Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

KIPATO KIDOGO TATIZO KUJIUNGA MIFUKO YA JAMII - Irene Isaka

$
0
0
 MKUU wa wilaya ya Mtwara  Mhe. Willman Kapenjama Ndile akitoa hotuba ya ufunguzi katika mafunzo ya siku moja ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii   kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika leo katika ukumbi wa  Boma mjini hapa, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walihudhuria.
 Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii SSRA Mama Irene Isaka, akisisitiza jambo wakati akitoa maelezo juu ya kazi za mamlaka hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mtwara, Willman Kapenjama Ndile kufungua mafunzo ya siku moja  ya SSRA kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika leo katika ukumbi wa  Boma mjini Mtwara, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walihudhuria.
 WASHIRIKI wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mtwara muda mfupi baada ya kufungua mafunzo hayo,yaliyotolewa na  mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii   kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika leo katika ukumbi wa  Boma mjini hapa, ambapo viongozi wa serikali wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walihudhuria.
 Viongozi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SSRA Mtwara
MKUU wa mawasiliano na uhamasishaji wa mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya jamii SSRA Bi. Sarah Kibonde Msika, akitoa mada katika mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na mamlaka hiyo kwa viongozi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika leo katika ukumbi wa  Boma mjini hapa, ambapo viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, viongozi wa vyama vya wafanyakazi na waandishi wa habari walihudhuria. 

Habari na picha  na Hassan Simba 
wa Globu ya Jamii, Mtwara
IMEELEZWA kuwa kipato kidogo miongoni wa jamii ni moja kati ya sababu zinazochangia watu wengi kushindwa kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii nchini na hivyo wengi wao kuishi katika maisha duni zaidi wanapokuwa wazee na kuishiwa nguvu ya kufanyakazi.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii  (SSRA) Mama  Irene Isaka, alipokuwa akitoa maelezo juu ya kazi za mamlaka hiyo kwenye mafunzo ya siku moja  ya mamlaka yake kwa viongozi wa serikali, mashirika ya umma na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi wa mkoa wa Mtwara, iliyofanyika katika ukumbi wa  Boma mjini hapa.
Mama Isaka alisema kuwa watu wengi wanashindwa kuchangia michango ya kila mwezi katika mifuko ya jamii licha ya serikali kuongeza wigo kwa wasio na ajira rasmi kujiunga na kunufaika na mifuko hiyo. Ambapo hata hivyo alisema ni jukumu la kila mfuko kuendelea kuwaelimisha ili waweze kuona umuhimu wa jambo hilo na kujiwekea kidogo wanachokipata kwa maisha yao ya baadae.
Alisema kuwa hadi sasa wanachama wa mifuko ya jamii nchini wamefikia asilimia 1.8 kati ya nguvu kazi yote iliyopo nchini, ambapo michango ya wanachama ni shilingi trioni  1.6 huku mafao yaliyokwishakutolewa yakifikia trion 1.06.
Mkurugenzi Mkuu huyo alifafanua pia  kuwa hadi sasa mifuko ya jamii nchini inahudumia wastaafu 87,000 ambapo vitegauchumi vilivyowekezwa vinafikia thamani ya shilingi trion 4.9 na mali zilizopo zikiwa na thamani ya shilingi trion 6.4.
Akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Mtwara, Mhe. Willman kapenjama Ndile alisema kuwa tabia ya baadhi ya waajili kushindwa kuwasilisha michango ya watumishi wao katika mifuko ya jamii kwa wakati ni dhuruma na inachangia kuwafanya wafanyakazi hao kuishi maisha mafupi mara baada ya kustaafu.

Mhe. Ndile alisema kuwa iwapo waajili watakuwa makini na kuwasilisha michango kwa wakati mifuko hiyo itaweza kuwahudumia wanachama wake kwa wakati na hivyo kumuwezesha mstaafu kuendelea kuishi maisha mazuri na marefu kutokana na kuukimbia umasikini kwa kupata mafao yatakayomwezesha kujikimu.


PINDA AHUDHURIA MAHAFALI YA YA CHUO KIKUU MZUMBE MJINI MOROGORO LEO

$
0
0
 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Jaji Barnabas Samata  (kushoto) akimtunuku Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu hicho,  Mbunge  wa Viti Maalum Pindi Chana  katika Mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo mjini Morogoro leo.
 Mbunge wa Viti Maalum, Pindi Chana  akishukuru baada ya kutunukiwa Shahada  ya Udaktari wa Falsafa ya Chuo Kikuu cha Mzumbe na Mkuu wa Chuo hicho, Jaji Barnabas Samatta  (wapili kulia) katika mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo mjini Morogoro leo.   Wa nne kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na wasita kulia ni mkewe Mama Tunu Pinda akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Mama Tunu Pinda wakopozi kwa furaha na Binti yao Janet Pinda  ambaye alipokea Shahada  ya Uzamili ya Uongozi katika Mifumo ya Afya kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe yaliyofanyika Chuoni hapo mjini Morogoro leo.
  Mtoto wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Janet Pinda  (kulia) akipongezwa na wadogozake, Nasirika  Nyema (wapili kulia) na  Namsi Pinda (kushoto) baada ya kutunukiwa  Shahada ya Uzamili  ya Uongozi  katika Mifumo ya Afya kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro leo.
  Mtoto wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda,  Janet Pinda,  akipongezwa na shangazi yake , Beatha Pinda Kaitira (kushoto) baada ya kutunukiwa shahada ya uzamili ya uongozi  katika mifumo ya afya kwenye mahafali ya chuo kikuu cha mzumbe mjini Morogoro December
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjiniMorogoro  Desemba 6, 2013. Katikati ni mkewe Mama Tunu Pinda. Picha na PMO

AIRTEL BINGWA KUFUNGUKIA MBAGALA ZAKHIEM KESHO

$
0
0
Haya sasa mabingwa woote WA AIRTEL BINGWA kula bata pamoja wikiendi hii Mbagalaaaaaa Kama wewe ni bingwa wa kusakata kabumbu na kuonyesha umahili wa kumiliki mpira njoo KESHO tuonyeshe Jumamosi hii MBAGALA ZAKHIEM kuanzia saa sita mchana mpaka saa 12 na nusu…..zawadi kibao kutolewa jezi, tisheti, N.K.………. 
 On stage atakuwa wasanii huku atakuwa Ney wa Mitego pande ya huku atakuwapo Young killer bila kuwasahau Vinoko shackers ndani, Piaaaa wadada kumi wazuriii watachuana kupiga dana dana live. Huku tukishuhudia draw ya Mimi Bingwa watu wanavyojishindia mamilioni na ticket ya kwenda old Trafford kuangalia live mechi za Man U bureee 
 Kama haitoishi Sasa screen kubwa ya ukubwa zaidi ya mita 4 itaonyesha live mchezo wa Man u na Newcastle united Kiingilio ni BUREEEEE 
 Bata hili linaletwa kwenu na Airtel kupitia Promotion ya Mimi ni bingwa

Article 18

yale yaleeeeee......

$
0
0
Hapa ni makutano ya barabara za Jamhuri na 
Azikiwe Avenue jijini Dar es salaam..

ubunifu katika ujasiriamali...

$
0
0
 Wajasiriamali wapiga picha wakiwa kazini kwenye mnuso katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam hivi karibuni. Vijana wengi nchini kote wamejiajiri wenyewe katika shughuli hii na inaonesha mambo si mabaya sana
Wajasiriamali wengine ni wabunifu kwa kuwa na 'mali' adimu ya mbwa. Ukipita barabara ya New Bagamoyo Road maeneo ya Victoria jijin Dar es salaam unaweza kujipatia rafiki huyu kwa binadamu kwa bei ya maelewano, kutegemea umri na aina ya mbwa. Globu ya Jamii haikupata nafasi ya kuuliza 'chanzo' cha mali hai hii, huenda anafuga mwenyewe nyumbani...

WANANCHI TUMIENI LIBENEKE KUU LA TAIFA - WITO

$
0
0
Tovuti_1_2_04ac8.jpg
Mkurugenzi wa Udhibiti wa Huduma za Serikali Mtandao nchini Bw. Michael Moshiro akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu upatikanaji wa taarifa za serikali kwenye Tovuti Kuu Serikali. Amewaomba watanzania kuitembelea tovuti hiyo ili wapate taarifa na huduma zinazotolewa na serikali.Kulia kwake Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshekangoto.
Tovuti_-_2_2_8e185.jpg
Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mkutano na watendaji wa Wakala ya Serikali mtandao leo jijini Dar es salaam. Mkutano umelenga kuwahamasisha watanzania kuitumia Tovuti Kuu ya Serikali inayopatikana kwa anuani ya: 
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

TCRA yaipa Azam Media leseni kuiwezesha kuendesha shughuli zake.

$
0
0
 Azam Media Ltd  leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake hapa Tanzania.

Hatua hii muhimu sasa inaiwezesha AzamTV kuanza kutoa huduma zake kwa wateja wake kote Tanzania kuanzia tarehe16 Desemba. Huduma hii itwapa fursa wateja kuangalia zaidi ya chaneli 50 za kitaifa na kimataifa ziliozosheheni burudani kwa ajili ya familia kwa bei nafuu ya shilingi 12,500/= kwa mwezi. Kutakuwepo wigo mpana wa kuchagua kifaacho kuangalia vikiwemo vipindi vya michezo, makala, watoto na tamthilia kutoka Tanzania, barani  Afrika na sehemu mbalimbali za dunia. 

Baadhi ya vipindi hivyo tajwa vitapatikana katika chaneli maarufu  kama vile National Geographic Gold na Nickelodeon, na pia matangazo yetu yatakuwa na chaneli za bila malipo zikiwemo TBC1, Channel 10, Clouds, ZBC na K24. Jambo la kusisimu zaidi  ni kwamba  AzamTV itakuwa na matangazo katika chaneli zake tatu:

AzamOne - Itakuwa na vipindi vya kiafrika, ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu masuala ya Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili. Hii ndiyo chaneli ambayo itakuwa ikirusha matangazo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara;
AzamTwo – Hapa vitapatikana vipindi vya burudani kwa familia amabavyo ni vya kimataifa na baadhi ya hiovyo vitakuwa katika lugha ya kiswahili;
SinemaZetu – Chaneli maalum kwa ajili ya tamthilia za kitanzania.

Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema: “Huu ni  wakati wa kujivunia  kwa Tanzania kwani sasa ina huduma za luninga zinazopatikana kwa  bei ambayo wengi wanaweza kuimudu.  Miezi michache ijayo tutaivusha huduma hii mipaka hadi katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata mbali zaidi. Nimefarijika kwamba tumewekeza vilivyo katika chombo hiki cha kitanzania na tutaendelea kufanya hivyo”.

Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja ambao hawatapenda kungojea kuzinduliwa rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya ofisi zake za Dar es Salaam itakuwa wazi kuanzia  leo (Ijumaa Desemba 6, 2013).  Watejawataweza kununua  vifaa muhimu kutoka duka la AzamTV na kwa mawakala walioidhinishwa  na hivyuo kuweza kujionewa vipindi mbalimbali kuanznia sasa – japo malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia Desember 16.

UPPER HILL RESIDENCE GOBA

$
0
0
 Goba is located in Mbezi, Kinondoni municipality in Dar es Salaam. This chosen site is only 5.5 km from Bagamoyo road (Turning left at Shamo Plaza, following the road past Massana hospital) 30 Minute drives to CBD facilities. The spacious Luxurious villas contain enough space for parking 3 cars, 3 bedrooms plus small room, Adequate water supply (Borehole and water tanks for each house), Paved roads, Gated community, High end finishes, Garden etc.. The houses are fitted with porcelain floor tiles and zinc coated aluminum roofing tiles which look similar to concrete tiles. At the moment we have completed 10 houses out of 42 houses.  
 
The price of each house is $110,000 USD +VAT and each owner will be provided with their own individual subtitle.  
 
 
More information about the house stages and Photos are available on our Facebook page. You can also get more details through our contact below: 
 
+255756145287 
+255789282971
 
 
"WHY JENGA WHEN YOU CAN BUY"

ILIKUWA SHUGHULI PEVU KWA DKT ASHAROSE MIGIRO LEO MKOANI NJOMBE.

$
0
0
 Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
 Juhudi ya kulinasua gari hilo zikiendelea kufanyika.
Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa iliponasa kwenye tope.
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo.
 Juhudi za kulinasua gari hilo zikiendelea.
 Eneo linavyoonekana
Gari ikiwa imekwishaondolewa kwenye eneo korofi tayari kwa kuendelea na msafara kutoka Wilaya ya Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe.Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,ItIkadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro amemaliza ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya na baadae kupitia mkoa wa Njombe kukagua baadhi ya miradi mbalimbali na kazi za kijamii.

CCM YAOMBOLEZA KIFO CHA MZEE NELSON MANDELA

IFC Helps Chinese Developer Construct Energy-Efficient Building in Tanzania to Increase Property Supply

$
0
0

IFC, a member of the World Bank Group, has agreed to provide financing to support Chinese developer CRJE Estate Ltd. to construct an energy-efficient commercial building in Dar es Salaam, the largest city in Tanzania. The project will significantly increase the supply of quality hotel rooms and office space in the African nation. 

IFC will provide CRJE Estate a $22 million long-term loan to fund a 29-storey commercial complex, which includes 250 hotel rooms and 8,200 square meters of office and retail space. CRJE Estate, a wholly owned subsidiary of China Railway Jianchang Engineering Co., is one of the largest construction companies in Tanzania. The project will adopt IFC’s green-building standards, which can help reduce a building’s energy consumption by 20 percent. 

“IFC’s advice is integral to the smart and sustainable design, construction and operation of our building and improves the project’s long-term prospects,” said Shi Yuan, Chairman of CRJE Estate. “We can now supply essential infrastructure to investors and travelers in order to facilitate business and create economic opportunities in Tanzania.”

Although Tanzania’s economy grew a robust 7 percent last year, with the World Bank forecasting that it will continue to grow at a similar pace in the coming years, Dar es Salaam’s property and hotel sectors remain significantly underdeveloped. In 2010, IFC already provided $10 million to CRJE Estate for the initial phase of this property project, which was IFC’s first loan to a Chinese company in Africa. The latest financing will more than double IFC’s funding to support the new development plan.   

“The CRJE Estate-led project demonstrates that Chinese developers can be a major force in Africa’s property investment and development,” said Oumar Seydi, IFC Director for Eastern and Southern Africa. “Office infrastructure and hotel development create business opportunities and good jobs, which can help spur further investment and development in Tanzania.”

The hotel will be managed by Rotana Hotel Management Corp., which runs 70 hotels and resorts in the Middle East and North Africa. The project is a partnership between CRJE Estate and Mwalimu Nyerere Foundation, a nongovernmental organization honoring the legacy of Tanzania’s first president, Julius K. Nyerere, which has a long-term lease on the building.

News alert: Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Mtandaoni lafikia tamati, Neema Urasa Kivugo wa Kibaya Kiteto ashinda

$
0
0

Mshindi wa shindano la Mama Shujaa wa chakula mtandaoni 
Neema Urasa Kivugo kutoka Kibaya Kiteto.akifurahia mara baada ya
 kutangazwa usiku huu jijini Dar es salaam

Neema, ambaye amepata kura 778 kati ya kura 1011 ambayo  ni sawa na asilimia 76.95 ya kura zote zilizopigwa, amejishindia vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 5 ambavyo atachagua yeye mwenyewe na nafasi ya moja kwa moja ya kushiriki shindano kubwa la Mama Shujaa wa Chakula linalofanyika sambamba na kipindi cha Maisha halisia cha Maisha Plus litakalozinduliwa rasmi siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013.

Shindano la Mama Shujaa wa Chakula mtandaoni lilifunguliwa rasmi tarehe 4/11/2013 na Balozi wa Kampeni ya Grow, mwanawavuti Shamim Mwasha kama mchango wake kwa wakulima wadogo wanawake.

Akiongea baada ya kutangazwa mshindi, Neema amelishukuru shirika la Oxfam kwa kufadhili shindano hilo na kwamba limemtia moyo kuendeleza kilimo na anaahidi kuwashirikisha wanawake wakulima wenzake.

Naye Shamim amewashukuru na kuwapongeza washiriki wote wa shindano hilo. Ametambua mchango wa wakulima wote hasa wanawake na kusema kwamba wote ni bora na wasivunjike moyo kwa sababu hawakushinda bali waendelee kuamini kwamba jamii inathamini sana mchango wao kwani chakula wanacholima ndicho tunachokula.

Washiriki waliobaki pia wana fursa ya kushiriki shindano kubwa la Mama Shujaa wa Chakula, kwa kujaza fomu, linalofanyika sambamba na kipindi cha maisha halisia cha Maisha Plus litakalozinduliwa rasmi siku ya Jumanne tarehe 10/12/2013.

Hafla hizo zilihudhuriwa na Bi. Anna Maembe, Katibu Mkuu wa Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto, mabalozi wa kampeni ya GROW, washiriki watatu kati ya watano bora ambao ni Ezeline Mujila, Neema Urassa ambaye ni mshindi pamoja na Gloria Kidulile.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

ngoma azipendazo ankal

$
0
0

Ngoma ya Chicco ya 'We Miss You Manelo' iliturusha sana Disko Toto enzi hizo. Hatukujuwa kwamba hio 'Manelo' ilimaanisha 'Mandela' ambapo wakati huo ilikuwa kosa la jinai kutaja jina hilo Afrika Kusini enzi hizo. Na Chicco alibadili jina na sio maudhui ya kuuliza u wapi Madiba. Tunakumiss sana, uko wapi??  Ankal aliiweka ngoma hii hewani  jana Desemba 5, 2013 bila kujua kwamba leo atatutoka.

MKURUGENZI MKUU WA MFUKO WA AKIBA YA WAFANYAKAZI SERIKALINI "GEPF" AONANA NA KUUTAMBULISHA MFUKO HUO KWA VIONGOZI WA MKOA WA RUKWA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) Bwana Daud Msangi akizungumza na viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya kwa lengo la kuutambulisha mfuko huo na faida zake. Mfuko huo una fursa mbili za kujiunga ambazo ni kwa njia ya lazima kama ilivyo kwa mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kwa watumishi wa Serikali na njia nyingine ni ya hiari kwa wafanyakazi wote wakiwemo wa Serikali, Sekta binafsi na hata wale waliojiajiri wenyewe. Kwa wale wateja waliojiunga na mfuko huo kwa hiari wana uwezo wa kuchukua mafao yao kwa muda mfupi tofauti na ule mfumo wa lazima wa Serikali ambao ni lazima mteja afikie umri wa kustaafu.
Wajumbe wa kikao hiki walikuwa Wakuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nkasi na Kalambo. Wakuu wa Idara wote katika Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa, Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbwanga, Kalambo na Nkasi pamoja na baadhi ya wataalamu kutoka katika maeneo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a (wa pili kulia) akichangia katika kikao hicho ambapo alisema Wilaya mpya ya Kalambo ina fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo sekta ya nyumba za ofisi na makazi ambayo ni fursa kwa mfuko huo wa GEPF kuwekeza kwa kujenga nyumba hizo katika Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. Kulia kwa Mhe Chang'a ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Albinus Mugonya na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Samson Mashalla.
Sehemu ya wajumbe katika kikao hicho. 
Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa

MHE. JANUARY MAKAMBA AWASILI WASHINGTON, DC

$
0
0
Naibu Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiwa na mkewe Ramona Makamba wakipokewa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga(wapili toka kushoka) na mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Mhe. Makamba amekuja maalum kama mgeni rasmi kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania itakayofanyika Jumamosi Desemba 7, 2013 Laurel, Maryland nchini Marekani.
Afisa Ubalozi Mindi Kasiga akimweleza jambo Mhe. January Makamba wakati alipokwenda kumpokea uwanja wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa  Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwenye picha ya pamoja na Makatibu Wakuu na Maafisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Bw. Paul Mwafongo (Kaimu Balozi), Bw. George Yambesi (Katibu Mkuu Utumishi), Mhe. January Makamba, Bw. Peter Ilomo (Katibu Mkuu Ikulu), Bw. Suleiman Saleh (Kaimu Mkuu wa Utawala).
Mhe. January Makamba Picha ya pamoja na  Ujumbe wa PSPF wakiwemo maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 Mhe. January Makamba na mkewe Ramona wakibadilishana mawili matatu na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Abbas Missana, Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Ramona Makamba na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba.

Miondoko ya kumeremeta kwenye mnuso

WAMERAKANI KUSAIDIA UJENZI WA CHUO CHA UUGUZI KARAGWE

$
0
0
 Na Mwandishi Maalum 
 Wilaya ya Karagwe iliyopo katika Mkoa wa Kagera nchini Tanzania, inatarajiwa kuwa na Chuo cha kwanza cha aina yake katikafani ya Uuguzi ( Nursing Collage )kitakachojengwa kwa misaada na ushirikiano kutoka Chuo Kikuu cha Wilkes kilichopo katika mji wa Pennyslavia, nchini Marekani. 
Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki na Professa Evene Estwick wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi. Mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi za Uwakilishi huo jijini New York. 
Akiwa ameambatana na Dkt. Andrew Cesari ( MD, MBA) ambaye ni msimamizi wa Mganga wa Hospitali Teule ya Nyakahanga wilayani Karagwe ambako chuo hicho kitajengwa , Professa Estwick alimweleza Balozi Manongi kwamba Chuo hicho kinatarajiwa kuwa tayari mwishoni mwa mwaka ujao na kwamba michoro tayari imeshakamilika. 
 Aidha ilibainishwa katika mazungumzo hayo kwamba, wataalamu wawili katika fani ya uuguzi wanatarajiwa kwenda mwakani huko Karagwe kwa lengo la kuangalia namna bora zaidi ya kushirikiana katika eneo hilo. 
Katika mazugumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Dkt. Andrew Mayala ( MD, MPH) ambaye ni Medical Officer wa Wilaya ya Karagwe na Bi. Lorienetter Williams ambaye ni Mwanafunzi kutoka chuo hicho, ilielezwa kwamba ujenzi wa Chuo hicho cha Uuguzi unatokana na uhusiano na ushirikiano wa takribani miaka kumi na tatu uliopo kati ya Chuo Kikuu cha Wilkes na Hospitali ya Nyakahanga. 
 Kwa mujibu wa Dkt Andrew Cesari ambaye ndiye mwanzilishi wa fikra hiyo ya kuwa na Chuo cha Uunguzi, alisema kwa kuanzia chuo kitakuwa kinatoa mafunzo ya uuguzi, lakini lengo ni kukipanua kwa kuongeza fani mbalimbali ili kuwapata wataalamu wengi Zaidi. 
“Nilipofika Wilayani Karagwe mwaka 2007, nilikuta wilaya hii ingawa ni kati ya wilaya kongwe nchini, ikiwa haina chuo cha aina yoyote hata cha VETA, ndipo likanijia wazo la kubuni mradi huu, na bahati nzuri marafiki zetu wameonyesha nia ya kutusaidia kufikia lengo hili na mambo yote yakienda sawa ujenzi wa chuo utaanza mwakani”. 
Akielezea umuhimu wa Chuo hicho, Dkt. Andrew Cesari anasema manufaa hayatakuwa kwa kuzalisha wataalamu wengi katika eneo la afya, lakini kitakuwa na manufaa makubwa kwa vijana wengi hasa wale wanaomaliza elimu na kushindwa nini cha kufanya au wapi pa kwenda hasa katika maeneo hayo na ya jirani. 
Kwa hiyo itakuwa ni fursa nzuri kwa vijana wengi kujipatia ujuzi zaidi na kupanua huduma na raslimali watu katika eneo hilo la afya. Anasema Dkt. Cesari 
Dkt. Cesari na Dkt. Mayala walikuwa hapa Marekani kwa mwaliko wa washirika wao yaani Chuo Kikuu cha Wilkes kupitia utaratibu wa kubadilishana wataalamu (exchange program) na wameshiriki katika mijadala mbalimbali ya kitaalam ukiwamo ule uliofanyika katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambapo walipata fursa ya kuelezea uzoefu wao na kubadilishana mawazo na washiriki wengine na pia walifanya ziara katika Chuo kijulikanacho kama Commonwealth Medical Collage kilichopo Scranton. 
Ushirikiano kati ya Chuo Kikuu hicho na Hospitali ya Karagwe ulilanza kwa utekelezaji wa miradi midogo ukiwamo ule wa upelekezaji wa vifaa vya hospitali, ubadilishanaji wa wataalamu na kuwasaidia watoto yatima wanne ambao wamepoteza wazazi wao kutokana na maradhi ya ukimwi. Watoto hao wanne husaidiwa ada na gharama nyingine za shule vikiwamo vitabu kupitia mradi ujulikanao kama “Embrace a Child”, mradi unaoratibiwa na Chuo hicho. 
 Na cha kutia moyo zaidi ni kwamba wanafunzi hao akiwamo Kihinga George wanafanya vizuri kiasi cha kupata nafasi ya kujiunga na kidato cha sita na matarajio yake ni kuwa daktari. “ maendeleo ya watoto hawa ni kati ya hadithi nzuri za ushirikiano wetu, ni watoto wenye akili sana, wanaojituma na walio makini. 
Tunaona matunda yake, hasa kwa kuzingatia kwamba watoto hawa walikuwa hawana msaada wowote tangu wakiwa wadogo” anasema Dr. Evene Estwick kwa furaha kubwa. Kama hiyo haitoshi, gharama za kuwasomesha yatima hao zikiwamo za ada na vitabu zinatokana na michango ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Wilkes kupitia harambee wanazozifanya wao wenyewe. 
Kwa upande wake, Balozi Tuvako Manongi, alielezea kufurahishwa kwake na uhusiano uliopo baina ya Chuo Kikuu cha Wilkes na Hospitali ya Nyakahanga na kwamba ni jambo linalotakiwa kuenziwa na kudumishwa. 
Akasema Serikali inathamini na kutambua mchango wa wadau mbali mbali katika kuchagiza juhudi za serikali za kufikisha huduma za afya karibu na wananchi. Kama sehemu ya utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia ( MDGs) ambayo ufanikishwaji wake wake unahitaji sana ushirikiano kati ya serikali, washirika wa maendeleo na sekta binafsi. 
Akabainisha kwamba uboreshaji wa sekta ya afya ni moja ya vipaumbele vya Serikali na hasa katika uboreshaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto na kwamba ujenzi wa Chuo cha Uuguzi siyo tu utakuwa unachagia juhudi hizo za serikali bali pia ni ukombozi mkubwa kwa wananchi kutokana na upungufu mkubwa wa wataalamu. 
Aidha Balozi Manongi akasema inatia faraja sana kwamba watoto yatima ambao wanasaidiwa kupitia ushirikiano huo wanafanya vizuri sana katika masomo yao na ni kielelezo kizuri kuwa michango inayotolewa na wahisani inawafikia na kuwanufaisha walengwa na akatoa shukrani zake kwa walimu na wanafunzi kwa moyo wao huo wa kujitolea.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, akizungumza na ujumbe ulioongozwa na  Professa Evene Estwick ( kushoto kwa Balozi) kutoka Chuo Kikuu cha Wilkes ( Marekani) ambacho kinaushirikiano na Hospitapi ya  Nyakahanga iliyopo  Wilayani Karagwe  Mkoani Kagera wengine  ni Dkt. Andrew Cesari aliyeketi kulia kwa Balozi ambaye ni  Msimamizi wa Hospitali hiyo  na anayefuatia ni Afisa  Ubalozi,  Bw. Khamis akifuatilia mazungumzo hayo aidha katika mazungumzo hayo  yupo pia Dkt. Andrew Mayala ambaye ni Medical Officer   wa Wilaya ya Karagwe na Bi. Lorienetter Williams  ambeye ni mwanafunzi kutoka Chuo cha Wilkes.
Balozi Tuvako  Manongi akiwa na  Madaktari Andrew Cesari na  Andrew Mayala kutoka Karagwe ambao walikuwapo nchini  Marakani kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa wenyeji wako Chuo Kikuu cha  Wilkes kupitia  mpango wa kubadilishana wataalam. wakiwa hapa  Marekani pamoja na mambo mengine walishiriki katika makongamano ya kitaaluma ambapo walibadilishana mawazo na uzoefu na  wenyeji wao kuhusu namna wanavyokabilliana na  changamoto zitokanazo na maradhi ya  ukimwi pamoja na utoaji wa huduma za afya.
 Balozi Manongi akiwa na Professa Estwick ambaye chuo chake kinauhusiano na  ushirikiano na  hospitali ya  Nyakahanga, uhusiano huo  unaokaribia miaka kumi na tatu sasa unahusisha utoaji wa misaada mbalimbali ikiwamo ya vifaa vya hospitali, usomeshaji wa watoto yatima na ujenzi wa Chuo cha Uuguzi ( Nursing Collage) kulia kwa Balozi ni  Bi. Williams ambaye ni mwanafunzi kutoka chuo hicho.

Waafrika Kusini waomboleza kifo cha Madiba - VOAKISWAHILI

PALE KANISA LINAPOJITOLEA KUKARABATI KITUO CHA POLISI

$
0
0
Mwezi uliopita nililazimika kwenda Kituo cha Polisi cha Osterbaykutimiza masharti au sheria inayohitaji gari kukaguliwa kila mwaka kama taratibu za usalama barabarani. Hii haikua mara yangu ya kwanza kufika kwenye kituo hiki kwani nimekua nikifanya hivi karibu kila mwaka. 
Nilipokua naelekea zilipo ofisi za Usalama barabarani ambazo ziko nyuma ya jengo kubwa la kituo, nikashangaa kuona mabadiliko makubwa ya mwenekano wa majengo ya kituo kile. Niliona ukarabati mkubwa uliokuwa unaendana na majengo kupakwa rangi. Nilipofika nyuma ya jengo nilikuta jengo dogo ambalo ndilo lina ofisi za Usalama Bararani nalo likiwa limebadilika na ofisi imehamishwa kwenye chumba kilichokua chatumika awali. Mshangao wangu uliendelea nilipoingia ofisini na kukuta maasifisa wa polisi waliokua mule ndani wamekaa kwenye ofisi safi na zenye samani (furnitures) mpya, safi na za thamani kama zilizo kwenye ofisini nyingine za kisasa.
Sikuweza kumuuliza yeyote juu ya mabadiliko yale na ndani mwangu nikajisemea kuwa ni nafuu kama polisi wameona umuhim wa kuboresha majengo yao na kuyafanya yawe na mvuto. Baada ya kumaliza kilichonipeleka, niliamua kuangalia kwa karibu bango linaloonesha ujenzi unaondelea ili nijue ni nani anafanya ukarabati ule. Kwa mshangao mkubwa, macho yangu yaligongana na Jina la kanisa la CHRIST EMBASSY TANZANIA  ambalo pia linaitwa LOVE WORLD kwenye kibao kile kama mfadhili wa ukarabati ule. Kwa maana nyingine kanisa la CHRIST EMBASSY TANZANIA ndio wamejitolea kukarabati KITUO CHA POLISI OSTERBAY.

Nilivutiwa sana na kibao kile na nikatamani nikipige picha ili nikaitumie nitakapoamua kuweka jambo lile kwenye maandishi. Lakini nikashtukia kuwa niko kwenye himaya ya usalama na kama ningetimiza haja ya moyo wangu huenda ningeshtuka baadaye sana nikiwa selo baada ya kupata mtikisiko wa ubongo (concussion)  ambao ungekua umesababishwa na  “mitama ya mfululizo” ambayo ningeipata hata kabla sijamaliza kupiga picha ya kwanza.

Nilitiwa moyo sana na kitendo hiki cha dhehebu la dini kujitolea kukarabati kituo cha polisi. Sina hakika kama walifanya hivi kwa kuombwa au kwa kukusudia wao wenyewe, lakini kwangu niliona ni aina mpya ya jinsi madhehebu ya dini na hasa kanisa kuonesha upendo wa kubadilisha maisha ya wengine kwa vitendo. 
Kilichonigusa zaidi kwa msaada huu ni ukweli kwamba vituo vingi vya polisi kote nchini, ni kati ya majengo ya umma ambayo  kwa sehemu kubwa yako katika mazingira duni, machafu, na yasiyo a mvuto kabisa jambo ambalo linavifanya visiwe rafiki sio tu kwa waonkwenda kutafuta huduma bali hata kwa polisi wenyewe wafanyao kazi humo. Huenda hali hii ya majengo na mazingira ya vituo vya polisi ndiyo imefanya watu wengi kutopenda kabisa kufika katika vituo vya polisi maana mazingira yake hayaoneshi kuwa ni maneo rafiki na salama kwa anayekwenda kutafuta haki, kulazimika kutoa haki kwa wengine au kuwajibika kwa matendo yao. 
Huenda mazingira haya ndio yanawafanya askari polisi wengi kutokua rafiki kabisa na raia na wenye jazba na hasira muda mwingi kwa vile mazingira ya kazi yanayowazunguka hayawaoneshi kuwa ni watu wa thamani na kazi yao ina heshima na hivyo kulazimika kutumia njia nyingine kujitafutia heshima.

Kwa wale waliojifunza manejimenti hasa katika nadharia (concepts) za hamasa (motivations) zinazoweza kumfanya mfanyakazi au mtumishi kutimiza wajibu wake vizuri, wanafahamu kuwa sio ukubwa wa ujira/mshahara pekee unaochangia hamasa bali kuna mambo (factors) mengine ambayo yako kisaikologia, kiutu na kitamaduni zaidi.  Kuthibitisha hili, unaweza kuona baadhi ya watu wanaacha kazi nzuri zenye cheo au kipato kikubwa katika kampuni, shirika au hata katika taasisi za serikali kwa kigezo cha kutoridhika na mazingira ya kazi.  
Ndio mana ni rahisi kusikia matapeli wakidanganya watu kuwa wao ni maafisa wa usalama wa taifa, wako TRA au BOT na sio maafisa magereza, fire au makarani wa mahakama. Hamasa ya kazi na kuipenda kazi vinachangiwa sana na mazingira ya ofisi au eneo la kazi kuwa na mvuto unaotokana na thamani ya ofisi yenyewe na samani zilizoko,  usafi wa ofisini na eneo ofisi ilipo. Ndio mana ni rahisi kumsikia mtu hata isivyo kweli kuona fahari kusema ofisi yake iko Posta au Masaki kuliko aseme anakwenda ofisini Tandale au Mburahati.

Nawapongeza sana uongozi na kanisa la Christ Embassy Tanzania kwa ufunuo huu wa kuboresha mazingira ya kituo cha polisi. Kazi yenu ni kubwa kwani hamujasadia tu kufanya majengo yawe na mvuto, bali mumewasaidia maafisa na askari wafanyao kazi katika kituo hiki kuona na kujisikia kazi yao ni ya muhim, yenye thamani na ya heshima na hivyo kuongeza hamasa ya utendaji kazi wao katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao huku wakitenda haki. 
Kuna tofauti sana ya utendaji kazi kati ya askari anayetoka nyumbani kwenye kazini huku akiwaza kuwa zaidi ya bunduki, ofisi yake ina tiles chini, ina ukuta msafi na anakalia kiti cha kuzunguka; ukimlinganisha na yule anayewaza bunduki iliyo kwenye ofisi chafu, isiyo na ukuta msafi na yenye kiti cha mbao kichafu, kibaya na wanachokalia kwa kupokezana kutegemeana na nani alitangulia kukaa.

Nawatia moyo madhehebu mengine ya Kikristo na dini zingine, kuiga mfano huu mzuri wa Christ Embassy wa kusaidia maeneno yanaoonekana sio rafiki kwa jamii kama Polisi. Kama kila kanisa katika eneo lililoko likijotolea kukarabati au kujenga vituo vya polisi, ni wazi dhana nzima ya POLISI JAMII itakua imeongezewa nguvu kwa namna ya kipekee na MATOKEO MAKUBWA SASA ya kiusalama yatakua dhahiri kwa kila mmoja.


Mwalim MM

mathewmndeme@gmail.com




Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images