Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA WIZARA YA ULINZI YA UJERUMANI, WIZARA YA NJE YA UJERUMANI PAMOJA NA BALOZI WA UJERUMANI HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Waechter mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Malte Loknitz kutoka Ujerumani (kushoto) ambaye alikuwa akitambulishwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Waechter katikati mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Waechter mara baada ya kumaliza kikao chao  na ujumbe kutoka nchini Ujerumani Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Waechter mara baada ya mazungumzo yao pamoja na Ujumbe kutoka nchini Ujerumani Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ujerumani hapa nchini Dkt. Detlef Waechter wasita kutoka kushoto, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi watatu kutoka kushoto, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo watatu kutoka kulia pamoja na wajumbe wengine kutoka Ujerumani na Tanzania.
 Mjumbe kutoka nchini Ujerumani Malte Loknitz akizungumza na vyombo vya habari kwa lugha ya Kiswahili mara baada ya kikao chao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mjumbe kutoka nchini Ujerumani Malte Loknitz mara baada ya kuzungumza na vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Madiwani wa Nzega Wang'aka kwa Kutolipwa posho zao Kwa Miezi Minne

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Wamemtaka Mkurungezi wa Halmashauri hiyo kueleza ni vifungu gani vya walaka vya Tamisemi anavyotumia kusitisha posho za kujikimu za Madiwani 

Yamesemwa hayo katika kikao cha madiwani kilichofanyika Wilayani Nzega Mkoani Tabora ambapo kikao hicho kimeudhuliwa na mmoja wa Wajumbe ambae ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Mhe. Hamis Kigwangalla ambaye ameibua hoja hiyo kwa lengo la kujua sababu zinazo sababisha kwa Kutolipwa posho kwa muda wa Miezi Minne

"Madiwani wote wanalazimika kulala kila wanapokuja hapa kufanya kikao, Sisi Mazingira yetu halisi ni Vijijini hapa tumekuja tu kufanya kikao tunamtaka Mkurugenzi azingatie sheria ya Fedha ya Serikali za mtaa"Amesema Kigwangalla

Nae Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Robert akamtaka katibu Msaidizi anayeshughulikia Serikali za mitaa Vitaris Linuma kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili

"Kila diwani Anatakiwa kulipwa posho ya usafiri Anatakiwa kulipwa posho ya kuhudhuria kikao na Fedha ya kujikimu ambayo Anatakiwa kulipwa pesa ya kulala"Amesema Linuma

Licha ya maelezo hayo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Vijijini akamsimamisha Mkurungezi wa Halmashauri hiyo Seleman Sekeiti nae akatoa maelezo."Suala la kulipwa posho nalilejesha kwa Mwenyekiti wa baraza hili maamuzi mtakayoamua hapa ndiyo yatakayo kuwa maamuzi ya baraza "Amesema Sekeiti

Aidha kutokana na kupata tafasiri sahihi ya mkanganyiko huo Wajumbe wa baraza la Madiwani wa Nzega wote kwa kauli moja wameridhia na kurejeshwa kwa posho za kujikimu.
 Pichani ni mbunge wa Nzega  vijijini Mhe. Hamis Kigwangalla akizungumza jambo katika kikao cha madiwani.
Pichani ni madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Mkoani Tabora wakiwa katika kikao kilichofanyika mjini Nzega.

SOKO KUU LA MADINI YA TIN LAZINDULIWA RASMI KYERWA - KAGERA.

$
0
0

Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Mkoa wa Kagera umeendelea kung'ara katika ramani ya kiuchumi na uwekezaji baada ya kuzindua rasmi Soko Kuu la madini ya Tin yanayopatikana Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera pekee, Huku wachimbaji hao wakitakiwa kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanalitumia soko hilo kujinufaisha wao pamoja na Taifa, na kuacha kabisa Biashara ya magendo ambayo ilikuwa ikifanyika kwa kuyatorosha madini hayo na kuyauza Nchi jirani kwa njia zisizo kuwa harali.

Akizungumza na Wananchi, wachimbaji na Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika shughuli hiyo ya Uzinduzi wa Soko kuu la Madini Wilayani Kyerwa, Naibu Waziri wa Madini Mh. Stanslaus H. Nyongo amesema ili soko hilo la madini liwe na Tija na kuvutia Wafanyabiashara ni lazima kuwa na wachimbaji walioombea Leseni hivyo wale wote ambao watakuwa wanamiliki Leseni za uchimbaji lakini wameshindwa kuziendeleza wanyanganywe mara moja, na huku akitoa maelekezo kwa afsa madini Mkoa kama kuna mtu binafsi, au kampuni iliyoshindwa kuendeleza leseni yake na wakati tayari lipo soko la uhakika, ndani ya Mwezi mmoja apatiwe hati ya makosa na afutiwe leseni yake, na leseni hiyo wapewe walio tayari.

Awali Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa yanapopatikana madini hayo Mh. Rashid Mwaimu ameendelea kutahadharisha wale wote waliokuwa wakifanya shughuli za magendo ya madini hayo kuwa, Serikali ipo macho na itaendelea kuelekeza nguvu zake zote katika sekta hiyo, ili kuhakikisha madini hayatoroshwi tena na huku akitoa rai kwa Taasisi zote zinazotoa huduma katika mnyororo wa thamani wa madini, kuweka mazingira rafiki ili kuvutia wafanyabiashara ambao wataanza kufika Sokoni hapo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema lengo la Mkoa wa Kagera ni Kuifanya Biasahara ya rasilimali Madini ya Tin, kufanya vizuri zaidi katika Soko la Dunia kwa kuanzia kuboresha mazingira kwa wachimbaji wadogo, kupitia kutatua changamoto zao zilizopo kwa sasa ikiwemo changamoto ya mitaji na umeme mgodini, ili uzalisahaji wa madini kuongezeka kulingana na Takwimu zilivyo kwa sasa, na kutoa wito kwa wawekezaji wakubwa Kufika Mkoani Kagera kuwekeza katika rasilimali hii yenye faida kubwa katika uzalishaji.

Madini ya Tini yamekuwa muhimu kupitia matumizi yake mbali mbali yakiwemo,Kutengenezea vifungashio vya chakula na vinywaji, rangi aina zote, risasi, vioo, magari, simu za mikononi, Kompyuta, Reli, vifaa vya Kijeshi n.k.
 Pichani Ni Meneja kutoka Kiwanda cha Uchenjuaji Tin (Tanzaplus) Ndg. Maarufu akitoa maelezo kwa Viongozi juu ya Namna madini hayo yanavyoandaliwa.
 Pichani ni Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akifurahia moja ya madini ya Tin ambayo yameshayeyushwa tayari kwa matumizi mbalimbali.
 Pichani ni Afsa madini Mkoa wa Kagera, Mhandisi Lucas M. Akisoma risala kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa soko kuu la madini ya Tin Kyerwa, Kagera. 
 Pichani Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akislimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Kyerwa Ndg. Mhagama, mapema Mara baada ya kuwasili Wilayani humo tayari kwa Uzinduzi wa Soko la Madini.
 Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akitoa salaam zake kwa Wananchi (hawapo pichani) katika  shughuli ya Uzinduzi wa Soko la Madini aina ya Tin Wilayani Kyerwa.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Madini Mh. Stanslaus Nyongo akihutubia Wananchi, viongozi na wachimbaji wadogo wadogo (hawapo pichani) katika Uzinduzi wa Soko Kuu la Madini ya Tin Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.
 Pichani kushoto Ni Naibu Waziri wa Madini Mh. Nyongo, Mbunge wa Kyerwa Mh. Bilakwate, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mh. Mwaimu, Mkuu wa Mkoa Kagera Mh. Gaguti na Katibu Tawala Mkoa Kagera Profesa Kamuzora wakisaidiana kuzindua kufunua jiwe kama Ishara ya Uzinduzi rasmi wa Soko la Madini ya Tin Kyerwa.
 Pichani Viongozi wakiwa wamebeba Tin iliyoyeyushwa kama ishara ya Uzinduzi wa Soko Kuu la Madini ya Tin.
 Jiwe la Uzinduzi kama linavyoonekana pichani.
 Pichani ni Tin ikiwa tayari imeyeyushwa ikisubiri matumizi mengine mbambali, na kila pande moja lina zaidi ya kilo 50, ambapo kila kilo moja huuzwa zaidi ya shilingi elfu kumi na tano.

Tigo na TECNO wazindua smart phone mpya aina ya Spark 3 na Spark Pro Wateja kupata GB 96 ya intanet bure kwa mwaka

$
0
0
 Mwandishi wa Habari kutoka Radio Times FM ya jijini Dar es Salaam Abdala Ally, akiwa katika picha ya pamoja na Meneja bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya (kulia) muda mfupi baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa kwa waandishi wa habari ambapo alifanikiwa kujishindia simu mpya ya kisasa ya Tecno Spark Pro iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
 Meneja Bidhaa za Simu wa TigoMkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusino wa Kampuni ya kutengeneza simu ya Tecno Eric Mkomoya, wakionyesha simu janja za kisasa na za gharama nafuu aina ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark 3 Pro zilizozindliwa jana jijini Dar es Salaam.
 Afisa mauzo kutoka kampuni ya tecno Mobile Tanzania Neema Khamis (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) simu mpya aina ya Tecno Spark Pro iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Bidhaa za Simu wa Tigo Mkumbo Myonga (kushoto) na Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya.
Meneja Bidhaa za Simu wa TigoMkumbo Myonga (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa zimu janja mpya za kisasa na za gharama nafuu aina ya Tecno Spark 3 na Tecno Spark Pro jijini Dar es Salaam jan. Kulia ni Meneja Uhusiano kwa umma wa kampuni ya Tecno Mobile Tanzania Eric Mkomoya.


Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na TECNO leo wamezindua simu janja mpya aina ya TECNO Spark 3 na TECNO Spark 3 Pro zenye ubora wa hali ya juu na ukubwa wa inchi 6.2 itakayomwezesha wateja kuweza kufanya matumizi bora ya simu janja kwa bei nafuu kabisa. 

Wateja watakaonunua simu hizi pia wataweza kufurahia huduma ya mtandao wenye kasi kutoka Tigo pamoja na kifurushi cha GB 96 bure watakachoweza kutumia kwa mwaka mzima. 

Akizungumza wakati uzinduzi wa simu hizo, Meneja Bidhaa za Simu kutoka Tigo, Mkumbo Myonga, alisema Tigo inashirikiana na TECNO Mobile kuleta aina mbili za simu janja za TECNO Spark 3 katika soko la Tanzania ili kuwafanya wateja wake wafurahie maisha ya kidijitali. 

“Moja kati ya simu tunazozindua leo hii ina mfumo wa intanet wa 3G ambayo ni TECNO Spark 3. Simu hii inapatikana kwa bei ya Shilingi 280,000 tu na ya pili yenye mfumo wa intanet ya 4G inaitwa Spark 3 Pro, ikiwa inapatikana kwa Shilingi 333,000 tu. Simu zote hizi zinapatikana katika maduka yetu yote ya Tigo nchi nzima,” alisema Myonga. 

Lengo la Tigo ni kuhamasisha maisha ya kidijitali katika jamii ya Kitanzania. Hii ndio sababu iliyowafanya kushirikiana na TECNO Mobile ili kuweza kuongeza idadi ya watumiaji wa simu janja na wa intanet katika soko la hapa nchini. Kampuni hii ya mawasiliano inaamini kuwa kushirikiana na watengenezaji wa simu ni mkakati unaoakisi lengo la kuwapatia Watanzania simu bora na za bei nafuu. 

Wakati huo huo, Meneja Mahusiano wa TECNO Mobile, Eric Mkomoya, alisema, “Ushirikiano wetu na Tigo umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya mawasiliano ya kidijitali nchini Tanzania. Pamoja, tumeweza kuongeza idadi ya watumiaji wa simu za mkononi nchini kwa kuwapatia simu janja za kisasa na kwa bei nafuu. Kwahiyo, tunaamini ya kwamba simu hizi za TECNO Spark 3 ambazo tunazizindua hii leo zitaweza kutoa kiwango bora cha utumiaji kwa wateja wetu.” 

Kwa maelezo ya Mkomoya, simu janja hizi pia zinakuja na kamera ya kiwango cha juu kabisa ambayo itawezesha wateja wanaopenda picha kuweza kupiga picha na video zenye mvuto na ubora wa juu. 

Simu ya TECNO Spark 3 inafanya kazi katika kiwango cha 3G intanet, ina kamera ya kisasa ya Mega Pixel 13, uwezo wa GB 16 ya RAM, na skrini ya nchini 6.2. Kifaa hiki pia kinaendeshwa kwa mfumo wa Android 9.0. 

Kwa upande mwingine, simu ya TECNO Spark 3 Pro inafanya kazi katika kiwango cha 4G LTE ya intanet, ina kamera ya kisasa ya Mega Pixel 13, uwezo wa GB 32 ya Rom na GB 2 ya RAM, pamoja na na skrini ya nchini 6.2. 

Simu hizi zinakuja na waranti ya miezi 13. 

Tanzania Mpya na Uwanja wa Kimataifa wa Jullius Nyerere

$
0
0
Na Lilian Shirima Maelezo 
Tanzania mpya imedhihirishwa na Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal 3)  katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Akizungumza na Idara ya Habari Maelezo hivi karibuni Msimamizi wa mradi  wa ujenzi wa uwanja huo kutoka Wakala wa Taifa wa Barabara TANROADS, Mhandisi Barton Komba amesema:

“Jengo la tatu la Abiria limesanifiwa kwa viwango vya Kimataifa vya daraja C vya Usafiri wa Anga – IATA. Hivyo linatarajiwa kwa sasa kuwa  kituo kikuu cha usafiri wa anga na kuleta tija kwa Tanzania”.
Mhandisi  Komba ameongeza kwa kusema, asilimia 70 ya gharama  ya  mradi zimetumika kwenye usimikaji wa miundombinu ya mifumo  maalum ndani ya jengo (airport special systems).

“Nasema ukizungumzia  uwanja wa ndege, unazungumzia usalama wa abiria na mizigo, gharama iliyotumika katika usalama wa eneo la ndani ya jengo  (Mechanical Eletrical Plumbing – MEP) pamoja na kufanyia kazi  eneo la uhamiaji ambapo ni zaidi ya asilimia 70  ya mradi, mitambo ndio imechukua sehemu kubwa ya gharama.” Aidha, Mhandisi Komba amesema kuwa, katika eneo hilo sehemu ya  uhamiaji  kumefungwa madawati  10  yenye  sehemu za kufanyia kazi   40  zenye   uwezo wa kuhudumia abiria arobaini wanaowasili au kuondoka kwa wakati mmoja.

Mhandisi Komba amesisitiza kwa kusema kuwa kwa abiria ambao wanaotumia hati za kusafiria za kieletroniki  (E Passport) hawatalazimika  kupita  kwenye huduma za uhamiaji bali kwenye lango  la kieletroniki ( E-Gate) ambapo watahakiki hati zao za kusafiria na alama za vidole.
Pia, kwa upande wa ukaguzi wa mizigo (Baggage Handling System HBS) umesimikwa  mfumo wa kisasa wenye uwezo wa kukagua mizigo katika madaraja matano tofauti  pamoja na  mashine za kukagua mizigo midogo ya mkononi . Ameainisha Mhandisi Komba

Komba amesema kuwa daraja la kwanza mzigo utaangaliwa kwa mashine (scanner) ili kubaini taswira ya kitu kilichomo ndani ambapo daraja la pili mzigo huo utachunguzwa tena kwa kutumia mashine (scanner) zenye nguvu zaidi ya kuona kwa kina. Daraja la tatu mzigo utachunguzwa kwa kutumia mashine zenye uwezo wa kuchanganua picha ya mzigo iliyoonekana kwenye daraja la pili kwa vipande mia moja tofauti (3 Dimention).  Hatua itakayofuata ni mzigo utaingia daraja la nne sehemu ya wataalamu wenye uwezo wa kutasiri picha iliyoonekana katika madaraja yote yaliyotangulia.
Mhandisi Komba amesema, endapo mzigo hautakuwa na dosari ukifika daraja la nne utapata  kibali na hivyo kuingizwa kwenye ndege.  Aidha, mzigo wenye dosari utaingia daraja la tano ambapo hatua za kisheria zitachukuliwa  na vyombo vya usalama.

Akifafanua Mhandisi Komba ameeleza kuwa eneo la kupokea mizigo lenyewe linayo mikanda minne yenye urefu wa mita 95, ukiwemo mmoja kwa ajili ya mizigo hatarishi inayotoka sehemu zisizokuwa na uhakika wa usalama kuingia kwenye nchi yetu. Akielezea miundombinu mingine Mhandisi Komba amesema “Miundombinu iliyosimikwa kwa viwango vya kimataifa ndani ya jengo hili ni mifumo ya tahadhari ya zima moto, utandazaji wa nyaya , ufungaji wa lifti na escalator pamoja na kazi nyingine za ndani  ambazo kwa ujumla wake zimekamilika kwa asilimia 96.8”.

Kwa mujibu wa Mhandisi Komba, eneo la maegesho ya ndege na viungio vyake lenye ukubwa  mita  za mraba 227,000, limekamlika kwa  asilimia 99.9 na kwamba ndege 19 za daraja C ambazo ni ndogo na ndege 11  za daraja E ambazo ni kubwa kama vile Boieng 787, Dreamliner   zinaweza kuegeshwa kwenye eneo hilo. Tofauti ya ndege za daraja C na daraja E pia inatokana na urefu wa ndege, upana wa mabawa yake na vilevile ukubwa na idadi ya abiria. 
Amesema, Mhandisi Komba kuwa, kazi nyingine iliyokamilika na kuupa uwanja huu muonekano wa kimataifa ni usimikaji wa vivuko vya abiria 12 (Passanger Boarding Bridges) pamoja na ujenzi wa barabara  za viungio kuingia na kutoka kwenye maegesho ya ndege. Kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kuwa chaguo la ndege nyingi zinazoruka kwenda nchi za Afrika na bara Asia na Ulaya.

 Eneo la nje ya jengo ambalo ni  maegesho ya magari ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98.6 na ipo nafasi ya kuegesha magari 2,000 kwa ajili ya abiria wanaokuja na kuondoka nchini. Katika eneo hili  imesimikwa mifumo ya kupoozea hewa na mifumo ya maji ya mvua na maji taka. Aidha, taa nyingi zimefungwa kwenye maegesho ya magari, jenerata 7 kwa ajili ya dharura kila moja ikiwa na uwezo wa 2MVA ili kuhakikisha huduma zinapatikana wakati wote hata inapotokea hitilafu ya umeme.

Akielezea historia ya uwanja wa ndege wa Kimatafa wa Julius Nyerere Mhandisi Komba amesema kuwa, ujenzi wa jengo la tatu la abiria ni mwendelezo wa majengo  mawili ya abiria ya zamani yaani Terminal 1 na Terminal 2. Kilianza kufanya kazi mwaka 1959 kikiwa na jengo moja la abiria lenyw uwezo wa kuhudumia abiria laki 5 kwa mwaka na barabara moja ya kuruka na kutua ndege.

Jengo la Pili la Abiria (Terminal 2) lilijengwa mwaka 1984, likiwa na uwezo wa kuhudumia abiria Milioni 1.5 kwa mwaka, idadi iliyofikiwa katikati ya miaka ya 2000. Hadi hii leo idadi ya abiria wanaohudumiwa katika uwanja  wa JNIA  imeongezeka na kufikia abiria Milioni 2.5 kwa mwaka. Kutokana na kuzidiwa kwa uwezo wa Jengo la Pili la abiria na kuzorota kwa huduma za abiria na mizigo kwasababu ya uchakavu wa jengo, mwaka 2000 wakati serikali ikiwa katika zoezi la uboreshaji wa  miundombinu mbalimbali ya viwanja vya  ndege ilionekana dhahiri hitaji la ujenzi wa jengo jipya  la abiria.

 Aidha, wastani wa ongezeko la ongezeko la abiria wanaotumia kiwanja hiki ni asilimia 12.5 kwa mwaka. Ongezeko hili ndilo chimbuko la mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria Milioni 6 kwa mwaka. Kukamilika kwa mradi huu kutawezesha uwanja huu kuwa kitovu cha usafiri wa anga kutokana na ukweli kwamba  majengo yote  mawili terminal one na two yalikuwa yamezidiwa  na wingi wa abiria wanaofikia Milioni  2.5 kwa mwaka. Amefafanua Mhandisi Komba.

Amemalizia, kwa kusema kuwa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal 3) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) unajengwa na Kampuni ya BAM International ya Uholanzi kwa gharama ya Euro milioni 276.7, sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 560 za kitanzania.
Uwanja wa JNIA umefikia asilimia 97.6 ya ujenzi na unatarajiwa kukabidhiwa rasmi kwa serikali mwishoni mwa mwezi Mei, 2019 ambapo uwanja una   uwezo wa kuhudumia abiria  milioni 6  kwa mwaka.
 Sehemu ya huduma mbalimbali kwa Wasafiri iliyopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataiafa Julius Nyerere Terminal 3, Jijini Dar es Salaam ambao ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.
 Sehemu ya Ukaguzi mizigo kwa abiria yenye miundombinu ya kisasa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataiafa Julius Nyerere Terminal 3, Jijini Dar es Salaam ambao ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.
 Moja ya majengo yanayotumika kwa Abiria wanaondoka na wanaofika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere, Terminal 3, Jijini Dar es Salaam, ambao ujenzi wake umekamilika hivi karibuni.
Sehemu inayotumika kwa abiria kuingia na kutoka kwenye ndege yenye miundombinu ya kisasa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, kama inavyoonekana kwenye picha.

TAARIFA YA KUPATIKANA KWA NDG.MDUDE MPALUKE NYAGALI.

$
0
0

Mnamo Mei 04, 2019 majira kati ya saa 19:00 na 20:00 usiku huko Vwawa, Wilaya ya Mbozi na Mkoa wa Songwe, Mtu mmoja aitwaye MDUDE MPALUKE NYAGALI [31] ilibainika kuwa amechukuliwa na watu ambao hakuweza kuwatambua na kupelekwa mahali pasipojulikana.

Taarifa zilifikishwa Polisi Mkoa wa Songwe na ufuatiliaji ulianza mara moja na mnamo tarehe 08 Mei, 2019 majira ya saa 21:00 usiku huko Inyala katika Kijiji cha Mtakuja kilichopo Mkoa wa Mbeya alionekana mtu anaomba msaada, ndipo Dereva wa Pikipiki @ Bodaboda aitwaye EMMANUEL KANAMGONDE na mwenzake AYUB WILSON walimbeba na Pikipiki hadi kwa uongozi wa serikali wa Kijiji cha Mtakuja. 

Mhanga wa tukio hili baada ya kufikishwa kwa viongozi wa Kijiji hicho alijitambulisha kuwa yeye anaitwa MDUDE MPALUKE NYAGALI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na akaomba wajulishwe viongozi wake. Kisha Mhanga alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu. 

Upelelezi wa shauri hili unaendelea ikiwa ni pamoja na msako mkali wa kuwatafuta waliohusika katika tukio hili. 

Imetolewa na: 

[ULRICH O. MATEI – SACP] 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 

Chelsea na Aresenal kutinga fainali EUROPA League?

$
0
0
Baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa jana usiku kwa staili ya aina yake, na kupelekea fainali ya waingereza kwenye shindano hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008. Usiku wa leo Chelsea na Arsenal watacheza michezo ya marudiano katika nusu fainali ya EUROPA huku wakiwa na matumaini ya kucheza fainali ya waingereza mwisho wa mwezi. Mara ya mwisho timu za Uingereza kukutana kwenye fainali ya EUROPA (kipindi hicho UEFA Cup) ilikuwa mwaka 1972, ambapo Wolverhampton Wanders walicheza dhidi ya Tottenham Hotspur na Spurs kushinda 3-2 baada ya michezo miwili (kwa muundo wa zamani).

Miaka 47 baadaye, Chelsea na Arsenal wana nafasi ya kufanya hivyo na kuandika historia. Itakuwa ni mara ya pili tu kwa timu za jiji moja kugombania Ubingwa wa Ulaya katika fainali, mara ya kwanza walikuwa mahasimu wa jiji la Madrid. Arsenal wanasafiri kuelekea Valencia wakiwa wanaongoza kwa 3-1, huku Chelsea watakuwa nyumbani baada ya kupata goli la ugenini katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa sare 1-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kocha wa Arsenal Unai Emery, ambaye alishuhudia matumaini ya timu yake kushiriki ligi ya mabingwa mwakani yakiyeyuka baada ya timu yake kulazimishwa sare na Brighton kwenye mchezo wa ligi Jumapili iliyopita hivyo nafasi ya pekee ni kushinda taji la Europa. "Tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye Europa na tutajaribu kufanya hivyo,” alisema Emery ambaye alishinda taji hilo mara tatu mfululizo akiwa na Sevilla.

Naye mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang anatamani kucheza na Eintracht Frankfurt kwenye fainali, kuliko kucheza na mahasimu wao, Chelsea. “Siwataki Chelsea.  “Tunawafahamu ni timu nzuri lakini nadhani sisi tutaingia fainali kwanza na ningependa tucheze dhidi ya Frankfurt kwa sababu Chelsea tumeshacheza nao [kwenye ligi]. Nafahamu Frankfurt ni wazuri sana kama sote tutaingia fainali utakuwa mchezo mzuri sana. Tunataka kushinda taji hili kwa sababu ndilo lengo letu tangu mwanzo wa msimu” 

Kocha wa Chelsea alizomewa na mashabiki wao kwenye mapumziko katika mechi dhidi ya Watford Jumapili iliyopita, lakini walirudi vizuri kipindi cha pili na kushinda kwa mabao 3-0 na kujihakikishia nafasi ya nne kwenye msimo wa ligi. Mchezo wa Valencia dhidi ya Arsenal utapigwa saa 4:00 Usiku na kurushwa Mubashara kupitia StarTimes Sports Premium HD, huku ule wa Chelsea vs Eintracht Frankfurt ukipigwa muda huo huo na kuonyeshwa kupitia StarTimes World Football HD.

Chaneli zote zinapatikana katika kifurushi cha UHURU (Antenna) kwa Tsh 18,000 tu kwa mwezi na SMART (Dish) kwa TSh 21,000 kwa mwezi.


SHIRIKISHO LA WALIMU MAKADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAKABIDHI MIFUKO 120 YA SARUJI.

$
0
0
Na Shushu Joel, Mkuranga. 

MBUNGE wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa mifugo na uvuvi amepokea msaada wa mifuko 120 ya saruji kutoka kwa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi  (CCM).

Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko hiyo mratibu wa shirikisho hilo  Bakari Msingili alisema kuwa kusudi la wao kufanya uamuzi huo ni kutokana na juhudi za kimaendeleo  zinazo fanywa na Mbunge huyo  kwenye nyanja za elimu,Afya na miundombinu kwenye wilaya ya mkuranga.

Aliongeza kuwa imekuwa  ngumu kuamini kwa kile ambacho tunakifanya kama walimu juu ya kuchangia fedha kwa ajili ya maendeleo kutokana na tabia iliyojengeka kwa watu kuwa walimu ni kundi la watumishi ambao ni wabaili  sana.

"Mifuko hii ya saruji itasaidia kwenye nyanja hii ya elimu lakini hata sie kama shirikisho la walimu makada wa ccm" Alisema Bakari.

Naye Afisa elimu ya watu wazima  Mektrida  Kahindi ambaye ni mjumbe wa shirikisho hilo alisema kuwa shirikisho hilo litaendelea kutoa  misaada mbalimbali katika wilaya hiyo kwa lengo la kusaidia maendeleo kwenye wilaya ya mkuranga.

Aliongeza kuwa mifuko hii ya 120 ya saruji ni mwanzo tu lakini kuna mambo makubwa ya nakuja mbele yetu.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Ulega  amewapongeza wana shirikisho hilo kwa kutambua juhudi wanazozifanya  jimbo humo hivyo amewataka wananchi wake kutumia  kwa uangalifu saruji hizo kwani mwezi wa kumi  watakuja  ili kuhakikisha usahihi wa kazi jinsiilovyoondoka


Aidha Ulega amewapongeza walimu hao kwa kuridhishwa na kuona kile kinachofanwa na Serikali ya awamu ya tano china ya Rais Dkt John Pombe Magufuli. 

Aidha Ulega amewataka walimu kuunda vikundi ili kupata mikopo ya wanyama kama ng'ombe na mbuzi ili waweze kuwaingizia kipato cha ziada mbali na kutegemea mshahara.
 Mbunge  wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  (wapili kuliua )akipokea  mifuko 120 ya saruji kutoka kwa shirikisho la walimu makada wa chama cha mapinduzi  (CCM)(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa wilaya ya  Mkuranga Filberto Sanga kulia na Mbunge  wa jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (wapili kulia) wakiwapongeza  walimu makada wa chama cha mapinduzi  (CCM kwa  kukabidhi   mifuko 120 ya saruji.

TAHADHARI YA HOMA YA DENGUE YAZIDI KUTOLEWA

$
0
0
NA WAJMW-DODOMA

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezidi kutoa tahadhari ya  kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue nchini hususani katika Jiji la Dar Es Salaam na Tanga.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo zilizoko jijini Dodoma.

Prof. kambi amesema hadi kufikia tarehe 6 Mei 2019, kati ya watu waliopimwa, wagonjwa 1237 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugonjwa wa Dengue na kati yao 1150 ni kutoka Dar Es Salaam, 86 ni kutoka Tanga na mtu mmoja kutoka Singida.

Aidha, Prof Kambi amesema takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2019 zinaonesha mwenendo wa ugonjwa huu kuwa na idadi ya wagonjwa 1237, vifo vya watu wawili na kuongeza kuwa waliofariki walikua na maradhi mengine.

Pamoja na hayo Mganga Mkuu huyo wa Serikali amelipongeza jiji la Dar Es Salaam kwa kuanza kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu ili kupambana na ugonjwa huu.

Vile vile amesema Wizara inaelekeza Mikoa na Halmashauri zote nchini kuendelea kuchukua hatua katika kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi ya maji, kunyunyizia dawa ya kuua viluwiluwi, kuondoa vitu vinavyosababisha mazalia ya mbu, kufyeka vichaka, kufunika mashimo ya maji taka kwa mifuniko pamoja kusafisha gata za paa la nyumba na kutoruhusu maji kusimama.

Prof. Kambi amesema Wizara kwa kushirikiana na Mikoa na Halmashauri zote nchini itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuangamiza mazalia ya mbu na viluwiluwi, kuweka mpango wa dharura wa miezi sita kuanzia Mei mpaka Oktoba ili kukabiliana na ugonjwa huu. Pia amesema Serikali imenunua Vitendanishi vyenye uwezo wa kupima wagonjwa 1870 na vimesambazwa kwenye vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu nchini kote.

Mwisho Prof. Kambi amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga kuumwa na mbu kwa kuvaa nguo ndefu, kutumia vyandarua vyenye viuatilifu, kutumia dawa za kufukuza mbu na kuweka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi ili kukabiliana na ugonjwa huu.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuwepo kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini.
 Baadhi ya waandishi wa habari waliojitokeza kusikiliza tamko la kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa Homa ya Dengue nchini wakati likitolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi Jijini Dodoma.

INTRODUCING "SAYANSI FULANI" BY ONE THE INCREDIBLE

Alamba tuzo ya mafanikio makubwa ya Thamani ya Mwanamke na ajira binafsi

$
0
0
MJASIRIAMALI Devotha David ambaye ni mmiliki wa First Supper Market iliyopo mbezi Mbeach kona ya Goba Dar es Salaam amefurahia kupewa tuzo ya mafanikio makubwa ya Thamani ya Mwanamke na ajira binafsi siku chache zilizopita Jijini Dar es Salaam. 

Kongamano hilo lenye mafanikio makubwa lilianza kuandaliwa mwaka 2017 limekuwa la malengo mazuri kwa kutambua kazi za jamii kwa wanawake. “Kwa mara hii nafurahia kufanikiwa kwangu ikiwa nimeweza kutambulika kama mwanamwake niliyejiajiri na Kusherekea Siku hii,”anasema Devota. 

Alisema nashukuru kupata tuzo yenye lengo la kuipa thamani Ajira binafsi sawa na Ajira rasmi ambayo inachukua kiasi kidogo cha wanawake kulinganisha na ajira binafsi. Aidha alisema kuwa amefanikiwa kukutanishwa katika jukwaa hilo la wanawake wanawake zaidi, na ameweza kujengewa ujasiri wa kuendeleza mapambano ya mafanikio kupitia jukwaa hilo na sasa ataweza kufanikiwa zaidi kwani maadhimio ya mafanikio yake hayo atayazidisha kwa bidii ili kuzidi kung’ara baada ya kongamano hilo . 

Amewaomba waandaaji kuendelea kufanya vizuri tena Kongamano hilo kwani kutakuwa na mafanikio makubwa yaliogusa maisha ya wanawake wa Tanzania. “Nawaomba wanawake wenzangu waliojiajiri kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kufanya maandalizi ya kukutana na wanawake wengine Siku nyingine tena ambapo hisstoria itajiandika tena,”alisema Devotha. Alisema kuwa ameweza kuendesha biashara zake kwa muda mrefu na kupata mafanikio makubwa zaidi anajivunia kupata msaada zaidi kutoka kwa mumewe.

“Nikiwa katika mazingira ya utoto zamani nilianza kuwa namsimamia mama yangu mzazi kipindi nikitoka shule niliachiwa biashara na mama , mama alikuwa akimili depo moja niliweza,”alisema Devotha. Alisema hivyo kutokana na kuanza mapema mazingira hayo aliyokuwa , alianza kupenda ajira za kujiajiri, ambapo kwa sasa taswira ya serikali ya awamu ya tano inapigania vipao mbele katika ajira za wajasiriamali binafsi. 

Kwa taswira ya ajira kwa serikari zinapambanuliwa kuwa ajira zinaweza kuwa moja kwa moja kutoka serikalini au kuweka mazingira ya kuziwezesha sekta binafsi kutekeleza jukumu yake. Hata hivyo kumekuwa na hatua za wanawake kupambaniwa , Siku ya wanawake Duniani ambayo uadhimishwa kila mwaka ifikapo Tarehe 8 Mwezi wa Tatu Kimataifa; kumekuwa na umuhimu mkubwa wa kuutambua mchango wa wanawake katika nyanja Mbalimbali na kumuinua mwanamke azidi kusimama na kuinuka kimaendeleo katika Jamii ulimwenguni. Lengo kuu la kuadhimisha siku hiyo adhimu ni kutathmini utekelezaji wa afua za kufikia usawa jinsi na uwezeshaji wanawake kiuchumi, kijamii,kisiasa katika kufikia maendeleo jumuishi. 

Maadhimisho haya, pia yanatoa fursa ya kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na jamii, serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na wadau wa maendeleo katika kumwinua mwanamke. Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu kupitia kaulimbiu ya ‘kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini’. Anasema kuwa amekuwa akiwataka wanawake kutambua kuwa serikali imekuwa ikiwahudumia, kuwathamini, kuwawezesha na kuwasimamia vyema ili kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwepo katika jamii. Devotha alisema kuwa juhudi hizo za serikali ni za ukweli zipo zinaelekeza juu ya kuweleka mafanikio bora kwa mwanamke . 

Licha ya kuziunga mkono juhudi hizo anaelezea heka keha zake kuelekea ukombozi zaidi juu yake katika anga za uchumi katika familia yake. Harakati za nyumani kwao kupitia mama yake mzazi bado zinaonekana kumjenga katika itaji lake la kuutaka msingi bora wa kufikia malengo makubwa ,anaeleza kuwa anayo jumla maduka matatu katika jiji la Dar es Salaam . 

“Najishughulisha na maduka yangu yanayouza bidhaa mbali mbali kama mabegi ya watoto viatu vya watoto pamoja na mambo mengine kama hayo ya mavazi ya aina yote kwa umri huo ,”alisema. Amesema First Supper Market iliyopo mbezi Mbeach kona ya Goba Dar es Salaam ni moja ya mafanikio yake mapya kwa sasa. 

Alisema kuwa kwa kufungua saloon yake ya kike hapa jijini, kila jambo huwa na safari yake kimafanikio, mtaji wa saloni ndio uliokuwa mtaji wake wa kwanza katika maisha yake . “Baada ya kuhapo nilifanikiwa kuanza biashara ya kwenda nje kununua mavazi ya biashara taratibu nilianza kupata uzoefu na hatimaye niliweza kumudu napo ikiwa moja ya mafanikio niliyo nayo,”alisema. Amesema kuwa angependa kuona furaha yake ikizidi kukua na kupata tabasamu lenye furaha kama ilivyo kwa mafanikio kutoa faraja ya kweli katika maisha. 

“Niliwahi pia kumiliki mtaji mkubwa wa kuendesha baa iliyokuwa na vyumba vya kulala wageni kupitia mradi huo niliweza kupata pesa nyingi lakini iliweza kunifanya niwe mbali na familia ,”alisema. Devota anaeleza kuwa mara baada ya kuendesha kwa mafanikio mradi wake wa Dipromatic Baa iliyokuepo maeneo ya tabata jijini hapa kimsingi ndio iliyo ujenga mtaji wake kuwa mkubwa katika biashara , Dipromatic iliweza kujizolea umaarufu mkubwa ,iliweza kuwa na wateja wengi alikuwa mbali na famili muda wa kukaa nyumbani ulikuwa mchache. 

Amesema kuwa Dipromatic Baa aliendesha kwa miaka kadhaa na ndiyo chachu ya mafanikio, na ndpo alipoaanzia mradi alionao sasa wa biashara nyingine alizonazo kwa sasa ambapo bahari Beach anaduka pamoja na Min Supper Market zote zikiwa na jina hilo la First Supermarket. 

Amesema kuwa anawakaribisha wateja kununua maitaji ya mavazi ya watoto yakiwemo mabegi pia mambo mbali mbali kama pombe za kidunia katika duka lake jipya kufunguliwa mapema mwezi ujao la First Supper Market iliyopo mbezi mbeach kona ya Goba

Balozi Seif awasilisha Makadirio ya mapato na Matumizi ya ofisi ya Makamu wa Rais wa Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Pato la Taifa kwa Mwaka 2019 linatarajiwa kukua kwa kasi ya wastani wa asilimia 7.8% itakayosababisha kuimarika zaidi kwa Uchumi wa Zanzibar kutokana na ongezeko la Uwekezaji katika Sekta ndogo ya usafirishaji na Uvuvi.

Alisema hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa Pato la Mwananchi mmoja mmoja kutoka Shilingi Milioni 2,104,000/- sawa na Dola za Kimarekani Mia 944 na kufikia Shilingi za Kitanzania Milioni 2,323,000/- sawa na Dola za Kimarekani Elfu 1.026.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Kibao cha Bajeti 2019/2020 kilichoanza Baraza la Wawakilishi Chukwani Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar tayari imekaribia kufikia kiwango cha Nchi ya kipato ca Kati cha Dola za Kimarekani Elfu 1,030 kwa mujibu wa vigezo vya Kimataifa.

Balozi Seif alisema Pato la Taifa kwa bei ya soko limefikia thamani ya Shilingi Bilioni 3,663,000,000/- kwa Mwaka 2018 kutoka thamani ya Shilingi Bilioni 3,228,000,000/- kwa Mwaka 2017 kulikosababishwa na ongezeko la pato la Mwananchi.

Alisema kasi ya mfumko wa bei pia umeshuka hadi kufikia wastani wa asilimia 3.9 Mwaka 2018 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.6 Mwaka 2017 baada ya kuchukuliwa hatua za udhitibi wa mfumko wa bei kwa kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula.

Balozi Seif alisema hali hiyo inatokana na uwezeshwaji waliopatiwa Wakulima kwa kupatiwa pembejeo na mafunzo ya kuongeza uzalishaji kwa kutumia Teknolojia ya gharama nafuu iliyokwenda sambamba na utafiti katika Sekta ya Kilimo uliosaidia kupata mbinu za kupiga vita changamoto zinazoyakabili mazao ya matunda na mboga za majani.

Alieleza kwamba Muelekeo wa Hali ya Uchumi wa Zanzibar kwa Mwaka 2019 unategemewa kwenda sambamba na Utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020, Mkakati wa Kukuza Uchumi Zanzibar {MKUZA 111} na ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduai ya Mwaka 2015 – 2020.

Balozi Seif alifahamisha kuwa mafanikio yote yaliyopatikana yanatokana na jitihada kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi mahiri wa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein katika kuona hali ya uchumi na Kijamii ya Taifa na Wananchi inazidi kuimarika kila kukicha.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifahamisha kwamba azma ya Serikali kuu ni kuhakikisha kwamba inakamilisha Miradi yote mikubwa ya Maendeleo kama ilivyoahidi katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 – 2020.

Aliitaja Miradi hiyo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa Jengo la Abiria {Terminal 3} katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar, Ujenzi wa Bandari ya Mpiga Duri iliyopo Maruhubi pamoja na Ujenzi wa Hospitali Binguni iliyopo Wilaya ya Kati.

Alisema miradi hiyo inakwenda sambamba na mpango wa Taifa wa kuendelea kuimarisha uzalishaji na usafirishaji wa zao la Karafuu kutokana na matarajio ya msimu mkubwa wa zao hilo kwa Mwaka huu wa 2019 pamoja na kupanuka kwa kiwango cha idadi ya Watalii kutokana na kupatikana kwa masoko mapya ya sekta hiyo.

Balozi Seif alifafanua wazi kwamba Serikali tayari imeandaa mikakati maalum ya kutafuta fedha kwa Nchi na Mashirika rafiki sambamba na kutenga Fedha kutoka katika vianzio vyake vya ndani ili itapotokezea kushindikana kupata msaada kutoka nje Serikali iendelee na ukamilishaji wa Ujenzi wa Miradi hiyo.

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa Mchanga, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mchanga ni Rasilmali muhimu hapa Nchini kutokana na matumizi makubwa katika Sekta ya Ujenzi.

Balozi Seif alisema kwa bahati mbaya eneo halisi linaloweza kuchimbwa mchanga katika Visiwa vya Zanzibar ni dogo zaidi kwa kuwa baadhi ya maeneo mengine tayari yameshachimbwa, wakati mwengine yanatumika kwa matumizi ya Kibinaadamu ikiwemo Makaazi, Kilimo na Huduma za Kijamii.

Alisema kutokana na changamoto hiyo Serikali Kuu ililazimika kutangaza utaratibu Mpya wa usimamizi wa uchimbaji, usafirishaji na uuzaji Mchanga ulioanza Tarehe 3 Machi Mwaka 2017 kwa lengo la kujaribu kudhibiti maeneo ya Ardhi na kuweza kutumika kwa shughuli nyengine hasa Kilimo.

Alifahamisha kwamba tokea kuanza kwa utaratibu huo unaosimamiwa na Serikali Kuu yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana ikiwemo gari zinazobeba mchanga kupimwa ili kupata Takwimu na malipo sahihi ya bidhaa hiyo, kupunguza msongamano wa Gari machimboni pamoja na uwepo wa bei elekezi inayowazuia Wafanyabiashara kupandisha bei ya mchanga kiholela ambayo huwaumiza Wananchi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliweka wazi kwamba katika kipindi cha kuanzia Mwezi Machi 2017 hadi Disemba 2018 chini ya usimamizi huo jumla ya Tani Milioni 1,690,122 za Mchanga zilichimbwa Visiwani Zanzibar.

Alisema kati ya Tani hizo Unguja ilichimbwa na kusafirishwa Tani Milioni 1,605,517 na Pemba zilizchimbwa na kusafirishwa Tani 84,605 sawa na asilimia 5% ya uchimbaji unaofanyika katika Kisiwa cha Unguja.

“ Kwa Takwimu hizi ni wazi kwamba ipo kasi kubwa ya uchimbaji wa mchanga katika Kisiwa cha Unguja ikilinganishwa na uchimbaji wa Mchanga katika Kisiwa cha Pemba”. Alifafanua Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa wito kwa Wananchi kwamba Serikali haitamvumilia Mtu ye yote yule ambae atachimba na kusafirisha mchanga kinyume na utaratibu uliowekwa au kuuza mchanga kinyume na bei elekezi iliyowekwa na Serikali.

Kuhusu Sekta ya Elimu Balozi Seif alisema Serikali Kuu kupitia Wizara inayosimamia Taaluma inaendelea kuchukuwa hatua kadhaa katika kuhakikisha mazingira ya Elimu yanakuwa mazuri ili Watoto wa Visiwa vya Zanzibar waweze kupata Haki yao ya Elimu bila ya Malipo.

Alisema inapendeza kuona asilimia ya Uandikishaji katika ngazi zote za Elimu ya lazima imeongezeka ikilinganishwa na Mwaka wa Fedha wa 2017/2018 ambapo ngazi ya Maandalizi uandikishaji umefikia asilimia 69.4% Mwaka 2018 kutoka asilimia 66.1 Mwaka 2017.

Balozi Seif alieleza kwamba kasi hii ya uandikishaji inatokana na upatikanaji wa nafasi, mwamko wa Jamii kuhusu Elimu na ushiriki mzuri wa Wananchi katika kuleta Maendeleo kwenye Sekta ya Elimu.

Alieleza kwamba katika juhudi za kuimarisha Sekta hiyo muhimu kwa Taifa lolote lile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mfuko wa OPEC tayari imekamilisha ujenzi wa Skuli Tisa za Ghorofa za Sekondari Unguja na Pemba.

Alisema Mradi huo mkubwa umekwenda sambamba na ujenzi wa Maabara, Maktaba na vyumba vya Kompyuta kwa Skuli 24 za Sekondari kwa mashirikiano na Benki ya Dunia.

Balozi Seif alifahamisha kwamba katika kuimarisha Elimu ya Sekondari Serikali imegawa vifaa vya Maabara na Kemikali kwa Skuli zote za Sekondari za Unguja na Pemba zenye Kidato cha Nne na cha Sita ili kuwawezesha Wanafunzi kusoma kwa vitendo na kujiandaa vyema na Mitihani yao.

Akigusia kadhia ya uvujaji wa Mitihani ya Darasa la Kumi iliyofanyika Disemba Mwaka 2018 na kupelekea Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali kufuta Mitihani hiyo Serikali tayari imeshachukuwa hatua za kuwasimamisha kazi Watendaji wote waliohusika kutoka Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya Habari kwa mujibu wa Sheria za Utumishi wa Umma.

Balozi Seif alisema kadhia hiyo isiyovumilika imepelekea Serikali kuiagiza Kamati ya Taifa ya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi wa kina na kujua chanzo chake ambapo tayari imeshakamilisha kazi yake iliyoagizwa na kuwasilisha rasmi Taarifa hiyo Serikalini.

Alisema Taarifa hiyo ya uchunguzi imebaini baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale kubainika kuhusiaka na kadhia hiyo iliyolitia aibu Taifa.

Balozi Seif alisema kwa mnasaba huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imeshalitaka Jeshi la Polisi Nchini kuwachukulia hatua za Kisheria kwa mujibu wa Makosa waliyofanya wale wote waliohusika na tukio hilo lililoleta hasara kubwa ya Fedha za Umma.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameliomba Baraza la Wawakilishi liidhinishe jumla ya Shilingi Bilioni Hamsini na Saba, Mia Tisa na Kumi na Moja Milioni, Laki Tatu na Arubaini na Tisa Elfu { 57,911,349,000/- } kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Taasisi zake kwa ajili ya kutekeleza Program 11 kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020.

Alisema katika mchanganuo huo Shilingi Bilioni Arubaini na Nane Kumi na Tatu Milioni na Laki Nne { 48,013,400,000/- } ni kwa Kazi za kawaida na Shilingi Bilioni Tisa, Mia Nane na Tisini na Saba Milioni, Laki Tisa na Arubaini na Tisa Elfu { 9,897,949,000/- } ni kwa kazi za Maendeleo.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika kikao cha Bajeti kilichoanza rasmi Mwaka huu wa Fedha wa 2019/2020.
 Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa Wizara za Serikali wakifuatilia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiongozwa na Katibu Mkuu wake Nd. Shaaban Seif Mohamed wa pili kutoka Kulia Mstari wa chini.
 Baadhi ya Watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakifuatilia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyowasilishwa na Balozi Seif.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakisikiliza hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyowasilishwa na Balozi Seif. Picha na – OMPR – ZNZ.

FORUM CC, UMOJA WA ULAYA WASHIRIKIANA KUKUTANISHA MASHIRIKA YA KIRAIA KUJADILINATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NA CHANGAMOTO ZAKE

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

FORUM CC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameamua kuwatanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali kwa lengo la kuwa na jukwaa ambalo litatumika kujadili masuala yanayohusu hali ya mabadiliko ya tabianchi.

Pamoja na mambo mengine Forum CC na mashirika hayo wamejadili kwa kina namna bora ya kufanya kazi kwa karibu na mamlaka za Serikali kwa lengo la kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo athari zake zinagusa kila mahali.

Akizungumza leo Mei 9, 2019 wakati majadiliano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC Rebecca Muna amefafanua wao kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wameamua kuwakutanisha wadau hao waliopo kwenye mashirika na asasi za kiraia kujadili kwa kina namna bora ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

"Sababu iliyotufanya tukutane hapa leo tunataka tuwe na ushirikiano wa karibu na Serikali.Tunataka kufanya kazi na viongozi, hivyo wadau wote wa maendeleo tutakuwa na jukwaa litakalotupa fursa ya kufanya kazi kwa pamoja hasa za kutatua changamoto za athari za tabianchi,"amesema Muna.

Amefafanua hali ya mabadiliko ya tabianchi yamesababisha nchi kuwa na ukame, mafuriko, kina cha bahari kuongezeka, kupanda kwa joto na magonjwa ya mazao , hivyo kusababisha madhara ya aina mbalimbali kwa jamii.

Amesisitiza kupitia jukwaa la majadiliano ambalo litaanzishwa na wadau maana yake watakuwa na eneo maalumu ambalo litawakutanisha na kujadili kwa kina hali ya mabadiliko ya tabianchi.

"Lengo letu ni kuwa na jukwaa la pamoja ambalo hilo litatuwezesha sote kwa umoja wetu kupata fursa ya kujadili na kupata ufumbuzi wa namna sahihi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,"amesema Muna.

Hata hivyo amesema umefika wakati wa kuwepo kwa mfumo sahihi ambao utawawezesha mashirika, asasi za kiraia na wadau wa maendeleo kushirikishwa kikamilifu na Serikali katika kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Forum CC Euster Kibona amesema kuwa pamoja na kuweka mikakati ya kujadili kuhusua mabadiliko ya tabianchi wamekumbusha kuhusu uwajibika ambapo kupitia mada yake iliyohusu dhana ya uwajibika alifafanua kwa kina huku akisisitiza uwajibikaji ni ushirikiano baina ya pande mbili.

"Uwajibikaji ni muhimu katika kufuatilia masuala mbalimbali ya kimaendeleo na hata hili la mabadiliko ya tabianchi nalo lazima tujadiliane kuhusu namna bora ya kuwajibika kwani eneo hilo limekuwa na changamoto kubwa.

"Katika kuwajibika lazima ufahamu nani anawajibika katika lipi na anawajibika kwani.Hata hivyo ili kufanikiwa ni jambo linalohusu uhusiano wa zaidi ya mtu mmoja.Hivyo ni wakati wetu kuweka mikakati ya namna bora itakayowezesha kila mmoja kwa nafasi yake kuwajibika,"amesema Kibona. 

Awali Ofisa Programu,Ushawishi na Utetezi kutoka TGNP Deogratius Temba amesema mabadiliko ya tabianchi yanagusa maeneo mbalimbali yakiwemo ya jinsia na athari zake zinakwenda moja kwa moja kwa mtoto wa kike.

"Athari za mabadiliko ya tabianchi ni nyingi ikiwemo ya ukame ambayo inasababisha hata maeneo ambayo wananchi walikuwa wanateka maji yakauka na kusababisha wanawake kuanza kufuata maji umbali mrefu na hivyo kusababisha hata matukio ya ukatili wa kijinsi.

"Hivyo eneo hili linagusa maeneo mengi na hivyo kila mmoja wa nafasi yake anayo nafasi ya kujadili na kuweka mipango na hasa ambayo inatokana na maoni ya wananchi katika maeneo husika.

"TGNP tumekuwa tukishirikiana na wananchi kuibua ajenda na kisha wananchi kuzipeleka katika mamlaka husika na hivyo hata haya masuala ya tabianchi ni vema wananchi wakajengewa uwezo ili kuwa na uelewa,"amesema Temba

Mwenyekiti wa Bodi ya Forum CC Euster Kibona akizungumza jambo wakati wa kikao cha mashirika ya kirai kujadili hali ya mabadiliko ya tabianchi na mchango wa mashirika hayo katika kutafuta ufumbuzi wake kwa kushirikiana na Serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Forum CC akizungumza na wadau wa maendeleo kupitia mashirika ya kiraia ambauo yamekutana kujadili namna bora ya kujadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na vongozi wa serikali.

Ofisa Programu,Ushawishi na Utetezi kutoka TGNP Deogratius Temba akifafanua jambo kuhusu mabadiliko ya tabianchi yanavyoarithi moja kwa moja masuala ya kijinsia nchini Tanzania wakati wa kikao kati ya Forum CC na mashirika ya kiraia ambayo yamekutana kwa malengo mbalimbali likiwemo la kuwepo kwa jukwaa la pamoja na wadau hao

Sehemu ya washiriki wa mkutano uliondaliwa na Forum CC kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya wenye lengo la kuangalia namna bora ya mashirika ya kiraia kushirikiana na Serikali kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Balozi Dkt. Abdallah Possi awasilisha hati za utambulisho kwa Rais Miloš Zeman wa Jamhuri ya Ucheki (Czech Republic)

$
0
0
 Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia anawakilisha nchi Ucheki Dkt. Abdallah Possi akiwa tayari kuwaasilisha hati za utambulisho kwa Rais Miloš Zeman wa Jamhuri ya Ucheki (Czech Republic) katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Prague Jumatano Mei 8,  2019
 Balozi Dkt. Abdallah Possi akiwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Miloš Zeman wa Jamhuri ya Ucheki (Czech Republic)

 Balozi Dkt. Abdallah Possi akimtambulisha mkewe baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Miloš Zeman wa Jamhuri ya Ucheki (Czech Republic)
Balozi Dkt. Abdallah Possi katika picha ya kumbukumbu baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Miloš Zeman wa Jamhuri ya Ucheki (Czech Republic)

RELI YA KATI NAYO YAUNGWA KWA UMEME,SHUHUDIA CHUO CHA RELI TABORA KINACHOZALISHA WATAALAMU


Waziri Biteko azindua Soko Kuu la Madini Mwanza

$
0
0
Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefanya uzinduzi wa Soko Kuu la Madini Mwanza na kutumia fursa hiyo kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kutumia soko hilo kuuzia madini yao na kuachana na tabia ya utoroshaji wa madini.

Uzinduzi wa soko hilo unganishi Kanda ya Ziwa umefanyika Mei 08, 2019 katika jengo la Rock City Mall ambapo Biteko amebainisha kwamba uanzishwaji wa masoko ya madini nchini umesaidia ongezeko la kiwango cha uuzaji madini tofauti na hapo awali ambapo yalikuwa yakiuzwa kiholela na hivyo kuikosesha Serikali mapato.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwenyekiti Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akitoa salamu za tume kwenye uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya hali ya uanzishwaji masoko ya madini nchini ambapo amebainisha kwamba zaidi ya mikoa 10 tayari imeanzisha masoko hayo.
Mfanyabiashara wa madini, Kakono Kaniki akitoa salamu kwa niaba ya wafanyabiashara wa madini mkoani Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Mongella ajivunia Soko Kuu la Madini Mwanza "tunataka nchi ifaidike"

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA DKT. MABODI SONGEA MJINI

$
0
0

 MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akiwasili katika Wilaya ya CCM Songea Mjini kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya kuimarisha Chama na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Wilaya hiyo.
 WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi Songea Mjini wakimvisha Vazi la Heshima la Kimila la kumtambua Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa kuwa ni Kiongozi Muadilifu aliyetambuliwa rasmi na Wazee wa Wilaya hiyo ambao ni Utaratibu wa Kimila uliasisiwa na Kiongozi Mkuu wa Kijadi ambaye ni Mzee Songea Mbano.
 MLEZI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akiwa katika Kikao cha ndani na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Songea  Mjini.
 WANACHAMA wapya waliojiunga na CCM wakila kiapo cha Uanachama mara baada ya kukabidhiwa Kadi za CCM na kupokelewa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM  Taifa huko katika Shina namba 4 Tawi la CCM Mtakuja na Kata ya Majengo Wilaya ya CCM Songea Mjini.
 WALIOKUWA Viongozi wandamizi wa CHADEMA waliojiunga na CCM na kupokelewa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Mabodi ambao ni Thimoth Tililo (kulia) aliyekuwa Mjumbe wa Mtaa wa Unangwa kupitia CHADEMA Wilaya ya Songea Mjini na aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Kata ya Misufini ndugu Juma Marwa Kionyori (kushoto) wakizzumgumza mara baada ya kujiunga na CCM na kupokelewa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma Dk.Abdulla Juma Mabodi.
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Killian Mwisho akizungumza katika Kikao cha ndani cha Viongozi na Watendaji wa Serikali kilichohitishwa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Dk.Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi'.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 09.05.2019

Prof. Kabudi akutana na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP anayemaliza muda wake, Balozi wa Vietnam na kuelezea mkutano ujao wa SADC

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na  kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Boucly, ambaye amemaliza muda wa kuliwakilisha shirika hilo nchini. Katika mazungumzo hayo, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) alimshukuru Bi.Natalie Boucly kwa uwakilishi wake mzuri katika nyanja mbalimbali katika kuchochea maendeleo nchini.

Pamoja na mambo mengine, Prof. Palamagamba John Kabudi alimweleza Bi.Natalie Boucly ajisikie nyumbani na asisite kuitembelea tena Tanzania pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini kama mbuga za wanyama na mlima Kilimanjaro pamoja na visiwa vya Zanzibar.  
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimsikiliza Bi. Natalie Boucly wakati wa mazungumzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Emmanuel Buhohela (wa pili kutoka kushoto), Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Charles Joseph Mbando (wa kwanza kulia) pamoja Afisa Mambo ya Nje Bi Diana Mhina wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Bi. Natalie Boucly (hawapo pichani)
Prof. Palamagamba John Kabudi akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa vivutio vya utalii nchini Bi. Natalie Boucly.



Posted: 09 May 2019 04:58 AM PDT
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh (kushoto), mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Kitengo cha mawasiliano serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Emmanuel Buhohela (katikati), wa kwanza kulia ni Katibu wa Waziri Bw. Magabilo Murobi na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Luangisha. E.F.L wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na  Balozi Doanh (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea
Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Doanh wakiwa katika picha ya pamoja.



Posted: 09 May 2019 03:41 AM PDT
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya Mkutano wa SADC unaotarajiwa kufanyika hapa nchini mwezi August 2019,ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anatarajia kupokea nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo na kutoa rai kwa Makampuni,taasisi za serikali na binafsi na wajasiriamali mbalimbali kuchangamkia fursa zitakazojitokeza wakati wa mkutano huo wa SADC.Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakinukuu mazungumzo ya Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kuhusu Mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika hapa Nchini mwezi August 2019 (hayupo pichani).
Sehemu ya wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na Waandishi wa Habari Kuhusu mkutano wa SADC utakaofanyika hapa Nchini mwezi August 2019.(hawapo pichani.)
Wapiga Picha wa Vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na waandishi wa Habari kuhusu mkutano wa 39 wa SADC kufanyika hapa Nchini mwezi August 2019.

MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA BRIG. JEN. MSTAAFU, DKT. YOHANA DAUDI BALELE

$
0
0

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,   Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele,  ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi Mkoani Simiyu
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiwa  wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi Mkoani Simiyu
 Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge wakiteta jambo kabla ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani  Mkoani Simiyu
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiweka  Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele,  ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani  Bariadi Mkoani Simiyu  
 Kulia ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume wake ,  ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
 Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Stanslaus Nyongo akiweka shada la Maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
 Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Mch.Elias Swita(wa pili kulia) akibariki kaburi ambalo umezikwa mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James (mwenye kofia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na wengine ni baadhia ya viongozi wakiondoka eneo alilozikwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Mkoani Simiyu  
 Kutoka kushoto Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael  Isamuhyo, Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Njelu Kasaka, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiteta jambo mara baada ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  akiweka shada la Maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam  na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi  Mkoani Simiyu.
Viewing all 110153 articles
Browse latest View live




Latest Images