananchi jijini Arusha

WAKALA WA VIPIMO (WMA) WAENDELEA KUHAKIKI VIPIMO KUELEKEA MAADHIMISHO YA VIPIMO DUNIANI

$
0
0
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akifanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi, Maadhimisho ya vipimo duniani yanatarajiwa kufanyika Mei 20, 2019 jijini Dar es salaam.

  
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akishuhudia wakati mafuta yakijazwa kwenye kipimo maalum cha mafuta wakati maofisa hao walipofanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu  kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo, kushoto ni Ally Mohamed Meneja wa kituo cha Total Mlimani City.

  
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akitoa maelezo kwa waandishi wa habari  wakati wakifanya  ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi anayejaza mafuta ni Mbaningo Mselem Afisa Vipimo.
  

Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akionyesha Stika ya uthibitisho kuwa pampu hizo zimekaguliwa wakati maofisa hao waliofanya ukaguzi kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.

  
 Ally Mohamed Meneja wa kituo cha mafuta Total Mlimani City akihojiwa na  waandishi wa habari kwenye kituo hicho jijini Dar es salaam leo baada ya wakala wa vipimo kukagua pampu na kujiridhisha kuhusu ubora wake wa vipimo.


  

 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akihojiwa na waandishi wa habari wa ITV mara baada ya  maofisa hao kufanya ukaguzi katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.kushoto ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)
  
Kituo cha Mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam.
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akifanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi, Maadhimisho ya vipimo duniani yanatarajiwa kufanyika Mei 20, 2019 jijini Dar es salaam.

  
 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akishuhudia wakati mafuta yakijazwa kwenye kipimo maalum cha mafuta wakati maofisa hao walipofanya ukaguzi wa Seal kwenye pampu  kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo, kushoto ni Ally Mohamed Meneja wa kituo cha Total Mlimani City.

  
Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akitoa maelezo kwa waandishi wa habari  wakati wakifanya  ukaguzi wa Seal kwenye pampu katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo ili kujiridhisha kama upimaji mafuta wa Pampu ni sahihi wakati wateja wanapofanya manunuzi anayejaza mafuta ni Mbaningo Mselem Afisa Vipimo.
  

Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akionyesha Stika ya uthibitisho kuwa pampu hizo zimekaguliwa wakati maofisa hao waliofanya ukaguzi kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.

  
 Ally Mohamed Meneja wa kituo cha mafuta Total Mlimani City akihojiwa na  waandishi wa habari kwenye kituo hicho jijini Dar es salaam leo baada ya wakala wa vipimo kukagua pampu na kujiridhisha kuhusu ubora wake wa vipimo.


  

 Kaimu Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Kinondoni Bw. Charles Mavunde akihojiwa na waandishi wa habari wa ITV mara baada ya  maofisa hao kufanya ukaguzi katika kituo cha mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam leo.kushoto ni Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Wakala wa Vipimo (WMA)
  
Kituo cha Mafuta cha Total Mlimani City jijini Dar es salaam.

AIRTEL YAFANYA USAJILI KWA ALAMA YA VIDOLE ENEO LA MTUMBA MJI WA SERIKALI

$
0
0
Airtel yaendeleza usajili kwa Watumishi mbalimbali kutoka Wizara na taasisi zake zilizopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma ambao ni wateja wa Airtel wakisajili laini zao kwa alama za vidole jana. Airtel inaendelea na usajili huo pia katika maduka yake zaidi ya 650 nchini. (Picha na Airtel).
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images