Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110105 articles
Browse latest View live

WATAALAMU WA TEHAMA WAKUTANA KATIKA KIKAO KAZI


WAZIRI MKUU MHE. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AJUMUIKA NA WAUMINI WA KANISA LA WASABATO MAGOMENI KATIKA IBADA YA KUADHIMISHA MIAKA 100 YA IDARA YA FAMILIA KANISANI

$
0
0
Na Derek Murusuri, Magomeni, Dar es Salaam
Sabato/Jumamosi 11 May 2019

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuheshimu uhuru wa kuabudu nchini."

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Serikali yetu itaendelea kushirikiana na dini zote katika taifa letu ili kuleta utulivu, amani na umoja wa kitaifa. Kuja kwangu hapa katika Kanisa la Waadventista Wasabato Magomeni kuabudu pamoja nanyi leo ni uthibitisho huo."

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Kitabu cha Ayubu 22:21 kinasema, "mjue sana Mungu ili uwe na amani; ndivyo mema yatakavyokujia."

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Serikali yetu itaendelea kumtegemea Mungu katika kuwaletea watanzania maendeleo."

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Nalipongeza kanisa la Waadventista wa Sabato katika kuandaa kitabu hiki cha Tumaini la Familia."

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Kitabu hiki kitatusaidia kufundisha maadili bora."

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Nawasihi, ili kujenga familia imara itakayosaidia kuwa na taifa imara, kitabu hiki kisomwe si na waadventista wasabato peke yenu, bali waislamu na wakristo wa madhehebu mengine pia." 

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Taifa imara siku zote, msingi wake hutegemea familia imara"

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: "Kitabu cha Ayubu 22:21 kinasema, mjue sana Mungu ili uwe na amani. Ndivyo mema yatakavyokujia. 

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: Serikali inatambua mchango wenu muhimu katika kuhubiri neno la Mungu na kuwahudumia watanzania wote kwenye elimu, afya na maafa, bila ubaguzi.

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: Nimetiwa moyo sana kuona mnajenga Kanisa kubwa na zuri sana. Watanzania tunaweza kufanya mambo makubwa pasipo kusubiri ufadhiri wa kutoka nje.

#Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa: Endeleeni kuwahimiza washiriki kutoa sadaka, zaka na kulipa kodi, ili kuendeleza kazi ya Mungu na vilevile kuchangia maendeleo ya taifa letu.*
Zawadi ya picha ya kuchorwa aliyozawadiwa Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanisa la Waadventista Wasabato la Magomeni Mwembechai katika ibada ya kuadhimisha miaka 100 tangu Kanisa hilo lianzishe idara ya familia. Mchoraji ni Sethi Samuel KENGURU, mwenye makazi yake katika jiji la Arusha.


Serikali Yasisitiza Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya "Rambo" Ifikapo Juni Mosi 2019

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine akitoa ufafanuzi kuhusu marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki wakati akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma. Serikali imepiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki ifikapo tarehe 1 Juni, 2019. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Kanizio Fredrick Manyika.

Na: Frank Shija, MAELEZO Dodoma.
Serikali yasisitiza marukufu ya matumizi ya mifuko ya plastiki ifikapo tarehe 1 Juni 2019 ipo palepale tofauti na inavyopotoshwa na baadhi ya watu wenye nia hovu ya kuleta mkanganyiko miongoni mwa jamii.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Balozi Joseph Sokoine alipokuwa akiongea na waandishi wa Hahabri leo jijini Dodoma.

Alisema kuwa katazo hilo la kupiga marufuku mifuko ya plastiki ya aina zote lilitolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akihitimisha Hotuba yake ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Mtakumbuka kuwa tarehe 9 Aprili 2019 Serikali ilitoa Tamko la kusitisha matumizi ya Mifuko ya plastiki hapa nchini ifikapo Juni Mosi 2019, katazo hili linalenga kuepusha athari za kiafaya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo” alisema Balozi Sokoine.

Balozi Sokoine amesema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo na si kubeza na kupotosha kama ambavyo imetokea hivi karibuni kwa mtu kutumia video clip kwa kuisambaza mitandaoni kwa lengo la kupotosha umma.
“Nitumie fursa hii kuwakumbusha wananchi wote kuwa ifikapo tarehe 1 Juni 2019, Serikali itaendesha operesheni kabambe nchi nzima ya kusaka mifuko hii, ambayo itahusisha wadau mbalimbali vikiwemo Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya, Mamlaka za Serikali za Mitaa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, TBS, TFDA, Ofisi ya Mashtaka, pamoja na Mamlaka za Viwanja vya Ndege,Bandari, Forodha, Uhmiaji, na Usafiri wa Nchi Kavu,”

Aliongeza kuwa katika kufanikisha zoezi hilo Serikali imeshafanya maandalizi mbalimbali ikiwemo kutunga kanuni zitakazo anza kutumika kuanzia tarehe 1 Juni, 2019 hivyo ametoa rai kwa watanzania wote kuzingatia maelekezo ya Serikali pamoja na matakwa ya Kanuni za kupiga marufuku matumizi na biashara ya mifuko ya plastiki nchini kwa mustakabali wa uhifadhi wa mazingira ya nchi yetu.

IDADI YA MADAKTARI NA WATOA HUDUMA ZA AFYA WALIOPATIWA MAFUNZO NA WCF YAFIKIA 856

$
0
0

Baadhi ya madaktari na watoa huduma za afya wakionesha stika watakazobandika kwenye ofisi zao, mara baada ya kushiriki mafunzo ya siku tano ya namna ya kufanya tahmni ya ugonjwa na ajali zitokanazo na kazi mjini Morogoro. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) yamefungwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mei 10, 2019.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) tayari umeweza kumetoa mafunzo kwa madaktari na watoa huduma za afya 856 Tanzania Bara kuhusu namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali zitokanazo na kazi

Akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kufunga mafunzo ya wiki moja kuhusu namna ya kufanya tathmini hiyo mjini Morogoro Mei 10, 2019, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omary alisema idadi hiyo ni kuanzia mwaka 2015 tangu Mfuko huo uanze kutekeelza majukumu yake hadi kufikia Mei 10, 2019.

Alisema washiriki waliohudhuria mafunzo ya Morogoro wanatoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro na licha ya kufundishwa namna ya kufanya tathmini washiriki pia walifundishwa shughuli za Mfuko ili wao nao wawe mabalozi pindi watakaporejea kwenye vituo vyao vya kazi.

Akifunga mafunzo hayo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob. Aliushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kutoa elimu hiyo kwani itasaidia sana kuongeza uwezo wa madaktari katika kutekeleza jukumu hilo kubwa la kufanya tathmini kwa mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi.

“Nahakika katika kipindi hiki mlichokuwepo hapa mtakuwa mmejifunza mambo mengi mapya na kuwapa ujuzi ambao huenda hamkuwa nao wakati mnakuja hapa.” Alsiema Dkt. Jacob.

“Mimi toka nimeanza kufanya kazi ya udaktari nina miaka 15 lakini ukiniuliza namna gani unaweza kufanya tathmini kwa mtu aliyepata ajali maeneo ya kazi bado nilikuwa Napata shida, nilikuwa najikanyaga kanyaga sikuwa na uelewa kuhusiana na tathmini ya watu waliopata ulemavu katika maeneo ya kazi.”Alisema
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Franck Jacob, (wapili kushoto), akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki Dkt. George mwishoni mwa mafunzo hayo. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt.Abdulsalaam Omary, na Daktari bingwa na mbobezi wa magonjwa ya mifupa na viungo, Dkt. Robert Mhina ambaye ni kiongozi wa jopo la watoa mada.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi stika, Dkt.Emmanuel M. Shija, kutoka Hospitali ya Rufaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akimkabidhi stika, Bi. Rosemary K. Mbaule kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt.Abdulsalaam Omary, akitoa hotuba ya utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufunga mafunzo hayo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Frank Jacob, akitoa hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo.
Dkt. Frank Jacob, (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na Meneja wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF), Dkt. Ali Mtulia, (watatu kushoto), Dkt. Robert Mhina, (wakwanza kushoto), kiongozi wa jopo la watoa mada,na Dkt. Hussein Mwanga Mhadhiri MUHAS.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia.
Dkt. Pascal Magessa kutoka WCF, akitoa mada juu ya namna ya ulipaji Fidia.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki kutoka Dar es Salaam
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na watoa mada.

WAZIRI LUGOLA AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI IRIS YA NCHINI MALAYSIA, WAKUBALIANA KUONGEZA KASI UZALISHAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Rais wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard ya nchini Malaysia, Dato’ Paul Poh (wapili kulia) katika kikao cha kujadili uzalishaji wa kasi wa vitambulisho vya taifa nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo. Pia, viongozi hao walikubaliana kuboresha mitambo ya uzalishaji wa vitambulisho hivyo kwa wingi zaidi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anord Kihaule. Kulia Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Rais wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard ya nchini Malaysia, Dato’ Paul Poh, mara baada ya kumaliza Kikao chao kilichoshirikisha Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na viongozi mbalimbali wa Kampuni hiyo, katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati) akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard ya nchini Malaysia, Dato’ Paul Poh (wapili kulia), alipokua anafafanua jambo katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, jijini Dodoma leo. Viongozi wa kampuni hiyo wamekubaliana na viongozi wa Wizara, kufanya kazi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika kuongeza kasi ya uzalishaji wa vitambulisho hivyo. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anord Kihaule. Kulia Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akimfafanulia jambo Rais wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard ya nchini Malaysia, Dato’ Paul Poh (katikati) katika kikao cha kujadili uzalishaji wa kasi wa vitambulisho vya taifa nchini. Pia, viongozi hao walikubaliana kuboresha mitambo ya uzalishaji wa vitambulisho hivyo kwa wingi zaidi. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Shaiful Subhan.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (watatu kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Anord Kihaule (kushoto), pamoja na viongozi mbalimbali wa NIDA, wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kampuni ya Iris Corporation Berhard ya nchini Malaysia, Dato’ Paul Poh (wapili kushoto), na viongozi mbalimbali wa Kampuni hiyo, nje ya jengo la Wizara hiyo, baada ya kumaliza kikao cha kujadili uzalishaji wa vitambulisho vya taifa, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

DKT. MWANJELWA AWATAKA WAHITIMU WA TPSC KUWA WAADILIFU, WACHAPAKAZI NA WAZALENDO WANAPOTEKELEZA MAJUKUMU YAO

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wahitimu na wananchi waliohudhuria mahafali ya 30 ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Kaimu Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel Shindika akitambulisha makundi ya wahitimu wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Charles Msonde akitoa neno la utangulizi wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Baadhi ya wanafunzi bora waliohitimu Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakiwa mbele ya meza kuu mara baada ya kukabidhiwa vyeti na zawadi wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) na baadhi ya wahitimu wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wakimsikiliza mgeni rasmi, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 30 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Mtwara.


Wahitimu wa mahafali ya 30 wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) wametakiwa kuwa waadilifu, wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao kwa ajili ya maslahi ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Dkt. Mwanjelwa alipokuwa akiwatunuku vyeti wahitimu hao katika mahafali yaliyofanyika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kampasi ya Mtwara.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, waajiri wote nchini wanatambua umahiri wa utendaji kazi wa wahitimu wanaotoka Chuo cha Utumishi wa Umma, hivyo amewataka wahitimu hao kuendelea kujenga taswira nzuri ya chuo kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na weledi.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, sasa ni wakati muafaka kwa wahitimu hao kuonyesha utofauti wao kiutendaji na wahitimu wengine ambao hawakupata fursa ya kusoma Chuo cha Utumishi wa Umma.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahimiza wahitimu hao, kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa wabunifu katika utendaji kazi ili kukidhi mahitaji ya wananchi na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anaiishi kwa vitendo kaulimbiu yake ya HAPA KAZI TU.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewakumbusha wahitimu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukizwa ambayo yanahatarisha nguvu kazi yao kwani elimu na maarifa waliyoyapata yatakuwa hayana maana, iwapo watashindwa kuyatumia kutokana na matatizo ya kiafya ambayo yanaepukika. Kutokana na umuhimu wa mafunzo yanayotolewa na chuo, Mhe. Dkt. Mwanjelwa kwa msisitizo, ametoa rai kwa waajiri wote nchini kuendelea kukitumia Chuo cha Utumishi wa Umma kuwajengea uwezo watumishi wa umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi.

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametumia fursa hii, kuwaasa watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii, na amewaonya kutojenga makundi ambayo kimsingi yatakwamisha utendaji kazi na maendeleo ya chuo kwa ujumla.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Charles Msonde amesema bodi ya taaluma ilipitia kwa kina taarifa za matokeo za wahitimu wote na kujiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa, wanastahili kutunikiwa vyeti.

Dkt. Msonde amesema, waajiri mbalimbali wamethibitisha kwamba, wahitimu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania wamekuwa ni bora kiutendaji katika maeneo yao ya kazi na kuongeza kuwa, ni lengo la chuo kuwaandaa wanafunzi wote wanaopata mafunzo TPSC kuwa lulu katika soko la ajira.

Awali, Kaimu Mtendaji Mkuu na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Emmanuel Shindika amewataka wahitimu kuitumia elimu waliyoipata kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla, na amewapongeza waelekezi katika kampasi zote kwa kuwapa mafunzo bora wahitimu hao, ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa mchango wake katika kukiboresha chuo hicho.

Jumla ya wahitimu 2686 walitunukiwa vyeti vya awali, astashahada, stashahada na shahada ya uzamili katika fani za Utunzaji wa Kumbukumbu, Uhazili, Sheria, Menejimenti ya Rasilimaliwatu, TEHAMA, Utawala wa Umma, Manunuzi na Ugavi.

WAGANGA WA JADI WILAYA YA TUNDURU WACHANGAMKIA VITAMBULISHO VYA WAJASILIAMLI

$
0
0
Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuhusiana na Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala walivyochangamkia vitambulisho vya wajasiliamli vilivyotolewa na Rais Dk John Magufuri

======
Waganga 150 wa Tiba asili na Tiba mbadala   wilaya ya Tunduru,katika mkoa wa Ruvuma tayari wameshapatiwa  vitambulisho vya wajasiliamali vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuri.

Mratibu wa Tiba asili na Tiba Mbadala wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema,  idadi hiyo inaweza ikawa imeongezeka hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuwa  waganga wengi wanakata vitambulisho kwa Watendaji wa vijiji na kata.

Alisema, waganga hao wameitikia  agizo la Serikali Dkt John Magufuri ambapo  kuanzia sasa ni marufuku kwa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kufanya kazi zao bila ya kuwa na vitambulisho vya Wajasilimali na vibali vinavyotolewa na Serikali.

Alisema, Serikali inamtaka  kila Mganga kuwa na kitambulisho hicho  ili kumwezesha kufanya kazi zake kwa amani na kuwataka wale ambao wamejificha mashambani au kufanya kazi zao porini kujisalimisha haraka.

Alisema, suala la  vitambulisho vya Wajasilimali na vibali vya Serikali  halina mjadala  ni lazima wahusika wote watekeleze ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza.

Alisema, kimsingi Serikali inatambua sana kazi hizo na kusisitiza kuwa,wakati umefika kila mmoja kutekeleza na kufuata sheria bila shuruti  badala ya kusubiri hadi  kutiwa nguvuni na vyombo vya dola.

Dkt Kihongole alisema, wanaendelea na msako wa kuwatafuta Waganga ambao hawana vibali vya Serikali  popote walipo na kila atakayekutwa akifanya shughuli zake kinyume na maagizo ya Serikali atachukuliwa hatua.

Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala  kata ya Misechela Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Nampesya Kaweje alisema,mbali na vitambulisho hivyo kuwasaidia katika majukumu yao, vimewaletea heshima kubwa katika jamii ambayo hapo awali iliwaona kama wababaishaji ambao wanajipatia fedha kwa njia  ya udanganyifu.

Alisema, tangu Serikali iwapatie vitambulisho  hivyo wamekuwa na Uhuru  na amani kubwa na hata wale waliokuwa wakifanya kazi zao porini ambako sio sehemua salama  sasa wamesogea maeneo ya mjini ambako kuna mazingira rafiki na salama kwa wateja wao.

Amempongeza Rais Dkt John Magufuri kwa kazi nzuri anayofanya ya kuimarisha na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na  kutambua kazi zinazofanywa na Waganga wa Tiba asili  na Tiba Mbadala ambazo zimewafanya nao kuwa sehemu ya Wajasiliamli wanaopaswa kuchangia Uchumi wa Nchi kutokana na kipato wanachopata.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala   Bimwana Aziz, ameiomba Serikali kuandaa utaratibu ambao utawanufaisha na kupata kipato   cha kutosha kulingana na kazi wanazo fanya, kwani licha ya kutoa Tiba nzuri kwa wateja  lakini baadhi yao wamekuwa wajanja na kushindwa kutumiza ahadi wanazo ahidi mara wanapofanikiwa jambo lililo changia waganga wengi kubaki maskini.

“tunaiomba Serikali itusaidie kuweka utaratibu mzuri ambao utatuwezesha na sisi kunufaika na jasho letu,kwa muda mrefu tunafanya kazi ya kuwasaidia watu ambao wanakwenda kunufika na kutajirika kutokana na Tiba na maombi yetu lakini sisi waganga tuna hali ngumu sana ya maisha”alisema Bimwana.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Liwanga Dau Nguche alisema,wameanza kutekeleza agizo la Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera linalokaza Waganga wa Tiba asili wenye vitambulisho vya wajasilimali kutozwa fedha.

Dkt. Kalemani aagiza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Geita uanze mwezi wa Sita

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha Mnadani wilayani Sengerema, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole.

Na Teresia Mhagama, Geita

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amemwagiza mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme wilayani Geita, kuanza ujenzi wa kituo hicho mwezi wa Sita  mwaka huu na kumaliza kazi hiyo mwezi wa Tano mwakani ili kuboresha hali ya umeme mkoani Geita.

Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya umeme inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Mwanza na Geita ambapo alikagua kazi ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme wilayani Geita na mradi wa usambazaji umeme vijijini  wilayani Sengerema na Chato.

"Msisubiri kusukumwa, jitumeni wenyewe ili mradi huu ukamilike mapema, na wananchi wapate umeme usiokatika mara kwa mara,  pia kukamilika kwa kituo hiki kutawezesha mgodi wa dhahabu wa Geita kuunganishwa na umeme wa gridi, kwani sasa wanatumia umeme wa mafuta ambao ni wa gharama kubwa." alisema Dkt Kalemani.

Alisema kuwa, kituo cha kupoza umeme cha Geita ni moja ya kazi zinazotekelezwa kupitia  mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kV 220  yenye urefu wa kilometa 55   kutoka Bulyanhulu hadi Geita ambao pia unahusisha upanuzi wa kituo cha kupoza umeme Bulyanhulu, usambazaji umeme katika vijiji 10 vinavyopitiwa na mradi na kubadilisha mita za umeme za kawaida 1500 mkoani Geita.

Aliongeza kuwa, mkandarasi anayejenga kituo cha kupoza umeme cha Geita pamoja na njia ya kusafirisha umeme ni kampuni ya CAMC kutoka China huku mkandarasi atakayesambaza umeme kwenye vijiji vinavyopitiwa na mradi ni kampuni ya STEG na kwamba gharama ya mradi mzima ni Dola za Marekani milioni 23.

Akiwa wilayani Sengerema, Waziri wa Nishati, aliwasha umeme katika Kijiji cha Mnadani na  Nyakato na kutoa Siku Saba kwa mkandarasi kampuni ya NIPO kusambaza umeme katika vijiji vyote vya Kata ya Tabaruka.

Dkt Kalemani alisema kuwa, Mkoa wa Mwanza umetengewa jumla ya shilingi bilioni 30 kwa ajili ya mradi wa usambazaji umeme vijijini unaoendelea na unatarajiwa kukamilika Juni mwaka 2020.

Akiwa wilayani Chato, Waziri wa Nishati, aliwasha umeme katika Kijiji cha Mulanda na Maweni ambapo aliwahamasisha wananchi kulipa shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe umeme huo utakaowawezesha kufanya shughuli  mbalimbali za maendeleo.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria kuanza kuwaka kwa umeme katika Kijiji cha Mulanda wilayani Chato. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Eng. Mtemi Msafiri Semeon.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kushoto) akimpongeza mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Nyakato wilayani Sengerema ambaye nyumba yake imeunganishiwa umeme kupitia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (kulia) akitoa maagizo mara baada ya kukagua eneo kutakapojengwa kituo cha kupoza umeme wilayani Geita. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO, Kanda ya Ziwa, Mcneal Mbonile.
Watendaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na mkandarasi wa umeme vijijini kutoka kampuni ya NIPO, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nyakato wilayani Sengerema.

Taswa FC kuanza na Rangers Ndondo Cup Mei 14

$
0
0
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) itaanza kampeni ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Ndondo Cup 2019  kesho (Jumanne Mei 14) kwa kupambana na timu ya Rangers.

Mchezo huo umepangwan kufanyika kwenye uwanja wa  Mwalimu Nyerere Mwembe Chai kuanzia saa 10.00 jioni.

Taswa FC ambayo inafanya mazoezi mara moja kwa wiki (Jumamosi)  itakuwa inashiriki kwa mara ya kwanza, ipo katika kundi D pamoja na timu za Ukwamani na Goba Kombaini.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa wamejiandaa vyema katika mchezo chini ya makocha wao, Ibrahim Masoud ‘Maestro’ na Saidi Seif.

Majuto alisema kuwa wanajua watapata ushindani mkali kutoka kwa timu ya Rangers, lakini hilo halitazuia kuibuka na ushindi.

Alisema kuwa kila mechi inakuwa na ushindani, lakini si kwa timu za kundi D na kuahidi kufanya vyema katika mechi zao zote.

“Tupo katika mashindano na wapinzani wetu pia wapo katika mashindano. Watashindana, lakini hawatashinda, tupo vizuri katika kila idara na malengo yetu ni kuonyesha kuwa hata waandishi wa habari nao wanaweza kucheza mbali ya kufanya kazi ya kuelimisha jamii,” alisema Majuto.

Alisema kuwa waandaaji wa mashindano ya Ndondo Cup 2019 hawakukosea kuwakubalia kushindana katika mashindano hayo ambayo mpaka sasa yamechangia kiasi kikubwa maendeleo ya soka hapa nchini.

“Nawapongeza waandaji kwa kuwa na mashindano ya soka yenye mvuto wa aina yake na kuhamasisha maendeleo ya soka,

Kuna vijana ambao wametokea katika mashindano haya na sasa wanatesa katika timu za madaraja ya juu, pia kuna wachezaji wamepata fursa ya kufanya majaribio nchi za Ulaya, hii nifaraja kubwa sana kwetu,” alisema.

 Alisema kuwa wanaamini hata Taswa FC itatoa wachezaji ambao watacheza timu kubwa mbali ya kuwa ni wana- habari.

HALMASHAURI TUNDURU YAAGIZA KUFUATILIA UTENDAJI WA WATUMISHI WAKE

$
0
0
Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole akiongea na wazazi wa kijiji cha Mchuluka kata ya Mchuluka wakati wa zoezi la uchunguzi wa vimelea vya ugonjwa Kifua kikuu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ikiwa ni kampeni ya wilaya hiyo kutokomeza ugonjwa huo.

====

Serikali   wilayani Tunduru,imewaagiza viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru kuwafuatilia  kwa karibu  watumishi wake  juu ya utendaji wao ili kubaini kama kweli wanawajibika  katika kuwatumikia Wananchi.

Agizo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera ,  katika kikao chake na  wanawake wa kijiji cha Mchuluka waliokusanyika katika Zahanati ya kijiji hicho wakipata huduma ya Kliniki.

Pia Mkuu wa wilaya alizindua  zoezi la uchunguzi wa ugonjwa wa  kifua kikuu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano iliyoendeshwa na kitengo cha kifua kikuu  Hospitali ya wilaya ya Tunduru ikiongozwa na Dkt Mkasange Kihongole.

Alisema, lengo la Serikali ni  kuona watumishi  wa umma wanakwenda vijijini kwa wananchi ili kusikiliza na kutatua kero zao.

Homera alisema,ni vema watumishi watumishi wa Umma  kila mara kutenga muda kwa ajili ya kutembelea wananchi kwa ajili ya kutatua kero zao, badala ya kutumia muda mwingi kukaa ofisini jambo linalolalamikiwa  sana na wananchi ambao bado wanakabiliwa na changamoto nyingi za maisha hususani kwenye upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii.

Alisema,Serikali haitakuwa na msalie mtume kwa watumishi wazembe na wale wanaofanya kazi kwa mazoea kwani itahakikisha inachukua hatua pale wanaposhindwa kuleta ufanisi sehemu za kazi.

Homera alisema, baadhi ya watendaji wa Serikali kuanzia ngazi ya  vijiji hadi wilaya wameshindwa kutumia nafasi zao ikiwemo  kutatua kero za wananchi, badala yake wanasubiri hadi viongozi wa wilaya na mkoa wafike jambo ambalo limezidisha  kuongezeka kwa matatizo katika jamii.

Homera,amewataka wazazi kuhakikisha wanapeka watoto wao kliniki kwa ajili ya uchunguzi Afya  za watoto wao na kujiepusha tabia ya kuwapa Dawa bila kupata vipimo vya Daktari.

Alisema,Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuboresha Sekta ya Afya kwa kujenga Zahanati,vituo vya Afya,Hospitali,vifaa Tiba na kuajiri watumishi, na hayo yanafanyika kama mpango wa kupunguza vifo vitokanavyo na ukosefu wa Huduma za Matibabu.

Mkuu wa wilaya,ameonya tabia ya wanawake wa wilaya hiyo kuzaa katika umri mdogo ili kuepuka matatizo wakati wa kujifungua ambayo imekuwa chanzo cha  kuongezeka kwa vifo kwa akina mama.

Alisema, wilaya ya Tunduru imekuwa kwenye wakati mgumu hasa kwa wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo chini ya miaka 16  kutokana na mila na Tamaduni na kupiga marufuku ngoma za usiku ambazo zinachangia sana wasichana wadogo kubakwa na kutiwa mimba.

Mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema,Serikali kwa kushirikiana na jamii inayo wajibu wa kuzuia mambukizi ya ugonjwa  wa Kifua kikuu kwa watoto chini ya umri wa miaka 5 kwa kuvuta Sigara,Tumbaku, na hata Bangi akiwa amemshika mtoto.

Alisema,ugonjwa wa Kifua kikuu licha ya kusababisha vifo lakini pindi mtoto anapougua hata mzazi anakosa muda wa kufanya kazi za  kiuchumi ikiwemo kwenda shambani hivyo kuchangia umaskini katika ngazi ya familia.

Amewataka wanawake wajawazito kuwa na mazoea ya kwenda Kliniki mara kwa mara kwa ajili ya kupata ushauri wa kitaalam  na kuhakikisha wanajifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma ili kuokoa maisha yao.

WACHEZA WA KARATE TANZANIA WAIBUKA KIDEDEA KATIKA MASHINDANO YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0

Na Mwandishi Wetu
WACHEZAJI  karate wa Tanzania, Mikidadi Kilindo na Elisiana Katani wameibuka washindi wa mashindano ya kata kwa upande wa wanaume na wanawake katika mashindano ya Afrika ya Mashariki na Kati yaliyomalizika jijini Kampala, nchini Uganda hivi karibuni.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la JKA Tanzania, Fedeliko Nestory amewasifu wachezaji hao kwa kushinda medal hizo, sio kwa wao binafsi, bali kwa nchi pia.


Kilindo, mwenye dani 4 ( maarufu Ganchan) ambaye pia ni Mkufunzi Mkuu msaidizi wa JKA/Tanzania, ameshinda medali ya dhahabu, baada ya kuwashinda washiriki wengine kutoka nchi zaidi ya 10 zilizoshiriki katika upande wa kata (kuonyesha maarifa ya kupigana) kwa upande wa wanaume. Hii ni mara ya tano kwa Ganchan kushinda taji hili.

Pia ni mara ya kwanza kwa kushinda taji hili, akiwa miongoni mwa wanawake wachache wanaocheza mchezo huu hapa nchini.

Katani, ambaye pia ni mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utoaji taarifa kwa Umma wa JKA/World Federation-Tanzania, ameshinda medali ya fedha , baada ya kushinda nafasi ya pili katika upande wa wanawake.

“Tunashukuru Mungu tumeshinda medali, tunaomba wadau wasaidie kuukuza mchezo huu hapa nchini,” wamesema Kilindo na Katani kutokea Kampala, kupitia ukurasa wa Facebook wa JKA/WorldFederation-Tanzania. 

Nestory amesema wawakilishi hao wameipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa, huku akiomba serikali, mashirika ya umma, makampuni na watu binafsi kusaidia katika ukuaji na ushiriki wa mchezo huo katika michuano ya kimataifa.




















“Tuna mashindano mengi katika kalenda yetu yam waka, hivyo tunaomba wadau watusaidie,”

Amesema kuanzia July 1-7, Tanzania itakuwa mwenyeji wa semina ya ya Gasshuku na Mashindano ya kimataifa ambapo nchi 15, ikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Angola, Botswana, Madagascar, Zimbabwe, Jamhuri ya Kongo na Afrika ya Kusini zimethibitisha ushiriki.

Miongoni mwa michuano mikubwa ambayo JKA Tanzania inategemewa kushiriki ni michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani mjini Tokyo, Japan, huku mchezo huo ukiwa miongoni mwa michezo shiriki kwa mara ya kwanza.


ASKOFU NKWANDE AKEMEA UCHAWI, USHOGA NA UTOAJI MIMBA

$
0
0
* Asema ni ushamba wa elimu, ni uuaji, ni dhambi              
ASKOFU MKUU wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhasahamu Renatus Nkwande anasikitika kila anaposikia watu wanaongelea mambo ya uchawi na kusema kwamba huo ni usahamba wa elimu.

“Mtu akivimba tumbo unasema amelogwa na tena unamtaja na fulani ndiye mchawi. Huo ni ushamba wa elimu na tena huko ni kukosa imani na kushindwa kumuamini Mwenyezi Mungu,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Mei 12, 2019) wakati akitoa shukrani kwenye ibada ya kumsimika kuwa Askofu Mkuu wa jimbo hilo iliyofanyika kwenye viwanja wa Kawekamo jijini Mwanza.

“Watu wetu wana hofu mbalimbali ambazo zimewakamata tangu utoto wao. Tuwasaidie waumini hawa ili wamwamini Mungu kwamba anaokoa na anaweza kuwaponya madhila waliyonayo. Tuwasaidie watu wetu wajikomboe kielimu, wajiendeleze kwenye masomo ya fizikia, kemia na kadhalika,” amesema.

Amesema anashangaa tabia ya Waafrika ya kupenda kuiga mambo ya ajabu kwa vile tu yameletwa na wazungu. “Sisi Waafrika ni watu wa ajabu tunaiga vitu visivyo na msingi. Wameleta ushoga, tunaiga! Wameleta utoaji mimba, tunaiga. Leo hii kuna taasisi zinasambaza hata vifaa vya kutolea mimba, nasi tumekaa tunaangalia tu.”

“Wazee wetu walipoona wamechoka ukoloni, walipigana ili kupata uhuru. Leo na sisi tupiganie uhuru kwa kukataa masuala ya ushoga na utoaji mimba. Huo ni uuaji, hiyo ni dhambi. Miongoni mwetu leo wapatikane watu wa kusimamia hayo ili ukoloni huu usiendelee kutawala akili za watu wetu,” amesema.

Amewaomba Watanzania wamuombe Mungu awabariki, alibariki Taifa la Tanzania ili yanayofanyika yawasaidie kwenda mbinguni.

Pia ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo na hatimaye kuwatoa kwenye umaskini. “Tunaamini yote anayofanya ni kwa manufaa ya Watanzania wote,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Magufuli na mamia ya waumini na viongozi waliohudhuria ibada hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema anatambua kuwa kuwaongoza watu kiroho na kimwili ni jambo lenye uzito mkubwa. Na kwamba uteuzi wake unadhihirisha kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya katika kumtumikia Bwana.

“Sisi viongozi na waumini kwa kutambua kazi nzuri uliyoifanya hadi kufikia kupata wadhifa huo tuna imani utaweza. Nakuomba upokee mzigo huo kwa matumaini na bila kusita kwani waumini wa kanisa hili wako pamoja nawe na viongozi wenzako wote tunategemea watatoa ushirikiano kwako. Tunachosema ni kwamba, jipe moyo kwa kuzingatia yaliyoandikwa katika Wafilipi 4:13 kwamba “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”. Jitwishe mzigo huo kwa imani na utaubeba bila kuchoka, sisi sote tuko pamoja nawe,” amesema.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kusisitiza suala la kutunza amani ya nchi na akawaataka viongozi wa dini na waumini kote nchini kuendeleza upendom hurma na kuwa na roho ya msamaha. “Tuhurumiane sasabu sisi si wakamilifu, kwa hiyo tuongeze msamaha miongoni mwetu,” amesisitiza.

“Nawaombeni wote, tuendelee kutumia nyumba zetu za ibada kuliombea Taifa hili ili tuendelee kuishi kwa amani, upendo na mshikamano. Tuepuke migogoro ya mara kwa mara katika nyumba zetu za ibada. Tuendelee kujenga waumini wetu wakue kiroho na kujenga dhana ya umoja na upendo katika Taifa letu. Watu wa Mungu ni watu wa upendo, watu wa Mungu ni watu wa amani, watu wa Mungu ni watu wa kiroho.”

Mapema, akitoa salamu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Rais wa TEC, Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga aliwataka waumini wa kanda ya ziwa wawe na mshikamano na wampe ushirikiano Askofu Mkuu Nkwande.

“Kuweni na upendo kama Bwana Yesu alivyofundisha na pia ombeeni utumishi mwema kwa viongozi wote wa Serikali na watumishi wote wenye jukumu la kuongoza watu.”

Askofu Nyaisonga aliishukuru Serikali kwa kulipa nafasi Kanisa Katoliki ya kushirikiana na Serikali kutoa huduma za jamii kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini hususani katika sekta ya elimu na afya.

“TEC inapenda kuhimiza mshikamano baina ya Serikali na kanisa ili kuwe na ufanisi wa huduma tunazotoa za kumlinda mama na mtoto na kijana. Ufanisi huu utapatikana kwa kuimarisha miundombinu hasa katika ngazi za chini,” alisema.

Waziri Mkuu ameondoka jijini Mwanza mchana huu kuelekea Arusha kupokea kundi la watalii zaidi ya 200 kutoka China ambao wanatarajiwa kuwasili leo jioni.

 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akipokelewa na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Gervas Nyaisonga wakati akiwasili kwenye sherehe za kumsimika Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akimpongeza Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, baada ya kusimikwa rasmi, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, akitoa neno la shukrani, baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo hilo, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na waumini waliohudhuria ibada ya kumsimika Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, baada ya kusimikwa rasmi, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akitoa sadaka wakati wa ibada ya kumsimika Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, akiwa ametulia baada ya kusimikwa kuwa Askofu wa Jimbo hilo, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa, akiwaaga wananchi na waumini, mara baada ya ibada ya kumsimika Askofu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Mhashamu Renatus Nkwande, katika viwanja vya Kawekamo, Mei 12.2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

NHIF KIGOMA YAHAMASISHA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU NA MFUKO WA FAO LA USHIRIKA AFYA.

$
0
0
Na Editha Karlo wa Michuzi TV, Uvinza.  
MKUU wa wilaya ya Uvinza Mwanamvua Hoza, amewataka wakulima wadogo wadogo kuchangamkia fursa ya kujiunga na mfuko wa fao la ushirika afya kutoka mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF), kwani wametambua umuhimu wa uwepo wao katika vyama vya ushirika.

Akizungumza leo na wakulima wa zao la tumbaku  katika kijiji cha Basanza wilayani uvinza mkoani Kigoma Mwamvua zao la tumbaku ni moja ya zao la kimkakati nchini na kwamba ni muhimu kuliboresha pamoja na wakulima wake. 

" Nichukue fursa hii kuwahamasisha wakulima kujiunga na mfuko huo kwani ugonjwa ukija hautoi taarifa ni muhimu kila mmoja wetu akawa na kadi ya bima ya afya yeye na familia yake," amesema Hoza.

Aidha Mkuu wa wilaya huyo amewataka wananchi kuuza mazao yao baada ya kuvuna na  kuhakikisha wanaweka na akiba ya chakula Kwani serikali haitampatia mtu chakula kwa kufanya uzembe kama huo. 

Mkulima Mwajabu Hassan ameiyomba serikali kupitia mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF), kupunguza kiwango cha fedha cha kulipia katika mfuko huo.

"Tunaomba serikali yetu kutusikia sisi wanakijiji cha Basanza wakapunguza kiwango kutoka Sh 76,800 hadi Sh 38,400 ili kila mmoja aweze kupata matibabu, "amesema Hassan.

Mkulima wa tumbaku Beatrice Musule amesema, amesema wakulima hawawezi kumudu gharama hizo kutokana na wakati mwingine wanakosa mavuno kwasababu ya wadudu wanaoharibu  mazao yao. 

"Afya ni jambo nzuri na wametuletea wakati mzuri lakini tunaomba serikali yetu sikivu ituangalie sisi wakulima wadogo wa tumbaku iweze kupunguza kiwango ili tuingie na familia zetu," amesema Masule. 

Naye Michael Stephano amesema ni vema wakaliangalia jambo hili kwa mara ya pili na kuwaruhusu kulipia taratibu kwa awamu nne kutokana na umuhimu wa jambo la afya. 

" Tutalipa kiasi hicho lakini tunaomba watuwekee utaratibu wa kulipa kwa awamu au watupunguzie kiwango kila mmoja anatamani kujiunga lakini tunashindwa," amesema Stephano. 

Meneja wa NHIF mkoa wa Kigoma Benard Katerengabo, amesema wataendelea kutoa elimu kwa wakulima na vyama vya ushirika mkoani humo lengo likiwa ni kila mkulima aweze kunufaika na matibabu yeye pamoja na familia yake.

Amesema baada ya kuwapa elimu wanaushirika wa vyama vya ushirika  Basanza, wametoa maoni yao pamoja na kukatwa kiasi hicho cha fedha kwa wanachama wakati wa kipindi cha mavuno kwa kutambua umuhimu wa matibabu. 
 Meneja wa mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF), mkoani Kigoma Benard Katerengabo akizungumza na wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha Basanza wilayani Uvinza(hawapo pichani) akitoa elimu kuhusiana na kujiunga na mfuko wa fao la ushirika afya.
 Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mrindoko akiwahamasisha wakulima wa zao la tumbaku katika kijiji cha Basanza kujiunga na fao la ushirika la afya ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao pamoja na familia zao.

Baadhi ya wakulima wa zao la Tumbaku katika kijiji cha Basanza Wilayani Uvinza wakisikiliza elimu ya kujiunga na fao la ushirika kupitia mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)

Wauguzi, wakunga wakumbushwa kuzingatia maadili ya kazi

$
0
0
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwaapisha wauguzi na wakunga kwenye maadhimisho ya Siku ya Uuguzi na Ukunga Duniani ambayo hufanyika Mei 12, kila mwaka. Leo wauguzi wameapishwa kukumbushwa kutoa huduma kwa kuzingatia kanuni na taratibu kama walivyojifunza. Wengine kushoto ni viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na viongozi wa Chama cha Uuguzi na Ukunga Tanzania (TANNA) wakishiriki katika shughuli ya kuwaapisha wauguzi leo.

Wauguzi wametakiwa kuendelea kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kitaaluma kwa lengo la kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa.

Wito huo umetolewa leo na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa katika maadhimisho ya siku ya Uuguzi na Ukunga Duniani ambayo yamefanyika Hopistali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kuudhuriwa na wauguzi na wakunga wa MNH na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).     

Maadhimisho hayo hufanyika Mei 12, kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wauguzi Sauti inayoongoza Afya kwa Wote.” Mwaka huu kitaifa maadhimisho yanafanyika mkoani Katavi.

Bi. Mtawa amewakumbusha wauguzi kuzingatia mafunzo yanayotolewa mahala pa kazi kwani ndio yanayochochea kutoa huduma bora ya afya kwa wagonjwa.

Amewataka wauguzi kutambua kwamba huduma wanayotoa kwa wagonjwa ni huduma ya kibinadamu kwani elimu inachangia kufikia malengo ya kutoa huduma bora.

“Hivi sasa mambo yetu yanakwenda vizuri. Malalamiko mengi yamepungua kwani ukifuatilia utabaini kwamba malalamiko mengi ni ya wagonjwa au mgonjwa kutaka kupewa kipaumbele kupata huduma ya afya badala ya kufuata utaratibu,” amesema Bi. Mtawa.

Pia, Msajili amewapongeza wauguzi kwa kutekeleza majukumu ya kutoa huduma za afya kwa kuzingatia taratibu za kitaaluma kwa asilimia 100.

Akisoma risala katika maadhimishisho, Katibu wa Chama cha Uuguzi na Ukunga Tanzania, tawi la Muhimbili, Bw. Seif Hamisi ameomba vitendo vya udhalilishaji kwa wauguzi vifanyiwe kazi kwa kuwa vitendo hivyo vinawapunguzia ari ya kufanya kazi.

Kupitia risala, Katibu ameishukuru Muhimbili kwa kuwapatia wauguzi mafunzo mbalimbali ambayo yamewasaidia kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani amewataka wauguzi kutoa taarifa kwa uongozi wa MNH endapo watadhalilishwa wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku ili watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria.

“Mmesikia jamani nendeni mkawaeleze wenzenu kwamba endapo muuguzi atadhalilishwa, bila kuchelewa naomba atoe taarifa kwa uongozi ili wanaofanya hivyo tuwafikishe mbele  ya vyombo vya dola,” amesema Bw. Makani.
Baadhi ya wauguzi wakishiriki kuapa katika maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani ambayo hufanyika Mei 12, kila mwaka.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Bw. Makwaia Makani akizungumza na wauguzi leo katika maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani.
Waauguzi na wakunga wakimsikiliza Bw. Makani wakati alipokuwa akizungumza nao leo.
Mmoja wa washiriki, Bi. Mwanahamisi Mvimba akiwasilisha mada kuhusu ‘Sababu zinazochangia maambukizi kwenye vidonda kwa watoto walioungua moto’.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Bi. Redemptha Matindi akishiriki kuwasha mshumaa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya uuguzi na ukunga duniani.
Mshiriki, Bi. Sofia Sanga akitoa mada kuhusu wauguzi kuzingatia taratibu na maadili wakati wa kuwahudumia wagonjwa.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwa katika picha ya pamoja na wauguzi na wakunga kwenye maadhimisho ya siku ya uuguzi na ukunga duniani.

VETA Kihonda yatoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa zaidi ya 1500

$
0
0
Chuo cha VETA Kihonda kimetoa mafunzo kwa madereva wa magari makubwa  zaidi ya 1500 kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari mwaka huu lengo likiwa ni kupunguza ajali ambazo zinatokana na makosa ya kibinadamu.

Chuo cha VETA Kihonda  ni  Chuo ambacho kimebobea katika utoaji wa mafunzo ya udereva magari makubwa ambapo madereva wa magari makubwa wanatakiwa kupata mafunzo hayo hapo au vyuo vingine vilivyosajiliwa vikiwa na mafunzo hayo.

Mwalimu wa Udereva wa Magari Makubwa na Mabasi wa chuo cha VETA Kihonda William Munuo amesema kuwa madereva wengi wanajua kuendesha kwa kunyoosha katika barabara lakini kurudi nyuma ni tatizo ambapo wengi ndio wanasababisha ajali au kuangusha magari hayo na kuleta hasara kwa makampuni.

Munuo amesema mafunzo waliyoyaanza ni endelevu na kutaka madereva kuzingatia mafunzo hayo na kuyaishi katika kuendesha na hatimaye watakuwa madereva bora.

Munuo amesema mafunzo hayo yanafanya magari makubwa kuishi muda mrefu kutokana  na wakati mwingine yanapata ubovu kwa uendeshaji usiofuata utaratibu wa uendeshaji wa magari hayo.

Amesema kuwa licha ya kuwa na leseni madereva wa magari makubwa wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara kutokana na teknolojia za magari kubadilika kila mara.

Aidha amesema katika mafunzo ya vitendo baadhi wanajua kuendesha magari makubwa ya tela moja wengine ni wale wa tela mbili ambapo wanaweza wote kuendesha lakini wakiwekwa katika urudishaji gari hizo nyuma kuna changamoto hivyo changamoto hizo zinatatuliwa kwa kuwapa mafunzo.

"Hatuwezi kuwaacha watu waendelee kuendesha magari makubwa katika ujuzi wa mazoea lazima wapate mafunzo bora ya kuweza kuwa madereva bora na sio bora madereva"amesema Munuo.

Munuo ameyataka  makampuni kuhakikisha madereva wao wanapata mafunzo kila mara kwa faida ya kampuni hizo na kusaidia utunzaji wa magari hayo.
 Mkufuzi wa Magari Makubwa na Mabasi wa Chuo cha VETA Kihonda William Munuo akitoa maelezo wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa madereva wa kampuni ya MeTL jijini Dar es Salaam.
 Dereva akiwa katika mafunzo  ya vitendo ya kurudusha gari nyuma wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa madereva wa kampuni ya MeTL jijini Dar es Salaam.
 Dereva akienda kuweka kifaa kwa ajili ya usalama wakati wa kuunga tera
 Dereva akiangalia namna ya kuunga tera mara baada ya kupata mafunzo ya Nadharia
 Alama zilizotumika katika mafunzo ya vitendo ya kurudisha gari nyuma.
 Wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja na madereva wa magari makubwa katika kampuni ya MeTL.
Mkaguzi wa Kikosi cha Polisi wa  Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja madereva wa MeTL mara kufungua mafunzo.

KAMPUNI YA PUMA ENERGY TANZANIA YAWAKUMBUSHA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI KUEPUKA AJALI

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhana(aliyevaa kofia nyekundu) akitoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva waliofika kujaza mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Puma jijini Dar es Salaam.Puma imeungana na Shirika la Umoja wa Mataifa kuadhimisha Wiki ya nenda kwa Usalama. Wengine waliokuwa wakitoa elimu hiyo ni wanafunzi wa Shule ya mzingi ambao ni mabalozi wa usalama barabarani.

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma  Energy Tanzania imeungana na Shirika la Umoja wa Mataifa kuadhimisha wiki ya usalama barabarani huku kampuni hiyo ikitoa mwito kwa madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabara kwa lengo la kuokoa maisha ya ya watoto.

Kwa mujibu wa Kampuni ya Puma ni kwamba moja ya vipaumbele vyao ni suala zima la usalama barabarani na ndio maana imeona umuhimu wa kuungana na shirika hilo kubwa duniani kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa elimu kwa madereva wa vyombo vya moto nchini Tanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah amewaambia waandishi wa habari kuwa wameamua kuitumia siku hiyo kutoa elimu kwa madareva ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya kimataifa ya nenda kwa usalama barabarani 'UN-Global Road Safety Week (UNGRSW).'

"Puma tumeungana na shiriki hili kutoa elimu ambapo kwetu hapa Tanzania ambacho tumekifanya elimu ya usalama barabarani imetoa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge ambao ni mabalozi wa elimu ya usalama barabarani hususani kwa mkoa wa Dar es Salaam.

"Pia tumeamua kuwatumia watoto kutoa elimu ya usalama barabarani lengo letu Puma ni  kuhakikisha wanaanza kupata uelewa kuhusu masuala ya usalama barabarani. Tupo nao leo kwa sababu hawa ni mabalozi wetu,"amesema Dhanah.

Dhanah amesema kampuni ya Puma Energy itaendelea kushirikiana na taasisi zitakazoendesha mipango mbalimbali ya usalama barabarani kwa lengo la kuhakikisha kuwa watu na vyombo wanavyotumia barabarani wanakuwa salama.

Awali Meneja Programu ya usalama barabarani kutoka Shirika la Neema Swai amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Sema Usikike, Okoa Maisha' na kufafanua maadhimisho hayo huadhimishwa kila baada ya miaka miwili.

"Kila siku watoto ndio wanaotumia barabara kwenda shule na kurudi nyumbani, wasipokuwa na elimu ya kutosha tutawapoteza wengi.

"Mtambue, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), watoto wenye umri kati ya miaka mitano hadi 29, wanapoteza maisha kwa wingi kutokana na ajali, si Malaria wala ugonjwa mwingine ni ajali," amesema Swai.

Amebainisha Serikali inatumia gharama kubwa kumtunza mtoto kunzia miaka 0-5 halafu anakuja kufa kwa ajali ya barabarani kutokana na uzembe wa madereva au kukosa elimu y usalama barabarani, hilo wamelikata na ndio maana wanasema wameamua kupaza sauti.

Mmoja wa wanafunzi walioshiriki kutoa elimu, Godbless Mlacha anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Bunge, amesema wanawashauri  maderva kuacha kutumia vilevi au kwenda mwendo kasi wakiwa barabarani kwa kuwa maisha yao yanakua hatarini.

"Nahitaji kuishi ili nitimize ndoto zangu, uzembe wa dereva unaweza kuondoa uhai wangu au kunipa kilema cha kidumu. Nimechagua kupaza sauti ili kumaliza hili tatizo," amesema Mlacha.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imeazimia kushirikiana na taasisi nyingine zitakazoendesha mipango mbalimbali ya usalama barabarani kwa lengo la kuhakikisha watu na vyombo wanavyotumia barabarani wanakua salama.

Wakati huo huo baadhi ya madereva ambao wamepata elimu hiyo ya usalama barabarani, wametoa pongezi kwa Kampuni ya Puma kwa jitihada ambazo inachukua kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu elimu ya usalama barabarani.

Wamesema elimu hiyo ambayo inatolewa kupitia wanafunzi ambao ni mabalozi wa usalama barabarani imewahamasisha kuzingatia sheria kwani faida zake ni nyingi ikiwemo ya usalama wa dereva mwenyewe lakini wakati huo huo kuepuka ajali ambazo zinatokana na kutozingatiwa kwa sheria za usalama barabarani.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhana akifafanua jambo kwa moja ya madereva kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria ya usalama barabarani kwa lengo la kupunguza ajali nchini.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam ambao ni mabalozi wa usalama barabarani wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa dereva aliyefika kujaza mafuta katika kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijini.Utolewaji wa elimu hiyo unafanywa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania.
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge ambao ni mabalozi wa usalama barabarani wakitoa elimu ya usalama barabarani kwa mmoja wa madereva aliyefika kujaza mafuta kituo cha mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijii Dar es Salaam
 Meneja Programu wa  Usalama Barabarani kutoka Shirika la Amend Neema Swai akielezea ujumbe wa usalama barabarani uliopo kwenye madaftari ya shule ambao unalenga kuwakumbusha wanafunzi na wananchi kwa ujumla kuheshimu sheria za usalama barabarani.
 Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam ambaye ni balozi wa usalama barabarani akitoa elimu hiyo kwa dereva taksi.
Dereva bodaboda akipata elimu ya usalama barabarani kutoka kwa wanafunzi wa shule ya msingi ambao ni mabalozi wa usalama barabarani ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya nenda kwa usalama ya Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania imeungana na shirika hilo kuadhimisha wiki hiyo jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUCHIKA AFUNGUA WARSHA KUHUSU HALI YA UTEKELEZAJI WA MKATABA WA KIMATAIFA WA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA JIJINI DODOMA

$
0
0
 Mwenyekiti Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Cpt. George Mkuchika akifungua warsha kuhusu hali ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), CP Diwani Athumani akiwasilisha maada mbele ya Wajumbe Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC) kuhusu hali ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Wajumbe Chama cha Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Rushwa (APNAC) wakiwa katika warsha kuhusu hali ya utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Mapambano dhidi ya Rushwa kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. SHEIN AJUMUIKA NA WANANCHI WA KIBELE KATIKA FUTARI NYUMBANI KWAKE

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Ali Mohameed Shein, akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja katika futari iliofanyika nyumbani kwake Kibele Unguja, kushoto Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Wananchi wakihudhuria futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, nyumbani kwake Kibele Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.(Picha na Ikulu)
 WANANCHI wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja wakijumuika katika Futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, nyumbani kwake Kibele Zanzibar Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
 WANANCHI wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja wakijumuika katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein nyumbani kwake Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja katika futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, iliofanyika nyumbani kwake Kibele, kushoto Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Balozi na Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi Salama Aboud Talib na kulia Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Dkt. Sira Ubwa.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia Dua, ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleoh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari iliofanyika Kibele Wilaya ya Kati Unguja, kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia Dua, baada ya kumalizika hafla ya futari, ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar kushoto Sheikh Saleh Omar Kabi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na kulia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid.(Picha na Ikulu)
 Mohamed Ali Mohamed akitowa neno la shukrani kwa niaba ya Familia ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk,Ali Mohamed Shein, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari ilioandaliwa kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibele Wilaya ya Kati Unguja nyumbani kwake Kibele.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kuagana na Waziri Asiyekuwa na Wizara Maalum Mhe. Soud Said Soud, baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliofanyika nyumbani kwake Kibele Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia Mtoto Sleyum Khamis mkaazi wa Kibele Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kumalizikwa kwa Futari aaliuowaandalia Wananchi wa Kibele iliofanyika nyumbani kwake Kibele Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na kuagana na Wananchi wa Kijiji cha Kibele, baada ya kumalizika kwa Futari ilioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekitri wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, nyumbani kwake Kibele Wilaya ya Kati Unguja.(Picha na Ikulu)

WAGANGA WA JADI WILAYA YA TUNDURU WACHANGAMKIA VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI

$
0
0
Waganga 150 wa Tibaasili na Tibambadala   wilaya ya Tunduru,katika mkoa wa Ruvuma tayari wameshapatiwa  vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais Dkt John Magufuli.

Mratibu wa Tiba asili na Tiba Mbadala wa wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole alisema,  idadi hiyo inaweza ikawa imeongezeka hadi kufikia mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kuwa  waganga wengi wanakata vitambulisho kwa Watendaji wa vijiji na kata.

Alisema, waganga hao wameitikia  agizo la Serikali Dkt John Magufuli ambapo  kuanzia sasa ni marufuku kwa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kufanya kazi zao bila ya kuwa na vitambulisho vya Wajasiriamali na vibali vinavyotolewa na Serikali.

Alisema, Serikali inamtaka  kila Mganga kuwa na kitambulisho hicho  ili kumwezesha kufanya kazi zake kwa amani na kuwataka wale ambao wamejificha mashambani au kufanya kazi zao porini kujisalimisha haraka.

Alisema, suala la  vitambulisho vya Wajasiriamali na vibali vya Serikali  halina mjadala  ni lazima wahusika wote watekeleze ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza.

Alisema, kimsingi Serikali inatambua sana kazi hizo na kusisitiza kuwa,wakati umefika kila mmoja kutekeleza na kufuata sheria bila shuruti  badala ya kusubiri hadi  kutiwa nguvuni na vyombo vya dola.

Dkt Kihongole alisema, wanaendelea na msako wa kuwatafuta Waganga ambao hawana vibali vya Serikali  popote walipo na kila atakayekutwa akifanya shughuli zake kinyume na maagizo ya Serikali atachukuliwa hatua.

Mwenyekiti wa Chama cha Waganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala  kata ya Misechela Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Nampesya Kaweje alisema,mbali na vitambulisho hivyo kuwasaidia katika majukumu yao, vimewaletea heshima kubwa katika jamii ambayo hapo awali iliwaona kama wababaishaji ambao wanajipatia fedha kwa njia  ya udanganyifu. 

Alisema, tangu Serikali iwapatie vitambulisho  hivyo wamekuwa na Uhuru  na amani kubwa na hata wale waliokuwa wakifanya kazi zao porini ambako sio sehemua salama  sasa wamesogea maeneo ya mjini ambako kuna mazingira rafiki na salama kwa wateja wao.

Amempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kazi nzuri anayofanya ya kuimarisha na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii na  kutambua kazi zinazofanywa na Waganga wa Tiba asili  na Tiba Mbadala ambazo zimewafanya nao kuwa sehemu ya Wajasiriamali wanaopaswa kuchangia Uchumi wa Nchi kutokana na kipato wanachopata.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala   Bimwana Aziz, ameiomba Serikali kuandaa utaratibu ambao utawanufaisha na kupata kipato   cha kutosha kulingana na kazi wanazo fanya, kwani licha ya kutoa Tiba nzuri kwa wateja  lakini baadhi yao wamekuwa wajanja na kushindwa kutumiza ahadi wanazo ahidi mara wanapofanikiwa jambo lililo changia waganga wengi kubaki maskini.

“tunaiomba Serikali itusaidie kuweka utaratibu mzuri ambao utatuwezesha na sisi kunufaika na jasho letu,kwa muda mrefu tunafanya kazi ya kuwasaidia watu ambao wanakwenda kunufika na kutajirika kutokana na Tiba na maombi yetu lakini sisi waganga tuna hali ngumu sana ya maisha”alisema Bimwana.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Liwanga Dau Nguche alisema,wameanza kutekeleza agizo la Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera linalokaza Waganga wa Tiba asili wenye vitambulisho vya wajasiriamali kutozwa fedha.
Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru Dkt Mkasange Kihongole akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana kuhusiana na Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala walivyochangamkia vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.

MBUNGE MAVUNDE ASHIRIKI NA WANANCHI UJENZI WA ZAHANATI, ACHANGIA SARUJI MIFUKO 100

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde ameshiriki katika hatua za awali za ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Msembeta, Kata ya Chigongwe Jijini Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake kwa wananchi hao aliyoitoa Tarehe 6.04.2019 wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi ambapo hoja ya ukosefu zahanati ilijitokeza na Mbunge Mavunde akaahidi kuanzisha ujenzi wake.

Mbunge Mavunde pamoja na kuchimba msingi wa zahanati hiyo akishirikiana na wananchi pia amekabidhi mifuko ya Saruji 100 na kuahidi kusimamia kukamilika kwa zahanati hiyo na kuondoa adha ya wakazi 2300 ambao wanatembea kilomita 10 kufuata huduma za Afya.

Akishukuru kwa niaba ya wananchi, Bi. Esther Masimami amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuanzisha mchakato huo wa ujenzi ambao utawapunguzia adha kubwa ya ukosefu huduma ya Afya kwa wakati na kuahidi kujitolea katika nguvukazi kama sehemu ya mchango wao kwenye zoezi la ujenzi.
 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa mtaa wa Msebweta mapema kabla ya Kushiriki zoezi la Uchimbaji Msingi.
 Baadi ya Wananchi wa Msebeta wakiendelea wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde alipofika Kijijini hapo kutimiza ahadi yake.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akishiriki kwa vitendo zoezi la uchimbaji wa msingi tayari kwa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji

 Mifuko 100 ya saruji iliyokabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde kama ahadi yake katika Ujenzi wa Zahanati ya Msembeta ili kuboresha utoaji wa huduma ya Afya.

Viewing all 110105 articles
Browse latest View live




Latest Images