Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

JESHI LA POLISI MOROGORO LAWASHIKILIA WATUHUMIWA 8 KWA KUCHOMA NYUMBA YA MFUGAJI

$
0
0
Na Hussein Stambuli, Morogoro.

Jeshi la polisi mkoani morogoro limewakamata na kuwashikilia watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji kwa sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese katika kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa waliokamatwa kwa kitendo hicho cha kuchoma nyumba.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Wilbroad  Mutafungwa amesema chanzo cha mgogoro huo ni kutokana na wananchi siku ya jana tarehe 13,5,2019 kuvamia nyumba ya mfugaji aliyefahamika kwa jina la mbega sultani boy kwa kudaiwa kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima kwa muda mrefu.
Ambapo wanakijiji hao wakaivamia nyumba yake na kuchoma moto jumla ya nyumba tano baada ya kumkosa mfugaji huyo anayedaiwa kwa muda huo kuwepo mahakamani kukabiliana na kesi nyingine zinazo mkabili za kulisha mifugo mazao ya wakulima na kusababisha nyumba hizo kuteketea vibaya huku wake wa 2 na watoto 19 akiwemo mtoto mmoja mlemavu wakinusurika kifo.

“kufuatia tukio hilo tumefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wane kwa kosa la kufanya fujo na kufunga barabara ambao ni ernest mkandula (25), machemba samiki (40), juma shabani (40) shaban ally (45) wakazi wa kijiji cha maseyu na misako mikali inaendelea katika kijiji hicho na tumefanikiwa kuyaondosha magogo yaliyokuwa yamewekwa barabara na safari zinaendelea. Amesema mutafungwa

Kamanda wa polisi akatoa wito kwa wananchi kutii sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani husababisha kukosa haki zao za msingi kwa kujiingiza kwenye makosa mengine..
 Kamanda  wa polisi mkoani morogoro wilbroad Mutafungwa na watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese
 magari yakiwa yamesimama kutokana na kufungwa barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese.
 watuhumiwa 8 walio jihusisha na tukio la kuchoma nyumba ya mfugaji sambamba na kufunga barabara kuu ya dar-es salamu –morogoro maeneo ya maseyu mikese
wilbroad mutafungwa kamada wa polisi mkoa wa morogoro, akizungumza na waandishi wa habari mkoani morogoro

MPINA ATOBOA SIRI YA ONGEZO LA GHAFLA LA VIWANDA VYA NYAMA

$
0
0
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina  (mwenye kizibao chekundu) akitoa maelekezo kwa  mmiliki wa kiwanda cha nyama cha Eliya Foods Overseas LTD kilichopo Longido  ndugu Shabbir Virjee(mwenye shati jeupe), kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (Mwenye nguo nyeusi) akishuka kwenye gari maalum ya kubebea maziwa baada ya kulikagua gari hilo la kiwanda cha maziwa cha Kilimanjaro Fresh alipotembelea kiwanda hicho kuangalia utendaji wake hivi karibuni.

Na John Mapepele

Serikali imewahakikishia wawekezaji wa viwanda vya mazao ya mifugo nchini kuwa hakuna atakayechezea masoko yao kwa kuingiiza bidhaa hizo sokoni kwa njia isiyo halali na badala yake serikali imetaka jitihada zinazofanywa na wawekezaji lazima zilenge kuwainua wafugaji kote nchini na kutoa majawabu ya changamoto zinazowakabili wafugaji ikiwa ni pamoja na ajira, masoko na nyama bora ili uwekezaji huo uwe wenye tija na endelevu.

Hayo amesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina alipofanya ziara ya kikazi mkoani Arusha leo kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya mifugo ambapo amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu  kuhakikisha  kuwa  hakuna mtu atakayekwepa kufuata taratibu za  biashara ya mazao ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi ili kuwa na ushindani wa halali.

Amesema  kutokana na udhibiti uliofanywa na serikali wa kuzuia ukwepaji wa kodi, uingizaji wa mazao ya mifugo na kwa udanganyifu na utoroshaji mkubwa mifugo kwenda nje ya nchi kwa njia za panya umesaidia kuwavutia wawekezaji wengi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vikubwa vya nyama na maziwa  kwa wingi kuliko kipindi chochote kuanzia nchi yetu ilivyopata uhuru hadi sasa.

“Mheshimiwa Waziri, tumekuwa tukitorosha  mifugo kwenda kuuza nchi za jirani kwa kuwa hapa kwetu  palikuwa hakuna soko la uhakika la kuuzia lakini sasa tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutusaidia kupata kiwanda hiki hapa Longido ambacho kitakuwa mkombozi wa soko la uhakika la mifugo yetu” alisisitiza  Mzee maarufu wa kimasai, Olesiyanda Sidala wakati Waziri Mpina alipomaliza kukagua kiwanda cha kusindika  nyama cha Eliya Foods Overseas LTD kilichopo eneo la Longido mkoani Arusha.

Mkurugezi Mtendaji wa Kiwanda hicho Shabbir Virjee alisema Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuchinja ng’ombe 500 hadi 1000 na  mbuzi na kondoo 2000 hadi 5000 kwa siku na kinatarajia kutoa zaidi ya ajira 300,ambapo pia aliiomba serikali eneo la ekari  100 kwa ajili ya kupumzishia mifugo kabla ya kuchinjwa na kuahidi kuwa ifikapo Oktoba mwaka huu kiwanda kitakuwa kimekamilika na kuanza kufanya kazi.

Aidha Waziri Mpina aliongeza kwamba hivi sasa wananchi na wawekezaji wengi wanajitokeza kuwekeza kwenye sekta ya mifugo baada ya muda mrefu kukimbia uwekezaji kwa sababu walikuwa wanafika mahala  wanachinja na kukosa masoko ya kuuza nyama hizo.

Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwalinda wawekezaji wote kwa sheria na kwamba  Wizara itaendelea na operesheni muda wote kila mahali kuanzia  bandarini,mipakani, viwandani, kwenye  maduka na katika  vya ndege  kukagua na kuona kama kuna mtu ameingiza  bidhaa kwa kufuata sheria na ubora wake.

Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi hivyo inaweza kutoa malighafi ya kutosha kwa viwanda  vya mifugo vinavyoanzishwa na kwamba asilimia 1.4 ya mifugo yote duniani ipo Tanzania na asilimia 11 kwa Afrika, ambapo ina jumla ya Ngombe milioni 30.5, Mbuzi milioni 18.8 na Kondoo milioni 5.3.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe  amepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya mifugo ambapo amesema  Wizara  imeonyesha kuwa siyo ya kupokea misaada kama ilivyokuwa inatazamwa awali bali inayoweza hata kusaidia wizara nyingine zisizozalisha na kuifanya nchi yetu isonge mbele.

“Mheshimiwa Waziri naomba kusema wazi kuwa umekuwa bega kwa bega kudhibiti utoroshaji na ukwepaji wa kodi na umeonyesha uwezo mkubwa wa kuitendea haki sera ya viwanda kwa kuweka mazingira mazuri ya kuvutia viwanda vingi kujengwa  naamini wizara nyingine zige mfano kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi “ aliongeza Mwaisumbi.

Mpina aliongeza kuwa Serikali inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuboresha kosaafu za mifugo ili kupata mifugo bora itakayoweza kushindana na mifugo mingine katika masoko ya kimataifa ambapo alisema  tayari madume bora ya ngombe yanayozalisha  mbegu bora yameletwa na serikali kwenye Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa  Usariver jijini Arusha ambayo yanauwezo wa kutosha kwa nchi nzima.

Katika kuhamasisha wafugaji wanawapeleka watoto wao kwenye mafunzo maalum ya ufugaji, Waziri Mpina alitoa nafasi kwa mtoto mmoja wa mfugaji anayeongoza kwa mifugo mingi kuweza kusomeshwa  bure na serikali kwenye Wakala wa Mafunzo ya Mifugo Tengeru na Kituo cha Uhimilishaji cha Taifa  Usariver jijini Arusha.

Katika ziara hiyo Waziri Mpina alitembelea  bwawa lililobomoka la Kimokowa  na kuelekeza kuwa Wizara na Halmashauri ya Longido  kukarabati bwawa hilo mara moja pia alimwelekeza katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo kukarabati majosho 8 kati ya 16 ya Wilaya ya Londigo kabla ya Julai mwaka huu, ambapo pia alisema tayari Wizara imeshatoa kiasi cha Shilingi milioni 150 kwa ajili ya kukarabati soko la kimataifa la mnada wa mpaka wa Longido.

Kaimu Msajiri wa Bodi ya Nyama nchini Imani Sichalwe alimhakikishia Waziri Mpina kuwa Bodi ya nyama itaendelea kushirikiana na wawekezaji katika kuwatafutia masoko ya bidhaa zao ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine  Waziri Mpina alitembelea kiwanda cha maziwa  cha Kilimanjaro Fresh chenye uwezo wa kuzalisha  lita 5000 hadi 50000 kwa siku ambapo kwa sasa kimeanza kuzalisha lita 5000 baada ya kuanza rasmi uzalishaji Februari 2, mwaka  huu,ambapo aliwahakikishi kuwapa ushirikiano na aliwataka  wamiliki kuangalia bei wanaonunua maziwa kwa wafugaji zisiwe kandamizi.

Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Irfhan Virjee amesema kuwa kiwanda hicho kimekuwa kikiuza jumla ya lita 4000 kwa siku na kwamba kiwanda kinatarajia kuongeza uzalishaji wa mazao mengine ya maziwa ikiwa ni pamoja na jibini na siagi ndani ya miezi miwili ijayo, ambapo kwa sasa kinaendelea kutoa maziwa yenye radha tofauti za matunda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Mifugo, Daktari  Asimwe Lovince alimshukuru Waziri Mpina na kumhakikishia kuwa amepokea maelekezo yote na kwamba atayafanyia kazi kikamilifu katika kipindi kifupi ili sekta ya mifugo iweze kukua kwa kasi  na kuleta mapinduzi yanayohitajika kwa sasa. 

Aidha alisema kufanya kazi kwa viwanda vya nyama na maziwa nchini kutasaidia kuliingizia taifa fedha za kigeni ambapo kwa upande wa viwanda vya nyama  vitasaidia kutoa mazao mengi zaidi kwenye damu(vyakula vya mifugo),pembe na ngozi.

Katika kipindi cha  miaka miwili sasa wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa  na mikakati mbalimbali ya kuleta  mageuzi ya sekta kuanzia mapato, kutafuta ufumbuzi wa migogoro baina ya wafugaji wa watumiaji wengine wa ardhi, kudhibiti magonjwa, kuboresha kosaafu za mifugo kwa njia mbalimbali.

BALOZI AMINA SALUM ALI AFANYA MAZUNUMZO NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA HARBAD

$
0
0
Na Ali Issa Maelezo -Zanzibar 

Ujumbe wa wanafunzi sita kutka Chuo Kikuu cha Harvad umefanya mazungumzo na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali Ofisini kwake Migombani.

Ujumbe huo upo Zanzibar kuangalia ubora wa chumvi inayozalishwa hapa nchini ukilinganisha na mataifa mengine ili hatimae iweze kutambulika na kuingia katika soko la kimataifa.

Akizungumza na Ujumbe huo Balozi Amina Salum Ali amesema Chumvi inayozalishwa Zanzibar ina ubora wa hali ya juu kutokana na mfumo unaotumika wakati wa uzalishaji na inaweza kutumika katika nchi yoyote duniani.

Amsema kufika kwa ujumbe huo ni mafanikio kwa mradi wa chumvi ya Zanzibar na ameeleza matarajio yake kuwa utasaidia kuhakikisha chumvi ya Zanzibar inaingia katika soko la kimataifa.

Aliutaka ujumbe huo kufanya uchunguzi wa kina kujua ubora wa chumvi ya Zanzibar na kuona tofauti iliyopo na chumvi inayozalishwa n nchi nyengine duniani.

Mbali na kuangalia ubora wa chumvi inayozalishwa Zanzibar, pia ujumbe huo utakagua kilimo cha pilipili na kilimo cha mwani ambacho kimekuwa maarufu sana katika maeneo mbali mbali ya pwani ya Zanzibar.

Wanafunzi hao kutoka Marekani wametawanywa katika mataifa mbali mbali na kwa hapa Tanzania wamekuja kumi ambapo wanne wamebakia Tanzania Bara.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Ujumbe wa wanafunzi sita kutoka Chuo Kikuu cha Harvad cha Marekani Ofisini kwake Migombani, wanafunzi hao wapo nchini kuangali ubora wa Chumvi inayotengenezwa Zanzibar.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali na ujumbe wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Harvad wakiangalia Paketi za Chumvi iliyotengenezwa Zanzibar Ofisini kwake Migombani.Picha Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar

WhatsApp: Fahamu namna ya kuwa salamu unapotumia mitandao ya kijamii

$
0
0

Taarifa kwamba "WhatsApp inaweza kudukuliwa" sio jambo ambalo mtumiaji yoyote wa mtandao huo wa kijamii anataka kusikia wala kuona katika kichwa cha habari.

Alafu kuongezea kwamba "Wadukuzi walifanikiwa kuweka mfumo wa uangalizi" na kitengo cha habari cha kampuni hiyo wana kibarua kikubwa mikononi mwao.

WhatsApp linasema akaunti kadhaa zililengwa na " mdukuzi mkuu wa mitandao".

Lakini iwapo kauli hii imekutia wasiwasi, haya ni baadhi ya mambo unayostahili kufanya kuhakikisha mawasiliano yako yapo salama.
Udukuzi huo uligunduliwa kwanza mapema mwezi huu.

Wakati huo Facebook, inayomiliki mtandao wa WhatsApp, iliwaambia maafisa wa usalama kwamba lilikuwa : "pengo katika mawasiliano ya sauti ya WhatsApp VOIP [voice over internet protocol] iliyoruhusu udukuzi kupitia vifurushi vya mfumo wa SRTCP [secure real-time transport protocol] vilivyotumwa kwa nambari ya simu ya mlengwa."
Sawa. 

Hebu tulifasiri hilo - ina maana wadukuzi walitumia simu ya WhatsApp kupiga kwa nambari ya mlengwa. 

Hata kama simu haikushikwa, mfumo huo wa udukuzi uliidhinishwa kutokana na pengo hilo katika mawasiliano ya sauti ambao hauna usalama wa kutosha. 

Simu pengine ilikatika na haionekani kwenye orodha ya waliopiga simu katika simu yenyewe, kwasababu wadukuzi walikuwa tayari wameidhibiti.

KUSOMA ZAIDI BOFYA  BBCswahili.com

Taarifa kwa umma kuhusu Nafasi za Kazi na Masomo

$
0
0


Dodoma, 14 Mei 2019

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi na masomo zilizotangazwa na jumuiya za kimataifa kama ifuatavyo:

  1.     i.        Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola;

Afisa Msaidizi wa Programu katika Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (Assistant Program Officer-Monitoring and Evaluation Unit na

Meneja wa Utafiti–Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Research Manager–Economic, Youth and Sustainable Development.
Maelezo kamili kuhusu nafasi hizi yanapatikana katika tovuti: http://thecommonwealth.org/jobs.  Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 23 Mei 2019.

Aidha, Jumuiya ya Madola imetangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree). Mwisho wa kuwasilisha maombi ya nafasi hizo zinazojulikana kama Queen Elizabeth Commonwealth Scholarship ni tarehe 26 Juni 2019.

Maelezo kuhusu taratibu za kuomba nafasi hizo yanapatikana kupitia tovuti: www.acu.ac.uk/scholarships/qecs.  

  1.   ii Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR);

Kamishina Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Hifadhi kwa Wakimbizi (Assistant High Commissioner for Protection).

Maelezo kuhusu nafasi hii yanapatikana kupitia tovuti: https://www.unhcr.org/career-opportunitiesambapo mwisho wa kuwasilisha mombi ni tarehe 20 Mei 2019 katika baruapepe recruitment.AHC-P@unhcr.org

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Watumishi NAOT Waaswa Kuzingatia Maadili

$
0
0
Watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Wameaswa Kuziungatia Maadili wakati wote Wanapotekeleza majukumu yao ili kuendana na dhamira ya Serikali kufikia maendeleo endelevu na uchumi wa kati.

Akizungumza wakati akizindua Baraza jipya la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis Michael amesema watumishi wote wa Ofisi hiyo wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia sharia kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuleta tija katika majukumu wanayotekeleza.

“ Sitarajii Wakaguzi wetu Wakawa miongoni mwa watumishi watakaokumbwa na kashfa za namna yoyote hivyo niwaase kujiepusha na vitendo vya utovu wa nidhamu,kudai na kupokea rushwa” Alisisitiza Dkt. Michael

Akifafanua amesema kuwa hatma ya makosa hayo ni kupoteza ajira na kufikishwa katika vyombo vya sheria ikiwemo mahakama ili sharia iweze kuchukua mkondo wake hali inayoweza kupelekea mhusika kufungwa jela.
Aidha, aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kutumia fursa za Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali kujiletea maendeleo kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ardhi.

Kwa upande wake Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Serikali Prof. Mussa Assad amesema kuwa Ofisi hiyo imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa weledi ili kutimiza lengo la kuanzishwa kwake ikiwemo kuhakikisha kuwa ripoti ya ukaguzi inatolewa kama inavyotakiwa kila ifikapo mwezi machi.
Aliongeza kuwa watumishi wa Ofisi hiyo wameendelea kujituma na kufanya kazi kwa bidii nyakati zote hali inayoonesha jinsi wanavyojitoa katika kuhakikisha kuwa kazi za ofisi hiyo zinafanyika kama inavyotakiwa.

Baraza la wafanyakazi wa NAOT linafanyika Jijini Dodoma kwa siku mbili likiwa na dhamira ya kuwaleta pamoja wajumbe kutoka katika Idara, Vitengo, Kada, baadhi ya Taasisi na vyama vya wafanyakazi likiwa ni Baraza la mwaka 2018/2019.
 Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael akisisitiza umuhimu  wa watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi  (NAOT) kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao , ameyasema hayo wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisisitiza umuhimu wa Baraza la Wafanyakazi  wakati wa hafla ya kufungua  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael  akikata utepe kuzindua  mkataba wa huduma kwa wateja wakati wa hafla ya kufungua baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akiteta jambo na Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael wakati wa hafla ya kufungua  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma. 
 Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi  (NAOT) mara baada ya kufungua  baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.

 Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi  wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi  (NAOT) wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa baraza hilo leo Jijini Dodoma.
 Naibu mkaguzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) Bi Wendi   Masoy akitoa neno  la shukrani mara baada ya uzinduzi wa  Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo Jijini Dodoma.
Naibu Katibu mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dkt. Francis  Michael akisisitiza jambo kwa  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad leo Jijini Dodoma baada ya kuzindua Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO)

Bilioni 20 Zakusanywa Ada ya Vitambulisho vya Wajasiriamali

$
0
0
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
TAKRIBANI Sh bilioni 20.3 zimefikishwa kwenye mfumo wa malipo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kugawa vitambulisho vya wajasiliamali vipatavyo 1,022,178.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na wakuu wa mikoa kabla ya kupitia tathimini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa wajasiriamali.

Jafo alisema kuwa kwa wakuu wa mikoa kugawa vitambulisho hiyo 1,022,178, wajasiriamali wameweza kuchangia Sh bilioni 20.44 ambapo Sh bilioni 20.3 ndizo zilizoingizwa kwenye mfumo wa TRA na takribani Sh milioni 135.6 bado ziko mikononi wa wakusanyaji.

“ Mpaka kufikia Aprili 30 mwaka huu kiasi cha Sh milioni 942.47 zilikuwa bado haijaingia kwenye mfumo wa mapato wa TRA, lakini nashukuru ndani ya siku mbili hizi tatu wakuu wa mikoa wameweza kuzifikisha kwenye mfumo fedha nyingi zaidi, niwapongeze kwa hilo.’
Jafo alisema endapo fedha zinazokusanywa kutokana na vitambulisho vya wajasiriamali hazitaingia kwenye mfumo wa mapato wa TRA basi fedha hizo zinakuwa mbichi na kuna hatari ya kuwapo upotevu au kutumika katika matumizi yasiyopangwa.

“ Nitumie fursa hii kuwahimiza wakuu wa mikoa na watendaji ambayo wamekusanya fedha za vitambulisho vya wajasiriamali na kutoziingiza kwenye mfumo wa malipo wa TRA kufanya hivyo mara moja,” alisema
 Aidha, Jafo aliwataka wakuu wa mikoa katika kuhakikisha azima ya Rais John Magufuli ya kutaka wafanyabiashara wadogo watambuliwe na kuwaondolewa usumbufu wanapofanya biashara zao na kushiriki katika uchumi wa nchi kwa kuwaelimisha faida ya kuwa na vitambulisho hiyo.

“ Rais John Magufuli kiu yake ni kuwalinda wafanyabiashara wadogo na kuwaona kuwa na sehemu ya kukuza uchumi wa nchi, alitaka wafanyabiashara wadogo waondokane na adhana zilizokuwa zikiwapata kupitia askari wa majiji ambao walikuwa wakitaifisha bidhaa zao na wakati mwingine kugawana jambo ambalo haikuwa ni haki,”

Kwa awamu ya kwanza na ya pili, vitambulishi vipatavyo 1,850,000 ambavyo vilikuwa na thamani ya Sh bilioni 37 vilitolewa na mpaka Aprili 30 mwaka huu, vitambulisho 1,022,178 vyenye thamani ya Sh bilioni 20.44 vimetolewa kwa wafanyabiashara wadogo.
Aidha, Jafo aliipongeza mikoa ambayo imefanya vizuri katika ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali na ambayo ni Dar es Salaam iliyogawa vitambulisho kwa asilimia 95.2. Tabora kwa asilimia 94.58, Kilimanjaro kwa asilimia 79.05, Pwani kwa asilimia 77.66 na Tanga kwa asilimia 72.

Mikoa ambayo imefanya viabaya na asilimia zake kwenye mabano ni Katavi(asilimia 5.96), Njombe (asilimia 11.14), Rukwa (asilimia 25.03), Iringa(asilimia 30.74) na Lindi (asilimia 33.58).
“ Tunajua changamoto ya baadhi ya mikoa na ndio maana tuko hapa tufanye tathimini ya ugawaji wa vitambulisho hivyo, lengo letu ni kuwa lengo la Rais la kuwalinda wale wasio na sauti lifikiwe kwa wajasiriamali wadogo kutambuliwa,” alisema.

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwandri alisema utaratibu wa kutoa vitambulisho hivyo ulikuwa mgumu hasa kutokana na wananchi kuwa na dhana ya kuwa Serikali inatumia vitambulisho hivyo kuwalipisha kodi.
 “ Ukweli ulikuwa ni kuwa kiasi cha Sh 20,000 ni cha kugharamia uchapishaji wa vitambulisho, lakini wengi waliona kuwa ni njia ya kuwalipisha kodi.

Mwandri aliongeza: “ Tuliweza kufanikiwa kwa kiasi hicho kwa kuwashirikisha viongozi wa kimila, dini na watendaji kuanzia ngazi ya kitongoji, na tukaitisha mikutano ya adhara ya kutoa elimu, na baada ya hapo mwitiko wa wananchi ukawa mkubwa.”
 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Mb) akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Mikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali kilichofanyika St. Gasper Jijini Dodoma.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Kichele akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Mikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali kilichofanyika St. Gasper Jijini Dodoma.
 Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara wakifuatilia kikao kazi kilichoitishwa na OR-TAMISEMI ambacho kimehusisha Mamlaka ya mapato Tanzania kufanya tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakifuatilia majadiliano wakati wa   kikao kazi cha Wakuu wa Mikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhusu tathmini ya ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali kilichofanyika St. Gasper Jijini Dodoma.

EAC – GERMAN BUSINESS AND INVESTMENT EXPERT DIALOGUE HELD IN ARUSHA

$
0
0
The East African Community-German Business and Investment Expert Dialogue co-organized by the East African Business Council (EABC) and the German-African Business Association was held today at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

The overall objective of the one-day Dialogue was to create business synergies in various sectors while showcasing the EAC as an ideal business destination for trade and investment.
 EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo makes his remarks

Addressing the forum on behalf of the EAC Secretary General, Amb. Liberat Mfumukeko, the Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo, said the draft EAC Investment Policy which is currently under consideration by the Council of Ministers, envisages a transformed upper middle-income EAC that is a competitive common investment area with a more liberal, predictable and transparent investment environment.
 Mr. Christoph Kannengiesser, the Chief Executive Officer of the German-African Business Association addressing the particpants during the dialogue

Hon. Bazivamo told the participants that the investment policy lays ground for Partner States to cooperate in investment promotion, facilitation, liberalization and protection of cross border investment.

"Partner States are to streamline and simplify administrative procedures related to investments, promote and maintain dialogue with the private sector and exchange business information," he added.
 Mr. Lamech Wesonga from EABC engages with the participants ( not in the picture) during the dialogue

He disclosed that at the regional level, through the Consultative Dialogue Framework, EAC has developed an open channel where the private sector, civil society and other interest groups interface with the Secretary General. He reaffirmed the Secretariat's role in advocating for a better and conducive climate investment in the region.

“I take this opportunity to thank our partners Afrika Verein and EABC for continued good working relationship and request for further collaboration in supporting the private sector to achieve the business goals and promote the region as an ideal place to invest and do business," said Hon. Bazivamo.
  Section of participants during the dialogue

On his part, the Executive Director  of the East African Business Council, Hon. Peter Mathuki said it is with no doubt that if all Non-Tariff Barriers (NTBs) hindering trade within the  EAC Common Market  are removed, the domestic demand and market of over 150 million people from the six EAC partner states will attract  investments from Germany and all over the world as it will be more economically viable for all Investors to invest in the EAC.

In his remarks read by EABC Manager Policy and Standards, Mr. Lamech Wesonga, Mathuki said EABC  will continue to ensure that the agenda of the Private Sector is well articulated and received by the policymakers in order to promote a business environment conducive to business formation, growth, expansion.

The Chief Executive Officer of the German-African Business Association, Mr. Christoph Kannengiesser, said the dialogue provides an opportunity for networking and supports information exchange as well as better mutual understanding.

He urged the EAC to prioritize collaborative approaches that will see supply chains strengthened across borders and Governments laying the groundwork for the ease of movement of goods and people in the region. The Dialogue brought together Policy-makers, experts, private sector representatives from East Africa and Germany.

Balozi Seif afuturu na wazee wanaoishi nyumba za serikali Zanzibar

$
0
0
Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini wanaendelea na harakati zao za kufutari pamoja zinakopelekea kushibana kiimani ya moyo ndani ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao umeteremshwa Kitabu Kitakatifu cha Quran kisichoshaka katika kubainisha Haki na Batil.

Futari hizo zinazojumuisha Waumini wa rika tofauti ufanywaji wake hupaswa kuzingatia utaratibu maalum wa hali ya Kiafya na Mazingira safi uliowekwa na Uongozi wa Manispaa pamoja na Halmashauri za Wilaya.

Futari hiyo iliyoandaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi iliwahusisha Wazee wanaohifadhiwa kwenye Nyumba za Serikai Sebleni pamoja na Wazee wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na kufanyika katika Ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni Mjini Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed alisema Balozi Seif bado anaendeleza tabia njema ya kuwashirikisha Wananchi mbali mbali katika Futari ya pamoja.

Waziri Aboud alisema kitendo cha kufutarisha ni maamrisho ya Mwenyezi Muungu aliyoawaagiza Waumini wake wenye uwezo kuwasaidia Waumini wenzao wenye maisha duni ili kuwaunganisha katika futari hiyo ambayo ni matendo anayoyafurahia Allah Subuhanahu wataala.

Mjumuiko wa kufutari kwa makundi ni utaratibu aliyojipangia Balozi Seif wakati anapopata wasaa wa kufanya hivyo katika muelekeo wa kuwashirikisha Wana Jamii kwenye mjumuiko huo wenye kuleta ushirikiano miongoni mwa Wananchi mbali mbali Nchini.


 Baadhi ya Wazee wanaoishi katika Nyumba za Serikali Sebleni Mjini Zanzibar waki katika Futari ya pamoja na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akitoa shukrani kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar mara baada ya futari ya pamoja na Wazee wa Nyumba za Serikali Sebleni.
 Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wazee Wanaume wanaoishi nyumba za Serikali Sebleni mara baada ya kufutari nao pamoja iliyowashirikisha pia baadhi ya Wazee wa Chama Mkoa Kaskazini Unguja.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na baadhi ya Wazee Wanawake wanaoishi nyumba za Serikali Sebleni mara baada ya kufutari nao pamoja iliyowashirikisha pia baadhi ya Wazee wa Chama Mkoa Kaskazini Unguja. Picha na – OMPR – ZNZ.

Bid Announcement

$
0
0
Dodoma, 15th May 2019



The Republic of Mauritius invites bids from the reputable Tanzanians companies as announced by its various institutions. The interested companies can download the bidding documents from the Public Procurement Website; http://publicprocurement.govmu.org.  


The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation encourages eligible companies to submit their bids on time.


Issued by:

Government Communication Unit,

 Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Benki ya CRDB kufanya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Ishirini na Nne - Mei 18, 2019, Jijini Arusha

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Mount Meru wakati wa kuwakaribisha Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa ishirini na nne utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 18 Mei, 2019, katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Mkutano huo utatanguliwa na Semina ya Wanahisa itakayofanyika ijumaa tarehe 17 Mei 2019. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Joseph Witts.
Baadhi ya wageni wakifatilia mkutano kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela na waandishi wa habari, uliofanyika mapema leo kwenye hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha.
Benki ya CRDB kufanya Mkutano Mkuu wa ishirini na nne wa Wanahisa tarehe Mei 18, 2019. Akizungumza na Wandishi wa Habari katika hoteli ya Mount Meru iliyopo Jijini Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Nsekela amesema Mkutano huo wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC uliopo katika Jijini hilo la Arusha.

“Kama ilivyo ada Benki ya CRDB imeandaa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki unaotarajia kufanyika tarehe 18/05/2019”, alisema Ndugu Nsekela.

Nsekela alisema Mkutano huo wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na Semina maalum kwa Wanahisa itakayofanyika tarehe 17/05/2019 katika ukumbi huo huo wa AICC ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Majaliwa. Ndugu Nsekela amesema katika Semina hiyo Wanahisa wa Benki ya CRDB watapata kufahamu juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa sehemu ya Wanahisa wa Benki.

Akiwahamasisha Wanahisa wa Benki wa Benki ya CRDB kuhudhuria katika Mkutano Mkuu, Ndugu Nsekela alisema kuhudhuria kwao ni muhimu sana kwani kunaisaidia Benki katika kupanga na kuidhinisha mikakati mbalimbali endelevu itakayoiwezesha Benki ya CRDB kufanikisha malengo iliyojiwekea na hivyo kuendelea kutengeneza faida kwa Wanahisa.

Akizungumzia kuhusu agenda za mkutano huo wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Ndugu Nsekela alisema ni pamoja na kupitisha na kusaini kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ishirini na tatu uliofanyika tarehe 19 Mei 2018, kupokea na kupitisha Taarifa za Fedha na ripoti za Wakurugenzi kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2018, kuidhinisha taarifa maalumu ya gawio kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2018, kuchagua wajumbe wapya wa Bodi, kuidhinisha uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaokubalika kisheria kwa mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2019, kupanga mahali na tarehe ya Mkutano Mkuu ujao pamoja na kujadili mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wanahisa wa Benki juu ya uboresha wa huduma za Benki.

Nsekela alimalizia kwa kuwahamasisha Wanahisa wa Benki ya CRDB kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo mkuu wa Wanahisa wa Benki YA CRDB, “Naomba nichukue fursa hii tena kuwakaribisha Wanahisa wote wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu kwani kuhudhuria kwao ndio mafanikio ya mkutano huo.

Kwa Mwanahisa ambaye hawataweza kuhudhuria yeye mwenyewe ana haki yakuchagua mwakilishi au wawakilishi kuhudhuria na kupiga kura kwa niaba yake”, alisema Ndugu Nsekela.

RAIS MAGUFULI NA USHINDI WA KULINDA RASILIMALI ZA MADINI

$
0
0
Na Judith Mhina -Maelezo

Adhima ya Tanzania kuwa kinara uuzaji wa dhahabu Afrika Mashariki na kuzuia utoroshaji ya madini yake imetimia.

Hii imetokana na kutekelezwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika kuratibu na kutambua madini yote, kuanzishwa kwa masoko ya ununuzi ya dhahabu ndani na uuzwaji wa madini nje ya nchi.

Kuzinduliwa kwa soko kuu la kimataifa la uuzaji wa madini ya dhahabu Mkoa wa Mwanza, lililopo katika jengo la Rock City Mall, kumedhihirisha nia ya Tanzania kuhakikisha inalinda rasilimali za madini ya Tanzania. Hii inawahakikishia wachimbaji wadogo kunufaika na kazi yao, pamoja kuchangia pato la Taifa.

Akiongoza utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli mapema mwezi Machi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alizindua mnada wa dhahabu katika Mkoa wa Geita, yenye masoko mawili, ili kuondoa changamoto ya wachimbaji wadogo kuhangaika kutafuta mahali pa kuuzia madini yao.

Baadhi ya Mikoa iliyotekeleza agizo la ujenzi vituo vya kuuzia dhahabu ni pampja na Geita, Mwanza, Shinyanga, Chunya (Mbeya) Mpanda, (Katavi), Mara, Arusha, Singida, Iringa, Mkinga (Tanga) na Manyara ambao wanajenga vituo viwili vya kuuzia madini ya Tanzanite na vito vingine.

Aidha, ujenzi huo utajengwa katika miji midogo ya Mererani maalum kwa ajili ya uuzwaji wa madini ya Tanzanite na vito, wakati soko la pilli linajengwa mji mdogo wa Orkesumet kwa ajili ya uuzwaji wa ruby, green tourmaline na vito vingine.

Jitihada za Rais Magufuli za kulinda na kupigania rasilimali za Watanzania zimemfanya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kutuma ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Peter Crolies, kukiri kuwa uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya madini ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika.

Waziri Crories amesema hayo katika ziara ya siku nne mkoani Mwanza na Geita ambapo lengo ni kujifunza, jinsi Tanzania inavyoendesha sekta ya madini na kufanikiwa kuwa na uhusiano mzuri baina ya serikali, wachimbaji wadogo na wakubwa kwa kudumisha amani.

“Tanzania na Uganda zitaendelea kushirikiana katika Nyanja za kitekinolojia na taarifa za kiolojia Tumekuja hapa kujifunza jinsi ya usimamizi wa rasilimali ya madini ili nasi kupata ujuzi kutoka TZ ambao tutakwenda kufikisha jatika serikali yetu na kuwafundisha wananchi wetu wanaojihusisha na uchimbaji” Amesema Waziri Clories.

Amesema ziara hiyo imekuwa na mafanikio kwao kwa kuwa hajawahi kushuhudia na kujifunza rasilimali za madini zinavyotakiwa kuendeshwa na kutunzwa hadi kufikia hatua ya jamii na serikali wa kupata uchumi mzuri.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Madini Stansilaus Nyongo amesema wachimbaji wadogo ndio watoroshaji wakubwa wa madini hususan dhahabu lakini Tanzania imejipanga kuthibiti na kupunguza namna ya utoroshwaji wa huo kwa kuanzisha masoko hayo ya kuuzia madini.

Watanzania wamekuwa na utamaduni au desturi ya kudharau na kubeza jambo lolote jema linaloanzishwa hapa nchini na kupenda kusifia na kuona mambo yanayofanyika nje ya Tanzania ndio mema tu. Waswahili husema “Mdharau kwao ni mtumwa”.

Lakini ubora wa Tanzania umethibitishwa na Waganda walioona ni vizuri kuja kujifunza kuhusu madini kutokana na nchi yetu kutunza vizuri rasilimali za madini hasa kwa wachimbaji wadogo. Ambapo imekuwa vigumu kwa nchi nyingine kufanya kazi kwa ushirikiano na kudumisha amani. Amesema Waziri Nyongo.

Ujumbe wa Uganda ulikuwa na maafisa waandamizi wa serikali pamoja na wachimbaji wadogo 35 ulitembelea maeneo yanayochibwa dhahabu katika migodi ya Geita Gold Mine- GGM Rwangwa Busonwa Mine, Msagano na maeneo ya kuchengulia dhahabu ya Rich Hill na Genge tatu.

Zoezi hili la uazishwaji wa vituo vya kuuzia madini ni utekelezaji wa maagizo kadhaa ya Rais Magufuli ambapo, itarahisisha serikali kuratibu wanunuzi wa madini na wanunuzi hao kujulikana wanapoyauza madini hayo, ndani na nje ya nchi, na kutambua kiasi cha fedha nchi ilizopata kutokana na mauzo hayo.

Aidha, kurejeshwa kwa utaratibu wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania-BOT, kuhusika na ununuaji na uuzaji wa dhahabu, iliyochenguliwa nje ya nchi na kuratibu mapato yatokanayo na uuzwaji wa dhahabu na madini mengine ambayo yanapatikana hapa nchini Tanzania. Itadhihirisha dhahiri kama nchi tunaongoza katika uuzaji wa dhahabu Afrika Mashariki.

Kulingana na taarifa ya mwezi April ya BOT kuna ongezeko la uuzwaji wa dhahabu nje ya nchi. Ongezeko hilo lililotokana na ulinzi na uangalizi sahihi wa uuzwaji wa madini ambapo watoroshaji walikuwa na mwanya wa kuiba katika migodi na kutorosha nje ya Tanzania.

Umakini wa serikali wa Awamu ya Tano umaezaa matunda katika migodi miwili mikubwa hapa Tanzannia ukiwemo Geita Gold Mining na North Mara Gold Mining baada ya kuzalisha kiasi kikubwa zaidi cha madini hayo na kuuzwa nje ya nchi .

Ongezeko hilo ni la Dolla za Marekani milioni 100 kuanzia Julai 2018, mpaka kuishia Machi 2019 ambapo ni sawa na fedha za Tanzania Bilioni 223. Ongezeko hilo ni la fedha za Marekeni ni sawa na bilioni 1.68 ikilinganishwa na mwaka 2018 mwezi Machi.

Pia, Mkoa wa Geita kilo 198 za dhahabu zimeuzwa kwa kipindi cha mwezi mmoja tangu soko hilo limeanzishwa tarehe 22 Machi mpaka April 2019. Vilevile Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Chunya ndani ya siku nne tangu soko kuanzishwa, kilo 22 zimeuzwa wakati hapo nyuma zilirekosiwa kuuzwa kilo 12 tu kwa mwaka mzima.

Ongezeko hili la dhahabu kuuzwa nje ya nchi, imesababisha kukuza pato la bidhaa na huduma zitolewazo na nchi ya Tanzania zilizotolewa kuishia Machi 2019 kufikia Dola za marakani Milioni 8.5 kutoka milioni 8.4 dola za marekani kwa mwezi Machi 2018.

Soko la dhahabu la Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya lilofunguliwa tarehe 05 Mei 2019 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akifungua soko hilo amesema “ Serikali imejipanga kuhakikisha soko a madini linatatua changamoto kubwa zinazowakabili wadau wa sekta ya madini”

Ameongeza kwa kusema “Kwa kuanzia serikali imeanzisha soko la pamoja la madini ambalo litatoa fursa kuanzia mchimbaji mdogo mpaka mkubwa na kuuza dhahabu yake sambamba na kuwatafutia wanunuzi”

Aidha, wafanyabiashara wa Chunya waliomba serikali kuwahakikishia usalama wa mali zao –madini na fedha zao katika soko hilo lililofunguliwa mjini Chunya, lakini bado wana wasiwasi kuhusu usalama wao. Hivyo ni vema serikali kuimarisha ulinzi na usalama kwenye eneo la soko na kwenye migodi.

Pia wanaipongeza serikali kwa kuweka soko la pamoja la madini ambalo litatoa nafasi kila mfanyabiashara wa dhahabu kuwa kwenye ushindani wa bidhaa yake.

Akitoa kasoro kadhaa zilizokuwepo kwenye sheria ya madini ya mwaka 2007 na kanuni zake Rais Magufuli aliagiza kufanya marekebisho ya sheria ambayo yalifanyika mwaka 2018 na kuagiza kurekebisha kanuni zake wakati wa Mkutano Mkuu na Wadau wa Sekta ya Madini mapema Januari 2019.

Marekebisho hayo yalihusu utaratibu wa uchimbaji wa dhahabu ikiwemo kuweka kumbukumbu ya dhahabu inayopatikana na mauzo yake, na kusaidia kupata takwimiu sahihi. Vilevile kujua ukweli katika Afrika Mashariki nchi ipi inayoongoza kwa uuzwaji wa dhahabu na madini mengine.

Maagizo hayo ya Rais Magufuli yalitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa madini uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere-JNCC uliofanyika kuanzia tarehe 22 Januari mpaka 24, Januari 2019 Jijini Dar-es-salaam.

Hata hivyo, zipo changamoto mbalimbali za madini ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wadau ili serikali iweze kufanya kazi kwa pamoja na wananchi – wachimbaji wadogo wadogo na migodi mikubwa ya wawekezaji.

Mfano hivi karibuni Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro wachimbaji wa madini kadhaa na mmliiliki wa madini wamewakimbia viongozi ambao ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Profesa Idris Kikula ambaye alifatana na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Seriel Mchembe na Kamishina wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeke.

Wadau hao waliacha madini aina ya Ruby, Nut, pikipiki na vitendea kazi baada ya kuona wanamiliki madini hayo kinyume cha sheria bila kuwa na kubali cha kumiliki. Hii ni uthibitisho kuwa sekta ya madini bado inahitaji ushirikishaji wa karibu wa wadau ili wajue wajibu wao wa kufata sheria, taratibu, kanuni na miongozo ya sekta husika.

HANSCANA AWATOLEA POVU VIJANA VIZUIZI WA MAENDELEO KWA WENZAO.

$
0
0
Na.Khadija Seif, Globu ya Jamii

Muandaaji na mtayarishaji maarufu wa video za muziki nchini Hance Richard maarufu kama hanscana amepasua jipu kwa vijana wanaoweka vikwazo katika mafanikio na ndoto za vijana wenzao.

Hanscana kwa sasa anamiliki moja ya kampuni kubwa ya utayarishaji wa video za muziki ijulikanayo kwa jina la hanscana brand, ambapo ameajiri waongozaji wengi vijana ili kufanya kazi pamoja na kuwaachia ujuzi tofauti tofauti.

Hanscana ambaye anaendelea kufanya vizuri kwenye tasnia ya utayarishaji wa video za muziki na kuleta mapinduzi makubwa,huku akifanya kazi lukuki zenye ubora sawa na za watayarishaji wakubwa kama Justin Campos kutoka Afrika kusini , Mr.moe musa kutoka nchini Nigeria.

Tasnia hiyo kwa kiasi kikubwa itaendelea kukua siku hadi siku kutokana na ubora wa video hizo kama cheche ya Ommy Dimpoz, subalkheri ya Aslay, wasikudanganye ya Nandy, utaniua ya Jux na zingine nyingi za wasanii mbalimbali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika kuwa “Ukishindwa kuwa daraja kwa wenzio basi usiwe ukuta", akimaamisha kuwa vijana wanatakiwa kuthamini na kupongeza juhudi za mtu mwingine pasi na kuwa kizuizi wa juhudi hizo au kubeza.

RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA RAFIKI YAKE MAREHEMU FESTO RUTAMIGWA ISOKOZA KATIKA HOSPITALI KUU YA JWTZ YA LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Festo Rutamigwa Isokoza alipoongoza waombolezaji kuaaga mwili huo katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo alifanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile JKT Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya sekondary katika Seminari ya Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa mkono wa pole kwa mjane Mama Anna Isokoza kuifariji familia ya marehemu Festo Rutamigwa Isokoza alipoongoza waombolezaji kuaaga mwili wa marehemu katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya sekondary katika Seminari ya Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwasindikiza mjane Mama Anna Isokoza na familia ya marehemu Festo Rutamigwa Isokoza baada ya kuongoza waombolezaji kuaaga mwili marehemu katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli akiagana na familia ya marehemu Festo Rutamigwa Isokoza baada ya kuongoza waombolezaji kuaaga mwili marehemu katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kuongoza waombolezaji kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji baada ya kuongoza hafla ya kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa zamani Mhe. Edgar Maokola Majogo aliyekuwa miongoni mwa waombolezaji baada ya kuongoza hafla ya kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na askari baada ya kuongoza hafla ya kuaaga mwili marehemu marehemu Festo Rutamigwa Isokoza katika Hospitali kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo jijini Dar es salaam leo Jumatano Mei 15, 2019. Marehemu, aliyekuwa mtaalamu wa kilimo aliyefanya kazi katika JWTZ na taasisi zake za kilimo kama vile makambi ya JKT ya Itende na Mgambo kabla ya kustaafu akiwa Shirika la Elimu Kibaha, alikuwa rafiki mkubwa wa Rais Dkt Magufuli ambaye walisoma pamoja tokea darasa la kwanza hadi la saba katika Shule ya Msingi ya Chato mkoani Geita na baadaye elimu ya secondary katika Seminari ya Katoke mjini Biharamulo mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

Habari za UN: Kila anapozaliwa msichana ndugu wa baba wana hesabu ngombe


MASHARTI YA MWEKEZAJI KATIKA UWEKEZAJI WA BANDARI YA BAGAMOYO

QUEEN DARLIN BADO AMKUMBUKA ALI KIBA,AKIRI DIAMOND ATAFIKA MBALI KISA TANASHA

$
0
0
     Na.Khadija seif,Globu ya jamii

MALKIA wa muziki wa Afro Pop nchini Mwanahawa Abdul  a.k.a Queen Darlin  ameiona nyota ya jaha kupitia muziki wa Diamond kufika mbali kisa  Mwanadada Tanasha.

Darlin amesema Tanasha anafanya muziki, na soko lake amelenga mbali sio Afrika Mashariki tu kutokana na kujuana na watu mbalimbali ambao alikuwa akifanya nao kazi kama video vixen .

"Kuwepo lebo ya wasafi classic baby (WCB) ambayo anasimamia kaka yangu diamond hamaanishi kuwa natoa ngoma nikijisikia au ninavopenda mwenyewe, bali ni kanuni na taratibu ambazo zimewekwa kwa kila msanii kutoa wimbo kwa wakati sahihi kulingana na soko linahitaji kitu gani "

Darlin ambaye amekuwa na muonekano wa kimanjonjo awapo jukwaani,amewashukuru mashabiki wake ambao wameupokea vizuri wimbo wake mpya "muhogo" unaofanya vizuri vituo mbalimbali na kujiongezea wigo wa mashabiki kila kona ndani na nje ya nchi,wakiwemo Wanaume kutokana na taswira inayojengeka kwenye wimbo huo.

"Muhogo ni wimbo ambao ulipita BASATAa na kupewa vibali vyote kutokana na wimbo huo kutumia tafisida na kuficha maana halisi, na ndio kitu pekee ambacho hata wimbo wa nyegezi uliotungwa na Rayvan aliomshirikisha Diamond ulifungiwa kutokana na kutokuwepo kwa tafisida kwa baadhi ya matamshi na kuleta ukakasi kwa hadhira, hivyo nilitumia nafasi hiyo katika kutengeneza na kuboresha wimbo wangu,"

Mwanadada huyo ambaye ameonaka kuendelea kutikia anga ya muziki wa Bongofleva kwa upande wa wasanii wa kike,Darlin amebainisha wazi kuwa bado anamkumbuka sana Alikiba katika kushirikiana nae kwenye kazi zake kimuziki na kutengeneza wimbo kama wajua nakupenda uliofanya vizuri miaka ya 2009.

"Alikiba akitoa ngoma mpya naingia Youtube natazama kama nzuri nasifia, kama mbaya naweka wazi sisi ni watu wa karibu sana "

Darlin amewaomba  mashabiki wake waendelee kumuunga mkono kwenye kazi zake na wiki hii anatarajia kutoa ngoma mpya mbili,moja itakayoitwa 'tawire' na 'mbali'aliomshirikisha msanii mwenza wa kundi la WCB .
Mwanahawa Abdul  a.k.a Queen Darlin

BEI ZA MATUNDA SOKO LA BUGURUNI JIJINI DAR ES SALAAM Inbox x

$
0
0
Wafanyabiashara wa matunda  katika Soko la  Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa kwa sasa matunda yanapatikana kwa wingi ,Wachuuzi hao wamebainisha bei ya matunda hayo kulingana na ukubwa na ubora wenyewe.

Wakizungumza leo na Michuzi Tv  jijini Dar es Salaam wafanyabiashara  hao wamesema kwa sasa hali iko shwari na matunda yanauzika,wateja wao wamekuwa wakipita sokoni hapo kujipatia matuda mbalimbali kuligana na mahitaji yao.

 

Bei ya Embe sokoni hapo ni kati ya Sh.300 hadi Sh.600  bei hiyo hiyo kwa wanaonunua kwa rejareja.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Bei ya machungwa katika soko la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam yanauzwa kati ya sh. 50 hadi 100 kwa bei ya jumla.
 Bei ya Nanasi katika Soko la Buguruni linauzwa kati shilingi. 500 hadi shilingi 3500.
Bei ya tikitiki maji ni kati ya Sh 500 hadi Sh. 3000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR IKULU NDOGO KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa uchumi wa Zanzibar umeendelea kuimarika sambamba na ukusanyaji mzuri wa mapato na matumizi yake.

Hayo aliyasema leo, katika ukumbi wa Ikulu ndogo Kibweni mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakati ilipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa Kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019.

Katika maelezo yake Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuipongeza Wizara hiyo ya Fedha na Mipango kwa kuendelea kusimamia vyema kuimarika kwa uchumi wa Zanzibar pamoja na mapato na matumizi yanayofanyika.

Alieleza kuwa katika ukusanyaji wa mapato licha ya udogo wake Zanzibar lakini inaonekana ni jinsi gani ilivyopiga hatua na kuweza kupata mafanikio makubwa yanayoonekana.

Hata hiyo, Rais Dk. Shein Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi na watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kushirikiana kwa pamoja na kusaidia sambamba na kuaminiana ili mafanikio zaidi yaweze kupatikana.

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza haja kwa uongozi wa Wizara hiyo kutoa taarifa kwa wananchi juu ya uendelezaji na mafanikio ya miradi ya Kuimarisha Huduma Za Jamii Mijini (ZUSP) ili wawwze kuelewa namna Serikali yao inavyojitahidi katika kutatua changamoto zilizopo na mafanikio yaliokwisha kupatikana sambamba na matarajio.

Kwa uapande wa ujenzi wa bandari ya Mafuta na Gesi asilia huko Magapwani Rais Dk. Shein alieleza hatua zinazoendlea kuchukuliwa na Serikali huku akieleza ujio wa ujumbe kutoka nchini Indonesia ambao utakuwepo nchini kuanzia Mei 16 hadi Mei 20 kuja kuangalia mradi huo na namna ya kuendeleza ushirikiana na Zanzibar katika uendelezaji wa mradi huo.  
Mapema Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akitoa taarifa fupi ya Wizara hiyo alieleza kuwa tathmini ya mwenendo wa Uchumi wa Zanzibar inaonesha wazi kwa viashiria vyote kwamba uchumi wake ni imara na unakuwa kwa kasi iliyokusudiwa.

Alieleza kuwa katika mwaka wa 2018 pato la halisi la Taifa lilikwua kwa TZS 2874 Bilioni ikilinganishwa na TZS 2684 bilioni kwa mwaka 2017, sawa na ukuaji wa asilimia 7.1.

Aliongeza kuwa ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2018 umetokanja na mambo mengi yakiwemo kuongezeka kwa idadi ya watalii waliofika nchini kwa asilimia 20.1 kufikia watalii 520,809 mwaka 2018  kutoka watalii 433,474 mwaka 2017.

Jengine ni kuongezeka kwa usafirishaji wa zao la mwani, kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula, kuongezeka kwa shughuli za sekta  ndogo ya usafirishaji pamoja na kuongezeka kwa muda wa kukaa wageni hasa watalii.

Pamoja na hayo, Balozi Ramia alieleza kuwa jambo la kwanza kabisa kwa umuhimu wake ni kuendelea kuwepo kwa hali ya Amani na utulivu mkubwa hapa nchini hali iliyowapa fursa nzuri wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo kwa ufanisi. 

Ne Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee aliipongeza Wizara hiyo kwa mafanikio makubwa iliyopata sambamba na uwasilishaji mzuri wa Mpango Kazi wake.

Nao uongozi wa Wizara hiyo ulieleza mafanikio na matarajio ya miradi ya Kuimarisha Huduma Za Jamii Mijini (ZUSP) ambayo tayari baadhi yake imeshakamilika na mengine imo ukingoni kukamilika kwa upande wa Unguja na Pemba.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) Salum Nasor alieleza mikakati ya uwekezaji inavyotekelezwa huku Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Ameir akieleza hatua za ujenzi wa Makao Makuu ya Benki hiyo unaoendelea huko Malindi mjini Zanzibar.

Wakati huo huo, Rais Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale chini ya Waziri wake Mahmoud Thabit Kombo ambapo katika taarifa ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2018 hadi Machi 2019 alieleza kuwa Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kuandaa tamasha la Urithi wa Utamaduni wa Mtanzania (Urithi Vestival).


Aidha, alieleza kuwa wizara imepokea vifaa vya kisasa vya kazi za Digitali na kuhuisha nyaraka zilizochakaa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo wa Serikali ya Oman vyenye thamani ya zaidi ya TZS 89,204,100 ambavyo ni kwa ajili ya kuhuisha na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka kwa matumizi ya sasa na baadae.

Pia, waziri Kombo alieleza kuwa Wizara hiyo imeandaa kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na sekta binafsi Tamasha la Utalii la Zanzibar ambalo lilifunguliwa rasmi na Rais Dk. Shein Novemba 17 mwaka jana 2018 katika hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.

Sambamba na hayo, Waziri huyo alieleza mafanikio ya Wizara kwa kuwasiliana na Kampuni ya DSTV ambayo inarusha matangazo yake karibu duniani kote, ambapo hatua za kufungua ofisi hapa Zanzibar zimekamilika ambapo hivi sasa wanafanya matengenezo ya jingo la ofisi lililopo Mlandege Unguja hatua ambayo pia itopanua soko la ajira katika tasnia ya utangazaji.

Nae Rais Dk. Shein kwa upande wake aliipongeza Wizara hiyo kwa mafanikio yaliopatikana pamoja na kupongeza hatua zilizochukuliwa hadi kufikia Kampuni ya DSTV kurusha matangazo ya Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) moja kwa moja.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, azungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa kipindi cha Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar, kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee , Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa. (Picha na Ikulu) 
 WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohammed Ramia Abdulwawa (katikati) akisoma taarifa ya mpango kazi ya Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar wakati wa mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, uliofanyika katika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar kulia Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee. 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara hiyo kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March2019, uliofanyika katiuka ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.15-5-2019.
 KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Ndg. Khamis Mussa akisoma ripoti ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake wakati wa Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi March2019, uliofanyika katuika ukumbi Mdogo wa Ikulu Kibweni Zanzibar. 
 KATIBU Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Ndg. Juma Reli akichangia wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu  Ndogo Kibweni Zanzibar, 
 MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Bi. Sabra Issa Machano, akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar kwa mwezi wa Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.
 MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg. Juma Ameir Hafidh, akichangia wakati wa mkutano huo wa Utekelezaji wa Mpangio Kazi wa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.


MAOFISA wa Idara mbalimbali za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar wakifuatilia mkuttano huo wa Utekelezaji wa Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi March 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Ndogo Kibweni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MUUZA NYAMA ARUSHA AJINYAKULIA KITITA CHA SH MILIONI MOJA KUTOKA BIKO

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images